A,a 1 herufi ya kwanza ya alfabeti ya Kiingereza. 2 barabara; tangu
mwanzo hadi mwisho he knows the subject from A to Z analijua hilo somo
barabara adj 1 (naut) -a daraja la kwanza. 2 (colloq) zuri sana I
am feeling an A 1 najisikia vizuri sana. 3 -a daraja la juu this essay is ~
material insha hii ni ya daraja la juu.
a/an indef art 1 -o ote, fulani, moja k.m. buy a
book nunua kitabu (chochote). 2 (a certain one) mmoja, yeyote mmojawapo
there is a man to see you kuna mtu anataka kuonana nawe a Mr. Juma Bwana
mmoja aitwaye Juma (`an' hutumika badala ya `a' kwa majina yanayoanza na
irabu k.m. an egg yai moja twenty miles an hour maili ishirini kwa
saa.
aback adv 1 (arch) nyuma kinyume. 2 be taken ~
shtuka, staajabu, shangaa, duwaa.
abacus n abakusi, abaki: kibao maalum chenye shanga
kinachotumika kusaidia kuhesabu.
abaft adv, prep (naut) katika tezi, kuelekea tezi, karibu na
tezi, nyuma ya chombo.
abandon vt 1 (desert) tupa; toka katika gea;
telekeza; jitenga na ~ wife and children; acha, tupa, telekeza mke na watoto. 2 (give
up) acha ~ rights/a property acha haki/mali. 3 (phr) ~
hope kata tamaa. 4 (phr) ~ oneself to something jiachia kabisa k.m.
huzuni, furaha, dhambi, tamaa n hali ya kutojizuia, kujisahau, kujiachia they
danced with ~ walicheza wakaji-jisahau. ~ed adj 1 (deserted)
-lioachwa, -liotupwa, -liotelekezwa, -kiwa an ed village kijiji kilichotelekezwa,
mahame, tongo. 2 (profligate) -ovu, -potovu, fisadi, -asherati. ~ment n
1 tendo/hali ya kutupa/kutupwa, kuacha kuachwa; tendo/hali ya ufisadi. 2 (carelessness)
ulegevu, uzembe. 3 (complete surrender) see abandon.
abase vt tusha,fedhehesha,dhalilisha, vunjia heshima/hadhi,
shushia hadhi
~oneself jitahayarisha, jifedhehesha, jiaibisha. ~ment n
utwezo, unyonge, udhalili, udhilifu. 2 unyenyekeo, unyenyekevu (kupita kiasi).
abash vt ona haya, aibishwa, fedheheshwa to be ~ed
tahayarishwa. ~ ment n fadhaa, haya, tahayuri, fedheha.
abate vt, vi 1 punguza; pungua, punguka. 2 komesha. ~
ment n 1 kupunguza; kupungua, kupunguka. 2 kukomesha.
abattoir n machinjioni.
abb n (lit) mtiririko wa vitendo see plot.
abbess n (rel) mama mkuu, bi mkuu (katika nyumba ya
watawa wa kike).
abbey n (rel) 1 makao ya watawa. 2 jumuiya ya watawa.
abbot n (rel) mkuu wa watawa katika nyumba ya watawa wa
kiume.
abbreviate vt fupisha (hadithi, hotuba, neno n.k.);
punguza, kusuru. abbreviation n ufupisho,kifupi, kifupisho, ufupishaji, k.m.
mt. badala ya methali, TZ badala ya Tanzania.
ABC, abc n 1 alfabeti. 2 maarifa ya msingi the ~ of
driving maarifa ya msingi ya udereva.
abdicate vi acha/ng'atuka kwenye cheo kikubwa k.v.
ufalme. abdication n kukimbia majukumu.
abdomen n fumbatio, tumbo. abdominal adj -a
fumbatio, -a tumbo ~ pain maumivu ya tumbo ~ operation operesheni ya tumbo.
abduct vt teka nyara (watu). ~ion n kuteka
nyara, kutorosha mtu. ~or n mtekaji nyara, mtoroshaji.
abeam adv (naut) kwenye mstari wa pembemraba na
chombo, kwa kukingama na chombo.
abed adj (lit or arch) kitandani.
aberrant adj -potovu, -liokengeuka; -enye kasoro. aberration
n mkengeuko, kupotoka (kwa njia, tabia au akili); kasoro.
abet vt saidia, shawishi, shirikiana na
(kutenda maovu). aid and ~ saidia kutenda jinai. ~ment n
msaada,
ushirika, mshawasha. ~ter, ~tor n mshiriki; mshawishi
(hasa kwa mabaya), mbuya; msaidizi jinai.
abeyance n kutokutumika kwa muda
this rule is in ~ sheria hii haitumiki kwa wakati huu.
abhor vt chukia sana, chukizwa sana
~cruelty to animals chukia ukatili kwa wanyama. ~rence n
chuki kubwa, karaha. ~rent adj
abide vt 1 ngoja, ngojea. 2 stahimili, vumilia he can't ~
him hawezi kumvumilia vi 1 (arch) kaa mahali, tulia mahali, shinda
mahali and they abode there three days wakakaa huko siku tatu. 2 (phr)
~ by tii, shikilia, fuata, zingatia (ahadi, kusudi, amri, n.k.) ~ by an
agreement fuata mapatano. abiding adj 1 -a kudumu, -a milele. 2 (leg)
tiifu law abiding person, mtii sheria, mwenye kufuata sheria.
ability n 1 uwezo (kimwili, kiakili) to the best of my ~
kwa kadri ya uwezo wangu a man of great ~ mtu mwenye uwezo mkubwa. 2 werevu.3
kipaji a boy of abilities mvulana mwenye vipaji vingi. able adj -enye
uwezo, hodari (kimwili, kiakili) to be able to do something kuweza kumudu/kufanya
jambo drinkable -a kunyweka. ably adv kwa ustadi, kwa akili.
ab initio adj (leg) toka mwanzo. void~ batili toka
mwanzo.
abject adj 1 duni, -nyonge kabisa, fakiri ~ poverty
ufukara, umaskini kabisa. 2 (of persons) -a kudharauliwa ~ behaviour matendo
duni, tabia ya kujidhalilisha mno an ~ apology kitendo cha kuomba msamaha kwa
kujidhalilisha mno. ~ly adv. ~ ion n. ~ness n.
abjure vt acha, kana (kwa kiapo). abjuration n.
ablate vt ondoa kwa kuyeyusha/ kukata/kumomonyoa/kukausha. ablation
n.
ablaut n ablauti: kubadilishwa irabu
ya mzizi wa neno ili kuonyesha
nyakati k.m.: sing, sang, sung,
ablaze adj,adv 1 -a kuwaka the house is~
nyumba inawaka moto. 2 -a kung'aa; -a kumeremeta (fig) the face of the bride was
~with happiness uso wa bibi harusi ulimeremeta kwa furaha.
ablution n 1 kuosha; kuoga; kunawa. 2 (ceremonial)
kutawadha, kutia tohara; kuosha maiti, kujitakasa perform one's ~s jiosha.
abnegate vt 1 kana. 2 jihini, jinyima. abnegation n.
abnormal adj 1 -siyo ya kawaida (hasa enye kuleta hisia
hasi). ~ity n.
aboard adv chomboni, katika ndege, melini go ~ panda
chomboni; welcome ~ karibu(ni) chomboni.
abode n (arch or lit) makao, makazi, maskani,
mastakimu.
abolish vt komesha, futa, ondoa kabisa ~ tax, futa
kodi ~ a law tangua sheria. abolition n (of slavery)
ukomeshaji wa utumwa.
A-bomb n bomu la atomiki.
abominate vt chukia mno, kirihi. abominable adj
-a kuchukiza mno, makuruhi. abomination n
aboriginal adj (of living creatures) -a asili, -a
kwanza, -a awali. aborigine n mwananchi wa asili. A ~s wananchi wa
asili ya Australia.
abort vi avya, haribu (mimba) vt. 1 toa mimba. 2
komesha kitu kisitokee. ~ed adj. ~ion n 1 kutoa mimba. 2
kuharibika mimba. 3 mimba iliyoharibika; (fig) (jambo, mradi au mpango)
usiofanikiwa. ~ionist n 1 mtoaji mimba. 2 mtetezi wa haki ya kutoa mimba. ~ive
adj -siofanikiwa, viza ~ive coup maasi yasiyofanikiwa prove ~ive kuwa
bila mafanikio, via.
abound vi 1 ~ (in/with) sheheni. 2 jaa tele the
river ~ in fish, mto umejaa samaki tele.
about1 adv kadiri ya, kama ~ as high as
that tree a kama mti ule.
about2 adv part potepote, huku na
huko, mahali pote the children were rushing ~ watoto walikimbia
huku na huko. 2 elekea nyuma. ~ face geuka nyuma.
about3 prep 1 hapa na pale he walked ~ the
town alitembea hapa na pale mjini. 2 kuhusu, juu ya he wrote a story
~ a lion aliandika hadithi juu ya simba he is careless ~ his personal
appearance hajijali. 3 karibia ~ to die karibia kufa, taka kufa he is ~ to
leave anakaribia kuondoka.
above1 adv 1 juu from ~ kutoka juu. 2
awali, juu as was stated ~ kama ilivyosemwa hapo awali. 3 mbinguni. ~ board adv
wazi wazi The discussion was ~ majadiliano yalikuwa bayana.
above2 prep 1 juu ya we flew ~ the
clouds tuliruka juu ya mawingu. 2 zidi wastani the temperature
has been ~ average halijoto imezidi wastani. 3 zaidi ya, kuliko to value humanity ~
wealth kuthamini utu zaidi kuliko mali. ~ all zaidi ya yote. over and ~
zaidi ya hayo. 4 safi, sio kifani, zuri mno she is ~ criticism hana doa.
abrade vt sugua, chubua, kwaruza, chuna (k.m. ngozi). abrasion
n (of the skin), mchubuko wa ngozi. abrasive n (tech)
kichubuo, kikwaruzo, msasa adj -a kuchubua -a kukwaruza; (fig) -a kuchukiza ~
voice sauti ya madende, ya kuchukiza.
abreast adv sambamba, chanjari (fig) be/keep ~
(of/with) the times jua mambo yanayotokea wakati huo.
abridge vt fupisha (hasa maandishi), punguza an ~ed
edition toleo lililofupishwa. ~ment n ufupishaji.
abroad adv 1 ughaibuni, ng'ambo,
ugenini be or travel ~ kuwa/safiri ng'ambo. 2 kila mahali there
is a rumour ~ that uvumi umeenea kwamba. 3 nje ya nyumba you are ~ early this
morning umetoka nje mapema sana asubuhi hii.
abrogate vt (leg) tangua, batilisha.
abrogation n.
abrupt adj 1 -a ghafula, -siotazamiwa. 2 (of speech,
writing or behaviour) bila nadhari, -a mkato. 3 (of a slope) -kali,
-kubwa.
abscess n usaha.
abscise vi pogoka, kongoka. abscission
n.
abscond vi toroka, jificha, kimbia kwa
kujificha. ~er n.
absence n 1 kutokuwako in my~ wakati
sipo. leave of ~ ruhusa ya kutokuwako. ~ of mind usahaulifu. 2 kutokuwapo
kimawazo. absent minded adj msahaulifu. absent mindedly adv.
absent mindedness n. 3 (lack) ukosefu, ukosekano there is an ~
of heat hakuna joto. absent adj 1 -tokuwepo. vt absent oneself
(from) acha kuja. absentee n. absentism n.
absolute adj 1 kamili ~ trust imani
kamili. 2 (despotic) -enye amri zote peke yake, -a kidikteta. 3
(infinite) huru, isiyo na masharti wala mipaka. 4 halisi, bila shaka ~ proof
ushahidi thabiti. ~ly adv. absolutism n udikteta; nadharia ya
siasa ya mtu mmoja kuhodhi madaraka yote.
absolution n 1 (rel) ghofira, msamaha. absolve
vt 1 samehe, achilia, epusha ~ from blame ondoa hatiani. 2 ghofiri, ondokana
na dhambi.
absorb vt 1 -fyonza, nyonya; sharabu ~ ink fyonza
wino. 2 shughulisha his work ~ed him kazi yake ilimshughulisha sana. ~ent adj
-enye kufyonza. ~er n kisharabu. ~ing adj an ~ing
novel riwaya inayoteka. absorption n 1 ufyonzaji. 2 (engrossment)
utekwaji (katika fikra au shughuli). absorptive adj.
abstain vi 1 jinyima, jihini, acha kufanya kutumia kitu he
~ed from smoking aliacha kuvuta sigara. ~er n (mtu) ajinyimaye total
~er: asiyekunywa mvinyo kabisa. abstemious adj -a kujihini (chakula
kinywaji n.k.). ~ness n.
abstention n 1 kutokupiga kura. 2 mzio. abstinence n.
~ (from) uzuiaji. abstinent adj.
abstract1 adj 1 dhahania, -a kuwazika tu. 2
-soweza kushikika. ~ noun nomino dhahania. in the ~ kinadharia.
abstract2 vt 1 toa katika, chomoa. ~ed adj
(engrossed) 1 -liotekwa kimawazo. 2 -lio fupishwa (k.m. kitabu au hotuba). ~edly
adv
abstraction n 1 usahaulifu; hali ya
kushughulika na kuacha kuzingatia mengine. 2 utoaji/ung'oaji wa kitu
k.m. ung'oaji jino. 3 dhana au wazo.
abstruse adj -gumu kueleweka/
kufahamika, tata, -enye kutatiza. ~ly adv. ~ness n
utatanishi.
absurd adj -a upuuzi, -a kipumbavu, -a kuchekesha. ~ity
n. ~ly adv.
abundant adj - ingi, tele. we have ~ food tuna
vyakula vingi sana. ~ly adv abundance n.
abuse vt 1 tumia vibaya. 2 tukana, tusi. 3 dhulumu, onea. ~
n 1 matumizi mabaya. 2 tabia mbaya. 3 matusi; maneno machafu/makali. abusive adj
abusive language lugha chafu. abusively adv. abusiveness n.
abut vi pakana na, -wa jirani na, egemea. ~ment n
mhimili (wa daraja au tao).
abyss n lindi kuu (fig) the ~ of despair
kukata tamaa kabisa abysmal adj ~ ignorance ujuha kabisa. abysmally
adv.
Abyssinia n Uhabeshi. ~n n
Mhabeshi adj -a kihabeshi.
academic adj 1 -a kitaaluma. 2
(discussion) -a kinadharia mno. ~ n ulama;
mhadhiri. ~ally adv. ~al adj. ~als n mavazi
(joho na kofia) wakati wa mahafali au sherehe rasmi za chuo.
academy n 1 chuo (cha elimu ya juu). Military ~ Chuo
cha Jeshi. 2 akademia (chama cha maulama). academician n mwanachama wa chama
cha maulama; mwanataaluma.
accede vi 1 kubali, ridhia. 2 pata au
rithi cheo when did he ~ to the throne? alirithi lini kiti cha
ufalme?
accelerando n, adv (music) mchapuko; kwa
mchapuko adj -enye mchapuko.
accelerate 1 vt, vi chapuka, chapuza,
zidisha mwendo; harakisha. acceleration n mchapuko. accelerator
n kichapuzi.
accent n (gram) 1 kiinitoni. 2 lafudhi. 3 (colloq)
msisitizo this year the ~ is on youth: mwaka huu msisitizo ni wa maendeleo ya
vijana tamka kwa lafudhi; sisitiza; tia shadda; bainisha. ~vt tamka kwa lafudhi. ~ed
adj. ~uate vt tia mkazo. ~uation n
accept vt 1 pokea ~ a bribe pokea
rushwa. 2 kubali, kiri ~ a fact kubali ukweli. ~able adj.
~ability n ukubalifu. ~ance n kukubali, ridhaa.
access n 1 (means of) njia ya kufikia.
~ road barabara ya kuingilia. 2 (liberty) fursa ya
(kukaribia, kutumia, kuingia) easy of ~ rahisi sana kuingia. 3 (sudden burst)
kupandwa ghafla (na hisia, homa) an ~ of anger kupandwa hamaki/ hasira. ~ible adj
-a kuingilika, -a kufikika; -a kupatikana.~ibility n ufikikaji; upatikanaji.
accessary n msaidizi, mshiriki, hasa katika jinai. accession
n 1 kupata au kupanda cheo. 2 (increase) nyongeza recent ~ to the library
nyongeza za karibuni za vitabu vya maktaba. accessory n 1 see accessary
2 n kifuasi, kitu cha ziada accessories of a bicycle vifuasi vya baiskeli
k.m. taa, kengele, pampu.
accidence n mbadiliko umbo.
accident n 1 ajali highway ~ ajali
barabarani. (prov) ~s will happen ajali haina kinga. 2
bahati I met him by ~ nimekutana naye kwa bahati. ~al adj -a bahati. ~ally
adv. kwa bahati.
acclaim vt 1 karibisha/pokea kwa
shangwe, tangaza kwa shangwe (k.m. rais/mfalme). n himidi,
shangwe. acclamation n shangwe he was elected by ~
alichaguliwa kwa kauli moja.
acclimatize vt (fig) zoea (mambo
mageni, mazingira).
acclivity n mwinuko.
accolade n himidi, sifa kuu.
accommodate vt 1 patia mahali
pakuishi. 2 patia nafasi the house ~s ten people nyumba ina
nafasi ya watu kumi. 3 (adapt) rekebisha. 4 (oblige) fadhili, kirimu, -pa to
~ somebody with a loan fadhili kwa kumpa mkopo mtu. accommodating adj -a
hisani, -enye hisani, maridhia. accommodation n 1 (board)
nyumba/vyumba vilivyo tayari kukaliwa/kupangishwa. 2 marekebisho 3 (kindness)
fadhila, hisani. 4 maafikiano.
accompany vt 1 enda na, fuatana na. 2 andamana na fever
accompanied with delirium homa iliyoandamana na kuweweseka. 3 (mus)
pamba. accompaniment n 1 kifuasi, kiambata. 2 (mus) ala saidizi. accompanist
n (mus) mpiga ala saidizi.
accomplice n mshiriki (jinai).
accomplish vt maliza, timiza,fanikisha. ~ment n
1 utimilifu, ufanikishaji. 2 ustadi. ~ed adj hodari, stadi an ~ed dancer
mcheza ngoma hodari.
accord1 n 1 makubaliano, maafikiano.2 mkataba. 3
uwiano. 4 (phr) of her own ~ kwa hiari yake, bila kulazimishwa.
accord2 vi 1 (with) patana (na),
lingana (na); kubaliana (na) vt (formal) jalia, pa, toa ~
permission toa ruhusa, -pa ruhusa ~ a warm welcome karibisha kwa shangwe. ~ance
n kukubaliana in ~ance with kwa mujibu wa, kwa kufuatana na. ~ant adj
-enye kupatana kulingana na. ~ing (conj) you will be paid ~ing as
you work hard or poorly: utalipwa kwa kadiri ya utendaji kazi wako. ~ing (prep)
he will be paid ~ing to his work atalipwa kufuatana
na kazi yake. ~ingly adv.
accordion n kodiani.
accost vt kabili, laki I was ~ed by a
stranger nilikabiliwa na mtu mgeni.
account1 n hesabu; akaunti. current ~ n
akaunti ya hundi. savings ~n akaunti ya akiba. deposit ~ n
akaunti ya amana. final ~ n hesabu za mwisho. ~ancy n uhasibu.
~ant n mhasibu.
account2 vi 1 fikiria He is ~ed
innocent until he is proved guilty anafikiriwa kuwa hana
hatia mpaka atakapotiwa hatiani. 2 eleza sababu ya. 3 -wa sababu ya angamizo, teka. ~able
adj -enye kuwajibika, -enye kuhusika. ~ability n 1 mkokotoo manufaa.
2 put something to good ~ tumia kitu kwa manufaa. 3 maelezo. call somebody to ~
taka mtu ajieleze. 4 (phr) give a good ~ fanya vizuri. 5 (phr) take
something into ~ zingatia sababu. 6 on ~ of kwa sababu ya.
accoutrements n 1 vikorokoro, vitu
vidogovidogo vinavyotumika katika shughuli fulani, hasa safari. 2 vifaa
vyote vya askari isipokuwa mavazi na silaha.
accredit vt 1 teua kuwa mwakilishi. 2
tambua. ~ed part adj -a kutambuliwa rasmi.~ation n
accretion n 1 uongezekaji au ukuaji wa kitu utokanao na
kuongezewa au kulimbikiziwa vitu vya nje. 2 ongezeko (hasa la polepole).
accrue vi ongezeka, tokana na the profits which ~ from
work faida zinazotokana na kazi.
acculturation n uzoeaji wa utamaduni/tabia ya kigeni.
accumulate vt kusanya, limbika. ~ vi
ongezeka, jikusanya. accumulation n. accumulator n
1 kilimbikizi umeme. 2 (computer) kilimbikizi namba.
accurate adj 1 -angalifu, barabara.
2 isiyo na hitilafu, sahihi. accuracy n. ~ly adv
sawasawa.
accursed adj -liolaaniwa.
accuse vt shtaki, laumu, kengemeka,
shutumu ~ somebody of commiting a crime shitaki mtu kwa kuvunja
sheria. accusation n mashtaka, lawama, shutuma, mkengemeko. ~r n
mshtaki. ~d n mshtakiwa. accusingly adv kwa shutuma.
accustom vt zoea, zoeza. ~ oneself to jizoeza. ~ed
adj 1 (phr) be ~ed zoea. 2 siku zote, his ~ place mahala pake
pa kawaida.
ace ji 1 ree: karata ya kuchezea yenye ng'anda moja au dadu
yenye alama moja. 2 (colloq) mtu hodari kabisa. k.m. mchezaji hodari wa mpira. 3 (phr)
within an ~ of chupuchupu, nusura.
acerbity n 1 ukali, uchungu (wa kitu,
moyo au maneno). 2 (pl) acerbities maneno makali.
acetate n (chem) asetati.
acetic adj -a siki, -a asetiki.
acetylene n asetilini: gesi inayotumika
kuwashia taa na kulehemia.
ache n mchonyoto, maumivu
(yanayoendelea). ~ vi uma, wanga, changa, chonyota, my
head ~s kichwa kinaniuma; (fig) my heart ~s moyo unaniuma;
(fig) tamani sana my heart ~d for her nilikufa juu yake.
achieve vt maliza; timiza; faulu;
fanikisha ~ one's purpose: timiza lengo. achievable
adj. ~ment n mafanikio.
Achilles n (fig) ~ heel n udhaifu
spelling is my ~ heel udhaifu wangu uko katika tahajia.
acid1 adj -kali, chachu, -a asidi (fig)
-a kubeza adv kwa bezo.
acid2 n asidi .~ify vt. 1 (chem)
fanya asidi. ~ity n 1 uasidi. 2 (heart burn) kiungulia. ~ic adj
-enye asidi. ~ulous adj (fig) 1 -enye chachu, kali. 2 -enye tabia ya
ukali.
ack-ack n (sl) kombora la kutungulia ndege.
acknowledge vt 1 kiri, kubali.
thibitisha he didn't ~ defeat hakukiri kushindwa; (receipt
of) I ~ your letter ninathibitisha kupokea barua yako. 2
shukuru. 3 (regard as) tambua he is ~d to be an expert of
this subject anatambulikana kuwa ni bingwa katika fani hii. 4 onyesha ishara ya
kutambua I passed her in the street but she didn't ~ me nilipishana naye barabarani
lakini akajifanya hakunitambua. ~d adj -naetambuliwa. ~ment n
1 kukubali, kukiri. 2 shukrani.
acme n upeo, kilele, kikomo he reached the ~ of his
ability alifikia upeo wa uwezo wake.
acne n chunusi.
acolyte n 1 mtumishi (kanisani).
2 mfuasi.
acorn n (bot) mbegu au tunda la muoka.
acoustic adj -a akustika, -a sauti, -a elimu ya sauti na
kusikia. ~s n 1 akustika, taaluma ya sauti. 2 mazingira sikizi the ~s of
this room are good mazingira sikizi ya chumba hiki ni mazuri.
acquaint vt 1 julisha, pasha habari,
fahamisha. 2 fahamiana na, zoeana na. 3 jizoeza ~ oneself with one's
work jizoesha kazi be ~ed withsomeone fahamiana
na mtu fulani. ~ance n 1 uzoefu, ujuzi, maarifa. 2 mtu unayemfahamu, jamaa.
acquiesce vi 1 kubali, ridhia (kimya
kimya). ~nce n ridhaa. ~nt adj.
acquire vt pata, jipatia kitu (hasa kwa kujifunza au
kujizoeza au kwa jitihada) ~d taste upendeleo zoefu. ~ ment n
upataji. acquisition n 1 kupata. 2 pato, kitu kipatikanacho. acquisitive
adj -enye uchu/tamaa ya kupata. acquisitiveness n.
acquit vt 1 (leg) achilia ~ somebody of an
offence hukumu mtu kuwa hana hatia. 2 tenda ~ oneself well (of a task n.k.)
tenda vizuri/vyema. ~tal n kuachiliwa.
acre n ekari, eka (fig). God's~ makaburini.
~age n.
acrid adj -chungu; -kali (hasa kwa ladha au kwa harufu); -a
ukali wa tabia au mwenendo. ~ity n.
~ ness n.
acriflavine n (chem) akrifilavini.
acrimony n ukali (wa tabia/maneno). acrimonious adj.
acrobat n mwanasarakasi. ~ic adj -a
kisarakasi. ~ics n michezo ya sarakasi.
acronymy n akronimi: neno
linaloundwa kutokana na herufi za mwanzo za majina k.m. UNO - United
Nations Organisation.
acrophobia n woga wa kina.
across prep 1 (vuka) toka upande
mmoja hadi upande mwingine walk ~ the street vuka barabara. 2
ng'ambo (ya), upande wa pili.
acrostic n aina ya chemshabongo.
acrylic n. ~ fibre n utembo bandia
unaotumiwa kutengeneza nguo.
act vt, vi 1 (take action) tenda, fanya. 2 (of
stage) cheza, igiza. 3 jifanya;(feign) ~ for (represent) wakilisha ~
(up) on 1 (a suggestion/ advice) fuata; fuatilia. 2 athiri this medicine ~s
upon the heart dawa hii inaathiri moyo. ~ as fanya kazi ya he ~ s as an
interpreter anafanya kazi ya ukalimani. ~ up 1 jifanya, jifaragua. 2 leta
maumivu au maudhi. ~n 1 tendo, kitendo, amali in the ~ katika
kutenda/kitendo. 2 sheria (iliyopitishwa na Bunge). 3 onyesho (katika tamthiliya). 4 (pretence)
kujifanya, kujifaragua. A~ of God kudura. ~or n 1 mtenda, mtendaji,
mhusika. 2 (player) mchezaji. ~ress n mtendaji wa kike. ~ion n
1 tendo, kitendo, amali. take ~ anza kutenda, chukua hatua. out of ~ mbovu.
2 (gesticulation) ishara za maungo. 3 (effect) athari, matokeo ~ of
medicine, salt n.k. matokeo ya kutumia dawa, chumvi n.k. 4 (fighting) mapigano.
5 (leg) madai; mashtaka, daawa criminal~ mashtaka ya jinai. ~able adj
(leg) -a kuchukuliwa hatua. 6 (lit) (action of a play) onyesho. ~ive
adj 1 -tendaji. 2 mashughuli. 3 hai ~ive members wanachama hai. ~ive
volcano n
volkeno hai. 4 (gram) tendi. ~ive voice n kauli
tendi. ~vate vt amsha, chochea. ~ivism n (polit)
uhamasishaji kwa vitendo. ~vist n mhamasishaji mtendaji. ~vity n
1 hali ya utendaji; kushughulika; bidii, juhudi. 2 shughuli, utendaji, amali.
actual adj halisi, -liopo ~ situation
hali halisi. ~ity n. ~ly adv kwa kweli. ~ize
vt 1 maliza, timiliza. 2 hakikisha. 3 thibitisha.
actuary n mtakwimu bima. actuarial adj.
actuate vt 1 anzisha, washa (mashine). 2 chochea,
shawishi be ~d by (love, jealousy etc) sukumwa na (mapenzi, wivu, n.k.).
acuity n welekevu, ukali, wepesi.
acumen n busara, upevu wa akili,
welekevu.
acupuncture n tiba vitobo. acupuncturist n
mtaalamu wa tiba hiyo.
acute adj kali. ~ angle n pembekali. ~
accent n alama ya lafudhi (phr) ~ condition mahututi. ~ ly
adv. ~ness n.
ad (colloq) tangazo la biashara (abbr of advertisement).
adage n methali; msemo wenye
hekima.
adagio adj (mus) kipande cha muziki
(kinachopigwa taratibu).
Adam n Adamu. (fig) Adam's apple
kikoromeo, zoloto, kongomeo.
adamant n 1 jiwe linalosemekana
kuwa haliwezi kukatika wala kuvunjika. 2 (fig) be ~ shika kani,
kaidi, kataa katakata. adamantine adj.
adapt vt rekebisha, badili, tengeneza, tohoa (ili kufaa
matumizi fulani) ~ ed from iliyotengenezwa kutokana na; iliyotoholewa the play
has been ~ed from English mchezo umetoholewa kutoka Kiingereza. ~ability n.
~ation n 1 mabadiliko, marekebisho. 2 utohozi. ~able adj 1
-enye kurekebishika. 2 epesi kubadilika (kufuatana na mazingira).
~er n adapta; kirekebishi.
add vt jumlisha, ongeza, unga. ~ up
jumlisha. ~ in tia ~ to vi ongeza. ~ed adj
ilioongezwa. ~ition n 1 ongezeko. 2 kuongeza. ~itional adj -a
ziada.
addendum n nyongeza.
adder n kifutu.
addict vi, vt be ~ed to zoea,
pendelea, tawaliwa na (hasa ubaya k.m. ulevi). n mtawaliwa (hasa
wa ulevi ama desturi mbaya) morphine ~ mtawaliwa wa afyuni. ~ion/ ~
edness n. ~ive adj ~enye kuzoesha tabia mbaya.
additive n viungio, nyongeza.
addle vt, vi 1 vuruga, kanganya, changanya. 2 (of
eggs) oza; ozesha. adj 1 -enye kukanganyikiwa. 2 viza. ~ brained mtu
aliye changanyikiwa.
address1 n 1 (postal) anwani. 2 (home)
maskani. 3 (speech) hotuba, mahubiri. 4 (arch) (manners) adabu, mwenendo. form
of ~ mtindo (wa mawasiliano au kuitana). ~ee n mpelekewa barua.
address2 vt 1 andika anwani. 2
hutubia. 3 ita kwa jina na cheo. (phr) ~ oneself to (a
piece of work) jishughulisha na.
adduce vt toa, leta (ushahidi, sababu
n .k.). adduction n.
adeem vt (leg) batilisha the legacy is ~ed hiba
imebatilshwa. ademption n (leg) batilisho, batiliko ~ of legacy
batilisho/batiliko la hiba.
adept adj, n stadi, -bingwa, hodari.
adequate adj -a kutosha,-a kufaa kwa kusudi fulani. adequacy/
adequateness n utoshelevu.
adhere vi 1 nata, gandama. 2 (to be
faithful to) shika ~ to a promise shika ahadi. ~nce
n ufuasi, uaminifu. ~nt n mfuasi. adhesion n 1 mnato,
unataji, wambiso. 2 (path) mng'ang'aniano, muunganiko. adhesive adj
-enye kunata/ kung'ang'ania n kitu kinachonata k.m. plasta.
adhibit vt 1 ingiza, anzisha; tumia. 2 tia dawa. 3
ambatisha. ~ion n 1 kuingiza mwanzo; matumizi. 2 kutia dawa. 3 ambatisho.
ad hoc (lat) kwa kusudi maalum ~
committee kamati ya dharura (maalum).
adieu interj kwa heri; buriani bid
somebody aga mtu
ad infinitum (lat) bila kikomo, milele, daima. ad
interim adv kwa muda huu.
adipose adj shahamu (mafuta ya
mnyama). adiposity n unono, shahamu ~ tissue tishu
ya shahamu.
adit n mlango hasa wa kuingilia
katika mgodi n.k. kujongea, kusogea.
adjacent adj -a kupakana, -a karibu;
-a jirani. adjacency n kupakana, ujirani, kukaribiana.
adjective n (gram) kivumishi. adjectival adj
-a kivumishi ~phrase kikundi vumishi ~clause kishazi vumishi.
adjoin vt, vi pakana na. ~ing adj -a
kupakana na, -a kuungana na ~ing rooms vyumba vinavyopakana.
adjourn vt, vi 1 ahirisha. 2 acha, funga (mkutano). ~ment
n uahirishaji.
adjudge vt 1 hukumu, amua, kata kesi. 2 amuru (mtu apewe
kitu kisheria).
adjudicate vt, vi 1 hukumu, amua. 2 sikiliza kesi. 3 tamka to
~ somebody bankrupt kutamka kuwa fulani mufilisi. adjudicator n 1
hakimu, jaji. 2 mwamuzi. adjudication n 1 hukumu. 2 tamko la ufilisi.
adjunct n l kiongezo, kiungo (kilichoongezewa) 2 (gram)
(in clause) kijalizo.
adjure vt 1 apisha. 2 (implore) taka
mtu afanye jambo fulani. adjuration n 1 kiapo, tendo la
kuapisha. 2 kusihi kwa moyo.
adjust vt rekebisha, weka sawa ~ oneself to the
climate jizoeza na mazingira mapya. ~er n mkadiriaji wamadai ya bima. ~ment
n 1
urekebishaji. 2 zana za kurekebishia virekebishio. ~able adj
-enye kurekebishika.
adjutant n mfawidhi. adjutancy n cheo cha
usaidizi, ufawidhi, upambe.
adjuvant adj -enye msaada, -enye
kusaidia. n msaidizi.
ad lib adv (colloq) (abbr of ad libitum)
huru, iso kipingamizi. ~ vi iga, rekebisha utakavyo.
ad libitum adv 1 huria. 2 (katika sanaa utendi) kwa
kuongezea tendo. 3 (music) kwa kuongeza sehemu mojawapo katika mwongozo wa muziki
(ambayo ni huria).
adman n (US sl) mtunzi wa matangazo ya biashara.
admass n watu wanaovutwa upesi
na matangazo ya vyombo vya habari.
administer vt 1 tawala, simamia, endesha. 2 toa, lisha ~
an oath to lisha kiapo, apisha ~ punishment toa adhabu, adhibu, tia adabu. administration
n 1 utawala; himaya; uendeshaji; usimamiaji administration of justice utoaji
wa haki. 2 sehemu ya uendeshaji katika serikali. administrative adj. administrator
n msimamizi, mtawala, kabidhiwasii.
admire vt 1 tazama na kupendezwa;
stahi, penda. 2 (wonder at ) staajabia, shangilia. admirable
adj -a ajabu, -zuri, -a kusifiwa, -a haiba. admirably adv kwa
mshangao. admiration n upendezewaji, uvutiwaji; mshangao, ajabu, tendo la
kupenda (kustahi, kusifu, kushangaza, kustaajabu). ~r n ashiki (wa
mwanamke). admiring adj -enye kuonyesha kustaajabia, kusifu; -enye kuvutiwa,
-enye kushangilia. admiringly adv kwa kustaajabu, kwa kusifu.
admiral n mkuu wa jeshi la wanamaji.
admit vi, vt 1 ruhusu kuingia, ingiza, pitisha ~ into a
house ruhusu mtu kuingia ndani ya nyumba. 2 chukua, kuwa na nafasi ya the hotel ~s
only 50 people hoteli inachukua watu 50 tu. 3 laza. be ~ted into hospital
lazwa hospitali. 4 (acknowledge) kiri, ungama, kubali ~ (to)
guilt kubali kosa. 5 ruhusu; acha nafasi kwa it ~s of no doubt haina shaka
hata. ~tedly adv hakika. admissible adj 1 (leg) -a kukubalika,
kubalifu, halali admissible evidence ushahidi wa kukubalika. 2 (formal) -a
kufaa. admissibility n kukubalika, ukubalifu. admission n 1
ruhusa ya kuingia; kiingilio. 2 kukiri, kukubali, kuungama on his own admission kwa
kukiri mwenyewe. no admission si ruhusa kuingia. ~tance ruhusa ya
kuingia, haki ya kuingia.
admix vt, vi changanya; changanyika. ~ture n.
mchanganyiko.
admonish vt onya, rudi, asa. admonition onyo dogo.
admonitory adj -a onyo, -a kuasa.
ad nauseam adv kwa kiasi cha kuudhi, kwa kiasi cha
kuchusha.
ado n udhia, fujo, ghasia, matata much ~ about nothing
fujo za bure.
adobe n matofali ya udongo (yasiyochomwa) na nyasi.
adolescent adj -a balehe n 1 kijana
(kuanzia kubalehe hadi miaka 18). 2 mzulufu, mzee kijana. adolescence
n ujana (kipindi kati ya utoto na utu uzima).
adopt vt 1 panga utoto ~ a child panga mtoto ~
ed child mwana wa kupanga. 2 kubali ~ a resolution/an idea kubali azimio/wazo.
3 chukua/twaa na tumia we have ~ted the British legal system tumechukua mfumo wa
sheria wa Kingereza. ~ion n 1 kitendo cha kupanga mtoto. 2 kukubali. 3
kuchukua/ kutwaa. ~ive adj -a kupanga.
adore vt 1 abudu, sujudu. 2 (colloq) penda mno,
husudu, heshimu sana. adorable adj -a kupendeka mno, mahabuba. adorably
adv. adoration n 1 kuabudu. 2 tendo la kusujudu. 3 (rel) ibada
ya kuabudu. ~r n.
adorn vt pamba, remba. ~ ment n 1 pambo,
urembo. 2 upambaji,
urembaji.
adrenalin n adrenalini. adrenal adj
adrift adj, adv 1 -a kuyoyoma, -a kuelea ovyo. 2 (fig)
he cut himself ~from us alijitenga nasi.
adroit adj stadi, bingwa. ~ly adv
kwa werevu, kwa ustadi. ~ness n.
adulate vt sifu mno (hasa kwa
kujipendekeza), vika kilemba cha ukoka. adulation n. adulator
n msifu, asifuye. adulatory adj.
adult n mtu mzima, ngumbaru;
mnyama aliyekua adj. ~hood n utu uzima, ukubwa.
adulterate vt ghushi, changanya na kitu duni. adulterant
n kighushi. adulteration n ughushi.
adultery n uzinzi, zinaa commit ~
zini. adulterer n mgoni, mzinzi. adulterous adj.
adumbrate vt 1 dokeza, gusia. 2 bashiri. adumbration n.
ad valorem adj, adv ~ (tax) (kwa)
kufuatana na thamani ya kitu.
advance n 1 maendeleo. 2 (finance)
chambele; mkopo. 3 (pl) kujipendekeza he made ~s
alitongoza. 4 mapema, kabla ya; rubuni he saw me in ~ of the meeting aliniona kabla
ya mkutano he booked in ~ alirubuni. ~ vt, vi 1 endelea mbele, songa mbele,
sogea. 2 toa ~ an opinion toa (kauli, shauri). 3 sogeza the date was ~d
tarehe ilisogezwa mbele. 4 (finance) kopesha, toa karadha. 5 (rare) (price/rent)
zidisha, pandisha. ~d adj 1 -liotangulia, -lioko mbele. 2 (of people and
ideas) -enye kuona mbele. ~d studies masomo ya juu. 3 -lioendelea. 4 (in
years/age) -zee. 5 -lioongezeka. ~ment n 1 maendeleo. 2 (position/rank)
kupanda.
advantage n 1 heri, nafuu. 2 faida,
manufaa, mafao. take ~ of tumia (kitu fulani) kwa manufaa ya;
jinufaisha; danganya. 3 have/ gain/win an ~ (over), piku, kuwa na hali bora kuliko vt
nufaisha. ~ous adj -a manufaa, -a kuleta faida.
~ously adv.
advent1 n (of important events, person etc)
majilio, kufika the ~ of independence majilio ya uhuru.
Advent2 n (rel) muda wenye Jumapili nne
unaotangulia Krismas; kuja kwa Kristo; kuja kwa Kristo kwa mara ya pili. ~ist n
mtu anayeamini kuwa Kristo atakuja tena hivi karibuni Seventh Day Adventist Msabato.
adventitious adj -a bahati, -a nasibu.
adventure n tukio; tukio lisilo la kawaida/la hatari/la
ajabu a life of ~ maisha yenye vituko. ~r/ress n mpenda vituko. adventurous
adj 1 -enye kuthubutu. 2 -a hatari. adventurism n ujasiri, bahatisho,
jusura.
adverb n (gram) kielezi. ~ial adj
ad verbum adv neno kwa neno.
adversary n adui; mshindani.
adverse adj -a kinyume; -baya, -siofaa ~ effect
athari mbaya ~ly adv vibaya. adversity n 1 shida, dhiki,
taabu. 2 mkasa, maafa.
advert1 vi 1 (pay heed) taja, gusia. 2
rejea.
advert2 see advertisement.
advertise vt, vi tangaza, eneza habari ~ment n
(abbr. advert). ~r n mtangazaji. advertising n
kutangaza matangazo (hasa ya biashara); utangazaji.
advice n 1 ushauri, nasaha; mawaidha
seek ~ tafuta ushauri. 2 (pl) (comm) taarifa
(kutoka mbali).
advise vt, vi 1 shauri, nasihi, waidhi. 2 (inform)
arifu, julisha. ~r n mshauri spiritual ~ muaidhi. ~d adj
well ~ -a busara ill ~ si -a busara. ~dly adv baada ya
kutafakari sana; kwa makusudi. advisory adj -a ushauri advisory committee
kamati ya ushauri. advisable adj bora, -a kufaa, -a busara.
advocate n 1 (general) mtetezi. 2 (leg)
wakili. ~ vt tetea, pigania. advocacy n utetezi, uteteaji.
adze n tezo.
aegis, egis n himaya, uangalizi usimamizi under the ~ of
chini ya uangalizi/usimamizi wa.
aegrotat n igrotati: hati ya
kuthibitisha kwamba mwanafunzi hawezi kuhudhuria mtihani kwa kuwa
mgonjwa. ~degree n shahada igrotati.
aeon, eon n dahari: kipindi kirefu cha wakati kisichopimika.
aerate vt 1 ingiza hewa au gesi (katika uoevu, udongo n.k.).
2 safisha kwa hewa (k.m. damu). aeration n.
aerial adj 1 -a angani, -a hewani. 2 (arch) -a hewa,
-a kama hewa. 3 (lit) (immaterial) -isoumbo. 4 -a ndege ~ photograph picha
toka angani. n eriali, kipokea mawimbi.
aerie, aery/eyrie, eyry n 1 kiota cha tai.
aerobatics n sarakasi.
aerobic adj -a hewa, -enye kutaka
oksijeni. ~s n mazoezi ya viungo vya kuongeza hewa.
aerodrome n kiwanja cha ndege
(kidogo).
aerodynamics n elimu mwendo (hewani).
aerogram n karatasi ya ndege.
aeronaut n mwanaanga, mwanahewa.
~ics n elimu ya usafiri anga.
aerophotography n upigaji picha
angani.
aeroplane n ndege.
aerosol n 1 erosoli, upulizaji (wa uturi, rangi, dawa ya mbu
n.k.). 2 kipulizaji.
aerospace n anga.
aery see aerie.
aesthete, esthetete n mjumi, mpenda uzuri (hasa katika
sanaa). aesthetic adj. aesthetics n ujumi.
aether see ether.
aetiology see etiology.
afar adv mbali. from ~ kwa mbali, kutoka mbali.
affable adj bashasha. affably adv
affability n ubashasha, uchangamfu.
affair n 1 shauri, jambo, shughuli, neno urgent ~
amara, jambo
muhimu. 2 (pl) mambo state ~s mambo ya dola. foreign
~s mambo ya nchi za nje. 3 have an ~ with tembea fanya mapenzi na. 4 tukio.
affect1 vt athiri; gusa, hisi our position
will not be ~ed by these events msimamo wetu hautaathiriwa na matukio haya. ~ing
adj -enye kuathiri, -enye kuchoma moyo. ~ed adj 1 (diseased;
injured) -lioumia, -lioathirika, -lioshikwa na ugonjwa maumivu. 2 -lioguswa (na
sikitiko, furaha, huzuni n.k.).
affect2 vt jifanya, jisingizia, jitendekeza,
jitia ~ ignorance jitia hamnazo, jitia mwapuza. ~ed adj. ~ation n
tabia ya kujifanya. ~edness n. ~ion n (love) upendo,
huba mutual ~ kupendana, urafiki. gain/win somebody's ~ion (s) pendwa na. ~ionate
adj -enye moyo wa kupenda, -a kupenda, mpenda. ~ionately adv yours
~ionately akupendaye.
affidavit n (leg) hati ya kiapo.
affiliate vt, vi shirikisha, jumuisha; kuwa sehemu ya. be
~d to/with shirikishwa na.~ n mshirika, majumui. affiliation n
ushirikishaji; kushirikishwa; kushirikisha, ushirikishwaji.
affinity n 1 udugu; ukoo. 2 uhusiano (baina ya mimea,
wanyama, lugha n.k.). 3 (attraction) mvuto.
affirm vt kiri, tamka kwa dhati;
thibitisha. ~ant n mthibitishaji. ~ation n
uthibitisho. ~ative adj, n -a kukubali, -a ndiyo he answered in
the ~ative alikubali.
affix1 vt funga, bandika, gandisha.
affix2 (gram) n kiambishi.
afflatus n wahayi (ufunuo wa kidini).
afflict vt umiza, tesa, (kimwili/kiakili) the ~ed
walio matesoni, wanaoteseka. ~ing adj tesi. ~ion n mateso,
huzuni. ~ive adj huzunishi.
affluence n ukwasi, wingi, utajiri. affluent adj
-a ukwasi.
affluent n kijito.
afford vt 1 mudu, kuwa na uwezo he
can ~ to pay anamudu kulipa. 2 diriki, thubutu I can`t ~ to
displease him sithubutu kumuudhi. 3 toa, pa he ~ed me no chance hakunipa
nafasi. ~able adj -enye kumudika.
afforest vt panda miti (ili kufanya
msitu). ~ation n.
affranchise vt toa utumwani, komboa utumwani. ~ment n
ukombozi wa mtumwa.
affray n fujo, ugomvi hadharani.
affront vt tukana, adhiri, fedhehesha. n izara, tusi,
kashifa. ~ed adj. -liochukiwa/chukia.
Afghan n 1 Mwafghan. 2 ukaya au
blanketi la sufi.
aficionado n mshabiki.
afield adv (far ~) (phr) mbali na
nyumba/lengo n.k.
afire adv, adj (poet) -a kuwaka, -a kubimbirika moto he
was ~with rage aliwaka kwa ghadhabu.
aflame adv, adj -a kuwaka, -a moto. 2 -ekundu kama moto. 3 (fig)
be ~d with jawa na, shikwa na.
afloat adj, adv 1 (floating) -a kuelea.
2 (on ship) chomboni, melini. 3 (awash) -liojaa maji. 4 (out
of debt) -sio na deni. 5 (of rumour) -lioenea (k.m. uvumi).
afoot adv, adj 1 -nayotayarishwa,
-nayopikwa. 2 (arch) kwa miguu.
afore adv, prep (naut) mbele ya, lio
tangulia. ~-said adj -liotajwa. (leg) ~ thought
kwa kusudi.
afortiori adv (lat) bila shaka, ni dhahiri.
afoul adv katika kugongana na.
afraid adj -oga, -a hofu be ~ ogopa,sikitika I`m ~
I can't come nasikitika sitakuja.
afresh adv tena, upya, kwa namna mpya.
Africa n Afrika ~ n adj -a Mwafrika;
Kiafrika. ~nization n Afrikanaizesheni: siasa ya kuwapa Waafrika kazi za
madaraka. ~nize vt.
Afrikaans n Kiafrikana. Africaner n
Mwafrikana.
Afro- adj -a Kiafro, -a kiafrika.
aft adv 1 nyuma; (naut) tezini. 2 -a
tezini.
after adj -a baadaye, -a nyuma, -a kufuata in ~
years miaka inayofuata adv baadaye, halafu conj; prep baada ya, nyuma
ya (phr) ~all hata hivyo; ingawaje pref -a baadaye ~noon alasiri. do
something ~a fashion fanya kitu kwa namna moja au nyingine. a man ~ my own heart
mtu ninayefanana naye kitabia (phr) be/get ~somebody andama mtu.~ birth
n kondo la nyuma. ~ care n utunduizi baada ya kupona ugonjwa au
kutoka gerezani. ~clap n 1 itiko. 2 matokeo yasiyotarajiwa (agh mabaya). ~piece
n fasi, mchezo mdogo baada ya tamthilia maalum. ~ cabin n (naut)
chumba cha sitaha ya nyuma. n (colloq) visindikizo (baada ya mlo).
afterwards adv baadaye, halafu;
hatimaye.
again adv 1 tena, mara nyingine. ~ and ~ tena na
tena. now and ~ mara kwa mara, never ~ kamwe, abadani. 2 vilevile.
against prep 1 kwa kupingana/ kushindana, dhidi ya. 2
pinga. 3 kinyume cha; hitilafu 4 jitahadharisha na. 5 egemeza. 6 over ~ kabiliana.
agape pred adj -a kuachama.
agar-agar n jeli ya mwani.
agaric n (bot) kiyoga tembo.
agate n ageti: aina ya jiwe gumu
lenye shondo.
agave n (bot) mkongepori.
agaze adv kwa kukodolea macho, kwa kutumbua macho.
age1 n 1 umri. (leg) ~ of consent n
umri wa idhini. over ~ n kuzidi umri uliowekwa. under~ n umri
pungufu wa uliowekwa. old ~ n uzee, ukongwe. ~ group n hirimu,
rika. be of an ~ -wa na umri wa kufanya jambo. 2 kipindi, zama stone ~
kipindi cha zana za mawe. 3 (period) kwa muda mrefu.
age2 adj (of persons) -zee, -kongwe an
~d man mzee; (of things) kuukuu, -a kale, -a zamani. ~ ing n
kuzeeka. ~less adj -a milele, -a kudumu mpaka mwisho, -siozeeka ~ long
adj -a umri mrefu. ~ old adj -a miaka mingi.
agenda n ajenda.
agent n 1 wakala, ajenti. 2 nguvu za
asili au mtu anayetenda kupata matokeo fulani rain and wind are ~s
that wear down rocks mvua na upepo ni nguvu za asili zinazomomonyoa miamba. agency
n 1 wakala, uajenti. 2 nguvu, njia ya kufanya kitu. 3 sehemu/ofisi ya biashara.
agglomerate vt kusanya kwa wingi,
rundika. vi kusanyika, songamana. agglomeration n.
agglutinate vt ambatisha, bandika. agglutination n
uambatishaji, uambishaji. agglutinative adj (ling) -enye kiambishi,
-enye kuambishika agglutinative language lugha ambishi bainishi.
aggrandize, aggrandise vt jiongezea/ jitwaza/jitwalia zaidi
(hasa madaraka, cheo, utajiri, umaarufu n.k.). ~ment n kujiongezea, kutwaza,
kujitwalia zaidi.
aggravate vt 1 kuza, ongeza ubaya (wakosa, maumivu, jambo,
taabu n.k.). 2 (provoke) kera, kasirisha, udhi. aggravating adj -a
kukasirisha, -a kuudhi. aggravation n.
aggregate vt kusanya. vi jikusanya,
kusanyika, jumlika, jumuika n jumla; mkusanyiko. in the ~
-ote pamoja, kwa jumla; (in construction) vifaa vigumu kama vile mawe, mchanga. aggregation
n kokoto n.k. vinavyochanganywa na saruji. aggregation n 1 kusanyiko
(la vitu).
aggression n uchokozi, ushari (wa
maneno au vitendo). aggressive adj 1 -shari, -gomvi,
-chokozi; jeuri. 2 -a kutaka maendeleo, -a hima ~ salesman mwuzaji mwenye hima. ~ness
n uchokozi, ushari; hima.
aggressor n mchokozi, mshari.
aggrieve vt (usu passive) 1 tia uchungu,
sikitisha, udhi, kera. 2 (leg) dhulumu. ~d adj.
aggro n (GB sl) uhasama, uchokozi.
aghast adj -lioshikwa na woga au
mshangao, -liopigwa butwaa.
agile adj -nyumbufu, -epesi (wa mwendo). agility n.
aging n see ageing.
agitate vt 1 tikisa/tingisha, koroga. 2 hamakisha,
fadhaisha, chochea. vi tikisika, hamasika; (~ for) shawishi; hamasisha;
pigania. ~d adj -enye wasiwasi, -enye kutia wasiwasi. agitation n
1 mkorogo, mtikiso/ mtingisho. 2 (perturbation of mind) msukosuko, wasiwasi,
fadhaa. 3 (discussion for) majadiliano, mabishano; uchochezi. agitator n
mchochezi (hasa wa kisiasa); mfitini.
aglow adj -enye kumeremeta, -enye kuwaka be ~ waka,
ng'aa, meremeta.
agnail n kigozikucha (kigozi kilichochanika ukingoni mwa
ukucha).
agnate n ndugu wa kuumeni adj 1 -a kuumeni, -a upande
wa baba. 2 (fig) -a damu moja, -a asili moja, -a kutoka taifa moja, -enye udugu. 3
-a kufanana, -a kushabihiana.
agnostic n agnostiki: asadikiye kuwa
hatuna habari za Mungu wala hatuwezi kuzijua. adj. ~ism n.
ago adv zamani, kale, kitambo,-liopita long ~
zamani sana a little while ~ punde hivi, kitambo kidogo.
agog adj kwa shauku be ~ for something ngoja kwa
hamu set ~ tia hamu moyoni be all ~ jawa na hamu shauku.
agony n masumbuko makali, maumivu makubwa. agonize,
agonise vi umia vibaya, -wa na maumivu makali, sumbuka, teseka sana (moyoni). vt
umiza vibaya, sumbua, tesa. agonizing adj -a kuumiza sana, -a mateso, gumu
sana.
agoraphobia n woga wa nafasi kubwa za wazi. agoraphobic
n, adj.
agrarian
agrarian adj 1 -a kuhusu ardhi, mashamba, nchi na umilikaji
ardhi. 2 -a wakulima.
agree vi 1 kubali. 2 patana, kubaliana, ridhiana, afikiana.
3 ~ (with) lingana, fanana. 4 ~ (with) chukua, afiki the
climate does not ~ with me hali ya hewa hainichukui. 5 (of sums, accounts
etc) oana, kuwa sawa. ~d adj -liokubaliwa, be ~d with somebody
on/about something kubaliana juu ya ~d upon iliyokubaliwa that's ~d!
imekubalika! sawa. ~able adj 1 -a kupendeza, -zuri, -tamu, -latifu. 2 -a
maridhia. be ~able to ridhiana na. ~ ableness n 1 kupatana,
kukubaliana. 2 adabu. ~ment n 1 maafikiano 2 (contract) mapatano,
kondrati, kandarasi, mkataba. come to/arrive at/make/reach an ~ment with somebody
patana na. 3 (gram) upatanifu.
agribusiness n viwanda vya huduma za kilimo.
agriculture n kilimo, ukulima, elimu ya kilimo. agriculturalist
n. agricultural adj agricultural officer bwana shamba/afisa
kilimo.
agronomy n agronomia: sayansi ya uchumi wa kilimo. agronomic
adj -a (kuhusu) ukulima, -a mashamba, -a kilimo. agronomist n
mtaalamu wa kilimo.
aground adj, adv (of ship) -liopwelewa/kwama run ~
pwelewa/ kwama miambani.
ague n (arch) homa. aguish adj 1
-a homa. 2 (of person) -enye-homa.
ah interj aa! (sauti ya kustaajabu,
ya furaha au ya kuhurumia) salale! Masalale!
aha interj enhe! sauti ya kustaajabu,
kufurahi au kukubali.
ahead adj, adv mbele; kabla. go ~
endelea, tangulia. ~ of mbele ya. look ~ jiandaa,
jitayarisha. get ~ faulu the years ~ miaka ijayo.
ahem interj ukohozi au mgumio maalum wa ishara au onyo.
air-brick
aid vt saidia, auni. (leg) ~ and abet
saidia katika jinai. n 1 msaada, amara ~ without strings
msaada bila masharti. first ~ n huduma ya kwanza. 2 (pl) visaidizi. visual
~s n vielelezo.
aide-de-camp n mpambe.
aide-memoire n kidokezi, kisaidizi
cha ukumbusho,ardhihali.
AIDS n Ukimwi (Ukosefu wa Kinga Mwilini).
ail vt, vi (arch) 1 taabishwa, sumbuliwa. 2 ugua,
umwa what ~s him? anasumbuliwa na nini?/anaumwa nini? ~ment n
ugonjwa, uele, maradhi.
aim vt, vi 1 piga shabaha, lenga. 2 elekeza, azimia. n
shabaha, lengo, kusudi, azma. ~less adj siyo na sababu, -siyo na lengo
maalum. ~ lessly adv.
ain't (infml) mkato wa maneno are/is/ am/have/has/not.
air n 1 hewa; upepo. in the ~ -sio na hakika,
-vumayo; hewani. clear the ~ safisha hewa (fig) ondoa mashaka (kwa kusema
ukweli). 2 by ~ kwa ndege. 3 (radio) on the ~ redioni, (sikika)
hewani. 4 upepo mwanana 5 umbo, mandhari has an ~ of importance onekana kuwa
mtu maarufu (usu pl). give oneself/put on ~s jidai, jitwaza, jifanya
mtu wa maana, ringa. vt 1 anika, kausha. 2 achia hewa ipite. 3 toa (mawazo n.k.). ~ing
n 1 kuanika give an ~ing anika kitu. 2 kupunga hewa go for an ~ing
punga hewa. ~less adj -enye fukuto, bila hewa, kutokuwepo upepo kabisa. airy
adj 1 -enye wingi wa hewa. 2 (trifling) -epesi.
air-base n kituo cha ndege(za jeshi
la anga).
air-bed n godoro la upepo/hewa ~-bladder n
kibofu hewa.
airborn adj (of plane) -liokwisha ruka hewani; (of
people etc) -liosafirishwa kwa ndege.
air brake n breki za upepo.
air-brick n matofali yenye matundu.
air-bus
air-bus n ndege kubwa isafiriyo masafa mafupi.
air-conditioner n kiyoyozi, kisafisha hewa. air-conditioned
adj (of houses, cars) -lioyoyozwa.
air-cooled adj -liopozwa kwa hewa.
aircover n ulinzianga (ulinzi wa
ndege za kivita kwa majeshi ya nchi kavu).
aircraft n ndege. ~ carrier n
manowari yenye kituo cha ndege.
air-crew n watumishi wa ndege.
air-cushion n mto wa upepo/hewa.
air-drop n kudondoshwa kwa watu, chakula, vifaa n.k. kwa
kutumia miavuli.
air-field n see aerodrome.
air-force n jeshi la anga.
air-freight n uchukuzi wa mizigo kwa ndege.
air-gun n bunduki ya upepo.
air-hole n 1 tundu la kuingizia hewa. 2 povu la hewa.
air-hostess n mhudumu wa kike wa ndege.
air-jacket n (naut) vazi la kujiokoa.
airletter n see aerogram.
air-lift n uchukuaji wa watu au vifaa
kwa ndege (aghalabu katika dharura) vt chukua askari na vifaa
kwa ndege.
air-line n shirika la ndege (za kuchukua abiria na bidhaa). ~r
n ndege ya abiria.
air-lock n 1 zuio la hewa, kizuizi cha hewa. 2 mvungu wa
hewa.
air-mail n barua za ndege ~ edition
toleo la gazeti la kupelekwa kwa ndege.
airman n mwanahewa, mwanaanga.
air-mass n masi hewa.
air-passage n koromeo, njia ya pumzi.
airpillow n see air cushion.
air-plane n ndege.
air-pocket n kiriba hewa: kifuko cha hewa kinachosababisha
ndege kushuka ghafla.
air-port n uwanja wa ndege.
air-pressure n kanieneo ya hewa.
air-raid n shambulio la ndege.
air-route n njia ya ndege.
alarm
air sea rescue n uokoaji wa watu kutoka kwenye ndege
iliyoangukia baharini.
air-shaft n bomba la kuingizia hewa mgodini.
air-shed n banda la ndege.
airship n chombo anga.
air-sick adj -liyechefukwa angani.
~ness n.
air-space n 1 anga ya nchi (yaani iliyo ndani ya mipaka
yake). 2 anga hewa.
air-terminal n kituo cha abiria wa
ndege.
air-tight adj 1 -sioruhusu hewa kuingia au kutoka. 2 (of
an argument etc) -liothabiti.
air-umbrella n see air-cover.
airway n see air route.
air-worthy adj (of plane) -nayofaa
kusafiri angani.
aisle n njia baina ya viti katika majengo maalumu (k.m.)
kanisa, sinema, bunge).
ajar adj (of door) -lio wazi kidogo,
-liofunguliwa kidogo.
akimbo adj, adv (phr) with arms ~ kwa kuweka
mikono kiunoni/ nyongani.
akin adj 1 ~ (to) -a kufanana na. 2
-liohusiana na.
alabaster n jasi, alabasta: jiwe jeupe laini lililofanana na
marumaru.
a la carte adj, adv alakati: kwa
mchaguo wa chakula kutoka katika orodha ya vyakula.
alacrity n wepesi, hima, pamoja na
bashasha do something with ~ fanya upesi sana.
a la mode adv kwa mtindo wa kisasa. alarm n 1
kamsa, king'ora; onyo la hatari; yowe. raise the ~ piga mayowe/king'ora,
hadharisha. 2 hofu, wasiwasi (iliyoletwa kwa hatari iliyokaribu), mshituko wa hofu. ~
vt shitua, kamsisha; ogofya be ~ed at something ogopa; shtuka, ~ clock n
saa ya kengele. ~ing adj -a kutia hofu, -a kutisha, -a kuogogofya. ~ist
n mvumishaji (wa
albeit
mambo ya kutisha).
albeit conj ingawa, ijapokuwa.
albino n zeruzeru, albino.
album n albamu: kitabu cha picha (majina ya watu, mashairi,
stempu za posta n.k.).
albumen; albumin n uteyai.
alchemy n alkemia: kemia ya karne za
kati iliyokusudia kugeuza metali ya kawaida kuwa dhahabu. alchemist
n mualkemia.
alcohol n kileo: dawa inayotokana na
sukari au vitu vyenye sukari vinapochacha, pombe; spiriti. ~ic adj
-a kileo, -a kulevya, -enye asili ya kulevya n mlevi sugu. ~ism n
taathira ya ulevi; dalili na hali ya ugonjwa uletwao na ulevi.
alderman n (GB) mjumbe; diwani
mshauri wa Baraza la Jiji au mji.
ale n (GB) aina ya bia. ~ house n kilabu ya
pombe.
alert adj -a macho, -changamfu,
tayari. n tahadhari. on the ~ wa katika tahadhari, -wa
macho, -wa tayari. vt tahadharisha. ~ness n hadhari, kuwa macho, kuwa
tayari.
alfalfa n (bot) alfalfa: majani ya
kulisha ng'ombe.
alfresco adj (of meals) -a kuliwa nje adv nje.
alga n mwani, mchipwi.
algebra n aljebra. ~ic adj -a kialjebra. ~
ically adv kwa aljebra; kialjebra.
Algerian n Mwaljeria adj -a Aljeria,
-a Kialjeria.
alias adv pia aitwaye, kwa jina
jingine. n lakabu, jina la kupanga, jina bandia.
alibi n 1 (leg) udhuru (madai kuwa
mtu aliyeshtakiwa hakuwako pale jambo lilipotendeka). 2 kisingizio.
alien n mgeni adj -geni. ~ to -enye tabia
zisizo sawa na, -a namna mbali, -siopatana na ~-environment mazingira ya kigeni.
alienable adj (of property) -a kusikika, kuuzika au
kuhamishika. alienate vt (from) 1 (of people) farakisha,
tenga; tenganisha. 2 (of property) sihia,
all
twaa, nyang'anya. alienation n 1 utenganishaji,
mfarakano. 2 kunyang'anya. 3 mkengeuko.
alight1 vi 1 shuka, teremka (kutoka
kwenye farasi, motokaa n.k.). 2 tua the bird ~ed on the
branch ndege alitua tawini. 3 (fig) ~ on pata kwa bahati.
alight2 adj (be) -inayowaka,
inayong'aa, inayomeka (fig) their faces were ~ with happiness nyuso
zao ziling'aa kwa furaha.
align vt, vi weka/panga katika mstari ulio sawa, linganisha.
2 fungamana. ~ment n mfungamano, mfuatano. ~ed adj
fungamanifu. non ~ed adj -sio fungamana.
alike adj sawasawa,-enye kufanana,
-a kulandana adv kwa namna ile ile, kwa namna moja treat everybody
~ mtendee kila mtu sawa.
alimentary adj -a chakula. the ~ canal n njia
ya chakula (mwilini).
alimony n masurufu (baada ya mume
kumwacha mke).
alive adj 1 -zima, hai. 2 -a kuendelea; -a kukumbusha keep
the discussion ~ endeleza mjadala the microphone is ~ maikrofoni inafanya kazi.
3 ~ to -enye kuelewa (fikra, wazo). 4 changamfu. look ~ changamka. 5 ~
with jaa ~ with lice amejaa chawa.
alizarin n (chem) alizarini.
alkali n alikali (k.m. magadi, potasi,
amonia). ~ne adj -a alikali. alikaloid n (chem)
alikaloidi
all1 adj 1 -ote, kila. ~ Saints' Day 1
Novemba siku ya watakatifu wote. ~ Souls' Day, 2 Novemba, siku ya Marehemu wote/ ~
the people watu wote. 2 -o -ote beyond ~ doubt bila shaka yoyote.
all2 adv kabisa, -ote she was ~ excited
alisisimkwa ~ alone peke yake, bila msaada wa mtu yeyote. ~ along -ote -zima
~ along the road barabara nzima; (colloq) muda wote, tokea mwanzo. ~
the same lakini; hata hivyo. ~the same to/ ~ one
all
to mamoja, sawa haidhuru; (colloq) choka sana. ~ out (colloq)
jitihada zote. ~ over kila mahali, pote; -kwisha. ~ right sawa. ~ told
kwa jumla. ~up (with) kwisha, malizika.
all3 n my/his/their etc ~ kila kitu,
mali yote he has lost his ~ amepoteza kila kitu.
all4 (in compounds) 1 adj prefix -a
kiwango cha juu kabisa; siyo na mipaka. ~ merciful mwenye rehema zote. 2 (of
radio) ~ -mains volteji zote. ~ -round -a kila kitu; stadi katika kila
fani. ~ time high/low (colloq) rekodi ya juu/chini/kabisa. (of an
aircraft) (phr) ~ up weight uzito wa jumla wa ndege angani.
all5 pron 1 -ote, kila kitu he wanted ~or
nothing alitaka kupata yote au kukosa yote. ~ (of) kila mtu, -ote ~ of us
want to go sisi sote tunataka kwenda. (not) at ~ kwa vyovyote; kabisa if
you are at ~ worried ikiwa una wasiwasi wowote he is not at ~ suitable hafai
kabisa. not at ~ si kitu. once (and) for ~ kwa mara ya mwisho; kwa jumla.
~ in ~ kwa jumla ~ in ~it was a good seminar kwa jumla semina
ilikuwa nzuri; tegemeo she is ~ in ~ to him yeye (mke) ndiye tegemeo lake
(mume). Allah n Mwenyezi Mungu (katika Uislamu).
allay vt tuliza, punguza (maumivu matatizo, wasiwasi n.k.).
allege vt dai ~ that somebody is a
thief dai kuwa fulani ni mwizi. allegation n dai. ~dly
adv kama inavyodaiwa.
allegiance n utii; wajibu. oath of ~
kiapo cha utii.
allegory n istiari. allegoric(al) adj
-a kiistiari.
alleluia interj see hallelujah
allergy n mzio she has an ~ to coffee ana mzio wa
kahawa. allergin n kizio. allergic adj -a kuziza/kuzia. be
allergic to -wa na mzio.
alleviate vt tuliza, punguza (ukali au uzito wa maumivu
n.k.), fariji.
allure
alleviation n faraja, tulizo.
alley n (also alley way) 1 kichochoro. blind ~
(dead-end) kichochorofunge: kichochoro kisichotoka. (fig) kazi ya
kijungujiko. 2 njia nyembamba, njia.
alliance n 1 ushirikiano. 2 mwungano.
allied see ally v.
alligator n mamba (wa Marekani).
-pear n parachichi.
alliteration n takriri: marudio ya
silabi za mwanzo k.m. kuno kunena kuno kwa nini. alliterative
adj -enye takriri. alliteratively adv.
allocate vt 1 tenga, gawia, gawanyia. 2 wekea ~ funds
tenga fedha. allocation n 1 ugawaji, mgawanyo. 2 fungu, sehemu iliyotengwa.
allocution n hotuba rasmi, mahubiri,
mawaidha.
allomorph n (ling) alomofu: umbo
jingine la mofimu moja.
allophone n alofoni: umbo jingine la fonimu moja.
allot vt gawa, gawanya; tenga
~ duties gawa kazi. ~ment n 1 mgao. 2 (ground)
kikataa, kitalu.
allow vt 1 ruhusu, kubalia. 2 (acknowledge, admit)
kiri, tambua. 3 (money) toa the bank ~s 5% interest benki inatoa riba ya
asilimia tano (5%). 4 ~ for zingatia, fikiria ~ for damages zingatia
uharibifu. ~able adj halali, -enye kuruhusiwa, -a kujuzu.
allowance n 1 kukubali, kukiri; ruhusa. 2 posho, ruzuku,
marupurupu. 3 kipunguzi.
alloy n aloi: mwungano wa metali zaidi ya moja kufanya
aina mpya ya metali. vt 1 changanya metali bora na fifi. 2 (fig) dhoofisha,
punguza thamani/ubora.
allude vi (to) dokeza, gusia, taja
juujuu tu. allusion n (to) dokezo. allusive
adj -enye vidokezo.
allure vt vutia, shawishi, tamanisha.
n mvuto, ushawishi. ~ment n kivutio,
kitamanishacho. alluring adj -a kuvutia, -a kutamanisha.
alluvium
alluvium n kitope: udongo unaoachwa na mto/mafuriko n.k. alluvial
adj -a kitope, -a aluvia.
ally vt (oneself) with/to ungana na; -wa na urafiki;
shirikiana na. allied to (of things) husiana na, patana na, fanana
na, fungamana na. allied adj -nayohusiana. n rafiki (person or
state) msaidizi.
alma mater n shule/chuo alichosomea mtu.
almanac n shajara ya mwaka;
shughuli maalum katika mwaka.
almighty adj -enye nguvu zote, -enye enzi. n (rel)
The A~ n Mwenyezi Mungu, Mweza.
almond n (bot) (tree) mlozi, (fruit)
lozi, badamu adj -a lozi/badamu, -liotengenezwa kwa badamu ~ sweetmeat
halua ya lozi. ~-eyed adj -enye macho ya lozi.
almost adv takriban, karibu, nusura.
alms n sadaka (itolewayo kwa maskini). ~box n
sanduku la sadaka. ~giving n utoaji sadaka. ~house n nyumba ya
mafukara. almoner n 1 (arch) mtoaji sadaka. 2 (hospital) afisa
ustawi wa jamii.
aloe n 1 mshubiri 2 (also bitter ~s)
shubiri.
aloft adv juu sana.
alone adj 1 pekee, pweke, -enyewe do it ~ ifanye peke
yako adv peke yake. 2 let ~ sembuse, kefu. let well ~ -siingilie,
-siguse, siendeleze, basi. let somebody ~ achana naye. along adv 1 all
~ siku zote, wakati wote. 2 move ~ (of movement) songa mbele. 3 ~
with pamoja na. 4 get ~ with kubaliana na, patana na, elewana na. 5 ~ side
kandokando, ubavuni.
aloof adv mbali, -liojitenga. hold/stand keep (oneself) ~
-jitenga, -jitoa, kaa peke adj -a kujitenga, peke He is ~ in character ana
tabia ya kujitenga. ~ness n.
aloud adv kwa sauti (ya kusikika, bilakunong'ona).
alp n 1 alpu: mlima mrefu. 2 (in Switzerland) malisho
ya milimani. 3
alternate
the Alps n safu za milima mirefu baina ya nchi za
Ufaransa na Italia n.k.
alpenstock n mkongojo mrefu (watumiao wapanda milima).
alpha n alfa: herufi ya kwanza ya
alfabeti, ya Kiyunani. A~ and Omega mwanzo na mwisho. ~ rays
miali alfa. ~ plus -zuri kabisa.
alphabet n alfabeti, abjadi. ~ically
adv. ~ical adj -a (kufuata) alfabeti in ~ical
order kwa taratibu ya alfabeti.
already adj tayari it is done ~
imekwishafanyika, imefanyika tayari.
Alsatian n mbwa (kama bweha) mlinzi (wa polisi) adj.
also adv na, tena, vilevile, pia. ~ ran n
mshinde.
altar n (rel) 1 madhabahu, meza ya
kutolea dhabihu au kafara. 2 (christian) altare: meza
panapopokewa ushirika Mtakatifu. (phr) lead (a woman) to the ~ oa ~ -
cloth n tandiko la altare. ~-piece n (rel) picha au sanamu
nyuma ya altare.
alter vt badilisha, geuza that ~s matters hiyo
inabadilisha mambo. ~ation n mabadiliko. ~able adj -a kuweza
kubadili/kubadilishwa.
altercate vi gombana, bishana vikali, zozana. altercation
n mzozo, ugomvi, mabishano makali.
alterego n (lat) mwandani, mwenzi,
sahibu.
alternate vt,vi (of two things)
1 kuja/fanya kwa zamu (moja baada ya moja), badilishana, pokezana wet days ~d with
sunny days siku za mvua zilibadilishana na siku za jua. 2 ~ between geuka kati
ya hali na hali. 3 ~ with fuatana, moja baada ya jingine adj -a moja baada
ya moja, -a mpokezano, (of dates) -a kwanza, -a tatu n.k. they met on ~ days
walikutana kila baada ya siku moja ~ member mwanachama mbadala. ~ ly adv
kwa zamu, kwa
although
mpokezano. alternating adj -a moja baada ya moja. alternating
current n mkondogeu: mkondo (wa umeme) unaogeuza mwelekeo baada ya kitambo
fulani. alternation n matukio ya zamu, ubadilishaji duru. alternative
n 1 uchaguzi badili: fursa ya kuchagua kati ya mambo mawili au zaidi. 2 mbadala,
kibadala I have no alternative sina uchaguzi/ hiari is there no
alternative hakuna njia nyingine? adj -ingine, -a pili, -enye hiari kati ya
mambo mawili, enye fursa ya kuchagua baina ya vitu viwili. ~ly adv badala
yake. alternator n altaneta: jenereta (inayogeuza mkondo wa umeme).
although conj ijapo (kuwa), ingawa.
altimeter n (phy) altimeta: chombo
cha kupimia urefu juu ya usawa wa bahari.
altitude n 1 mwinuko (kutoka usawa wa bahari) at high ~
juu kutoka usawa wa bahari. 2 palipo juu kulingana na bahari.
altogether adv 1 pamoja, kwa pamoja; kwa jumla, pia I
will take them ~ nitavichukua pamoja. 2 kabisa it is ~ untrue ni uwongo kabisa n
in the ~ uchi.
altruism n ubinadamu; uungwana; utu: tabia ya kufikiria
wengine kuliko nafsi yako au kuishi na kutenda mambo kwa ajili ya manufaa ya wengine. altruist
n mwungwana, mwenye ubinadamu, mwenye utu. altruistic adj - sio na
ubinafsi/choyo. altruistically adv kwa utu.
alum n shabu.
aluminium (US) aluminum n aluminiamu; (chem)
alumini.
alumna n alumna: mwanafunzi wa kike aliyepitia chuo fulani.
alumnus n alumnasi: mwanafunzi wa kiume aliyepitia chuo
fulani.
alveolar n adj (phon) -a ufizi.
always adv daima, sikuzote, kwa
kawaida, kila mara.
a.m. (abbr) (lat) ante meridiem
asubuhi, baada ya saa sita usiku na
kabla ya adhuhuri.
amah n yaya.
amalgam n 1 mchanganyiko. 2 aloi ya zebaki. 3 (dental)
aloi risasi. ~ate vt, vi (of classes, societies, races people,
business companies) changanya, unganisha, ungana. ~ation n muungano,
muunganisho, mchanganyiko, mchanganyo.
amanuensis n karani wa imla, mnakili; katibu.
amaryllis n nargisi.
amass vt kusanya, rundika, limbika.
amateur n 1 ridhaa: hali ya kujishughulisha na sanaa,
michezo au utendaji wowote kwa kupenda bila kutegemea malipo. 2 mwanaridhaa adj -a
ridhaa; -siostadi. ~ish adj sio kamili; -sio stadi. ~ishness n
uanagenzi.
amaze vt staajabisha, shangaza be ~d staajabu,
shangazwa. ~ment n mshangao, mastaajabu. blank ~ment n
bumbuazi, hali ya kuduwaa, butwaa. amazing adj -a kushangaza, -a
kustaajabisha. amazingly adv kwa mshangao.
Amazon n 1 Amazoni: mto mkubwa wa Amerika ya Kusini. 2
jikedume: mwanamke mwenye nguvu na tabia kama za mwanaume.
ambassador n balozi. ~rial adj -a kibalozi. ~ship
n ubalozi ambassadress n balaozi wa kike.
amber n kaharabu adj -a rangi ya kaharabu.
ambergris n ambari.
ambidextrous adj -enye kuweza kutumia mikono miwili kwa
ustadi ulio sawa. ambidexterity n ustadi wa kutumia mikono yote miwili sawa.
ambience n mazingira, hali, mandhari. ambient adj
-a mazingira, -a pande zote.
ambiguity n utata: hali ya kuwa na
maana nyingi.
ambiguous adj tata, -enye maana nyingi.
ambit n eneo, mipaka au viwango vya
ambitious
mamlaka na madaraka.
ambitious adj -enye nia au tamaa ya makuu, -a kutaka makuu. ~ly
adv kwa tamaa ya makuu. ambition n 1 tamaa ya makuu. 2 lengo I
have achieved my ambition nimetimiza lengo langu.
ambivalent adj kinzani, -enye hisia/maana za kugongana k.m.
"kupenda na kuchukia sawia." ambivalence n hisia kinzani.
amble vi enda dalji. ~ n dalji.
ambrosia n ambrosi: chakula cha miungu (fig) kitu
kitamu chenye harufu ya kupendeza.
ambulance n gari la wagonjwa.
ambulatory adj -a kusogezeka, -a kuhamishika; (leg)
-a kubadilika. ~ will n wasia wa kubadilika; -enye nguvu ya kwenda.
ambuscade n see ambush.
ambush n uvamizi, mavizio lay an ~ tayarisha uvamizi.
vt vamia.
ameba n see amoeba.
ameer n see emir.
ameliorate vt, vi tengeneza, fanya zuri zaidi. amelioration
n
amen n (rel) amina, amin, na iwe hivyo.
amenable adj (to) 1 (of people) -sikivu,
-epesi kuongozwa, tiifu. 2 (of cases, situations) -a kufuata kawaida this case
is ~ to ordinary rules shauri hilo lafuata kanuni za kawaida ~ to jurisdiction
-a kuwajibika. amenability n (leg) dhima.
amend vt, vi sahihisha, fanya zuri zaidi tengeneza,
rekebisha. ~able adj -a kurekebishika. ~ment n marekebisho.
amends n fidia. make ~ to somebody fidia.
amenity n uzuri (wa mahali na mazingira) (pl)
vistawishi: huduma zinazofanya maisha kuwa mazuri.
America n Marekani, Amerika. ~n adj -a
Kimarekani ~n Mmarekani. ~ism n Umarekani.
amethyst n ametisti: kito cha thamani chenye rangi ya
zambarau.
amorous
Amharic n Kiamhari: lugha mojawapo
ya wahabeshi.
amiable adj maridhia, -pole, -ema, latifu. amiability
n urafiki, usuhuba. amiably adv kwa upole, kisuhuba.
amicable adj -a amani, -a urafiki ~
relationship uhusiano wa amani. amicably adv kwa
amani, kwa urafiki. amicability n.
amid prep see amidst.
amidst also amid prep (poet) kati
ya, katikati ya, miongoni mwa, baina ya.
amidships adv (naut) katikati ya
chombo.
amir n see emir.
amiss adj, adv -enye kasoro, -sio
sawa. take something ~ chukizwa, udhika, onea chuki (uchungu) (arch.)
(phr) what is ~? kuna nini?
amity n urafiki, uhusiano mwema.
ammeter n ameta: chombo cha kupimia mawimbi ya umeme kwa
kutumia ampea.
ammonia n (chem) amonia: gesi yenye harufu kali ya
kuchoma (mtu akiinusa huumia puani). ~ted adj (chem) -enye amonia,
-enye kuchanganyikana na amonia.
ammunition n risasi, baruti n.k. (zinazotumika katika
silaha k.v. bunduki, kombora).
amnesia n usahaulifu.
amnesty n msamaha (hasa kwa
makosa ya kisiasa/kiserikali) grant ~ toa msamaha.
amoeba n (biol) amiba: jamii ya vijidudu vidogo
sana visivyoonekana kwa macho, ambavyo huishi katika maji na udongo. amoebic dysentry
n kuhara damu kunakosababishwa na vijidudu hivyo.
amok adv (phr) run ~ charuka.
among(st) prep miongoni mwa, kati
ya I'm ~ many mimi ni miongoni mwa wengi.
amoral adj potovu, siojali maadili.
amorous adj -enye ashiki nyingi,
-a kuhusu/kuonyesha mapenzi. ~ly adv .~ness n.
amorphous
amorphous adj -sio na umbo wala
sura maalum.
amortize/amortise vt weka akiba, tenga fedha (kwa
ajili ya kulipia deni). amortization n
amount vi fikia, pata, -wa sawa (na)
his debt ~s to 100,000 shs. deni lake linafikia
shilingi laki moja it ~s to the same thing ni sawa tu. n 1 idadi, jumla,
yote pamoja the ~ of books idadi ya vitabu. 2 (quantity) kiasi, kadiri he
paid only a small ~ of money alilipa kiasi kidogo tu cha fedha.
amour n mapenzi.
amour-propre n 1 kujistahi. 2.
majivuno, majisifu.
amp n see ampere.
ampere n ampea: kizio cha kupimia mkondoumeme. amperage n
nguvu za umeme kwa ampea.
ampersand n alama ya & (= na). amphetamine n
amfetamini: aina ya
dawa ya kulevya.
amphibia n (zoo) amfibia: ngeli ya wanyama wanaoweza kuishi
nchi kavu na majini pia. ~n n 1 (zoo) amfibia: mnyama anayeishi nchi
kavu na majini. 2 (aircraft) ndege inayoweza kutua nchi kavu na majini. 3 (mech)
gari linaloweza kutembea nchi kavu na majini. amphibious adj -a kiamfibia. amphibiology
n amfibiolojia: taaluma ya elimuwanyama inayoshughulikia amfibia.
amphitheatre n 1 uwanja duara
(wenye safu za viti kwa watazamaji). 2 safu za viti vilivyopangwa
nusu-duara (kwenye jumba la maonyesho) natural ~ uwanda uliozungukwa na vilima.
ample adj 1 kubwa; -enye nafasi. 2
-ingi, tele. 3 -a kutosha, maridhawa a thousand shillings
will be ~ for my needs shilingi elfu moja zatosha kabisa kwa haja zangu. amply
adv -vya kutosha na zaidi. ~ness n.
amplify vt 1 kuza nguvu; pazasauti. 2 eleza zaidi, zidisha,
kuza, ongeza.
anagram
amplification n 1 ukuzaji nguvu, upazaji sauti. 2
ukuzaji, ziada, amplifier n amplifaya.
amplitude n 1 tambo: upepo wa
mbembeo. 2 ukubwa, upana, wingi.
ampoule n (med) kitabakero: kichupa
kidogo cha dawa ya sindano.
amputate vt kata kiungo cha mwili
(k.m mguu au mkono. amputation n kukata/kukatwa kiungo
cha mwili. amputee n aliyekatwa kiungo cha mwili.
amuck adv see amok.
amulet n hirizi.
amuse vt chekesha, burudisha, furahisha ~ oneself
jifurahia. ~ment n kiburudisho, burudani, kichekesho, furaha places of
~ment sehemu za burudani. amusing adj. amusingly adv.
an see a.
anabolism n (zoo) uanaboli: hali ya jumla ya ujenzi
wa kemikali mwilini.
anachronism n 1 jambo lililopitwa na wakati. 2 kosa la
kikronolojia (k.m. Mkwawa alitazama saa yake wakati asingeweza kuwa na saa). anachronistic
adj -a kizamani; -a kukosewa tarehe.
|
|
anaconda n (zoo) chatu (wa Amerika ya Kusini).
anaemia n (med) anemia: upungufu
wa damu. anaemic adj -enye anemia, -enye kupungukiwa
damu.
anaerobe n (bio) anerobi: viumbe vyenye kuishi
bila oksijeni katika mazingira yao. anaerobic adj -a anerobi.
anaesthesia n 1 (med) unusukaputi: hali ya
kutokuwa na hisia; ganzi (za maumivu, baridi). 2 (chem) (general) ~
nusukaputi local ~ ganzi. anasthetic n nusukaputi, ganzi; tawi la
kemia lishughulikalo na dutu zenye kutoa unusukaputi. anaestetist n (med)
mtaalamu wa unusukaputi. anaesthetize vt. (med) tia nusukaputi, tia
ganzi.
anagram n anagramu: neno liundwalo
anal
kwa kubadilisha herufi za neno jingine k.m. sukuma - sumaku.
anal adj. see anus.
analgesia n hali ya kutosikia maumivu. analgesic adj
(med) -a kutuliza
maumivu. n kituliza maumivu.
analogy n analojia: hali au tabia ya
kitu kufuata mkondo au sura ya kitu kingine kilichotangulia. analogize
vi linganisha kwa kufananisha. analogical adj -a mfanano; -a
ulinganifu. analogous adj -a kulingana, -a kufanana, -a kushabihiana. analogous
conditions n hali zinazofanana. analogue n kifanani: kitu
kinachofanana na kitu kingine (ingawa si cha asili moja nacho) mshabaha.
analyse vt 1 changanua; chambua. 2
chunguza ~ the cause of failure chunguza sababu za
kutofaulu. 3 (gram) tenga sentensi katika sehemu mbali mbali za kisarufi. analysis
n uchanganuzi; uchambuzi: utafiti wa asili ya vitu ili kuvumbua sheria zinazotawala
nguvu zake mbalimbali. analytical adj. analytically adv. analyst
n mchanganuzi; mchambuzi. analytics n taaluma/sayansi ya
uchanganuzi.
anapeast n (poet) kipande cha mstari wa shairi chenye silabi
fupi mbili na ndefu moja.
anarchy n 1 hali ya utawala huria. 2 kutokuwepo na serikali.
3 vurugu. anarchism n utawala huria; nadharia ya kisiasa inayosema kuwa
serikali na sheria havitakiwi. anarchist n 1 mfuata utawala huria. 2
mpinzani wa aina yeyote ya serikali. anarchical adj -enye machafuko ya mambo
ya kisiasa, -liojaa fujo.
anathema n 1 apizo la kanisa, laana. 2 kitu kichukiwacho
sana. vt (rel) laani, apiza.
anatomy n 1 anatomia: sayansi inayohusu mwili na viungo
vyake jinsi vilivyo. 2 (slang) mwili. 3 (fig) uchambuzi, uchanganuzi. anatomical
adj -a anatomia. anatomist n mwana
anemometer
anatomia, mchangua maiti. anatomize vt 1 tenga sehemu (za
mwili n.k.), katakata. 2 (fig) chambua, changanua.
ancestor n mhenga, babu/mababu (wa zamani) common ~ jadi
moja. ancestral adj -a mababu, -a nasaba. ancestress n. ancestry
n ukoo, jadi, kizazi cha mtu.
anchor n nanga ~ rope amari: kamba ya nanga. let
go/drop/cast the ~ tia nanga, tosa nanga. vt, vi 1 tia/toa nanga. 2
funga/kaza barabara drop ~ tia nanga. ~age n 1 maezi/ melezi; mahali
pa kutia nanga. 2 (fig) kivuli. jambo ambalo mtu analitegemea kwa hifadhi. 3
ushuru:gharama ya kutia nanga bandarini. ~ man n mratibu wa kazi ya kikundi,
mkuu wa kikundi.
anchorite n 1 sufii: mtu aliyejitenga na malimwengu (hasa
kwa ajili ya dini). 2 mtu wa pekee. anchoress n sufii (wa kike).
anchovy n aina ya dagaa wa maji chumvi.
ancient adj si -a siku hizi, kongwe n mkongwe. the
~s n watu wa kale ~ monuments magofu, majengo ya zamani.
ancillary adj. 1 -dogo (kwa cheo/madaraka) ~ road
barabara ndogo. 2 -saidizi ~ staff wafanyakazi wasaidizi.
and conj na: neno linalounganisha na kuendeleza sentensi he
came ~ ate food alikuja na kula chakula.
andante adj (of music) -a mwendo wa taratibu
kiasi/polepole.
andiron n kishika vijinga (cha chuma).
androgen n (bio) androjeni: jamii ya homoni inayoleta
hali ya uume katika kiumbe. androgynous adj 1 (bio) -a huntha, -a
kiume na kike.
anecdote n mchapo, hadithi fupi (juu ya mtu au tukio la
kweli). anecdotal adj.
anemia n see anaemia.
anemometer n (met) anemometa:
kipimaupepo.
aneurism; aneurysm
aneurism; aneurysm n (med) perema:
ugonjwa wa kuvimba tezi.
anesthesia n see anaesthesia.
anew 1 adv tena, upya, kwa mara
nyingine.
angel n 1 malaika. 2 (fig) mtu mzuri, mtu mpole na
mwema. ~ic adj -a malaika, -ema sana, takatifu.
angelica n (bot) mzizi wenye harufu
nzuri unaotumika katika dawa na upishi.
angelus n (rel) (kengele ya) Sala ya
Bikira Maria.
anger n hasira, ghadhabu, hamaki. vt hamakisha,
ghadhibisha, kasirisha.
angina (pectoris) n (med) angina:
ugonjwa wa moyo unaosababisha maumivu kifuani.
angle1 n 1 pembe from all ~s kutoka kila
sehemu/pembe. 2 pembenukta: sehemu baina ya mistari miwili ikutanayo corresponding ~
pembe mshabaha right ~ pembe mraba acute ~ pembe kali straight ~
pembe mstari reflex ~ pembe kuu. 3 (fig) mtazamo look at something from
all ~s angalia jambo kuzingatia mitazamo yote. vi, vt 1 geuka kipembe,
pinda. 2 mili. angular adj -enye pembe au kona kali. 2 (of a person)
king'onda, embamba sana na -enye mifupa iliyotokeza. 3 -gumu, -zito kufanya jambo. angularity
n hali ya kuwa na pembe.
angle2 vi vua samaki kwa mshipi.
~r n mvuvi wa mshipi. angling adj uvuvi wa
mshipi. ~ for something (fig) pembeja: tumia mbinu/hila/ ujanja
kupata kitu.
Anglican n Anglikana adj -a Kianglikana.
anglicize vt fanya kuwa kama Kiingereza. anglicism n
umombo:msemo wa Kiingereza unaotumika katika lugha nyingine. anglo adj -a
Kiingereza. Anglophone adj Anglofoni: -enye kutumia Kiingereza.
angora n 1 angora: paka, mbuzi au
sungura mwenye manyoya marefu. 2
annex
kitambaa kilichotengenezwa kutokana na manyoya ya angora.
angry adj 1 -enye hasira, -enye
chuki, -enye hamaki be ~ kasirika. 2 (of a cut, wound)
-enye kupwita. 3 (sea, sky, clouds) -a kutisha, iliochafuka. angrily adv
kwa hasira/ghadhabu chuki.
angst n hofu kubwa (inayosababishwa na hali ya
ulimwengu).
anguish n maumivu makali (ya moyo au akili), uchungu. ~ed
adj a kuonyesha/kusikia uchungu.
anima n 1 undani wa mtu. 2 hulka ya kike aliyonayo
mwanamume.
animal n 1 mnyama domestic ~
mnyama afugwaye. 2 kiumbe mwenye uhai anayeweza kuhisi na kujongea
k.m. mtu, mbwa, samaki n.k. 3 hayawani adj -a kinyama; -enye tamaa nyingi za
kimwili. ~ism 1 n unyama, uhayawani. 2 imani ya kuwa binadamu ni mnyama tu. ~ity
n unyama.
animate vt 1 huisha. 2 changamsha,
sisimua the debate was ~d majadiliano yalikuwa ya
kusisimua adj hai, -enye uhai, -a kuchangamka, -a kusisimua. ~ed cartoon
n katuni hai (wa sinema). animation n 1 uhai. 2 bidii, shauku. 3
utengenezaji wa katuni. animism n imani kuwa vitu vyote (miti, mawe upepo
n.k.) vina roho.
animosity n chuki, uadui, uhasama. animus n 1
chuki. 2 hulka ya kiume
aliyonayo mwanamke.
ankle n kifundo au tindi ya mguu ~
deep mpaka miguuni. ~ socks n soksi. ~t n
mtali, furungu.
annals n kumbukumbu za kihistoria
(mwaka hadi mwaka). annalist n mwandishi wa matukio ya
mwaka hadi mwaka.
annex vt 1 teka, nyang'anya, pokonya, twaa kwa nguvu
(nchi au shamba). 2 unga, ambatisha, jaliza. ~ation n 1 kutwaa kwa nguvu,
kunyang'anya, kupokonya, utekaji. 2 kuunga, kuambatisha. ~e n 1 jengo dogo
annihilate
(lililounganishwa kutoka jengo jingine). 2 (document)
kiambatisho.
annihilate vt hasiri, angamiza,
teketeza. annihilation n maangamizo, kuteketea.
anniversary n 1 siku ya ukumbusho (wa jambo kila mwaka). 2
maadhimisho ya siku ya ukumbusho (yaani baada ya kuzaliwa Kristo).
Anne Domini adv katika mwaka wa Kristo.
annotate vt fafanua, ongeza
maelezo, fasili, eleza. annotation n maelezo, ufafanuzi.
announce vt 1 tangaza, piga mbiu. 2 fahamisha. 3 tambulisha.
~ment n tangazo, mbiu. ~r n mtangazaji.
annoy vt udhi, sumbua, kera, kefya.
~ance n udhia, usumbufu, kero a look of ~ance
jicho kali. ~ing adj -a kuudhi, -a kusumbua, -a kukera. ~ingly adv.
annual adj 1 -a kila mwaka ~ public
holiday sikukuu ya kila mwaka. 2 -a mwaka ~ income mapato ya
mwaka. 3 (of plants) a mwaka mmoja tu. n toleo maalum la kitabu la kila
mwaka; tukio la kila mwaka; mmea wa msimu. ~ly adv kila mwaka.
annuitant n mlipwa malipomwaka. annuity n 1
malipomwaka. 2 haki ya kupata au kulipwa malipomwaka. 3 bima ya malipomwaka.
annul vt batilisha, futa, tangua,
sitisha.
annunciate vt 1 tangaza, taja; bashiri. Annunciation n
1 (rel) the ~ Kupashwa habari Bikira Maria na Gabrieli kwamba atamzaa Yesu
Kristo. 2 sikukuu ya kukumbuka tangazo hilo.
anode n anodi: ncha chanya ambapo mkondoumeme huingilia
kichanganuziumeme.
anodyne n (med) anodini: dawa itulizayo maumivu.
anoint vt (rel) paka mafuta. ~ment n. anomalous
adj -siokawaida; -a kipekee. anomaly n kioja: kitu kisicho
kawaida.
antagonize
anon adv (arch) punde, halafu kidogo. ever and
~ mara kwa mara.
anonymous adj bila jina, -siyotiwa
jina, -enye jina lisilojulikana an ~ letter barua
bila jina the author remains ~ mwandishi hajulikani.
anopheles n anofelesi: mbu aambukizaye ugonjwa wa
malaria.
anorak n anoraki: koti fupi
(la baridi/mvua) lenye kofia.
anorexia n ugonjwa wa kukosa hamu ya chakula. anorexic
n mtu mwenye ugonjwa huo.
another adj (additional) -ingine ~ thing kitu
kingine give me ~ shirt nipe shati jingine; (difference) come ~ time njoo
wakati mwingine; (similarity ) he will be ~ Shaaban Robert atakuwa kama Shaaban
Robert one way or ~ kwa njia moja au nyingine.
anoxia n unyongeo: hali ya kukosa
oksijeni hata ukapata ugonjwa wa nyongea (hasa kwa watoto wadogo).
answer n 1 jibu, itiko. 2 (maths) jawabu. 3 (leg)
utetezi. vt, vi 1 jibu, itika ~ the door itikia hodi. 2 (satisfy)
ridhisha, tosheleza. 3 (solve) toa jawabu, tambua. 4 (be useful) faa ~
somebody's purpose faa mtu. ~ to a description of somebody/ something fanana
na. 5 (correspond) lingana. 6 ~ for wajibika, kubali lawama no case to ~
hakuna kesi. 8 ~ somebody back jibu, jibiza. ~able adj -a kuweza
kujibiwa; -a kuwajibika, he is ~ able for his son's actions anawajibika kwa
matendo ya mwanawe.
ant n (soldier) chungu; (termite, whiteant)
mchwa; (brown) siafu; (red) maji moto; koyokoyo; (small black)
sisimizi, nyenyere ~ hill kichuguu.
antacid n kizimuaasidi: dawa izimuayo asidi, dawa ya
kutuliza kiungulia.
antagonize vt chokoza, sababisha
uhasama/adawa. antagonism n uhasama, utesi, uadui, chuki,
adawa. antagonistic adj. antagonist n mpinzani, adui.
antarctic
antarctic adj -a ncha ya kusini (ya dunia). n
Antaktiki.
ante1 n dau, chambele.
ante2 adj -a kutangulia, -a kabla.
antecedent adj -liotangulia. n 1 (of
event, circumstance) kitangulizi. 2 (gram)
nomino/kishazi/sentensi tangulizi: nomino, kishazi au sentensi inayorejewa na kiwakilishi
au kirai. 3 (pl) mababu, wahenga; historia ya mtu au watu. antecedence n
aula, kipaumbele, utangulizi.
antechamber n chumba cha kungojea. antedate vt
1 weka/toa tarehe ya nyuma (hasa kurudisha nyuma tarehe ya hati n.k.) 2 tangulia, tokea
kabla ya.
antediluvian adj 1 -a zamani sana,
kongwe. 2 -liotangulia gharika kuu. n mtu wa kizamani.
antelope n paa; palahala.
antemeridiem adj -a wakati kati ya saa 6 usiku na saa 7
adhuhuri.
antenatal n -a kabla ya kuzaliwa au
kuzaa.
antenna n 1 kipapasio. 2 (of redio)
antena: waya za kupokelea mawimbi ya sauti; erio.
antenuptial adj -a kabla ya ndoa.
antepenultimate adj -a tatu toka mwisho.
anterior adj -a kutangulia, (tech) mbele ya.
anteroom n see antechamber.
anthem n 1 (of nation) wimbo wa taifa/nchi. 2 (rel)
wimbo wa kanisa (aghalabu wa kwaya na kinanda).
anther n (bot) chavulio: sehemu za
stameni katika ua ambapo chavuo hutengenezwa.
anthill n see ant.
Anthology n diwani, koja (la kazi ya fasihi).
anthrax n kimeta.
anthropoid adj -a kufanana na mwanadamu au sokwe n
sokwe (k.m. gorila).
anthropology n anthropolojia: elimu
ya binaadamu (hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo
antiquary
yake ya awali). anthropologist n mwana anthropolojia. anthropological
adj.
anti- (pref) -sopendelea; dhidi ya:
kinyume na.
anti- aircraft adj -a kutungua ndege. antibiotic n
kiua vijasumu.
antibody n zindiko; kingamwili.
antic n (usually pl) tendo/mwendo chekeshi.
Antichrist n (rel) mpinga Kristo, aduiwa Kristo (hasa
anayesadikiwa kuwa atakuja muda mfupi kabla ya Kiyama).
anticipate vt 1 tangulia. 2 (expect) tumaini, dhani.
3 tazamia, tarajia. anticipation n. anticipatory adj -a
kungojea, -a kutazamia, -a kuwaza ya mbele.
anticlerical adj dhidi ya ukasisi ~laws sheria
dhidi ya ukasisi.
anticlimax n 1 mpomoko: upeo wa chini. 2 (of
speech/story) kupwaya kwa ghafla.
anticlockwise adv kinyume saa. anticyclone n
kitanguakimbunga, kinga ya kimbunga.
antidote n kiuasumu: dawa ya kupoza nguvu ya sumu.
anti-freeze kishushamgando.
antigen n antijeni.
anti-hero n shujaa pwaya.
anti-knock n (of engine) kizuianoki.
antimacassar n (arch) foronya ya kiti.
antipathy n uhasama, chuki, uadui.
antipathetic adj.
anti-personnel adj -a kuumiza au kuangamiza watu.
antipode n 1 kinyume kabisa. 2 (usu (pl) n
~s upande wa pili wa dunia (aghalabu kutoka hapo ulipo).
antipoison n see antidote
antiquary n mkusanya mambo ya kale. antiquarian adj
-a kuhusu wakusanya mambo ya kale. antique n kitu cha kale/tunu antique
shop duka la vitu na sanaa za kale adj -a kale. antiquated adj
kuukuu, -siotumika. antiquity n 1 zamani za kale. 2 (pl) mambo ya
kale k.v.
antisepsis
nyaraka, majengo; magofu n.k.).
antisepsis n zindiko.
antiseptic n antiseptiki: aina ya kemikali inayozuia kukua
kwa bakteria kwenye jeraha, ngozi, n.k.
anti-social adj 1 -a kupingana na jamii. 2 -enye kuelekea
kuvuruga ustawi wa jamii. 3 -siopatana na watu.
anti-tank adj (milit) -a kupigia vifaru ~gun mzinga
wa kupigia vifaru.
antithesis n tabaini, kinyume. antithetical adj.
antithetically adv. antitoxin n antitoksini: dawa au
kemikali ya kuzuia au kuzimua sumu mwilini. antitoxic adj.
antitradewind n upepo (wa magharibi unaovuma kaskazini ya
nchi za tropiki).
antler n pembe (ya paa).
antonym n kinyume.
anus n mkundu adj -a mkundu.
anvil n 1 fuawe. 2 (anat) kifuawesikio.
anxiety n 1 wasiwasi, dukuduku.
2 hamu. anxious adj -a wasiwasi, -a dukuduku be anxious
pata wasiwasi. dukuduku. anxiously adv.
any pron/adv -o ote in ~ case/at ~ rate kwa
vyo vyote vile the patient is not ~ better mgonjwa hana nafuu.~ body/
~ one will tell you yeyote atakuambia. is there ~body? kuna mtu
yeyote. ~ how/ ~way adv 1 vyovyote vile. 2 ovyo ovyo. 3 kwa njia
yoyote. ~thing pron kitu chochote she does not do ~thing hafanyi
chochote. ~ place/ ~where adv popote. ~wise adv kwa
kadiri yoyote, kwa namna yoyote.
aorta n (bio) mkole: mshipa mkubwa wa damu wa upande
wa kushoto wa moyo.
apace adv kwa haraka, kwa kasi,
hima, chapuchapu.
apanage n 1 mirathi: mali anayopata mtu kutokana na urithi
au cheo. 2 vifuasi asilia vya mtu au kitu.
apart adv 1 mbali. 2 pembeni, faraghani; chemba. 3 (separately)
tofauti a thing ~ kitu tofauti. 4 (asunder, parted) mbalimbali. 5 (out
apogee
of consideration) ~ from isipokuwa set ~
weka mbali, tenga force/draw ~ mamanua.
apartheid n siasa ya ubaguzi wa rangi.
apartment n 1 chumba, fleti US ~
house fleti. 2 (pl) ~s vyumba vya kuishi (aghalabu
hupangishwa).
apathy n hali ya kutojali. apathetic
adj -siojali. apathetically adv.
ape n 1 sokwe. 2 mwigaji (wa sauti na matendo ya wengine). 3
(colloq) mjinga, -sio na umbo au adabu nzuri. vt iga. apish adj
1 -a kisokwesokwe. 2 -a kuiga kipumbavu. apishness n.
aperient n (medicine) haluli: dawa yakuharisha adj -a
kuharisha.
aperitif n kiamshahamu: kinywaji cha alkoholi kinywewacho
kabla ya kula ili kuamsha hamu ya kula.
aperture n kitundu, kiupenyo, uwazi mfinyu k.m. wa
kupitishia mwanga katika kamera.
apex n kilele, ncha; kipeo.
aphasia n (path) afasia: ukosefu wa uwezo wa kusema
au kuelewa lugha kwa sababu ya kuumia ubongo.
aphorism n methali, maneno/msemo mfupi wa busara.
aphrodisiac n mkuyati: dawa ya kuamsha tamaa (ya kiume au
kike).
apiary n mahali penye mizinga ya nyuki; mahali pa kufugia
nyuki. apiarist n mfuga nyuki. apian adj -a kuhusu nyuki. apiculture
n ufugaji nyuki.
apiece adv kila moja, kila mojawapo it costs two shillings
~ inagharimu shilingi mbili kila moja.
aplomb n kujiamini.
apocalypse n (rel) ufunuo (hasa wa maarifa kutoka kwa
Mwenyezi Mungu) the A~ kitabu cha mwisho cha Agano Jipya chenye Ufunuo wa mtakatifu
Yohana. apocalyptic adj -a kutabiri hali ya maafa makubwa; -a kiyama.
apocryphal adj -a wasiwasi; -a kubuniwa; siyothibitishwa.
apogee n 1 upeo wa sayari ikiwa mbali
apologia
kabisa na dunia. 2 upeo wa juu kabisa.
apologia n utetezi wa kimaandishi.
apology n 1 kuomba radhi
unconditional ~ kuomba radhi bila masharti. 2 utetezi (wa imani,
vitendo, maisha n.k.). 3 (fig) mfano mbaya ~ for a meal mfano mbaya
wa mlo. apologize vi omba radhi, kiri kosa I beg to apologize
kumradhi, niwie radhi. apologetic adj. apologetically adv. apologist
n mtetezi.
apophthegm n see apothegm.
apoplexy n (med) kiharusi. apopleptic adj 1 -a
kiharusi. 2 -lioghadhibika sana (kiasi cha kubadilika rangi).
apostasy n ukanaji, uasi (wa dini,
imani, siasa). apostate n mwasi. apostatize vi
asi.
a posteriori adv, adj (lat) (reasoning)
mkasakisa (kupata sababu kutokana na matokeo/athari).
apostle n 1 (rel) mtume (mmojawapo wa mitume kumi na
wawili wa Yesu Kristo). 2 kiongozi (wa imani mpya au tapo la kurekebisha dini fulani). ~s
creed n Imani ya Mitume adj 1 -a kitume 2 -a Papa.
apostrophe n 1 apostrofi: alama ya
kifupisho k.m. can't (badala ya cannot) Moh'd (badala ya
Mohamed). 2 alama ya herufi k.m. ng'ombe.
apothecary n (arch) mfamasia: mtu anayechanganya na kuuza
madawa.
apothegm msemo mkali.
apotheosis n. 1 ugeukaji mungu au
mtakatifu. 2 uondokanaji na maisha ya kilimwengu. 3 kilele cha heshima
au fahari. 4 mfano kamili, mfano bora sana she is the ~ of womanhood yeye ni mfano
bora wa wanawake.
appal vt tisha, ogofya, shtua ~ling adj 1 -a
kutisha, -a kuogofya. 2 -a hali mbaya sana. ~lingly adv.
appanage n see apanage.
apparatus n 1 (seti ya) zana za kazi, vifaa; mashine (yenye
kazi maalum). 2 ogani za mwili, sehemu za mwili zinazokamilisha mfumo wa kawaida
applaud
mwilini the breathing ~ ogani zote zinazohusiana na kupumua.
apparent adj 1 dhahiri, wazi heir ~
mrithi dhahiri. 2 -a kuonekana the ~ cause sababu inayoonekana. ~ly
adv inavyoonekana.
apparition n 1 shani la ajabu. 2 kivuli cha mfu
(kionekanacho), mzuka.
appeal vi 1 omba, sihi. 2 kata rufaa. 3 vutia, pendeza n
1 (for mercy) ombi. 2 (petition) maombi, rufaa allow an ~ kubali
rufaa. 3 mvuto, tamanisho. ~ing adj 1 -a kusihi. 2 -a kuvutia. ~ingly.
adv appellant n mkata rufaa. appellate adj -a kukata
rufaa. appellate court n mahakama ya kukata rufaa.
appear vi 1 tokea, onekana; jitokeza.
2 hudhuria, enda mbele ya (k.m. mahakama). 3 elekea, onekana he ~s
to be a hard worker anaelekea kuwa mchapakazi. ~ance n 1 kujitokeza,
kuhudhuria put in an ~ hudhuria, (agh kwa muda mfupi). 2 sura, wajihi, umbo.
3 (pl) to all ~ kadiri ionekanavyo.
appease vt tuliza; ridhisha. ~ment n
kuridhisha (hasa adui kwa kulegeza msimamo).
appellant n see appeal.
appellation n jina, cheo.
append vt ambatisha: ongeza mwishoni. ~age n
1 kiambatisho. 2 nyongeza.
appendix n 1 kiambatisho. 2 (med)
kidole tumbo, kibole. appendicitis n ugonjwa wa kidole
tumbo/kibole. appendectomy n upasuaji wa kuondoa kidole tumbo/kibole.
appertain vi (to) husu, husiana na.
~ing adj.
appetite n 1 hamu (ya chakula,
kinywaji n.k.) the cook has no ~ for food mpishi hana hamu ya
chakula. 2 tamaa, uchu. appetizer n kiamsha hamu: zoezi, kitafunio, kinywaji
(kinachoongeza hamu ya chakula). appetizing adj -a kutamanisha; a
kuchapukia.
applaud vt 1 piga makofi (kwa
apple
kushangilia). 2 unga mkono. applause n makofi; kusifu
(kwa makofi, vifijo n.k.).
apple n tufaha of the ~ eye kipenzi.
Adam's ~ kikoromeo, zoloto upset the ~cart vuruga
mipango.
appliance n chombo, kifaa household ~s vifaa
vya nyumbani k.m. pasi, jiko la umeme n.k. fire ~ kifaa cha kuzimia moto.
applique n nguo ya mapande, kipambio (juu ya kitambaa
kingine).
apply vt, vi 1 tia, tumia. 2 (of med) paka; bandika,
funga ~ a bandage funga bendeji. 3 (for) omba ~ for a job omba kazi.
4 (refer to) husika na, nenea, fanyia bidii, zamia (k.m. kimawazo). applicable adj
-a kutumika, -faayo, -husikayo. applicant n mwombaji. application n
1 kutumia; kutumika. 2 mpako; mbandiko. 3 ombi, maombi application form fomu ya
maombi. 4 (use) matumizi. 5 (hardwork) bidii. applied adj -a
matumizi.
appoint vt 1 ajiri; teua ~ a minister
teua waziri. 2 panga (saa, siku au mahali pa kukutana). 3 (formal)
amuru, agiza. ~ee n mteule, mteuliwa. ~ed adj 1 -liopangwa, -a
miadi. 2 -lioteuliwa, -lioajiriwa. 3 (of room) -enye vyombo,- enye samani. ~ment
n 1 miadi: ahadi ya kuonana. 2 uteuzi, kuteua. 3 cheo cha kazi, wadhifa. 4 samani
(fanicha).
apportion vt gawa, gawanya, kasimu,
~ment n.
apposite adj mwafaka, -a kufaa kabisa. ~ly adv.
apposition n (gram) mrejeosawa appositive n
(gram) kijalizo.
appraise vt tathmini, kadiria thamani; panga bei. ~r n
mthamini. appraisal n tathmini.
appreciable adj -a kuonekana, -a kutambulikana; -a kupimika.
appreciably adv kwa kiasi kikubwa. appreciate vt, vi 1 (understand)
fahamu, tambua vyema. 2 (enjoy) furahia, pendezewa na. 3 (estimate
appropriate
highly) thamini sana. 4 (thank) shukuru he appreciated
his help alimshukuru kwa msaada wake. 5 (of land, property etc) ongezeka
thamani. appreciation n tathmini write an appreciation of this
poem andika tathmini ya shairi hili. 2 kuthamini. 3 shukrani. 4 ongezeko la thamani. appreciative
adj -a kuonyesha shukrani; -a kuelewa; -a kufurahia.
apprehend vt (leg) 1 kamata (mwizi
n.k.), shika, tia mbaroni. 2 (arch) (understand) fahamu,
elewa, tambua. 3 (formal) (fear) hofia. apprehensible adj -a
kukamatika. apprehensive adj -enye hofu, -enye wasiwasi. apprehension
n 1 welewa. 2 hofu, wasiwasi. 3 ukamataji.
apprentice n mwanagenzi: mwanafunzi wa ufundi (k.m.
useremala, uashi n.k.). ~ship n 1 uanagenzi. 2 muda wa kujifunza.
apprise vt (formal) arifu, pasha habari be ~d
of arifiwa juu ya.
approach vt, vi (come nearer) 1 karibia, sogea,
sogelea, jongelea. 2 (go to) endea ~ one's employer for higher pay endea
mwajiri na kuomba nyongeza ya mshahara. n 1 kukaribia. 2 njia, mlango wa kufikia. 3
kuongea (na mtu kwa mara ya kwanza). 4 mtazamo. ~able adj 1 -kunjufu, -a
kuingilika. 2 -a kufikia.
approbate vt (formal) kubali, idhinisha. approbation
n 1 kukubali; idhini, kibali sifa. approbatory adj -a kusifu.
appropriate1 adj -a kufaa. ~ness n.
~ly adv.
appropriate2 vt 1 jitwalia, iba. 2 (set apart)
tenga; tengea, weka upande (kwa kazi muhimu). appropriation n 1 kutenga wrongful
appropriation matumizi songo, kitengo songo appropriation bill muswada wa
matumizi ya fedha. 2 fungu (la fedha n.k.). 3 (tendo la) kujitwalia, wizi.
approve
approve vt, vi 1 sifu, penda. 2 (sanction) afiki,
kubali, thibitisha, idhinisha ~ the minutes of the meeting thibitisha
kumbukumbu za mkutano. approving adj. approvingly adv. approval
n kibali, idhini; kukubali.
approximate vt, vi 1 karibia. 2 leta
karibu na (k.m. bei) adj ~ (to) -a kukaribia, karibu sana. approximation
n kisio, kadirio. approximately adv takriban, karibu sawa na.
appurtenance n (usu pl) (leg) kiambato,
kifuasi, kiongezo. appurtenant adj -a kuambata, -a kuhusu.
April n Aprili: mwezi wa nne adj -a Aprili.
a priori adj, adv kisamkasa (kupata matokeo kutokana
na sababu).
apron n 1 kimori, aproni: nguo maalum inayovaliwa hasa
wakati wa shughuli za uchafu tied to mother's/ wife's ~ strings
anayetawaliwa na mama yake/mkewe. 2 sehemu iliyosakafiwa kwenye uwanja wa ndege kwa ajili
ya kupakia, kupakua na kugeuzia ndege. 3 ~ stage n jukwaa chomozi: sehemu ya
jukwaa kwenye thieta inayochomoza kuelekea watazamaji.
apropos adv, adj -a kufaa his points were very ~
hoja zake zilifaa sana. 2 ~ of prep kuhusu.
apse n sehemu ya kanisa yenye umbo la mviringo.
apt adj 1 -a kufaa an ~ word neno la
kufaa. 2 -epesi (kwa kujifunza n.k.), hodari. 3 -a kuelekea, -epesi wa he
is ~ to forget ni mwepesi wa kusahau. ~ ness n. ~ly adv.
aptitude n 1 (for) kipaji ~ test mtihani wa
kupima vipaji.
aqualung n kipafumaji: chombo cha
kupumulia kinachotumiwa na wapiga mbizi.
aquamarine n 1 zumaridi: kito cha thamani chenye rangi ya
kijani iliyopauka. 2 rangi ya kijani
arbor; arbour
iliyopauka.
aquanaut n mzamiaji, mpigambizi
(anayeishi na kufanya kazi chini ya maji kwa muda).
aquaplane n ubaomaji: ubao maalum unaotumiwa katika mchezo
wa kuvutwa na boti. vi 1 fanya mchezo huu. 2 teleza (kama gari juu ya barabara
iliyojaa maji).
aquarium n tangisamaki, hodhisamaki: tangi la maji la
kuwekea na kuonyeshea samaki na mimea ya bahari.
Aquarius n Ndoo: alama ya kumi na moja ya buruji.
aquatic adj -a majini, -a kuishi majini ~ sports
michezo ya majini.
aquatint n 1 uchoraji kwenye shaba. 2 picha ya aina hii.
aqueduct n mfereji wa maji (agh.
hujengwa na mawe juu ya ardhi).
aqueous adj -a maji, -a majimaji.
aquiline adj -a tai, -enye kufanana na tai ~ nose pua
kali (iliyopindika kama ile ya tai).
Arab n Mwarabu adj -a Kiarabu; -a Uarabu, Arabuni. ~ian
adj -a Kiarabu the ~ Nights Alfu lela ulela. ~ic adj -a
Kiarabu n Kiarabu. ~ist n mwanafunzi au mtaalam wa mambo ya Waarabu.
arabesque n 1 (art) mchoro maalum
(wenye nakshi nyingi). 2 miondoko maalum (ya aina ya mchezo wa bale).
arable adj -nayolimika ~ land ardhi
inayolimika.
arachnid n araknida: jamii ya anthropoda inayojumuisha
nge, buibui, chawa, kupe, n.k.
arbiter n see arbitrator.
arbitrary adj 1 holela, -sio na mantiki, -sio na misingi
maalum. 2 (despotic) -a kidikteta, -dhalimu.
arbitrate vt, vi 1 toa uamuzi.
2 patanisha, suluhisha. arbitration n maamuzi;
usuluhishi. arbitrator n also arbiter msuluhishi, mpatanishi.
arbor; arbour n mahali penye kivuli cha miti (katika
bustani). ~eal adj
arc
-a miti, -a mtini. ~eous adj 1 penye miti mizima 2 -a
mitini ~animals wanyama wa mitini. ~escent adj -kama mti, -enye
matawi. ~tum n mahali penye mkusanyo wa miti kwa ajili ya maonyesho na
mafunzo. ~culture n ukulima wa miti.
arc n tao: sehemu ya duara au pindo ~ welding
kulehemu kwa umeme. vi fanya tao.
arcade n njia tao (njia yenye paa la
tao). ~d adj.
Arcadia n Arkadia: eneo mashambani ambapo watu wanaishi raha
mustarehe. ~ n adj, n.
arcane adj -a kunga.
arch1 n 1 tao; jengo la tao (lenye njia juu yake)
a bridge with three ~ es daraja lenye matao matatu. 2 (also ~ way)
lango.
arch2 adj 1 tundu. 2 chepe. ~ly adv
kitundu; kichepe. ~ness n.
arch3 (pref) -kuu; see archangel
n.k. archaeology n akiolojia, elimukale. archeologist n
mwanaakiolojia. archaeological adj.
archaic adj -a zamani, -a kale,
-siotumika sasa. archaism n kikale: neno au msemo wa kale
(usiotumika sasa).
archangel n (rel) malaika mkuu.
archbishop n (rel) askofu mkuu. ~ric
n cheo (cha askofu mkuu); jimbo (la askofu mkuu).
archdeacon n (rel) kasisi mkuu.
archdiocese n jimbo la askofu mkuu. arch-enemy n
1 adui mkuu. 2 (rel) Shetani.
archer n mpiga mishale. ~y n upigaji mishale,
ufundi/mchezo wa kupiga mishale.
archetype n chapaasili, umboasili, kielelezoasili.
archipelago n funguvisiwa:
mkusanyiko wa visiwa vingi pamoja au bahari yenye mkusanyiko huu.
architect n 1 msanifu majengo. 2 muasisi (wa mipango maalum)
the ~ of our victory muasisi wa ushindi wetu. ~ure n usanifu majengo.
arid
~ural adj.
archives n 1 nyaraka. 2 hifadhi za nyaraka. archivist
n mhifadhi nyaraka.
archway n see arch.
arctic 1 adj -a akitiki, -a kaskazini ya
dunia. 2 baridi sana.
ardent adj motomoto, -a shauku.
ardency n.
ardour n shauku, hamasa.
arduous adj 1 (of work) -a sulubu,
ihitajiyo nguvu, gumu. 2 (of road) -enye mwinuko mkali. ~ly
adv.
are v see be.
area n 1 eneo, kipimo cha eneo. 2 sehemu ya dunia. 3 (subject)
mawanda (ya shughuli za kitaalam).
areca n 1 (tree) mpopoo. 2 (fruit) popoo.
arena n uwanja (wa michezo, maonyesho n.k.) ~ of war
medani.
aren't = are not, see be.
arete n ukingo mkali wa mlima.
argent adj -a rangi ya fedha.
argon n agoni: gesi iliyomo hewani, hutumika kwenye baadhi
ya taa za umeme.
argot n msimo wa kikundi maalum.
argue vi, vt 1 toa hoja/sababu/maneno
ya kuthibitisha au kukanusha. 2 shindana kwa maneno, hojiana, bishana,
gombana. ~ somebody into/out of something shawishi mtu afanye/asifanye jambo. 3
jadili. argument n 1 hoja. 2 mabishano, mashindano, majadiliano. 3 muhtasari
wa habari zilizo katika kitabu. argumentative adj -bishi. arguable adj
1 -a kujadilika. 2 -wezayo kujengewa hoja/ushahidi. argumentation n
kubishana, kutoa hoja, kuhojiana.
Argus n zimwi lenye macho mia moja. ~ eyed adj
-enye kutazama sana, -angalifu, makini.
argy-bargy (colloq) n mabishano.
aria n wimbo wa sauti moja katika opera.
arid adj -kavu sana, yabisi, kame; (fig)
-siovutia. ~ity n ukame. ~ness n
Aries
hali ya ukame.
Aries n Kondoo (alama ya kwanza ya buruji).
aright adv (arch) sawasawa, barabara.
sahihi, kwa jinsi iliyopasa.
arise vi 1 tokea, tukia; (arch) inuka. aristocracy
n 1 tabaka/utawala wa
makabaila. 2 waungwana. 3 (fig) walio bora katika shughuli
fulani. aristocrat n mtoto wa watu, mtu wa ukoo bora. aristocratic adj
-a kikabaila, -a jamii ya watu wakuu aristocratically adv.
Aristotelean adj -a Aristotle.
arithmetic n sayansi ya namba.
~al adj.
ark n 1 safina: chombo kikubwa alichounda Mtume Nuhu kabla
ya gharika Noah's ~ safina ya Nuhu. 2 sanduku kubwa, (rel) the A~ of the
Covenant Sanduku la Agano.
arm1 n 1 mkono. an infant in ~s
mtoto mchanga. keep somebody at ~'s length epukana na, epuka urafiki au
kuzoeana na. with open ~s kwa mikono miwili. 2 chochote kitokacho kama mkono k.m ~
of the sea mkono wa bahari, ghuba. 3 tawi kubwa (la mti). 4 sehemu ya vazi inayofunika
mkono. 5 ~chair n kiti cha mikono adj (fig) -a kinadharia ~
chair critic n mhakiki wa kinadharia. 6 ~pit kwapa. 7 the (long) ~ of
the law mamlaka ya sheria. 8 ~ hole n mkono wa vazi. 9 ~let n
1 kikuku. 2 kitambaa kinachovaliwa mkononi juu karibu na bega (hasa wakati wa msiba au
kuonyesha cheo).
arm2 n 1 (usu pl) silaha, zana za vita. in
~s -enye silaha. lay down ~s salimu amri. take up ~s
jiandaa- kupigana. 2 up in ~s (about) pinga n sana na kuwa tayari
kupigana. 3 ~s ngao ya heshima. 4 coat of ~s n nembo. 5 tawi
la jeshi, k.m. the air ~ jeshi la anga. ~orial adj -a nembo, -a
shajara ~ orial bearings n nembo; shajara. ~ada n armada: kundi kubwa
la manowari. ~ment n (usu pl) 1 zana za vita (hasa mizinga
around
ya manowari). 2 jeshi lenye silaha. 3 matayarisho ya vita. ~s-race
n mashindano ya silaha. ~our (U.S. ~or) n 1 vazi la kujihami
wakati wa mapigano. 2 ngao chombo: bamba la metali liwekwalo kwenye chombo ili kukihami
kisitobolewe na risasi au mizinga ya adui. 3 vyombo vya kivita (magari, vifaru, manowari,
n.k.) vilivyowekewa mabamba ya chuma adj -enye vazi la kivita la chuma, -enye
dereya. ~our plate n dereya, bamba la chuma. ~ourer n
mtengeneza silaha; mtunzaji silaha za jeshi. ~oury n 1 ghala ya silaha. 2 (US)
kiwanda cha silaha. ~y n 1 jeshi. 2 jumuiya ya watu wenye madhumuni maalum. The
Salvation ~y Jeshi la Wokovu. 3 kundi kubwa an ~y of helpers kundi la wasaidizi
an ~y of red ants kundi la siafu.
arm3 vi, vt pa silaha, pa kitu cha
kulinda, tega bomu ~ with answers to likely questions
tayarisha majibu ya maswali yanayoelekea kuulizwa. ~ed adj -enye silaha ~ed
robbery unyang'anyi wa kutumia silaha ~ed forces majeshi.
armadillo n armadilo: mnyama kama
kakakuona
Armageddon n amagedoni: (medani ya) vita; vita vya mwisho
kati ya wema na waovu; (fig) mapambano makali ya vita.
armature n 1 deraya. 2 (in motor
cars) amecha: misuko ya waya katika jenereta au mota ya umeme
ambayo huzunguka katika uga sumaku.
armistice n. mapatano ya kusimamisha vita kwa muda.
armoire n (Fr) kabati kubwa (aghalabu la nguo).
aroma n 1 harufu nzuri. 2 (fig) hali
au mazingira fulani maalum. ~tic adj -enye kunukia
vizuri, -enye kukolea viungo.
arose v see arise.
around adv 1 pande zote (za) kuzunguka, kandokando, pote,
kila
arouse
mahali I have been ~ nimeona mengi. 2 mnamo ~ two o'clock
mnamo saa nane. 3 karibu.
arouse vt 1 amsha, shitua. 2 tia nguvu, tia ashiki, tia
shonga.
arraign vt 1 shtaki. 2 laumu, kosoa.
~ment n.
arrange vt, vi 1 (put in order) panga,weka kwa
utaratibu, safidi. 2 (organize) panga (kwa baadaye) ~ a date for a
meeting panga tarehe ya mkutano. 3 tayarisha ~ a meeting tayarisha mkutano. 4 (with/for)
afikiana, kubaliana. 5 suluhisha, patanisha. ~ment n 1 mpango, utaratibu. 2 (pl)
~ments n matayarisho, mipango I made ~ments to send books
nilifanya mipango ya kupeleka vitabu. 3 (music) see adaptation.
arrant adj (always of something or somebody bad)
(derog) -a hali ya juu, -a kupindukia an ~ thief mwizi wa kupindukia, mwizi
mkubwa/ aliyekubuhu.
arras n (arch) mkeka wa kiwambazani, (namna ya) zulia
la kupamba ukutani, kihangaisho.
array vt 1 panga askari tayari kwa
vita. 2 valia ~ed in professorial attire amevalia
kiprofesa. n 1 upangaji wa askari kwa ajili ya vita. 2 vazi in ceremonial ~
katika vazi la sherehe.
arrears n 1 karisaji. 2 kiporo: kazi
iliyopaswa kuwa imefanywa lakini haijafanywa.
arrest vt 1 (stop) simamisha, zuia.
2 (seize) kamata, bamba, shika, tia mbaroni. 3 (catch
attention) vuta nadhari. n 1 kukamata resist an ~ goma kukamatwa under
~ chini ya ulinzi. 2 (stoppage) kizuizi cardiac ~ shituko la moyo. ~ing
adj -a kuvuta.
arriere pensee n (Fr) nia ya undani
katika fikra.
arrive vi 1 fika, wasili. 2 ~ at fika
mahali; fikia ~ at a conclusion fikia tamati/hitimisho. 3
tokea, fanyika.
arteriosclerosis
arrival n 1 ufikaji; majilio; mjo, ujaji. 2 (pl)
wanaowasili.
arrogance n kiburi; majisifu; ufidhuli.
arrongant adj -enye kujisifu/ kujigamba, -enye kupenda
makuu; fidhuli; -enye kiburi. arrogantly adv.
arrogate vi, vt 1 jitwalia bila haki,
jipatia (hasa kwa ujeuri), jitwaza, jipachika. 2 (fig) twaza,
ambika, pachika.
arrow n 1 mshale. 2 alama ya mshale. ~ head n
chembe.
arrowroot n aina ya chakula chenye wanga kinachotokana na
mimea.
arse n (sl) mkundu, matako. silly ~/ ~hole n
pumbavu ~ around/ about poteza muda.
arsenal n 1 ghala, silaha. 2 kiwanda
cha zana za vita. 3 (fig) hifadhi ya nguvu.
arsenic n aseniki: kemikali (ngumu)
ya sumu yenye maumbile mengi white ~ aseniki nyeupe (namna moja
ya sumu inayotumika pamoja na kemikali nyingine) adj -a kiaseniki.
arson (leg) uchomaji wa mali kwa makusudi commit ~
choma kwa makusudi.
art n 1 sanaa. Theatre A~s n Sanaa za
Maonyesho. 2 ustadi/ufundi (k.m. wa kupiga muziki, kupiga picha, kuchora sanamu n.k.). 3 (pl)
~ s n fani. fine ~s n sanaa, faculty of ~s
kitivo cha fani ~ exhibition maonyesho ya sanaa ~ school chuo cha sanaa work
of ~ kazi ya sanaa. 4 (cunning) werevu, ujanja. 5 ~ist n msanii. ~iste
n msaniitendi, mwanasanaa. ~istic adj -a sanaa, -stadi, -sanii,
-zuri. ~istically adv. ~istry n ustadi, urembo, usanii.
artefact n see artifact.
arterial adj 1 -a kiateri, -enye kufanana na ateri. 2 (fig)
(of road) barabara kuu.
arteriosclerosis n (med) mkakamo ateri: hali ya mkauko wa
vikole vya damu.
artery
artery n 1 ateri: mshipa mkubwa
upelekao damu toka moyoni mpaka kila sehemu ya mwili. 2 (road)
njia kuu, barabara kuu. arteriole n kiateri, tawi la ateri.
artesian well n kisima cha chemchem. artful adj
janja, erevu/-enye ustadi,
-enye hila. ~ness n ujanja, udanganyifu, hila. ~ly
adv.
arthritis n ugonjwa wa baridi yabisi. artichoke n
(bot) ua la rubaruti,
rubaruti.
article n 1 makala. 2 (leg) ibara,
kifungu. 3 kikorokoro household ~s vikorokoro vya
nyumbani. 4 kibainishi.
articulate vt 1 eleza kwa ufasaha. 2
fungamana viungo. 3 tamka adj semi, -enye kueleweka. ~ness
n ufasaha. articulation n 1 hali ya kujieleza kwa ufasaha. 2 (bio)
kiungo (cha goti n.k.), uungaji. articulator n kitamka.
artifact n kitu kilichobuniwa,
chombo/silaha (aghalabu ya kale), ughushi.
artifice n 1 ustadi. 2 hila, ulaghai, ujanja. ~r n
msani.
artificial adj 1. bandia 2. -a kinafiki. ~ respiration n
uvutishaji hewa, upumuaji bandia. ~ insemination n uhimilishaji kibandia:
utiaji shahawa za tovi (dume lililochaguliwa) kwenye uterasi ya mnyama ili atunge mimba. ~fertilizer
n mbolea ya chumvi chumvi. ~lly adv kwa kughushi. ~ity n
ubandia, tabia ya kughushi.
artillery n 1 mizinga mikubwa. 2 jeshi lenye kutumia mizinga
ya namna hii. ~ wagon n gari la kukokotea mizinga.
artisan n msanii, fundi mchundo.
artless adj -sio hila. ~ly adv.
~ness n.
arty adj -a kujifanya/kujidai kuwa mpenda sanaa.
as adv, conj 1 (in that degree, in like
manner) hivyo hivyo do ~ I do fanya hivyo hivyo such ~
kama such things ~ chairs vitu kama viti he did the same ~ so and so
alifanya
ash
kama alivyofanya fulani. 2 (since, because) kwa sababu, kwa
maana, kwa kuwa. 3 (when, while) wakati, pale, -po-, -poki- ~ he was going (when
he was going) alipokuwa akienda. 4 ~ for instance kwa mfano. 5 so ~ to
ili he ran so ~ to overtake him alipiga mbio ili kumpita. 6 as...as
almradi, madhali, kwa wakati wote ~ long ~ you are here let's
finish the work almradi uko hapa njoo tumalize kazi ~ far ~ (ever)
I can kwa kadiri niwezavyo this ~ well ~ that hiki na kile pia, hiki
pamoja na kile men ~ well ~ women wanaume kwa wanawake. ~ to; ~ for kwa
mintarafu ya. ~ yet hadi sasa. ~ from kuanzia. ~ if/though
kana kwamba. same ~sawa na.
asafoetida n mvuje.
asbestos n asbesto.
asbestosis n uasbesto: ugonjwa uletwao na asbesto.
ascar n (pl) (bio) minyoo mviringo,askari.
ascend vt, vi panda, paa ~ the thronekuwa mfalme. ~ancy/~ency
n mamlaka. ~ant/~ent adj. ascent. upaaji, upandaji the
~ of mountain upandaji mlima.
ascension n 1 see ascent. 2 mpao, kupaa. 3 The
A ~ sikukuu ya kupaa Yesu Kristo mbinguni.
ascertain vt hakikisha, yakinisha. ~able adj.
~ment n.
ascetic n mtu anayejinyima raha na anasa adj -a
kujinyima anasa za mwili. ~ally adv. ~ ism n.
ascorbic adj -enye vitamini c. ~ acid n
asidi askobiki, vitamini c.
ascribe vt 1 dhani kuwa sababu ya he ~d his failure to
bad luck alidhani alishindwa kwa bahati mbaya. 2 -pa, patia, pachika. ascription
n.
asdic n kipeleleza nyambizi.
aseptic adj -sio na bakteria. asepsis n.
asexual adj 1 -siojinsi. 2 -sio na nyege. ~ity n.
ash1 n (bot) mjivujivu (aina ya mti).
ash
ash2 n jivu; (fig) reduce to ~s
teketeza. ~y adj (fig) -eupe kwa uso. ~-bin/~-can n
pipa la taka adj (bot) -a mjivujivu; -a (rangi ya) majivu, kijivu. ~-pit
n shimo la kufukia majivu. ~-tray n kisahani cha majivu. A~
-Wednesday n (rel) Jumatano ya Majivu, siku ya kwanza ya Kwaresima.
ashamed adj -enye kuona haya,
-enye kutahayari be ~ of somebody/ something aibishwa na, onea
haya I am ~ of you unaniaibisha.
ashlar n jiwe la pembe mraba (lililochongwa).
ashore adv pwani, ufukweni go ~ shuka pwani.
Asia n Asia. n adj Mwasia. ~tic n
adj.
aside adv 1 upande, kando, pembeni. 2 (in private)
faraghani, kwa siri set ~ (judgement) futa, tangua hukumu. n 1 maneno ya
pembeni an ~ maneno (hasa katika tamthiliya) ambayo waigizaji wengine hawapaswi
kuyasikia. 2 (of speech) mchepuko: maneno yanayoingizwa katika hotuba ambayo yako
nje ya hotuba.
asinine adj 1 -a punda, -a kama
punda. 2 (fig) -pumbavu sana.
ask vt, vi 1 (question) uliza hoji. ~ after
ulizia hali ~ the way/the time uliza njia/saa. ~ for tafuta don't ~ for
trouble usitafute balaa. 2 (request) taka, omba, sihi. 3 (invite) alika,
karibisha. ~ing n it's yours for the ~ing ukiomba utapewa.
askance adv (only in) look ~ at a
person tazama (mtu) kichongochongo, tazama kwa shaka/kwa wasiwasi.
askew adv mshazari, upande her
nose was ~ pua yake ilikuwa ya mshazari.
aslant adv, prep. upande, mshazari.
asleep adv, pref, adj usingizini (be) ~
lala sound/fast ~ lala fofofo. 2 (of joints of the body)
-fa ganzi.
aslope adj -a (kwa) kuinama.
ASP abbr. of Afro-Shirazi Party
assail
(Muungano wa chama cha Waafrika na Washirazi).
asp n (bot) nyoka sumu(wa Misri na
Libya).
asparagus n (bot) asparaga: aina ya
boga.
aspect n 1 (of people or things)
sura. 2 kipengele. 3 (of house, thing etc) mwelekeo a
house with a southern ~ nyumba inayoelekea kusini. 4 (gram) hali. ~ual
adj.
asperity n ukali, hamaki, harara. (pl)
asperities n makali (k.m. maneno, hali ya hewa, ya
maisha).
asperse vt kashifu, singizia, zulia jambo, sengenya;
shutumu. aspersion n 1 kitendo cha kumkashifu mtu (only in) cast ~
kashifu. 2 unyunyiziaji maji ya baraka.
asphalt n lami vt tandaza lami.
asphodel n (bot) asfodeli: aina ya myungiyungi.
asphyxia n hali ya kukosa hewa ya
kutosha. asphyxiate vt kaba, nyima pumzi. ~tion n.
aspic n nyamaute.
aspiration n 1 (gram) mpumuo. 2 hamu ya kupata
(kitu bora n.k.). aspire vi gombea, tamani, weka lengo la kupata kitu
fulani. aspirant n mgombea, mtamani.
aspirator n (tech) aspireta:
kisharabu.
aspirin n aspirini.
ass1 n 1 punda/kihongwe. 2 (fig)
mjinga, baradhuli don't make such an ~ of yourself usiwe mjinga kiasi hicho a
perfect ~ mpumbavu mkubwa.
ass2 n see arse.
assagai n see assegai.
assail vt 1 (~ somebody/something with)
shambulia vibaya, chokoza, sumbua ~ somebody with questions shambulia kwa maswali ~ed
with the worries sumbuliwa na mawazo. 2 (fig) he ~ed the
question with vigour alilikabili swali kwa uthabiti. ~able adj -a
kushambulika. ~ant n
assasin
mshambuliaji.
assasin n mwuaji. ~ation n mauaji ya namna
hiyo. ~ate vt ua (aghalabu kwa kukodiwa na kwa sababu za kisiasa au dini).
assault n 1 uvamizi, shambulio (lolote la maombi, n.k.). 2 ~
(on, upon) shambulio la ghafula (k.m. katika vita), uvamiaji; (leg) ~ and
battery mashambulio ya nguvu, mapigo. vt 1 vamia. 2 najisi.
assay vt 1 pima ubora wa metali
(uliomo katika mawe yenye madini). 2 changanua kiasi cha dutu n.k. n
(chem) uchanganuzi wa kiasi cha dutu (iliyomo katika mawe ya madini).
assegai n sagai, mkuki (wa Wazulu).
assemble vt 1 kusanya, leta pamoja. 2 (mech.) unga
pamoja sehemu za mashine vi kusanyika, kutana pamoja. assemblage n 1
(of people/things) mkusanyiko, kongamano; (art) kitu kilichoungwaungwa k.m.
mashine. 2 kuweka pamoja, kuunganisha. assembly n 1 kusanyiko, mkutano. 2
baraza National assembly Bunge. 3 uunganishaji pamoja wa sehemu za (mashine
n.k.) assembly shop/plant karakana ya kuunganishia assembly hall bwalo,
ukumbi wa mkutano assembly line mashine na/au watu wanaofanya kazi hatua kwa hatua
katika kuunda au kutengeneza kitu. 4 (mil) kuita askari (kwa ngoma au tarumbeta).
assent vi (to) kubali, idhinisha. n
idhini, kibali, ikibali, ruhusa by common ~ kila mtu akikubali
with one ~ kwa kauli moja.
assert vt 1 dai, tetea (haki) kwa
dhati. 2 tangaza, sema. ~ oneself onyesha madaraka, jionyesha
haki. ~ive adj. ~vely adv. ~ion n utetezi wa
haki; dai thabiti mere ~ion maneno matupu ~ion of his rights dai la haki
yake.
assess vt 1 kadiria, panga kiasi (cha kodi, faini n.k.). ~ing
officer mkadiriaji. ~able adj 1 ~ment n ukadiriaji,
makadirio. ~or n 1
associate
mkadiriaji. 2 (leg) mzee wa baraza.
asset n 1 (usu pl) ~s raslimali, mali.
2 sifa au kitu chenye manufaa (k.m. ujuzi, elimu, kipaji, n.k.).
asseverate vt (formal) nena kwa uthabiti. asseveration
n
assiduity n 1 uangalifu katika
utendaji. assiduous adj -angalifu. assiduously adv.
assign vt 1 toa, -pa, gawia (vitu, kazi) ~ the task to
Ali mpe kazi Ali. 2 teua, taja ~the professor to the presidency teua profesa
kwa uraisi. 3 weka/panga (tarehe, siku ya kufanyika jambo). 4 (leg) hawilisha. ~able
adj. ~ment n 1 utoaji. 2 uteuzi. 3 upangaji. 4 uhawilishaji. ~ation
n ahadi ya kukutana (aghalabu wapenzi), kuonana, miadi.
assimilate vt, vi 1 lishiza (chakula)
baada ya mmeng'enyo food that ~s easily chakula kinacholishizwa
kwa urahisi. 2 -wa/fanya mwenyeji; staarabika/staarabisha. 3 similisha. 4 chukua, pata
(maarifa, fikra n.k). assimilation n 1 mlishizo. 2 usimilishaji: sera ya
Wareno na Wafaransa ya kuwageuza wenyeji wafanane kama wao. assimilative adj.
assist vt, vi saidia, auni. ~ance n
msaada/muawana. ~ant n msaidizi.
assize n kesi inayoongozwa na jaji
na wazee wa baraza.
associate vt husisha, shirikisha, unganisha (watu au
mambo katika fikira) ~ Egypt with the Nile husisha Misri na mto wa Nile. vi
shirikiana na, ongea na, fanya urafiki na a person to ~ with mtu wa kushirikiana
naye. n mshiriki, mwenzi, rafiki adj -lioshiriki, shiriki ~judge jaji
mshiriki. association n 1 ushirikiano, mwungano ~ of ideas mwungano
wa mawazo. 2 (society) ushirika, jumuiya, shirikisho, chama articles of ~
kanuni ya kampuni form an ~ unda chama. 3 (meaning) maana, ukumbusho it
has many old ~s for us inatukumbusha mambo
assonance
mengi yaliyopita. associative adj.
assonance n (ling & lit) mshabaha wa irabu za
shadda katika maneno mawili au zaidi. assonant adj.
assort vt gawanya, panga namna
mbalimbali vi patana, afiki, chukuana na ~well with something
patana/chukuana vyema na. ~ed adj 1 anuwai, -a namna mbalimbali. 2
-liochanganyika, -liopangwa vizuri, -enye kupatana. ~ment n mkusanyiko wa
vitu anuwai.
assuage vt tuliza, punguza, poza
(maumivu, hamu) ~ thirst tuliza kiu. assuasive adj
-a kupoza.
assume vt 1 sadiki, ona (bila ushahidi/uthibitisho),
(ji)chukulia. 2 twaa, chukua ~office twaa ofisi. 3 jifanya. assumption n
1 wazo, dhana, neno lisilohakikishwa on the ~that kwa kuamini kuwa 2
utwaaji. 3 (rel) The ~ of Our Lady Kupazwa kwa Bikira Maria Mbinguni.
assurance n 1 (confidence) imani, moyo wa kujiamini.
2 ahadi, uhakika. 3 (rare) majivuno/ufidhuli. 4 (guarantee) bima/dhamana life
~ bima ya maisha. 5 yakini, uhakikisho. assure vt 1 ahidi. 2 thibitisha
hakikisha. 3 aminisha. 4 dhamini, wekea bima. rest assured (that)
ondoa wasiwasi, poa, amini kuwa. assuredly adv kwa yakini, kwa hakika.
asterisk n. kinyota*: alama ya nyota
ambayo hutumika kuashiria jambo katika maandishi.
astern adv 1 (naut) shetrini. 2 (kwa) nyuma fall ~
(of) baki nyuma.
asteroid n asteroidi: gimba dogo, sayari ndogo.
asthma n pumu. ~tic adj -enye pumu.
astigmatism n (med) 1 uastigmati:
dosari katika jicho/lenzi inayozuia fokasi sahihi. astigmatic adj.
astir adj, 1 -enye kusisimkwa,
-a kufuruka. 2 (dated) -a macho, -lio amka adv kwa
msisimko, kwa kufuruka.
astonish vt staajabisha, shangaza.
asymmetry
~ed adj -lioduwaa, -lioshangazwa. ~ing adj.
~ingly adv. ~ment n mastaajabu, mshangao, mduwao.
astound vt shangaza, staajabisha, tia
bumbuazi; shtusha. ~ing adj.
astraddle adv, adj see astride
astral adj -a nyota, -a kutoka kwenye nyota.
astray adv nje ya go ~ potea, wa nje ya mstari;
potoka lead ~ potosha, poteza.
astride adv kwa kutagaa, kwa kumagamaga, kimagamaga.
astringent n kunyasi: kitu kinachosababisha tishu laini
kujikunyata na kubana mishipa ya damu adj 1 -a kunyasi. 2 (fig) kali ~
remarks maneno makali.
astro (pref) -a nyota,-a anga la juu.
astrodome n dirisha dogo (juu ya
ndege linalotumiwa na rubani).
astrolabe n astrolabu: chombo kilichotumiwa zamani
kupimia urefu wa jua, nyota n.k.
astrology n unajimu. astrological adj. astrologer
n mnajimu.
astronaut n mwanaanga.
astronomy n falaki. astronomer n
majusi, mwanafalaki. astronomical adj -a kifalaki/elimu
ya sayari; (fig) -ingi mno.
astrophysics n astrofizikia: sayansi
ya hali ya nyota kikemikali na kimaumbile.
astute adj 1 -erevu, -epesi wa kung'amua. 2 -janja. ~ly
adv. ~ness n.
asunder adv 1 (of two or more things) mbalimbali
they were split ~ walitenganishwa mbalimbali. 2 vipande vipande come ~ vunjika
vipande vipande tear ~ chana vipande vipande.
asylum n 1 kimbilio; mahali pa amani na usalama political
~ kimbilio la hifadhi ya kisiasa. 2 (old use) hospitali watunzwapo wenda
wazimu.
asymmetry n isopacha. asymmetrical adj kwa
namna isopacha.
at prep 1 (indicating place) -ni, kwa ~ home
nyumbani ~ someone's kwa fulani. at-home n tafrija inayofanyika nyumbani kwa
wakati uliopangwa. 2 (indicating direction or goal) aim ~ lenga throw ~ rushia.
3 (indicating action) ~work kazini the children are ~ play watoto wanacheza she
is good ~ athletics yeye ni hodari katika riadha. 4 (indicating time) ~ once
mara moja ~ five saa kumi na moja ~ first mwanzoni ~ last hatimaye,
mwishoni. 5 (value) bei ~ two shillings a kilo shilingi mbili kwa
kilo ~ a loss kwa hasara. 6 ~ war vitani ~ rest mapumzikoni ~
length kwa kirefu; (Idiom) not ~ all sivyo kabisa; si kitu ~ any rate
kwa vyovyote.
atavism n uibukaji wa tabia, sura, umbo n.k. la zamani au
ambalo halikutokea kwa vizazi vingi. atavistic adj.
ate v see eat.
atelier n. (Fr) 1 studio. 2 karakana.
atheism n ukanaji Mungu: imani
kwamba hakuna Mungu. atheist n mkanamungu. atheistic
adj -a kukana Mungu.
athirst adj (for) -enye kiu, -enye
shauku ya/-enye uchu wa.
athlete n. mwanariadha. athletic adj 1 -a
riadha. 2 aliyekakawana, shupavu wa mwili; -a miraba minne. athletics n
riadha.
athwart adv (naut) kwa kukingama.
atilt adj -a upande, -liokaa upande run or ride ~
shambulia kwa farasi na mkuki with one's hat ~ akiwa na kofia upande.
Atlantic adj -a Atlantiki ~ Ocean Bahari ya
Atlantiki.
atlas n atlasi: kitabu cha ramani.
atmosphere n 1 angahewa. 2 hewa ya mahali. 3 (surroundings)
mazingira, hali ~of peace and calm hali ya amani na utulivu. atmospheric adj
-a hewa atmospheric condition hali ya hewa, -a angahewa. atmospheric pressure
n kanieneo ya angahewa.
attach
atmospherics n mikwaruzo (ya redio).
atoll n kisiwa cha matumbawe.
atom n 1 atomu. 2 kipande kidogo
mno, chembe not an ~ hakuna hata chembe smashed to ~s
imepondwa kabisa. ~ic adj -a atomu. ~ic bomb n bomu la
atomu. ~ize vt 1 fanya kuwa chembechembe. 2 puliza manukato kwa mrashi. ~zation
n.~zer n mrashi, kirashi.
atonal adj (mus) -siofuata mfumo
maalum wa sauti. ~ity n.
atone vt (for) lipia kosa. ~ment n
the A~ment (rel) upatanisho wa Mungu na binadamu kwa maisha na
kifo cha Yesu; mateso na kifo cha Yesu.
atonic adj (phon) -sio -a toni.
atop adv ~ (of) juu ya.
atrabilious adj (rare) -a huzuni,
-a majonzi.
atrocious adj 1 -ovu, -a kikatili,
-baya mno. 2 (colloq) -baya sana. ~ness n. ~ly
adv. atrocity n 1 uovu, ukatili. 2 (pl) maovu.
atrophy n. (med) kufifia, kupungua,
kupotewa na nguvu mwilini; (fig) kuharibika kwa tabia. vt
fifisha (mwili). vi fifia, pungua, potewa na nguvu (mwilini).
attaboy interj (sl) heko!
attach vt, vi 1 fungia, shikiza. 2 (of documents etc)
ambatisha no suspicion ~es to them hawatiliwi shaka. 3 (passive)
be ~ed to someone penda mtu sana, ganda. 4 ~ oneself to jitia,
jiingiza ~ oneself to a party jiingiza katika chama. 5 (mil) ~ed to
teuliwa kuwa kwenye kikosi kingine kama mtaalam. 6 (seize) tilia maana, ona, dhani ~
much importance to tilia maanani sana. 7 (leg) shika, kamata, chukua kisheria. ~ment
n 1 uambatishaji. 2 kiambatisho, kifuasi. 3 penzi, upendo. 4 kushika mali ya
mtu kisheria. 5 an ~ment to kuteuliwa kufanya kazi fulani. ~e'
n mwambata cultural ~e n
attack
mwambata wa utamaduni. ~e -case n mkoba (wa hati
n.k).
attack vt 1 shambulia. 2 (of words)
suta. 3 (of disease) pata, shik(w)a. 4 anza. n 1
shambulio. 2 masuto. 3 kupat(w)a. 4. uanzaji. ~er n mshambuliaji.
attain vt,vi 1 (to) fikia, fika ~ to
perfection fikia ukamilifu/ upeo. 2 pata ~ power etc. pata
mamlaka n.k. ~able adj. ~ment n. 1. kupata easy/difficult
of ~ment rahisi/-gumu kupatikana. 2 (pl) ~ments elimu, ujuzi.
attainder n (leg) upotezaji wa haki za uraia na umilikaji wa
mali (kufuatia hukumu ya kifo au kuharamishwa). attaint vt (leg)
hukumiwa kukosa haki za uraia na umilikaji wa mali.
attar n halwaridi: manukato ya maua ya waridi.
attempt vt jaribu. n jaribio. an ~
on/upon somebody's life jaribio la kuua mtu. 2 ~ to do
something/at doing something jaribio la kufanya kitu. 3 an ~ at babio.
attend vt, vi 1 shughulikia, sikiliza, tumikia. 2 (on/upon)
uguza/ hudumia, lea. 3 hudhuria. 4 (formal) (accompany) fuatana/ambatana na a
method ~ed by great difficulties njia inayoambatana na shida kubwa. ~ance
n 1 kuhudumia be in ~ance on ngojea, fuatana na, hudumia. 2
mahudhurio. 3 mkusanyiko. ~ant adj 1 -a kufuatana na, -a kuambatana na. 2 -a
kungojea, -uguzi. ~ n 1 mtumishi, mhudumu library ~ant mhudumu wa maktaba. 2
(pl) msafara, wajumbe wa mtu mashuhuri Premier and his ~ants Waziri
Mkuu na msafara wake. attention n 1 uangalifu, usikivu, usikizi pay give
attention to angalia, zingatia sikiliza, fanya kwa makini. attract attention
vuta macho draw attention vuta nadhari. 2 (pl) wema. attention Mr. X
aione X. 3 (mil.) attention ! mguu sawa! come to /stand at attention
tulia, kakamaa. attentive adj (to)
attrition
sikivu, angalifu. attentively adv. attentiveness n.
attenuate vt (formal) fanya -embamba,
kondesha, dhoofisha, punguza.
attest vt, vi 1 shuhudia, thibitisha.
~ a signature rasimisha sahihi. ~ed adj mjarabu ~ed
milk maziwa mjarabu: yaliyothibitishwa kuwa hayana ugonjwa. 2 apa; apisha. 3 jiunga
na jeshi. ~ to shuhudia. ~ation n uthibitisho.
attic n darini.
attire vt vaa, vika, visha n mavazi,
nguo.
attitude n 1 (position) jinsi (namna)
ya kusimama au kukaa, mkao. 2 mtazamo, fikra, msimamo, mwelekeo a
negative ~ mtazamo hasi dhidi ya mtu fulani. attitudinize vi jifanya,
jifaragua (kwa kuchukua tabia na vitendo vya mwingine)/ sema, andika, tenda kwa namna ya
kuathiriwa.
attorney n 1 wakili, mwanasheria,
power of ~ uwakili. 2 A~-General Mwanasheria Mkuu. 3 State A
~ Wakili wa Serikali.
attract vt 1 vuta a magnet ~s iron
sumaku huvuta chuma. 2 pendeza, vutia. feel ~ed to
somebody jihisi kuvutiwa/kupendezwa na mtu fulani. ~ion n 1 mvuto. 2
kivutio ~iveness n uvutivu. ~ive adj. ~ively adv.
attribute vt ona/dhani ndiyo sababu ya, fikiria kuwa
tabia/matokeo ya I ~ his illness to the rain naona mvua ndiyo sababu ya ugonjwa
wake. n 1 tabia, sifa ya kiasili ya Mercy is an ~ of God Huruma ni sifa ya
Mungu. 2 ishara ya mtu au cheo chake. attributable adj. attribution n.
attributive adj (ling) vumishi ~ adjective kivumishi angama.
attrition n 1 msuguano. 2 kulika kwakusuguana war of ~
vita ya msuguano (ambapo kila upande unasubiri vita idhoofishe kabisa upande mwingine). 3 (Theol)
majuto.
attune
attune vt (to) oanisha, patanisha;
zoeza. ~ment n.
atypical adj -isio kawaida.
aubergine n (bot) biringani.
auburn adj (of hair) hudhurungi/ kahawia.
auction n mnada public ~ mnada wa
hadhara vt nadi put up to ~ piga mnada. ~eer n
dalali, mnadi.
audacious adj 1 jasiri, shupavu. 2 fidhuli, safihi. 3 shujaa
pite. audacity n. ~ly adv.
audible adj -a kusikika his speech
was ~ hotuba yake ilisikika. audibly adv. audibility
n.
audience n 1 hadhira have an ~ with the President
kutana na Rais (kwa mazungumzo rasmi). 2 wasikilizaji (wa pamoja na waliosambaa). 3 (of
a book) wasomaji.
audio pref/ adj -a kusikia. ~ visual aids n
vielelezo (vya kusikia na kuona).
audit n ukaguzi wa mahesabu. vt kagua mahesabu. ~ing
n ukaguzi. ~ n mkaguzi wa mahesabu.
audition n 1 uwezo wa kusikia. 2
majaribio ya sauti/uigizaji/utumiaji wa ala n.k. vt give an ~
to jaribu/pima sauti n.k. (kwa ajili ya kuajiriwa). auditor n msikizi. auditorium
n bwalo/ukumbi (wa mikutano, maonyesho n.k.). auditory adj -a
kusikia, -a kusikizia.
au fait adj (Fr) -juzi, -stadi, -zoefu.
au fond adv (Fr) kimsingi.
auger n kekee.
aught n (arch) chochote, kitu chochote for ~ I
care/know sijali chochote/sina habari.
augment vt/vi kuza, ongeza, zidisha; ongezeka. ~ation
n kuongeza, kuongezeka, ongezeko.
augur n mbashiri, mtabiri. vi, vt bashiri, tabiri ~
well/ill ashiria uzuri/ubaya wa jambo. ~y n. ubashiri; (omen)
ndege, ishara.
august adj -tukufu, adhimu.
August n Agosti: mwezi wa nane.
aunt n shangazi, mama mdogo/
author
mkubwa, mke wa mjomba au mke wa baba mdogo au mkubwa.
au pair n mtumishi wa nyumbani wa
kike (wa kutoka nchi nyingine ambaye ujira wake ni chakula,
mavazi/malazi na masomo.
aura n hali inayoashiria wema au ubaya wa mtu.
aural adj -a sikio, -a kusikika ~
surgeon daktari wa masikio. aurist n mtaalam wa
magonjwa ya masikio.
aureole; aureola n 1 (rel) duara (inayochorwa
kuzunguka vichwa vya watakatifu katika picha, kuonyesha utukufu wao/taji ya dhahabu). 2
taji takatifu. 3 duara linalozunguka mwezi.
au revoir int (Fr) kwa heri ya kuonana.
auric adj -a dhahabu.
auricle n 1 orikali: sehemu ya nje ya
sikio. 2 mojawapo ya chemba mbili za juu katika moyo.
auricular adj 1 -a kuhusiana na sikio, -liopatikana kwa
kusikika. 2 -liofahamika kwa kutolewa taarifa.
auspice n (pl) 1 mtabiri anayetumia nyendo za
ndege/ishara. 2 bahati njema. auspicious adj -heri -a bahati, -a ndege
njema. auspiciously adv. auspiciousness n msaada, himaya,
fadhili, under the ~ of kwa msaada wa.
Aussie n (sl) Mwaustralia.
austere adj 1 (of person, his behaviour) -a
kushikilia maadili, -kali. 2 (of a way of living, places, styles) -a kawaida,
sahili. ~ ly adv. austerity n.
Australian n Mwaustralia adj -a Kiaustralia; -a
Australia.
autarchy n mamlaka kamili, udikteta. autarky n
kujitosheleza (hasa kwa
uchumi wa nchi).
authentic adj halisi, thabiti, -a kweli, hakika. ~ally
adv. ~ity n uhalisi. ~ate vt hakikisha, thibitisha
(kuwa ni kweli). authentication n.
author n 1 mtunzi, mwandishi. 2 muumbaji. ~ship n
1 utunzi. 2 utambulishi wa mwandishi wa kazi ya sanaa. ~ess n mwandishi
mwanamke.
authority n 1 mamlaka: uwezo wa kisheria wa kutenda jambo lawful
~ mamlaka halali. 2 mtu mwenye mamlaka/amri; mkuu he is the ~ here yeye ndiye
mwenye mamlaka hapa. 3 serikali local ~ serikali za mitaa. 4 bingwa he is an ~
on Kiswahili yu bingwa wa Kiswahili. authoritarian adj -enye kulazimisha
utii, -a mabavu, -enye kuunga mkono mfumo wa namna hii. authorita-nianism n.
authoritative adj 1 -enye mamlaka. 2 -a amri 3 -a kuaminika. authoritatively
adv. authorize vt 1 (give leave) toa idhini, ruhusu. 2. (order)
amuru, toa mamlaka. authorized agent. ~ ajenti mwenye mamlaka. authorization
n.
autism n (psych) ugonjwa wa akili wa watoto. autistic
adj.
auto pref -enyewe. ~car n motakaa. ~biography
n tawasifu, habari za maisha ya mtu zilizoandikwa na yeye mwenyewe. ~biographic;
~biographical adj. ~biographer n mwandishi wa tawasifu.
autocracy. n udikiteta: utawala wa mtu mmoja. autocrat
n dikteta, mtawala pekee. autocratic adj. autocratically adv.
auto-dafe n (pl) autos-dafe: hukumu za mazishi ya
kidini - (agh. huchomwa moto), kitendo cha imani.
autograph n 1 mwandiko binafsi,
sahihi halisi ya mtu. 2 (book/album) kitabu chenye sahihi, agh.
za watu maarufu. ~y n sayansi ya miandiko ya watu.
automatic adj 1 -a kujiendesha. 2
(actions) -liofanywa bila kufikiri breathing is ~ kuvuta
pumzi hufanywa bila kufikiri. n mashine ya kujiendesha. ~ally adv. automate
vt fanya ijiendeshe yenyewe. automation n utumiaji wa mitambo
inayojiendesha. automatism n. automaton/automate n 1 roboti:
kitu
aver
kiendacho chenyewe au kwa mashine iliyowekwa ndani yake. 2 (fig)
mtu atendaye kama roboti.
automobile n (US) motakaa.
autonomy n kujitawala. autonomous
adj huru.
autopsy n see postmorterm.
autumn n majira ya kupukutika kwa majani. ~al adj
-a wakati wa kupukutika.
auxiliary adj saidizi, -a kuongeza nguvu/msaada ~ workers
wafanyakazi wasaidizi ~ verb kitenzi kisaidizi n 1 msaidizi/kisaidizi. 2 (pl)
jeshi lisaidialo.
avail vt, vi 1 (lit) saidia; nufaika. 2 (phr) ~
oneself of tumia, jipatia ~ yourself of every opportunity tumia kila
nafasi. n mafanikio, faida, manufaa it is of little ~ ina faida ndogo it
was of no ~ ilikuwa ya bure to no ~ bila mafanikio. ~able adj 1
-a kupatikana the book is not ~able kitabu hakipatikani your
ticket is ~able for one week only tikiti yako ni halali (inaweza
kutumika) kwa juma moja tu. 2 (of person) -wa na nafasi are you ~able
tomorrow? una nafasi kesho? ~ability n.
avalanche n 1 poromoko theluji (mlimani). 2 (fig)
lundo (k.m. la barua).
avant garde (Fr) n watu wanaovumbua na kujaribu mawazo
mapya kabisa yasiyokubalika kwa urahisi; (fig) viongozi wanamapinduzi adj -a
majaribio.
avarice n ulafi wa mali, uchoyo, hamu kubwa mno ya kupata
kitu.
avaricious adj.
avenge vt lipiza kisasi. ~ oneself
- lipa kisasi. avenging adj.
avenue n 1 barabara yenye miti kando kando. 2 mtaa mpana
wenye majengo pembeni. 3 (fig) njia ya kufikia jambo au lengo fulani (usitawi,
utajiri n.k.)
aver vt 1 nena kwa uthabiti. 2 (leg)
average
thibitisha.
average n wastani, kadiri general
~ wastani wa jumla adj -a wastani, -a kadiri, -a katikati,
-a kawaida. vt, vi 1 tafuta wastani (kwa kuhesabu). 2 fikia wastani fulani the
rainfall ~s 40 inches a year mvua hufikia wastani wa inchi 40 kwa mwaka.
averse adj -ona karaha, -wa na chuki ya he is ~ to it
akirihishwa nacho. ~ness/aversion n 1 chuki kubwa. 2 kitu
kinachochukiwa my pet aversion is nichukiacho sana ni.
avert vt 1 zuia, kinga. 2 (from)
kengeua/geuza (macho, fikra n.k.) mbali na.
aviary n tundu kubwa, mahali pa kufugia ndege (hasa katika
bustani ya wanyama).
aviation n sayansi na ufundi wa
vyombo vya anga. aviator n rubani.
avid adj (for) -enye shauku, -enye uchu. ~ity n.
~ly adv.
avocado n parachichi.
avocation n shughuli za ziada.
avocet n (bio) chokowe.
avoid vt epa, epuka; ambaa.
~able adj. ~ance n.
avouch vt (arch) 1 thibitisha.
2 kiri, ungama, ahidi.
avow vt kiri, sema kwa waziwazi,
kubali. ~al n.
avuncular adj ~ (for) -a mjomba. await vt
1 ngoja, ngojea, subiri. 2 tarajia.
awake/awaken vt,vi 1 amka; amsha, toa usingizini. 2 (to)
tambua, zinduka adj -enye kuwa macho he is ~ yu macho be ~ fahamu,
jihadhari, changamka. ~ing n 1 kuzinduka. 2 utambuzi wa jambo (hasa baya)
kwa mara ya kwanza.
award vt 1 zawadia/tunza. 2 lipa, toa~ damages lipa
fidia. n 1 tunzo, zawadi. 2 ruzuku ya masomo. 3 hukumu, uamuzi.
aware adj fahamivu, tambuzi, -enye kuwa macho, -wa -enye
habari be ~ jua, fahamu I am ~ that ninafahamu kuwa,
nina habari kuwa. ~ ness n
axes
kutambua self ~ness kujitambua.
awash adj jawa na maji; elea.
away adv 1 (kwa) mbali, kutoka I saw him some
distance ~ nilimwona kwa mbali go ~ ondoka be ~ -tokuwepo he
has gone ~ amekwenda zake he is ~ hayuko, amekwenda zake. 2 (onward,
forthwith) mara moja right ~ sasa hivi. 3 (phr) take ~ with
him! mchukue, mwondolee mbali! ~with you! toka hapa. 4 (continuously)
bila kuacha. 5 make ~ with iba. 6 do ~ with achana na, futa; (sl) ua. 7
mbele ~ across the horizon mbele kupita upeo wa macho. 8 pass ~ kufa.
9 ~ match mechi ya nje ya nyumbani.
awe n 1 heshima (iliyochanganyika
na hofu). 2 kicho, hofu, woga keep somebody in ~
tisha stand in ~ of somebody heshimu, stahi sana ~ stricken ingiwa na hofu.
awful adj 1 -a kutisha, -a kuogopa,
-a kicho, -baya sana. 2 -a kuogofya he is an ~ scoundrel yeye ni
mtu mbaya sana I am in ~ pain naumwa sana. ~ly adv. sana.
awhile adv kwa muda mfupi, kitambo.
awkward adj 1 (clumsy) -iso stadi,
-zito kuelewa au kutenda; (embarass) -enye kufedhehesha. 2 gumu,
si rahisi. 3 baya ~ corner kona
mbaya. 4 (of person) korofi an ~ customer mteja mkorofi. 5 (embarrassed)
-a kuleta mfadhaiko ~ silence ukimya wa kuleta mfadhaiko. ~ness adj. ~ly
adv.
awl n msharasi.
awning n mfuniko (agh, wa turubai juu ya mlango/dirisha
kuzuia jua, mvua n.k.).
awry adj 1 -liopinda. 2 kombo go ~enda kombo.
ax/axe n shoka he has an ~ to grind ana sababu zake. vt
1 punguza (gharama, huduma, ajira). 2 fukuza (kazini) (phr) get the ~ fukuzwa
kazi.
axes n see axis.
axil n 1 kwapa. 2 (bot) kwapajani: sehemu iliyo kati
ya kikonyo cha jani na shina. ~lary adj (bot) -a kwapajani ~lary
bud tumbakwapa: chipuko iliyoko kwenye kwapajani.
axiom n usemi unaochukuliwa kuwa kweli bila uthibitisho wala
hoja. ~atic adj. ~atic (al)adj -enye hakika dhahiri (bila
uthibitisho).
axis n 1 (math) jira. 2 (geo) mhimili axial
adj 1 -a jira. 2 -a mhimili.
axle n ekseli. ~-tree n ekseli ya gari
inayovutwa na ng'ombe, punda n.k.
ayah n yaya, mlezi wa watoto,
aye adv ndiyo, naam. n (Parliament) (pl)
kura za ndiyo. (old) daima.
azure adj -a samawati, -a buluu. n samawati, buluu,
rangi ya samawi.
|