TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

C,c n 1 herufi ya tatu katika alfabeti ya Kiingereza. 2 (mus) noti ya kwanza ya skeli ya kawaida. 3 mia (katika namba za Kirumi).

cab n 1 teksi, gari la kukodisha. taxi-~ n teksi. ~-man n dereva wa teksi. ~-rank n (also ~ -stand) kituo cha teksi. 2 chumba cha mwendeshaji (katika gari-moshi au katika lori kubwa).

cabal n njama, siri (kikundi kidogo chasiri, cha kula njama). ~istic adj. ~ler n mla njama; wasiri.

cabaret n (also ~show) tumbuizo (la nyimbo au dansi) mkahawani wakati wa chakula.

cabbage n kabichi. (bio) ~ butterfly kipepeo mweupe. (bot) ~ rose n waridi,taji.

cabin n 1 kibanda, kijumba cha makuti na magogo. 2 dambra; chumba katika ndege. 3 ~boy n mhudumu melini. 4 ~class n daraja la II (melini). ~-cruiser n motaboti kubwa yenye dambra.

cabinet n 1 chumba kidogo, almari au sefu ya kuwekea ama kuonyeshea vitu; kabati. medicine ~ n kabati la kuwekea madawa. filing ~ n kabati yenye saraka za kuhifadhia mafaili. 2 baraza la mawaziri. C ~ Minister n Waziri katika Baraza la Mawaziri. ~ maker n fundi samani.

cable n 1 kebo; kamba nene (ya katani au ya waya). 2 (naut) amari, utari, waya wa kushikia daraja /kuvutia vigari. ~car n kigari cha kamba (milimani). 3 waya nene la kupelekea habari/umeme kupita chini ya bahari. 4 habari ichukuliwayo kwa sauti. ~gram n kebo, simu. vt 1 peleka habari kwa simu (kupita baharini n.k.).

caboodle n (sl) kundi,jamii yote. the whole ~ watu wote,vitu vyote; kila kitu.

caboose n 1 jiko kwenye staha ya meli. 2 (US) behewa la gadi (katika gari

ca`canny n 1 mgomo baridi. 2

uangalifu.

caesura

cacao n kakao. ~-tree n mkakao.

cache n maficho ya vitu (k.m. dafina, silaha n.k.). vt ficha (fedha, vyakula n.k.), hifadhi mafichoni.

cachet n alama teule (ya ubora/uhalisi). cachou n kachu au lozenji, kipoteza harufu (peremende kwa ajili ya kupoteza harufu ya mdomoni).

cackle n 1 mteteo wa kuku. 2 kicheko cha sauti kubwa. 3 mpayuko. (sl) cut the ~ funga mdomo vt (of hen) 1 tetea. 2 payuka. ~r n mpayukaji. cacography n mwandiko au tahajia mbaya.

cacology n 1 uchaguzi mbaya wa maneno. 2 ukosefu wa matamshi.

cacophony n makelele, sauti kali zisizokubaliana, ukosefu wa ulinganifu katika sauti. cacophonous adj.

cactus n (pl) dungusi kakati, (jamii ya mimea kama mpungate n.k.).

cad n mhuni. ~dish adj.

cadaver n (med) maiti. ~ous adj kama maiti; dhaifu, ng'onda, -a kukonda sana.

caddy1 kadi: kikopo cha kuwekea majani ya chai.

caddy2; caddie n (in golf) mbeba vingoe. ~ car/ ~ cart n kigari cha kubeba vingoe vt bebea vingoe.

cade adj (of young animals)

-liyelelewa na binadamu (baada ya kumpoteza mamake).

cadence n 1 (of music) kiimbo mpandoshuko.

cadet n kadeti: mwanafunzi katika shule ya maofisa wa jeshi.

cadge vt,vi ~ from ombaomba vitu (hasa kwa rafiki, ndugu), doea, dusa, pandia. ~r n mdoezi.

cadi n kadhi.

cadre n 1 kada. 2 maofisa wa jeshi.

caduceus n nembo ya uganga.

caecum n (anatomy) sikamu:tawi butu

la utumbo kati ya utumbo mpana na utumbo mwembamba.

Caesar n Kaizari. ~ian operation/

section n kuzaa kwa kupasuliwa/ kisu. ~ian n.

caesura n kituo katika ushairi hasa

katikati ya mstari.

cafe n 1 mkahawa. 2 kahawa. ~ au lait n kahawa ya maziwa.

cafeteria n kafeteria; hoteli, mkahawa (ambamo wateja wanaji-hudumia wenyewe).

caffeine n (chem) kafeini.

caftan n kaftani; (for males) aina ya kanzu yenye masombo kiunoni; (for females) aina ya kanzu isiyokaza mwilini.

cage n 1 kizimba, tundu. ~d bird ndege afungiwaye tunduni. 2 (fig) gereza. vt fungia tunduni.

cagey adj (colloq) -enye hadhari/siri. cagily adv kwa hadhari.

cagoule n koti la mvua (lenye kofia na mikono mirefu).

cahoots n (sl) be in ~ with -la njama, shirikiana na/panga na (hasa katika maovu).

caiman; cayman n (bio) kaimani: mamba wa Amerika Kusini.

cain n (rel) katili, kaini. raise ~ (sl)

fanya fujo.

cairn n haram, rundo, chungu (ya mawe kama alama au kumbukumbu).

caisson n 1 (mil) kasha la kigari cha makombora. 2 keisoni: kitundu cha kuzuia maji yasiingie ambacho wajenzi wa majini hutumia. ~ disease n maumivu ya viungo yasababishwayo na kufanya kazi ndani ya hewa iliyobanwa/nzito.

caitiff n (poet) (arch) 1 mtu mbaya, mtu mnyonge. 2 mwoga adj -baya, -a woga.

cajole vt 1 ~ somebody into doing something bembeleza, vuta kwa werevu, danganya kwa kusifusifu, rairai fulani apate kufanya ulitakalo. 2 ~ something out of somebody pata taarifa kwa hila, ujanja au werevu. ~ry n.

cake n 1 keki. (selling) like hot ~s

(nunulika) sana na kwa haraka. take the ~ -wa wa kwanza, anza. you can't have your ~ and eat it amua moja. piece of ~ rahisi, nyepesi. 2 mseto, mchanganyiko wa mapishi/ vyakula. fish ~s n keki/mseto wa

samaki. 3 kipande, donge, bumbaa. ~ of soap kipande cha sabuni. vi ganda, gandamana.

calabash n kibuyu; mboko. ~ pipe n buruma.

calaboose n (US sl) gereza, korokoro, mahabusi.

calamary n (bio) kalamari: ngisi mkubwa.

calamine n kalamini: aina ya mawe yenye zinki. ~ lotion n kimiminiko cha kalamina.

calamint n mkalaminti: aina ya mnanaa.

calamity n janga, balaa, msiba mkubwa; maafa. calamitous adj.

calcareous adj -enye chokaa; -enye kufanana na chokaa.

calcify vt,vi fanya (kuwa) chokaa; geuza/geuka kuwa chokaa. calciferous adj. calcine vt,vi 1 choma chokaa. 2 choma kwa moto mkali. calcination n 1 uunguzaji: uchomaji kwa nguvu kitu chochote. 2 mgeuko chokaa.

calcium n kalisi: metali laini nyeupe (hutokea kwenye mifupa, meno, na sehemu ya chokaa, marumaru n.k.).

calculate vt,vi 1 kokotoa. 2 dhani, ona, fikiri; pima. 3 (intend, plan) kusudia, kisia, azimia. ~ up (on) (US) tumainia. 4 pangwa. calculating adj. calculation n. calculator n kikokotoo.

calculus n 1 kijiwe. 2 (maths) kalkulasi.

calendar n 1 kalenda. 2 orodha ya kesi mahakamani, miswada bungeni n.k. inayofuata kalenda vt orodhesha.

calender n 1 mashine ya kunyoosha nguo. 2 (textile) kukuto. vt nyoosha; fingirisha.

calf n 1 ndama, mtoto wa mnyama. cow in/with ~ ng'ombe mwenye mimba. slip her ~ avya. the golden ~ n kuabudu mali, kuandaa kwa shangwe. ~-love n mapenzi ya kitoto.

calibrate vt kadiria au rekebisha chombo cha kupimia au geji.

calibration n alama za vipimo/nyuzi (kwenye chombo).

calibre; caliber n 1 kipenyo cha mwanzi (wa bunduki au bomba lolote). 2 ubora wa tabia au akili. 3 (capacity) ukubwa; uhodari.

calico n kaliko: kitambaa kigumu cha pamba kama marekani au gamti.

caliph, calif n khalifa. ~ate n milki ya

khalifa.

calk1 n 1 (of horse) njumu. 2 msumari wa kisigino cha kiatu. vt tia njumu.

calk2 see caulk.

call n 1 mwito. within ~ karibu (karibu). 2 (cry/shout) yowe, mlio, ukelele (kilio cha mnyama au ndege). 3 matembezi, maamkio, ziara fupi. port of ~ n bandari ya kupitia tu. 4 (vocation) wito. 5 (demand) jambo la kupasa (la kubidi), dai. ~ loan/money; money on ~ n mkopo unaoweza kudaiwa mara moja bila taarifa ya awali. 6 ujumbe. ~-bell n kengele ya hatari; kengele ya kuita. ~ box n kibanda cha simu. ~ boy n tarishi (kijana). ~ girl n malaya (atongozwaye kwa simu). ~-house n danguro. 7 haja there is no ~ to blush hakuna haja ya kuona haya. 8 (radio) ~ sign n alama ya kuitia. ~-over/roll-~ n kuita majina (shuleni,jeshini n.k.). ~ing n wito; weledi. ~er n 1 mgeni. 2 mpiga simu. vt 1 ita kwa sauti; piga mayowe. 2 zuru, pitia, tembelea, amkia I ~ed on him nilimtembelea this train ~s at Mpanda Station treni hii inapitia Mpanda. 3 ita, taja kwa jina la we ~ him boss tunamwita bosi it is ~ed inaitwa. ~ somebody names tusi, tukana. ~ something one's own dai (kitu) kuwa mali ya. ~ into being buni, unda, umba, jaalia. ~ it a day funga kazi, pumzika. ~ into play ingiza, shirikisha, ita. 5 fikiria, chukulia. ~it a deal jichukulie kuwa umebarikiwa. 6 (compounds) ~ a halt (to) simamisha. ~ a strike itisha mgomo. 7 (of cards) otea; ita.

calm

8 (phrases) ~ somebody to account ita mtu ajieleze. ~ attention to vuta nadhari ya. ~ into question shuku, tilia (ma)shaka. ~ a meeting to order anzisha mkutano. 9 (with adverbial particles and preps) ~ by (colloq) pitia. ~ somebody down karipia. ~ something down ita; ombea. ~ for dai, hitaji. ~ for prayer adhini. ~ something forth sababisha; tumia, changia. ~ something in taka kitu kirudishwe. ~ something off shikisha adabu; simamisha. ~ somebody out ita (haraka); toa amri ya kuanzisha mgomo. ~ over ita/soma (majina). ~ something/somebody up pigia simu; kumbuka jambo; ita/andikisha jeshini. ~ up n mwito, kuitwa jeshini. ~ on/upon agiza, shurutisha; sihi, omba msaada. ~ up kumbusha; ita juu. ~ off vunja, simamisha, ondoa; ita kwingine please ~ off your dog zuia mbwa wako.

calligraphy n kaligrafia: sanaa ya kuandika vizuri.

callipers n 1 kalipa: bikari ya

kupimia. 2 vyuma vya miguu vya kumsaidia kilema.

callisthenics n mazoezimwili (ya kutia viungo nguvu na uzuri).

callosity/callus n (med) sugu, sagamba. callous adj 1 -gumu, sugu. 2 (of person) -sio hisia, baridi, -siojali. callously adv. callousness n. callow adj -siyo na manyoya; -siyo na ndevu; -changa a ~ youth kijana asiyepevuka. ~ness n.

calm adj 1 (of weather) shwari, -tulivu. 2 pole, kimya, makini, -nyamavu. ~ water n maji matulivu. pretty ~ about it baridi, hata mshipa haumgongi. n 1 utulivu, amani, raha. 2 shwari a dead ~ utulivu mkubwa. vi tulia, nyamaza. ~ down tulia. vt tuliza, nyamazisha, fariji. ~y adv. ~ness n. ~ative adj (med) -a kutuliza, -a kupoza n kipozamaumivu.

calomel n kalomeli: dawa ya kuharisha, aina ya haluli.

calorie/calory (also calory) n 1 kalori: kizio cha joto. 2 kizio/kipimo cha joto litolewalo na chakula. calorific adj.

calumniate vt zushia, zulia. calumny n (formal) uzushi, usingiziaji (wenye lengo la kuharibu jina).

Calvary n (rel) 1 Kalivari: kilima nje ya Jerusalem aliposulubiwa Yesu. 2 uwakilishi wa kusulubiwa kwa Yesu. 3 mateso makubwa.

calve vi 1 (of cow etc) zaa. 2 (of a

piece of ice) meguka. calves see calf.

Calvinism n (rel)mafundisho ya Calvin: kwamba kila kitu kilikwisha amuliwa na Mungu, amri ya Mungu. Calvinist n.

calypso n kalipso: wimbo wa ki-West Indies.

calyx n kalisi: sehemu ya nje kabisa ya ua iliyojengwa na sepali.

cam n (mech) kemu: kibadili mwendo.

camaraderie n urafiki; udugu.

camarilla n kikundi cha njama.

camber n mbinukotuta, mbinuko. vt

binua.

cambiat n mlanguzi wa fedha.

cambium n (bio) kambi: seli kuzi.

cambric n kambriki: kitambaa chororo

cha lineni au pamba. came see come.

came v (pt of) come

came n risasi ya fremu ya dirisha.

camel n 1 ngamia. ~ ('s) -hair

n manyoya laini aghalabu ya ngamia. 2 chelezo. 3 rangi ya madafu. 4 ~ -back n kiraka, mpira hafifu wa kutengenezea tairi. ~eer n mtunza ngamia.

cameo n 1 kito; sanamu. 2 taswira ya kitu, mtu au mahali.

camera n 1 kamera. on ~ inapigwa picha. 2 (leg) chumba cha mkuu wa mahakama. in ~ katika chumba cha hakimu; faraghani, si mbele ya watu; (see in chambers) kwa siri. ~ -man n mpiga picha.

camisole n shimizi.

camlet n 1 (arch) kitambaa chepesi cha

can

hariri na manyoya ya ngamia. 2 nguo ya kitambaa hicho.

camouflage n kamafleji, majificho. vt

ficha kwa njia ya kudanganya.

camp1 n 1 kambi; kituo; kigono. 2 (fig) kundi la watu wenye msimamo/imani/ itikadi moja. ~-meeting n (US) mkutano wa kidini unaofanyika nje. eye -~ n kambi ya matibabu ya macho. ~ -stool n kiti cha kukunja; kiti cha safari. ~-follower n 1 raia anayefuatana na jeshi wakati wa vita (hasa malaya). 2 barakala. vi ~ (out) fanya kambi, tua safarini, piga hema. vt (mil) weka kambini. ~ing- ground n uwanja wa kupigia kambi.

camp2 n 1 basha; msenge. 2 tabia/sura ya mwanamke.

campaign n 1 kampeni. 2 mapambano ya kijeshi. vi 1 fanya kampeni. 2 gombea uchaguzi. ~er n mfany(i)a kampeni.

campanile n mnara wa kengele. campanulate adj -a mfano wa kengele;-enye umbo la kengele.

camphor n kafuri, kafuri maiti. campus n kampasi: eneo la shule kubwa au chuo.

camshaft n (mech) mtaimbokemu, kemshafti.

can1 n 1 kopo; debe; mkebe a ~ of sardines kopo la dagaa milk ~ chombo cha maziwa. 2 (US) pipa la taka. 3 (US sl) gereza; choo; filamu iliyowekwa tayari kwa kutumia carry the ~ wajibika. vt 1 tia koponi ~ned fruit/ vegetables matunda/ mboga za kopo. 3 (US sl) fukuza, toa kazini. 4 (US sl) acha ~ that noise acha kupiga kelele. ~nery n kiwanda cha kutia vyakula makoponi. ~-opener n kiboko, kifungua kopo.

can2 v 1 weza, fahamu he ~ read anaweza kusoma I ~ not understand sifahamu, sielewi. 2 wezekana it ~ not be true haiwezi kuwa kweli the food ~ be eaten chakula kinalika as often as I (possibly) ~ kila

niwezapo. 3 (colloq) ruhusiwa ~ I leave now? naruhusiwa kuondoka?

canal n 1 mfereji. Suez ~ n mfereji

wa Suez. 2 (bio) mfereji wa chakula. ~ize vt chimba mfereji; (fig) elekeza.

canap'e n kitafunio.

canard n taarifa ya uwongo.

canary n kurumbiza.

canasta n kanasta (mchezo wa karata).

canaster n 1 see canister 2 (arch) tumbaku ya mnoga.

cancel vt,vi 1 futa. 2 batilisha. 3 ~ out sawazisa. ~lation n.

cancer1 n 1 (astro) kaa. 2 (geog) Tropic of ~ n Tropiki ya Kansa.

cancer2 n (med) 1 kansa. lung ~ n kansa ya mapafu. 2 (fig) uovu 3 (sl) ~ stick n sigara. ~ated; ~ous adj -a kansa. cancroid adj 1 (med) -a kufanana na kansa. 2 (bio) - a kufanana na kaa. n kansa ya ngozi.

candelabrum n kinara cha mishumaa mingi. ~ tree n mti wenye umbo la kinara cha mishumaa.

candescent adj -nayong'aa. candescence n.

candid adj 1 wazi. 2 (of photo) bila kupanga. ~ camera n kamera ya picha zisizopangwa. ~ly adv.

~ness n.

candidate n 1 (of election) mgombea uchaguzi; mteuliwa; mtaradhia. 2 (of examination) mtahiniwa. candidacy; candidature n ugombea uchaguzi.

candle n mshumaa the game is not

worth the ~ jambo halina maana/faida burn the ~ at both ends jichosha kwa kazi he cannot hold a ~ to you si kufu yako. ~ stick n kinara cha mshumaa.

candlemas n (rel) mweuo.

candour n unyofu, uwazi: tabia ya kunena bila kupendelea; tabia ya kunena ukweli.

candy n pipi, peremende, lawalawa. vt hifadhi kwa kuchemsha na kupika na sukari.

cane n henzirani; ufito wa mwanzi.

~-brake n kichaka cha mwanzi.

~ chair n kiti cha henzirani. ~ furniture n samani/fanicha ya henzirani. sugar~ n muwa. vt 1 piga na fimbo ya henzirani. 2 suka kiti cha henzirani.~ -sugar n sukari muwa.

canine adj -a mbwa; kama mbwa n 1 ~ tooth n chonge. 2 mbwa. 3 mnyama wa jamii ya mbwa (k.v. fisi bweha n.k.).

canister n 1 kopo (la kuwekea majani ya chai, unga n.k.) 2. kombora (k.m. ya gesi ya machozi).

canker n 1 (med) ugonjwa wa vidonda, (kinywani, masikioni), kidonda cha kinywani. 2 (of plants) kikwachu. 3 (fig) uovu. vt ozesha, haribu. ~ous adj.

cannabis n bangi.

cannibal n mtu mla watu; mnyama alaye wenziwe. ~ism n. ~istic adj. ~ize vt toa vipuli (kutoka kwa mashine iliyoharibika au kuukuu) ili kutengeneza nyingine.

cannon n 1 mzinga. ~-ball n tufe la mzinga. ~-bone n (of horse) mfupa baina ya goti na kwato. ~-fodder n askari wanaofikiriwa si muhimu hivyo waweza kuteketezwa bila wakuu wao kujali. 2 mgongano katika mchezo wa biliadi (mpigo mmoja unaogusa mipira miwili) vt gonga kwa nguvu. ~ade n mpigo wa mizinga mingi; mfululizo wa risasi.

canny adj -erevu, -janja; -enye hadhari, -angalifu. cannily adv.

canoe n mtumbwi, kiperea, nchoro.

outrigger ~ n ngalawa. vi endesha kiperea. ~ist n mpiga makasia.

canon n 1 (rel) sheria/kanuni ya kanisa. ~ law n kanuni/sheria za kanisa. 2 kigezo. 3 vitabu vinavyotambulika (hasa vitabu ya Biblia ambavyo vinatambuliwa na kanisa). 4 orodha rasmi. 5 padri wa kanisa kuu. 6 sehemu kuu ya misa. ~ ical adj -a kuhusu sheria za kanisa. ~ ical hours n saa za sala. ~icals n mavazi rasmi ya ibada;

(gram) kuhusu msingi wa neno. ~ize vt 1 takatifuza: dumisha/tangaza kuwa mtakatifu. 2 idhinisha moja kwa moja. ~ization n.

canopy n 1 kanopi: kitambaa/kipaa

kinachoning'inizwa juu ya kiti, kitanda n.k. 2 (aircraft) mfuniko wa chumba cha rubani 3. (fig) mwavuli; kivuli chochote kinachoning'inia the ~ of the sky anga, mbingu.

cant1 n 1 mwinamo. 2 msukumo wa ghafula unaosababisha kuinama. ~ vt,vi ~ (over) laza upande; pindua; pinduka.

cant2 n 1 ulaghai, unafiki. 2 misimu (ya tabaka/kikundi fulani).

cantaloup(e) n aina ya tikiti.

cantankerous adj -gomvi, -enye hasira.

~ness n.

canteen n 1 kantini. 2 bweta/sanduku

la vyombo vya kulia. 3 (mil) vyombo vya chakula/maji vya askari.

canter n (of horse) mwendo wa matao win in a ~ shinda kwa urahisi. vt,vi enda kwa matao.

canticle n (rel) wimbo mfupi wa kidinihasa unaotokana na Biblia.

cantilever n shikizowenza. ~ bridge n daraja shikizowenza.

canto n sehemu kuu ya shairi refu.

canton n jimbo, mkoa (hasa Uswisi).

~al adj.

cantonment n kambi, makao ya wanajeshi.

cantor n (rel) kiongozi wa waimbaji katika kanisa au sinagogi.

canvas n 1 turubai. 2 (sacking) gunia. 3 (of painting) turubai ya kuchorea under ~ kambini, hemani win by a ~ shinda kwa nafasi ndogo.

canvass vt,vi 1 (for) pita na kuomba

(kura, michango n.k.); jadili kwa undani. ~er n.

canyon n korongo kuu (lenye mto),

genge kuu.

cap n 1 chepeo (aina ya kofia) put on one's thinking ~ fikiria jambo kwa makini. ~ and gown (for University) bushuti na kofia ya mahafali. ~ in hand kwa

unyenyekevu if the ~ fits ukiona kwamba yanakuhusu. ~ a pie adv (arch) tangu kichwani hadi miguuni, kabisa set one's ~ at somebody (of girl) jaribu, vutia mwanamume a feather in one's ~ kitu cha kujivunia. 2 fataki. 3 (of bottle) kifuniko. ~ block n faruma. 4 (biol) kikungu cha uyoga. 5 Dutch ~ n (see diaphragm). vt 1 vika chepeo. 2 funika. 3 shinda, pita, -wa bora kuliko. ~ a joke toa utani unaochekesha zaidi. to ~ it all mwisho wa hayo. 4 tunuku.

capability n 1 uwezo, uwezekano. nuclear ~ n uwezo wa kupigana vita vya nuklea. 2 (pl) vipaji (vinavyoweza kuendelezwa) that boy has great capabilities mtoto yule ana vipaji vingi. capable adj 1 hodari, -stadi,-enye akili. 2 (of persons) -enye uwezo. 3 (of things/situations) -enye uwezekano. capably adv.

capacity n 1 nafasi, ujazo, ukubwa filled to ~ (of a room etc.) -liojaa kabisa, liojaa pomoni, tele seating~ idadi ya viti. 2 (of person) uwezo (wa kukumbuka au kujifunza) show one's ~ onyesha uwezo wako. 3 wadhifa, cheo in my ~ as Director nikiwa ni Mkurugenzi. capacious adj -enye nafasi kubwa ndani. capaciousness n. caparison n (of horse) matandiko yaliyopambwa. vt tandika (farasi) matandiko yaliyopambwa.

cape1 n juba.

cape2 n rasi: The ~ (of Good Hope) n Rasi ya Tumaini Jema.

caper vi rukaruka kwa furaha, chachawa. n 1 kurukaruka kwa furaha, kuchachawa. 2 utundu. cut a~/~s rukaruka kwa furaha; tenda kama mwenda wazimu.

capita n see per capita.

capillary adj -a kapilari ~ attraction mvuto wa kapilari ~ repulsion msukumo wa kapilari n (anat) kapilari: mshipa mdogo wa damu. capillarity n ukapilari: uwezo wa

capital

kushuka au kupanda kwa kioevu katika neli kutokana na kani za mshikamano na mng'ang'anio kusukuma kwa nguvu za unywele.

capital1 n (arch) kombe ya nguzo.

capital2 n 1 makao makuu. 2 (of letters of the alphabet) herufi kubwa (eg. A,B,C.). 3 mtaji; raslimali; fedha. floating ~ n mtaji geu. fixed ~ n mtaji wa kudumu. make ~ of tumia kwa faida adj 1 (arch colloq) -zuri sana. a ~ speech n hotuba nzuri sana. 2 -kuu. ~ city n Makao Makuu, jiji kuu; mji mkuu. 3 -a kifo. ~ punishment n adhabu ya kifo. ~ offence n kosa linaloadhibiwa kwa kifo. 4 -a mtaji. ~ levy n kodi ya mtaji. ~ goods n bidhaa zinazotumika kuzalisha mali. ~ expenditure n matumizi ya mitambo/majengo. ~ gain n faida tokana na mauzo ya raslimali.

capitalism n ubepari. capitalist n

bepari adj -a kibepari. capitalistic adj. capitalize vt,vi 1 andika kwa herufi kubwa. 2 geuza kuwa mtaji. 3 (fig) ~ (on) tumia kwa faida yako. capitalization n.

capitation n kodi ya kichwa. ~ grant n ruzuku maalum kwa kila mtu mzima.

capitulate vi salimu amri kwa masharti, jisalimishe (kwa masharti). capitulation n.

capon n. jogoo (aliyehasiwa). cappuccino n kapuchino: kahawa ya maziwa yenye povu.

caprice n (mwelekeo wa) kubadilisha wazo/msimamo/tabia ghafla. capricious adj 1 -geugeu. 2 kipande cha muziki mwanana.

caps abbr of capital letters. see capital2.

capsize vt,vi (esp of a boat in water) pinduka, pindua.

capstan n (naut) roda/kapi kubwa; kitu kama gogo la kuzungusha kamba ya nanga n.k. na kuivuta.

capsule n 1 (bot) fumbuza. 2 (med)

kapsuli, kidonge. 3 kapsuli: sehemu

ya roketi yenye ala ambayo inaweza kutenganishwa. capsular adj.

captain n 1 (mil) kapteni. 2 (of games) kapteni, nahodha. 3 (of ship)iation) rubani. vt ongoza. ~cy n.caption n 1 maelezo mafupi (ya habari katika kitabu, gazeti au chini ya picha). 2 kichwa cha makala.

captious adj 1 (formal) -epesi kulaumu/ kukosoa. ~ness n.

captivate vt pendeza mno, vuta kwa uzuri. captivation n mvuto.

captive n mfungwa; mateka adj fungwa, -a kutekwa. ~ state n hali ya kufungwa. ~ audience n hadhira tekwa: isiyoweza kuondoka (hivyo rahisi kushawishiwa). take ~ chukua mateka, teka nyara. captivity n. captor n.

capture vt 1 (of people) kamata, teka.2 (of land) twaa. 3 (of mind) vutia, teka. 4 (of photograph) hifadhi. n kukamata, kuteka; kukamatwa, kutekwa.

car n 1 gari, motokaa. ~ park n maegesho ya magari. ~ port n banda la kuwekea motokaa. 2 behewa; kiberenge. dining ~ n behewa la chakula.

carafe n chupa ya maji/divai (ya mezani).

caramel n karameli: sukari iliyounguzwa, gubiti.

carapace n gamba, ng'amba (la wanyama kama kobe, kaa, kasa).

carat n karati: kipimo cha kupimia usafi wa dhahabu/uzito wa vito vya thamani.

caravan n 1 msafara. 2 gari linalotumiwa kama nyumba vi ishi/safiri kwenye msafara. ~ serai n Asia) nyumba ya wageni (yenye ua mkubwa wa kuhifadhi ngamia, farasi, magari n.k. ya misafara).

caravel n (arch) jahazi.

caraway n kisibiti.

carbine n karabini:bunduki fupi.

carbohydrate n 1 kabohaidreti. 2 (pl) vyakula vya wanga (k.v. viazi, muhogo, mkate n.k.).

carbolic adj -a kaboliki. ~ acid n asidi kaboliki: dawa ya sumu itokayo katika makaa ya mawe, hutumika sana kusafisha vidonda na vyombo vya nyumbani au hospitalini.

carbon n 1 kaboni. ~ dioxide n dioksidi ya kaboni. 2 (electrode) elektrodi ya kaboni. 3 ~ paper n kaboni. ~ copy n nakala halisi. ~ copying n kunakili kwa kaboni. ~ dating n njia ya kupima umri wa vitu vya kale kwa kupima kiasi cha kaboni. carbonize vt kabonisha, geuza kuwa kaboni. ~iferous adj. carbonated adj -enye dioksidi ya kaboni. ~ation n.

carboy n chupa kubwa ndani ya jamanda, chupa ya ubapa.

carbuncle n 1 kito chekundu. 2 jipu kubwa.

carburettor n kabureta: kifaa kinachochanganya hewa na petroli kutoa msombo ulipukao.

carcase; carcass n 1 mzoga. 2 (sl) ~ meat n nyama mbichi. 3 gofu la kitu (k.v.jengo, chombo n.k.). 4 (sl) mwili wa mtu. save one's ~ jiokoa maisha.

carcinogen n (med) kisababisha kansa. ~ic adj.

card1 vt chambua (sufi au katani). n

chombo cha kuchambua sufi.

card2 1 kadi. wedding ~ n kadi ya arusi. post ~ n postakadi. membership ~ n kadi ya uanachama. library ~ n kadi ya maktaba. 2 mtu wa mizaha, mcheshi. 3 playing ~ n karata put one's ~s on the table julisha mambo, nia play one's ~s well cheza vizuri, tumia akili on the ~s wezekana have a ~ up one's sleeve -wa na mpango wa siri. ~index n faharisi vt weka faharisi, tia faharisi. ~sharp/ ~sharper n mfyatuzi, mlaghai katika mchezo wa karata.

cardamom n iliki.

cardboard n kadibodi (karatasi nene kama ubao mwembamba).

cardiac adj -a kuhusu moyo. ~ arrest

career

n shtuko la moyo. cardiogram n kadiogramu. cardiograph n kadiografu. cardiology n kadiolojia: taaluma (ya) moyo. ~ muscle n msulimoyo.

cardigan n sweta, fulana yenye vishikizo upande wa mbele.

cardinal1 n (rel) kadinali: askofu mwenye cheo cha juu. ~ate/~ship n.

cardinal2 adj -kuu; -a maana; -a kiini cha jambo. ~ numbers n namba kamili. ~ points n sehemu kuu za dira (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi). ~ vein n vena kuu.

care n 1 (attention) uangalifu, utunzaji. take ~ of angalia, tunza, shughulikia. take ~ angalia, tahadhari, jihadhari. 2 (responsibility) uangalizi, wajibu, usimamizi. ~ of (of letter) kupitia kwa (k.k). ~taker n mwangalizi; mlinzi; msimamizi; kabidhi. ~taker government serikali ya muda. 3 mashaka, taabu,wasiwasi he is free from ~ hana taabu. ~laden adj enye wasiwasi/mawazo mengi. 4 (US pl) mzigo, tatizo the ~s of bringing up a large family matatizo ya kulea familia kubwa. ~free adj bila mawazo, changamfu; (derog) siojali; purukushani. vi 1 ~ (about)jali I don't ~ , I couldn't ~less, who ~s! nani anajali. 2 ~ (for) (like) penda; (look after) tunza would you ~ to come? ungependa kuja; karibu. ~ful adj - angalifu, -a makini, -enye kujali. ~fully adv kwa uangalifu, kwa hadhari, kwa makini. ~fulness n. ~less adj -zembe, vivu, -a ovyo ovyo. ~lessness n.

careen vt,vi laza upande, (chombo au meli) ili itengenezwe chini, inika; pindua. vi lala upande (ubavuni). ~age n (naut) ulazaji upande wa chombo; gharama zake; mahali pa kufanyia kazi hiyo.

career n (profession) 1 kazi, amali. ~

master/mistress n mwalimu,

mshauri kuhusu maisha/kazi baada ya kumaliza masomo. ~ girl n mwanamke anayejali sana kazi yake (k.m. kuliko kuolewa). 2 (matendo ya) maisha (ya watu). 3 mkurupuko. in full ~ kwa mwendo wa kasi sana vi kurupuka. ~ along/through kwenda ovyo. ~ist n mtu anayejali kusonga mbele katika amali.

caress vt papasa (kwa mahaba). n mpapaso (wa mahaba). ~ ing n. ~ingly adv.

caret n kareti: alama katika mstari wamaandishi inayojulisha kuwa neno lililosahauliwa limeandikwa juu yake.

cargo shehena, kago, mizigo. ~-ship/ plane n meli/ndege ya mizigo.

caribou; cariboo n kuro, (wa Amerika ya Kaskazini).

caricature n 1 karagosi: picha/sanamu

iliyokuzwa mno kuliko kawaida yake kwa nia ya kuchekesha. 2 kuiga mtu kwa kusisitiza mambo fulani kwa nia ya kuchekesha; igiza, fuatisha na kugeuza picha (tendo, jambo) hata lichekeshe. caricaturist n mchora vikaragosi.

caries n karisi: kuoza kwa jino/mfupa. carious adj -enye (ugonjwa wa) karisi, -liooza (hasa jino). cariosity n.

carillon n seti ya kengele kwa ajili ya

kutoa ghani.

carmine n adj -ekundu.

carnage n mauaji ya watu wengi; umwagaji damu.

carnal adj -a mwili, -a kuhusu mwili; -a tamaa za mwili. ~ knowledge n ngono. ~ly adj.

carnation n aina ya ua.

carnival n 1 kanivali: sikukuu kubwa. 2 kipindi chenye sikukuu hizi kabla ya kwaresima.

carnivore n (pl) (of animals) wala nyama.

carob n karuba: mbegu zinazotumika badala ya kakao kutengeneza chakleti n.k.

carol n 1 (rel) wimbo wa Krismasi. 2 (lit) wimbo wa furaha. vi 1 imba kwa

carrick

furaha. 2 imba nyimbo za Krismasi. ~ler n mwimbaji wa nyimbo za namna hii.

carotene (also carotid) karotini.

carouse vi sherehekea, fanya karamu (ya ulevi). carousal n.

carp1 n kambare mamba, kamongo wa

maji baridi; samaki mrefu, mkubwa na hufanana na mamba.

carp2 vi ~(at) kemea, karipia, lalamika, lalamalalama (kwa makosa madogomadogo yasiyo na msingi).

carpel n kapeli.

carpenter n seremala. vi fanya kazi ya seremala. carpentry n useremala.

carpet n zulia. (colloq) be on the ~ karipiwa, kemewa. sweep something under the ~ sukumizia kando, ficha, weka pembeni (ili kuchelewesha utekelezaji/kukwepa lawama). stair~ n zulia la ngazini. ~ sweeper n kifagia zulia. vt tandaza, tanda ~ with fallen leaves tanda na majani makavu; laumu, karipia.

carpology n kapolojia: tawi la elimu mimea linaloshughulikia matunda na mbegu.

carpus n (anat) kiungo cha kiganja na mkono. carpal adj (anat) -a kiungo cha kiganja na mkono.

carriage n 1 gari la farasi. baby ~ n

(US) gari la mtoto. 2 behewa la garimoshi. 3 uchukuzi, upagazi. ~forward n gharama za usafirishaji zinazolipiwa na mpokeaji bidhaa. ~ free/paid n gharama zilizolipwa na mpelekaji bidhaa. 4 gurudumu bebaji. 5 sehemu ya mashine inayohamishika na inayoshikilia sehemu nyingine. 6 mkao wa mwili, mwendo wa kutembea. 7 ~ way n (part of road) sehemu ya barabara inayotumiwa na magari. 8 dual ~ way n njia mbili: barabara iliyogawanywa sehemu mbili (kwa tuta, majani n.k.). ~able adj (of roads) -a kuweza kupitika kwa magari.

carrick n (naut) ~ bend n fundo

linalounganisha kamba mbili.

carrion n mzoga, nyama iliyooza;

chochote kichukizacho adj -liyooza; -a kuchukiza. ~ crow n (bio) kunguru mla mizoga.

carrot n 1 karoti; (fig) kishawishi, kivutio. 2 (pl) nywele nyekundu; mtu mwenye nywele nyekundu. 3 rangi ya karoti. ~y adj. the stick and the ~ vitisho na hongo; tunzo au faida inayoahidiwa (na mara nyingi isiyokuwa yakini). hold out/offer a ~ to somebody shawishi kwa kutoa tunzo au kufaidika na kitu.

carry vt,vi 1 beba, chukua, eleka she carried the child on her back alimweleka mtoto he is ~ing the load on his head ameubeba mzigo kichwani mwake. 2 peleka, pitisha the pipes ~ water to the town mabomba hupeleka maji mjini copper carries electricity shaba hupitisha umeme. 3 (conquer) shinda, faulu our team carried the day timu yetu ilishinda timu zote. ~ everything before one fanikiwa kila kitu, shinda kabisa. ~ one's point ungwa mkono. 4 himili these pillars ~ the weight nguzo hizi zinahimili uzito. 5 (be pregnant) she is ~ing a child yu mjamzito. 6 refusha, zidisha, endeleza ~ the wall to ten feet zidisha ukuta kufikia futi kumi. 7 (with phrases) ~ weight -wa na uzito your reasons ~ no weight sababu zako hazina uzito. 8 simama/ tembea they ~ themselves like soldiers wanatembea kama askari. 9 (of guns) enda mbali, fikia mahali/masafa. 10 (of disease) eneza. 11 ~ too far zidi; vuka mpaka. ~ about tembea na, enda na (kila mahali). ~ away beba. be carried away jisahau. ~ off nyakua, shinda; ua. ~ it off fanikiwa (katika hali ngumu) cholera carried off 10 people kipindupindu kiliua watu 10. ~ on endelea (licha ya matatizo); lalama. ~ (with) fanya mapenzi na. ~ings on vitendo vya kijinga/ajabu. ~ out maliza,

cartoon

tekeleza. ~ through kamilisha. ~ back kumbusha I was carried back to my youth nilikumbuka ujana wangu their courage will ~ them through ujasiri wao utawasaidia. n 1 (of a gun range) masafa. 2 uchukuzi, ubebaji. carrier n 1 mchukuzi common carrier uchukuzi wa aina yoyote; mpagazi; hamali; kampuni ichukuayo bidhaa. 2 aircraft carrier n manowari ya kuchukulia ndege (agh. za vita). 3 keria: kiungo cha chuma cha kuchukulia mizigo n.k. katika baiskeli au motokaa. 4 electric carrier n kipitisha umeme. 5 (biol) kichukuzi. 6 (of disease) mwenezaji. carrier-bag n mfuko wa karatasi au plastiki. carrier-pigeon n njiwa-kijumbe.

cart n mkokoteni, rukwama. put the ~ before the horse pindua jambo, fanya visivyo, fanya kinyume cha mambo. ~ away ondolea mbali. ~ bad n mzigo wa kujaa rukwama; vitu vingi. ~ wright n mtengeneza rukwama; mwendesha rukwama. vt,vi 1 beba/chukua kwa mkokoteni. 2 (colloq) (around) beba kwa mkono. 3 (derog) swaga. ~ wheel n 1 gurudumu (la mkokoteni). 2 kuvingirika kisarakasi.

carte blanche (F) n mamlaka kamili. give a person ~ pa mtu mamlaka

afanye apendavyo.

carte du jour (F) n menyu (ya siku ile).

cartel n 1 muungano wa wakiritimba (ili kudhibiti biashara).

cartilage n gegedu, tishu.

cartography n usanifu wa ramani.

cartographer n.

carton n katoni.

cartoon n 1 katuni. 2 picha ya kuchekesha. ~ist n mchora katuni hasa ya kuigiza mambo yanayotendwa na watu. vi,vt chora picha ya kuchekesha kama kielezo. 3 filamu ya sinema ambayo wahusika wake ni picha zilizochorwa; ashiria mtu maalum katika picha ya

cartouche

kuchekesha.

cartouche n katushi: 1 kibamba cha madini chenye maandiko. 2 ganda la risasi lililotengenezwa kwa karatasi.

cartridge n 1 ganda, kibweta cha risasi. ball ~ n risasi bila baruti. 2 kikuto cha filamu, ukanda (wa kunasia sauti n.k.). 3 kibweta cha wino (katika kalamu za wino). ~-belt n ukanda wa risasi.

carve vt 1 chonga. 2 kata nakshi. 3 piga mtai; kata nyama (iliyopikwa) mezani. ~ out bandua; gawanya katika vipande vingi; (fig) fanikiwa kwa juhudi kubwa he ~d out a career for himself in the army alifanikiwa (baada ya jitihada kubwa) kupanda cheo jeshini. ~r n mchongaji; mkata nyama.

caryatid n kariatidi: sanamu ya mwanamke iliyotumika kama nguzo.

cascade n 1 maporomoko (makali lakini madogo) ya maji. 2 kitu kilichopangwa katika mfululizo wa matukio. 3 kitu kitokeacho ghafula na kwa vurumai; kitu kiangukacho kwa wingi.

case1 n 1 (affair) jambo, kadhia it is a~ of stupidity not negligence ni suala la ujinga si uzembe. a ~ in point mfano. a ~ study n uchunguzi kifani. 2 it is the ~ ndiyo, naam, ni kweli. in any ~/in no ~ kwa vyovyote. 3 (med) mgonjwa anayeuguzwa five ~s of malaria wagonjwa watano wa malaria. 4 (of grammar) uhusika. 5 (leg) kesi, daawa. ~ at bar kesi inayosikilizwa. make out a ~ (for) jengea hoja za

kutetea jambo fulani ~ for the defence/ prosecution hoja ya mshitakiwa/mshitaki. ~-law n sheria ya desturi.

case2 n 1 kasha; sanduku; bweta, jamanda. 2 (covering) kifuniko. pillow ~ n foronya. 3 (printing) upper-~ n herufi kubwa. lower-~ n herufi ndogo. vt 1 tia, weka bwetani, kashani; fungia ndani. 2 (US sl) chunguza kabla ya kuiba. casing see

case n kifuniko, kizingio. ~ of rubber kizingio cha mpira. vt tia matiki adj ~-hardened (fig) sugu (kutokana na maisha).

casein n (chem) kasini: protini kuu ya maziwa.

cash n pesa, fedha (noti na sarafu). hard (spot) ~ n fedha taslimu. ~ sale n kuuza kwa fedha taslimu, fedha mkononi. ~ on delivery/~ down n malipo wakati wa kupokea bidhaa. ~ discount n aheri.~ customer n mnunuzi anayelipa fedha taslimu. petty ~ book n daftari ya matumizi madogomadogo. ~ book n daftari ya fedha taslimu. ~-desk n kaunta ya keshia. ~ flow n mapato halisi.~-register n mashine ya kuhesabia fedha. ~ dispenser n mashine maalumu inayotunza na kutoa fedha. vt,vi 1 lipa/pata fedha. ~ a check lipwa fedha (kwa kutoa cheki). 2 faidi; tumia kwa faida. cashier n keshia.

cashew 1 n korosho, kanju. 2 mkorosho, mkanju.

cashier vt fukuza jeshini.

cashmere n kashimiri: kitambaa

cha sufi/manyoya ya mbuzi wa Kashmiri.

casino n kasino: jengo la starehe hasa ya kamari.

cask n pipa, kasiki. casket n kibweta, kijaluba, kikasha; (US) jeneza.

cassava n muhogo. dried ~ n makopa. ~ leaves n kisamvu.

casserole n 1 maziga. 2 chakula

kilichookwa kwenye maziga.

cassette(s) n kaseti, kanda.

cassock n (rel), kanzu/vazi la

makasisi, wahudumu na waimbaji wa kanisani.

cast vt 1 tupa, rusha. ~ a dice tupa

dado. ~ an anchor tupa/tia nanga. ~ a vote piga kura. ~ing vote n kura makata. ~ something in somebody's teeth laumu. 2 kalibu, subu; mimina katika kalibu. 3 (of snake), jinyonyoa jichuna, jiambua.

castanet(s)

4 ~ up jumlisha, kokotoa. 5 geuza, elekeza (macho). ~ about for angaza, tafutatafuta. ~ an eye over tupia jicho. 6 (theatre) pangia wahusika dhima katika mchezo. 7 (naut) legeza (kamba). 8 (printing) kadiria nafasi (itakayohitajiwa). 9 (knitting) ~ on fuma safu ya kwanza ya vitanzi. ~ a net tupa wavu. ~ a horoscope piga falaki, bao ~ a new light on a problem leta mtazamo/ mwanga mpya (juu ya jambo). ~ somebody aside achana na mtu, telekeza. ~ away (usually pass) acha (kutokana na kuvunjika kwa meli). ~ down sononesha ~ (in one's lot) with somebody jiunga pamoja na. ~ off anza safari. ~ off clothes tupa nguo. ~ offs n mitumba. ~ off legeza, fumua. ~ out toa, fukuza. ~ out devils fukuza pepo. ~ away n mtu aliyevunjikiwa na meli. adj -enye kuvunjikiwa na meli. n (throw) 1 mtupo, mrusho. 2. kalibu. ~ iron n kalibu ya chuma adj (fig) kaidi, bishi, gumu. 3 kitu kilichoumbwa katika kalibu. 4 (squint) kengeza kidogo. a ~ in the eye kuwa na kengeza kidogo. 5 wachezaji: seti ya wachezaji (k.m. katika filamu ya sinema) aina, sifa.

castanet(s) n kitoazi, kayamba.

caste n 1 (Ind.) tabaka (litokanalo na

kazi, vyeo, weledi, n.k.). 2 (fig) hadhi, nafasi katika jamii. lose ~ shuka hadhi.

castellan n liwali.

castellated adj -enye buruji; -enye

ngome.

castigate vt 1 adhibu vikali (kwa kupiga au kukemea). 2 rudi. castigation n. castigator n.

castle n ngome, husuni, nyumba yenye boma; kasri. ~s in the air/~s in Spain njozi, ndoto za mchana; mawazo ya tamaa isiyowezekana.

castor1 n 1 gurudumu (la samani): gurudumu lifungwalo kwenye miguu ya samani (kiti, meza n.k.) kurahisisha mjongeo wa samani 2.

kijaluba cha chupa au bati cha kuwekea sukari, chumvi, n.k.

castor2 n 1 (bot) mbarika, nyoyo, mbono. ~ oil n mafuta ya mbarika, kastoroli. ~ bean n mbegu za mbarika, nyonyo. ~ sugar n sukari laini.

castrate vt hasi; hanithisha.

castration n.

casual adj 1 (accidental) -a bahati, -a

nasibu; -a ajali. 2 (occasional) -a nadra, -siyo -a kudumu. ~ labourer n kibarua. 3 (informal) -a kawaida, -sio rasmi. ~ clothes n nguo za kawaida. ~ friendship n urafiki wa kawaida/usio wa karibu; -liotokea bila mpango au bila kutegemewa. ~ness n.

casualty n 1 ajali (agh. mbaya) inayosababisha kifo. 2 majeruhi: mtu aliyejeruhiwa; aliyeuawa au aliyepotea vitani. ~ ward n wadi ya majeruhi.

casuarina n mvinje.

casuistry n (derog) (fig) ulaghai: kupindua mambo kwa kutumia hoja za ulaghai. casuist n.

casus belli n (latin) kisa cha vita (mapigano, ugomvi).

cat n 1 paka, nyau. wild ~ n gwagu, paka shume, paka nunda. let the ~ out of the bag fichua siri (bila kukusudia) it's raining ~s and dogs mvua inanyesha kwa wingi. wait for the ~ to jump bana, tulia kwanza (mpaka uone upepo unaelekea wapi). see which way the ~ jumps ngojea fikira za watu wengine kabla ya kutoa shauri lako. like a ~ on hot bricks -enye wasiwasi sana. set/put the ~ among the pigeons leta vurugu, sababisha wasiwasi. ~-and-dog life maisha ya ugomvi. has the ~ got your tongue (sl) wabana kimya. it makes a ~ laugh inafurahisha sana. even a ~ may look at the King hata watu wa chini wana haki zao. when the ~ is away the mice will play paka akiondoka panya hutawala. (compounds etc.) ~

catabolism

burglar n mwizi wa kuparamia kuta. ~ call v zomea. n zomeo. ~ fish n kambare. ~ nap/sleep n usingizi (wa kuiba). ~ walk n ujia, uchochoro (hasa kwenye daraja). ~er waul vi lia kama paka n mlio kama wa paka. ~'s eye n 1 kiashiria njia. 2 aina ya kito ambacho huonyesha mwale wa mwanga ndani yake. ~ 's pan n 1 kibaraka, kikaragosi. 2 (naut) upepo mdogo ufanyao viwimbi vidogo juu ya maji wakati bahari imetulia. ~gut n uzi wa utumbo wa mnyama, kano.

catabolism n (biol) ukataboli.

cataclysm n 1 gharika, mafuriko ya maji. 2 maafa makubwa (badiliko la ghafla k.v. mafuriko, vita, n.k.). 3 mabadiliko ya ghafla ya mambo.

catafalque n jukwaa lililopambwa kwa ajili ya jeneza (agh la mtu mashuhuri).

catalepsy n mkakamao (wa miguu

na mikono). cataleptic adj.

catalogue n 1 katalogi. 2 orodha ya vitu. vt andika katalogi; ingiza katika katalogi.

catalysis n (chem) uchocheaji. catalyst n kichocheo catalytic adj.

catamaran n (naut) chelezo au muunganisho wa mitumbwi miwili pamoja.

catapult n 1 manati, panda, fyata. 2 (inancient times) mtambo wa kutupia mawe katika vita. 3 chombo cha kurushia ndege katika manowari au ndege nyingine. vt rusha ndege.

cataract n 1 maporomoko ya maji. 2 (of the eye) mtoto wa jicho: aina ya ugonjwa wa macho.

catarrh n 1 mafua; ugonjwa wa makamasi mengi. 2 makamasi. ~al adj.

catastrophe n msiba mkuu,

machafuko, maangamizi, balaa. catastrophic adj.

catboat n mashua ya mlingoti na

tanga moja.

catch vt,vi 1 kamata, gwia, bamba ~a thief kamata/bamba/gwia mwizi. 2 shika, daka ~ the ball daka mpira

~a knife shika kisu. 3 (fig) pata, shikwa na ~ a cold pata mafua. ~fever shikwa na homa. 4 kuta, fuma I caught the boys stealing niliwakuta watoto wakiiba ~ somebody in the act of doing something gundua mtu kosa lake. 5 wahi. ~ a train wahi treni. ~ somebody fuma mtu akifanya jambo. 6 ~ (up) fikia aliye mbele you have to work hard to ~ up with the rest huna budi kufanya kazi sana uwafikie wenzako. 7 nasa, kwama the nail caught her dress msumari ulinasa nguo yake. 8 fahamu, tambua; sikia I ~ your meaning nafahamu maana yako. 9 ~ sight of ona kwa kitambo kidogo. 10 piga he caught me on the nose alinipiga pua. 11 pata you will ~ it utaipata; (of woman) (sl) pata mimba. 12 jaribu kushika. a drowning man ~es at straws mfa maji haachi kutapatapa. n 1 kudaka. 2 hila; mtego there's a ~ in it pana mtego. 3 vuo. 4 mwindo; pato la bahati. ~ one's breath ziba pumzi (kwa mshtuko). ~ fire shika moto. ~er n (basketball) mdakaji. ~ing adj 1 (esp. of disease) -a kuambukiza. 2 (attractive) -a kuvutia; -a kuwaka. ~ crop n mazao yanayokua kwa haraka sana yanayopandwa kati ya mimea mingine (k.m. maharage kati ya mahindi).

catchment n eneo lililo chanzo cha maji ya mto/bwawa. ~ area/basin n (of school) eneo ambamo wanafunzi wa shule moja wanatoka.

catchpenny adj 1 (derog) zuri nje tu lakini hafifu sana. 2 -lotengenezwa kwa madhumuni ya kuuza haraka bila kuweka makini.

catchword n 1 kidahizo. 2 (mil)

(password) neno la siri. 3 neno linalorudiwarudiwa. ~ phrase n msimu.

catchy adj 1 -a kusikiza, -a kuvuta

masikio (sauti, wimbo n.k.). 2 (tricky) -danganyifu, -a hila; -erevu.

catechism

catechism n (rel) katekisimu.

catechist n mkatekista. catechetic(al) adj -a kujibizana. catechize vt (rel) fundisha, pima ujuzi wa dini kwa maswali na majibu; fundisha katekisimu. catechumen n mkatekumeni: mwanafunzi wa dini ya Kikristo (anayetaka kubatizwa).

category n. aina, namna, jinsi; jamii, kundi. categorical adj dhahiri, -a hakika, halisi, pasi shaka. caregorically adv. categorize vt

ainisha, pambanua, bainisha.

cater vi andaa; patia. ~ for patia (chakula, michezo, mazungumzo n.k.). ~er n mwandazi, mchukuzi wa chakula. ~ing n.

caterpillar n 1 kiwavi. 2 katapila, tingatinga.

catharsis n 1 (med) kuharisha, kuendesha. 2 (psych) kutoa/ kupoza hisia zilizochemka, mtakaso hisia. cathartic n aina ya haluli.

cathedral n kanisa kuu la dayosisi.

catheter n (med) katheta: neli ya kuingiza uoevu katika mishipa ya mwilini.

cathode n (phys) kathodi.

catholic adj pana (wa mawazo, mitazamo n.k.). the ~ church n Wakristo wote. Roman C ~ n Mkatoliki. C ~ism n ukatoliki, mafundisho na imani ya dini ya Katoliki.

ca-o'nine-tails n kato la ncha tisa; kiboko, mjeledi.

catsup n see ketchup

cattle n (pl oxen) ng'ombe (sl). head of ~ kundi la ng'ombe. ~ cake n mashudu. ~ grid n kizuio cha ng'ombe: shimo barabarani linalofunikwa na vyuma linaloruhusu gari kupita lakini si ng'ombe. ~ trespass n kuingia kwa mifugo (kusiko halali). ~ man n mchungaji wa ng'ombe. ~ pen/~ shed n zizi, boma la ng'ombe.

catty adj (used esp. of a woman)

-enye chuki ya kichini chini. cattiness n.

cavalier

Caucasian n wa jamii/asili ya Kihindi -Kizungu.

caucus n 1 mkutano (wa siri) wa wanachama wa kuchagua wagombea viti.

caul n (physiol) tandabui, zalio. born with a ~ (fig) -enye bahati.

cauldron n sufuria kubwa, jungu kubwa.

cauliflower n koliflawa: aina ya

kabichi.

caulk vt (naut) kalafati.

cause n 1 asili, chanzo the ~ of

the fire was carelessness chanzo cha moto ule kilikuwa ni uzembe. 2 sababu there is no ~ for anxiety hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi. 3 kusudi, ajili fight in the ~ of justice pigana kwa ajili ya haki. 4 (leg) kesi, daawa. ~-list n (leg) orodha ya kesi vt sababisha. ~less adj bila sababu. causation n 1 usababisho; kusababisha. 2 wiano wa sababu. causative adj -a kuleta, -a kufanyiza, -a kutendesha, -a kusababisha.

causerie n 1 mjadala usio rasmi.

causeway n barabara iliyoinuka juu

kidogo (hasa kupitia maji au kinamasi).

caustic adj 1 -enye kuchoma kama

moto, -a kuunguza ~ soda magadi. 2 (of words) -kali, -chungu, -a dhihaka n namna ya dawa ichomayo bila moto, kwa mfano magadi. ~ally adv.

cauterize vt (med) choma kwa chuma au dawa kali (ili kuondoa vijidudu mwilini), tia pisho; unguza. cautery; cauterization n.

caution n 1 uangalifu, hadhari,

tahadhari. 2 onyo; shauri. 3 (sl) mchekeshaji ~ money arubuni vt onya; tahadharisha. cautious adj -angalifu, -enye hadhari. cautiousness n. cautiously adv. ~ary adj -a kushauri/onya.

cavalcade adj maandamano ya wapanda farasi.

cavalier n (arch) mpanda farasi

cavalry

mvulana adj 1 -fidhuli, -a kiburi, -a kutakabari. 2 (arch) kunjufu.

cavalry n 1 askari farasi. 2 kikosi cha

magari ya deraya n.k.

cave n 1 pango; shimo (kwenye mwamba/kilima). 2 tundu. vi ~ in 1 achia, poromoka; poromosha; bomoka. 2 (surrender) shindwa, salimu amri. ~-dweller n. mtu aishiye mapangoni agh wa zamani. ~ -man n mkazi wa mapangoni; mshenzi.

caveat n 1 (leg) uahirishaji wa kesi.

2 (formal) tahadhari; kivuo.

cavern n (lit) pango, shimo. ~ous adj.

cavil vi ~ (at) lalamika; laumu, kosoa bila msingi. ~ler n.

cavity n pengo, kijishimo, mvungu.

cavort vi (colloq) chacharika, rukaruka.

caw vi lia (kama kunguru). n mlio wa kunguru.

cayenne, (~pepper) n pilipili kichaa, mwachaka.

cease vi,vt koma; isha, acha, hulu. ~ from komesha, simamisha. without ~ kwa mfululizo. ~-fire n kusimamisha mapigano/vita; kukoma kwa vita. ~less adj -isiyo na/bila mwisho, -a daima. ~ lessly adv.

CCM n (abbr of) Chama Cha Mapinduzi.

cedar n seda: mti wa mbao aina ya mkangazi.

cede vt toa kwa mwingine (haki, ardhi n.k.), achia.

ceiling n 1 dari; (of boat) darumeti. 2 kikomo cha juu (bei, mshahara, kuruka kwa ndege).

celebrate vt,vi 1 adhimisha, sherehekea. 2 sifu, heshimu, tukuza. 3 ainisha (misa). ~d adj maarufu. celebrant n (rel) padri (aongozaye misa maarufu); kasisi afanyaye Ushirika Mtakatifu. Concelebrant n (mapadri) kusoma misa kwa pamoja. celebration n maadhimisho, sherehe. celebrity n. umaarufu, umashuhuri; mtu maarufu, mashuhuri.

celerity n wepesi.

celery n figili.

celestial adj -a mbingu;-a peponi.

The C~ Empire n Ufalme wa China.

celibacy n useja, ujane (hasa

kwa misingi ya dini). celibate n mjane, mseja, mtu asiyeoa, (hasa kasisi) adj kapera; -a ujane.

cell n 1 seli, chumba kidogo (hasa

katika gereza n.k.). 2 kijumba cha sega. 3 seli, chembe ya uhai living ~ chembe hai single living ~ chembe moja hai the brain ~s ubongo. 4 (electricity) betri, jiwe. dry ~ n seli umeme kavu. electric ~ n seli umeme. 5 (of a party) shina ~ leader mjumbe, balozi. ~ular adj 1 -enye seli. 2 -enye vitundu vitundu vidogo; -a vitundu tundu.

cellar n sela: ghala iliyo chini ya ardhi. ~age n 1 ushuru wa kukodi sela. 2 ukubwa wa sela.

cello n selo: vailini kubwa. ~ist n mpiga selo.

cellophane n selofeni: aina ya karatasi

ya plastiki.

celluloid n 1 seluloidi; aina ya

plastiki. 2 filamu.

cellulose n selulosi: tishu iundayo sehemu kubwa ya mti na mmea.

Celsius n selisiasi.

cement n 1 saruji. 2 (in teeth etc)

sementi. vt tia sementi juu/ndani ya; unga kwa sementi; (fig) imarisha, unganisha. ~friendship imarisha urafiki. ~ation n. ~ mixer n kichanganya saruji.

cemetery n makaburini, mavani, maziara.

cenotaph n mnara wa kumbukumbu

ya wafu (waliozikwa kwingine).

cense vt 1 fukiza. 2 fanya ibada kwa kufukiza. ~r n chetezo.

censor n 1 mkaguzi (wa vitabu,

filamu n.k.). 2 mdhibiti. 3 (ancient Rome) afisa anayehesabu wafu na kusimamia maadili ya taifa. vt kagua, ondoa sehemu za kitabu n.k. ambazo zinadhaniwa zina walakini.

~ial adj. ~ship n ukaguzi, udhibiti. ~ious adj -kali, dodosi, -a kutafuta makosa/kasoro.

censure n lawama; karipio motion of ~ hoja ya lawama pass ~ laumu. vt laumu; karipia; kosoa. ~ (for) laumu; kwa. censurable adj.

census n sensa; hesabu ya idadi ya

watu.

cent n 1 senti. 2 per ~ n asilimia five per ~ tano kwa mia, asilimia tano agree one hundred per ~ kubali kabisa.

centaur n kentauro: mnyama wa hadithini aliye nusu binadamu nusu farasi.

centenary/centennial n miaka mia; sikukuu ya ukumbusho ya kila mwaka wa mia; kipindi cha miaka mia adj -enye miaka mia; -a baada ya miaka mia. centenarian n mzee mwenye umri wa miaka mia au zaidi adj -enye miaka mia au zaidi.

center n see centre.

centering/centring n kishikiza tao.

centigrade adj sentigredi, -enye

digrii 100.

centimetre/centimeter n sentimita: kipimo cha sehemu moja kwa mia ya mita.

centipede n tandu.

centre n 1 kati, katikati at the ~

of the town katikati ya mji; (fig) sehemu muhimu sana. ~ of gravity n kitovu cha mvutano. 2 kituo; kitovu. health ~ n kituo cha afya. 3 kiini ~ of the question kiini cha swali ~ of the fruit kiini cha tunda. 4 ~ of interest mtu anayevutia au mahali panapovutia. 5 msimamo wa kati; wale wenye msimamo wa kati (kisiasa, kidini, kifalsafa). vt 1 weka/chukua katikati; -wa katikati. 2 lenga; waza all eyes were ~d on the teacher macho yote yalimlenga mwalimu ~ one's hopes on something weka matumaini yote juu ya jambo fulani. 3 -wa katikati. centric(al) adj. centricity n (tech). ~-bit n kitoboleo, kekee. ~-fold/ ~

ceremonious

spread/ ~-piece n pambo la katikati ya meza. ~ -spread n kurasa mbili za katikati za gazeti. central adj -a katikati; hasa karibu na katikati; (principal) -kuu; -a maana. central registry n masijala kuu. central heating n upashaji joto katika mabomba (kutoka kituo kikuu) central committee kamati kuu. the central government n serikali kuu (US) kituo cha simu. centralism n mfumo wa mamlaka kutoka sehemu moja, mfumo katikati, ukatikati. centralize vt,vi leta/weka katikati; weka chini ya makao makuu. centralization n.

centrifugal adj pewa; kirukia pewa: mwendo unaoelekea nje. ~ force n kani nje, -enye kuelekea nje ya nukta. centrifuge n mashinepewa.

centripetal adj tovu ~ force n kani tovu -enye kuelekea ndani ya nukta. ~ acceleration n mchapuko kitovu.

centring n see centering.

centrist n mwanasiasa mwenye msimamo wa kati.

century n 1 karne. (muda wa miaka mia). 2 (in cricket) mabao 100.

ceramic adj -a ufinyanzi; -a vyombo vilivyofinyangwa; -a kauri. ~s n 1 vyombo vya udongo. 2 sanaa ya ufinyanzi. ceramist n mfinyanzi.

cereal n 1 nafaka k.v. mahindi, ngano n.k. 2 chakula cha nafaka (hasa cha kifungua kinywa) adj -a nafaka.

cerebral adj 1 -a ubongo. 2 -enye kutumia akili tu. ~ palsy n (med) ugonjwa wa kupooza. cerebellum n

ubongonyuma. cerebration n ufanyaji kazi wa ubongo, kufikiri. cerebro-spinal adj (anat) -a ubongo na uti wa mgongo. cerebro-spinal meningitis (fever) n homa ya uti wa mgongo. cerebrum n ubongombele.

ceremonious adj 1 -a sherehe; -a ibada, -a mviga. 2 -a kupenda utaratibu/itifaki/uungwana. stand on ceremony shikilia mno utaratibu. ceremony n 1 mviga/utaratibu/ vitendo maalumu (agh. vinavyo-

cerise

ambatana na dini/ibada n.k.) katika sherehe (k.v. arusi, maziko, uzinduzi wa jengo, tambiko nk.). 2 kawaida za desturi na za kiungwana. Master of ceremonies n Mfawidhi wa sherehe. ceremonial adj -a kufuata utaratibu maalum (hasa wa dini, ibada n.k.) rasmi, -a sherehe. n utaratibu rasmi, sherehe n.k., taadhima, utaratibu. ~ness n.

cerise adj -enye rangi nyekundu isiyoiva.

cert n (sl) kitu chenye uhakika see

certain.

certain adj 1 yakini, -a hakika, bila

shaka make ~ hakikishia feel ~ -wa na uhakika for ~ kwa yakini, hakika. 2 fulani a ~ place mahali fulani a ~ man mtu fulani. 3 kidogo; kiasi there was a ~ doubt about his health kulikuwa na shaka kidogo kuhusu afya yake to a ~ degree kwa kiasi fulani. 4 (fixed) maalum. 5 (inevitable) -a hakika; hapana budi he is ~ to go ana uhakika wa kwenda he is ~ to die ni lazima afe. ~ly adv bila shaka. ~ly not! la hasha, katu! hata! ~ty n 1 hakika, yakini it is a dead ~ty ni hakika kabisa, hakuna shaka yoyote. 2 jambo linalokubalika; jambo linaloelekea kuwa hakika. for a ~ty kwa hakika.

certificate n 1 hati (ya uthibitisho)/ cheti ~ of birth, marriage etc. cheti cha kuzaliwa ndoa n.k. degree ~n shahada. vt -toa cheti/hati n.k. ~d adj iliyohitimu. certify vt,vi hakikisha, thibitisha this is to ~ that hii ni kuthibitisha kwamba. certifiable adj -a kuthibitika (agh. kwa kutoa hati) certifiable as a lunatic -a kuweza kuthibitika kuwa na wazimu. certified cheque n hundi halali he was certified insane alithibitishwa kuwa mwenda wazimu. vi (to) certify toa ushahidi kuwa kitu ni sahihi.

certitude n (formal) yakini, uhakika. cerulean adj (formal) -a (rangi ya) samawati, -a buluu.

cervix n (anat) mlango wa kizazi. cervical adj.

cess n kodi, ushuru, (agh. wa mazao).

cessation n kukoma; kuacha (kwa muda) ~ of hostilities kuacha kupigana/uhasama.

cession n (leg) 1 kutoa, kuachia kwa mapatano. 2 kilichoachiliwa, kilicho-tolewa.

cesspit n (also cesspool) n 1 shimo la maji machafu. 2 (fig) mahali pachafu ~ of iniquity mahali palipojaa maovu.

chafe vt 1 chua, sugua (ngozi n.k. ili kupasha moto). 2 chubua, kwaruza vi (fig) ona udhia, ghadhibika, -wa na hasira ~ under insults udhika kwa sababu ya matukano. n hasira, uchungu.

chaff1 n 1 kapi, kumvi, wishwa. 2

majani yaliyokatwa na kukaushwa kwa chakula cha ng'ombe, farasi n.k. 3 kitu cha bure. vt kata majani kwa ajili ya chakula cha mifugo. ~ -cutter n kikataukoka.

chaff2 n utani; mzaha. vt tania; fanyia

mzaha.

chaffinch n kurumbiza: aina ya ndege aimbaye.

chaffing-dish n kipashamoto.

chagrin n hangaiko/uchungu wa moyo (kwa sababu ya kushindwa, kufanya kosa n.k.). vt huzunisha.

chain n 1 mnyororo; mkufu. in ~s kifungoni au utumwani. 2 mfuatano/ mfululizo/mtungo, mlolongo wa mambo, vita, matukio n.k. ~ of mountains (lakes, villages etc) safu ya milima, maziwa, vijiji n.k. 3 kipimo cha urefu wa futi 66 vt funga (kwa mnyororo). ~-gang n. kikundi cha wafungwa (waliofungwa minyororo wakifanya kazi). ~ letter n barua -mkufu: barua maalum ambayo mpokeaji huombwa kutoa nakala na kuzipeleka kwa watu wengine ambao nao hufanya vivyo hivyo. ~-mail n deraya. ~-smoker n mvutaji sigara kwa mfululizo (akizima anawasha nyingine). ~

chair

stitch n mshono - mkufu. ~-stores n mtungo wa maduka (ya tajiri mmoja). ~ reaction n mlipizano/mjibizano. ~ saw n msumeno wa mnyororo.

chair n 1 kiti. 2 kiti, mahali au cheo; mwenyekiti; uenyekiti address (appeal to) the ~ elekeza mazungumzo kwa mwenyekiti. take the ~ shika uenyekiti; -wa mwenyekiti. 3 nafasi na kazi ya profesa. 4 (US) electric ~ kiti cha kuua. vt 1 ongoza (mkutano). 2 chukua mtu kitikiti (agh. kwa shangwe); beba juu. ~man/ ~ person n mwenyekiti, kinara. ~manship n uenyekiti.

chalet n 1 nyumba ndogo hasa katika milima ya Uswisi. 2 nyumba ndogo katika kambi ya kupumzikia.

chalice n (rel) 1 kalisi: kikombe maalum cha divai kitumiwacho wakati wa ibada ya Kikristo. ~ veil n kifuniko cha kalisi.

chalk n 1 chaki; chokaa. ~-pit shimo la chokaa. he does not know ~ from cheese mbumbumbu. better by a long ~ bora zaidi. as different/ like as ~and cheese tofauti kabisa. vt 1 paka chaki, fanya alama kwa chaki. 2 ~ up weka rekodi; (of sport) pata. 3 ~ out eleza kwa jumla. by a long ~ kwa mbali sana. ~y adj.

challenge vt 1 ita kuja kushindana (katika michezo n.k.), karibisha kwenye mashindano. 2 (mil) simamisha na kudai jina. 3 (leg) pinga, kana, bisha. 4 taka sababu za kuthibitisha shauri au neno. 5 tania; toa changamoto this situation is a ~ to the government hali hii ni changamoto kwa serikali. n 1 mwito wa kuja kushindana issue a ~ ita kuja kushindana. 2 neno la kukaidi, kubishana. 3 ulizo la mlinzi (k.m. Ni nani anayekuja?). 4 kichocheo. 5 chochezi. ~r n mpinzani.

chamber n 1 (arch) chumba (hasa cha kulala). 2 (pl) chumba cha jaji (cha kusikizia kesi); (not US) vyumba

vingi katika jengo kubwa. 3 baraza la wabunge. Upper C~ n baraza la juu (seneti). 4 Ofisi za wanasheria (hasa katika mahakama). 5 chama. C~ of Commerce n chama cha wafanya biashara. 6 chemba (nafasi ndani ya mwili wa mnyama au mmea) nasal ~ chemba ya pua. ~lain n (old use) msimamizi mkuu wa nyumba yamfalme; mtunza mali. ~ of horrors n chumba cha maonyesho ya vitu vya kuogofya. ~-maid n mhudumu wa kike (aandaliaye vyumba vya kulala hotelini). ~ -pot n chombo cha kuendea haja.

camelion n 1 kinyonga, lumbwi. 2

kigeugeu.

chammy-leather n see chamois leather.

chamois n (pl chamois) swala. ~ leather (also chammy/ shammy leather) ngozi laini (ya swala, mbuzi kondoo) (agh. hutumika kung'arishia vitu, hasa magari).

champ vt,vi (of horse) tafunatafuna

chakula au lijamu kwa sauti. (fig) ~(at the bit) -tokuwa na subira, -wa na harara. n (sl) see champion.

champagne n shampeni.

champaign n mbuga, tambarare.

champion (also champ) n 1 bingwa,

mshindi (wa mashindano ya mbio, ngumi n.k.); shujaa. 2 mtetezi, mgombea. vt tetea, pigania, saidia, linda adj (colloq) bora, -a kwanza, -a kupita ingine. ~ship n ubingwa, ushindi, mashindano.

chance n 1 bahati by (any) ~ kwa bahati a happy ~ bahati njema. 2 nasibu a game of ~ bahati nasibu. 3 (opportunity) nafasi he lost his ~ alipoteza nafasi yake the ~s are against me inaelekea nitashindwa. 4 (probability) uwezekano: there is no~ of it haiwezekani; si yumkini an off ~ matumaini kidogo. take one's ~ jaribu bahati. the main ~ nafasi ya kupata pesa. vt 1 (risk) bahatisha; jaribu I'll ~ it

chancel

nitabahatisha. 2 tukia, kuta kwa bahati ~ upon kuta if I ~ to see him nikibahatika kumwona it ~d that ilitokea kwamba. chancy adj (colloq) -a hatari; mashaka; -sio ya uhakika.

chancel n (rel) sehemu ya wanakwaya na makasisi kanisani.

chancellery 1 nafasi/idara/nyumba ya Mkuu. 2 ofisi ya ubalozi.

chancellor n 1 Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu (k.m. katika Shirikisho la Ujerumani). 2 Mkuu wa Chuo Kikuu the. C~ of the Exchequer n (GB) Waziri wa Fedha. The Lord High C~ n Jaji Mkuu wa nchi (katika Uingereza). 3 (GB) Katibu Mkuu wa Ubalozi. ~ship; ~ry n.

chancery n 1 mahakama kuu katika

Uingereza inayoshughulikia haki na usawa. 2 masijala ya nyaraka za umma.

chancre n kidonda (agh.cha kaswende).

chancrous adj.

chandelier n shada la taa zenye

mapambo linaloning'inia.

chandler n mwuzaji (au mtengenezaji) mishumaa, sabuni, mafuta n.k. ship's ~ mwuza kamba na zana za meli.

change vt,vi 1 badili; badilisha; geuza; geuka. ~ step badili mwendo, badili hatua ~ one's mind ghairi. the property ~d hands mali iliuzwa kwa mwingine. 2 vunja, chenji ~ a 100 shillings note vunja noti ya shilingi mia moja. 3 ~ up/down badili gia. ~into geuka. n 1 mageuzi, mabadiliko; mabadilisho; badiliko ~ of administration mabadiliko ya utawala. 2 kitu cha lazima ili kugeuza/kubadili; kitu cha kubadilisha take a ~ of clothes with you chukua nguo za kubadili for a ~ kwa kubadilisha hali/mambo get no ~ out of (somebody) (colloq) kutopata msaada wowote. 3 (coins) senti, kichele; (fig) get ~ out of somebody -mlipia/lipiza kisasi. 4 baki no ~ given hakuna baki/chenji. ~able adj -a kigeugeu, -a kuweza kubadilika badilika, badilifu; -a

kuelekea kubadilibadili. ~less adj. ~ ableness; ~ability n ugeuzo, ugeukaji. ~ful adj. ~ling n 1 kubadilisha mtoto mzuri kwa mbaya (kwa siri). 2 (in traditional stories) mtoto mbaya/mjinga, kioja aliyebadilishwa na mwingine aliyeibiwa.

channel n 1 mlangobahari. 2 mlizamu, mfereji, mfumbi. 3 njia (ambayo kwayo habari, mashauri n.k. yaweza kupitia) follow the proper ~s fuata ngazi (zilizowekwa). 4 mkanda. 5 (radio, TV) idhaa; bendi. vt 1 chimbua/elekeza mfereji. 2 (fig) elekeza he ~ed his abilities into business alielekeza uwezo wake kwenye biashara.

chant vt imba ~ somebody's praises (fig) sifia, sifu fulani kila mara. n 1 mkarara, uimbaji wa zaburi. 2 (of crowd) kurudia kuimba.

chantry n wakfu.

chanty n (also shanty) wimbo wa

kuvutia makasia.

chaos n machafuko, vurumai, vurugu, fujo. chaotic adj. chaotically adv.

chap1 vi,vt chubuka, pasuka; chubua, pasua the skin of my hands is ~ped ngozi ya mikono yangu imepasuka. n mchubuko.

chap2 n (sl) mtu (mwanamme), jamaa a funny/queer ~ mtu wa ajabu young ~ kijana a good ~ mtu mwema.

chap3 n taya ya chini (hasa ya mnyama k.m. nguruwe); mashavu. lick one's ~s ngojea kwa shauku/hamu kubwa. ~/crest fallen adj -lokata tamaa, -sohali.

chapel n 1 kanisa dogo. 2 (arch) kanisa la wasio Waanglikana au Wakatoliki; ibada katika kanisa hilo. 3 tawi la chama cha wafanyakazi wapiga chapa. ~goer n.

chaperon n mchunga/mtunza mwari, somo. vt fuatana na msichana mahali asiporuhusiwa kwenda peke yake.

chaplain n kasisi (wa jeshi, Chuo Kikuu n.k.). ~cy n.

chaplet

chaplet n 1 taji la maua. 2 tasbihi. 3

mtungo wa shanga.

chapman n mchuuzi.

chapter n 1 sura; mlango, somo a ~ of accidents mfululizo wa ajali to the end of the ~ mpaka mwisho kabisa wa mlango. ~ and verse rejeo kamili. 2 (rel) mkutano wa mapadri. 3 tawi, kikundi cha chama n.k. 4 enzi.

char1 vi safisha nyumba, ofisi n.k. kwa malipo ya saa au siku. ~-woman; ~-lady n mwanamke mnadhifishaji: mwanamke anayelipwa kusafisha nyumba. vt unguza. vi ungua mpaka kuwa mkaa, fanya/kuwa nyeusi kwa kuungua.

char2 n (sl) chai.

charabanc n basi (linalotumika kwa

safari za burudani).

character n 1 tabia; moyo; silika ya mtu, hulka. in/out of ~ ilio/isio kawaida (ya mtu fulani) he has a bad ~ana tabia mbaya. 2 sifa bainifu. 3 unyoofu, ukunjufu wa moyo takes ~ to speak the truth always inahitaji unyoofu kusema kweli daima. 4 mtu wa ajabu; wa tabia za kiajabu/kipekee that man is a real ~ mtu yule ni wa ajabu. 5 mhusika (katika riwaya, tamthiliya n.k.). 6 herufi in large ~s kwa herufi kubwa. 7 (arch) uthibitisho wa sifa zilizobainishwa. ~less (derog) bila sifa; -a kawaida. ~istic adj -a kawaida/tabia (ya mtu, kikundi) it is ~istic of him to ask for money ni kawaida yake kuomba hela n sifa bainifu what are the ~istics of a savannah plain? Ni nini sifa bainifu za ukanda wa savana? ~ization n (lit) uchoraji, uumbaji wa mhusika (katika riwaya n.k.); ubainishaji wa tabia. ~ize vt 1 eleza sifa (tabia, kawaida), ainisha. 2 -wa kawaida ya, -julikana kwa his work is characterized by sloppiness kazi yake huonyesha uzembe, the indigenous cow is ~ized by its hump ng'ombe wa kienyeji ajulikana kwa nundu yake.

charge' d'affaires

charade n (usu pl) ~s n mchezo wa

kukisia neno kutokana na viigizo bubu; (fig) kitendo kisicho cha maana, kitendo cha kupotosha ukweli/cha uongo.

charcoal n 1 mkaa, makaa. ~ burner n mchoma makaa; sigiri.

chard n Swiss ~ n mchadi:aina ya kiazi sukari ambacho majani na shina lake huliwa.

charge1 vt,vi 1 shtaki. ~ somebody (with) shtaki mtu kwa. 2 (attack) shambulia, rukia, endea kwa nguvu. 3 (load) shindilia fataki; pakia chomboni; tilia, jaza (pomoni). 4 (demand price) toza, dai malipo. he ~ed me twenty shillings alinitoza shilingi ishirini. 5 (with responsibility) kabidhi, dhaminisha, -pa jukumu au wajibu, -wa na dhima he ~d himself the task of looking after our school alichukua dhima ya kuiangalia shule yetu. 6 (command, instruction) amuru, lazimisha, agiza the judge ~d the jury jaji aliwaamuru wazee wa baraza. 7 (of battery) chaji. 8 dai he ~d that I don't work alidai kwamba sifanyi kazi. 9 ~ up to rekodi, weka. ~able adj -a kutozwa; -a kushtakiwa; -a kuweza kulaumiwa. ~d adj -liochemka; nyeti face a ~ jibu mashtaka, kabiliwa na mashtaka. ~- sheet n kitabu cha mashtaka.

charge2 n 1 shtaka bring a ~ fungulia shtaka, shtaki. 2 shambulio the soldiers made a sudden ~ askari walifanya shambulio la ghafla. 3 bei, malipo. ~ account n akaunti ya malipo. 4 mshindilio, fataki, kiasi cha baruti au cha umeme katika chombo cha kuwekea nguvu za umeme; marisau. 5 wajibu, madaraka. put somebody/be in ~ (of) kabidhi pesa madaraka. take ~ twaa madaraka. 6 maagizo, maelekezo. 7 take/give somebody in ~ peleka mtu polisi/ shtaki.

charge' d'affaires n balozi mdogo,

kaimu balozi.

charger1 n 1 (arch) farasi (wa ofisa mwanajeshi).

charger2 n (arch) sahani kubwa, sinia.

chariot n kibandawazi (cha kukokotwa na farasi). ~eer n dereva wa kibandawazi.

charisma n 1 haiba kubwa. 2 kipaji (kitolewacho na Mungu). ~tic adj.

charity n 1 sadaka. live on ~ ishi kwa sadaka. a ~ ball densi la kuchangisha fedha kusaidia maskini. ~ walk n matembezi ya hisani (ya kuchangia fedha). 2 wema, fadhila, hisani, huruma. out of ~ kwa moyo, kwa wema. 3 shirika au chama cha kusaidia wenye shida. ~ begins at home (prov) wema wa mtu huanza kwao. charitable adj 1 -enye huruma, -enye fadhila, -enye hisani. 2 (of institutions etc.) -a kutoa msaada. charitably adv.

charivari n kelele nyingi (za sauti

mchanganyiko).

charlady n see char1

charlatan n tapeli, laghai, mjuvi. ~ry n.

charlock n (bio) mharadali mwitu. charm n 1 ucheshi, uzuri, haiba, mvuto. 2 hirizi, talasimu, kago, fingo. vt 1 (attract) vuta kwa uzuri/mapenzi n.k.; sisimua, furahisha, pendeza kwa wema. I'm ~ed to see you! nimefurahi sana kukuona. 2 roga, fanyia uchawi. ~er n 1 mchawi. 2 mtu mcheshi, mtu mwenye haiba. snake ~er n mcheza na nyoka. ~ing adj -cheshi, changamfu. ~ingly adv.

charnel-house n nyumba ya kuhifadhia maiti au mifupa.

chart n 1 ramani (inayotumiwa na

mabaharia), chati. 2 chati (yenye michoro, jedwali n.k.). vt 1 chora ramani; onyesha katika chati. 2 chunguza hali ya safari baharini. 3 sawiri mawazo.

charter n 1 hati; mkataba; idhini. ~ member n mwanachama mwanzilishi the Great C ~ (Magna Carta) Hati

chatter

ya Haki za Binadamu. ~ed accountant n (GB) mhasibu msajiliwa. ~ed bank n benki yenye idhini. 2 kukodi meli, ndege n.k.. vt kodi chombo; idhinisha. ~-party n (comm) mapatano ya kukodi (chombo, meli n.k.).

charterhouse n nyumba ya watawa. charwoman n see char1.

chariness n hadhari. charily/chary adj -enye hadhari, -angalifu. chary (of) -woga (wa).

chase1 vt,vi 1 fukuza, kimbiza. give ~ (to) kimbilia, saka, fuata, kimbiza, fukuza. 2 ~ away/off fukuza. 3 ~down/up jaribu kupata. 4 ~ about kimbiakimbia (colloq) n msako. goon a wild goose ~ tafuta kitu bure (bila tumaini la kufaulu), ufukuzaji.~r n 1 msakaji. woman ~r n mfukuzia mabibi. 2 farasi mruka viunzi.

chase2 n 1 fremu, nakshi, mfuo. 2

(of gun) kasiba. vt tia temsi/nakshi.

chasm n shimo kubwa, genge, ufa

mkubwa, korongo; (fig) tofauti kubwa iliyopo baina ya hisia za watu.

chassis n (pl) 1 chesisi, kiunzi, fremu ya chombo km. gari, redio n.k.

chaste adj 1 -siozini; bikira, safi. 2 - siyopambwa, sahili. ~ly adv. chastity n.

chasten vt 1 (discipline) rudi; hidi, taadibu. 2 pambua, zima, nyosha.

chastise vt adibu, tia adabu. ~ment n. chasuble n (rel) kasula.

chat vi 1 ongea, piga soga/

gumzo, porojo. 2 ~ somebody up tongoza; piga porojo. ~ty adj -ongezi, -gumzi. n maongezi, mazungumzo; soga, porojo have a ~ zungumza.

chateau n kasri, ngome.

chattel n mali inayohamishika (km.

viti, gari n.k.).

chatter vi 1 payapaya, bwabwaja, payuka, ropoka. 2 lia/toa sauti kama tumbili, ndege n.k. 3 tatarika (k.m meno kwa baridi au hofu). n 1

mpayuko, mbwabwajo be involved in idle ~ piga domo. 2 (of machine) mtatariko. ~box; ~er n mpayupayu, mpayukaji, mlimi.

chauffeur n dereva, mwendeshaji

wa motokaa (wa mtu binafsi).

chauvinism n 1 uzalendo pofu. 2

ujinsia. chauvinist n. chauvinistic adj.

chaw vt (vulg) tafuna. ~-bacon n

mshamba.

cheap adj 1 rahisi, bahasa. go ~ uzwa rahisi. on the ~ (colloq) rahisi, bila shida, kwa bei tupa. 2 hafifu, isiyo na thamani, duni. ~jack adj hafifu, duni. 3 -sio ungwana; -sio staarabu; -sio aminifu. feel ~ ona haya/aibu. hold ~ dharau, dunisha. make oneself ~ jihakirisha, jishusha hadhi, jidhalilisha. 4 -a kilemba cha ukoka. ~ flattery kilemba cha ukoka. 5 ~ gibe utani mbaya n urahisi (of price) dirt ~ rahisi mno. ~ly adv kwa urahisi he got off ~ly aliupatia. ~ness n. ~en vt, vi shuka/shusha thamani, pungua/punguza bei. 2 vunjia heshima, dhalilisha, fakirisha don't ~ yourself usivunje heshima yako, usijivunjie heshima, usijidhalilishe. ~skate n (sl) bahili; mnyimi.

cheat n 1 mdanganyifu, laghai. 2 udanganyifu, hila. vt,vi 1 danganya, laghai, hadaa, kenga. 2 (of shopkeeper) punja. 3 (in exam) iba, ibia.

check1 vt 1 cheki, pima usahihi, peleleza, angalia kwa makini. 2 zuia, simamisha. 3 ~ something off tia alama ya kuonyesha usahihi, usawa. ~ something up. ~ up on something kagua au linganisha kupata usahihi. ~ up on somebody chunguza usahihi wa sifa/madai ya mtu. 4 (US) weka, hifadhi (mzigo, bahasha, koti) chini ya ulinzi. 5 ~ in jiandikishe (hotelini, kazini) kwamba umefika. 6 ~out ondoka, aga; toa (kwa mfano kitabu maktabani). ~ over kagua, angalia.

cheer

~er n 1 kitu/mtu anayecheki. 2 mtu anayepokea mizigo n.k. 3 mpokea hela (dukani n.k.). 4 (US) (pl) dama. ~er-board n (US) bao la mchezo wa dama au sataranji. n 1 zuio, kizuio; udhibiti. hold somebody in ~ zuia. ~s and balances taratibu za vyombo vya dola kudhibitiana ili kuzuia matumizi mabaya ya madaraka. 2 usahihi, kupima, kusahihisha; kuhakiki. ~ list n orodha ya kupimia/kukagulia. ~point n kituo cha ukaguzi wa magari/mashindano n.k. ~ up n (med) kupimwa. 3 tikiti, cheti, risiti, stakabadhi ya uthibitisho wa kuwekea kitu. ~room n chumba cha mizigo. 4 hundi. bad ~ n hundi batili. ~ book n kitabu cha hundi. 5 (chess) ~ mate n kushindwa kabisa. vt shinda (fig) zuia na shinda.

check2 n mirabamiraba; kitambaa cha

kunguru adj -a milia, -a miraba.

cheek n 1 shavu. ~ by jowl iliokaribiana; -naoshirikiana. turn the other ~ -tolipiza kisasi. ~bone n kituguta, kitefute. 2 tako. 3 (impudence) usununu, ufidhuli, usafihi. ~y adj -enye kiburi, fidhuli, safihi. ~ly adv kitefute. vt safihi, fanyia ufidhuli.

cheep vi lia (kama makinda ya ndege yaliavyo). n mlio wa namna hii.

cheer n 1 (arch) hali ya kuwa na

matumaini, furaha be of good ~ furahia, changamka. 2 (old use) good ~ vyakula na vinywaji vizuri. 3 ukelele wa kufurahia, kushangilia, kusifu, kutia moyo au bidii. ~ leader n kiongozi wa mashabiki (wakati wa mashindano). 4 kwa afya yako: msemo wa kunywa na kutakia heri/afya. ~y adj -a furaha, -changamfu, -kunjufu, -a bashasha. vt, vi 1 ~ somebody (up) changamsha, fariji. 2 ~ (on) shabikia kwa nguvu. ~ful changamfu. ~fulness n. ~less adj -a huzuni, bila chochote cha kufurahisha, -liosonona.

cheerio

cheerio (int) (at parting) kwa heri;

buriani.

cheese1 n jibini, chizi. 2 (sl) picha ya mwanamke mzuri. ~cloth n shashi. ~monger n mchuuza jibini. ~ paring n ubahili uliokithiri. cheesy adj -a jibini, -enye jibini; kama jibini; (sl) duni; hafifu. ~ cake n keki ya jibini; (sl) picha ya umbile la kiwiliwili cha mwanamke.

cheese2 vt (sl) ~off chosha, udhi sana. say ~ cheka.

cheetah n duma.

chef n mpishi mkuu (katika hoteli).

chef- d' oeuvre n kazi bora kabisa (ya

msanii n.k.).

chemical adj -a kemia. n kemikali; madawa.

chemise n (arch) shimizi.

chemist n 1 mkemia; mtaalam wa kemia. 2 mfamasia.

chemistry n kemia

chemotherapy tibakemikali.

chenille n uzi wa mahameli

(unaoshonewa kupambia mavazi na samani).

cheque n cheki, hundi; (draft) hawala. cross a ~ funga hundi. travellers ~ n hundi ya wasafiri. dishonoured ~ n cheki iliyokataliwa. ~-book n kijitabu cha hundi.

chequer n 1 ruwaza yenye miraba ya rangi tofauti. 2 ~ed cloth n nguo yenye mirabaraba. vt tia/andika mirabaraba kwa rangi tofauti. ~ed career n maisha ya kupanda na kushuka.

cherish vt 1 tunza, lea, hifadhi kwa

upendo mkubwa. ~ illusions fuga/ ishi na matumaini/hisia/njozi.

cheroot n biri iliyo wazi pande zote.

cherry n (tree) mcheri; (fruit) cheri

adj -ekundu. ~ lips n midomo myekundu.

cherub n 1 malaika mdogo: mmoja wa makerubini. 2 (of child) mtoto mzuri. ~ic adj.

chess n sataranji, chesi. ~man n kisanamu cha sataranji. ~board n ubao wa sataranji.

chessel n kalibu ya jibini.

chest n 1 kasha, sanduku (la kuhifadhia nguo, fedha, madawa n.k.). ~ of drawers n almari. medicine ~ n sanduku la madawa. 2 kifua; (of animals) kidari. ~ complaint n maumivu ya kifua. get something off one's ~ toa dukuduku. keep/hold one's cards close to one's ~ -wa msiri, bania siri.

cheval-glass n kioo kikubwa (kilichotundikwa).

chevron n tepe ya V (ionyeshayo cheo cha askari cha koplo au sajini).

chew vt vi 1 ~ (up) tafuna. ~ing gum chingamu. bite off more than one can ~ jaribu kuliko uwezo. 2 ~ over; ~ (up) on fikiria, tafakari. ~ the rag (dated sl) jadili mambo (hasa ya magomvi au tofauti za zamani); lalamika. ~ the cud cheua. ~ out (colloq) karipia. n 1 kutafuna. 2 kipande cha tumbaku. ~ed up adj enye wasiwasi sana.

chiaroscuro n msambazo wa mwanga wa vivuli (hasa katika uchoraji).

chic n ulimbwende, umaridadi

adj maridadi, -a kufuata mtindo.

chicanery n ulaghai wa kisheria, hila, werevu, udanganyifu; hoja potofu.

chick n kifaranga (cha kuku), kinda (la ndege); (sl) msichana, kijana.

chicken n 1 kifaranga don't count

your ~s before they are hatched usinunue mbeleko na mwana hajazaliwa. 2 (fig) (also spring ~) msichana mzuri. she is no ~ amezeeka, si kijana. 3 (used mainly by children) joga. ~ hearted/ livered adj joga. ~ out of acha kufanya kwa sababu ya woga. 4 nyama ya kuku. ~ feed n chakula cha kuku; (fig) kitu kisicho na thamani. ~pox n tetekuwanga. ~ -run n uga wa kuku.

chicle n ubani.

chide vt ~ somebody (for) karipia, kemea.

chief adj -kuu, -enye cheo cha juu kabisa. C~ Justice n Jaji Mkuu; -a

chiffon

kwanza (kwa umaarufu). the ~idea wazo kuu. ~ly adv hasa, aghalabu. n 1 mkuu wa kundi; idara au shirika n.k. 2 mtemi, kiongozi, chifu. Commander -in- C~ n Kamanda Mkuu, Amiri Jeshi. C~ of Staff Mnadhimu Mkuu. in ~ /~ly adv hasa, aghalabu. ~tain n mtawala wa jadi, mtemi. ~taincy n utemi.

chiffon n shifoni.

chiffonier n almari, saraka.

chignon n julfa/shungi la kisogoni.

chigoe/chigger n see jigger

chilblain n uvimbe unaotokana na baridi kali (hasa mikononi na miguuni). ~ed adj.

child n 1 mtoto, kijana. ~'s -play n (fig) kazi rahisi be with ~ (arch) -wa mjamzito have a ~ zaa, jifungua. ~ welfare n usitawi wa watoto. ~-bearing; ~ birth n kuzaa, kujifungua. ~ hood n utoto. second ~hood n ukongwe. ~ish adj -a kitoto; -puuzi; jinga. ~ishness n utoto; upuuzi, upumbavu; ujinga. ~less adj bila mtoto; gumba, tasa. ~like adj -a kama mtoto; -nyofu, tiifu, -sikivu. 2 (follower) mfuasi. 3 zao.

chile; chili n see chilli.

chiliad n elfu; miaka elfu moja.

chill n mzizimo take the ~ off something pasha moto kidogo. 2 homa ya baridi. 3 (fig) fadhaa, kuvunjika moyo cast a chill over vunja moyo, poozesha adj 1 -a mzizimo a ~ breeze upepo wa baridi. 2 sio -a kirafiki a ~ welcome makaribisho yasomlahaka. vt, vi 1 tia baridi, zizimisha. 2 (depress) vunja moyo, fadhaisha. 3 zizima, geuka kuwa baridi. ~y adj 1 -a mzizimo. 2 (of person) -baridi, asiye rahisi kufanya naye urafiki.

chilli n (also chilly, chile, chili) pilipili; pilipili hoho.

chime1 n 1 (usu pl) sauti za seti ya

kengele. 2 sauti ya kengele. vt,vi 1 lia; liza kengele, piga kengele; tambulisha saa kwa kugonga. 2 ~ in

ingilia mazungumzo (kwa kukubali) au kuunga mkono ~ in with patana na, lingana na.

chime2 n (of cask etc.) ukingo uliojitokeza.

chimera n 1 (myth) kimaira: mnyama katika hadithi mwenye kichwa cha simba, mwili wa mbuzi na mkia wa nyoka, atokaye moto kinywani. 2

zimwi. 3 wazo/ndoto yoyote ya ajabu sana. chimerical adj -a kubuniwa tu.

chimney n 1 dohani. ~-sweep n msafisha dohani. 2 (of lamp) yai, chemli; (mountaineering) mwanya.

chimpanzee/chimp n sokwe.

chin n kidevu keep one's ~ up (colloq) piga moyo konde. ~ -wag n (colloq) mazungumzo; soga; umbea.

china n 1 kauri. ~ closet n kabati la vyombo. ~ware n vyombo vya udongo. ~-clay n udongo laini mweupe wa mfinyanzi, wa kauri. 2 vyombo (vikombe, sahani, mabakuli) vya kauri.

chine n 1 uti wa mgongo (wa

mnyama). 2 sarara.

chink1 n tundu, upenyu/ufa

mwembamba, mwanya (wa ukuta).

chink2 n mlio (kama wa fedha, glasi

n.k. zikigongana). vt,vi toa mlio (wa fedha, glasi n.k. kwa kuzigonganisha).

chintz n kaliko: kitambaa cha pamba

kilichotiwa rangi (agh. hutumika kwa mapazia na kufunikia samani).

chip vt,vi 1 ~ (off/from) bambua; bambuka; banja. 2 kata vibanzi, chonga. 3 ~ away banduka, meguka. 4 ~ in ingilia kati (mazungumzo); changa, toa mchango. n 1 kibanzi. ~ board ubao wa vibanzi. 2 kokoto. a ~ of the old block mwana anayemshabihi sana baba yake. have a ~ on one's shoulder -wa -kali kutokana na kuogopa/kujiona kudharauliwa/ kudhalilishwa. 3 (gambling) kibao. when the ~s are down mambo yakiiva; mambo yakiwa magumu

sana 4. (usu pl) chipsi fish and ~s chipsi na samaki. 5 (electr) kisilikoni. 6 kindu, upapi. ~ping n (usu pl) kokoto, vibanzi.

chiromancy n utabiri (wa kuangalia

kiganja/kitanga cha mkono, kupiga ramli (kwa kiganja).

chiropody n utabibu wa vitengele vya mguu. chiropodist n tabibu wa vitengele vya mguu.

chiropractor n tabibu maungo: mtaalam wa kurekebisha maungo.

chirp/chirrup n mlio mwembamba (wa ndege au mdudu). vi 1 lia kama ndege au mdudu. 2 ongea kwa uchangamfu. ~y/chirrupy adj -changamfu, -a furaha. ~ily adv. ~iness n.

chisel n patasi; juba. vt 1 kata, chimba, umba (kwa patasi). 2 (sl) danganya, laghai, ghilibu. ~ler n mdanganyifu, tapeli.

chit1 n (sl) 1 kitoto. 2 kisichana.

chit2 n cheti, kinoti, barua ndogo. chitchat n porojo, soga,mazungumzo, maongezi.

chitterlings n utumbo wa nguruwe n.k. unaopikwa.

chivalry n 1 uungwana, adabu; uadilifu. 2 (arch) mila, desturi (za waungwana wa Enzi za Kati). chivalrous adj.

chive n kitunguu jani.

chivy/chivvy vt fuatafuata; sumbua, kera.

chloride n kloridi ~ of lime shabu (hutumika kusafishia maji na kuua vijidudu).

chlorinate vt tia klorini (hasa kwenye maji). chlorination n. chlorine n (chem) klorini.

chloroform n klorofomu; nusu kaputi.vt tia nusukaputi.

chlorophyll n klorofili: kemikali ya

rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea.

chock vi kaza kwa kabari; (boat) zuia kwa kipande cha ubao. ~ up kaza kwa kabari/jaza pomoni. n kigingi, kipande, kabari ya kukuzia. ~-a-

chop

block adj -a kujaa kabisa, pomoni. ~full (of) adj -liojaa kabisa.

chocolate n chokoleti adj 1 -a chokoleti. 2 (colour) kahawia hot ~ kinywaji moto cha chokoleti.

choice n 1 chaguo, uchaguzi my ~ chaguo langu. 2 Hobson's ~ n chaguo lisilo chaguo (kwa sababu hakuna hiari nyingine). 3 haki au uwezo wa kuchagua adj 1 -zuri, bora; -teule, -liochaguliwa kwa uangalifu. 2 (of language) -a matusi. ~ness n.

choir 1 kwaya. 2 eneo la wanakwaya

kanisani. ~-boy; chorister n mwanakwaya. ~master n kiongozi wa kwaya. choral adj -a kuimba au waimbaji ~ service ibada ya kuimba. choral(e) n 1 wimbo rahisi wa kanisani unaoimbwa na kwaya pamoja na waumini. 2 kiitikio, mkarara. 3 kwaya.

choke vt,vi 1 kaba/songa roho, zuia

pumzi, tia kabali. 2 kabwa, paliwa a voice ~ed with sobs sauti ya kwikwi. 3 ~ (up)(fill up) zibwa, jaa kabisa the pipe is ~d up with rubbish bomba limezibwa na takataka. 4 ~ back zuia, ficha (hasira, masikitiko n.k. kwa shida). 5 ~ down meza haraka au kwa shida. 6 ~ off (fig) epua; kemea, karipia. n 1 kukabwa, kupaliwa. 2 (of vehicle) choki. ~-damp n gesi ya kaboni (migodini).

choker n 1 kola iliyosimama. 2 ushanga wa skafu ya kubana shingo.

choky n (sl) jela, korokoro.

choler n (arch, lit.) hasira. ~ic adj.

cholera n kipindupindu, waba.

choose vt,vi 1 chagua, hitari, pambanua pick and ~ chagua.2 amua (baina ya kitu kimoja na kingine). 3 taka, hiari, kusudia whether he ~s or not akitaka asitake. choos(e)y adj angalifu katika kuchagua, gumu kupendeza.

chop1 vt,vi 1 kata, katakata. 2 (of wood) chanja, changa, tema (kuni) ~ping block gogo la kuchanjia kuni.

3 (strike) piga (kuelekea chini). 4 ~ away/off kata; katilia mbali. 5 ~ down chengua. 6 ~ out toa ~ out part of the play toa sehemu ya tamthilia. 7 ~ up katakata, kata vipandevipande. 8 (of wind) badili mwelekeo ghafla. ~ and change badili kila mara (mipango, mawazo n.k.). ~ logic bishabisha (juu ya vitu vidogo). n 1 pigo la kukata. 2 kipande cha nyama chenye mfupa wa mbavu. 3 pigo (la mkono). 4 kishindo cha maji yakirushwa. ~py adj (of the sea) -a mawimbi mawimbi; (of wind) -nayobadilika- badilika. ~per n 1 shoka. 2 (sl) helikopta. 3 (pl) meno. ~ house n hoteli/mkahawa (hasa unaopika nyama). be for/get the ~ fukuzwa.

chop2 n muhuri; rajamu.

chopchop adv chapuchapu.

chopper n (in India) paa, kipaa, kisusi.

chop-sticks n pl vijiti (wanavyotumia Wachina kulia chakula).

chop-suey n chopsue (chakula cha kichina cha nyama ya kukaanga kwa wali na vitunguu).

chord1 n 1 utari. 2 upote. 3 mtambuko (mstari unaounga nukta mbili za kivimbe). 4 (anat.) ukano, mshipi, ugwe.

chord2 n (mus) kordi: noti za msingi

zinazoafikiana zikipigwa kwa wakati mmoja au pamoja. touch the right ~gusa hisia. strike a ~ kumbusha.

chore n 1 kazi ya kuchosha. 2 kazi ndogo ndogo za kila siku.

choreography n koregrafia: elimu ya miondoko ya dansi/ngoma jukwaani choreographer n.

chortle vi chekelea n kuchekelea.

chorus n 1 kiitikio, kibwagizo, mkarara, kipokeo. 2 kwaya. 3 mlio/ sauti za umati wa watu/watu wengi pamoja. in ~ wote kwa pamoja a ~ of approval mlio wa kukubali/ kuitikia. 3 (drama) wazumi. 4 kikundi cha waimbaji na wachezaji katika tamthilia/filamu. vi imba/sema kwa pamoja. ~-girl n msichana (wa

chronology

kikundi) aimbaye na kucheza katika tamthilia/ filamu/maonyesho.

chow n (sl) chakula.

chowder n (US) mchuzi wa samaki auchaza na mboga.

chrism n (rel) krisma: mafuta matakatifu ya ibada nyingine za Kikristo.

Christ n (rel) Kristo Jesus C~ n Yesu Kristo C~ Child Mtoto Yesu. C~ian n mkristo adj -a kikristo ~ian name jina la ubatizo ~ian era enzi ya ukristo (tangu kuzaliwa kwa Kristo), zama za ukristo. ~ianity n ukristo. C~ endom n wakristo, mataifa ya Kikristo. ~en vt 1 batiza. 2 -pa jina la kubatiza. ~ening n. C~ mas n (also Xmas). C~mas day n Noeli, Krismasi: siku ya kuzaliwa kwa Yesu, tarehe 25 Desemba a merry/happy C~mas heri/salam za Krismasi Father C~mas Baba Krismasi: mtu ambaye anaaminiwa hutoa zawadi kwa watoto wakati wa Krismasi. ~mas box n zawadi ya Krismasi (itolewayo kwa watu ambao wamehudumia mwaka mzima k.m. wazoa takataka. ~mas carol n wimbo wa Krismasi. ~mas eve n mkesha wa Krismasi. ~mas tree n mkrismasi, mvinje.

chrome n kromu: chumvichumvi inayotumiwa kutoa rangi ya manjano. ~ steel n aloi ya chuma cha pua na kromiamu. chromatic adj -a rangi; enye rangi nyingi.

chromium n (chem) kromiamu.

chromosome n (biol) kromosomu: nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni; uwezo wa/ programu ya kurithisha tabia na maumbile.

chronic adj 1 -a kudumu; -a kuendelea siku nyingi; -a donda ndugu; -a kuselelea (kama ugonjwa au mazoea) ~ invalid mgonjwa wa siku zote. 2 (sl) kali mno. ~ally adv.

chronicle n tarihi, wendo vt andika

(tarihi).

chronology n 1 wendo, utaratibu wa

kupanga miaka na matukio. 2 elimu

wendo. chronological adj -a wendo ~ age umri makuzi.

chronometer n kipimawakati, kronometa; saa.

chrysalis n buu.

chubby adj nenenene, tipwatipwa,

-liojaa.

chuck n 1 kofi la mahaba. 2 mtupo; kuacha kazi. give somebody the ~ fukuza. vt 1 tupa ~ me the ball nitupie mpira. 2 ~ under the chin papasa/piga kimchezo/mahaba chini ya kidevu. 3 ~ away tupa. 4 ~ in/up acha. ~ up ones job acha kazi ~ it (sl) Acha! 5 ~ out fukuza. ~er out n mbabe n 1 kufukuzwa kazi he got the ~ alifukuzwa kazi. 2 kofi la mahaba (chini ya kidevu).

chuckle n kicheko cha chinichini. vi

jichekea, chekelea. ~-head n (sl)

mpumbavu, bwege.

chug vi titima.

chum n 1 rafiki.2 (US) mwenzi katika chumba. vi 1 ~ up with jenga urafiki na; suhubiana. 2 kaa chumba kimoja na. chummy adj kirafiki, kama rafiki.

chump n 1 kigogo. 2 pande la nyama~ chop pande la nyama ya paja la kondoo. 3 (sl) mpumbavu, mjinga. silly ~ n mpumbavu. 4 (sl) kichwa. off one's ~ wazimu.

chunk n 1 kipande kinene (cha kitu chochote, k.m. cha mkate, jibini

n.k.). ~y adj.

church n 1 kanisa. ~ register n rekodi za uzazi, harusi, na vifo katika parokia. ~ yard n sehemu ya makaburi katika eneo la kanisa. 2 ibada katika kanisa. ~ goer mwenda kanisani mara kwa mara. 3 jamii ya makasisi go into the ~ -wa kasisi, ingia ukasisi. 4 the C~ of Christ Wakristo wote, kundi zima la wakristo. the C~ of England kanisa la Anglikana. ~ service n ibada ya kanisa.

churl n 1 mtu asiye na adabu, mshenzi; mtu wa hasira. 2 (arch) mtu wa tabaka la chini (hasa mkulima). ~ish

cine

adj. ~ishness n.

churn n 1 chombo cha kusukia maziwa, tungu. 2 gudulia kubwa la maziwa. vt,vi 1 ~ up tengeneza siagi kwa kusuka maziwa. 2 vurugavuruga (kama upepo unavyovuruga bahari). 3 charuka, vurugika. 4 ~ out tengeneza/toa kwa wingi bila ubora.

chute n 1 njia ya kuteremshia magogo,

makaa n.k. 2 poromoko la maji. 3 (colloq abbr. of parachute) mwavuli.

chutnee; chutney n achari.

cicada n nyenje.

cicatrice/cicatrix n kovu.

cicerone n gambera, kiongozi (wa kuonyesha na kuelezea sehemu za kuvutia/kitalii).

cide n 1 tendo la kuua mtu. 2 mtu au kitu kinachoua. cidal adj

cider n sida: kinywaji/pombe ya matufaha. ~press n kikamua tufaha.

cigar n biri. ~ette n sigara, sigareti. ~holder n kishika sigara. ~ lighter n kiberiti cha sigara.

cilia n pl (anat) kope (bot, bio) vijisinga, vinywele vya jani. ~ry adj ~ry muscles visuli lensi.

cinch n 1 (of horse) mkanda wa tandiko. cincture n (arch.lit) mshipi, ukanda. vt zungusha ukanda/ mshipi. 2 (sl) jambo la uhakika/ yakini vt hakikishia.

cinchona n (bot) mkwinini: jamii ya miti ambayo magome yake hutumika kutengenezea dawa kama kwinini n.k.

cinder n 1 kipande cha mkaa/kuni ambacho kimeungua kiasi. 2 kipande cha lava. 3 mabaki baada ya kutoa chuma chenye matapo. 4 (pl) majivu. ~ -track n (athletics) uwanja wa kukimbia (uliotengenezwa na majivu).

cinderella n 1 kisonoko. 2 (metaph.) mtu au kitu ambacho uzuri/uwezo wake haujatambulika.

cine pref (used for cinema in compounds) ~ camera n kamera senema.

cinema

cinema n 1 jumba la kuonyeshea filamu. 2 filamu, sinema. ~tograph n chombo cha kupigia picha za sinema. ~tography n elimu/sanaa ya upigaji picha za sinema.

cinnamon n mdalasini adj -a kahawia

isiyoiva.

cipher; cypher n 1 tarakimu 0, sifuri. 2 tarakimu ya kiarabu (yoyote toka 1 hadi 9). 3 (secret writing) maandishi ya kimafumbo ~ key kifumbuzi. 4 (fig) mtu/kitu duni, yahe, hohehahe. vt, vi (colloq) 1 jumlisha; fanya hesabu; gawa. 2 andika maandishi ya kimafumbo.

circa adv, prep (lat.) mnamo (mwaka fulani). ~ 1500 mnamo mwaka 1500.

circle n 1 duara; mviringo (kama wa sahani), kitu mfano wa duara; familia moja have black ~s under the eye kunjamana kwa ngozi za macho na kuwa nyeusi zaidi achokapo mtu. 2 (ring) pete, taji. 3 mfululizo kamili come full ~ malizia, rudia mahali pa kuanzia. 4 jamii ya watu wenye mawazo/kazi zinazofanana he was praised in academic ~s alisifiwa na jamii ya wanataaluma. in business ~s miongoni mwa wafanyabiashara. vt, vi zungusha; zunguka, enda mwendo wa duara. ~t n 1 kiduara. 2 kitaji. circular adj kiduara, -a duara, -a mviringo. circular saw n msumeno gurudumu. n waraka, ilani (kwa wote wanaohusika). circularize vt peleka kwa watu wengi.

circuit n 1 duru, mzunguko, njia ya kuzunguka you have to make a wide ~ inakupasa uzunguke mbali. 2 ziara: safari ya kutembelea eneo maalumu (k.v. jaji anayetembelea mahakama na walio chini yake). 3 (electr) mzunguko umeme, saketi a short ~ mkato wa mzunguko wa umeme. 4 kundi la sinema, chini ya utawala/kampuni moja. vt zungusha. vi zunguka. ~ous adj -a kuzunguka zunguka. ~ously adv.

circulate vt,vi 1 zunguka blood

circus

circulates in the body damu inazunguka mwilini. 2 (spread) enea; eneza, vumisha the news ~d rapidly habari zilienea haraka circulating library maktaba (ya kuazimisha vitabu). circulation n 1 mzunguko (agh wa damu). 2 uenezaji, usambazaji. 3 jumla ya magazeti yanayouzwa kila toleo. circulatory system n mfumo wa mzunguko wa damu.

circumcise vt tahiri, tia jando, tia kumbi. circumcision n 1 tohara. circumcision rites n jando, kumbi.

circumference n mzingo, kivimbe. circumlocution n maneno ya kuzungusha, maneno mengi.

circumnavigate vt zunguka kwa meli ~ the globe zunguka dunia kwa meli. circumnavigation n.

circumscribe vt 1 zungushia mstari. 2 wekea mipaka; zuia. circumscription n 1 kuweka/wekewa mipaka. 2 (coins) mwandiko (unaozungukia sarafu).

circumspect adj 1 -enye hadhari, -a

kuangalia kila upande, -angalifu. ~ion n uangalifu, hadhari. ~ly adv.

circumstance n (usu pl) 1 hali, hali ya

mambo the ~s do not permit it hali hairuhusu. under good ~ you can see the island hali (ya hewa) ikiwa nzuri unaweza kuona kisiwa. in/ under the ~s kwa hali ilivyo under no ~s kamwe, kwa hali yoyote ile. 2 mazingira you must know the ~s of the crime huna budi kufahamu mazingira ya jinai. 3 jambo you have overlooked one ~ umesahau jambo moja. circumstantial adj 1. (of description) -enye kueleza habari zote. 2 ~ evidence ushahidi usio kizibiti. ~ly adv.

circumvent vt 1 (formal) zuia (mpango) usitekelezwe. 2 epuka (tatizo, sheria) kwa ujanja, ghilibu. ~ion n.

circus n 1 sarakasi. 2 kiwanja mfano wa duara cha kuonyeshea michezo.

3 wachezaji wazungukao mjini kuonyesha michezo yao; tamasha. 4 makutano: sehemu ambapo barabara nyingi hukutana.

cirrus n (Meteorol) mavundevunde;

mawingu mepesi mepesi ya juu sana.

cissy n, adj see sissy.

cistern n tangi la maji (k.m.juu ya choo au nyumba).

citadel n ngome (ya kulinda mji). 2 (fig) mahali pa usalama, mahali pa kukimbilia (wakati wa hatari).

cite vt 1 dondoa kama mfano (kutoka kitabuni n.k.) ili kuthibitisha hoja. 2 (US) taja (mtu) kwa ujasiri wake vitani. 3 (leg) ita shaurini/ mahakamani. citation n 1 dondoo. 2 mtajo. 3 hati inayoambatana na tamko la tuzo. 4 (US) tamko katika kutaja kumbukumbu rasmi (k.m. ushujaa katika vita).

citizen n 1 raia; mwananchi born ~

raia wa kuzaliwa naturalized ~ raia wa kuandikishwa. ~ of the world mlimwengu: mtu afurahiaye popote atakapoishi. ~ship n 1 uraia. 2 mambo yampasayo raia bora. ~ry n kundi zima la wananchi/raia.

citrus n, adj mti wa jamii ya mchungwa, mlimau, mdimu, n.k. citric adj sitriki. citric acid n asidi sitriki: asidi itokanayo na matunda ya jamii michungwa, milimau n.k., mbalungi; balungi. citron n,adj -a mti wa jamii ya michungwa, milimao n.k.

city n 1 jiji; mji mkubwa. 2 mji

uliopewa haki maalum za kujitawala ~ centre katikati ya mji. ~ fathers n madiwani wa jiji. ~ slicker n jambazi au mhuni (aghalabu wa jijini). 3 raia wa jiji.

civet n 1 ~ cat ngawa. 2 fungo.

civic adj 1 -a kiraia, -a uraia. 2 -a jiji; -a kuhusu mji au wakaao mjini ~ centre mahali palipo na ofisi za jiji na majengo ya serikali. ~s n uraia: elimu ya utawala wa mji, kazi na haki za raia.

civil adj 1 -enye kuhusu raia. ~

clam

servant n mtumishi wa serikali. the ~ service n utumishi wa serikali. ~ marriages n ndoa za kiserikali. ~ rights n haki za raia (kisiasa, kisheria, kijamii). ~ war n vita vya wenyewe kwa wenyewe. 2 -a madai. ~ case n kesi ya madai. ~Defence Corps n ulinzi wa raia (dhidi ya shambulio la adui hasa kutoka angani). ~ defence corp n mgambo. ~ disobedience n uasi, uvunjaji sheria. 3 -a kuhusu ujenzi. ~ engineer n mhandisi ujenzi (barabara, daraja, n.k.). civilly adv kwa adabu, kwa unyofu, kwa unyenyekevu. civility n unyenyekevu, adabu heshima, uungwana. civilian n raia (asiye askari) adj in ~ian clothes -enye kuvaa nguo za kiraia.

civilization n ustaarabu; hali bora ya kuishi the ~ of Egypt ustaarabu wa Misri. civilize vt staarabisha.

civvies/civies n pl (sl) nguo za kiraia adj in ~ -liovaa nguo za kiraia.

clack vi fanya kishindo; alika. n 1

kishindo. 2 mwaliko.

clad old pp. of clothe adj poorly ~

-liojiambika maguo, -lovalishwa, -lofunikwa.

claim vt 1 dai, taka haki. 2 (assert oneself) nena kwa dhati (ili kuthibitisha ukweli); taja. 3 stahili, hitaji. n 1 dai, madai ~ of right madai ya haki. 2 statement of ~ maelezo ya madai a ~ for damages madai ya gharama lay ~ to something dai ujira au ushuru a legal ~ to something daawa. 3 kilichodaiwa. 4 machimbo/miliki ya mtu. ~ant n mdai.

clairvoyance n ubashiri. clairvoyant mbashiri.

clam n chaza; (sl) mnyamavu. ~ bake n (US) mandari ya ufukoni ambapo chaza na vyakula vingine huokwa; tafrija; mkutano wa siasa. vt 1 chimba chaza, enda kutafuta chwago. 2 ~ up (colloq) nyamaza (ghafla), kataa kuongea.

clamber

clamber vi panda, kwea kwa shida

(hasa kwa kutumia mikono na miguu), paramia, sombea. n mpando, mparamio, usombeaji.

clammy adj 1 -a kunata a face ~ with sweat uso unaonata jasho. 2 -a unyevu, -a baridi na -enye kunata, ~ hands mikono baridi. clammily adv.

clamour n makelele, ghasia, (hasa ya watu wanaolalamika kwa hasira au

wanaodai haki). vi, vt fanya makelele/ghasia. ~ for piga kelele kwa ajili ya kitu fulani the troops were ~ing to go home majeshi yakipiga makelele kutaka kwenda nyumbani. ~ against something pinga jambo kwa kupiga kelele. clamorous adj -a makelele, -a ghasia. clamp1 n klempu, kibanio; (naut.) kipingo. vt bana, kaza, funga kwa gango. ~ down (on) (colloq) bana, tia shinikizo (ili kuzuia kitu); -wa mkali. ~ down n kubanwa.

clan n 1 ukoo, uzawa; mbari; jamii ya watu wa mlango mmoja. ~ nish adj (derog) -a kupenda ukoo, -a kulindana kiukoo; -a kukaa kiukoo. ~s man n mtu wa ukoo. ~nishness n.

clandestine adj (formal) -a siri, -a

kificho. a ~ marriage n ndoa ya siri. ~ly adv.

clang vi,vt fanya sauti kubwa (k.m.

vyuma vikigongana) he ~ed the bell alipiga kengele. n sauti kubwa (ya kengele, tarumbeta au ndege). ~er n. (sl) drop a ~er sema kitu cha kuaibisha; kashifu. ~our n sauti kubwa ya mfululizo. ~rous adj.

clap1 vt, vi 1 piga makofi (kwa kushangilia) ~ one's hands piga makofi (ya shangwe). 2 ~ in prison tia mtu jela ~ duty on goods toza ushuru. ~ eyes on somebody (colloq) ona. 3 pigapiga kwa kiganja kuonyesha upen do.~per n 1 mtu/kitu kifanyacho mlio/sauti ya mpasuko (k.v. ulimi wa kengele). 2 mtu ashangiliaye. 3 ulimi wa mtu anayesema sana. n 1 sauti ya

mpasuko kama wa radi. 2 kofi.

clap2 n (sl) kisonono.

claptrap n. (colloq) maneno matupu, mapuo (hasa ya kujipendekeza ili kuwavuta watu).

claque n 1 washangiliaji wa kukodishwa. 2 kundi la watu wanaowarairai watu wengine kwa ajili ya manufaa yao. 3 upuuzi, jambo lisilo na maana.

claret n 1 bordo (namna ya divai nyekundu). 2 (sl) damu. tap somebody's ~ toa damu ya pua kwa kumpiga mtu konde. 3 rangi nyekundu; ngeu.

clarify vt 1 eleza wazi, bainisha. 2

safisha; safika; chuja. clarification n. clarity n uwazi, ubayana.

clarinet/clarionet n (mus) zumari. ~ist n mpiga zumari.

clarion n panda, parapanda, baragumu (attrib) -a sauti kuu na -lio wazi; (fig) ~ call wito ulio wazi.

clarionet n see clarinet.

clash n 1 mgongano. 2 mapigano, makinzano, mabishano, mapambano. vt, vi 1 gonganisha, pambanisha; gongana, pambana; ingiliana. the two weddings ~ed harusi hizo mbili ziliingiliana. 2 (oppose) ~ with kinzana (na), umana (na) colours that ~ rangi zisizooana.

clasp n 1 kifaa (chenye sehemu mbili) cha kufungia au kushikia vitu pamoja (k.m. kifungo, bizimu). 2 kipande cha madini ya fedha, n.k. kwenye medali chenye jina la vita (kwa askari) au kampeni inayofanywa. 3 kushika kwa nguvu (kwa vidole au mikono). 4 kupeana mkono. 5 mkumbatio. vt 1 funga (k.m. kwa kifungo au bizimu). 2 (embrace) kumbatia. 3 kamata, shika. 4 fumbata ~ hands shikana/peana mikono. ~ knife n kisu cha kukunja.

class n 1 (social) tabaka working ~

tabaka la wafanyakazi. ~ consciousness n hisia za kitabaka. ~ struggle n mapambano ya

classic

kitabaka, harakati za kitabaka. 2 (of travel) daraja. 3 (of school) darasa (la watu wafundishwao pamoja). ~room n darasa. ~mate n mwanafunzi mwenza. 4 jamii ya vitu vya namna moja more in a ~ (of its own) -a pekee. 5 (mil) marika. 6 (gram) ngeli. vt ~ify 1 tabakisha. 2 ainisha. ~ified adj 1 -loanishwa. ~ified ad n tangazo dogo (katika gazeti la biashara). 2 -a siri ~ified information habari za siri. ~ification n 1 upambanuzi; uainishaji. 2 mpango wa aina mbalimbali; mgawanyo wa aina mbalimbali. ~ism n 1 urasimi. 2 fani, kauli bora; usomi wa fasihi (sanaa) iliyothaminiwa kuwa bora. ~y adj (colloq) -a mitindo, -a tabaka/daraja la juu. ~less adj -siyo na tabaka.

classic n 1 sanaa au kazi ya kiwango cha juu sana (inayotambuliwa na kutumiwa kama mfano bora). 2 fasihi, historia na falsafa ya Wayunani na Warumi. the C~s n maandishi/maandiko bora (hasa ya Wayunani na Warumi wa zamani) adj 1 -lio bora kabisa; -lio maarufu sana. 2 (of style in costume, etc.) -a jadi, -a kimapokeo. 3 -siopambwa sana; -sionakshiwa. ~ist n. classical 1 adj -a kuhusu utamaduni na elimu ya Wayunani na Warumi wa zamani. a ~al scholar n mwanazuoni wa elimu na lugha. 2 (music) muziki dhati.

clatter n 1 sauti ya vitu vinavyogongana. 2 makelele, maongezi yenye makelele. vt vi fanya makelele; gonganisha ~ down anguka kwa kishindo, teremka kwa kishindo.

clause n (gram) kishazi. 2 (leg) sharti; mlango, sura moja katika mapatano au sheria, ibara attestation ~ ibara ya ushuhuda.

claustrophobia n 1 (med) klaustrofobia: woga aupatao mtu awapo shimoni/pangoni. 2 chumba kidogo; mahali (popote)

palipofinywa/palipobanwa.

clavicle n mtulinga.

claw n 1 kucha (la mnyama au ndege). 2 (of crab, lobster etc.) gando/ koleo. vt, vi 1 papura, piga makucha. 2 shika kwa kucha au kwa vidole. ~ away (off) (of ship) acha bandari. ~ at/back (colloq) pata kitu tena kwa jitihada. ~ hammer n nyundo koleo.

clay n 1 udongo wa mfinyazi. 2 (arch) mwili wa mwanadamu; maiti we are but ~ sisi ni udongo tu ~-cold adj -a baridi sana (hasa kwa maiti). ~ey adj -enye/ -liofunikwa na udongo wa mfinyanzi.

clean adj 1 safi, -eupe. 2 -sio na waa; -sio na hatia have ~ hands wa bila kosa wala hatia. 3 -enye udhu/tohara. make a ~ breast of something ungama. 4 mpya, -sotumika bado start a ~ slate anza upya 5 -enye kupendeza. ~ -limbed adj -a maungo mazuri. 6 stahifu have a ~ tongue -wa na lugha stahifu. 7 kamilifu kabisa. 8 (of tree) bila mafundo. 9 aminifu. 10 stadi a ~ boxer mwanamasumbwi stadi. 11 -enye kufaa kwa chakula un ~ animals wanyama haramu/ wasioruhusiwa na dini kuliwa (k.m. nguruwe) adv kabisa, pia we ~ forgot you were coming tulisahau kabisa kuwa unakuja come ~ jitakasa kabisa ~ cut adj -lotengenezwa vizuri ~living adj bikira ~shaven, adj lonyolewa vizuri. ~ through katikati; kote. vt,vi 1 safisha, takasa; osha. 2 fua. 3 (sl) be ~ed out filisiwa. ~out 1 safisha. 2 chukua fedha zote (kwa kushinda au kuiba). ~up safisha sana (fig) ~up the city safisha mji (kwa kuondoa wahalifu). ~ er n mnadhifishaji. take somebody to the ~ers filisi. dry ~er n dobi ~ fingers (fig) -siopokea wala kutoa hongo. ~ly adj nadhifu adv kwa unadhifu. ~liness n.

cleanse vt 1 safisha sana; eua. ~r n

clear

kifaa cha kusafishia.

clear adj 1 -eupe, -angavu. 2 dhahiri,

wazi make ~ eleza wazi; dhihirisha, funua. ~cut adj dhahiri kabisa ~ headed/sighted -enye kuelewa haraka a ~ case jambo la wazi, dhahiri. 3 bila kizuizi wala shida; bila shaka. it's ~ sailing hakuna taabu yoyote the coast is ~ hakuna hatari yoyote. 4 bila hitilafu, bila hatia/lawama, bila mgogoro. 5 kamili three ~ days siku tatu kamili ~ voice sauti wazi (isikikayo vizuri) ~ speaker msemaji asikikaye vizuri. ~ about/on -enye hakika. in the ~ -siotuhumiwa adv 1 kwa wazi, kwa dhahiri. 2 kabisa the prisoner got ~ away mfungwa alitoroka kabisa. 3 ~ (of) pasipo, bila, mbali na. vi,vt 1 safisha, takasa; safika, takata, ondolea (vizuizi, shida, mashaka, hatia). 2 epuka, jihadhari. keep ~ of something jitenga. 3 weka wazi. ~ the way! acha njia (iwe) wazi ~ the ground for negotations ondoa vikwazo ili kurahisisha mazungumzo. 4 (of liquids etc.) chuja. 5 fyeka ~ the bush fyeka magugu/gugu. 6 kiuka, pita juu ya au kando ya bila kugusa kitu. 7 pata faida ya we ~ ed shs 50,000 tumepata faida ya sh. 50,000.8 (tax etc.) lipa he ~ed his debts alilipa madeni yake. 9 ~ away ondoa ~ away the plates ondoa sahani; (of mist) tanzuka the clouds have ~ed away mawingu yametanzuka ~ (something) off ondoa, maliza (ote); uza rahisi; potelea mbali; (fig) penya, puruka. ~ out kumba; ondoka; ondoa. ~(something) up tengeneza, panga vizuri (of weather) takata; fumbua, tatua they ~ed their problems walitatua matatizo yao; safisha. ~ly adv kwa dhahiri he is not ~ly intelligent ni dhahiri kwamba hana akili. 10 (pass over) pitisha (for cargo, ship) maliza taratibu za kuondoa (mizigo, meli) bandarini. 11 pata idhini (ya kuingia bandarini,

clergy

kutua uwanjani). ~ance n 1 kusafisha, kuondoa (vizuizi, shida n.k.). ~ance sale n seli ya kumaliza vitu. 2 ruhusa ~ance certificate hati ya ruhusa (ya kuondoa mizigo). 3 nafasi (iliyoachwa baina ya vitu viwili). 4 (mil) kibali cha kujiuzulu jeshini; kibali cha kusoma nyaraka za siri. ~ing n 1 mahali peupe (pasipo miti katika mwitu); palipofyekwa, chenge. 2 tendo la kusafisha. ~ing house n ofisi ya kubadilishia hundi za benki.

cleat n 1 (naut) makari anchor~

mangili. 2 njumu: msumari unaojitokeza kwenye kiatu cha mwanariadha.

cleave vt 1 pasua, kata, (vipande viwili), tenga kwa nguvu, chana chana. 2 (penetrate) penya ~ one,s way through the crowd penya katikati ya watu cloven hoof kwato yenye pande mbili (k.v. ng'ombe mbuzi n.k.); (fig) kwato ya shetani. cleavage n 1 mpasuo; mpasuko. 2 mfarakano, mgawanyo. 3 (colloq) nafasi katikati ya matiti. vi (arch) nata, shikamana na, ganda ~ to one's opinion shikilia mawazo (yake). ~r n shoka au kisu kikubwa agh. cha kukatia nyama.

clef n (music) kitambulisho (cha mistari ya noti).

cleft1 n ufa, mwanya.

cleft2 n see cleave ~ palate kaakaa lililopasuka in a ~ stick katika hali ya kutokuwa na njia, katika hali ya kutokuwa na tamaa.

clemency n 1 huruma; upole. 2

(of atmosphere etc) hali nzuri; joto kidogo; hali mwanana. clement adj -anana, -pole, -enye huruma, -ema.

clench vt 1 kaza msumari kwa kuukunja na kuugandamiza. 2 funga sana, shika sana, kaza sana (k.m. meno, ngumi), fumba sana (mikono)

clergy n (collective) n 1 mapadri, wachungaji, makasisi wa kanisa. ~man/cleric n mhudumu wa kanisa, padri; kasisi ~ in holy

orders padri.

clerical adj -a kuhusu mapadri, wachungaji na makasisi. n mbunge, mfuasi (mjumbe) wa chama cha dini.

clerihew n (liter) kipande cha ubeti

chenye mzaha.

clerk n 1 karani. clerical adj -a kuhusu makarani a clerical error kosa la maandishi, kosa katika kunakili (kufuatisha) town ~ katibu wa mji chief ~ karani mkuu ~ of the works msimamizi wa majengo ~ to the cabinet karani wa baraza la mawaziri. 2 (US) (of shop) mwuzaji.

clever adj 1 stadi, mahiri, -juzi be ~

with one's hands wa hodari kwa kazi ya mikono a ~ workman fundi, stadi, waria. 2 -enye akili, hodari be ~ at something wa hodari kwa jambo fulani ~ dick mtu anayetambia akili yake. 3 janja. ~ness n.

clew (US clue) n 1 bonge la uzi. 2 (naut) kitanzi. vt,vi 1 (of ball of e.g. thread) zonga zonga, kunjakunja. 2 (naut) ~ up kunja tanga; maliza kazi; pambana na kazi.

cliche n mchuuko, istiari iliyochakaa.

click1 n 1 mwaliko sauti: sauti ya kualika kama vile kidole, mtambo wa bunduki, n.k. 2 kidoko. 3 (of horse) mwaliko wa kwato (wa miguu ya mbele na nyuma inapokutana). vt alisha, liza kidoko, piga kidoko ~one's tongue piga kidoko ~ one's heels gonganisha visigino (vya miguu).

click2 vi (sl) 1 eleweka the point suddenly ~ed up wazo lilieleweka. 2 elewana mara moja.

client n mteja ~ ele n wateja.

cliff n jabali; mteremko wa ghafula

agh. wa mwamba (wa mlima au

mahali palipochongoka), genge, (hasa ukingoni mwa bahari) ~ -hanger tukio la taharuki sana. ~y adj.

climacteric n (med) mabadiliko

muhimu katika maisha ya mwanadamu (kati ya miaka 45 na 60).

climate n 1 tabia ya nchi (yaani joto,

clip

baridi, upepo, mvua n.k.); hali ya mambo ilivyo political ~ hali ya siasa ilivyo. climatic adj. climatology n taaluma ya hali ya nchi. climatologist n.

climax n upeo; kilele. vt,vi fikia/fika/

fikisha kilele(ni). climactic adj -a juu kabisa, -a upeo, a kileleni.

climb vi,vt 1 (slope upwards) kwea,

panda. 2 (of plants) tambaa. ~ing plant n (mmea) mtambazi. ~ up 1 paramia, panda, sombera. ~ down shuka; kubali kosa. 2 paraga. n 1 upandaji, uinukaji. 2 ukwezi; (fig) -ja kwa matao ya chini (kiri kosa) ~ing irons pingu za mkwezi. ~er n mkwezi; mtu anayejiendeleza; mmea unaotambaa.

clime n (poet) tabia ya nchi.

clinch vt 1 see clench. 2 kaza msumari kwa kuugongomea. 3 (of boxers) shikana; kamilisha ~ a deal/an agreement fikia/kamilisha mapatano. 4 (colloq) kumbatiana. n mshikamano, mkazo. ~er n jambo/neno mkata.

cling vi ~ to/together shikilia, ng'ang'ania; gandama, ambatana. ~y adj.

clinic n 1 kliniki. 2 hospitali maalumu. 3 mahali pa ushauri (wa kiganga) au matibabu. ~al adj 1 -a hospitali, -a kuhusu mafundisho ya utibabu (uganga) yanayotolewa katika hospitali. ~al thermometer n kipima joto. 2 adilifu.

clink1 n sauti ya mgongano wa kauri au glasi. vt,vi fanya/ fanyiza sauti ya mgongano wa kauri au glasi.

clink2 n (sl) gereza, jela be in ~ -wa gerezani go to ~ nenda jela.

clinker1 n mabaki ya mkaa.

clinker2 n (sl) kosa kubwa.

clip1 vt shikiza, bana, funga weka pamoja kwa kibao (n.k.) n kishikizo, kibano.

clip2 vt 1 kata (kwa makasi), dira, punguza, fupisha ~ a hedge (or the wool from a sheep's back) dira, (kata) uga wa mimea, manyoya

(mgongoni mwa kondoo). 2 ~ somebody's wings fanyia mtu inda asifikie lengo lake. 3 (of ticket) toboa. 4 (colloq) piga vizuri; ruka au fupisha sauti mwishoni mwa neno. n 1 kukata; mkato. 2 (for hair) kudira. 3 (of sheep) kunyoa. 4 pigo. 5 (colloq) mwendo wa kasi. ~ping n makala iliyokatwa kutoka gazetini. ~per n 1 (of person) mkataji manyoya. 2 (pair of) ~pers n mkasi. 3 merikebu iendayo kasi sana (kwa matanga) .

clique n genge: kikundi cha watu

wenye mawazo yanayofanana. cliquish adj.

clitoris n kinembe, kisimi.

cloak n 1 joho. 2 kifuniko; pazia; kitu

kinachoficha sababu/mawazo ya ukweli. vt ficha; setiri, valisha; funika. ~and dagger adj -a kuhusu upelelezi, -a siri. ~-room n 1 chumba cha kuwekea makoti, mizigo n.k. 2 (euphem) choo.

clobber1 n (GB sl) mavazi na vifaa.

clobber2 vt 1 (sl) twanga, umiza vibaya. 2 shinda vibaya.

clock1 n 1 saa kubwa (ya mezani, ukutani, au mnarani) put the ~ back rudisha nyuma; rudia mambo ya zamani. (arch) against the ~ kabla ya saa iliyopangwa. (sl) sleep/work around the ~ lala/fanya kazi saa 24. vt,vi 1 pima muda unaotumiwa kwa jambo. 2 (GB sl) piga. 3 ~ in (out) ripoti, jiandikisha saa ya kufika/ kutoka kazini. ~ up fikia. ~wise adv kwa mzunguko wa akrabu, kisaa turn the handle ~wise zungusha mkono upande wa kulia. anti ~wise adj, adv kinyume saa. ~work n mtambo wa saa, chombo cha aina hiyo like ~work; with ~ work kwa taratibu, kwa mpango uliowekwa, bila tatizo lolote. ~ watching n tabia ya kungoja saa ya kufunga kazi ifike.

clock2 n kipambo kinachofumwa kwenye soksi.

clod n 1 bonge, donge (hasa la

close

udongo). 2 (colloq) mjinga, mshamba. ~hopper n mtu mzito wamwili, mshamba. ~hoppers n (colloq) viatu vizito kama vya mkulima. ~dish adj.

clog1 n 1 kizuizi, kizibo. vt ziba (agh. kwa uchafu), zuia; zibika, zuilika.

clog2 n 1 mtalawanda, kiatu cha gongo (kiatu chenye soli ya mti). 2 kibao kinachofungwa miguuni mwa mnyama ili asizurure; (fig) kizuizi. vt 1 ziba (bomba nk.). 2 zuia. ~gy adj.

cloister n 1 makazi ya watawa.

utawani. 2 ujia (mrefu, mwembamba) wenye matao, (agh. wa nyumba ya watawa). vt 1 weka/ishi kwenye nyumba ya watawa. 2 (fig) live a ~ed life ishi maisha ya kutengwa kama watawa.

clone n (bio) aina ya kiumbe kilichoumbwa na kiumbe kimoja bila kujamiiana.

close1 adj 1 karibu ~ to the house karibu na nyumba. a ~ call/ thing/shave kuponea chupuchupu. ~ up picha ya karibu ~ friends marafiki sana. 2 -liopangwa karibu karibu; -liosongana. ~ weave n mfumo wa karibu. 3 kali in ~ confinement chini ya ulinzi mkali keep a ~ watch chunga vikali. 4 -a makini make an ~ inspection kagua kwa makini. 5 -a siri; -a faragha: -liofichwa she is very ~ about her life ni msiri sana kuhusu maisha yake. 6 ~fisted adj bahili, -nyimifu; -choyo. 7 (sports, games) karibiana sana it was a ~game walikaribiana sana (katika mashindano). 8 (weather) -enye jasho na joto; -inayobana; zito sana; inayokaza the sweater is a ~ fit sweta inabana. 9 ~ friend mwandani, -a kusafiana nia. 10 (phonetics) (of vowels) -a juu. ~d n funge. (season) ~ season wakati ambapo uwindaji ni marufuku (ili wanyama wazae) adv karibu karibu sana. ~ at hand hapa hapa. ~

close

by/to karibu na. ~ upon karibia. ~ up to karibiana na. ~ness n. ~ly adv kwa makini; karibukaribu sana.

close2 n 1 uwanja, uga (wa kanisa/shule). 2 njia iliyofungwa break ~ kumwingilia mtu katika ardhi yake. ~ cropped adj (hair, grass) fupi sana. ~ together karibu karibu adv sail ~ to the wind karibia kuvunja sheria/mila/miiko. ~hauled adj -lioenda joshi.

close3 vt,vi funga ~ the doors funga milango; (fig) -fa. ~d book n fumbo, jambo lisiloeleweka, uchawi; jambo lililokwisha. ~ accounts funga hesabu. 2 ~ one's eyes funga, fumba macho, -totia maanani, jifanya huoni ~ a debate maliza mjadala. ~ down funga (duka n.k.). ~ up sogeza/ziba kabisa. 3 fungika, fumbika, jifunga the theatre ~s on Monday thieta hufungwa kila Jumatatu. 4 songa, kubali. ~ with (agree) kubali, patana, -wa karibu; (of war) ~ with the enemy anza kupigana. ~ with the land karibia pwani. ~d circuit n -a nyaya maalum. ~d shop n wanachama (tu); (of a shop etc) fungwa. ~ in -wa fupi the days are closing in siku zinakuwa fupi (of radio) maliza matangazo. ~ in/on/~ d upon zingira na shambulia the enemy ~ d upon us adui alituzingira na kutushambulia n mwisho, hitimisho at the ~ of the day jioni at the ~ of this century mwisho wa karne hii draw/bring something to a ~ maliza.

closed adj (of society, system) -liojitenga, -liotengwa kwa shughuli maalum; -a siri. ~ session n mkutano wa siri, wa faragha .

closet n 1 chumba cha faragha. 2 (US) chumba cha kuhifadhia vitu; kabati. 3 (arch) water ~ choo, msala. vt ~ oneself jitenga; jifungia. be ~ed with somebody (together) kutana faraghani (kwa shauri, kwa kusoma n.k.) adj -a siri come out of the ~ tangaza kwamba ni msenge/msagaji/

basha.

closure n 1 ufungaji. 2 (Parl) uamuzi (wa kufunga kwa kura). move the ~ toa hoja ya kumaliza mkutano (kwa kupiga kura); funga mkutano.

clot n 1 donge (la damu). 2 (sl) jinga; pumbavu. vi ganda the blood is ~ted damu imeganda.

cloth n 1 nguo, kitambaa cha namna

yoyote; (woollen) sufu; (linen) kitani, bafta; (calico) marekani, ulaiti, gamti; (black) kaniki; baibui; (of gold) zari; (loin-cloth) shuka, kikoi, kitambi; (table cloth) kitambaa cha meza; turban ~ kilemba. 2 (naut) tanga, gamti, maradufu. 3 (rel) a man of the ~ kasisi. ~es n 1 mavazi, libasi, nguo; in plain ~es katika nguo za kiraia put on/take off one's ~es vaa/vua. 2 (bed-clothes) nguo za kitandani. ~es -basket n tenga la kuwekea nguo za kufua. ~es -horse n ubao wa kuanikia nguo. ~ es-line n kamba ya kuanikia nguo. ~es -man n mchuuzi wa mitumba/nguo kuukuu. ~ es-moth n nondo mla nguo. ~es -peg n kibanio. ~ es-prop n (also ~es-post) mwegamo (wa kamba ya kuanikia nguo). ~ier n (arch) mchuuza nguo au vitambaa. ~ing n nguo, mavazi, libasi articles of ~ing mavazi. the ~ing trade n biashara ya nguo. ~e vt 1 vika, visha. ~ oneself vaa, jivisha. 2 (fig) fumba, eleza ~ in a sweet language fumba/eleza kwa lugha tamu.

cloture n (US) closure.

cloud n 1 wingu; mavundevunde. ~ bank n mawingu mazito yaliyo chinichini. ~-burst n tufani ya mvua. ~capped adj -lofunikwa na mawingu. 2 (of mass of things moving together) kundi. ~ of bees kundi la nyuki. 3 (of smoke, dust, sand) ghubari. 4 jambo linalotia hofu, wasiwasi, tishio, n.k. the ~ of hunger tishio la njaa. 5 utusitusi ulio kwenye uoevu au kioo. have one's head in the ~s (fig) wa ndotoni, -

clout

wa mbali kimawazo. 6 fifisha age has ~ed his memory umri umefifisha kumbukumbu yake. vt 1 tia kivuli/giza, ficha mwangaza it has ~ed over kumetanda. ~ up/over tanda, funika (na mawingu) ~ed her eyes machozi yalimlengalenga. 2 (aggrieve) kanganya, vunga, huzunisha. 3 (defame) aibisha, tweza, pata huzuni. ~y adj. ~less adj. ~iness n.

clout n (arch) 1 (colloq) pigo (hasa la

mkono). 2 kitambaa (hasa cha kusugulia au kusafishia). 3 (of shoe) njumu. 4 (US sl) uwezo wa kushawishi/kutenda hasa kisiasa. vt 1 (colloq) piga. 2 pigilia njumu ya kiatu.

clove1 n garlic ~ kidole cha kitunguu saumu.

clove2 n 1 mkarafuu. 2 karafuu,

clover n (bot) klova: jamii ya mimea yenye majani ya pande tatu (hupendwa sana na ng'ombe, mbuzi n.k). live in ~ kaa katika hali ya neema.

clown n 1 chale, damisi/ mcheshi. 2

mpumbavu. 3 mtovu wa adabu. vi chekesha.

cloy vt kinaisha, kifu. ~ the appetite toa hamu ya kula. ~ing adj

club n 1 rungu. ~ footed adj -enye miguu iliyopindika. 2 (in cards) pau, mavi ya mbuzi. 3 chama, shirika la watu; klabu. vt 1 piga kwa rungu; 2 ungana; shirikiana. ~ together shirikiana. ~bable adj - kunjufu; in the ~ mjamzito.

cluck n 1 kidoko. 2 mlio (wa kuku

anayeita vifaranga vyake). vi 1 piga kidoko. 2 lia, fanya mlio kama kuku.

clue n alama, dalili, dokezo, ishara (ya kuonyesha njia, maana n.k.) give somebody a ~ dokeza, ashiria be without a ~ wa gizani; tokuwa na habari. ~in/up (sl) arifu. ~less adj jinga.

clump n 1 kichaka. 2 bonge (la

udongo). 3 fungu. 4 soli (nene);

kishindo. vt, vi 1 tembea kwa kishindo. 2 panda pamoja.

clumsy adj 1 (of person) -zito, -si stadi, si -elekevu. 2 -a ovyo, -jinga; goigoi. clumsily adv. clumsiness n.

clung pt, pp of cling.

clunk vi, n (fanya) sauti ya mgongano wa metali nzito.

cluster n 1 kishada. 2 (of people,

things etc) fungu, kundi. vi kusanyika; zunguka. ~ together/ round zunguka, kusanya, konga.

clutch1 vt ~ (at) 1 kamata imara, fumbata, shika. 2 ~ at jaribu kukamata a drowning man will ~at any straw mfa maji haachi kutapa n 1 kukamata, mfumbato. 2 klachi.

clutch2 n jumla ya mayai yanayoatamiwa; idadi ya makinda yaliyototolewa.

clutter n mparaganyo, vurugu,

mkusanyiko wa ovyo wa vitu. vt ~ up panga ovyoovyo, paraganya, vuruga. ~ up the paths zagaa njiani.

co- pref 1 mshiriki katika kazi, mwenzi ~ editor mhariri mshiriki ~wife mke mwenza. 2 pamoja na, -a mchanganyiko wa vitu viwili ~education shule ya mchanganyiko. ~adjutor n 1 mshirika katika kazi; msaidizi, mwenzi. 2 (rel) msaidizi wa askofu. ~axial adj -enye mhimili wa pamoja.

coach n 1 matwana farasi. drive a ~ and horses through something kwamisha jambo kwa kufichua upungufu wake, onyesha kasoro zake. 2 behewa la abiria. 3 (motor~) basi (liendalo safari ndefu). 4 kocha, mwalimu wa michezo. 5 (US) daraja la pili (katika vyombo vya usafiri). vt zoeza, fundisha kwa undani (hasa kwa kuandaa).

coagulate vt gandisha. vi ganda, tungamana. coagulant n dutu inayogandisha kioevu. coagulation n.

coal n makaa ya mawe. live ~s n

coalesce

makaa ya moto. dead ~s n makaa baridi. carry ~s to Newcastle rudisha tende Manga. haul somebody over the ~s kemea, karipia. heap ~s of fire on somebody lipa me ma kwa maovu vi,vt pakia makaa melini. ~ field n bondemakaa, machimbo ya makaa (mahali penye machimbo ya makaa). ~ gas n gesi ya makaa. (arch) ~ing station n (for ships) stesheni ya makaa. ~ -mine/pit n mgodi wa makaa. ~ scuttle n ndoo ya makaa. ~ face n kiambaza cha makaa. ~ tar n lami.

coalesce vi ungana, changanyika. ~nce n.

coalition n muungano, mseto ~

government serikali ya mseto.

coaming n kizibalango: ukingo

ulioinuka kuzuia maji yasiingie melini.

coarse adj 1 (rough)-a kukwaruza;

(nguo) isiyo laini. 2 (inferior) duni, hafifu. 3 (rude) -shenzi, bila adabu, -sio na adabu ~ language lugha ya matusi. 4 -enye chengachenga. ~n vi kwaruza; potosha. ~ness n.

coast n 1 pwani; mwambao, ufuko. 2 (US) mtelemko (ambapo unaweza kushuka kwa kuteleza the ~ is clear hamna hatari. vi ~ (along) 1 pita pwani pwani kwa, ambaa pwani, sairi. 2 (of cars, bicycles etc) telemka mlima bila kutumia nishati. ~ guards n walinzi wa pwani. ~-line n ukanda wa pwani. ~-wise adj & adv (a) pwani pwani. ~er n 1 chombo cha mwambao. 2 chombo cha kuteleza kisicho na magurudumu. 3 kikalio cha glasi/sahani/sinia (kuzuia meza isipate unyevu/maji). 4 mkeka mdogo wa kuwekea glasi.

coat n 1 koti ~ hanger kitundika nguo; kitundika koti. turn one's ~ badili msimamo/chama n.k; jiunga na adui au kundi jingine. you must cut your ~ according to your cloth fanya jambo kulingana na uwezo wako. trail one's ~ (-tails) zusha ugomvi. on someone's ~ tails (US)

kwa msaada wa mwingine. 2 kitu chochote kinachofunika (k.m. manyoya/sufu/nywele n.k.). 3 mpako; mkono give something a ~ of paint paka rangi. vt 1 funika. 2 paka (kwa rangi). ~ tail n sehemu ya chini ya koti iliyo pana. ~ing n 1 mkono. 2 kitambaa cha kutengenezea koti. ~tee n kikoti.

coax vt bemba, bembeleza, rairai,

shawishi; (of fire) vuvia ~ somebody into doing something bembeleza mtu afanye jambo fulani ~ something out of somebody pata kitu kwa kumbembeleza mtu. ~er n. ~ing n. ~ingly adv.

cob n 1 (corn) bunzi, guguta. 2 farasi mfupi mnene. 3 kotwe dume.

cobalt n kobalti: aina ya chuma ~ blue rangi ya nili iliyoiva.

cobble1 n (also ~stone) (jiwe) mango. vt tandaza mawe chini (wakati wa kujenga barabara).

cobble2 vt 1 shona (hasa viatu vilivyoharibika), tia kiraka. 2 weka ovyo ovyo. ~r n 1 mshona viatu. 2 mlipuaji. 3 kinywaji baridi cha divai, sukari na malimau. 4 aina ya pai ya matunda.

cobra n swila, firi.

cobweb n utando wa buibui.

coca n (bot) 1 koka: mojawapo ya magugu yapatikanayo Amerika ya Kusini yenye majani yanayofanana na majani ya chai. 2 majani yaliyokaushwa ya mikoka.

cocaine n kokeini: aina ya dawa ya kulevya.

coccyx n (anat) kifandugu, kitokono.

cochineal n kochinili: rangi nyekundu

inayotokana na kochinili jike.

cochlea n (anat) komboli: sehemu iliyoko ndani kabisa ya sikio ambayo inafanana na kitu kama springi ambamo mawimbi ya sauti hufasiriwa kuwa fahamu).

cock1 n 1 jogoo, jimbi; kikwarakucha.~ and bull story hadithi ya kipuuzi isiyo ya kuaminika. ~ -a doodle -doo kokoriko, mlio wa jogoo. ~

cock

-a hoop adj -a kufurahi sana, -enye kujigamba adv kwa kujigamba. ~ crow n alfajiri. ~-fight n mashindano ya kuchi. live like fighting ~s -ishi kama lodi. ~ of the walk (often derog) kiongozi, mtu anayetawala/kandamiza wengine. ~erel n kijogoo, pora. 2 ndege dume. 3 (of water tap) bilula, chombo/vali ya kufungulia na kufunga k.v. maji n.k. 4 (of gun) kibiri. position of ~ iliyopangwa tayari kufyatuliwa. go off at half ~ anza (sherehe/mipango) kabla matayarisho hayajawa sawa. 5 (vulg sl) mboo. ~up simamisha. ~ up one's ears tega masikio. ~ed to one side iliyokaa/-simama. 6 ~ up (sl) haribu, chafua, udhi they completely ~ed up our plans waliharibu mipango yetu. vi (colloq) tambatamba; injika risasi. ~ up weka upande (kofia/ kichwa). ~ed adj. ~-eyed adj 1 (sl) -enye makengeza, -a upogo. 2 (sl) -pumbavu; puuzi. ~y adj -enye majivuno, -enye kiburi -enye sodai, -a kujiamini mno.

cock2 n rundo (la majani makavu; samadi n.k.). vt rundika. ~ade n 1 kishada cha kasha la kofia. ~atoo n 1 kasuku kishungi. 2 (Aust. & NZ colloq) mkulima mdogo. ~chafer n tutu.

cock-horse n kinyago cha farasi wa

kuchezea watoto.

cockle n 1 (Phr.) ~s of the heart hisia za moyo. warm the ~s of one's heart pendeza sana. 2 mashua, boti ya bapa. 3 (of shell fish) kamba; kaa; chaza.

cockney 1 mkukni: mtu wa London

(hasa sehemu ya mashariki). 2 lafudhi ya kikukni.

cockpit n 1 (of aeroplane) dungu, chumba cha rubani; (fig) eneo ambapo vita vimewahi kupigwa mara nyingi. 2 kiwanja cha kupiganishia kuchi.

cockroach n mende, kombamwiko. cockscomb/coxcomb n 1 undu, kilemba, upanga wa jogoo. 2 mmea kishungi (mmea wenye vishada vya maua ya njano na mekundu). 3 chepeo ya mchekeshaji.

cocksparrow n shoredume (fig)

mgomvi, kijana mgomvi; mwenye kujiona.

cock-sure adj 1 hakika kabisa. 2 -juvi tena -enye majivuno; -enye kujiamini sana.

cocktail n 1 kokteli: kileo kikali cha mchanganyiko wa divai n.k. 2 mchanganyiko wa maji ya matunda. 3 mseto wa saladi na matunda.

coco n (also ~ palm, ~nut palm)

mnazi. ~nut n nazi. green ~nut n dafu; koroma ~ leaf kuti; (for thatch) makuti ya mbale, makuti ya viungo; (for screen, enclosure) makuti ya kumba, makuti mazimi (fibre,) ~ coir makumbi (cleaned fibre) usumba ~ shell kifuu ~ oil mafuta ya nazi ~shoot kitale ~ grate chicha ~ milk tui which accounts for the milk in the ~ nut (joc) sasa yote imeelezwa.

cocoa n kakao. ~ bean n kokwa za kakao. ~ nib n kotiledoni ya kakao.

cocoon n kifukofuko.

cod1 n (also ~-fish) chewa. ~-liver oil n mafuta ya chewa. ~ling n

chewa mdogo.

cod2 vt,vi (arch, colloq) fanyia mzaha, cheza shere.

coddle vt 1 ivisha taratibu (kwa joto lisilo kali sana). 2 engaenga, tendekeza, dekeza; endekeza.

code n 1 mkusanyiko wa sheria zilizopangwa kwa mfumo maalum. penal ~ n kanuni ya adhabu. 2 mfumo wa kanuni na taratibu zilizokubaliwa na jamii/tabaka/ kikundi cha watu. 3 ishara (mfumo wa alama zinazo- tumiwa katika maandishi ya siri au yaliyofupishwa; alama ya siri. break a ~ gundua jinsi ya kufumbua siri. vt (also en~) andika kwa kutumia alama za

codeine

maandiko ya siri; simba. codify vt panga kanuni, weka katika mpango ulio wazi. codification n.

codeine n kodeini : kitulizaji

kitengenezwacho kutokana na kasumba.

codex n kodeksi: kitabu cha miswada ya kale.

codger n (colloq) mzee wa vituko;

jamaa.

codicil n kiambatisho cha wasia

(kinachofafanua zaidi au kutangua sehemu ya wasia huo).

codling n tofaa la kupikwa.

coefficient n 1 kizigeu wiano kati ya vipimo viwili. 2 (maths) kizidishi.

coequal adj, n sawasawa (hasa kwa umri, cheo, uwezo n.k.).

coerce vt 1 shurutisha, lazimisha,

gagamiza. 2 (often pass) dhibiti, onea. coercion n. coercive adj.

coeval adj 1 -enye hirimu, rika moja. 2 -a wakati mmoja.

coexist vi ishi pamoja chanjari (kwa amani). ~ence n .~ent adj.

coffee n kahawa. ~-bean n buni.

~cup n kikombe cha kunywea kahawa. ~-grounds n (pl) machicha ya kahawa. ~-house n mkahawa. ~-mill/ grinder n kinu cha kusagia kahawa (buni iliyokwisha kukaangwa). ~-pot n mdela. ~-room n mkahawa mdogo. ~-set n seti ya vyombo vya kahawa. ~-stall n. genge la kahawa. ~-tree n mbuni.

coffer n 1 sanduku, kasha kubwa (hasa la kuwekea fedha au vito). 2 (pl) mahali pa kuhifadhia dafina. the C~s of the State Hazina ya Serikali. 3 kibao cha nakshi; darizi. ~ dam n see caisson.

coffin n jeneza. (fig) a nail in one's ~ kitu kinachoharakisha kufa mtu. vt tia maiti katika sanduku.

coffle n mlolongo wa wanyama, watumwa n.k. waliofungwa pamoja.

cog n 1 jino la gurudumu (agh. gia). be a ~in the machine (fig) mtu/kitu kisichokuwa muhimu katika shirika, serikali, tasnia n.k. ~ -wheel n

gurudumu meno.

cogent adj (of arguments) -zito na kubalifu; -a maana. cogency n.

cogitate vi,vt tafakari cogitation n 1

kutafakari. 2 (pl) mawazo, mafikara, tafakuri. cogitative adj. cogitatively adv.

cognac n brandi (ya Kifaransa). cognate adj 1 ~ (with) -enye asili au chanzo kimoja (k.m. viumbe, lugha). 2 inayohusiana (na). n 1 neno lenye uhusiano na neno jingine. 2 (pl) ~s n jamaa wa damu. 3 (gram) ~ object n shamirisho yenye mzizi mmoja na kitenzi (k.m. ota ndoto).

cognition n utambuzi, ufahamu, ujuzi. cognitive adj tambuzi. cognizable adj -a kutambulikana. cognizance n 1 (leg) utambuzi, uzingatifu; kutambua. take cognizance of tambua; zingatia 2. haki/mamlaka ya kushughulikia jambo kisheria fall within one's cognizance -wa ndani ya uwezo wa ... (kushughulikia). 3 nembo. cognizant adj.

cognomen n 1 (surname) jina la ukoo. 2 jina la kupachikwa.

cohabit vi kaa kinyumba. ~ation n.

cohere vi 1 (of parts or whole)

ambatana, shikamana, fungamana. 2 (of arguments) fuatana kwa taratibu, chukuana, patana. ~nce n. ~nt adj 1 -a kuambatana, -a kufungamana. 2 -a kuchukuana (of speech) -a wazi,-enye kueleweka. cohesion n mwambatano, mshikamano; hali ya kuendelea kushikana pamoja. cohesive adj.

cohort n 1 (in ancient Roman

Armides) divisheni. 2 kundi la watu waliofungamana. 3 mwenzi, rafiki.

coiffeur n (fr) mtengeneza nywele. coiffure n (fr) mtindo wa utengenezaji nywele; mchano wa nywele.

coign n (US fig) ~ of vantage n mahali pafaapo kuonea kitu vizuri.

coil vt,vi zungusha, zongomeza, kunja, viringisha. n 1 koili: sukepindi la

coin

nyaya (za umeme). 2 mzingo, mkunjo. ignition ~ n koili mwasho 3 (of contraceptive) koili, kidude.

coin n 1 sarafu. false ~ n sarafu za

bandia the other side of the ~ (fig) kwa upande mwingine pay somebody back in his own ~ tendea mtu kama alivyokutendea, akutendaye mtende, mche asokutenda. vt 1 tengeneza sarafu. ~ money n (fig) pata donge kubwa. 2 (of new words) buni, tunga ~ a new terminology unda istilahi mpya. ~age n. ~er n mtengeneza sarafu bandia.

coincide vi 1 ~ (with) (of two or more objects) lingana, fanana (kwa eneo au umbo). 2 (of events) tukia, sawia/ wakati mmoja. 3 (of ideas etc) patana, oana, afikiana. ~nce n 1 ulinganifu, upatanifu, utukizi. 2 jambo litukialo kulingana na jingine (kwa nasibu au ajabu). ~nt; ~ntal adj -a nadra, tukizi.

coir n makumbi ya nazi; (cleaned)

usumba.

coitus/coition n ngono, mtombo;

mtombano, mlalano. ~interruptus n azili, katiza kujamiiana, chomoa kumwaga nje.

coke1 n mkaazimawe: makaa ya mawe yasiyo na gesi.

coke2 n koka-kola.

coke3 n (sl) kokeini.

col n mwegama, genge (la mlimani).

cola n (bot) mkola; kola.

colander n kung'uto; chujio.

cold1 adj 1 -a baridi ~ weather hali ya (hewa) ya baridi. ~ storage n chumba cha baridi. give somebody the ~ shoulder (fig) -tothamini, dharau have ~ feet -wa na hofu ya kufanya jambo leave one ~ -tovutwa na. in ~ blood kikatili. ~ -chisel n patasi ya kukatia metali baridi. ~ -fish n mtu asiyechangamkia watu. ~ -snap n kipindi (kifupi) cha baridi. ~ -sore n kidonda cha homa (mdomoni). ~ -steel n silaha ya kukatia au kuchomea. ~ -sweat n kijasho

chembamba. ~ -war n vita ya maneno na propaganda. ~ -blooded adj (fig) (of persons, actions) katili; -a damu baridi: -enye damu inayobadilika kufuatana na hali ya hewa. ~ hearted adj -sio na huruma, -siostuka; baridi. 2 (fig) sio -ema, hasimu; (of sex) -sionyegereka/ashiki. 3 (of colours) -agiza. ~ly adv. ~ness n 1 baridi (be left) out in the ~ dharauliwa, sahauliwa kabisa. 2 mafua. catch a ~ shikwa na mafua. 3 (phys) kiwango cha kuganda.

coleslaw n kachumbari ya kabichi.

colic n mchango: msokoto wa tumbo (bila kuharisha). ~ky adj.

coliseum n uwanja mduara.

colitis n (med) uvimbe wa utumbo mpana.

collaborate vi 1 shiriki katika kazi. 2 shirikiana kisaliti na adui. collaboration n collaborationist n mshiriki katika usaliti. collaborator n mshiriki, kibaraka.

collage n kolagi: picha itengenezwayo kwa kugandishwa vipande vipande vya karatasi, nguo, metali n.k.

collapse vi,vt 1 vunjika, anguka,

poromoka, gwa. 2 zimia, zirai, poteza fahamu/nguvu/uwezo/moyo. 3 (apparatus) kunjana, kunjamana. 4 kunjisha, fanya -jikunje. collapsible adj -a kukunjika. n 1 poromoko, uangamio. 2 mzimio, kukata tamaa. 3 ~ of the lung mzimiko wa pafu. ~of the dollar kuporomoka kwa (thamani) ya dola.

collar n 1 ukosi, kola. 2 ukanda wa shingo ya farasi/mbwa. 3 mkwiji, skafu, kashda. ~ -stud n kifungo, kibanio. 4 kiungo cha chuma cha kuungia mabomba. 5 ~ -bone n mtulinga. vt 1 kamata the police ~ed the thief polisi alimkamata mwizi. 2 (dated, colloq) chukua bila ruhusa.

collate vt 1 linganisha, pambanisha

(hasa maandiko). 2 (arrange) panga kwa taratibu (k.m. kurasa za vitabu

collateral

tayari kutiwa jalada). 3 weka pamoja (habari). 4 (rel) teua, chagua (kiongozi wa dini). collation n 1 ulinganisho. 2 chakula chepesi.

collateral adj 1 sambamba, bega kwa

bega. 2 -enye asili moja lakini wazazi mbalimbali (k.m. watoto wa ndugu wawili). 3 -a ziada, -a nyongeza. ~ -evidence n ushahidi wa nyongeza. n dhamana ya mkopo.

colleague n mwenzi, mshiriki (mmojawapo wa watu wawili au zaidi wafanyao kazi pamoja).

collect1 n (rel) sala fupi ambayo

inabadilika kufuatana na siku.

collect2 vt vi 1 kusanya, leta pamoja, changa. 2 chukua, zoa ~-a child chukua mtoto. 3 kusanyika, kutanika; konga. 4 ~ oneself jitayarisha; jikusuru. 5 hifadhi, pata nakala/sampuli (ya kitu). ~ed adj tulivu, makini. ~edly adv. ~ion n mkutano; halaiki, mkusanyiko/ ukusanyaji. 2 mchango (wa fedha)/ sadaka. 3 (of poems) diwani. 4 lundo. ~ or n mkusanya. ~ of customs mtoza ushuru/kodi. ~ive adj 1 -a pamoja n kundi, shirika linalomilikiwa na wafanyakazi wake. ~ive leadership n uongozi wa pamoja. 2 -a umma. ~ivefarm n shamba la umma/ujamaa. 3 (gram) ~ivenoun n nomino wingi. ~ively adv. ~ivism n ujima: mfumo a ujamaa ambamo nyenzo/zana kuu za uzalishaji mali humilikiwa na dola au umma. ~ivize vt unganisha; jumuisha; weka chini ya mamlaka moja; fanya jamaa. ~ivization n ujima, ujumuishaji.

colleen n (Irish) msichana.

college n 1 chuo cha elimu (agh sehemu ya chuo kikuu); walimu na wanafunzi wanaofanya sehemu ya Chuo Kikuu. C~ of Agriculture n Chuo cha Kilimo. 2 baraza, chama; jamii ya watu wenye nia moja. Sacred C ~; the C~ of Cardinals baraza la makadinali. collegiate adj. collegian n 1 mwanachuo.

collide vt ~ (with) gongana; pambana the ships ~d in the fog meli ziligongana katika ukungu. collision n mgongano, dafrao; mapambano be in/come into collision (with) pingana, pambana; gongana head-on collision mgongano wa uso kwa uso.

collier n 1 mchimba makaa (ya mawe). 2 meli (ichukuayo shehena) ya makaa ya mawe. ~y n mgodi wa makaa ya mawe.

colligate vt,vi 1 unga, unganisha, jiunga, jihusisha. 2 leta, weka pamoja (matukio au habari).

collocate vt (with) (of words) tangamana, tokea/enda pamoja.

collocation n tangamano, utokeaji/uendaji pamoja wa maneno.

colloquial adj (of words, phrases, style) kimazungumzo; -a simo. ~ly adv. ~ism n

colloquium n kongamano, semina ya

wataalamu. colloquy n (formal) mazungumzo, maongezi. engage in ~ zungumza.

collude vi (arch) kula njama, shirikiana, saidiana (hasa katika hila au udanganyifu). collusion n njama, ushirika, mapatano (hasa katika udanganyifu); maafikiano ya siri (ya hila, ujanja).

collywobbles n (pl) (colloq) kuumwa tumbo; woga, wasiwasi.

colon1 n utumbo mpana.

colon2 n koloni, nukta pacha.

colonel n kanali. ~ship n ukanali, cheo cha kanali.

colonnade n safu ya nguzo.

colony n 1 koloni. 2 (collection) jamii/kundi la wanyama/mimea, watu wa maslahi moja a ~ of plants/insects kundi la mimea/ wadudu wanaoishi pamoja. colonial adj -a kikoloni: (Hist) Colonial Office n (GB) Wizara ya Makoloni. colonial hangover n kasumba ya kikoloni. colonialism n ukoloni. ukoloni mkongwe. neo- colonialism ukoloni mamboleo. colonist n mkoloni; mlowezi, setla; mkazi wa

koloni. colonize vt tia ukoloni, anzisha koloni, tamalaki/twaa nchi ya wengine. colonization n ukoloni. colonizer n mkoloni, mtwaa nchi ya wengine.

color n (US) see colour.

~imeter n kipimarangi, kibainisha rangi.

colossal adj -kubwa mno; -enye nguvu kubwa. colossus n 1 sanamu kubwa mno. 2 (giant) jitu, pandikizi la mtu,sifa za mtu zilizozidiana.

colostrum n dang'a.

colour1 n 1 rangi there isn't enough ~ in the picture picha haina rangi ya kutosha ~ blind kipofu rangi. ~blindness n upofu rangi. ~scheme n mpangilio/ mchanganyo/mfumo wa rangi. ~ -wash n rangi (za maji) za kupaka kuta. 2 rangi za wasanii. powder ~s n rangi za unga. oil ~ n rangi ya mafuta. water ~ n rangi ya maji. 3 (of events, descriptions) sura, maana, maono. give/lend ~ to elekea kuthibitisha jambo fulani give false ~ing to sema uwongo; danganya. 4 (of facial expression) high ~ n uso wa kunawiri/ mwekundu. ~ful adj -liosharabu rangi, changamfu, -a kupendeza. ~less adj -sio na rangi/ -angavu; a ~less person mtu baridi, asiyechangamka. be off ~zingia. change ~ geuka rangi. 5 (of skin) rangi ya mtu. ~ bar n kalabaa: ubaguzi wa rangi. ~ problem n tatizo la ubaguzi. 6 (pl) bendera, beramu called to the ~s -itwa jeshini. nail one's ~ s to the mast amua, tangaza/ng'an g'ania/shikilia msimamo. sail under false ~s (fig) -wa mnafiki. show oneself in one's true ~ s bainisha tabia halisi ya mtu ilivyo. come off/pass an examination with flying ~s fanikiwa vizuri kabisa. stick to (one's) ~s kataa kabisa kuacha imani yako/shikilia imani yako. 7 local ~ (lit) maelezo ya kina/kinaganaga kuonyesha hali halisi ya mahala au

combat

wakati. ~ ful adj.

colour2 vt,vi 1 paka/tia rangi, -wa mwekundu. 2 (up) pata rangi; (blush) iva uso, geuka rangi. 3 (exaggerate) piga chuku, tia chumvi, potosha his hate ~ed his account chuki yake iliathiri maelezo aliyoyatoa; (misrepresent) potosha; singizia. ~in jaza rangi. ~ing n kitu kinachotia rangi, rangi (ya ngozi) ya uso; mtindo wa utiaji rangi wa msanii. coloration n 1 mpangilio wa rangi. 2 jumla ya imani/ misimamo n.k. ya mtu/kundi/ taifa. colorific adj 1 -a rangi nyingi. 2 -enye kutoa rangi.

colt1 n 1 mwana farasi dume. 2 (youth) kijana mdogo asiye na uzoefu. ~ish adj 1 -a mwana farasi. 2 -enye ujuzi mdogo.

column n 1 nguzo, mhimili; mnara. 2 kitu chenye umbo la nguzo. spinal~ n uti wa mgongo. 3 safu ya chapa. 4 mpango wa vitu kwa safu safu. 5 mlolongo. a ~ of cars/ships mlolongo wa magari/meli. ~ of figures safu ya tarakimu. ~ist n mwandishi wa habari anayeshughulikia mada au makala maalum.

coma n usingizi mzito; hali ya kuzimia. be in a ~. go into a ~ wa katika usingizi mzito, poteza hisia/fahamu, zirai, zimia kwa muda mrefu adj 1 -enye kuzimia. 2 -enye usingizi/kusinzia.

comb n 1 kitana; chanuo. 2 undu wa jogoo. 3 honey ~ sega la nyuki. 4 kichambuzi, kichaguzi (mashine inayochagua k.v. pamba). 5 kuchana give one's hair a ~ chana nywele. vt,vi 1 chana. ~ one's hair chana nywele. 2 (for wool, cotton etc.) chambua kwa chanuo au kichambuzi. 3 chakura, tafuta kila mahali. 4 ~out (fig) ondoa (vitu, watu wasio takiwa). 5 (of waves) kunjamana na inuka, vimba.

combat vt,vi (against/with) 1 pigana,

shindana na. n mapambano,

mapigano. single ~ n mapigano kati ya watu wawili tu. ~ant adj enye kupigana. n mpiganaji adj -a kupigana, -a kushindana, -a vita. ~ive adj chokozi, -enye uchu wa kupigana. ~iveness n upiganaji, tabia ya ugomvi. ~ively adv.

combine1 n 1 shirika la makampuni ya biashara. 2 ~ harvester n kivuna nafaka (kinachovuna na kupurura sawia).

combine2 vt,vi ~ (with) ungana; unga, unganisha; changanya, shirikisha. ~d operations/exercises n shughuli mchangamano. combination n 1 mchanganyo; muungano; uunganishaji. 2 mchanganyiko; ushirikiano enter into combination with ungana na. combination room n see common room chumba (kitumiwacho na wanafunzi na walimu shuleni/chuoni) cha kupumzikia. 3 (pl) combination n nguo ya ndani (inayovaliwa mwili mzima). 4 pikipiki yenye kigari ubavuni. 5 fomula. combination lock n kufuli la kufunguliwa kwa namba.

combustion n mwako. internal ~

engine n injini ya mwako wa ndani. combustible adj 1 -a kuweza kuwaka.2 (excitable) -a harara. n kitu chenye mwako. combustibility n (physics) uunguzaji, mwako.

come vi 1 ~ (to/from) (with) ja, wasili, fika ~ and see me njoo tuonane ~ this way pita huku. 2 ~ (into/ onto/in/on etc) ingia. ~ into the room ingia/karibu chumbani. 3 ~to something fikia the number of his children ~s to thirty idadi ya watoto wake inafikia thalathini. ~ to little/nothing tofanikiwa, -wa kazi bure she never came to much hakufanikiwa. ~ to this/ that maanisha, wa na maana ya, -wa hivyo (ilivyo) if it ~s to that kama mambo ndiyo hayo. (with fixed phrases) ~ to an agreement afikiana. ~ to blows (with) anza kupigana. ~ to a decision amua. ~

come

to an end isha; malizika. ~ to fruition iva, komaa, zaa matunda. ~ to a halt/standstill simama. ~ to light julikana, tangazwa. ~ to one's notice/attention tambuliwa fahamika. ~ to one's senses/oneself zinduka pata fahamu; jirudi. ~ to terms (with somebody) fanya suluhu, kubaliana, afikiana. 4 (tokea) (anza) kuwa. ~ into flower tokea/anza kuwa ua; chanua. ~ into bud chipua. ~into contact kutana, gusa,wasiliana. ~ into focus jitokeza, jiengua. ~ into money/ a fortune/legacy etc rithi/ pata/pesa. ~into operation anza kufanyakazi. ~ into one's own stahiki, pata heshima/sifa. ~ into power twaa madaraka.~ into sight/ view tokeza, onekana. 5 ~ to somebody (from somebody) achiwa, rithi (shwa). 6 ~ to somebody tukia, tokea, -ja nothing will ~to you hutadhurika. 7 elewa/tambua/ona hatimaye. ~ to realize -ja kung'amua. 8 how ~ (that) vipi, imekuwaje. 9 ja, jia; tokea; wa (mahala) her decision came as a surprise uamuzi wake ulitushangaza. 10 -wa, tokea kuwa, -ja kuwa. be as clever/stupid as they ~ kuwa hodari/ mpumbavu sana. 11 (colloq) jifanya, jitia don't ~ the bully usijitie ungambi/ubabe/ umwamba. 12 to ~ baadaye the life to ~ maisha ya baadaye. 13 (colloq uses) ifikapo, ijayo she will be 15 ~ December atakuwa na miaka 15 ifikapo Desemba. 14 (colloq) (of sex) mwaga/tema/kojoa (with adverbials and preps) 1 ~ about fanyika, tukia, jiri. 2 ~ across kuta, kutana na; ona kwa bahati; tokea (kwa) I ~across John in the market nilikutana na John sokoni. 3 ~ after somebody fuatia, fukuzia, fuata kwa kukimbilia. 4 ~ again rudi. please ~ again karibu tena. 5 ~ against kuta, gongana; shambulia. 6 ~ along fanya haraka, jitahidi,

come

endelea, fika ~ along now you know the answer jitahidi, unalijua jibu. 7 ~ alongside egeka, egemea. 8 ~ apart vunjika, katika, pasuka. 9 ~ at somebody/something fikia, pata, shambulia. 10 ~ away (from) achia, ondoka. 11 ~ back rudi, kumbuka his name came back to me nilikumbuka jina lake. ~ back at jibu, lipiza (kisasi). 12~ before somebody/something sikilizwa na, shughulikiwa na; tanguliwa na. ~ back n kurudi (tena); majibu; fidia his case will ~ before Judge Nyalali kesi yake itasikilizwa na Jaji Nyalali. 13 ~ between (interfere) ingilia kati; zuia it is not good to ~ between a man and his wife haifai kuingilia kati ya mume na mke. 14 ~ by pita; jia; pata kitu (kwa juhudi/bahati) ~ by my house pita nyumbani kwangu. 15 ~ down (collapse) anguka, poromoka; (of rain, snow etc) nyesha, -nya; (of prices) shuka, teremka; (be reduced) pungua. ~ down a peg shuka cheo. ~ down in the world angamia, shuka cheo. ~s /boils down to ~ ishia; maanisha; (of tradition) pokewa, rithishwa. ~ down upon kemea, adhibu, wia mkali. ~ down on the side of somebody unga mkono. ~ down to earth amini kama ilivyo, acha ndoto, tambua hali ilivyo. 16 ~ forth jitokeza, tokea mbele. 17 ~ forward karibia; jitokeza, jongea karibu, patikana. 18 ~ from zaliwa, chimbuka, tokea. 19 ~ in (of the tide) jaa (become seasonable) anza (kupendwa) when do mangoes ~ in

maembe yanapatikana lini? (fashionable) how does this style ~ in mtindo huu unapendelewaje/ unapokelewaje? ~ in handy/ useful faa, -wa na manufaa. ~ in for, pata, vuta you'll ~ in for a scolding utakaripiwa she's ~ in for a large amount of money amerithi fedha nyingi. ~ in on shiriki, jiunga. 20 ~ near jongea, karibia he

come

came near to failing alikaribia kushindwa. 21 ~ of -wa -a nasaba; tokana na; tokea she ~s of a given family -wa -a ukoo/ nasaba fulani what came of your conversation mazungumzo yenu yalikuwa na matokeo gani? 22 ~ off toka, tukia, fanyika; fanikiwa. ~ (something) dondoka; kimbia, okoka, banduka. ~ off a winner/loser shinda/ shindwa. ~ off victorious /badly pata ushindi/ hasara (colloq) ~ off it! acha! 23 ~ on fuata you go first I'll ~ on later tangulia nitakufuata baadaye; endelea his child is coming on fine mtoto wake anaendelea vizuri; kuta, vumbua, gundua. ~ on! njoo! endelea! (kwa mchezaji) anza kucheza ~ on let's have game njoo tucheze. 24 ~out tokea wazi, tangaa/bainika his book has ~ out kitabu chake kimechapishwa the whole affair has ~ out jambo lote limejulikana ~ out with a remark sema ghafula the workers will ~out again wafanyakazi watagoma tena. ~out first -wa wa kwanza ~ out in a rash pata vipele ~ out at so much afiki jumla (of stains etc.) these ink stains won't ~ out madoa haya hayatoki. ~out against/ for pinga/unga mkono. 25 ~ over (from a distance) fika; (change) geuka, enda upande mwingine, badili mawazo what has ~ over you limekutokea jambo gani ~ over funny/dizzy/faint jisikia vibaya, taka kuzimia. 26 ~ round zunguka; (visit) zuru, tembelea; (recover) pata fahamu ~ round to somebody's way of thinking badili mawazo. 27 ~ short of pungukiwa na; -wa na upungufu wa. 28 ~ through (recover from illness) pata nafuu, pona; pita your posting has just ~ through ajira yako imepitishwa. 29 ~ to pata fahamu ~ to one's senses pata fahamu baada ya kuzimia; husu when it ~s to politics inapohusu siasa; (colloq) jitambua. ~ to grief

patwa na ajali (matata n.k.). ~ to a head iva. ~ to pass fanyika, -wa, tukia, jiri. 30 ~ under something -wa chini ya. 31 ~ up (grow) mea, ota, kua; fikia; (appear) tokea, zuka, onekana ~ up against somebody pambana, gongana, kutana your work has not ~ up to expectations kazi yako hairidhishi. ~up with fikia 32. ~ upon somebody shambulia ghafla.

comedy n 1 futuhi; tamthiliya kuchekesha. 2 tukio au mkasa unaochekesha musical ~ futuhi yenye muziki. comedian n chale, mtu wa mikasa/mizaha; mchekeshaji. comedienne n chale wa kike.

comely adj (old) (arch) (usu of

person) -zuri, -enye sura, maungo ya kupendeza. comeliness n.

comer n mjaji, anayekuja. all ~s n wajaji wote. first ~ n mja awali, anayekuja kwanza. late-~ n mchelewaji.

comestible n (formal, usu pl) chakula, kitu cha kula, kitu kinachofaa kuliwa.

comet n kimondo.

comeuppance n adhabu/maafa stahilifu.

comfit n (old (arch) 1 haluwa. 2 tunda

lililogandishwa kwa sukari. 3 kashata.

comfort vt fariji, liwaza, ondolea, majonzi. n 1 faraja, maliwazo; jamala. cold ~ n maliwazo yasiyoridhisha. take ~ (from) jifariji. 2 tumbuizo, burudani. 3 raha, hali njema, starehe, anasa. creature ~s n mambo ya anasa (US) ~ station n (US) choo cha umma. ~able/also comfy adj -a kustarehesha; -a raha it's so ~able here hapa pana starehesha kweli. 2 -a kufariji, kutuliza be ~able about somebody, ridhika na. ~ably adv. be ~ably off -wa na pesa za kutosha. ~er n 1 mfariji. the C~er Roho Mtakatifu. 2 (GB) shali/ skafu/kashida ya sufu ya kuvaa shingoni. 3 (GB) chuchu (ya mtoto). 4 (US) blanketi zito.

commemorate

comic adj 1 -a kuchekesha, -chekeshaji; -a mzaha. 2 -a futuhi n 1 chale (katika sanaa za maonyesho/ muziki). 2 ~ book n gazeti lenye hadithi za katuni.~al adj -a kuchekesha; -a kimzaha. ~ally adv. coming adj see come -a kuja; -naokuja; baadaye. n 1 majilio the Second Coming Majilio ya Pili ya Yesu Kristo.

comity n uhusiano wa kirafiki ~ of

nations uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa.

comma n mkato, koma. inverted ~s n

alama za kufungua na kufunga usemi, yaani ("....") au (`....').

command vt 1 amrisha, amuru. 2 (control) (govern) tawala; ongoza; -wa na amri juu ya (watu mali n.k.). 3 (emotions) zuia, tawala. 4 -wa na uwezo juu ya. 5 stahili, kuwa na ~ respect and sympathy stahili kupewa heshima na huruma. ~ a high price stahili kuuzwa kwa bei ya juu. 6 (front, overlook) tawalia/dhibiti uwanda (kwa sababu ya kuwa juu) the hill ~s the plains kilima kinadhibiti uwanda. n 1 (order) agizo, amri. 2 utawala; ukuu I'm at your ~ niko chini ya amri yako. at the word of ~amri inapotolewa. 3 uwezo have a ~ of several languages fahamu lugha kadhaa. have ~ over oneself jitawala. ~ post n kituo cha kamanda. ~ing adj 1 -kuu; -nayotawala ~ing heights of the economy nguzo kuu za uchumi; nayostahili heshima. ~ant n (mil) mkuu (wa boma, ngome, kikosi, kambi n.k.). ~eer vt twaa (magari, nyumba) kwa matumizi ya jeshi. ~er n kamanda, mkuu wa kundi la askari au manowari; amiri jeshi. C~er- in -Chief n Amiri Jeshi Mkuu. ~ment n 1 amri ya Mungu. the Ten C~ments n amri kumi za Mungu. 2 amri, agizo.

commando n komando: kundi la jeshi kwa kazi maalum.

commemorate vt fanya ukumbusho wa,

commence

fanya kumbukumbu ya, adhimisha sikukuu ya kukumbuka mtu (jambo fulani). commemorative adj. commemoration n ukumbusho (kwa sala, heshima, sikukuu, mchezo, karamu n.k.). in commemoration of kwa ukumbusho wa, kwa kumbukumbu ya.

commence vt,vi anza; amiri, anzisha. ~ment n 1 mwanzo. 2 (in US Universities, and at Cambridge and Dublin) sherehe ya mahafali ya kutunuku shahada/stashahada.

commend vt 1 (praise) sifu, tukuza. 2(entrust) weka amana, weka mikononi mwa. he ~ed his soul to God aliweka roho yake mikononi mwa Mungu. 3 ~ me to so-and-so nisalimie fulani. 4 ~ oneself/itself to pendwa na; kubaliwa na. ~ble adj -a kustahili kusifiwa. ~ation n sifa.

commensurable adj -a kupimika kwa jinsi moja; -a kulingana, -a kadiri moja. commensurate adj 1 -a kipimo/kadiri iliyo sawa. 2 -a kufaa.

comment n neno, fasiri, wazo, maoni. no ~ sina neno. vt ~ (on/upon) toa mawazo/maoni. ~ary n 1 sherehe. 2 tangazo mfululizo (juu ya tukio) wakati likitendeka broadcast ~ on a football match tangazo la mchezo wa kandanda. ~ate vi toa maoni juu ya jambo fulani. ~ator n 1 mtoa maoni. 2 mtangazaji (wa tukio).

commerce n 1 biashara, (hasa baina ya mataifa); ubadilishanaji na ugawaji wa bidhaa. Chamber of C~ n chama cha wafanyabiashara. Faculty of ~ n Kitivo cha Biashara. commercial adj 1 -a biashara commercial radio, redio ya biashara (inayojigharamia kutokana na malipo yatozwayo kwa vipindi vya biashara). commercial traveller n mchuuzi msafiri: mtu asafiriye kuonyesha vitu vya biashara na kupokea maagizo juu yake. 2 -nayoweza kuleta faida. 3 -a kupenda faida tu. n tangazo la biashara (katika vipindi vya TV au redio). commercially adv.

commercialize vt geuza -a biashara ili kupata faida commercialize sports geuza michezo iwe biashara. commercialism n.

commination n tishio la kulipiziwa kisasi na Mungu (hasa kwa wafanyao dhambi). comminatory adj.

commingle vt,vi changanya,

changanyika.

commiserate vt,vi (with) -pa mtu pole, sikitikia, hurumia. commiseration n.

commissar n kamisaa. Political C~

n kamisaa wa siasa: afisa wa chama, Wizara, Shirika, Jeshi n.k. katika jeshi la Urusi. ~iat n 1 (out of use) idara ya jeshi kwa ajili ya ugawaji wa chakula. 2 ugawaji wa chakula. ~y n 1 naibu, mjumbe; wakili; kamisaa wa jeshi (anayehusika na ugawaji wa chakula). 2 duka la chakula (la jeshi, kampuni n.k.). ~ial adj.

commission n 1 tume. Presidential C~ n Tume ya Rais. 2 utoaji mamlaka/wajibu (kwa mtu au kundi la watu); agizo, amri. 3 (crime) tendo, utendaji. ~ of a crime tendo la jinai. 4 hati ya kibali cha kupewa cheo katika jeshi. get one's ~ pata cheo cha ofisa. 5 asilimia ya faida (anayopewa mwuza bidhaa) sell goods on ~ uza bidhaa na kupata asilimia ya faida yake. 6 kazi (yenye ujira wake maalum) she received the ~ to paint the President's picture alipewa kazi ya kuchora picha ya Rais. 7 in ~ (of ship) -wa tayari kusafiri (yenye mabaharia na vyakula vyote vinavyohitajika). 8 out of ~ iliyoharibika, isiyofanya kazi tena my radio is out of ~ redio yangu imeharibika. vt 1 teua; agiza kazi kwa malipo maalum. 2 (mil) pa mtu cheo cha ofisa. 3 (of warship) tayarisha kwa pigano. ~ed adj -enye cheo cha ofisa. ~er n 1 mwanatume. 2 mkuu; kamishna. District C~er n Mkuu wa Wilaya. Regional C ~er n Mkuu wa Mkoa/

commissionaire

kamishna. 3 wakili wa serikali, mwenye kuagizwa, mwenye amri. ~er for oaths n wakili wa kuapisha. High C~er n Balozi (katika nchi za Jumuiya ya Madola).

commissionaire n bawabu (wenye yunifomu maalum wa hoteli, senema n.k.).

commit vt 1 tenda, fanya. ~ adultery zini. ~ a crime fanya kosa la jinai. ~ murder ua. ~ suicide jiua. 2 peleka; kabidhi; tia. ~ somebody for trial peleka mahakamani ~ a child to someone's care kabidhi mtoto kwa mwingine ili amtunze. ~ to writing tia katika maandishi. ~ to memory jifunza kwa ghibu, hifadhi kwa moyo. ~ to the flames unguza ~ to the earth zika. 3 ~ oneself jipa sharti; ahidi he has ~ted himself amejipa sharti, ameahidi without ~ting myself bila ya kujifunga. 4 ~oneself to diriki, kubali wajibu. ~tal n 1 upelekaji, uwekaji the ~tal of a body to the earth kuzika. ~tal of somebody to jail kupeleka mtu gerezani. warrant of ~tal hati ya kifungo. ~ted adj 1 -enye msimamo. 2 -a kujitolea nafsi. ~ ment n 1 sharti; ahadi honour your ~ments heshimu ahadi zako.2 wajibu. 3 moyo, msimamo. political ~ment n msimamo wa kisiasa. 4 tendo la kupeleka (kifungoni n.k.).

committee n kamati. executive ~ n kamati ya utendaji. steering ~ n kamati ya uendeshaji member of the ~ mwanakamati.

commode n 1 almari. 2 kibago cha kuwekea kibakuli cha haja cha chumbani. 3 (US) choo.

commodious adj -enye nafasi (ya kutosheleza), -a kufaa; -kubwa, enevu. ~ness n.

commodity n bidhaa, kifaa. essential ~ n bidhaa muhimu.

commodore n kamadori: ofisa wa jeshi agh. la majini au angani mwenye cheo cha juu ya kapteni; kapteni mwandamizi wa meli za biashara.

commune

common adj 1 -a pamoja,-a wote.

a ~ land n ardhi ya wote, ardhi ya umma. ~ consent n makubaliano ya pamoja/wote. ~ knowledge n habari inayojulikana na wote. ~ ground n (fig) hoja inayokubaliwa na wote katika majadiliano. ~ room n (in schools, college) chumba cha mapumziko. 2 -a kawaida. ~ soldier n askari wa kawaida, kuruta. ~ sense n maarifa ya kawaida. ~ practice n jambo la kawaida (kutendwa). 3 (Math) -a shirika ~ factor/multiple kigawo/kigawe shirika. (GB) ~ Law n sheria zisizoandikwa. ~-law wife n kimada. ~ market n soko la ushirikiano/ pamoja. 4 ~ noun (gram) n nomino ya jumla. 5 (colloq) (of persons, their behaviour and possessions) hafifu, -baya. ~ manners n tabia mbaya. ~ly adv, n 1 eneo la ardhi lisilo na mwenyewe, ardhi ya jumuiya yote. 2 in ~ kwa ajili ya wote, kwa wote. in ~ with pamoja na; sawa na out of the ~ si -a kawaida. ~er n mwanachi wa kawaida. ~s n (pl) (arch) 1 umma. 2 the House of C~ n (sometimes the Commons) Bunge la Uingereza lililochaguliwa na wananchi). 3 short ~s n uchache/upungufu wa chakula be on short ~s -topata chakula cha kutosha. ~alty n watu wa kawaida, makabwela. ~wealth n 1 dola; jumuiya ya madola. 2 The C~wealth n (also ~wealth of Nations) Jumuiya ya Madola: jumuiya ya nchi huru zilizokuwa chini ya utawala wa Kiingereza.

commotion n (disorder, uproar) vurugu, ghasia, makelele, vurumai, rabsha. make a ~ piga kelele, fanya ghasia in a state of ~ katika hali ya ghasia.

commune1 n 1 wajima: kikundi cha

watu wanaoishi pamoja na kugawana mali zao. 2 kikundi cha watu wanaofanya kazi pamoja kwa faida ya wote. 3 eneo la kikundi. 4 (in

France etc) Halmashauri. communal adj 1 -a jumuia; -a kutumiwa na watu wote. 2 -a kuhusu vikundi mbalimbali katika jamii communal disturbances fujo kati ya vikundi mbalimbali (kwa sababu ya dini, taifa, rangi n.k.). communalism n ujima.

commune2 vi 1 (with) jisikia kuwa

pamoja. ~ with the night vaa usiku. 2 (together) badilishana mawazo n.k. 3 (rel) pokea komunyo/ushirika mtakatifu. communicant n 1 (informer) mpasha habari. 2 (rel) mpokeaji wa komunyo.

communicate vt,vi 1 (share, pass) toa, pasha, pitisha (habari n.k.). 2 (with) wasiliana na. 3 ungana na (kama nyumba, bustani, chumba kwa njia ya mlango, geti n.k.). 4 (rel) pokea Ushirika Mtakatifu/komunyo. 5 jieleza that student can't ~ well yule mwanafunzi hawezi kujieleza vizuri. communication n 1 mawasiliano. 2 njia za mawasiliano (k.m. simu, reli n.k.). 3 habari, taarifa communication from the chair taarifa ya mwenyekiti. communication cord (in train) mnyororo ya tahadhari. communicable adj 1 -enye kuwezekana kuelezwa. 2 (of disease) -a kuambukiza. communicable disease n maradhi ya kuambukiza. communicative adj -enye kupenda kuwasiliana. communicativeness n. communicator n.

communion n 1 (sharing) ushirikiano,

umoja. 2 kupeana/kushirikiana (mawazo, n.k); urafiki. 3 ushirika: jamii ya watu wenye kanuni zile zile za imani. 4 (rel) (Holy) Communion Komunyo: Karamu Takatifu, Ushirika Mtakatifu.

communique n taarifa. joint ~ n taarifa ya pamoja.

communism n ukomunisti. communist n mkomunisti. communist party n chama cha kikomunisti.

community n 1 jumuia religious ~

jumuia ya watawa/mapadre. 2 umoja,

company

usawa a ~ of interests watu wenye mawazo sawa. C~ Centre n Jumba la Starehe. ~ chest n akiba ya fedha ya jumuiya za kuwasaidia wenye dhiki. ~ singing n uimbaji wa pamoja. in ~ pamoja.

commute vt,vi 1 badilisha (aina ya

malipo k.m. pesa badala ya huduma). 2 punguza adhabu, toa tahafifu, -pa tahafifu. 3 badilisha (mkondo umeme). 4 safiri kila siku mjini (kwa treni/gari n.k.). ~r n msafiri wa aina hii. commutable adj -a kuweza kubadilishiwa/ kupunguzwa au kusahilishwa . commutation n 1 ubadilishaji. 2 (of punishment) tahafifu. 3 (US) commutation ticket n tiketi ya muda. commutator n komutata: chombo cha kugeuzia mwelekeo wa mkondo umeme.

compact1 n mapatano, maafikiano,

mkataba.

compact2 n bweta la poda (daima

huwa na kioo).

compact3 vt unganisha; gandamiza;

gandisha adj (firm) -gumu, -a kubanana, imara; thabiti. 2 (close) -a karibukaribu. 3 (brief) fupi, -lioshikamana vizuri. ~ness n.

companion1 n 1 mwenzi, rafiki,

mwandani. ~ in distress mwenzi katika shida. 2 ~ volume n kitabu cha rejea/ mwongozo. ~able adj. ~ship n.

companion2 n (naut) 1 dirisha la kupitisha mwangaza chini melini. 2 ~ ladder way ngazi ya ndani ya meli.

company n 1 kuwa pamoja na

wengine I shall be glad of your ~ nitafurahi kuwa pamoja nawe. sin in good ~ watu bora zaidi wamefanya vile vile keep ~ with kuwa na urafiki na (hasa mwanamume kwa mwanamke) keep (bear) somebody ~ enda naye, kaa naye. part ~ achana (na) two's ~ three's a crowd wawili ni sawa akiongezeka mmoja ni vurugu. 2 wageni walioalikwa a

man is known by his ~ tabia ya mtu hujulikana kutokana na marafiki zake. in ~ mbele ya watu. 3 mwenzi he is good ~ ni mwenzi mzuri. 4 Kampuni. private ~ n kampuni ya binafsi. 5 (mil.) kombania. 6 kundi la watu wafanyao kazi pamoja (k.m. wasanii, mabaharia).

compare vt,vi 1 ~(with) linganisha ~these poems linganisha mashairi haya this is large ~d with that hii ni kubwa ikilinganishwa na ile. ~ notes badilishana mawazo. 2 ~ (to) tofautisha/fananisha, mithilisha it is not to be ~d to mine isifananishwe na yangu he ~d music to food alifananisha muziki na chakula. 3 (gram) linganisha. n beyond/ without/past ~ -sio kifani, bila mfano. comparable (to, with) adj -a kuweza kulinganishwa na, -a kufananishwa na. comparative adj 1 linganishi. comparative linguistics n isimu linganishi. 2 -a kulinganisha live in comparative luxury ishi maisha ya anasa ukilinganisha na. 3 (gram) linganishi comparative adjective n kivumishi linganishi. comparatively adv. comparison n 1 ulinganishi; mlingano. 2 (likeness) mfano, mithili, kifani there is no comparison between them havifanani hata kidogo, havilingani. 3 (gram) degrees of comparison viwango

linganishi make/draw a comparison between A and B linganisha baina ya A na B stand (bear) comparison with weza kulinganishwa na by comparison kwa kulinganisha. comparisons are odious si vizuri kulinganisha.

compartment n chumba (agh. behewa au ofisi iliyogawanywa katika sehemu kadhaa). ~alize gawa katika vyumba; tenganisha.

compass n 1 (magnetic) dira. 2 (circle) duara, mzingo. 3 (pl) also a pair of ~es bikari. string ~ n bikari ya uzi. 4 (extent) eneo, (limit) upeo, kikomo, mpaka. ~-window n dirisha roshani

competent

vt see encompass.

compassion n huruma, kite have ~ on somebody onea (fulani) huruma. ~ate adj -enye huruma, -pole. ~ate leave n likizo ya huruma.

compatible adj ~(with) 1 (of ideas,

arguments principles etc) -a kupatana; -a kulingana. 2 (of people) -a kutangamana,-a kuweza kuchukuana. compatibility n upatanifu, ulinganifu, hali ya kuchukuana.

compatriot n ndugu wa kwetu, wa nyumbani.

compeer n (arch) 1 mwenzi. 2 mtu aliyelingana na mwingine (kwa cheo au uwezo).

compel vt (-ll-) 1 (to something) lazimisha, shurutisha, juburu. ~ling adj -a kuvutia sana. a ~ling film filamu ambayo inavutia sana.

compendious adj (of authors, books

etc). -enye ufupisho kamili/makini. compendium n ufupisho kamili /makini.

compensate vt,vi fidia, toa fidia; lipia~ for the lost book fidia kitabu kilichopotea. compensatory adj. compensation n 1 fidia, dia.

compere n (F) mtangazaji (wa sanaa

za maonyesho, kipindi cha TV n.k.). vt tangaza.

compete vi shindana. competition n mashindano open competition mashindano ya wazi throw something open to competition tangaza ili kushindaniwa business competition mashindano ya biashara. competitive adj 1 -a ushindani, -a mashindano competitive examination mtihani wa mashindano. 2 (of people) -a kupenda kushindana. competitor n mshindani.

competent adj 1 -enye ustadi/uwezo/ uhodari. 2 (legitimate) halali,-a sheria. 3 -a kutosha -a kuridhisha. competence/competency n 1 uwezo, ustadi, uhodari; ufarisi. 2 (lit) (moderate means), riziki, mali (si nyingi ila) za kutosha. 3 (of a court,

compile

a magistrate) uwezo wa kisheria.

compile vt 1 tunga; kusanya (maarifa, habari n.k.) ~ a dictionary tunga kamusi. compilation n mkusanyiko, mtungo. ~r n.

complacence/complacency n ridhaa

(kupita kiasi). complacent adj 1 -a kuridhika, mno, -a kupendezwa. 2 complacently adv.

complain vi 1 nung'unika, lalamika. 2 (accuse) shtaki. ~ant n (leg) mlalamikaji, mshtaki. ~t n 1 (lament) malalamiko. 2 (grumbling) manung'uniko. 3 (illness) ugonjwa. children's ~ ts magonjwa ya watoto. 4 (leg) mashtaka. lodge a ~t andikisha shitaka.

complaisance n hulka ya kupendezesha/kuridhisha watu wengine; uelekevu. complaisant adj.

complement n 1 kijalizo, kitimizo, kikamilisho; kiasi kamili. (maths) ~ of a set kikamilisho cha seti. 2 (gram) shamirisho. vt kamilisha, timiza; shamirisha. ~ary adj 1 -a kutimizana, -a kukamilishana, -a kufanya kamili; -a -ote pamoja farming and industry are ~ary kilimo na viwanda hukamilishana. 2 (maths) ~ary angles n vikamilisho vya pembe mraba.

complete adj 1 kamili, -zima, kamilifu, -timilifu. 2 kabisa a ~ stranger mgeni kabisa. ~ surprise n jambo lisilotegemewa kabisa. vt timiza, maliza ~ ones education maliza masomo/kamilisha, ishiliza. ~ly adv kabisa my watch is lost ~ly saa yangu imepotea kabisa. ~ness n ukamilifu. completion n ukamilishaji, umalizaji; ukamilisho you will be employed on completion of your studies utaajiriwa umalizapo/ukamilishapo masomo yako.

complex adj 1 -enye sehemu/tabia nyingi, changamani. 2 -gumu kufahamika,-sioelezeka kwa urahisi, (gram) changamano. ~ sentence n sentensi changamano (commerce) ~

interest riba changamano. (Bio) ~sugar n sukari changamano. ~ situation n hali ngumu isiyoelezeka kwa urahisi. (Psy) inferiority ~ n hisia za udhalili. superiority ~ n majikwezo. ~ity n.

complexion 1 rangi ya uso, (ya asili),

takaso ~ cream krimu ya uso. 2 (disposition, quality) sura, hali that puts a new ~ on the matter hiyo inalipa sura mpya jambo hilo/hili.

complicate vt tatiza, tatanisha, fumba;

fanya kuwa changamano. ~d adj 1 -enye utata, mashaka, mafumbo, changamano a ~d machine mashine yenye muundo tata ~d business deals mambo changamani. 2 gumu ~d questions maswali magumu. complication n 1 hali ya kuwa tata; ugumu, kitu kiongezacho utata/ ugumu. 2 ugonjwa wa ziada; (med) ugonjwa mpya au unaotokea zaidi ya ule mtu alionao (na kufanya matibabu kuwa magumu) measles with eye and ear complications surua inayoambatana na matatizo ya macho na masikio.

complicity n ~(in) ushiriki (katika mabaya); tendo la kula njama.

compliment n 1 sifa, maneno ya

kusifu pay/make somebody a ~ sifu; taadhimu fish/angle for ~s tafuta kusifiwa. 2 (formal) salamu return the ~ rudishia sifa. my ~s to so and so nisalimie fulani. with ~s pamoja na salamu za ... pay one's ~s to somebody enda kuamkia (n.k.) ~s (of the season) heri ya Krismasi na mwaka mpya. vt 1 toa heshima, sifu. 2 salimu. ~ary adj 1 -a kusifu; -a kusalimu; -a kuheshimu; -enye kutoa heshima. 2 -a dibaji ~ title (in letter, book) dibaji. 3 -a bure, -a hisani, -a heshima. ~ary ticket n tikiti iliyotolewa bure.

complin(e) n (rel) (RC and AC) sajio: sala za mwisho jioni.

comply vi,vt tii, fuata, kubaliana. ~

(with) timiza, tekeleza (matakwa ya

component

mtu au kitu fulani). compliance n 1 tendo la kukubaliana, kuafikiana na; kulingana na, kufuatana na. in compliance with kulingana na. 2 radhi; ridhaa, ikibali, ukubalifu. compliant adj 1 -enye ikibali/ ridhaa; tiifu, sikivu, maridhia. 2 (of yield) -a kufuata wengine.

component adj -lio sehemu n (component part) kijenzi; kitu kisaidiacho kukamilisha kitu kingine.

comport vi,vt 1 heshimu, stahi ~ oneself with dignity jiheshimu, jistahi. 2 patana na, faa, chukuana na his conduct does not ~ with his rank tabia yake haichukuani na madaraka yake. ~ment n mwenendo mzuri, staha. compos adj (also compos mentis) (colloq) -enye akili timamu, -enye welekevu kamili. non compos mentis n afkani, mwendawazimu, punguwani.

compose vt,vi 1 fanyiza, tengeneza be ~d of -wa na sehemu (nyingi); tengenezwa kwa; umbwa kwa it is ~d of rock -metengenezwa kwa jiwe. 2 tunga, buni, andika (wimbo, shairi, mawazo, hotuba). 3 (printing) panga herufi za chapa ili kuunda maneno au sentensi. 4 tuliza. ~ oneself jituliza, -wa makini. ~d adj tulivu. ~dly adv. ~ r n mtungaji. composing frame n fremu ya kupanga herufi. composing machine n mashine ya kupanga herufi. composing stick n chombo cha kuwekea herufi. composition n 1 utungo, insha, kitu. 2 kazi ya sanaa k.v. kitabu, maandiko, nyimbo n.k. 3 utungaji/usanii wa kitu. 4 (agreements) mapatano. composition of creditors n mapatano ya wawia. 5 (mixture) mchanganyiko. 6 (ingredients) vijenzi, sehemu mbalimbali, asili za kitu. 7 kupanga herufi za chapa. 8 (Maths; Physics) kivungo. composite adj -enye sehemu (vitu, tabia) zaidi ya moja, -liofanywa na sehemu nyingine au na vitu

comprehend

mbalimbali. compositor n mpanga herufi za chapa. composure n utulivu, makini.

compost n mchanganyiko (hasa wa

mimea kufanya mbolea), mboji, mbolea mkusanyiko. vt fanya mboji/ mbolea mkusanyiko.

compound1 vt 1 (mix) changanya pamoja ili kupata kitu kipya na tofauti; unga. 2 (settle) tatua (tatizo), maliza ugomvi/deni. 3 (add to, increase) ongezea (tatizo, kosa, n.k.) adj 1 iliyotengenezwa kwa kuchanganya vitu viwili au zaidi; -lioungwa. 2 (gram) ambatani. ~ noun n nomino ambatani. 3 (make) -enye sehemu nyingi ~ interest riba mchanganyiko. ~ fracture n mvunjiko mkuu. ~ sentence n sentensi ambatani.~ word n neno ambatani. n 1 mchanganyiko/ msombo: kitu kilichochanganywa au kutengenezwa na vitu viwili au zaidi.

compound2 n 1 eneo maalumu (pengine hujengwa boma) lenye majengo, viwanja n.k. a school ~ n eneo la shule. a factory ~ n eneo la kiwanda. 2 ua, uga, kiwanja cha nyumba. 3 kambi ya wafanyakazi.

comprador n (arch) wakala wa kampuni au shirika la kigeni katika nchi. (fig) ~ bourgeoisie n bwanyenye kibaraka.

comprehend vt 1 fahamu, tambua, jua. 2 -wa na, ingiza, jumuisha. comprehensible adj -a kufahamika, -a kueleweka, -a maana, -a kutambulika. comprehension n 1 uwezo wa kufahamu, ufahamu, ujuzi, akili tambuzi it is beyond my comprehension siifahamu, siielewi, nashindwa kuelewa, inanizidi kimo, iko nje ya uwezo wangu wa kutambua. 2 eneo kubwa la maana au matumizi a term of wide comprehension neno lenye maana na matumizi mengi. 3 (of exercise) (zoezi la) ufahamu. comprehensive adj 1 pana the comprehensive faculty

uwezo wa kufahamu, akili tambuzi. 2 -enye vitu/ maarifa/ mambo mengi he took a comprehensive view of the subject alichungua alielewa habari zote za jambo hilo a ~ school shule ya sekondari kwa wote (bila vipaji au tabaka). comprehensiveness n. comprehensively adv .

compress vt 1 gandamiza, bana; shinikiza. 2 (of ideas, words, etc) fupisha. ~ible adj -a kushindilika, -a kupunguzika kwa kugandamizwa/

kwa kushindiliwa. n kigandamizo: kipande cha nguo kilichobandikwa katika sehemu ya mwili kuzuia damu kutoka, kutuliza homa, n.k. ~ion n 1 mgandamizo, mbano, msongo; shinikizo. 2 ufupisho. ~or n kishinikizi: kitu chochote kinachokaza kwa kushindilia (au kubana, au kugandamiza); kompresa: mashine itumikayo kubana hewa au gesi.

comprise vt -wa na... ndani yake the

book ~s all sort of knowledge kitabu kina maarifa ya namna mbalimbali.

compromise n mwafaka, masikilizano, maafikiano (ambapo kila upande hulegeza masharti/madai yake). vt 1 patana, ridhiana, afikiana, kubaliana juu ya jambo. 2 (endanger) tia hatarini, tia matatani. 3 tuhumisha vibaya. ~ oneself jiaibisha; jikashifu. comptroller n (accounts) (also controller) mdhibiti fedha.

compulsion n 1 shurutisho, ulazimishaji, sharti. under ~ kwa kushurutishwa. compulsive adj - siyoweza kudhibitika: -a lazima, -a kulazimisha. compulsive -liar n mwongopaji aliyekubuhu. compulsive smoking n uvutaji ulokithiri. compulsory adj -a lazima, -a sharti mathematics is a compulsory subject hisabati ni somo la lazima.

compunction n majuto; haya, aibu.

compunctious adj.

compute vt kokotoa, fanya hesabu. computation n mkokotoo.

computer n kompyuta. ~ services

division n idara ya huduma za

conceive

kompyuta. ~ise vt hifadhi kwenye kompyuta, tumia kompyuta.

comrade n 1 rafiki, mwenzi, sahibu, mwandani. 2 ndugu, komredi. ~ in arms n mwanajeshi mwenza. ~ship n.

con1 adv pro and ~ pande zote (hasi na chanya). the pros and ~s n hoja za pande zote.

con2 vt (naut) shika usukani wa chombo.

con3 vt (forml) chunguza kwa makini; jifunza kwa ghibu sana. ~ over sema kwa akili.

con4 n mfungwa.

con5 vt (colloq) danganya mtu. ~man n tapeli.

conation n (philos) uelekeo hiari: nia ya kutenda kwa hiari.

concatenate vt unganisha (kwa mfuatano), fuatana. concatenation n.

concave adj -a kubonyea, -enye shimo. ~ lens n lenzi mbonyeo. concavity n mbonyeo; ubonyevu.

conceal vt ficha, setiri ~ something from somebody ficha mtu jambo/kitu fulani. ~ment n. maficho. a place of ~ment mafichoni.

concede vt,vi 1 (admit) kubali, kiri, jitoa ~ a point in an argument kubali hoja katika majadiliano. 2 (grant) toa ruhusa, achia. 3 jitoa, jiweka chini (bila pambano). ~ defeat kubali kushindwa; salimu amri.

conceit n 1 majivuno, kiburi, makuu. 2

wazo/kauli chekeshi. ~ed adj -enye makuu/kiburi/majivuno.

conceive vt,vi pata/tunga/shika/chukua mimba. 2 ona, waza, dhani, fahamu ~a liking for somebody -mtia moyoni. ~ an idea tunga wazo. conceivable adj -a kuweza kubuniwa/kufikiriwa, -a kuwezekana. conceivably adv yawezekana. conception n 1 utungaji mimba; utungaji dhana. 2 wazo, dhana. concept n wazo, fikra, dhana. conceptualism n (philos)

umawazo, udhanifu. (conceptive, also conceptual) adj -a maana, -a akili, -a kuwaza moyoni, -a mawazo. conceptualize v -buni.

concentrate vt,vi 1 kusanya mahali

pamoja; leta pamoja, unganisha. 2 (condense) fanya -zito kwa kukausha maji/kushindilia/kugandamiza au kubana; ongeza nguvu ya kitu. 3 kolea ~d solution mmumunyo kolezi. 4 makinikia. ~ upon (on) something makinikia jambo. ~d adj. kali; -liokolea. concentration n 1 kukoleza; mkusanyo wa mahali pamoja. concentration camp n kambi ya wafungwa wa siasa /wakimbizi/mateka wa vita. 2 ukolezi. 3 umakinifu.

concentric adj -a kati moja, -enye kitovu shirika a system of ~ circles mfumo wa duara za kati moja. ~ity n.

concern vt,vi 1 (with/in/ about) husu it doesn't ~ you haikuhusu. 2 shughulisha; hangaisha don't ~ yourself with minor issues usijishughulishe na vitu vidogo. 3 sikitisha his very poor health ~s us afya yake mbaya sana inatunyima raha. n 1 uhusiano, ipasayo; ihusuyo it's no ~ of mine hainihusu. 2 jambo, shughuli. 3 ushirika; shirika; kampuni. a going ~ kampuni inayofanyakazi, kampuni hai. 4 (interest) hisa he has a ~ in business ana hisa katika biashara. 5 masikitiko, (anxiety) shaka, hangaiko, tatizo, shauku. ~edly adv.

concert n 1 (mus) burudani/ maonyesho ya muziki. 2 umoja wa shauri acting in ~ tenda kwa pamoja. in ~ with pamoja na. vt,vi fanya shauri pamoja, tengeneza kwa mapatano. ~ed adj 1 -enye kufanywa kwa pamoja. 2 kali.~ed action n tendo lililofanywa kwa pamoja. ~ina n (mus) konsertina: aina ya ala ya muziki mithili ya kinanda cha mivukuto; kodiani.

concerto n koncheto (muziki wa ala

conclude

moja unaojitokeza zaidi katika okestra kuliko ala nyingine).

concession n 1 kukubali. 2 tahafifu. 3milki. concessive adj 1 -enye kuruhusu. 2 -a ridhaa; -tulivu; -sikivu. 3 (gram) -a kuridhia. ~aire n miliki; mwenye hati ya kumiliki.

conch n kombe. ~ology n elimukombe; elimu ya konokono na kombe za pwani.

concha n 1 (bio) sikio la nje; mvunguwa sikio. 2 (arch) paa la duara.

conchy n (sl) conscientious objector see conscientious.

concierge n (Fr.) bawabu, mlinda mlango.

conciliate vt 1 patanisha (hasa mtu

asiye rafiki), suluhisha. 2 tuliza (hasira ya fulani). 3 ungwa mkono. conciliation n usuluhishi, upatanisho court of conciliation baraza la usuluhishi. conciliatory adj.

concinnity n ufasaha (wa maneno);

umbuji.

concise adj (speech or style of writing) fupi, -enye habari nyingi katika maelezo machache; -dogo; -a muhtasari. ~ly adv. ~ness n.

conclave n 1 baraza la siri la makadinali linalomchagua papa; (fig) mkutano wa faragha.

conclude vt,vi 1 (make an end) hitimisha, maliza. 2 (agreement) fikia/panga mapatano. ~ a treaty kamilisha mkataba. ~ a bargain fikia mapatano; patana. 3 (come to an end) isha, fika mwisho; koma. 4 fikia uamuzi. conclusion n 1 hitimisho. 2 (judgement) uamuzi, hukumu; maoni (yanayotokana na kuzingatia suala zima) jump to conclusion amua jambo upesi bila kuzingatia suala zima. in conclusion mwishowe, hatimaye. try conclusions with shindana na. a foregone conclusion kitu cha wazi kabisa; kitu kilichokwishaamuliwa. conclusive adj -enye kuthibitisha, -enye kuondoa shaka, -a mwisho. conclusive evidence n ushahidi

unaothibitisha. conclusiveness n.

concoct vt 1 tengeneza kwa kuchanganya pamoja ~ a new kind of soup changanya namna mpya ya supu. 2 buni, tunga shauri/maneno ya uwongo/hadithi. ~ion n.

concomitant n kiambata adj ambatani. concomitance n hali ya kuambatana au kufuatana na (kitu kingine).

concord n 1 mapatano, maelewano, upatanishi, itifaki. 2 mpangilio wa kialfabeti (wa maneno muhimu ya kitabu k.m. biblia). 3 mkataba na. ~ance n upatano. ~ant adj (with) -enye kupatana. n mapatano (kati ya dini na dola kuhusu dhima ya dini katika jamii).

concourse n 1 mkusanyiko, kundi,

umati. 2 makutano: sehemu ya wazi ambapo barabara na njia hukutana. 3 (place) uwanja wa mikutano, riadha n.k.; ukumbi wa stesheni ya gari moshi.

concrete adj 1 -a kushikika, -a kuonekana (wala si -a kuwazika tu); thabiti ~ example mfano thabiti ~ noun nomino mguso. 2 -a saruji. ~ block n tofali la saruji. ~ mixer n kichanganya zege reinforced ~ zege imara. vt,vi tia saruji, paka saruji; ganda (kama saruji).

concubine n 1 hawara, kimada. 2 mke mdogo (katika ndoa za mke zaidi ya mmoja). concubinage n uhawara.

concupiscence n ashiki, nyege.

concur vi 1 tokea/tukia tendeka kwa wakati mmoja. 2 (agree in opinion) afiki, kubali. ~rence n. ~rent adj -enye kulingana/kupatana; -enye kutendeka/kuwapo au kufuatana pamoja. ~rently adv.

concuss vt (often passive) jeruhiwa

ubongo (kutokana na kupigwa/ kishindo/mtikisiko mkali). ~ion n 1 jeraha la bongo linalotokana na kupigwa/kugongwa). 2 (shock) mshtuko, mtikiso (wa nguvu).

condemn vt 1 laumu, shutumu; laani we ~ed his bad behaviour tulilaani tabia yake mbaya. 2 (to convict)

hukumu, tia hatiani. 3 weka, tuma, agiza fulani kuishi katika hali ya taabu au maumivu. ~ation n shutuma; laana; lawama. 4 (reject) kataza, tupa ~ed house nyumba iliyopigwa marufuku kukaliwa na mtu (kwa sababu ya ubovu). 5 (arch) twalia, taifisha k.v. mali ya magendo.

condense vt,vi 1 fanya zito; fanya umande/wingu; punguka na kuwa zito zaidi. 2 (of steam) tonesha: geuza mvuke uwe maji. 3 (shorten) fupisha, fanya muhtasari a ~ed account of an event muhtasari wa habari. n 1 kijazi, kondensa: chombo cha kukusanyia au kugeuzia nguvu ya umeme. 2 kitoneshi: chombo cha kugeuza hewa kuwa majimaji. condensation n 1 mtonesho. 2 ufupisho.

condescend vi ~ to somebody/ something; ~ to do something 1 (in a good sense) fanya kitu, kubali kazi/cheo kilicho chini ya hadhi yako. 2 (in a bad sense) jishusha hadhi. 3 tenda wema (kwa lengo la kusimanga/kujionesha bora). condescension n.

condign adj (of punishment) kali,

iliyostahili.

condiment n kiungo, kikolezo cha kutia ladha katika chakula k.m. chumvi/pilipili.

condition n 1 sharti on no ~ bila ya sharti/mapatano on ~ that ikiwa/endapo kwamba contrary to the ~ we agreed upon kwa kinyume cha mapatano yetu. 2 (state) hali, tabia; (pl) ~s hali ya mambo muhimu kwa uhai. under existing ~s katika hali ya mambo ilivyo. 3 (health) afya, siha, rai, zima out of ~ katika hali mbaya, -lioharibika the ~ of my health hali ya afya yangu be in no ~ to do something -toweza kufanya (jambo). 4 nafasi (ya kitabaka) katika jamii people of all ~s attended watu wa matabaka yote walihudhuria. vt shurutisha,

condole

lazimisha be ~ed tawaliwa my expenditure is ~ed by my income matumizi yangu yanatawaliwa na mapato yangu. ~ed adj 1 -enye masharti ~ed reflex tendo la kujiendea ~ed reaction mlipizo zoevu. 2 -enye hali fulani nzuri/mbaya n.k.. ~ed adj. ~al adj 1 sharti, -enye masharti, kutegemeana na. ~al sale n uuzaji kwa masharti. 2 (gram) ~al sentence n sentensi sharti.

condole vi (grieve with) hani, toa

(salamu za) rambirambi, -pa mkono wa pole. ~nce n mbirambi, rambirambi, liwazo. letter of ~nce barua ya rambirambi.

condom n kondomu, mpira wa kiume. condominium n 1 miliki bia, utawala bia (wa nchi mbili au zaidi); mamlaka bia. 2 (US) nyumba ya majumui imilikiwayo na wakazi.

condone vt 1 samehe, jifanya kutoona, puuza. 2 (of an act) toa kafara, fidia. condonation n.

condor n aina ya tai mkubwa (wa Marekani ya Kusini).

conduce vi faa, saidia, elekea kuleta, changia. conducive adj.

conduct1 n 1 mwenendo, tabia (nzuri

au mbaya), maadili mema. code of~ n kanuni za maadili mema. 2 usimamizi, uongozi, uendeshaji, ufuataji maadili mema. ~ of business etc n utaratibu wa shughuli n.k. ~ -money n gharama za shahidi.

conduct2 vt 1 (lead) ongoza, peleka, chukua ~ed tour ziara iliyoongozwa. 2 (manage) endesha. 3 (phys) pitisha/ruhusu iron ~s heat chuma hupitisha joto. 4 ~ oneself (behave) tenda. 5 (mus) ongoza, imbisha. 6 fanya kazi ya kondakta. ~ oneself towards somebody jiweka kwa jambo la mtu fulani. ~ion n upitishaji (k.m. umeme katika waya). ~ion of heat upitishaji wa joto. ~ion system n mfumo wa upitishaji joto, umeme, maji. ~ive adj -enye

uwezo wa kupitisha. ~ivity n.

conductor n 1 (guide) mwongozaji,

kiongozi. 2 (US) msimamizi; mwangalizi wa abiria, kondakta anayekusanya nauli. 3 (phys) kipitishi (cha joto au umeme) ~ rail reli inayopitisha umeme. conductress n kondakta wa kike.

conduit mfereji, bomba (la maji);

bomba la kupitishia waya/nyaya za umeme.

cone n 1 pia. 2 (bio) sonobari. 3 koni. 4 (of ice cream) koni. ~-pulley n. kapi ya pia.

coney n see cony.

confabulate vi (also inform confab)

zungumza, ongea. confabulation n mazungumzo (ya kirafiki, faragha).

confection n 1 tamutamu. 2 vazi (agh. kwa wanawake). 3 mchanganyo; (of clothes) tayari kwa kuuza. ~er n mtengezaji/mwuzaji vitamutamu. ~ery n vitamutamu, kiwanda/duka la vitamutamu.

confederacy n 1 shirikisho; mwuungano (wa majimbo, nchi, vyama au watu). 2 njama. be in ~ kula njama (na). confederate adj -lioungana pamoja kwa mapatano au mkataba. n 1 mwenzi. 2 mshirika, msaidizi katika uovu. vt,vi 1 ungana kwa mapatano. 2 fanya njama. confederation n.

confer vt,vi 1 ~ something on/upon tunukia, tunza (shahada; heshima; n.k.). ~ a degree tunukia shahada. ~ (with somebody) (on/about something) shauriana, jadiliana na ~ment n.

conference n mkutano.

confess vt,vi 1 kiri, kubali kosa he ~ed that he stole the money alikiri kuwa aliiba zile fedha. 2 tubu, ungama. ~edly adv. ~ion n 1 kukiri, kukubali. 2 ungamo. 3 (creed) tangazo la imani, ushuhuda. 4 (rel) maungamo adj -a maungamo, -a imani. ~ional adj, n (rel) kizimba cha maungamo. ~or n (rel) 1 mwungamishi (padri mwenye

mamlaka ya kusikiliza maungamo). 2 muungamaji. 3 shahidi (mtu anayejitolea kuteswa au kufa kwa ajili ya dini yake).

confetti n (pl) chengechenge za rangi mbalimbali (ambazo hutupiwa maarusi n.k.).

confide vt,vi 1 ~ to ambia siri. 2

kabidhi they ~d their children to the neighbour walikabidhi watoto wao wa jirani. 3 ~ (in) -wa na imani. confiding adj -a kweli; -a kuaminika, -a kuamini wengine. confidingly adv. confidant n msiri (agh. wa mambo ya mapenzi). ~nce n 1 matumaini, imani put one's ~nce in somebody wa na imani naye. have ~nce in tegemea, tumainia. 2 maneno ya siri, siri iliyotolewa kwa mtu mwingine give a ~nce to somebody dokolea siri. take into ~nce mwamini. ~nce trick/ ~ence game n kuiba kwa ghiliba kima- chomacho, ulaghai, utapeli. 3 hakika I had every ~nce that we should win nilikuwa na hakika kwamba tutashinda. ~ nt adj 1 -tumainifu, -enye imani. 2 -enye hakika, -enye kujiamini. ~ntly adv. ~ntial adj 1 (of information) -a siri. 2 (of a person) -enye kuamini mno. ~ntiality n. ~ntially adv.

configuration n umbo, sura; namna ya

kupanga.

confine vt 1 wekea mipaka ~ your

remarks to the subject usitoke/ usizungumze nje ya mada. 2 fungia, zuia she is ~d to her room amezuiliwa chumbani mwake. 3 be ~d (passive only) (old use) jifungua, zaa; -wa kitandani tayari kwa kujifungua. ~d adj. ~ment n 1 kifungo. 2 uzazi, kuzaa, kujifungua. ~s n 1 mipaka beyond the ~s of human knowledge nje ya mipaka ya ujuzi wa binadamu.

confirm vt 1 (strengthen) thibitisha,

imarisha (nguvu, maoni, haki n.k.); tia nguvu, tegemeza. 2 (ratify) idhinisha, sahihisha, yakinisha. 3 (rel) tolea kipaimara, tia (bandika)

Confucian

mikono baada ya ubatizo. ~ed adj imara; kabisa, -a siku nyingi. ~ation n 1 uthibitisho; shahada, ushahidi, hakika. 2 (rel) kipaimara.

confiscate vt (as punishment) nyang'anya, chukua ngawira; taifisha. confiscation n.

conflagration n moto mkubwa, (hasa unaoteketeza majengo na misitu).

conflict n 1 mapigano; vita; mapambano; ugomvi. 2 (of opinions, desires etc) mgongano. ~ of law n mgongano wa sheria. be in ~ with pingana na, -tokubaliana na. a wordy ~ ushindani wa maneno, ubishi mkali, mzozano, mgogoro. vi (~ with) pingana au -tokubaliana na. ~ing adj.

confluence/conflux n ndagano: mahali mito miwili inapoungana. confluent adj.

conform vt,vi 1 ~ (to) fuata, kubali (sheria, kanuni, viwango vilivyokubaliwa), tii, patana na. ~ oneself kubali kupatana na. 2 ~ (to) fanya sawa na. ~able adj tiifu, kubalifu, -a kukubaliana na. ~ity (also ~ance) n usawa, ulinganifu, ukubalifu, tendo au tabia inayokubaliana na. in ~ity with kwa kupatana na, kwa kufuata. ~ist n mfuata kanuni/desturi n.k.

confound vt 1 (perplex) shangaza, fadhaisha, staajabisha, tunduwaza. 2 (arch) ~ (with) changanya (mawazo n.k.). 3 angamiza, shinda (mpango, tumaini). 4 aibisha. ~ed adj 1 -lostaajabu, -lofadhaika. 2 -a laana. ~edly adv. ~ly adv sana.

confraternity n kundi la kidini linalotenda jamala na kutoa sadaka

kwa jamii.

confrére n mwenzi (wa kazi, wa chama).

confront vt 1 (oppose) ~ somebody with kabili. 2 (set opposite , bring before) kabiliana ana kwa ana. 3 -wa mkabala na. ~ation n.

Confucian adj n -enye kumfuata Konfyushasi (mwana falsafa na

mwalimu wa maadili wa Kichina). ~ism n.

confuse vt 1 ~ (with) changanya, tinga, tanza. 2 (perplex) hangaisha, tia wasiwasi, tatiza, tatanisha. 3 (fail to distinguish) kanganya don't ~ me with Joseph usifikiri mimi ni Joseph. ~dly adv. confusion n 1 mchafuko, kakara, shaghalabaghala. 2 rabsha, ghasia. 3 kiwewe.

confute vt bainisha/dhihirisha kosa,

onyesha, bainisha ukweli. confutation n.

congeal vt,vi ganda, gandisha, -wa ngumu his blood ~ed (fig) mwili ulimsisimka (kwa hofu), kacha.

congenial adj 1 (of persons) -enye hulka moja. 2 (of things, occupation etc.) -inayofanana/kukubaliana na matakwa/hulka ya mtu a ~ job kazi inayochukuana na hulka ya mtu. ~ity n. ~ly adv.

congenital adj (esp disease or defect) -a kuzaliwa na, kizaliwa a ~ disease ugonjwa wa kuzaliwa nao. ~ idiot n mpumbavu; (fig) mpumbavu kabisa.

conger (also ~ eel) n mkunga wa baharini.

congest vt 1 songa, jaza sana, banana.

2 (med) jaa/jaza uoevu his lungs are ~ed mapafu yake yamejaa. vi 1 -wa na damu nyingi mno. 2 fanyiza msongano. ~ed adj 1 (over crowded) -a kusongana mno, -a kujaa sana the streets were ~ed with people kulikuwa na msongamano wa watu barabarani. 2 (of parts of the body eg. brain) -enye mavilio ya damu, -enye damu nyingi kuliko kiasi his lungs were ~ed mapafu yake yalikuwa na damu nyingi. ~ion n.

conglomerate 1 adj, n -liyoundwa

katika bonge; bonge. 2 mkusanyiko wa vitu. 3 (comm) shirikisho; makampuni. vt,vi kusanya/unda katika bonge/kitu kimoja. conglomeration n.

congratulate vt 1 pongeza, -pa mkono wa tahania, -pa hongera, hongeza. 2 ~ (oneself) jipongeza; (after

conjunct

accident/danger) shukuru. congratulatory adj. congratulation n (often pl) hongera, pongezi, mkono wa tahania.

congregate vt,vi kusanya; kusanyika, kutana, kutanika people quickly ~d around the speaker watu walikusanyika haraka na kumzunguka msemaji. congregation n 1 mkusanyiko wa watu; mkutano, usheha. 2 (rel) mkusanyiko wa waumini, usharika. 3 (of a University) mahafali. congregational adj.

congress n 1 mkutano wa watu (wa shughuli maalum). 2 (US) Bunge la Marekani; (India) chama cha siasa cha Kongresi. ~ional adj. ~man/woman n. mbunge.

congruence/congruency n mlingano, ulinganifu. congruent n, adj. congruous adj 1 -a kupatana, -a kulingana. 2 (geom) -a mlingano, -liolingana. congruent lines n mistari iliyolingana. congruity n.

conic(al); coniform adj kama pia,

-enye umbo la pia.

conifer n aina ya msonobari, mpia. ~ous adj.

conjecture vt bahatisha, kisia, dhani, bunia. n kisio, bahatisho. conjectural adj.

conjoin vt unga, unganisha. vi ungana.

~t adj. ~tly adv.

conjugal adj -a ndoa; -a mume na

mkewe, -a unyumba. ~ rights n haki za unyumba/ndoa.

conjugate vt (gram) nyambua kitenzi. vi (biol) ungana. conjugation n.

conjunct adj, n -a kuunga, -liounganika; muungano. ~ly adv. ~ion n 1 mwungano. in ~ion with pamoja na, kwa kuungana na. 2 (gram) kiungo (k.m. na, ya, wa). 3 mwingiliano, mchanganyiko. ~ion of circumstances mwingiliano wa mambo. ~ive adj 1 -a kuunganisha, -a kiunganishi. n kiunganisho. ~ively adv. ~ure n mwungano wa matukio that ~ure of flood and

conjure

drought resulted in famine mwungano wa mafuriko na ukame ulisababisha njaa.

conjure vt, vi 1 fanya mizungu, kiinimacho, mazingaombwe. 2 omba, sihi sana. 3 ~ up (of spirits) ita; (fig) buni, vuta picha, kumbusha; (of meal) tengeneza. a name to ~ with mtu muhimu. ~r/conjuror n mfanya kiinimacho, mazingaombwe, mizungu. conjuration n 1 maneno ya kunuizia uchawi; matabano, matagonya.

conk1 n (GB) (sl) pua.

conk2 vi ~ out 1 (colloq) (of machine) haribika, shindwa (kufanya kazi ipasavyo) the engine ~ed out injini iliharibika/imenoki.

conman n tapeli.

connect vt, vi 1 unganisha; unganika the two towns are ~ ed by a railway miji miwili hii imeunganishwa na reli. 2 (associate) husu; husisha the subjects are ~ed mambo haya yanahusiana, yanafungamana. ~ with husiana na. well ~ed husiana na watu maarufu. ~er n. ~edly adv. ~ion. connexion n 1 uhusiano/mwunganisho; (coherence) uwiano these affairs have no ~ion with each other mambo haya hayawiani, hayahusiani. 2 kuunganisha kiungo. 3 (relation ) ndugu; jamaa, ahali. 4 kuunganisha safari kwa kubadili vyombo vya usafiri. 5 (context) muktadha, mintaarafu ya. in ~ion with this kwa mintarafu ya. 6 (rel) madhehebu. 7 (in business) mbinu, washiriki katika biashara. 8 (collection) wateja. ~ive adj 1 -a kuunganishia. 2 (gram) kiunganisho. 3 kiangama cha ushirikisho.

conning-tower n (on warship) mnara wa rubani wa manowari.

connive vi ~ at something 1 fumbia macho, achilia kwa makusudi (kosa lifanyike), jitia mwapuza. 2 kula njama; (abet) shiriki katika tendo kwa siri ~ at a crime kula njama.

connivance n. ~r n.

connoisseur n mwonjaji, mjuzi, mfahamivu, mmaizi.

connote vt maanisha kwa maana nyingine, ashiria connotative meaning n maana matilaba connotation n kidokezo.

connubial adj -a mke na mume, -a unyumba.

conquer vt 1 shinda (adui, tabia au mazoea mabaya). 2 kamata, twaa (kwa nguvu hasa wakati wa vita). ~or n mshindi. conquest n 1 ushindi; ushinde. 2 (spoils) mateka, nyara, nchi zilizotekwa. 3 kipenzi make a conquest (of) vutia mtu (kwa mapenzi), pata, pendwa.

consanguinity n udugu wa nasaba. conscience n dhamiri. good bad ~ n dhamiri njema/mbaya; moyo wenye raha/wasiwasi kwa ajili ya matendo. have a clear ~ -wa na moyo safi. guilty ~ n shitakiwa na dhamiri. for ~ 'sake tosheleza dhamiri I would not have the ~ to do that nisingalikuwa na moyo wa kufanya hivyo. in all ~/upon my ~ kwa dhamiri yangu/ kwa mawazo yangu. have no ~ -toweza kutofautisha mema na mabaya. ~ money n malipo ya ria. ~-stricken adj jawa na majuto. conscientious adj -a kufanya kwa makini, -angalifu sana. conscientious objector n mtu akataaye kufanya kitu (k.m. huduma ya jeshi) kwa sababu hakipatani na maadili yake. conscientiousness n.

conscious adj 1 -a kuona, -a kufahamu, -a kusikia he was ~ of a smell alisikia harufu become ~ of something tambua jambo the man who was hurt was still ~ yule mtu aliyeumia alikuwa bado na fahamu zake. 2 (of others, feelings) -a kujua, -a kufahamu moyoni (nafsini). 3 -a kuweza kufikiri na kuamua. 4 -a makusudi. ~ly adv. ~ness n 1 fahamu, utambuzi. 2 (perception) akili. he lost ~ness alizimia, alizirai. he regained ~ness alipata

conscript/conscribe

fahamu tena.

conscript/conscribe n (US conscriptee) mwanajeshi kwa mujibu wa sheria vt andikisha jeshini kwa mujibu wa sheria. ~ion n.

consecrate vt ~ (to) 1 weka wakfu. 2 toa (tenga) kwa ajili ya dini, Mungu au kusudi fulani. 3 tukuza, fanya takatifu. 4 (inaugurate) zindua ~d adj -liofanywa takatifu, wakfu. consecration n 1 ufanyaji wakfu, kuweka wakfu. 2 consecration in Mass mageuzo. consecrator n mweka wakfu. consecratory adj. -a kutunzwa, -enye kuwekwa wakfu.

consecutive adj 1 mfulizo, -a kufuatana/kufuata, moja baada ya moja three ~ days siku tatu mfulizo. 2 (gram) (of a sentence) -enye matokeo yaliyofuatana. ~ly adv. consecution n mfululizo, mfuatano wa matukio.

consensus n muafaka, makubaliano

(juu ya shauri). consensual adj 1 -enye muafaka, -a kuridhiana, -a kukubaliana, pamoja. 2 (phys) -a

kisilika (kwa mwendo).

consent vi ~ (to) ridhia, kubali,

wafiki, toa idhini. n ridhaa, idhini, ruhusa, radhi. age of ~ umri wa utu uzima. with one ~ kwa kauli moja.

consequence n 1 matokeo (ya jambo). in ~ (of) kwa sababu hiyo. in ~ of something kwa ajili ya jambo fulani. bear the ~s kubali matokeo. 2 umuhimu, umaarufu, cheo. it is of no ~ sio muhimu. a person of ~ mtu maarufu. consequent n tokeo la jambo, mfululizo; (gram) kishazi kifuasi adj 1 consequent on/upon -a kufuata, -a kufuatana na. (law) consequent damage n hasara inayofuatia. 2 (maths) consequent number namba fuasi katika uwiano. consequential adj -a kufuata. consequential loss n hasara inayoandamana na. 2 (pompous) -enye majivuno, -enye makuu. consequently adv kwa hiyo, hivyo.

conservatoire n (esp. in Europe) chuo

consider

cha muziki.

conservatory n (US) 1 kibanda cha kukuzia miche. 2 (mus) chuo cha muziki.

conserve vt linda, tunza, hifadhi, weka vizuri. n (usu pl) ~s n matunda ya kopo; jamu. conservation n 1 hifadhi; (of game, forest) hifadhi ya wanyama/misitu; (mech) conservation/of momentum hifadhi ya nguvu mwendo. conservancy n 1 tume ya hifadhi ya mali asili. 2 hifadhi rasmi ya mali asili. conservatism n ushikiliaji (wa) ukale/mfumo uliopo; kutopenda mabadiliko. conservator n 1 mhifadhi. 2 mwangalizi (wa makumbusho n.k.). conservative adj 1 -enye kushikilia ukale; -siyependa kubadili mambo The Conservative Party Chama cha Conservative. 2 -a kulinda, -a kutunza. 3 -enye hadhari, -a kiasi. n mtu asiyependa mabadiliko.

consider vt 1 (deliberate on) fikiria, dhukuru, angalia. one's ~ed opinion wazo la mtu baada ya kufikiria sana. 2 (take into account) zingatia, kumbuka, pima. all things ~ed baada ya kufikiria yote. 3 wazia, dhania, fikiria, ona. ~able adj kubwa, -ingi. ~ably adv mno, sana. ~ate adj (important) -a kustahili kufikiriwa; -enye kufikiria wengine; -enye huruma; -enye busara it was ~ate of him alifanya busara. ~ately adv. ~ateness n. ~ation n 1 (deliberation) fikira, shari, nadhari. take into ~ation angalia. under ~ation inayofikiriwa. give something careful ~ ation fikiria kwa makini. leave out of ~ation sahau, shindwa kufikiria. 2 (kindness) huruma, wema. 3 (motive, reason) sababu, kisa, jambo, hoja these are the ~ations which influenced him in making his plans haya ndiyo mambo ambayo yalimwathiri sana katika kufanya mipango yake. on no

consign

~ation (isiwe) kwa vyovyote vile, hapana kabisa. 4 (rare use) umuhimu. 5 (compensation, reward) tuzo, malipo. ~ing prep -kwa kuzingatia, -kwa kulinganisha he scored highly ~ing his long illness amefaulu sana ukilinganisha na kipindi kirefu alichokuwa mgonjwa.

consign vt (to) 1 peleka, pelekea, safirisha (mizigo, bidhaa n.k.). 2 toa, tokea, pa, aminisha. ~ee n wakili. ~er, ~or mwakilishaji. ~ment n mali. ~ment note n hati ya mali.

consist vi 1 (of) -wa na. 2 (in) tegemea. ~ence/ ~ency n 1 kuwa na msimamo, hali ya kuwa na fikira (desturi, tabia n.k.) zile zile daima. 2 uthabiti. 3 uzito, ugumu mix flour and milk to the right ~ency koroga pamoja unga na maziwa ili kupata uzito (ugumu) ufaao. ~ent adj 1 (of person, his behaviour, principles etc) -enye msimamo, thabiti, -aminifu, -a kulingana, sawa. 2 (with) kwa kupatana/kukubaliana, -a kushikilia jambo; -nyofu. ~ly adv.

consistory n (rel- R.C.) (also C~ Court) Baraza linaloundwa na Papa na Makadinali (kwa shughuli za kanisa). consistorial adj.

console1 vt fariji, tuliza, liwaza, poza moyo ~ somebody for a loss tuliza mtu kwa hasara aliyoipata. consolable adj -enye kuweza kufarijika. consolation n faraja, maliwazo, kitulizo; (of person) mfariji. (sports) consolation prize n zawadi ya kufariji/ kufuta jasho. consolatory adj -enye faraja, -a kufariji.

console2 n 1 kiweko. ~ mirror n kioo

chenye kiweko. ~ table n meza yenye kiweko. 2 chumba cha vifaa vya elektroniki. 3 redio au TV ya kabati.

consolidate vt,vi 1 (make firm) imarisha, (ji)zatiti. 2 (unite) unganisha, fanya moja. ~d fund n mfuko wa jumla. consolidation n.

consomme n supu nyepesi ya nyama.

consonance n 1 upatanifu. 2 ulinganifu be in ~ with lingana na; (mus) ulinganifu wa sauti. 3 konsonanti: upacha wa konsonanti za mwisho za maneno tofauti (k.m. t katika maneno fit, hot, bet ya Kiingereza). consonant adj -a kupatana, -a kulingana, sawa. consonant with -enye kuchukuana na. consonant to muwafaka, kubalifu, kabuli. consonant n konsonanti consonantal adj.

consort1 n 1 mume au mke (hasa) wa mtawala the queen ~ mke wa mfalme the prince ~ mume wa malkia. 2 meli inayofuatana na nyingine (hasa kwa ajili ya ulinzi wakati wa vita).

consort2 vi ~ with 1 andamana na, fuatana na. 2 patana, afikiana. ~ium n ubia (wa mashirika, mabenki n.k.).

conspectus n muhtasari; maelezo ya jumla, vidokezo.

conspicuous adj 1 -enye kuonekana

waziwazi, -enye kuvutia. be ~ onekana wazi make oneself ~ jionyesha. ~ consumption n matumizi ya ufahari/kujichana. ~ly adv. ness n.

conspire vt,vi 1 -la njama. 2 (of events) unganisha, jumuisha, ungana events ~d to bring about his failure kushindwa kwake kumetokana na mambo mengi. conspirator n mla njama, haini. conspiracy n njama, kigwena. conspiratorial adj.

constable n (GB) 1 konstebo; polisi (wa daraja la chini). special ~ n raia afanyaye kazi ya polisi wakati maalumu. 2 (hist) ofisa mkuu wa kifalme. constabulary n jeshi la polisi.

constant adj 1 -a siku zote, -a daima, -a kawaida. 2 (firm) thabiti, imara n (maths) kisobadilika. ~ rate n kima kisichobadilika. ~ly adv. constancy n 1 uthabiti. 2 uaminifu.

constellation n kilimia; (fig) kundi.

consternation n fadhaa, hofu kuu na

constipate

mshangao.

constipate vt funga choo. ~d adj. constipation n kufunga choo, hali ya kufunga choo (ya kutopata choo barabara); uyabisi wa tumbo (choo).

constituent adj 1 -a sehemu ya kitu kizima. 2 (of assembly) -enye haki na uwezo wa kufanya au kubadilisha katiba. n 1 mpiga kura. 2 sehemu ya kitu kizima. 3 (gram) ~ part n kiamba jengo. constituency n jimbo la uchaguzi.

constitute vt 1 (establish) anzisha (shirika), toa madaraka kwa (kamati n.k.). 2 (form, compose) fanya, fanyiza; -wa na; -wa na. 3 (appoint) teua, weka madarakani. constitution n 1 katiba ya nchi, chama n.k. 2 (of a person) gimba, tambo, zihi. 3 (of a thing) umbile; (act/ manner) the constitution of the solar mjengo wa mfumo wa jua. constitutional adj 1 -a kikatiba constitutional law sheria ya katiba. 2 (lawful) halali, -a kutii sheria. 3 -a asili, -a umbile, -a afya n (dated colloq) matembezi mafupi kwa ajili ya afya take a constitutional walk tembea, nyosha miguu, (kwa ajili ya afya). constitutionalism n imani kwamba serikali sharti ifuate misingi ya katiba. ist n. ~ly adv kwa mujibu wa katiba. constitutionalize vt fanya -a katiba. constitutive adj 1 jenzi. 2 (original) -a asili. 3 -a katiba -a sehemu ya kitu.

constrain vt 1 lazimisha, shurutisha. 2 bidi. 3 (limit) zuia. ~ed adj -lobanwa. ~t n kikwazo, kizuizi, kigingi. ~edly adv.

constrict vt 1 bana, songa, minya, binya. 2 zuia ukuaji, dumaza; (fig) finya. ~ed adj a ~ed outlook mtazamo finyu. ~ion n. ~or n 1 (surgical) kibano. 2 (anat) msuli bana. 3 chatu.

construct vt 1 jenga. 2 fanya, fanyiza; unda. 3 buni. ~ion n 1 ujenzi, uundaji. 2 jengo, nyumba (chochote kilichojengwa au kuundwa). 3 mjengo. 4 (gram) muundo wa

consume

maneno au sentensi. 5 tafsiri, maana his statement does not bear such a ~ion maelezo yake hayana maana hiyo. ~ive adj -a kutoa maoni yanayosaidia; jenzi.

construe vt,vi 1 fasiri; tafsiri; eleza maana, chambua; (infer) fahamu maana yake he was mis ~d alieleweka vibaya. 2 changanua; chambua; unda, unganisha kisarufi ~ a sentence chambua sentensi. 3 (of sentence) wezekana kuchambuliwa au kutafsiriwa.

consubstantiation n (rel) imani kuwa damu na mwili wa Yesu Kristo upo pamoja na divai na mkate (katika Ekaristi Takatifu). consubstantial adj -enye asili moja.

consul n balozi mdogo. ~ar adj.~ship n Ubalozi Mdogo. ~ate n 1 ofisi ya balozi mdogo. 2 Ubalozi Mdogo.

consult vt,vi 1 taka shauri. 2 tafuta maoni (katika kitabu n.k.). 3 shauri, elekeza, fanya shauri. ~ in toa shauri. ~ with shauriana. ~ant n mshauri, mwelekezi; bingwa. ~ation n 1 ushauri, uelekezi, mashauriano. 2 mkutano wa kushauriana. 3 kitendo cha kushauriana. ~ative adj.

consume vt,vi 1 -la, -nywa. 2 (of fire) teketeza; tumia; maliza. 3 haribu, fuja ~ away haribika, oza. consumable adj. consuming adj. ~r n mlaji, mnunuzi, mtumiaji. ~r goods n bidhaa zitumiwazo (chakula, nguo, gari n.k.) ~r cooperative shop duka la ushirika la walaji ~r wants mahitaji ya wanunuzi ~r sales resistance uzito wa kununua bidhaa (wa wateja). consumption n 1 ulaji. 2 utumiaji; ufujaji. 3 (med) kifua kikuu. consumptive adj 1 -enye kifua. 2 -haribifu; -a kutumia. n mgonjwa wa kifua kikuu. consumptiveness n. consummate vt 1 kamilisha, timiliza, maliza, isha. 2 kamilisha/timiliza ndoa kwa ngono. ~d marriage n ndoa

iliyokamilishwa, /ndoa kamilifu. ~ly adv,adj 1 -kamili, -timilifu, bora; stadi. consummation n 1 kilele, ukamilisho; tendo la kumaliza kutimiza/kukamilisha. 2 consummation of marriage mfumo wa kukamilisha ndoa kwa ngono; kukamilishwa kwa ndoa.

contact n 1 mgusano, mawasiliano, mpambano come into ~ kutana, wasiliana; gongana, pambana. be in ~ with gusana be in ~ with somebody wasiliana na mtu, gusana na mtu, kabiliana na mtu. ~ lens n lenzi (ya plastiki) inayoambatanishwa na mboni (kuonea vizuri). 2 (med) mtu aliyekutana na/kuwa na mgonjwa mwenye maradhi ya kuambukiza ~ infection uambukizaji kwa kugusana ~ poison sumu mgusano. 3 (elect) kiungo cha umeme; (device) kipitishio make ~ unganisha waya za umeme (ili nguvu ya umeme iweze kupita) break ~ kata umeme. 4 (pl) ~s n mwunganisho; (of people) uhusiano miongoni mwa watu ~s man mpatanishi (wa kesi ya kampuni na serikali); mtu wa kati, msuluhishi. ~s n wahusika, washirika. business ~s n watu unaohusiana nao kibiashara. vt, vi kutana, gusana, wasiliana, ungana.

contagious adj (of people or disease) -a kuambukiza. ~ disease n ugonjwa wa kuambukiza; (fig) -a kuenea upesi kwa kuigana; -a kuathiri. contagium n kiambukizi (k.m. virusi). contagion n 1 uambukizaji (kwa kugusana, kukaribiana). 2 ugonjwa wa kuambukiza; (fig) uenezaji wa mawazo potofu/mashauri maovu/ umbeya/uvumi.

contain vt, vi 1 -wa na (vitu) ndani this cup ~s water kikombe hiki kina maji ndani yake. 2 -wa kadiri ya, -wa sawa na a gallon ~s eight pints galoni ni sawa na painti nane. 3 chukua/weka how much does this bottle ~? chupa hii huchukua kadiri gani? 4 dhibiti, zuia (uharibifu)

content

~oneself jizuia. 5 (geom) -wa mpaka wa. 6 (maths) ~ a number gawanyika. ~er n 1 chombo (agh. sanduku, chupa n.k.) cha kutilia vitu. 2 kontena: kasha kubwa la chuma la kusafirishia mizigo.

contaminate vt chafua, tia uchafu,

najisi (k.m. kwa kugusa). contamination n.

contemn vt (liter) dharau, tweza, hizi, beza.

contemplate vt,vi 1 tazama sana (kwa macho au kwa kufikiri) it is ~d inafikiriwa. 2 tafakari; zingatia. 3 (intend) kusudia, azimu, nuia. 4 (look forward) tazamia. 5 taamali, dhukuru. contemplation n. comtemplative adj 1 -enye kufikiri sana; -a kutafakari. 2 (rel) -a kisufii n sufii; usufii.

contemporary adj 1 -a wakati ule ule. 2 -a kisasa, -a siku hizi n 1 mtu wa hirimu au rika lilelile (la mwingine). 3 (persons, newspaper etc) wakati ule ule we were contemporaries at school tulisoma wakati uleule mmoja chuoni (pl) our contemporaries wenzetu wa kisasa/siku hizi. contemporaneous adj ~ (with) -a kutokea/kuanza/ kuishi wakati mmoja.

contempt n 1 (scorn ) dharau, twezo, bezo treat with ~ dharau, beua, tweza, hakiri. beneath ~ adj hastahili hata kudharauliwa; hata tusi ghali. 2 aibu. 3 ~ of court n kudharau mahakama. ~ible adj -a kudharauliwa, duni, hafifu. ~uous adj.

contend vt,vi 1 pambana, shindana,

pingana, bishana. ~ for/with shindania. 2 shikilia kauli, dai. ~er n. ~ing adj.

content1 n 1 kadiri the gold ~ of the ring kadiri ya dhahabu ndani ya pete. 2 (pl) yaliyomo, fahirisi table of ~s fahirisi. 3 (subject matter) maudhui. 4 ujazo, uwezo (wa kuchukua).

content2 adj 1 ~ (with) ridhi, ridhika.

contention

2 (to) -wa radhi/ tayari (kufanya n.k.) I am ~ to work in Mtwara niko tayari/nafurahi kufanyia kazi Mtwara n radhi; ridhaa, kinaa to one's heart's ~ kwa kutoshelezeka, ridhika. vt,vi ridhisha. be ~ed ridhika, -wa radhi. be self ~ed kinai. ~ed adj. ~edly adv. ~ment n.

contention n 1 ushindani, ugomvi,

ukinzani bone of ~ chanzo cha ugomvi. 2 hoja. contentious adj -gomvi; -shindani, -bishani, -a kuleta ubishi. contentiousness n.

conterminous adj 1 (see coterminous) -a jirani; -liopakana. 2 -lioafiki.

contest vt,vi 1 jadili, toa hoja, bisha. 2

~ a seat in Parliament gombea kiti cha Bunge (strive for) shindana, shindania, gombea; pinga ~ an action pinga madai. n 1 shindano, pambano. ~able adj -a kujadilika. ~ant n mgombea, mshindani. ~ed adj -a kugombewa.

context n 1 muktadha. 2 mazingira ambamo jambo hutokea. ~ual adj. ~ure n 1 taratibu, mtindo. 2 ufumaji.

contiguous adj ~(to) -a kugusana, -a kupakana, -a karibu, -a jirani; (geom) -liotangamana. contiguity n ujirani; hali ya kuwa karibu.

continent1 adj -a kujizuia, -enye

kutawala tamaa (hasa ashiki). continence n kujizuia/kutawala tamaa (hasa ashiki).

continent2 n bara, kontinenti. ~al adj -a bara, -a kontinenti. n 1 mkazi wa bara la Ulaya. ~al breakfast kifungua kinywa cha chai/kahawa na mkate tu.

contingency n 1 tukio la nasibu/bila kutarajiwa in such a ~ we cannot agree mambo yakitokea hivi hatuwezi kukubali. 2 (pl) contingencies matumizi yanayotokea/ya dharura; matumizi mengine be prepared for all contingencies -wa tayari kwa lolote litakalotokea. contingent adj 1 -sio hakika, -a bahati, -a kuwezekana (lakini hakuna hakika kwamba

itatokea). 2 contingent upon yamkini; -a kutegemea jambo jingine. n (mil) kikosi cha ziada/saidizi.

continuant n (gram) kifulizwa: sauti ambazo hutamkwa kwa mwendelezo.

continue vt,vi 1 endeleza, fuliza, zidi,

sedeka ~ the debate endeleza mjadala. 2 anza upya/baada ya/tena. 3 dumu, kaa, shinda ~ in (at) a place (office etc.) endelea kukaa. ~d adj. continual adj -a moja kwa moja, -a mfulizo; -a siku zote, -a kila siku, -a daima, -a kuendelea n continually adv. continuance n 1 kudumu, kuendelea of long continuance -a kudumu, -a muda mrefu. 2 ufulizaji, wakati ambapo jambo linaendelea. 3 (leg) kuahirisha continuance of drought kuendelea kwa ukame. continuation n 1 mfulizo. 2 mwandamano, mwendelezo. continuity n 1 mwendelezo, mfululizo, mfulizo. 2 maneno ya kuendelea/kuunganisha sehemu za kipindi. 3 uendelezaji; hali ya kuendeleza. continuous adj -a moja kwa moja, -a siku zote; isosita continuous furnace tanuu isiyozimika (math) continuous function husisho endelevu; continuous numbers nambari endelevu. continuously adv. continuum n mwendeleo (phys. math) endelezo.

contort vt 1 umbua, potoa, nyonganyonga. 2 (of face) kunja, finya, kunyata. ~ion n 1 upotozi, mageuzo. 2 (of face) finyo, kasikasi, kunjo. ~ionist n mpindaviungo.

contour n 1 umbo, sura, namna. 2 (geog) kontua. ~ line n kontua ~ interval nafasi kati ya kontua. vt piga kontua. ~-farming n kilimo cha kontua. ~-map n ramani ya kontua.

contra (pref) dhidi ya, kinyume cha.

contraband n 1 uingizaji au utoaji wa magendo. 2 bidhaa za magendo.

contraceptive n kuzuia mimba; dawa

contract

ya kuzuia mimba, kingamimba adj -a kuzuia mimba. contraception n uzuiaji mimba.

contract1 vt ~ (with)/(for) fanya mkataba; fanya mapatano; afikiana. 2 ~ out (of) kataa, tupilia mbali (masharti ya mkataba). 3 (illness) pata/patwa na, shikwa na. 4 (of debts) wiwa, daiwa. ~or n kontrakta. ~ual adj -a mkataba. n 1 mapatano, maafikiano, maagano, mkataba; kondrati breach of ~ kuvunja mkataba ~ of carriage mkataba wa uchukuzi. 2 (of marriage) ahadi ya ndoa.

contract2 vt,vi 1 punguza, fupisha;

punguka, nywea iron ~s when it cools chuma hunywea kinapopoa. 2 bana, kacha, -wa -embamba, fanya kunyanzi. ~ile adj -a kuweza kunywea. ~ility n. ~ion n 1 mpunguo; ufupisho, mnyweo; kunywea. 2 (wrinkle) mfinyo/ mkunyato muscle ~ion kukaza/kubana kwa misuli, maumivu ya misuli. 3 (gram) kufupisha, mkato.

contradict vt 1 kana, kanusha; pinga, bishia (jambo lililotajwa). 2 (of facts) hitilafiana, pingana. ~ion n ukinzani, kujipinga; kupingana be in ~ion with hitilafiana na ~ion in terms mikingamo; maelezo yanayopingana yenyewe. ~ory adj.

contradistinction n tafautisho

linganishi. contradistinguish vt contradistinguish from tofautisha kwa kulinganisha.

contralto n sauti ya chini ya kike; mwanamke mwenye sauti ya chini.

contraption n (colloq) dude, dubwana. contrary adj 1 -a kinyume, -a namna nyingine kabisa. 2 (of the wind) -sio faa, hasimu, kingamo. 3 bishi, kaidi. n kinyume. ~ to kinyume cha. to the ~ kinyume. on the ~ hata, sivyo, hasha have you just come? on the ~ I came a long time ago ndio kwanza umekuja? hasha, nimekuja kitambo advise to the ~ shauri

vinginevyo. 3 by contraries kinyume cha mategemeo; kinyume. contrariety n (formal) ukinzani, uhasama (wa asili n.k.). contrariwise adv kinyume, kwa namna nyingine.

contrast vt,vi ~ A (with) and B -wa mbalimbali na; -wa kinyume cha, -wa namna nyingine kabisa; tofautisha ~ with onyesha tofauti kwa kulinganisha. n 1 utofautishaji; tofauti, hitilafu, kinyume. by/in ~ with hitilafiana na, kinyume cha, tofauti na sharp ~ hitilafu kubwa sana, tofauti kubwa.

contravene vt 1 vunja (sheria n.k.),

halifu, asi. 2 pinga. contravention n uasi, uhalifu, uvunjaji wa sheria.

contretemps n (Fr) mgogoro; bahati mbaya.

contribute vi,vt ~ to 1 saidia; toa. 2 changa; changia, shiriki. 3 (of newspaper) andikia (makala). contributor n. contribution n 1 msaada, sadaka. 2 mchango; hisa. 3 habari, makala za gazeti. 4 malipo ya lazima lay under contribution lazimisha mtu/nchi kulipa mchango. contributory adj -enye kusaidia; -enye kusababisha contributory negligence uzembe unaosababisha.

contrite adj -enye toba, -enye majuto. ~ly adv. contrition n majuto, toba perfect contrition majuto kamili.

contrive vt,vi 1 panga kwa ustadi;

simamia. 2 tunga, buni; vumbua, fanya n mvumbuzi; msimamizi. contrivance n 1 hila. 2 uwezo wa kuvumbua. 3 kitu kilichovumbuliwa. ~d adj a ku(ji)lazimisha.

control n 1 madaraka au mamlaka ya kuongoza, kuamuru au kuzuia. be in ~of -wa na amri juu ya. get/be/come/bring under ~ dhibiti, zuia. get out of ~ shindikana kutawala, as your children are out of ~ wanao hawaambiliki/ hawakanyiki. have/keep/get ~ over tawala, -wa na mamlaka juu ya, amirisha have ~ over your children

controversy

tawala wanao. lose ~ shindwa kuzuia hasira take ~ of this project chukua uongozi wa mradi huu. 2 usimamizi udhibiti, uongozaji ~ of finance udhibiti wa fedha. birth ~ n upangaji (wa) uzazi. 3 kuzuia, kurekebisha. a ~ over something kuzuia jambo (lisifanyike). 4 (of experiments etc.) kigezo/kiwango cha jaribio. 5 (of machines etc.) virekebishi, kidhibiti, viendeshi volume ~ urekebishaji wa sauti aircraft ~ tower mnara wa kuongozea ndege. 6 kituo cha magari ya mashindano. vt 1 tawala, amrisha, zuia, simamia, dhibiti ~ oneself jitawala/jiheshimu. ~ing interest n umilikaji hisa kubwa wa kumwezesha mtu kuwa na kauli kubwa juu ya sera (katika kampuni). 2 chunguza, hakiki. 3 (of prices) rekebisha. ~able adj. ~ler n msimamizi, mtawala/ mdhibiti.

controversy n ubishani, mabishano.

without/beyond ~ bila kupingwa. controversial adj -a kuelekea kuleta mabishano; (of person) -enye kupenda ubishani. controversialist n mbishani. controversially adv. controvert vt (rare) pinga, bishania, kanusha, kana.

contumacy n ukaidi, ubishani wa kupita kiasi. contumacious adj -kaidi, bishi mno. contumely n 1 ufidhuli, ujuvi, twezo. 2 matusi. contumelious adj -a ufidhuli, juvi, -a kutweza.

contuse vt viliza, vilisha damu. contusion n mavilio (ya damu).

conundrum n kitendawili, fumbo,

chemsha bongo (la kuchekesha) set

~s tega vitendawili, mafumbo.

conurbation n muunganomiji: mwingiliano wa miji ambayo hapo awali ilikaa mbalimbali kuunda jamii moja kubwa.

convalesce vi pata ahueni, pata ashekali. ~nce n muda wa kupata ahueni. ~nt adj -enye ashekali. n ahueni. ~nt home n nyumba ya

converse

mapumziko. ~nt period n kipindi cha ahueni.

convection n myuko (upitishaji wa joto katika uoevu). convector n kifaa cha kupitisha joto (chumbani n.k.).

convene vt,vi ita/itisha/fanya mkutano; kusanyika kwa mkutano. ~r n mwitishaji.

convenience n 1 hali inayofaa, isiyo na taabu au wasiwasi. at your ~ kwa nafasi yako at your earliest ~ mapema iwezekanavyo a marriage of ~ ndoa ya kufaana. a public ~ n choo cha umma. make a ~ of tumia huduma ovyo. ~ food n chakula kilicho rahisi kutayarisha. convenient adj 1 -a kufaa. 2 -enye kufikika kwa urahisi, karibu be convenient for somebody -mfalia would it be convenient for you to come tomorrow unaweza kuja kesho; (colloq) -lioko mahali panapofikika kwa urahisi. ~ly adv kwa kufaa/urahisi/manufaa; bila matata/shida.

convent n (rel) 1 jumuia ya watawa

wanawake. 2 makazi ya watawa wanawake. enter a ~ -wa mtawa.

conventicle n (rel) 1 (jengo la) mkutano wa siri wa dini.

convention n 1 mapatano, maagano, makubaliano. the Hague C~ n Mapatano ya Hague. 2 mkutano (wa siasa, dini n.k.) wa wanachama kwa kusudi maalum k.m. uchaguzi. 3 jambo la desturi, kawaida, mila. ~al adj 1 (often derog) -a desturi, -a kawaida, -a mazoea. a ~al greeting salamu ya kawaida. 2 -enye kufuata mila, jadi n.k. ~alist n mwanadesturi.

converge vi (at, on, upon) kutana,

elekea. ~nce n (maths) kukutana. convergent adj (maths) -enye kukutana.

conversant adj -zoefu, -enye kujua/

kufahamu vizuri. be ~ with a subject -fahamu vema mada. conversance n.

converse1 vi zungumza, ongea, sema,

semezana n (arch) mazungumzo, maongezi. conversation n mazungumzo, maongezi. enter into conversation anza kuzungumza hold/have conversation wa na mazungumzo. conversational adj 1 -a maongezi, -a mazungumzo in a conversational tone kwa sauti ya maongezi. 2 (of words) -a kawaida. conversationalist n msemaji sana, mtu anayejua sana kuzungumza.

converse2 adj 1 a kinyume cha, -a upande wa pili; -liogeuzwa au kubadilika. n (logic) kinyume chake. ~ly adv.

convert n mtu aliyebadili dini, msimamo. make a ~ ingiza mtu katika imani nyingine (dini, siasa n.k.) vt 1 (change) geuza, badili (hali, dini, fedha matumizi n.k.). 2 (of religion) badili. ~ to Islam silimu. ~ from Islam ritadi. ~ from Islam to Christianity tanasari. 3 (Rugby football) kamilisha (jaribio) kwa kufunga goli. ~ed adj. ~ible adj 1 -a kuweza kubadilika, a kugeuka, -a kubadilika a ~ible (car) kigeukaumbo, kibandawazi. 2 ~ible currency n fedha yenye kubadilishika/kusarifika. conversion n 1 ubadilishaji, kubadili, ugeuzaji. conversion of something into something else ubadilishaji wa kitu kuwa kitu kingine. 2 (rel) kubadili dini. ~er n 1 tanuri ya kutengeneza chuma. 2 chombo cha kubadilisha mwelekeo wa umeme. 3 chombo cha kubadilisha masafa. 4 chombo cha kubadilisha umbo la habari.

convex adj -a mbinuko/ -a mbenuko, -a kubinuka. ~ lens n lenzi mbinuko. ~ly adv. ~ity n.

convey vt (to) (from) 1 chukua, beba, peleka. 2 wasilisha, fikisha, julisha, eleza words cannot ~ my feelings maneno hayatoshi kueleza hisia zangu ~ one's meaning beba maana yake this ~s nothing to me hii haina maana kwangu. 3 (leg) hawilisha. ~land hawilisha ardhi. ~or/~er n

convulse

mchukuzi/kichukuzi. ~er belt n mkanda wa kuchukulia. ~ace n 1 gari, chombo cha uchukuzi. 2 uchukuzi, upelekaji. 3 (leg) uhawilishaji; hati ya kuhawilisha (mali). ~ancer n mwanasheria anayeandaa hati ya kuhawilisha. ~ancing (leg) n kuhawilisha.

convict vt tia hatiani, ona na hatia. be ~ed onekana na hatia n mfungwa. ~ion n 1 kupatikana na hatia. 2 kusadikisha, kusadiki sana. carry ~ion sadikisha kabisa, ondoa shaka. be open to ~ion tayari kuthibitishiwa. 3 imani, msimamo it is my own ~ion ni imani yangu, ndivyo ninavyoamini.

convince vt thibitishia, ridhisha we

couldn't ~ him of his mistake tulishindwa kumridhisha kwamba amekosea I am ~d that he is honest nimeridhika kabisa kwamba ni mwaminifu. ~d adj. convincing adj -a kusadikisha, -a kuaminisha, -a kuondoa mashaka.

convivial adj 1 anisi, changamfu, kunjufu. 2 -a raha/anasa; -a kupenda raha. ~ity n.

convoke vt ita, itisha (mkutano). convocation n 1 mkutano. 2 (rel) baraza la wakuu wa kanisa. 3 baraza la watu waliohitimu kutoka chuo kimoja.

convoluted adj 1 (bio) -lioviringika. 2 (of argument etc) -gumu kueleweka. convolution n mzingo.

convoy vt sindikiza kwa ajili ya ulinzi. n 1 ulinzi wa njiani. 2 (guard) walinzi wa msafara. 3 msafara wenye walinzi.

convulse vt sukasuka, tikisa sana the country was ~d by civil war nchi ilitikiswa na vita vya wenyewe kwa wenyewe be ~d with laughter angua kicheko be ~d with anger fura kwa hasira. convulsion n 1 (violent disturbance) msukosuko, machafuko. 2 kicheko cha kuvunja mbavu. 3 mtukutiko wa maungo (kwa kifafa, dege, mashetani n.k.).

cony/coney

convulsive adj.

cony/coney n 1 sungura; kwanga, pelele, wibari. 2 ngozi ya sungura.

coo vi lia polepole (kama njiwa); sema kwa sauti ya chini. n kulia polepole (kama njiwa).

cook vt,vi 1 pika; pikwa; pikika; iva. ~ somebody's goose komesha mtu. 2 andika kwa uongo ~ the books/ accounts andika hesabu za uongo. 3 ~ up buni; zua habari. n mpishi too many ~s spoil the broth manahodha wengi chombo huenda mrama. ~house n jiko la kambi/meli. ~er n jiko, chombo cha kupikia. ~ery n upishi. ~ery book (also ~ book) n kitabu cha mapishi.

cookie(cooky) n (US) biskuti.

cool adj 1 -a baridi kidogo. get ~ poa. 2 -tulivu as ~ as a cucumber (fig) tulivu kabisa, asiyetaharuki kabisa. keep ~ (fig) tulia. 3 play it ~ shughulika bila kuhangaika it cost me a ~ hundred shillings imenigharimu takribani shilingi mia moja. 4 (impudent) -shupavu; -fidhuli; -safihi. 5 baridi, -so -a kirafiki. 6 (sl) -zuri you look real ~ unapendeza sana. vt,vi 1 poa, poza; zimua. 2 tulia; tuliza. ~ it tulia. 3 ~ down/off tulia, poa. a ~ing off period kipindi cha kutulizana (wakati wa ugomvi kati ya wafanyakazi na menejimenti). 4 ~ one's heels ngojeshwa. ~ing tower n mnara poza. n 1 baridi. 2 utulivu. ~ness n. ~ant n kimiminiko cha kupozea. ~er n 1 kipozaji. 2 (sl) jela.

coolie n (sl. derog) kibarua, kuli.

coop n tundu, kizimba (cha kuku n.k.). vt funga, zuia (katika tundu au kizimbani).

co-op n (colloq) see cooperative.

cooper n mtengeneza mapipa.

cooperate vi shirikiana. co-operation n ushirikiano in cooperation with kwa kushirikiana na. co-operative adj -a kushirikiana, -a ushirika, -a kupenda kusaidia a cooperative spirit moyo wa kushirikiana. cooperative societies n

(also coops) vyama vya ushirika. cooperative shop n duka la ushirika. co-operator n mshiriki.

co-opt vt (of a committee) shirikisha. ~ed member n mjumbe mshirikishwa.

co-ordinate adj 1 -a namna sawa, -a kadiri/cheo kile kile. 2 -a kulingana sawa. 3 ambatanishi. ~ clause n kishazi ambatani. vt ratibu n watu/vitu sawa. co-ordination n 1 uratibu. 2 hali ya kuwa namna/kadiri/cheo sawa coordination point kituo cha uratibu. 3 (of muscles) kupatana, kukubaliana. co-ordinator n mratibu.

coot n 1 aina ya ndege anayeishi mjini. 2 (sl) mjinga/mpumbavu as bald as a ~ -enye upara kabisa.

cootie n (army sl) chawa.

cop1 n see cooper2.

cop2 vt,vi 1 ~ it adhibiwa. 2 ~ out (of) kwepa, acha (jambo/wadhifa n.k.). ~ -out n kukosa/kukwepa kuwajibika. 3 ~ a plea kiri kosa na kuomba radhi. n (sl) kushika, kukamata it's a fair ~ ni kukamatwa kihalali/palepale unapokosea. not much ~ sio na maana, bure.

copal n sandarusi.

cope vi ~ (with) weza, vumilia.

copeck/kopek n kopeki: senti ya

Kirusi.

coping n (archit) kigongo cha ukuta. ~ stone n (fig) kiishilizo.

copious adj 1 ingi, furufuru, tele, -a

kufurika. 2 (of writer) -lioandika sana. ~ly adv. ~ness n.

copper1 n 1 shaba nyekundu. (attrib) ~ wire n udodi. ~ cable n kebo ya shaba. 2 (vessel) sufuria kubwa (hasa ya kuchemshia nguo). 3 (coin) senti, fulusi, sarafu ya shaba. 4 ~ beech n mti (wa) shaba: mti wenye majani ya rangi ya shaba. ~ bottomed adj meli iliyopakwa shaba kwenye kitako; (fig) salama kabisa, -enye uhakika. ~plate n bamba la shaba

(lililonakshiwa) ~ plate hand writing mwandiko mzuri. ~ smith n mfua shaba. vt paka shaba kitako cha meli.

copper2 (also cop) n (sl) polisi.

copra n mbata.

coppice/copse n msitu mdogo.

Copt n Mkhufti: mtu wa asili wa Misri.

copula n 1 (gram) kitenzi shirikishi, kopula. 2 (med) kiungo.

copulate vi ~ (with) jamiiana. (of animals) pandana. copulation n. copulative adj 1 (formal) -a kuunga, -a kuunganisha. 2 (gram) shirikishi. copulative verb n kitenzi shirikishi. n (gram) kishirikishi.

copy vt,vi 1 (out) nakili make a ~ of something nakili. 2 iga, fuatisha. 3 ~ from/off ibia (mitihani n.k.). n nakala. attested ~ n nakala iliyoshuhudiwa. certified ~ n nakala iliyothibitishwa fair ~ nakala safi did you get your ~ of the book/ newspaper? ulipata nakala yako ya kitabu/gazeti?. 2 maandiko (tayari kuchapwa). good ~ n habari za kuvutia. ~-cat n mwigaji. ~ist n mtu anayenakili; mwigaji mtindo; mtengeneza nakala. ~- book n daftari la hati mkato blot your ~book haribu sifa yako. ~-boy/girl n kijana tarishi (katika ofisi ya gazeti). ~-desk n meza ya mhariri. ~hold (GB) n ukodishaji wa ardhi; ardhi iliyokodishwa n mkodishaji wa ardhi. ~right n haki ya kunakili. vt pata haki ya kunakili. ~writer n mwandishi wa matangazo (agh ya biashara).

coquette vi piga ubembe, bemba, tia

ashiki kwa kujishaua. coquetry n ubembe; tabia ya kushawishi/vutia/ tamanisha wanaume. n mbembe. coquettish adj. coquettishly adv.

coracle n mashua ndogo ya fito na ngozi.

coral n (red) marijani, fedhaluka;

(white) matumbawe. ~ reef n mwamba tumbawe adj -enye rangi ya

corn

waridi au nyekundu. ~ lips n midomo myekundu.

cord n 1 kamba; mshipi; ugwe. 2 kiungo cha mwili kilicho kama mshipi. the vocal ~s n vitunga mlio, nyuzi sauti. umbilical~ n kiungamwana/rulela. spinal ~ n uti wa mgongo. 3 (elec) waya, uzi. 4 see corduroy (pl). vt funga kamba. ~age n 1 kamba. 2 kamba zitumiwazo melini.

cordial adj 1 -kunjufu, -changamfu give a ~ welcome pokea kwa furaha, karibisha vizuri. 2 -kali, -enye nguvu. a ~ hatred n chuki kali/ya dhati. n kinywaji (hasa cha matunda cha kuchangamsha mwili). ~ly adv. ~ity n.

cordite n baruti (isiyotoa moshi).

cordon n kizuizi cha askari. a sanitary ~ n kizuizi cha askari cha karantini. corduroy n 1 kodrai. 2 (pl) (also cords) suruali za kodrai. ~ road n njia ya miti (kupita matope n.k.).

core n 1 (of fruit) kokwa. 2 kiini, maana get to the ~ of the subject fikia kiini, gusa kiini/maana rotten to the ~ -liooza kabisa. vt toa kokwa. ~r n kisu cha kutolea kokwa.

co-respondent n mshitakiwa mwenzi

(kwa kuzini na mume/mke wa mshitaki katika daawa ya talaka).

coriander n giligilani. ~ leaves n kitimiri.

cork n 1 koki, gome muoki, gome jepesi la muoki. 2 kizibo (cha gome muoki). vt ~ (up) ziba; (feelings) zuia kabisa. ~ed adj 1 -enye ladha mbaya (kutokana na koki iliyooza). 2 (sl) liolewa sana. ~screw n kizibuo. ~age n malipo ya huduma kwa ajili ya vinywaji vilivyoletwa na wanywaji wenyewe mkahawani.

corker n (dated sl.) 1 jambo la ajabu. 2 wazo lisilopingika.

cormorant n mnandi.

corn1 n 1 (grain) nafaka (hasa mahindi, mchele, ngano na mtama) ~ meal unga wa sembe n.k. ~ flour/starch

corn

unga wa mahindi n.k. ~-cob n konyo au gunzi la hindi. ~ pone n mkate wa mahindi. 2 punje moja ya nafaka au pilipili manga. ~crake n kwekakweka (ndege).

corn2 n sugu/sagamba katika kitengele cha mguu hasa katika kidole cha mguu. tread on somebody's ~s udhi mtu.

corn3 vt hifadhi nyama kwa chumvi. ~ed beef n nyama ya kopo, bifu (iliyohifadhiwa kwa chumvi).

cornea n konea: sehemu ya mbele ya jicho (iliyo ngumu) inayowezesha miali ya mwanga kupenya.

cornelian n akiki.

corner n 1 pembe, kona standing at a street ~ kusimama kwenye pembe ya barabara just round the ~ nyuma (hapo) kwenye kona; karibu sana turn the ~ kata kona; (fig) pata ahueni/nafuu (baada ya maradhi/kipindi kigumu) cut off a ~ pita moja kwa moja (badala ya kuzunguka). cut ~s tumia njia za mkato, pinda sheria (ili kufanikisha kitu). drive somebody into ~ tia mashakani. be in a tight.~ -wa hatarini, -wa katika hali ngumu. 2 (secret or remote places) mahali pa siri they searched all ~s walitafuta kila kipembe. 3 (region quarter) sehemu to the four ~s of the earth pote duniani, pembe zote za dunia. 4 (comm) kununua bidhaa zote za aina fulani (kwa ajili ya kuhodhi na kudhibiti bei). 5 (foot- Hockey) kona. ~ kick n mpira wa kona. ~ stone n jiwe la msingi; (fig) msingi/kiini cha jambo. vt, vi 1 sukumia kwenye pembe/kona; (fig) weka katika hali ngumu. ~ed animal n mnyama aliyezingwa. 2 dhibiti (kwa kununua bidhaa zote). 3 (of vehicles) kata/ pinda kona.

cornet n buruji.

cornucopia n 1 (myth) pembe itoayo chakula na vinywaji bila kikomo. 2 alama (ya pembe hii) inayoonyesha wingi wa neema.

corny adj (sl) -a kale, -liochakaa. ~joke n mzaha uliochakaa.

corolla n (bot) korola: jumla ya petali

katika ua.

corollary n matokeo.

corona n (pl.) korona, taji la nuru, kianga cha mwezi; jua. ~l adj -a korona/kaakaa. coronet n 1 kitaji, shada la maua, taji dogo, pambo la kichwa 2 (bot) shada.

coronary adj (med) -a moyo. ~

arteries n ateri za moyo. ~ thrombosis n kitomoyo, shtuko la moyo.

coronation n kutawaza/kutawazwa.

coroner n (leg) afisa mchunguzi wa

vifo (vya ghafla/visivyo vya kawaida). ~'s inquest n baraza la utafiti wa sababu ya kifo.

corporal1 n (mil) koplo.

corporal2 adj -a mwili, -a kuhusu

mwili ~ punishment adhabu ya kutandikwa. corporeal adj -a kimwili (badala ya kiroho). ~ needs n mahitaji ya mwili.

corporate adj -a shirika, -a pamoja ~ body shirika ~ name jina la shirika ~ responsibility madaraka ya pamoja. corporation n 1 ushirika, shirika public corporation shirika la umma. 2 madiwani, manispaa the mayor and corporation meya na madiwani wake. 3 (colloq) kitambi. 4 (US) kampuni, shirika corporation tax kodi ya shirika.

corps n 1 kundi la wanajeshi (agh wa kazi). carrier ~ n kikosi cha wachukuzi. 2 jeshi la askari. 3 diplomatic ~ n jamii ya mabalozi. 4 kundi.

corpse n maiti; mzoga.

corpulent adj -nene sana. corpulence n.

corpus n 1 mkusanyo (wa maandishi

yote ya mwandishi mmoja/aina moja/mada moja). 2 mwili. 3 (leg) writ of habeas ~ n amri ya kufikisha mfungwa kortini. 4 (rel) C~ Christ Sikukuu ya Ekaristi Takatifu.

corpuscle

corpuscle n chembechembe za damu, chembedamu. corpuscular adj -a chembe za damu.

corral n 1 zizi. 2 boma. vt 1 tia zizini. 2 (sl) teka, kusanya; fungia zizini, tengeneza boma.

correct vt 1 rekebisha, sahihisha,

kosoa. 2 (punish) rudi, tia adabu. 3 rekebisha, ondoa kasoro ~ a malformity/disorder ondosha kilema cha mwili; ponyesha adj 1 sahihi, fasaha ~ (clear) style mtindo fasaha. 2 (of manner, conduct) muwafaka, barabara; bila kosa. ~ly adv. ~ness n. ~ion n 1 usahihishaji, utoaji makosa; sahihisho, rekebisho. 2 (arch) a house of ~ion chuo cha mafunzo, jela speak under ~ion sema kwa sharti (kwamba unaweza kusahihishwa). 3 (punishment) adhabu, marudi, rada. 4 (improvement) matengenezo. ~ional adj.

correlate vi,vt ~ (with) wiana, husiana, patana; patanisha. correlation n uwiano, uhusiano. correlative adj 1 (word or thing) -a uwiano, -enye uhusiano. 2 (gram) correlative conjunction n kiunganishi wiani.

correspond vi 1 ~ (with) fanana,

kubaliana, tangamana; lingana. 2 ~ (to) -wa sawasawa, fanana na. 3 ~ (with) andikiana barua; wasiliana (kimaandishi). ~ingly adv. ~ing adj the ~ing time last year ikilinganishwa na) mwaka jana wakati kama huu. ~ence n 1 ulinganifu, tangamano, kukubaliana, uhusiano one-to-one ~ence uhusiano wa moja kwa moja. 2 barua; mawasiliano (ya kimandishi); kuandikiana barua ~ence education elimu kwa njia ya posta. ~ent n 1 mwandishi wa makala (katika magazeti n.k.); mleta habari. 2 mtu anayeandikiana barua na mwingine. 3 (comm) vyombo vinavyohusiana (k.m. benki, mashirika).

corridor n ushoroba. ~ train n garimoshi lenye ushoroba/ujia wa kuingilia vyumbani. ~s of power n mahali panapofanyiwa kampeni zisizo rasmi; mlango wa nyuma.

corrigendum n korijenda: orodha ya makosa na masahihisho katika kitabu.

corrigible adj -a kurekebishika.

corroborate vt thibitisha, (kwa kutoa ushahidi wa ziada). corroboration n uthibitisho, ushuhuda. in corroboration (of) kwa ithibati. corroborative adj -a kuthibitisha, -a kuelekea kuthibitisha. ~ evidence n ushahidi wenye ithibati.

corrode vt, vi -la, haribu, lika. corrosion n uharibifu, ulikaji (k.m. wa kutu). corrosive adj (substance) -enye ukali wa kuharibu/kubabua. n dawa yenye ukali.

corrugate vt,vi kunjakunja (kama migongogongo midogo), kunjamana, weka matuta. ~d adj -enye mikunjo. ~d iron (sheets) n mabati (ya kuezekea). corrugation n migongogongo, mikunjokunjo, makunyanzi.

corrupt vt,vi 1 potosha, shawishi kufanya mabaya he was ~ed by the life in the city alipotoshwa na maisha ya mjini. 2 toa rushwa/hongo. 3 haribu, chafua. 4 oza, ozesha. ~ible adj. ~ibility n adj 1 (of persons, their actions) -ovu, -so na maadili, -soaminika kuhongeka. 2 -enye kupokea/kutoa rushwa. ~ practices n vitendo vilivyopotoka, matendo maovu; (of language) potovu this is a ~ text haya ni matini yaliyoharibiwa/ghushiwa. ~ion n 1 utoaji/ulaji rushwa/hongo/mlungura, ufisadi, upotovu. 2 uozo, ubovu, uchafu. 3 uharibifu.

corsage n 1 badisi. 2 (US) shada (la

kifuani).

corsair n (hist) 1 haramia wa baharini.

2 meli ya haramia wa baharini.

corse n (arch or poet) maiti.

corset n koseti (nguo ya ndani ya

cortege

kubana kuanzia kiunoni hadi mapajani).

cortege n wasindikizaji, waandamanaji wa sherehe maalum (ya rais, mfalme n.k.) agh. kwa ajili ya mazishi, n.k.

cortex n gamba; ganda; gome; tabaka la nje ya ubongo. cortical adj.

coruscate vi metameta, memeteka,

ng'aa. (fig) coruscating wit n uchekeshaji werevu. coruscation n.

corvee n (arch) shokoa.

corvette n manowari ndogo (ya kusindikiza meli ya shehena).

cosh n (GB sl) rungu. vt (GB sl) piga kwa rungu.

cosher adj, n see kosher.

co-signatory adj, n mtiaji sahihi mwenzi.

cosmetic adj -a kipodozi. n (usul. pl) kipodozi. ~ian n mtaalamu wa vipodozi.

cosmopolitan adj 1 -a kuhusu/kutoka sehemu zote za dunia. 2 -a kidunia; pana (kutokana na uzoefu wa sehemu nyingi za dunia) a ~ outlook mtazamo wa kidunia adj (person) -enye mtazamo wa kiulimwengu. n 1 msafiri wa dunia. 2 mlimwengu: mtu mwenye mtazamo wa kimataifa. 3 kiumbe/mmea wa duniani pote. cosmopolitism n.

cosmos n ulimwengu. cosmic adj -a

(kuhusu) ulimwengu mzima. cosmic rays n miali ulimwengu. cosmogony n nadharia kuhusu chanzo cha ulimwengu. cosmography n kosmografia: maelezo ya sura ya dunia katika ramani. cosmology n 1 kosmolojia: sayansi kuhusu ulimwengu. 2 tawi la sayansi lishughulikalo na muundo na umbo la ulimwengu. cosmonaut n also astronaut mwanaanga (wa Kirusi).

cosset vt engaenga, endekeza; dekeza.

cost1 vt,vi 1 (cost) gharimu, patikana kwa bei/gharama fulani the house ~s 4 ml shs to build nyumba inagharimu shs mil 4 kujenga dictionary making ~s much time kutunga kamusi huchukua muda mwingi. 2 (result in

cosy;2 cosey

the loss of) patisha/ingiza hasara; hasiri careless driving may ~ you your life uzembe katika kuendesha gari unaweza kuhasiri maisha yako. 3 (industry and comm) kadiria bei (kwa kuzingatia gharama za uzalishaji). ~ing n (Industry) upangaji/uwekaji/ ukadiriaji bei the ~ing department idara ya kupanga bei n 1 bei, gharama the ~ of living gharama za maisha the ~ of a house gharama/bei ya nyumba the ~ price of an article gharama za kutengeneza kitu; bei ya kununulia (itolewayo na mfanyabiashara). ~ accounting n hesabu za kuonyesha gharama. 2 ~s (leg) gharama za kesi (zitolewazo na aliyeshindwa kesi). at all ~s kwa vyovyote vile. at the ~ of kwa kupoteza count the ~ kadiria hasara. ~ly adj 1 -a gharama kubwa, -a thamani kubwa. 2 -enye kufanywa kwa gharama kubwa.

co-star vt 1 -wa nyota pamoja (na),

shiriki na wengine kama mababe. 2 ingiza mababe wawili katika filamu. n mbabe mwenzi.

coster monger n mchuuzi anayeuza matunda/mboga mitaani.

costive adj (liter) -enye kufunga tumbo; -a kufunga choo, -enye uyabisi wa tumbo. ~ness n.

costume n 1 mavazi (maalum) (agh.

kwa kipindi, nchi, cheo maalum au taifa fulani) national ~ vazi la taifa. 2 maleba: mavazi ya shughuli/majira maalumu. vt ~ a theatre etc. leta/ shona maleba n.k. kwa ajili ya michezo. 3 suti ya mwanamke. swimming ~ vazi la kuogelea ~ jewellery vito bandia. costumier n mtengenezaji, muuzaji na mwazimishaji wa mavazi ya sherehe mbalimbali.

cosy1 adj -a kufurahisha/kuburudisha

na kuleta raha it's very ~ here mahali hapa pazuri/panaburudisha. a ~ little job kazi ndogo ya malipo makubwa adv kwa furaha/raha.

cosy;2 cosey n kifuniko (cha birika la

cot

chai) au yai lililochemshwa.

cot1 n 1 (poet) kibanda. 2 kifuniko

(hasa kinachofunika kidole ili kisiumie).

cot2 n 1 kitanda kidogo chembamba

(kinachoweza kubebwa kwa urahisi) cha mtoto mdogo. 2 kitanda cha safari. ~ death n kifo cha ghafla cha mtoto mchanga (agh usingizini bila kuugua).

cotangent n (maths) kotanjiti.

cote n kibanda (kwa ajili ya kuku, njiwa n.k.).

coterie n genge (watu wenye mawazo mamoja).

coterminous adj enye mpaka/kituo kimoja.

cottage n nyumba ndogo hasa ya

kijijini/shambani. ~ hospital n hospitali ndogo ya kitongojini. ~ industry n kiwanda kidogo. cotter n mkazi katika nyumba ndogo mashambani. ~r n mtu aishie kwenye nyumba ndogo (mkulima; kibarua wa mashambani).

cotton1 n pamba. ~ wool n pamba. ~-cake n mashudu ya pamba agh. hutumiwa kama chakula cha ng'ombe. ~-gin n kinu cha kuchambulia pamba. ~-grass n pamba mwitu. ~-mouth n nyoka wa majini mwenye sumu. ~-tail n (US) mnyama aina ya sungura.

cotton2 vi (sl) 1 kubaliana. 2 -wa na urafiki. ~ on (to) (colloq) fahamu, elewa. ~ up to jenga urafiki; jaribu kufanya urafiki.

cotyledon n kotiledoni.

couch vt,vi 1 jilaza (kwa ajili ya kupumzika au kulala). 2 lala kwa kuvizia; weka mahali pa maficho au pa kuvizia. 3 (of animals) jikunyata na kulala usingizi. 4 fuma, tarizi. 5 kuweka maelezo katika mtindo maalumu. 6 shusha (mkuki, panga, n.k.) tayari kwa kushambulia. n 1

kochi: samani itumiwayo kwa kukalia au kulalia. 2 kitanda cha mgonjwa wakati anapofanyiwa uchunguzi.

couchant adj (heraldry, of animals)

-liolalia miguu na kuinua kichwa juu (kama afanyavyo paka).

couch-grass n (bot) ukoka.

cough vi, vt 1 kohoa. ~ out kohoa, toa kohozi. 2 (draw attention) jikohoza ~ down a speaker nyamazisha msemaji. ~ up ondoa kooni kwa kukohoa. ~ up a fish bone toa mwiba wa samaki kwa kukohoa. ~ up (sl) toa, changa, kabidhi bila kupenda. ~-drops n vidonge (peremende) vya kikohozi.

could pt of can.

council n 1 halmashauri; baraza. City C~ n Halmashauri ya Jiji. Revolutionary C~ n Baraza la Mapinduzi Executive C~ (Cabinet) Baraza la Mawaziri. Legislative C~ n Baraza la Kutunga Sheria. 2 mkutano. ~ of war mkutano wa kushauriana mambo ya vita. ~ board n meza ya mkutano ya halmashauri. ~ chamber n chumba cha mikutano ya halmashauri. ~lor (also ~-man) n diwani, mjumbe wa baraza.

counsel n 1 (also advice) ushauri, mawaidha, wasia. give ~ shauri, toa ushauri/wasia take/ hold ~ with somebody pata ushauri kutoka kwa mtu keep one's own ~ setiri siri. 2 (with indef. art or in pl but not with numerals) a ~ of perfection ushauri mzuri kabisa ambao hauwezi kufuatwa. 3 mshauri; wakili, mwanasheria ~ for defence wakili wa utetezi ~ for prosecution wakili wa mashitaka. King's/ Queen's ~ n wakili mwandamizi (wa serikali) vt shauri, nasihi/usia. ~lor n 1 mshauri. 2 (US) wakili.

count1 n aina ya lodi (katika Bara la Ulaya isipokuwa Uingereza). ~ess n mke wa lodi.

count2 vt,vi 1 ~ (from) (to) hesabu, taja mlolongo wa idadi. (colloq) ~noses hesabu idadi ya watu. ~less adj bila idadi, -ingi mno, -siohesabika, pasi na idadi there are ~less examples etc. kuna mifano

countenance

chungu mzima there are 10 ~ without the visitors wako 10 tukiacha wageni. ~able noun n nomino ya idadi. 2 jumlisha, ingiza. 3 (fig) (ji) hesabu. 4 -wa na thamani/maana he doesn't ~ hana maana every minute ~s kila dakika ina thamani. ~ against athiri, fanya mtu afikiriwe vibaya. ~ among fikiriwa. ~ down hesabu kurudi nyuma. ~ in ingiza, ongeza/jumuisha. ~ me in nimo. ~ on tegemea, tumainia may ~ on you naweza kukutegemea. ~ out hesabu moja moja; (boxing) hesabia muda; ondoa; (of parliament) tangaza kuwa hakuna akidi. ~ up jumlisha it ~s for much ina maana sana/kubwa. n 1 hesabu; kuhesabu ask for a ~ omba kuhesabu kura. keep ~ of something weka hesabu ya. lose ~ shindwa kuhesabu. take the ~/be out for the ~ hesabiwa muda. 2 kujali take no ~ of -tojali. 3 shitaka.

countenance n 1 uso, sura a person

with a fierce ~ mtu mwenye sura ya ukatili. 2 fikra zilizotulia, utulivu, udhibiti wa nafsi. put out of ~ fadhaisha, tahayarisha. keep one's ~ tulia, -toonyesha hisia, kaza uso kuzuia kicheko n.k. give ~ to a plan kubali shauri vt kubali, unga mkono I cannot ~ it siikubali.

counter1 n 1 kaunta: sehemu ya mfuto k.m. meza, ambapo vitu hununuliwa/huuziwa. sell under the ~ uza kwa mlango wa nyuma. 2 kipande, sarafu (ya kuhesabu katika michezo fulani). 3 mtu ahesabuye. 4 (math.) kihesabio.

counter2 adv kinyume, kwa kubadili run ~ to shindana na; enda kinyume na, pinga adj -a kinyume; -a kukabili. vt,vi 1 kabili, jibu mapigo, pinga (pref) 1 kinyume cha. 2 jibu la. 3 lingana na. 4 dhidi ya.

counteract vt kinza, zuia, shinda. ~ion n. ~ive adj.

counter-appeal n rufani dhidi ya rufani. vt kata rufani dhidi ya rufani.

counter-attack n jibu la mapigo. vt

rudishia shambulio/pigo.

counter-attraction n mvuto shindani; mivutano.

counterbalance see counterpoise vt

sawazisha. n usawazisho (uzito ulio sawa na uzito mwingine k.m. mizani).

counterblast n jibu kali na lenye nguvu; upepo mshindani.

counterblow n pigo linalojibu pigo jingine; midundano.

counter-change n kubadilisha (nafasi/ sehemu/vifaa n.k.); mabadilishano.

counter charge n (leg) shitaka la mshitakiwa (dhidi ya mshitaki).

countercheck n 1 kuzuia kinachopinga. 2 kaguo. vt 1 kagua tena. 2 zuia kinachopinga.

counter-claim n dai kinzani. vt leta dai juu ya dai.

counter-clockwise adv see anti clockwise.

counter-espionage n ujasusi pinzani: ujasusi dhidi ya ujasusi.

counterfeit vt ghushi, buni; iga, (kwa nia ya kudanganya). n bandia,mfano adj -a bandia, -a kubuni; -a kughushi; -a kuiga. ~er n. ~ing n.

counterfoil n kishina (cha stakabadhi, barua ya fedha, hawala n.k.)

counter intelligence n see counter espionoge

counter-irritant n kipoza maumivu.

countermand vt 1 tangua amri, (kwa kutoa amri ya kinyume). 2 kurudisha nyuma (k.m. kundi la askari) kwa kutoa amri kinyume na ile iliyotolewa kwanza. n utoaji amri inayotangua amri ya awali.

countermine vt,vi 1 tega bomu dhidi ya bomu lingine. 2 zuia pigo kwa kulivuruga kabla ya kutokea kwake. n mpango wa kupinga shambulio; mpango dhidi ya shambulio la adui lililopangwa.

counteroffensive n kujibu (mapigo/shambulio).

counter offer n fadhila ya kujibu fadhila.

counterpane n firashi.

counterpart

counterpart n 1 nakili. 2 (of a person)

mwenzi. 3 (of a thing) kifanani.

counterplot n hila ya kupindua hila, hila dhidi ya hila.

counterpoint n (mus) 1 utumbuizo;

kijalizo cha wimbo. 2 ujalizaji wa wimbo.

counterpoise vt sawazisha, tia uzito

upande ulio mwepesi ili kusawazisha pande zote mbili. n 1 (jiwe lenye) uzito ulio sawa na uzito mwingine. 2 hali ya urari/mizani/usawazisho.

counterpoison n dawa inayozuia sumu. counter revolution n kupinga mapinduzi. ~ry n, adj.

countersign vt 1 tia sahihi (hati n.k.) iliyokwisha tiwa sahihi na mwingine. 2 thibitisha kwa kutia sahihi. n 1 (mil) neno, ishara, itikio la siri (ya

kupishwa askari walindao zamu). 2 utiaji/uwekaji sahihi.

countersink vt 1 (tech) panua tundu la kuingizia skrubu. 2 shindilia skurubu ndani ya tundu.

countervail vt,vi 1 sawazisha; tumia

nguvu dhidi ya kikinzani chenye athari mbaya au chenye hatari. 2 -wa/pata nguvu sawa ya kufidia. 3 pata/lipwa sehemu ya ushuru juu ya maduhuli (yaliyofidiwa na nchi iingizayo bidhaa).

counterweight n uzito wa kusawazisha. country n 1 nchi. 2 shamba in the

~side mashambani. ~life n maisha ya shamba. town and ~ planning mpango wa miji na vijiji. go up ~ enda bara. 3 the ~ n wananchi; taifa kwa jumla. go to the ~ itisha uchaguzi mkuu (kwa haki ya kuunda serikali mpya). 4 (as attrib.) ~ club n klabu ya kiungani. ~ cousin n (colloq). jogoo la shamba, mshamba ~-folk n wenyeji wa mashambani, wanavijiji, watu wa vijijini. ~gentleman n mwinyi. ~ party n chama cha maslahi ya wakulima. ~ house n nyumba ya shamba. ~man/women n 1 mwananchi. 2 mkazi wa shamba. ~ seat n nyumba kijijini (agh. ya mtu tajiri). ~side n

shamba. countrified adj -a kimashamba, -enye desturi za kishamba.

county n (GB) mkoa; (US) wilaya. ~

family ukoo wa asili (katika mkoa/ wilaya).

coup n mapinduzi. ~d'etat n mapinduzi ya serikali. ~de grace n pigo la kifo.

coupe n 1 gari la farasi la abiria wawili. 2 (US) motokaa ya watu wawili yenye milango miwili.

couple n 1 vitu au watu wawili

wanaohusiana (mtu na mkewe); wachumba, maharusi. 2 (fig) they go in ~s huenda wawili wawili. 3 mbilitatu, kadhaa. vt,vi 1 (on) unga, unganisha; ungana (fikirani). 2 oana; jamiiana. 3 (of animals) pandana. 4 ~ with unganisha, husisha. ~d with this pamoja na hayo. ~r n kiunganisho. coupling n 1 kiungo. 2 uunganishaji; uunganaji. 3 njia inayounganisha mizunguko miwili ya umeme ili umeme upite kati yake. coupling-pin n (tech) pini ya kiungo.

coupon n 1 kuponi: hati itolewayo kumwezesha mtu kupata kitu, huduma au malazi. 2 kipande cha tangazo lililochapishwa kinachokatwa na kutumiwa kama fomu ya kuagizia kitu au maelezo. 3 sehemu ya/kipande cha hisa kinachoonyesha kiasi na tarehe ya riba.

courage n ushujaa, ujasiri, ushupavu. take ~ jipa moyo. take one's ~in both hands jipiga moyo konde have the ~ of one's convictions -wa na moyo wa kufanya unaloamini. ~ous adj.

courier n 1 mjumbe; tarishi. 2 mtu

anayesindikiza na kuwafanyia watalii mipango ya safari.

course1 n 1 mwendo. the ~of events jinsi mambo yanavyoenda. in the ~ of his childhood wakati wa utoto wake. in the ordinary ~ of nature kwa kawaida. in (the) ~ of time

course

hatimaye in the ~ of the conversation wakati wa mazungumzo. in due ~ kwa wakati wake let nature take her ~ yaache mambo yalivyo. 2 njia, uelekeo (naut) a northerly ~ uelekeo wa kaskazi there is no other ~ open hapana njia nyingine. take a middle ~ fuata njia isiyoelemea upande mmoja take a different ~ fanya vingine. as a matter of ~ mambo kama yalivyo/yanavyotarajiwa kuwa. 3 (series of lectures, treatments etc.) kozi: mfulizo wa masomo; mfululizo wa matibabu. 4 (part of meal) sehemu ya mlo. 5 uwanja (wa kushindania mbio za farasi n.k.). stay the ~ endelea hadi mwisho (licha ya matatizo); -tokata tamaa. 6 tabaka, mstari (wa matofali au mawe katika nyumba). 7 on/off ~ sawa/mrama.

course2 vt,vi 1 kimbiza, fukuza (hasa sungura) kwa kutumia mbwa. 2 (of liquids) tiririka.

courser n (poet) farasi mwenye mbio.

court1 n 1 kitala. 2 mahakama, korti. appellate ~ n mahakama ya rufani. civil ~ n mahakama ya madai. high ~ n mahakama kuu. primary ~ n mahakama ya mwanzo. contempt of ~ n kudharau mahakama. open ~ n mahakama ya wazi, (ambapo wasikilizaji wowote wanaruhusiwa). be ruled/put out of ~ kataliwa mahakamani. take to ~shitaki. 3 ua (wa nyumba). ~yard n uga, uwanja. 4 kiwanja cha michezo. ~card n karata ya mzungu (katika mchezo wa karata). ~ier n mtumishi wa kitala. ~ martial n mahakama ya kijeshi vt shtaki kijeshi. be ~ martialled shtakiwa kijeshi.

court2 vt 1 jipendekeza kwa heshima. 2 bembeleza pay ~ to (a woman) fanya urafiki, posa (mwanamke), bemba. 3 karibisha/chokoza (hatari, maafa, n.k.). ~ship n 1 posa, uchumba, ubembelezi. 2 kipindi cha posa.

courtesan n malaya, kahaba (hasa wa matajiri).

cover

courtesy n 1 adabu, heshima, ustahifu, uungwana treat with ~ stahi, heshimu. 2 kuheshimu, kitendo cha heshima. 3 ~ title (GB) cheo cha heshima. 4 by ~ of kwa fadhila ya. courteous adj -a adabu, -a heshima, stahifu. courteousness n. courtly adj -enye adabu, -a heshima, stahifu. courtliness n.

cousin n binamu: ndugu (waliozaliwa

na ndugu wa baba na mama). ~ly adj.

cove1 n ghuba ndogo.

cove2 n (GB dated sl.) jamaa.

coven n mkutano wa wachawi. covenant n 1 (leg) mkataba, hati, mapatano. deed of ~ hati iliyothibitishwa kisheria (agh. kuhusu mali). 2 ahadi ya maandishi ya kutoa malipo ya ufadhili kwa vipindi vilivyopangwa. vt,vi agana, patana, kubaliana, andikiana mkataba. ~ed adj liofungwa na mkataba.

coventry n (phr) send a person to ~ tenga mtu kabisa (kwa kukataa kuongea naye).

cover vt 1 funika; funikiza. 2 ~ over

tandaza. ~ up fungia, ficha, funika kabisa. n kuficha; mbinu/namna (ya kuficha). vi danganya; enea, tanda the water ~s the whole plain maji yameenea uwanda mzima. 3 be ~ ed with pambwa na; jaa; rashia; pakaza (tope). 4 (of money) tosha 100 shs will ~ my needs shilingi mia zitanitosha/tosheleza. 5 (protect) kinga, wekea bima, tetea, linda. 6 (of guns/fortress) tawala. 7 safiri; maliza ~ten miles in an hour safiri maili kumi kwa saa moja. 8 (sports) linda; kaba. 9 (comprise) jumlisha, -wa na the speech ~ed all the main issues hotuba ilikuwa na mambo yote muhimu. 10 (of a journalist) he ~ed the meeting alielezea habari za mkutano he ~s sports yu mwandishi wa habari za michezo. ~ing letter n barua iliyoambatishwa ya maelezo (ya ziada). 11 ~ in fukia kabisa

(shimo n.k.); funika. 12 jiingiza; jitetea. ~ oneself with disgrace jiingiza fedhehani. n 1 kifuniko, kawa. 2 nguo (kitambaa cha maandalizi) ya meza. 3 kinga, maficho. take ~ jificha. break ~ jifichua. 4 jalada. read a book from ~ to ~ soma kitabu chote. ~ girl n msichana anayepigwa picha za kuwekwa kwenye majalada ya magazeti. 5 (insurance) fedha za fidia (dhara likitokea). ~ note n hati ya bima ya muda. 6 (comm) fedha, dhamana. 7 under ~of kwa kisingizio cha. 8 bahasha. under separate ~ ndani ya bahasha nyingine. 9 under plain ~ isiyo na kitambulisho/alama. 10 magugu. ~age n taarifa za matukio. ~let n firashi.

covert1 n maficho, kichaka.

covert2 adj -a siri, -liofichwa, -a hila. ~glances n kutupa macho kwa siri. ~ly adv.

covet vt tamani (hasa mali ya mwingine), taka sana; ona shauku ya (kitu kisicho halali au kisicho chako). ~ous adj. ~ous (of) -enye tamaa (shauku, uchu) (hasa ya mali ya mwingine). ~ousness n.

covey n kundi (la ndege).

cow1 n 1 ng'ombe jike. 2 jike la mnyama (kama tembo, kiboko n.k.). 3 (derog sl) mwanamke till the ~s come home daima. ~-bell n kengele inayofungwa ng'ombe. ~ boy n 1 chunga ng'ombe (katika tambarare za Amerika). 2 mfanyabiashara asiye mwaminifu. 3 mhuni, mdanganyifu.

~-catcher n ngao (ya gari), fremu ya chuma iliyofungwa mbele ya injini ya garimoshi inayoondoa vizuizi vya relini. ~-fish n samaki-ng'ombe (samaki mwenye kichwa kama cha ng'ombe). ~herd n mchunga ng'ombe, mchungaji wa ng'ombe. ~hide n ngozi ya ng'ombe. ~man n (pl) ~men mkama ng'ombe. ~shed/ ~-house n zizi la ng'ombe. ~-pox n ndui ya ng'ombe.

cow2 vt ogofya, tisha.

cowage n upupu, kiwavi.

coward n mwoga adj -oga,-enye hofu. ~ly adj. ~ice n woga.

cower vi nywea, jikunyata; jikunja (ili kujificha au kwa hofu).

cowl n 1 ukaya (namna ya kofia); kifuniko cha bomba la moshi. 2 kifuniko (cha injini ya gari). 3 kanzu yenye kofia. ~ing n kifuniko (cha mashine n.k.).

cowpea n kunde.

cowrie; cowry n kauri.

coxa n (anat) nyonga. ~l adj.

coxcomb n fidhuli; mfuauji, mtanashati. coxswain n sarahangi.

coy adj -enye haya,-enye soni, -enye

kudai kuona haya. ~ly adv. ~ness n.

coz n (arch) (sl) binamu.

cozen vt danganya, laghai, ghilibu, nyenga. ~ somebody into doing something danganya mtu afanye jambo. ~ something out of chukua kitu kwa hila. ~age n udanganyifu.

cozy n see cosy.

crab1 n 1 kaa. (fig) catch a ~ piga kasia vibaya. ~ wise adj upogoupogo

crab2 n (also ~-apple). tofaa pori.

crab3 vi (colloq) lalamika; nung'unika; kosoa, laumu. ~bed adj 1 -epesi kughadhabika. 2 (of hand writing) -siosomeka kwa urahisi. 3 (of writings/authors) -sioeleweka kwa urahisi.

crack1 vt,vi 1 tia ufa, fanya upenyu.

the ~ of dawn (colloq) wakati wa mapambazuko. 2 alisha; alika, fanya mwaliko; (of voice) wa kali; kwaruza. 3 banja; kwaruza. 4 (chem) safisha; yeyusha mafuta mazito. 5 (colloq and sl. uses). ~ down on chukulia hatua kali (za kinidhamu). ~ up (to be something) sifu mno, kuza. ~ up kosa nguvu (kwa uzee); pata kichaa; (of a vehicle) haribu; haribika, vunjika. ~ a bottle fungua chupa na nywa kilichomo. ~ a joke toa

mchapo, piga porojo.

crack2 n 1 ufa, mwatuko. 2 kishindo, mwaliko. the ~ of doom siku ya kiyama. 3 kipigo cha ghafula. give somebody a ~ on the head piga kichwani. 4 mzaha, dhihaka, jibu la kuchekesha. 5 (sl) stadi, mwenye akili, bora, bingwa. 6 (sl) majaribio. have a ~ at something jaribu kitu. 7 ~-brained adj -enye kichaa/ wazimu; pumbavu. ~ed adj -enye wazimu. ~er n 1 biskuti/mkate mkavu. 2 fataki ya kuchezea (ialikayo ikipasuka). 3 kibanguzi: chombo cha kubangulia (mathalani korosho, nyonyo n.k.). ~-jack n 1 (sl) mtu stadi, bora kabisa. 2 kitu bora kabisa. ~ers adj (GB sl) -enye wazimu.

crackle vi lia, data, chakarika; alikaalika (kama fito zikipasuka au kuchomwa moto). n mwaliko. crackling n 1 (see crackle). 2 ngozi ya nguruwe (iliyookwa).

crackpot n mtu mwenye mawazo ya

ajabu; pumbavu. ~ ideas n mawazo ya ajabu.

cracksman n mwizi (wa kuvunja nyumba).

cradle n 1 susu, kitanda kidogo cha mtoto; mlezi. 2 (fig) chanzo, chimbuko Lamu is the cradle of Swahili poetry Lamu ni chanzo cha ushairi wa Kiswahili. 3 (naut) kiunzitegemeo. 4 farasisimu. vt 1 laza, weka (katika kitanda n.k.). 2 (hold) lea; shika ~ the telephone receiver rudisha simu.

craft n 1 ufundi, ustadi. 2 hila; werevu, ujanja; udanganyifu. 3 (handicraft) kazi ya mikono. arts and ~s n sanaa na kazi za mkono. 4 chombo, mashua, jahazi, meli; muundo. ~ly adv. ~iness n. ~y adj janja. ~sman n fundistadi. ~smanship n ufundistadi.

crag n jabali, mwamba uliochongoka. ~giness n. ~gy adj. ~sman n fundi wa kupanda majabali.

cram vt,vi 1 jaza kabisa, shindilia, songa, sokomeza. 2 bukua. to ~

crash

(up) a subject kariri, hifadhi, andaa kwa mtihani (kwa kufundisha harakaharaka). ~mer n mbukuzi. ~full adj pomoni.

cramp n 1 (also ~ iron) gango, jiriwa. 2 mkakamao (wa ghafla hasa kutokana na baridi au kazi). vt 1 bananisha, weka katika nafasi ndogo; viza. 2 sababisha mkakamao misuli. 3 tia gangoni. ~ed adj 1 -enye nafasi ndogo. 2 -liyobanwa.

crampon n upanga njumu (unaowekwa

kwenye viatu ili kupanda milima/ kutembelea kwenye barafu).

crane n 1 korongo. 2 winchi. vt,vi nyosha (shingo).

cranial adj (anat) -a fuu la kichwa. craniology n kraniolojia: elimu ya fuu la kichwa. cranimerty n upimaji wa ukubwa wa fuu la kichwa. cranium n fuu la kichwa.

crank1 n kombo. ~shaft n fito kombo. vt 1 komboa. 2 hendeli. ~ up anzisha kazi ya mashine kwa kuzungusha mpini wake.

crank2 n mtu mwenye mawazo ya ajabu na kuyashikilia sana a fresh air ~ mtu apendaye kuwa na madirisha wazi hata kama kuna baridi kiasi gani. ~y adj (of people) -enye mambo ya ajabu; -enye wazimu; (of machines) -sio imara; (naut) -enye uwezekano wa kupinduka.

cranny n ufa mdogo, mwanya. crannied adj -enye nyufa nyingi.

crape n kitambaa cheusi chenye

mikunjo (kilichotumiwa zamani kushonea nguo ya mfiwa). vt funika, visha kitambaa hicho.

crap vt nya. n 1 mavi. have a ~ nya. 2 (sl) upuuzi.

craps n mchezo wa kamari unaochezwa kwa dadu. shoot ~ cheza mchezo huu.

crash1 n 1 kishindo (cha kuanguka au mpasuko). 2 mgongano. ~ barrier n kizuizi cha hatari. ~-dive n uzamaji ghafla wa nyambizi kuepa shambulio. vi 1 tua/zama kwa haraka. 2 anguka/vunjika vipande

crash

vipande kwa kishindo. 3 gonga; gongana. 4 pata kwa nguvu. gate ~ ingia kwa nguvu. ~-landing n (of

aircraft) kutua/anguka (kwa nguvu na kwa kishindo). ~ helmet n kofia ya kinga. ~ pad n (sl) mahali pa kulala wakati wa dharura. ~-programme n mpango wa dharura. 5 (of company) filisika. ~ing adv (sl) sana, kabisa. a ~ing fool n mpumbavu kabisa.

crash2 n kitambaa cha kitani.

crass adj (of such qualities as

ignorance, stupidity etc) sana, kabisa. ~ ignorance/stupidity n kipeo cha ujinga/upumbavu. ~ behaviour n vitendo vya kijinga. ~ness n.

crate n 1 sanduku/kasha la kuchukulia bidhaa. 2 (of fish etc) tenga. 3 (of beer) kreti. 4 (sl) mkweche, ndege au gari la zamani lililochakaa. vt funga ndani ya kasha n.k.

crater n 1 kasoko: shimo la katikati ya mlima/zaha/volkano. 2 shimo (baada ya mpasuko).

cravat n skafu.

crave vt,vi 1 ~ (for) sihi, omba. 2 tamani sana, taka sana, onea shauku/uchu; hitaji. craving n.

craven n mwoga adj -oga.

craw n tumbo la kuku.

crawfish n see crayfish.

crawl vi 1 tambaa; jikokota. ~ to somebody jipendekeza. 2 enda polepole. 3 jaa viumbe watambaao ~ with vermin etc. jaa wadudu n.k. 4 (of skin) sisimka. n 1 kutambaa, mtambao. 2 kuogelea kipaka. ~y adj. ~y feeling n msisimko. ~er n 1 mtambaazi. 2 (of baby) ovaroli ya kutambalia. 3 (GB sl.) mtu mwenye kujidhalilisha.

crayfish (also crawfish) n kamba wa maji baridi.

crayon n 1 chaki/penseli laini ya rangi. 2 picha/mchoro wa chaki/penseli ya rangi au makaa. vt chora kwa chaki/ makaa.

craze vt,vi 1 tia kichaa; tia wasiwasi, rusha akili. 2 pata wazimu. n 1 wazimu, kichaa. 2 mtindo

(unaopendwa sana na kudumu kwa muda mfupi).

crazy adj ~ (about) 1 -enye

kupenda/kutamani sana. 2 jinga; -enye wazimu (kichaa, mafuu). go ~ pata wazimu. drive somebody ~ tia wazimu. 3 -liochangamka, -enye kupenda sana kuliko kiasi he is ~ about the cinema mshabiki wa sinema. 4 (of buildings etc.) -sio salama, karibia kuvunjika au kuanguka; (of a ship) -lioharibika, isiyofaa kwa safari. ~ bone n see funny bone. craziness n. crazily adv.

creak vi 1 toa sauti ya mkwaruzo, kereza. n mkwaruzo, mkerezo. ~y adj. ~ily adv.

cream n 1 malai. 2 sehemu iliyo bora ya kitu au jambo lolote the ~ of the students wanafunzi bora. 3 dawa ya viatu (ifananayo na malai). 4 (chem) ~of tartar hamira, soda. vt engua malai, fanya kama malai. ~y adj -enye rangi ya malai. ~er n 1 mashine ya kutenga malai. 2 mwiko au chombo cha kukusanyia malai. ~ery n 1 duka la kuuza siagi, maziwa, jibini. 2 kiwanda cha kutengenezea siagi.

crease n 1 (on cloth) mkunjo, mfinyo, upanga. 2 (cricket) mstari katika kiwanja cha kriketi. vt,vi 1 kunja. 2 chekesha sana, vunja mbavu.

create vt 1 umba, huluku. 2 sababisha, onyesha. 3 (invent) buni, vumbua, tunga, anzisha. creation n 1 uumbaji, kuhuluku. 2 vitu vyote vilivyoumbwa. 3 kazi za sanaa the women were wearing the newest creations of the Paris dress designers wanawake walikuwa wakivaa mitindo mipya kabisa ya washonaji wa Paris. creative adj -a kubuni; bunifu. creativity n kipaji cha kubuni/kutunga. creator n muumba, mwumbaji; (rel) Mwenyezi Mungu.

creature n 1 kiumbe dumb ~s wanyama poor ~ maskini! lovely ~ mrembo/mtu mwenye sura

creche

nzuri. 2 kibaraka, kikaragosi.

creche n (GB) kituo cha kulelea

watoto wachanga.

credence n 1 imani. give ~ to amini, sadiki. letter of ~ hati ya utambulisho. credentials n hati ya utambulisho, sifa.

credible adj -a kusadikika, -a kustahili kusadikika, -a kuaminika. credibility n.

credit n 1 muamana. 2 mkopo, karadha. buy/sell on ~ nunua/ uza kwa mkopo. ~ account n (US charge account). ~ card n kadi ya mkopo. ~ note n hati ya kudai. letter of ~ n hati ya muamana. ~ squeeze n sera ya kubana utoaji mikopo. ~ balance n baki ya upande wa malipo. 3 (book-keeping) mpe: maingizo ya fedha zilizotolewa. 4 sifa njema, heshima. give ~ (to) sifia, tambua. do/reflect ~ ongezea sifa. 5 imani the rumour is gaining ~ uvumi unazidi kuaminika she has five books to her ~ ameandika vitabu vitano. vt 1 amini. 2 kopesha. 3 fanya maingizo ya. ~able adj. ~or n mwia. ably adv.

credo n see creed

credulity n 1 wepesi wa kuamini

(kusadiki) bila ushuhuda. 2 ujinga.

credulous adj 1 -epesi kuamini (kusadiki) bila ushuhuda. 2 -jinga.

creed/credo n imani; kanuni za imani.

creek n 1 (GB) hori. 2 kijito. be up the ~ wa taabuni.

creel n tumbi.

creep vi 1 tambaa. 2 (of age, time) enda polepole, fikia/ingia polepole. 3 nyata, nyapa. ~ up to nyatia, nyemelea. n the ~s (sl) mtu anayejipendekeza; misisimko, hali ya damu kusisimka. it gave me the ~s ilinisisimsha damu kwa hofu. ~er n 1 kiumbe mwenye kutambaa, mtambaa. 2 (kwa nafaka) mtambo wa uchukuzi. ~y adj -enye msisimiko.

cremate vt unguza/choma maiti (badala ya kuzika). cremation n. crematorium/crematory n tanuu ya

kuchomea maiti.

creole n 1 chotara. 2 (ling) krioli: lugha ya machotara/ vizalia.

creosote n (chem) kresoti: aina ya mafuta mazito yatokanayo na lami (hutumika kuhifadhia mbao). vt paka kresoti.

crepitate vt,vi alika; alisha. crepitation n.

crepuscular adj tusitusi; (zool) -a kuonekana au kusikika wakati wa utusitusi.

crescent n 1 hilali, mwezi mwandamo, mwezi kongo. 2 safu ya nyumba yenye umbo la hilali. the ~ n (fig) Uislamu adj -a hilali, -enye umbo la mwezi mwandamo.

crest n 1 (tuft) shungi, kishungi; kilemba, kishada. 2 (top) kilele, ncha ya juu. on the ~ of a wave wakati wa nyota ya jaha. 3 upanga wa jongoo, undu. 4 nembo ya kinasaba. 5 kufika kileleni. ~ed adj. ~fallen adj -liovunjika moyo, -a huzuni, -sio na raha.

cretaceous adj (geol) -a chaki .~ age n kipindi ambapo miamba ya chaki iliumbika.

cretin n 1 mdumavu wa akili. 2 (sl)

mpumbavu. ~ism n. ~ous adj -liodumaa.

crevasse n mwanya, ufa mkubwa (hasa katika mto wa barafu).

crevice n ufa mdogo, mwanya (kwenye

mwamba, ukuta n.k.).

crew1 n (collective noun) 1

wafanyakazi melini, katika ndege au gari moshi. ground ~ n mafundi ndege (katika kiwanja cha ndege). 2 kundi la watu wafanyao kazi pamoja. ~-cut n mtindo wa kukata nywele na kuwa fupi sana. ~ list n koli. vi I'll ~ for you next week nitakuwa baharia wako wiki kesho.

crew2 pt of crow2.

crib1 n 1 hori (ya kuwekea chakula cha mfugo). 2 mlezi. 3 (US) tangi, boksi, kasha (la kuhifadhi mahindi n.k.).

crib2 n kazi iliyonakiliwa kwa kuibiwa,

crick

maandishi yaliyoghushiwa, maandishi yaliyokaririwa. vt,vi (of students) ibia (kazi ya mwingine kwa kunakili), ghushi, nakili.

crick n kishingo.

cricket1 n (bio) nyenje, chenene.

cricket2 n kriketi. (colloq) not ~ si desturi, si haki. ~er n mcheza kriketi.

crier n 1 mnadi. town ~ n mpiga mbiu. 2 (of a young child) mlia ovyoovyo.

crikey (int) (colloq) loo!, lahaula.

crime n 1 jinai, uhalifu, kosa. ~fiction n riwaya za jinai. commit a ~ tenda kosa la jinai. 2 manza, kosa la kijinga. 3 (in the army) uvunjaji kanuni; kuvunja sheria. 4 aibu, jambo la kutia huruma, dhambi. ~ sheet n rekodi ya makosa ya askari. criminal adj -a jinai, halifu. criminal court n mahakama ya jinai. criminal record n historia/kumbukumbu ya jinai. criminal procedure n taratibu za kesi ya jinai. of a criminal nature -a jinai, -a kijinai institute criminal proceadings against somebody shtaki mtu Criminal Investigation Department Idara ya Upelelezi wa Jinai n mhalifu, mvunja sheria. habitual criminal n mhalifu sugu. criminally adv. criminology n elimu jinai.

crimp vt sokota, tia mawimbi (agh. katika nywele).

crimplene n krimplini.

crimson n nyekundu iliyoiva, damu ya mzee adj -ekundu iliyoiva. turn ~ geuka rangi kuwa nyekundu iliyoiva. vt,vi -wa nyekundu iliyoiva.

cringe vi 1 ~ (at) nywea, jikunyata. 2 ~(to/before somebody) nyenyekea, jifanya kama mtumwa. 3 ~ (at) udhika. n kujikunyata; unyenyekevu.

crinkle vt,vi vungavunga; kunjakunja; nyonganyonga. n mkunjo. crinkly adj (of materials) -enye mkunjo; (of hair) -enye kusokotana.

crinoline n 1 nguo nzito na ngumu. 2 (arch) skuta (kitanua sketi).

cripes int (expressing astonishment etc) mshangao, mstuko: lahaula! Mungu Wangu! Yesu! Mtumee!

cripple n kiwete. vt 1 fanya mtu

kiwete. 2 haribu, dhoofisha kabisa, hasiri, vunja adj -a kiwete, -a kwenda chopi; ~dom; ~hood n.

crisis n 1 kipeo/upeo wa mgogoro;

kilele cha hatari/ugonjwa n.k. 2 hali ya hatari, hali ya wasiwasi mkubwa reach a ~ fikia upeo wa tatizo.

crisp n kaukau adj 1 (esp. of food) ngumu, kavu, -a kuvunjika kwa urahisi. 2 (of hair) -a pilipili,-a kipilipili. 3 (of weather) -a baridi. 4 (of style, manners ) -epesi, thabiti, bila shaka. 5 (firm) -gumu kidogo, -bichi. vt,vi 1 sokota; sokoteka. 2 kausha; wa kavu. ~ly adv. ~ness n. ~y adj.

criss-cross n mistari mkingamo adj (of lines) -liokingama. vt,vi kingama adv kinyume.

criterion n kigezo.

critic n 1 mhakiki. 2 (fault finder) mkosoaji. ~al adj 1 (of a crisis) -a kipeo (cha matatizo n.k.). 2 (of the work of art) -a kihakiki. ~al thinking n umakinifu. 3 (of fault finding) -a kukosoa. ~ally adv she is ~ally ill yu mgonjwa taabani.

criticism n 1 kazi ya mhakiki, ufundi wa kutoa maoni kuhusu sanaa, fasihi n.k. 2 uhakiki. 3 ukosoaji. criticize vt vi criticize (for) 1 hakiki. 2 kosoa. critique n tahakiki, uhakiki.

croak vi 1 ~ (out) koroma, lia kama chura au kunguru), kwaruza his voice was ~ing sauti yake ilikuwa ikikwaruza. 2 (grumble) nung'unika, guna. 3 bashiri mabaya. 4 (sl) -fa. n 1 mlio kama wa chura/ kunguru. 2 mkoromo, mkwaruzo.

croceate adj -a zafarani.

crochet n kroshia. ~-hook; ~-needle n kulabu. vt,vi fuma kroshia.

crock1 n mtungi; chungu/gae. ~ery n

vyombo vya udongo (vikombe n.k.).

crock2 n 1 (colloq) farasi mkongwe. 2 (of motorcar) mkweche. 3 (colloq)

crocodile

mkongwe (dhaifu, asiyejiweza). vt, vi 1 ~ up dhoofisha; dhoofika, kongoka. 2 zeeka; zeesha.

crocodile n 1 mamba, ngwena. (idiom)~ tears n majonzi ya uongo. 2 (GB- colloq) mlolongo wa watu katika safu mbili.

croft n (GB) shamba dogo (agh. lililozungushiwa uzio). ~er n mpangaji wa mwenye shamba dogo.

cromlech n kaburi la kale.

crone n ajuza, bi kizee.

crony n mwandani, shoga.

crook n 1 bakora. 2 mapindi (ya mto,njia). ~-back(ed) n kibiongo. 3 (colloq) mkora, jambazi; mdanganyifu. 4 on the ~ (sl) kwa ukora. vt vi pinda, potoa; pindika, potoka. ~ed adj -sionyooka, -enye matege, -a upogoupogo; halifu, -sio aminifu.~edly adv. ~edness n.

croon vt,vi imba (bila kutamka maneno au kwa sauti ndogo). ~er n mwimbaji atumiaye sauti ndogo.

crop1 n 1 zao. cash ~ n zao la biashara. food ~s n mazao ya chakula. forage ~s n mazao ya malisho. ~ rotation n mbadilisho wa mimea. 2 (pl) mavuno. 3 kundi la watu au vitu vinavyoonekana au kutengenezwa pamoja. vt,vi 1 nyoa, kata fupi (nywele n.k.). 2 (of animals) -la machipukizi/vilele vya mimea. 3 ~ (with) otesha, panda mazao. 4 zaa the peas ~ped well njegere zimezaa vizuri. 5 ~ up onekana kwa ghafula, tokea, onekana, zuka. ~ out tokeza juu ya ardhi. ~-eared adj -enye masikio yaliyofupishwa, yaliyokatika kidogo.

crop2 n 1 gole. 2 mpini wa mjeledi/ mchapo. 3 mkato mfupi wa nywele. ~per n 1 mmea utoao mazao. a good/bad/heavy ~per n mmea unaotoa mavuno mazuri/mabaya/ mengi. 2 mtu au chombo cha kuchengea. 3 come a ~per (colloq) anguka sana, shindwa (k.m. katika mtihani).

croquet n (sports) krokei (mchezo wa

kupitisha tufe za mti kwenye duara za chuma kwa kuzipiga kwa nyundo. vi cheza tufe za miti.

croquette n kababu, chopsi.

crosier;crozier n (rel) fimbo ya kiaskofu.

cross1 n 1 msalaba pectoral ~ msalaba wa kifuani. 2 alama ya msalaba (k.m. x, +). make one's ~ tia dole. 3 (fig) jaribu/taabu, majonzi. bear one's ~ beba msalaba/mzigo wako. 4 mchoro/mstari unaokata herufi (k.m. katika herufi `t'); (bot, bio) uzazi mchanganyiko. 5 njia panda. 6 (dress making) mshazari, mshono kingamo 7 nishani ya ushujaa (e.g. Victoria~).

cross2 vt,vi 1 pitana; kingama, kingamana, kunja (mikono, miguu). ~ somebody's palm with silver patia hela (hasa mtabiri). ~ words with somebody pigana/bishana na mtu. keep one's fingers ~ed (fig) tumaini (kuwa kila kitu kitakwenda sawa). ~ my heart! kweli! haki ya Mungu. 2 ~ (off/out/ through) kata kwa mistari. ~ a cheque funga cheki. ~ed cheque n cheki iliyofungwa. ~ one's t's and dot one's i's wa sahihi na mwangalifu sana. 3 (of river, road etc) ~ (from); ~ (to) vuka, enda ng'ambo ya pili. ~ somebody's path kutana na; (pass) pita; kata. ~ one's mind kumbuka, jiwa na wazo, ingia ghafula katika fikira. 4 zuia, kingama, pinga. 5 kutana njiani, pishana. ~ed line n kuingiliana kwa makosa katika simu. 6 (be athwart) kata, kingamiza. 7 ~ (with) zalisha kwa kuchanganya (mbegu n.k.). 8 (rel) ~ oneself fanya/onyesha alama ya msalaba. 9 ~ off/out futa.

cross3 adj 1 (colloq) -kali, -a hasira, -a chuki, -a kuchacha. as ~ as two sticks -enye kukasirika sana, -enye hamaki mbaya. be ~ fanya chuki. 2 -a kwenda upande, -a mshazari, kingamizi. 3 -a kukabili, -a kuelekea. 4 -a kukingama, -a

kupandana, -a kupinga njia; (of winds) mbisho, tanga mbili. ~ness n. ~-bones n (pl (of a sign) mifupa ya paja iliyopandana inayochorwa chini ya fuvu la kichwa kuashiria mauti au hatari. ~-breed n uzalishaji mtambuka. vt zalisha kwa mtambuka. ~-bred adj. ~-current n mikondo pishani; fig) maoni tofauti na (maoni) ya wengi. ~-fertilization n uchavushaji mtambuko. ~-fire n (mil) mashambulio ya risasi kutoka pande mbili; (fig) hali ya kuulizwa maswali na watu mbalimbali be caught in ~ fire jikuta katikati ya mambo/mzozo. ~-grained adj 1 (of wood) -enye nyuzi zinazopishana. 2 (fig) -kaidi, -a chuki, korofi. ~-index n see ~ reference. ~-legged adj -a kukaa kimarufaa. ~-over n 1 kipito cha reli. 2 koti lenye kufunga. 3 mbadilishano wa jeni kati ya kromosomu. ~-pollination n (bio) uchavushaji mtambuko. ~-purposes n (of persons) kuwa na malengo yanayopingana; hali ya kutoelewana, suitafahumu they were talking at ~ purposes kila mtu alikuwa akiongea vyake. be at ~ purposes -toelewana, pingana. ~ -reference n marejeo mtambuko (ili kupata maelezo zaidi). ~-roads n (pl) njia panda; (fig) (in life) kipindi cha kufanya maamuzi muhimu ya maisha. ~-stitch n mshono kingamo. ~-word n (also cross-word puzzle) chemsha bongo, fumbo la maneno (katika jedwali mraba).

crossbar n mwamba.

cross-beam n boriti ya kukingama, mtambaapanya.

cross-bench n (in U.K Parliament) benchi la wabunge huru wasiopigia kura chama chochote.

crossbow n uta, upinde.

cross-check vt vi thibitisha tena (kwa njia nyingine).

cross-country adj -a kukatambuga.

crosscut n mkato; njia ya mkato. vt kata toka upande huu mpaka upande

wa pili wa adj (of a saw) -enye meno maalum ya kukata nyuzi za mbao.

cross-examine vt (also cross-question) dodosa; dadisi, hoji, saili (ili kuthibitisha ushahidi uliotolewa). ~-examination n.

cross-eyed adj -enye (macho ya) makengeza.

cross-heading n (in a newspaper) kichwa kidogo cha habari kinachodokeza yaliyomo.

crossing n 1 kivuko. (of roads) zebra~ n kivuko cha miguu. 2 makutano ya barabara na reli, tambukareli. 3 safari ya meli did you have a good ~ ulikuwa na safari nzuri?

cross-patch n 1 (colloq) mtu mwenyehasira. 2 hasira, ghadhabu.

crossquestion vt see cross -examine.

cross-section n 1 picha ionyeshayo sehemu za ndani ya kitu. 2 (fig) kiwakilishi; kundiwakilishi, mfano halisi wa kitu au jambo ~ of the voters kundi wakilishi la wapiga kura.

cross-walk n kivuko cha barabara, kivuko milia.

cross-wise adv kwa kukingama.

crotch n 1 (of a tree) panda. 2 pachipachi (ya suruali, kaptura, miguu n.k.). 3 (of person) msamba.

crotchet n 1 mawazo ya ajabu na kijinga. 2 ulalamishi. 3 (music) robo noti. ~y adj lalamishi, -enye hasira.

crouch vi jikunyata; jikunja; chutama. n hali ya kujikunyata; kujikunja; kuchutama.

croup1 n kifaduro. ~y adj.

croup2 n (of certain animals) tako.

croupier n mhazini, mkusanyaji na

mlipaji pesa katika mchezo wa kamari.

crow1 n 1 (of a cock) kuwika. 2 (of a baby) kucheka. vi 1 wika. 2 cheka, lia kwa furaha. 3 ~ about/over jivunia. 4 cheka, shangilia.

crow2 n 1 kunguru. as the ~ flies kwa mwendo wa moja kwa moja. to eat ~ salimu amri kwa lazima;

dhilishwa, twezwa. have a ~ to pick (to pluck) (with somebody) kamia, -wa na jambo baya la kuzungumza na mtu. 2 see ~ bar. ~ 's-foot n kijikunjo kwenye pembe la jicho. ~'s -nest n kidungu juu ya mlingoti wa chombo.

crowbar n nondo.

crowd n 1 kundi, halaiki, umati, kaumu. 2 watu, umma follow the ~ fuata mkumbo/mkondo. 3 (colloq) genge. 4 lundo. vt,vi (colloq) songa, jaza sana; jaa, songamana. ~ round zunguka, songa. ~ on sail tweka matanga yote. ~ in penya/penyeza kwa wingi. ~ through gagamiza, penyeza kwa wingi. ~ out (of a group) toka, zuia your article was ~ed out makala yako haikupata nafasi/ilizuiliwa. ~ed adj -liojaa, -liosongamana.

crown n 1 taji la mfalme/malkia; uwezo/amri ya mfalme/utawala wa mfalme; mfalme. ~ colony n koloni la kifalme. ~ ed head n mfalme/ malkia. ~ lands n milki za kifalme. ~ prince n mwana wa mfalme atakayerithi ufalme. ~ witness n shahidi upande wa serikali. 2 utosi, sehemu ya juu ya kofia, kileleta; sehemu ya jino inayoonekana. 3 uzuri; ukamilifu, utimilifu. 4 taji la maua la kichwani kama dalili ya ushindi. 5 (arch) sarafu ya Kiingereza ya thamani ya shilingi tano. vt 1 visha taji, tawaza. 2 (reward) tuza. 3 kamilisha. 4 tukuza. 5 -wa matokeo ya; fanikisha success will ~ his efforts ushindi utakamilisha/ utapamba jitihada zake; atafanikiwa katika juhudi zake. that ~s it all hiyo inakamilisha yote. 6 -wa juu ya a hill ~ed with trees kilima chenye miti kileleni. 7 ziba jino. ~-wheel n (tech) gurudumu lenye meno.

crozier n see crosier.

crucial adj -a maana sana; (colloq) -a muhimu sana.

crucible n 1 kalibu; kikalibu. ~ steel

n chuma cha pua cha kalibu; chungu

cha kuyeyushia madini. 2 (colloq) majaribio makali. ~ of suffering majaribio ya matuo (maumivu n.k.).

crucify vt 1 sulubisha, sulubu. 2 (torment) tesa. crucifixion n. crucifix n (rel) msalaba (wenye sanamu ya Yesu Kristu).

crude adj 1 -bichi, -siosafishwa (k.m.kama sukari guru)/ghafi. ~oil n mafuta yasiyosafishwa. 2 (rude) -sio adilifu. 3 -sio stadi, -siokamilishwa vema au -liofanywa ovyoovyo. 4 (of statistics) -siorekebishwa, -siosahihishwa, -sioficha. ~ly adv. ~ness n. crudity n.

cruel adj katili, jahili, dhalimu. ~ly adv. ~ty n.

cruet n 1 ndiani (kichupa cha kuwekea viungo k.v. pilipili, chumvi n.k. mezani). 2 (rel) chombo kidogo chenye divai au maji. ~ stand n kiweko cha ndiani.

cruise vi 1 (of ships) vinjari, enda huko na huko, zunguka. 2 (of vehicle) enda kwa kadiri. 3 tafuta mpenzi barabarani. 4 linda doria. n safari za burudani/kutalii. ~r n 1 manowari ya kasi. 2 (of a police vehicle) gari la doria. cabin ~r n motaboti yenye nafasi ya kulala.

crumb n 1 chembe ya mkate. 2 the ~n (of a loaf) nyama ya mkate. pick up the ~ okota/lamba makombo. 3 (fig) kiasi kidogo. vt 1 funika kwa chembechembe za mkate. 2 fikicha. ~y adj.

crumble vt,vi 1 fikicha, vunja, meng'enya. 2 (fig) hopes that ~d to dust matarajio yaliyoshindikana kabisa. crumbly adj.

crummy adj (sl) chafu; hafifu, -a thamani ndogo.

crump n (army sl.) pigo kubwa, mlio wa kombora lipasukalo. vt (colloq) piga kombora.

crumpet n 1 (cookery) mkate laini wa hamira. 2 (US) sl kichwa. 3 (sl) (female) mtia ashiki.

crumple vt,vi 1 kunjakunja. 2 ~ (up) kunjakunja; vunjavunja; kunjamana.

crunch

crunch vi,vt 1 saga kwa meno, chakacha, tafuna kwa kelele/kishindo. 2 kanyaga/vunjavunja changarawe, theluji kwa miguu/gurudumu. n 1 kusaga kwa meno when it comes to the ~ (colloq) wakati wa kukata shauri ukifika..., mambo yakiiva.

crupper n 1 mtafara, kitanzi cha

mkiani cha tandiko la punda (farasi n.k.). 2 tako (la farasi).

crusade n 1 vita vya msalaba, vita vya dini (vya zamani), vita vitakatifu. 2 harakati au mapambano yoyote dhidi ya yale yanayoaminika kuwa maovu. vi ~ (for/against) shiriki katika vita takatifu kwa/dhidi ya. ~r n.

crush vt,vi 1 seta, ponda, vyoga, gandamiza; kunjika, pondeka. ~ ruthlessly ponda. 2 tiisha, vunja nguvu ya; (ruin) angamiza ~ one's way through penya, swaga. ~ out kamua. n 1 msongano (wa watu), ghasia. 2 mbano, msongo. 3 (colloq) have a ~ on somebody husudu mtu; tamani mtu. 4 (biol) kilingo. 5 sharubati/kinywaji cha matunda. ~ing -a ushindi/ushinde; -baya mno ~ing blow pigo angamizi.

crust n 1 gamba la mkate. 2 (on rice) matandu. 3 (on teeth) ukoga. 4 (on water) ukoga, gaga. 5 umbo/uso wa dunia. 6 (of salt) chunyu. 7 (biol) ganda, kigaga. vt,vi gandamanisha; gandamana. ~y adj 1 -enye gamba. 2 kali, -enye ghadhabu.

crustacean n krasteshia: wanyama

wenye magamba kama kaa, kamba, uduvi.

crutch n 1 gongo (la kutembelea mgonjwa au kilema). 2 (support) tegemeo; (fig) msaada wa hali. 3 pachipachi ya suruali, kaptura na miguu; kiraka (see crotch).

crux n 1 sehemu ya jambo ambayo ni ngumu kutatuliwa. 2 kiini (cha jambo) ~ of the matter kiini cha jambo.

cry vi,vt 1 toa sauti, guta, paza sauti; piga yowe. 2 lalama, lalamika. ~ for the moon omba miujiza. 3 lia,

toa machozi. ~ one's eyes/heart out lia sana. ~ oneself to sleep lia mpaka kupatwa usingizi. give a child something to ~ for/about adhibu mtoto kwa kulia pasi sababu. 4 tangaza. 5 ~ at lilia, pigia kelele. ~ down dharau, shusha heshima, punguza thamani. ~ off jitoa (katika jambo uliloahidi au kupatana juu yake). n 1 kilio, mlio, ukelele, ukemi. give a ~ piga kelele. in full ~ (of dogs) bweka wote pamoja; (of peoples) (fig) shambulia (mtu) much ~ and little wool (prov) mwenye kelele hana neno. within ~ (of) hapa hapa, kando. 2 (of sorrow) yowe, unyende. 3 (of happiness) kigelegele, hoihoi. 4 (of complaint) lalamo. 5 kugutia. (fig) a far ~ mbali sana; tofauti sana. 6 kilio have a good ~ lia sana ili kupata tulizo have one ~ out acha alie mpaka atulie. ~ing n, adj kubwa sana. ~ing need n haja kubwa sana. ~ing-baby n mlialia.

crypt n chumba chini ya ardhi (hasa chini ya kanisa). ~ic adj -a siri, -a fumbo, -a kufichwa. ~ically adv.

crypto - adj -a siri, -a mficho. a ~ fascist n mtetezi wa siri wa mafashisti. ~gram n maandiko ya mficho (ya siri). ~grapher n mwandishi/mfichua msimbo.

crystal n 1 fuwele. 2 chembechembe

(jiwe kama kioo). as clear as ~ angavu kabisa, dhahiri kabisa adj -angavu, -a kung'aa. ~line adj -liotengenezwa kwa fuwele; kama fuwele, angavu mno. ~lography n elimu ya fuwele. ~-gazing n utabiri wa kutumia tufe la kioo. ~lize vt, vi 1 ganda/gandisha; fanya, fanyika kitu kama kioo. 2 dhihirika/ dhihirisha (kwa mawazo n.k.). 3 gandisha kwa shata la sukari. ~lization n. ~lized fruits n matunda yaliyogandishwa kwa sukari, kashata za matunda.

cub n 1 mtoto wa wanyama fulani wamwitu (kama simba, chui, mbweha).

cube

2 (of a person) limbukeni; safihi. 3 chipukizi, kijana anayejifunza ufundi fulani, mkurufunzi ~ (scout) skauti chipukizi ~ reporter mwandishi wa habari chipukizi. vt,vi 1 (of animals) zaa. 2 saka watoto hasa wa dubu. ~bing n; ~by hole n 1 kijichumba. 2 mahali padogo.

cube n 1 mchemraba, mchemrabasawa. ~ root kipeo cha tatu. 2 (of sugar n.k.) kidonge cha sukari vt 1 (math) peua mara tatu. 2 (cookery) kata vipande vidogo vidogo vya kimraba. cubic adj -a mchemraba. cubic unit n kizio cha ukubwa. cubism n uchoraji wa kutumia maumbo ya jometri. cubist n. cubital adj. cuboid adj kimchemraba.

cubicle n 1 kijichumba agh hutengwa kwa bango. 2 behewa dogo.

cubit n dhiraa.

cuckold n (arch) mume wa mke

aliyezini. vt zini.

cuckoo n kukuu adj (sl) mjinga, kichaa.

cucumber n tango, tangopepeta.

cud n cheua. chew the ~ cheua, tafuna- tafuna (kama ng'ombe, mbuzi); (fig) fikirifikiri, dhukuru.

cuddle vt,vi 1 kumbatia. 2 ~ up (to/together) kumbatiana, lala karibu/unono, jongele(an)a, pakana. n kukumbatiana; kupakatana. ~some; cuddly zuri kwa kukumbatia.

cudgel n kigongo, kirungu. take up the ~s for pigania, tetea vt 1 piga kwa gongo. 2 (fig) ~ one's brains fikiri sana, tafuta sana shauri la kufaa, jaribu kukumbuka.

cue1 n 1 ishara (k.m. maneno ya mwisho ya mwigizaji katika tamthiliya) inayoonyesha jambo la kufanywa na mwenzake. 2 kidokezi. take one's ~ from somebody fuata nyayo. ~ in (fig) toa habari kwa, fuata msimamo wa mwingine.

cue2 n fimbo ya kuchezea biliadi.

cuff1 kofi. vt piga kofi.

cuff2 n 1 sijafu (la mkono au mguu).

culture

off the ~ papohapo, bila kujiandaa, kiurafiki an off the ~ speech hotuba isiyoandaliwa play it off the ~ faragua (kufuatana na hali ilivyo). 2 (pl) ~s n pingu. ~-links n vipingu vya sijafu.

cuirass n deraya (vazi la kiaskari

kama kizibau cha ngozi ngumu au chuma). ~ier n (mil) mpanda farasi aliyevaa deraya.

cuisine n upishi, mapishi.

cul-de-sac n see blind alley.

culex n kuleksi: aina ya mbu.

culinary adj -a jikoni, -a upishi, -enye kupikika.

cull vt 1 chuma; chagua; kusanya;tenga. 2 ua (wasiohitajika kudhibiti ustawi). ~ elephants punguza/ua tembo. n kitu kilichotengwa, takataka.

cullender n see colander.

cullet n kipande cha kioo.

culminate vt ~ in (of hopes, careers etc) fikia kilele/upeoishia. culminant adj. culmination n.

culottes n (pl) sketi; kaptura.

culpable adj -a kulaumika; -a kustahili adhabu. ~ negligence n uzembe unaostahili adhabu. culpably adj. culpability n.

culprit n mkosaji, mhalifu, mkosefu.

cult n 1 (also religion) madhehebu.

2 upendo wa mtu (kwa kitu, kazi, mchezo n.k.). 3 kikundi cha watu wanaopenda sana vitu vya kisasa, mitindo ya kisasa n.k.

cultivate vt 1 lima; palilia. 2 (improve) endeleza, kuza (mtu, tabia); -wa makini, lea kwa wema. 3 jengaurafiki. cultivable adj. cultivation n. cultivator n mkulima; kaltiveta. ~d adj 1 -enye elimu na adabu njema. 2 -liolimwa.

culture n 1 utamaduni. 2 kukua na kukomaa (kwa akili na mwili wa binadamu kutokana na mafunzo au uzoefu wa kutenda kazi). 3 hali ya maendeleo ya maarifa, elimu ya watu. 4 ulimaji, utunzaji (wa nyuki n.k.). 5 ustaarabu: fani zote, imani,

culvert

mila na desturi, asasi za kijamii zitambulishazo jamii/mbari. 6 (bio) ukuzaji wa bakteria (kwa ajili ya matibabu au uchunguzi wa kisayansi). ~d adj (of persons) 1 -lioelimika, -liostaarabika. 2 (of artifact) -liosanifiwa/tengenezwa na binadamu. cultural adj.

culvert n kalvati, mtaro (chini ya ardhi) wa kupitishia maji au kebo za umeme.

cumber vt ~ (with) zuia; pinga; sumbua, elemea. n kipingamizi, kizuizi. ~some adj -zito, -a kulemea; -a udhia, -sumbufu.

cumbrous adj see cumbersome.

cummerbund n mahazamu, masombo. cumulative adj -a kukusanywa kidogo kidogo, -a kulimbikiza. ~ records n kumbukumbu za kulimbikiza/ limbikizi.

cumulus n kumulasi: wingu zito kiasi.

cuneiform adj -a kikabari.

cunning adj 1 -erevu, -janja; -a hila,

baramaki, karamshi. 2 (arch) hodari, -stadi. 3 (US) -a kuvutia. n 1 werevu, ujanja; hila. 2 (old use) ustadi, ufundi.

cunt n 1 kuma. 2 kujamiiana. 3 (vulg) (of woman) malaya. 4 (of person) korofindo.

cup n 1 kikombe. he is in his ~s amelewa. 2 (fig) kufikwa, kitu kinachomjia mtu his ~ was full uchungu, furaha yake ilikamilika between ~ and lip kitambo kidogo kabla ya kupata. the parting ~ n kinywaji cha mwisho kabla ya kuagana. one's ~ of tea kitu kimpendezacho. 3 (of sports) kombe. World ~ n Kombe la Dunia vt fanya umbo la kikombe; umika, piga chuku. ~ping n mwumiko, umiko ~ glass chuku, ndumiko. cup final (football) fainali ya mashindano (ya kugombea kikombe). ~ bearer n mwandazi divai katika karamu kitaluni au makao ya mfalme.

cupboard n kabati. ~ love n mapenzi

njaa, mapenzi tumbo.

cure

cupel n kupeli: chombo cha kuchuja, kujaribu dhahabu, fedha n.k..

Cupid n 1 Mungu wa mapenzi (wa Kirumi). 2 picha/sanamu (ya mvulana mzuri) ya alama ya mapenzi.

cupidity n uchu, tamaa (hasa ya fedha au mali).

cupola n 1 kuba. 2 ~ furnace tanuri la kuba.

cuppa n (sl) (GB) kikombe cha chai.

cupping n see cup.

cupric adj enye kupri/shaba.

cur n 1 mbwa (koko), kijibwa. 2 mtu mwoga; safihi. ~rish adj.

curate n padre/kasisi msaidizi. curacy n ofisi/kazi ya padre msaidizi.

curator n afisa mwangalizi (wa jumba la makumbusho/sanaa n.k.).

curb n 1 lijamu. 2 (fig) kizuio, udhibiti. 3 see kerb. 4 sugu lililoota katika kifundo cha mguu (wa nyuma) wa farasi. vt 1 dhibiti, zuia (hasira, matumizi ya fedha n.k.). 2 tawala (farasi).

curd n magandi, maziwa ya mgando, mtindi. vt,vi 1 ~(le) gandisha; ganda; gandamana. 2 (fig) ogofya, ogopesha, tisha his blood ~ led mwili ulimsisimka, alijaa hofu.

cure n dawa this disease has no ~ maradhi haya hayana dawa. 2 matibabu his ~ took a year matibabu yake yalichukua mwaka no ~ for the disease maradhi haya hayana dawa. 3 kupona I can't guarantee you a ~ sikuhakikishii kuwa utapona. 4 (rel) nafasi/kazi ya upadre; kasisi. vt,vi 1 ponya, ponyesha. ~-all n kiponya madhila/maradhi yote. 2 hifadhi (nyama, samaki n.k. kwa kutia chumvi au dawa asioze), kausha; koleza. 3 ondolea mbali; tatua tatizo, ondoa. ~ poverty ondoa ufukara. curative adj -a kuponya, -a kuweza kuponya (ugonjwa). n dawa what can't be ~d must be endured lililovia limevia. curable adj -a kuponyeka, -a kuweza kuponyeshwa.

curette

curability n.

curette n chombo cha madaktari cha kuchunia au kukwangulia.

curfew n 1 amri ya kutotembea

wakati fulani (agh usiku fulani). 2 ishara ya kuanza kutotembea. 3 kipindi cha kutotembea.

curio n kazi ya sanaa (yenye thamani kutokana na upekee wake). ~shop n duka la sanaa.

curious adj 1 chunguzi, -enye kutaka kujua. 2 (inquisitive) dadisi it was a ~ situation ilikuwa hali ya ajabu. 3 -a tunu, -a kipekee. ~ly adv. curiosity n 1 (inquisitiveness) upekuzi, udadisi, uchunguzi, utafiti. 2 kitu cha pekee, tunu, udaku as a matter of curiosity ningependa kujua.

curl vt,vi 1 (of hair) kunja, pinda,

pota, tia mawimbi. 2 jipindapinda. 3 jinyonganyonga. 4 ~ up anguka, kunjamana. ~er n kitia mawimbi. ~ing irons/tongs n (arch) vifaa/ vikoleo vya kunyoshea/kutilia mawimbi nywele. ~y adj a mawimbi. ~y kit n seti ya kutengeneza nywele.

curmudgeon n (colloq) mtu mwenye hamaki; bahili.

currant n 1 zabibu kavu 2. tunda dogo kama zabibu la rangi ya zambarau.

current1 adj 1 -a desturi, -a kawaida. 2 -liyopo, -a wakati uliopo, -a sasa, -a kukubaliwa na wengi ~ events/ affairs mambo leo ~ periodical jarida la sasa. 3 (of money) zinazotumika ~ assets raslimali ~ account akaunti ya hundi. ~ly adv. currency n 1 desturi, matumizi, kuenea give currency to a rumour eneza uvumi. 2 sarafu, fedha currency note noti foreign currency fedha za kigeni.

current2 n 1 mkondo (wa maji, hewa, gesi, umeme n.k.). 2 mfulizo wa mambo, mfuatano (wa mambo).

curriculum n mtalaa. ~ developer n mkuza mitalaa. ~ vitae n maelezo binafsi ya mtu (kuhusu elimu, ujuzi n.k.).

cushitic

curry1 vt 1 chana nywele za farasi n.k. 2 tengeneza ngozi iwe laini, isioze. ~ favour jipendekeza.

curry2 n mchuzi wa viungo. ~-powder n bizari. vt unga (mchuzi) na viungo.

curse n 1 laana, apizo, hizaya. be under a ~ laaniwa, teseka kwa laana. 2 sababu ya hasara, nuksi gambling is often a ~ kucheza kamari ni nuksi. 3 tusi. 4 (colloq) the ~wakati wa hedhi. 5 not give/care a (tinker's) ~ -tojali kabisa. vt,vi 1 laani, apiza. 2 ~d with teseka na, sumbuliwa na. 3 tukana sana, tolea matusi. ~d adj (also curst) -laanifu, -liolaniwa; -a kuchukiwa, -a kuchukiza mno. ~ly adv.

cursive adj (of handwriting)

ulioviringwa na kuunganishwa.

cursory adj -a haraka, -a juu juu tu

give a ~ glance to tupia macho. cursor n kishale.

curt adj (of speech) -a maneno ya mkato, -a kukatiza; -sio adabu.

curtail vt katiza, fupisha, punguza,

kata. ~ment n.

curtain n pazia. draw a ~ over something (fig) -tozungumzia tena jambo hilo. ~-call n kuita mchezaji mbele ya pazia apigiwe makofi. ~ raiser n mchezo mfupi kabla mchezo halisi. ~s n (sl) mwisho it'll be ~s for you itakuwa mwisho wako. vt funika kwa pazia. ~ off kata/gawanya (k.m. chumba) kwa pazia.

curts(e)y n heshima (itolewayo kwa

kukunja goti). vt toa heshima (kwa kukunja goti).

curve n 1 kizingo, tao, pindi. 2 (math) mchirizo. vt, vi kunja, pinda, peta ~ to the right pinda kulia. curvature n mpindo, mpindiko.

cushion n 1 mto. 2 takia. vt 1 tia mto chini. 2 linda (kutokana na dhiki) mabadiliko mabaya. 3 punguza nguvu.

cushitic n Kikushi: mojawapo ya lugha

cushy

za kundi la Afro-Asia.

cushy adj (sl) (of a job etc.) -siohitaji juhudi kubwa; -enye raha, -a dezo.

cusp n ncha (agh. ya jani/jino).

cuspidor n chombo cha kutemea mate.

cuss n 1 (sl) laana. not give/care a ~

-tojali kabisa. not worth a tinker's ~ bure kabisa. 2 mtu. ~ed adj kaidi. ~ness n.

custard n faluda, kastadi.

custard-apple n 1 (tree) mtopetope, mtomoko. 2 (fruit) topetope, tomoko.

custody n 1 ulinzi, utunzaji/usimamizi, uangalizi. 2 ulezi, malezi. 3 kifungo. take somebody into ~ funga/ kamata. give into ~ peleka polisi. be in ~ -wa rumande. custodian n mtunzaji, mlinzi; mwangalizi, msimamizi.

custom n 1 desturi, mila native law and ~ sheria na mila za kienyeji. 2 kawaida, mazoea, ada. 3 uteja fulani I shall take my ~ elsewhere nitanunua mahali pengine. 4 (pl) ushuru (wa nje). ~s house n forodha. ~s clearance n hati ya utakaso (wa ushuru). ~s duty n ushuru wa forodha the. Customs n idara ya Forodha. 5 ~built n -a matakwa ya mteja. ~made adj -a kupima. ~ary adj 1 -a desturi, -a mazoea, -a kawaida. 2 -a mila. ~ary law n sheria ya mila. ~arily adv. ~er n mteja mnunuzi, mshitiri; (colloq) jamaa, mtu.

cut1 vt,vi 1 kata; (of minor cuts) chanya, kwaruza; (of grass) fyeka; (of nails) punguza; (of parts) mega; (of time, story etc.) fupisha; (of inscription) chonga, toboa. 2 (suitability for use) kata the matchet ~s well panga linakata vyema; (of material) katika. 3 (of class, lecture etc.) kacha. 4 (of lines) kata, pishana. 5 (of sport) betua. 6 choma moyo, umiza his words ~ me deeply to the quick maneno yake yaliniumiza sana. 7 (with nouns or pronouns) ~firewood tema/chanja/changa kuni.

~planks pasua mbao. ~ the cards/ pack kata karata. ~ one's coat according to one's cloth tumia kulingana na mapato; -tokuwa na tamaa mno katika mipango. ~ (off) a corner katiza. ~ a disc/record rekodi kwenye sahani ya santuri. ~ the ground from under someone's feet bomoa misingi yake (ya hoja, mipango n.k.). ~ no/not much ice tovutia, -tostua. ~ one's losses acha mpango kabla ya kula hasara zaidi. ~ a tooth ota jino. ~ one's teeth on jifunza; pata uzoefu. ~ both ways -wa msumeno the law ~ both ways sheria ni msumeno. ~ somebody to ribbons adhiri, umbua kabisa. 8 (with an adj as comp) ~ somebody dead -pa kisogo, jifanya huoni. ~ it fine (colloq) acha hadi dakika ya mwisho. ~ open tumbua, pasua. ~ short fupisha to ~ a long story short kwa kifupi. 9 C~! ingilia; wacha, simamisha (kupiga picha). 10 (with pp) ~ and dried adj -lokwisha amuliwa. ~ flowers n maua ya mapambo. ~ glass n gilasi zilokatwa nakshi. ~place/rate n bei poa/tupa, bwerere, dezo. ~tobacco n tumbaku iliyo katwakatwa. 11 (with adv and prep) ~ across katiza; pinga; vuka mipaka. ~ at lenga kupiga. ~ away ondoa kwa kukata. ~ back punguza ~ back expenses punguza gharama. ~ down angusha; ua; jeruhi (kwa silaha ya kukata); punguza kuvuta sigara ~somebody down to size punguza majivuno/ujeuri, onyesha kuwa mtu hastahili anachodai.

cut2 n 1 ukataji; mkato. ~ and thrust n (fig) mabishano makali. 2 upunguzaji. 3 makato. 4 pande. let kipande. 5 (of clothes) mtindo, mshono. 6 mbetuo, mchinjo. 7 simango. 8 msuso. 9 short ~ n njia ya mkato. 10 a ~ above bora zaidi. 11 tambuka reli, tambuko. 12 mchongo, kinyago. ~out n kidhibiti umeme. ~ in ingilia; (of cars)

jipachika. ~ into katiza. ~ into pieces gawanya. ~ off (from) ondoa kwa kukata; zuia; ingilia;

tenga; gawanya; nyima urithi; (mil) zingira. ~ out kata; (of engine etc.) acha kufanya kazi, simama; (omit/stop) acha; (of competition) shinda. ~ it/that out! acha magomvi/maneno. be ~ out for toa kwa have one's work ~ out for one kabiliwa na kazi kubwa. ~ up katakata; (mil) teketeza (usu pass) umia; (sl) kosoa, lima. ~up rough -wa mgomvi. 13 (in compounds) ~purse n mchomozi, mwizi wa mfukoni. ~throat n mwuaji adj kali sana; katili ~ throat competition mashindano makali sana. ~throat razor n kisuwembe. ~ting n 1 korongo maalum. 2 (of newspaper) kipande cha gazeti (kilichokatwa na kuhifadhiwa). 3 (of plants) kipandikizi, kitawi. 4 (of films etc.) uhariri (kwa kuondoa sehemu zisizotakiwa adj kali, -a kuumiza, -a kuchoma. ~ter n 1 dau. 2 kikata. 3 mkataji. tailor's ~ter n mkataji wa nguo.

cutaneous adj -a ngozi.

cute adj 1 -erevu, -enye akili. 2 (US

colloq) bashashi, -zuri, -a kuvutia. ~ness n. ~ly adv.

cuticle n (bio) ukaya wa ukucha.

cutlass n 1 panga. 2 jambia.

cutler n mjumu: mfua na mwuza visu, nyembe n.k. ~y n 1 biashara ya mjumu. 2 vilia: vyombo vitumiwavyo kulia mezani k.m. kisu, uma, kijiko.

cuttlefish n ngisi.

cutworm n sota.

cwt see hundred weight.

cyanide n (chem) sianidi: aina ya sumu kali.

cybernetics n saibenetiki: sayansi ya mfumo wa mawasiliano na nadharia ya udhibiti wake (katika wanyama na mashine).

cycle n 1 muhula mzima, kipindi au

mambo yanayojirudia (k.m. majira),

mbembeo. 2 duru, mzunguko wa kitu, mafuatano the ~ of the seasons of the year mafuatano ya nyakati za mwaka the life-~ of bee mzunguko wa maisha ya nyuki. 3 (of woman) hedhi. 4 mkusanyiko wa mashairi/nyimbo (agh. unaohusu tukio moja au mtu mmoja). vi panda baisikeli. cyclic n, adj. cyclical adj. cyclist n mpanda baiskeli.

cyclone n tufani, kimbunga. cyclopaedia n see encyclopaedia

cyclops n (myth) zimwi lenye jicho

moja tu, kashkash.

cyclostyle n 1 mashine ya kurudufu. 2 (of a pencil) kalamu ya kuandikia stensili. vt rudufu.

cygnet n mtoto wa bata maji.

cylinder n 1 (geom) silinda. 2 mcheduara, mwanzi; (tech) silinda two ~s silinda mbili. 3 (of a pistol) silinda ya risasi working on all ~s kwa nguvu/bidii zote. cylindric(al) adj.

cymbal n matuazi, tasa.

cynic n mbeuzi. ~al adj beuzi.

~ism n ubeuzi. ~ally adv.

cynocephali n 1 (myth) mtu mwenye

kichwa cha mbwa. 2 nyani mwenye kichwa cha mbwa.

cynosure n 1 kivutio kikuu he was the ~ of every eye kila mtu alivutiwa naye (na uzuri wake).

cypher n see cipher.

cypress n mvinje (wenye majani ya

rangi nzito ya chanikiwiti).

cyst n uvimbe (uliojaa maji). ~

its n (med) kuvimba kibofu.

cytology n sitolojia: tawi la biolojia

linaloshughulikia mambo yote yanayohusu seli.

cytoplasm n sitoplazimu: sehemu izingirayo kiini cha seli na iliyozungukwa na kiwambaseli.

Czar(also tsar) n Zari (mfalme wa

Urusi kabla ya mapinduzi). C~ina n Zarina.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.