TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

G,g herufi ya saba ya alfabeti ya Kiingereza; (US sl) dola elfu moja.

gab n (colloq) porojo. stop your ~

(sl) nyamaza. have the gift of the ~ -wa na kipaji cha kuzungumza. vt (colloq) piga porojo. ~by adj -enye porojo.

gabardine;gaberdine n gabadini: aina ya kitambaa cha sufu laini na imara.

gabble vt,vi sema upesi upesi bila kutamka vizuri maneno, tatanika; (of traditional doctor) rogonya. n msemo usioeleweka; urogonyaji.

gable n ukuta wa pembetatu katikati ya paa la nyumba ya mgongo. a ~ house n nyumba ya mgongo.

gad vi ~ about (colloq) tangatanga,

zurura kutafuta buruda. ~ about n mzururaji.

gadfly n 1 nzi (anayeuma ng'ombe/ farasi), pange. 2 mtu anayeudhi wengine makusudi kwa chokochoko na uchokozi, mtu mwenye gubu.

gadget n (colloq) kifaa cha kazi kidogo, kidude. ~ry n ala, zana (zote) pamoja.

gaff1 n uloo. vt vua kwa uloo.

gaff2 n blow the ~ (sl) toa siri; (US) stand the ~ vumilia.

gaffe n kosa; tendo la kutia aibu.

gaffer n 1 (colloq) msimamizi, mnyapara. 2 mzee, shaibu.

gag n 1 kifaa cha kuweka mdomoni (ili kinywa kikae wazi). 2 maneno anayoongezewa mtu na mwigizaji, ufaraguzi wa ziada. 3 kichekesho, hadithi ya kuchekesha. vt,vi 1 tiakifaa (tambara, pamba n.k.) kinywani; nyamazisha; (fig) nyima uhuru wa kujieleza/kusema. 2 ingizia maneno, semea. 3 (colloq) tapika (kiuongo).

gaga adj punguani.

gage1 n (old use) 1 dhamana; ahadi, amana. 2 glavu/changamoto ya kupigana (kushindana), mwaliko wa kupigana (kushindana). throw down the ~ to somebody alika mtu kupigana. vt (old use) weka amana/rehani; weka ahadi.

gage2 n see gauge.

galax

gaggle n 1 kundi la mabata Bukini.

2 (hum) kundi la wasichana/ wanawake wasemi.

gaiety n 1 uchangamfu; shamrashamra. 2 sherehe; maadhimisho; tafrija.

gaily adv see gay.

gain n ongezeko la mali/uwezo/

nguvu; chumo, pato; faida. ill-gotten ~s faida/pato lisilo halali a ~ in wealth ongezeko la utajiri a ~ in strength ongezeko la nguvu. ~ful adj -a pato, -enye kuzalisha mali/fedha. ~fully adv -kwa manufaa, kwa faida. vt,vi 1 pata; chuma; ongeza ~ experience pata uzoefu ~ weight nenepa ~ wealth chuma mali. ~ ground piga hatua. ~ time chelewesha kwa hila kwa manufaa yako, vuta muda, pata muda zaidi wa kufanya jambo baada ya kuchelewa. ~ the upper hand shinda. 2 ~ (from) faidi he ~ed a lot from his trip alifaidi sana kutokana na safari yake. 3 (of a watch or clock) -enda haraka, kimbia our clock ~s four minutes a day saa yetu hukimbia dakika nne kwa siku. 4 ~ on/upon karibiana na, sogelea, pita, fika mbele kabla/mbele ya; enda kasi kuliko; (of the sea) momonyoa ardhi. 5 fika mahali (baada ya juhudi). ~ings n (pl) tija; pato; ushindi.

gainsay vt (liter) (chiefly in neg and interr) kana, kaidi there's no ~ing haipingiki, hakuna upinzani, haikanikiki.

gainst (poet) see against.

gait n mwendo an unsteady ~ mwendo wa kupepesuka, kuyumbayumba.

gal n (dated colloq) msichana.

gala n tamasha, shangwe (attrib) a ~ day siku ya shangwe/fete ~ week wiki ya shangwe/fete.

galantine n nyama nyeupe ya mifupa (iliyoungwa, ikakunjwa, ikapikwa na kuliwa baridi).

galaxy n (pl -xies) 1 kundi la nyota. the G ~ n kundi la nyota na sayari ikiwemo yetu. 2 kundi la watu mashuhuri/wazuri. galactic adj (astron) -a galaksi, -a falaki kubwa

gale

angani.

gale n 1 upepo mkali, dhoruba it is

blowing a ~ kuna dhoruba. 2 mpasuko wa kelele a ~ of laughter kicheko kikubwa.

gall1 n 1 nyongo. ~ bladder n kibofu nyongo. ~ stone n jiwe: ugumu unaoota kwenye nyongo. 2 uchungu, chuki. 3 (colloq) ufidhuli.

gall2 n (of an animal esp a horse)

lengelenge, kidonda, chubuko vt. 1 chubua; kwaruza. 2 (fig) tweza, dhilisha; umiza.

gall3 n kinundu cha mti kinachooteshwa na wadudu.

gallant adj 1 shujaa, hodari. 2 (gay) -zuri, bora, -a fahari. 3 (chivalrous) -enye kuheshimu/kujali wanawake. n maridadi, mshaufu (anayejali/ heshimu sana wanawake). ~ly adv. ~ry n 1 ushujaa. 2 kujali/ kupendelea/kuheshimu wanawake. 3 (pl -ries) matendo/maneno ya kupamba/kubemba.

galleon n jahazi kubwa la zamani (la Kihispania).

gallery n 1 nyumba ya sanaa. 2 watu wakaao kwenye viti rahisi vya juu kwenye thieta. play to the ~ jipendekeza kwa umma. 3 (in theatre, church etc) orofa ya juu. 4 ujia (mrefu mwembamba) ulioezekwa juu. 5 chumba kirefu na chembamba. 6 njia (ya mlalo ndani ya machimbo ya madini).

galley n 1 (hist) manchani inayoendeshwa na watumwa au wahalifu. ~ slave n mtumwa aliyehukumiwa kuvuta makasia katika manchani. 2 trei ya kuwekea herufi. ~ proof n gali: chapa ya kwanza katika kipande kirefu cha karatasi.

Gallic adj -a Wafaransa; -a Ufaransa; -a Kifaransa. ~ism n neno/msemo wa Kifaransa katika lugha ya kigeni.

gallivant vi ~ about/off (not used in the simple tenses) tangatanga, tembeatembea, zurura, chungachunga (kutafuta burudani).

game

gallon n galoni, lita 4½

gallop n (of a horse, etc) mwendo wa

shoti at full ~ mbio sana. vt,vi 1 enda shoti; endesha shoti. 2 fanya (soma, enda n.k.) kwa haraka, chapuka.

gallows n (pl) (usu with sing v) kiunzi

cha miti cha kunyongea. ~ bird n mtu anayefikiriwa anastahili kunyongwa send somebody to the ~ hukumu mtu kunyongwa.

Gallup poll n kura fatiishi; kura ya kupima mawazo ya watu juu ya masuala mbalimbali (kwa kuuliza kikundi kiwakilishi cha watu).

galore adv kwa wingi, teletele.

galoshes n (pl) (pair of) ~ mabuti ya mvua (yanayovaliwa juu ya viatu).

galumph vi (colloq) rukaruka kwa furaha kuu.

galvanize vt 1 paka madini (chuma, bati). ~d iron sheet n bati. 2 ~ somebody (into doing something) shtua, amsha. galvanization n. galvanometer n galvanometa. galvanism n nguvu ya umeme kutoka kwenye betri. galvanic adj 1 -a nguvu ya umeme wa betri. 2 (fig) (of smiles, movements, etc) -liotokea ghafla.

gambit n 1 mwanzo wa mchezo wa sataranji. 2 (fig) mwanzo wa jambo (shughuli).

gamble vi,vt cheza kamari; bahatisha. ~ away one's fortune poteza mali kwa kamari n kubahatisha it's pure ~ ni kubahatisha tu. take a ~ (on something) jaribu bahati. ~r n mchezaji kamari; mtu anayebahatisha. gambling n kucheza kamari. gambling den/house n mahali pa kuchezea kamari/nyumba ya kamari.

gambol n (usu pl) mruko, kuchachawa. vi rukaruka, chachawa.

game1 n 1 mchezo (wenye sheria/ kanuni). be off one's ~ -tokuwa katika hali nzuri ya kucheza. have the ~ in one's hands -wa na hakika

game

ya kushinda. play the ~ fuata kanuni ya mchezo; (fig) -wa wazi na mwaminifu ~s master/mistress mwalimu wa michezo shuleni. ~smanship n (colloq) mbinu ya kushinda michezo. 2 vyombo vya kuchezea bao n.k. 3 (international contest) Olympic/Commonwealth/ East African G~s Michezo ya Olympiki/Madola/Afrika Mashariki. 4 (single round in some contests e.g. tennis) raundi win five ~s in the first set shinda raundi tano katika seti ya kwanza. 5 (scheme, plan) hila, shauri play a dangerous ~ -wa na shabaha yenye hatari/hila za kichinichini. beat somebody at his own ~ shinda mtu katika ujanja wake. make ~ of somebody fanyia mzaha/dhihaki mtu the ~ is up mambo/njama yame-fichuka don't play ~s with me usinichezee, usinidanganye. give the ~ away toa siri/nia. play somebody's ~ endeleza hila/ mpango wa mtu (bila kujua). 6 (collective) mawindo, wanyama/ndege wa kuwinda. big ~ n wanyama wakubwa (agh. tembo, simba, nyati n.k.). fair ~ n wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa; (fig) mtu/shirika linaloweza kukosolewa/kushutumiwa. ~ bag n mfuko wa mawindo. ~ bird n ndege wa kuwinda. ~ cock n kuchi. ~ keeper n mlinzi wa wanyama/ndege wa kuwinda. ~laws/act n sheria za kuhifadhi wanyama. ~ licence n leseni ya kuwinda na kuua wanyama wa kuwinda. ~ reserve n hifadhi ya wanyama. gamy adj -enye harufu ya wanyama pori.

game2 adj shujaa. be ~ for/to do something -wa tayari. ~ly adv kwa uhodari, kwa ushujaa.

game3 vi,vt cheza kamari. gaming house/room/table n nyumba ya kamari iliyokatiwa leseni.

game4 adj (of arm, leg) -enye kilema. gamete n gameti: seli pevu za uzazi.

gamma n gama: herufi ya tatu ya

gap

alfabeti ya Kigriki. ~-rays n miali gama.

gammon n paja la nguruwe (na sehemu ya mgongo); nyama ya nguruwe iliyokaushwa kwa moshi. vt kausha kwa moshi nyama ya nguruwe.

gammy adj (colloq) lemavu.

gamp n (colloq) mwavuli (agh mkubwa, ovyoovyo).

gamut n the ~ n upeo wa kitu/jambo/ hisia. run the ~ (of something) pitia mambo yote.

gander n bata dume la bukini.

gang n 1 kundi/jamii ya watu wafanyao kazi pamoja (agh. wahalifu), genge. 2 (colloq) kundi la wahuni. vi ~ up (on) piga maro, changia. ~ster n jambazi ~ster films filamu za kijambazi. ~er n msimamizi, mnyapara.

gangling adj (of a person) mtu njorinjori/ngongoti.

ganglion n ganglioni: kifundo cha

neva; (fig) kitovu cha kani/juhudi/ shughuli.

gang-plank n ubao wa kuingilia/ kushukia melini.

gangrene n 1 gangrini: uozo wa sehemu ya mwili kutokana na ukosefu wa damu. 2 (fig) uovu. vt, vi ozesha; oza. gangrenous adj.

gangway n 1 njia, ulalo, ubao wa kuingilia melini. 2 (US aisle) nafasi kati ya viti au safu za watu; (GB in the House of Commons) members above the ~ wabunge mashuhuri int hodi! nipishe!

gannet n membe mweusi.

gantry n mhimili wa chuma wa kushikilia winchi au selo ya reli.

gaol;jail n (usu jail in US) gereza, kifungo put in ~ funga jela four years in ~ miaka minne kifungoni. ~ bird n mfungwa. ~ break n kutoroka gerezani. ~er/jailer, jailor n mlinzi wa gereza, askari jela.

gap n 1 ufa; kipenyo; uwazi. 2 nafasi, pengo; hitilafu. bridge/fill/stop a ~ ziba/zuia pengo. credibility ~ n

gape

kutoaminika, ukosefu wa kuaminiana. generation ~ n migongano ya kizazi. ~-toothed adj -enye mwanya. 3 mlango (kati ya milima).

gape vi ~ (at somebody/something) 1 achama. 2 piga miayo; (of earth etc) atuka, pasuka, fanya ufa. n miayo, mwachamo wa mdomo. (pl) the ~s n miayo ya ugonjwa wa kuku; (joc) kushikwa na miayo.

garage n 1 gereji. vt weka gereji.

garb n 1 (style of) vazi, nguo. 2 kuvaa mavazi/nguo maalum in clerical ~ katika mavazi ya kipadre. vt (usu passive) valia, vaa ~ed as a sailor -liovaa mavazi ya kibaharia.

garbage n 1 takataka za chakula, (US) takataka zozote. ~ can n (US) pipa la taka. 2 (colloq) karatasi n.k zisizokuwa na maana, data isiyo na maana katika kompyuta literary ~ maandishi yasiyo na maana/machafu.

garble vt potoa wazo (kwa kutoka-milisha au kuchagua upande fulani; changanya wazo ~d version of a story mateuzi potofu ya hadithi.

garden n 1 bustani market ~ bustani (ya maua/matunda/mboga) ya biashara kitchen ~ bustani ya mboga (kwa matumizi ya nyumbani). lead somebody up the ~ path (colloq) danganya mtu common or ~ variety aina ya kawaida. 2 (pl) ~s n bustani kubwa kwa maburudisho ya wote; bustani ya hadhara. 3 (compounds) ~ centre n mahali panapouziwa mbegu, mimea au vifaa vya kulimia bustani. ~ city/suburb n mji/kitongoji chenye sehemu nyingi wazi zilizopandwa miti mingi. ~ party n karamu bustanini. vi lima bustani. ~er n mkulima wa bustani. ~ing n kilimo cha bustani.

gardenia n mgadenia.

gargantuan adj -kubwa sana.

gargle vt,vi gogomoa. n dawa/maji ya kusukutua/kugogomoa; ugogomozi.

gargoyle n mlizamu ambao kinywa chake ni sanamu ya mtu au mnyama.

garish adj -shaufu, -a rangi nyingi

gas

sana, -enye marembo kupita kiasi. ~ly adv. ~ness n.

garland n shada la maua. vt visha shada la maua.

garlic n kitunguu saumu a clove of ~ tumba la kitunguu saumu.

garment n vazi, nguo.

garner n (poet, rhet) ghala, bohari. vt

weka ghalani, hifadhi; kusanya.

garnet n ganeti; kito chekundu.

garnish vt ~ with pamba (hasa chakula mezani) meat ~ed with vegetables nyama iliyopambwa na mboga. n kipamba chakula.

garret n upenu.

garrison n askari walinzi wa mji, ngome, boma. vt weka askari walinzi (bomani/mjini/ngomeni).

garrotte; garotte vt ua (mtu) kwa kukaba koo/kutia kabali; nyonga. n kunyonga; chombo cha kunyongea mtu.

garrulous adj semi, -enye kubwabwaja. garrulity n.

garter n ukanda (wa mpira) wa kushikiza soksi. the G~ n nembo ya/cheo cha heshima kubwa sana Uingereza.

gas n 1 gesi. ~ bag n mfuko wa gesi; (colloq) mtu anayebwabwaja. ~ bracket n kiango cha gesi. ~ fire n moto wa gesi (wa kutia joto chumba). ~ fitter n fundi gesi, fundi wa kutia vifaa vya gesi katika jengo. ~ helmet; ~ mask n chombo/kofia/helmeti la kuzuia gesi isiingie puani. ~ holder/~ meter n mita ya gesi. ~ main n bomba kubwa la kugawia gesi majumbani. ~ tar n lami ya gesi. ~ chamber n chumba chenye gesi cha kuulia watu/wanyama. ~cooker/ stove/oven n jiko la gesi. ~ fittings n vifaa k.m. mabomba kwa ajili ya kuwashia gesi. ~light n mwanga utokanao na gesi. ~poker n kiwashia moto cha gesi. ~works n (pl) mahali gesi ya makaa inapotengenezwa. 2 laughing ~ nusu kaputi. 3 (US colloq)(abbr of

gash

gasoline) petroli. step on the ~kanyaga eksileta; ongeza mwendo; (fig) harakisha, tia mwendo. ~ station n (US) kituo cha petroli. 4 (fig) (colloq) mbwabwajiko; kuringa. vt,vi. 1 ua/kufa kwa gesi. 2 (colloq) bwabwaja, piga soga. ~eous adj -a gesi, kama gesi. ~ify vt,vi geuza/geuka kuwa gesi ~ ification n. ~sy adj 1 -a gesi, -liojaa gesi. 2 (of talk etc) -a kubwatabwata; -a mbwembwe. ~oline/~olene n (US) petroli.

gash n jeraha kubwa. vt jeruhi kwa kukata.

gasket n gasketi.

gasp vi,vt 1 tweta I ~ed with surprise nilitweta kwa kushtuka. 2 ~ (out) sema kwa kutweta ~ out life kata roho. n kutweta; kuhema kwa shida kwa sababu ya maumivu au mshangao beat one`s last ~ (fig) choka kabisa; karibia kufa; -wa hoi.

gastric adj -a tumbo ~ fever homa ya tumbo ~ juice n majitumbo ~ ulcer kidonda tumbo. gastritis n uvimbe -tumbo.

gastronomy n gastronomia: sayansi ya mapishi, uchaguzi, utayarishaji na ulaji bora. gastronomic adj.

gate n lango; kizuizi. ~ crash vt ingia (katika nyumba, tafrija au uwanja) bila idhini au kiingilio. ~ crasher n mpandiaji. ~ house n nyumba iliyo karibu na lango. ~ keeper n bawabu. ~legged table n meza ya miguu ya kukunjuka. ~ money n fedha za kiingilio. ~ post n nguzo ya lango. between you(and) me and the ~ post n kwa siri sana. ~ way n njia inayofungwa kwa lango; (fig) mbinu/njia ya kukabili/kufikia (jambo). vt zuia mwanafunzi abakie shuleni (kama adhabu).

gateau n (F) keki ya malai.

gather vt,vi 1 (of people, things etc) dunduliza, kusanya; kusanyika, konga ~ crowd of people kusanya umati wa watu the clouds are ~ing mawingu yanakusanyika. be ~ed to one's

gay

fathers fariki. 2 (of flowers, berries etc) chuma. 3 pata polepole ~ rust pata kutu ~ information pata habari kidogo kidogo, duduliza/kusanya habari ~ speed ongeza mwendo. 4 (understand, conclude) elewa, fahamu what did you ~ from his statement? ulielewa nini kutokana na usemi wake? 5 (in sewing) fanya marinda. 6 (of a boil) tunga usaha, iva. ~ing n 1 kukutana; mkutano; mkusanyiko. 2 kutunga usaha.

gauche adj shamba. ~rie n mshamba. gaucho n mchunga ng'ombe (wa Amerika ya Kusini).

gaud n urembo. ~y adj -a urembo

mno. ~iness n.

gauge; (US gage) n 1 geji standard ~ geji ya kawaida take somebody's~ (fig) pima, tathmini, kisia tabia ya mtu. 2 kipimia mvua/nguvu ya upepo/unene n.k. rain ~ kipimia mvua. 3 (railway) geji: upana kati ya reli. 4 (of wire etc) geji: unene wa waya, bati n.k.. vt pima, kadiria, kisia; (fig) kisia.

gaunt adj (of a person) ~ liokonda sana kwa dhiki. ~ness n.

gauntlet1 n 1 glavu ya chuma (iliyova- liwa na askari wa zamani sana). throw down/pick up/take up the ~ dai/kubali kupigana. 2 glavu ngumu ya kuendeshea gari n.k..

gauntlet2 n (only in) run the ~ kimbia kati ya safu mbili za watu na pigwa nao kadri upitavyo; (fig) kabiliwa na hatari/kashfa n.k..

gauze n 1 shashi; kitambaa chembamba sana kinachoona; wavu wa nyuzi (kama chandarua). 2 wavu wa nyuzi za madini wire ~ wavu. gauzy adj.

gave pt of give.

gavel n nyundo ya dalali, mwenyekiti n.k. ya kunyamazishia watu/kutulizia fujo.

gawk n thakili, mtu mzito, mwenye aibu. vi (colloq) kodolea macho. ~y adj. ~iness n uzito.

gawp ~ (at) see gawk vi.

gay adj 1 -changamfu, bashashi. 2 -a

gaze

kufurahisha, -a kupendeza ~ colours rangi zinazofurahisha/zinazopendeza. 3 (colloq) hanithi, msenge; basha. gaily adv kwa uchangamfu. ~ness n.

gaze vi ~ (at) angaza/kazia macho. ~ (upon, on) ona.

gazelle n swala.

gazette n gazeti la kiserikali (kuhusu ajira mpya, vyeo n.k.). vt (usu passive) be ~d chapishwa katika gazeti la serikali.

gazetteer n faharasa ya majina ya kijiografia.

gazump vi,vt (colloq) danganya kwa kuongeza bei (baada ya makubaliano na kabla ya kusaini mkataba).

gear n 1 gia (k.v. ya gari) change ~

badili gia. high/low ~ n gia kubwa/gia ndogo. in/out of ~ n katika gia/bila gia. top/bottom ~ n gia ya juu/ya chini. ~ box n giaboksi. ~ shift/lever/stick n mkono wa kubadilishia gia. 2 zana zenye kazi maalum the landing ~ of an aircraft miguu ya kutulia ndege. 3 vifaa jumla hunting ~ vifaa vya kuwindia (modern, colloq) nguo, mavazi party ~ nguo za sherehe. vt,vi ~ up/down weka gia ya juu/ya chini. ~ to rekebisha kitu kikidhi matakwa ya wakati huo ~ the country's economy to wartime requirements rekebisha uchumi wa nchi kukidhi mahitaji ya wakati wa vita.

gecko n mjusi kafiri.

gee1 (also ~ up) interj (command to horse) endelea; hamasisha. ~ -~ n neno atumialo mtoto kwa farasi.

gee2 (also ~-whiz) int (US) mshangao unaoonyesha kupenda au kustaajabu, salaale! lo!

geese n pl of goose.

geezer n (sl) shaibu.

Geiger n (esp G~-counter) gaiga:

kipima mnururisho.

geisha n geisha: msichana au

mwanamke wa Kijapani anayewaburudisha watu kwenye tafrija n.k. kwa kuimba na kucheza.

general

gel n kitu kiteketeke kama jeli. vi fanya kuwa jeli; gandisha it doesn't ~ (colloq) haiji, haileti.

gelatin(es) n jelatini:gundi-gundi (ya mifupa, nyama n.k.). ~ous adj.

geld vt hasi. ~ing n maksai.

gelignite n baruti (ya asidi naitriki na gliserini).

gem n 1 kito; johari. 2 kitu kinachotha- miniwa sana kwa sababu ya uzuri wake. ~med adj -liopambwa na vito.

geminate adj -a jozi. vt gawa/panga

katika jozi. gemination n.

Gemini n mapacha.

gen (sl) (the) ~ habari. vt ~ up toa/pasha habari, elewesha.

gendarme n (in France and some other countries, but not in GB or US) polisi. ~rie n (collective sing) kikosi cha polisi.

gender n 1 jinsi (mume au mke); jinsia ~ question suala la kijinsia. 2 (gram) ngeli (za maneno) feminine ~ jinsi ya kike masculine ~ jinsi ya kiume neuter ~ jinsi isiyo ya kike wala ya kiume.

gene n jeni: sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani. ~tic adj 1 -a jeni/-a jenetiki. 2 -a kinasaba/kijeni a ~tic defect hitilafu ya kinasaba. ~s n jenetiki. genealogy n (elimu ya) nasaba, kizazi, ukoo. ~tree n shajara ya nasaba. genealogical adj. genealogically adv.

genera n pl of genus.

general adj 1 -a jumla; -a -ote; si maalum a matter of ~ interest jambo la kuhusu watu wote. ~ knowledge n maarifa, malimwengu ~ paper karatasi ya maarifa. ~ practitioner n daktari anayetibu magonjwa yote ~ clauses ibara za jumla. ~ degree n digrii ya jumla; (common) -a desturi, -a kawaida, -a siku zote. in ~; as a ~ rule kwa kawaida/-desturi, mara nyingi of ~ application -a kutumika kwa kawaida. 2 -a kudokeza, -a jumla

generate

jumla ~ idea/outline dokezo, maelezo ya juujuu tu a ~ statement maelezo ya juu-juu tu. 3 (chief, principal) -kuu, -kubwa. ~ election n uchaguzi mkuu. ~ meeting n mkutano mkuu n (milit) jenerali. ~ization n 1 jambo, shauri, neno, maono maarifa n.k. ya kijumla jumla (bila kuhoji au kufikiria mambo yote), jumuisho. 2 majumui. ~ize vi, vt ize~(from/about) 1 fikia hitimisho la jumla; toa kauli ya jumla. 2 eleza jambo jumlajumla, jumuisha. 3 ingiza katika matumizi ya jumla, sambaza/fanya itumike kote. ~ly adv 1 mara nyingi, kwa kawaida/desturi. 2 kwa jumla. ~ship n 1 ujenerali. 2 maarifa ya vita. 3 ustadi wa usimamizi (wa shughuli n.k.). ~issimo n jemadari mkuu wa majeshi yote (ya nchi kavu, anga na majini). ~ity n 1 kauli ya jumla. 2 the ~ity (of) idadi kubwa (ya); wengi the ~ity of students passed the examination wengi wa wanafunzi walifaulu mtihani.

generate vt fanyiza; leta; zalisha ~ electricity zalisha umeme. generator n jenereta. generation n 1 kizazi three generations vizazi vitatu (baba na wanawe na mjukuu). 2 kufanyiza, kuzalisha. 3 kizazi: kipindi cha wastani cha umri wa mtu wa kuoa na kuwa na watoto. 4 rika, watu waliozaliwa wakati mmoja, wa rika moja. generative adj -zazi generative organs viungo vya uzazi generative grammar sarufi fafanuzi/zalishi.

generic adj -a jenasi; -a ainasafu; -a kuhusu -ote.

generous adj 1 (liberal) karimu; paji. 2 -ingi, kubwa a ~ portion fungu kubwa/jingi. ~ly adv. generosity n ukarimu.

genesis n 1 asili, mwanzo, chimbuko. 2 (rel) G~ n Mwanzo: kitabu cha

kwanza cha Agano la Kale.

genial adj 1 -kunjufu, -changamfu;

-enye huruma. 2 -enye kupendeza, a joto. ~ly adv. ~ity n ukunjufu,

gentleman

uchangamfu.

genie n jini.

genital adj -a viungo vya uzazi. n (pl) ~s. viungo vya uzazi.

genitive adj ~ (case) (gram) -a chanzo; milikishi.

genius n 1 kipaji. 2 mtu mwenye kipaji hicho. 3 a ~ for kipaji/uwezo asilia wa a ~ for languages kipaji cha lugha. 4 the ~ (of) busara, roho ya namna fulani maalum. 5 one's good/ evil/ ~ pepo mwema/mbaya anayetawala, anayelinda, anayeongoza mahali au watu wengine; mtu anayewaathiri sana wenzie ~ loci mazingira ya mahala; (evil) afriti. 6 (pl genii) jini, zimwi.

genocide n uangamizaji wa kabila, taifa kwa mauaji au uwekaji wa masharti muhali kuishi.

genre n (F) 1 namna, aina, jinsi. 2 (of liter) tanzu. ~-painting n uchoraji wa picha kutokana na mambo ya kawaida ya maishani.

gent n (colloq abbr of gentleman) mwanamume. the/a G~s n (GB colloq) choo cha wanaume.

genteel adj (usu ironic in modern use; but serious in former use) -a kiungwana; -a daraja kubwa living in ~ poverty jaribu kuishi maisha ya juu ingawa maskini sana; kufa kiofisa. ~ly adv. gentility n uungwana; ubwana living in shabby gentility jitwaza, iga maisha ya juu.

gentian-violet n (med) jivii.

gentile n mataifa adj -a mataifa;

asiye Myahudi.

gentle adj 1 -pole, raufu; latifu, si kali a ~ breeze upepo mwanana a ~ slope mteremko usio mkali. 2 (of a family) ungwana. ~folk n (pl) waungwana. ~ness n upole, uraufu. vt 1 fundisha/ongoza farasi kuwa mpole. 2 bembeleza, tuliza. gently adv kwa upole, kinyerenyere; kwa uangalifu hold it gently shika kwa uangalifu.

gentleman n 1 muungwana, bwana,

mwanaume. ~'s agreement n

gentry

kuaminiana; mapatano ya kiungwana. 2 (hist) mtu wa daraja kubwa. ~ at arms mlinzi wa mfalme. 3 (hist) mtu aliyeruhusiwa kuwa na silaha ingawa si wa daraja kubwa. 4 (dated use) mwinyi. 5 (pl) njia ya heshima ya kuwaita wanaume waliohudhuria Ladies and G~ Mabibi na Mabwana. 6 njia ya kuanza barua rasmi. ~ly adj -a kiungwana. gentle- woman n (pl gentlewomen) see lady.

gentry n (pl) (the) ~ n watu wa daraja kubwa kidogo.

genuflect vi piga goti (katika kuabudu au kuheshimu). ~ion; genuflexion n.

genuine adj -a kweli; halisi ~ article

bidhaa halisi a ~ purchaser mteja halisi. ~ly adv. ~ness n.

genus n 1 jenasi: uainishi spishi zenye sifa zinazofanana; (bio) nasaba ~ Homo wanadamu. 2 jinsi, namna, aina; jamii.

geo pref dunia. ~centric adj -enye/-a kuwakilisha dunia kama kitovu. ~dess n upimaji dunia. ~physics n elimu ya fizikia ya dunia. ~politics n (pl) siasa ya nchi kama inavyoathiriwa na jiografia.

geography n jiografia. geographer n mtaalam wa jiografia. geographical adj. geographically adv.

geology n jiolojia. geologist n mtaalamu wa jiolojia. geological adj. geologically adv.

geometry n jiometri analytical ~ jiometri changanuzi/chambuzi. geometric; geometrical adj -a kijiometri. geometric progression n mwendelezo jiometri. geometrically adv.

George n 1 St ~ Mtakatifu George

(mtakatifu mlezi wa Uingereza) St ~s` cross Msalaba mwekundu kama ule wa bendera ya Uingereza 2. (sl) (aircraft) kiendeshaji kinachoji- endesha int by G~ (dated) aaa! lo!

georgette n hariri nyembamba.

Georgian adj 1 -a wakati wa mfalme George I, II na wa III wa Uingereza. 2 mkazi wa Georgia (ya Urusi na ya

get

Marekani).

geriatric adj -a utibabu wa wazee. ~s n utibabu wa wazee. ~ian n daktari wa magonjwa ya wazee.

gerontology n jerontolojia: sayansi inayohusika na uzeekaji (hasa wa binadamu).

germ n 1 mbegu ~ cell seli zazi; (fig) asili, chanzo cha wazo n.k. 2 kijidudu; kiini cha maradhi. vi (fig) chipua, mea. ~icide n kiua vijidudu (hasa bakteria). ~icidal adj. ~inate vi,vt chipua, mea, ota. ~ination n uotaji, kuchipua, kumea.

German n Mjerumani; lugha ya Kijerumani adj -a Kijerumani; -a Ujerumani. ~ic adj -a kundi la lugha zinazohusiana na Kijerumani.

germane adj ~ (to) -nayohusu kabisa.

gerrymander vt fanya hila katika uchaguzi (katika kupanga mpaka wa majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya kupendelea mtu/chama/tabaka fulani. n hila katika uchaguzi.

gerund n kitenzi nomino.

Gestapo n Gestapo: polisi wa siri wa Kijerumani wakati wa utawala wa Nazi.

gestation n 1 kuchukua mimba; ujauzito. 2 also ~ period n kipindi cha kuchukua mimba; ujauzito; (fig) kipindi cha kukua kwa wazo.

gesticulate vi ashiria, tumia mikono,

kichwa n.k. wakati wa kuzungumza. gesticulation n.

gesture n 1 ishara ya mikono au kichwa (kutoa wazo, hisia n.k.). 2 tendo la kuonyesha hisia/mtazamo as a ~ of friendship he gave us his new book alitupatia kitabu chake kipya kama ishara ya urafiki; utumiaji wa ishara. vi ashiria.

get vi,vt 1 (obtain, receive) pata ~ a present pata zawadi. ~ an illness pata ugonjwa. 2 -wa ~ wet rowa ~ lost (sl) ambaa! potea! ondoka! 3 fanya, sababisha ~ the food ready andaa chakula. ~ something done kamilisha, maliza kufanya. 4 anza; anzisha ~ going anza when the

get

women ~ talking wanawake wanapoanza kuongea. 5 pata (kujua, kusikia, n.k.) when you ~ to know her you will like her utakapomfahamu vizuri utampenda. 6 shawishi, leta you'll never ~ him to understand huwezi kumwelewesha I can't ~ him to talk nashindwa kumshawishi aongee. 7 pewa adhabu ~ six months pewa kifungo cha miezi sita. ~ told off (colloq) semwa, karipiwa. 8 (colloq) elewa, pata I didn't ~ the joke sikuuelewa mchapo wenyewe I don't ~ you sikuelewi/pati. 9 (esp. in perfect tenses) tatanisha, pata I have got you there! Nimekupatia! 10 -wa na, miliki we have got a big house tuna nyumba kubwa. 11 have got to paswa, lazima I have got to finish this job lazima nimalize kazi hii. 12 weza, fanikiwa. 13 (non idiomatic intransitive uses with adverbial particles and preps) enda. ~ across vuka. ~ back rudi. ~ home fika nyumbani. ~ off toka. ~ a move on fanya haraka where can it have got to? iko wapi/imepotelea wapi? ~somewhere piga hatua. ~ nowhere/not ~ anywhere -tofika popote. ~ there (colloq) fanikiwa. 14 (non idiomatic transitive uses) peleka. patisha: I'll ~ you home before midnight nitakurudisha kabla ya saa sita usiku ~ your clothes on vaa I'll ~ you to the station early nitakupeleka/fikisha stesheni mapema. 15 (idiomatic uses with adverbial particles and preps) ~ about (of somebody who has been ill) tembeatembea, pata nafuu; (of news, rumour, story) enea; (of a person infml) safiri, zunguka. ~ above oneself jivunia, jiona. ~ something across (to somebody) (colloq) elewesha. ~ ahead (of somebody) pita (mtu); fanikiwa zaidi. ~ along weza; endelea; ondoka. ~ along with elewana na/patana na. ~ along with you! (colloq imper) ondoka; acha! usiniambie! ~ around see ~

get

round. ~ at somebody/something fikia; pata. ~-table adj -enye kufikika; -enye kupatikana. ~ at somebody (bribe) honga, -pa rushwa; (taunt) chokoza, kera. ~ at something gundua, pata ~ at the truth gundua/pata ukweli. be ~ting at (colloq) maanisha. ~ away toroka. ~ -away n kutoroka make one's ~ away toroka. ~ away with something fanikiwa bila kugunduliwa (katika jambo ovu) you'll never ~ away with it watakugundua. ~ back rudia kwenye madaraka (baada ya kuyapoteza). ~ back at somebody/~ one's own back (on somebody) lipa kisasi. ~ by pita/kubalika, weza, ishi. ~ down (of children) ondoka mezani (baada ya kula); shuka, teremka; shusha. ~ somebody down (colloq) sononesha; fadhaisha. ~ something down (swallow) meza; (write) andika. ~ down to something anza kufanya kitu kwa makini. ~ home (to) somebody eleweka wazi. ~ in fika; (to a car etc) panda; (of election) chaguliwa. ~ somebody in ita mtu (fundi, daktari n.k.) nyumbani (ili kutoa huduma). ~ something in kusanya; jaliza, weka akiba. ~ into (of clothes) vaa; ingia katika hali fulani ~ into trouble ingia matatani. ~ a girl into trouble (colloq) tia msichana mimba. ~ into bad company shirikiana na waovu; jifunza, zoea. ~ into one's head that elewa kuwa. ~ off anza. ~ off lightly/cheaply -topata adhabu kali. tell somebody to ~ off/where he ~s off (colloq) -pa mtu ukweli wake. ~ somebody/-something off tuma, peleka (barua n.k.). ~ off (bus etc) shuka, telemka. ~ somebody off okoa (kwenye adhabu). ~ somebody off to sleep laza. ~ something off ondoa; vua. ~ something off (by heart) kariri.

get

~ off with somebody (colloq) fanya mapenzi na. ~ off with something pata (adhabu ndogo) he got off with a fine alipata faini tu. ~ on endelea, songa mbele; (of time) pita. ~ on something panda. ~ on one's feet simama; (fig) pata nguvu mpya; fufuka, inuka. be ~ting on for (of time age) karibia. ~ on to somebody wasiliana na (colloq) tambua/gundua (ujanja, hila n.k.). ~ on (with somebody) elewana/patana na. ~ on (with something) endelea na. ~ on with it! fanya haraka! ~ out (of secret etc) julikana, fichuka. ~ something out (of words) sema; (of produce) toa; chapisha; tawanya; (of meeting etc) ondoka. ~ out of (doing) something kwepa; (fig) acha polepole. ~ something out of somebody pata jambo kutoka kwa mtu. ~ over somebody (colloq) sahau. ~ over something (of ilness etc) pata ahueni/nafuu; (overcome) shinda. ~ something over (with) maliza, fikia mwisho wa (kitu kibaya au chenye matatizo). ~ something over (to somebody) elewesha I can't ~ over it nashindwa kuamini. ~ round somebody shawishi mtu. ~ round something epa; zunguka. ~ round to doing something (pata muda wa kushughulikia jambo (baada ya mengine yenye maana kushughulikiwa). ~ through (to) fikia, fika, wasiliana na. ~ through (something) pita, faulu, shinda ~ through an examination faulu mtihani. ~ through (with) something maliza, fikia mwisho. ~ through to somebody that elewesha mtu/pasha mtu habari kuwa. ~ somebody through (something) saidia mtu kushinda/kufaulu. ~ something through hakikisha jambo linatekelezwa; (of proposal, bill in parliament etc) pitisha kuwa sheria; pitisha. ~ to fikia hali fulani. ~ together kutana (kwa dhifa, majadiliano n.k.). ~ together n

ghost

kukutana; mkusanyiko (kwa ajili ya tafrija, mkutano n.k.). ~ it/something together (colloq) panga, ratibu/simamia jambo. ~ oneself together (colloq) weza kujizuia; jitawala. ~ people/things together kusanya. ~ up inuka; (from bed) amka; (mount) panda; (of wind, sea) anza kuchafuka/ kucharuka. ~ somebody/something up inua; amsha, andaa vizuri (kitabu n.k.). ~ up n mtindo/mpango wa kitabu/jarida/mavazi (hasa usio wa kawaida). ~ something up tayarisha, panga. ~ up to something fikia; shughulika/fanya lisilo la kawaida. ~ somebody with child (arch) tia mimba.

gewgaw n kishaufu, pambo.

geyser n 1 chemchemu ya maji moto. 2 chombo cha kupashia maji moto (hasa kwa kutumia gesi au umeme).

gharry n (India) gari (linalovutwa na farasi).

ghastly adv kama kifo adj 1 mahututi; -a kupauka he was looking ~ alionekana mahututi. 2 -a kutisha, -a kuogopesha a ~ accident ajali mbaya mno. 3 (colloq) -a ovyo, -siopendeza.

ghee n samli.

gherkin n namna ya tango dogo (la kutengenezea achari).

ghetto n 1 (hist) (of a town) mtaa wanakokaa Wayahudi. 2 sehemu ya jiji wanakokaa maskini au watu wanaobaguliwa.

ghost n 1 pepo, zimwi there are ~s in the room chumbani mna pepo/vizuka. raise a ~ ita/pandisha pepo I don't believe in ~s siamini mambo ya pepo. 2 roho. give up the ~ kata roho, -fa, fariki dunia. the Holy G~ n Roho Mtakatifu. 3 kivuli, kitu hafifu a ~ of a smile kicheko hafifu sana. not have the ~ of a chance -toweza kufanikiwa/ kushinda kabisa. ~ town n mahame, ganjo. 4 ~writer n mwandishi anayemtungia mwingine

ghoul

kazi (bila yeye kutajwa jina). 5 (television) taswira, rudufu. vt,vi tungia mwingine. ~ly adj 1 kivuli; hafifu; -a mzuka; -a kama mzuka. 2 (spiritual) (arch) -a kiroho. ~ly advice ushauri wa kiroho.

ghoul n 1 (in stories) zimwi mla maiti. 2 mtu katili sana. ~ish adj.

Gl n askari wa jeshi la Marekani.

giant n 1 (in fairy tales) jitu. 2 pandikizi (la mtu/mnyama n.k.); (fig) mtu mwenye akili au kipaji kikubwa. 3 (attrib) -kubwa sana, -enye nguvu sana. ~ess n jitu la kike.

gibber vi tatarika; payapaya, bwata. ~ish n payo; maneno ya kipuuzi.

gibbet n 1 kiunzi cha kunyongea. 2 kifo cha kunyongwa. 3 kiunzi cha kuonyesha walionyongwa. vt nyonga kwa kitanzi; (fig) dharau.

gibbon n sokwe.

gibbous adj 1 -a mwezi mwandamo. 2 -enye kubenuka; -a kibyongo.

gibe (also jibe) vi ~ (at) kebehi, dhihaki; beza. n bezo.

giblets n sehemu za ndani za ndege (nyuni).

giddy adj 1 -enye kizunguzungu. 2 -enye kupenda raha; -sio na makini; -sio na msimamo thabiti. giddily adv. giddiness n.

gift n 1 zawadi, hiba, tunu. 2 kipaji. ~ from God karama, kipawa. 3 uwezo/ mamlaka ya kutoa kitu. vt tunukia, -pa zawadi. ~ed adj -enye kipaji, -liojaliwa.

gig n 1 (hist) gari dogo la farasi lenye magurudumu mawili. 2 (naut) mashua ndogo (ya meli kubwa agh. kwa matumizi ya nahodha). 3 (colloq) onyesho la muziki.

gigantic adj -kubwa kabisa, -refu mno, -a kupita kiasi he has a ~ appetite yu mlaji sana.

giggle vi chekacheka. n kicheko. giggly adj.

gigolo n 1 mwanamume anayekodishwa na mwanamke (kucheza naye dansa). 2 kijana kipenzi cha mwanamke mzee tajiri (anayetunzwa naye).

grid

gild1 vt chovya/paka dhahabu. ~ the lily haribu uzuri wa kitu kwa kukipamba sana. ~ the pill pendezesha kitu kinachochukiza. ~ed youth n kijana maridadi na tajiri. ~er n. ~ing n. gilt n mpako wa dhahabu. take the gilt off the ginger bread ondoa uzuri wa kitu. gilt-edged stocks/securities n vitegauchumi madhubuti.

gild2 see guild.

gill n yavuyavu: shavu la samaki. vt

toa/tumbua mashavu (ya samaki).

gillie n (Scot) mhudumu wa mwindaji au mvuvi.

gimbals n vigango (vya dira, horometa n.k.); viungo viunganavyo katika mashine.

gimcrack n kinyangarika, kitakataka, kitu hafifu adj -a ovyo, bure. ~ ery n.

gimlet n kekee ndogo. ~ eyes n macho makali.

gimmick n (colloq) hila/ujanja wa ku(ji)tangaza/kujitambulisha, vitimbi.

gin1 n 1 mtego (wa wanyama). 2 (cotton) ~ kinu cha kuchambulia pamba. vt 1 tega mtego wa kufyuka. 2 chambua pamba kwa kinu.

gin2 n jini: aina ya pombe kali.

ginger n 1 tangawizi. ~ beer/ale n soda ya tangawizi. ~ bread n keki/mkate wa tangawizi. 2 bidii; nguvu; uchangamfu ~group (in parliament) kikundi cha kuchemsha/ kuchangamsha serikali. 3 rangi ya hudhurungi nyekundu. ~y adj. ~ly adv kwa hadhari sana, kwa uangalifu sana, kwa makini sana. ~ up changamsha.

gingham n ging'amu.

gipsy;Gypsy n 1 ~ mzururaji. 2 G~ n mhamaji mzururaji (agh. mwenye asili ya kihindi apataye riziki yake kwa biashara ya farasi, kuuza vikapu, utabiri n.k.).

giraffe n twiga.

gird vt (poet or rhet) 1 ~ on vaa, funga (kiunoni). 2 ~ up funga (kwa

girder

shipi). ~ up one's loins jiweka tayari/jitayarisha (kwa kazi, vita); jifunga kibwebwe. 3 zunguka, zingira (mji, kisiwa, n.k.) a town ~ed with mountains mji uliozingirwa na milima.

girder n boriti, mhimili (wa mbao au chuma).

girdle1 n 1 kanda; (after child birth) mkaja. 2 kitu kinachozingira kama mkanda. vt ~ about/around/with zunguka, zingira.

girdle2 n (Scot) see griddle.

girl n 1 msichana. 2 mwanamke afanyaye kazi katika ofisi, dukani n.k.. house ~n msichana wa kazi. ~ (friend) n rafiki wa kike, mpenzi. (GB) G~ Guide n (US). G~ Scout n skauti wa kike. ~ hood n usichana. ~ish adj -a msichana; -a kisichana. ~ishly adv. ~ishness n.

giro n mfumo wa kuhawilisha fedha/ mali, jiro.

girth n 1 kipimo cha mzingo a circle/ waist/barrel 30 metres in ~ duara/ kiuno/pipa lenye mzingo wa mita 30 his ~ is increasing ananenepa. 2 (in harness) ukanda unaopitishwa tumboni mwa farasi (kufungia matandiko).

gist n the ~ n kiini; mambo muhimu the ~ of somebody's remarks kiini cha (maneno ya mtu), maana hasa the ~ of the matter kiini cha jambo.

give vt,vi 1 ~ (to) -pa, toa, patia, gawia ~ alms toa sadaka ~ a message toa/pa ujumbe ~ medicine -pa dawa the sun ~s us light jua hutupa mwanga. 2 ~ for something; ~ to do something -lipa, lipia How much did you ~ for your new farm? ulilipa kiasi gani kwa shamba lako jipya? 3 ~ (to) kabidhi, wekesha, salimisha; -pa ~ the customs officer your luggage kabidhi mizigo yako kwa afisa wa forodha. 4 ruhusu, kubali, achilia, -pa. ~ somebody ten minutes ruhusu mtu dakika kumi. ~ somebody trouble sumbua; fanyia fujo/matata. 5 ambukiza you have

give

~n me a rash umeniambukiza upele. 6 jitolea. ~ your life to the cause of God jitolea maisha kwa ajili ya kazi za Mungu. 7 (used in the imper to show preference) ~ us a proper salary or fire us tupe mshahara halali ama sivyo tufukuze. 8 (used with a noun in a pattern that may be replaced by one in which the noun is used as a verb) ~ a push sukuma ~ somebody a ring pigia mtu simu ~ a smile tabasamu. 9 (in fixed phrases) ~ or take kama/ kiasi cha he is forty years old, ~ or take a year ana kiasi cha miaka arubaini. ~ somebody to best (old use) kiri/ kubali ubora (wa mtu) ~ somebody understand that taarifu, fahamisha, hakikishia (mtu fulani) kuwa. ~ it to somebody to (colloq) adhibu, karipia G~ it to him! Mpe! ~ somebody what for/a piece of one's mind (colloq) adhibu, kemea, -pa ukweli wake. ~ way rudi nyuma; (of support) shindwa kuhimili. ~ way (to something/somebody) pisha; (replace) badiliwa na; (abandon oneself) jiachia; (concede) kubaliana na ~ way to demands kubaliana na madai. 10 legea; pinda, nepa, bonyea the bow does not ~ well upinde haupindiki vizuri this matress ~s comfortably godoro hili linabonyea vizuri. 11 ~n (pp) (in formal documents) -liotolewa ~n under my hand and seal on this tenth day of February, 1996 -liotolewa kwa idhini na muhuri wangu leo tarehe kumi mwezi Februari, 1996; (in reasoning) ikiwa, iwapo ~n the opportunity he could make a good politician ikiwa atapewa nafasi anaweza kuwa mwanasiasa bora; -liokubaliwa; -liopangwa the ~n time and place mahala na saa iliyopangwa the ~ n conditions masharti tuliyo kubaliana. be ~n to something/ doing something -wa na tabia ya, penda ~n to gossiping -enye tabia

give

ya utetaji ~ n to drink penda kunywa pombe. 12 what ~s (colloq) kuna nini? 13 (uses with adv particles and prep).~ somebody away kabidhi bibi arusi (kwa bwana arusi wakati wa arusi). ~ something away toa sadaka; -pa mtu; (lose unnecessarily tupa; (distribute) gawa, toa bure ~ awa clothes gawa/toa nguo bure; fichua, toa siri ~ away a secret fichua siri. ~away n (colloq) vitu vitolewavyo bure at ~ away prices rahisi sana the examination was a ~ away mtihani ulikuwa rahisi mno; kitu kifichuliwacho the child's face was a ~ away uso wa mtoto ulifichua kosa lake. ~ something back (to somebody); ~ somebody back something rudisha ~ the book back to the teacher rudisha kitabu kwa mwalimu. ~ something forth (old use or liter) toa (moshi, hewa n.k.). ~ in (to somebody) kubali kushindwa terrorists gave in magaidi walikubali kushindwa. ~ something in kabidhi, wasilisha (ripoti, karatasi n.k.) the commission gave in the report to the Minister tume iliwasilisha ripoti kwa Waziri. ~ one's name in (to somebody) julisha/tangaza nia/madhumuni (ya kugombea uchaguzi n.k.). ~ something off toa (moshi, hewa n.k.). ~ on to elekea; chungulia. ~ out (finish) isha, malizika. ~ something out gawa; peleka ~ out tea gawa chai. ~ out to be; ~ it out that somebody is tangaza The Minister ~s Mr Pandu out to be the Director Waziri amemtangaza bwana Pandu kuwa Mkurugenzi. ~ upon; ~ on to; ~ over (sl) acha ~ over gabbling acha kubwata. ~somebody/something over (to somebody) kabidhi, peleka ~ somebody over to the police peleka/kabidhi mtu polisi. be ~n over to something jiachia, jikita,

jishughulisha sana (katika tamaa, dhambi, huzuni n.k.); (set aside)

glad

tengwa kwa shughuli maalumu the last week before examinations was ~n over to revision wiki ya mwisho kabla ya mitihani ilitengwa kwa ajili ya marudio. ~ up salimu amri. ~ somebody up (lose hope in) achana na, pigia mahuru; (colloq) acha, achana na she gave up her friend ameachana na rafiki yake (lose hope of seeing) -tomtarajia mtu, kata tamaa our mother arrived after we had ~n her up mama yetu aliwasili baada ya sisi kukata tamaa. ~ somebody up for lost kata tamaa (ya kumwona au kumwokoa). ~ somebody/one self/something up (to somebody) salimisha, kabidhi the bandit gave himself up to the police jambazi lilijisalimisha kwa polisi ~ up one's seat to someone pisha mtu. ~ something up acha. ~ up drinking acha kunywa pombe. ~ up the ghost -fa, aga dunia n hali ya kunyumbuka/pindika/ nepa/bonyea wooden chairs have no ~ up in them viti vya mbao havibonyei; (fig) (of a person) hali ya kujitoa/kushindwa/ kujisalimisha/ kukubali. ~ and take maafikiano, makubaliano there must be a ~ and take in settling any dispute lazima kuwa na maafikiano katika kusuluhisha ugomvi wowote. ~r n mpaji, mtoaji.

given pp of give.

gizzard n firigisi; finingi; (fig, colloq) koromeo it ticks in my ~ ni wazo/ jambo nisilopenda kabisa.

glace adj (of fruits) -liotiwa sukari;

(of leather, cloth) laini, iliyong'arishwa.

glacial adj 1 -a theluji, -a barafu,

-a enzi ya barafu the ~ era/epoch kipindi ambacho eneo la kaskazini mwa dunia lilifunikwa na barafu; (fig) -a baridi sana ~ manner tabia baridi. ~ly adv. glaciation n. glacier n mto (wa) barafu.

glad adj 1 (pred only) -enye furaha they will be ~ to hear watafurahi

glade

kusikia make ~ furahisha. 2 -a kufurahisha ~news habari za kufurahisha. give somebody the ~

eye (sl) tazama kibembe, kwa macho ya kurembua. give somebody the ~ hand (sl) karibisha, salimu kwa uchangamfu (hasa kwa lengo la kufaidi kitu). ~ rags n (sl) nguo za sherehe/tafrija. ~den vt. furahisha. ~ness n. ~some adj (liter) -a furaha. -kunjufu. ~ly adv.

glade n uwanja/uwazi (katika mwitu).

gladiator n (in ancient Rome) mtu

aliyefunzwa kupigana na watu au wanyama kwa silaha kwa ajili ya maonyesho. ~ial adj.

glamour (US glamor) n 1 heba/haiba,mvuto. 2 ubembe, uzuri unaovutia kimapenzi ~ girl msichana mwenye ubembe. glamorize vt -fanya kuwa zuri (kwa kupiga chuku). glamorization n.

glance vi,vt 1 ~ at tupia jicho, angalia kidogo, chungulia, tazama mara moja he ~d at his watch alitazama saa mara moja. 2 ~ at/ through/over/down pitia kwa haraka, pitisha macho. 3 ~ aside/ off(of weapon or blow) paruza. 4 (of bright objects, light) mweka, metameta. n 1 tazamo la haraka, mtupo wa jicho loving ~ tazamo la mahaba/kimapenzi cast a ~ tupia jicho. at a ~ kwa tazamo la haraka; mara moja. at first ~ kwa kuangalia mara ya kwanza; kwa kuangalia juujuu. 2 mweko (wa visu, mapanga, taa n.k.).

gland n 1 tezi swollen ~ (in groin) mtoki; (in throat) makororo, findofindo. adrenal ~ n tezi adrenali. 2 (bot) kitunga utomvu. ~ular adj -a (kama) tezi. ~ule n tezi ndogo.

glare n 1 mweko, mng'ao mkali. 2 jicho la hasira/ukali n.k. (fig) in the full ~ of publicity machoni mwa watu, hadharani. vi,vt 1 mweka. 2 ~(at) kazia macho. glaring adj 1 -a kutia kiwi. 2 kali. 3 -a waziwazi,

gleam

dhahiri. 4 (of colours) -siovutia.

glass n 1 kioo he has a ~ eye ana jicho la bandia. 2 kitu kilichotengenezwa kwa kioo; gilasi, bilauri give me a ~ of milk please tafadhali nipe gilasi ya maziwa he has had a ~ too much amelewa; darubini the captain looked through his ~ nahodha alitazama katika darubini yake; barometa. the ~ is falling kanihewa/anga inashuka; (also looking~) kioo; (pl) (rarely eye ~es) miwani I can't see without my ~es sioni bila miwani yangu; (binoculars) darubini ya vioo viwili. magnifying ~ n kioo cha kukuza kitu. 3 (compounds) ~-blower n mtengenezaji vyombo vya kioo agh chupa, bilauri n.k.. ~ cutter n mkataji vioo; kikata kioo. ~ house n jengo la kioo, kibanda cha kioo, (kwa kuotesha mimea). (prov) people who live in ~ houses shouldn't throw stones usiwalaumu wenzio ilihali wewe unatenda vivyohivyo. ~ware n vyombo vya kioo. ~-wool n nyuzi nyembamba za kioo. ~-works n (pl) kiwanda cha kioo. vt ~ (in) tia kioo (madirishani n.k.). ~ful n bilauri tele, glasi nzima. ~y adj 1 -a kama kioo. 2 (of the sea). -eupe. 3 (of a look/stare/eye) baridi.

glaucoma n glakoma: ugonjwa unaotanua mboni ya jicho na kutatiza kuona.

glaucous n,adj 1 -a kijani/buluu jivu. 2 (of leaves, etc) -enye mavumbi/ ukungu.

glaze vt,vi ~ (in) 1 tia/weka kioo. 2 ~ (over) ng'arisha; weka utando (wa kioo). 3 ~(over) (of the eyes) kauka, -wa baridi, poteza hisia. n mpako wa rangi ya kioo; ng'arisho. glazier n fundi wa kutia kioo (madirishani n.k).

gleam n 1 kimulimuli. 2 (fig) kiasi

kidogo, dalili ndogo (ya kutu-mainisha, kufurahisha n.k.) a ~ of hope dalili ya matumaini. vi ng'aa,

glean

mulika.

glean vt,vi 1 buga. 2 kusanya,pata kidogo kidogo (habari n.k.). ~er n mbugaji. ~ings n (pl) masazo ya mavuno; (fig) habari ndogondogo (zinazokusanywa hapa na pale).

glebe n 1 shamba lililowekwa wakfu (kwa matumizi ya dini au maskini). 2 (poet) shamba, ardhi.

glee n 1 raha (inayotokana na mafanikio). 2 wimbo wa kwaya. ~ club n kwaya, chama cha waimbaji. ~ful adj. ~fully adv.

glen n bonde jembamba.

glib adj 1 (of a person) -epesi wa

kusema (lakini si mkweli), -enye ulimi laini, -a maneno matamu (matupu). 2 (of words) rahisi a ~ answer jibu rahisi. ~ly adv. ~ness n.

glide vi nyiririka, teleza. n 1 kunyiririka, kuteleza. 2 (phonetics) kiyeyusho. ~r n (aviation) nyiririko. gliding n mchezo wa kunyiririka.

glimmer vi mulika kidogo kidogo n

mwangaza hafifu (wa taa, mshumaa n.k.), kimeto; (fig) dalili there's not a ~ of hope hakuna dalili ya matumaini hata kidogo.

glimpse n tazamo la mara moja, kuona kidogo tu. vt (also ~ of) ona mara moja.

glint vi metemeta; ng'aa. n kimeto.

glissade vi teleza. n kuteleza.

glisten vi nang'anika, mweka mweka, meremeta, waka her eyes ~ed with tears macho yake yalilengalenga machozi.

glitter metameta, ng'aa n kimulimuli, kimeto. ~ing adj -a kuvutia, -a kumetameta.

gloaming n (poet) the ~ n utusitusi wa jioni.

gloat vi ~ (over something) angalia (kwa wivu/uchoyo/ubaya/husuda); chekelea/cheka (kwa bezo/inda). ~ingly adv.

globe n 1 tufe, mviringo. the ~ dunia. 2 ramani ya tufe. 3 bakuli la mviringo la kioo.~-fish n bunju.

glow

~-trot vi zunguka dunia, safiri nchi nyingi. ~-trotter n msafiri duniani, mtembezi sana. global adj -a ulimwengu; -a jumla. globally adv. globule n tone. globular adj -enye umbo la tufe, -enye umbo la tone.

glockenspiel n marimba ya chuma.

gloom n 1 utusitusi. 2 (sorrow) huzuni, majonzi, ghamu, sononeko cast a ~ over tia ghamu, sonenesha, huzunisha. ~y adj 1 -a gizagiza. 2 -a huzuni,-a ghamu -zito become ~y sononeka, kuwa na huzuni see the ~y side of things ona ubaya tu.

glory n 1 sifa kuu, adhama. 2 uzuri. 3 fahari the glories of Zimbabwe fahari za Zimbabwe. 4 hali ya kuwa tukufu; utukufu (wa Mungu na malaika) G ~ to God in the highest Utukufu kwa Mungu juu. 5 raha ya mbinguni go to ~ fariki dunia. ~-hole n chumba/dawati lenye vikorokoro vi jivunia, furahi. glorify vt tukuza; adhimisha, faharisha, kuza. glorification n. glorious adj 1 adhimu. 2 -a kuleta sifa kuu. 3 (colloq) -a kupendeza; -a kufurahisha have a glorious time furahi sana. 4 (ironic) -ubaya sana it's a glorious mess! ni fujo tupu! gloriously adv.

gloss1 n 1 mng'ao, king'aa uwongo. ~ paint n rangi inayong'aa. 2 sura (danganyifu). vt ~ over sitiri, funika. ~y adj. ~iness n.

gloss2 n maelezo, ufafanuzi. vt,vi fasiri, fafanua. ~ary n sherehe, faharasa.

glottis n koo. glottal adj -a koo/glota. glottal stop sauti ya koo/glota.

glove n glavu. be hand in ~ with kuwa chanda na pete na. fit like a ~ kaa sawasawa. handle somebody without ~s bishana vikali/bila huruma handle with kid ~s shughulikia kwa hadhari sana. ~ compartment n kidawati/kishubaka garini.

glow vi 1 ng'aa, waka (bila kutoa ndimi za moto). 2 (fig) waka; chachawa, sisimka ~ with pride sisimka kwa fahari n mng'aro the ~

glower

of the sky at sunset mng'aro wa mbingu wakati wa magharibi. ~-worm n kimulimuli. ~ing adj -a kung'ara; (fig) -enye shauku. ~ingly adv.

glower vi ~ (at) kunja uso, tazama

kwa hasira au kwa kutisha. ~ingly adv.

glucose n glukosi.

glue n gundi. vt 1 ~ (to) ganda; gandisha, natisha (kwa gundi) ~ up a broken object unga kwa gundi kitu kilichovunjika. 2 kazia, ambatana, ganda his eyes were ~d to the picture alikodolea macho picha Mary is always ~d to her mother Mary anamganda mama yake, habanduki kwa mama yake. ~y adj.

glum adj -enye masikitiko, -enye uzito wa moyo/jitimai. ~ly adv. ~ness n.

glut vt ~ (with) 1 sheheneza, furisha, jaza sana. 2 kula mno; shiba kupita kiasi. n furiko, ulevi. ~ton n 1 mlafi. 2 mpenzi mkubwa wa kitu fulani a ~ ton for work mpenda kazi sana. ~ tonous adj lafi. ~ ton ously adv. ~tony n ulafi.

gluten n protini inayobaki baada ya

kutoa wanga. glutinous adj -a kunata.

glycerine (US glycerin) n gliserini.

gnarled adj (of tree trunk) -enye vifundo vingi, -a kupindapinda, -a vinundunundu; (of hands/ fingers) -a misuli iliyokakamaa, -liofinyangika, -liovingirika.

gnash vt,vi (of teeth) kereza, saga meno.

gnat n aina ya visubi; (fig) jambo dogo linaloudhi. strain at a ~ sita kwa jambo dogo.

gnaw vt,vi 1 ~ (at) tafuna; guguna, ng'wenya the rats ~ed a basket panya waliguguna kapu. 2 ~ (at) (of feelings) tesa, sumbua, udhi.

gnome n (in tales) kizimwi (kinachoishi chini ya ardhi na kulinda dafina) the ~s of Zurich wenye mabenki Uswisi.

gnu n kongoni.

go vi 1 ~ (from to) -enda, ondoka she

go

will ~ to Arusha atakwenda Arusha let them ~ waache waondoke. ~ away nenda zako all hope has gone matumaini yote yameondoka. 2 kaa, -wa mahali pake pa kawaida where does the book go? kitabu kinakaa wapi?; ingia (ndani ya). 3 ~ (from/ to) fika, fikia the river ~es to the ocean mto huu hufika baharini the differences between the friends ~es back a long way kutoelewana kwa hawa marafiki wawili ni kwa muda mrefu. ~ a long way (last) dumu he makes his wages ~ a long way hutumia mshahara wake kwa uangalifu; (endure) (colloq) -wa kiasi cha kuvumilika. ~ a long way/far towards doing something changia, saidia. ~ (very) far dumu; (of a person, future tense) fanikiwa. ~ too far vuka mpaka, zidi you've ~ne too far! umezidi. ~ (any) further pita/kiwango fulani I've ~ne as far as I can in this job I can't ~ any further nimefikia kikomo changu katika kazi hii. ~ as/so far as to do something thubutu. as far as it ~es kwa kiasi fulani. His views are valid as far as they ~ hoja zake ni za msingi kwa kiasi fulani. ~ to great lengths/ trouble (to do something) jitahidi/hangaika sana; -wa mwangalifu kufanya jambo vizuri. ~ as low/high as (of a price) shuka/panda hadi, fikia kiwango fulani. ~ one better (than somebody) fanya vizuri zaidi (kuliko mtu mwingine). 4 ~ on a journey/trip/outing safiri, fanya safari. ~ for a walk/swim enda kutembea/kuogelea. ~ walking tembea. 5 (in the pattern ~ prep n) enda (mahali palipodhamiriwa). ~ to school enda shule. ~ to church enda kanisani. ~ to sea -wa baharia. 6 ~to somebody -wa mali ya mtu, rithiwa, gawiwa, enda kwa when the man died his property went to his grand children mtu yule

go

alipokufa mali yake iligawiwa/ ilirithiwa na wajukuu zake the gold medal went to Bayi medali ya dhahabu ilienda kwa Bayi. 7 -wa he went red with rage aliwiva kwa hasira he will ~ mad atakuwa kichaa. ~ broke ishiwa fedha; -tokuwa na fedha. ~ flat (of liquid) -tokuwa na gesi. ~ native iga maisha ya wenyeji. ~ put (colloq of machines) haribika (fig) my project has gone put mradi wangu umeharibika. ~ scot-free/ unchallenged/unpunished -toadhibiwa, -topingwa. 8 fanya kazi, enda my watch is not ~ing saa yangu haiendi, haifanyi kazi. a ~ing concern n shughuli hai iliyostawi I've been ~ ing all day nimekuwa nikifanya kazi siku nzima. 9 zoea, -wa katika hali fulani (kila mara) you need not ~ armed while in town huhitaji kuwa na silaha unapokuwa mjini she is six months ~ne ana mimba ya miezi sita. 10 (after How) endelea How's the work ~ing? Kazi inaendeleaje? His plans are ~ing well mipango yake inaendelea vizuri. ~ easy (on/with somebody/ something) -tokuwa mkali, fanyia uungwana; wa mwangalifu; -wa mpole ~ easy asteaste! ~ slow (of traffic) sota, enda pole pole; (of workers in factories etc) fanya mgomo baridi. ~ slow n mgomo baridi. be ~ing strong endelea kusitawi, -wa na

nguvu bado Born in 1900 but still ~ing strong alizaliwa 1900 lakini bado ana nguvu. 11 tumia, fanya kazi kwa this car ~es by petrol gari hili linatumia petroli. 12 (in progressive tense only) patikana that's the best house ~ing hii ndiyo nyumba bora inayopatikana. 13 ~ (to somebody) for uzwa kwa bei (fulani) the radio went cheap radio iliuzwa kwa bei rahisi. 14 ~ on/in (of money) tumika kwa half my income ~es on food nusu ya pato langu hutumika kwa

go

chakula. 15 telekezwa, potea his sight is ~ing uwezo wake wa kuona unapotea. 16 semekana, sadikiwa the story ~es that.... inasemekana kuwa... 17 kwa wastani, kwa jumla, ilivyo. as people ~ watu walivyo kwa wastani one hundred and fifty for a button is not bad as things ~ today bei ya shilingi mia moja na hamsini kwa kifungo kimoja sio mbaya sana ukifikiria jinsi bei ya vitu ilivyo siku hizi. 18 anguka, poromoka, angamia first the roof and then the walls went in the storm paa liling'oka kwanza kisha kuta ziliporomoka she is far gone yu mahututi; (colloq) yu mwenda wazimu. let oneself ~ jifurahisha. 19 -fa he has gone amekufa. dead and ~ne amekufa na kuzikwa. 20 amuliwa The election went in his favour alishinda uchaguzi. 21 (various phrases) ~ it tenda kwa bidii; jiingiza katika ubadhirifu. ~ it alone fanya pekee (bila msaada). 22 (of words, tune) pangiliwa I'm sure of how the words ~ nina hakika jinsi maneno yanavyo pangiliwa. 23 (colloq as informal request) enda ~ and dust the table nenda kafute meza now you have ~ne and done it ((sl) umeshaharibu. 24 toa mlio au sauti maalum `Bang'went the door mlango ulijifunga `mba'. 25 (of competitors in a race) anza ready, steady ~ kuwa tayari, kaa sawasawa, anza (kukimbia) here ~es haya tunaanza. 26 (to express future) -ta I'm ~ing to live on campus nitaishi chuoni we are ~ing to have rain today huenda mvua itanyesha leo my son is ~ing to be ten tomorrow mwanangu atatimiza umri wa miaka kumi kesho. 27 ~ as you please (atrrib adv) huru. 28 (idiomatic uses) ~ about tembea, randaranda; (of rumours, stories) enea; (of a ship) badili njia. ~ about something anza kuifanya kazi.

go

please ~ about it more carefully tafadhali ifanye kwa uangalifu zaidi. ~ about one's business jishughulisha na mambo yako. ~ about with somebody fuatana na, -wa na mtu mwingine mara kwa mara. ~ after/something jaribu kupata kitu fulani. ~ against somebody pinga do not ~ against your employer usipingane na mwajiri wako; elekea/tokea vibaya the game is ~ing against them wanaelekea kushindwa. ~ against something enda, -wa kinyume na it will not ~ against my tastes haitakuwa kinyume na vionjo vyangu. ~ ahead endelea they are ~ ahead people ni watu wanaopenda maendeleo may I leave? yes ~ ahead naweza kuondoka? ndiyo bila wasiwasi. ~ ahead n ruhusa ya kuendelea. ~ along endelea: the lessons will be easy as you ~ along masomo yatakuwa rahisi kadiri unavyoendelea. ~ along with somebody sindikiza, fuatana na she will ~along with her boy friend atamsindikiza mpenzi wake; (agree) kubaliana na we can't ~ along with him on that argument hatuwezi kukubaliana na yeye katika hoja ile. ~ at somebody/something shambulia, vamia they went at it tooth and nail/hammer and tongs walishambuliana vikali; shughulikia kikamilifu. ~ away ondoka. ~ away with somebody ondoka na, chukua she has ~ne away with my book ameondoka na kitabu changu. ~ back rudi; rudi nyuma our friendship ~es back to the 1960s when we were at Makerere urafiki wetu ulianza zamani katika miaka ya 60 tulipokuwa Makerere. ~ back on/upon vunja (k.m. ahadi). ~ before (something) tangulia. ~ behind tafuta. ~ behind somebody's back sengenya, fanyia mtu kitu pasipo yeye kujua. ~ beyond something vuka mpaka, zidi you are ~ing beyond your

 

go

responsibility umevuka mpaka wa madaraka yako that's ~ing beyond a joke imezidi. ~ by pita he went by in a hurry alipita haraka sana. ~ by something fuata, ongozwa na ~ by the book fuata sheria barabara. ~ by/under the name tumia jina (fulani), itwa (fulani). ~ -by n. give somebody/something the ~-by (colloq) puuza, dharau. ~ down (of a ship) zama; (of the sun, moon) tua; (of food and drink) telemka, mezwa the piece of meat won't ~ down siwezi kuimeza nyama hii; ondoka chuo kikuu (baada ya kuhitimu; (of the sea, wind etc) pungua, tulia; (of prices) poa, shuka the price of meat has ~ne down bei ya nyama imeshuka. ~ down to the coast/ village tembelea pwani/kijijini n.k. ~ down before somebody shindwa au pinduliwa. ~ down (in something) andikwa; kumbukwa you will ~ down in history as a hero utakumbukwa kuwa shujaa mkuu. ~ down to be endelea the liberation of man ~es down to the present century ukombozi wa binadamu umeendelea hadi karne hii. ~ down (with somebody) (of a story) kubaliwa, pendwa (na msikilizaji) the story won't ~ down with my son mwanangu hatapenda hadithi hii the idea of the second wife does not ~ down well with the first wife fikra za kuoa mke wa pili hazikubaliwi na mke wa kwanza. ~ down (with something) ugua; pata ugonjwa the beggar has gone down with cholera yule ombaomba amepata kipindupindu. ~ for somebody -enda kumchukua (fulani) ~ for the children enda kuchukua watoto; shambulia the audience went for me in the seminar wasikilizaji walinishambulia katika semina; husu what I said about your friends ~ es for you too nilichosema kuhusu rafiki zako kinakuhusu na wewe pia; penda I don't ~ for detective nowels

go

sipendi riwaya za upelelezi. ~ for nothing/little puuzwa; -tothaminiwa. ~ forth (formal) tolewa. ~ forward enda mbele; endelea. ~ in ingia (of the sun, moon etc) funikwa na mawingu; ingia mashindanoni. ~ in for something fanya, shiriki (katika mtihani; mashindano n.k.). ~ into something ingia ~ into the army ingia jeshini; (investigate) peleleza, chunguza kwa makini ~ into fits of laughter kauka kucheka. ~ into mourning vaa nguo nyeusi kama ishara ya msiba. ~ off (explode) lipuka; fyatuka; (go bad) poteza uzuri/ubora; (of milk) ganda; (of meat etc) oza; (of fish) china; (sleep) lala; poteza fahamu; (sale of goods) uzwa rahisi; (of events) enda/endelea (vema) the discussion went off well mjadala uliendelea vema; (as a stage direction in a printed play) toka jukwani. ~ off somebody/ something chushwa na; kinai. ~ off with somebody/something iba, toweka na (kitu), torosha He has ~ne off with your sister amemtorosha dada yako. ~ on (of time) pita As days went on kadiri siku zilivyopita; (behave) endelea na tabia (hasa mbaya) if she ~es on like this she will be divorced akiendelea na tabia hii atatalikiwa; (happen) tokea, endelea kufanyika there is nothing ~ing on there hakuna lolote linalofanyika pale; (theatre) tokea jukwaani; (take one's turn) fanya zamu. tell him to ~ on mwambie afanye zamu yake. ~ on something kubali, saidiwa na (k.m. ushahidi). ~ on the dole/social security (US) welfare lipwa posho na serikali wakati wa kukosa ajira. ~ on the pill anza kutumia vidonge vya kuzuia mimba. ~ on about something ongea kirefu, bwata. ~ on (at somebody) gombeza, kefyakefya, zoza. be ~ing on (for) (of age/time) karibia I'm ~ing on (for) fifty nakaribia miaka hamsini. be ~ne on

go

(sl) pumbazwa. ~ on to something/ to do something endelea (na) ~ on to the next item on the agenda endelea na dondoo linalofuata katika ajenda. ~ on (with something/doing something) endelea, vumilia. ~ on (with you)! (colloq) ondoka hapa. ~ings-on n pl (colloq) matukio, mambo (agh. ya ajabuajabu). on ~ing adj -enye kuendelea. ~ out toka, ondoka (chumbani, nyumbani n.k.); toka (kwenda kwenye burudani karamu n.k.; (of fire, light) zimika; (of fashion) -wa zilipendwa; (of a government) acha madaraka, jiuzulu (kutoka madarakani); (as used by the workers) goma. we shall get better by ~ing out tutapata mishahara mizuri zaidi kwa kugoma; (of a year) isha. ~ out to hama nchi yako; safiri. ~ out to somebody (of the heart, feelings) hurumia, -wa pamoja na. ~ out with somebody (colloq) -tembea na, -wa mpenzi wa. ~ over (colloq) pokelewa, furahisha the game did not ~ over well with the spectators mchezo haukuwafurahisha watazamaji. ~ over something chunguza kwa makini; (review) rudia. ~ing over n (colloq) kuchunguza; uchunguzi; (sl) piga; (beating) kung'uta they gave him a thorough ~ing -over walimkung'uta. ~ over to somebody/something badili kitu kimoja kwa kingine he went over to Rex amebadili sigara aliyokuwa akivuta kwa Rex. ~ round tosheleza wote we don`t have enough drinks to ~ round hatuna vinywaji vya kuwatosheleza wote; zunguka. ~ round (to a place/ to do something) zuru, tembelea, tembea. ~ round the bend (colloq) pata wazimu, kasirika, -wa mwehu. ~ through pitishwa, idhinishwa the motion did not ~ through pendekezo halikuidhinishwa. ~ through something (of discussion)

go

jadili kwa undani; (paper, book etc) pitia; (search) pekua, shiriki; (suffer) teseka, pitia you `ll have to ~ through the hardships utalazimika kuteseka; (of a book, edition etc) uzwa; maliza, tumia (fedha). ~ through with something timiza, kamilisha, endelea hadi mwisho. ~ to/towards something changia, saidia kufanya the savings will ~ towards the car I want to buy akiba itachangia fedha za kununulia gari nililokusudia. ~ together enda pamoja, ambatana war and famine ~ together vita na njaa huenda pamoja; endana, chukuana the black coat and white

shirt ~ together koti jeusi na shati jeupe vinachukuana. ~ under zama; fig) shindwa; (of business) filisika. ~ up panda the prices will ~ up bei zitapanda; (of buildings) jengwa; (explosion, fire) lipuliwa, teketezwa; ingia chuo kikuu; -enda mjini (agh. mji mkuu). ~ up something panda, kwea mlima, mti, ngazi. ~ with somebody/something ambatana; fuatana ~ with him fuatana naye; (of views etc) kubaliana; (together) enda pamoja; ambatana the table ~es with the dining chairs meza inaambatana na viti vya kulia; (match) chukuana this suit doesn`t ~ with white shoes suti hii haichukuani na viatu vyeupe; (colloq) (of a young man and a girl) tembea/fuatana. ~ without (something) kosa, vumilia kutokuwa (na kitu fulani) you will have to ~ without a breakfast utalazimika kuvumilia kukaa pasipo kifungua kinywa ~ without saying inafahamika pasi kuelezwa, bila kupingwa. ~ing n 1 hali ya njia, barabara kwa matembezi n.k. go while the ~ing is good ondoka wakati hali inaruhusu. 2 kuondoka (usu) (pl) (lit, and fig). comings and ~ings kuja na kuondoka. 3 mwendo, kasi. n (all uses colloq) all systems ~ mambo tayari (kuondoka). all the ~ -enyewe, -a kisasa. at one

god

~ kwa mpigo mmoja. be full of ~; have plenty of ~ -wa na bidii/juhudi nyingi. be on the ~ shughulika. have a ~ (at something) jaribu. near ~ ponea chupuchupu. no ~ mwanzo mbaya; (impossible situation) hali isiyowezekana/mbaya it's no ~ asking to ~ to the disco haiwezekani kuomba kwenda disko. no ~ area eneo lililopigwa marufuku. ~ between msuluhishi; tarishi; (of a marriage) mshenga; (of seduction) kuwadi.

goad n 1 mkosha, fimbo (ya kuswaga ngo'mbe). 2 (stimulus) mchocheo, kichocheo. vt swaga; chochea.

goal n 1 kikomo, mwisho (wa mbio). 2 (football posts) goli; (score) bao,

goli. ~ keeper n (~ie colloq) n golikipa, mlinda mlango. ~ line n mstari wa goli. ~ post n nguzo ya goli. ~ mouth n golini. 3 (in life etc) lengo.

goat n mbuzi. he-~ n beberu; denge la mbuzi. she ~ (or nanny ~) n mbarika. get one's ~ (sl) udhi, kasirisha. play/act the giddy ~ fanya upumbavu. separate the sheep from the ~s tenga wema na wabaya. ~ee n ndevu (kama) za mbuzi (beberu). ~ -heard n mchunga mbuzi. ~skin n vazi lililotengenezwa kwa ngozi ya mbuzi.

gob1 n (vulg) ute unaoteleza, fundo

(la mate).

gob2 n (derog sl) mdomo. shut your ~ funga kidomo/bakuli lako.

gob3 n (US sl.) baharia, mwanamaji.

gobbet n tonge; (of meat) chinyango. gobble1 vt ~ up -la kwa pupa.

gobble2 vt gooka.

gobbler n bata mzinga dume. gobbledygook Kichina; lugha isiyoeleweka.

goblet n bilauri (agh ya divai).

gobblin n zimwi, jini, afriti.

go-cart n gari la mkono.

god n 1 mungu. the ~s n miungu. 2

godown

G~ n Mungu, Mola, Allah, Muumba. G~ willing Mungu akipenda G~ be with you Mungu awe nanyi G~ forbid! ~ preserve us! Mungu aepushie mbali G~'s truth! haki ya Mungu! thank G~! shukuru Mungu. 3 mungu mdogo he thinks he is a ~ anajifanya mungu mdogo. 4 (theatre) the ~s n viti vya juu. 5 (compounds) ~child n; ~daughter/~son n mtoto wa ubatizo. ~father/~mother n baba/mama wa ubatizo. ~-damn (ed)/(US) ~dam adv,adj (sl vulg) mno, sana. ~ fearing adj -chaji mungu, -cha mungu. ~forsaken adj 1 (of place) -a ovyo, baya sana, la kukatisha tamaa. 2 G~'s acre n (old use) makaburini, uwanja wa kanisa. ~s end n bahati kubwa (isiyotegemewa). ~speed n wish somebody ~speed takia mtu safari ya heri. ~dess n Mungu wa kike. ~head n uungu. the G~head mungu. ~less adj kafiri, -siomjua/-siotambua Mungu, -ovu. ~like adj -a kimungu, kama mungu. ~ly adj -enye kucha mungu. ~liness n.

godown n ghala, bohari.

go-getter n (colloq) mwenye bidii, jasiri.

goggle vi ~ (at) kodolea macho. ~-box n (sl) televisheni. ~-eyed adj -enye macho ya gololi/tunguja. ~s n miwani mikubwa ya kuzuia upepo, maji, vumbi n.k.

goitre n tezi.

gold n 1 dhahabu. worth one's weight in ~ -enye thamani kubwa, muhimu sana. 2 utajiri. 3 (fig) kitu cha thamani sana; tabia nzuri a heart of ~ moyo mkunjufu/mkarimu. 4 rangi ya dhahabu. ~ beater n mtengeneza mabamba ya dhahabu, mfua dhahabu. ~-digger n mchimba dhahabu; (sl) mwanamke anayetafuta mapenzi kwa sababu ya hela. ~ field n machimbo ya dhahabu. ~-dust n mavumbi ya dhahabu. ~-foil; ~-leaf n jaribosi/ bamba/karatasi ya dhahabu. ~mine

good

n mgodi wa dhahabu; (fig) mradi wa utajiri/tija. ~-plate n vyombo (vijiko, sahani n.k.) vya dhahabu. ~-rush n kikaka cha kutafuta dhahabu iliyogunduliwa. ~ smith n sonara, mfua dhahabu. ~en adj 1 -a dhahabu, kama dhahabu, -enye rangi ya dhahabu. 2 -a thamani sana, -a tunu; -zuri mno a ~en opportunity nafasi ya kufaa sana. the ~en age n (katika hadithi za kiyunani) zamani za ustawi, heri na furaha kubwa; kipindi cha upeo wa ustawi wa fasihi na sanaa. ~en handshake n kiinua mgongo kikubwa anachopewa mtu wa cheo anapostaafu. the ~en mean n kanuni ya kutovuka mpaka/ya suluhu (katika tabia ya mtu). the ~en rule n kanuni ya muhimu/ya msingi/gezi (k.m. watendee wenzio kama unavyopenda kutendewa). ~en wedding n maadhimisho ya miaka 50 ya ndoa.

golf n gofu vi cheza gofu. ~ball n mpira wa gofu. ~-club n 1 klabu ya gofu. 2 kigoe/kingoe cha gofu. ~-course n uwanja wa gofu. ~er n mchezaji wa gofu.

Goliath n Goliati; (fig) pandikizi la

mtu.

golliwog n mwanasesere mweusi.

golly int (sl) loo! tamko la kuonyesha mshangao.

golosh n see galosh.

gondola n gondola: mtumbwi/mashua ndefu iliyotumika katika mifereji ya Venice ~ car jukwaa la bidhaa la reli. gondolier n mwendesha gondola.

gone pp of go.

goner n (sl) kitu kilichoharibika kabisa/liokwisha.

gong n upatu; (sl) nishani, medali. vt

ashiria kwa upatu.

goniometer n goniometa (kipima

pembe).

gonna (US sl) going to see go.

gonorrhoea/rhea n kisonono.

good adj 1 -ema, -zuri a ~ car gari zuri a ~ blade (i.e. sharp) wembe

good

mkali. 2 -a kufaa; -a maana. 3 -enye kumudu/kuweza kutenda, hodari, bora she is a very ~ teacher yeye ni mwalimu hodari sana. 4 -a kupendeza, -a manufaa the news he brought was ~ habari alizotupasha zilitupendeza. have a ~ time jifurahisha (colloq) a ~ time girl msichana mpenda starehe tu. (all) in ~ time kwa wakati unaofaa. be a ~ thing -wa jambo la manufaa lower taxes are a ~ thing for all the people kodi nafuu ni jambo la manufaa kwa watu wote. be a ~ thing that -wa na bahati kuwa. have a ~ night lala vizuri. start/arrive/in ~time anza/fika/ondoka mapema. put in/say a ~ word for somebody tetea mtu. 5 fadhili, karimu be ~ enough to tafadhali. be ~ to somebody fadhili mtu. (in exclamations of surprise, shock etc) ~God!~ Heavens! Mungu wangu! subuhana. 6 kamili, -a kutimiza, mno give somebody a ~ scolding mkaripie mno he had a ~ excuse alikuwa na kisingizio/sababu nzuri. have a ~ mind to do something tamani, -wa na hamu kubwa kufanya kitu. all in ~ time wakati utakapowadia. 7 kakamavu, -enye nguvu her hearing is still very ~ bado anasikia vizuri. 8 -a kuchekesha she told us a ~ story alitusimulia hadithi ya kuchekesha as ~ as a play kichekesho, senema ya bure. 9 -a kufaa kuliwa, -pya, -bichi this meat is still ~ nyama hii bado inafaa kuliwa. 10 -a kuaminika, -a hakika the brakes on this car are ~ breki za gari hili zinaaminika ~ for 1000/= inayofaa kwa sh 1000/= my car is ~ for another two years gari langu litafaa kwa muda wa miaka miwili ijayo be ~ for a ten mile walk -wa tayari kutembea maili kumi this ticket is ~ for one year tiketi hii inafaa kwa muda wa mwaka mmoja. 11 (of behaviour) -enye adabu; -pole a ~ child mtoto mwenye adabu. as ~ as gold -ema sana/tulivu. 12

good

adilifu. a ~ person n mtu mwadilifu. ~ works n misaada, fadhila kwa wasiojiweza. 13 sawa I thought it ~ niliona sawa. 14 (in forms of greetings) ~ morning/afternoon/evening hujambo? habari za asubuhi/ mchana/jioni. ~ morning subalkheri. ~afternoon masalkheri. ~night alamsiki, usiku mwema. 15 (as a polite but often ironical, patronizing or indignant form of address) my ~ man mume wangu (we). your ~ lady mke wako. the ~ people malaika. 16 (considerable) -ingi it takes a ~ deal of time inachukua muda mrefu. 17 zaidi ya, si chini ya we waited for a ~ hour tulingojea kwa zaidi ya saa moja. 18 mno a ~ deal of money fedha nyingi mno. 19 as ~ as sawa na he is as ~ as called me a thief aliyoyasema ni sawa na kuniita mwizi. 20 make ~ faulu, shinda, fanikiwa he made ~ as a mechanic alifaulu katika kazi yake ya umakanika. make something ~ fidia make ~ a loss fidia hasara, timiza (shabaha, haja) they made ~ their escape walitimiza shabaha yao ya kutoroka the wall will have to be made ~ before painting itakubudi kutengeneza ukuta (kuziba nyufa n.k.) kabla ya kupaka rangi; thibitisha madai. 21 (phrases and compounds) ~ breeding n adabu, uungwana; jamala. ~ fellowship n adj uhusiano mzuri, urafiki mwema; ukunjufu. ~ for-nothing n, adj -onyo; nyangarika. ~ hearted adj -pole. ~ humoured adj changamfu, -enye uchangamfu. ~ looking adj -enye sura ya kupendeza, jamili. ~ looks n sura ya kupendeza. ~ luck n bahati njema. ~ money n fedha halisi; (colloq) mshahara mzuri. throw ~ money after bad poteza fedha kwa kujaribu kunusuru zilizopotea. ~ natured adj tulivu, -karimu. ~

goods

neighbour n jirani mwema. ~ sense n busara. ~-tempered adj -pole. n 1 (kitu) chema/adili/-a faida/-a thamani. do ~ auni, saidia. for the ~ of kwa manufaa/faida ya. do somebody ~ nufaisha mtu. be up to no ~ tenda/jishughulisha na maovu. be no/not much/any/some ~ (-wa) kazi bure, -tosaidia. 2 for ~ kabisa. 3 to the ~ faida. 4 (pl) wema, -wa bora. ~-bye int n kwa heri say ~-bye to aga; agana na. G~ Friday n Ijumaa Kuu. ~ish adj kubwa, mbali/zuri kidogo a ~ distance away mbali kidogo ~ food chakula kizuri kiasi. ~ly adj 1 -zuri, -enye sura mwanana. 2 -ingi, kubwa. ~ness n 1 wema, uzuri, hisani. have the ~ ness to kwa hisani yako. 2 (strength, quality) nguvu, utamu (in exclamations) G~ness Gracious/G~ness me! Mungu wangu! Thank ~ness! shukuru Mungu! ~ness knows! sijui!; Mungu Shahidi! ~will n 1 urafiki, ukarimu, mapenzi. 2 (of trade) sifa njema, jina. ~y n (colloq) peremende; halua; kitu kizuri. ~y n mtu ajifanyaye kuwa mtakatifu.

goods n (pl) 1 bidhaa, mali inayohami- shika. ~ and chattels n (leg) mali ya mtu. 2 shehena, mizigo (ichukuliwayo na garimoshi n.k.). ~ train n (US) (freight train) gari (moshi) la mizigo. piece of ~ (colloq) mtu.

goof n (sl) mjinga; mpumbavu. vt,vi ~ (of) fanya jambo la kijinga, bananga.

goon n (sl) 1 mjinga; zebe. 2 (US) mtu anayeajiriwa kutisha watu.

goose n 1 bata bukini. cook somebody's ~ zima mtu; komesha. kill the ~ that lays the golden eggs (prov) haribu cha baadaye kwa tamaa ya sasa, kula mbegu. be unable to say boo to a ~ -wa mwoga sana. all one's geese are swans chongo kuona kengeza, sifu mno kila kitu. ~-flesh n kimbimbi. ~step n kwenda bila

Goth

kukunja magoti. 2 mbumbumbu. gosling n mtoto wa bata maji/bukini.

gooseberry n zabibubata. play ~berry -wa kisikimtu wa wapenzi wawili.

Gordian adj (only in) ~ knot n fundo/ fumbo gumu kufungua; jambo gumu (kutatua). cut the ~ knot tatua tatizo kwa nguvu au bila kujali masharti.

gore1 n damu iliyoganda. gory adj

-enye/ -liotapakaa damu; -a kumwaga damu, -a kikatili.

gore2 n (of cloth) kijambia; pembe;

kipande cha pembe tatu cha nguo n.k.. vt piga pembe, guta.

gorge1 n 1 korongo. 2 umio; vilivyo

kwenye matumbo it made his ~ rise kilimtia kichefuchefu; kilimuudhi.

gorge2 vi,vt ~ (oneself) (on/with something) lafua. n ulafi, kuvimbiwa.

gorgeous adj 1 -zuri sana, -enye marembo (mapambo) mengi. 2 -a kufurahisha, -a kupendeza, tamu. ~ly adv.

Gorgon n (Gk myth) Gogoni: mmoja wa ndugu wa kike watatu wenye nywele za nyoka; mtu anayetisha; mwanamke anayechukiza.

gorilla n sokwe.

gosh int (sl) (also by ~) kumbe, loo.

gosling n see goose.

gospel n 1 G~ injili. 2 (doctrine, tenets) imani. 3 ~ truth n (jambo la) kweli kabisa.

gossamer n 1 utando. 2 kitambaa cha shashi nyepesi sana (attrib) a ~ veil veli ya shashi nyepesi.

gossip n 1 umbeya, udaku. 2 uandishi wa habari za watu za binafsi k.m. katika gazeti. (attrib) the ~ column n safu ya habari za binafsi. 3 (chat) soga, maongezi. 4 mbeya, mdaku vi sema/andika habari za binafsi; piga domo/umbeya.

got pp, pt of get.

Goth n 1 Mgothi (kabila mojawapo la

Ujerumani); mshenzi. G~ic adj 1 -a Kigothi; -a Wagothi. 2 (arch) -a matao yaliyochongoka; (of printing

gotta

type) -nene; -a kijerumani. n (of language) Kigothi (archit) mjengo wa Kigothi.

gotta (Us sl have got to ) ni lazima.

gotten (US) pp of get.

gouache n rangi ya maji; upakaji wa rangi hiyo.

gouge n patasi, bobari, ukombe. vt ~

(out) chimba kwa ukombe; toa, ngo'a. ~ out somebody's eye toa jicho.

goulash n nyama na mboga iliyoto- koswa na kutiwa pilipili hoho, supu (ya nyama).

gourd n kitoma, kibuyu.

gourmand n mlafi, mtu apendaye chakula. gourmet n kidomo (wa chakula); mjuzi wa kuchagua chakula kizuri, mvinyo n.k. gormandize vi lafua, -la sana

gout n jongo. ~y adj -enye jongo.

govern vi,vt 1 tawala. 2 (control) zuia; dhibiti ~ one's temper zuia hasira. 3 (usu passive) ongoza be ~ed by the opinions of others ongozwa na mawazo ya watu wengine. 4 (gram esp of verb or prep) miliki, goeka. ~ing adj -enye kutawala, -a utawala. ~ance n utawala; uongozi; udhibiti. ~ment n 1 serikali. G~ment House n Ikulu. responsible ~ment n serikali ya madaraka. 2 utawala democratic ~ment utawala wa kidemokrasi adj -a kiserikali. ~or; guv'nor n 1 gavana. G~or General n Gavana Mkuu. 2 mjumbe wa bodi ya shule, hospitali n.k. 3 (colloq) mkuu; mwajiri; baba; (sl) bosi. 4 kirekebisho kinachojiendesha (katika mashine, kudhibiti gesi, mvuke n.k) msimamizi. 5 (tutor) mlezi. ~ess n mwalimu wa kike wa watu binafsi/ wa familia fulani.

gown n 1 gauni. 2 joho (linalovaliwa agh. na majaji, wahadhiri n.k.). vt visha. ~ed solicitor n mwanasheria mwenye joho.

grab vt ~ (at) nyakua; chopoa. n 1 unyakuzi make a ~ at something nyakua kitu. up for ~s (US sl) -enye

gradation

kupatikana kwa urahisi. 2 kinyakulio. ~ber n mpendapesa; mnyakuzi. land ~ber n mnyakuzi ardhi.

grabble vi tutusa; chakura; tambaa.

grace n 1 (elegance) uzuri, madaha,

madahiro, matuko. 2 airs and ~s namna ya kusema/kutenda iliyokusudiwa kuleta mvuto. 3 huba, upendeleo, hisani, nia njema. an act of ~ jambo la hiari/bure/upendo. days of ~ muda wa nyongeza (unaoruhusiwa baada ya siku ya kudaiwa kupita). be in somebodys good ~s ungwa mkono/pendelewa na. 4 have the ~ to do something tambua kuwa ni haki na sawa kufanya jambo. do something with a good/bad ~ fanya jambo kwa hiari/shingo upande. 5 sala ya mlo. 6 Rehema na neema za Mungu. in a state of ~ katika hali ya neema fall from ~ kosa/jikosesha rehema. 7 (title) His/Her/Your G~ muhasham mtukufu. vt pamba; tunuka. ~ful adj 1 -zuri, -enye madaha. 2 -a upendeleo. ~fully adv. ~less adj 1 -baya, bovu. 2 bila adabu. 3 -a bila neema ya Mungu. ~lessly adv. gracile adj -embamba, zuri. gracious adj 1 -fadhili; -zuri; -enye hisani; -enye neema. 2 (of God) rehema. 3 Good Gracious! lahaula; masikini wee! graciously adv. graciousness n.

gradation n 1 mgeuko wa polepole. 2 daraja la maendeleo/ustawi. 3 mabadiliko ya tabaka. 4 (philol) apofonia. gradate vi,vt panga katika madaraja, geuka polepole. grade n 1 cheo, daraja, hadhi. 2 (US) darasa. 3 alama, maksi. make the grade (colloq) fikia kiwango kinachotakiwa.4 (US) mteremko, mwinamo. on the up/down grade kupanda/kushuka. grade crossing n njia panda (ya reli), tambukareli. vt 1 panga katika madaraja. 2 sawazisha ardhi. 3 grade up pandisha mbegu bora (ya ngo`mbe).

gradient

gradient n mteremko, mwinamo. gradual adj (of a slope) -sio na

mteremko mkali; -a polepole, asteaste. ~ly adv. ~ness n.

graduate n 1 mtu aliyepata digrii ~/ post ~ student mzamili. 2 (US) mtu aliyehitimu mafunzo katika taasisi ya elimu (chuo, shule n.k.). vt,vi 1 tia alama za vipimo. 2 panga kwa madaraja. 3 pata digrii, hitimu. 4 (chiefly US) toa digrii/diploma/cheti n.k.). graduation n mahafali.

graffiti n (usu pl) grafiti: michoro ya mikwaruzo/maneno ukutani.

graft1 n 1 kipandikizi: chipukizi lililopandikizwa katika mmea mwingine. 2 (surg) kipandikizi: kipande cha ngozi au cha mfupa n.k. cha mtu au mnyama kilichotiwa mwilini mwa mtu mwingine au katika sehemu nyingine ya mwili uleule. vt pandikiza chipukizi/ngozi katika mti, mtu au mwili; unganisha.

graft2 n rushwa. vi 1 -la rushwa. 2 suka mpango, fuata desturi ya udanganyifu (mara nyingi katika biashara). ~er n mla rushwa.

grail n (usu the Holy G~) kikombe

ama sahani iliyotumiwa na Kristo wakati wa Alhamisi kuu/Karamu ya Mwisho.

grain n 1 (collective sing) nafaka.

~ elevator n ghala. 2 mbegu; punje. 3 chembe ~s of sugar chembe- chembe za sukari; (fig) kiasi kidogo. 4 kizio kidogo kabisa cha uzito. 5 mpangilio asili wa fumwale katika mbao. be/go against the ~ fanya kinyume cha msimamo/ada.

gram1 n choroko green/black ~ choroko kijani/nyeusi.

gram2 n gramu.

grammar n 1 sarufi. 2 kitabu cha sarufi. ~ school n (GB) shule ya sekondari (inayoelemea taaluma). ~ian n mwanasarufi. grammatical adj -a kisarufi grammatical error kosa la kisarufi. grammatically adv.

gramme n see gram

gramophone n santuri, gramafoni.

grant

grampus n pomboo; mtu anayekoroma.

granary n ghala ya nafaka.

grand1 adj 1 -kubwa; -kuu (official title) G~ Master Mkuu, ashrafu; (sports) bingwa wa mchezo wa sataranji. G~ Vizier n (arch) Waziri Mkuu Uturuki ~ finale kilele, mwisho maalum. ~ entrance n lango kuu. 2 muhimu; maalum. 3 -tukufu; -a fahari ~ clothes nguo za fahari. 4 -enye kujiona, -a majivuno. 5 (colloq) -a kupendeza, zuri sana. 6 kamili the ~results of our efforts matokeo kamili ya jitihada zetu. 7 -adilifu. 8 (phrases) ~ opera n opera: maigizo ya dhamira makini yatekelezwayo kwa kuimba. ~ piano n piano babu kuu. G~ Prix n mashindano ya kimataifa ya mbio za magari. ~ stand n jukwaa maalum (lenye paa). ~ly adj. ~eur n fahari, ukuu, utukufu. ~iloquent adj -a kujivuna/maneno; -semi, -a kupiga domo. ~iose adj 1 -a fahari, -a kujionyesha. 2 -a kujivuna; adhimu.

grand2 (pref) ~ child n mjukuu. ~

son/daughter n mjukuu wa kiume/kike. ~ parent n babu/bibi. ~ father/mother n babu/bibi. ~ nephew/niece n mjukuu wa mjomba/shangazi. ~uncle/aunt n mjomba/shangazi wa baba/mama. ~ father clock n saa babu kuu. ~-dad/grandad n (colloq) babu. ~ma n (colloq) bibi. ~pa n (colloq) babu.

grandee n (hist) Mhispania au Mreno wa cheo cha juu.

grange n nyumba ya shamba.

granite n itale/matale.

granivorous adj -a kula nafaka.

granny;grannie n (colloq for) bibi, nyanya ~ knot fundo la lifu lililofungwa vibaya.

grant vt 1 toa ruhusa, toa idhini, ridhia ~ somebody permission/a request to do something toa idhini kwa mtu kufanya jambo fulani. 2 kubali (kuwa jambo fulani ni kweli) ~ the

granule

truth of what someone says kubali ukweli wa mtu. take something for ~ed chukulia jambo fulani kuwa la kweli au litatukia. take somebody for ~ed ona wa kawaida, -totambua hadhi ya mtu. n hiba.

granule n chembe ndogo, kijichembe. granular adj -a chembechembe. granulate vt,vi fanya chembechembe. granulated adj chembechembe granulated sugar sukari mchanga. granulation n. granulator n.

grape n zabibu. sour ~s n zabibu mbichi (kwa kuzikosa) (comp) ~-shot n marisau. ~-sugar n glukozi; sukari matunda. ~-vine n mzabibu; (fig) mnong'ono, uvumi.

grape-fruit n balungi.

graph n grafu. ~ paper n karatasi ya

grafu. ~ic adj 1 -a ishara/alama zinazoonekana (k.m. maandishi, michoro, vielelezo n.k.). 2 -a wazi, -a bayana, -enye kutoa picha wazi (akilini) (comp) ~ic arts n sanaa za maandishi, kuchora, kunakshi n.k.. n vitu vitokanavyo na sanaa hizo. ~ically adv kwa kuandika au kuchora; (fig) bayana, waziwazi, dhahiri.

graphite n grafati: aina ya kaboni laini, nyeusi (ya kutengeneza penseli).

grapnel n 1 nanga ndogo (-enye makombe mengi). 2 chombo cha kushikia meli za adui.

grapple vi 1 ~ (with) kamatana na,

ng'ang'ania; pambana na. 2 ~ with (fig) shughulikia, jitahidi sana kushinda/kukamilisha jambo fulani. n grappling-iron/grappling-hook n kulabu; ndoana.

grasp vt,vi 1 shika, fumbata kitu kwa nguvu; fahamu/elewa ~ somebody's hand, shika mkono wa fulani ~ somebody's meaning elewa hoja ya fulani. 2 ~ at jaribu kukamata/kuchukua; pokea/kubali kwa moyo mkunjufu ~ at an opportunity jaribu kuchukua nafasi a man who ~s at too much may lose everything mtaka yote hukosa yote.

n (power) kushika kwa nguvu; uwezo wa kushika, umahiri, ufahamu have a thorough ~ of the problem, elewa vizuri tatizo within/beyond one`s ~ -enye kueleweka/sio eleweka. ~ing adj -enye uchu/uchoyo wa (fedha n.k.).

grass n 1 majani. not let the ~ grow under one's feet (fig) tekeleza jambo (bila kuchelewa), -tochelewesha jambo. 2 nyasi. 3 malisho ya wanyama; malishoni put land under ~ geuza shamba liwe malisho. turn/put animals etc out to ~ peleka wanyama malishoni. 4 (comp) ~roots n (polit) umma. ~snake n ukukwi. ~ widow(er) n mjane wa muda; mwanamke anayeishi mbali na mume kwa muda. ~land n ukanda wa mbuga. vt,vi 1 funika kwa majani/nyasi; lisha wanyama majani/ nyasi. 2 ~ (on somebody) (GB sl) chongea, toa habari, saliti. ~y adj.

grasshopper n panzi.

grate1 vt,vi 1 kuna, paruza ~ coconut kuna nazi. 2 ~ (on) kwaruza (kwa makelele) (fig) udhi, sumbua. gratingly adv. ~r n kikalio/mbuzi. coconut ~r n mbuzi.

grate2 n chanja ya chuma kwenye tanuri. grating n kiunzi cha nondo (agh. huwekwa dirishani kwa usalama).

grateful adj 1 ~ (to somebody) (for something) -a kushukuru, -enye shukurani we are ~ to you for your help tunakushukuru kwa msaada wako. 2 (liter) tamu, -a kupendeza trees that afford a ~ shade miti yenye kivuli cha kupendeza. ~ly adv. ~ness n. gratitude n. ~ (to somebody) (for something) shukrani. gratify vt 1 pendeza, furahisha, anisi we were all gratified with/at the results tulifurahishwa na matokeo. 2 tosheleza gratify a child's thirst for knowledge kidhi haja ya mtoto ya kutaka kupanua maarifa. gratifying adj.

gratis

gratification n.

gratis adv bure adj -a bure.

gratuitous adj 1 -a bure, bilashi. 2 bila kisa/sababu a ~ insult matusi bila sababu.

gratuity n 1 kiinua mgongo. 2 bahashishi.

grave1 n kaburi. have one foot in the ~ chungulia kaburi. ~-clothes n sanda. ~ stone n tofali linalowekwa juu ya kaburi likiwa na jina la marehemu. ~yard n makaburini, sehemu ya makaburi. ~ digger n mchimba kaburi.

grave2 adj -a kuhitaji makini, -kubwa;

-a mashaka, -a hatari. ~ offence n kosa kubwa the situation is more ~ hali ni mbaya.

grave3 vt (arch or liter) chora/chonga ~n image sanamu ya kuabudika.

grave4 n alama itumikayo kuonyesha jinsi irabu inavyotamkwa katika neno fulani.

gravel n changarawe. ~-pit n shimo la changarawe. ~ly adj (of a voice) madende/makwarukaru. vt 1 mwagia changarawe. 2 kanganya.

graving-dock n gati kuu, jahabu.

gravitate vi ~ to/towards elekea, vutiwa young people in the rural areas seem to ~ towards the urban areas vijana wa vijijini wanavutiwa na maisha ya mijini. gravitation n. gravity n 1 (phys) mvutano. 2 (phys) specific gravity n uzito halisi. 3 kiwango (cha juu) cha umakini. 4 (of a situation) uzito, ukubwa.

gravy n 1 mchuzi; n rojo. ~ boat n bakuli la mchuzi. 2 (sl) marupurupu, michuzi. ~-train n chanzo cha fedha nyingi na za urahisi get on the ~-train ajiriwa katika sehemu kama hiyo.

gray adj,n see grey

graze1 vt,vi 1 (of cattle, sheep etc) -la majani. 2 lisha, chunga. grazingland n malishoni, machungani. grazier n mchungaji wanyama.

graze2 vt,vi 1 paruza, chubua kidogo. 2 gusa, papasa. n mchubuko,

great

mkwaruzo.

grease n 1 shahamu iliyoyeyushwa. 2

grisi; bereu. ~-gun n chombo cha kuingizia grisi katika mashine. ~-paint n (of actors) rangi iliyochanganywa na shahamu ya kupaka usoni. vt paka, tia grisi (hasa katika viungo vya mashine). ~ one's palm n -pa rushwa. ~r n mpaka/mtia grisi katika mashine. ~ proof adj (of paper) isiyoruhusu grisi ipite. greasy adj -enye shahamu, -enye grisi; -a kuteleza a greasy path njia ya kuteleza. greasy-spoon n (sl) mkahawa mchafu. greasily adv. greasiness n.

great adj 1 kubwa, -ingi a ~ enemy

adui mkubwa a ~ deal of rain mvua nyingi ~ with child (old use) mja mzito; (attrib. only) she is a ~singer yeye ni mwimbaji mkuu/mkubwa. ~ coat n koti zito. 2 -enye/-a uwezo mkubwa; mashuhuri ~ men watu mashuhuri. 3 adhimu, -kuu, muhimu. 4 (colloq) (preceding another adj which is weakly stressed; implying surprise, contempt etc) what a ~ big lie from a child! uwongo gani mkubwa huo kutoka kwa mtoto mdogo! 5 (also G~er) used as a distinctive epithet of the larger of two. G~ Britain n (abbr GB) Uingereza, Wales na Scotland ukiondoa Ireland ya Kaskazini. the G~ Lakes n mfululizo wa maziwa matano makubwa katikati ya mpaka wa Kanada na Marekani. the G~ War n vita vikuu vya 1914-18. 6 (with agent nouns; attrib only) -enye umaarufu; -a umashuhuri sana a ~ eater mlaji sana ~ landowner kabaila maarufu. 7 (combined with words indicating quantity) a ~ deal -ingi sana a ~ number of idadi kubwa ya a ~ while ago zamani sana. 8 (colloq) -zuri, safi; -a kuridhisha that`s ~! safi sana. 9 (colloq pred only) ~ at -enye uwezo wa. ~ on -enye weledi (prefixed to

greaves

a kinship words in grand to show further stage in relationship) ~-grandchild kilembwe ~ grandfather babu wa baba/mama ~-grandmother bibi wa baba/mama. ~ly adv sana, kwa wingi. ~ness n ukuu, ukubwa, umuhimu, umashuhuri.

greaves n (pl) deraya (za miguuni).

grebe n kibisi.

greed n ulafi, uroho. ~y adj 1 ~y (for something/to have something) -lafi, -enye uroho; -enye tamaa ~y for honours -enye tamaa ya cheo. 2 ~y (to do something) -enye shauku. ~ily adv. ~iness n.

Greek n Mgiriki, Giriki; (ancient) Myunani; lugha ya Kigiriki, Kiyunani. be ~ to one -toeleweka it's all ~ to me haieleweki kabisa adj -a Kigiriki/Kiyunani. Grecian adj -a Kigiriki, -a Kiyunani.

green adj 1 -a kijani, -a chanikiwiti give somebody/get the ~ light (colloq) -pa mtu/pata ruhusa ya kuendelea na jambo fulani. 2 (of fruit, wood) -bichi ~ oranges machungwa mabichi ~ wood does not burn well kuni mbichi haziwaki vizuri. 3 -sio na uzoefu; -sioendelea, mshamba, -sioelimika he is still ~ at his job hana uzoefu katika kazi yake. 4 (fig) -a kusitawi, -enye nguvu. 5 (of the complexion) -a kufifia, -gonjwa, -a kusawajika. ~-eyed adj -enye wivu/ husuda, -a kijicho. the ~-eyed monster n kijicho, husuda. ~ with envy -enye kijicho sana. 6 (special compounds) ~-back n (US) dola, noti ya fedha za Marekani. ~-fingers n (colloq) ustadi katika shughuli za bustanini. ~-fly n (aina ya) kidukari. ~-grocer n muuza duka la mboga na matunda. ~ grocery n biashara/uuzaji wa mboga na matunda. ~-horn n zuzu, mshamba. ~-house n nyumba ya kioo (ya kuhifadhi mimea). greenroom n chumba (cha mapumziko). ~-stuffs; ~s n (pl) mboga za majani. ~-tea n majani ya

grey;gray

chai yaliyokaushwa kwa mvuke. ~-wood n mbuga (hasa wakati wa kiangazi); msitu uliostawi. n 1 kijani, chanikiwiti. 2 (pl) mboga za majani (kabla au baada ya kupikwa) (US) Christmas ~s matawi ya msonobari ya kupambia. 3 eneo linaloota majani kwa matumizi ya wote/kwa mchezo wa tufe kuzunguka shimo katika uwanja wa gofu. ~ery n majani ya kijani, kijani cha mimea michanga. ~ish adj -a kijanikijani (in compounds) ~ish-yellow n njano-kijani ~ishness n. Greenwich n Griniwichi. Greenwich mean time n (abbr GMT) wastani wa majira ya jua; saa ya ulimwengu.

greet vt ~ (with) 1 salimu, amkia;

pokea kwa kuonyesha hisia; (in a letter) andika maneno kuonyesha urafiki, heshima n.k. the news was ~ed with dismay habari zilipokewa kwa fadhaa. 2 (of sights and sounds) onekana, sikika. ings n maamkizi, salamu. ~ing-card n kadi ya salamu.

gregarious adj -a kuishi makundi- makundi; -enye kupenda kushirikiana na wengine. ~ly adv. ~ness n.

Gregorian adj -a Papa Gregory. 1 ~ chant muziki wa ibada wa Papa Gregory. 2 ~ calendar n kalenda ya Papa Gregory (iliyopangwa kama ilivyo sasa).

gremlin n zimwi (linalosemekana linasababisha matatizo ya mitambo).

grenade n kombora. grenadier n (formerly) askari mtupa makombora; (now) askari wa kikosi cha miguu cha Uingereza.

grenadine n sharubati ya komamanga.

grew pt of grow.

grey;gray adj 1 -a rangi ya kijivu. 2

-enye mvi she has ~ hair ana mvi. ~-board n shaibu. ~-headed adj -zee, -a siku nyingi. ~ matter n ubongo. n kijivu she is dressed in ~ amevaa nguo ya kijivu. vt,vi -wa na rangi ya kijivu, ota mvi. ~ish adj

grid

kijivukijivu. ~hound n mbwa mwindaji. ocean ~ n meli ya abiria iendayo kasi.

grid n 1 (of electricity) fito umeme (mfumo wa waya wa kupitisha umeme). 2 miraba fito, mstari ramani. 3 kiunzi cha fito (za chuma) zinazokingamana, chanja. 4 kiunzi cha waya za redio. 5 fitokaangio (za kukaangia nyama). ~dle n kiokeo, chuma. ~iron n 1 fito, kaango, chanja. 2 (US) kiwanja cha mpira wa miguu.

grief n 1 huzuni, ghamu. 2 kitu kiletacho huzuni. bring to ~ tia nuhusi. come to ~ pata maumivu, balaa, huzuni n.k.; angamia. ~-stricken adj -liopatwa na msiba/hasara/majonzi, -enye huzuni. grievance (against) n nung'uniko, lalamiko, dai air one's grivance toa manung'uniko have a grievance against somebody -wa na kisa na, lalamikia mtu. grieve vt,vi 1 sikitisha, huzunisha. 2 sikitika, huzunika. grievous adj 1 -a kuhuzunisha, -a kusikitisha a grievous massacre mauaji ya kuhuzunisha. 2 kali sana grievous pain maumivu makali grievous punishment adhabu kali. grievously adv.

griffin (also griffon; gryphon) n (GK

myth) mnyama (katika hadithi) mwenye mwili wa simba na kichwa na mbawa za tai.

grill n 1 chanja/wavu wa kuchomea nyama n samaki n.k. 2 nyama/ samaki n.k. iliyochomwa. ~ room n chumba cha kuuzia vyakula vilivyobanikwa katika hoteli. mixed ~ n mchanganyiko wa nyama tofauti k.m. steki, maini n.k.. vt,vi 1 choma nyama, samaki n.k.; jianika katika jua/joto kali sana. 2 (of the police) hoji mkosaji kwa ukali.

grille n dirisha lenye nondo.

grim adj 1 -kali; -zito; -katili. 2 (ghastly) baya, -a kutia hofu, -a kuogofya. hold on like ~ death, shikilia kwa nguvu zote. ~ly

grip

adv.~ness n.

grimace n mkunjo wa uso. make ~s

finya uso vi kunja uso kwa maumivu au kuchekesha n.k..

grime n masizi; nongo; uchafu. vt chafua kwa masizi/taka/uchafu. grimy adj -enye taka, -chafu, -enye masizi. ~ faced adj -enye uso mchafu. ~ness n.

grin vi,vt 1 kenua. ~ and bear it vumilia maumivu/hasara n.k. bila kulalamika, jikaza kisabuni, kufa na tai shingoni. 2 eleza/jieleza kwa tabasamu. n tabasamu.

grind vt,vi 1 ~ (down) (to/into) saga ~ down to flour saga mpaka kuwa unga. 2 sagika. 3 ~ (down) (usu passive) (fig) dhalilisha ~ down the poor onea watu maskini. 4 (of tools etc) noa ~ a knife noa kisu. 5 kereza, kwaruza; (of teeth) saga meno. ~ to a halt (of a vehicle) simama kwa breki za kukwaruza; (fig) (of a process) simama polepole the scarcity of raw materials brought our industry ~ing to a halt uhaba wa mali ghafi umesababisha kiwanda chetu kusimama polepole. 6 endesha kwa kuzungusha ~ a coffee mill endesha kinu cha kahawa kwa mkono. 7 ~ (away) (at) fanya kazi/soma kwa bidii na kwa muda mrefu ~ away at one's work fanya kazi kwa bidii sana ~ for an examination bukua. n (colloq) kazi ya kuchusha ya muda mrefu. ~er n 1 mashine/kisagio; chego, gego coffee ~er mashine ya kusaga kahawa. 2 (in compounds) msagishaji; mnoaji a knife ~er mnoa kisu. ~-stone n kinoo, cherehe; (for grinding grain) kijaa. keep one's nose to the ~stone shurutisha kufanya kazi kwa bidii bila kupumzika.

grip n 1 kushika, kukamata sana kwa mkono n.k. be at ~s with; come to ~s with the enemy shambulia, shikamana sana have a strong ~ shika imara; lose one's ~ on

gripe

something ponyokwa na kitu. 2 nguvu/uwezo wa kushika have a good ~ of a problem (fig) fahamu sana jambo. take a ~ on oneself (colloq) jikaza. 3 (in a machine etc) sehemu inayoshika/bana; klachi. 4 (also ~ sack) (US) begi/mfuko wa msafiri. vt,vi 1 shika, kamata sana. 2 vutia the film ~ped the audience filamu ilivutia hadhira. 3 fahamu jambo. 4 (of tires) shikamana, kwama.

gripe vt,vi 1 uma/umwa tumbo. 2 nung'unika, lalamika. n malalamiko. ~r n mlalamikaji. (the) ~s n (colloq) maumivu makali ya tumboni, msokoto wa tumbo. ~ water n dawa ya msokoto wa tumbo.

grippe n the ~ n mafua.

grisly adj -a kutisha, -a kuogofya.

grist n nafaka ya kusagwa. it's all ~ to the mill/all is ~ that comes to his mill (prov) yote ni faida kwako, kila kitu kinaleta faida. ~-mill mashine ya kusaga nafaka.

gristle n wamba-ngoma; nyama ngumu

inayovutana.

grit n 1 mchanga; changarawe throw ~ in the bearings haribu mpango. 2 (courage) ujasiri na uvumilivu he has no ~ si jasiri. vt ~ one's teeth kereza meno; (fig) jikaza kisabuni. ~ty adj 1 -enye mchanga. 2 mtu jasiri/imara. ~s n, pl nafaka (aina ya shayiri) iliyokobolewa; unga wa nafaka (aina ya shayiri).

grizzle vt (colloq) (esp of children)

lialia, nung'unika bila kuacha. n kulialia have a good ~ nung'unika.

grizzled adj -enye mvi; -a kijivu. grizzly -a kijivu; -enye mvi. n (also grizzly bear) dubu mkubwa na mkali wa Marekani ya kaskazini.

groan vi,vt 1 gumia, piga kite; koroma. 2 (of things) toa sauti ya kuelemewa. 3 ~ (out) simulia kwa sauti ya huzuni/maumivu. 4 ~ down zomea. n kite, mgumio.

groats n pl unga wa nafaka zilizokobolewa (hasa aina ya shayiri).

gross

grocer n mwuza duka (la vyakula na

bidhaa ndogo ndogo). ~'s (shop) n duka la bidhaa za vyakula na matumizi ya nyumbani (k.m. sabuni n.k.). ~y n 1 biashara ya kuuza vyakula. 2 duka (la vyakula k.m. pilipili, bizari). 3 (pl) ~ies n bidhaa za vyakula na matumizi ya nyumbani.

grog n pombe kali inayochanganywa na maji.

groggy adj dhaifu; legevu.

groin n 1 kinena. 2 (archit) ukingo katika paa. 3 (US) see groyne. vt jenga kwa kuba.

groom n 1 saisi. 2 bride~ n bwana arusi. vt 1 (of horses) tunza (kwa kulisha, kusafisha, kuchana). 2 (of apes, monkeys) safisha manyoya. 3 (usu in pp, of persons) well ~ed -liopunwa, nadhifu (hasa nywele, ndevu, nguo); (colloq) andaa/tayarisha mtu kwa wadhifa fulani.

groove n 1 mfuo. 2 (routine) mazoea, desturi. be stuck in/get into a ~ fuata kawaida/desturi/mkondo. in the ~ (dated sl) katika hali nzuri ya kufanya jambo; furahishwa. vt tia mfuo. ~r n (sl) mtu asiyepitwa na wakati. groovy adj -a sasa, kisasa, kileo.

grope vi,vt ~ (about) (for/after) (lit or fig) tafuta kwa kupapasa (kama kipofu au mtu aliye gizani), papasa (in the dark) tutusa ~ one's way tafuta njia kwa kupapasa. gropingly adv.

gross1 n dazeni kumi na mbili.

gross2 adj 1 -sio na adabu, chafu ~ language tusi. 2 (of food) -baya (kisichovutia); -enye mafuta mengi ~ eater mlaji anayependa chakula kibaya. 3 (of the senses) zito na -siochangamka. 4 wazi, dhahiri sana ~ injustice udhalimu dhahiri. 5 (of vegetation) -a kusitawi sana. 6 (of persons) -nene kupita kiasi, nono. 7 jumla, kamili/yote; ghafi ~ profit faida ya jumla. ~ national product

grot

(GNP) n Jumla ya Pato la Taifa. 8 in (the) ~ jumla jumla. vt leta kipato cha jumla exports sales of cotton ~ed one million last month mwezi jana uuzaji wa pamba umechuma pato ghafi la shilingi milioni moja. ~ly adv. ~ness n.

grot n (poet) see grotto.

grotesque adj 1 -a ajabu (hata kuchekesha), -a kioja. 2 (art) -enye sura (za binadamu/wanyama n.k.) za ajabu. n jambo la kuchekesha, kioja cha kuwazika. ~ly adv. ~ness n.

grotto n pango.

grotty adj (sl) -a kuchukiza, -a kutopendeza.

grouch vi (colloq) nung'unika; lalamika. n mnung'unikaji; mlalamikaji. ~y adj.

ground1 n 1 chini; ardhi fall on the ~ anguka chini (in compounds) ~ to air missiles makombora ya kutungulia ndege ~ controlled kuelekezwa/ dhibitiwa kutoka chini. above ~ adj hai. below ~ adj -liokufa na kuzikwa. fall/be dashed to the ~ shindikana, fifia, shindwa, katishwa tamaa. get off the ~ (of an aircraft) ruka; (fig) anza utekelezaji, zinduliwa. 2 nafasi, eneo. cut off the ~ from under somebody's feet wahi/bashiri/gundua mipango ya mtu (na kumuaibisha). cover (much) ~ safiri sana; (fig. of lecture, meeting etc) shughulikia mambo mengi. gain ~ songa mbele, piga hatua; fanikiwa. give/lose ~ rudi nyuma, rudishwa nyuma. hold/stand/keep one's ~ simama imara, shikilia msimamo. shift one's ~ geuza/ badili msimamo. suit somebody down to the ~ faa kikamilifu/sana common ~ mwafaka. forbidden ~ n mwiko. meet somebody on their own ~ kutana na mtu mahali pake, kubaliana na masharti, ridhisha. 3 ardhi, udongo. break fresh/new ~ lima shamba jipya; (fig) anza jambo jipya; chimbua kitu. 4 (of sports) eneo, kiwanja, uwanja; (of fishing

group

~s) mvuo; (of hunting) eneo. 5 (pl) bustani the State House ~ bustani inayozunguka Ikulu. 6 chini (ya bahari, mto n.k.). touch ~ (of a ship) pwelewa; (fig) fikia mambo muhimu baada ya mazungumzo ya juujuu tu. 7 (pl) punjepunje (agh. za kahawa), mashapo. 8 (usu pl) sababu. on the ~s of kwa sababu ya. ~s for divorce sababu za kutoa/kudai talaka. be/give/have ~s for -wa/-pa/-wa na sababu ya. 9 mji, sehemu wazi (isiyo na mapambo) a dress with blue flowers on a white ~ gauni lenye maua ya buluu na mji mweupe. 10 (compounds) ~-bait n chambo. ~-fish n samaki wa kilindi. ~ -floor n orofa ya chini. be/get in on the ~-floor (colloq) wa waanzilishi. ~nut n (also earthnut/peanut) karanga. ~-plan n ramani ya nyumba ardhini. ~-rent n kodi ya kiwanja. ~sman n mtunzaji kiwanja cha mchezo. ~sheet n turubai la kutandika agh. chini ya hema. ~speed n (aviat) kasi ya ndege ardhini. ~crew/staff n (aviat.) wahudumu uwanjani. ~swell n mawimbi mazito (yanasabaishwa na dharuba ya mbali). ~work n (usu fig) maandalizi, matayarisho ya kazi n (usu fig) msingi. vt,vi 1 (of a ship) kwama baharini, panda mwamba; (of aircraft) zuiliwa kuruka. 2 ~ arms (mil) weka silaha chini. 3 ~ something on something tumia kama msingi. 4 ~ somebody in something funda/-pa mtu (mafunzo ya) msingi; (elect.) unganisha waya n.k. wa umeme na ardhi. ~ing n mafundisho hasa ya msingi. ~less adj bila sababu/msingi maalum.

ground2 vt pt pp of grind ~ rice unga wa mchele. ~ glass n kioo kisichoona (kwa kusagwa).

group n 1 jamii, kundi, kikundi so and so's ~ kundi la akina fulani. 2 (cultivating together) chaa. 3 (mil) kikosi. ~-captain n ofisa kiongozi

grouse

wa jeshi la anga. 4 (math) kikundi. 5 (mus) bendi. vt,vi panga/weka katika makundi ~ed data data ya vikundi.

grouse1 n kwale wa Ulaya.

grouse2 (colloq) vi nung'unika,

lalamika n manung'uniko, malalamiko.

grout1 n (construction) niru, chokaa

laini, rojo cement ~ machicha ya saruji. vt paka niru; ziba kwa chokaa.

grove n kijisitu.

grovel vi tambaa, lala kifudifudi; (abase oneself) jidhili, pigia magoti, angukia ~ in the dirt (fig) nyenyekea kabisa, jifanya mnyonge. ~ler n.

grow vi,vt 1 kua; mea, ota the child is ~ing well mtoto anakua vizuri maize ~ well in Iringa mahindi yanaota vizuri huko Iringa. ~ out of -wa kubwa kuliko/kua; zidi. 2 (increase) zidi, ongezeka. ~ on/upon zidi kupendeza she ~s on you anazidi kukupendeza the book grows on me kitabu kinaniteka, kinazidi kunipendeza; acha kufanya (kwa uzee) I' ve ~n out playing football nimeacha kucheza mpira; tokana na his troubles ~ out of his laziness matatizo yake yanatokana na uvivu wake. ~ up komaa, pevuka, -wa -zima what do you want to do when you ~ up? unataka kufanya nini utapokuwa mtu mzima?; kua friendship grew up between the two students urafiki ulikua kati ya wanafunzi hawa wawili. ~ing pains n pl maumivu ya viungo; (fig) matatizo ya mwanzoni mwa shughuli fulani ~n up n mtu mzima. 3 -wa ~ older konga, chakaa ~ smaller pungua ~ taller refuka. ~ dark -wa giza. 4 (agrc.) panda, lima, otesha he ~s three crops a year anapanda mara tatu kwa mwaka. 5 fuga, acha kitu kikue ~ a beard fuga ndevu, acha ndevu zikue. 6 ~ to be/like etc zoea I grew to like cheese when I lived in Germany nilipokuwa Ujerumani nilianza kuzoea jibini. ~er n 1. mwoteshaji 2. mmea (unaokua kwa

guano

njia fulani) a fast/slow ~er mmea unaokua upesi/polepole. ~th n 1 kuzidi; kukua; ukuaji. 2 ongezeko. ~th rate n kima cha ongezeko. 3 (vegetatition) ulimaji, uotaji this year's ~th of maize has been good uotaji wa mahindi mwaka huu ulikuwa mzuri. 4 maendeleo; kuenea eneo. 5 maotea. 6 (med) kushika ugonjwa k.m. kansa, donda ndugu.

growl vi,vt 1 nguruma. 2 (complain)

nung'unika. 3 ~ (out) sema kwa kunguruma. n mngurumo; manung'uniko. ~ingly adv.

grown pp of grow.

groyne (US groin) n bomazuizi, kinga (baharini).

grub1 n 1 funza. 2 (sl) chakula. ~by adj 1 -chafu, -enye taka. 2 (of fruit) -enye funza. ~bily adv. ~biness n.

grub2 vi,vt (sl) -la; pekua. ~ about chimbachimba. (of soil) ~ up tifua; fukua;

grudge vt sunza, toa shingo upande. n mfundo, kinyongo bear a ~ against -wa na kisasi dhidi (ya), -wa na kinyongo na. grudgingly adv.

gruel n (of rice) ubwabwa, fuka, uji wa mapande; (of milk and maize flour) uji, farne.

gruelling adj gumu sana, -a kuchosha. gruesome adj -a kutisha, -a kuogofya; kuchukiza. ~ly adv. ~ness n.

gruff adj (of behaviour) -a tabia mbaya; (voice) -nene, -a kukwaruza. grumble vt,vi 1 ~(at/about/over something) lalamika; nung'unika ~ over trivial issues lalamika kwa mambo yasiyo na maana. 2 ~ (out) nung'unika. 3 vuma, nguruma. n lalamiko. ~r n.

grumpy adj -enye harara, -enye hamaki; -enye chuki. grumpily adv. grumpiness n.

grunt vt,vi 1 koroma. 2 (of persons)

guna ~ out an answer mumunya jibu n mkoromo. ~er n 1 mguno. 2 nguruwe.

gryphon n see griffin

guano n guano: mavi ya ndege wa

guarantee

baharini yatumikayo kama mbolea.

guarantee n (in law guaranty) 1 (written promise) dhamana. 2 mdhamana. 3 (guarantor) mdhamini. 4 (in law guaranty) (something offered) rahani he offered his house as a ~ aliweka nyumba yake rahani. 5 (colloq) (assurance) hakikisho passing an examination is not always a ~ of getting a job kufaulu mtihani hakumhakikishii mtu kupata kazi. vt 1 dhamini, weka rahani, toa uhakikisho he does not ~ habitual criminals hadhamini wahalifu sugu. 2 (colloq) (without legal obligation) ahidi we ~d to pay you well tuliahidi kukulipa vizuri. guarantor n mdhamini. guaranty n (leg) dhamana, mdhamana; rahani.

guard n 1 ulinzi you will be on ~ today utakuwa mlinzi leo the militia was orderd to keep ~ mgambo aliamriwa kulinda lindo. 2 tahadhari, kujihadhari, kujikinga. be on/off one's ~ jihadhari, jikinga he was on his ~ against pick pockets alijihadhari na wezi wa mifukoni. 3 askari, kikosi cha askari walinzi, mlinzi. change ~ (mil) badilisha walinzi. mount ~ ingia lindoni (kama mlinzi). relieve ~ chukua nafasi ya mlinzi aliyemaliza zamu. stand ~ kuwa mlinzi, linda. 4 (also called warder) askari jela (wanaolinda jela). 5 (GB) (of a

railway train) gadi. 6 (pl) G~s n walinzi wa kiongozi wa nchi/mfalme. 7 gadi, askari (wenye kumlinda, kumpa heshima, kumsindikiza mtu) the President inspected the ~ of honour Rais alikagua gwaride la heshima. 8 (compounds) ~ boat/ ship n. mashua/meli ya doria. ~ house n (mil) nyumba ya walinzi; mahabusu. ~ room n chumba cha walinzi; mahabusu. vt 1 linda ~ a bridge linda daraja. 2 ~ against (ji) hadhari, (ji)linda kwa uangalifu ~ against malaria jikinge dhidi ya malaria. ~ed adj (of statements) -a

guide

hadhari ya ~ed answer jibu la hadhari. ~edly adv kwa hadhari. ~ian n 1 (official or private legal use) mlezi. 2 mwangalizi. ~ianship n ulezi; ulinzi.

guava n (tree) mpera; (fruit) pera.

gubernatorial adj (US, Nigeria) -a

gavana, -a kuhusu gavana.

gudgeon n samaki wadogo ambao

hutumiwa kama chambo.

guerden n (poet) zawadi, tuzo, malipo vt toa zawadi, tuza.

guerrilla;guerilla n askari wa msituni; mpiganaji wa kuvizia (agh. wa vita vya msituni), apiganaye katika vikundi vidogo msituni. urban ~ n mpiganaji wa kuvizia (wa mjini). ~ warfare/war n vita vya msituni/vya askari wa msituni.

guess vt,vi 1 ~ (at) kisia, bahatisha

I should ~ your age as kwa kukisia/ kubahatisha umri wako ni. 2 (think) ona, dhani I ~ you got it wrong (US colloq) nadhani umekosea. n dhanio, kisio. it is any body's ~ hakuna mtu mwenye hakika. at a ~ kwa kubahatisha. make a lucky ~ bunia, bahatisha your ~ is as good as mine ni vigumu kukisia. by ~ kwa kubahatisha. ~timate (modern colloq) n kubahatisha kwa kukisia na kufikiri. ~ work n kazi ya kubahatisha.

guest n mgeni. ~ room n chumba cha wageni. ~ of honour n mgeni wa heshima. ~ house n nyumba ya wageni. ~ night n usiku wa karamu (ya wageni wa klabu). paying ~ n mgeni alipaye kodi ya malazi na chakula (kwenye nyumba ya mtu).

guffaw n kicheko kikubwa. vt angua kicheko.

guide n (of a person or instruction)

1 kiongozi. Girl G~ n skauti wa kike teacher's guide kiongozi cha mwalimu railway ~ kiongozi cha safari za gari moshi. 2 kiashirio, kishawishi. ~lines n mwongozo (agh. kutoka kwa wenye madaraka). 3 ~ book n kitabu cha kuongoza

guild

wageni/wasafiri. 4 kielekezi. ~d missile n kometi inayoongozwa. vt ongoza, elekeza, onyesha njia. guidance n 1 kuongoza; kuongozwa; uongozi for your guidance kwa mwongozo wako. 2 ushauri(kwa kazi).

guild n chama, ushirika (wa watu wenye matakwa au shughuli za namna moja). ~ socialism n mfumo wa kuongoza kiwanda kwa baraza la wanachama.

guilder n gilda (sarafu ya Uholanzi).

guile n hila, ujanja get it by ~ pata kwa ujanja. ~less adj. ~ful adj.

guillotine n gilotini: bamba la kukata kichwa (kwa wahalifu Ufaransa); kisu cha kukatia makaratasi; (in parliament) ukatishaji mjadala (wa kupinga mswada). vt kata (kwa bamba/kisu) kichwa, karatasi.

guilt n hatia. ~less adj -tokuwa na hatia; -safi ~less of robbery -siokuwa na hatia ya ujambazi. ~y adj. ~y (of) 1 -liofanya kosa plead ~y of an offence kiri kosa. 2 -enye hatia, -enye kuonekana na hatia ~y look -enye uso wa hatia look ~y onekana kuwa na hatia ~ y conscience hisia ya hatia, majisuto be found ~y onekana na hatia find ~y ona/patwa na hatia. ~y or not ~y una makosa au huna.

guinea n gini (sarafu ya zamani ya

dhahabu yenye thamani ya shilingi ishirini na moja) ~-corn n mtama. ~-fowl n kanga; (crested) kororo; chepeo. ~-pig n 1 nungubandia (agh. hutumiwa kwa majaribio). 2 mjaribiwa.

guise n 1 (old use) mtindo wa vazi. 2 in/under the ~ of kwa kusingizia, kwa kutumia/kujifanya; -enye umbo la.

guitar;guitor n gita.

gulch n (US) bonde jembamba.

gulf n 1 ghuba. Persian ~ n Ghuba ya Uajemi. 2 (cavity) shimo kubwa; korongo refu; (fig) tofauti kubwa bainishi.

gull1 n shakwe.

gun

gull2 n (simpleton) mjinga, zuzu, mshamba. vt danganya, ghilibu, laghai. ~ibility n. ~ible adj -enye kudanganywa.

gullet n umio; koo.

gully mvo, korongo. ~ hole n mfereji wa maji machafu, mtaro.

gulp vt,vi ~ (down) gugumia (maji,

chakula); meza kwa pupa, bwia. ~ back/down tears n zuia machozi.

gum1 n ufizi wa meno, sine. ~boil n jipu la ufizi.

gum2 n 1 sandarusi; gundi, ulimbo.

2 chewing ~ ubani. 3 (also ~ tree) mkalitusi. up a ~ tree (sl) kwa shida sana. ~ boot n buti ya mpira. ~ shoe n (US) raba; (sl) mpelelezi. vt gandisha, tia gundi, paka gundi. ~my adj.

gum3 n (esp. N England) (in oaths etc) Mungu.

gumption n (colloq) akili, busara.

gun n 1 bunduki. be going great ~s

endelea vizuri sana. blow great ~s of the wind vuma kwa nguvu sana. stand/stick to one's ~s shikilia msimamo wako (be) sure as a ~ (-wa na) hakika kabisa. ~ barrel n mtutu. ~ boat n manowari ndogo inayobeba mizinga. ~ boat diplomacy n (fig) diplomasia ya vitisho. ~ cap n fataki. ~ carriage n gari la mzinga. ~ cotton n baruti ya pamba iliyolowekwa kwenye asidi. ~ fire n mlio/mapigo ya bunduki/mzinga. ~ man n jambazi. ~metal n mchanganyiko wa madini ya shaba na bati au zinki. ~ powder n baruti. ~ room n (in a warship) chumba cha maofisa wa ngazi za chini. ~ running n magendo ya silaha. ~ runner n mwendesha/mfanya magendo ya silaha. ~ shot n mpigo wa bunduki; masafa ya bunduki. ~ smith n mfua bunduki. 2 mwindaji. 3 big ~ n (colloq) mtu maarufu au mwenye madaraka makubwa, mheshimiwa. vt ~ somebody (down) piga mtu risasi. ~ner n

gunny

mpiga mizinga; (in the navy) ofisa msimamizi wa silaha. ~nery n utengenezaji/utumiaji wa mizinga.

gunny n gunia.

gunwale n ukingo wa juu wa meli/mashua.

gurgle vi bubujika; sukutua; gugumia. n mbubujiko wa maji.

guru n guru: mwalimu wa dini wa Kihindu; (colloq) mwalimu au mtu mashuhuri anayeheshimiwa.

gush vi 1 (of water) foka, mwagika. 2 (talk too much) bubujika, zungumza kwa shauku. n (outburst) bubujiko; kufoka. ~er n kisima cha mafuta yanayofoka. ~ing adj ~ingly adv.

gusset n upapi wa nguo, kijambia.

gust n dharuba (ya ghafla); mvua, moto n.k. wa ghafla (fig) a ~ of passion fumuko la hamaki, hasira,huba. ~y adj.

gustation n (formal) kuonja.

gusto n kufurahia kufanya jambo fulani eat with ~ kula kwa kufurahia.

gut n 1 (colloq) matumbo; utumbo. hate somebody's ~s chukia mtu mno. 2 (pl) (colloq) yaliyomo (katika kitu/jambo fulani) his speech had no ~s hotuba yake haikuwa na lolote (la maana). 3 (pl) (colloq) ujasiri: he has no ~s yu mwoga. 4 uzi wa utumbo (utumikao kwa kutengenezea zeze n.k.). vt 1 (remove ~s) tumbua. 2 (destroy) teketeza a house ~ted by fire nyumba iliyoteketezwa kwa moto. ~less adj -oga.

gutta-percha n (aina ya) mpira.

gutter1 n 1 mchirizi, mfereji; mlizamu. 2 the ~ n (fig) ufukara, ukata thelanguage of the ~ lugha ya matusi take the child out of the ~ toa mtoto kwenye ufukara. the ~ press n magazeti ya matusi na kashifa. ~snipe n msikwao.

gutter2 vi (of a candle) waka kwa

vipindi (hata nta kutiririka upande mmoja).

guttural adj (of sounds) -a kooni.

guv'nor n bosi see governor.

guy1 n 1 (sl)jamaa. vt dhihaki; fanya/

gyro

onyesha sanamu ya mtu (kwa lengo la kubeza, kuchoma moto n.k.). 2 sanamu (inayovalishwa na kuchomwa moto siku ya Novemba 5 Uingereza). 3 mtu aliyevaa kiajabuajabu; kinyago.

guy2 (also ~rope) n kamba ya kukazia/ kuinulia hema n.k.

guzzle vt,vi la/ nywa kwa pupa. ~r n. gybe (US jibe) vi,vt (naut) (of a sail or boom) zinga, pembea toka upande mmoja wa tanga hadi wa pili.

gymkhana n tamasha ya michezo (agh. ya farasi, magari n.k.).

gymnasium (also gym) n 1 ukumbi wa michezo ya mazoezi ya viungo. 2 shule ya sekondari.

gymnast n mwanasarakasi. ~ics n mazoezi ya viungo vya mwili, sarakasi. ~ic adj.

gynaecology; gynecology n jinakolojia: elimuuzazi. gynaecologist n mwana jinakolojia. gynaecological adj.

gyp1 n udanganyifu. vt danganya.

gyp2 n give somebody ~ (sl) karipia/adhibu (bila huruma); tesa.

gypsum n jasi.

Gypsy n see gipsy.

gyrate vi zunguka katika duara. gyration n mzunguko; kuzunguka. gyratory adj.

gyro (pref) giro (duara). ~compass n diragiro. ~scope n gurudumu tuzi.

 

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

İTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.