hijack
changamfu, -epesi, kunjufu; (of a horse) -enye kwenda
mbio. ~ spot n tukio muhimu. ~ street n barabara kuu/muhimu
(katika mji). ~ table n meza kuu. ~ tea n mchanganyiko wa chai na chakula cha
jioni. ~-tension adj (electric) -enye volteji kubwa. ~ tide n maji
kujaa, maji makuu. ~ toned adj -a juu (katika jamii au kisomo). ~ treason n
uhaini. ~ up n (colloq) mtu mashuhuri; mtu wa cheo cha juu. ~ water n see ~tide.
~-water mark n alama yenye kuonyesha kikomo cha juu cha maji kujaa; (fig) upeo wa
mafanikio. ~way n; ~ road barabara kuu. H~ way Code n
kanuni/sheria za barabara. ~-way-man n haramia, mnyang'anyi adv juu (lit,fig) lipa bei
kubwa. live ~ ishi kitajiri (kwa vinono na vinywaji kochokocho). fly ~ (fig)
-wa na tamaa kubwa. hold one's head ~ jiamini, jiona. run ~ (of the sea) kabiliwa na mkondo mkali na maji
makuu; (of the feelings) chacharika. search/look/hunt ~ and low (for something) tafuta kila
mahali. ~ly adv sana he spoke ~ ly of her
alimsifu sana. ~ ness n 1 (opposite of lowness) hali/sifa ya juu. 2 (title) Mstahiki, mtukufu.
hijack (also high-jack) vt teka nyara. ~er n mteka
nyara.
hike vi (colloq) tembea umbali mrefu (kwa burudani). n matembezi
marefu. ~r n mtembeaji wa masafa marefu. hitch-~ vi (colloq abbr hitch) omba
lifti.
hilarious adj -a kikwakwa. hilarity n kikwakwa. ~ly adv.
hill n 1 kilima. ~ side n ubavuni mwa kilima a steep ~ kilima kikali. ~ top n juu ya kilima, kilele cha kilima. 2 mwinuko. 3 ant~ n kichuguu. ~y adj -enye vilima. ~-billy n (colloq often used derog, in SE of the US) mshamba, mkulima, mfanya kazi wa
hint
shambani/wa milimani; (attrib) -a wakulima wa milimani.
hillock n kiduta.
hilt n mpini, (wa upanga, sime au
jambia n.k.). (up) to the ~ kabisa.
him pers pron yeye (mwanamume); yule give it to ~ mpe that's ~ ndiye hasa
(yeye). ~self pron 1 (reflex) mwenyewe (mwanaume) the injured man came to ~self mtu aliyeumia alipata fahamu tena he found ~ self in the ditch alijikuta
shimoni. (all) by ~self peke yake; bila msaada he lives by ~self anaishi peke
yake. 2 (emph) mwenyewe did you see the Director ~self? ulimwona Mkurugenzi
mwenyewe? 3 hali ya kawaida (ya mtu) he is not ~self today hayupo katika hali yake ya kawaida
leo.
hind1 n paa jike.
hind2 adj -a nyuma ~ legs miguu ya nyuma (ya
mnyama). ~ quarters n (of mutton or beef) nyama ya miguu ya nyuma na
kiuno. ~most adj -a nyuma kabisa; -a mwisho. ~sight n utambuzi
(baada ya jambo kutokea).
hinder vt zuia ~ somebody from doing something zuia mtu kufanya kitu fulani; (delay) kawilisha, chelewesha. ~ance n kizuizi, kipingamizi.
Hindi n, adj (of a language) Kihindi; -a Kihindi.
Hindu n Baniani, Mhindu. ~ism n dini ya
Kibaniani/Kihindu. ~stani adj -a Kihindustani. n Kihindustani
(mojawapo ya lugha za Kihindi).
hinge n bawaba; (fig) kiini cha jambo; kanuni kuu (ya jambo fulani) his mind is off its ~s (or un~d) ana wazimu. vt,vi 1 pigilia bawaba. 2 ~ on/upon tegemea.
hint n dokezo. drop (somebody) a ~ dokeza kwa kufumbia. take a ~ tambua na kufanya
lililodokezwa. vt,vi 1 ~ (to
hinterland
somebody) dokeza. 2 ~ at gusia, dokezea.
hinterland n bara.
hip1 n nyonga. smite ~ and thigh
shinda sana. ~-bath n kipipa ambacho kinamfika mtu kwenye nyonga. ~-bone n (biol) mfupa wa nyonga. ~-pocket n mfuko wa pembeni (mwa suruali n.k.). ~-flask n chupa ndogo (ya brandi) inayochukuliwa katika mifuko ya nyonga.
hip2 n tunda la waridi mwitu.
hip3 adj (also hep) (sl) kisasa,
-nayofuata mambo/ mitindo ya kisasa.
hippie n see hippy.
hippo n (colloq abbr of hippo potamus).
Hippocratic adj ~ oath kiapo cha uaminifu cha madaktari.
hippodrome n (in ancient Greece and Rome) kiwanja cha mashindano ya magari ya
kukokotwa.
hippopotamus n kiboko.
hippy;hippie n (late 1960s) hipi, mwasi wa mila/utamaduni.
hire vt ~ (out) kodi; kodisha; panga; pangisha ~out boats kodisha
mashua; kodi. n kodi, malipo ya kukodisha/kupangisha. for ~ kwa ajili ya
kukodishwa. (pay for/buy) on ~ purchase bandika, (lipa/ nunua) kwa
polepole; mkopo. ~ling n (derog) mfanyakazi wa kukodiwa;
mamluki.
hirsute adj -enye nywele kuruwili;
-enye nywele na ndevu ndefu na za matimutimu.
his adj, pron -ake (mwanamume) a friend of ~ rafiki
yake.
hiss vi,vt 1 fanya sss kama nyoka. 2 ~ (off); ~ (at) fanya
zii! zomea. n 1 sauti ya sss kama ya mlio wa nyoka. 2 sauti ya zii!
history n 1 historia. make ~ fanya
kitendo/jambo la kihistoria. ancient ~ n historia ya kale; hadithi ya zamani. modern ~ n historia ya sasa (kuanzia 1453). 2 maelezo ya
hit
matukio ya zamani. 3 matukio yanayohusishwa na mtu au kitu the inner ~of an affair undani wa
jambo. 4 natural ~ n elimu viumbe; maelezo yenye mpango kuhusu hali za
maisha. historian n mtaalamu wa historia, mwanahistoria. historic adj -a
kihistoria, -enye kukumbukwa katika historia, -enye umuhimu kihistoria. historic times n nyakati ambazo historia yake ipo na
imerekodiwa. historical adj 1 -a historia; si -a hadithi tu. historical events n matukio ya kihistoria
halisi; -sio ya kufikiria tu. 2 -a kuhusiana na historia. historically adv. historicity n tabia ya
historia, uhalisi wa matukio. historiographer n mwandishi wa
historia. historiography n uandishi wa historia.
histrionic adj 1 tamthilia/thieta/ uigizaji. 2 -a unafiki, -a
uwongo. ~s n 1 maigizo (ya kwenye thieta). 2 tabia za kitamthilia au kithieta
(hasa zilizotiwa chumvi).
hit vt,vi 1 piga; gonga ~ somebody on the head piga mtu
kichwani. ~ a man when he is down; ~ a man below the belt fanya kinyume cha sheria za
masumbwi; (fig) shinda kwa hila. ~ it; ~ the nail on the head
pata, patia kabisa. ~ it off (with somebody togather) patana. ~-and-run attrib adj (of a road accident) -a kugonga mtu na
kukimbia. 2 ~ somebody hard hasiri. 3 pata, fikia. ~ the right path pata
njia. ~ the head lines (colloq of news) pewa umuhimu wa kwanza katika
gazeti; vuma sana gazetini. ~ the road (colloq) anza safari. 4
piga. ~ out (against) piga kwa nguvu; (fig) shambulia kwa nguvu. 5 ~ on/upon something pata kwa
bahati/bila kutegemea. 6 ~ something/ somebody off (colloq) elezea kwa kifupi na kwa
usahihi; dokeza. n 1
hitch
pigo. ~ man n (sl) mtu anayelipwa ili aue. 2 ushindi. ~ songs n nyimbo
zinazovuma/zinazosifika sana. make a ~ (with somebody) (colloq) pendeza sana
mtu; penya moyoni. ~ parade n orodha ya rekodi mashuhuri zinazouzika
sana. 3 utani mkali, kebehi, dhihaka.
hitch vt,vi 1 ~ something up vuta. 2 funga;
fungia; nasa ~ a horse to a fence fungia farasi bomani. 3 (also-hike) ~ (a ride/lift) (colloq) omba
lifti/msaada wa gari. n 1 mvuto; kumbo. 2 fundo. 3 kikwazo.
hither adv (old use) huku. ~-to adv
mpaka sasa.
HIV (abbr) kirusi kinachoondosha kinga ya mwili/kinachosababisha UKIMWI be ~positive wa na
Ukimwi.
hive n 1 (also bee~) mzinga wa nyuki; nyuki walio
mzingani. 2 mahali penye watu wengi wanaoshughulika. vt,vi 1 kusanya nyuki katika
mzinga. 2 ingia mzingani; ishi pamoja kama nyuki. ~ off (from) (fig) jitenga
(na kuwa chombo kinachojitegemea); gawa na fanya huru.
hives n ugonjwa wa mabaka ngozini.
hoar adj (liter) (of hair) -a mvi, (of a person)
-enye mvi. ~frost n jalidi. ~y adj -enye mvi (kwa
uzee); zee sana. ~iness n.
hoard n akiba; hodhi; hazina. vt,vi ~ (up) weka
akiba; hodhi. ~er n. (US bill board) (often temporary) ua wa mbao
(unaotumika kwa matangazo).
hoarse adj 1 (of voice) -liopwelea,
-a madende. 2 (of a person) -enye sauti iliyopwelea, -enye madende. ~ly adv. ness n.
hoax n mzaha, shere, dhihaka; hila. vt dhihaki, cheza
shere, fanyia mzaha; danganya kimzaha.
hob n bamba la chuma juu ya moto
jikoni.
hobble vt,vi 1 chechemea; chopea, pecha. 2 funga miguu miwili ya
hoi polloi
mnyama (k.m. punda/farasi) ili asiende mbali n mwendo wa kuchopea. ~ skirt n sketi inayobana sana
(inayomzuia mvaaji kutembea vizuri).
hobby n 1 jambo alipendalo mtu; jambo la kupitishia muda (kwa
kujiburudisha). 2 (arch) farasi mdogo. ~-horse n farasi wa mbao
(wa kuchezea/kwenye bembea), farasi wa fito au matete; (fig) (of conversation etc) mada anayoipenda mtu na anayoirudia
rudia.
hobgoblin n pepo mbaya.
hobnail n njumu. ~ed adj (of boots
etc ) -enye njumu.
hob-nob vi ~ (together) (with somebody) suhubiana (na); fanya urafiki
(na).
hobo (US sl) mzururaji.
Hobson's choice n see choice.
hock1 n goti la mguu wa nyuma wa
mnyama.
hock2 vt (sl) weka rehani. n in ~
rehani.
hockey n hoki: mpira wa magongo. ice ~ n hoki ya
barafuni. ~ stick n kigoe cha mpira wa magongo.
hocus-pocus n mrogonyo, udanganyifu. vt,vi rogonya,
vunga, chezea.
hod n chano, karai.
hodge-podge n see hotch-potch.
hoe n jembe. vt, vi lima; palilia (kwa
jembe). Dutch ~ n jembe la kusukuma.
hog n nguruwe; (fig) mtu mchafu/
mlafi/mchoyo. go the whole ~ fanya kitu kwa ukamilifu. ~-wash n
makombo, rojorojo; (fig) (esp of something said or written) -sio na
maana, upuuzi. vt,vi chukua/-la zaidi ya unavyotakiwa; chukua/-la kwa ulafi na
uchoyo. ~ish adj lafi na -enye choyo.
hogshead n 1 pipa kubwa, (hasa la kutilia pombe). 2 kipimo cha lita 240.
hoi polloi n (derog) the ~ n (pej)
hoist
makabwela, polo.
hoist vt inua, pandisha kwa roda. ~ a sail tweka tanga. n
chombo/kifaa cha kuinulia/kupandishia; roda; (colloq) kuvuta, kusukuma. give somebody a ~
sukuma/vuta mtu ili kumsaidia kupanda.
hoity-toity adj (colloq) -enye kichwa kikubwa, -enye
maringo/kujidai don't be so ~ usiwe na kiburi, usijidai.
hold1 vt,vi 1 shika, kamata. ~oneself well jiweka
imara; simama vizuri. ~ the line shikilia simu. 2 zuia. ~ one's breath zuia pumzi
(kwa woga n.k.). ~ one's fire acha kupiga risasi kwa muda. ~ one's tongue/peace
nyamaza, kaa kimya. there is no ~ing somebody/ something
haizuiliki, haiwezekani kumzuia/kuzuia. 3 shikilia. ~ oneself in readiness (for) jitayarishe
(kwa hatari), kaa tayari (kwa dharura). ~ one's sides with laughter shikilia
mbavu, cheka sana/vunjika mbavu. 4 weka; -wa na uwezo wa kuweka; chukua this tank ~s 30 litres tangi hili linaweza kuweka lita 30. (not) ~ water
(isiyo) kubalika. ~ something in one's head kumbuka. 5 fanya watu
wasikilize, sisimua the speaker held his audience spellbound msemaji aliwasisimua wasikilizaji wake. 6
ona; chukulia, amini. ~ somebody in high/low esteem heshimu/dharau mtu. ~ something dear/cheap
kuza/shusha thamani ya kitu, thamini sana/ kidogo. 7 linda; shikilia. ~ the fort (fig)
-wa na madaraka mwenyewe anapoondoka. ~ one's ground simama tisti. ~ one's own
kacha, -torudi nyuma. 8 fanya, anzisha, endesha ~ a meeting fanya mkutano. ~ court (fig)
karibisha, starehesha, kubali kuwa na maongezi na (washabiki/ wapenzi). 9 -wa na haki
ya, miliki. 10 -endelea vizuri. 11 shika nafasi. office ~er n mwenye
ofisi. 12
hold
himili, beba the new car ~s the road well gari hili jipya linahimili
barabara. 13 (uses with adverbial particles and preps). ~ something against acha kitu kiathiri wazo la mtu don't ~ his political views against him usimchukulie kuwa na makosa kwa sababu ya
mawazo/ msimamo wake kisiasa. ~ back sita. ~ somebody/something back fanya
mtu/kitu kisite; zuia; (of secret) ficha. ~somebody/ something down shikilia;
kandamiza. ~ a job down (colloq) dumu kazini (kwa kuonyesha uwezo). ~ forth sema kwa
kujikweza; jigamba; hubiri. ~ something forth toa; pendekeza. ~ something in zuia ~ in one's temper jizuia
(hasira). ~ off jitenga, kaa/baki mbali; chelewesha. ~ somebody/ something off zuia
mtu/kitu mbali. ~ on simama imara (kwenye matatizo/hatari); (usu imper) acha ~ on a minute acha kwanza
kidogo! ~ on to shikilia; -tokubali kutoa mali n.k.. ~ something on
shikilia; weka bolts and nuts ~ the wheels on parafujo na nati hizi vinashikilia magurudumu mahali
pake. ~ out shikilia; -tojisalimisha; dumu, endela kuwepo; (of hand) nyosha the workers are still
~ing out for higher wages wafanyakazi bado wanaendelea kudai mishahara ya
juu. ~ out on kataa kupatana/ kushirikiana. ~ somebody/ something out wa na
mtu/kitu; toa. ~ something over ahirisha. ~ something over somebody tumia kitu
kutisha; tishia. ~ to something fanya mtu atimize ahadi/mkataba, shikilia kuwa mwaminifu
kwa; endelea kushikilia. ~ somebody to something fanya mtu aweke ahadi
n.k.. ~ somebody (up) to ransom shikilia mtu mateka (ili kudai vitu
hold
mbalimbali). ~ together shikamana. ~ somebody/ something together fanya
ishikamane. ~ somebody/ something up shika, zuia; chelewesha; shikilia kwa
nguvu/vitisho (ili kuibia n.k.). ~ up n ushikiliaji wa nguvu,
wizi; fanya kuwa mfano. ~ somebody up to derision/scorn/ ridicule dhihaki
mtu. ~ with something kubali.
hold2 n 1 mshiko; kushika; uwezo wa kushika. 2 amri, madaraka he has great ~ over him ana madaraka makubwa juu
yake. 3 mahali pa kushikia. 4 (boxing and wrestling) mashiko. ~all n begi kubwa la kubebea
nguo. ~er n 1 kishikizi, kishikilia. 2 mwenye madaraka; mpangaji;
mmiliki; mshikaji. ~ing n kiwanja, shamba; umilikaji (agh wa
ardhi). small ~ ing n shamba dogo. ~ing company n kampuni mama.
hold3 n sehemu ya meli ya kuwekea mizigo.
hole n 1 tundu, shimo. make a ~ in tumia kiasi kikubwa cha the hospital charges made a large ~ in his savings gharama za hospitali zilipunguza kiasi kikubwa cha akiba
yake. pick ~s in tafuta kosa. a square peg in a round ~ mtu asiyefaa katika cheo
fulani. 2 (colloq) hali ngumu, mbaya; hali ovyo ovyo. 3 shimo la mnyama; (fig)
maficho; pango. ~-and-corner adj (colloq attrib) -a
chinichini, -a siri. 4. (golf) goli; pointi za magoli. vt,vi 1
toboa. 2 ~ (out) tia mpira (wa gofu) shimoni. ~ up (sl)
jificha.
holiday n 1 sikukuu; siku ya mapumziko. 2 (often pl) (US vacation)
likizo. ~-maker n mtu aliye likizoni; mtalii.
Holiness n utakatifu, uwalii. His/ Your H ~Baba
Mtakatifu.
holistic adj 1 -a jumla; -enye
holystone
kujali/chukulia kitu kizima/chote badala ya sehemu za kitu a ~ approach mkabala wa
jumla. 2 (medical) tiba ya mgonjwa.
holler vt,vi (sl) piga makelele.
holloa interj halo.
hollow adj 1 tupu; -a wazi. ~ ware n kibia. 2 (of sounds) sauti kama itokeayo sehemu
wazi/shimoni. 3 (fig) -enye hila; ongo, nafiki ~ victory ushindi wa kirahisi
mno. 4 -a kuingia ndani; -a kubonyea. ~ eyed adj -enye macho
ndani. 5 (colloq; as adv) beat somebody ~shinda hasa, kabisa. n
shimo; kibonde. vt ~ (out) fukua; komba.
holly n mholi: mti wenye majani yaliyo na ncha kali.
Hollywood n makao makuu ya utengenezaji filamu Marekani.
holm n kisiwa kidogo katika mto (hasa wakati wa mafuriko).
holm-oak n mwaloni.
holocaust n maangamizi makuu (hasa
ya watu kwa kuchomwa moto, mabomu n.k.) a nuclear ~ maangamizi ya watu kwa bomu la nyuklia.
holograph n holografu: maandishi yaliyoandikwa na mtu mwenyewe.
holster n mfuko wa bastola.
holy adj 1 -takatifu; -a kuhusiana na Mungu/dini. the H~ Bible; H-Writ n Biblia
Takatifu. the H~ Land n nchi ya Palestina. the H~ City n
Yerusalemu. H~ Week n Juma la Mateso. H~ Communion n
Komunyo; Ekaristi Takatifu. H~ Father n Baba Mtakatifu. ~ ground n sehemu
takatifu. ~ water n maji ya uzima. a ~ war n jihad, vita vya
kidini. 2 -a kumcha Mungu a ~ man mcha Mungu live a ~ life ishi kwa kumcha
Mungu. 3 a ~ terror n (sl) mtoto mtundu. n the H~ of Holies n
chumba/ mahali patakatifu, takatifu; (fig) mahali popote patakatifu.
holystone n jiwe la mchanga laini la
kusugulia meli/sitaha ya meli. vt
homage
sugua (kwa mchanga).
homage n 1 heshima kuu. do/pay ~ (to somebody) toa
heshima. 2 (in feudal times) heshima, utiifu kwa mtawala.
homburg n kofia laini.
home n 1 nyumbani, makazi, maskani. at ~ nyumbani; (football, etc) uwanja wa nyumbani. the ~ team n timu ya wenyeji/nyumbani; (of invitation) -wa nyumbani (kupokea wageni). at ~ n tafrija ya nyumbani (ambayo wageni wanatarajiwa kufika wakati maalum). not at ~ (to) -tokaribisha/-topokea wageni. make oneself/be/ feel/ at~ starehe, ondosha ugeni; jisikia nyumbani. at ~ in zoea. be ~ and dry (colloq) fanikiwa. a ~ from ~ mahali mtu anapojisikia yu mwenyeji. nothing to write ~ about (colloq) hakuna cha ajabu/maana. 2 kituo cha wasiojiweza. 3 (often attrib) maisha ya kifamilia. ~ economics n sayansi kimu. ~ help n (GB) mtu aliyeajiriwa kusaidia wasiojiweza. 4 (see habitat) maskani, makazi asilia. 5 (in sport and in various games) golini; kituoni. (baseball) the ~ plate n kituo cha nyumbani. ~ run mzunguko wa mpigo mmoja. the ~ straight/stretch n mwisho wa mbio fulani. 6 (attrib) one's ~ town makazi ya kudumu. Ministry for H ~ Affairs n wizara ya mambo ya ndani. 7 (compounds) ~-baked adj -liopikwa/ -liotenge nezwa nyumbani. ~ brewed adj pombe iliyotengenezwa nyumbani/ya kienyeji. ~coming n kurudi nyumbani. ~cured adj (of food esp bacon) -liokaushwa nyumbani. the ~ front n raia (wakati wa vita). ~grown adj (of food) -liopandwa/-liozalishwa nchini. ~ guard n mwanamgambo wa Uingereza (1940-57). ~land n nchi ya asili. ~ made adj (of bread, cakes, etc.) -liotengenezwa
homo
nyumbani. ~ Rule n utawala wa wananchi wenyewe. ~sick adj -a
kutamani/kukumbuka nyumbani. ~spun adj nguo iliyofumwa kwa mkono; -a
nyumbani. ~stead n nyumba iliyozungukwa na shamba; (US) shamba lililotolewa na serikali kwa kuishi na
kulima. ~ thrust n shambulio (kwa silaha au maneno) la nguvu. ~truth n ukweli
unaouma. ~work n kazi ya nyumbani, zoezi (kwa mwanafunzi) la kufanyiwa
nyumbani; (colloq) matayarisho (ya majadiliano, kuandika ripoti n.k.). ~ less adj
-sio na makazi like ~ -a kama nyumbani. ~ward adj -a kuelekea
nyumbani. ~ward(s) adv kwa kuelekea nyumbani adv 1 nyumbani,
nchini. 2 hasa, barabara. bring something/come ~ to somebody fahamisha
barabara. drive a point/an argument ~ eleza barabara. ~ly adj 1 -a kawaida a ~ meal mlo wa
kawaida. 2 -a kama nyumbani, -a kukumbusha mtu nyumbani kwao. ~liness n (US) (also of people, their features)
-siovutia. ~y (also homy) adj (US colloq) -a kama
nyumbani. homing adj (of pigeons) -enye silika ya kurudi
nyumbani; (of torpedoes, missiles) -enye uwezo wa kufikia shabaha
iliyolengwa.
homicide n uuaji wa binadamu; muuaji wa binadamu. ~ squad n (US) kikosi cha upelelezi wa mauaji
hayo. homicidal adj.
homily n hotuba, mahubiri, waadhi.
homiletic adj. homiletics n ustadi wa kuhutubia,
kuhubiri.
hominy n uji.
homo1 n (lat) mtu. ~ sapiens n ukoo safu wa kisasa, binadamu.
homo2 (pref) -a kufanana, -a jinsi moja. ~genous adj (formed of parts) -a jinsi
moja. ~geneity n namna moja, hali moja. ~genize vt fanya kuwa -a jinsi
moja; suka
homocentric
maziwa (ili kuchanganya mafuta na mtindi).
homocentric adj -enye kiinishirika.
homoeopathy n tiba inayotoa dalili za ugonjwa (kwa mtu asiye na ugonjwa
huo) homoeopath n tabibu wa tiba hiyo.
homograph n homografu: neno lenye tahajia sawa na lingine lakini maana au matamshi
tofauti.
homonym n homonimu: neno linalofanana na jingine lakini lenye maana
tofauti.
homophone n homofoni: neno linalotamkwa kama jingine lakini tofauti katika
tahajia, maana au chanzo.
homosexual n basha; msenge adj -a
kibasha; kisenge, -enye kuvutiwa na jinsi yake. ~ practices n vitendo vya kibasha (ubasha). ~ity n ubasha; usenge.
Hon, (abbr) see honorary; honorable.
hone n kinoo, jiwe la kunolea. vt noa. honest adj
-aminifu, -nyofu; -a kweli. to be quite ~ about it kusema ule
ukweli. make an ~ woman of somebody (dated use) oa mwanamke (baada ya
kujamiiana). ~ intention n nia njema. earn an ~ penny pata fedha
kihalali. ~ly adv kwa uaminifu. ~y n uaminifu;
ukweli.
honey n 1 asali ya nyuki. (fig) ~-dew n asali ya
mimea; utomvu; tumbaku tamu (tumbaku iliyotiwa asali). 2 (colloq) mpenzi. ~ed adj -a kama
asali, tamu kama asali. ~-comb n sega; (piece of) pambo lenye umbo la
sega. vt toboa matundu matundu.
honeymoon n fungate; (fig) kipindi cha maelewano mazuri mwanzoni mwa shughuli
fulani. vt kaa fungate.
honk n mlio wa bata bukini mwitu; honi. vt,vi piga/liza
honi; lia.
honour(US honor) n 1 heshima,
utukufu, adhama show ~ to one's parents heshimu, onyesha heshima
honour
kwa wazazi. do somebody ~; do ~ to somebody toa heshima/ heshimu mtu. maid of ~ n mpambe
(hasa wa malkia) guard of ~ gwaride la heshima. 2 sifa njema; uaminifu;
uadilifu. on one's ~ kwa sifa/uaminifu wake. an affair of ~ (hist) pambano la kutetea
hadhi. be/feel (in) ~ bound to do something wajibika (sio kwa sheria). one's word of ~
ahadi, kutimiza jambo. pay/incur a debt of ~ lipa deni kwa heshima. put somebody on his ~ amini
mtu. 3 (in polite formulas) kuheshimu, kustahi (mtu). do somebody the ~ of fanyia mtu
heshima. have the ~ of/to -wa na heshima ya (formal style) I have the ~to write to you nina heshima
kukuandikia. 4 Your/His ~ Mheshimiwa, Mtukufu. 5 an ~ n
mtu/jambo lenye kuleta sifa she is an ~to her group yeye ni mfano mzuri kwa kikundi
chake. 6 (pl) maadhimisho ya heshima, cheo, nishani. full military ~ n heshima zote za kijeshi
(agh. kwa mazishi ya shujaa au kukaribisha kiongozi wa heshima). do the ~s (colloq) (of the table,house etc.)
karibisha. 7 (pl) (in universities) nafasi ya juu katika digrii. ~s degree n digrii ya daraja la
juu. 8 (in card games) karata ya thamani kubwa. vt 1 heshimu,
tukuza, adhimu. 2 (comm) pokea na lipa kwa wakati maalum ~ a debt lipa deni ~ one's signature
kiri/kubali sahihi na kulipa fedha. honorary adj 1 (shortened in writing to Hon) (of a position)
-sio na malipo the honorary secretary katibu asiyelipwa. 2 (of a degree, rank) -a heshima an honorary member mjumbe wa
heshima. honorarium n honoraria, tunzo (isiyodaiwa). honorific adj (of expression) -a
heshima. ~ able (US honorable) adj 1 -a heshima, tukufu ~able
hooch
burial mazishi ya heshima. 2 ~able (abbr. Hon)
Mheshimiwa. Right ~able (abbr. Rt Hon) jina la heshima kwa wenye vyeo maalum
k.m. waziri n.k. ~ably adv.
hooch n (US sl) pombe kali.
hood n kifuniko; (of rain coats) ukaya; (of universities)
skafu; (of cars) kifuniko; (US) boneti. vt (chiefly in pp)
-funika na.
hoodlum (also hood) n jambazi (la
kutisha).
hoodoo n (chiefly US) kisirani, ndege mbaya. vt leta
mkosi/bahati mbaya.
hoodwink vt ~ somebody (into) hadaa.
hooey n (sl) upuuzi; puo.
hoof n kwato. cattle on the ~
ng'ombe wazima/hai. vt piga kwa kwato; (sl) piga teke.
hook n 1 kiopoo. a clothes ~;a crochet ~ n
kulabu. a fish ~ n ndoana/chango. ~ line and sinker (from fishing) (fig)
kabisa, zimazima, -ote. a fruit ~ n kigoe, upembo. be on the ~ (colloq)
-wa/kabiliwa na uamuzi mgumu wa kufanya. be/get off the ~ ondokana na
tatizo. ~ nosed adj -enye pua iliyopinda. ~ worm n
tegu. 2 (for cutting) nyengo. by ~ or by crook kwa vyovyote vile. 3 (cricket, golf) pigo la
kushoto; (boxing) pigo (la) kiko. vt,vi 1 vua; ngoeka, koeka; ~ a quiet husband (fig) koeka mume
mpole. 2 tengeneza ndoana/kiopoo. 3 ~ it (sl) toroka. 4 ~-up n (of radio) idhaa mbili au zaidi zenye matangazo ya
kufanana; idhaa muungano. ~ed adj 1 -enye umbo la kulabu, -enye
viopoo. 2 ~ed (on) (sl) -lioathiriwa na; -liotawaliwa na. ~er n (US sl)
malaya.
hookah n buruma.
hooky;hookey n play ~ v (US sl) toroka (shuleni).
hooligan n mhuni. ~ism n uhuni.
hoop1 n pete (la chuma/plastiki/mti);
hop
(of circus, game/croquet) duara, gurudumu put somebody/go through the ~(s) (fig)
ingiza/pitia katika mateso, sumbua sana; (of a cask) zingirisha bamba
mbavuni.
hoop2 n see whoop.
hooray int see hurrah.
hoot n 1 mlio wa bundi. 2 mlio wa honi. 3 sauti ya kuzomea. not care a ~/two ~s (sl)
-tojali kabisa. vi,vt 1 piga honi; lia kama bundi. 2 zomea students ~ed and jeered at the teacher wanafunzi walimzomea
mwalimu. ~er n king'ora, honi. (sl, GB) pua.
Hoover n kivuta vumbi. vt safisha
zulia n.k. kwa kivuta vumbi.
hooves pl of hoof.
hop1 n 1 mhopi: mmea mrefu wa kutambaa. 2 (pl) mbegu za
mhopi. ~garden/~field n shamba/bustani ya mhopi. ~-pole n
nguzo/waya za kusimamisha mhopi. ~picker; ~per n mchuma
mhopi, mashine ya kuchuma mhopi. vi chuma mhopi.
hop2 vi,vt 1 (of persons) ruka kwa mguu mmoja, chupa (of other living creatures e.g. frogs)
rukaruka. ~ off/it (sl) ondoka, ambaa. ~ping mad adj (colloq)
-liokasirika sana, -liofura hasira. 2 vuka dimbwi kwa kuruka. n 1 mruko wa mguu
mmoja. on the ~ -a kuchachawa, -a mchachariko . catch somebody on the ~ shughulisha
mtu. 2 mruko mfupi, mchupo. ~ skip/step and jump n zoezi la (mchanganyiko
wa) kuchupa, kupiga hatua na kuruka; (athletics) miruko mitatu (colloq) densi isiyo
rasmi. 3 (flying) kituo katika safari ndefu. ~ scotch n (of children) mchezo wa
vipande/ vyumba. ~ped-up adj (US sl) -liochajiwa kupita kiasi,-liozidishiwa
nguvu. ~per n chano, mdudu arukaye (k.m. tunutu, panzi n.k.); (in Australia)
Kangaruu. ~-light/~-casement n dirisha
hope
lifunguliwalo kwa juu lenye bawabu chini.
hope n 1 matumaini; tarajio have ~ of something tarajia kupata
kitu. hold out some/no/little/not much ~ (of something) -wa/tokuwa na matarajio ya kitu
fulani. be past/beyond ~; not have a ~ -wa bila/ondoa matumaini in the ~ of doing something kwa matarajio ya kufanya jambo
fulani. live in ~ (s) of something -wa na matarajio ya kitu fulani. raise somebody's ~s -pa mtu
moyo/matumaini. 2 tegemeo, tumaini the village farm was the ~ of the villagers shamba la kijiji lilikuwa ndilo tegemeo la
wanakijiji. ~ chest n (US) saraka la vifaa vya harusi (kwa msichana anayetaka
kuolewa); (GB see bottom drawer). vt,vi tumaini; tarajia; tegemea I ~ -to do something natarajia kufanya jambo
fulani. ~ against ~ endelea kutarajia ingawa matumaini hayapo hoping to hear from you natarajia utawasiliana
nami. ~ful adj 1 -enye matumaini. 2 -a kutia/leta matumaini. 3 (as n) (young) ~ful n mtoto anayeelekea
kufaulu; tumaini. ~fully adv 1 kwa mategemeo/ matarajio. 2
natarajia; itarajiwe. ~ fulness n. ~less adj 1 -sio na
matumaini; -sioleta matumaini. 2 -sioponyeka. ~lessly adv. ~lessness n.
horizon n 1 upeo wa macho. 2 (fig)
upeo wa fikira, elimu, ujuzi n.k.. ~tal adj -a mlalo, (-a kwenda) sambamba na upeo wa macho. ~ tal bar n mtaimbo wa mlalo. ~tally adv.
hormone n homoni.
horn n 1 pembe (ya mnyama). 2 kitu/ chombo cha pembe a ~ handle spoon kijiko cha pembe. ~ rimmed adj (of spectacles) -enye fremu ya pembe. a ~ of plenty see cornucopia. 3 (mus) baragumu, siwa, mbiu, gunda. 4 honi a motor
hors de combat
~ honi ya motakaa. 5 kitu kama pembe (k.m. kichwani mwa konokono). draw in one's ~s
tulia; jivuta; jirudi. 6 pembe za mwezi mchanga. on the ~s of a dilemma kabiliwa na uchaguzi mgumu
(kati ya vitu viwili visivyopendeza), -tokuwa na uchaguzi wa haja. 7 (compounds) ~ bill n hondohondo ~ blower mpiga
baragumu/gunda/siwa. ~pipe n dansi la baharia (la mtu mmoja). vi (sl, only in) ~ in (on) ingia bila
kukaribishwa, dukiza, vamia. ~ed adj -enye pembe. a ~ed goat n mbuzi mwenye
pembe. ~less adj -sio na pembe. ~like adj -a kama
pembe. ~y adj -a pembe; gumu kama pembe, sugu; (sl) -liojaa
nyege, mshongo.
hornet n nyigu, mavu. stir up a ~s'
nest; bring a ~s' nest about one's ears chokoza maadui; jiletea matata.
horology n maarifa ya kutengeneza
saa, wakati, usanifu saa.
horoscope n buruji (hasa kwa
kutazama nyota zilivyo mtoto azaliwapo) cast a ~ piga falaki. horoscopy n ufalaki, uaguzi.
horrendous adj -a kuogofya, -a kutisha. ~ly adv.
horror n kitisho, tisho; chukizo. chamber of ~s n makusanyo ya vitu, vielelezo n.k. vya kutisha/kikatili. strike with ~ ogofya; shtusha. ~ film n filamu ya kutisha. ~ struck/stricken adj -a kutishwa, -a kustushwa. horrible adj 1 -a kuogofya; -a kutisha. 2 (colloq) -baya, -siopendeza. horribly adv. horrid adj 1 -a kutisha. 2 (colloq) -a kuchukiza be horrid to somebody fanyia vibaya, sumbua, chukiza mtu. horridly adv. horridness n. horrific adj (colloq) -a kutisha. horrify vt ogofya, shtusha, tisha.
hors de combat pred adj (F) -sioweza kuendelea kupigana
(hasa kwa
hors-d'oeurve
sababu ya kujeruhiwa).
hors-d'oeurve n pl kuchangamsha
kinywa (mwanzo wa mlo).
horse n 1 farasi. a dark ~ n mtu ambaye bahati/nyota yake haijajulikana. a ~ of another colour jambo tofauti kabisa. back the wrong ~ unga mkono mshinde katika shindano. be/get on one's high ~ dai/kazania kupewa heshima inayostahili. eat/work like a ~ -la sana/fanya kazi kwa bidii. hold one's ~ taradadi, sita. look a gift ~ in the mouth pokea kitu bila shukrani. (straight) from the ~'s mouth (of tips, advice, information) halisi, toka kwa mwenyewe/ mhusika. 2 (collective sing) askari wapanda farasi ~ and foot askari wapanda farasi na wa miguu. ~ artillery n mizinga inayovutwa na farasi. 3 kiango, kitegemezi, farasi a clothes ~ kiango cha kuanikia nguo a towel ~ kiango cha kutundikia taulo. 4 (compounds) ~back n. (only in) on ~back mgongoni mwa farasi. ~box n gari la kubebea farasi. ~ breaker n mfunga farasi. ~droppings/dung n samadi/mavi ya farasi. ~flesh n nyama ya farasi; (pl) farasi. ~fly n nzi mkubwa (asumbuaye farasi/ ng'ombe). ~hair n manyoya (ya shingo/mkia) ya farasi. ~laugh n kikwakwa, kicheko cha kukwaruza na cha kelele. ~man n mpanda farasi (hasa bingwa). ~manship n ubingwa wa kupanda farasi. ~meat n nyama ya farasi. ~ play n mchezo wenye ghasia na kelele. ~pond n bwawa la farasi la kuogea na kunywa maji. ~power n (hp) nguvu farasi. ~ race n mashindano ya mbio za farasi. ~ sense n busara ya kawaida. ~ shoe n njumu/kiatu cha farasi; (kitu) -enye umbo la kiatu cha farasi a ~ shoe desk dawati lenye umbo la kiatu cha farasi. ~ whip n mjeledi/kiboko cha farasi. ~ woman n mwanamke
hot
mpanda farasi. horsy adj 1 -a kupenda farasi. 2 -a kuhusu
farasi.
hortative adj (formal) -a kuonya; -a
kutia moyo/kuhimiza.
horticulture n kilimo cha bustani, ukulima wa bustani. horticultural adj. horticulturalist n mkulima wa
bustani.
hosanna n int hosana (tamko) la
kumsifu Mungu au kumwabudu).
hose1 n mpira wa maji (wa kunyweshea bustani au kuzimia moto). ~pipe n bomba la mpira. vt 1 ~ (down) nywesha/mwagilia maji (bustani n.k.). 2 safisha (motokaa n.k.) kwa kutumia bomba la mpira.
hose2 n (collective, as pl) soksi. hosier n mwuza soksi, nguo za ndani. hosiery n bidhaa za mwuza soksi, fulana n.k.
hospice n 1 nyumba ya kupumzikia wasafiri. 2 hospitali ya wagonjwa
mahututi.
hospitable adj -karimu. hospitably adv. hospitality n
ukarimu.
hospital n hospitali. hospitalize vt laza mgonjwa
hospitalini.
host1 n 1 wingi. 2 (arch) jeshi.
host2 n 1 mwenyeji, (mwenye kukaribisha wageni). 2 mwenye hoteli reckon without one's ~ fanya mipango bila mawasiliano na wanaohusika. 3 (bio) kimelea. ~ess n mwenyeji wa kike mhudumu wa kike. air ~ mhudumu wa kike katika ndege.
Host n hostia: Mkate Mtakatifu.
hostage n 1 kole, mateka. 2 give ~s to fortune fanya uamuzi unaoweza kudhuru
baadaye.
hostel n hosteli, dahalia youth ~
hosteli ya vijana. ~ry n (arch) hoteli.
hostile adj -a uadui, -a uhasama, -enye uadui. ~ly adv. hostility n 1
uadui, uhasama. 2 (pl) vita.
hot adj 1 -enye joto, -a moto it's ~ today leo kuna joto I like ~ tea napenda chai ya
moto. be in/get
hot
into ~ water -wa matatani, aibika. be/get ~ under the collar
kasirika/ pandwa mori. make a place/make it too ~ for somebody (fig) fanyia mtu visa mpaka
ahame. 2 -kali this curry is ~ mchuzi huu ni mkali. 3 -a hasira; -a
kisirani; -kali. he has a ~ temper ana hasira; mkali. be ~ on the trail of somebody/on somebody's tracks karibia windo
(kinachofuatiwa). 4 (in hunting) (harufu) kali, bichi. 5 (of music, esp jazz)
motomoto. 6 (sl) (of stolen goods) -sioweza kuuzwa hadharani, bomu. 7 (as adv)
sasa. blow ~ and cold (fig) yumbayumba (katika uamuzi), shindwa kuwa na
uamuzi. give it to somebody ~ adhibu/ karipia vikali. 8 -enye nyege. 9 (special use with nouns and particles) ~ air n maneno
matupu/ ahadi za uongo. ~bed n tuta lenye mbolea au samadi, la kuotesha
mboga; (fig) mahali penye maovu (mabaya, fitina) mengi. ~blooded n
-enye harara (ya moyo), -a hamaki. ~ cross bun n keki yenye alama ya msalaba
(inayoliwa Ijumaa Kuu). ~ dog n soseji katika mkate. ~foot adv kwa
bidii, enda upesi. ~gospeller n (colloq) mhubiri mwenye
mhemko/bidii sana; ~head n mkaidi; mkali. ~ headed adj
-enye harara, -kali; -kaidi. ~house n kibanda (agh. cha kioo) cha kuoteshea maua na
matunda. ~ line n simu ya moja kwa moja kati ya wakuu wa serikali
mbalimbali. ~ money n mfuko wa fedha unaopelekwa mahali penye kupata riba
kubwa. ~ news n habari motomoto. ~plate n kisahani cha
jiko, jiko la kisahani kimoja. ~ potato n (fig) (colloq) jambo gumu au lisilopendeza
kushughulikia; suala nyeti. ~ rod n (US sl.) gari lenye; mbio kuzidi magari
yote. the ~ seat n kiti cha umeme (cha kunyongea); (fig) hali ya mtu ambaye analazimika kuamua mambo
hour
magumu (k.m. wakuu wa serikali). ~ spot n (colloq) sehemu yenye
matatizo/fujo za kisiasa. ~ spring n chemchemi ya maji moto. ~stuff n (sl)
mtu/kitu bora. ~tempered adj -enye hasira. ~water-bottle n mpira wa
majimoto. vt,vi ~ something up (colloq) pasha moto; (fig)
iva; shikwa na harara. ~ly adv kwa harara, kwa hamaki.
hotchpotch n mchanganyiko his article is a ~ of other people's ideas makala yake ni mchanganyiko wa mawazo ya
wengine.
hotel n hoteli. residential ~ n hoteli yenye makazi the ~ trade biashara ya
hoteli. ~ier n mtunza hoteli.
hottentot n 1 Mhotento/Mkhoisan (mtu mweusi wa kabila moja la Afrika
Kusini). 2 Kikhoisan.
hound n 1 mbwa mkubwa wa kuwindia follow the ~s winda na mbwa Master of H ~s Mkuu wa
Uwindaji. 2 (dated, colloq) mtu mbaya, (mjuvi), fidhuli; duni, mshenzi. vt
fukuza, winda na mbwa; fuatafuata, sumbua.
hour n 1 saa a four ~s' journey mwendo wa saa nne. at the eleventh ~ katika dakika za
mwisho. the small ~s usiku mkubwa/wa manane. ~glass n
shisha. ~ hand n akrabu, mkono wa saa. 2 kipindi, muda, wakati wa siku come at an early ~
wahi, fika mapema they bother me at all ~s of the day and night wananisumbua wakati wote in the ~ of danger wakati wa
hatari. 3 (pl) wakati agh wa kazi. work long ~s fanya kazi mchana
kutwa. after ~s adv baada ya saa za kazi. out of ~s baada/nje ya saa za
kawaida. keep good/bad/early/late/regular ~s amka/lala, anza/maliza kazi,
ondoka/rudi nyumbani/mapema/ umechelewa. ~ly adj -a kila saa, -a kutokea
(kufanyika) kila saa moja
houri
adv baada ya kila saa, saa yoyote, wakati wowote.
houri n hurulaini.
house n 1 nyumba. get on like a~ on fire (of people) elewana haraka sana, fanya urafiki baada ya muda mfupi wa kufahamiana. under ~ arrest kuzuiliwa nyumbani. 2 (usu with a pref) kibanda, jengo, nyumba hen ~ kibanda cha kuku store~ ghala. ware~ n bohari. custom~ jengo la ushuru. the H~ of God n Nyumba ya Mungu, kanisa. ~ of cards n nyumba ya karata; (fig) mpango wa wasiwasi. ~ of ill fame (old use) danguro. on the ~ kwa gharama ya kilabu au kampuni. 3 bunge enter the H~ chaguliwa kuwa mbunge. 4 keep a good ~ fadhili/kimu nyumba vyema. keep open ~ -wa tayari kupokea wageni nyumbani wakati wowote, -wa mkarimu. set/put one's ~ in order nyoosha mambo yako. 5 ukoo, jamaa agh. ya watawala. 6 (theatre) hadhira. bring down the ~/bring the ~ down shangiliwa sana na wote waliopo. 7 (compounds) ~ agent n wakala wa nyumba. ~boat n mashua nyumba, mastakimu. ~bound adj -liozuiliwa nyumbani. ~ breaker (US ~wrecker) n jambazi (avunjaye nyumba ili aibe); mtu anayeajiriwa kubomoa majumba. ~coat n koti la nyumbani. ~craft n maarifa ya utunzaji wa nyumba. ~dog n mbwa mlinzi/anayelinda nyumba. ~ father/mother n mlezi wa makazi ya watoto. ~ flag n bendera ya shirika la meli. ~fly n nzi. ~ful n nyumba iliyojaa (watu). ~hold n kaya. ~hold guards n watumishi/ wanajeshi wa mfalme. ~hold word n neno/jina litumikalo na wengi. ~holder n mwenyeji, mwenye nyumba. ~keeper n msimamizi/ mtunzaji wa nyumba. ~lights n taa za sinema (n.k.). ~maid n mhudumu wa nyumbani. ~ maid's
how
knee n uvimbe wa goti. ~man n (GB) daktari msaidizi wa mtaalam akaaye
hospitali. ~master n mwalimu mlezi wa bweni. ~ party n wageni wa siku kadhaa
shambani. ~ physician n daktari akaaye hospitali. ~proud adj
-enye fahari kubwa ya kutunza nyumba. ~room n nafasi. ~sparrow n
shorewanda. ~ surgeon n daktari mpasuaji akaaye hospitali. ~ top n (chiefly in) cry/publish/proclaim something from the ~tops tangaza
hadharani. ~ trained adj (of domestic pets) -liofunzwa,
-liofundishwa kuwa safi katika nyumba. ~ warming n sherehe ya kuhamia nyumba
mpya. ~wife n mke afanyaye kazi za nyumbani. ~ wifely adj -a kuhusu mke afanyaye kazi za
nyumbani. ~wifery n kazi za mke wa nyumbani. ~work n kazi za
nyumbani. vt 1 -pa nyumba, karibisha. 2 weka/hifadhi vitu (agh. vyombo na
vitabu) n makazi. housing association shirika la kujenga na kugawa nyumba
(bila kupata faida). housing estate eneo la nyumba za kupanga au kuuz(w)a.
hove pt, pp of heave.
hovel n kibanda kibovu.
hover vi 1 vinjari, zungukazunguka
angani the helicopter ~ed over the airport helikopta ilizungukazunguka juu ya uwanja wa ndege. ~craft n hovakrafti: chombo kiendacho majini na nchi kavu kwa kuelea juu ya hewa. 2 (of persons) ngojea. (fig) ~ between life and death karibia kifo.
how adv 1 jinsi (gani); namna gani;
je; kwa vipi ~ is the car driven? gari linaendeshwa namna gani? ~ did they catch you? walikukamata namna gani/walikukamataje? ~'d ye do n (colloq) vurumai, hali ya mambo ni shaghalabaghala. 2 kiasi
howdah
gani, -ngapi ~ much? kiasi gani? ~ old are you una umri gani?/una miaka mingapi? And H~! naam! Sawa! Na kweli! 3 (introducing an indirect statement) jinsi, he told me ~ he had been mistaken for a thief alinieleza jinsi alivyodhaniwa kuwa ni mwizi. 4 (in exclamations!) ~ intelligent he is! ana akili kama nini! 5 (in asking for opinion etc.) ~ is that una maoni gani? unaonaje? una maana gani? H~ come? kwa nini; vipi ~ come you are always late? kwa nini unachelewa kila wakati. H~ so kweli? kwa vipi? unaweza kuthibitisha kuwa hivyo ndivyo? H~ about going for a walk unaonaje tukitembea kidogo ~ do you find your new home? unayaonaje makazi yako mapya? ~ beit (conj. arch) hata hivyo. ~ever adv kwa hali yoyote, hata kama I will never agree ~ ever hard you try to persuade me sitakubali kwa hali yoyote/hata unishawishi namna gani conj hata hivyo. ~soever adv kwa hali yoyote.
howdah n (Ind) kiti chenye mwavuli (kilichofungwa mgongoni mwatembo).
howitzer n mzinga wa masafa mafupi.
howl n 1 mlio mkali (agh. wa mbwa mwitu). 2 kilio cha maumivu makali.3 (of amusement) kikwakwa. 4 (of wind) mvumo. vt,vi lia kwa ukelele (k.m. mbwa); (of wind) vuma; (with laughter) cheka kwa sauti kubwa. ~ down zomea, zima ~ down the lecturer zima mhadhiri. ~er n kosa la kijinga; kichekesho. ~ing adj (sl) sana, mno, -a wazi, tupu it was a ~ing injustice ulikuwa uonevu wa wazi kabisa. a ~ing shame n aibu kubwa sana/tupu.
hoyden n jikedume, msichana mjeuri/ shupavu. ~ish adj.
hub n hebu: kitovu cha gurudumu;
hullo
(fig) kitovu cha shughuli (agh. biashara n.k.).
hubble-bubble n buruma.
hubbub n makelele, ghasia, zahama.
hubby n (GB) (colloq) mume
hubris n (Gk) kujiona, kiburi, kujivuna.
huckaback n kitambaa kigumu cha
kutengenezea taulo.
huckster n mchuuzi.
huddle vt,vi 1 songa; songamana; songana, banana. 2 ~ up against banana, jibana na. 3 rundika. n rundo, chungu, mkusanyiko (wa vitu au watu). be in/go in a ~ (colloq) (of persons) kutana pembeni/faragha.
hue1 n rangi. ~d adj (in compounds) -enye rangi.
hue2 n (only in) ~ and cry n makelele (agh ya kufukuza mwizi au kutoridhika) raise a ~ cry piga makelele.
huff1 n hasira, chuki. be in/get into a ~ nuna, -wa na shonde. ~ish; ~y adj -enye kuchukia upesi.
huff2 vi pumua kwa nguvu, tweta.
hug vt 1 kumbatia. 2 (fig) ng'ang'ania, shikilia ~ old beliefs ng'ang'ania imani za zamani. 3 ~ the shore (of a ship) ambaa pwani. 4 ~ oneself (with pleasure/ delight) over something jawa na furaha, jipongeza n kumbatio.
huge adj -kubwa mno. ~ly adv. ~ness n.
hugger-mugger n vurugu; siri adj
-enye vurugu; -a siri adv kwa vurugu; kwa siri.
hula n hula: dansi/ngoma kama nachi ya wenyeji wa Hawaii.
hulk n 1 (old ship) chombo cha zamani (kitumiwacho kama stoo, zamani kilitumiwa kama jela); meli ya ovyo. 2 jitu la ovyo, kubwa (na jinga).
hull n ganda, kumvi. vt menya kumvi, ambua, goboa.
hullabaloo n ghasia, makelele.
hullo (also hallo, hello) interj 1 aisee!,
hum
halo! 2 (in answering a telephone)
hum vi 1 vuma (kama nyuki); imba
(hali midomo imefungwa). ~ming bird n ndege mvumaji. ~ming top n pia. 2 pamba moto, changamka. 3 (sl) nuka. 4 (usu ~ and haw/ha (colloq)) uma ulimi, sitasita katika kusema. n mvumo.
human adj 1 -a binadamu, -a watu ~ rights haki za binadamu. 2 -enye ubinadamu, -enye utu. ~ly adv. ~e adj -ema, -enye huruma, pole. ~eness n. ~ism n 1 elimu ya ubinadamu (inayohusu binadamu kwanza na mahitaji yake kuliko misingi ya dini). 2 utu, moyo wa kupenda watu. 3 sanaa (karne 14-16) yenye misingi ya Ugiriki na Urumi. ~ist n mwanafunzi/mfuasi wa elimu ya ubinadamu, mpenda utu; mwanafunzi wa sanaa ya Ugiriki/Urumi adj -a ubinadamu. ~itarian adj -a hisani, -a fadhila, -a huruma. n mfadhili, mwanahuruma. ~itarianism n. ~ity n 1 binadamu. 2 ubinadamu. 3 huruma, wema, utu. 4 the ~ities sayansi za jamii. ~ize vt fanya/kuwa binadamu; staarabisha; fanya -a utu. ~kind n wanadamu, walimwengu.
humble adj 1 -nyenyekevu, -enye soni, -siyetaka makuu eat ~ pie omba radhi (kupita kiasi), piga magoti; jidhalilisha. 2 (of persons) -a chini, -nyonge, -siokuwa muhimu; (of things) -a kimaskini, duni a ~ occupation kazi duni. vt dunisha, shusha hadhi, dhalilisha. humbly adv.
humbug n 1 unafiki; ghiliba, ulaghai. 2 mnafiki; laghai, ayari (GB) gubiti interj upuuzi. vt laghai, danganya ~ somebody into doing something ghilibu mtu atende jambo.
humdinger n (US sl) mtu/kitu kilicho bora au cha ajabu.
humdrum adj -a kuchusha; -a kawaida.
humerus n (pl) muungabega.
hung
humid adj (esp of air, climate) -enye unyevunyevu. ~ify vt fanya nyevu. ~ity n unyevu.
humiliate vt aibisha, fedhehesha; shushia/vunjia hadhi, dhalilisha. humiliation n aibu, fedheha. humility n unyenyekevu.
hummock n kilima kidogo, kiduta. ~y adj.
humour, (US humor) n 1 kichekesho, uchekeshaji, ucheshi sense of ~ ucheshi the book has a lot of ~ kitabu kina vichekesho vingi. 2 hali ya mtu he is in a good ~ yu mchangamfu, yu mkunjufu he is not in the ~ for playing with the children hana moyo wa kucheza na watoto. out of ~ kutojisikia mkunjufu, kutofurahi, kusonona. 3 ridhisha, kubalia ~ a patient ridhisha mgonjwa (kwa kutimiza matakwa yake). ~ist n mchekeshaji, chale. ~ous adj. ~ously adv.
hump n 1 kibyongo (of a cow, camel etc.) nundu. ~back n mtu mwenye kibyongo. ~backed adj -enye kibyongo, -enye nundu. 2 kero, hasira; mfadhaiko. have/give somebody the ~ (sl) kera/kereka vt ~ (up) bong'oa, pinda.
humph int mmh! sauti ya kuonyesha wasiwasi/kutoridhika.
humus n mboji.
hunch n 1 kipande kinene; kibyongo; nundu .~backed n -enye kibyongo. 2 have a ~ that (colloq) fikiri/hisi kwamba. vt ~ (up) bong'oa, pinda.
hundred n adj mia two ~ mia mbili ~s mamia ~s of people mamia ya watu in ~s kwa mamia a ~ and one mno a ~ to one kwa bahati sana. a ~fold adj -a mara mia adv kwa mia adj -a mia, -a sehemu mia kwa moja. n sehemu mia kwa moja. ~weight n ratili mia na kumi na mbili. ~th n, adj sehemu moja ya mia; -a mia.
hung pt,pp of hang.
hunger
hunger n 1 njaa. be/go on (a) ~
strike goma kula (kwa sababu ya kupinga/kudai kufunguliwa. ~ march n maandamo ya wasio na kazi kutangaza mateso yao.~marcher n. 2 hamu, tamaa, shauku a ~ for love hamu ya mapenzi. vi ~ for tamani/taka sana. hungry adj 1 -enye njaa; -enye kuleta njaa. 2 (of soil, land) -sio na rutuba. 3 (fig) -enye shauku ~ for something -wa na shauku ya kitu fulani. hungrily adv.
hunk n kipande kinene (hasa cha mkate).
hunkers n pl (colloq) matako; mapaja. on one's ~ kwa kuchutama/chuchumaa.
hunky-dory adj (sl) shwari; bora,
-zuri.
hunt n 1 a/the ~ kuwinda; mawindo. 2 msako, kutafuta the ~ for the criminals msako wa wahalifu. 3 (esp in GB) kundi la wawindaji (wa mbweha na paa) wanaotumia mbwa na farasi; mawindoni. ~ ball n sherehe rasmi ya wawindaji. ~er n mwindaji; farasi wa kuwindia. 4 saa ya mfukoni (yenye kifuniko cha chuma). ~ing n kuwinda, uwindaji. (attrib) ~ ing horn n baragumu la kuwinda. ~ing ground n (fig) mawindoni: mahali penye mategemeo ya mtu kupata anachokitafuta. happy ~ ing ground (joc) mbinguni. ~ress n (liter) mwanamke mwindaji. vi,vt 1 winda. 2 tafuta, saka. ~ for a lost pencil tafuta kalamu iliyopotea. ~ down saka, tafuta na pata ~ down a criminal saka mhalifu. ~ for/out/up tafuta. ~ out tafuta. 3 fukuza ~ the dog out fukuza mbwa. ~sman n 1 mwindaji. 2 kiongozi wa mbwa wa kuwindia.
hurdle n 1 kiunzi (cha kufanyizia zizila muda n.k.). 2 kiunzi, (kinachorukwa katika mashindano ya mbio na ya farasi) ~ race mbio za kuruka viunzi. 3 (fig) kikwazo,
husk
jambo lililo gumu kufanywa. vt,vi 1 ~ off tenga kwa viunzi. 2 ruka viunzi. ~r n mtengeneza viunzi; mruka viunzi.
hurdy-gurdy n kinanda, (agh hupigwa kwa kuzungusha mkono).
hurl vt tupa kwa nguvu, vurumisha. n mtupo wa nguvu; kutupa kwa nguvu.
hurling n mchezo wa Ireland unaofanana na mpira wa magongo.
hurly-burly n makelele, fujo, ghasia, vurumai.
hurrah interj mlio wa shangwe (wa
kushangilia); riboribo! shangalia.
hurricane n tufani, kimbunga ~lamp/lantern kandili, fanusi, taa ya chemni.
hurry n 1 haraka. in a ~ haraka haraka. don't ~ usifanye haraka be in a ~ -wa na haraka. 2 mapema, hivi karibuni I won't go there again in a ~ sitaenda tena pale hivi karibuni. vt,vi harakisha, fanya haraka. ~ away enda/ ondoka haraka. ~ up fanya haraka, harakisha. hurried adj -liofanywa kwa haraka; -enye haraka. hurriedly adv.
hurt vt,vi 1 umiza; dhuru; uma, wanga. 2 (of feelings) tia uchungu, sononesha. 3 (bad effect) leta madhara. n 1 maumivu; madhara. ~ful adj -enye kuumiza; -a kudhuru; -enye kutia uchungu.
hurtle vi enda, ruka kwa mbio sana; vurumishwa.
husband n mume. vt hifadhi, tumia kwa uangalifu ~ one's strength hifadhi nguvu. ~man n (old use) mkulima. ~ry n ukulima animal ~ ufugaji.
hush vt, vi nyamaa, nyamaza, nyamazisha. H~! Nyamaza! kimya! ~ something up ficha, fanya iwe siri. n a/the ~ ukimya; utulivu. ~ money n (pesa) kifunga mdomo. ~-~ adj (colloq) -a siri sana.
husk n ganda, kapi, kumvi, kumbi. vt
hussar
koboa, ambua; fua. ~y adj 1 kavu kama kapi. 2 (of voice) -a mikwaruzo, -liopwelea. 3 (of a person) (colloq) kipande. n 1 mbwa wa Kieskimo. 2 kipande cha mtu. ~ily adv. ~iness n.
hussar n askari mpanda farasi, askari
wa farasi.
hussy n mwanamke asiye na maana/
thamani; msichana mjeuri/mjuvi.
hustings n (pl) the ~ kampeni ya uchaguzi (hotuba, mabango n.k.).
hustle vt,vi 1 songa, sukumiza, sukuma, harakisha (kwa mkukumkuku). 2 (esp US) (colloq)
laghai, uza/pata kitu kwa nguvu (hasa kwa kudanganya). 3 (US sl) -wa malaya. n (sing only) mkukumkuku Manzese bus stop was a scene of ~ and bustle kituo cha basi cha Manzese kilikuwa mahala pa mkukumkuku. ~r n 1 pwaguzi, laghai. 2 (US sl) malaya.
hut n kibanda. ~ment n ago/kambi la vibanda. ~ted adj.
hutch n tundu, kirimba, kizimba (hasa cha sungura).
hybrid adj mahuluti. ~ maize n mahindi mahuluti. n 1 chotara. 2 (bio) mvyauso. ~ize vt vyausa, zalisha chotara. ~ization n uvyausaji.
hydra (myth) n haidra: joka kubwa labaharini lenye vichwa vingi.
hydrant n bomba la maji (la mtaani
linaloweza kutumika kuzima moto, kusafisha barabara n.k.).
hydrate n (chem) haidreti: chumvi
maji. vt,vi changanya kemikali na maji.
hydraulic adj haidroli: -nayoendeshwa kwa maji/kioevu. hydraulics n pl haidroliki: sayansi ya matumizi ya maji kupata nishati.
hydro pref haidro -a kuhusiana na
maji, -a maji. ~electric adj -a umeme wa nguvu za maji. ~foil, ~ plane n boti mpao. ~logy n haidrolojia: sayansi ya maji. ~meter n haidromita: chombo cha
hypocrisy
kupimia uzito wa maji na viowevu. ~pathy n utabibu kwa kutumia maji. ~phobia n 1 kalabi: ugonjwa wa kushindwa kunywa maji kwa sababu ya koo kujikaza; ugonjwa wa kichaa cha mbwa. 2 woga wa maji. ~phyte n kimeamaji (k.m. mpunga, majimbi). ~phitic adj -a majini. ~tropism n uelekeomaji. ~ponics n haidroponi: sayansi ya kuotesha mimea kwenye maji. ~us adj -a majimaji. ~gen n haidrojeni. ~ gen bomb (also H -bomb) bomu la haidrojeni. ~carbon n haidrokaboni. ~chloric adj. -a haidrokloriki. ~electric umeme wa nguvu za maji, -a
hyena, hyaena n fisi.
hygiene n elimusiha; usafi. hygienic adj -a afya, -a kuleta afya, -a bila vijidudu vya maradhi. hygienically adv.
hymen n kizinda.
hymn n wimbo wa kidini (wa kumsifu Mungu). vt tukuza Mungu kwa kuimba. ~al n kitabu cha nyimbo za dini.
hyper pref -a zaidi, -a kupita kiasi.
~bole n mbalagha: kutia chumvi sana katika kuelezea kitu. ~bolic adj. ~critical adj -enye kukosoa mno, -enye kuhakiki mno, -enye kutafuta makosa. ~market n duka kuu (lenye eneo kubwa na aina zote za bidhaa agh nje ya mji).
hyphen n kistariungio (-). vt (also ~ate) unganisha na kistari ungio.
hypnosis n kiinimacho; hiponozi: hali ya kuwa kama katika usingizi mzito ambapo mtu anaweza kukuamrisha na wewe ukatenda bila kujijua. hypnotic adj. hypnotism n. hypnotize vt laza/pumbaza akili. hypnotist n mtu apumbazaye akili.
hypochondrial n kunyong'onyea; unyong'onyevu, ulegevu wa moyo (hasa wa kuona mashaka juu ya afya). hypochondriac adj, n.
hypocrisy n unafiki, uzandiki.
hypodermic
hypocrite n mzandiki, mnafiki. hypocritical adj. hypocritically adv.
hypodermic adj (of drugs etc) -a chini ya ngozi. ~ syringe n sindano ya kuingiza chini ya ngozi n dawa ya kuingiza chini ya ngozi.
hypotenuse n kiegana: upande mrefu wa pembetatu, -enye pembe mraba.
hypothesis n nadharia tete. hypothetical adj -a nadharia tete; -a kubuni, -sio na uhakika.
hysteria n 1 umanyeto, mpagao. 2 mpwitompwito (wa jumla), jazba. hysterical adj. hysterically adv.