I,i n herufi i; (herufi ya tisa katika alfabeti ya Kiingereza); namba moja (1) ya Kirumi pron mimi.
ibex n mbuzi mwitu (mwenye pembe kubwa zilizopinda) wa milima ya Alps na Pyrenees).
ibid; ibidem adv (Lat) katika kitabu (msitari, kifungu, ukurasa) kile kile kilichotajwa.
ibis n kwarara.
ice1 n 1 barafu. break the ~ (fig) anza kuchangamkiana na mgeni; anza kitu kigumu/nyeti; vunja ukimya cut no ~ (with somebody) -toathiri; -toingia. keep something on ~ weka kwenye friji/jokofu; (fig) weka akiba be skating on thin ~ (fig) tembea mleoleoni, chezea hatari. 2 chakula kitamu kilichogandishwa. cream ~s n malai. 3 (compounds) ~ Age n Enzi ya Barafu. ~ berg n siwa barafu; (fig) mtu baridi. ~boat n mashua barafu. ~ bound adj (of harbours, etc.) -liokingwa na barafu. ~box n sanduku la barafu (la kuwekea chakula). ~cap n kilele barafu (k.m. kilele cha mlima wa Kilimanjaro). ~-cream n aiskrimu. ~cube n kipande cha barafu (agh. kilichogandishwa katika friji). ~ fall n poromoko barafu. ~field n uwanda barafu. ~floe n barafu tandavu (inayoelea).~-lolly n shikirimu ya kijiti. ~ man n (US) mtembeza/ muuza barafu. ~pack n mapande ya barafu yaliyotanda juu ya bahari; mfuko wa barafu (agh. hutumika kutuliza homa). ~-show n maonyesho juu ya barafu. ~pick n chombo cha kuvunjia barafu. ~rink n uwanja wa ndani wa barafu. ~-skate n kiatu cha kutelezea barafuni.
ice2 vt,vi 1 fanya kuwa baridi sana. ~d drinks n vinywaji baridi sana. 2 ~ over/up funika, funikwa na barafu;tanda kwa barafu the pond was ~d over bwawa lilifunikwa na barafu. the wings of the aircraft had ~d up mabawa ya eropleni
identify
yafunikwa na barafu. 3 funika (agh. keki) kwa sukari unga.
icicle n mchirizi wa barafu.
icing n 1 kiikizo. 2 mkusanyiko wa barafu kwenye mabawa ya eropleni.
icy adj -a kama barafu, baridi sana; -liofunikwa kwa barafu. icy cold adj baridi sana. icily adv (lit, fig) kwa kupooza.
ichneumon n 1 nguchiro mla mayai ya mamba. 2 (also ~ fly) nzi mtagia mayai kwenye mabuu ya wenzake.
icon n taswira (in the Eastern Church) ikoni: sanamu/picha ya mtakatifu, sanamu/picha takatifu. ~clast n mpinzani wa mila ya kuabudu sanamu k.m. katika Ulaya Mashariki na Walokole wa Uingereza katika karne ya 17; (fig) mtenguamila.
id n (psych) (the) ~ silka.
idea n 1 dhana, wazo, nia I have no ~ sijui, sina habari/wazo lolote. 2 (plan) mpango; azimio; nia, lengo. 3 (opinion) fikira, shauri. 4 (feeling) imani, hisia, jinsi ya kufikiri the young ~ fikira ya kitoto. 5 (conception) kujua, kutambua, utambuzi. put ~s into somebody's head mpe mtu tumaini. 6 (in exclamations): what an ~! haya mambo gani!
ideal adj 1 -lio bora, kamilifu. 2 (unreal, fanciful) -a njozi. n maadili/ wazo/mfano bora/kamilifu. ~ly adv. ~ize vt fanya/ona kama kamilifu. ~ization n. ~ism n 1 kanuni za maisha fulani. 2 (in art) (opposite of realism) ulimbwende. 3 (in philosophy) udhanifu.~ist n mdhanifu. ~istic adj.
identical adj 1 ~ (to/with) sawa sawa. 2 pacha, -a kufanana be ~ fanana. 3 ~ twins n mapacha. ~ly adv.
identify vt 1 tambua; tambulisha. 2 ~ something with something fananisha. 3 ~ with somebody/ something jihusisha; tegemeza; shirikisha, funganisha. identification n. identity n 1 sura, kufanana, kuwa sawa kabisa give one's identity jitambulisha. identikit n sura ya mtu iliyochorwa (agh. ya
ideogram
mhalifu) prove one's identity thibitisha nafsi. identity card/disc/certificate n kitambulisho. 2 utambulisho.
ideogram ideograph n idiogramu:
maandishi yasiyohusishwa na sauti bali dhana au kitu. ideographic adj.
ideology n itikadi. ideological adj.
ideologically adv.
id est (i.e.) yaani.
idiolect n lugha ya binafsi.
idiom n 1 lugha; lahaja. 2 nahau; mbinu. ~atic adj 1 -enye nahau, -a mbinu. 2 -a nahau. ~atically adv.
idiosyncrasy n upekepeke, tabia (nia, desturi, mwenendo, mazoea n.k.) ya mtu peke yake.
idiot n 1 zuzu. 2 (colloq) mpumbavu. idiocy n uzuzu; (folly) upumbavu mtupu. ~ic adj. ~ically adv.
idle adj 1 -sio na kazi; -liotulia,
-siotumika. 2 vivu, legevu. 3 -sio faa; -a bure. vi,vt 1 ~ (away) -wa bila kazi; -wa vivu/zembe. 2 (of a car) endelea kuwaka (wakati gari limesimama). ~r n. idly adv. ~ness n.
idol n 1 sanamu; kijimungu. 2 (great favourite) kipenzi he is the ~ of his parents anapendwa na wazazi wake. ~ater n 1 mwabudu sanamu, mwabudu kijimungu. 2 mpenzi. ~atress n mwanamke mwabudu sanamu. ~atrous adj -a kuabudu sanamu. ~atrously adv. ~atry n 1 kuabudu sanamu; mapenzi makubwa. ~ize vt abudu kama mungu; penda mno. ~ization n.
idyll n 1 masimulizi mafupi (hasa mashairi) ya habari za maisha ya shambani/vijiji. 2 kipindi cha amani na furaha. ~ic adj -zuri sana; -a kupendeza sana (kuhusu maisha ya shambani).
if conj 1 ikiwa, iwapo, kama ~ you ask me, I will help you kama ukiniomba nitakusaidia ~ he should come please call me iwapo atakuja niite ~ you will wait a moment I will help you kama utasubiri kidogo
ilk
nitakusaidia ~ I were rich I would buy a car laiti ningekuwa tajiri ningenunua gari ~ we'd started in time we would have finished earlier kama tungeanza mapema tungemaliza mapema. 2 (if meaning when, whenever) kama/kila ~ you mix yellow and blue you get green ukichanganya manjano na buluu unapata kijani. 3 (even) ~ hata kama we'll finish even ~ it takes us all week tutamaliza hata kama itatuchukua wiki nzima even ~ ingawa, ijapokuwa l'll escort her even ~l'll be late for the movie nitamsindikiza ingawa nitachelewa sinema. 4 as ~ kana kwamba it isn't as ~ we don't know the work si kana kwamba hatujui kazi. 5 (colloq) (if replacing whether, to introduce an interrogative clause) kama let me know ~ you are coming niambie kama utakuja. 6 (a wish or unfulfilled condition) ~ only laiti (kama) n too many ~ s and buts ngonjera, taraghani.
igloo n msonge (wa barafu).
igneous adj (of rocks) -lioundwa na volkano.
ignite vt, vi washa, tia moto. ignition n mwako. ignition key n ufunguo wa gari.
ignoble adj -sioheshimika; -a aibu. ignobly adj. ignominious adj -a aibu, -a kufedhehesha, -a kutahayarisha, -a kuadhirika. ignominy n aibu, fedheha, utwezo.
ignorance n ~(of) n ujinga. ignoramus n mjinga. ignorant adj 1 ignorant (of) -jinga, -siojua (to) be ignorant of a subject kuwa mbumbumbu; -tojua jambo fulani. 2 -a kijinga an ignorant question swali la kijinga.
ignore vt -toangalia, -tojali.
iguana n gongola: mjusi mkubwa kuliko gonda.
ikon n see icon.
il- pref kinyume cha, -sio.
ilk n of that/his ~ (colloq hum) -a
ill
namna (jinsi, jina) ile.
ill adj 1 (usu pred) -gonjwa. fall/be taken ~ -wa mgonjwa, ugua. 2 (attrib) baya, -ovu, -a madhara. it's an ~ wind that blows nobody any good (prov) hakuna baya lisilokuwa na uzuri wake. ~ weeds grow apace (prov) ubaya huvuma haraka kuliko wema. 3 (compounds) ~-advised adj -sio na busara, pumbavu. ~ affected (towards) adj -siopendelea jambo fulani.~-bred adj -liolelewa vibaya; jeuri. ~-breeding n tabia mbaya. ~-favoured adj -baya, -enye sura mbaya, -a kuchukiza. ~-gotten adj -liopatikana kwa njia mbaya (magendo, wizi n.k.). ~-humoured adj -enye usununu. ~-judged adj -lioamuliwa vibaya. ~-looking adj -enye sura mbaya. ~-mannered adj -sio na adabu nzuri, fidhuli. ~-natured adj -kali, -enye hasira. ~omened adj -enye bahati mbaya, kisirani, chimvi. ~-tempered adj -gomvi. ~-timed adj -liopangiwa muda mbaya, -liofanywa wakati mbaya/usiofaa. n 1 madhara, uovu. do ~ fanya baya/uharibifu. 2 mkosi, kisirani; matatizo, shida the ~s of life matatizo ya maisha. 3 (compounds) ~-disposed (towards) adj -enye nia ya kudhuru; -a kutopenda jambo fulani. ~-fated adj -enye kisirani, -enye mkosi. ~-luck n bahati mbaya. ~-starred adj -enye bahati mbaya -enye nyota mbaya. ~ treat; use vt tesa, dhulumu. ~-treatment;~ usage n ukatili, uonevu, dhuluma. ~-will n uadui; ukatili, roho mbaya adv vibaya; ovyoovyo, -kwa kutoridhisha. be/feel ~ at ease -jiona vibaya/pweke; -ona haya. speak ~ of somebody sema mtu vibaya, sengenya. ~ness n ugonjwa.
illegal adj haramu, -a kinyume cha sheria, -sio halali ~ act kitendo cha kinyume cha sheria. ~ly adv. ~ity n.
illustrate
illegible adj -siosomeka. illegibly adv. illegibility n.
illegitimate adj. 1 -a kinyume cha sheria. 2 -a haramu ~ child mwana haramu. 3 (of a conclusion in an argument, etc) -sio na mantiki, -liohitimishwa vibaya. ~ly adv. illegitimacy n.
illiberal adj 1 -siostahili mtu huru; -
siopenda uhuru (wa mawazo, maisha n.k.) -enye fikra finyu, -siokuwa na uvumilivu. 2 bahili. ~ly adv. ~ity n.
illicit adj haramu; -liyokatazwa ~ trade biashara ya haramu ~ relationship uhusiano usio halali/usioruhusiwa. ~ly adv. ~ness n.
illimitable adj -kubwa sana, -sio na
mipaka/kikomo.
illiterate adj (person) -tojua kusoma wala kuandika ~ person mtu asiyejua kusoma na kuandika; mjinga. illiteracy n.
illogical adj -sio na mantiki. ~ly adv. ~ity; ~ness n.
illuminate vt 1 tia nuru, angaza, mulika. 2 pamba (barabara n.k.) kwa taa. 3 pamba herufi kwa rangi ya dhahabu. 4 (explain) eleza, fafanua. illumination n 1 mwanga, nuru, mwangaza. 2 (pl) (coloured illustration) herufi za mapambo za rangi ya dhahabu/fedha; rangi za kumetameta. 3 (usu pl) kupamba mji (barabara n.k.) kwa taa; taa za kupambia mji (barabara n.k.). illumine vt (liter) 1 tia nuru. 2 -pa mwanga wa kiroho.
illusion n 1 njozi, uongo entertain/ indulge in ~ jitia katika ndoto/fikra za uwongo. be under an ~ danganyika. cherish an ~/the ~ that... penda kuamini. have no ~s about somebody/something -todanganyika; fahamu fika 2. kudanganyika kimawazo. ~ ist n mfanya mazingaombwe. illusive; illusory adj -a kinjozi, -a uongo.
illustrate vt 1 eleza kwa mifano, picha
im
au kielezo. 2 chora picha/vielezo katika kitabu/jarida. illustrator n mchoraji picha/vielezo katika vitabu. illustration n 1 kielezo. 2 (explanation) kueleza kwa mifano. illustrative adj -enye kutoa ufafanuzi au mifano kwa jambo fulani. illustrious adj maarufu, mashuhuri; adhimu. illustriously adv.
im- (pref) kinyume cha; siyo, pasipo, bila.
image n 1 sanamu, picha an ~ of Jesus Christ sanamu (picha) ya Yesu Kristo. 2 kifani, mfano, nakala he is the ~ of his father anafanana na baba yake God created man in his own ~ Mungu amemuumba binadamu kwa mfano wake. be the (very/spitting) ~ (of something/ somebody) fanana kabisa na mtu/kitu fulani. 3 taswira; fikra, dhana. 4 tamathali za usemi speak in ~ zungumza/andika kwa kutumia tamathali za usemi. 5 sura (kama inavyoonekana katika kioo, maji, kamera n.k.). vt 1 chora/chonga sanamu, picha (ya kitu fulani). 2 akisi. ~ry n matumizi ya tamathali za usemi katika mazungumzo/ maandishi; sanamu, picha, michoro.
imagine vt 1 (for a mental picture of) waza, fikiria, dhani I can't ~ being a doctor sifikirii kuwa daktari. 2 dhania, kisia, amini I ~ him to be clever namkisia kwamba yu hodari. imaginable adj -a kuweza kufikirika/ kubunika. imaginary adj -a mawazo tu, -a kufikirika, -a kubuni. imagination n 1 ubunifu. 2 wazo, fikra, dhana. imaginative adj bunifu, -enye uwezo wa kufikiri/kubuni; -enye mawazo/fikra nyingi.
imam n imamu.
imbalance n kutolingana uzito/nguvu, kutokuwa na urari (k.m. wa hesabu).
imbecile adj -punguani; -pumbavu. n
punguani; bozi, zembe, pumbavu. imbecility n 1 upuuzi; upunguani. 2 (pl) matendo/maoni ya kipumbavu/ kipuuzi.
immediate
imbed vt see embed.
imbibe vt 1 (formal) -nywa, sharabu. 2 (learn) jifunza, hifadhi akilini (mawazo, maarifa n.k.).
imbroglio n ghasia, machafuko, nazaa, (hasa ya kisiasa au hasira).
imbue vt ~ with (formal) tia moyoni, jaza (shauku) ~d with sympathy/ hatred etc. -liojaa huruma/chuki n.k.
imitate vt 1 iga, fuatisha, nakili it is
advisable to ~ good manners ni bora kuiga tabia njema parrots ~ human speech kasuku huiga sauti ya binadamu. 2 fanana; fananisha na, wa kama a paper was designed to ~ a Bank note karatasi ilisanifiwa ili ifanane na noti ya benki. imitator n mwigaji. imitation n 1 uigaji. 2 mfano, bandia. 3 mwigo imitations of animal cries miigo ya sauti za wanyama. imitative adj -a kuiga; -a kufuatisha. imitativeness n.
immaculate adj safi kabisa, pasipo
mawaa; pasipo kosa, pasipo dhambi. the ~ conception n (RC Church) Bikira Maria, Mkingiwa Dhambi ya Asili. immaculacy n. ~ly adv.
immanent adj ~ (in) (of qualities)
-a ndani, -a asili; (of God) -a kuwepo kila mahali daima. immanence n.
immaterial adj 1 ~ (to) (unimportant) -sio na umuhimu/maana sana, si kitu it is quite ~ haidhuru; haina maana ~ alterations mabadiliko yasio na maana. 2 -sio na mwili, -a pepo, -a roho.
immature adj -changa, -siopevuka ~ seeds mbegu changa ~ girl kigori. immaturity n uchanga, hali ya kuwa bado kukomaa/kupevuka.
immeasurable adj -siopimika; -a
kupita kiasi; -sio na mwisho/mpaka, kadiri. immeasurability n.
immediate adj 1 (instant) -a mara moja; -a sasa hivi ~ answers majibu ya mara moja. 2 (close) -a karibu sana; -a jirani the ~ relatives ndugu wa karibu the ~ heir to the throne mrithi wa ufalme anayefuata.
immemorial
immediacy n. ~ly adv 1 sasa hivi; papo hapo; moja kwa moja; mara moja. 2 karibu moja kwa moja (conj) mara tu ~ I have the news I will let you know mara nipatapo habari nitakuambia. ~ness n.
immemorial adj -a zamani za kale,
-a kale sana. from time ~ tangu zama (ni) za kale.
immense adj -kubwa sana. ~ly adv
mno, kwa kiasi kikubwa; (colloq) sana; kwa wingi; hasa; tele. immensity n ukubwa (wa kupita kadiri); (pl. immensities) vitu vikubwa mno.
immerse vt ~ (in) 1 chovya; tosa; zamisha; tumbukiza. 2 (occupy fully) shughulisha, zama katika shughuli (mawazo, kitabu n.k.). immersion n 1 mchovyo; mzamo; tumbukio. 2 (occupation) kushughulika, uzamaji katika shughuli (mawazo, kitabu n.k.). immersion heater n kichemshio (cha umeme).
immigrate vi ~ (to/into) ingia nchi kwa kusudi la kukaa, hamia nchi nyingine. immigrant mhamiaji. immigration n uhamiaji immigration officer ofisa uhamiaji.
imminent adj (of events, esp dangers) -a karibu sana, -a kuelekea kutokea upesi rains are ~ mvua ziko karibu his death is ~ kifo chake kiko karibu. ~ ly adv. imminence n.
immobile adj -sioenda; -siojijongeza;
-sioweza kuendeshwa; tuli kabisa. immobilize vt -fanya isiweze kusogea/kujongea; simamisha kabisa, fanya jeshi/gari lishindwe kusonga mbele; zuia fedha zisitumike. immobilization n. immobility n.
immoderate adj -a kupita kiasi, -ingi mno, -a kukithiri, -sio na kadiri. ~ly adv.
immodest adj 1 pasipo haya. 2 -chafu, -baya, -potovu ~ acts matendo machafu/ya upotovu. ~y n 1 upujufu, ukosefu wa haya/adabu. 2 uhayawani, upotovu. ~ly adv.
immolate vt ~ (to) (formal) tolea
impair
kafara, dhabihu, tambika. immolation n kutolea kafara, kudhabihu, kutambika.
immoral adj 1 -baya, -ovu. 2 -enye
tabia mbaya, -sio adilifu; (licentious) fisadi;fasiki/asherati ~ purposes dhamira ya kifisadi/potovu. 3 (of books) chafu. ~ity n 1 ubaya, uovu. 2 tabia mbaya, upotovu, ukosefu wa maadili; ufisadi acts of ~ vitendo vya kiovu/kifisadi.
immortal adj -a kuishi milele, -siokufa; -siosahauliwa n the ~s miungu ya Kiyunani na ya Kirumi; wasiokufa. ~ity n maisha ya milele, uzima/uhai usio na mwisho, kutokufa; sifa njema ya milele/inayodumu. ~ize vt -pa maisha ya milele; -pa sifa za daima.
immovable adj 1 -siohamishika (k.m. jengo, mimea) ~ property mali isiyohamishika. 2 thabiti, imara, madhubuti n (pl) ~s mali zisizohamishika. immovability n. immovably adv.
immune adj ~ (from/against /to)
(from disease) -enye kingamaradhi; (from harm by poison etc.) -sioweza kudhurika kwa sumu n.k.. immunity n 1 (exemption) kinga diplomatic ~ kinga ya kidiplomasia (kuhusu kodi ya forodha, upekuzi n.k.). 2 (from disease) kinga maradhi. immunize vt -pa kingamaradhi; kaga; fanya sugu. immunization n. immunology n. elimu ya kingamaradhi.
immure vt (formal) funga, tia ndani; weka kizuizini.
immutable adj (formal) -siobadilika, -siogeuka. immutably adv. immutability n.
imp n shetani mdogo, kishetani, pepo mbaya. ~ish adj -tundu. ~ishly adv. ~ishness n.
impact n ~ (on) 1 mgongano; dharuba. 2 athari, matokeo. vt gonga; pambanisha; songanisha (kwa kugonga).
impair vt haribu; dhoofisha. ~ mentn.
impala
impala n swalapala.
impale vt fuma. ~ment n.
impalpable adj -sioonekana; -sio shikika; -siohisika; -sioeleweka. impalpability n. impalpably adv.
impanel vt see empanel.
impart vt 1 ~(to) pa, gawa. 2
arifu, pasha ~ news to somebody pasha mtu habari.
impartial adj adilifu, -adili;
-siopendelea, -enye haki. ~ly adv kwa uadilifu, kwa idili. ~ity n uadilifu, idili.
impassable adj -siopitika the rivers are ~ mito haipitiki, haivukiki. impassability n.
impasse n 1 kichochoro kisichotoka/ kilichofungwa mwishoni. 2 shida kubwa; kipingamizi, kizuizi.
impassioned adj -enye hamaki/hamasa. impassive adj baridi, -tulivu,
-sioonyesha hisia. ~ly adj. ~ness n. impassivity n.
impatient adj 1 ~ for something/to do something -a haraka, -enye pupa, bila subira. 2 ~ (at something/with somebody) -sio vumilivu, -sio mili grow ~ kosa subira, -wa mwenye pupa. 3 be ~ of kasirishwa na kitu fulani. ~ly adj. impatience n.
impeach vt 1 onyesha wasiwasi juu ya tabia ya mtu. 2 tuhumu. ~ somebody for/of/ with something, ~ somebody for doing something (legal) shtaki mtu (agh. kwa kosa la kutumia madaraka vibaya). ~ment n.
impeccable adj maasumu, -siokosea,
bila kosa. impeccability n. impeccably adv. impeccant adj.
impecunious adj (formal) fukara, mkata.
impede vt zuia, kwamisha. impediment n kizuizi, kikwazo (of speech) kigugumizi (of marriage) kipingamizi cha ndoa. impedimenta n (pl) mizigo ya msafiri, vikorokoro (agh. vya majeshi).
impel vt ~ (to) sukuma; lazimisha;
himiza; chochea. ~lant adj, n. ~ler
impersonal
n.
impend vi karibia, -wa karibu. ~ence; ~ancy n. ~ing adj.
impenetrable adj. ~ (to) 1 -siopenyeka; -siopitika ~ to water -siopenya maji. 2 (unintelligible) sioeleweka, -siotambulikana, -a fumbo. impenetrability n.
impenitent adj -siotubu; -a moyo mgumu. ~ly adv. impenitence n.
imperative adj 1 -a haraka, muhimu, -a kuangaliwa mara moja. 2 -a kuamuru; (necessary) -a lazima, -a sharti. 3 -a kusikiwa, -a kutiiwa; -liotolewa (-liofanywa) kwa thabiti. n (gram) kitenzi cha kuamuru k.m. Go! Nenda! ~ly adv.
imperceptible adj -sioeleweka; -siotambulika (kwa sababu ya udogo). imperceptibly adv.
imperfect adj 1 -enye dosari, -kosefu, (in growth, development) -viza, -liovia. 2 (gram) ~ (tense) n isiotimilifu. n (gram) hali inayoendelea/isiyotimilifu. ~ion n. ~ly adv.
imperial adj 1 -a kifalme (hasa wa Kiingereza); -a kibeberu ~ laws sheria za ufalme/kifalme. 2 (grand, magnificent) bora, -kubwa. 3 (of weights and measures) -a Kiingereza ~ measurements vipimo vya Uingereza (k.v. painti, galoni. n 1 kionja mchuzi. 2 kipimo cha ukurasa (63 x 95 cm). ~ly adv. ~ism n ubeberu (kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni). ~ist n. ~istic adj. imperious adj 1 -a kuamrisha he is very ~ anajiona; -a sharti. 2 -a haraka sana. imperiously adv. imperiousness n. imperium n dola, ufalme wenye mamlaka makubwa.
imperil vt hatarisha.
imperishable adj -sioharibika; -siooza; -a kudumu milele.
impermeable adj. ~ (to) (formal) -siopenyeka.
impermissible adj -sioruhusiwa.
impersonal adj 1 -sioathiriwa na hisia (za mtu binafsi); -siohusishwa na
impersonate
mtu maalum. 2 (of verbs) vitenzi visivyohusishwa na vitu hai it is raining mvua inanyesha. 3 -sio a kibinadamu ~ forces nguvu za asilia (k.v. upepo). ~ ly adv.
impersonate vt iga, jifanya (mtu mwingine), jisingizia. impersonation n 1 kuiga/kuigwa. 2 hali ya kuiga. impersonator n.
impertinent adj 1 -fidhuli, -safihi,
-a ufyosi/fyosi he was ~ at me alinifidhulikia. 2 -siohusiana (na kitu kinachonenwa). impertinence n. ~ly adv.
imperturbable adj (formal) -tulivu,
-siosisimka, -siohangaika/ hangaishwa. imperturbability n.
impervious adj ~ (to) 1 -siopitisha kitu, -siopenyeka ~ to water -siopenya maji, -siovuja. 2 (fig) -kaidi, -siosikia he is ~ to criticism hasikii ushauri.
impetigo n upele ambukizi wa malengelenge.
impetuous adj -a harara; -a haraka; -a bidii (bila kufikiri); -a kishindo. ~ly adv. impetuosity n.
impetus n kichocheo, nguvu, msukumo.
impiety n 1 kufuru. 2 tendo/neno la
kukufuru. impious adj -a kukufuru, bila heshima. impiously adv.
impinge vi,vt ~on/upon athiri, husu.
~ment n.
implacable adj -siosuluhishika;
-sioridhika; -siotulizika. implacability n. implacably adv.
implant vt 1 ~ in tia/kaza/jenga fikira moyoni, tia/kaza ndani imara. 2 (bio) pandikiza, gandamanisha (mnofu au mmea) katika kiumbe kingine. ~ation n.
implausible adj -siowezekana kuwa kweli, -a shaka. implausibly adv.
implement n kifaa, chombo (cha kazi). vt tekeleza ~ a contract tekeleza mkataba. ~ation n.
implicate vt ~ (in) husisha/ingiza mtu (lawamani/hatarini). implication n 1 kuhusisha/kuingiza lawamani/
impose
hatarini. 2 maana, kidokezi.
implicit adj ~ (in) 1 inayojitokeza (bila kutajwa), -liodokezwa. 2 thabiti. ~ belief n imani thabiti. ~ly adv. imply vt (indicate) dokeza, -wa na maana, onyesha bila kutaja.
implore vt ~ (for) omba sana, sihi, rairai ~ something from somebody omba sana kitu kutoka kwa mtu fulani. imploring adj. imploringly adv.
implosion n mlipuko kwa ndani. implode vi pasukia/lipukia ndani.
impolite adj -sio na adabu, pasipo heshima; -sio staha.~ly adv. ~ness n.
impolitic adj -sio busara.
imponderable adj (phy) 1 -siokadirika, -sio nzito. 2 (fig) -siopimika, dogo sana. n (pl. ~s) visivyokadirika, visivyopimika, sifa/hisia zisizopimika.
import vt ~ (from/into) 1 ingiza bidhaa kutoka nchi za nje. 2 maanisha, -wa na maana; onyesha. n (usu pl) 1 maduhuli: bidhaa ziingizwazo ~s & exports maduhuli na mahuruji: bidhaa zinazoingia na zinazotoka. 2 uingizaji. 3 maana, umuhimu matters of ~ mambo ya maana. ~er n. ~ation n.
important adj 1 -a maana, muhimu. 2 (of a person) -enye madaraka makubwa, kubwa look ~ jifanya kuwa mtu wa maana. ~ly adv. importance n.
importunate adj 1 -a kuombaomba, -a
kuchosha kwa maombi, -enye udhia. 2 (of affairs) -a muhimu na haraka. ~ly adv. importunity n. importune vt importune (for) 1 ombaomba sana. 2 (of a prostitute) dai; omba mno; tongoza.
impose vt,vi 1 ~ on somebody amuru, lazimisha. 2 (exact) ~ on toza, lipiza ~ a tax on something toza kodi kitu. 3 ~ upon something tumia nafasi/nzuri/kasoro n.k. (kwa manufaa) ~ an obligation upon somebody lazimisha mtu ~ hands on
impossible
somebody wekea mikono. imposing adj -a kuvutia (kwa sababu ya ukubwa, sura n.k). imposingly adv. imposition n kutoza; kuweka; kutumia (vibaya). imposition of something upon somebody kutoza mtu ushuru wa kitu imposition of conditions kuweka masharti.
impossible adj -siowezekana; -siofanyika it is ~ for me to haiwezekani make it ~ for somebody to fanya iwe ngumu kwa mtu (kufanya) you are ~ wewe ni mtu mgumu, huwezekani. the ~ n kisichowezekana suppose the ~ fikiria jambo lisilowezekana (kutokea). impossibly adv. impossibility n kutovumilika.
impost n kodi; ushuru; ada.
impostor n ayari, laghai (ambaye anajifanya mtu mwingine). imposture n ulaghai, utapeli.
impotent adj pasipo nguvu, dhaifu,
-siofaa neno; (of males) hanithi, -siofaa. ~ly adv. impotence n.
impound vt 1 kamata (mali) kisheria. 2 fungia (wanyama waliopotea) bomani.
impoverish vt 1 fukarisha, fanya kuwa maskini. 2 (weaken) punguzia nguvu, dhoofisha, chakaza. ~ed adj maskini; -liochakaa, dhaifu. ~ment n 1 umaskini, ufukara. 2 udhaifu.
impracticable adj -siotekelezeka,
muhali; (of routes) -siopitika, -sioweza kutumika. impracticably adv. impracticability n. impractical adj -siofaa/weza kutendwa; -sioweza kutenda.
imprecate vt ~ on/upon somebody (formal) laani mtu. imprecation n laana, apizo imprecatory adj.
imprecise adj -sio sahihi, -enye kosa.
imprecision n. ~ly adv.
impregnable adj -sioshindika; -a
kuweza kuzuia/kuhimili mashambulio yote, -sioingilika. impregnably adv. impregnability n.
impregnate vt ~ (with) 1 tia/-pa mimba. 2 kifu. 3 jaza.
impresario n 1 meneja wa kikundi cha
impromptu
sanaa. 2 mdhamini wa burdani, hadhara.
impress vt ~ (on/upon)/with 1
gandamiza, (imprint) piga chapa/ mhuri n.k. 2 (influence) shawishi; athiri, vutia ~ something on somebody's memory tia kwenye/athiri fikra za mtu I was not much ~ed sikuvutiwa sana how did that ~ him? jambo hilo lilimvutia namna gani? be favourably ~ed pendezwa mno. n chapa; alama ya muhuri. ~ion n 1 chapa, alama. 2 toleo, chapa (jumla ya nakala za vitabu zilizopigwa chapa pamoja). 3 (notion) fikra, wazo, maono; picha it is my ~ion nionavyo be under the ~ion that fikiria kwamba, pata picha/wazo, ona. ~ionism n mbinu ya uchoraji, uandishi, uandikaji (usiotiwa madoido). ~ionist n. ~ionistic adj. ~ionable adj -epesi kuathiriwa, -epesi kushawishika. ~ ionability n. ~ive adj -a kuvutia; -enye kuathiri; -enye kuchochea hisia (za ndani) ~ive ceremony sherehe iliyovutia. ~ively adv. ~iveness n.
imprest n masurufu: fedha anayopewa mtumishi wa umma kutumia kwa kazi maalum.
imprimatur n (RC Church) kibali rasmi; ithibati ya kupiga chapa kitabu the book has received the ~ of the Government kitabu kimepata ithibati ya serikali; (fig) kibali, idhini.
imprint vt ~ with/on 1 chapa; piga
muhuri. 2 tia moyoni ideas ~ed on the mind fikra zilizotiwa moyoni n alama, wazo moyoni.
imprison vt funga, tia kifungoni/ gerezani/jela. ~ment n kifungo life ~ment kifungo cha maisha.
improbable adj si yamkini, -sioelekea kuwa kweli; -sioelekea kufanyika I think the story is ~ ninafikiri hadithi hii si yamkini. improbably adv. improbability n kutoelekea kuwa kweli.
impromptu adj -a papohapo,
improper
-siotayarishwa kabla ~ speech hotuba ya papo kwa papo (bila kutayarishwa kabla) adv papo hapo; bila maaandalizi he spoke ~ aliongea pale pale.
improper adj 1 -siofaa vulgar language is ~ before children lugha ya matusi haifai mbele ya watoto; -sio vizuri, si adabu it is ~ for children to shout while adults are talking sio vizuri kwa watoto kupiga kelele watu wazima wanapoongea. 2 (indecent) -chafu. 3 -sio sawa, sio sahihi. ~ly adv. impropriety n utovu wa adabu, (indecency) upujufu, uchafu; jambo lisilofaa.
improve vt,vi 1 endeleza; -wa -zuri zaidi; fanya vizuri zaidi. ~ on/upon tengeneza vizuri zaidi things are improving mambo yanaanza kutengemaa; (of health) pata nafuu. 2 tumia vizuri (wakati, faida, hali). ~ment n 1 kuendeleza. 2 maendeleo; kufanya vizuri zaidi. improvable adj -enye kutengenezeka, -enye kustawishika.
improvident adj (formal) -siofikiria wakati ujao; badhirifu. ~ly adv. improvidence n. ubadhirifu.
improvise vt,vi 1 faragua. 2 tunga (tengeneza, vumbua) papo hapo ~d song wimbo uliotungwa wakati ulipokuwa ukiimbwa; tengeneza kwa haraka bila vifaa vyake hasa. improvisation n. ufaraguzi.
imprudent adj -sio busara, -a kijinga. ~ly adv. imprudence n tendo la kijinga.
impudent adj -fidhuli, -juvi, -safihi;
jeuri. ~ly adv. impudence n ufidhuli, usafihi.
impugn vt (formal) bisha, tia/tilia
shaka. ~able adj -enye kubisha, bishi.
impulse n 1 msukumo give an ~ to
endesha, sukumiza; (desire) shauku, raghba, hamu, mihemko ya ghafula. on the ~ of the moment mvuto wa ghafla insane ~ msukumo wa kiwazimu irresistible ~ msukumo
in
usiozuilika. 2 mhemko wa ghafla on (an) ~ mara moja, bila kutafakari. impulsion n msukumo, kutaka kwa ghafla; kichocheo. impulsive adj (of persons, their conduct) -a msukumo; -a harara; -a kuamua ghafla. impulsively adv. impulsiveness n.
impunity n kupona/kuepuka adhabu. with ~ bila hofu ya kuadhibiwa wala kuumia.
impure adj 1 -chafu; -enye najisi; -liochanganywa. 2 -a ashiki, -kware. n unajisi. impurity n uchafu, takataka; najisi.
impute vt ~ (to) (formal) shutumu, tuhumu, zulia; dhania. imputation n tuhuma, shutuma; kudhania, kuzulia imputation on a character kusingizia, kusuta.
in1 adv part (contrasted with out) 1 ndani ya (used with many vv) come ~ ingia. give ~ salimu amri. 2 be ~ -wa nyumbani; fika, wasili is the train ~ yet? garimoshi limefika? (of crops) vunwa; patikana mangoes are ~ now embe zinapatikana sasa; ingia the new fashion is ~ mtindo mpya umeingia the new Director is ~ power mkurungezi mpya ameshika madaraka/ameingia kwenye madaraka. 3 be ~ for something patikana na jambo baya; -wa tayari kufanya jambo, pata. have it ~ on something taka kulipiza kisasi. be ~ on something (colloq) husika kwenye shirika, -wa na sehemu/fungu kwenye jambo/kitu. day ~, day out; week ~, week out; year ~, year out siku nenda rudi, kila siku, mara nyingi. ~ and out kuingia na kutoka mara kwa mara. be (well) ~ with somebody patana na, -wa katika hali ya urafiki na, elewana na mtu. 4 (preceding a n). an ~-patient n mgonjwa aliyelazwa hospitalini.
in2 prep (for use of/ in/ with many nn and vv) 1 (of place) -ni, katika, kwenye the village ~ which he was born kwenye kijiji alichozaliwa ~
in
Tanzania Tanzania; children playing ~ the street watoto wanaocheza mtaani ~ school/church/mosque shuleni/kanisani/msikitini. 2 (of direction) kwa ~ this direction kwa upande huu ~ all directions (kwa) pande zote. 3 (indicating direction of motion or activity) ndani ya, katika he put his hands ~ the pockets aliweka mikono yake mifukoni they fell ~love walipendana cut the orange ~ two kata chungwa katika vipande viwili. 4 (of time when) kwenye, mnamo, wakati wa ~ 1990 mnamo mwaka wa 1990, mnamo mwaka 1990 ~ his youth katika ujana wake ~ the morning wakati wa asubuhi. 5 (of time) katika, baada ya ~ the presence of wakati akiwepo I shall be back ~ a short-time nitarudi katika muda mfupi/baada ya muda mfupi. 6 (indicating inclusion) kwenye seven days ~ a month siku saba kwenye mwezi ~ his thirties kwenye miaka ya thelathini. 7 (indication of ratio) kwa one ~ five moja kwa tano. 8 (of dress etc) -wa na/-enye/katika, -liovaa the woman ~ white yule mwanamke mwenye nguo nyeupe ~ uniform katika sare. 9 (indicating physical sorroundings, circumstances etc) go out ~ the rain nenda, toka kwenye mvua sleep ~ the open lala nje/sehemu ya wazi. 10 (indicating state or condition) ~ good order katika hali nzuri ~ a hurry kwa haraka ~ secret kwa siri ~ poverty kwenye/katika umasikini. 11 (indicating form, shape, arrangement) ~ three parts katika sehemu tatu ~ groups katika makundi. 12 (indicating the method of expression, the medium, means, material etc) speaking ~ Kiswahili akisema kwa Kiswahili ~ two colours kwa rangi mbili ~ few words kwa maneno machache. 13 (indicating degree or extent) kwa ~ large quantities kwa kiasi kikubwa ~ great numbers kwa idadi kubwa. all
inane
kwa jumla. 14 (indicating identity) you will always have a good friend ~ me nitakuwa rafiki yako siku zote. 15 (indicating relation, reference, respect) ~ every way kwa kila njia young ~ year mdogo kwa miaka weak ~ the head sio na akili, punguani. 16 (indicating occupation, activity etc) he is ~ the army ni askari. 17 ~ camera (leg) faragha; (colloq) kwa siri. ~ that kwa sababu, kwa kuwa. ~ as/so far as kwa kiasi kwamba, kwa vile. ~ itself hasa, katika uhalisi wake. ~ as such/much as adv kwa sababu/ kwa kuwa. 18 ~ for it! patwa, patikana you are ~ for it! umepatikana. be ~ for something fungwa. ~lieu of badala ya. ~ itself yenyewe.
in3 n (only in) the ~s and (the) outs
chama cha kisiasa kilichoshika hatamu na kile kilichoondoka; sehemu tofauti; undani wa jambo.
inability n kutoweza.
inaccessible adj -siofikika, -sioendeka (of book) -sioeleweka. inaccessibility n.
inactive adj 1 -a kimya, -liotulia, zima. 2 (dull) -vivu, -legevu, -zito. inactivate vt fanya kuwa tuli. inactivity n. inaction n kimya; kuzubaa.
inaccurate adj si sahihi. inaccuracy n. inadequate adj ~ for something/to do something -siotosha; -siofaa; -pungufu. ~ly adv. inadequacy n.
inadmissible adj -sioruhusiwa, -sio halali, -siokubalika, -a kutokubalika. inadmissibility n.
inadvertent adj (formal) -sio -angalifu, -a kupitiwa, -a kughafilika. ~ly adv. inadvertence n kutokuwa mwangalifu, kupitiwa.
inalienable adj (formal) (of rights etc)
-sioondolewa; -sioachanika; -sioachanishika.
inalterable adj -siogeuzika;
-siobadilika. inalterability n.
inane adj -sio na maana, -puuzi,
inanimate
-pumbavu. ~ly adv. inanity n.
inanimate adj 1 -fu, -siokuwa na uhai. 2 (spiritless, dull) baridi, -liopooza, chapwa ~ conversation mazungumzo (maneno) yaliyopooza.
inanition n (formal) 1 utupu. 2 udhaifu/kuwa hoi kutokana na njaa.
inapplicable adj ~ (to) -siofaa, -siopasa.
inappreciable adj 1 -dogo sana. 2
-siothaminika, -siotambulika.
inapproachable adj -siosogelewa, -siofikika; (of person) -sioambilika.
inappropriate adj ~ to -siofaa. ~ness n.
inapt adj 1 -siohusiana (na somo/jambo linalojadiliwa). 2 (unskilled) -si stadi, mbumbumbu. ~itude n kutohusiana na; kukosa ustadi.
inarticulate adj (of speech) 1
-siotamkwa vizuri; -sioweza kusema dhahiri, -sioweza kujieleza kwa ufasaha. 2 -siounganika.
inattention n kutokuwa makini; uzembe; kutokuwa na usikivu. inattentive adj.
inaudible adj -siosikika. inaudibility n. inaugural adj -a kuzindua, -a kuanzisha, -a kufungua ~ ceremony sherehe ya kuzindua. inaugurate vt 1 zindua, fungua, ingia rasmi. 2 (begin) anzisha, simika/tawaza. 3 tambulisha (afisa mpya, profesa n.k.) katika sherehe maalum/rasmi. inauguration n.
inauspicious adj -a ndege mbaya, -a kisirani, -a nuksi. ~ly adv.
inauthentic adj isio kweli wala halisi; isioaminika wala kutegemewa. ~ity n.
inboard adj (naut) -wa ndani ya kiunzi.
inborn adj -a kuzaliwa nao; -a asili; -a silika, -a maumbile.
inbound adj (of ship) -a kuelekea nyumbani.
inbred adj 1 -a kuzaliwa nao; -a asili.
2 -liozaliwa na wazazi wa nasaba moja. inbreeding n uzao baina ya wazazi wa nasaba moja.
incentive
inbuilt adj (of feelings qualities etc) -a kuzaliwa nayo; -a kuundwa nayo.
incalculable adj 1 -siopimika (kwa kuwa -kubwa au -ingi). 2 -siotabirika. 3 (of a person, character etc) geugeu; -sioaminika.
incandescent adj -a kutoa nuru ikiwa na joto. incandescence n.
incantation n nuio, tabano.
incapable adj ~ (of) -sioweza. drunk and ~ adj -levi kabisa. incapability n.
incapacitate vt ~ somebody (for/from) 1 ondolea nguvu/ uwezo/haki n.k.; -towezesha. 2 toa (kwa kutofikia kiwango), -topasisha. incapacity n. ~ (for something/for doing something/to do something) kutoweza; ukosefu wa uwezo.
incarcerate vt (formal) funga jela. incarceration n.
incarnadine (poet) adj -ekundu. vt fanya kuwa nyekundu.
incarnate adj 1 -enye mwili (kiwiliwili), (of somebody's character) -enye umbo (hasa la binadamu) a devil ~ shetani mwenye umbo la binadamu. 2 (of an idea, ideal etc) -a kujitokeza kama binadamu. vt 1 -pa umbo la mtu; -pa mwili. 2 tekeleza wazo. 3 (of a person) -wa mfano wa binadamu (kisifa). incarnation n 1 kuwa na mwili; kuwa na umbo (hasa la binadamu). the incarnation n kupata mwili (kwa Yesu Kristo). 2 kuwa mfano halisi ( wa tabia n.k.).
incautious adj -sio hadhari, si -angalifu; -a harara. ~ly adv.
incendiary n 1 (person) mchomaji mali (kwa moto) kwa nia mbaya. 2 mchochezi adj 1 -a kuchoma, -a kuteketeza; chochezi. 2 (bomb) -a kusababisha moto. incendiarism n.
incense1 n ubani; udi; (smoke) buhuri burn ~ fukiza.
incense2 vt kasirisha, ghadhibisha.
incentive n ~ (to something/to do something/to doing something) kichocheo, kifuta jasho,
inception
marupurupu; motisha give ~ toa motisha.
inception n (formal) mwanzo; chanzo.
incertitude n (formal) wasiwasi, shaka. incessant adj -a kufululiza; -naorudiwa, -siokwisha. ~ly adv.
incest n kujamiiana kwa maharimu.
~uous adj -a kujamiiana kwa maharimu, -enye kosa la kujamiiana baina ya maharimu.
inch n 1 inchi. 2 kiasi kidogo, chembe. ~ by ~ kidogo kidogo. by ~es kidogo tu the bus missed me by ~es basi lilinikosakosa kidogo tu; kidogokidogo. every ~ kabisa, hasa she is every ~ a doctor ni daktari hasa. within an ~ of karibu sana. not yield an ~ kutokubali hata chembe. vt,vi sogea kidogokidogo.
inchoate adj (formal) -a kuanza; -lioanza tu; -siokamilika, -siokuzwa inchoative adj -a kuonyesha mwanzo wa tendo/hali. (gram) ~ verbs n vitenzi vianzishi (vya tendo/hali) k.m. get katika get dark na fall katika fall ill.
incidence n 1 jinsi jambo linavyoathiri mambo the ~ of disease jinsi ugonjwa ulivyoathiri (kwa kuenea, hatari zake n.k.). 2 (phys) tokeo angle of ~ pembe ya kuingilia.
incident1 adj ~ to (formal) -a kawaida/kutegemewa katika (jambo fulani) the social obligations ~ to life in diplomatic services shughuli za kijamii ambazo ni za kawaida katika kazi za kibalozi.
incident2 n 1 kadhia, tukio. border ~ n tukio (la mapigano madogo) mpakani. 2 (in a play/poem) tukio katika mchezo/shairi. 3 (modern use) tukio linalozibwazibwa na utawala (ili lisijulikane). 4 tukio linalovutia wengi. ~al adj. ~al (to) 1 inayo-ambatana na (lakini si -a lazima). 2 -dogo -dogo; -a dharura; -a ziada. 3 -nayoweza kutokea; -a kawaida (katika mazingira fulani) discomforts ~ to pregnancy matatizo ya kawaida wakati wa ujauzito. ~ally adv.
incognito
incinerate vt choma (mpaka kuwa majivu), teketeza. incinerator n tanuri la kuchomea taka. incineration n uchomaji (mpaka kuwa majivu); uteketezaji.
incipient adj -a kwanza, -inayoanza.
incise vt kata, chanja, toja. incision n mkato, chanjo; (small) mtai; (ornamental) chale, tojo. incisive adj 1 -kali, -enye kukata. 2 (of a person's mind) -enye akili, -erevu; -a kuenga. 3 (of remarks) -kali. incisively adv. incisor n (of human beings) kato, chonge; meno ya mbele.
incite vt ~ somebody (to something/ to do something) chochea; shawishi, vuta. ~ment n.
incivility n (formal) ufidhuli, utovu wa adabu, ujuvi.
inclement adj (formal) (of weather or climate) kali; baridi; -a dhoruba inclemency n.
inclination n 1 mwinamo an ~ of the
head kuinamisha kichwa an ~ of the body kuinama (kwa kuonyesha heshima) ~ of a roof mwinamo wa kipaa. 2 ~ (to something/to do something) mwelekeo; matakwa, kupenda. 3 (math) mbetuko. incline vt,vi 1 inama; inamisha; inika. 2 (liter) (usu passive) elekeza. 3 (math) betuka. 4 incline to/towards something elekea. n mwinamo; mteremko.
inclose;inclosure n see enclose; enclosure.
include vt -wa pamoja na; tia/weka
ndani; -wa na ndani Price is sh. 500/= postage ~d bei ni sh. 500/= pamoja na gharama za posta. inclusion n. inclusive adj. inclusive (of) 1 pamoja na. 2 -ote pamoja inclusive terms (at a hotel etc) gharama ya huduma zote, bei yote (bila kuwa na gharama nyingine k.m. za chakula n.k.). inclusively adv.
incognito adj -liojificha; -siotambulika (kwa kutumia jina la bandia) adv
incognizant
bila kutambulika.
incognizant adj -a -sio na dhamira/
hisia, -a kutotambua be ~ of something kutokuwa na habari. incognizance n.
incoherent adj -sioeleweka, (of speech) -sioshikamana, -siofungamana, -sio na taratibu. ~ly adv. incoherence n.
incombustible adj (formal) -siochomeka; -siowaka, -sioungua.
income n mapato, chumo, pato, kipato live within one's ~ ishi kwa kutumia pato lake. national ~ n pato la taifa. ~ tax n kodi ya mapato.
incoming adj -nayoingia, -liofika. ~ tide n maji kujaa.
incommensurate adj ~ (to/with) 1 -siolinganishika, -siofananishika. 2 -siolingana (kwa ukubwa, hadhi n.k.) -siopimika, -siofanana.
incommode vt (formal) sumbua, udhi,
bughudhi.
incommunicable adj 1 -sioelezeka. 2 (of a person) baridi. incommunicado adj (of somebody in confinement) -liotengwa; -siowasiliana, -liokatiwa mawasiliano (na watu wengine). incommunicative adj -siowasiliana, -siosema.
incommutable adj -siobadilishika, -a hali moja.
incomparable adj 1 ~ (to/ with) -siolinganishika, -sioweza kufananishwa, -siofanana (na kitu). 2 -a kupita -ote; bora sana. incomparably adv.
incompatible adj ~ (with) kinyume; -siopatana, -siochukuana (na); -sioingiliana na excessive smoking is ~ with good health kuvuta sigara kupita kiasi ni kinyume cha afya bora. incompatibility n.
incompetent adj -siojimudu, -sioweza. ~ly adv. incompetence/ incompetency n.
incomplete adj -siokamili, pungufu. ~ly adv.
incomprehensible adj -sioeleweka. incomprehesion n kutoelewa, kushindwa kuelewa.
inconvenience
incompressible adj -sioweza
kushindiliwa; -siobanika; gumu sana.
inconceivable adj -siowazika;
-siofahamika; (colloq) -sioaminika; -a kushangaza.
inconclusive adj (of evidence, arguments, discussions, actions) -enye shaka; -siohitimishwa; -sioamuzi; -siosadikisha. ~ly adv.
incondite adj (of literary compostion
etc) -siosanifiwa; -sio -a kistadi.
incongruous adj ~ (with) -siopatana; -siofaa mahali. ~ly adv. incongruity n hitilafu, tofauti.
inconsequent adj -siofuatana; -siofungamana (na yaliyosemwa au kutendwa hapo awali) (of a person) -nayesema/-nayefanya mambo bila mpango. ~ly adv. ~ial adj.
inconsiderable adj -dogo, -sio na thamani.
incosiderate adj -siojali hisia za wengine, -siofikiria wengine.
inconsistent adj ~(with) 1 -siopatana, -siowiana, -siofuata utaratibu. 2 kinzani. ~ly adv. inconsistency n.
inconsolable adj -siofarijika, -siotulizika.
inconsonant adj -siopatana.
inconspicuous adj -sioonekana kwa
urahisi; -siojitokeza; -dogo sana. ~ly adv.
inconstant adj -enye kubadilika, -sio
(na) msimamo, geugeu. inconstancy n.
inconsumable adj 1 -sioungua. 2 (in
Pol Econ) -siofaa kutumiwa (bila kutengenezwa kwanza).
incontestable adj -siopingika; -siokanika; -siokanushika.
incontinent adj -sioweza kujizuia;
(med) -sioweza kujizuia kukojoa na kunya. incontinence n. ~ly adv (lit.) mara moja; huria; holela.
incontrovertible adj (formal)
-siokanika; -siopingika.
inconvenience n usumbufu, taabu, takilifu; maudhi. vt sumbua, taabisha, udhi. inconvenient adj -sumbufu; -siofaa. inconveniently
inconvertible
adv.
inconvertible adj -siobadilishika,
-siosarifika. inconvertibility n.
incorporate vt, vi ~ (in/into/with)
unga, unganisha, shirikisha, ungana na, -wa shirika. incorporate adj -liounganishwa; -lioshirikishwa. incorporation n.
incorporeal adj (formal) -sio na mwili (umbo la wazi).
incorrect adj -kosefu, -sio sahihi.
~ness n. ~ly adv.
incorrigible adj (of a person, his faults, etc) -siorudika; -siorekebishika.
incorruptible adj 1 -sioharibika,
-siochakaa, -siooza. 2 (honest) -sioshawishika, -siohongeka. incorruptibility n.
increase n nyongeza, ongezo,
ongezeko ~ in kuongezeka; kukua, kupanuka be on the ~ anza kukithiri, ongezeka. vt, vi ongeza, zidisha; kithiri. increasingly adv.
incredible adj -siosadikika; (colloq) -a kushangaza; -sioaminika, -a ajabu sana. incredibility n incredibly adv. incredulous adj -siosadiki, -sioamini be ~ tosadiki ~ smile tabasamu la mshangao. incredulity n.
increment n 1 nyongeza. 2 faida, mapato. ~al adj.
incriminate vt tia hatarini; ponza. incrimination n. incriminatory adj.
incrust vt,vi see encrust.
incrustation n utando, mtomo, gamba; kufanya gamba.
incubate vt,vi 1 atamia (mayai); atamiza mayai (kwa kutumia taa kubwa). 2 (of bacteria etc.) pevuka; pevusha, kuza. incubation n kuatamiza, kukuza incubation period muda wa kupevuka (agh. wa vijidudu vinavyoleta ugonjwa). incubator n kitamizi, kiangulio, kitotoa. incubative adj. incubatory adj.
incubus n (nightmare) jinamizi; ndoto mbaya; balaa.
inculcate vt ~ something (in somebody) (formal) funda, fundisha,
indecision
kazia mawazo inculcate in young people the `ujamaa' ideology, fundisha/kazia vijana itikadi ya ujamaa. inculcation n.
inculpate vt (formal) tia hatiani; shutumu; laumu inculpative adj. inculpatory adj.
incumbent adj be ~ on/upon somebody (to do something) hapana budi, -wa wajibu, -a kubidi it is ~ upon me imenipasa, imenibidi, ni wajibu wangu, ni juu yangu. n 1 padri wa mji, kasisi. 2 mtu ashikiliaye cheo fulani ~ Member of Parliament mbunge aliyepo. incumbency n.
incur vt ingia/pata ~ a debt ingia/pata
deni ~ expenses gharamia, lipia ~ the expenses lipia gharama.
incurable adj -sioponyeka, -siotibika. n mtu asiyeponyeka. incurably adv.
incurious adj -siodadisi, -a kutodadisi. incuriosity n.
incursion n ~ on/upon vamio la ghafla (la askari wa adui); (fig) kuingilia, mwingilio.
incurved adj -liobonyea, -liobinukia
ndani. incurvation n.
incus n fuawe (ya sikio).
indebted adj ~ to somebody -enye kuwiwa, -enye deni; -a kupaswa kushukuru be ~ wiwa, -wa na deni; paswa kushukuru; fadhiliwa he is ~ to me anawiwa nami. ~ness n.
indecent adj 1 (of behaviour, talk etc) (immodest, obscene) -sio na heshima, -a aibu. ~ assault n shambulio la kuaibisha mtu hadharani. ~ exposure kuonyesha uchi hadharani. ~ behaviour n tabia mbaya. 2 (colloq) -sio sahihi, -siofaa. indecency n. ~ly adv.
indecipherable adj -siosomeka;
-siotambulikana, -sioweza kueleweka; siosimbulika.
indecision n kusita moyoni, kutoamua, kutoweza kuchagua/kukata shauri. indecisive adj -a shaka, -sio dhahiri; -a kusita; -sio amuzi. indecisiveness n. indecisively adv.
indeclinable
indeclinable adj (gram)
-sionyambulika.
indecorous adj (formal) -sio adilifu,
-sio na heshima/staha; -siofaa. ~ly adv. indecorum n utovu wa adabu/ heshima/staha; ufidhuli; jambo lisilofaa.
indeed adv 1 kweli, hasa, ndiyo, naam. 2 (to intensify) sana I am very glad ~ nimefurahi sana thank you very much ~ asante sana; hasha. 3 (as a comment to show interest, suprise, irony etc) kweli, hasa who is she ~! kweli/hasa yeye ni nani!
indefatigable adj (formal) -siochoka, -siochoshwa.
indefeasible adj (formal) -siotanguka.
indefectible adj -sioshindwa; -siokosa;
-sioharibika.
indefensible adj -siolindika ~ behaviour -sioweza kutetewa.
indefinable adj -sioelezeka; siofasilika.
indefinite adj -sio dhahiri; -sio na
mwisho, -sio na mipaka the ~ article see a, an. ~ly adv.
indelible adj (of marks, stains, ink or (fig) of disgrace) -siofutika; -sioondoleka ~ ideas fikra zisizofutika ~ pencil marks alama za penseli zisizofutika.
indelicate adj (of a person, his speech, behaviour etc) si -a adabu, -siofaa, -chafu, pujufu. indelicacy n.
indemnify vt 1 ~ somebody (for something) lipa, fidia, (agh. gharama aliyoipata mtu mwingine). 2 ~ somebody (from/against something) linda, kinga. indemnification n. indemnity n fidia bima.
indemonstrable adj -sioonyesheka, -siodhihirika.
indent vt,vi 1 tia pengo, bonyeza.
2 (in printing) jongeza msitari ndani you must ~ the first line of each paraghaph lazima kujongeza ndani msitari wa kwanza wa kila aya. 3 ~ (on somebody) for something (comm) agiza bidhaa kwa njia ya agizo maalum. n (comm UK) hati ya kuuza bidhaa nje; hati maalum ya
India
kuagizia vitu. ~ation n 1 kuagiza; kuagizwa. 2 pengo; kighuba; kujongeza.
indenture n mkataba, (agh. wa watumishi au mwanagenzi) take up one's ~s pata/pokea/rudishwa nakala ya mkataba (baada ya kipindi kwisha); maliza mkataba (wa utumishi). vt fanya mkataba (wa utumishi).
independent adj 1 ~ (of) huru ~ means pato lisilotegemea kazi. 2 -enye kujitawala, -lio huru, -enye kujitegemea. n ~ MP n mbunge anayejitegemea. ~ly adv. independence n uhuru; upweke, upekee; kujitegemea. independency n.
indepth adj -a kina an~ analysis uchanganuzi wa kina.
indescribable adj -sioelezeka, -a kushangaza. indescribably adv.
indestructible adj -sioweza kuharibika. indestructibility n.
indeterminate adj -sio wazi, -sio -a dhahiri; si yakini. indeterminable adj. indeterminably adv. indeterminacy n. indetermination n.
index n 1 kielezo, alama, ishara. ~
finger n kidole cha shahada. 2 faharasa the ~ card kadi ya faharasa. 3 ~number/figure n nambari faharasa. 4 (alg) nambapeo. vt faharisisha, orodhesha. ~er n.
India n Uhindi ~ paper karatasi
nyembamba sana. ~man n (formerly) meli (iliyosafiri baina ya Uhindi na Ulaya). ~-rubber n kifutio. Indian n 1 Mhindi. 2 American ~n/West ~n Mhindi mwekundu adj 1 -a Kihindi. ~ n Ocean n Bahari ya Hindi. ~n club n rungu la mazoezi. ~n corn n mahindi. in ~ n file -moja baada ya ingine. ~n ink n wino mweusi agh hutengenezwa Uchina na Ujapani. ~n red adj -ekundu, udongo mwekundu. ~n summer n mwisho wa majira ya joto; (US) (fig)
indicate
kurudiwa na mawazo ya ujana uzeeni.
indicate vt (fig) onyesha; elekeza; dokeza; ashiria. indication n alama, dalili, ishara. indicative adj 1 -a kuarifu indicative mood hali ya kuarifu. 2 ~indicative of/that -wa dalili, alama ya. indicator n indiketa; kiashirio; dalili, alama.
indices n pl of index.
indict vt (leg) shitaki rasmi. ~able adj. ~ment n shtaka rasmi lililoandikwa.
indifferent adj ~ (to) 1 -siojali he is ~ to everything hajali chochote. 2 -a kawaida; (of medium, quality) -a vivi hivi, -a kadiri. ~ly adv. indifference n kutojali, kutojiingiza, kutojihusisha it is a matter of indifference to me sijali.
indigenous adj ~ (to) -a asili, -enyeji. ~ tribe n mbari/kabila la asili.
indigent adj (formal) fukara. indigence
n.
indigestion n kuvimbiwa. indigested adj 1 -sio na umbo. 2 -siofikiriwa vyema; -siomeng'enywa; -sio na mpango. indigestible adj -siomeng'enyeka.
indignant adj -a kuudhika, -enye
uchungu (hasira, hamaki, hasa kwa sababu ya kudhulumiwa) feel ~ at something udhika kwa jambo fulani he was ~ to learn about the news alikasirishwa na habari. ~ly adv. indignation n uchungu,hasira (isababishwayo na dhuluma/tabia mbaya); msononeko.
indignity n ufidhuli, kitu kinachomvunjia mtu heshima.
indigo n nili. ~ (blue) n bluu iliyoiva. indirect adj 1 -sionyooka, -a kuzunguka, sio dhahiri ~ rule utawala wa kuwatumia viongozi wananchi usio wa moja kwa moja ~ taxation kodi isiyo dhahiri. 2 -siokusudiwa, -siolengwa an ~ outcome matokeo yasiyokusudiwa. 3 (gram) ~ speech n kauli taarifa iliyotajwa. ~ object n yambiwa.
individual
~ly adv. ~ness n.
indiscernible adj -siofahamika; -sio tambulika, -siobainika.
indiscipline n utovu wa adabu; ukosefu wa nidhamu.
indiscreet adj 1 si -a busara/akili.
2 -sio na hadhari; -sio na adabu. indiscretion n kuvunja miiko ya jamii; kusema/kutenda bila hadhari.
indiscrete adj -siogawanyika katika sehemu.
indiscriminate adj -sio chagua kwa busara/mpango. ~ly adv. indiscrimination n.
indispensable adj ~ to -a lazima/ sharti/msingi. indispensability n.
indisposed adj 1 -gonjwa kidogo he is ~ yu mgonjwa kidogo. 2 ~ for/to do something -a kutopenda/ kutotaka/kutoridhika he is ~ to go hapendi/hataki kwenda. indisposition n 1 ugonjwa, kutojisikia vizuri. 2 ~ for/to do something kutopenda, karaha.
indisputable adj -siokanika,
siopingika, dhahiri. indisputability n.
indissoluble adj 1 -siotanguka, -siovunjika, -a daima. 2 -sioyeyuka.
indistinct adj si wazi/dhahiri shahiri/ bainifu,-siotambulikana vizuri. ~ly adv. ~ness n. indistinguishable adj -sio tafautishika; -siotambulikana; -siobainika; -sioonekana dhahiri.
indivertible adj -siogeuzika; -sioweza kupelekwa upande mwingine.
individual adj 1 -a binafsi. 2 -a mmoja mmoja ~ help msaada wa mtu mmoja mmoja ~ problems matatizo ya binafsi. n 1 mtu binafsi. 2 (colloq) mtu, binadamu. ~ly adv. ~ism n 1 ubinafsi. 2 nadharia ya ubinafsi. ~ist n mbinafsi; mfuasi wa nadharia ya ubinafsi. ~istic adj -enye ubinafsi, -a kujipendelea; -a nadharia ya ubinafsi. ~ity n 1 nafsi, (tabia, sifa za mtu binafsi). 2 hali ya pekee. 3 (usu pl) ~ities n mapendeleo, matakwa ya mtu binafsi. ~ize vt 1 bainisha,
indivisible
pambanua. 2 shughulikia kipekee/kimoja kimoja. ~ization n.
indivisible adj -siogawanyika, -sio
changulika. indivisibility n.
Indo- pref (in compounds) -a Kihindi I~ European language familia ya lugha zizungumzwazo sehemu za Ulaya na Magharibi ya Asia.
indoctrinate vt ~ somebody with funza, fundisha, funda (hasa dhana au fikra maalum), tia kasumba. indoctrination n.
indolent adj 1 -a ukunguni, -vivu, -tepetevu. 2 (med) -sioleta maumivu. indolence n.
indomitable adj -sioshindika; thabiti; -siokata tamaa.
indoor adj (attrib only) -a ndani (hasa ndani ya nyumba), -a kufanywa ndani ya nyumba. ~s adv ndani ya nyumba, ndani keep ~s kaa nyumbani.
indorse vt see endorse. ~ment n. indrawn adj 1 -liovutwa (ndani). 2 -sio changamfu, baridi, -liojivuta.
indubitable adj pasipo shaka; bayana, wazi; hakika.
induce vt 1 ~ somebody to do something vuta, shawishi, pembeja. 2 (cause) anzisha, sababisha ~ labour (in child birth) anzisha uchungu. 3 (of electricity) dukiza; toa umeme. ~ment n mvuto, kishawishi, kivutio, motisha.
induct vt ~ somebody (to/into as) ingiza; simika; (US) ita jeshini. ~ion n 1 kuingiza, kusimika. 2 kudukiza umeme; kupitisha umeme. 3 matumizi ya visa kufikia kanuni/wazo la jumla. 4 (maths) hoja tama. 5 (US) kuitwa jeshini. ~ coil n pindi la kuingiza umeme. ~ -pipe n bomba la kuingiza umeme. ~ -valve n vali ya kuingiza umeme. ~or n kidukiza/kiingiza umeme. ~tive adj 1 -a kufuata mantiki kupata wazo la jumla. 2 -a kudukiza/ kuingiza umeme au sumaku.
indue vt see endue.
indulge vt, vi 1 endekeza;deka ~
inebriate
somebody in his whims etc. endekeza matakwa ya mtu. ~ oneself jipendeza, jiachia, jifurahisha. 2 ~ in jiingiza ~ oneself in excessive drinking jiingiza katika ulevi wa kukithiri ~ oneself in prayer jitoa kwa sala, shikilia sala ~ in sin jiingiza katika dhambi. ~nt adj -pole, -ema mno, taratibu ~nt parents wazazi dekezi/wema mno. ~ntly adv. ~nce n 1 kudekeza, kuendekeza. 2 (of desires) ~ in kujiachia, kujitoa kwa kujiingiza katika uzoefu wa kujifurahisha. 3 (rel) rehema, kipenda roho, upendeleo. 4 kitu mtu anachopendelea; starehe to have a cup of coffee every evening is my ~nce kahawa ndio kitu ninachopendelea kila jioni.
induna n jumbe.
indurate vt,vi fanya sugu/-gumu; gandamiza; shupaza. induration n. indurative adj.
industry n 1 bidii ya kazi, uchapaji kazi. 2 viwanda, tasnia. industrial adj -a kiwanda. industrial action n mgomo take industrial action goma. industrial alcohol alkoholi ya viwanda industrial dispute mgogoro wa kiwanda/kazi industrial estate eneo la viwanda industrial workers wafanyakazi wa viwandani industrial states nchi za viwanda industrial relations uhusiano wa wafanyakazi kiwandani. industrial revolution n mapinduzi ya viwanda. industrialism n utasinia, mfumo wa uchumi unaotegemea viwanda. indutrialist n 1 mwenye kiwanda, mtasinia. 2 shabiki wa viwanda. industrialize vt jenga kiwanda, anzisha/endeleza mfumo wa viwanda. industrialization n ujenzi wa viwanda. industrious adj -enye bidii ya kazi, -chapakazi.
indwelling adj (formal) -enye kukaa
ndani; -enye kukaa moyoni.
inebriate vt (formal or joc)levya. n
mlevi adj -levi. inebriation;
inedible
inebriety n ulevi.
inedible adj -siolika .
ineffable adj (formal) -siyoelezeka.
~ happiness n furaha isiyoelezeka, furaha isiyokifani.
ineffaceable adj -siofutika.
ineffective adj -sio na nguvu uwezo/ ufanisi; hafifu, dhaifu, -siofaa. ~ness n.
ineffectual adj -sioweza kufanikisha jambo; -siojiamini.
inefficient adj -zembe, -sio na ufanisi -siofanya kazi vizuri. ~ly adv. inefficiency n uzembe.
inelastic adj yabisi/kavu; -sionyumbuka, -siovutika; -sioweza kubadilika/kufaa hali fulani. ~ity n. inelegant adj si -zuri, -sio na madaha, -siopendeza. ~ly adv. inelegance n.
ineligible adj ~ (for) -siostahiki,
-siofaa, -siojuzu (kuchaguliwa/ kuteuliwa n.k.). ineligibility n.
ineluctable adj -siozuilika; -sioepukika, -siokwepeka death is ~ kifo hakiepukiki.
inept adj 1 -siostadi, -sioelekevu. 2
-pumbavu, -siofaa, -a upuuzi. ~ly adv. ~itude n upumbavu, upuuzi.
inequality n 1 kutokuwa sawa; tofauti, (ya cheo, utajiri n.k.). 2 (pl) (of surface) kutokuwa tambarare.
inequity n upendeleo; dhuluma. inequitable adj (formal) -sio haki.
ineradicable adj -sioondoleka; -siong'oleka; -siofutika.
inert adj 1 -fu, kama kifu, kama kufa. 2 -tepetevu, baridi. ~ia n 1 ukunguni, uzito. 2 (phy) inesha.
inescapable adj -sioweza kuepukwa, -sioepukika.
inessential adj -sio -a lazima, siyo
muhimu, -sio -a msingi.
inestimable adj -siokadirika (kwa ukubwa, thamani, wingi, n.k.).
inevitable adj -sioepukika; -siozuilika
~ accident ajali isiyoepukika accidents are ~ ajali hazina kinga fig) -a kuonekana/kusikika kila mara; -a kutarajia (kuwepo/kutokea).
infant
inevitability n.
inexact adj -sio sahihi, -enye kosa,
-enye hitilafu; si halisi. ~itude n terminological ~itudes (joc euphem) uongo.
inexcusable adj -siosameheka. inexhaustible adj 1 -sioisha,
-siomalizika (kwa kuwa ingi), -ingi mno. 2 (unwearied) -siochoka. inexhaustibility n.
inexorable adj -sio na huruma, -siosamehe; -kali; -siobadilika wala kuzuilika. inexorably adv.
inexpedient adj -siofaa, siyo faida. inexpedience n. inexpediency n.
inexpensive adj -sio ghali, rahisi, -a bei nafuu. ~ness n.
inexperience n ukosefu wa uzoefu/ujuzi. ~d adj -sio na uzoefu/ujuzi/tajriba.
inexpert adj si -stadi, si -bingwa.
inexpiable adj (of offence) -siolipika; -siosameheka; (of resentment etc)
-siotulizika, -siofutika.
inexplicable adj -sioelezeka; -siofumbulika.