TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

J,j n herufi ya kumi katika alfabeti ya Kiingereza.

jab vt,vi 1 ~ at dukua, piga mduke.2~ something into something/somebody piga kwa nguvu. 3 ~ something out chokoa n mdukuo, kipigo cha nguvu, dharuba (colloq) sindano.

jabber vt,vi payuka, bwabwaja, bwata. n kupayuka. ~er n mpayukaji.

jacana n sile, maua.

jacaranda n mjakaranda.

jack n 1 J~ (familiar form of) John. J~ Frost n jalidi. J~ in Office n kiongozi mdogo mwenye makuu/ kujikuza, mrasimu; kimangimeza. a~ of all trades mjuaji wa kila kitu, mwenye kujaribujaribu kila kazi. before one can say J~ Robinson kufumba na kufumbua. J~ is as good as his master mtumishi na mwajiri wake wote sawasawa. 2 (colloq) mtu. every man ~ kila mtu. 3 (usu portable) jeki. 4 (in the game of bowls) mpira. 5 bendera ya meli (kuonyesha utaifa). the Union J~ Bendera ya Uingereza. ~ staff n mlingoti wa bendera kwenye meli. 6 (in a pack of playing-cards) mzungu wa tatu, ghulamu. 7 (compounds) ~-in-the-box n mwanasesere katika kasha. ~-o- lantern kitu kisichoshikika (mf. moshi, gesi); (fig) fikra za kinyozi; boga lililokatwa mfano wa uso wakati wa sherehe ya Halloween. ~rabbit n sungura mkubwa. ~tar n (old name for) baharia. vt ~ something in (sl) telekeza. ~ something up inua kwa jeki.

jackal n mbweha.

jackanapes n 1 mtu mwenye majivuno; mtukutu. 2 mtoto mtundu/mtukutu.

jackass n punda dume; mpumbavu. laughing ~ n (in Australia) mkumburu.

jack-boot n buti buti linalofika magotini (k.m. buti ya mpanda

jamb

farasi).

jackdaw n ndege mweusi jamii ya

kunguru.

jacket n 1 jaketi. dust a person's ~ piga mtu. 2 (cover) kifuniko, kidhibiti joto. 3 maganda ya viazi. 4 ganda (la kitabu). vt funika.

jack-fruit n fenesi.

jack-knife n kisu kikubwa cha kukunja. vi (esp of an articulated truck) kunjika.

jack-plane n randa ya kati.

jackpot n jumla ya fedha za kushindaniwa katika mchezo wa karata. hit the ~ kuwa na bahati, pata ushindi mkubwa.

jacobin1 n mwanamapinduzi wa

wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa (1789) adj -a kishindo. ~ism n.

Jacobin2 n njiwa mwenye kishungi.

jade1 n jiwe la thamani lenye rangi ya kijani kibichi.

jade2 n 1 farasi aliyechoka na kuzeeka. 2 (either contemptuous or playful) mwanamke. ~d adj hoi.

jag n ncha chonge; jino (la msumeno). ~gy; ~ged adj. vt keketa, kata (pasua) na kufanya mapengo; chana ovyoovyo.

jaguar n chui (wa Amerika ya Kusini na Kati).

jail n see gaol.

jakes n (sl) choo.

jalopy n (colloq) mkweche, gari au ndege mbovu.

jalousie n dirisha la luva.

jam1 n mraba, jemu. money for ~ (sl) kitu kipatikanacho bure/kwa bahati. ~- jar; ~-pot n kopo la jemu. ~ session n kupiga mziki papo kwa papo; faraguzi la muziki.

jam2 vt,vi 1 ~ (in/under/between etc) bana; banwa; shindilia. 2 ~ (on) kwama; kwamisha; funga kwa nguvu ~ on the brakes funga breki kwa nguvu. 3 songamana; rundika. 4 zuia, ingilia mawasiliano ya redio n 1 msongamano. 2 kukwama; mkwamo. 3 (sl) hali ngumu/ matata/ mashaka.

jamb n 1 mwimo, mhimili. 2 (pl) kuta za meko; mafiga.

jamboree

jamboree n 1 jamborii: hafla ya furaha. 2 mkusanyiko mkubwa (wa watu) hasa wa maskauti.

jampack vt (colloq) furika; jaa pomoni.

jangle vt,vi lia ovyo; kwaruza (kama kengele zisizopigwa vizuri); (quarrel) gombana, zozana. n ukelele; mikwaruzo.

janitor n 1 bawabu. 2 (US) mhudumu wa ofisi.

January n Januari, mwezi wa kwanza.

japan n vanishi ngumu nyeusi. vt paka vanishi.

jape n (old use) mzaha, utani.

jar1 n 1 (usu harsh) mkwaruzo/ mtetemeko (wa sauti). 2 mshtuko.

jar2 n gudulia; chupa kubwa, dumu,

mtungi. ~ful n. vt,vi 1 ~ against/on gonga na kutoa sauti inayokera. 2 ~ on chukiza, kera. 3 shtua; shtuka. 4 ~ (with) achana; gongana; farakana. ~ring adj -a kusababisha mfarakano; kali. ~ringly adv.

jardiniere n chungu/dumu lililopambwa (la kuwekea maua ndani ya nyumba au dirishani).

jargon1 n (aina ya) madini ya zirikoni.

jargon2 n 1 istilahi, lugha ya kitaalamu. 2 lugha isiyoeleweka.

jasmine n yasimini/asmini.

jaundice n homa ya nyongo ya manjano; (fig) wivu, husuda. vt (usu passive) athiri kwa wivu/husuda.

jaunt n mandari; matembezi. vt fanya mandari. ~ing car n gari la farasi la mandari. ~y adj -a madaha, -enye kujiamini/kutosheka. jauntily adv. jauntiness n.

javelin n mkuki (agh. katika michezo) ~ throw kutupa mkuki.

jaw n 1 (lower/upper) ~ taya, utaya. ~-bone n mfupa wa taya. ~-breaker n (colloq) neno gumu kutamka. 2 (pl) kinywa (sing) sehemu ya chini ya uso; taya la chini. 3 mwingilio wa bonde, pango (hasa wa

jemmy;jimmy

mahali pa hatari) (fig) into/out of the ~s of the death ingia/toka kwenye hatari. 4 (pl) (machine) kibanio. 5 (colloq) kidomo, payo; soga kubwa. 6 (colloq) mahubiri/wasifu/hotuba ndefu na ya kuchosha. ~ (at) (colloq) piga domo; hubiri.

jay n ndege kama kunguru mdogo mwenye rangi nyingi na milio mingi; (fig) mlimi, mpayukaji. ~-walker n mtu atembeaye bila kujali usalama barabarani. ~-walk. vi kata barabara bila kujali usalama barabarani.

jazz n jazi (muziki uliobuniwa na

Wamarekani weusi tangu karne ya 20). ~ dancer n mcheza jazi. vt 1 cheza katika mtindo wa jazi. 2 ~ something up (fig, colloq) changamsha. ~y adj (colloq) -a kijazi; maridadi, -zuri; -enye kelele.

jealous adj 1 -wivu. be ~ ona wivu. 2 ~ (of somebody/something) -enye ngoa kijicho. 3 ~ (of somebody/ something), -wa mwangalifu. 4 (in the Bible of God) -enye kutaka upendo wote. ~ly adv. ~y n.

jean n 1 aina ya kitambaa kigumu cha pamba. 2 ~s jinzi.

jeep n jipu: aina ya gari la sulubu/kazi.

jeer vi,vt ~ (at somebody) zomea. ~ingly adv.

jehad n see jihad.

Jehovah n Mungu (katika Agano la Kale).

jejune adj (formal) (of writing) -siovutia, -siosisimua, -sioridhisha; kavu, chapwa; -a kitoto; -a kipuuzi. ~ly adv. ~ness n.

jell vi,vt (colloq) (cause to) ganda,

dhihirika (katika umbo), pangisha, tengemaa. ~(ish) adj kama jeli.

jellaba n juba lenye kofia (linalovaliwa na waarabu wanaume).

jelly n jeli. ~-fish n kiwavi (wa baharini). vt,vi gandisha kuwa jeli. jelled adj -a jeli.

jemmy;jimmy n mtaimbo/mtalimbo, nondo (agh. hutumiwa na wezi

jeopardize

kufungulia milango).

jeopardize vt hatarisha. jeopardy n be/place put in ~ -wa/weka/ingia hatarini.

jeremiad n malalamiko, manung'uniko (marefu).

jerk1 n 1 (of a thing/muscles) mkutuo,mshtuko the tractor started to move with a ~ trekta lilianza kuondoka kwa mshtuko. 2 physical ~ s (colloq) michezo/mazoezi ya viungo. 3 (sl) boza, bwege, mpumbavu vt,vi shtua; shtusha; shtuka; kutua ~ somebody out of something shtua mtu atoke katika hali fulani. ~y adj. ~ily adv. ~iness n.

jerk2 vt ng'onda/hifadhi nyama kwa kuikata vipande virefu na kukausha juani.

jerry n 1 ~ builder/building n mjenzi/ujenzi wa nyumba duni. 2 ~can n jarikeni, kipipa. 3 (army sl) askari wa Kijerumani. 4 (sl) msala; chombo cha kujisaidia (chumbani).

jersey n 1 (~ wool) kitambaa cha sufu; fulana nzito, jezi, sweta. 2 ng'ombe wa kisasa (ambaye asili yake ni Jersey).

jest n kichekesho; masihara, mzaha, utani. in ~ kwa mzaha, kimzaha a standing ~ kichekesho. vi ~ (with) toa mzaha; chekesha; fanya masihara, tania it's not a matter of ~ si utani. ~ing adj. ~ingly adv.~er n mcheshi, damisi.

Jesuit n 1 Mjesuti: mwanachama wa chama kimojawapo cha Kikristo. 2 (derog) mtu mwenye hila/mwerevu sana. ~ical adj.

Jesus Yesu: mwasisi wa dini ya Kikristo.

jet1 n 1 mchirizi wa ghafla (wa maji,

mvuke) kutoka kwenye upenyo. ~ propulsion (engine) n injini ya jeti. ~ (air craft/air liner/fighter) n jeti. the ~ set n matajiri (agh. husafiri sana kwa ndege). 2 upenyo, bomba (la kutokea maji, hewa, n.k.). vt,vi 1 to(k)a kwa nguvu, bubujika, foka (kwa nguvu). 2 (colloq) safirisha kwa

jiggered

jeti.

jet2 n 1 jeti: namna ya jiwe jeusi

sana linalotumika kufanya vifungo na mapambo ya mavazi. ~ black adj -eusi tititi.

jetsam n shehena n.k. iliyotoswa baharini kupunguza uzito wa jahazi (meli, chombo n.k.); shehena iliyotupwa baharini na kukokotwa pwani. flotsam and ~ n (fig use) watu wasio na mbele wala nyuma, watu wasio na kazi wala makazi.

jettison vt tupa shehena baharini (ili kupunguza uzito wa jahazi n.k.) tupa/acha kitu/jambo lisilohitajika ~ redundant workers fukuza/ punguza wafanyakazi wasiohitajika.

jetty n gati, bunta.

Jew n Myahudi. ~ess n Myahudi wa kike. ~ish adj.

jewel n 1 kito (k.m. almasi). 2 almasi bandia. 3 (fig) (beloved) kipenzi; tunu, mtu/kitu cha thamani. vt 1 pamba kwa vito (usu in pp) a ~led ring pete yenye vito a ~led watch saa yenye almasi bandia. ~ler n muuza vito. ~ry; ~lery n mapambo ya vito.

Jezebel n (derog) kahaba, malaya.

jib1 n 1 tanga la mbele la pembe tatu. the cut of man's ~ sura ya mtu. 2 mkono wa winchi.

jib2 vi (of a horse, etc) simama ghafla; kataa kwenda; (fig) kataa kuendelea. ~ at (fig) sita.

jibe vi (US)1 see gibe. 2 see gybe.

jiffy n (colloq) muda mfupi. in a ~

sasa hivi, punde, mara moja I shall come in a ~ nitakuja sasa hivi, punde.

jig n 1 muziki wa dansi la yosayosa. 2 (appliance) kiongozi. vt,vi 1 cheza dansi la yasayosa. 2 rukaruka; rusharusha.

jigger n 1 tekenya, funza. 2 toti: kipimo cha pombe kali kwenye mabaa.

jiggered adj (pred only, colloq) 1 -lioshangazwa (well) I 'm ~! nimeshangazwa. 2 hoi, -liochoka I'm

jiggery-pokery

~ niko hoi.

jiggery-pokery n (colloq) udanganyifu, ulaghai, upuuzi; mapayo.

jiggle vt,vi tingisha, vuta/sogeza kwa kushtua taratibu.

jigsaw n msumeno mdogo wa kutengenezea mapambo. ~ (puzzle) n mchezo-fumbo (wa kupanga vipande ili kupata picha kamili).

jihad n jihadi; vita takatifu; (fig) kampeni kali (inayopinga au kuunga mkono mafundisho ya jambo fulani).

jilt vt vunja uchumba/mapenzi. n mvunja uchumba.

Jim Crow n (Us derog) mtu mweusi.

jiminy int (colloq) lahaula.

jim-jams n (pl (sl) the ~ n woga wa kupita kiasi; wasiwasi, kutetemeka (kwa woga).

jimmy n see jemmy.

jingle n 1 mlio (wa njuga, sarafu,

funguo, kengele n.k.). 2 maneno yenye vina (yenye lengo la kuvutia k.m. katika tangazo la biasahra). vt 1 liza (njuga, sarafu, funguo, kengele n.k). 2 (of verse) tia vina rahisi.

jingo n (pl) mzalendo bubu (anayedharau nchi nyingine); ushari (kwa sababu ya uzalendo huu). By ~ (dated sl) lahaula, kweli (kabisa). ~ism n ugomvi, ushari, tabia ya kutaka vita. ~ist n. ~istic adj zalendo mno; -a shari, -anayetaka vita.

jinks n (only in) high ~ n vigelegele,

hoihoi, shangwe, vifijo.

jinn n see genie.

jinx n (colloq) mtu/kitu chenye mkosi; nuksi. put a ~ on somebody tia mtu mkosi.

jitney n (US colloq) 1 (old use) senti tano. 2 basi dogo.

jitters n (pl) the ~ n (sl) wasiwasi; woga wa kupita kiasi; kutetemeka kwa woga.

jittery adj ~bug n dansi la yosayosa (miaka ya 1940); mtu achezaye dansi hilo. vt cheza dansi la yosayosa.

jive n jaivu: aina ya dansi.

job1 n 1 kazi. on the ~ (colloq) -wa

Job2 n (from the Book of ~ in the old Testament) Ayubu; mvumilivu, mstahamilivu. try the patience of ~ -wa ngumu kuvumilia; kera sana, -wa sumbufu. a ~'s comforter n mtu anayeongeza uchungu kwa mtu aliyetakiwa kumliwaza.

jockey n mpanda farasi katika mashindano vt,vi hadaa, laghai, danganya, ghilibu. ~ for position (in racing) kumbakumba washindani wengine ili kupata nafasi nzuri; (fig) jaribu kwa ufundi au ujanja kupata manufaa fulani.

jocose adj (formal) cheshi; -a mzaha.

jocund

~ly adv. ~ness; jocosity n. jocular adj cheshi, -a mzaha. jocularly adv. jocularity n. mzaha, masihara.

jocund adj (liter) cheshi, changamfu, kunjufu. ~ity n ucheshi, uchangamfu, ukunjufu.

jodhpurs n (pl) jodipa: suruali za kupandia farasi.

jog vt,vi 1 shtua; shtusha; tingisha kidogo, kutua, piga kikumbo. (sl) ~ somebody's memory kumbusha fulani. 2 (go slowly) enda polepole kwa mwendo wa wasiwasi. 3 ~ along/on jikongoja, endelea pole pole kwa uvumilivu. 4 (mod colloq) jogi: kimbia polepole kama zoezi la viungo. ~ger n mkimbiaji wa zoezi la viungo. ~ging n 1 kujogi, zoezi la viungo la kukimbia. 2 kikumbo, mkutuo. 3 (also ~ trot) mwendo wa polepole.

joggle vt,vi tikisa, sogeza/vuta kwa kushtua taratibu. n mtikiso mdogo wa pole pole.

john n (sl) choo.

John Bull n Mwingereza (yeyote); taifa la Waingereza; Mwingereza hasa, tabia ya Kiingereza.

joie de vivre n (F) kufurahia

maisha.

join vt,vi 1 ~ something to something/ ~things together/up unga, unganisha ~ battle anza kupigana. ~ hands shikana mikono; (fig) ungana, shirikiana. ~ forces (with...) fanya kazi na, shirikiana na. 2 jiunga na, ingia ~ the university jiunga na/ingia chuo kikuu ~ the association jiunga na/ingia chama. ~ up (colloq) jiunga na jeshi. 3 ~ (somebody) in something ungana na, changanyika na, fuatana na the next group will ~ us tomorrow kikundi kingine kitaungana nasi kesho. n kiungo, fundo. ~er n seremala (agh. katika ujenzi wa nyumba). ~ery n useremala (agh. wa shughuli za ujenzi wa nyumba). ~t adj -a pamoja ~ account akaunti ya pamoja

Jonah

~ communique taarifa ya pamoja during their ~ lives walipokuwa wanaishi pamoja. ~ly adv kwa pamoja. n 1 maungio 2 kiungo, fundo. out of ~t (of bones) teguka, shtuka. put somebody's nose out of ~ (fig) pindua; fadhaisha; komesha. 3 (of an ox, a sheep etc) pande la nyama (k.m. mguu, paja, mkono). 4 (sl) mahali pa kuchezea kamari, kunywea vileo au madawa ya kulevya. clip ~t n baa ya gharama kubwa. 5 (sl) sigara yenye bangi. vt 1 unganisha kwa kiungo. 2 gawanya kiungoni.

jointure n (leg) urithi wa mke (mali

inayowekwa kwa urithi wa mke baada ya mume kufariki.

joist n boriti (for carrying deck of vessel) darumeti.

joke n kichekesho; dhihaka, mzaha,

masihara. have a ~ with somebody fanyia masihara; taniana na. make a ~ about fanyia mzaha/kichekesho. a practical ~ n utani (wa vitendo). play a practical ~ on somebody tania mtu (kwa vitendo). it's no ~ siyo mchezo; sio utani. the ~ of the village kichekesho. vi fanya mzaha/dhihaka/utani. jokingly adv. ~r n 1 chale, mcheshi, mfanya mzaha/masihara. 2 (sl) jamaa. 3 (playing cards)jokari.

jolly adj -a furaha, -changamfu,

-liochangamka adv (colloq) sana he was ~ miserable alikuwa na huzuni sana he'll ~ well have to do it lazima afanye. vt (colloq) bembeleza. jollification n shamra shamra. jollity n.

jolly-boat n mashua (ya meli).

jolt vt,vi tingisha, rusharusha; (fig) shtua the news ~ed us habari zilitushtua ~ along the road rushwarushwa (na gari n.k.). n 1 mshtuo, mtikisiko. 2 (fig) mshtuko. ~y adj.

Jonah n kisirani; mtu atolewaye kafara ili asilete nuksi.

josh

josh (US) (sl) vt,vi cheza shere; fanya utani, tania.

joss n (China) sanamu ya mungu (iliyochongwa kwenye jiwe). ~-house n hekalu la Kichina. ~-stick n udi.

jostle vt,vi songa, sukuma, kumba. don't ~ against me usinisukume.

jot1 vt ~ something down andika upesi/mara moja (ukumbusho). ~ter n kidaftari. ~tings n pl kumbukumbu.

jot2 n kipande kidogo, nukta there's not a ~ of truth in it si kweli hata kidogo.

joule n (elect.) (abbr.J) jouli.

journal n 1 gazeti; (periodical) jarida. 2 shajara, kitabu cha mambo ya kila siku, habari za kila siku (naut) batli. 3 daftari la kuwekea hesabu kabla ya kuandika katika daftari kubwa. 4 (sl) the ~s n (katika bunge) rekodi za shughuli za kila siku. ~ese n lugha chapwa za magazeti. ~ism n uandishi wa habari. ~ist n mwandishi wa habari. ~stic adj -a uandishi wa habari.

journey n safari, mwendo prepare for

a ~ funga safari set out on a ~ anza safari. pleasant ~ n safari njema. vi safiri.

joust n (hist) mapambano (vita) ya

mikuki mirefu kwa kutumia farasi. vi shindana (hasa kwa wapanda farasi).

Jove n Jupita: Mungu wa Kirumi. by~! Loo!

jovial adj -a bashasha, -liojaa furaha. ~ly adv. ~ity n.

jowl n taya; mashavu. ~y adj.

joy n furaha, shangwe, nderemo full of ~ furaha tele wish somebody ~ (of something) kumtakia mtu furaha (ya). ~-bells n kengele za shangwe. ~-ride n (sl) matembezi kwa motokaa (agh. bila ruhusa ya mwenye gari). ~-stick n (sl) (aviation) usukani. vt,vi furahia, furahiwa na. ~ful adj. ~fully adv. ~less adj -sio na furaha. ~lessly adv. ~fulness n. ~lessness n. ~ous adj. ~ously

judiciary

adv. ~ousness n.

jubilant adj -a shangwe; -a ushindi. be ~ -wa na shangwe. ~ly adv. jubilation n. jubilee n jubilii; sikukuu ya ukumbusho. silver jubilee n jubilii ya mwaka wa ishirini na tano. golden jubilee n sikukuu ya ukumbusho wa mwaka wa hamsini. diamond jubilee n sikukuu ya ukumbusho wa mwaka wa sitini.

Judaism n 1 Uyahudi. 2 dini ya Kiyahudi. Judaic adj.

Judas n 1 Yuda (aliyemsaliti Yesu), mhaini, msaliti. 2 ~-hole n (kwa mlango) kitundu cha kuchungulia.

judder vi tetemeka sana, tingishika

sana.

judge n 1 (leg) hakimu; kadhi (High Court) jaji. ~ made law n kanuni zinazotokana na maamuzi ya mahakama. 2 (competition) mwamuzi. 3 (critics) mhakiki, mtaalam. vt,vi 1 hukumu, toa hukumu. 2 amua. 3 (estimate) kisia, dhani, ona ~ it good to do something ona vema kufanya jambo fulani ~ a man by his actions mpime mtu kwa matendo yake. ~ment n 1 hukumu binding ~ment makataa. concurring ~ment n hukumu ya mwafaka dissenting ~ ment hukumu isiyowafiki. the Last ~ment/~ment Day n siku ya kiyama/hukumu ya mwisho sit in ~ on somebody hukumu mtu fulani ~ ment seat n kiti cha hukumu. 2 (opinion) shauri, maoni in my ~ment kwa maoni yangu. 3 (wisdom) akili, busara; ujuzi. 4 (taste) akili ya kutambua au kuchagua mazuri use your ~ment tumia uamuzi wako.

judiciary n Idara ya Mahakama; jamii ya majaji independence of the ~ uhuru wa mahakama. judicature n 1 usimamiaji haki. 2 jamii ya majaji. judicial adj 1 -a jaji, -a kimahakama judicial murder hukumu ya kifo isiyo haki. 2 -a haki,

judo

-siopendelea. judicious adj (formal) -enye akili, -a busara. judiciously adv. judiciousness n.

judo n judo: mchezo wa mieleka uchezwao sana na Wajapani.

jug1 n 1 jagi, dumu. 2 (sl) gereza, jela. ~ful adj.

jug2 vt 1 (usu in pp) pika katika chungu kilichofunikwa. 2 (colloq) funga gerezani.

juggernaut n 1 imani ya kutoa kafara/mhanga. 2 (colloq) tela, gari kubwa la usafirishaji.

juggle vi,vt 1 ~ (with) fanya kiinimacho; fanya mizungu. 2 (distort etc) chezea (ili kudanganya); ghushi. ~r n.

jugular adj -a shingo, -a koo ~ vein halkumu.

juice n 1 maji ya matunda/nyama n.k.; juisi (of grated coconut) kasimile, tui. 2 digestive/gastric ~ maji- tumbo. 3 (colloq) mafuta; umeme; gesi. juicy adj 1 -enye maji mengi. 2 (colloq) nayovutia (kwa sababu inaongelea tabia/kashfa za mwingine) give me all the juicy details leta umbeya wote. juiciness n.

ju-jitsu n (Japan) mchezo wa mwereka wa kujilinda/kujihami.

juju n (West Africa) 1 uchawi, ushirikina, ulozi. 2 kinyago cha uchawi.

juke-box n sanduku la santuri.

July n Julai: mwezi wa saba.

jumble vi,vt ~ (up) changanya, vuruga, fuja. n fujo, vurugu, mchanganyiko. ~-sale n seli ya mtumba/vikorokoro.

jumbo adj kubwa sana.

jump n mruko, ruko; chupo. long/

high ~ n (mchezo wa) kuruka chini/juu. 2 mshtuo. give somebody a ~ shtua. the ~s n (colloq) kutetemeka. 3 kupanda kwa ghafla yesterday there was a ~ in the price of rice jana bei ya mchele ilipanda ghafla. vi,vt 1 ruka; chupa. ~ down somebody's throat varanga. ~ing-off place mahali pa kuanzia.

junta

~ed-up adj (colloq) -enye majivuno, -enye kujidai, mjivuni. 2 ruka juu yao. ~ the rails/track acha reli. 3 shtuka, chachawa. 4 panda ghafla, ruka the price of oil has ~ed bei ya mafuta imepanda ghafla. 5 ~ at ruka, pokea kwa furaha, vamia. ~ to conclusions fikia uamuzi bila kutafakari. ~ on/upon karipia. 6 ~ (one's bail) toroka dhamana. ~ a claim pokonya eneo la mwingine (kwenye machimbo). ~ the gun anza mapema, wahi. (go and) ~ in the lake (colloq) toka hapa. ~ the queue ruka foleni, (fig) -tofuata utaratibu.

jumper n 1 sweta. 2 (US) aproni. 3 mrukaji, kirukaji.

junction n 1 njia panda. 2 mwungano ~ box kasha la mwungano wa waya za umeme.

juncture n 1 mwungano. 2 hali ya jambo. (esp in the phrase) at this ~ kwa hali ya mambo yalivyo/yalivyokuwa.

June n Juni: mwezi wa sita.

Jungle n (usu the ~ sing, or pl) msitu. the law of the ~ (fig) kanuni ya mwenye nguvu mpishe/mabavu. jungly adj -a kimsitu.

junior n mdogo (wa umri au cheo) he is my ~ yeye ni mdogo kwangu (US schools and colleges) mwanafunzi wa mwaka wa tatu (kati ya minne) ~ common room ukumbi wa wanafunzi adj -dogo (kwa umri); -a chini ~ class darasa la chini.

juniper n mreteni.

junk1 n 1 (rubbish) takataka, vikorokoro. ~ dealer/shop n mwuza/duka la vikorokoro/bidhaa kuukuu (zilizotupwa).

junk2 n jahazi la Kichina.

junket n 1 mtindi mtamu. 2 mandari yenye chakula. vi enda mandari ya chakula. ~ing n kufanya karamu.

junkie;junky n mlevi wa madawa ya kulevya.

junta n halmashauri ya utawala, baraza la majeshi (waliopindua

Jupiter

serikali).

Jupiter n 1 (of ancient Rome) Jupita: Mungu Mkuu wa Warumi. 2 Jupita (sayari iliyo kubwa).

jury n 1 baraza la wazee wa mahakama. grand ~ n baraza la uchunguzi wa awali. ~ box n kizimba cha mzee wa mahakama. coroner's ~ n wazee wa mahakama wanaotoa uamuzi wa sababu ya kifo. 2 (in competition) waamuzi (fig) the ~ of public opinion uamuzi wa umma. ~man n mzee wa baraza; mwamuzi. jurist n mwanasheria. juror n mzee wa baraza. 3 mtu anayeapishwa, mtu anayekula kiapo. juridical adj -a sheria; -a taratibu za kisheria. jurisdiction n mamlaka; mamlaka ya kisheria; utekelezaji wa sheria the issue is within my jurisdiction suala hili lipo katika mamlaka yangu. jurisprudence n 1 sayansi na falsafa ya sheria za binadamu. 2 maarifa ya sheria.

jury-mast n (naut) mlingoti wa muda (uliotiwa badala ya mwingine uliovunjika au kupotea).

just1 adj 1 -a haki, nyofu, -adilifu a ~ sentence hukumu ya haki a ~ person (mtu) mwadilifu. 2 (well-deserved) -enye kustahiki; -liostahili. ~ification n 1 kitu au sababu zinazothibitisha. 2 kuthibitisha jambo kuwa ni haki, kusadikisha. 3 haki, halali without ~ification bila ya haki/ uthibitisho. in ~ification (for/of something/somebody) kwa kuthibitisha/ kutetea jambo. ~ify vt 1 tetea, thibitisha uhalali wa jambo/ tendo ~ify the punishment you meted out thibitisha uhalali wa adhabu uliyoitoa. 2 -wa na sababu ya kufanya jambo, halalisha finishing your work early does not ~ify your loitering kumaliza kazi kwako mapema sio sababu ya kukufanya uzurure. 3 (of print) rekebisha. ~ifiable adj. ~ ifiably adv.

just2 adv 1 used (GB) in the perfect

tenses and (US often) with the simple

justice

past tense placed with the v to indicate an immediate past (GB) sasa hivi, ndio kwanza I have ~ finished my work ndio kwanza nimemaliza kazi yangu. ~ now sasa hivi. 2 (followed by n phrases and clauses) hasa this is ~ the person I wanted to see huyu ndiye hasa mtu niliyetaka kumwona. 3 ~ as (+adj+as) sawasawa na it is ~ as good as mine ni kizuri sawasawa na changu (introducing adverbials of time) wakati he brought it ~ as you were leaving alikileta wakati ule ule ulipokuwa unaondoka (introducing clauses of comparison) jinsi ~ as you find it difficult to depend on your pay jinsi inavyokuwia vigumu kutegemea mshahara wako. 4 (with adv) ~ here hapa hapa. 5 (used to indicate approximation) takribani it was ~ about 9.00 a.m. Ilikuwa takribani saa 3.00 asubuhi tu. 6 (only) He ~ managed to get the fare amefanikiwa kupata nauli tu I have ~ enough money for food nina fedha za kununulia chakula tu I am ~ an ordinary person mimi ni mtu wa kawaida tu. 7 (used in familiar colloqual style) hebu ~ look at this and see how good it is hebu tazama hiki na uone jinsi kilivyo kizuri. 8 (colloq) sana, mno the story was ~ too good hadithi ilikuwa nzuri mno. 9 wakati huuhuu/uleule. ~ now muda huu; muda kitambo, punde Saida left ~ now Saida ameondoka punde.

justice n 1 haki treat all men with ~ tendea watu wote haki. do ~ to tenda haki. do oneself ~ jitendea haki, -fanya jambo kulingana na uwezo wako. 2 mamlaka ya kisheria. bring somebody to ~ peleka mhalifu mahakamani akahukumiwe. 3 jaji wa Mahakama Kuu. Chief J~ Jaji Mkuu. ~ of the Peace (JP) hakimu wa Amani. Department of ~ (US) Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. justiciary n Mamlaka ya Jaji

jut

au Jaji Mkuu.

jut vi ~ out tokeza. n kutokeza.

jute n kitani.

juvenile n kijana, mtoto ~ court mahakama ya watoto ~ books vitabu vya watoto ~ delinquency uhalifu wa vijana.

juxtapose v weka sambamba.

juxtaposition n.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.