TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

K,k n herufi ya kumi na moja katika alfabeti ya Kiingereza).

kaaba n kaaba: jengo takatifu (linalozungukwa wakati wa hija, Makka).

Kaiser n Kaizari: mfalme wa Ujerumani kabla ya 1918.

kampong n (in Malaysia) boma, uzio, kijiji.

kale n kale: aina ya kabichi. kaleidoscope n nelibini.

kangaroo n kangaruu. ~ court n mahakama isiyo halali (iliyoundwa ili kuwaadhibu watu walioikosea jamii).

kaolin n kauri.

kapok n sufi.

kaput adj (pred only) (sl) -lioharibika; -liokwisha.

karat n see carat.

karate n kareti: mbinu za kujihami kwa mikono na miguu.

kayak n kayaki: mtumbwi wa Kieskimo uliofunikwa kwa ngozi ya sili.

kebab n mshikaki.

keel1 n 1 meli ya wachimba mkaa/kuchukua mkaa. 2 shehena ya makaa.

keel2 n mkuku. (keep) on an even ~ (of a ship) bila kuyumbayumba; (fig) tulia. vi,vt pindua; pinduka ~ over pinduka. ~ haul vt 1 buruza mtu majini nyuma ya meli (kama adhabu). 2 kemea/adhibu vikali.

keen1 adj 1 (of feelings, points & edges etc) kali, -enye makali; (fig) a ~ wind n upepo mkali. 2 (of persons, their character) -enye bidii, hodari. 3 (of the mind, interest) sana, -enye kupenda sana. be ~ on (colloq) penda. ~ly adv. ~ness n.

keen2 (Irish) n maombolezo. vi,vt omboleza.

keep vt,vi 1 weka, zuia; fanya kuwa ~ the class quiet nyamazisha darasa. ~ somebody indoors zuia mtu asitoke nje. ~ eye on (colloq) angalia kwa makini, linda. ~ something in mind kumbuka. 2 endeleza, weka ~

keep

somebody waiting ngojesha, fanya mtu aendelee kungoja. ~ somebody going wezesha mtu kuendelea shs 10,000/= will ~ me going for four days shiiling 10,000/= zitanitosheleza kwa siku nne. 3 ~ somebody/something from doing something zuia, kinga you must ~ the wall from falling lazima uzuie ukuta usianguke we couldn't ~ from crying hatukuweza kujizuia kulia. 4 ~ something (back) (from) ficha I can't ~ anything (back) from you siwezi kukuficha kitu; zuia, kata the employer ~s back 3000/= a month for my pension mwajiri wangu hukata 3000/= kila mwezi kwa ajili ya kiinua mgongo changu. ~ something to oneself (often imper) hifadhi, dhibiti, kaa na (kitu) ~ your views to yourself usiseme/usitoe maoni yako; nyamaza. 5 (with an implied complement) timiza ~ a promise timiza ahadi ~ the law fuata sheria. 6 adhimisha ~ one's birthday adhimisha siku ya kuzaliwa. 7 linda. 8 hifadhi, tunza ~ the money for me nitunzie fedha zangu. ~ a firm/tight hold on shika imara. 9 ruzuku, kimu; fuga his salary ~s him and his family mshahara wake unamkimu yeye na familia yake he ~s cattle on his farm anafuga ng'ombe katika shamba lake. 10 weka ~ a note of something weka kumbukumbu ya kitu ~ a ledger tunza daftari. ~ accounts tunza mahesabu. 11 -wa na, miliki ~ a shop -wa na duka. shop~er n mwuza duka. 12 tunza, simamia. ~ a house tunza nyumba. ~ open house -wa tayari kukaribisha wageni/marafiki. 13 ~ on/to endelea. K~ cool (fig) tulia! poa! ~fit kaa imara/bora wa afya ~ to the left enda upande wa kushoto ~ straight on enda moja kwa moja ~ right enda upande wa kulia. 14 ~ (on) doing something endelea kufanya jambo, fanya jambo mara kwa mara ~ smiling endelea kutabasamu my shoe ~s (on)

keep

coming off kiatu changu kinatoka mara kwa mara. ~ going endelea bila kusimama/kukoma. 15 (of food) -toharibika, kaa the food will ~ till tomorrow evening chakula hakitaharibika/kitakaa hadi kesho jioni. 16 (uses with adverbial particles and preps) ~ at something shikilia; kazania; fanyia kazi, sikate tamaa. ~ somebody at something kazania mtu aendelee na jambo fulani, himiza, tia ari. ~ away (from) (something) epuka, kaa mbali na ~ away from the dog mwepuke yule mbwa. ~ somebody/something away (from) epusha, zuia asikaribie. ~ back (from something) kaa/baki nyuma. ~ somebody back zuia mtu asiende mbele. ~ somebody down gandamiza, dhulumu. ~ something down zuia ~ down your anger zuia hasira yako; punguza ~ down your expenses punguza matumizi yako. ~ in (eg of fire) endelea kuwaka the fire will ~ in till I come back moto utaendelea kuwaka mpaka nitakaporudi. ~ in with somebody endelea kuwa na uhusiano mzuri, elewana/patana. ~ somebody in zuia kama adhabu. ~ off kaa mbali. ~ off something -sikaribie kitu fulani, -tojihusisha na. ~ somebody/ something off zuia ~ your hands off me usiniguse. ~ on (doing something) endelea, shikilia. ~ on working endelea kufanya kazi. ~ something on endelea kuvaa. ~ somebody on endelea kumwajiri mtu. ~ on at somebody sumbua kwa malalamiko, maswali n.k. ~ out (of something) kaa mbali, -tojiingiza. ~ somebody/something out (of something) zuia kuingia ~ out of my business usingilie shughuli zangu. ~ to something timiza, fanya jambo lililokubaliwa ~ to your promise fanya kama ulivyoahidi, timiza ahadi yako. ~ to oneself jitenga, epuka kukutana na watu. ~ somebody/ something under tawala, zuia ~ the

kernel

fire under zuia moto usienee. ~ up (with somebody) enda kwa kasi/ mwendo sawa na mtu mwingine Juma kept up with his classmates Juma aliendelea sawa na wenzake. ~ up with the Joneses shindana na majirani (katika kuhodhi vitu) (gari, nguo n.k.). ~ somebody up chelewesha mtu kulala mapema Don't ~ the children up usiwacheleweshe watoto kulala. ~ something up zuia kitu kisizame au kuteremka chini ~ up your courage jijasirishe zaidi; fuata, heshimu ~ up old customs endeleza/fuata mila za kale; endelea we will ~ up the discussion the whole day tutaendelea kujadili mchana kutwa; tunza it costs me a great deal to ~ up my farm inanigharimu sana kulitunza shamba langu. ~ it up endelea. n 1 riziki, chakula. 2 mnara wa ngome/boma. 3 for ~s (colloq) kwa kudumu, daima, abadani this is mine for ~s hii ni mali yangu kabisa/abadani. ~er n 1 mlinzi, mwangalizi. 2 (in compounds) gate ~er n bawabu. park ~er n mwangalizi wa hifadhi. ~ing n 1 hifadhi, ulinzi. in safe ~ing mahali pa usalama. 2 (in verbal senses) ufugaji. in/out of ~ ing (with) -a kupatana/-siopatana na. ~sake n kumbukumbu, ukumbusho.

keg n kikasiki, kipipa.

kelp n 1 majani ya bahari, mwani. 2 majivu ya mwani.

ken n (only in) beyond/outside my ~ (colloq) nje ya ujuzi/utambuzi wangu. vt (Scot) fahamu, tambua.

kennel n 1 kibanda cha mbwa. 2 chaa ya kufuga na kufundisha mbwa vt,vi weka/tunza mbwa.

kept vt see keep.

kerb (also curb) n ukingo wa barabara (wa kikuta). ~stone n jiwe la ukingo wa barabara.

kerchief n kitambaa; leso.

kerf n mkato wa msumeno.

kernel n kiini wheat ~ kiini cha

mbegu ya ngano; (fig) ~ of

kerosene

argument kiini cha hoja.

kerosene n kerosini, mafuta ya taa.

ketch n mashua/chombo kidogo cha milingoti miwili.

ketchup n kechapu: nyanya na viungo tamutamu.

kettle n birika, kandirinya put the ~ on teleka birika.

kettle-drum n ngoma ya shaba nyeupe.

key1 n 1 ufunguo (wa mlango, saa n.k.). ~ hole n tundu la ufunguo. ~ money n kilemba. ~ring n pete ya ufunguo. master/skeleton ~ n ufunguo malaya. 2 ~ (to) (fig) ufumbuzi. 3 ufunguo wa saa. 4 (of text book) majawabu, (translation) tafsiri. 5 (also attrib) mlango a ~ position nafasi maalumu. 6 (attrib) muhimu ~ industry tasnia muhimu (kwa ajili ya uendelezaji wa viwanda vingine). ~stone n (archit) jiwe la kiungo kwenye tao; (fig) msingi/jambo muhimu. 7 kibao cha tapureta/piano/kinanda/filimbi ~ board msururu wa vibao hivyo. 8 (music) ufunguo (mfululizo wa noti wenye mfumo maalumu); (fig) namna/mtindo wa sauti/mawazo in a minor ~ kwa huzuni all in the same ~ bila kuonyesha hisia; kwa sauti ya namna moja. ~ note n noti ya msingi; (fig) wazo linalojitokeza.

key2 vt linganisha sauti (kwa kukaza/ kulegeza nyuzi). ~ something in patanisha kitu na vingine. ~ something into something patanisha/ unganisha vitu. ~ somebody up chochea/amsha mtu.

key3 n kisiwa kidogo/tambarare (cha matumbawe).

khaki n kaki adj -enye rangi ya kaki, -a kaki.

khan1 n khan: cheo cha watawala na maofisa wa Asia ya Kati, Afghanistan n.k. (in olden times) (jina la cheo la) mfalme wa Waturuki; Watarta wa Mongolia.

khan2 n (in the East) hoteli yenye ua (inayotumiwa na misafara).

kibbutz n kibuzi; shamba/makazi (ya

kid

kijamaa Israeli). ~nik n mwanakibuzi.

kick1 n 1 teke. get more ~s than halfpence shukrani ya punda ni mateke. ~ back n (US sl) bahashishi; kiasi cha fedha (apewacho mtu kwa kumpatia mwingine mapato). 2 (colloq) msisimko. do something for ~s fanya kwa kusisimka. be on a ~ (sl) zama katika shughuli. 3 (colloq) nguvu. he has no ~ left in him amechoka, yu hoi. 4 kushtua kwa nguvu. ~ start (er) n pedali ya kuwashia pikipiki. vt,vi 1 piga teke. ~ the bucket (sl) fariki. ~ a goal (Rugby football) funga goli. ~ one's heels kaa bure/bila kazi. ~ somebody up stairs (fig) toa mtu mahali fulani kwa kumpa cheo kikubwa zaidi. 2 (of a gun) shtuka baada ya kufyatuliwa. 3 (special uses with adverbial particles and preps) ~ against/at pinga, onyesha kuudhika/kulalamika/kutoridhika; kaidi. ~ off (football) anza mchezo. ~ something off vua kwa kupiga teke, kwa kutupa/kurusha miguu ~ off one's slippers vua ndara kwa kupiga teke. ~off n kuanza. ~ somebody out fukuza mtu. ~ something up pandisha kitu kwa kukipiga. ~ up a fuss/shindy/ row/stink (colloq) sababisha fujo, leta vurumai kwa kubisha. ~ up one's heels (of a horse) rukaruka baada ya kutumikishwa; (fig) jifurahisha.

kid1 n 1 mwana mbuzi. 2 ngozi ya mwana mbuzi. ~ gloves n glavu za ngozi ya mwanambuzi. handle somebody with ~ gloves (fig) shughulikia kwa unyenyekevu (pasipo kuwa mkali). 3 (sl) mtoto (US sl) kijana college ~s vijana wa chuo. ~dy n (sl) kitoto, mtoto mdogo. vt (of a goat) zaa.

kid2 vt,vi (sl) (kwa kuongopa) tania; danganya don't ~ yourself, usijidanganye.

kidnap

kidnap vt iba mtoto; teka nyara. ~per n mtekaji nyara; mwizi wa watoto.

kidney n 1 figo. ~ bean n haragwe jekundu. ~ machine n mashine ya figo (mashine itumiwayo kufanya kazi ya figo kwa mgonjwa wa mafigo).

kill vt,vi 1 ua; fisha. ~ somebody/ something off ua; ondosha ~ time jishughulisha wakati wa kungoja. 2 poteza, haribu, fifisha the red carpet ~s your curtains zulia jekundu linafifisha rangi ya) mapazia. 3 shinda; piga kura ya vito. ~ joy n mtu anayeharibu furaha ya wengine. 4 vutia sana. ~ somebody with kindness haribu mtu kwa kumfanyia huruma sana, dekeza sana. dress to ~ vaa ili kuvutia watu. n 1 kuua. be in at the ~ shuhudia kuuawa mnyama. 2 (in hunting) windo. ~ing adj (colloq, dated) -a kuchosha, -a kuchekesha sana. make a ~ing fanikiwa sana. ~ingly adv. ~er n muuaji.

kiln n tanuru, joko. vt kausha jikoni.

kilo1 n pl (abbr of) ~gram kilo.

kilo2 pref 1000. ~gram n kilo: (gramu 1000). ~metre n kilomita: mita 1000.

kilt n sketi ya mikunjo ifikayo magotini, kitambaa cha tarta. ~ed regiment n askari wa kiskoti wavaao sketi hizo.

kimono n kimomo: kanzu refu jembamba la Kijapani.

kin n aali; ukoo, mlango; jamaa, ndugu. next of ~ n ndugu wa karibu zaidi. ~dred n 1 ukoo, udugu claim ~dred with somebody dai kuwa wa ukoo mmoja na fulani. 2 familia, ndugu, jamaa adj (attrib only) -a asili moja; -a namna moja, -a kufanana. ~ly adj 1 -ema, -pole. 2 (of climate) tulivu. 3 halali. ~liness n. ~folk n ndugu, jamaa. ~sman n ndugu/ jamaa wa kiume. ~swoman n ndugu/jamaa wa kike. ~ship n uhusiano wa damu; kufanana kwa tabia.

kind1 adj -ema, -enye huruma,

king

-karimu. ~ hearted adj -ema, -enye huruma. ~ly adv 1 kwa huruma/ ukarimu. 2 (in polite formulas) will you ~ly close the door tafadhali funga mlango. 3 kirahisi, kawaida take ~ ly to kubali kirahisi. ~ness n wema, huruma. out of ~ness kwa huruma. do/show somebody ~ness onyesha huruma/wema.

kind2 n 1 namna, kabila. 2 aina, ngeli, namna a ~ of dog namna ya mbwa all ~s of things kila aina ya vitu coffee of a ~ kinywaji kama kahawa. nothing of the ~ si kitu kama hicho, si hivyo; hata kidogo. something of the ~ kitu kama hicho this ~ of -a aina hii ya what ~ of? -a namna gani? ~ of; ~a kwa kiasi fulani I ~ of expected nilitarajia kiasi. 3 asili, tabia they differ in ~ wanatofautiana sana. 4 in ~ (of payment) vitu/bidhaa (si fedha) repay somebody in ~ tendea fulani jinsi ulivyotendewa naye; lipiza kisasi.

kindergarten n shule ya chekechea, shule ya watoto wadogo, shule ya awali.

kindle vt,vi 1 washa moto. 2 (excite) amsha, chochea. kindling n vijiti vya kuwashia moto.

kine n pl (old form) ng'ombe.

kinetic adj -a mwendo. ~ art n sanaa mwendo. ~ energy n nishati mwendo. ~s n pl (with sing v) elimumwendo.

king n 1 mfalme. turn ~'s evidence toa ushahidi dhidi ya mhalifu mwenzi. 2 mtu mashuhuri. 3 (chess game) kete kuu; (playing cards) mzungu wa nne. 4 kitu kikubwa katika kundi la vitu/wanyama. the ~ of beasts n simba. the ~ of the forest n mwaloni. the ~ of terrors n kifo. 5 (compounds) ~bird n shore. ~ bolt n komeo kubwa. ~crab n kaa mkubwa. ~craft n ustadi wa kutawala. ~ cup n ua kubwa la njano. ~fish n nguru. ~fisher n mdiria/chepea. ~

kink

-maker n mtu mwenye kuathiri uteuzi wa mfalme/uchaguzi wa viongozi. ~pin n komeo; (fig) mtu muhimu. ~size(d) adj kubwa sana ~ size cigarettes sigara kubwa sana. ~like; ~ly adj -a kifalme; -a fahari, -kuu. ~ship n ufalme, utawala. ~dom n 1 ufalme, himaya. the United K~dom (the UK) Uingereza. 2 (of God) ufalme wa Mungu gone to ~dom come (colloq) aga dunia. 3 migawano mikuu ya viumbe/maumbile duniani the animal ~dom jamii ya wanyama na binadamu the vegetable ~dom jamii ya mimea the mineral ~dom ulimwengu wa madini/miamba/ mawe. 4 (realm or province) eneo, sehemu.

kink n 1 pindokombo; waya/nywele; kasoro, dosari. 2 (fig) wazo lisilo kawaida. vt,vi fanya pindokombo. ~y adj -enye tabia ya ajabu, -a kichaa.

kiosk n 1 kibanda cha simu. 2 kibanda cha kuuzia bidhaa.

kip1 n ngozi ya mnyama mdogo iliyotengenezwa.

kip2 n (GB. sl) chumba, kitanda cha wageni (katika nyumba ya kupanga). vi lala, korota.

kipper n samaki aina ya heringi (ainaya samaki aliyekaushwa kwa moshi na kutiwa chumvi). vt kausha samaki (aliyetengenezwa kwa chumvi).

kirk n (Scot) kanisa.

kismet n (Turk) kudura.

kiss vt,vi busu. ~ the hand busu mkono. ~ the book apa kwa neno la Mungu. ~ the dust/ground onyesha utii, uwawa. ~ the rod kubali adhabu ya viboko. ~-in- the-ring n mchezo wa watoto ambao mmoja humfukuza mwenziwe na akimkamata humbusu. n 1 busu. 2 peremende. the ~ of life n kuingiza hewa ndani ya mtu kwa kutumia njia ya mdomo kwa mdomo. ~er n (sl) domo; bakuli.

kit n (collective sing) 1 vyombo, vifaa,

knack

zana (agh nguo) za askari au msafiri, the whole ~ and Kaboodle (colloq) (US sl) watu/vitu/vikorokoro vyote. ~-bag n fuko, shanta 2 vifaa vya kazi. 3 do-it- yourself ~ n seti ya sehemu za kifaa zinazoungwa na mnunuzi. vt ~ somebody out/up (with something) -pa vifaa vyote vinavyohitajika katika shughuli fulani.

kitchen n jiko, meko; (GB) chumba cha kulia (chakula) pamoja na shughuli nyingine. everything but the ~ sink vitu vingi mno (zaidi ya inavyohitajika). ~-garden n bustani ya mboga na matunda. ~-sink drama n (GB in 1950's and 1960's) tamthilia inayoakisi maisha ya mfanyakazi (agh jinsi anavyotambua hali ya kisiasa, uchumi, kijamii n.k.). ~ unit n vifaa vya jikoni vilivyounganishwa pamoja. ~ware n vifaa vya jikoni. ~ette n chumba kidogo cha kupikia chakula.

kite n 1 mwewe; kipanga. 2 tiara, kishada. fly a ~ (fig) pima mawazo ya watu kwa jambo fulani. ~-balloon n putotiara la kijeshi.

kith n (only in) ~ and kin jamaa, ndugu na marafiki.

kitsch n, adj (in the arts, design etc) -enye ulimbwende/madoido yasiyo na maana.

kitten n mtoto wa paka have ~s (colloq) -wa na wahaka/ wasiwasi, wayawaya. ~ish adj. kit n mtoto wa paka.

kitty n 1 (in some card games) mfuko wa fedha za michezo; (colloq) mfuko wa fedha. 2 (of a child's language) nyau.

kiwi n kiwi: ndege (wa New Zealand) asiye na mbawa; (sl) mwenyeji wa New Zealand.

kleptomania n udokozi. ~c n mdokozi.

knack n welekevu, weledi, ustadi there's a ~ in it lazima ujifunze kwa kutenda get the ~ -wa na ustadi (ubingwa), elewa have the ~

knacker

of doing something -wa na ustadi wa kufanya kitu.

knacker n 1 mchinja farasi. 2 mtu anayenunua nyumba, meli, mashine kuukuu ili avunje na kupata vifaa. ~'s yard n mahali pa kuvunjia vyuma vikuukuu. vt chocha. ~ed adj (GB) -enye kuchoka sana, hoi.

knap vt vunja mawe kwa nyundo.

knapsack n shanta.

knave n 1 (old use) ayari, laghai. 2 (laying cards) mzungu wa tatu, ghulamu. ~ry n. knavish adj. knavishly adv.

knead vt (dough/clay/muscles) kanda.

knee n 1 goti. bring somebody to his ~s tiisha mtu. fall drop on one's ~s angukia (kwa kuomba msamaha). be on/go down on one's ~s piga magoti (kwa kuabudu). 2 sehemu ya nguo (agh suruali) inayofunika magoti. 3 (compounds) ~breeches n suruali fupi iliyofungwa chini ya magoti. ~ cap n pia ya goti/kifuu cha goti/kibandiko cha goti. ~-deep adj, adv -nayofikia magoti. ~capping n kupiga risasi miguuni. ~high adj,adv -a magotini.

kneel vi ~ (down) piga magoti.

knell n mlio wa kengele (ikigongwa moja moja kama kwa maziko); (fig) ishara ya mwisho/kifo cha kitu. vt (fig) piga kengele (agh kama onyo).

knelt vi pt, pp of kneel.

knesset n Bunge la Israeli.

knew vt pt of know

knickerbocker n ~s kaboka.

knickers n pl 1 (US) (inform) chupi ya

mwanamke. 2 (old use) kaptura mkunjo. get one's ~ in twist (GB sl) changanyikiwa.

knick-knack n kikorokoro.

knife n (pl knives) kisu; jisu, (for tapping palm -trees) kotama pocket ~ kisu cha kukunja, kijembe. get one's ~ into somebody dhamiria kudhuru. war to the ~ uhasama mkali, kukinzana na, vita vya kufa na kupona before you could say ~ kufumba na kufumbua. ~ edge n

knock

makali ya kisu. on a ~-edge of (a person awaiting important outcome, result etc.) -enye mashaka/wasiwasi mwingi be/go under the ~ pasuliwa. vt kata/choma kwa kisu.

knight n 1 (in the Middle Ages) shujaa wa ukoo bora anayepewa daraja la juu katika jeshi baada ya kuonyesha uhodari wote. ~ -errant n shujaa wa ukoo bora aliyekwenda kutafuta ushujaa. 2 (GB modern use)cheo cha hadhi/heshima kinachotolewa kwa kulitumikia taifa (mwenye cheo hiki huitwa "Sir" kabla ya jina lake). 3 (GB history) ~ (of the shire) Mbunge wa jimbo. 4 (game of chess) kete yenye kichwa cha farasi. vt pa cheo, tunza cheo cha 'Sir'. ~hood n 1 cheo/heshima ya shujaa wa ukoo bora. 2 watu wenye cheo hiki. ~ly adj.

knit vt,vi ~ something (up) (from/into) 1 fuma ~ a sweater fuma sweta. 2 (join closely) unga; unganisha. 3 weka pamoja. ~ one's/the brows kunja uso. ~ter n mfumaji. ~ting n 1 kufuma. 2 nyuzi za kufumia. ~ting-machine n mashine ya kufumia. ~ting-needle n sindano ya kufumia. ~wear n (trade use) nguo zilizofumwa.

knives n pl of knife.

knob n 1 kirungu. 2 kifundo, kinundu. ~ kerrie n rungu. ~bly adj -enye fundo. ~ble n kirungu kidogo.

knock n 1 pigo; bisho a ~ at the door kupiga/kubisha hodi, bisho mlangoni he got a slight ~ on the fore-head alipata pigo hafifu pajini. ~ for ~ (of an Insurance Company) kulipia kile kile kilicholipiwa bima. 2 (of a petrol engine) kuvunjika, kuharibika, kunoki. 3 (cricket) zamu (ya kupiga). 4 (sl) lawama; hasara. ~er n 1 mtu/kitu kinachobisha mlango. ~ up n mtu anayeamsha wafanyakazi asubuhi. vt,vi 1 bisha, gonga ~ at the door bisha mlango, bisha/piga hodi. ~ against something/somebody

knock

gonga/gongana na kitu/mtu. ~ one's head against a brick wall (fig) jisumbua bure. 2 (sl) shangaza; shtusha 3 (of a petrol engine) noki, vunjika, haribika. 4 (sl) kosoa. 5 (compounds). ~-about adj (of clothes) zinazofaa kwa kazi. ~-down adj (of prices eg at an auction) -a bei nafuu; -a chini na mwisho; (fig) -a kushangaza, -a kuduwaza. ~-kneed adj, -enye magobwe. ~out adj, n (abbr KO) pigo la ushindi/ushinde (kwenye mchezo wa masumbwi); (sl) -a usingizi (of a tournament) mashindano ya kutoana; (colloq) (person, thing) -a kuvutia, -a kupendeza, -a usingizi ~out pills dawa za usingizi. 6 (uses with adverbial particles and props). ~ about (colloq) kuzurura. ~ about (with somebody) -wa na uhusiano (wa kimapenzi) na, tembea na. ~ somebody/something about piga mara kwa mara; fanyia ubaya. ~ something back (sl) -nywa ~ back a pint of beer -nywa bia; shangaza. ~ somebody down angusha; gonga. you could have ~ed me down with a feather nilishangaa sana, niliduwaa/shikwa na bumbuazi. ~ something down bomoa, haribu; changua katika sehemu ~ down the furniture fungua fanicha katika sehemu (kupata wepesi wa kusafirisha). ~ something/somebody down (to something) uzia mtu kitu kwenye mnada. ~ down prices punguza bei. ~ something in pigilia, gongomea ~ in a nail pigilia msumari. ~ off (work) pumzika. ~ somebody off (sl) tongoza na kutelekeza. ~ something off punguza/tunga/maliza haraka; (cricket) funga haraka haraka; (sl) vunja; iba ~ off a bank vunja benki. ~ it off (sl) acha! ~ on (Rugby) gonga mpira kwenda mbele wakati wa kujaribu kuudaka ~ or effect n (colloq) matokeo mabaya; mwambukizano. ~ somebody out

know

(boxing) angusha mpinzani kiasi cha kushindwa kuendelea; (fig) shangaza; duwaza, zimisha. ~ somebody out (of) toa shinda (mpinzani). ~ something out kung'uta ~ out one's pipe kung'uta kiko (ili kutoa tumbaku). ~ (things) together gonganisha/weka vitu haraka haraka, haraka/ovyo ovyo. ~ your/their heads together tumia nguvu kuzuia mtu/watu wasigombane, waache ujeuri; gonganisha vichwa vyenu. ~ up (tennis) zoezi fupi kabla ya mchezo. ~ somebody up, (GB colloq) amsha mtu (GB colloq) chosha, taabisha, (US sl) shambulia, piga; (US vulg sl) (of a man) jamiina na; tia mimba. ~ something up piga/rusha juu kwa ngumi; panga/weka/tengeneza pamoja haraka; (of cricket) funga. ~ up copy (in newspaper etc) tayarisha mswada kwa uchapishaji. ~ into fundisha kwa nguvu; kutana na (bila kutegemea). ~ off ua.

knoll n kilima kidogo; mwinuko, kiduta, kuchuguu.

knot n 1 fundo tie/make a ~ piga fundo make a ~ (fig) funga the marriage ~ kufunga ndoa/pingu za maisha. 2 utepe wa mapambo (wenye mafundo). 3 shida, taabu, tatizo. tie oneself in/up in/into ~s jibabaisha; changanyikiwa. 4 (of trees) kifundo.~ hole n shimo la kifundo. 5 (of persons) kikundi. 6 (naut) noti: mwendo wa futi 6080 (mita 1853) kwa saa ship of 16 ~s meli inayokwenda noti 16 kwa saa. vt,vi fanya/funga fundo. ~ty adj 1 -enye kifundo ~ ty tree mti wenye vifundo. 2 gumu kufahamu. ~ty problem n tatizo gumu kutatuliwa.

knout n mjeledi wa ngozi (uliotumika Urusi kutolea adhabu). vt piga kwa mjeledi.

know vt,vi 1 jua, fahamu, elewa, tambua ~ one's business/what's what/the ropes/a thing or two -wa na ujuzi wa jambo fulani; elewa

knuckle

utaratibu wa jambo fulani; -wa na uamuzi wa busara; jua unachofanya. ~ better than to do something jua ni vizuri kutofanya jambo fulani. ~ about/of fahamu jambo fulani, -wa na habari kuhusu. 2 fahamu, tambua, jua (mtu), fahamiana na; tofautisha/pambanua mtu/kitu. make oneself ~n to somebody jitambulisha. be ~n to julikana na he's ~n to the police anajulikana na polisi. be ~n as julikana kama. ~ somebody from somebody tofautisha, pambanua. ~ something from something weza kutofautisha kitu. not~ somebody from Adam/from a bar of soap (colloq) -tofahamu (mtu) kabisa. 3 jua vizuri. 4 weza kutambua. (compounds) don't-~ n (colloq) msailiwa asiyejua maswali ya kura ya maoni. ~-all n (derog) sogora, mjuaji. ~-how n akili ya kutengeneza vitu n.k., ujuzi wa mbinu za utekelezaji; ufundi ustadi, ubingwa wa ufundi. n (only in) in the ~ (colloq) -enye habari. ~able adj ~ing adj. -stadi, -juzi, -enye maarifa; -erevu, -janja. ~ingly adv 1 kwa makusudi. 2 kwa ujuzi in a ~ing manner kwa ujuzi, kwa utambuzi. ~ledge n 1 elimu; maarifa. ~ledgeable adj -enye maarifa mengi/akili/ fahamu. 2 ujuzi. 3 ufahamu, utambuzi.

knuckle n 1 konzi. 2 (in animals) goti, kongoro. vi ~ down to something (colloq) anza kazi fulani kwa bidii, zamia. ~ under jitoa, salimu amri.

koala n (zool) koala: dubu mdogo wa Australia migodini.

kohl n wanja wa manga.

kohlrabi n aina ya kabichi.

kola n mkola. ~ nuts n kola.

kook n (sl) mjinga. ~y adj -a ujinga.

kookaburra n (Australia) mkumburu.

kopec(k) n see copeck.

kopje; koppie n (in South Africa) kilima kidogo, mwisho, kiduta.

Koran n Kurani, Msahafu.

kosher n adj (food, foodshop) -enye

Kwela

kutimiza kanuni za Kiyahudi.

kourbash n (in Turkey/Egypt) mjeledi; kiboko.

kowtow; kotow n (former Chinese custom) kusujudu (kama ishara ya heshima/utii), kusujudia. vt ~ (to), sujudia; rairai, nyenyekea.

kraal n (in South Africa) 1 kijiji (kilichozungushiwa boma). 2 zizi.

Kremlin n Kremlin: ngome ya mji wa Moscow. the K ~ Makao Makuu ya Chama na Serikali ya Urusi.

krona n korona: sarafu ya fedha ya Sweden.

krone n sarafu ya fedha ya Denmark au Norway.

kudos n (colloq) heshima (kwa sababu ya tendo); sifa.

kudu n tandala.

Ku-Klux-Klan n jumuia ya siri ya ubaguzi wa rangi Marekani.

kulak n (Russian) kulaki: mkulima tajiri.

kungfu n kungfu: riadha ya kujihami, karate ya Kichina.

kwashiorkor n unyafuzi, chirwa.

Kwela n (South Africa) Kwela: aina ya jazi.

 

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.