TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

Ll n 1 herufi ya kumi na mbili katika alfabeti ya Kiingereza. 2 namba 50 ya Kirumi.

la n (music) la: noti ya 6 katika muziki.

laager n 1 (in S. Africa) kambi iliyopangwa kati ya duara ya magari. 2 (mil) maegesho ya magari ya kivita. vt,vi 1 egesha magari katika duara. 2 jihami nyuma ya magari.

lab n (colloq) (abbr of) laboratory.

label n 1 kitambulisho (chenye maelezo/anwani ya mzigo). vt weka kitambulisho chenye maelezo/anwani ya kitu/mzigo. (fig) ~ somebody (as something) -pa/pachika mtu (cheo, sifa, jina) he was ~led a thief alipachikwa jina la wizi.

labial adj -a midomo; -a kufanyika kwa midomo; (phon) ~ sounds sauti za midomo k.m. m,p,b. labio- pref -a mdomo.

laboratory n maabara, lebo.

labour (US)labor n 1 kazi division of ~ mgawanyo wa kazi. hard ~ n kazi ngumu. manual ~ n kazi ya mikono/sulubu. ~ saving adj -a kupunguza kazi. 2 kazi. a ~ of love kazi afanyayo mtu kwa upendo. 3 wafanyakazi. ~ Exchange n ofisi ya leba. the ~ Party n Chama cha Leba/Wafanyakazi. ~ leaders n viongozi wa Chama cha Leba; viongozi wa Chama cha Wafanyakazi. ~ Day n (US) sikukuu ya wafanyakazi; Jumatatu ya kwanza ya mwezi Septemba. ~ union n (US) Chama cha Wafanyakazi. 4 uchungu wa uzazi a woman in ~ mwanamke mwenye uchungu. vt,vi 1 fanya kazi, tumika; jitahidi. 2 enda/ pumua polepole na kwa shida. 3 ~ under somebody/something teseka, pata shida ~ under a disadvantage teseka kwa shida ~ under a delusion jidanganya. 4 fanya kazi kwa undani/urefu mno. ~ed adj 1 -a shida/taabu. ~ breathing n upumuaji wa shida, taabu. 2 -enye kutafakuri mno. ~er n mfanyakazi, kibarua.

lactate

~ite n mwanachama/shabiki wa chama cha Leba. ~ious adj 1 (of work etc) -harubu, -a kuchosha. 2 -enye kuhitaji makini. 3 gumu. ~iously adv.

labret n ndonya.

labyrinth n 1 njia za mzingo; (fig) matata mengi, mchanganyiko wa mambo. 2 (bio) sikio la ndani. ~ine adj.

lace n 1 (shoes) kamba. 2 lesi, gangiri, kimia. ~-glass n kioo chenye marembo. ~-pillow n mto wa kufuma lesi. vt,vi ~ (up) 1 funga viatu kwa kamba. 2 pamba nguo kwa lesi. 3 ~ something with something etc tia (pombe kali) kidogo n.k. 4 ~ into somebody piga mtu. lacing n. lacy adj -a kimia, -a lesi.

lacerate vt 1 papura, kwaruza (agh. ngozi). 2 (fig) tia uchungu. laceration n.

lachrymal adj -a machozi ~ glands tezi za machozi. lachrymose adj lizi, -enye machozi.

lack n utovu, ukosefu, upungufu, uhitaji no ~ of tele for ~ of kwa sababu ya ukosefu wa (naut) ~ of stability mleoleo. vt,vi ~ (in) -tokuwa na; kosa, pungukiwa na, hitaji we ~ books hatuna vitabu they ~ed for nothing hawakuhitaji/ hawakukosa kitu he ~s good manners hana adabu the borrower ~s not, he who ~s is the owner of the vessel mwenye kuazima hatoi, mtovu ni mwenye chombo; -tovu, -enye kukosa. ~-lustre adj -a mazimbwezimbwe, bila uhai.

lackadaisical adj -enye kupuuza, -enye kuchoka, zembezembe, -sio na bidii. ~ly adv.

lackey n mtumishi wa kiume; (fig) mnyonge; kikaragosi.

laconic adj -a maneno machache. ~ally adv. laconism n.

lacquer n vanishi; behedani vt paka vanishi/behedani.

lactate vt tunga maziwa; nyonyesha maziwa. n (chem) chumvi ya maziwa. lactation n. lactic adj -a

lactose

maziwa ~ acid asidi ya maziwa yaliyochachuka.

lactose n (chem) laktosi.

lacuna n uwazi, pengo. ~l; ~ r adj.

lacustrine adj -a ziwa ~ dwelling kijiji cha ziwani ~ plain uwanda wa ziwa.

lad n kijana (mwanamume); mvulana. ladder n 1 ngazi, (naut) kipande mount/climb the ~ panda ngazi. 2 (US=run) kufumuka kwa soksi. ~ proof adj -siofumukika. vi (of stockings) fumuka.

laddie n see lad.

lade vt pakia shehena, sheheni. n (with) adj 1 -enye shehena, -enye mizigo, -liojaa. 2 (over-burdened by grief) -a kulemewa. lading n shehena, mizigo. bill of lading n hati/idhini ya kuchukulia mizigo; orodha ya mizigo melini.

la-di-da adj -a mzofafa, -a mbwebwe; -a kujifaragua, kujidai.

ladle n (of soup) upawa, ukasi; (of water) kata. vt ~ (out) gawa kwa upawa/kata; (fig) toa (heshima/sifa n.k.) kwa wingi. ~ful n kata tele.

lady n 1 bibiye, mke wa lodi. 2 bibi. ~ in-waiting n bibi mpambe. ~ of the house mama mwenye nyumba. 3 mwanamke yeyote; (pl) mabibi. Ladies and Gentlemen mabibi na mabwana. 4 mke your ~/wife mke wako 5 Ladies (used as sing n) choo cha wanawake. 6 (attrib) -a kike a ~ doctor daktari wa kike. 7 (compounds) (rel) Our L~ n Bikira Maria L~ Day n (rel) sikukuu ya kupashwa habari ya kuzaliwa bwana (tarehe 25 Machi). ~-killer n (slang) mtekaji wanawake. ~-love n mchumba/mpenzi (mwanamke). ~'s maid n mtumishi wa bibi. ladies' man n mwanaume anayependa wanawake. ~ like adj -a adabu, -a malezi mazuri.

lag1 n (sl) mfungwa an old ~ mtu aliyefungwa mara nyingi. vt 1 tia gerezani. 2 bamba.

lag2 vi kawia, chelewa, enda polepole ~behind kawia. n (time) ~ muda wa

lambaste

kuchelewa. ~gard n mvivu, goigoi mchelewaji.

lag3 n kihami. vt hami/fungia/vingirishia kitu (kuzuia joto kupita).

lager n bia isiyo nzito wala kali sana; lagoon n wangwa.

laic adj -siokuwa -a dini, -a kawaida.

n mtu wa kawaida, mlei. ~al adj. ~ize vt toa katika utawala wa dini, fanya (agh. padri) awe mtu wa kawaida.

laity n mlei, watu wa kawaida (wasio weledi).

laid pp of lay.

lain pp of lie.

lair n 1 malalo ya mnyama wa mwitu; tundu/pango; (fig) pango/maficho ya majambazi. 2 banda (la ng'ombe). vt,vi enda mlaloni; -wa/-weka mlaloni.

laird n (Scot) kabaila, mmilikaji ardhi, lodi.

laissez-faire n uholela: hali ya kuacha mambo yajiendee kiholela.

lake1 n ziwa. ~ dwellings n makazi

fukweni mwa ziwa. The Great ~s n (N. America) maziwa matano makubwa. the L~ District n (GB) sehemu yenye maziwa mengi. ~ poets n washairi waliokaa huko (Coleridge, Wordsworth n.k.)

lake2 n (colour) ngeu.

lakh n (India and Pakistan) laki.

lam vt,vi (sl) bubuta, dunda, kung'uta. ~ into somebody bubuta mtu, karipia.

lama n mchungaji/mtawa wa madhehebu ya Kibuda (Tibet na Mongolia). ~sery n makao ya watawa wa kibuda.

lamb n 1 mwanakondoo, nyama ya mwanakondoo. 2 maasumu; mpenzi. like a ~ (to the slaughter) (kufa) kingoto, kimyakimya. vt zaa (vikondoo), gwisha. ~ kin n mwanakondoo mchanga. ~skin n ngozi ya mwanakondoo. ~'s wool n sufu ya mwanakondoo.

lambaste vt (sl) tandika, kong'ota,

lambent

buta; karipia sana.

lambent adj (liter) 1 -a kumetameta. 2 (of eyes/sky) -a kung'aa. 3 (of humour, wit) bashasha. lambency n.

lame1 adj 1 kiguru, kiwete be ~ chechea, -enda chopi he has a ~ leg amelemaa mguu. 2 (of metre) -a mikingamo. 3 (unsatisfactory) -siofaa, si -zuri, -a wasiwasi. vt lemaza. ~ly adv. ~ness n.

lame2 n kitambaa chenye nyuzi za dhahabu au fedha.

lament vt,vi ~ (for/over) lia, omboleza; sikitika. n 1 kilio, maombolezo; sikitiko. ~able adj. ~ably adv. ~ation n.

laminate vt, vi fanya tabaka jembamba, chana (katika) tabaka; funika kwa tabaka. ~d adj ~ plastic sheets fomeka.

lamp n 1 taa. street ~s taa za barabarani. table ~ n taa ya kusomea (lantern) kandili, fanusi; kibatari. 2 ~light n mwanga/nuru ya taa. ~lighter n (hist) mwasha taa barabarani. ~-post n nguzo ya taa (barabarani). ~-shade n kifuniko cha taa.

lampoon n stihizai, kushtumu/ kukashifu mtu. vt stihizai.

lance n (hist) mkuki, fumo, lansi break a ~ with somebody bishana sana na mtu. ~ corporal n koplo lansi. ~r n askari wa farasi. ~s n pl (with sing v) dansi ya watu wanane au zaidi. vt choma kwa fumo; pasua, tumbua (jipu) n.k. ~t n kisu kidogo (kinachotumika kupasulia). lancinating adj (of pain) -a kuchoma, kali.

land n 1 ardhi, nchi kavu travel over ~ safiri nchi kavu go by ~ enda kwa gari, treni n.k. 2 shamba, konde; kiwanja work on the ~ fanya kazi shambani. ~army n (GB) kikosi cha wafanyakazi wa kike wa shamba wakati wa vita vikuu vya pili Our ~ is about ten hectares shamba letu lina ukubwa wa hekta kumi. ~ agent n (chiefly GB) (US real estate agent)

land

mwangalizi/msimazi wa shamba; wakala wa mashamba/viwanja. 3 nchi, taifa (la asili ya mtu) my native ~ nchi yangu ya asili distant ~s nchi za mbali. the ~ of the living maisha ya sasa I'm still in the ~ of the living bado nipo the promised~/ the ~ of Promise Nchi ya Ahadi (Canaan). 4 (compounds) ~ fall n kukaribia nchi kavu (kutoka majini). ~ forces n jeshi la nchi kavu. ~ holder n mmilikaji wa ardhi. ~ lady n mwanamke mwenye hoteli/nyumba ya kupangisha. ~ locked adj -liozungukwa na nchi kavu ~ locked countries nchi zisizokuwa na bandari. ~ lord n kabaila; mwenye hoteli/nyumba ya kupangisha. ~ lubber n (used by sailor) (mtu) asiye baharia. ~mark n alama (k.m. mnara, n.k.); alama ya mpaka; (fig) jambo/tukio/wazo muhimu (linalodhihirisha) upeo au mabadiliko. ~ mine n mabomu ya ardhini. ~ owner n mmiliki ardhi. ~ rover n landrova: gari madhubuti la barabara mbaya. ~ slide n mporomoko wa ardhi; (in election) ushindi mkubwa ~slide victory ushindi mkubwa sana. ~ slip/slide n. ~s man n mtu asiye baharia. vt,vi 1 (of aircraft) tua; (of ship) fika pwani, teremka pwani the aeroplane ~ed at night ndege ilitua usiku the passangers ~ed when the ship anchored at the harbour abiria waliteremka (pwani) meli ilipotia nanga bandarini. ~ on one's feet (fig) -wa na bahati; nusurika. 2 ~ somebody/oneself in something ingia matatani. ~ up (colloq) wasili; jikuta, ishia because of his bad behavior one day he ~ed up in jail kutokana na tabia yake mbaya siku moja alijikuta jela Juma ~ed up this morning unexpectedly Juma aliwasili asubuhi hii bila kutegemewa. 3 (colloq) pata ~ a good job pata kazi nzuri. 4 (sl) piga/ chapa (kibao/ngumi) he ~ed him

landscape

one... alimpiga kibao kimoja ... ~ed adj -a ardhi; -enye kumiliki ardhi/shamba. ~less adj -siokuwa na ardhi/shamba. ~ing n 1 kushuka/ kutua/ kuteremka pwani (nchi kavu). ~ craft n meli ya kushushia pwani/ufukoni (magari ya kivita, askari n.k.). ~ field/strip n kiwanja cha kutua ndege. ~ gear n marandio. ~ net n fuko la kutilia/kuzolea samaki. 2 (also ~ place n) gati, bunta. ~ party n kikosi cha askari (agh. wa kutuliza fujo). ~ stage n kikwezo. 3 jukwaa la ngazi.

landscape n 1 mandhari, sura ya nchi. 2 uchoraji/usanii wa mandhari. ~ gardening/architecture n usanifu wa bustani/majenzi kimandhari.

lane n 1 barabara nyembamba,

uchochoro. it is a long ~ that has

no turning hakuna marefu yasiyo na ncha. 2 ujia; (in sports) mstari inside ~ mstari wa ndani. 3 njia ya meli/ndege n.k.

language n 1 lugha the ~ of the Nyamwezi Kinyamwezi. dead ~ n lugha ya kale (ambayo haizungumzwi tena). ~ laboratory n maabara ya lugha. professional ~ n lugha ya kitaalam/kieledi. 2 ishara zitumiwazo kwa mawasiliano. computer ~ n lugha ya kompyuta. 3 maneno, misemo itumiwayo katika kikundi fulani. technical ~ n lugha ya kifundi. 4 bad/strong ~ n lugha chafu, kali, -liojaa matusi n.k.

languish vi nyong'onyea, dhoofika, fifia, punguka. ~ for somebody taka mtu sana ~ for love teseka kwa mapenzi. languid adj -legevu; -chovu, -nyong'onyevu be ~ nyong'onyea, choka. ~ly adv. languor n unyong'onyevu, udhaifu, ulegevu; uchovu.

langur n ngedere (mwenye mkia mrefu).

lank adj 1 -embamba na refu, -a kimbaombao. 2 (of hair) -ilionyoka. ~y adj (of a person, his arms or

lapse

legs) -a njorinjori; -lonjo.

lanolin n lanolini: shahamu inayotokana na sufu.

lantern n fanusi, kandili. ~jawed adj -enye mataya marefu membamba.

lanyard n 1 ugwe wa filimbi. 2 kamba (ya kufungia vitu melini).

lap1 n 1 paja; mapaja. 2 kipande cha

vazi (kinachofunika mapaja). be/live in the ~ of luxury ishi maisha ya anasa. in the ~ of the Gods (of future event) kwa kutegemea kudra, mashakani. ~ dog n kijibwa cha kupakata. ~top n kompyuta ndogo ya kupakata. vt,vi 1 funika/funga kwa nguo n.k. 2 pitana, pandana the iron sheets on the roof ~ over mabati yamepandana. n mapandano; mzunguko mmoja (katika mbio).

lap2 vi,vt ~ up 1 -nywa (kwa kulamba kama paka). 2 (colloq)(of human beings) pokea, twaa upesi/kwa shauku, papia. 3 (of water) piga (piga), fanya sauti kama mnyama anayekunywa kwa ulimi (k.m. mawimbi madogo pwani). 4 -wa mbele kwa mzunguko mmoja (kwenye mashindano), zunguka wenzako. n kunywa kwa ulimi kulambalamba; sauti ya unywaji kwa ulimi.

lapel n mkunjo (wa koti) kifuani.

lapidary adj -enye kutia nakshi katika mawe/kito; -lionakshiwa; (fig) nadhifu, fasaha a ~ speech hotuba fasaha. n mtianakshi mawe/kito.

lapis lazuli n kito cha nili na zari, rangi ya nili.

lapse n 1 kuteleza (kwa ulimi/matendo/ maandishi) ~ of memory kupitiwa ~ of the tongue kuteleza ulimi. 2 ~ (from) (into) kupotoka, kuanza kutoka kwenye mstari/kuwa na tabia isiyohisi. 3 (of time) kupita the ~ of time kupita kwa muda. 4 (leg) kupotea, kuisha kwa haki (kwa kutotumia au kutoiomba tena). vi 1 ~ (from) (into) potoka; shuka hadhi. 2 (leg) poteza haki (kwa kutodai au kutoihuisha).

lapwing

lapwing n pigile: aina ya ndege.

larboard n (arch see port side).

larceny n (leg) wizi, wivi. larcener n. larch n mti wa aina ya msonobari.

lard n mafuta ya nguruwe. vt tia mafuta ya nguruwe (katika nyama), tia bekoni kuongeza utamu. ~ with (fig)(often derog) tia mbwembwe (hadi kuchusha).

larder n chumba au kabati ya kuhifadhia chakula na nyama.

large adj 1 (in size, importance) -kubwa; (in quantity) -ingi. ~ of limb -enye miguu, mikono mikubwa. ~ scale adj kubwa ~ scale farmer mkulima mkubwa (mwenye shamba kubwa) ~ scale map ramani yenye vipimo/skeli kubwa. 2 (liberal) -ema, -karimu ~ hearted -ema, -a huruma, -karimu ~ minded -enye kupokea mawazo ya wengine. n (only in) at ~ huru the bandits are still at ~ yale majambazi bado hayajaka- matwa/yako huru; kwa undani talk at ~ zungumza kwa undani; kwa jumla; hobelahobela, bila lengo. ~ly adv kwa majivuno his failure was ~ly due to laziness kushindwa kwake kumetokana hasa na uvivu wake; kwa ukarimu, bure. ~ness n. largish adj kubwa kiasi.

largesse; US largess n zawadi; ukarimu mkubwa.

largo (music) adj kwa polepole kabisa.

lariat n kamba ya kufungia mifugo (farasi, ng'ombe n.k.); kamba yenye kitanzi.

lark1 n kipozamataza.

lark2 vi cheza kwa furaha/kimzaha. n mzaha, mchezo what a ~!, inafurahisha namna gani! furaha iliyoje!

larn vt,vi (dial) -jifunza/funza.

larrup (colloq) charaza viboko.

larva n lava; (of mosquito) kiluwiluwi; (of a bee) jana; (of a fly) buu; (of a butterfly) kiwavi. ~l adj.

larynx n zoloto: sehemu ya mwanzo ya koromeo inayohusika na utoaji sauti,

laryngitis n uvimbe wa zoloto.

lascar n baharia wa Kihindi.

lascivious adj -kware, -a kiasherati. ~ly adv. ~ness n.

laser n leza: chombo cha kukuza na kushadidisha miale kuelekea upande mmoja. (attrib) ~ beams n mwangaza leza.

lash n 1 mjeledi; mchapo, kiboko; kipigo cha mjeledi/kiboko. the ~ n adhabu ya kupigwa viboko. 2 eye ~ n kope. vt,vi 1 chapa, piga; sukuma (k.v. kiungo cha mwili) the rain was ~ing (against) the window mvua ilipiga dirishani. 2 ~ somebody into (a state) amsha, chochea. ~ out (against/at somebody/ something) shambulia (kwa kupiga au kwa maneno). 3 ~ one thing to another; ~ things together fungasha, funga pamoja kwa nguvu. ~ something down kaza, funga. ~ up n chombo kilichofaraguliwa/ kilichoundwa kwa haraka/bila makini. ~ing n 1 kamba ya kufungia. 2 kipigo, mchapo. 3 (pl, colloq) tele, chungu nzima mangoes with ~ings of cream embe na malai chungu nzima ~ings of drink vinywaji tele.

lass/lassie n msichana; mpenzi. lassitude n uchovu, kuchoka.

lasso n kamba yenye kitanzi (ya kukamatia wanyama). vt kamata kwa kamba yenye kitanzi.

last1 adj 1 -a mwisho. ~ but not least -a mwisho katika orodha lakini si kwa umuhimu this is our ~ hope hili ndilo tumaini letu la mwisho he is the ~ person I would like to talk to yeye ni mtu wa mwisho ambaye ningependa kuongea naye; nisingependa kuongea naye the ~ thing in mass media kitu cha mwisho/kitu kipya kabisa katika utawanyaji wa habari. 2 -liopita. ~ year mwaka uliopita/jana ~ night usiku wa kuamkia leo. n the ~ of mwisho. breathe one's ~ (liter) kata roho; fariki. at (long) ~

last

mwishowe, hatimaye. to/till the ~ hadi mwisho (liter or rhet) hadi kifo. ~ly adv (in making a list) mwisho, mwishoni. 2 mwisho she was well when I saw her ~ alikuwa na afya njema nilipomwona mara ya mwisho. vi 1 ~ (out) endelea, dumu, kaa will Salehe ~ in his new job? Salehe atakaa kwenye kazi yake mpya? 2 tosha we have enough food to ~ (us) four days tuna chakula cha kututosha kwa siku nne. ~ing adj -a kudumu.

last2 n foroma (kiatu); mguu: kibao cha

kutengenezea viatu stick to one's ~ fanya yale tu uwezayo kuyamudu.

latch 1 kia; komeo, kiwi the door is on the ~ kitasa hakijafyatuliwa, mlango umefungwa kwa komeo. 2 kitasa, kikomeo. ~-key n ufunguo wa kikomeo/kitasa. ~-key child n (colloq) mtoto anayeachwa peke yake (wazazi wake wanapokwenda kazini). vt,vi 1 funga kwa komeo. 2 ~ on (to) (colloq) ng'ang'ania; elewa.

late adj 1 -liochelewa, -liokawia be ~ chelewa. 2 (of night) -kuu, -kubwa ~ night usiku mkuu, usiku wa manane. 3 mwishoni ~ summer mwishoni mwa majira ya joto. 4 -pya, -a kisasa. 5 -liopita. 6 hayati, marehemu. 7 of ~ (hivi) karibuni. at (the) ~ st kabla au siyo zaidi ya adv 1 baadaye, kwa kuchelewa. Better ~ than never (prov) kawia ufike. ~ in the day baadaye sana. ~r on baadaye. early ~ wakati wote and she is at school early and ~ yuko shuleni muda wote. sooner or ~r sasa au wakati mwingine ujao. 2 karibuni. latish adj -enye kuchelewachelewa, -liotaahari. ~ly adv hivi karibuni, juzijuzi.

lateen n (naut) (only in) ~ sail n tanga la pembe tatu.

latent adj fiche. ~ ambiguity n utata fiche.

lateral adj 1 pembeni, -a mbavuni, -a kando. ~ erosion n mmomonyoko wa kingoni. 2 (phon) kitambaa.

laterite n ngegu.

laugh

latex n ulimbo wa mpira.

lath n uwasa; upapi.

lathe n kerezo.

lather n 1 povu (la sabuni). 2 jasho jingi. vt,vi 1 toa jasho. 2 toa povu. 3 (colloq) chapa, piga.

Latin n Kilatini; watu wenye asili ya

Kilatini adj -a Kilatini. ~ America n Amerika ya Kusini. the ~ Church n Kanisa Katoliki. the ~ Quarter n (of Paris) Sehemu ya ukingo wa kusini wa Mto Seine (wanakoishi wanafunzi na wasanii kwa karne nyingi). ~ist n msomi wa Kilatini. ~ize vt fanya -a Kilatini. ~ phrases n nahau za Kilatini I speak Latin ninasema Kilatini.

latitude n 1 latitudo. 2 (pl) maeneo. high ~s n maeneo yaliyo mbali na Ikweta. low ~s n maeneo yaliyo karibu na Ikweta. 3 (space, liberty, choice) nafasi, uhuru, hiari. 4 (photo) wakati wa salama wa kuangaza filamu. latitudinal adj. latitudinarian adj,n mvumilivu, mwenye upeo/upana wa mawazo.

latrine n choo.

latter adj 1 -a karibuni, -a baadaye. ~ -day adj -a sasa. 2 (also as pron) the ~ -a pili, (miongoni mwa yali-yotajwa), -liofuata. the former and the ~ -a kwanza na -a pili. ~ly adv karibuni, sasa.

lattice n kiunzi cha fito; waya zinazokingamana. (attrib) ~ window n dirisha la vipande vya vioo kwenye fremu ya risasi. ~d adj.

laud vt (formal) sifu; himidi adj -enye kusifika. ~ably adv. ~atory adj (formal) -a kusifu.

laudanum n laudanumu: dawa ya kupoza itengenezwayo kwa afyuni.

laugh vi,vt 1 cheka. ~ at cheka dhihaki; dharau; puuza. ~ in somebody's face dharau bayana. ~ one's head off vunja mbavu (kwa kicheko). ~ on the other side of one's face badilika (kutoka kwenye

launch

furaha na kuwa na majonzi). ~ over cheka huku unaendelea kufanya jambo. ~ up one's sleeve cheka/ furahi kirohoroho/kwa siri. He ~s best, who ~s last, He who ~s last ~ longest (prov) kutangulia si kufika. 2 ~ away puuza kwa kucheka kwa dharau. ~ down nyamazisha kwa kicheko. ~ off ondoa aibu kwa kucheka. 3 -wa katika hali fulani kwa kucheka. ~ oneself silly vunja mbavu (kwa kucheka). have the last ~ shinda/fanikiwa hatimaye. ~able adj -a kuchekesha. ~ably adv. ~ing adj -a furaha/kuchekesha. ~ gas n gesi ya usingizi. ~ingly adv. ~ter n kicheko.

launch1 vt,vi 1 (of a ship, esp one newly built) shua, zindua. 2 ~ something (against/at) (fig) anzisha/anza; lenga; tuma. 3 anza ~ a man into business tia mtu katika biashara. ~ out; ~ (out) into anza. n 1 kushua (merikebu, meli mpya). 2 kutuma chombo angani.

launch2 n mashua (agh. itumiayo injini).

laundry n 1 udobi. 2 the ~ n nguo chafu (zinazohitaji kufuliwa na kunyooshwa). ~ man n dobi wa kiume. launder vt,vi fua na nyoosha nguo, -wa dobi. launderette n mahala/mashine ndogo ya kufulia (ya kukodi). laundress n dobi wa kike.

laureate n poet ~ malenga wa ushairi.

laurel n laurusi: mti aina ya mdalasini. look to one's ~ chunga heshima; fahamu jinsi ya kuwashinda washindani. rest on one's ~s ridhika na mafanikio mtu aliyoyapata. win/ gain one's ~s pata heshima/sifa. ~led adj.

lav (colloq abbr of) lavatory.

lava n lava.

lavatory n maliwato, msala.

lave vt (poet) nawa; ogesha; (of a stream) tiririka (polepole).

lavender n mrujuani; rangi ya urujuani. ~ water n manukato ya

lay

mrujuani.

lavish adj 1 ~ (of something/in doing something) -karimu mno, paji mno. 2 (of what is given) -ingi mno, tele; -a kupita kiasi ~ expenditure on luxuries matumizi makubwa katika anasa. vt ~ on toa kwa wingi; toa kwa ukarimu mno ~ care on the first child jali mno mtoto wa kwanza. ~ly adv.

law n 1 sheria ~-giver n mtoaji sheria (k.m. Musa kwa Wayahudi, Soloni kwa Wagiriki). ~-officer n mwanasheria wa serikali (US) polisi. break the ~ vunja sheria. lay down the ~ toa hoja ya nguvu; amuru, sema kwa nguvu. ~ abiding adj -enye kufuata/kutii sheria. ~ breaker n mvunja sheria. take the ~ in one's hands jichukulia sheria mkononi. go to ~ (against somebody); have the law on somebody (colloq) shitaki mahakamani. ~ court n mahakama. ~ suit n daawa, kesi; madai. 2 (esp of games or art) kanuni. be a ~ unto oneself puuza kanuni. 3 (natural~) kanuni the ~ of self-preservation kanuni za kujihifadhi. ~ful adj -a kufuata sheria; halali. ~fully adv. ~less adj -a kuvunja sheria, halifu. ~less acts n vitendo vya kihalifu. ~lessly adv. ~lessness n. ~yer n mwanasheria.

lawn1 n (uwanja wenye) nyasi zinazotunzwa vizuri. tennis ~ n uwanja wa tenisi. ~-mower n mashine ya kukata nyasi. ~tennis n tenisi.

lawn2 n bafta.

lax adj 1 -zembe; -sio kali; -sio angalifu. 2 (of the bowels) -a kuhara have ~ bowels hara. ~ity n. ~ly adv. ~ative n haluli, dawa ya kuharisha adj -a kuharisha, -a kuendesha.

lay1 n (chiefly in) the ~ of the land sura ya nchi.

lay2 adj 1 (RC) -a mtu wa kawaida, -a

lay

mlei ~ brother bruda mfanyakazi. 2 -sio -eledi ~ opinion mawazo ya watu wa kawaida. ~man n (mtu) mlei, asiye mtaalam.

lay3 n (lit) wimbo; utenzi.

lay4 n mwenzi katika kujamiiana/ kukazana.

lay5 vt,vi 1 weka, laza; tandaza he laid his hand on my shoulder aliweka mkono wake begani mwangu. ~ a snare/trap/an ambush (for somebody/something) tega mtego/tegea mtu, tayarisha mtego/uvamizi. 2 (of non-material things, and fig uses) weka. ~ (one's) hands on something/somebody) nyang'anya; chukua he keeps everything he can ~ his hands on huchukua kila kitu anachokiona; umiza, jeruhi; pata; (eccles) bariki. ~ing-on of hands uwekaji wakfu; kufanya kasisi; uthibitisho. ~ the blame for something on somebody laumu, twisha/tupia lawama. ~ a (heavy) burden on somebody pa kazi/wajibu mzito; pa mateso. ~ one's hopes on wekea matumaini. ~ a strict injunction on somebody (to do something to) amuru. ~ great/ little store by/on something, thamini sana/kidogo. ~stress/emphasis/ weight on something fanya kuwa muhimu, sisitiza. ~ a tax on something toza kodi. 3 sababisha hali fulani. ~ somebody to rest zika. ~ somebody under a/the necessity/ obligation lazimisha, shurutisha. ~ somebody under contribution lazimisha mtu atoe mchango. ~ something to somebody's charge -pa wajibu. 4 (~+n, adj or adv phrases) ~ something bare onyesha kwa uwazi kabisa, fichua. ~ something flat sambaza, tandaza. ~ something open fichua, onyesha waziwazi, funua, eleza; kata. ~ oneself open to something jiweka katika hali ya kulaumiwa, kushukiwa n.k. ~ something waste angamiza, teketeza. 5 tuliza. ~ somebody's doubts

lay

ondosha mashaka. ~ a ghost/spirit fukuza/punga mizimu/mashetani. 6 (of birds and insects) taga mayai. 7 (usu passive) (story) tokea (katika mahali fulani). 8 tayarisha, andaa, panga ~ the table andaa meza ~ the fire tayarisha moto mekoni. 9 weka dau. 10 tandika, funika ~ carpet on the floor tandika zulia sakafuni. 11 (sl) jamiiana; kaza, tia. 12 (use with adverbial particles and preps) ~ about one (with something) pigapiga, piga pande zote. ~ something aside weka akiba; weka chini, acha (tabia fulani n.k.). ~ something back laza geuza/geuka, pindua/pinduka. ~ something by weka akiba. ~ somebody/oneself down laza/jilaza. ~ something down lipa; anza kujenga meli n.k.; geuza shamba kuwa sehemu ya malisho; hifadhi (divai) ghalani (agh. chini ya ardhi). ~ something down; ~ it down that agiza, panga (kanuni, sheria, utaratibu n.k.). ~ down one's arms weka silaha chini (kama ishara ya kusalimu amri). ~ down the law amuru. ~ down one's life jitolea mhanga. ~ down office jiuzulu. ~ something in weka akiba ya. ~ off (colloq) acha kufanya kazi; pumzika; acha kufanya jambo la kuudhi. ~ somebody off achisha kazi kwa muda. ~ off n muda ambao watu wanakuwa wameachishwa kazi. ~ something on weka gesi, maji, umeme kwenye jengo; colloq) toa, panga. ~ it on (thick/with a trowel) visha kilemba cha ukoka. ~ something out tanda, tandaza; osha/tayarisha (maiti) kwa kuzika; (colloq) tumia fedha; panga. ~out n mpango; mpangilio wa (kurasa, tangazo, kitabu n.k.), utaratibu. vt ~ out one's money carefully tumia fedha kwa uangalifu; weka mipango/utaratibu wa kazi, panga. ~ oneself out (to do something) jitahidi; jiandaa. ~ over (US) (GB

lay

stop over) (journey) simama kwa mapumziko. ~over n mapumziko ya safarini. ~ something up weka akiba; jichimbia kaburi you're ~ing up trouble for yourself in the future unajichimbia kaburi; simamisha shughuli za meli kwa ajili ya matengenezo. ~ somebody up (usu passive) sababisha (mtu abaki kitandani).

lay6 pt of lie2

lay-about n (GB sl) lofa, mtu asiyetaka kufanya kazi.

lay-by n (GB) sehemu ya kuegeshea magari kando ya barabara.

layer n 1 safu, tabaka, rusu. ~-cake n keki ya rusu. 2 (gardening) chipukizi lililofungiwa ardhini. 3 kuku wa mayai. vt panga juu kwa juu, fungia chipukizi/kichomozi cha mti ardhini; chomeka ardhini.

layette n mavazi na mahitaji mengine ya mtoto mchanga.

layfigure n sanamu ya binadamu (agh. hutumiwa kuvalishwa nguo kwa maonyesho).

lay-man n see lay.

lazar n (arch) mtu maskini mwenye ugonjwa (agh. mkoma). ~etto (also ~ et, ~ette) n 1 nyumba ya kuuguza maskini wenye ukoma na magonjwa ya kuambukiza. 2 jengo/meli iliyowekwa karantini.

Lazarus n ombaomba; fukara, fakiri. lazy adj -vivu, -zembe, -tepetevu. ~-bones n mvivu, mkunguni, mtepetevu. lazily adv. laziness n. laze (away). vt,vi jikalia, kaa kwa uvivu, -wa vivu.

lea n (poet) mbuga, uwanja wa nyasi.

leach vt chuja ~ out/away ondosha. n mchujo ardhi, chujuko (la ardhi).

lead1 n 1 risasi an ounce of ~ risasi ya bastola. ~-ore n miamba iliyo na risasi. ~ poisoning n ugonjwa unaosababishwa na sumu ya risasi. ~ works n kalibu ya risasi. 2 (also black ~) risasi ya kalamu. 3 timazi; chubwi. cast/heave the ~ pima urefu wa maji. swing the ~ (sl)

lead

kwepa/kacha kazi kwa kulaghai. 4 (pl) bati la risasi, mapaa yaliyoezekwa na mabati ya risasi; fremu za risasi. ~ed adj. ~en adj 1 -a risasi. 2 -enye rangi ya kijivu. 3 zito. ~en heart n moyo mzito. ~ing n nafasi kati ya mistari ya chapa.

lead2 n 1 kuongoza; mwongozo, welekezo. follow somebody's ~ fuata uongozi wa. give somebody a ~ mpe mtu mfano/dokezo. take the ~ tangulia, ongoza. 2 the ~ n nafasi ya kwanza. (attrib) the ~ story n (journalism, news broadcasting) habari iliyopewa uzito wa kwanza. a ~ n kadiri ya kutangulia have a ~ of five metres tangulia kwa kiasi cha mita tano. take over/lose the ~ tangulia/rudi nyuma (katika shughuli). 3 kamba ya kuongoza mbwa, kigwe. 4 (drama) mhusika mkuu; mwigizaji mkuu. 5 mfereji (uelekeao kwenye kinu). 6 (electr) waya wa umeme. 7 (in card games) haki ya kucheza kwanza. vt,vi 1 ongoza ~ an army ongoza jeshi ~ the way tangulia, ongoza njia. ~ in n utangulizi; waya wa simu za upepo na televisheni. 2 ongoza ~ a blind man ongoza kipofu. ~ somebody astray (fig) potosha mtu, shawishi ~ somebody by the nose tawala mtu kabisa. ~ somebody on (fig) shawishi mtu afanye zaidi ya alivyotegemea ~ a woman to the altar (joc) oa. 3 tangulia. ~ off anza. 4 ongoza/ athiri/shawishi (mawazo au vitendo); fanya (kufikiri) what led you to this idea kitu gani kilikufanya ufikiri hivyo. 5 elekea; (fig) sababisha, leta your work seems to be ~ing no where kazi yako inaonekana haielekei popote. ~ up to fanya matayarisho. All roads ~ to Rome (fig) kuna njia nyingi za kukufikisha mahali fulani. 6 (cause somebody to) ishi, pitisha, endesha maisha. ~ somebody a dog's life fanya mtu

leaf

aishi maisha ya dhiki, taabisha (in card games) anza. 7 ~ with (journalism) pa uzito wa juu/kwanza. ~er n 1 kiongozi, mkuu, msimamizi. 2 wakili mkuu (kwa kesi fulani). 3 (GB) (newspaper) habari yenye uzito wa kwanza. 4 chipukizi. 5 ukano. ~erless adj. ~ership n uongozi. ~ing adj kuu; -a kwanza; maarufu. a ~ ing article n maoni ya mhariri. ~ ingcase n kesi ya msingi. ~ inglight (colloq) n mtu maarufu. ~ ing question n swali linaloelekeza kwenye jibu n uongozi, usimamizi. ~ingrein n hatamu (ya kuongoza farasi). ~ingstrings n pl kamba ya kumwongoza mtoto anayefundishwa kutembea. in ~ing-strings (fig) kuongozwa/kuelekezwa kama mtoto mdogo.

leaf n 1 jani; (of a coconut tree) kuti; (colloq) petali. in ~ adj -enye majani. come into ~ ota majani. ~-bud n sehemu jani linapoota. ~-mould n mboji. 2 karatasi (katika kitabu). take a ~ out of somebody's book fuata mfano wa mtu, -iga, chukua mtu kama mfano. turn over a new ~ ongoka, jirekebisha na anza upya. 3 bamba, kipande chembamba cha chuma (agh. cha dhahabu). 4 kipandemeza: ubao unaoweza kutolewa kufanya meza iwe ndogo zaidi vi ~ through (a book, etc) pitia (kwa kusoma) haraka haraka. ~less adj -siokuwa na majani. ~y adj -liofunikwa na majani, -enye majani .~let n 1 jani changa. 2 ukurasa (wenye matangazo).

league1 mapatano baina ya watu/ vikundi/mataifa yenye malengo sawa; shirikisho, washiriki, wanachama katika mapatano. The L~ of Nations n Shirikisho la Mataifa (1919-1946). be in ~ with shirikiana na; -wa na shauri moja na. 2 (sports) ligi. vt,vi shiriki, shirikiana.

league2 n (old) kipimo cha urefu (kama maili 3).

leak vt,vi 1 vuja. ~ (out) to (of

learn

news, secrets etc) (cause to) toka; fichuka, julikana. n 1 upenyu, mvujo, ufa, tundu. 2 gesi/maji yanayovuja. ~age n 1 kuvuja, mvujo. 2 kufichuka (siri). 3 kiasi kinachovuja/kinachofichuka. ~y adj.

leal adj (Scot or lit) -aminifu, -tiifu.

lean1 adj 1 (of persons and animals) -embamba, -liokonda become ~ konda, dhoofika; (of meat) -nofu -siokuwa na mafuta. 2 -siozalisha; hafifu; ~ years miaka ya mavuno machache/mwambo. n mnofu/nyama isiyokuwa na mafuta. ~ness n.

lean2 vi,vt 1 enda upande, egama. ~ over backward(s) (to do something) (colloq) fanya juu chini kumridhisha mtu, kupata kitu. 2 ~ (on/upon) egemea. 3 egemeza. 4 ~ towards elekea. 5 ~on/upon tegemea. ~ing n (of mind) mwelekeo. ~-to n kibanda kinachoegemea nyumba nyingine.

leap vi,vt 1 ruka; chupa. ~ at pokea/ kubali kwa furaha nyingi. look before you ~ fikiri kabla ya kutenda. 2 ruka; rusha ~ a horse over a fence rusha farasi juu ya ua. n mruko; ruko. by ~s and bounds upesi sana. a ~ in the dark jaribio (ambalo matokeo yake hayabashiriki. ~-frog n mchezo wa kurukiana. ~-year n mwaka mrefu (ambamo mwezi wa Februari unakuwa wa siku 29).

learn vt,vi 1 jifunza ~ one's lessons jifunza masomo. ~ by heart kariri. 2 arifiwa, pata habari, ambiwa I have yet to ~ if the train arrived sijapata habari kama treni ilifika. 3 (vulgar or dialect) fundisha I'll ~ you! nitakufundisha! ~ed adj -enye elimu, -juzi ~ed man n msomi the ~ed professions utaalamu (ualimu, uhakimu, n.k.) my ~ed colleague msomi mwenzangu. ~edly adv. ~ed n mwanafunzi. ~ing n elimu, ujuzi, usomi a man of great ~ing mtu mwenye ujuzi, mtaalamu.

lease

lease n mkataba wa kupangisha/ kukodisha nyumba, duka, shamba n.k.; hati ya kukodisha. let on ~pangisha, kodisha. take on ~ panga, kodi. give/get a new ~ of life -pa/pata nguvu mpya. vt panga/pangisha; kodi/kodisha. ~hold n nyumba/duka/shamba lililopangishwa/iliyokodishwa adj -a kukodi; -a kupanga. ~holder n mpangaji.

leash n ukanda/ugwe wa kufungia/ kuongoza wanyama (hasa mbwa) hold in ~ zuia kwa ukanda; (fig) dhibiti. strain at the ~ (fig) wa na shauku kuwa huru; -wa na shauku kupata fursa ya kufanya jambo. vt zuia/funga kwa ukanda/ugwe.

least adj 1 dogo kuliko -ote, -lio dogo. (maths) ~ common multiple n kigawe kidogo cha shirika (KDS). ~ common denominator n kigawe kidogo cha asili (KDA). the ~ said the better ni bora kukaa kimya ~ said soonest mended (prov) heri kutosema zaidi. 2 (phrases) at ~ angalau (not) in the ~ kidogo tu; hata kidogo to say the ~ (of it) bila kutia chumvi adv (the) ~kidogo, kwa kiasi kidogo. ~ of all kabisa; jambo la mwisho no one can object ~ of all Mariamu hakuna anayeweza kupinga, hata Mariamu I would ~ of all want to hurt you jambo la mwisho ninalotaka kufanya ni kukuudhi wewe. ~wise; ~ways adv walao, angalau.

leather n 1 ngozi (iliyotengenezwa iwe laini na isioze). 2 (compounds) ~ jacket n lava wa aina ya inzi. ~ neck n (US,sl) askari mwana maji. vt chapa, piga (hasa na ukanda wa ngozi). ~y adj -a ngozi, -gumu kama ngozi. ~ette n ngozi mwigo/bandia.

leave vt,vi 1 toka, ondoka; we shall~ here tomorrow tutaondoka hapa kesho. ~ for ondoka kwenda/ kuelekea (mahali fulani) ~ for Nairobi ondoka kwenda Nairobi. 2 (of a thing, person, work, place) acha

leave

~ your books here acha vitabu vyako hapa ~ a guest at home acha mgeni nyumbani she expects to ~ the job anatarajia kuacha kazi when did you ~ school? ulimaliza shule lini? be/get nicely left (colloq) danganywa; telekezwa. ~ somebody/something behind sahau, acha don't ~ me behind usiniache. ~ somebody/something alone -tosumbua, -toingilia, -togusa. ~ well alone (prov) usitie ufundi kwenye kitu kizuri, acha mambo yalivyo. ~ off acha; koma, isha, hulu where did we ~ off? tulikomea/tuliachia wapi when did you ~ off your spectacles? lini umeacha kuvaa miwani yako? ~ something/somebody out ruka, acha (kumshughulikia). ~ something over ahirisha, acha (kwa muda). ~ it at that achia hapo, acha kusema/ kufanya zaidi. ~ somebody to himself/to his own devices acha huru. ~ something unsaid acha kusema jambo. ~ much/a lot/ something/to be desired -toridhisha. ~ nothing to be desired ridhisha. ~ go/hold (of something) achilia. 3 baki, bakisha ~ some money for clothes bakisha kiasi cha fedha kwa ajili ya nguo eight from ten ~s two kumi ukitoa nane hubaki mbili. to be left until called for ikae/iachwe hadi mwenyewe aje kuchukua. 4 -pa, achia; kabidhi. ~ word (with somebody) (for somebody) -pa/ achia maagizo n.k. ~ the matter to somebody achia mtu shauri alishughulikie ~ a teacher on duty in charge of the school achia/kabidhi madaraka ya shule kwa mwalimu wa zamu. 5 ~ something (to somebody); ~ somebody something (at the time of one's death) rithisha, acha/achia (mali, madeni, mjane, watoto n.k.). 6 (of directions) pita ~ the post office on your right pita posta upande wa kulia. n 1 ruhusa, idhini. ~ of

leaven

absence likizo/ruhusa (ya kutokuwepo) ~ to appeal ruhusa ya kukata rufaa. by/with your ~ kwa ruhusa yako, kumradhi. 2 likizo, livu emergency ~ likizo ya dharura sick ~ likizo ya ugonjwa. take French ~ toroka, enda likizo bila ruhusa. on ~ likizoni. 3 kuondoka. take (one's) ~ (of somebody) aga, agana na. ~ taking n kuaga/kuagana. take ~ of one's senses fanya kama mwenda wazimu; pata wazimu. leavings n (pl) mabaki, masalio, masazo, makombo.

leaven n 1 chachu, hamira. 2 (fig) athari, kichocheo. vt 1 chachua, tia hamira. 2 athiri, geuza.

lecher n fisadi; fasiki, mzinzi, mkware (wa kiume). ~ous adj -zinifu, kware, asherati. ~y n ukware, uzinzi, uasherati.

lectern n marufaa: meza ya kusomea kitabu (agh. kanisani au darasani).

lecture n 1 mhadhara deliver a ~ toamhadhara; makaripio. 2 hotuba ya kuonya. vt,vi 1 ~ (on) toa mhadhara. 2 ~ somebody (for) kemea/onya (kwa hotuba ndefu); hubiri. ~r n mhadhiri. ~ship n uhadhiri.

led pt, pp of lead2

ledge n 1 kishubaka, shubaka, kibao (kitokezacho ukutani). 2 (of rock) mwamba chini ya maji (hasa karibu ya ufukwe).

ledger n 1 leja: daftari kubwa ya hesabu. 2 ~/legerline n (music) mstari mfupi chini au juu ya mistari mitano ya noti.

lee n mahali pasipoelekea upepo. ~ (side) n demani under the ~ of a house upande wa nyumba usioelekea upepo. ~ward adj -a demani. ~way n 1 mwendo wa chombo kikichukuliwa upande wa demani. 2 (fig) uhuru wa kuwa na fikra/ matendo tofauti make up ~-way fidia muda, rudia mahali.

leech n 1 ruba stick like a ~ (fig) ganda. 2 mnyonyaji. 3 (old use)

leg

daktari.

leek n liki: mmea kama kitunguu (wenye tumba jeupe).

leer n jicho/tabasamu la husuda/ufisadi. vi ~(at somebody) tazama kwa jicho la husuda/ufisadi.

lees n masira, masimbi. drink/drain to the ~ (fig) pata matatizo/mateso makubwa, teseka kupita kiasi.

left1 pt,pp of leave. ~overs n masazo, makombo; kiporo.

left2 adj, n, adv kushoto; -a kushoto ~side upande wa kushoto turn ~geuka kushoto. the ~ (wing) n wanasiasa wa mrengo wa kushoto (wapendao mabadiliko ya kijamaa). ~hand adj -a kushoto. ~handed adj (of a person) -enye kutumia mkono wa kushoto. a ~ handed compliment n wasifu tata; wasifu wenye mashaka. ~ist n mwanasiasa wa mrengo wa kushoto.

leg n 1 (of animal, person, garment, chair, table, stool etc.) mguu. be all ~s (of a person) -wa -lonjo, njorinjori. be off one' s ~ pumzika. be on one's ~s (or joc on one's hind ~s) simama (ili kuzungumza/ kuhutubia); (after an illness) -wa mzima, pona. be on one's last ~s choka, -wa na mavune, -wa hoi; chungulia kaburi, karibia kufa. feel/find one's ~s (of a baby) anza kusimama/kutembea; (fig) tambua uwezo/kipaji, vipaji n.k,; jiamini. give somebody a ~ up saidia mtu wakati wa shida. pull somebody's ~ tania. ~ pull; ~ pulling n utani. run somebody off his ~s chosha (mtu) kwa kazi shake a ~ (colloq) cheza dansi; (imper) fanya haraka; anza show a ~ (colloq) amka kitandani; (imper) ongeza bidii not have a ~ to stand on shindwa kujitetea stretch one's ~s nyoosha miguu (kwa matembezi), punga hewa take to one's ~s kimbia walk one's ~s off; walk somebody off his ~s chosha mtu kwa kutembea. 2 (support of a bed) tendegu be on its

legacy

last ~s karibia kwisha. 3 sehemu ya safari; sehemu moja ya mfululizo wa mashindano ya michezo. ~ged adj (in compounds) long ~ged enye miguu ya milonjo, njorinjori two ~ged -enye miguu miwili three ~ gedrace mbio za miguu mitatu (kufungana miguu). three ~ged stool n kigoda. ~ging n (usu pl) soksi ndefu za ngozi/nguo. ~gy adj -lonjo, njorinjori.

legacy n 1 urithi; hiba leave a ~ to rithisha, achia urithi; (for religious purposes) wakifia. 2 (fig) kitu kinachorithishwa na mababu au waliotangulia, urithi.

legal adj halali; -a haki; -a kisheria. ~advice n ushauri wa kisheria. ~ adviser n mshauri wa kisheria. ~ aid n msaada wa kisheria. ~ capacity n uwezo wa kisheria. ~ practitioner n mwanasheria ~ profession jamii ya wanasheria, uwakili ~ tender fedha halali kwa malipo. ~ly adv. ~ism n ushikiliaji mno wa sheria. ~ity n uhalali; haki. ~ize vt halalisha. ~ization n uhalalisho.

legate n balozi (wa Papa). legation n ubalozi mdogo.

legatee n (leg) mrithi.

legend n 1 ngano, hekaya. 2 ngano na hekaya hizi kwa jumla. 3 maandishi katika sarafu/medali/ramani n.k.. ~ary adj -a hadithi za kale.

leger see ledger (2)

legerdemain n 1 kiinimacho, mizungu, miujiza. 2 (fig) hoja za uongo.

leghorn n 1 kuku wa Mediterania. 2 kofia ya majani makavu.

legible adj (of handwriting, print) -a

kusomeka, dhahiri. legibly adv. legibility n.

legion n 1 kikosi cha askari 3,000-6,000 wa Kirumi. 2 British L~ n Chama cha askari wa Kiingereza waliotoka vitani 1921. Foreign ~ n (French) askari wa kigeni wanaopigana vita katika nchi ya kigeni. the L~ of Honour n

lend

nishani ya Wafaransa. 3 (Lit or rhet) wingi, jeshi. ~ary adj, n 1 askari wa Kirumi. 2 askari wa kigeni katika jeshi la Ufaransa adj -a askari wa Kirumi; -a askari wa kigeni wa jeshi la Ufaransa.

legislate vt tunga sheria. legislation n utungaji sheria; sheria zilizotungwa. legislative adj -a kutunga sheria. legislative assembly n baraza la kutunga sheria. legislative draftsman n msawidi sheria. legislator n mbunge. legislature n baraza la kutunga sheria, bunge.

legitimate adj 1 -halali, -a ndoa ~

son/daughter mtoto wa ndoa/halali. 2 -a maana ~ purpose kusudi la maana. 3 halisi the ~ theatre tamthilia halisi. 4 halali. ~ly adv. legitimacy n. legitimatize vt halalisha.

legume n jamii kunde. leguminous adj -a jamii kunde.

leisure n 1 wasaa/nafasi/wakati (wa mapumziko). at ~ bila kazi at your ~ kwa nafasi yako. 2 (attrib) wakati wa mapumziko ~ time/hours muda/saa za mapumziko. ~ly adv taratibu, polepole work ~ly fanya kazi polepole. ~d adj -enye wasaa/nafasi the ~d classes matabaka tajiri.

leitmotif/leitmotiv n dhamira kuu (yenye kujirudia); dhamira, ishara (inayoashiria wazo/mtu).

lemon n 1 limau. 2 mlimau. 3 rangi ya limau. 4 bwege. ~ drop n bonge la sukari iliyochemshwa na kutiwa limau. ~ squash n kinywaji cha limau. ~ squezer n chombo cha kukamulia limau. ~ sole n aina ya samaki mpana. 4 (GB) (sl) mtu mjinga na asiyevutia. ~ade n maji ya limau (yaliyotiwa sukari na maji).

lemur n komba wa bukini.

lend vt 1 azima; (of money) kopesha. ~ a hand (with something) saidia, auni ~ an ear sikiliza. ~ing-library n maktaba ya kuazimisha (vitabu). ~ something

length

to somebody; ~ somebody something azima/azimisha. 2 ~ something to something changia, ongeza his ideas lent expertise to the discussion mawazo yake yalichangia utaalamu kwenye mjadala his actions ~ credence to his good reputation matendo yake yanaonyesha ukweli wa sifa yake. 3 ~ oneself to something kubali, -faa it ~s itself to inafaa kwa. ~er n.

length n 1 urefu be 5 miles in ~ -wa na urefu wa maili tano; (period of time) muda wa the ~ of our stay was two days tulikaa kwa muda wa siku mbili. at ~ mwishowe; hatimaye; kwa muda mrefu; kwa undani. (at) full ~ lala kwa kujinyoosha. keep somebody at arms ~ kataa urafiki na mtu, epa. 2 kadiri, kiasi. go to any ~ (s) fanya kila linalowezekana (kupata utakacho). 3 kipande cha (nguo, bomba n.k. kinachotosha shughuli fulani) I need a ~ of dress material ninahitaji kipande cha kitambaa cha gauni. 4 kipimo cha kitu mwanzo hadi mwisho; urefu. ~en vt,vi refusha. ~ways; ~wise adv, adj kwa urefu. ~y adj -refu mno.

lenient adj -pole; -enye huruma. lenience/leniency n. ~ly adv. lenity n (formal) huruma, upole.

lens n lenzi, kioo (cha miwani, darubini n.k.) concave ~ lenzi mbonyeo; convex ~ lenzi mbinuko.

lent pp of lend.

Lent n kwaresima ~en adj -a kwaresima with a ~ en face -enye uso wa huzuni.

lentil n dengu; adesi.

lento adj, adv (music) polepole. Leo n Simba: alama ya Zodiaki. ~nine adj -a kama simba.

leopard n chui. ~ess n chui jike.

leper n mkoma, (fig) mtu anayeepukwa na wengi kwa ajili ya ufidhuli wake.

leprosy n ukoma. leprous adj.

leprechaun n (Irish) zimwi mwema.

lesbian n msagaji adj -enye kusaga

lest

~ism n.

lese-majesty n 1 uhaini. 2 (joc) ujeuri.

lesion n donda, jeraha.

less adj 1 (for what is measured by size, degree, duration, number etc) -dogo zaidi, -dogo there is ~ money these days siku hizi fedha ni ndogo no ~ a person than the President came Rais ndiye aliyefika hasa adv kidogo (zaidi) he drinks ~ these days amepunguza kunywa. any the ~ bado ... ingawa I don't think any the ~ of her for failing her exam bado ninamwamini ingawa ameshindwa mtihani wake. even/still ~ sembuse/seuze I don't believe he stole the money still ~ the car siamini kuwa aliiba pesa sembuse gari. no ~ than si chini ya she bought no ~ than 6 pairs of khangas alinunua siyo chini ya jozi sita za khanga. none the ~ hata hivyo, walakini I know he's cunning none the ~ he's very charming najua ni mjanja hata hivyo ni mchangamfu n kidogo the ~ the better kikiwa kidogo ni bora zaidi in ~ than an hour -siozidi saa moja; prep kasoro, kosa, toa a month ~ two days mwezi kasoro siku mbili; 500/= ~ 50/= tax Shilingi 500/= kasoro Shilingi 50/= za kodi. ~en vt,vi punguza; punguka; fanya -dogo. ~er adj -dogo zaidi, -lio -dogo to a ~er degree kwa kiasi/kadiri ndogo zaidi.

lessee n (leg) mpangaji. lessor n mpangishaji.

lesson n 1 somo. 2 (portion of Bible) somo, sura. 3 onyo; fundisho let that be a ~ to you naliwe fundisho kwako teach him a ~ mrudi, mwadhibu asifanye tena.

lest conj 1 ili...si; sijekuwa (kwa hofu) take heed ~ he falls tahadhari asije akaanguka I hurried ~ I be late niliharakisha ili nisichelewe. 2 (after fear) kuwa we were afraid ~ he should get here too late tulihofu kuwa atachelewa.

let

let1 vt,vi 1 ruhusu, toa ruhusa, acha her father ~ her go to the film with us baba yake alimruhusu aende sinema nasi ~ me know niarifu. 2 (imper use) ~ 's go twende ~ them all come na waje wote ~ me see hebu nione ~ the water boil acha maji yachemke. 3 (hire) pangisha, kodisha she ~s rooms in her house anapangisha vyumba nyumbani mwake he ~s his car anakodisha gari lake. 4 (with adj/n/v/prep). ~ alone licha ya, sembuse. ~ somebody alone mwache, usimsumbue ~ him alone now usimsumbue sasa. ~ be acha ~ him be mwache. ~ drive at lenga, tupa (kupiga). ~ blood toa damu. blood-~ting n kutoa damu. ~ down angusha; (clothes) refusha you'll have to ~ the hem down itakubidi kurefusha gauni lako. ~ somebody down sikitisha you ~ me down by not finishing the work umenisikitisha kwa kutotekeleza kazi yako. ~-down n sikitiko ~ drive/fly piga kwa nguvu. ~ drop/fall angusha (fig) toa siri (kwa makusudi au kwa bahati tu). ~ go acha, achia huru, fungulia ~ pass samehe, fumbia macho the judge ~ the prisoner go hakimu alimwachilia mfungwa ~ oneself go acha kujizuia; jiachia. ~ in ruhusu kuingia; fungua; fumbulia he ~ Maria in on the secret alimfumbulia Maria siri. ~ oneself (somebody) in for jiingiza/jitia bila kujua (katika taabu, shughuli n.k.). ~ into ingiza, ruhusu kuingia he ~ the children into the room aliwaruhusu watoto waingie chumbani the window ~s good air into the room dirisha linaingiza upepo mzuri chumbani. ~ loose acha huru, fungulia he ~ the goat loose alifungulia mbuzi; (fig) ondoa, acha, onyesha he ~ loose his anger at us alituonyesha hasira yake. ~ off piga, fyatua (bunduki n.k.); samehe (fulani) I'll ~ you off this time but don't do it again sasa ninakusamehe lakini

letter

usirudie tena. ~ on (colloq) toa (siri) he didn't ~ on that he knew anything hakuonyesha kuwa anajua mambo yoyote. ~ out toa, ondoa she ~ the water out of the sink aliachia maji kutoka kwenye beseni; (clothes) ongeza upana because she put on weight she had to ~ out her clothes kwa sababu alinenepa ilimbidi aongeze upana wa mavazi yake. ~ something pass puuza; -totia maanani. ~ through ruhusu kupita, pisha please ~ me through nipishe. ~ up pungua ukali, punguza jitihada the rain ~up after an hour baada ya saa moja mvua imepungua he never ~ up working hard hapunguzi jitihada yake kazini. ~-up n (colloq) pungufu, kikomo it was raining all day without ~-up mvua ilinyesha siku nzima bila kikomo.

let2 n kupangisha, kukodisha this room is a good ~ chumba hiki ni kizuri kupanga/kupangisha. ~ting n chumba/nyumba ya kupangisha.

let3 vt (archaic) zuia. n kizuio; mgogoro; pingamizi.

lethal adj -a (kusababisha) mauti, -a kuua.

lethargy n uchovu, kukosa nguvu, uzito. lethargic adj -zito, -enye usingizi. lethargically adv.

lethe n (Gr) mto wa jehanamu unaosababisha kusahau yaliyopita.

letter n 1 (of alphabet) herufi. 2 barua, waraka. ~-bomb n bomu la barua. ~-box n (US mailbox) sanduku la posta. ~-case n mkoba wa barua. ~head n karatasi yenye anwani. ~-paper n karatasi za barua. ~-perfect adj -enye kujua kwa moyo. ~-press n maandiko (katika kitabu cha picha). 3 (phrases) keep (to) the ~of an agreement fuata sheria/makubaliano neno kwa neno bila kuzingatia maana. to the ~ kwa makini, kabisa. 4 (pl) elimu, fasihi a man of ~s mwandishi; msomi the profession of ~s

lettuce

uandishi. ~ed adj -enye elimu. vt chapa herufi; pamba na herufi za alfabeti. ~ing n maneno; uandikaji wa herufi.

lettuce n saladi.

leucocyte (US leukocyte) n selidamu nyeupe.

leukaemia (US) leukemia n lukemia: ugonjwa wa damu.

levant vi toroka (hasa pasi kulipa gharama au madeni fulani).

levee n (US) boma la kuzuia maji, ukingo wa udongo/kitope.

level n 1 usawa on a ~ with sawa na (cheo, daraja, ardhi n.k.) on different ~s usawa usiolingana, mbalimbali be on the ~ -wa sawa; (fig) sema ukweli; (flat area) mahali pa sawa find one's ~ fikia kiwango chako sawa. 2 pimamaji. 3 kiwango rise to higher ~s fikia viwango vya juu zaidi; ngazi top ~ officials maafisa wa ngazi ya juu. 4 on the ~ (colloq) kweli, wazi adj 1 sawa (bila kuinuka) a ~ crossing tambuka reli; njia panda ya reli na barabara, chekereni; makutano. 2 usawa ~ race mbio za kukaribiana. 3 have a ~ head -wa tulivu, bila papara. ~ headed adj tulivu. do one's ~ best fanya vizuri uwezavyo. vt,vi 1 sawazisha. ~ something down/up linganisha/ sawazisha vitu. 2 bomoa (nyumba, ukuta n.k.), angusha; shusha ~ to the ground bomoa kabisa. 3 (aim) elekeza, lenga ~ a gun at lenga shabaha. 4 ~ off (airplane) fanya ndege iwe sambamba na ardhi; (fig) fikia kiwango (ambapo hutegemei kupanda zaidi). ~ler n msawazishi: mtu ambaye anataka kuondoa tofauti zote za jamii.

lever n wenzo. vt inulia (vitu vizito). ~age n nguvu ya wenzo (fig) n nguvu, uwezo wa kushawishi.

leveret n mtoto wa sungura, kititi.

leviathan n 1 (in the Bible) lewiathani, mamba. 2 kitu chochote kikubwa mno; dubwana.

levitate vt,vi anga; angama; elea.

liar

levitation n.

levity n 1 purukushani. 2 utovu wa staha.

levy vt,vi 1 ~ (on) toza. 2 (of soldiers) andikisha kwa lazima. ~ war upon/ against anzisha vita. 3 ~ on twaa/ kamata kisheria. n 1 ada, kodi. 2 pl makundi ya wanajeshi development ~ kodi ya maendeleo.

lewd adj -pujufu, fisadi; asherati, -zinifu. ~ness n. ~ly adv.

lexicon n 1 msamiati, maneno. 2 kamusi. lexical adj -a msamiati/maneno. lexically adv. lexis n msamiati. lexicographer n mwana leksikografia. lexicography n leksikografia; usawidi kamusi. lexicology n (ling.) elimu msamiati, leksikolojia: sayansi ya maana na matumizi ya maneno.

liable adj 1 ~ for -a kuwajibika kisheria John is ~ for his son's debts John anawajibika kisheria kulipa madeni ya mwanae. 2 -a kupaswa, -a kustahili. be ~ to something paswa, stahili tax evaders are ~ to heavy penalty wanaokwepa kodi wanastahili adhabu kali. 3 -a kuelekea, -enye kuwezekana. be ~ to do something -wa na uwezekano wa kufanya jambo he is ~ to get a loan anaelekea atapata mkopo. liability n 1 dhima. limited liability n dhima ya ukomo. limited liability company n kampuni ya dhima zenye ukomo. public unlimited liability n dhima isiyo ukomo. 2 wajibu, kupaswa ~ to military service wajibika kujiunga na jeshi. 3 (pl) liabilities n madeni; kuwiwa. 4 (colloq) kikwazo.

liaise vi ~ (with/between) (colloq) -wa kiungo kati ya kikundi kimoja na kingine; wakilisha, shirikiana, husiana. liaison n 1 ushirikiano, uhusiano; kiungo. ~ officer n afisa ushirikiano. 2 kufanya mapenzi yasiyo halali.

liana n mtambaa.

liar n mwongo.

lib

lib n (colloq abbr for liberation)

ukombozi women's ~ ukombozi wa wanawake.

libation n tambiko/sadaka ya kinywaji (mvinyo, maziwa n.k.).

libel n 1 (kuchapisha) maandishi ya kukashifu; maandishi yenye kutweza hadhi ya mtu criminal ~ kashifa za kijinai. 2 ~ on (colloq) dhalala, kashfa. vt kashifu (kwa maandishi), singizia vibaya/bure. ~ler n. ~lous;(US) ~ ous adj.

liberty n 1 uhuru; haki/uwezo wa kujiamulia la kufanya people defended their ~ watu walilinda uhuru wao. at ~ (of a person) huru we are at ~ to stay with them tuko huru kuishi nao. set somebody at ~ achia mtu, pa mtu uhuru, toa mtu utumwani. ~ of conscience uhuru wa kuamini agh. dini. ~ of speech uhuru wa kusema (fikra za mtu) hadharani. ~ of the press uhuru wa kuandika na kuchapisha (majarida, vitabu n.k.) bila kuingiliwa. 2 kutenda jambo bila ruhusa ya mwenyewe; kutenda yasiyo haki. take the ~ of doing something jiamulia he took the ~ of using my car while I was away alijiamulia kutumia gari langu pasi na ruhusa yangu nilipokuwa sipo. take liberties with somebody zoeana na mtu kupita kiasi. 3 (pl) fadhila au haki zilizotolewa na mamlaka fulani the liberties given by Scopo haki zilizotolewa na Scopo. libertarian n mpigania uhuru wa mawazo, dini;

uhuru wa kufikiri na kutenda.

liberal adj 1 -karimu, -paji; -ema she is ~ with her money yu mkarimu na fedha zake. 2 -enye mawazo mapana na huru; -siokuwa na upendeleo. 3 (of education) -a elimu (ya kupanua mawazo). the ~ arts n masomo ya sanaa na sayansi za jamii k.m. historia, lugha n.k. 4 (politics in GB) -a chama (cha Liberal) chenye kupendelea mabadiliko ya wastani. n mpenda maendeleo na mabadiliko. n

licence

mwanachama wa chama hicho. ~ism (views/ideas/principles) n msimamo, fikra za kupenda mabadiliko. ~ize vt panua, legeza masharti (ya biashara n.k.). ~ization n. ~ity n ukarimu, upaji, ufadhili, kutobagua, kutopendelea his ~ities have made him poor ukarimu wake umemfilisi.

liberate vt ~ from komboa, fanya huru. liberation n ukombozi liberation committee kamati ya ukombozi.

libertine n mwasherati, mkware chartered ~ mkware anayevumiliwa na jamii.

libido n (psych) ashiki, nyege.

libidinous adj -a ashiki.

Libra n Mizani: alama ya Zodiaki.

library n 1 maktaba a walking ~ (fig) mjuzi. mobile ~ n maktaba inayosafiri public ~ maktaba ya umma reference ~ maktaba ya marejeo. 2 (attrib) -a maktaba ~ edition toleo la kitabu kikubwa na chenye jalada gumu. 3 chumba cha kuandikia na kusomea katika nyumba binafsi. 4 mfulululizo wa vitabu vya aina na jalada la namna moja vilivyotolewa na mchapishaji mmoja. librarian n mkutubi: mwangalizi wa maktaba librarianship n ukutubi.

libretto n kitabu cha maneno ya opera. lice n pl of louse.

licence; (US license) n 1 (permission) ruhusa, hati; leseni driving ~ leseni ya kuendesha gari teaching ~ hati ya kufundishia. on ~ n (GB) leseni ya kuuza vileo katika baa. off ~ n (GB) leseni ya kuuza vileo katika stoo (bila ruhusa ya kunywa hapo hapo), duka lenye vileo. 2 kupuuza sheria/kanuni/mila n.k.; ufisadi, kuutumia vibaya uhuru. poetic ~ n uhuru wa kishairi (wa kukiuka kanuni za kawaida za lugha). license (also ~). vt pa leseni shops ~d to sell alcohol maduka yenye leseni ya kuuza vileo ~ the hawker to sell

lichen

clothes -pa mchuuzi leseni ya kuuza nguo. ~e n mtu mwenye leseni (hasa ya vileo). ~er n mtoa leseni. licentiate n mtaalam mwenye leseni/ cheti cha kazi yake. licentious adj -asherati; fisadi; -kware. licentiously adv. licentiousness n.

lichen n kuvu, ukungu (wa miti na miamba).

lich-gate/lychgate n lango la kupitishia maiti kanisani.

licit adj halali, -a sheria, -nayo kubalika kisheria.

lick vt 1 ramba. ~ a person's boots ramba miguu, jipendekeza sana. ~ one's lips jiramba kwa uchu. ~ one's wounds jipa nguvu baada ya kushindwa. ~ something off/ ~something up ramba. ~ into shape (fig) funza/tengeneza barabara. ~ the dust (rhet) anguka chini, shindwa kabisa; -fa. 2 (esp waves/flames) gusa gusa, pitia the waves ~ed the banks of the river mawimbi yalipita katika kingo za mto. 3 (colloq) shinda, piga sana, twanga. ~ an opponent shinda mpinzani wako. 4 (sl) piga mbio, enda mbio as hard as one can ~ upesi sana. n 1 kuramba. a ~ and a promise (colloq) kunawanawa/ kusafisha/kuogaoga. 2 (also salt ~) mahali mifugo inapopatia magadi/chumvi. 3 (sl) at a great ~; at full ~ mwendo mkubwa; kwa kasi sana. ~ing n (colloq) kurambisha; kipigo; ushinde Pan African FC got a ~ing last night timu ya Pan African ilipata kipigo/ilirambishwa mchanga.

licorice n see liquorice

lid n 1 kifuniko tea pot ~ kifuniko cha birika. 2 eye ~ ukope wa jicho. ~less adj.

lie1 vi danganya, sema uwongo she is lying anadanganya. n uwongo tell a ~sema uwongo. give somebody the ~ shitaki mtu kwa kudanganya. ~ detector n kijaluba cha kupimia mabadiliko kifiziolojia (k.m. mapigo ya moyo, kupumua hasa wakati mtu

lie

anapohojiwa); kibaini uongo.

lie2 vi 1 lala, jinyoosha juu ya kitanda, ardhi n.k. ~ on one's back lala chali ~ back jinyoosha ~ face downwards lala kifudifudi her body ~s at the cemetery amezikwa makaburini. take something lying down kubali kutukanwa pasi na ubishi. ~ down under (an insult) kubali bila kupinga. ~ in kawia kuamka (kutoka kitandani); -wa katika uchungu kitandani (ili kuzaa mtoto). lying -in hospital (old use) hospitali ya uzazi. ~ up lala kitandani au chumbani kwa ugonjwa. ~ with (old use biblical, now usu sleep with) jamiiana. let sleeping dogs ~ (prov) usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe. ~-a bed n mvivu, asiyetaka kuamka kitandani. 2 (of things) -wa juu ya the coat lay on the floor the whole night koti lilikuwa juu ya sakafu usiku kucha. 3 (of abstract things) -wa, -wa katika hali fulani I know where his interest ~s nafahamu mambo anayoyapendelea the car's trouble ~s in the gear box tatizo la gari limo ndani ya gia boksi. ~ at somebody's door husika, laumika at whose door should the defeat ~? nani alaumiwe kwa kushindwa kwetu? ~ with somebody wajibika it ~s with you to appoint your deputy unawajibika kumteua naibu wako. as far as in me ~s kwa kadri ya uwezo wangu. 4 -wa mahali. ~ to (of a ship) karibia kusimama, kabili upepo. 5 kaa, baki the youth are lying around idle in town vijana wanakaa bure mjini the soldier lay in the cell for one more night askari alikaa rumande kwa usiku mmoja zaidi. ~ heavy on something lemea, dhuru. ~ over ahirishwa kwa jambo. 6 enea, zagaa, tanda the game lay before us wanyama walizagaa kila mahali mbele yetu. find out/see how the land ~s (fig) jifunze, chunguza,

lied

dadisi jinsi hali ya mambo ilivyo. 7 (legal) kubalika his appeal will not ~in the court of law rufaa yake haitakubaliwa na mahakama. n (sing only) mkao/mlalo wa kitu. the ~ of the land jinsi sura ya nchi ilivyo (fig) hali ya mambo.

lied n (G) wimbo/shairi la Kijerumani. ~er-singer n mwimbaji wa nyimbo hizo.

liege adj (leg) (only in) ~ lord/ sovereign n (feudal times) mtawala, mwinyi. ~ man n (pl) watwana wa mwinyi.

lien n dai la kumiliki (mpaka deni limelipwa).

lieu n (only in) in ~ (of) badala ya.

lieutenant n 1 luteni. 2 (in compounds) second ~ luteni usu ~colonel luteni kanali ~ general luteni jenerali ~ commander luteni kamanda. 3 naibu, mbadala, wakili. Lord L~ n (of the Country) Mwakilishi wa Malkia. lieutenancy n uluteni.

life n 1 uhai. ~ force n nishati uhai. 2 viumbe/vitu hai (watu, wanyama na mimea). 3 maisha. a matter of ~ and death struggle mapambano ya kufa na kupona ~ insurance bima ya maisha. bring to ~ huisha. come to ~ pata fahamu baada ya kuzimia; changamka. run for ones ~/for dear ~ kimbia ili kujiokoa/kunusuru maisha. this ~ maisha ya hapa duniani. the other ~; future/ eternal/everlasting ~ n maisha ya peponi; ahera. with all the pleasure in ~ kwa raha mustarehe. 4 take somebody's ~ ua mtu. take one's own ~ jiua, jinyonga. a ~ for a ~ mtu kwa mtu, kulipiza kisasi. can not for the ~ of one haiwezekani hata kama mtu akijitahidi kiasi gani. not on your ~! (colloq) la hasha! thubutu. 5 kipindi katika maisha (k.m. kuzaliwa hadi kufa) he lived here all his ~ aliishi hapa maisha yake yote the ~ of the government maisha ya serikali ilipokuwa inafanya

life

kazi he was given a ~ sentence alipata kifungo cha maisha. ~ annuity n fedha alipwazo mtu mpaka atakapokufa for ~ kabisa, kwa maisha. ~ cycle n hatua anuwai za maisha kamili ya kiumbe (k.m. mbu kuanzia yai, kiluwiluwi, pupa hadi mdudu kamili). ~ interest n (legal) mapato (kutokana na mali fulani) apewayo mtu wakati wa uhai wake tu. ~ peer n mjumbe wa baraza la malodi (Uingereza) ambaye cheo chake hakirithiki. have the time of one's ~ (colloq) jistarehesha sana. early/late in ~ mapema, mwanzoni/mwishoni mwa maisha. 6 uhusiano, uchangamfu, starehe there is little ~ in the villages vijijini hakuna shughuli nyingi/hapakuchangamka; maisha yamedorora vijijini the children are full of ~ watoto wamechangamka/ wana raha. true to ~ (of a story, drama etc.) -enye kutoa picha halisi ya maisha; (of interest/way of living) -a kupendeza, -a kuvutia put more ~ in your work fanya kazi yako ivutie, changamkia kazi zaidi. the ~ (and soul) of the party mtu aliye mchangamfu sana katika kikundi. 7 wasifu a ~ story of Julius Nyerere wasifu wa Julius Nyerere. 8 mfano/ kielezo chenye uhai a ~ drawing picha iliyochorwa kwa kutumia mfano wa kiumbe hai, vitu hai. to the ~ kwa usahihi. as large as ~ -enye ukubwa wa kawaida (colloq and in joke) -enyewe, binafsi; kwa uhakika; pasipo shaka yoyote. 9 maisha baada ya kunusurika. 10 (compounds) ~belt n mkanda wa kujiokolea. ~-blood n kiini; damu muhimu kwa uhai; (fig) jambo lenye athari kubwa; kitu kinachotia nguvu. ~-boat n mashuaokozi (ya kuokolea watu au inayochukuliwa melini). ~buoy n boyaokozi (chelezo cha kuopolea/kuokolea watu katika hatari ya majini). ~ estate n milki ya maisha (ambayo mtu hutumia hadi

lift

anapokufa na hairithishwi). ~ expectancy n miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi. ~-giving adj -a kuhuisha. ~-guards n walinzi, waokozi katika sehemu za kuogelea. L~ Guards n (pl) kikosi cha farasi katika jeshi la Kiingereza. ~ history n (biol) kumbukumbu ya maisha kamili ya kiumbe. ~ insurance/ assurance n bima ya maisha. ~-jacket n jaketi/koti okozi. ~like adj -enye kufanana na kiumbe chenye uhai; -enye kufanana na kiwakilishwa. ~line n 1 kambaokozi: kamba ya kuokolea maisha (ambayo hufungwa kwenye boya au meli); kamba ya wapiga mbizi; (fig) tegemeo kuu; kitu kinachotegemewa kwa uhai wa mtu. ~long adj -a maisha, -a maishani. ~-office n ofisi ya bima ya maisha. ~-preserver n (US) ~ jacket n (GB) rungu la kujilinda. ~-saver n (colloq) kitu/mtu amsaidiaye mwenzake katika matatizo (esp in Australia); mwogeleaji aokoaye watu waliozama. ~-sentence n adhabu ya kifungo cha maisha. ~-size(d) adj (picha) -enye ukubwa sawa na kitu chenyewe. ~-span n (biol) maisha ya kiumbe/kitu. ~-support system n vifaa kwenye chombo cha anga/ hospitali ambavyo humsaidia mtu kuishi. ~time n maisha. the chance of a ~ time bahati inayotokea mara moja katika maisha. in somebody's ~ time katika maisha ya mtu. ~-work n kazi ya kudumu, kazi yenye kumshughulisha mtu maisha yake yote. ~less adj -fu, -liokufa; -siokuwa na uhai; -enye kuchusha, -siovutia. ~lessly adv. ~r n (sl) mtu aishiye kwa namna fulani (sl) mfungwa wa maisha.

lift vt,vi 1 inua, pandisha, nyanyua, kweza. ~ up one's eyes (to) angalia, tazama (juu). ~ up one's voice paaza sauti. 2 ~ off (of a space craft) tweka; ruka, ondoka. 3 (of clouds, fog) panda, potea the fog

light

began to ~ ukungu ulianza kutoweka. 4 chimbua; (root crops) ng'oa. 5 iba, sogeza. 6 ondoa (agh kizuizi, upigaji marufuku). n 1 kuinua; msaada. give somebody a ~-pa mtu lifti/msaada, beba; (of a person's spirits) fariji, changamsha. 2 (US elevator) lifti ~-and-force pump pampu la kuvuta na kusukuma. ~-attendant/boy/man n opereta wa lifti.

ligament n kano.

ligature n 1 uzi, bendeji itumikayo kufunga mishipa n.k. 2 (printing) herufi zilizounganishwa f na l kuwa fl.

light1 adj 1 (of colour) -siokoza, -sioiva angazi, -a ~ brown kahawia isioiva, hafifu. 2 (of a place) -enye mwanga.~ coloured adj -enye rangi isiyoiva. n 1 nuru, mwanga the ~ begins to fail mwanga unaanza kufifia day ~ mchana. in a good/bad ~ (of picture etc) -a kuonekana vizuri/vibaya; (fig) eleweka vizuri/vibaya. see the ~ (liter or rhet) zaliwa; baini; tangazwa; tambua; -okoka. be/stand in one's ~ kinga nuru; (fig) zuia mtu mafanikio/maendeleo yake. stand in one's own ~ zuia kazi yako isionekane; fanya kinyume na matakwa yako. ~ year n (astron) kipimo cha umbali kati ya nyota. 2 taa. ~s out muda wa kuzima taa. the northern/southern ~s n miali ya mwanga katika ncha za kaskazini na kusini. 3 mwako wa moto; kiberiti strike a ~ washa moto; washa kiberiti. 4 uchangamfu (usoni mwa mtu). the ~ of somebody's countenance (biblical) kupendezwa kwake. 5 ufafanuzi; uvumbuzi unaobainisha, kuelewa. come/bring something to ~ funua, funuka, (ji)tokeza, bainisha. shed/throw (a) new ~ on something fafanua zaidi, toa habari/taarifa mpya. in the ~ of kutokana na, kwa kuzingatia by the ~ of nature kwa akili za asili. 6

light

jinsi (ya utendaji); hali I have never looked upon the matter in that ~ sijawahi kuchukulia jambo hili katika mtazamo huu. 7 uwezo, kipaji. according to one's ~s kufuatana/ kulingana na kipaji chake. 8 mtu maarufu, mashuhuri, mtu anayechukuliwa/tolewa kama mfano. 9 dirisha, sehemu ya kupitishia mwanga. 10 (paintings) uangavu, sehemu ya mwanga (ya picha). 11 (compounds) ~house n mnara wa taa wa kuongozea meli. ~ship n meli yenye taa za kuongozea meli nyingine. vt,vi 1 washa. 2 toa mwanga, mulika. 3 ~ up washa, mulika ~ing-up time muda wa kuwasha taa za barabarani pamoja na magari; (colloq) anza kuvuta/washa (sigara au kiko). 4 furahia mno. ~ up (with) (of a person's face or expression) -wa angavu. 5 ongoza; ongozwa kwa mwanga wa kitu. 6 ~ something up fanya iwe na mwanga. ~er n 1 kiberiti cha chuma/plastiki. 2 mtu/kitu kihusikacho na kuwasha taa. ~en vt,vi 1 ng'arisha; mulika. 2 -wa angavu. 3 toa mwale wa radi; metameta.

light2adj 1 (in weight) -epesi, rahisi, sahala. ~horse/~-armed adj askari wenye silaha nyepesi. 2 polepole; -a makini, -tulivu, -angalifu walk with ~ footsteps nyemelea; nyata. ~-handed adj. -a mkono mwepesi. ~ handedly adv ~-fingered adj -epesi kutumia vidole; stadi katika kuiba. 3 pungufu, shoti. 4 (of beer, wines) -sio kali sana; (of food) laini; (of meals) -dogo; (of sleep) lepe, -sio zito; (of books, plays, music) -a kuburudisha; (of soil) laini, -epesi; (of work) rahisi; -epesi; (of taxes, punishment) -dogo, -epesi; (of a syllable) -siokuwa na mkazo. make ~ work of something fanya bila shida. 5 -sio nguvu; -sio muhimu; -dogo a ~attack of illness ugonjwa usiokuwa na nguvu/mdogo. make ~ of dharau. 6 pumbavu; -sio makini; -

like

puuzi. ~minded adj. ~mindedness n. 7 changamfu. ~ heart n moyo mchangamfu. ~ hearted adj. ~ heartedly adv. ~ heartedness n. 8 -enye tabia mbaya, fisadi, kware. 9 -a kizunguzungu. ~ headed adj. ~ headedly adv. ~ headedness n. 10 (compounds) ~-o-love n mwanamke kigeugeu; malaya. ~weight n,adj (man or animal) chini ya uzito wa wastani; (boxing) uzito mwepesi (kati ya kg 57 na 61); (fig) mtu asiye muhimu. ~-heavyweight n mwanamasumbwi mwenye uzito kati ya kg 72.5 na 79.3 adv kwa wepesi, kwa urahisi travel ~ safiri na mizigo michache. ~ly adv. ~ness n. ~en vt,vi punguza; punguka uzito ~en a ship's cargo punguza shehena melini. ~some adj -epesi; -enye miondoko ya kupendeza; cheshi. vi ~ on/upon bahatisha ~ upon a rare commodity in a village shop bahatisha kupata bidhaa adimu katika duka la kijiji.

lighter n tishali. vt safirisha kwa tishali. ~age n nauli ya tishali.

lightning n radi a flash of ~ mwale/ kimulimuli cha radi. like ~ adj -epesi kama radi. with ~ speed haraka sana. ~bug n (US) kimulimuli, kimetameta. ~ rod-conductor n ufito wa kuzuia radi. ~ strike n mgomo wa kushtukiza.

lights n mapafu; yavuyavu (ya wanyama kama kondoo, nguruwe nk.) kwa ajili ya chakula.

ligneous adj -enye mti; -a mbao. lignite n makaamawe yasiokomaa.

like1 adj sawa, -a kufanana. as ~ as -enye kufanana kabisa, sawasawa kabisa. in ~ manner hivyo. ~ father ~ son (prov) rupia kwa nyenzie, mtoto wa nyoka ni nyoka; kufanana kwa baba na mtoto. be ~ fanana na, landa; -wa sawa, twaana. ~-minded adj -lio na mawazo/ malengo n.k. sawa adv 1 ~ as (archaic) kwa namna ile ile. 2 kwa

like

uwezekano, labda. ~ enough; most/very ~; as ~ as not penginepo; kwa uwezekano mkubwa conj 1 kama she can't cook ~ her father does, hawezi kupika kama baba yake. 2 (non-standard use) kama vile, kana kwamba it looks ~ rain inaonekana kana kwamba mvua itanyesha. n 1 mtu/kitu kama hicho I never heard the ~ (of it) sijasikia kitu kama hicho. 2 the ~ of (colloq) watu/vitu vya namna hiyo the ~ of us watu kama sisi prep 1 kama, kama vile. nothing ~ pasipo kifani. something ~ kitu kama. 2 elekea feel ~ jisikia kama do you feel ~ having a rest? ungependa kupumzika? looks ~ onekana kama he looks ~ winning inaonekana kama anashinda. 3 ndivyo ilivyo that is just ~ him ndivyo alivyo. 4 namna, kama don't talk ~ that usizungumze namna hiyo. 5 (colloq, sl). ~ anything mno; kama inavyopaswa. ~ mad/crazy mno. ~ hell/blazes kwa nguvu; (as an int) wala! ~n vt ~n something to something fananisha, linganisha. ~ness n 1 mshabaha, mlingano, ufanani have a ~ness -wa mfano mmoja, fanana, landa they have a great ~ness wamefanana sana. in the ~ of katika mfanano. 2 kifani, taswira, sanamu, picha inayofanana na mtu mwenyewe take somebody's ~ness fanya mchoro wa sanamu ya mtu fulani.

like2 vt 1 penda she ~s him anampenda. 2 (In neg sentences) kataa, sita, -topenda I didn't ~ to disturb you sikutaka kukusumbua. 3 (with should, would) they would ~ to come wangependa kuja. 4 pendelea, chagua, taka I ~ this more than that napendelea hii kuliko ile. if you ~ kama unataka, ukipenda. 5 faa kiafya, penda the food doesn't ~ me chakula hiki hakinifai. likable/~able adj -enye kupendeka she is likable/ ~able anapendwa. liking n mapenzi, matakwa, upendeleo have a linking

lime

for penda to one's liking kama mtu apendavyo.

likely adj kuelekea, -a kufaa, -a kutaka kuwa it is ~ to yaelekea ku they are ~ to lose wanaelekea kushindwa he is not ~ to succeed haelekei kufaulu adv huenda, labda. very/most ~ huenda. as ~ as not haikosi. likelihood n uwezekano, uelekeo (wa jambo kutokea kuwa kweli n.k.) there is small likelihood that he is telling the truth kuna uwezekano mdogo kuwa anasema kweli.

likewise adv kadhalika, vivyo do ~ fanya hivyo conj pia; zaidi ya hayo.

lilac n lilaki: maua ya rangi ya zambarau isiyoiva.

Lilliputian n kibeti, kiduranga adj -dogo sana, -a kibeti.

lilt n mwendo/mpigo wa wimbo/ ngoma; mahadhi. vt imba kwa mapigo yenye mkazo.

lily n yungiyungi. ~-livered adj -oga. ~-white adj -eupe pepepe

limb n 1 kiungo (mkono, mguu) there is pain in all my ~s maungo yote yaniuma. 2 tawi. leave somebody/ be/go out on a ~ acha mtu; jitenga; (colloq) jiweka katika hali ya hatari. 3 (colloq) ~ of the devil/satan mtoto mkaidi. ~er adj laini. vt,vi ~ (oneself) up -fanya mazoezi ya mwili (kwa ajili ya kuulainisha).

limbo n 1 in ~ kusahaulika. 2 sehemu ya kuzika vitu. 3 limbo (rel.) sehemu ya ahera ziendako roho za watoto na watu wema wasiobatizwa.

lime1 n ndimu. ~ tree n mdimu. ~ juice n juisi/maji ya ndimu.

lime2 n 1 chokaa. 2 ~-kiln n tanuu, chomeo la chokaa. (bird) ~ n ulimbo. vt 1 paka kwa ulimbo. 2 nasa ndege kwa ulimbo. ~light n taa yenye nuru kali (kwenye jukwaa) he is fond of the ~ light apenda kujitokeza, kujionyesha mbele ya watu. be in the ~light wa maarufu, julikana. ~stone n gange, mawe ya

limerick

chokaa.

limerick n shairi cheshi (lenye mistari mitano).

limey n (US sl) Mwingereza.

limit n 1 mpaka, upeo, kikomo that's the ~ ! basi! there's a ~ to my patience uvumilivu wangu una kikomo there's a ~ to every thing hakuna lisilokuwa na kikomo you're the ~ umezidi, mtu hawezi kukuvumilia set a ~ weka mpaka. within ~s kwa kiasi fulani city ~s mipaka ya jiji. without ~ bila kikomo. off ~s ni marufuku. 2 (of business) mpango. 3 ua, mzingo. vt 1 zuia, wekea mpaka/kikomo. ~ ed adj -dogo, finyu, chache; -enye mipaka. ~ed liability company (Ltd). n kampuni yenye dhima ya kikomo L~ ed Monarchy utawala wa kifalme ulio na mipaka. ~less adj bila kikomo. ~ation n 1 kikomo, mpaka. 2 ufinyu, upungufu; udhaifu he knows his ~s anafahamu udhaifu wake.

limn vt (old use) chora (picha), fanya taswira.

limousine n limuzini: gari la anasa (agh. kiti cha mbele na cha nyuma vimetengwa na kioo).

limp1 vi chechemea, chopea. n mwendo wa chopi.

limp2 adj 1 teketeke, laini; legevu, -nyong'onyevu. 2 -sio na nguvu. ~ly adv. ~ness n.

limpet n 1 koanata. 2 (fig) mtu anayeshikilia (kwa kupachikwa/ ng'ang'ania cheo). ~ed mine n bomu linalotengwa kwenye meli.

limpid adj -eupe, -angavu. ~ly adv. ~- ity n uangavu, weupe; usafi.

linchpin n kipini cha chuma (mwisho wa ekseli) kinachofanya gurudumu lisiachie; (fig) kiungo muhimu,

mtu/kitu muhimu katika shughuli/ sehemu fulani.

line1 n 1 (cord) kamba; ugwe; uzi; waya. fishing ~ n ugwe wa kuvulia samaki telephone ~ waya wa simu hang the clothes on the ~ anika nguo

line

kwenye kamba. party/shared ~ n simu inayomilikiwa na watu zaidi ya mmoja. 2 mstari (uliochorwa) (games) cross the ~ vuka mstari. linage n 1 idadi ya mistari. 2 malipo juu ya idadi ya mistari katika aya. 3 alama ya mstari mwilini, kunyanzi; mistari kwenye kiganja. 4 kontua; umbo la nje. 5 (of people/things) safu, foleni. in (a) ~ kwenye mstari on the ~ (of exhibitions) sawa na macho ya watazamaji. 6 mpaka the ~ between Kenya and Uganda mpaka kati ya Kenya na Uganda. 7 Ikweta cross the ~ vuka Ikweta. 8 reli, njia moja ya reli. reach the end of the ~ (fig) fikia mwisho; fikia kuachana. 9 shirika la usafiri an air~ shirika la usafiri wa ndege shipping ~ shirika la usafiri wa meli. 10 mwelekeo; mkondo; njia you should keep to your own ~ shikilia msimamo wako communication ~s, njia za mawasiliano. choose/follow/take the ~ of least resistance fuata njia iliyo rahisi. take a strong/firm ~ (over something) chukua mweleko imara. do something along/on sound/ correct etc ~s tumia njia/mbinu sahihi. (be) in/out of ~ (with) kubaliana/-tokubaliana na. bring something into ~ patanisha, sababisha makubaliano. come/fall into ~ (with) kubali, shawishi maafikiano. toe the ~ (fig) -wa na nidhamu, tii. the party ~ n itikadi ya chama. 11 mfuatano, ukoo. 12 (writing/print) mstari wa maneno. drop somebody a ~ (colloq) andikia barua. read between the ~s (fig) ona maana iliyofichika. Marriage ~s n (GB colloq) cheti cha ndoa. ~s n maneno ya mwigizaji; mistari inayoandikwa kama adhabu (agh. kwa wanafunzi wa shule za msingi). 13 mstari wa mbele. front ~ n vikosi vilivyo mstari wa mbele karibu na adui. all along the ~ katika kila hali. go up

line

the ~ enda mstari wa mbele. 14 (mil) safu ya mahema, vibanda kambini. 15 the ~ n (GB army) jeshi la askari wa miguu; (US army) jeshi. 16 (mil) safu mbili sambamba za askari. 17 (naval) ~ abreast n (meli) zilizokaa sambamba. 18 shughuli; kazi. his ~ is banking anafanya/kazi benki. 19 (trade use) aina ya bidhaa. 20 Hard ~s n bahati mbaya! pole. 21 (sl) shoot a ~ jigamba. ~ shooting n. ~ shooter n. 22 (colloq) give somebody/get/have a ~ on something toa/pata habari zaidi juu ya jambo fulani. ~ar adj -a mstari; -a mistari ~ar measure vipimo; (maths) ~ar combination matangamano mstari ~ar equation milinganyo mstari ~ar geometry jometrii mstari ~ar translation uhamisho mstari ~ar transformation mbadiliko mstari. ~ation n uchoraji mistari. ~man n (electricity) fundi (wa) waya (za simu/umeme). vt,vi 1 tia alama za mstari. ~d paper n karatasi zenye mistari ~ in a contour chora kontua kwenye ramani. 2 -wa na mistari, funika na mistari; kunjika katika mistari pain had ~d her forehead maumivu yalisababisha uso wake kujikunyata. 3 ~-up panga mstari/foleni; simama mstarini. up n mpangilio; foleni, safu; ratiba. 4 fanya, panga mstari/jipanga crowds of people ~d the street to cheer their leader vikundi vya watu vilijipanga katika mtaa kumshangilia kiongozi wao.

line2 vt ~ something (with something) 1 weka kitambaa ndani; ongeza vitu katika sanduku, mfuko. 2 (fig) jaza, -wa na fedha nyingi he ~d his purse well amepata pesa nyingi, alitengeneza pesa kweli.

lineage n nasaba, ukoo, jadi. lineal adj -a nasaba, ukoo, jadi. lineal descendant n dhuria.

lineament n (formal) sura, umbo.

linen n kitani, nguo ya kitani (hasa shati na nguo za meza na kitanda).

links

~-draper n mwuza nguo za kitani na pamba. wash one's dirty ~ in public toa siri za nyumbani hadharani adj -a kitani.

liner n 1 meli/ndege ya abiria 2 ~ (train)/freight ~ n gari moshi la bidhaa.

linesman n (sports) mshika kibendera.

linger vi kawia, limatia, kaa karibu. n ~ing adj -a muda mrefu, -a kudumu ~ing disease ugonjwa wa muda mrefu. ~ingly adv.

lingerie n nguondani za kike.

lingo (joc or derog) kilugha, lugha isiyofahamika; istilahi.

lingual adj -a ulimi, -a lugha.

audio-~methods n mbinu za kusikiliza na kusema. bi~ adj -a lugha mbili. multi~ adj -a lugha nyingi. lingua franca n lugha ya biashara/mawasiliano (k.m. Kiswahili katika eneo la lugha nyingi mbalimbali).

linguist n 1 mwana isimu. 2 mjuzi wa lugha kadha. ~ic adj -a isimu, -a lugha. ~ics n isimu: sayansi ya lugha (maumbo, miundo, matamshi, maana na matumizi). applied ~ics n isimu matumizi.

liniment n dawa ya kuchua, fututa.

lining n bitana. every cloud has a silver ~ (prov) baada ya dhiki faraja.

link1 n 1 pete (ya mnyororo). 2 (person or thing) kiungo missing ~ kiungo muhimu kinachokosekana; mnyama (kiungo) kati ya sokwe na binadamu. ~man n mtu wa kati; (in games) mchezaji (wa) kiungo. 3 kifungo (cha mkono wa shati). 4 kipimo cha urefu (sawa na sentimita 20). vt,vi ~ (up) unga; ungana; jiunga na; unganisha; husiana; husisha ~-arms unganisha mikono. ~age n; ~up n unganisho.

link2 n (hist) mwenge, tochi, taa. ~boy; ~man n mbeba mwenge/ tochi/taa. ~ man n mtangaza programu.

links n (pl) 1 kiwanja cha kuchezea

linnet

gofu. 2 mbuga za majani karibu na bahari.

linnet n biliwili (wa nchi za baridi).

lino; ~leum n zulia la mpira/plastiki.

Linotype n linotaipu: herufi za kupangwa.

linseed n mbegu za kitani. ~-oil n

mafuta ya kitani.

linsey-woolsey n kitambaa cha sufu na pamba hafifu.

lint n nyuzi za pamba; kitambaa (cha kufungia kidonda), bandeji.

lintel n linta.

lion n 1 simba. a ~ in the way pinga-mizi. the ~'s share fungu kubwa kabisa put one's head in the ~`s mouth jihatarisha. ~ hearted adj shujaa. 2 mtu mashuhuri. ~ess n simba jike. ~ hunter n 1 mwindaji wa simba. 2 (fig) mtu anayekusanya watu mashuhuri. ~ize vt tendea mtu kama mtu mashuhuri, tukuza.

lip n 1 mdomo. bite one's ~ onyesha hasira/ghadhabu. curl one's ~ onyesha dharau/beza. pay/give ~ service to something unga mkono kwa maneno matupu au kinafiki. hang on/upon somebody's ~s sikiliza kwa shauku smack/lick the ~s lambitia, onyesha (dalili za) furaha. keep a stiff upper ~ jizuia, vumilia. 2 ukingo pouring ~ mdomo wa chombo 3 (sl.) (maneno ya) ujuvi/ufidhuli none of your ~ acha ufidhuli. vt 1 gusa kwa midomo, busu. 2 tamka. 3 (of waves) lamba/piga (mwamba n.k.). ~ped adj -enye mdomo/ukingo (combined forms) ~reading n (to deaf people) kusoma midomo. ~ring n ndonya. ~salve n dawa ya midomo. ~-service n maneno matupu. ~stick n rangi ya midomo.

liquefy vt,vi yeyusha; yeyuka. liquefice yeyusha barafu. liquefaction n. liquescent adj epesi kuyeyuka, -nayoyeyuka.

liqueur n kinywaji kikali, kitamu.

liquid n 1 uwoevu kitu kama maji, kimiminiko. 2 (phon) konsonanti l au

listen

r adj 1 -oevu, -a majimaji, -a kimiminiko. ~ gas n gesi oevu/ miminiko. 2 (of sound) laini, -ororo. 3 -eupe, angavu. 4 -enye kubadilika-badilika. 5 (in finance) epesi kusarifika ~ assets mali rahisi kubadilishika kwa pesa taslimu. ~ate vt,vi 1 lipa deni. 2 filisi, filisika. 3 (sl) ua. ~ation n ulipaji deni. go into ~ ation filisi; filisika. ~ated adj filisika/filisiwa. ~ator n mfunga hesabu (wa kampuni/duka); mfilisi. ~ity n umajimaji, uoevu; uwezo wa kupata pesa, ukwasi. ~ize vt ponda matunda n.k. yawe rojorojo. ~izer n kigeuza maji, kioeshaji.

liquor n 1 (GB) pombe, kileo; (US) pombe kali. 2 (cooking) maji ya kupikia pombe. 3 maji yatokanayo na kupika/kuloweka chakula. vt chuja, keneka, tonesha. ~up -lewesha na pombe kali. ~ish adj (of person) -liopenda ulevi.

liquorice n urukususu, susi.

lira n (sl. lire) lira: fedha ya Kitaliana.

lisle n kitambaa kigumu cha pamba.

lisp vt,vi sema kitembe, piga kitembe.

n kitembe. ~ing adj. ~ingly adv.

lissom; ~e adj -epesi, -a madaha. ~ness n.

list1 n 1 orodha. (leg) ~ price n bei iliyotangazwa. the active ~ n orodha ya maofisa wa jeshi (wanaoweza kuitwa jeshini). the free ~ n bidhaa zisizolipiwa ushuru; watu wanaoingia senema/mchezoni nk. bila kulipa. 2 ukingo; mtanda (wa nguo). 3 (arch) pl. kiwanja cha mashindano enter the ~ against jiandikisha kushindana na. vt orodhesha; andikisha.

list2 vi (of ship) egemea, lala upande. n kuegemea, kulala upande.

list3 vt,vi (old use) sikiliza.

list4 vi (old use) taka, chagua, penda he does as he ~s anafanya apendavyo.

listen vi sikiliza; sikia ~ to somebody singing sikiliza mtu akiimba ~ in

listeria

(to) somebody pulikiza, sikiliza mtu katika redio; sikiliza (kwa siri). ~er n msikilizaji. ~ing post n (mil) kituo cha kupulikiza maadui; (fig) mahali pa kupata maelezo mbalimbali.

listeria n bakteria yenye kusumisha chakula.

listless adj -tepetevu, -legevu,

-nyong'onyevu, -zito (kutokana na uchovu). ~ly adv. ~ness n.

lit pt, pp. of light.

litany n litania: sala za kuomba za padri na watu wakiitikia.

litchi n see lychee.

liter n see litre.

literal adj 1 (exact) hasa, halisi, -a maneno yenyewe, -a maana iliyo wazi ~ translation tafsiri sisisi. 2 -a herufi ~ error kosa la kuruka herufi. 3 (of person) kavu; -a kawaida; -siobunifu. ~ly adv neno kwa neno he did ~ nothing hakutenda chochote.

literacy n kujua kusoma na kuandika.

literary adj -a maandishi, -a fasihi; -a waandishi ~ man mwandishi au mpenda fasihi ~ property haki ya mwandishi/mtunzi ya mrabaha na faida zinazotokana na kazi yake ~ criticism uhakiki wa fasihi. literate adj 1 -enye elimu, -somi. 2 -enye kujua kuandika na kusoma. n mtu ajuaye kuandika na kusoma, mwenye elimu ya kadiri/ya kutosha. literati n wasomi, maulama, wanazuoni. literature n 1 fasihi. 2 vitabu/ maandiko mbalimbali (ya nchi au kipindi fulani). 3 maelezo; matangazo.

lithe adj -a kupinda/kunengua/kugeuka kwa urahisi, -epesi, -a madaha. ~ness n.

lithography n lithografia: tendo la kuandika/kuchora na jiwe. lithograph n lithografu. lithographic adj -a lithografu.

litigate vi,vt enda mahakamani, fungua madai mahakamani. litigation n. litigious adj 1 gomvi, -a kupenda daawa. 2 -enye kuleta ubishi. litigant

little

n mdai, mwenye daawa adj -a daawa.

litmus n (chem) litmasi: dutu/utomvu wa zambarau (ambao hugeuka kibuluu kwa asidi na mwekundu kwa alkali). ~-paper n karatasi iliyopakwa litmasi.

litotes n tamshi poza/kinyume lenye

kurahisisha mambo agh. husemwa kinyumenyume k.m. si mbaya, nzuri n.k.

litre/liter n lita.

litter n 1 takataka. ~bin/~basket n pipa/kapu la takataka. ~ bug n; ~ out n (colloq) anayetupa takataka. 2 a ~ fujo, machafuko. 3 majani ya kulalia wanyama. 4 vitoto vyote vya uzazi mmoja (mkumbo mmoja); (pigs) vibwangala. vt,vi 1 ~ something (up) with something chafua, fuja; tia takataka. 2 ~ something (down) tandika majani chini. 3 (of animals) zaa.

little adj 1 -dogo; chache; haba the ~ finger kidole kidogo a ~ money pesa chache. 2 fupi a ~ sleep lepe la usingizi. 3 kijana a ~ boy mvulana mdogo the ~ ones watoto the ~ Nyereres Nyerere wadogo. the ~ people/folk n (esp. Ireland) vichimbakazi. 4 (to emphasize a feeling) -zuri she's a nice ~ thing ni kisichana kidogo kirembo her poor ~ efforts to please jitihada zake ndogo za kupendeza so, that's your ~ game ndiyo mchezo wako ehe! he knows his ~ ways anajua hila zake. 5 a ~ kidogo a ~ rice wali kidogo. not a ~ (euph) -ingi not a ~ trouble matatizo mengi. 6 (of a person) -dogo, -fupi a ~ man mtu mfupi. 7 (insignificant) -nyonge, hafifu, duni. 8 (of intelligence) pungufu n 1 kidogo. ~ by ~ kidogo kidogo take up ~ by ~ chota kidogo kidogo a ~ of everything kidogo kila kitu a ~ of this and a ~ of that kidogo hapa na kidogo pale a ~ makes us laugh hata jambo dogo linatuchekesha. ~

littoral

or nothing si chochote, kidogo sana he got a ~ of it alipatapata what ~ remained kidogo kilichobaki. (of time) after a ~ baadaye kidogo. for a ~ kwa muda mfupi adv 1 kidogo, punde a ~ complicated -a matatizo kidogo a ~ more bado kidogo ~ tired -enye kuchoka kidogo ~ more than a thief ni mwizi kweli. 2 (with verbs think, dream, suspect) ~ did I suspect sikushuku hata kidogo think~ of somebody dharau. ~ness n 1 udogo. 2 unyonge, udhaifu, uhafifu, uduni.

littoral adj -a pwani. n pwani.

liturgy n liturujia: kawaida ya ibada na sala ya dini, kawaida ya Ushirika Mtakatifu. liturgial adj.

live1 adj 1 -hai, -enye uhai ~ weight uzito wa mnyama hai. 2 -a moto; motomoto; -a kuwaka; (of issues) motomoto, -a kisasa, sasa hivi ~ coals makaa ya moto; (of bullets, bombs) -enye marisawa; (elect) -enye umeme. ~ wire n waya moto/wenye umeme; (fig) (persons) mchangamfu. 3 (radio/TV) a ~ broadcast tangazo la moja kwa moja (lisilorekodiwa kabla). 4 ~ -birth n mtoto aliyezaliwa hai. 5 -a nishati; mashughuli; -a hima.

live2 vt,vt 1 ishi, -wa na uzima, -wa hai. 2 endelea kuishi, dumu. ~ on jikongoja, endelea kuishi. you/we ~ and learn kuishi kwingi kuona mengi. ~ and let ~ -wa mvumilivu long ~ somebody! adumu fulani maisha marefu! ~ honestly -ishi kwa uaminifu ~ to be.... ishi hadi... ~ through, shinda majaribio mengi, vumilia ~ as man and wife kaa kinyumba. ~ to oneself jitenga, ishi pekee. 3 pata riziki. ~ by tegemea. what does he ~ by kazi yake nini? ~ by one's wits ishi kwa ujanja/mbinu. ~ off the land tegemea riziki kwa kilimo. ~ on something ishi kwa kutegemea kitu. ~ on your salary ishi kwa kutegemea mshahara wako what does

livid

he ~on anaponea nini? ~ on one's name/reputation ishi kwa sifa/jina zuri. 4 ~(in/at) (reside) ishi, -kaa; (of room etc) not fit to ~in haifai kuishi ndani yake, haikaliki. 5 ~ on (in memory etc) dumu, ishi katika kumbukumbu ya watu. ~ together ishi pamoja. ~ in/out (of domestic servants) ishi kazini/ nyumbani, nenda na kurudi kila siku. 6 nenda. ~ up to something fuata; fikia matarajio fulani. ~ something down sahaulisha yaliyopita. ~ with something vumilia. 7 ~ it up ishi maisha ya mishughuliko na anasa, furahia maisha. 8 ishi uonavyo; chagua kuwa mwaminifu. ~ a lie ishi kinafiki. livable; ~able adj 1 -a kukalika; -enye kufaa kuishi. 2 -a kuvumilika. ~lihood n kazi, riziki. earn a ~lihood chuma riziki. ~long adj (only in) the ~long day mchana kutwa. the ~long night usiku kucha adj 1 -epesi; changamfu, -cheshi, -kunjufu. 2 (of non-living things) -a kwenda mbio have a ~ly time sisimkwa, changamka. look ~ly changamka. make things ~ly for somebody changamsha, sisimua mtu. 3 (of colour) kali, -enye kung'aa. 4 hai, kama kweli/halisi. ~liness n. ~n vt,vi ~ up changamsha, sisimua; sisimka. ~r n mtu apendaye kuishi kwa namna yake (nzuri au mbaya).

liver n ini. ~ish adj -enye kuugua ini;

-enye kukasirika ovyo.

livery n 1 mavazi maalum, sare ya mtumishi ~ servant mtumishi mwenye sare rasmi. in/out of ~ -liovaa/-siova sare rasmi. 2 (fig) (poet) vazi. 3 ~ (stable) n banda la farasi wa kukodishwa. liveried adj -liovaa vazi rasmi. ~ man n mtunza farasi.

lives pl. of life.

live-stock n (esp. farm) mifugo.

livid n rangi ya risasi; samawati; kijivu (of person or his looks) -liokasirika sana, -liofura kwa hasira. ~ly adv.

living

living adj 1 hai, -zima not a ~ soul hakuna mtu yeyote. within ~ memory -enye kukumbukwa na watu walio hai. 2 (of a likeness) hasa, halisi she is the ~ image of her mother anafanana sana na mama yake. 3 -enye nguvu; hai, -enye kusisimua. the ~ n 1 (watu) wanaoishi/wazima the ~ and the dead wazima na wafu. n (conditions) hali za kuishi ~ standard kiwango cha maisha. 2 maisha; riziki. a ~ wage n mshahara wa kujikimu earn one's/make a ~ pata riziki. for ~ ili kupata riziki ~ costs gharama za maisha. ~ room n sebule, baraza good ~ maisha ya starehe, raha. 3 kazi na mshahara wa padri/mchungaji.

lizard n mjusi; (burrowing) guruguru. monitor -~ n kenge.

Llama n lama: mnyama kama kondoo

wa Amerika ya Kusini.

lo int (old use) tazama. ~ and behold ajabu iliyoje!

load n 1 mzigo, shehena; (fig) wajibu, madaraka makubwa (ya usimamizi au utunzaji wa jambo) a heavy ~ on one's shoulders madaraka makubwa aliyonayo mtu. take a ~ off somebody's mind ondolea mtu mashaka. ~s of (colloq) kiasi kikubwa, tele. ~ line n mstari wa ujazo/shehena ya meli. 2 kiwango cha kazi ifanywayo na dainamo, mota, injini n.k.; kiasi cha umeme kinachotolewa na jenereta. ~shedding n kukata umeme mahala fulani na kuupeleka unakohitajika zaidi. vt, vi 1 ~ something into something pakiza, sheheni, pakia. ~ somebody with something twisha, bebesha; (fig) lemeza. 2 (of a gun) tia risasi he ~ed him with favours alimtendea/alimsheheneza fadhili nyingi. ~ dice (against somebody) (fig) fanyia mtu jambo lisilokuwa na manufaa kwake a ~ed question swali lenye mtego. ~ed adj (sl) -liojaa, -enye fedha nyingi. ~er n. ~ing n

lobe

upakiaji.

loadstar/loadstone n see lode.

loaf1 n 1 mkate, boflo a ~ is better than none afadhali kidogo kuliko kukosa kabisa. 2 ~ sugar sukari kibonge. 3 chakula chenye umbo la boflo. 4 (sl.) use one's ~ fikiri kwa makini, tumia akili.

loaf2 vt,vi (colloq) randa, zurura ~ away one's time zurura. n kuzurura. ~er n mzururaji; lofa.

loam n udongo tifutifu wenye rutuba. ~y adj.

loan n 1 mkopo, karadha take a ~ kopa. 2 kukopesha; kukopa; kuazima have something on ~ (from somebody) azima kitu, chukua kitu kwa mkopo. collection n picha n.k. zilizoazimwa (kwa maonyesho). ~ office n ofisi ya mkopo/karadha. ~ word n neno la mkopo. vt (of money) kopesha; azima.

loath;loth adj (pred only) ~ to do something -totaka kufanya jambo. nothing ~ adj -enye kutaka; kwa hiari be ~ for somebody to do something -tokubali mtu kufanya kitu. ~e vt chukia kabisa, zia I ~e him namchukia kabisa ~e doing something chukia kufanya kitu; (colloq) -topenda. ~ing n chuki; karaha. ~some adj -a kuchukiza, makuruhu.

loaves n pl.of loaf.

lob vi,vt rusha mpira juu mfano wa tao. n mpira uliorushwa juu.

lobby n 1 sebule, ukumbi. 2 (division)

~ (in House of Commons) ukumbi wa mahojiano baina ya wabunge na watu wengine, ukumbi wa bunge; kikundi shawishi: kikundi kinachowashawishi wabunge juu ya mswada/sheria fulani. vt shawishi wabunge (ili kupigia au kutopigia kura mswada). ~ist n mshawishi wabunge.

lobe n 1 (of an ear, lung, brain etc) ndewe adj -enye umbo la ndewe. 2 kitu kinachofanana na umbo la ndewe.

lobster

lobster n kambamti; kambakoche. ~ pot n mtego wa kamba.

local adj 1 -a mahali maalum, -a mahali palepale. ~ colour n mambo ya kienyeji (yanayoongezwa katika hadithi ili kuipa ladha). ~ custom n mila ya mahali. ~ government n serikali ya mitaa ~ habitation makao, makazi. ~ option/veto n mfumo wa kukataza jambo kwa kupiga kura k.m. kukataza uuzaji wa pombe. ~ purchase order n dhamana ya ununuzi ~ relief not indicated by contours sura ya mahali ambayo haikuonyeshwa kwa kontua. ~ time n saa za mahali pale. 2 -a (kuathiri) sehemu ~ anaesthetic dawa ya ganzi n (usu. pl.). 1 mkazi wa mahali fulani, mwenyeji. 2 (colloq) kilabu, baa. 3 habari za mahali pale pale (katika gazeti). ~ly adv. ~e n mahali; mandhari. ~ism n 1 kupendelea mambo ya mahali pake (mji, mkoa n.k.); fikra finyu (kutokana na kujua mambo ya mahali pake tu). 2 mbinu, nahau, matamshi (ya lahaja fulani). ~ity n 1 mahali. 2 (neighbourhood) janibu; mtaa. 3 (a sense) utambuzi wa mahali. ~ize vt fanya (kuwa) ya mahali fulani, weka/zuilia mahali maalum ~ the disease zuia maradhi katika eneo fulani tu. ~zation n.

locate vt 1 tambua/onyesha mahali pa ~ the industrial area on the map onyesha eneo la viwanda katika ramani. 2 weka mahali. 3 be ~d -wa/wekwa mahali. location n 1 mahali maalumu. 2 kuonyesha/ kutambua mahali. 3 mahali pa kupigia (sehemu ya) picha za sinema. 4 (South Africa) kitongoji (walikolazimika kuishi Waafrika). locative n, adj (gram) -a mahali.

loci n pl of locus.

lock1 n 1 shungi la nywele. 2 pl. ~s n nywele.

lock2 n 1 kufuli, kifungio be under ~ and key fungwa kwa ufunguo. ~smith n mtengeneza makufuli. 2

locus

(of a gun) mtambo. ~ stock and barrel n kitu kizima, zimazima; kabisa. 3 (of canal) mlango ~ chamber mlango/ chumba cha kuzuia maji. ~ keeper n mlinda lango (la mfereji). 4 hali ya kukwama, kushikamana. ~jaw n pepopunda. ~nut n nati kifungo. 5 (motoring) mkato wa usukani. vt,vi 1 funga kwa ufunguo. ~ the stable door after the horse has bolted/has been stolen fanya tahadhari baada ya mambo kuharibika. ~ something away hifadhi kitu mahali pa salama; (fig) tunza/hifadhi (moyoni). ~ somebody in fungia mtu ndani. ~ somebody out fungia mtu nje; zuia mtu asiingie. ~ out n kufungia nje (kuzuia wafanyakazi wasiingie sehemu zao za kazi mpaka masharti fulani yatimizwe). ~ something/ somebody up fungia kwa ufunguo; funga nyumba n.k. (kwa funguo); tia mtu ndani; weka/wa na rasilimali isiyouzika kwa urahisi. ~up n korokoroni, mahabusi; (colloq) jela adj -enye kufungika kwa kufuli. 2 fungika. 3 funga; kwama. 4 fungamana. ~ on to (of a missile) tafuta na fuata (shabaha) kwa rada. ~er n 1 kabati ndogo (agh. ya kuwekea nguo za michezo, kazi, n.k.). 2 kasha/chumba kidogo melini (cha kuhifadhia nguo, risasi, mavazi, n.k.). be in/go to Davy Jone's ~er zama baharini.

locket n kibweta kidogo (agh. huvaliwa shingoni kwenye mkufu).

loco adj (sl) mwendawazimu.

locomotion n mwendo; uwezo wa

kwenda. locomotive adj -enye nguvu ya kwenda. n kichwa cha garimoshi locomotive works kiwanda cha garimoshi.

locum (tenens) n padri/daktari anayekaimu/fanya kazi kwa muda badala ya mwingine.

locus n 1 sehemu/mahali maalum pa kitu; kituo. 2 (maths) mchirizo; lokaso. 3 ~ classicus n aya muhimu

locust

(katika somo fulani).

locust n nzige.

locution n msemo, mtindo wa kusema, mbinu ya kutumia maneno; nahau.

locutory n ukumbi, baraza (ya nyumba ya watawa).

lode n mstari, uzi wa madini ndani ya mawe; tabaka ya madini ardhini. ~star n nyota iongozayo, nyota ya Kaskazini; (fig) mwongozo, kiongozi. ~stone n sumaku.

lodge n 1 nyumba/chumba cha bawabu, mpagazi, n.k. 2 nyumba ya shamba. 3 (GB) makao ya mkuu wa chuo. 4 nyumba ya kukutania wanachama. vt,vi 1 pangisha mtu chumba cha kulala (kwa muda); weka (watu) kwa muda. 2 ~ at/with panga. lodging n (usu. pl.) 1 nyumba/chumba/vyumba vya kupanga kwa muda take lodgings panga (katika nyumba ya kupanga). I'm lodging here nimepanga hapa. 3 ~ in ingia; kwama; tia; kwamisha. 4 ~ a complaint (against somebody) shtaki, toa lalamiko dhidi ya ~ an appeal kata rufaa. 5 weka, tia. ~r n mpangaji wa muda take ~rs pangisha. lodging house n nyumba ya kupanga.

lodgment n 1 kushtaki. 2 (mil) eneo lililotekwa kutoka kwa adui. 3 (accumulation) limbikizo.

loft1 n 1 darini. 2 roshani (katika kanisa au ukumbi).

loft2 vt (of golf, cricket) piga juu. ~y adj 1 (not used of persons) -a juu sana, -refu. 2 (of thoughts, aims, feelings etc.) -a fahari sana. 3 -a kiburi, -a kujidai, shaufu. ~ily adv. ~ness n urefu, kiburi, ubora.

log1 n gogo la mti, kigogo like a ~ bila fahamu, bila kujitambua. sleep like a ~ lala fofofo. ~ cabin n nyumba ya magogo. ~ jam n mkwamo wa magogo yanayoelea majini; (US) mkwamo. ~ rolling n kuungana mkono. ~ging n ukataji miti.

log2 n 1 kipimamwendo wa meli baharini. 2 (also ~book) batli:

long

kitabu chenye habari zote za safari ya merikebu (meli). 3 kitabu cha safari za ndege, gari n.k.; (colloq) kitabu cha usajili wa motakaa. vt andika katika batli.

logarithm n (maths) logi. ~ic adj.

loggerheads n (only in) at ~ (with somebody) gombana, -topatana, sigana.

logic n mantiki. ~al adj -enye mantiki

a ~al argument hoja yenye mantiki. ~ally adv. ~ality n kuwa na mantiki. ~ian n.

logistics n (mil.) utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu.

logo n nembo; msemo.

loin n 1 kiuno. gird up one's ~ (biblical) jitayarisha kwa safari; jifunga kibwebwe. sprung from the ~s of zaliwa na. ~-cloth n msuli.

loiter vi zurura, randa, tanga. n mzururaji.

loll vi,vt ~ (about/around) 1 jikalia, pumzika/lala/kaa kivivu. 2 (of a tongue) ~ out ning'inia/ning'iniza ulimi nje the dog ~ed its tongue out mbwa alining'iniza ulimi nje.

lollipop n peremende kijiti. ~ man/ woman n (colloq) mtu avushaye watoto barabarani.

lolly n 1 (colloq) peremende kijiti. iced ~ n aisikrimu ya kijiti.

lone adj 1 (attr only) -a pekee, -a kukaa peke yake. play a ~ hand (fig) fanya jambo pasipo msaada. ~ly adj -pweke, bila rafiki, -a ukiwa feel ~ly jisikia upweke. 2 pweke, -siotembelewa mara kwa mara. ~liness n upweke. ~ some adj pweke, -a ukiwa.

long1 adj 1 -refu. 2 (in phrases) kubwa; -enye uwezo. have a ~ arm onyesha madaraka. the ~ arm of the law uwezo mkubwa wa sheria. make a ~arm for something nyosha mkono (kuchukua). 3 -a muda mrefu, -a kukaa. ~ time no see (colloq as greetings) habari za siku nyingi/masiku. 4 (in phrases concerned with extent in time) ~

long

bond n (fin) mkataba wa miaka ishirini au zaidi. take a ~ cool/hard look at something fikiria kwa makini, fikiria kwa mapana na marefu. take the ~ view angalia mbali. in the ~ term kwa kuangalia mbali. ~ term attrib adj -a muda mrefu. 5 (compounds). ~ boat n mashua kubwa kuliko zote melini. ~bow n upinde mrefu. draw the ~bow tia chumvi, piga chuku. ~ distance attrib adj -a masafa marefu a ~-distance runner (athletics) mkimbiaji wa masafa marefu. ~ drink n kinywaji kinachoandaliwa kwenye bilauri kubwa k.m. bia. a ~ dozen n kumi na tatu. ~hand n mwandiko wa mkono (ukilinganisha na hati mkato). ~-haired adj -enye nywele ndefu; (fig) -somi; -a sanaa; si -a kawaida. ~ headed adj -janja, erevu; -enye kuona mbali (kwa mawazo). the ~ jump n (athletics) kuruka chini. ~ metre n ubeti wenye mistari minne yenye silabi nane. ~ odds n pl (in betting) -siowiana kabisa, -a kupishana sana. ~ play(ing) disc/record n (abbr LP) sahani ya santuri ndefu. ~range attrib adj -a muda mrefu/masafa marefu. ~ shore-man n kuli. ~ sighted adj -a kuona mbali; -enye kufikiri mbele. ~ time attrib adj -a muda mrefu. ~ ton n ratili 2240. ~ wave n mawimbi ya masafa marefu. ~-winded adj -refu na -a kuchosha (katika mazungumzo/maandishi), -enye maneno mengi. n 1 muda mrefu, kipindi kirefu the experiments will take ~ majaribio yatachukua muda mrefu. at the ~est sanasana; muda mrefu kabisa I can wait three days at the ~est siwezi kungoja zaidi ya siku tatu. the ~ and the short of it hali ya jumla; yote yanayohitajiwa kusemwa. 2 (esp in Latin) silabi ndefu adv 1 (for) ~ (kwa) muda mrefu. as/so ~ as (conditional) mradi you may lend me some money as ~ as you do not attach strings

look

to it unaweza kunikopesha pesa mradi huweki masharti yoyote. 2 (in numerous compounds) ~-drawn out adj -liorefushwa (bila sababu). ~lived adj -lioishi sana, -enye maisha marefu. ~standing adj -liodumu muda mrefu, -a muda mrefu (bila kutimizwa). ~-suffering adj -stahamilivu. 3 muda mrefu, zamani. ~ ago zamani sana ~ after her wedding muda mrefu baada ya ndoa yake. 4 (with n indicating duration) -zima, -ote all day ~ siku nzima; mchana kutwa all my life ~ maisha yangu yote. 5 no/any/much ~er zaidi (ya muda fulani), tena I cannot wait any ~er siwezi kungoja zaidi she is no ~er working here hafanyi kazi hapa tena hivi sasa. ~evity n maisha marefu. ~itude n longitudo. ~itudinal adj 1 -a longitudo. 2 -a kukata kwa urefu. ~ways; ~wise adv see lengthways.

long2 vi ~ for something/for somebody to do something tamani sana. ~ing n hamu, shauku adj -enye (kuonyesha) hamu/shauku the children are ~ing for a break watoto wanatamani sana kupumzika. ~ing eyes n macho yaonyeshayo hamu/shauku (hasa ya mapenzi). ~ingly adv.

loo n (GB colloq) msala.

loofah, loofa n dodoki.

look vi,vt 1 ~ (at) tazama, angalia. to ~ at him/it etc. (in passing judgement) ukimwangalia kwa nje. L~ before you leap (prov) tahadhari kabla ya kufanya jambo. ~ing glass n kioo (cha kujitazamia). ~ somebody/something in the eye(s)/face angalia mtu usoni; kabili. 2 onekana ~ ill onekana mgonjwa ~ oneself onekana kama kawaida ya mtu alivyo. ~one's age lingania/oana na umri wake you don't ~ your age huonekani kuwa mzee kiasi hicho. ~ one's best pendeza she ~s her best in skirts anapendeza akivaa sketi. ~black

look

(at) angalia kwa hasira. ~ blue sononeka; nuna. ~ good pendeza vutia; onekana kuwa na maendeleo mazuri. good~ing adj -enye sura/umbo la kupendeza. ~ small onekana duni. L~ alive! Changamka! L~ here! Sikiliza! Angalia! L~ sharp! Changamka! Fanya haraka! ~ well (of persons) onekana mwenye afya njema; (of things) onekana -a kupendeza, vutia; (of a person wearing something) pendeza. 3 ~ like/as if onekana kama, elekea it ~s like we will win inaelekea tutashinda. 4 angalia ~ where you are going angalia unakokwenda! 5 onyesha (kwa sura). 6 (uses with adverbial particles and preps) ~ about (for something) tafuta; angalia kwa makini, chunguza. ~ about one fanya uchunguzi ~ after somebody/something tunza; sindikiza kwa macho. ~ at something (special uses) not ~ at something (usu with

will, would) -toangalia, -tofikiria; -tochunguza; (in polite requests) angalia. good/bad etc. to ~ at -enye sura ya kupendeza/kuchukiza n.k,. onekana vizuri, vibaya n.k. ~ away (from something) kwepesha macho. ~ back (on/to something) (fig) tazama nyuma, kumbuka ya nyuma. never ~ back usirudi/tazame nyuma; endelea (bila kukatishwa). ~ down on somebody/something (colloq) angalia kwa dharau/chuki. ~ for somebody/something tafuta; tarajia it is too early to ~ for results ni mapema mno kutarajia matokeo. ~ forward to something ngojea kwa hamu/shauku. ~ in (on somebody) tembelea (mtu) kwa muda mfupi. give somebody/get a ~-in (colloq, sport, etc.) toa/pata nafasi, fursa (ya kushinda n.k.) you won't get a ~- in with such strong competition hutapata fursa ya kushinda/huwezi kushinda katika ushindani mkali namna hiyo. ~ into something chunguza;

look

peleleza; soma kwa kupitia (kitabu n.k.); angalia ndani ya kitu. ~ on -wa mtazamaji, tazama, ~er on n mtazamaji. ~ on/upon somebody/something as ona kama do you ~ on him as an authority on biology? unamwona kama bingwa wa biolojia? ~ on/upon somebody something with ona mtu/jambo kuwa ni he seems to ~ on me with distrust anaelekea kutoniamini. ~ on to elekea the hotel room ~s on to the beach chumba cha hoteli kinaelekea ufukoni. ~ out (of something) (at something) tazama. ~ out on (to)/over elekea. ~ out (for somebody/something) jihadhari, -wa macho -wa tayari kwa. L~ out! Tahadhari! ~-out n keep a good ~-out (for); be on the ~-out (for) -wa mwangalifu, -wa macho; (mil) mahali pa kulindia, ulingo; mlinzi (sing only) (prospect) jambo la kutarajiwa, matarajio that's your own ~ out! shauri yako! ~ something out for somebody chagulia mtu kitu (baada ya kukichunguza). ~ over something kagua, chunguza. ~ something over kagua sehemu mojamoja. ~-over n ukaguzi. ~ round (fig) angalia uwezekano (kabla ya kufanya jambo); geuza kichwa (kuangalia kila upande). ~ round (something) tembelea/zungukia mahali, (ili kuangalia). ~ through something durusu. ~ something through kagua kitu kwa makini. ~ to something chunga, angalia. ~ to somebody for something/to do something tegemea mtu kwa jambo/ kwa ajili ya kufanya jambo. ~ to/towards elekea. ~ up angalia juu; tengemaa, ongezeka bei au ufanisi. ~ something up tafuta kitu kitabuni n.k. ~ somebody up tembelea mtu. ~ somebody up and down kagua mtu; tazama (mtu) kwa dharau. n 1 mtazamo, kutazama let me have a ~ at your leg hebu

loom

nitazame mguu wako. 2 sura, kuonekana. give something/get a new ~ -pa/pewa sura mpya. 3 (pl) sura (ya mtu). ~er n a good ~er mtu mwenye sura nzuri.

loom1 n kitanda cha mfumi.

loom2 vi (large) onekana kama

-kubwa (kwa kutisha); (fig) tisha (kwa kufikiriwa kubwa).

loon n (Scot and arch) mjinga, mkunguni. ~y n, adj (sl) -enye kichaa, wazimu he is a ~y ana wazimu. ~y bin n (sl) nyumba/ hospitali ya wendawazimu.

loop n 1 kitanzi, kishwara; (colloq)

(contraceptive) kitanzi. 2 (also ~line) reli au waya wa simu wa mzingo. 3 mzingo (unaofuatwa na ndege au pikipiki) wenye umbo la kitanzi. 4 pindo katika herufi. vt,vi 1 piga kitanzi. 2 pinda ili kufanya umbo la kitanzi. ~hole n 1 kitundu (cha kupenyezea bunduki, kuangalia, kupitishia hewa n.k.). 2 (way of escape) mwanya, njia ya kuokoka.

loopy adj (sl) -enye wazimu, kichaa.

loose adj 1 (unfastened) -liofunguka,

-lioachwa (huru), -lioachiwa. break/ get ~ funguka; jitoa kifungoni, toroka. let something ~ achia huru. ~box n sehemu katika zizi/behewa ambayo humwezesha farasi kutembea tembea). ~leaf attrib adj (of a notebook) -siounganishwa, -siofungwa. 2 (not tight) -siokazwa, -a kupwaya, -liolegea a ~ tooth jino linalolegea. come ~ legea. have a screw ~ (colloq) fyatuka akili, -wa na kasoro kichwani. have a ~ tongue ropokaropoka. have ~ bowels endesha, harisha. ride with a ~ rein achia farasi huru; (fig) achia mtu (afanye apendavyo); (of a bolt etc) legea. 3 -siofungika vizuri. at a ~ end (fig of a person) -wa bila shughuli, kutojua la kufanya. 4 (of talk, behaviour etc). -potovu, -baya. (be) on the ~ -wa fisadi. play fast and ~ (with somebody) chezea, ghilibu, danganya. 5 -sio sahihi; -

lorgnette

siofuata taratibu. 6 (of the human body) -sioshikana vizuri, -siopangwa vizuri. 7 -legelege, zembe. vt 1 legeza. 2 achia huru. vt,vi ~n (up) 1 fungua; fumua; legeza. 2 (of soil) chimbua, tifua.

loot vt,vi pora, teka nyara. n mali iliyoporwa; mateka; nyara; kuteka nyara. ~er n mporaji, mteka nyara.

lop1 vt ~ (away/off) kata; pogoa; punguza matawi.

lop2 vi (chiefly in compounds) ning'inia. ~ eared adj -enye masikio yanayoning'inia. ~ sided adj -a kwenda upande.

lope vi tembea/ruka kwa hatua kubwa

(k.v. sungura). n hatua za kuruka.

loquacious adj -enye domo, -enye maneno mengi, -semaji, -limi. ~ly adv. ~ness n. loquacity n.

lord n 1 mtawala mkuu (wa kiume) our

sovereign ~ and king mfalme mtawala wetu. 2 the L~ n Mungu, Mwenyezi Mungu, Mola; Bwana. L~! Good L~! L~ knows! Yarabi! Our L~'s Bwana Wetu Yesu Kristu the L~'s Day n siku ya Bwana, Jumapili. the L~'s Prayer n sala ya Bwana, Baba Yetu. L~'s Supper n Ushirika Mtakatifu. 3 (peer, nobleman) lodi, mwungwana; gabi. as drunk as ~ -liolewa chakari. House of L~s n Baraza la Malodi (Uingereza). 4 (in feudal times) bwana, mwinyi. 5 (joc,also ~ and master) mume; kiongozi wa tasnia the ~s of creation binadamu. 6 mtu mwenye cheo/madaraka. 7 Mheshimiwa. My ~ Mheshimiwa vt (chiefly in) ~ it over somebody tawala/ongoza kimwinyi. ~ly adj 1 -a heshima; -a fahari. 2 (arrogant) -a kama mwinyi; -enye kiburi. ~liness n. ~ship n 1 ~ over n utawala, miliki, mamlaka. 2 His/Your ~ship Mheshimiwa, Bwana.

lore n elimu, maarifa ya mapokeo.

lorgnette n miwani yenye mpini (ishikwayo mkononi).

lorn

lorn adj (poet of hum) pweke.

lorry n lori.

lose vt,vi 1 poteza ~a knife poteza kisu ~ weight konda. ~ one's cool (colloq) hamaki; haha. ~ in choka na, -tovutwa tena na. ~ one's reason/senses pata wazimu, pandwa na jazba. ~ one's temper kasirika. ~ A to B nyang'anywa/pokonywa A na B. 2 (passive) potea, -fa, they were lost in the forest walipotea msituni. be lost to -toathiriwa na kosa, -tosikia he is lost to shame hasikii, hana aibu. be lost in shikwa/jawa na (mawazo, mshangao n.k.) be lost in astonishment shangaa, shikwa na mshangao be lost in thought zama katika mawazo. 3 poteza. ~ one's place (in a book etc.) poteza. ~ oneself/one's way potea. ~ sight of sahau, -tozingatia, -toweza kuona he lost sight of the fact that alisahau kwamba. 4 chelewa. 5 kosa kuona/kusikia n.k. lost the last part of the speech sikusikia sehemu ya mwisho ya hotuba. 6 kosesha your obstinacy will ~ you your job ujeuri wako utakukosesha kazi yako. 7 shindwa we lost the match tulishindwa katika pambano a lost cause jaribio/tendo ambalo limeshindwa/litashindwa tu. (play) a losing game (cheza) mchezo wa kushindwa ~-out to rithiwa na. 8 ~ by/in/on something haribikiwa, pata hasara the story does not ~ in the telling hadithi haipotezi utamu katika kusimulia. 9 (of a watch etc.) chelewa, poteza majira. 10 poteza bure (muda, juhudi, nafasi n.k.) I shall ~ no time in doing it nitaifanya mara moja be lost on shindwa kushawishi/kuvutia my arguments were not lost on him hoja zangu

zilimwingia. 11 ~ oneself in something (reflex) zamia, jisahau he lost himself in his work alijisahau katika kazi yake. ~r n 1 mshinde. loss n kupotea; upotezaji; kupotewa loss of blood kupoteza damu loss of

lotus

expectation of life kupoteza matazamio ya uhai loss of memory kupotewa na kumbukumbu we retired without loss of life tulirudi bila mtu kuuawa. 2 msiba; maangamizi. 3 hasara insure against loss katia bima za hasara total loss hasara tupu loss leader (comm) bidhaa inayouzwa kwa bei ndogo ili kuvutia wateja. 4 kukosa, kushindwa kupata the loss of a contract kukosa mkataba. 5 kipunguo, hasara be a ~ deal (of a person) -wa bure/hasara tupu. 6 (in expressions) be at a loss changanyikiwa, tatanika; -tojua (la kufanya/kusema).

lot1 n (colloq) 1 the whole ~; all the ~ idadi yote, -ote. 2 a ~ (of); ~s (and ~s) -ingi a ~ of people watu wengi, umati wa watu a good ~ -ingi -a kutosha quite a ~ -ingi -a kutosha. 3 (used adverbially) sana he is a ~ better today anajisikia afadhali sana leo.

lot2 n 1 bahati nasibu. draw/cast ~s piga kura (kwa kuokota karatasi kutoka kwenye kasha). 2 the ~ n uamuzi/uchaguzi unaotokana na bahati nasibu it fell to my ~ iliniangukia. 3 bahati (ya mtu). cast/throw in one's ~ with somebody amua kushirikiana na. 4 namba ya kitu katika orodha ya vitu vinavyouzwa kwa mnada. 5 fungu la vitu vinavyofanana. 6 a bad ~ (colloq) mtu mbaya. 7 sinema, studio na uwanja unaoizunguka (esp US) kiwanja a parking ~ mahali pa kuegeshea magari a vacant ~ kiwanja cha kujengea. ~tery n bahati nasibu. ~tery ticket n tikiti ya bahati nasibu (fig) is marriage a ~tery? Je, ndoa ni bahati nasibu? ~ to n mchezo wa bahati nasibu; bingo; tombola.

loth see loath.

lotion n losheni.

lotus n yungiyungi (la Misri na Asia). ~ eater n mpenda starehe, mtu anayejitumbukiza katika anasa.

loud

loud adj 1 -enye sauti kubwa, -a makelele; -a kusikika kwa urahisi a ~ speech hotuba yenye kusikika kwa urahisi; kubwa. ~-hailer n kipaza sauti. ~-speaker n kipaza sauti, bomba. 2 (of behaviour, colours) -a kujitangaza, -a mvuto adv kwa sauti kubwa. ~ly adv. ~ness n.

lough n (in Ireland) mkono wa bahari, ghuba; ziwa.

lounge vi kaa, simama (kwa kujiegemeza)/kivivu; jikalia, tandawaa. ~r n mtu akaaye/ asimamaye namna hii. n 1 kukaa/ kusimama kivivu. 2 ukumbi, sebule (agh. katika hoteli) wa kupumzika. ~ suit n suti (ya kiume). ~ chair n kiti cha kupumzikia. ~ lizard n (dated sl) mwanamme ambaye analipwa kwa kucheza dansi na wanawake kwenye mahoteli. ~-bar n baa nzuri katika nyumba ya vileo.

lour;lower vi 1 ~ at/on/upon nuna, onekana na hasira. 2 (of the sky, clouds) -wa zito sana. ~ ingly adv

louse n chawa. (sl) lousy adj -enye chawa; (colloq) -baya, -ovyo a lousy trick hila mbaya; (sl) -ingi be lousy with money -wa na fedha nyingi, jaa kishenzi.

lout n baradhuli. ~ ish adj.

louvre;louver n luva. ~d adj.

love n 1 upendo, mapenzi, huba a mother's ~ for her children mapenzi ya mama kwa watoto wake. give/ send somebody one's ~ tuma salamu (zenye upendo). play for ~ cheza kwa kujifurahisha tu. not to be had for ~ or money -sioweza kupatikana (kwa njia yoyote). there is no ~ lost between them hawapendani. a labour of ~ kitu mtu anachofurahia kufanya; kumfanyia mtu kitu kwa sababu ya upendo. for the ~ of (in appeals etc) kwa jina la..... ~feast n (rel) karamu ya pamoja (iliyoadhi- mishwa na Wakristo wa zamani kudumisha upendo); ibada ya pamoja. 2 mapenzi, mahaba. be in ~ (with

love

somebody) penda mwanamke/ mwanamme John is in ~ with Mary, John anampenda Mary. fall in ~ (with somebody) penda mwanamke/mwanamume. make ~ (to somebody) lala; jamiiana, fanya mapenzi; onyesha kupendana na. 3 (compounds) ~ affair n uhusiano wa kimapenzi. ~ bird n kasuku mdogo; (pl) watu waliopendana sana. ~-child n mwanaharamu. ~-knot n fundo mapenzi. ~-letter n barua ya mapenzi. ~-lorn adj -a simanzi (agh. kwa kumkosa mpenzi); -a kunyong'onyea (agh. kutokana na mapenzi). ~-making n kujamiiana (na mambo yote yanayohusiana na kitendo hicho). ~-match n ndoa itokanayo na mapenzi tu. ~-philtre/-potion n dawa ya mapenzi. ~-seat n benchi mfano wa S yenye sehemu mbili za kukalia zilizopeana migongo. ~-sick adj -a simanzi, nyong'onyevu (kwa sababu ya mapenzi). ~sickness n ugonjwa wa mahaba. ~-song n wimbo wa mapenzi. ~-story n hadithi ya mapenzi/huba. ~-token n hidaya. 4 (colloq) mpenzi, kipenzi (agh. mke, mme, au mtoto) come here my ~ njoo hapa kipenzi changu. 5 mpenzi. 6 (in games) bila, bure. ~ all bila bila; hakuna bao pande zote. ~less adj -siopenda; -siopendwa; pasipo penzi. vt 1 penda ~ one's parents penda wazazi. 2 abudu. 3 (colloq) penda sana; furahia. lovable adj -a kupendeka. ~ly adj 1 -zuri sana, -a kupendeza; -a kufurahisha. 2 (colloq) safi, -a kuchangamsha, -a kuburudisha what a ~ly meal! chakula safi sana. ~liness n. ~r n 1 mpenzi they are ~rs ni wapenzi. 2 (of music, football etc.) mpenzi, shabiki. ~like adj -enye mapenzi. loving adj -enye upendo. ~-cup n bilauri/kata ya pombe (ambayo huzungushwa kwa zamu kutoka mnywaji mmoja hadi mwingine). ~-kindness n wema,

low

huruma, (of God) rehema. lovingly adv.

low adj 1 -a chini; fupi a ~range of hills vimilima vifupi. ~ shoe n kiatu kisicho cha mchuchumio. ~-lying land n nyanda za chini. 2 -a chini ya (usawa wa) kawaida. ~ tide/water n maji kupwa. ~-water mark n alama ya chini kabisa, mwisho mwa kupwa. be in ~ waters (fig) wamba. 3 (of sounds) -a chini ya pole; -a kunong'ona speak in a ~voice ongea kwa sauti ya chini; nong'ona. ~-keyed adj (fig) -sio makeke. ~-pitched adj (music) -a sauti ya chini. 4 (of people) -a tabaka duni/la chini; nyonge men of ~ birth watu wa tabaka duni. be brought ~ dhalilishwa. 5 shenzi ~ manners tabia za kishenzi. ~ life n maisha ya kishenzi. 6 dhaifu, nyonge he is in a ~ state of health afya yake imedhoofu. be in ~ spirits sononeka; -wa nyonge; -tochangamka. ~spirited adj. 7 (of a supply of anything) be/run ~ punguka, karibia kwisha, -wa haba food supplies are running ~ in this town, kuna uhaba wa chakula mjini hapa; -a kiasi kidogo, -dogo, a chini. 8 (of amounts) ~ prices bei za chini. ~ latitudes n latitudo karibu na Ikweta. have a ~ opinion of somebody -tomthamini. L~ church n waumini (wasiopenda utawala msonge na ulibwende katika kanisa). L~ churchman muunga mkono. 10 (phrases) bring/lay somebody/ something ~ dhoofisha; (bankrupt) filisisha; fedhehesha; dunisha. lie ~ (fig) kaa kimya; fichama. 11 (compounds) ~-born adj -a koo duni. ~-bred adj -enye tabia za kishenzi, -siostaarabika. ~brow n adj (person) -siosomi, -siopendelea mambo ya kitaaluma, hasa sanaa. ~er case n (in printing) herufi ndogo. L~er Chamber/House n Bunge (la kutunga sheria). ~ comedian n chale kwenye

lucerne

kichekesho. ~ comedy n vichekesho. ~er deck n (in the navy) baharia wa kawaida. ~-down adj (colloq) -a kishenzi, -a fasiki. give somebody/get the ~ down (on something/somebody) (colloq) toa/ fahamu siri juu ya jambo/mtu. ~lander n mkazi katika nyanda za chini. ~ lands n (pl) (maeneo yaliyo katika) nyanda za chini. L~ Latin n Kilatini kisichosanifu (kikilinganishwa na Kilatini kikongwe). L ~ Mass n Misa ndogo (agh. iendeshwayo bila ya nyimbo). L~ Sunday/Week n Jumapili na Wiki mara baada ya Pasaka. L~ermost adj -a chini kabisa. L~ness n. ~adv chini buy ~ and sell high nunua kwa bei ya chini uza kwa bei ya juu. n kitu, jambo, hali ya chini. ~er vt,vi 1 shusha, teremsha; inamisha ~er a flag teremsha bendera. L~er away (naut.) teremsha/shusha (mtumbwi, nanga, tanga n.k.). 2 punguza ~ er the rent of a house punguza kodi ya nyumba. 3 ~er oneself -tojiheshimu, jishushia hadhi, jidhalilisha. 4 dhoofisha. ~ly adj duni, -a hali ya chini. ~liness n.

lower vi see lour.

loyal adj -aminifu; -tiifu. ~ist n

mwaminifu (kwa mkuu wa serikali). ~ly adv. ~ty n 1 uaminifu. 2 (pl) aina za mahusiano, uwajibikaji, utiifu.

lozenge n 1 pipi/peremende ya kifua. 2 msambamba; (of playing cards) uru, kisu.

LSD n dawa kali ya kulevya.

Ltd see limited.

lubber n mtu mzito.

lubricate vt 1 lainisha, legeza kwa mafuta. 2 (fig) rahisisha kufanyika kwa jambo. lubricant n mafuta ya kulainisha. lubrication n kutia mafuta, ulainishaji.

lucent adj (liter) 1 -angavu, -a kung'ara. 2 -eupe.

lucerne n luserini: majani ya kulisha

lucid

ng'ombe (US alfalfa).

lucid adj 1 -a kufahamika kwa urahisi, wazi, dhahiri. 2 -enye akili timamu ~ interval wakati wa mzinduko. 3 (poet) -angavu, -eupe. ~ly adv. ~ity n uangavu, weupe, udhahiri.

Lucifer n 1 shetani, ibilisi. 2 zuhura.

luck n 1 bahati, nasibu, sudi. as ~ would have it kwa bahati mbaya/ nzuri. bad ~ n bahati mbaya, shari, kisirani, nuksi. bad~ pole! bahati Mbaya! out of ~ -enye bahati mbaya better ~ next time bahati njema safari ijayo good ~ kisimati he is in ~ ana bahati nzuri; anapendelewa, ameneemeka good ~ (to you) nakutakia mafanikio/kila la kheri it's just my ~ nina mkosi/nuksi. be down on one's ~ (colloq) -wa na bahati mbaya, -wa na matatizo, -wa na nuksi try one's ~ bahatisha worse ~ kwa bahati mbaya. ~less adj -enye kisirani. ~y adj -enye bahati, -a bahati njema, -a heri. be ~y wa na bahati nzuri, bahatika he 's a ~y dog! ana bahati njema! how ~y bahati nzuri. ~ily adv.

lucrative adj -a kuleta faida, -enye faida.

lucre n (in a bad sense) fedha, faida,

mali; (filthy) ~ fedha iliyopatikana kwa njia mbaya for filthy ~ kwa hela tu.

ludicrous adj -a kuchekesha, -puuzi, -a mzaha; pumbavu.

ludo n ludo: aina mojawapo ya michezo ya kutumia dadu/kete.

luff n (naut.) mbele ya tanga. vt,vi (naut) bisha.

lug vt kokota, burura, buruta. n mkokoto, mbururo.

luge n (Fr) luji: gari telezi katika theluji.

luggage n mizigo. ~ carrier n uchaga wa mizigo. ~-rack n kichaga cha mizigo kwenye basi au treni. ~-van n behewa la mizigo.

lugger n chombo chenye tanga la pembe nne.

lugsail n (naut.) matanga pembe nne.

lunacy

lugubrious adj (formal) -a majonzi,

-zito. ~ly adv. ~ness n.

lukewarm adj 1 (of liquids etc) -a uvuguvugu, fufutende. 2 (fig) be ~ vuvuwaa. ~ly adv. ~ness n.

lull vt, liwaza, bembeleza, tuliza. n utulivu. ~aby n wimbo wa kubembeleza mtoto; sauti nyororo zitokanazo na upepo au mawimbi.

lumbar adj -a kiuno. ~lumbago n maumivu ya kiuno.

lumber1 n 1 (GB) makorokoro. ~

room n chumba cha kuhifadhia makorokoro. 2 (timber) mti; mbao; magogo. ~man; ~jack n mkataji miti, mpasua mbao. ~ mill n kiwanda cha mbao. vt ~ something (up) (with) jaza makorokoro (takataka n.k.).

lumber2 vi enda kwa kishindo, -wa zito the army tanks ~ed past vifaru vya jeshi vilipita kwa kishindo.

luminous n 1 -a kung'aa ~paint rangi ya mng'ao. 2 (fig) dhahiri, wazi; -a kufahamika kwa urahisi. ~ity n. luminary n 1 jua, mwezi, nyota, kitu kingaacho angani. 2 (fig) mtu mashuhuri (kwa usomi au maadili yake).

lummy;lumme (GB sl.) lahaula!

lump1 vt (only in) ~ it (colloq) vumilia

jambo, mezea if you don't like it you can ~it upende usipende inakupasa kumezea.

lump2 n 1 bonge, fumba; jumla. ~ sum n malipo yote (kwa pamoja). in the ~ kwa bunda, kwa jumla, kwa pamoja. ~ sugar n sukari ya kibonge. 2 uvimbe mwilini. a ~ in the throat msongo wa moyo, donge. 3 (colloq) mtu mnene na mzito. vt,vi ~ together 1 tia pamoja, changanya; jumuisha. 2 budaa. ~ish adj (of a person) fupi na nene, bongebonge; pumbavu; zito. ~y adj -liobudaa, -enye mabongebonge; (of water) -enye viwimbi.

lunacy n 1 wazimu, kichaa, umajinuni. 2 (pl) matendo ya kichaa. lunatic n kichaa, majinuni. lunatic asylum n

lunar

hospitali ya kutibu vichaa adj -enye kichaa. lunatic fringe n kundi la watu wachache wenye siasa/mawazo makali, wenye vitendo vya ajabu.

lunar adj 1 -a mwezi a ~ month mwezi unaofuata kuandama kwa mwezi. 2 -a umbo la mwezi mwandamo. ~ module n njia ya chombo kinachozunguka na kutua mwezini. ~ orbit n kuzunguka mwezi.

lunch n chakula cha mchana vt,vi 1 -la chakula cha mchana. 2 karibisha kwa chakula cha mchana. (formal) ~eon n.

lung n 1 pafu, buhumu; (of animal) yavuyavu. ~ish n kambaremamba. ~ power n nguvu ya sauti. 2 (fig) eneo wazi/uwanja karibu na jiji.

lunge n mwendo/mrukio wa ghafla mbele. vi enda/rukia (k.m. kwa lengo ya kupiga) ~ forward enda/rukia mbele ~ out at somebody lenga kupiga mtu ghafla.

lurch1 n msepetuko. vi sepetuka, enda mrama, pepesuka; (naut) lalia/elemea upande mmoja.

lurch2 n (only in) leave in the ~ acha katika shida.

lure vt vuta, shawishi; tega. n 1 (bait) chambo. 2 (attraction) mvuto, kishawishi.

lurid adj 1 -a rangi za kuwaka. 2 (fig)

-a kutisha, -a kuogofya. ~ly adv. ~ness n.

lurk vi jificha, jibanza, vizia ~ing place n mafichoni.

luscious adj 1 tamu sana; -enye harufu

nzuri. 2 (of the arts) -enye madoido sana.

lush adj 1 (of vegetation) -a kusitawi sana. 2 -a anasa. n (us. sl.) mlevi.

lust n ashiki, hawaa; tamaa. vi ~ after/for tamani ~ after a woman tamani mwanamke. ~ful adj. ~fully adv.

lustre;luster n 1 mng'aro. 2 (fig) sifa, heshima, fahari. lustrous adj.

lusty adj -a nguvu, -enye afya njema/ siha. lustily adv.

lysol

Lutheran adj 1 -a Kilutheri, -a mfuasi

wa Luther n Mlutheri.

luxuriant adj 1 -a kuota sana, -a kusitawi sana, tele. 2 -liopambwa sana, -a ufasaha. luxuriance n.

luxury n 1 anasa. 2 (attrib) -a anasa. ~ hotel n hoteli ya anasa. 3 (rare pleasure) tunu. luxuriate vi (in) furahia, jistarehesha. luxurious adj 1 -a anasa; -a tunu. 2 -enye kustarehesha/kuanisi. 3 tele. luxuririously adv. luxuriousness n.

lycee n shule ya sekondari Ufaransa.

lyceum n (U.S) ukumbi (wa mikutano, maonyesho n.k.).

lye n maji magadi.

lying see lie2 adj -nayolala. n kulala. ~-in n kuzaa.

lymph n limfu ~ glands tezi za limfu. ~atic adj 1 -a limfu. 2 (of person) tepetepe, zito. ~ fluid n giligili ya limfu ~ system mfumo wa limfu.

lynch vt ua kiholela (agh kwa kunyonga na bila nafasi ya kujitetea) the crowd ~ed him kundi la watu lilimuua. ~ law n kunyonga bila kufuata sheria.

lynx n linksi: pakamwitu mwenye macho makali sana. ~-eyed adj -a macho makali sana.

lyre n kinubi.

lyric n 1 shairi la hisia. 2 (pl) maneno ya wimbo. ~al adj 1 -a shairi la hisia. 2 -enye kusisimka, -liojaa shauku. ~ist n mtunzi wa (maneno ya) nyimbo.

lysol n dawa ya mafuta inayotumika

kama kidhurubakteria na kiuavijidudu.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.