TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

Mm n herufi ya kumi na tatu katika alfabeti ya Kiingereza; alama ya Kirumi yenye maana ya elfu moja.

ma (colloq abbr of) mama

ma'am n bibie.

mac see mackintosh.

macabre adj -a kutisha; -a kuashiria kifo; uchuro. danse ~ n ngoma ya uchuro/kifo.

macadam n ~ road n barabara (iliyotengenezwa kwa maki kadhaa za mawe na changarawe). ~ize vt fanya barabara ya namna hiyo.

macaroni n makaroni: aina ya tambi.

macaroon n keki au biskuti ndogo iliyotengenezwa kwa sukari, yai na nazi/lozi.

macaw n aina ya kasuku wa Amerika Kusini (mwenye mkia mrefu).

mace1 n 1 rungu. 2 (of Parliament etc) fimbo, mesi. ~ bearer n (Parliament) mbeba fimbo/rungu a ceremonial ~ fimbo rasmi.

mace2 n (spice) basibasi.

macerate vt lainisha (kwa kulowesha majini), dhoofisha kuwa laini. maceration n.

Mach n (aviation) mechi. ~ number n uwiano wa mwendo wa ndege na mwendo wa sauti.

machete n panga, mundu.

machiavellian adj -erevu; danganyifu.

machination n njama, hila.

machine n 1 mashine, mtambo; (sewing) cherahani. 2 kikundi kinachoongoza chama cha siasa. 3 (of person) mtu atendaye bila kufikiri. ~ -gun n bombomu. ~-made adj -liotengenezwa kwa mashine. ~ tool n mashine ya samani. vt endesha mashine, fanya kitu kwa kutumia mashine. machinist n mtengeneza mashine, mwangalizi wa mashine. ~ry n 1 sehemu au vyombo vya mashine kwa jumla. 2 utaratibu (k.m. wa serikali, chama n.k.), urasimu.

machismo n ujana dume, udume.

mackerel n samaki wa jamii ya bangala. ~ sky n mawingu yenye mistari.

mackintosh n GB koti la mvua, mpira.

macro- (pref) -kubwa, -makro. ~ biotic adj -nayorefusha uhai. ~biotic food n chakula cha mboga asilia tu. ~cosm n ulimwengu, jumla.

macron n makroni: alama ya urefu (-) juu ya vokali.

mad adj 1 -enye wazimu, -enye kichaa. go ~ shikwa na wazimu, rukwa na akili. drive somebody ~ sumbua sana mtu a bit ~ punguani. as ~ as a hare/hatter kichaa kabisa. 2 -enye kutaharuki/jazba, -liojaa shauku, -enye mhemko. be/go ~ taharuki, hamaki, chukia sana. like ~ sana sana, mno. be ~ about somebody penda sana mtu. 3 -enye kukasirika, -enye hasira. be ~ about something kasirikia kitu/jambo. ~cap n mtu mwenye harara. ~ house n hospitali ya wendawazimu; (fig) ghasia nyingi, vurumai. ~ man/woman n mwendawazimu. ~ly adv kwa hasira nyingi, kwa wazimu. (colloq) ~ ness n wazimu; ujinga. ~den vt tia wazimu, kasirisha sana; kera sana.

madam n 1 bibi, mama. 2 (colloq) kuwadi wa kike (anayeongoza danguro). 3 (colloq) mwanamke/ msichana mpenda kuamrisha (watu).

madame n pl (sl) Bibi (hutumika mbele ya majina ya wanawake walioolewa).

madder n 1 (bot) mmea utoao rangi nyekundu. 2 rangi nyekundu (ya mmea).

made pt, pp of make.

mademoiselle n pl mesdemoiselle(s)

(Bi kwa wasichana au wanawake wasioolewa).

Madonna n (rel) Bikira Maria (sanamu au picha yake). ~ lily n lili (ua jeupe).

madrigal n 1 wimbo wa kupokezana. 2 shairi fupi la mapenzi.

maelstrom n 1 (fig) machafuko, fujo, msukosuko. 2 kizingia cha maji, chunusi.

maestro n bingwa wa muziki.

Mae West n (sl) koti la uokoaji

maffick

maffick vt sherehekea sana ushindi.

Mafia n Mafia: chama cha siri katika Sisilia, Italia na Marekani kinachopinga serikali halali na kujishughulisha na ujangili na ujambazi.

magazine n 1 ghala/bohari/stoo ya silaha na zana nyingine za vita. 2 chemba (ya risasi katika bunduki). 3 gazeti (agh la wiki/mwezi/mwaka).

magdalen n malaya aliyeongoka.

magenta adj -a rangi ya damu ya mzee

n rangi ya damu ya mzee.

maggot n 1 funza, buu. 2 (arch) matamanio. have a ~ in one's head -wa na wazo la ajabu.

Magi n Majusi, Mamajusi.

magic n 1 uchawi. as if by ~; like ~ -a kimaajabu, ajabu. black/white ~n uchawi/uganga. 2 (for finding offender) mburuga. 3 (conjuring) mazingaombwe, kiinimacho, mzungu. 4 (fig) mvuto adj -a uchawi, -enye uchawi. ~ eye n (colloq) kiongozea mbali, kiongoza toka mbali n.k. ~ lantern n projekta. ~al adj -a ajabu; -a mwujiza; -a kichawi. ~ally adv. ~ian n mchawi; mfanya mazingaombwe.

magistrate n hakimu, mwamuzi District ~ Hakimu wa Wilaya Resident ~ Hakimu mkazi. magistracy n uhakimu. the magistracy mahakimu kwa jumla. magisterial adj 1 -a hakimu, -a kihakimu. 2 -a nguvu, -enye mamlaka, -enye amri.

magnanimous adj karimu. ~ly adv. magnanimity n.

magnate n mkwasi: mtu tajiri sana. magnesium n (chem) magnesi. magnesia n magnesi ~ oxide oksidi ya magnesi.

magnet n 1 sumaku. 2 (fig) mtu/kitu kinachovutia. ~ic adj 1 -a sumaku. ~ic pole n ncha sumaku. ~ic field n ugasumaku. ~ic North n Kaskazini kisumaku. ~ic tape n ukanda/utepe wa sumaku. 2 -enye

nguvu ya kuvuta. ~ism n 1 nguvu ya sumaku; usumaku. 2 (fig) nguvu ya kuvuta; mvuto. ~ize vt tia sumaku; (fig) vuta (kwa ajili ya tabia, akili n.k.).

magneto n (tech) mashine ya umeme; magneto.

Magnificat n (rel) utenzi wa Maria.

magnificent adj -zuri kabisa, -tukufu,

-adhimu. ~ly adv. magnificence n.

magnify vt 1 kuza. 2 tia chumvi. 3 tukuza, adhimisha, sifu, kuza. magnifier n kiookuzi. magnification n ukuzaji, uadhimishaji.

magniloquent adj -a maneno; -a maneno ya fahari; shaufu, -piga domo. ~ly adv. magniloquence n.

magnitude n 1 (size) ukubwa. 2 (greatness) ukubwa, ubora, ukuu, cheo.

magnolia n mti wenye majani meusi na maua yanayong'aa na kunukia.

magnum n chupa kubwa ya mvinyo (nusu galoni).

magpie n 1 (bio) ndege wa jamii ya kunguru. 2 (fig) mpiga domo. 3 (fig) kijizi, mdokozi.

magus n see magi mnajimu.

Mahatma n (India) jina apewalo mtu mwenye heshima kuu (kutokana na mapenzi na utu wake).

mahogany n 1 mkangazi, mbambakofi. 2 (arch) meza ya kulia. 3 rangi ya mbambakofi.

maid n 1 mwanamwali, mwali, bikira. old ~ n mwanamke asiyeolewa. ~ of honour n mtumishi wa malkia au binti yake; mpambe wa Malkia/Bibi arusi; matroni. 2 (arch poet) msichana. 3 (house servant) mtumishi mwanamke. ~en n 1 (arch or poet) msichana, binti. 2 mwali, mwanamwali. 3 (hist) mashine ya kukata shingo adj 1 -a msichana/-a mwanamwali. 2 -a kwanza. ~en name n jina la ukoo (kabla ya kuolewa). ~en speech n hotuba ya kwanza Bungeni (kwa/Mbunge mpya). 3 -a bikira. 4 (compounds) ~en head n ubikira.

~en like; ~enly adj -a kibinti; -enye adabu, pole, tulivu.

mail1 n 1 barua za posta. ~ bag n mfuko wa barua za posta. ~ boat n meli ya barua. ~ box n (US letter box) sanduku la posta. ~ man n mtu anayepeleka barua. ~ order n ununuzi kwa posta. ~ train n gari moshi lenye behewa la posta. 2 posta. vt peleka kwa posta, postia. ~ing list n orodha ya watu wanaopelekewa matangazo n.k.

mail2 n (arch) daraya, nguo za pete za chuma. the ~ed fist n (tishio la) wanajeshi.

maim vt lemaza, atilisha (mguu, mkono, jicho n.k.) he was ~ed in the war alilemazwa vitani.

main1 adj (attrib only) 1 kuu ~ road

~idea wazo kuu, muhimu. 2 -ote, kubwa. do something by ~ force fanya jambo kwa nguvu zote. 3 (compounds) ~ deck n sitaha kuu. ~land n bara Tanzania ~ land Tanzania bara. ~ mast n mlingoti mkuu. ~ spring n spiringi kuu; kamani ya saa; (fig) kiini, chanzo hasa cha jambo. ~ stay n kamba itokeayo kwenye mlingoti mkuu hadi kwenye mlingoti wa mbele; (fig) tegemeo kuu, nguzo. ~ stream n mwelekeo tawala, mawazo ya walio wengi. ~ly adv kwa kiasi kikubwa, hasa.

main2 n 1 (often the ~s) bomba kuu (la maji, gesi); njia kuu ya umeme; bomba/mfereji mkuu wa maji machafu. ~ s set n redio ya umeme. 2 in the ~ kwa kiasi kikubwa, kwa jumla, aghalabu. 3 (poet) bahari.

maintain vt 1 dumisha, endeleza ~order dumisha amani ~ friendship dumisha urafiki. ~ an open mind on something wa tayari kusikiliza, kuzingatia maoni ya wengine. 2 (support) lisha, kimu, gharimia. 3 (assert) shikilia, sema, sisitiza; thibitisha. 4 tunza ~ roads tunza/ fanyia matengenezo barabara. 5 hifadhi, linda. ~able adj.

maintenance n 1 kukimu; matengenezo. maintenance order n (leg) amri ya kukimu mke, mtoto au mume (itolewayo na mahakama). maintenance gang/men n kikosi cha kufanya matengenezo ya barabara. retail price maintenance n udumishaji bei za rejareja.

maisonette n nyumba ndogo ya

ghorofa moja.

maize n 1 (plant) muhindi. 2 (grain) mahindi. 3 (cob) gunzi, kigunzi, kibunzi. 4 roasted ~ bisi. 5 (flour) unga wa mahindi; sembe; dona.

majesty n 1 ukuu wa enzi, utukufu, uadhama, ujalali/ujalalati. 2 your/his/her M ~ Mtukufu/jalali Mfalme, mtukufu, jalalati Malkia. majestic adj -adhimu, -tukufu, -a fahari. majestically adv

major1 adj 1 -kubwa, kuu, -enye maana zaidi ~ road barabara kuu ~ operation operesheni kubwa. ~ scale n (music) skeli kuu. vi ~ in something taalimikia somo fulani katika chuo kikuu ~ in linguistics taalimikia isimu.

major2 n 1 meja. ~ general n meja jenerali.

major-domo n mtumishi mkuu wa nyumba kubwa (agh ya mwana mfalme/mtawala/mfalme mdogo).

majority n 1 wingi, zaidi ya nusu. 2 a/ the ~ (of) walio wengi ~ judgement hukumu ya wengi. be in the ~ -wa zaidi ya nusu. a ~ verdict n uamuzi wa wengi. 3 (full age) umri wa utu uzima. attain one's ~ fikia utu uzima kisheria; pata umeja (cheo cha meja).

make vt,vi 1 ~ something from/(out) of something; ~ something into something tengeneza ~ a brick tengeneza tofali. ~ a boat unda boti. ~ a house jenga nyumba; (create) umba, huluku God made man Mungu alimuumba, alimhuluku binadamu; (of tea, coffee etc) pika ~ tea pika chai. show somebody/let somebody see what one is made of

make

be as clever etc as they ~ them -wa na akili sana. 2 chimba, toboa ~ a hole toboa/chimba shimo ~ a hole in the ground chimba shimo ardhini. ~ a hole in one,s finances mega/ punguza sana fedha. 3 tunga, weka the laws were made to protect people sheria zilitungwa kuwalinda watu. 4 fanya, sababisha (kufanyika kwa jambo) ~ a treaty fanya mkataba ~ a disturbance fanya fujo the news made him sad ile habari ilimsikitisha his jokes made us laugh masihara yake yalituchekesha. ~ one's hackles rise kasirisha. ~ one's hair stand on end tisha. ~ something go round fanya kitu kitoshe/kidumu. ~ oneself useful saidia. ~ it worth somebody's while (to do something) lipa. ~ do with something ridhika na. ~ do and mend mudu kwa kushikiza. 5 ~ believe jifanya, jisingizia. 6 kadiria, fikiria, chukulia how large do you ~ the audience unafikiria hadhira ni kubwa kiasi gani. 7 chukuana, enda pamoja; (of persons) -wa kufu ya Asha and Ali are made for each other Asha ni kufu ya Ali bread and butter are made to be eaten together mkate na siagi huliwa pamoja. 8 pata he ~s nine hundred shillings every day anapata shs 900 kila siku he made a name for himself alijipatia umaarufu. ~ a pile/packet (colloq) jipatia fedha nyingi sana. ~ one's living jipatia riziki. 9 (of games) funga; shinda. 10 (of the tide) anza the tide is making fast maji yanaanza kujaa kwa haraka. 11 fanikiwa. ~ or break/mar ama ushinde au uangamie. a made man mtu aliyefanikiwa. 12 lazimisha, shurutisha she made me drink beer alinishurutisha kunywa bia. 13 onekana kama, onyesha kama kwamba, fanya kuonekana kama. 14 lingana, -wa sawa na twelve things ~ a dozen vitu kumi na viwili ni sawa

na dazeni moja. 15 it ~ s sense! ni sawa. 16 -wa (in a series); mara this ~s the second time you are late umechelewa (tena) kwa mara ya pili sasa. 17 (colloq uses) safiri/enda kitambo. ~ it in time wahi, fika kwa wakati uliotakiwa. 18 chagua; teua he was made the Prime Minister aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu. 19 toa he made two proposals alitoa mapendekezo mawili. 20 ~ something of somebody/something; ~ something/somebody something fanya kuwa the coach wants to ~ them an excellent team kocha anataka wawe timu bora don't ~ smoking a habit usiwe na mazoea ya kuvuta sigara. 21 ~ (an) application (to somebody) (for something) omba. ~ arrangements for panga, fanya mipango. ~ a decision amua. ~ a guess at kisia. ~ an impression on vuta, vutia. ~ a request for omba. ~ a success of something fanikiwa. 22 (of arguments, evidence etc) lenga. ~ against dhuru, haribu, athiri. 23 (compounds) ~ shift adj -a muda. ~ up n mpangilio wa chapa/herufi, tabia, hulka; vipodozi. ~ weight n punje, kiasi kidogo cha kujazia; (fig) kitu cha thamani ndogo kinachojazia pengo. 24 (with adverbial particles and prepositions) ~ after somebody kimbilia; fukuza, fuatia. ~ at somebody fuata kwa hasira. ~ away with something -iba. ~ away with oneself jiua. ~ for somebody/ something elekea; changia. ~ off toroka. ~ off with iba na kutoroka. ~ something out elewa I couldn't ~ out her handwriting sikuelewa maandishi yake. ~ out that/~ somebody out to be dai. he ~s himself to be extremely wealthy anajidai ni tajiri sana. ~ out (with somebody) endelea, patana how are you making out with your new boss? unaendeleaje na mkuu wako mpya? ~ out a case

jenga hoja. ~ over badilisha, hamisha, hawilisha. ~ something up kamilisha we need one more player to ~ up the team tunahitaji mchezaji mmoja zaidi kukamilisha timu yetu; buni your reason for being late is made up sababu ya kuchelewa kwako ni ya kubuni tu; (colloq) patana (baada ya kugombana); unda, -wa na the committee is made up of ten people kamati ina watu kumi; tayarisha, tengeneza; ongeza mafuta ~ up a bed tandika kitanda. ~ somebody/ oneself up (ji)tayarisha (kwa mchezo n.k.) (ji)paka vipodozi. ~ up one's/somebody's mind fikia uamuzi juu ya jambo fulani. ~ up for fidia. ~ up for lost time harakisha (ili kufidia muda uliopotea). ~ up to somebody jipendekeza. ~ it up to somebody fidia mtu kwa kitu alichokosa au madhara/hasara aliyopata. ~ it up (with somebody) maliza uhasama/ugomvi. n 1 utengenezaji, mtindo these shoes are a good ~ viatu hivi vimetengenezwa vizuri. on the ~ (sl) -enye kutaka faida; (US sl) -enye kutongoza. 2 (elect) kutana, kamilisha (mzunguko). ~r n the/our M~r Muumba, Mungu; (esp in compounds) mtengenezaji, muundaji. making n 1 kufanya, kusitawi, kuendelea. be the making of sababisha kustawi be in the making tayarishwa. 2 have the makings of -wa na sifa za/zinazostahili he has in him the makings of a leader anazo sifa za kiongozi. 3 (pl) viambajengo; viambaupishi.

malacca n ~ cane n bakora.

malachite n malakati: jiwe lenye rangi ya chanikiwiti/kijani.

maladjusted adj -liorekebishwa visivyo; (of a person) -sioweza kujirekebisha kulingana na mazingira, -siochukuana na mazingira. maladjustment n.

maladroit adj -zito, -siostadi. ~ly adv.

~ ness n.

malady n ugonjwa, uele, maradhi.

malaise n uchovu, unyonge.

malapropism n matumizi mabaya ya maneno (hasa kwa kuyafananisha).

malapropos adj -siofaa kimatumizi/-ki wakati adv -sio kwa wakati, mahali pake.

malaria n malaria adj -a malaria. malcontent adj -sioridhika. n mtu asiyeridhika.

male adj 1 -a kiume. 2 (of parts/tools) dume: enye kuingia ndani ya nyingine. n (man). dume

malediction n laana, maapizo. maledictory adj -a laana.

malefactor n mwovu, mhalifu (k.m. mwizi, mwuaji n.k.).

maleficent adj -a kudhuru. maleficient n.

malevolent adj -enye nia mbovu/ mbaya, -a kukubuhu, habithi. ~ ly adv. malevolence n.

malfeasance n uhabithi; (leg) kutenda ubaya; tendo ovu/haramu (kinyume cha sheria).

malformation n hitilafu katika ujenzi/

uundaji/uumbaji. malformed adj -liolemaa, -enye kilema/hitilafu.

malfunction vi -wa na hitilafu/kasoro,

-totenda ipasavyo. n kasoro, kushindwa kutenda.

malice n ~ (towards) n uovu, kijicho, nia ya kudhuru wengine. ~ aforethought n uovu wa kudhamiria; kusudio la uovu. bear ~ to somebody onea mtu kijicho. malicious adj -ovu, -enye kijicho, -enye nia mbaya.

malign adj (of things) -a kudhuru. vt

singizia; sengenya; kashifu. ~ancy n 1 hali ya kuwa na uovu, ubaya, chuki. 2 (of disease) dhara; donda ndugu. ~ity n chuki kuu, uovu mkuu. ~ ant adj 1 (of persons) -enye nia mbaya. 2 (of diseases) -enye kudhuru/kuua ~ant disease ugonjwa unaoelekea kuleta kifo. ~antly adv.

malinger vi jisingizia kuugua, tega

mallard

~er n mtegaji.

mallard n bata mwitu.

malleable adj 1 -a kufulika/kubadilika umbo. 2 (fig) (of a person's character) -elekevu, -epesi kuongozwa. malleability n kufulika, kufulikana.

mallet n 1 nyundo ya mti. 2 rungu la kuchezea polo.

malnutrition n utapiamlo.

malodorous adj (formal) -a kunuka vibaya, -enye harufu mbaya.

malpractice n mwenendo mbaya; upurukushani kazini, kuzembea kazi/wajibu.

malt n kimea cha pombe ~ liquor pombe ya kimea. vt,vi (fanya) kuwa kimea. ~ star n mtengeneza kimea.

malthusianism n nadharia ya Malthus (kuwa idadi ya watu inaongezeka haraka zaidi kuliko uzalishaji mali).

maltreat vt onea; dhulumu. ~ment n uonevu; dhuluma.

malveration n (formal) matumizi mabaya (ya fedha za umma); ubadhirifu (wa fedha za umma).

mamba n black ~ n songwe. green ~ n hongo.

mamma/mama n (colloq) mama.

mammal n mamalia. ~ian adj -a mamalia.

mammary adj (bio) -a ziwa. ~gland tezi ya ziwa.

mammon n utajiri, ukwasi (unaofikiriwa kuwa na athari mbaya). M ~ n Mungu wa uchoyo/ulafi.

mammoth n mamothi: tembo wa kale adj kubwa mno.

mammy n 1 (child's word) mama. 2 (US derog) yaya mweusi wa watoto wa wazungu.

man n 1 (human being) mwanaadamu, binadamu. one's ~ of business wakala, wakili wake (mtu). 2 (individual person) mtu all men watu wote. a ~ about town mpenda starehe/kula maisha. ~ of the world mjuzi wa mambo ya ulimwengu. a new ~ aliyebadilika (tabia, nia). the ~ in the street mtu wa kawaida. a

~ of letters n msomi, mwandishi (wa vitabu, fasihi). the inner ~ n tumbo. old ~ n mzee. young ~ n mvulana, kijana. white ~n mzungu. I 'm your ~ nakubali shauri lako. best ~ n kungwi, mfuasi mkuu wa bwana arusi. every ~ for himself (and devil take the hindmost) kila mtu na wake. to a ~; to the last ~ wote. be one's own ~ wa huru, fanya utakalo. 3 mwanamume my young ~ mvulana wangu; mtu wa kiume! how can a ~ stand it? mtu awezaje kuvumilia? 4 (husband) mume they are ~ and wife wao ni mume na mke. 5 mtumishi wa kiume (jeshini, kazini, nyumbani). 6 (of chess) vipande. 7 (as a vocative) bwana listen ~ sikiliza bwana! 8 (in compounds) ~ at-arms n (middle ages) askari mpanda farasi. ~ eater n mlawatu. ~handle vt vurumisha; sogeza kwa nguvu, sukuma. ~-hater n siyependa wanadamu wanaume. ~-hole n shimo kwenye maungio ya bomba. ~hour n kazi inayofanywa na mtu mmoja kwa saa moja. ~-hunt n uwindaji (wa watu). ~-made adj -liyotengenezwa na watu. ~of-war n manowari. ~ -power n ikama: idadi ya watu wanohitajika (kiwandani, vitani n.k.); utumishi. ~ servant n mtumishi wa kiume. ~-sized adj kubwa; -a kufaa wanaume; -a kipimo cha mtu mzima. ~ slaughter n uuaji wa mtu bila makusudi. ~-trap n mtego wa kutegea watu. vt 1 toa/peleka, tia watu (kwenye amali); pakia wanamaji; wekea wanajeshi. 2 ~ oneself piga moyo konde. ~ful adj shupavu. ~fully adv. ~fulness n. ~hood n 1 utu uzima (wa mwanaume). 2 ujana-dume, urijali. 3 uanaume. ~ kind n 1 wanadamu. 2 (contrasted with womankind) wanaume. ~like adj -a kiume, -enye tabia (nzuri au mbaya) za kiume. ~nish adj 1 -a kiume. 2 (of

manacle

) -a kama mwanaume.

manacle n pingu. vt tia pingu.

manage vt,vi 1 ongoza; simamia;

(control) tawala, tiisha. 3 ~ (to do something); ~ (with/ without something/ somebody) weza; fanikiwa I could ~ another glass naweza kunywa gilasi nyingine. 4 (transact) fanya shughuli; (be in charge of) tunza I can ~ (do by myself) naweza we will ~ very well tutafaulu vizuri. ~able adj 1 -liowezekana. 2 (tractable) -a kutii, -tiifu; -sikivu. ~ment n 1 uongozi; menejimenti. 2 (skill) werevu, shauri la akili, mbinu. ~r n meneja. ~ress n meneja wa kike. ~rial adj -a meneja, -a uongozi, -a utawala.

manatee n nguva.

mandarin n 1 (hist) afisa wa juu katika serikali ya China. 2 Kichina sanifu. 3 mrasimu; kiongozi (agh mpinga maendeleo). 4 ~ duck n bata mdogo wa China. ~ orange n chenza; kangaja.

mandate n 1 amri, agizo; hukumu. 2 uwakili; mamlaka. 3 udhamini ~; government serikali ya udhamini. vt weka chini ya udhamini (wa). ~d adj 1 see mandate. 2 (of country) -a kudhaminiwa. mandatory n mtu, nchi iliyopewa uwakili, mamlaka, agizo au amri adj -a lazima mandatory injunction amri ya kutenda; amri ya kulazimisha/lazima.

mandible n 1 utaya. 2 (kwa ndege)

mandolin n gambusi.

mandragora n mandragora: mmea wenye sumu unaofanyiwa dawa ya kutapisha au ya usingizi.

mandrill n (bio) nyani mkubwa mkali wa Afrika ya Magharibi.

mane n manyoya ya shingoni (mwa mnyama k.v. farasi au simba); nywele za singa.

manes n (lat) mizimu (ya watu wa

maneuver n,v see manoeuvre.

manganese n manganizi.

mange n ugonjwa wa upele wa wanyama. mangy adj 1 -enye upele huu. 2 hafifu, -liochakaa, duni. mangily adv.

manger n hori.

mangle1 n guruto. vt gurutia, kamua

kwa guruto.

mangle2 vt 1 rarua, tatua, pasua. 2 (fig) (spoil) haribu (kwa kufanya makosa mabaya).

mango n (tree) mwembe; (fruit) embe; (large) dodo.

mangrove n mkandaa, mkoko, msindi ~ swamp bwawa la mikoko.

mania n 1 wazimu. 2 ~ (for) moyo wa kupenda sana; shauku kubwa, ushabiki mkubwa he has a ~ for dancing anapenda sana kucheza dansi. ~c n. ~cal adj. manic-depressive adj, n (mtu) anayefurahi na kuhuzunika kupita kiasi.

manicure n 1 utunzaji wa mikono na kucha. 2 tiba ya mikono na kucha. vt tunza kucha. manicurist n mtunzaji mikono na kucha.

manifest adj dhahiri, wazi, bayana. vt onyesha, toa wazi; dhihirisha; baini ~ oneself jidhihirisha, jionyesha, jitokeza n orodha ya shehena melini. ~ation n 1 onyesho, kufunua, kutoa wazi. 2 dalili, alama. ~ ly adv. ~o n manifesto: hati/ilani ya kutangaza sera, kanuni n.k.

manifold adj -a namna nyingi, -a mara nyingi. vt (US duplicate) rudufu. n bomba.

manikin n 1 kibete, kijitu, mbilikimo. 2 (figure) sanamu ya binadamu.

manila, n 1 ~ (hemp) katani, mkonge. 2 ~ paper/envolope n karatasi/bahasha ngumu. 3 biri la manila. 4 mji mkuu wa visiwa vya Philippine.

manioc n 1 muhogo. 2 wanga wa muhogo.

manipulate vt 1 fanya; endesha; tengeneza; tawala kwa ufundi. 2 (of persons) miliki/tawala kwa werevu au hila; chezea. manipulation n. manipulator n.

manna

manna n 1 (bible) mana: chakula walichopewa Wayahudi walipokuwa jangwani. 2 (fig) kitu kinachotolewa/ patikana bila matarajio; kiburudisho cha roho kisichotarajiwa.

mannequin n 1 mwonyesha mitindo; mwanamke anayeonyesha mitindo ya nguo. 2 sanamu ya kujaribia/ kuonyesha nguo.

manner n 1 njia; jinsi, namna. (as) to the ~ born fanya jambo kama mtu amezaliwa nalo. 2 (sing only) mwenendo. 3 (pl) tabia, adabu. comedy of ~s mchezo wenye kichekesho kuhusu tabia za (sehemu fulani ya) jamii; dhihaka (ya tabia/ desturi). 4 (literature/art) mtindo. 5 aina, namna. all ~ of kila aina ya. by no ~ of means kwa vyovyote vile. in a ~ kwa namna/kiasi fulani. in a ~of speaking kwa namna fulani. ~ed adj 1 (in compounds) ill ~ed adj -enye tabia mbaya. well ~ ed adj -enye tabia nzuri. 2 -enye kuonyesha upekee. ~ism n 1 upekee (kitabia/mazungumzo). 2 mtindo (unaotumika mno) maalumu katika sanaa/fasihi. ~ly adj -enye adabu njema, -enye heshima.

manoeuvre; maneuver n 1 maneva, luteka. 2 werevu, hila, ujanja. vi,vt 1 fanya maneva/luteka. 2 tumia hila/ werevu/ujanja; shawishi. manoeuvrable adj -a kushawishika. manoeuvrability n. ~er n.

manor n 1 shamba kubwa la mwinyi/ kabaila. 2 ~ house n (modern use) jumba kuu linalozungukwa eneo la ardhi ~ial adj.

mansard n ~ (roof) paa la migongo miwili (ambapo mmoja una mteremko mkali zaidi ya mwingine).

manse n nyumba ya mchungaji (hasa

mansion n 1 kasri, jumba kubwa. 2 (pl, in proper names) jumba la ghorofa.

mantel n maungio ya meko; (in modern houses, usu ~ piece) shubaka juu ya meko.

mantilla n mtandio, mdongea

(unaovaliwa na wanawake wa Kihispania).

mantis n (praying ~) vunjajungu: aina ya panzi.

mantle n 1 joho; (fig) kifuniko. 2 utambi wa taa ya gesi. vt,vi 1 funika, tanda. 2 (old use or liter) (of blood) ingia, jaza/jaa kwenye mishipa, enea; (of the face) iva.

manual adj -a mikono (mil) ~ exercises mazoezi ya mikono ~ labour kazi za mikono. n 1 kitabu cha mwongozo; kitabu cha kiada. 2 see key board.

manufacture vt 1 tengeneza, zalisha (katika kiwanda). 2 tunga, buni. n 1 utengenezaji; uzalishaji. 2 (pl) vitu vilivyotengenezwa/zalishwa kiwandani. ~ r n mtengenezaji; mwenye kiwanda.

manumit vt achia huru, toa utumwani. manumission n.

manure n 1 samadi; mbolea. vt tia mbolea katika ardhi.

manuscript n muswada. in ~ bado

kuchapishwa.

many adj,n 1 -ingi, maridhawa, tele; kadha wa kadha. a great/good ~ kadha wa kadha; -ingi sana. one too ~ zaidi, -ingi kuliko inavyotakiwa/ inayostahili. have one too ~ (colloq) lewa kidogo. be one too ~ for shinda (kwa werevu), weza. the ~ umma, kaumu. 2 ~ a (used with sing n rather liter, usu replaced by ~ and pl n) -ingi ~ a man watu wengi. ~ sided adj -enye pande nyingi; (fig) -enye uwezo/vipengele vya aina nyingi.

Maoism n nadharia ya siasa na

matendo ya Mao Tse-Tung. Maoist n mfuasi wa nadharia hiyo.

map n ramani ~ reading usomaji ramani. ~ reader n msomaji ramani. ~ scale n kipimia ramani, skeli. off the ~ (colloq), -siofikika/ ingilika; mbali; (fig) -sio muhimu. on the ~ (colloq) -a muhimu. vt chora ramani; onyesha kwenye

maquis

~ out panga ~ out one's time jipangia wakati.

maquis n the ~ n maki; wapigania uhuru/jeshi la msituni la wazalendo wa Kifaransa wakati wa Vita Kuu II.

mar vt haribu, hasiri, umbua be ~red sawajika, umbuka, haribika. make or ~ fanikiwa sana au haribu kabisa.

marabou n (bird) kongoti.

marabout n 1 murabiti: mtawa wa Kiislamu, hasa wa Afrika Magharibi. 2 hekalu juu ya kaburi la murabiti.

marasmus n nyongea.

marathon n marathoni: mbio za masafa marefu (kiasi cha maili 26); (fig) majaribio ya ustahamilivu.

maraud vi nyang'anya, teka nyara. ~er n.~ing adj.

marble n 1 marumaru. 2 (pl) sanaa za marumaru. 3 gololi. 4 (attrib) -a kama marumaru a ~ breast mtu asiye na huruma. ~d adj -enye kupakwa rangi ya marumaru.

marcel n utengenezaji wa mawimbi katika nywele.

March1 n Machi: mwezi wa tatu.

march2 vi,vt 1 tembea/enda kama askari Quick ~! mbele tembea! ~ing orders n amri ya kwenda maneva, vitani n.k.; (fig) kufukuzwa. ~ out toka (hasa kwa kususa/ kukasirika). 2 peleka. n 1 mwendo wa kijeshi. a ~ past n gwaride. steal a ~ on somebody wahi mtu. on the ~ kwenda kama askari. a line of ~ njia inayofuatwa na askari. a forced ~ kutembea kwa haraka na dharura. 2 mwendo; safari. 3 (time) matukio. the ~ of events matukio; maendeleo ya mambo. 4 wimbo/muziki wa kijeshi. ~er n.

march3 n (usu pl) (hist) mpaka wa nchi (hasa baina ya Uingereza na Uskoti au Walesi); eneo linalogombaniwa vi ~ upon/with (arch) pakana.

Mardi Gras n (F) siku ya mwisho kabla ya kuanza Kwaresma.

mare n farasi jike. a ~'s nest uvumbuzi wa uongo au usio na maana.

margarine n majarini.

margin n 1 ukingo, ubavu, pembeni. 2 (of book, writing) pambizo, nafasi (ya kandoni). 3 (extra amount) ziada. 4 sehemu/eneo karibu na mpaka/ kikomo/mwisho. escape something by a narrow ~ ponea chupu chupu. 5 tofauti baina ya bei halisi na bei ya kuuzia kitu; faida ya muuzaji. vt eleza pembeni. ~al adj -a pembeni. ~al land ardhi isiyo na rutuba. ~al seat/constituency n kiti cha ubunge ambapo Mbunge alimzidi mpinzani wake kwa kura chache.

marijuana, marihuana n (also called hashish, cannabis, pot) bangi.

marimba n (mus) marimba.

marinade n marinadi: achari ya mvinyo, siki na viungo. vt (also marinate) lainisha kwa kutia marinadi.

marine adj 1 -a bahari, -a baharini; -a mambo ya bahari ~ painter mchoraji picha za baharini. 2 -a meli; -a majini; -a biashara ya baharini ~ insurance bima ya meli na mizigo. n 1 askari wa manowari. 2 (shipping) merchant/mercantile ~ n jamii ya marikebu/meli zote za taifa fulani. 3 ~ corps jeshi la wanamaji. the M~s n jeshi zima la wanamaji. tell that to the ~s acha uongo! waeleze watoto. marina n bandari, mapumziko/starehe (ya ngarawa za kujifurahishia). maritime adj -a bahari, -a ubaharia; -a pwani, iliyo pwani. ~r n baharia, mwanamaji (hasa anayesaidia kuongoza meli). master ~ n nahodha (wa meli ya biashara).

marionette n karagosi.

marital adj 1 -a ndoa. ~ obligations n majukumu ya ndoa. 2 -a mume.

marjoram n majorama: aina ya kiungo cha chakula (pia hutumika kama dawa).

mark1 n 1 alama; doa a ~ on the face alama usoni a ~ on the shirt doa kwenye shati. 2 dalili, ishara. 3

mark

give somebody/get/gain good/bad ~ pa/maksi nzuri/mbaya. 4 shabaha. be/fall wide of the ~ kosa; kosea. hit/miss the ~ (fig) patia/kosea. easy ~ (colloq) mtu anayedanganyika kwa urahisi. beside the ~ haihusiki/haimo. 5 umashuhuri. make one's ~ -wa mashuhuri. 6 the ~ n kiwango; kawaida not be/feel (quite) up to the ~ -tojisikia vizuri. be up to/below the ~ fikia/-tofikia kiwango. 7 mkato (ufanywao na mtu asiyejua kusoma na kuandika) badala ya saini. 8 (athletics) mstari (wa kuanzia mashindano) on your ~ s kwenye mstari. 9 (with numbers) alama ya kuonyesha aina ya chombo. vt 1 ~ something on/with something; ~ something down/up tia alama; piga chapa. ~-up n ongezeko la bei. ~ing-in n wino wa kutilia alama (usiofutika). 2 (passive) -wa na alama (ya asili/ inayoonekana) a zebra is ~ed by stripes pundamilia ana mistari. 3 toa maksi; sahihisha. 4 tia alama ya pata/ kosa. 5 zingatia, angalia. 6 ~ my words zingatia maneno yangu. a ~ed man mtu anayeangaliwa kwa jicho baya. 7 -wa kitambulisho cha; onyesha. 8 -wa dalili ya, ashiria. 9 ~ time chapa miguu; (fig) subiri (mpaka hali itakapo ruhusu kuendelea). 10 (use with adverbial particles) ~ something off weka alama juu ya kitu (kuonyesha mipaka, vipimo n.k.). ~ something out tia mipaka ya kitu. ~ somebody out for something amua tangu mapema kumpa mtu kitu/cheo n.k. ~ ed adj dhahiri, wazi. ~edly adv. ~ing n (esp) madoadoa (ya manyoya, ngozi). ~r n 1 mtu au chombo kitiacho alama. 2 mtu anayerekodi pointi/magoli/alama mchezoni. 3 alama ya bendera/jiwe n.k. lionyeshalo masafa. 4 msahihishaji.

mark2 maki: fedha ya Kijerumani.

market n 1 soko. the ~ sokoni. (to)

bring one's egg/hogs to the wrong~ haribikiwa na mipango/shindwa kwa kuomba msaada pasipostahili. ~ day n chete, gulio. ~ place/square n sokoni. ~-town n gulio. go to ~ enda sokoni (kununua vitu). go to a bad/good ~ (to) fanikiwa. ~ garden n bustani ya ya mboga za kuuza. ~ price n bei ya sokoni. 2 utashi, kutakiwa kwa soko. 3 ununuzi na uuzaji. be on/come on (to) the ~ uzwa. be in the ~ for something -wa tayari kununua; (fig) -wa tayari kufikiria jambo fulani. put something on the ~ uza kitu. up/down ~ adj -a tabaka la juu/ chini. ~ research n utafiti wa soko. vi,vt 1 uza/nunua sokoni. 2 peleka/ tayarisha kwa ajili ya kuuza. ~ able adj -a kuuzika, -inayouzika. ~ing n elimu ya soko.

marksman n mlengaji hodari. ~ ship n uhodari wa kulenga.

marl n maga: udongo mzuri wenye chokaa. vt tia maga.

marlinespike n kitenga mshipi, kipande cha chuma cha kutengea nyuzi za kamba.

marmalade n mamaledi: jemu iliyotengenezwa kwa machungwa.

marmoreal adj (poet) -eupe, baridi,

-liong'arishwa kama marumaru; -a marumaru.

marmot n panyabuku.

marocain n marokoni: aina ya kitambaa chepesi cha hariri au sufu.

maroon1 vt acha/weka/telekeza (mtu au watu) katika kisiwa au nchi isiyo na watu.

maroon2 adj (rangi ya) damu ya mzee.

maroon3 n fataki (agh. hutumika kama kitoa ishara/hadhari)

marque n(hist) letters of ~ kibali cha uvamizi; mamlaka anayopewa mtu kutumia meli kwa mashambulizi, uvamizi, uharibifu n.k.

marquee n hema kubwa. marquetry n

nakshi za fanicha.

marriage n 1 ndoa, nikahi. ask in ~

marrow

give in ~ oza. take in ~ oa/olewa. ~ lines n (colloq) cheti cha ndoa. 2 (usu wedding) harusi. ~able adj (of a young person) -a kufaa kuoa/kuolewa a person of ~able age mtu aliyefikia umri wa kuoa/kuolewa. ~ability n. married adj 1 -enye kuoa/kuolewa married woman mwolewa: mwanamke aliyeolewa. 2 -a ndoa. marry vt,vi 1 funga ndoa; (of male) oa; (of female) olewa. 2 (of a priest, a civil official) fungisha ndoa. 3 marry (off) oza. 4 pata kwa ndoa. marry wealth pata mali kwa ndoa.

marrow n 1 uboho. chilled to the ~ ona baridi kali. 2 (fig) kiini. the pith and the ~ sehemu ya lazima. 3 (vegetable) mumunye, mung'unye.

Mars n 1 (Roman myth) mungu wa vita. 2 (astron) Mars (jina la Sayari mojawapo).

marsh n bwawa, ziwa lenye matope;

~-gas n mitheni. ~y adj.

marshal n 1 jemadari. field ~ n jemadari mkuu. 2 msimamizi wa sherehe/matukio muhimu. 3 afisa wa mahakamani. 4 (US) mkuu wa idara ya polisi/zimamoto. vt 1 panga. ~ling yard n mahali pa kupanga (mabogi ya) treni. vt ongoza kwa heshima/taadhima. ~ somebody into a room ongoza mtu chumbani.

mart n 1 soko; gulio. 2 duka la dalali/ mnadi.

martial adj 1 -a vita, -a kijeshi. ~ law n sheria za kijeshi. 2 shujaa; -enye kupenda vita. ~ly adv.

martin n (house) ~ mbayuwayu.

martinet n kidikteta.

martingale n 1 hatamu. 2 (of cards) kamari marudufu.

martyr n shahidi (wa dini), mfiadini. make a ~ of oneself jitoa mhanga. be a ~ to something teswa/umwa sana kutokana na. vt ua/umiza kishahidi. ~dom n mateso/kifo cha kishahidi.

marvel n 1 ajabu, kitu/jambo la

its no ~

si ajabu. 2 ~ of something mfano wa ajabu/zuri/bora. vi 1 ~ at something shangaa, staajabu, ona ajabu. 2 ~ that/why etc shangaa kwamba/kuwa/kwa nini. ~lous adj -a ajabu, -a kushangaza. ~lously adv.

Marxist n Mfuasi wa Maksi ~ criticism uhakiki wa Kimaksi ~ party chama cha Kimaksi. Marxism n (esp) Umaksi.

marzipan n haluwa au keki (ya unga wa mlozi na sukari).

mascara n wanja.

mascot n nyota (ya jaha); kileta bahati, mleta bahati.

masculine adj -ume, -a kiume, dume. (gram) ~ gender n jinsia ya kiume. masculinity n uume.

maser n chombo cha kuongeza wimbimaikro.

mash n (of food and feed) 1 mseto

(kwa ajili ya kuku, ng'ombe, nguruwe n.k.) 2 togwa. 3 viazi vya kupondwa. vt 1 seta; ponda; ~ ed potatoes viazi vilivyopondwa. ~ er n kipondeo.

mask n barakoa; (of head, face) kinyago. do something under a/the ~ of friendship jifanye rafiki, fanya kwa kujifanya; kificho; kisingizio. throw off one's ~ (fig) jifichua, jionyesha wazi (tabia na malengo ya mtu) (gas) ~ n kichuja hewa. vt 1 vaa kinyago/barakoa. 2 ficha.

masochism n kufurahia/kupata ashiki kutokana na kuumia/kudhalilishwa.

mason n mwashi. ~ic adj. ~ry n.

masque n tamthiliya ya muziki na ngoma.

masquerade n 1 dansi ya vinyago. 2 (fig) kujifanya kisingizio. vi ~ (as) jifanya. ~r n.

mass1 n 1 ~ (of) fungu; wingi; bonge. 2 the ~es n umma the great ~ of the people idadi kubwa ya watu, watu wengi sana in the ~ kwa jumla the workers in the ~ did not want to strike wafanyakazi kwa

mass

~ meeting mkutano wa hadhara. ~ communications; M~ Media n vyombo vya habari. ~ observation n uchunguzi/mafunzo ya desturi za watu wa kawaida. ~ production n uzalishaji kwa wingi (wa bidhaa moja). 3 (science) masi/tungamo. vt,vi kusanya; kusanyika. ~y adj imara; kubwa sana; zito. ~ive adj 1 kubwa, -nene; -zito. 2 (fig) imara. ~ively adv. ~ iveness n.

mass2 n (rel) misa high ~ misa kuu low ~ misa ndogo.

massacre n mauaji ya kinyama (ya

vt ua ovyo watu wengi.

massage vt kanda, chua. n kuchua musuli, kusinga. masseur n msingaji mwanaume. masseuse n msingaji mwanamke.

massif n mrundikano wa milima.

mast n mlingoti; nguzo. sail before the ~ fanya kazi kama baharia wa kawaida. ~ head n ncha ya mlingoti.

master n 1 tajiri, mwajiri. be one's

-wa huru (attrib) stadi (anayejitegemea). 2 mkuu wa kaya mwanamume. be ~ in one's own house mudu mambo yako mwenyewe. 3 nahodha, kapteni. 4 mwenye mbwa, punda n.k. 5 mwalimu wa kiume the Kiswahili ~ mwalimu wa Kiswahili. head ~ n mwalimu mkuu (wa kiume). 6 ~ of waria, stadi he is ~ of the language ni stadi wa lugha hii; mwamuzi. 7 the M~ n Yesu Kristu. M~ of Arts/Science etc n shahada ya pili. 8 (with a boy's name) bwana mdogo, kibwana. 9 old ~s n wachoraji maarufu wa karne kati ya 13 na 17; michoro ya wachoraji hawa. 10 ~mind n mwanzilishi mwamba. ~ mind up vt panga, endesha, anzisha mipango; (attrib) tawala, -a juu. ~ thought n fikra tawala. 11 cheo. M~ of Ceremonies n Msimamizi Mkuu wa Sherehe. 12 (compounds) ~ at arms n Afisa wa polisi katika

manowari na melini. ~-key n ufunguo malaya. ~piece n kazi bora. ~stroke n ustadi mkubwa; tendo la akili sana. ~ plan n mpango mkuu. vt 1 -wa mjuzi/ mweledi/mmbuji/hodari n.k. 2 shinda, tawala. ~less adj -sio na ujuzi. ~ful adj -enye makuu, -enye kupenda kutawala wengine; stadi. ~ly adj stadi sana. ~ship n 1 utawala, madaraka. 2 ualimu. ~y n 1 ~y (of) ustadi, ujuzi, uwezo kamili, umahiri (to) gain the ~y of tawala (kabisa). 2 ~ (over) madaraka, utawala.

masticate vt tafuna. mastication n.

mastiff n mastini:jibwa lenye masikio lepelepe.

mastitis n uvimbe wa titi (of animals) kinyungi.

mastodon n mastodoni: mnyama mkubwa wa kale kama tembo.

mastoid n mfupa wa nyuma ya sikio. ~itis n uvimbe wa mfupa huu.

masturbate vi,vt (of a man) piga punyeto; (of woman) jisaga. masturbation n.

mat1 n mkeka; kirago; jamvi; busati. vt 1 tandika jamvi n.k. 2 tatizika; tatiza.

mat2, matt (US also matte) adj (of

surfaces, eg paper) -siong'aa.

matador n matadoo: mcheza ng'ombe.

match1 n njiti ya kiberiti. ~ box n ganda la kiberiti. ~ wood n miti itumikayo kutengenezea viberiti; vipande vya mbao.

match2 n 1 (equal) mwenzi; sawa;

mshindani be a ~ for -wa sawa na, weza be more than a ~ for -wa na uwezo zaidi ya mwingine. 2 kulingana we shall never see his ~ hututaona mtu anayefanana naye they are a good/bad ~ wanalingana vizuri/vibaya. 3 mechi return ~ mechi ya marudiano. 4 (marraige) ndoa; mwenzi wa ndoa. make a ~ of it oana. ~ maker n mtu apendaye sana kuwa mshenga. vt,vi 1 lingana na; linganisha, landanisha.

matchet

(arch) oza; oana.

matchet n see machete.

matchlock n goboli: bunduki ya kizamani.

mate1 n 1 (colloq) mwenzi; rafiki yes,no ~ ndio, siyo yakhe! aisee! 2 (colloq) mume/mke. 3 (naut) sarahangi. 4 msaidizi cook's ~msaidizi wa mpishi surgeon's ~ msaidizi wa mpasuaji. 5 (of animals) dume/jike. vt ~ (with) (of animals) pandana.

mate2 n,v (in chess) see checkmate.

matelot n baharia.

material1 n 1 nyenzo, vitu vya kutengenezea/kujengea vitu vingine raw ~ mali ghafi. 2 kitambaa. 3 vifaa writing ~s n vifaa vya kuandikia. 4 taarifa inayotumiwa kuandikia maandiko.

material2 adj 1 -a mwili. 2 yakinifu. 3 (leg) muhimu, -a kiini ~ evidence ushahidi unaoathiri kesi. 4 muhimu, zito. ~ism n 1 uyakinifu. 2 tamaa ya vitu/anasa. ~ist n myakinifu. ~istic adj. ~istically adv. ~ize vt,vi fanya kuwa kitu, tokea; pata umbo/mwili, timizwa/kamilishwa. ~ization n.

maternal adj -a mama, -a upande wa mama. ~ly adv.

maternity n -a uzazi ~ nurse mkunga ~ hospital hospitali ya uzazi.

matey adj ~(with) (colloq) changamfu, rafiki; zoeana na (to) get ~ with somebody fanya urafiki na mwingine.

mathematics n (abbr maths; US math) hisabati, hesabu. mathematical adj. mathematically adv. mathematician n.

matinee n maonyesho ya alasiri.

matins n (rel) sala ya alfajiri.

matriarch n mamamkuu (katika familia au kabila). ~y n utaratibu wa jamii ambapo mama ndiye mkuu wa familia. ~al adj.

matric n see ~ulation.

matricide n 1 kumwua mama yako. 2 aliyemuua mama yake.

matriculate vt,vi 1 ingiza; ingia katika Chuo Kikuu, ingizwa katika Chuo Kikuu; shinda mtihani wa kuingia Chuo Kikuu. 2 (formally) shinda mtihani wa mwisho. matriculation n.

matrilineal adj -a kufuata nasaba kukeni. matrilocal adj -enye mila ya maharusi kuhamia kukeni.

matrimony n ndoa, kuoana. matrimonial adj -a ndoa. matrimonial cases n kesi za ndoa.

matrix n 1 chanzo. 2 (mould) kalibu.

3 mawe ya asili (yenye madini, vito n.k.). 4 (math) solo. 5 (bio) matriki.

matron n 1 matroni: mwanamke wa makamo anayetunza shule n.k.. 2 mwanamke anayeangalia wauguzi wa hospitali. 3 mwanamke aliyeolewa au mjane. ~ly adj.

matt adj = mat2.

matted adj see mat1.

matter n 1 mata, maada. 2 maudhui. 3 machapisho/maandishi. postal ~ n waraka wa posta. printed ~ n vitabu, magazeti. reading ~ n -a kusomwa, vitabu n.k.. 4 jambo, kisa, hoja, habari defamatory ~ kiumbuzi, kashifa. ~ of fact n jambo la kweli (hakika). ~ -of-fact adj (of a person, his manner) -a kawaida; -lio baridi ~ of law jambo la sheria. subject ~ of course jambo la kawaida/kutarajiwa, desturi. ~-of course adj -a kutarajiwa; -a kutegemewa. no laughing ~ jambo zito, si mchezo, si masihara. no ~ haidhuru, mamoja what is the ~? kuna nini? a hanging ~ n kosa la kunyongwa leave the ~ hanging achia jambo hewani (bila ufafanuzi/jibu kamili) as ~s stood kama mambo yalivyokuwa. for that ~ ilivyo (to) make ~s worse vuruga/chafua mambo. 5 umuhimu, maana. with/be) no ~ haidhuru, si kitu, isio na maana/umuhimu. no ~ who/ what/where etc yeyote (awaye), chochote/lolote (litokealo). 6 be the

mattins

with) -wa na. 7 (quantity, amount) kadiri, kiasi cha a ~ of 10 miles kadiri ya maili kumi. vi pasa, faa, -wa na maana/umuhimu it ~s a lot ni cha maana sana what does it ~ kwani ina umuhimu/maana gani?

mattins n see matins.

mattock n jembetezo.

mattress n godoro.

mature vt,vi 1 pevuka; pevusha; iva,

(of bills) -wa tayari (kwa madai) adj 1 -zima; -pevu; -bivu. 2 (ready) kwa makini, kamili, -liotengenezwa. 3 (of bills) tayari kulipa. ~ly adv. maturity n. maturate vi pevuka. maturation n upevu, kukua.

matutinal adj (formal) -a kutokea asubuhi.

maudlin adj lizi, -epesi kuona huzuni kipumbavu.

maul vt umiza vibaya, ponda the critics ~ed his new play wahakiki waliponda tamthiliya yake mpya.

maulstick n fimbo nyepesi ishikwayo na mpiga rangi kusaidia mkono ulioshika brashi.

maunder vi enda, sema, tenda kivivu.

Maundy Thursday n (rel) Alhamisi Kuu.

mausoleum n kaburi kubwa (zuri).

mauve n (rangi ya) urujuani adj -enye rangi ya urujuani.

maverick n (US) 1 ndama wa mwaka mmoja asiyepigwa chapa. 2 mpinzani.

maw n (of animals) 1 tumbo, shingo/ koo. 2 (fig) kitu cha hatari (kinachoweza kumeza/kuangamiza watu n.k.).

mawkish adj -a (kuonyesha) hisia ya kijinga. ~ly adv. ~ness n.

maxi-/ pref kubwa; refu.

maxilla n (bio) taya (agh. la juu).

maxim n neno la hekima, kanuni,

maximum n upeo, mwisho adj -a mwisho, -a upeo. maximize vt ongeza hadi upeo. maximization n.

May1 n Mei, mwezi wa tano. M~

Queen n Malkia wa uzuri. M~ Day n Mei Mosi; sikukuu ya wafanyakazi duniani. ~fly n mdudu aonekanaye mwezi Mei tu.

may2 aux verb 1 (of possibility or probability) weza; wezekana I ~ go naweza kwenda; labda nitakwenda; omba (ruhusa). 2 (of permission) ~ I go? Niende? ~ you be happy nakutakia heri. 3 (to express purpose) we eat that we ~ live tunakula ili tuishi. ~ be adv labda, huenda. as soon as ~ be mapema iwezekanavyo. ~day n (radio telephone) (neno la) ishara/ilani ya kimataifa ya kuomba msaada wakati wa shida angani au baharini.

mayhem n 1 (old use, and US) kosa la kuharibu kiungo cha mwili. 2 msukosuko, fujo, vurumai.

mayonnaise n kachumbari nzito ya mayai, malai, mafuta, siki n.k.

mayor n meya. ~ess n 1 mke wa meya. 2 meya mwanamke. ~alty n muda/cheo wa/cha umeya.

maze n 1 mzingile, mwanambije. 2 tazaa, mazonge. ~d adj.

me object pron mimi, -ni-; mi it is ~ ni mimi he called ~ aliniita with ~ pamoja nami from ~ toka kwangu.

mead n pombe ya asali.

mead;meadow n malisho, konde la majani.

meagre (US=meager) adj 1 (of persons) -embamba, -a kimbaombao. 2 (of things) haba, -chache, kidogo. ~ly adv. ~ness n.

meal1 n 1 mlo. 2 chakula. ~ time nwakati wa chakula/kula.

meal2 n unga (wa nafaka). ~ly adj -a unga; (of potatoes when boiled) -enye unga. ~ bug n kidungata. ~y mouthed adj -oga kusema ukweli, -enye kukwepa kusema wazi.

mealie n (South Africa) (pl) mahindi; kibunzi cha muhindi. ~ meal n unga wa mahindi.

mean1 adj 1 ovyo, baya, duni. 2 (of

behaviour) -a aibu, -a hila a ~ trick hila feel ~ ona haya/aibu. 3 bahili,

mean

(US) katili. 5 (of rank) chochole, kabwela, -sio nasaba. ~ness n. ~ie; ~y n.

mean2 adj 1 -a kati, -a kadiri/wastani ~ price bei wastani n 1 kati, wastani. happy/golden ~ n wastani wa kufaa. 2 (maths) wastani. 3 (pl) ~s n njia, uwezo jinsi, namna. by all ~s! hakika, Inshallah! by any ~s! kwa njia yoyote. by fair ~s or foul kwa njia yoyote ile. by no ~s hasha, hata kidogo by some ~s or other kwa namna, njia moja au nyingine. by ~s of kwa njia ya, kwa kutumia. by no manner of ~s haiwezekani kabisa ~s of communication njia ya mawasiliano ~s of payment njia ya malipo. ways and ~s njia/mbinu (hasa za serikali za kupatia pesa). 4 (pl) (wealth) fedha, mali, utajiri a man of ~s tajiri. ~s test n kipimo cha uwezo/kipato. 5 wasaa, maishilio, nafuu it is within my ~s nina uwezo. (to) live beyond one's ~s kuishi kupita kipato/kutumia zaidi ya uwezo wako.

mean3 vt 1 (of words, sentences etc) maanisha that's what I ~ hiyo ndiyo maana yangu what did he ~ by saying that? alikuwa na maana gani kwa kusema vile? who do you ~? nani? it ~s yaani; maana yake. 2 ~ (by) dhamiria, taka, kusudia vema. (to) ~ business (colloq) dhamiria sana (kufanya kitu); amua. (to) ~ mischief dhamiria madhara. (to) ~ no offence -todhamiria kosa. 3 ~ something to somebody -wa na maana. ~ a lot to somebody pendwa na mtu it ~s a great deal to me ina maana kubwa kwangu. 4 ashiria; elekea. 5 ~ well (by) -wa na nia njema. ~ ing n maana, kusudi adj -lio na maana. ~ingful adj. ~ingfully adv. ~ingless adj -sio maana. ~ingly adv.

meander v (of a river) fuata mkondo;

~ings n mipindopindo; uzururaji; uporojoaji.

meantime n see meanwhile. in the ~ kwa sasa.

meanwhile adv wakati ule ule; kitambo, sasa hivi, punde si punde; kwa sasa.

measles n 1 surua. 2 (of pigs) tegu. measly adj 1 -enye surua. 2 (fig) -enye tegu. 3 duni, hafifu.

measure n 1 kipimo; kimo. take somebody's ~ (fig) pima/angalia tabia, akili, uwezo n.k. wa mtu. give full/short ~ toa kiasi kamili/ pungufu give extra ~ toa nyongeza. made to ~ (of clothes) iliyopimwa ~ of spread kipimo cha mweneo. 2 kiasi, kiwango. in some ~ kwa kiasi fulani. beyond ~ kupita kiasi. without ~ bila kiasi. 3 (music, poetry) mapigo, mwendo. tread a ~ with somebody cheza dansi na. 4 chenezo, kipimo, kigezo. greatest common ~ n (abbr GCM) namba kubwa kabisa inayogawa namba nyingi zote sawasawa/bila kuacha mabaki. 5 hatua, mashauri, matendo take ~s to rectify the situation chukua hatua za kurekebisha hali. set ~s to wekea mipaka. 6 sheria (iliyopendekezwa). vt,vi 1 pima (ukubwa/kiasi n.k.). 2 tathmini. ~ somebody angalia tabia ya mtu. 3 ~ up to the job -wa na uwezo wa kufanya kazi. ~ one's length anguka kifudifudi. ~ swords against/with somebody (fig) pimana nguvu na. ~ one's strength (with somebody) jaribu nguvu/uwezo. 4 fikia, -wa na (urefu wa n.k.). it ~s six feet urefu wake ni futi sita. 5 ~ out/off toa kidogo kidogo; pambanua. ~d adj -a taratibu; -a sawasawa; (of language) -liofikiriwa, zito. measurable adj -a kupimika. ~less adj bila kikomo, -sio na mipaka. ~ment n 1 kipimo. inside ~ment n vipimo vya ndani; (transportation) bidhaa zinazogharimiwa kwa kipimo badala ya uzito. 2 (pl) vipimo (vya marefu, mapana na kina).

meat

meat n 1 nyama; (without bones) mnofu, chinyango; (with rice etc) kitoweo lean ~ mnofu (bila shahamu); (US of fruits, nuts, shellfish) nyama. 2 (arch) chakula, mlo. one man's ~ is another man's poison halali yako ni haramu ya mwingine. ~ and drink kipenzi, -enye kupendwa sana football is his ~ and drink mpira wa miguu ni mchezo anaopenda sana, ndio ulevi wake. 3 (fig) uzito, mambo ya maana this short article contains a lot of ~ makala hii ndogo ina mambo ya maana. 4 (combined forms) ~ball n kababu. ~ chopper n kishoka. ~ grinder n kisagio nyama ~loaf bofulo ya nyama. ~-safe n kabati ya nyama, chakula. (GB) ~ tea n chai kuu (jioni); chai pamoja na nyama. ~less adj bila nyama. ~y adj (fig) -enye maana, muhimu.

Mecca n 1 Maka. 2 (fig) tarajio,

mechanic n 1 makanika, fundi mitambo. 2 mbinu ~s of writing short stories mbinu za utunzi wa hadithi fupi. ~al adj 1 -a umakanika, -a mitambo ~ al engineer mhandisi mitambo ~al advantage (of machine) manufaa ya kimakanika ~al efficiency (of engines) ufanisi wa kimakanika (katika injini); -a kufanya, kufanyika kama kwamba kwa mitambo. 2 (persons) -enye kutenda bila kufikiria, -a kufanya kama mashine. ~ally adv kimashine, bila kufikiri. ~s n umakanika. mechanism n 1 mashine, mtambo. 2 utaratibu wa kufanya jambo. mechanistic adj. (phil) ~ theory n nadharia inayoamini kwamba asili ya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ni mata. mechanize vt tumia mashine. mechanization n.

medal n nishani. ~list n mpewa nishani. ~lion n nishani kubwa; pambo.

meddle vi 1 ~ (in something) ingilia don't ~ in other people's affairs

usiingilie mambo ya watu wengine. 2 ~ (with something) gusa, chezea. ~r n mdukizi, mdakuzi. ~some adj -liopenda kudukiza.

media n the ~ vyombo vya habari, njia za mawasiliano (redio, magazeti n.k.).

mediaeval adj see medieval.

medial adj 1 -a kati. 2 -a wastani. median adj -a kati n (math) kati.

mediate vi,vt 1 ~ (between) patanisha, suluhisha. 2 leta suluhu/mapatano adj -a kati ya. mediation n upatanisho.

medicine n 1 sayansi na fani ya kuzuiana kutibu maradhi; uganga, tiba, udaktari. 2 dawa give ~ to -pa dawa, nywesha dawa. ~-ball n mpira wa babucheza. ~-chest n sanduku la dawa. ~-glass n bilauri ya dawa. 3 adhabu inayostahili. take one's ~ (fig) stahimili machungu/ adhabu. get a dose of one's own ~ fanyiwa kama ulivyomfanyia mwenzako. 4 uganga (wa kienyeji) practise ~ fanya uganga vt (arch) ponyesha; tibu. ~- man n 1 mganga. 2 mchawi. medic n (colloq abbr for medical student) mwanafunzi wa tiba/uganga. medical adj -a tiba, -a uganga, -a dawa to be under medical orders/ treatment endelea na matibabu, tibiwa medical man/practitioner daktari, mganga, tabibu medical examination uchunguzi wa kitabibu medical juris-prudence sheria za tiba n (colloq) mwanafunzi wa tiba; matibabu. medically adv. medicament n dawa. Medicare (US) n mpango wa serikali wa kutibu watu (agh. wazee). medicate vt tibu, tumia dawa, wekea dawa. medicated soap n sabuni yenye dawa. medicinal adj 1 -a dawa. 2 -a kuponya. medico n (colloq) daktari, mwanafunzi wa uganga.

medieval adj -a enzi za kati (mnamo

miaka 1100-1500). ~ist n msomi wa mambo za zama za kati.

mediocre

mediocre adj hafifu, duni, -a hivi hivi;

mediocrity n.

meditate vt,vi 1 taamali, tafakari, zingatia. 2 ~ (up) (intend) azimu. meditation n taamuli, tafakuri, mazingatio. meditative adj -a mazingatio. meditatively adv.

Mediterranean n -a Mediterania the

Bahari ya Mediterania.

medium n 1 wastani, tabia/sifa ya wastani. the happy ~ kukwepa misimamo, kutobana sana wala kulegeza mno, wastani wa kufaa. 2 (means) njia, chombo ~ of circulation njia ya mawasiliano by the ~ of kwa njia ya ~ of exchange kibadilishio. 3 mtu anayewasiliana na mizimu. 4 (pl) mazingira adj -a kati, -a kadiri, wastani. ~ wave n masafa/mawimbi ya kati (-a urefu kati ya mita 100 na 1000).

medley n 1 mchanganyiko. 2 (mus) wimbo mseto (unaochanganya nyimbo mbalimbali).

medulla n (bio) medula: kiunga ubongo cha wanyama.

meed n 1 (poet) (reward) tunzo,

(merit) stahili.

meek adj pole, vumilivu, sikivu, nyenyekevu. ~ly adv. ~ness n.

meerschaum n shamu: udongo laini mweupe unaotumika kufanyizia viko vya tumbako. ~ (pipe) n kiko cha mishamu.

meet1 adj (arch) -zuri, -a kufaa, -a kustahili; -a haki it is ~ and just ni vyema na haki.

meet2 vt,vi 1 kutana. ~ (with) pata/ patwa, kumbana na ~ with impediments kumbana na vikwazo. 2 fahamu, fahamiana, juana they met the professor at the farm walifahamiana na profesa shambani. 3 pokea, laki, ridhia ~ somebody's wishes ridhi(sha) matakwa ya mtu ~ somebody's request kidhi ombi la mtu ~ the requirements tosheleza mahitaji. 4 faa. ~ the case tosheleza. ~ somebody half way (fig) patana, fanya suluhu. ~ all

expenses lipa gharama zote. 5 gusa; gusana, patana; kimu, tosheleza mahitaji. make (both) ends ~ ishi kulingana na mapato. 6 onekana, sikika. ~ somebody's eye/ear onekana/sikika; ridhisha. there is more than ~s the eye kuna mambo mengi zaidi ya yanayoonekana kwa macho, kuna mengi yaliyojificha. 7 -wa tayari, jiandaa kwa ~ with political changes jiandaa kwa mabadiliko/mageuzi ya kisiasa. 8 pambana, pinga, kabili (kwa vita). ~ ing n mkutano, kusanyiko annual general ~ing mkutano wa mwaka a secret ~ing mkutano wa siri. ing~-house n jengo la mikutano (agh. ya Quakers) ya sala. ~ing-place n mahali pa kukutania.

meet3 n 1 (GB) mkutano (wa wawindaji, watu wanaosaka, wapanda baiskeli n.k.). 2 (US) mashindano athletic ~ mashindano ya riadha.

megacycle n mibembeo milioni.

megadeath n kifo cha watu milioni kwa mpigo, hasa kwa (bomu la nyuklia).

megalith n megalithi: jabali, mnara wa

(miamba mawe).

megalomania n (ugonjwa wa) kupenda makuu. ~c n mpenda makuu.

megaphone n megafoni, bomba, paza sauti.

megaton n megatoni: nguvu ya baruti/ bomu sawasawa na tani milioni moja.

melancholy n ghamu, huzuni adj -enye uzito wa moyo. melancholia n ugonjwa wa ghamu. melancholic adj -enye huzuni, -enye uzito wa moyo.

melange n mchanganyiko.

melee n vurumai, ghasia nyingi.

meliorate vt,vi rekebisha, (kuwa zuri zaidi). melioration n.

meliorism n imani ya kuwa wanadamu wanaendelea kujirekebisha kuwa bora.

mellifluous adj (of sounds) -tamu, laini, -zuri, ororo.

mellow

mellow adj (of fruit) 1 -bivu, -lioiva vizuri, laini na tamu. 2 (of earth) -enye kukomaa vizuri. 3 (of colour) zito. 4 (of sound) ororo. 5 -enye busara, tulivu. 6 (colloq) changamfu, levi kidogo. vt,vi iva, -wa tamu.

melodrama n 1 melodrama: mchezo wa kuigiza wa kusisimua hisia, kupiga chuku, kuchoma moyo, kusikitisha, kuhuzunisha (agh. wenye mwisho mwema). 2 tabia, lugha ya kutia chumvi. ~tic adj. ~tically adv.

melody n tuni, lahani. melodic adj

-a sauti tamu. melodious adj -a tuni, -a maghani. melodiously adv.

melon n tikiti maji.

melt vt,vi 1 yeyusha; yeyuka. ~ away isha, malizika, yeyuka. ~ something down yeyusha kitu (ili kukitumia kama mali ghafi). 2 (of food) lainisha, mung'unya; meng'enyeka. 3 (of persons) lainika; tia/sikia huruma ~ into tears toa machozi. 4 (of colours) fifia. ~ing adj (fig) tamu sana, laini, ororo; -a kusikitisha. ~ing-pot n chungu cha kuyeyushia madini/metali; (fig) mahali pa mchanganyiko mkubwa wa wahamiaji. ~ing point n kiwango cha kuyeyukia.

member n 1 mwanajumuiya ~ of a party, society etc mwanachama M~ of the household mwanakaya. M~ of Parliament (MP) Mbunge (Mb). 2 sehemu, kiungo cha mwili the unruly ~ (arch) ulimi. ~ ship n uanachama.

membrane n utando. membranous adj.

memento n ukumbusho, kumbukumbu.

memo n see ~randum.

memoir n 1 kitabu cha kumbukumbu. 2 (pl) habari za maisha.

memorandum n 1 taarifa ~ of appeal rufani ~ of association katiba ya kampuni. 2 maandiko ya kukumbusha habari.

memory n 1 kumbukumbu; kukumbuka; (past event) mambo

yaliyokwisha pita. commit something to ~ kariri, hifadhi, tia moyoni. repeat/speak from ~ kariri keep in ~ tia moyoni, kumbuka not in the ~ of man zamani sana (hata mtu hawezi kukumbuka). to the best of my ~ kadiri ninavyokumbuka childhood memories kumbukumbu za utotoni. in ~ of somebody; to the ~ of somebody kwa kumbukumbu ya. 2 kipaji/uwezo wa kukumbuka; nafasi/kiasi cha kurekodi mambo (ndani ya kompyuta) Asha has a bad ~ Asha ana kumbukumbu mbaya/ hakumbuki. 3 kina (masafa) cha kuweza kukumbukia. within living ~ wakati wetu loss of ~ kupotewa na kumbukumbu refresh one's ~ jikumbusha. 4 heshima baada ya kifo of blessed ~ marehemu of sad ~ -a kukumbusha majonzi. memorable adj -a kukumbukwa, -a sifa kubwa, mashuhuri. memorably adv. memorial n 1 kumbukumbu, ukumbusho/kumbukizi. 2 hati yenye maombi. 3 sanamu ya ukumbusho. 4 (pl) memorials n makumbusho adj -a kumbukumbu. memorialize vt 1 peleka hati ya maombi. 2 wekea ukumbusho. memorize vt kariri, soma kwa ghaibu. memorization n.

memsahib n mamsabu, bibi.

men n pl of man.

menace vt hamanisha, ogofya, kamia,

tisha ~ a country with war tishia nchi kwa vita. n hamaniko, tishio, kamio, hatari. menacing adj. menacingly adv.

menage n kaya.

menagerie n nyumba za wanyama (kwa maonyesho), mkusanyiko wa wanyamapori (hasa wa sarakasi).

menarche n kuvunja ungo, kuingia

hedhi mara ya kwanza.

mend vt,vi 1 rekebisha, fanyiza ~ the clothes tengeneza nguo ~ matters rekebisha mambo. 2 ongoka. its never too late to ~ bado kuna muda wa kujiongoa. 3 pona, pata

mendacious

my leg is ~ing well mguu wangu unapona vizuri. 4 ongeza ~ the fire chochea moto ~ one's pace ongeza mwendo. on the ~ -enye kupata nafuu/ahueni. ~er n mtengenezaji. ~ing n utengenezaji.

mendacious adj -ongo, danganyifu. ~ly adv. mendacity n (formal) uwongo, udanganyifu.

Mendelian adj -a nadharia ya jenetiki ya Mendel.

mendicant n mwombaji adj -a kimaskini, -a ombaomba.

menfolk n (pl) (colloq) wanaume.

menial adj -a mtumishi wa nyumbani;

~ duties utumishi, (kazi za) uboi. n mtumishi wa nyumbani, boi.

meningitis n (med) uvimbe wa tando za uti wa mgongo na ubongo; homa ya uti wa mgongo.

menopause n (wakati wa) kukatika

menses n hedhi. menstruate vi -wa na hedhi, ingia mwezini. menstrual adj. menstruation n.

mensuration n 1 mpimo (wa marefu na maeneo). 2 elimu ya kupima marefu na maeneo. mensurable adj.

mental1 adj 1 -a akili, -a kichwa. ~ age n umri/ukomavu wa akili. ~ arithmetic n hesabu za kichwa ~ aberration kosa la akili. ~ cruelty n ukatili wa kiakili. 2 -enye ugonjwa wa akili; mwenye kichaa (wazimu). ~ deficiency n upungufu wa akili ~ health utimamu wa akili. ~ home/hospital n mahali pa wagonjwa wa akili. ~ illness n ugonjwa wa akili. ~ patient n mgonjwa wa akili. ~ reservation n kusita kimoyomoyo. ~ retardation n taahira ya akili. ~ly adv. ~ly defective adj -enye akili pungufu/taahira. ~ity n akili; tabia, fikira.

mental2 adj -a kidevu.

menthol n mentha. ~ated adj -enye mentha.

mention vt taja nena. not to ~; without ~ing licha ya it was

expressly ~ed ilitajwa wazi. don't ~ it si kitu, haidhuru. n kutaja she made no ~ of your coming hakutaja lolote kuhusu kuja kwako. honourable ~ n tuzo la sifa (ya mwanafunzi katika mtihani). ~ed adj.

mentor n mshauri, mnasihi.

menu n menyu, orodha ya vyakula.

mercantile adj -a biashara, -a kufanya biashara. ~ marine n meli za biashara ~ agent wakala wa biashara ~ law sheria ya biashara. mercantilism n nadharia kongwe ya uchumi yenye kuthamini zaidi utajiri wa fedha.

Mercator's Projection n mtupo Mercator: Uchoraji wa ramani ya dunia kwa mistari mustatili toka ikweta na meridiani.

mercenary n mamluki, askari wa kukodiwa adj -enye kufanya kwa tamaa ya fedha; -a kutaka faida tu for ~ ends kwa ajili ya faida.

mercer n mwuza nguo (za hariri, za pamba na za sufu). ~ize vt imarisha nyuzi za pamba.

merchandise n bidhaa.

merchant n 1 mfanyi biashara ~ law sheria ya biashara. ~ navy n meli za biashara (za nchi moja); baharia/ mwanamaji wa meli hizo ~ prince mfanya biashara tajiri. 2 mwenye duka. 3 (GB sl) shabiki; mlevi; mtu mwenye tamaa (ya kitu) a speed ~ shabiki wa spidi, mtu apendaye kuendesha gari kwa kasi sana. ~ man n meli merikebu ya kupakia bidhaa.

mercury n 1 (chem) zebaki. 2 M ~

(Roman Myth) Mjumbe wa miungu; (astronomy) Zebaki. mercurial adj 1 (of persons) geugeu. 2 -a zebaki. 3 (fig) changamfu; janja; erevu n dawa ya zebaki.

mercy n 1 rehema, huruma, upole,

wema they had no ~ on me hawakunionea huruma. 2 (pardon) msamaha beg for ~ omba msamaha. be at the ~ of -wa chini

mere

be left to the tender ~/mercies of achiwa kwa/ uteseke. 3 bahati njema, faraja, liwazo. ~ killing n (colloq) see euthanasia, 4 M~ on us! Mungu! Tusamehe! merciful adj -enye rehema, -a huruma; -pole. merciful(to) -enye kuonyesha huruma mercifully adv. merciless adj dhalimu, katili, bila huruma, merciless (to) -sioonyesha huruma. mercilessly adv.

mere1 adj tu, tupu ~ accident ajali tu ~ words maneno matupu. ~ly adv tu he said it ~ ly as a joke alisema tu kwa utani.

mere2 n dimbwi, ziwa dogo.

meretricious adj -enye uzuri wa sura tu; -enye kung'aang'aa tu, kudanganya macho. ~ly adv.

merge vt,vi 1 ~ (into/in/with), (comm) (of business companies) unganisha; ungana our company ~d with the company which sells machines kampuni yetu imeungana na kampuni inayouza mashine the government will ~ the chemical industries serikali itaunganisha viwanda vya kemikali. 2 ~ into badilika polepole, geuka taratibu. ~r n kuunganisha; kuungana; muungano.

meridian n 1 meridiani; nusu ya

(fig) upeo, kipeo, usitawi. meridional adj -a kusini, -a kusini ya Ulaya; -a meridiani.

meringue n keki (ya ute wa mayai

merino n merino: namna ya kondoo

merit n 1 ustahili, tabia nzuri, sifa njema. 2 matendo mema. affidavit of ~s n kiapo cha ustahilifu on its ~s kwa ustahilifu wake. vt stahili; -wa na thamani ya. make a ~ of something dai stahili/utambuzi/ kutambuliwa; stahili. he ~s it ni stahili yake, amestahili. ~ocracy n

mfumo wa serikali unaoongozwa na wataalamu na weledi. ~orious adj -enye kustahili -a kupongeza/kutunuka. ~oriously adv.

mermaid n (in children's stories) nguva (jike). merman n nguva (dume).

merry adj 1 -a furaha; -a kufurahisha,

-changamfu, kunjufu wish somebody a ~ Christmas takia mtu heri ya Krismasi a ~ laugh kicheko cha furaha. make ~ -wa na furaha, -wa mchangamfu. ~ maker n mcheshi, mtu mchangamfu. ~ making n kufurahi, kuwa na furaha. ~ go round n bembea yenye farasi, magari ya kuwafurahisha watoto. 2 (old use) -a kufurahisha. 3 -liolewa kidogo.

mesalliance n kuoana na mtu wa tabaka la chini.

mescal n meskali: aina ya mpungate.

Mesdames n pl of madame.

mesdemoiselles n pl of mademoiselle.

mesh n 1 tundu la wavu, kimia, jicho (la wavu). 2 (pl) ~es n wavu, kimia. (mechanics) in ~ -lioingiana. vt,vi tega, nasa. ~ (with) ingiana, umana; (fig) patana. ~y adj.

mesmerism n (old use) kiinimacho,

kutia usingizi. mesmeric adj. mesmerist n mtia kiini macho. mesmerize vt tia mtu usingizi, fadhaisha.

mess1 n 1 fujo, machafuko, takataka

here's pretty ~ mambo gani haya! haya matata ya kutosha make a ~ of things haribu, fanya vibaya. vt,vi 1 ~ something (up) vuruga. ~ up 1 n (colloq) fujo, kutokuelewana. 2 ~ something/somebody about chezea; fanya mambo bila mpango, fanya purukushani make a ~ of something vuruga watu. ~y adj -a fujo, -chafu.

mess2 kikundi cha watu wanaokula

chakula pamoja (hasa wanajeshi); mlo; mesi, bwalo la kulia chakula. ~jacket n jaketi la mesi. ~ mate n

message

vt,vi ~ with somebody; ~ together -la chakula pamoja.

message n 1 habari, taarifa, agizo special ~ risala. 2 ujumbe. messenger n mjumbe, mtume; tarishi.

Messiah n Masiha, Kristo. Messianic adj -a Masiha, Masiha, -a Kristo.

Messieurs n pl of monsieur.

Messrs n (abbr of Messieurs) Mabwana.

messuage n (leg) nyumba pamoja na kiwanja.

met pt pp of meet.

Met n (abbr of) Meteorological.

metabolism n umetaboli: hali ya ujenzi na uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini. metabolic adj -a umetaboli.

metacarpal adj (anat) -a mfupa wa

metacarpus n kiganja cha mkono.

metal n 1 metali. 2 ~ work n kazi ya

~ worker n 1 mfua metali/ chuma. 2 kitu cha metali. 3 kokoto (za kutengenezea barabara/reli. 4 (pl) reli ya gari moshi the train left/ jumped the ~s gari liliacha reli. vt tengeneza barabara kwa kokoto. ~lic adj -a metali. ~lurgy n ufuaji metali; maarifa ya ufuaji wa metali. ~lurgist n bingwa wa metali. ~lurgical adj. ~-works n kiwanda cha metali.

metamorphose vt,vi ~(somebody/ something) (into) geuza, badili kabisa (tabia, umbo). metamorphosis n metamofosisi: ugeuzaji kabisa umbo/tabia.

metaphor n sitiari. ~ical adj -a sitiari. ~ically adv.

metaphrase n tafsiri (inayokaribia) sisisi.

metaphysics n 1 metafizikia: falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa. 2 mazungumzo ya hewani, udhanifu. metaphysical adj.

metatarsal n (anat) -a mfupa wa

mete vt ~ out gawa. ~ to pimia.

meteor n kimondo. ~ic adj -a kimondo; kimondo (fig) -a kuvuma kwa muda mfupi; -a haraka sana. ~ite n mavi ya nyota; jiwe lililotoka katika nyota.

meteorology n metorolojia: elimu inayohusika na upimaji wa hali ya hewa. meteorologist n mwanametolojia. meteoroligical adj.

meter1 n mita electricity ~ mita ya

umeme.

meter2 n see metre.

methane n methani.

methinks vi (old use) nionavyo mimi.

method n 1 (system, order) utaratibu, desturi. there is ~ in madness jambo analolifanya si la kijinga. 2 (way, plan) mbinu; njia ~ of teaching mbinu za kufundishia. ~ical adj -liofanywa kwa utaratibu; -enye utaratibu. ~ically adv. ~ology n methodolojia.

Methodism n Umethodisti:madhehebu ya Kikristo yaliyoanzishwa na John Wesley. Methodist adj -a imani ya Methodist n muumini wa umethodisti.

methought pt of methinks.

meths n pl (colloq abbr for)methylated spirits.

Methuselah n (in the Bible) Methusela: mtu aliyeishi muda mrefu kuliko wote (miaka 969); (fig) mtu mwenye umri mkubwa sana.

methyl n (chem) ~ alcohol n alkoholi

methili. ~ated adj -liyomethilishwa. ~ated spirit(s) n spiriti iliyomethilishwa.

meticulous adj -angalifu sana katika mambo madogo madogo; -angalifu na sahihi. ~ly adv. ~ness n uangalifu sana (katika mambo madogo).

métier n kazi/weledi/shughuli (inayomfaa hasa mtu); ubingwa wa mtu (katika kazi, biashara n.k.).

metre1 (US = meter) n mizani,mapigo. metrical adj -enye mizani.

metre2 (US = meter) n mita, meta.

Metro

adj -a mita. metric system n mfumo wa mita. metricize; metricate vt geuza kuwa katika mfumo wa mita. metrication n. metrical adj -a mita.

Metro n the ~ metro: reli za chini ya ardhi.

metronome n metronomi: chombo cha kupiga/kuongoza mwendo wa mapigo (ambacho mwendo wake unaweza kubadilishwa); kupigia mapigo.

metropolis n mji mkuu wa nchi; makao makuu. metropolitan adj 1 -a mji mkuu. 2 -a uaskofu mkuu metropolitan bishop askofu mkuu (wa sehemu/jimbo lenye maaskofu wengi). metropolitan France n Ufaransa. n 1 mkazi wa makao makuu. 2 M~ n askofu. metropole n nchi za kati contradictions between the metropole and the periphery mikinzano kati ya nchi za kati na nchi za pembezoni.

mettle n ushupavu, ujasiri. be on one's~; put somebody on his ~ amka/hamasisha mtu aonyeshe ushupavu wake. ~ some adj hodari, kunjufu sana.

mew n (also miaow) nyau, mlio wa

vi fanya mlio wa nyau the cat is ~ing paka analia nyau.

mews n 1 (old use) mtaa wa vibanda (mazizi) vya farasi nyuma ya mtaa wa makazi. 2 (modern use) mabanda yaliyogeuzwa kuwa nyumba/gereji.

mezzanine n mezanini: ghorofa kati ya ghorofa ya chini na ghorofa ya kwanza.

mezzo adv (musical direction) kwa

~ soprano n mwimbaji wa sauti ya kati (ya sauti ya kwanza na sauti ya pili).

mi,me n (mus) noti ya tatu (katika mfumo wa do-re-mi-fa).

miaou;miaow n see mew.

miasma n ukungu mbaya (wa kuleta

(fig) mazingira machafu; athari mbaya. ~tic adj -enye ukungu mbaya.

mica n ulanga. ~ceous adj.

mice n pl of mouse.

mickey n take the ~ (out of somebody) (sl) kejeli, cheza shere.

mickle, also muckele n (Scot) wingi, chungu nzima many a little makes a ~ haba na haba hujaza kibaba.

micro- pref mikro, dogo sana.

microbe n vijiumbe maradhi.

microbiology n mikrobiolojia.

microchip n microchipu: kijipande cha silikoni chenye sakiti changamano ya elektroniki.

microcosm n mfano mdogo wa ulimwengu; binadamu; mfano (mdogo); mwakilishi wa mfumo mzima prisons are a ~ of society magereza ni mfano mwakilishi wa jamii.

microdot n mikronukta: picha ambayo imepunguzwa hadi ukubwa wa nukta.

microelectronics n mikroelectroniki.

microfiche n kipande cha mikrofilamu.

microfilm n mikrofilamu: filamu ya picha zilizopunguzwa kabisa vt piga picha za mikrofilamu.

micrometer n mikromita:chombo chakupimia vitu vidogo sana.

micron n mikroni: kipimo cha urefu cha moja ya milioni ya mita.

micro-organism n kijiumbe, kidubini.

microphone n mikrofoni.

microprocessor n maikro-prosesa:kompyuta ndogo.

microscope n hadubini. microscopic;

microscopical adj dogo sana (kuweza

kuonekana kwa macho).

microwave n wimbi maikro.

mid adj -a kati in ~ air angani ~ course katikati ya njia in ~ August katikati ya mwezi wa Agosti ~ latitude latitudo ya kati pref (poet) katikati ya, miongoni mwa. ~ most adj,adv (-lio) katikati kabisa. ~day n adhuhuri, jua la utosini, saa sita ya mchana ~day meal chakula cha mchana. ~land n sehemu ya katikati ya nchi. The M~lands n Wilaya za kati ya Uingereza. ~night n 1 saa sita ya usiku. 2

midden

atrrib) usiku wa manane. burn the ~night oil kesha, kaa usiku kucha ukifanya kazi. the ~night sun jua la usiku la nchi za Aktiki na Antaktiki. ~ship n katikati ya meli/merikebu. ~shipman n mwanamaji manowarini (mwenye cheo chini ya Luteni); afisa mwanamaji mkurufunzi. ~st n (lit or arch) sehemu ya katikati. in our ~ist miongoni mwetu prep katikati ya, miongoni mwa. ~stream n katikati ya mkondo, mto. in ~ stream (fig) katikati ya jambo/shughuli/tukio n.k.. ~summer n katikati ya majira ya joto ya ulaya. M~ day n Juni 24. ~ madness n kilele cha wendawazimu. ~way adj,adv ~ way between katikati (ya), nusu kwa nusu. ~- week n siku za kati ya juma (Jumanne hadi Alhamisi, hasa Jumatano). ~ winter n katikati ya majira ya baridi ya ulaya.

midden n fungu la taka au mavi.

middle n 1 the ~ katikati the ~ of the room katikati ya chumba. ~ of the road (of policies) kati kwa kati, -a kadiri. 2 (colloq) kiuno. 3 (atrrib use). ~ age n utu uzima. M~ Ages n Enzi ya Kati. ~ aged adj -a makamo. ~ spread n (colloq) kitambi (kinachotokana na kuanza kuzeeka). ~-class adj tabaka la kati. take/follow a ~ course fuata njia ya kati. ~ distance n masafa ya kati. ~ finger n kidole cha kati. the M~ Kingdom n (old name for) China. ~man n mtu wa kati; mlanguzi. ~most adj -a kati kabisa, -a katikati. ~-watch n (on ships) zamu (baina ya saa sita na saa kumi za usiku). ~ weight n uzito wa kati (kati ya kilo 66.6 na 72.5). ~ blouse n blausi mpwayo. middling adj -a katikati; (moderate) -a wastani adv kiasi, kwa wastani. n (usu pl) bidhaa za daraja la pili.

middy n (colloq)(abbr of)

.

midge n usubi.

midget n 1 kibete.2 (attrib)-dogo sana. midriff n 1 kiwambotao. 2 fumbatio; tumbo.

midwife n mkunga. ~ry n ukunga.

mien n sura ya mtu (inayoonyesha hali aliyonayo).

might n uwezo, nguvu, ukuu. with all

one's ~; with ~ and main kwa nguvu zote ~ is right mwenye nguvu umpishe. ~y adj 1 (lit, biblical) -enye nguvu/uwezo/ amri/ukuu. 2 kubwa sana. high and ~y -enye majivuno sana adv (colloq) sana think oneself ~y clever jifikiria kuwa na akili sana. ~ily adv.

migraine n kipandauso.

migrate vi ~ (from/to) hama, hajiri;

hamia. migration n kuhama, uhamiaji; wahamaji (kwa pamoja). migratory adj -enye tabia ya kuhama. migrant n mhamiaji adj -hamaji. migrant labour n wafanyakazi wahamaji.

mike n (colloq abbr for) microphone.

milady n (dated form of address) siti.

milage n see mileage.

milch adj -enye kutoa maziwa, -a maziwa ~ cow ng'ombe wa maziwa.

mild adj 1 -pole; -dogo; laini ~ attack of fever homa kidogo. 2 (of food, drink, tobacco) sio kali. 3 ~ steel n chuma cha pua (kinachopindika bila kukatika). ~ly adv kwa upole. to put it ~ly bila kutia chumvi.

mildew n kuvu, ukungu. vt,vi ota ukungu/kuvu.

mile n maili he is feeling ~s better today (colloq) anajisikia afadhali sana leo. ~ometer n mita inayoonyesha maili zilizosafiriwa na gari. ~stone n jiwe la maili; (fig) jambo/tukio muhimu la kihistoria. ~age n 1 umbali (kwa maili). 2 malipo/posho ya usafiri/usafirishaji (kwa maili).

millieu n mazingira.

militant adj -liotayari kupambana, -a

kutaka mapambano. n mtu

militancy n mapambano, hali ya kuwa katika mapambano.

military adj -a kijeshi, -a kivita. n the ~ n askari, wanajeshi; jeshi. militarism n kuamini/kupenda kutumia nguvu za kijeshi katika siasa. militarist n mtu apendaye/anayeamini katika nguvu za kijeshi. militaristic adj.

militate vi ~ against zuia, pinga.

militia n (usu the ~) jeshi la mgambo. ~man n mwanamgambo.

milk n 1 maziwa the ~ of human kindness huruma ya kibinadamu. It's no use crying over spilt ~ maji yaliyomwagika hayazoleki. ~ and water (fig) hafifu; baridi. 2 (compounds) ~ bar n mkahawa wa kuuzia vinywaji vya maziwa, shikirimu n.k. ~-churn n gudulia la maziwa. ~ loaf n mkate mtamu. ~maid n mkama maziwa (mwanamke). ~man n muuza maziwa (majumbani). ~-powder n maziwa ya unga. ~round n njia anayopitia mwuza maziwa. ~ shake n sharubati, maziwa (baridi). ~sop n mwanamume mwoga/mnyonge;kijana mwoga. ~-tooth n jino la utoto. ~-white adj -eupe kama maziwa. 3 utomvu wa mimea/maji ya mimea (yaliyo kama maziwa) coconut ~ tui; maji ya nazi. ~ weed n nyasi zenye utomvu kama maziwa. 4 dawa iliyo kama maziwa ~ of magnesia maziwa magnesi. v,vi 1 kama ng'ombe/mbuzi/kondoo n.k.; gema utomvu n.k. (kutoka kwenye miti); (fig) kamua mtu (ili atoe fedha, habari). 2 toa maziwa. ~ing machine n mashine ya kukama ng'ombe. ~y adj -a maziwa; kama maziwa. the ~y way n kilimia: nyota ndogo nyingi sana pamoja (kama wingu jeupe) mbinguni usiku.

mill n 1 kinu. flour ~ n kinu cha

sugar ~ n kinu cha kusindika miwa. steam ~ n kinu cha

mvuke oil ~ kinu cha kusindika mafuta. put somebody/go through the ~ -pa/fanya mazoezi makali; pitisha/pitia katika hali ngumu. ~ dam n bwawa la kinu. ~ pond n dimbwi (kinu) (of the sea) tulivu/shwari kabisa. ~ race n mkondo wa maji kwa ajili ya kuzungusha gurudumu la kinu. ~ stone n jiwe la kusagia. ~ stone round the neck (fig) mzigo mzito. be between the upper and nether ~ stone banwa sana. ~wheel n gurudumu la kinu. ~wright n mjenzi na mtengezaji wa vinu (hasa vya maji na upepo). 2 kiwanda; karakana. ~ hand n mfanyakazi wa kiwanda. 3 kijimashine/kijinu cha kusaga (k.m. kahawa, pilipili n.k.). vt,vi 1 saga kwenye kinu ~ flour saga unga. 2 unda kwenye kinu ~ steel unda chuma cha pua katika fito chuma. 3 fanya mikato kwenye ukingo (k.v. wa sarafu). ~ about/around (cattle, crowds of people) enda hobelahobela, zunguka/tembea katika makundi na bila mpango. ~er n msagishaji.

millennium n 1 kipindi cha miaka elfu. 2 (rel) milenia: miaka elfu ya utawala wa Kristo duniani kama ilivyotabiriwa katika Biblia; (fig) kipindi cha baadaye cha furaha na neema ndani ya jamii. millenarian n mtu anayeamini kutokea kwa milenia. millenary adj -a miaka elfu, -a milenia.

millepede n see millipede.

millet n mtama; serena, lulu bullrush ~ wimbi, ulezi; uwele ~ stalk bua stalks of sweet ~ vikita ~ flour unga wa mtama.

milli- pref mili: sehemu moja ya elfu ya kipimo. ~gram n miligramu. ~litre n mililita. ~metre n milimeta.

milliard n (GB) (US see billion) elfu moja milioni.

milliner n mshona kofia za kike; mwuza mapambo na kofia za kike;

million

million n milioni, 1,000,000. make a ~ -wa milionea. ~aire n milionea; mtu mwenye dola/pauni milioni moja na zaidi; tajiri mkubwa. ~th n sehemu moja ya milioni adj -a milioni. ~ fold mara milioni moja.

millipede jongoo.

milometer n see mile.

milord n (Fr word formerly used for) bwana (wa Kiingereza), Mwingereza tajiri.

milt n 1 (spleen) wengu. 2 (of fish)

vt (of fish) toa mbegu za kiume. ~er n samaki dume atoaye mbegu.

mime n 1 uchezaji bubu. 2 mchezo

vi iga. ~sic n uigaji, ufananisho. ~tic adj -a kuiga, -lioigwa. mimic adj -liyoigwa; -liyoigizwa. n 1 mwigaji. 2 mwigo wa lafudhi. vt 1 iga, (hasa kwa dhihaka). 2 (of things) fanana sana. mimicry n uigaji, wigo.

mimeograph n kirudufu. vt rudufu.

minaret n mnara wa msikiti.

minatory adj -a kutisha, -a kuogofya.

mince vt,vi 1 kata vipande vidogo,

not to ~ matters/one's words sema waziwazi, bila kuficha. 2 sema/tembea kwa kujifanya/kujifaragua/kujidaidai. n kima (nyama ya kusaga). ~meat n minsi: mchanganyiko wa zabibu, matunda, mafuta, sukari, unga n.k. wa kufanyia keki. make ~meat of (colloq) shinda kabisa (mtu au majadiliano); maliza; (US) nyama. ~r n mashine ya kusaga (nyama). mincing adj -a madaha, -a maringo take mincing steps tembea kwa maringo. mincingly adv.

mind n 1 kukumbuka; kumbukumbu. call/bring something to ~ kumbuka. have/keep/bear something in ~ kumbuka jambo fulani. go/pass from/out of ones ~ sahaulika. it passed from my ~ niliisahau. put somebody in ~ of something

kumbusha. out of sight out of ~ (prov) asiyekuwepo na lake halipo. time out of ~ mara nyingi. 2 maoni; mawazo. presence of ~ uwezo wa kuamua/kutenda haraka. be out of one's/not in one's right ~ -wa na wazimu. be of the same ~ -wa na mawazo sawa; (of one person) shikilia wazo/uamuzi wa awali. to my ~ kwa mawazo yangu, nionavyo. bend one's ~ athiri, tia athari za kudumu katika mawazo ya mtu (kwa imani n.k.). ~ing adj -a kuathiri mawazo ya mtu. blow one's ~ (colloq) (of drugs, extraordinary or sensational sight, sounds etc) tia jazba (katika mawazo). ~-blowing adj -a kutia jazba. ~ boggling adj -a kustaajabisha. have something on one's ~ sumbuliwa na wazo fulani. keep one ~ on endelea kumakinikia /kufikiria. read somebody's ~ soma mawazo ya mtu. ~ reading n kubuni; ung'amuzi. ~ reader n. take one's/somebody's ~ off something (ji) sahau (lisha) (mawazo). 3 nia dhamira, dhati. be of/in two ~s sita; -wa na mashaka, vutwa huko na huko. change one's ~ ghairi; badilisha mawazo/nia. give one's ~ to something makinikia, shughulikia. have a good ~ to (do something) taka, elekea (kuamua). have half a ~ to do something elekea/vutiwa kufanya jambo. know one's ~ jua unalotaka, -wa na uamuzi. make up one's ~ amua, azimu, kusudia, kata shauri. make up one's ~ to do something amua kufanya jambo; (reconcile) kubali we are poor we must make up our ~ to that lazima tukubali kwamba sisi ni maskini. set one's ~ on doing something kusudia, dhamiria. speak one's ~ sema ukweli wake bila kuficha. 4 moyo, fikra. enter somebody's ~ ingia katika fikra za mtu. have/give one's ~ to something fikiria sana. an open ~ on something -wa tayari

mine

great ~s n watu mashuhuri; wataalam. sound in ~ -enye akili timamu. person of unsound ~ mtu asiye na akili timamu. vt,vi 1 (observe, watch) angalia, tunza. ~ out (for something) jihadhari, angalia. ~ your own business shika lako, usijitie (si yako). ~ one's S's and Q's wa na adabu nzuri. ~ you! unajua! 2 sumbuliwa (na), jali do you ~ my smoking? naweza kuvuta sigara? would you ~ shutting the door tafadhali ufunge mlango. never ~ haidhuru; usijali, si kitu. ~er n (in compounds) mwangalizi machine ~er mwangalizi wa mashine. ~ed adj 1 ~ to do something -a kuelekea/kutaka kufanya. 2 -enye mawazo ya. strong- ~ed adj jeuri, -enye msimamo, imara, -enye kujali. ~ful adj. ~ful of zingatifu. ~fully adv. ~fulness n. ~less adj 1 ~less of -siojali; -sahaulifu. 2 -sio na akili, -siohitaji akili. ~lessly adv. ~lessness n.

mine1 n 1 mgodi, shimo; chimbo (la

(fig) hazina; (explosive) bomu la kutega. ~ detector n chombo cha kugundua mabomu. ~ disposal n kutegua mabomu. ~-field n sehemu iliyotapakazwa mabomu ya kutega; sehemu yenye migodi mingi. ~-layer n meli/ndege ya kutega mabomu baharini. ~-sweeper n chombo cha kuondoa mabomu baharini. vt,vi 1 chimba mgodi; chimba. 2 weka mabomu; haribu kwa mabomu. 3 (fig) dhoofisha. ~r n 1 mchimba madini. 2 askari wa kutega mabomu ardhini. ~ral n madini adj -a madini. ~ ral pitch n lami. ~ral water n maji yenye madini (hasa yanayoweza kutibu); (GB) maji ya soda. ~ral wool n sufu madini. ~ralogy n elimu madini. ~ralogist n mtaalamu wa madini. mining n uchimbuaji wa madini mining

company kampuni ya migodi.

mine2 poss pron -angu through no fault of ~ si kosa langu poss adj (in poet & biblical style only) ~ eyes macho yangu.

mingle vt,vi ~ (with) changanyika, changanya.

mingy adj (GB colloq) -choyo,bahili.

mini (pref) dogo; fupi.

miniature n 1 kisanamu; mfano mdogo. in ~ -dogo. 2 (atrrib) -dogo ~ model mfano mdogo wa kitu. miniaturist n mtengenezaji wa sanamu/picha ndogo ndogo.

minim n minimu: nusu noti.

minimum n kiasi/kadiri iliyo ndogo

iwezekanavyo adj -a mwisho (kwa dogo), -dogo sana; -a chini kabisa. ~ wage n kima cha chini. minimal adj -dogo kabisa. minimize vt 1 punguza kabisa. 2 punguza sifa; dharau.

minion n (derog) mtumishi (anaye

jipendekeza). the ~s of the law polisi; askari jela.

minister n 1 waziri Prime M~ Waziri Mkuu ~ without portfolio waziri bila wizara maalumu. 2 mjumbe wa serikali (chini ya balozi). 3 ~ of religion mchungaji; mhubiri. vi ~ to tumikia; saidia. ~ial adj 1 -a waziri. 2 -a wizara/baraza la mawaziri. ministration n utumishi; msaada. ministry n 1 wizara. 2 the ministry n jamii ya makasisi na wachungaji; uchungaji. enter the ministry -wa mchungaji. ministrant attrib adj (formal) -a kutumikia n msaidizi, mtumikiaji.

minnow n samaki mdogo wa mtoni. Triton among the ~s mtu aonekanaye mkubwa mbele ya wanyonge.

minor adj 1 -dogo, -a chini, hafifu ~ breach uvunjaji mdogo. 2 (mus) in a ~ key (fig) kwa huzuni, kwa kusononeka. n (leg) mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nane. ~ity n 1 (leg) utoto. 2 wachache, walio wachache. be in a ~ity -wa

Minotaur

I'm in a ~ity of one niko peke yangu. ~ity government n serikali ambayo ina chini ya nusu ya nafasi za wabunge. ~ity programme n (TV, radio) kipindi kwa ajili ya wachache. ~ity judgement n hukumu ya wachache.

Minotaur n (Gk myth) Minoto: zimwilionekanalo nusu mtu na nusu mnyama.

minster n kanisa kubwa.

minstrel n 1 (in the Middle Ages)

~sy n sanaa na nyimbo za watunzi na mwimbaji msafiri.

mint1 n (leaves) nanaa;(plant)mnanaa.

mint2 n 1 kiwanda cha kutengenezea/ kupiga chapa sarafu. 2 make/earn a ~ (of money) pata pesa nyingi. 3 (atrrib of medals, stamps, prints, books etc) -pya. in ~ condition -pya; safi kabisa. vt 1 piga chapa sarafu. 2 buni (maneno n.k.).

minus prep kasoro, bila he came back

alirudi vitani bila mkono mmoja adj ~ sign n alama ya kutoa. n kutoa.

minuscule adj -dogo sana.

minute1 n 1 dakika. ~ gun n mzinga

~ hand n mshale wa dakika. ~man n mwanamgambo (aliye tayari kupigana wakati wowote). 2 (short time) kitambo kidogo muda mdogo just a ~ ngoja kidogo any ~ wakati wowote. in a ~ sasa hivi. to the ~ juu ya alama. the ~ (that) mara tu. up-to-the ~ attrib adj -a kisasa kabisa. 3 (pl) kumbukumbu (za mkutano n.k.). vt andika kumbukumbu.

minute2 adj 1 -dogo sana, -dogodogo.2 (trifling) hafifu. 3 (exact) halisi, barabara; angalifu sana. ~ly adv. ~ness n.

minutiae n pl mambo madogo madogo.

minx n msichana fidhuli, asiye na

miracle n 1 muujiza. ~ play n (in the

Middle Ages) maigizo ya maisha ya Kristo/Watakatifu wa Kikristo. 2 ~ of maajabu ya, mfano wa ajabu. miraculous adj -a muujiza; -a kustaajabisha. miraculously adv.

mirage n 1 mazigazi. 2 alinacha.

mire n kinamasi, matope. be in the ~ (fig) pata matatizo. sink into the ~ kwama. drag somebody/ somebody's name through the ~ fedhehesha, chafua jina. vt,vi 1 pakaza matope, kwamisha kwenye matope. 2 (fig) tatiza. miry adj -enye tope.

mirror n 1 kioo (cha kujitizamia). ~

image n taswira geu. 2 (fig) kiakisi. vt akisi.

mirth n furaha, kicheko. ~ful adj. ~fully adv. ~less adj bila furaha.

mis- pref -baya, vibaya; (ku)to...~trust n kutoamini.

misadventure n shari. death by ~ kifo cha ajali.

misadvise vt potosha, shauri vibaya/

visivyo.

misalliance n uhusiano mbaya (hasa

katika ndoa); ndoa ya wasokufu.

misanthrope n mchukia wanadamu

wenziwe; mkaa pweke. misanthropic adj -a kuchukia watu; -a kudharau (kuepukana na) watu. misanthropy n kuchukia watu; chuki ya watu.

misapply vt tumia vibaya the town

council officials misapplied our development levy maafisa wa halmashauri ya mji walitumia vibaya kodi yetu ya maendeleo. misapplication n.

misbecome vt -siowezekana. misbecoming adj -siofaa.

misbegotten adj 1 mwanaharamu, haramu. 2 (colloq) duni, nyonge, -a kudharaulika, -a bure.

misbehave vt,vi kosa adabu, -wa na tabia mbaya. misbehaviour (US= misbehavior) n.

miscalculate vt,vi kokotoa vibaya,

kosea. miscalculation n.

miscall vt ita kwa jina lisilo, kosea

miscarry

miscarry vt 1 (of plans, etc) -tofaulu, tokea vibaya, haribika, enda kombo the plan miscarried mpango haukufaulu/haukufanikiwa. 2 (of letters etc) kosa kufikishwa/kufika the letter miscarried barua haikufika. 3 (of a woman) haribu mimba. miscarriage n 1 kuharibika mimba. 2 miscarring of justice n upotoshaji wa haki. 3 kutowasilisha, kutofika mahala utakiwapo.

miscast vt 1 (of a play) pangia sehemu vibaya, chagua vibaya waigizaji. 2 (of an actor) pangiwa, pewa nafasi -siyoimudu.

miscegenation n uchotara, usuriama; kuzaa watoto chotara.

miscellaneous adj 1 anuwai. 2 (of person) mtu mwenye sifa/tabia anuwai/kadha/tafauti-tafauti. miscellany n mchanganyiko wa vitu vya namna mbalimbali. miscellanea n mchanganyiko wa maandishi.

mischance n bahati mbaya by ~ kwa bahati mbaya.

mischeif n 1 madhara; hasara; uharibifu. to do somebody a ~ kumdhuru. 2 fitina. make ~ (between) tia fitina. ~ making n kufitini. 3 utundu, utukutu the child did it out of ~ mtoto alifanya kwa utundu. 4 utani (usio na nia mbaya). 5 mtundu. mischievous adj 1 -enye fitina. 2 -tundu. 3 -tani, -enye utani. mischievously adv. mischievousness n.

misconceive vt,vi 1 elewa vibaya. 2 ~ of elewa jambo visivyo. misconception n.

misconduct n 1 mwenendo mbaya,

professional ~ kinyume cha miiko ya weledi, tabia mbaya ya kazi. 2 uongozi mbaya. vt 1 ~ oneself (with somebody) -wa na tabia mbaya. 2 ongoza vibaya.

misconstrue vt elewa vibaya. mis-

n welewa/fasili mbaya.

miscount vt,vi 1 hesabu vibaya. 2 kosa makisio n 1 kuhesabu vibaya (hasa

kura, vitu n.k.).

miscreant n (dated) baa, mtu mwovu.

misdate vt kosea tarehe.

misdeal vt,vi (of playing cards) gawa vibaya. n mgawanyo mbaya (wa karata).

misdeed n tendo baya; kosa.

misdemeanour (US) misdemeanor n (leg) kosa dogo.

misdirect vt ongoza/elekeza/onyesha

vibaya. ~ion n.

misdoing n see misdeed.

mise en scene n (of a play) mandhari; (fig) mazingira (ya tukio).

miser n 1 bahili. ~ly adj. ~liness; ~y n umaskini, taabu, mateso, maumivu suffer ~y from the stomach ache pata maumivu tumboni; teseka. put the animal out of its ~y ua mnyama (aliyeumia sana). 2 (pl) baa. 3 (colloq) hohehahe; mlalamishi. ~able adj 1 -enye taabu; maskini; duni, -nyonge what a ~able life! maisha gani haya ya taabu! 2 -enye kusababisha taabu/umaskini. 3 hafifu.

misfire vi 1 (of a gun) -tolipuka;

-tofyatuka. 2 (of motor-engine) -towaka. 3 (colloq of joke, etc) -tofanikiwa. n kutofyatuka; kutowaka; kutolipuka; kutofanikiwa.

misfit n 1 vazi lisilo sawa na kimo,

vazi lisilokaa. 2 (fig) mtu asiyefaa/ asiyechukuana na wenziwe.

misfortune n msiba, taabu, balaa; bahati mbaya.

misgive vt -wa na shaka, -wa na wasiwasi my heart ~s me moyo wangu umejaa wasiwasi. misgiving n -wasiwasi, mashaka.

misgovern vt tawala vibaya. ~ment n.

misguide vt 1 elekeza vibaya. 2 shauri vibaya. ~d adj -jinga, -liopotoka.

mishandle vt 1 shughulikia vibaya. 2 tendea mtu vibaya.

mishap n bahati mbaya; ajali.

mishear vt elewa vibaya, -tosikia vema.

mishmash n shaghalabaghala.

misinform vt potosha I was ~ed

misinterpret

~ation n.

misinterpret vt tafsiri/elewa/eleza vibaya. ~ation n.

misjudge vt,vi pitisha uamuzi/kadiria vibaya; elewa/ fikiria vibaya.

mislay vt weka (kitu) pasipo pake,

I have mislaid my wallet nimepoteza pochi yangu.

mislead vt potosha be misled potoshwa.

mismanage vt simamia/ongoza vibaya; haribu madaraka/taratibu. ~ment n

mismatch v tochukuana. n kutochukuana

misname vt (usu possive) taja kwa jina lisilo lake.

misnomer n matumizi mabaya ya neno/ jina; kosa, kioja.

misogamy n kuchukia ndoa. misogamist n.

misogyny n kuchukia wanawake. misogynist n mchukia wanawake.

misplace vt 1 weka mahali pasipo pake; weka mahali pasipofaa/ pasipostahili. 2 (usu passive) penda mtu/kitu isivyo stahili.

misprint vt chapa vibaya. n mategu.

misprision n (leg) kuficha kosa. ~ of treason n kuficha uhaini.

mispronounce vt tamka vibaya.

n.

misquote vt dondoa vibaya. misquotation n.

misread vt 1 soma visivyo. 2 elewa

misrepresent vt wasilisha/hudhurisha visivyo, tafsiri vibaya.

misrule n kutawala vibaya. vt tawala vibaya.

miss1 n 1 M~ binti, Bi. M~ (Anna) Kyomo Bi Anna Kyomo. 2 msichana; binti. 3 (vocative) dada, mama. ~y n (colloq familiar) msichana; binti.

miss2 n kukosa shabaha, kutopata, kutofanikiwa, kutofuma. give something a ~ (colloq) acha makusudi, kwepa. a ~ is as a good as mile (prov) kukosa ni kukosa hata kama ni kidogo. vt,vi 1 kosa kupata/kuona/kusikia/kufuma. ~ the

target kosa shabaha,kosea lengo ~ one's way potea njia he ~ed the train alichelewa garimoshi can't ~ it huwezi kuikosa; usikose ~ the obvious toelewa iliyo wazi/dhahiri. 2 kumbuka (kwa hamu ya kuona tena) we all ~ you tunakukosa sote we shall ~ you if you go ukienda tutakukumbuka. 3 ~out (on something) (colloq) kosa nafasi, kosa kufanya jambo. ~ something out acha; sahau; -toingiza kitu. ~ing adj -sioonekana, -liopotea.

missal n (rel) misale.

misshapen adj -lioumbuka, -lioumbika vibaya.

missile n kombora (attrib) ~ site/base n kituo cha kurushia makombora. guided ~ n kombora linaloongozwa kwa mitambo ya elektroniki.

mission n 1 ujumbe (kwa kazi maalumu) (agh. katika nchi ya kigeni). 2 (rel) misheni. 3 ~ in life wito. 4 (esp. US) kazi maalum. ~ary n mmisionari adj -a misheni, -a misioni.

missive n (hum) barua (agh ndefu),

waraka.

misspell vt kosea tahajia.

misspend vt tumia vibaya, poteza, fuja Kiro misspent his youth Kiro alitumia vibaya ujana wake.

misstate vt kosea kusema/kueleza.

~ment n.

missus;missis n (colloq/sl) (used with the, my, his, your) mke where is your ~ mke wako yuko wapi?

mist n 1 umande; ukungu. 2 utando

machoni (agh. hutokana na machozi); (fig) ukungu; kitu chochote kinachosababisha mtu kushindwa kuelewa maana. vt,vi ~ (over) funika na ukungu/utando. ~y adj. ~ily adv. ~iness n.

mistake n kosa. by ~ kwa makosa. and no ~ bila shaka he is a fool and no ~ yeye ni mpumbuvu bila shaka. vt,vi 1 kosa, kosea, fahamu/fikiria visivyo. there is no mistaking ni dhahiri. 2 ~

mister

dhania visivyo kweli, changanya na I always ~ Kurwa for Doto mara kwa mara huwa nadhania Kurwa kuwa ni Doto. be ~n (about something) kosea if I'm not ~n kama sikosei. by ~ bila kukusudia.

mister vt, n always written Mr Bwana (jina la kumtaja mwanamume pamoja na jina lake Mr Mugabe Bwana Mugabe.

mistime vt fanya kitu wakati usio wake.

mistletoe n mlimbo: mmea ambao matunda yake hutoa ulimbo.

mistook v pt of mistake

mistranslate vt tafsiri visivyo. mistranslation n.

mistreat vt tesa, sumbua, fanyia/tendea vibaya. ~ment n.

mistress n 1 mwanamke mkuu wa kaya; bimkubwa. 2 mwalimu wa kike the Kiswahili ~ mwalimu (wa kike) wa Kiswahili. 3 bingwa/mweledi wa kike she is a ~ of handcraft ni mjuzi wa kazi za mikono. 4 (in stories of the 18th c) bibi. 5 (poet) mpenzi. 6 kimada, hawara.

mistrial n (leg) kesi iliyobatilishwa/ batili.

mistrust vt -toamini, tilia shaka, dhania vibaya. n ~ (of) shaka, tuhuma. ~ful adj -enye kutia shaka. ~fully adv.

misunderstand vt elewa visivyo,elewa

~ing n kutoelewana, kukosa maelewano, suitafahamu there is some ~ ing between Mary and John kuna suitafahamu kati ya Mary na John.

misuse vt tumia vibaya. n matumizi

mite1 n 1 kimchango, msaada kidogo contribute one's ~ toa uwezayo. 2 kitu kidogo a ~ of a child kitoto kidogo sana.

mite2 n mdudu mdogo mharibifu (k.v. utitiri, nyenyere n.k.).

mitigate vt,vi punguza; punguka ukali (k.v. wa maumivu) ~ pain punguza

maumivu. mitigating circumstances n hali inayopunguza uzito/ukali wa makosa, madhambi n.k. mitigation n.

mitre(US= miter) n 1 kofia ya kiaskofu. 2 (carpentry) kingamo: namna ya kuunga vipande viwili vya mbao.

mitt n 1 glovu (yenye tundu moja la

vidole vinne na moja la kidole gumba). 2 glovu ya besiboli. 3 (sl) ngumi; mkono.

mitten n 1 see mitt 2 glovu (inayo

funika kiganja na nyuma ya kiganja tu).

mix vt,vi 1 changanya ~ work with

pleasure changanya kazi na starehe. 2 ~ (with) (of persons) ishi pamoja katika jamii/jumuiya) he doesn't ~ well haelewani na watu. 3 ~ something/somebody up (with something/somebody) vuruga, boronga; kosea (kwa kufananisha) dont ~ me up with my brother usinifananishe na kaka yangu. be/get ~ed up in/with something ingizwa/ jihusisha na shughuli fulani don't get ~ed up in this business usijiingize katika shughuli hii. ~-up n hali ya kutatanisha. ~ed -up adj -enye kuchanganyikiwa. n mchanganyo, mchanganyiko; mseto. ~ed adj -enye mchanganyiko a ~ school shule ya mchanganyiko (wavulana na wasichana). have ~ed feelings (about something) wa na shaka/ wasiwasi juu ya mtu/kitu. ~ed blessing n kitu chenye faida na hasara/uzuri na ubaya. ~ed farming n ukulima wa mchanganyiko/mseto. ~ed grill n nyama mchanganyiko iliyobanikwa. ~ed marriage n ndoa ya watu wasiokuwa na rangi/dini moja. ~ed metaphor n sitiari mchanganyiko. ~er n 1 mchanganyaji; kichanganyi. 2 (colloq) a good/bad ~er n mtu aishiye vizuri/vibaya na watu. ~ture n mchanganyo; mchanganyiko; (medical) dawa (ya

miz(z)en

a cough ~ture dawa ya kikohozi. the ~ture as before (colloq) utaratibu ule ule (kama ilivyokuwa hapo nyuma).

miz(z)en n (naut) ~ (mast) n galme. ~ (sail) n tanga la galme.

mizzle vi (dial or colloq) nyunya.

mnemonic adj -a kusaidia kukumbuka. ~s n mbinu elimu ya kumbukumbu.

mo (sl abbr for) moment.

moan vi,vt piga kite.

moat n handaki la maji (linalozunguka boma). vt zungushia (boma) handaki la maji.

mob n 1 kundi la watu wenye fujo; ghasia ya watu ~ law/rule sheria mkononi. 2 the ~ n watu; umma; (sl) kundi la majambazi. vt,vi songamana (kwa ghasia). ~ster n mmojawapo wa majambazi.

mob-cap n kitambaa/ushungi/kofia ya mwanamke (ivaliwayo ndani ya nyumba inafunika nywele zote).

mobile adj 1 -a kwenda; -a kuweza kwenda. 2 (of face, person) -epesi kugeuka. ~ clinic n kliniki itembeayo (agh. kwa gari). mobility n.

mobilize vt,vi andaa watu kufanya jambo, hamasisha. mobilization n.

mocassin n 1 ngozi ya swala; sapatu za ngozi ya swala. 2 (bio) ~ snake nyoka mkali kama pili (Amerika).

mocha n 1. moka: kahawa safi kabisa. 2 ladha ya mchanganyiko wa kahawa na chokleti.

mock vt,vi 1 ~ somebody; ~ at somebody dhihaki. ~ing bird n ndege mwigo (anayeiga milio ya ndege wengine). 2 katisha tamaa. make a ~ of fanyia mzaha/dhihaki. ~-up n mfano wa kitu (kinachokusudiwa kutengenezwa); (printing) pesta mwigo; mzaha; dhihaka adj -a kuiga; -a mzaha; bandia; -siohalali ~ exam mtihani wa majaribio. ~er n. ~ingly adv. ~ery n dhihaka. ~-heroic n -enye kudhihaki ushujaa (katika fasihi).

mod adj (colloq) -a kisasa; -a madaha.

n M~ (1960 GB) kijana aliyevaa nguo za kisasa na kupanda skuta.

mode n 1 namna; mtindo. 2 (gram)

hali. 3 (maths) modi. 4 (music) hali ya ngazi. 5 (commerce) kati. modal adj 1 (gram) -a hali. 2 (maths) modi. ~modal class n daraja modi. modality n hali, namna. ~l n 1 mfano, kielelezo, mtindo; kifani. 2 artist's ~l kifani cha msanii. 3 (perfect example) kitu/mtu mwendo, mfano mzuri. 4 mtu anayeonyesha mitindo mipya ya nguo she is a fashion ~l anaonyesha mitindo mipya ya nguo.

model vt,vi 1 ~ (in) finyanga, fanyiza (umba) kwa kufuata mfano; fanya mfano. 2 onyesha mtindo. 3 ~ oneself on/upon somebody fuata mfano wa mtu mwingine, iga mtu mwingine. ~ler n mfinyanzi. ~ling n ufinyanzi; uonyeshaji mitindo.

modem n modemu: kidude cha kuunganisha kompyuta na vifaa vingine kupitishia data.

moderate adj -a kiasi; -a kadiri; -a

wastani n mtu mwenye siasa, tabia, mwendo wa kiasi. ~ly adv. vt,vi 1 punguza (joto, ukali, harara, nguvu); tuliza ~ one's demands punguza madai. 2 simamia mjadala/mtihani (wa chuo kikuu); rekebisha mtihani. moderation n 1 kiasi; kadiri; wastani; usimamizi wa mjadala/ mtihani. 2 pl moderations n (also mods) mitihani ya shahada ya kwanza (oxford). moderator n 1 msimamizi (wa mjadala, michezo n.k.) mtahini. 2 mpatanishi. 3 (physics) kipunguzo cha nutroni katika funguatomu. 4 msimamizi wa baraza/mahakama ya kanisa.

modern adj 1 -a kisasa. 2 -a siku hizi;-pya. n mtu (mwandishi n.k.) wa kisasa. ~ism n 1 usasa; zama hizi. 2 (rel) kufuata mambo ya kisasa badala ya desturi za kale. ~ist n mtu wa kisasa. ~istic adj. ~ity n kuwa wa kisasa, usasa. ~ize vt fanya kuwa -a kisasa, geuza upya.

modest

ization n.

modest adj 1 -siojivuna. 2 -a wastani,

~y n staha; wastani with due ~y pamoja na adabu zipasazo in all ~y bila kujivuna.

modicum n kadiri, kiasi kidogo.

modify vt 1 geuza, badilisha, badili

(gram) vumisha. modifier n (gram) kivumishi. modification n ubadili; badiliko; uvumishi. modifiable adj -a kubadilishika; -a kugeuzika.

modish adj -a kisasa, -a (kufuata) mitindo.

modiste n (formal) mshonaji (nguo).

modulate vt,vi rekebisha; geuza; (mus) badili ufunguo (sauti n.k.). modulation n kubadili sauti; urekebishaji. modulator n

module n 1 kipimo. 2 kitengo/kiunzi huru. 3 sehemu sawa/lingano. command ~ n kiunzi/kitengo huru cha nahodha; chombo cha anga. modular adj.

modus operandi n (Lat) utaratibu/mbinu ya utendaji, jinsi ya kufanya/kushughulikia jambo.

modus vivendi n (Lat) namna ya kuishi; mapatano ya muda.

mogul n (colloq) mtu maarufu, tajiri, kigogo.

mohair n mahea: nguo/nyuzi/kitambaa kilichotengenezwa kwa manyoya ya mbuzi, (wa aina ya Angora).

Mohammedan n see Muhammad.

moiety n sehemu/nusu ya kitu (kilichokatwa/gawanywa).

moil vi (only in) toil and ~ fanya/chapa kazi kwa bidii.

moist adj -a majimaji, -a unyevu;

chelema a ~ atmosphere hewa yenye unyevunyevu. ~en vt rowesha kidogo, tia maji kidogo. ~ure n unyevu.

moke n (GB sl) punda.

molar n gego.

molasses n molasi.

mold n see mould.

mole1 n (spot) kiwaa cheusi, baka

jeusi.

mole2 n fuko: mnyama mdogo anayefukua chini. blind as a ~ /bat pofu; toona vizuri.~hill n kichuguu. make mountains out of ~ hills tia chumvi, kuza jambo.

mole3 n (breakwater) bomazuizi (baharini).

molecule n (chem/physics) molekuli.

molest vt sumbua, udhi, kera, (kwa

makusudi). ~ation n.

moll n mwanamke hawara/mwenzi wa mhalifu; malaya.

mollify vt tuliza, ridhisha mtu, bembeleza. mollification n.

mollusc (US mollusk) n moluska: vinyama kama konokono, koa, kombe, pweza, ngisi n.k.

mollycoddle n mlimbwende kupindukia vt engaenga; dekeza.

Moloch n (Bible) Mungu ambaye

watoto walitolewa kwake kama dhabihu; (fig) tishio; janga.

Molotov n (saying, mil) ~ cocktail n

bomu la mkono.

molt v see moult.

molten n pp of melt adj -lioyeyuka; -a kuyeyushwa ~ metal metali iliyoyeyuka.

molto adv (mus) sana.

mom n US (colloq) mama.

moment n 1 kitambo kidogo, muda

mfupi sana, kufumba na kufumbua; wakati at that ~ wakati ule ule go this ~ nenda sasa hivi for the ~ kwa sasa. not for a ~ hata kidogo, kamwe! 2 the ~ (used as conj) mara. 3 (importance) maana, thamani. man of the ~ mtu mwenye sifa za siku hizi. of great/ small/little/no ~ -enye maana kubwa/ndogo/n.k. sasa. ~ary adj -a mara moja, -a kupita upesi sana; -a kuweza kutokea wakati wowote be in ~ ary expectation of something tumaini kuwa jambo laweza kutokea wakati wowote (hivi karibuni). ~ arily adv. ~ous adj -a maana sana. ~ously adv. ~ousness n.

momentum n 1 momenta: nguvu

monarch

(fig of events) msukumo, nguvu.

monarch n 1 mfalme; (fig) mtawala mkuu. 2 (biol) kipepeo mkubwa (wa rangi nyeusi na ya machungwa). ~ic; ~al adj. ~ism n mfumo wa ufalme. ~ist n mfuasi wa ufalme. ~y n ufalme.

monastery n nyumba kubwa ya utawa. monastic adj -a utawa; -a nyumba ya watawa. monasticism n maisha ya utawa.

monaural adj -a sikio moja, -a kipazasauti kimoja, -a mono.

Monday n Jumatatu.

money n fedha (sarafu, noti) inayotumika katika kuuza na kununua. be coining/minting ~ tajirika harakaharaka. be in the ~ (sl) tajirika. make ~ chuma fedha. (pay) ~ down lipa fedha taslimu. put ~ into something wekeza. ready ~ n fedha taslimu. monetary adj -a mambo ya fedha, -a fedha. monetary policy n sera ya fedha. monetize vt 1 toa fedha zianze kutumika nchini. 2 panga thamani ya sarafu; utajiri. marry ~ oana na tajiri. get one's ~'s worth faidi; pata kitu cha thamani ya fedha alizotoa mtu. ~ makes the mare go fedha ni motisha ya mambo. pl monies n raslimali, fedha, mali. (compounds) ~ bags n sl tajiri, kizito. ~-box n sanduku la fedha. ~ changer n mvunja fedha. ~-lender n mkopesha fedha, mkopeshaji fedha. ~-order n hawala ya fedha. ~ spinner n (colloq) kitabu, mchezo, mradi wenye kumimina hela. ~ed adj -enye mali the ~ed interest mabepari. ~less adj fukara.

monger n mfanyi biashara, mchuuzi, mwuzaji.

mongolism n upunguani wa kuzaliwa na kichwa bapa. mongol n punguani, taahira.

mongoose n nguchiro.

mongrel n mbwa chotara; (person) (derog) chotara, suriama adj -a

chotara, -a mchanganyiko.

monies n see money.

monitor n 1 msimamizi; (school)

kiranja. 2 (radio) msikilizaji na mtoaji habari za kituo cha nje. 3 (warship) manowari ndogo. 4 chombo cha kujaribia usafirishaji wa matangazo ya redio/TV; chombo cha kufuatilia urukaji wa makombora, n.k. vt,vi fuatia, simamia; (radio) sikiliza kituo cha nje.

monk n mtawa wa kiume, sufii. ~ish adj.

monkey n (small light) tumbili; ngedere; (small dark) kima;(colobus) mbega. ~ business utundu. have a ~ on one's back (sl) -wa mlevi wa bangi n.k.; -wa na chuki/kinyongo/ donge ~ face uso wa paka. get one's ~ up (sl) -wa na hasira, kasirika. put somebody's ~ up (sl) kasirisha mtu. (compounds) ~-bread n buyu. ~-jacket n koti fupi (livaliwalo na mabaharia). ~-nut n karanga, njugu (nyasa). ~ puzzle n arokaria: mti usiopandika kwa sababu una miiba mingi. ~ tricks n utundu. ~-spanner; ~ wrench n 1 (tech) spana (ya matairi). 2 (mischievous child) mtundu. 3 (sl) pauni 500 au dola 500. vi ~ about (with) 1 chezea. 2 iga.

mono- (pref) -a moja tu, -a mara moja tu, -enye moja tu.

monochrome n picha/mchoro wa rangi moja adj -a rangi moja.

monocle n rodi: miwani ya jicho moja.

monoculture n kilimo cha zao moja.

monogamy n ndoa ya mke/mume

mmoja. monogamist n mtu mwenye mke/mume mmoja. monogamous adj -a ndoa moja. ~ marriage n ndoa ya mke/mume mmoja.

monogram n monogramu: chapa ya herufi mbili au zaidi zilizo changanyika pamoja, moja juu ya nyingine.

monograph n monografia: kitabu,

makala yenye habari ya jambo/kitu/ elimu moja tu.

monolingual

monolingual adj -a lugha moja a ~ dictionary kamusi ya lugha moja.

monolith n nguzo ya jiwe tu; nguzo

~ic adj -a mnara mkubwa; -a mfumo wa mawazo ya aina moja.

monologue n mazungumzo binafsi.

monomania n monomania: kushikia

~c n -enye monomania; mgonjwa wa wazimu/wazo moja.

monoplane n ndege ya bawa moja.

monopoly n 1 uhodhi; ukiriritimba. ~

n ubepari kiritimbi. 2 haki ya pekee. monopolist n mhodhi. mkiritimba. monopolize vt kiritimba, hodhi. monopolization n.

monorail n reli moja; mfumo wa treni ya reli moja.

monosyllable n silabi moja k.m. la, tu answer in ~s jibu "ndiyo au la"; jibu kwa mkato. monosyllabic adj

monotheism n imani kwamba kuna Mungu mmoja tu. monotheist n mwamini Mungu mmoja. monotheistic adj -enye kuamini Mungu mmoja.

monotone n toni moja, kidatu kimoja speak in ~s sema kwa toni/kidatu kimoja.

monotonous adj -siobadilika; -a kukinaisha, kinaishi. monotony n ukinaifu, kutobadilika mwenendo; uchovu (ubaridi, uchoshi) (kwa kutobadilika mambo). ~ly adv.

monotype n monotaipu: mashine inayopanga/chapa herufi kwa herufi.

monsieur n (Fr) bwana.

monsoon n monsuni: pepo za msimu katika Bahari ya Hindi; masika (yatokanayo na pepo hizo).

monster n 1 jitu la kutisha, dubwana. 2 (unnatural) jinamizi. 3 (brutalperson) mtu mkali; katili. 4 (giant) pandikizi. monstrous adj 1 -kubwa mno, -a ajabu. 2 (terrifying) -a kuogofya, -a kuchukiza. 3 pumbavu, baya sana. monstrosity n dubwana; udubwana, kitisho; kioja. monstrously adv.

montage n kupanga filamu.

montane adj -a milima.

month n mwezi what ~ is it? huu ni mwezi gani? it is the fifth ~ ni mwezi wa tano. a ~ of Sundays muda mrefu sana. ~ly adj ~ly pay mshahara wa mwezi. n 1 jarida linalotoka kila mwezi. 2 (pl) (arch). ~lies n hedhi, damu, mwezi adv kila mwezi, a mwezi. calendar ~ n mwezi wowote katika mwaka. lunar ~ n kipindi mwezi unapokamilisha mzunguko wa dunia.

monument n 1 (memorial) jengo/

mnara/sanamu ya ukumbusho, kumbukumbu. 2 kazi ya mfano bora (istahiliyo kukumbukwa). ~al adj -kubwa sana; -a sifa za daima; -a ukumbusho ~al ignorance ujinga mkubwa mno ~al mason mwashi wa mawekaburi.

moo n mlio wa ng'ombe. vt (of cows) lia. ~-cow n (child's word for) ng'ombe.

mooch vt,vi 1 ~ (about) (colloq) tangatanga, susurika, zurura; (sl US) doea.

mood1 n (gram) hali.

mood2 n (temper) hali ya moyo be in the ~ for something tamani kitu; jisikia have ~s -wa na sununu. ~y adj -enye tabia ya kubadilika-badilika, -enye kununa; -enye kukasirika. ~ily adv. ~iness n usununu.

moolah n (sl) fedha.

moon1 n 1 the ~ mwezi full ~ mwezi mpevu new ~ mwezi mchanga. once in a blue ~ (colloq) mara chache tu. cry for the ~ taka sana kitu kisichowezekana. promise somebody the ~ toa ahadi nyingi. 2 (compounds) ~beam n mbalamwezi, mwali wa mwanga wa mwezi. ~-calf n 1 dubwana. 2 mpumbavu. ~-face n uso mviringo. ~light n mbalamwezi. vi fanya kazi nyingine na kulipwa (wakati umeajiriwa kwingine). ~light night usiku wa mbalamwezi. a/no ~ -a/sio mbalamwezi. ~lit adj -liomulikwa na mwezi. ~ shine n

moon

(sl US) gongo. 3 (poet) mwezi. ~less adj bila mbalamwezi; usiku wa giza. ~stone n kito rangi ya buluu yenye kijani kibichi. ~struck adj -enye wazimu.

moon2 vi,vt 1 ~(about/around) zurura, susurika; zama ndotoni. 2 ~ away pitisha wakati ovyo. ~y adj -enye kunyong'onyea.

Moor n chotara wa Kiberiberi na Kiarabu. ~ish adj.

moor1 n mbuga, nyika. ~-fowl/game n kwale mwekundu. ~-cock n kwale dume. ~ hen n kwale jike. ~ land n mbuga.

moor2 vt funga chombo ufukoni; tia

~ing mast n mlingoti wa kufungia chombo. ~ings n (pl) 1 kebo, amari, minyororo. 2 maezi.

moose n aina ya kongoni (apatikanaye Amerika Kaskazini).

moot adj (only in) a ~ point/ question -nayohitaji kujadiliwa; -a kinadharia, -sio na maana kiutendaji/ -kuigiza ~ court mahakama bandia. vt leta kwa majadiliano.

mop1 n 1 ufagio; tamvua. 2 a ~ of hair nywele za matimutimu. vt pangusa kwa ufagio; tamvua/piga deki. ~ up futa ~ up ones tears futa machozi; (colloq) maliza, komesha. ~ the floor with somebody shindwa kabisa.

mop2 n (arch only in) ~ and mow kunja uso.

mope vi huzunika, jisikitikia, sononeka. the ~s n huzuni. ~y adj -enye huzuni/masikitiko.

moped n baiskeli moto.

moquette n kitambaa kizito cha mazulia.

moral adj 1 -adilifu, -nyofu. 2 -ema, adili. 3 (having moral sense, free will) -enye hiari/akili ya kuchagua mema au mabaya, -enye utashi. 4 -enye kuonyesha haki. a ~ certainty n jambo linaloelekea kuwa kweli ~ law kanuni ya mema na mabaya a matter of ~ obligation wajibu,

lipasalo he gained ~ victory alishindwa, lakini akashinda uungwana/utu. ~ courage/ cowardice n moyo wa kuthubutu/ kutothubutu. give somebody ~ support saidia kwa kuunga mkono mawazo yake. n 1 (of story etc) fundisho. 2 (pl) maadili he has no ~s mtu huyu si mwadilifu, hana murua offensive to the ~s of the community -a kukiuka maadili ya jamii. ~ly adv. ~ist n mwadilifu; mwalimu wa maadili. ~istic adj (often derog) -enye kuhubiri. ~ity n 1 uadilifu, murua; maadili. 2 (character) tabia. 3 ~ity (play) n mchezo/tamthiliya ya maadili. ~ize vt,vi 1 fafanua/elezea wema au ubaya. 2 ~ (about/on/upon) adilisha. 3 (often derog) hubiri. ~e n moyo, imani, nguvu,hamasa.

morass n kinamasi; (fig) utata. ~y adj -enye kinamasi.

moratorium n ruhusa ya kukawiza

malipo ya deni/jambo lolote kwa muda.

morbid adj 1 -gonjwa, -enye kuugua. 2 (of the mind) chafu; -enye kuwaza mambo ya kutisha au mambo ya kuchukiza. ~ity n. ~ness n. ~ly adv.

mordant adj -a kuuma; -a kukejeli.

more adj 1 zaidi. neither ~nor less si zaidi wala si pungufu. 2 no ~ hakuna tena zaidi what ~? nini tena. 3 a little ~ kiasi kidogo zaidi (of food) have some ~ ongeza (chakula) have you any ~ apples unayo matofaa mengine? I have some ~ nina mengine kuzidi; (of epidemics) ~ outbreaks milipuko zaidi ~ than enough zaidi kupita kiasi ~ than kuliko, zaidi ya, fauka ya see ~ of somebody ona mtu mara nyingi adv 1 zaidi and what is ~ zaidi ya hayo you need to rest ~ unapaswa kupumzika zaidi ~ beautifully kwa vizuri zaidi the ~ zaidi you should work ~ fanya kazi zaidi. be no ~ -fa, isha

mores

zidi kuwa. 2 tena, once ~ rudia tena/mara nyingine we saw him no ~ hatukumwona tena. 3 ~ or less takriban, kwa kadiri. 4 ~ and ~ kwa hatua, zaidi na zaidi. no ~ than si zaidi ya n zaidi, nyongeza. ~over adv aidha, zaidi ya.

mores (pl) desturi, mila, maadili.

Moresque adj -a Kiislamu.

morganatic n. ~ marriage n ndoa baina ya mume mwenye nasaba/hadhi ya juu na mke wa nasaba/hadhi ya chini.

morgue n 1 nyumba ya maiti. 2 (in newspaper or office) jalada la kumbukumbu ya maisha ya watu mashuhuri ambao hawajafa bado.

moribund adj mahututi, -a kukaribia

morn n (poet) asubuhi.

morning n asubuhi early ~ alfajiri, mapambazuko good ~! subalkheri. ~s adv asubuhi/kila asubuhi. ~-room n sebule ndogo. ~-sickness n kichefuchefu cha mjamzito asubuhi. the ~-star n zuhura, nyota ya asubuhi.

morocco n ngozi laini iliyotokana na ngozi ya mbuzi (hutumika kufanyia majadala ya vitabu.).

moron n punguani, taahira, mtu aliyevia akili, mtu mwenye akili afkani; (colloq) mpumbavu, zuzu. ~ic adj.

morose adj -a uchusa, -enye huzuni, -enye kununa; -a chuki. ~ly adv. ~ness n.

morpheme n (ling) mofimu.

morphia; morphine n afyuni.

morphology n mofolojia; umbo. morphological adj.

morrow n 1 (liter) siku inayofuata/ iliyofuata, kesho yake on the ~ of war baada ya vita. 2 (arch) asubuhi.

morsel n chembe; funda.

mortal adj 1 -enye kufa all human beings are ~ binadamu wote hufa. 2 -a kufisha; -liosababisha kifo. ~sin n dhambi ya mauti. 3 -a kudumu hadi kifo. ~ enemies n uadui unaodumu

hadi kufa/kifo. ~ combat n mapambano baina ya watu wawili (hadi mmoja kufa). 4 (colloq) sana, kubwa/ndefu sana. n binadamu. ~ly adv 1 kwa kufisha. 2 sana, mno. ~ity n 1 hali ya kuweza kufa, mauti. 2 vifo. ~ity rate n kiwango cha vifo. 3 idadi ya vifo there was a high ~ ity watu wengi walikuwa wanakufa. ~ity tables n (insurance) jedwali za makadirio ya uhai.

mortar n 1 (for building) mota. 2 (forpounding) kinu. 3 (gun) kombora. vt changanya sementi na mchanga. ~- board n 1 kibao cha udongo, ubao mota (mwashi anapojenga). 2 (cap) kofia inayovaliwa na wanachuo wa chuo kikuu.

mortgage n 1 rehani, poni.2 (document) hati ya kuweka rehani chattel ~ rehani ya chombo. vt,vi ~ (to) (for) weka rehani. be ~d up to the hilt weka rehani kila kitu. ~r n mwekewa rehani. mortagagor n mweka rehani.

mortician n (US) msimamizi wa mazishi.

mortify vt,vi 1 aibisha, dhalilisha.

2 ~ the flesh jinyima, jirudi, tawala matamanio. 3 oza. mortification n.

mortise;mortice n tunduunganishi. vt unga kwa kilimi; tia kilimi. ~ lock n kia.

mortuary n nyumba ya maiti adj -a mazishi.

mosaic1 n picha mpangilio; nakshi

(za mawe n.k.) adj -a picha mpangilio.

Mosaic2 adj -a Musa. (the) ~ law n Taurati: vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale.

mosey vi (sl) ~ along zurura, tembea tembea.

Moslem n Mwislamu adj -a Kiislamu.

mosque n msikiti.

mosquito n mbu. ~net n chandalua. ~ proof adj -siopitisha mbu. ~craft n manowari ndogo yenye (mwendo wa kasi).

moss n kuvumwani. ~ grown adj

most

~y adj -liofunikwa kwa kuvumwani. a rolling stone gathers no ~ (prov) mtu asiyetulia mahali pamoja hawezi kufanikiwa.

most adj -ingi kupita -ote; -ingi sana. at~ si zaidi ya. at the very ~sanasana, sio zaidi ya. for the ~ part kwa kawaida; kwa jumla in ~cases mara nyingi ~ people karibu watu wote. make the ~ of tumia kila nafasi, tumia vizuri sana adv 1 kupita/kuliko yote ~ faithful mwaminifu kuliko wote. 2 hasa, zaidi what pleased you ~? ni kitu gani kilikufurahisha hasa zaidi? 3 kabisa, sana ~ certainly kabisa. 4 (dial and US colloq) karibu ~ everyone enjoys football karibu kila mtu anafurahia mpira. ~ly adv kwa kawaida; hasa; karibu yote.

mote n chembe (k.m. ya vumbi). the ~ in somebody's eye kosa dogo alilofanya mtu (likilinganishwa na makosa ya wengine).

motel n moteli: hoteli ya wenye magari.

moth n nondo. ~ ball n dawa ya mende. in ~ balls (fig) ghalani. ~ eaten adj 1 -lioliwa na nondo. 2 (fig) -liochakaa, -a zamani. ~proof adj -sioliwa na nondo. clothes ~ n nondo mla nguo.

mother n 1 mama (mzazi, mlezi wa kike); (term of respectful reference) mama. 2 kiini, chanzo. necessity is the ~ of invention (prov) shida hufunza. 3 kiongozi wa jumuiya ya watawa (wa kike). M~ Superior n Mama Mkuu. 4 the ~ counrty n nchi ya kuzaliwa. ~-of pearl n lulumizi. ~ in law n mama mkwe. ~liness n umama. ~ tongue n lugha mama, ya kwanza. ~ wit n 1 akili ya kuzaliwa. ~ ship n meli inayopatia meli nyingine vifaa ~ 's day sikukuu ya mama. 2 asili, chanzo. ~ hood n umama. ~ less adj -siokuwa na mama. ~ like adj kama mama. ~ly adj. vt tunza/lea

kama mama.

motif n motifu: wazo/kipengee kinachorudiwa (hasa katika muziki).

motion n 1 mwendo put/set something in ~ sababisha kitu kiende. ~ pictures n sinema. 2 msogeo. go through the ~s (colloq) fanya kitu kwa namna isiyo ya dhati. 3 (proposal) pendekezo, hoja move a ~ toa hoja/pendekezo. 4 (kwenda) choo have a ~ pata choo. vt 1 ashiria, (kwa mkono); konyeza. 2 elekeza, ongoza. ~ somebody in ashiria mtu aingie ndani. ~ away fukuza (kwa mkono). ~less adj -siojongea.

motive n 1 nia, maarubu, matilaba. 2

(reason) sababu (ya kutenda jambo) adj -enye kuendesha; -a kusogea/ tenda. motivate vt tia hamasa/ motisha; sababisha. motivation n motisha; sababu ya kufanya jambo.

motley adj 1 -a rangi anuwai. 2 -enye tabia mbalimbali. n vazi la mchekeshaji. wear the ~ cheza/ fanya kama mpumbavu au mchekeshaji.

motor n 1 mota. ~-cycle; ~ bike n pikipiki ~ boat motaboti. ~ car n motokaa. ~ cade n msafara wa motokaa, pikipiki n.k.. ~ coach n basi la kitalii. ~way n baraste kuu, barabara ya motokaa ziendazo kasi. ~ man n dereva wa garimoshi. 2 musuli wa mwendo. ~ nerve n neva mwendo adj 1 -a mwendo. 2 -a musuli. vt,vi enda kwa motokaa. ~ize vt,vi tayarisha magari/ motokaa/pikipiki kwa uchukuzi; patia magari. ~-vehicle n motokaa.

mottle vt tia madoadoa. ~d adj -enye madoadoa.

motto n wito.

mould/mold1 n udongo wa mboji, udongo mweusi mzuri.

mould/mold2 n 1 kalibu. 2 (pattern)

kielezo. 3 tabia. be cast in the same ~ -wa na tabia zinazofanana be cast in heroic ~ -wa na tabia ya kishujaa. vt ~ something

mould

in/from/out of) 1 (in clay) finyanga, umba. 2 (in metal) subu kwa kalibu. 3 (character) ongoza; nyoosha. ~ing n 1 kusubu, kuumba. 2 (of wood) nakshi, mchoro.

mould3 n 1 kuvu development of ~ kuota kuvu. 2 kunyonyoka. vt ota kuvu. ~ly adv. ~er vi oza, liwa na kutu, kuvu kama koga; vunjikavunjika; chakaa.

moult v nyonyoka manyoya, mabawa nk.

mound n 1 tuta.2 kilima. 3 lundo. vt

mount vi,vt 1 panda, kwea ~ the pulpit panda mimbari ~ a horse panda farasi. ~ the throne tawazwa, kuwa mfalme. 2 (of blood) sisimka his colour ~ed alikuwa mwekundu (kwa hasira). 3 ~ (up) zidi; ongezeka. 4 onyesha mchezo jukwaani. 5 weka mahali pake; angika/tundika (picha); wekea fremu. 6 (mil uses) fanya. ~ a guard (at over) linda ~ an offensive fanya shambulio; (of large animals) panda (jike). n 1 (of a picture) kiunzi. 2 farasi. 3 baiskeli.

mountain n mlima. ~ chain/range n safu ya/msururu wa milima. ~ pass n ujia mwembamba mlimani. ~sickness n hali ya ukosefu wa oksijeni kwenye milima mirefu. ~ dew n wiski ya kiskoti. ~eer n 1 mkaa mlimani. 2 mpanda mlima. ~eering n kupanda milima. ~ous adj -enye milima; kubwa sana. mount n mlima, kilima.

mountebank n ayari; mdanganyifu;

Mountie n (Canada colloq) polisi mpanda farasi.

mourn vt,vi ~ (for/over) huzunika; omboleza; lilia huzunikia. ~er n mwombolezaji. ~ful adj -enye huzuni/majonzi. ~fully adj kwa majonzi, kwa huzuni. ~ing n 1 huzuni, majonzi, kilio, msiba. 2 go into/be in ~ing anza kwenda

eda/kuvaa nguo za kufiwa (nyeusi)/msiba. ~ing band n utepe wa msiba. ~ing-ring n pete ya ukumbusho wa marehemu.

mouse n 1 panya; (fig) (mtu) mwoga. ~-trap n mtego wa panya vi (of a cat) kamata. ~r n paka akamataye panya. mousy adj (esp of hair) -a rangi kahawia kavu; (of a person) -oga, -enye haya.

mousseline n melimeli.

moustache; (US mustache) n masharubu.

mouth n 1 mdomo. by word of ~ kwa mdomo. down in the ~ -enye majonzi, -nayosikitika. out of the ~s of babes and sucklings (prov) kauli ya busara/hekima inayotolewa na maasumu. laugh on wrong side of one's ~ lalamika; sononeka. look a gift-horse in the ~ pokea kitu bila shukurani. put words into somebody's ~ ambia mtu la kusema, sema kuwa mtu amesema neno, singizia. take the words out of somebody's ~ dakia maneno, wahi kusema. ~ful n kinywa tele; funda. ~-organ n kinanda cha mdomo. ~piece n mdakale; chombo cha kupulizia kinanda au chombo cha muziki; msemaji (kwa niaba ya). 2 uwazi, tundu. vt,vi 1 sema bila sauti. 2 sema kwa madaha. 3 kula; gusa kwa mdomo.

move vt,vi. hama; sogeza; hamisha. ~ heaven and earth fanya kila liwezekanalo. 2 ~ (house) hamishia (vyombo, samani) kwenye nyumba nyingine. ~ out hama. ~ in hamia. 3 ~ on sogea, enda mbele (kwa shuruti). ~ somebody on shurutisha mtu kwenda mbele/ kusogea. ~ along/down/up endelea mbele. 4 (excite) sisimua, gusa hisi. 5 (advice) toa pendekezo/hoja ~ the court omba mahakama (kufanya jambo fulani). 6 sukuma/tuma Salome's appeal ~ed (us) to come ombi la Salome lilitusukuma/vuta kuja. 7 ~ for omba rasmi. 8

movie

(in compounds) ~ away ondoka. ~ forward sogea mbele. movable adj 1 -a kusogezeka. 2 (varying) -a kubadilika n (pl) mali inayosogezeka/ hamishika (k.v. samani n.k.); mali binafsi. n 1 mwendo. 2 (turn) zamu (katika mchezo). 3 (action) tendo, jambo (katika kazi). 4 on the ~ kusonga mbele; kuhamahama. get a ~ on! (sl) fanya haraka. make a ~ hamia mahali pengine; anza kufanya/ kutenda. 5 uhamisho. ~ment n 1 mwendo, mwondoko; mabadiliko; tendo/kitendo. 2 mzunguko. 3 (progress) maendeleo; kubadili/ kuhama mahala. 4 (of mus composition) sehemu ya mtungo. 5 (commerce) kupanda na kushuka bei. 6 kunya. 7 (of group) tapo. ~r n mtoaji hoja/pendekezo. the prime ~r n mtu anayehusika hasa katika kuanzisha jambo; muasisi.

movie n (colloq) 1 filamu. 2 the ~s

mow vt 1 fyeka/kata majani, nyasi. ~ down fyeka. ~er n mashine ya kukatia majani. n rundo la majani ya ng'ombe; banda la majani.

Mozambique n Msumbiji.

Mr (abbr) Bwana, see Mister

Mrs (abbr) Bibi, mke wa.

Ms Bi, Bibi.

much adj -ingi, tele ~ time wakati mwingi ~ pain maumivu mengi. how ~ (is it)? bei gani? kiasi gani; idadi gani? be up to ~ -wa na thamani/maana ~ trouble matatizo mengi. not ~ of a si zuri, si -a haja. make ~ of elewa; tia maanani; kuza. think ~ of penda, heshimu. this/that ~ kiasi hiki (kidogo). ~as ingawa. ~ the same vilevile. (with)/without so ~ as (na)/bila hata adv sana, mno it is too ~ (costly) ghali sana ~ too dear ghali sana/mno. ~ more zaidi sana. be too ~ for zidi nguvu, shinda, lemea. ~ to somebody's surprise kwa

mshangao.~ more/less seuze; sembuse ~ as I hate it, I must... ingawa nachukia, sina budi I thought as ~ nilifikiri hivyo it is as ~ (as) saying ni kama kusema. as ~ bali kile kile; hivyo so ~ kubwa mno/ sana so ~ so that kwa kiasi kikubwa kwamba not so ~ X as Y y kuliko x. ~ness n (only in colloq phrase) ~ of a ~ness karibu sawasawa, hakuna tofauti.

mucilage n ulimbo; gundi la mimea.

mucilaginous adj.

muck n 1 samadi, uchafu. ~-raker n (usu fig) mdaku. ~ raking n udaku. 2 taka; (colloq) kitu kitiacho kinyaa. vt,vi ~ something (up) chafua, vuruga, haribu. 2 ~ about (GB sl) zurura. 3 ~ out safisha zizi. ~ heap n lundo la taka. make a ~ of something (colloq) chafua, haribu. ~ y adj chafu.

mucus n ute, utetelezi; kamasi, golegole. mucous adj -a kamasi; -a ute. ~ membrane n utando telezi.

mud n tope ~ hut kibanda cha udongo ~ wall ukuta wa udongo. fling/ sling/throw ~ at paka mtu tope, haribia mtu jina. ~-bath n kuoga tope za madini (dawa ya yabisi); kuoga matopeni. ~ flat n upwa tope. ~ slinger n mchafua jina/sifa. ~guard n madigadi. vt tia tope, tibua; chafua, vuruga. ~dy adj 1 -enye tope. 2 -a giza, -sio safi, -lio chafuka; (fig) -liokanganyikiwa.

muddle vt,vi 1 ~ (up) vuruga, tatanisha; chafua, tibua. ~ something/somebody up with something/syomebody (colloq) changanya vitu/watu wawili. 2 ~ along/on boronga, bananga. ~ through maliza jambo kwa kubahatisha. n (usu a muddle) mkanganyo. ~ headed adj pumbavu; -liokanganyika.

mudfish n kambare.

muesli n muzili: kiamshakinywa cha

nafaka, njugu na matunda makavu.

muezzin n mwadhini.

muff

muff1 n nguo za kuzuia baridi (mikononi au miguuni).

muff2 n mchezaji mzito (hasa kwenye kriketi). vt shindwa kudaka mpira; shindwa kufanya vizuri, fanya kosa.

muffin n mafini: mkate mdogo wa

muffle1 vt 1 ~ (up) funika kwa nguo (hasa shingo na kichwa). 2 punguza kelele kwa kufunika (ngoma, kengele) kwa nguo. ~r n 1 kitambaa cha shingoni. 2 (US) see silencer n.

muffle2 n mdomo wa juu (wa mnyama k.v. panya).

mufti n 1 mufti. 2 (usu in ~) nguo za kiraia (avaazo mtu anayevaa sare).

mug1 n 1 magi. 2 (sl) uso, mdomo.

mug2 n (sl) mpumbavu a ~'s game kitu ambacho hakiwezi kuleta faida.

mug3 vt (colloq) vamia mtu na kumwibia; iba kwa nguvu. ~ger n mvamizi, jambazi. ~ging n uvamizi.

mug 4 vi (sl) ~ something up soma sana (kwa ajili ya mtihani). n mtu asomaye sana.

muggins n (colloq) mpumbavu.

muggy adj (of the weather, a day etc)

mugginess n.

mugwump n (US) mshaufu.

Muhammad n Muhammad: Mtume na Mwasisi wa Uislamu.

mulatto n chotara, suriama.

mulberry n forosadi.

mulch n matandazo: majani yanayotiwa shinani mwa miche kuhifadhi unyevu. vt weka matandazo.

mulct vt ~(in/of) 1 toza faini. 2 nyang'anya. n faini.

mule n 1 nyumbu, baghala. as obstinate/stubborn as a ~ kaidi sana. 2 (colloq of a person) mkaidi; shupavu. 3 aina ya mashine ya kusokotea. ~ teer n mwendesha nyumbu. mulish adj -kaidi, -shupavu. mulishly adv. mulishness n.

mull1 vt unga, tengeneza (divai, bia)

mull2 n rasi.

mull3 vt ~ something over/over something fikiria jambo.

mulla(h) n sufii, ulama.

mullet n aina za changu.

mulley adj (US) bila pembe. n (US) ng'ombe asiye na pembe.

mullion n nguzo ya mawe kati ya dirisha. ~ed adj -enye nguzo ya mawe kati ya dirisha.

multi- (pref) -enye -ingi. ~ coloured adj -enye rangi nyingi. ~cellular adj -enye seli nyingi. ~ farious adj

-a namna nyingi; -ingi tena mbalimbali. ~ form adj -enye maumbo mengi, -a namna nyingi. ~lateral adj -enye wahusika wengi ~lateral trade biashara kati ya nchi tatu au zaidi. ~ millionaire n tajiri sana (mtu mwenye kiasi cha milioni kadhaa za fedha). ~ national adj -a kimataifa; -a zaidi ya mataifa mawili. n kampuni ya kimataifa. ~party adj -a vyama vingi.

multiple adj -enye sehemu nyingi, -a mara nyingi. ~ choice (question) n (swali) lenye majibu mengi. n kigawe 40 is a multiple of 10, 40 ni kigawe cha 10.

multiplex adj -enye sehemu/maumbo mengi.

multiply vt,vi zidisha, leta wingi. ~ something by something zidisha namba fulani kwa namba nyingine. multiplican n kizidishio; hesabu ya kuzidishwa. multiplication n kuzidisha. ~ table jedwali la kuzidisha. multiplicity n wingi. multiplier n kizidishi.

multitude n 1 wingi, kundi. 2 the ~

jeshi; umati, kaumu. multitudinous adj -ingi, tele.

mum1 adj (colloq) keep ~ kaa kimya int kelele! kimya! ~'s the word usiseme chochote, kimya, usimwambie mtu!

mum2 n (colloq) mama. ~my n

(chiefly child's word) mama.

mumble vt,vi 1 munyamunya. 2 (of

eating) mumunya.

mumbo-jumbo n marogonyo; mapayo.

mummer

mummer n mwigizaji wa mchezo bubu. ~y n 1 mchezo bubu. 2 sherehe zisizo na maana (hasa za kidini).

mummify vt tia mumiani. mummification n. mummy n maiti iliyotiwa mumiani.

mumps n matumbwitumbwi.

munch vt,vi tafuna kwa nguvu.

mundane adj 1 -a ulimwengu huu, -a kidunia. 2 -a kawaida sana; -a kuchosha, -siosisimua. ~ly adv.

municipal adj -a manispaa ~ corporation shirika la manispaa. ~ly adv. ~ity n manispaa, baraza la mji.

munificent adj -karimu, -paji. munificence n (formal) (of something given) wingi wa ukarimu, ukarimu mkubwa. ~ly adv kwa wingi.

muniments n (leg) nyaraka ambazo

munition n (usu pl, in combination)

there was no shortage of ~s hatukupungukiwa na silaha, tulikuwa na silaha tele. vt -pa silaha. ~ factory n kiwanda cha zana za vita/silaha.

mural adj -a ukutani. n sanamu/picha iliyochorwa ukutani.

murder vt 1 ua (kwa kusudi). 2 haribu, vunja. n 1 kuua (kwa kudhamiria); mauaji yasiyo na sababu. 2 (colloq) mateso, jambo gumu kabisa. cry blue ~ (colloq) piga mayowe/makelele sana. M~ will out (prov) mambo hayafichiki. ~er n mwuaji. ~ess n mwuaji wa kike. ~ous adj 1 -a kiuaji. 2 katili. ~ously adv.

murk n giza, utusitusi. ~y adj -eusi,

~ily adv.

murmur vt,vi 1 vuma. 2 ~ (at/against) nung'unika. 3 nong'ona. n 1 mvumo. 2 manung'uniko. 3 mnong'ono.

murphy n (sl) kiazi, mbatata.

murrain n 1 ugonjwa wa kuambukiza wa ng'ombe k.m. kimeta. 2 (old use) a ~ on you! Mungu akulaani!

muscle n musuli, tafu, (sinew) ukano. a ~ man n pande la mtu. he did not move a ~ alitulia tuli. vi (colloq) ~ in (on something) jishirikisha kwa nguvu. ~ -bound adj -enye musuli, kakamavu, -lioshupaa. muscular adj 1 -a musuli. 2 -enye nguvu ya mwili, -enye maungo; -a kukakawana.

muscovite n mkazi wa Moscow.

muse vt ~ (over/on/upon) fikiri; tafakari, waza, taamali. n 1 taamuli. musingly adv. M~ n (GK myth) Mungu wa kike (kati ya watoto tisa wa Zeus waliolinda na kuendeleza ushairi, nyimbo, dansi n.k.). 2 kipaji/kipawa cha mshairi.

museum n (jumba la) makumbusho. a ~ piece n kifaa/kitu kinachofaa kuhifadhiwa makumbusho; (fig) kitu/mtu aliyepitwa na wakati.

mush1 n kitu kirojorojo; (US) uji (wa mahindi). ~y adj (colloq) lizilizi; -enye kuonyesha hisia.

mush2 vi tembea katika theluji (kwa gari linalokokotwa na mbwa) n matembezi katika theluji na mbwa.

mushroom n uyoga. (attrib) ~growth

-liokua upesi ~ cloud wingu la bomu la nyuklia ~ poisoning sumu ya uyoga. vi 1 go ~ing enda kung'oa uyoga mbugani. 2 enea, sambaa upesi.

music n muziki (attrib) ~ lesson/ ~teacher somo/mwalimu wa muziki. face the ~ kabili matatizo/ wahakiki/shutuma kijasiri. set/put something to ~ tunga/tia sauti (ya muziki). ~ box n kisanduku cha muziki. ~-hall n (GB) ukumbi wa maonyesho. ~-stand n dawati la kuimbishia. ~ stool n kigoda cha mpiga kinanda. ~al adj -a muziki, -enye kipaji cha muziki; -a kupenda muziki. ~-chairs n mchezo wa viti na muziki. ~ comedy n 1 komedi yenye muziki. 2 sinema yenye muziki. ~ally adv. ~ian n mwanamuziki. ~ianship n ustadi wa muziki.

musk

musk n 1 maski: tezi ya kulungu itumikayo katika utengenezaji wa manukato. ~deer n kulungu asiye na pembe. ~ rat n panya wa majini. 2 mimea yenye harufu ya maski. ~ melon n tikiti. ~ rose n waridi lenye kunukia vizuri sana. ~y adj -enye harufu ya maski.

musket n gobori. ~eer n askari wa

~ry n 1 maarifa ya kupiga bunduki. 2 (old use) kupiga gobori.

Muslim n mwislamu.

muslin n melimeli.

musquash n manyoya ya panya wa

muss n (US) vurugu, fujo. vt ~ (up)

mussel n kome.

must1 aux v 1 havina budi; sharti, lazima you ~ go sharti uende he ~ be honest yampasa kuwa mwaminifu ~ you shout! kwani mpaka upige kelele! 2 hakika it ~ be Mary hakika ni Mary. n (colloq) jambo la lazima (la kuona au kusikia) that film is a ~ ni lazima uone filamu hiyo.

must2 n maji ya zabibu.

must3 n ukungu; kuvu. ~y adj -enye koga/kuvu, -baya; (fig) -liopitwa na wakati; -liopooza. ~iness n.

must4 n hasira kali adj (of male elephant or camel) -kali sana. go ~ pata wazimu; (of animals) kasirika.

mustache n (US) see moustache

mustachio n (arch) masharubu (agh. marefu).

mustang n farasi mwitu.

mustard n 1 mharadali. 2 haradali. ~ gas n sumu ya mvuke (iliyotumika katika vita kuu ya kwanza). ~ plaster n plasta ya haradali. as keen as ~ hodari, epesi sana. grain of ~ seed kitu kidogo kinachoweza kukua na kuwa kikubwa sana.

muster n gwaride. pass ~ faa, tosha;

vt,vi kutana; kutanisha; piga paredi. ~ (up) courage jipa moyo, thubutu; ita, kusanya nguvu.

mutate vt,vi badilika; badilisha. mutable adj -enye kuweza

kubadilika. mutability n. mutation n mabadiliko.

mutatis mutandis adv (Lat) pamoja na mabadiliko yanayofaa.

mute1 adj 1 kimya. 2 (of a person)

bubu. 3 (of a letter in a word) hafifu. n 1 bubu. 2 (of musical instrument) kibana sauti. vt punguza sauti. ~ly adv.

mute2 vi,vt (of birds) nya.

mutilate vt kata, ondoa, haribu sehemu ya; kata kiungo cha mwili; (cripple) lemaza; (remove essential part) ondoa (toa, haribu) sehemu yenye maana sana. mutilation n kuatilika.

mutiny n maasi, uasi, (agh. ya mabaharia na maaskari). vi ~ (against) asi, halifu. mutineer n mwasi. mutinous adj -a kuasi, halifu.

mutt n (sl) 1 mtu anayekosea bila kutambua, mjinga. 2 mbwa chotara.

mutter vt,vi 1 semea mashavuni/

chinichini. 2 nung'unika. 3 (of thunder) nguruma. n manung'uniko. ~er n mnung'unikaji.

mutton n nyama ya kondoo. as dead as ~ -liokufa kabisa. ~ dressed as lamb (hutumika kwa) mzee anayevaa kama kijana; mzee kijana. ~-head n (colloq) mpumbavu. ~-chop n (fig) sharafa.

mutual adj -a wote wawili, -a wenyewe; -a pande mbili ~ affection upendano ~ agreement maafikano, mapatano ~ help kusaidiana; (in cultivating, building) ujima ~ friend rafiki wa wote wawili. ~ insurance company n bima ya ubia ~ wills wasia za kuhusiana. ~ly adv.

muumuu n gauni pana na refu/kanzu.

muzzle n 1 pua na mdomo wa

wanyama (uliochongoka kama wa mbwa, mbweha, n.k.). 2 (to prevent biting) kifungo cha mdomo. 3 (rifle) mdomo, kitundu (cha kasiba, mtutu). ~ velosity n mwendo wa risasi

inapoacha mtutu. vt fungia mdomo, tilia kifungo cha mdomo (wa mbwa

muzzy

(fig) zuia (mtu, jamii, vyombo vya habari n.k.) kutoa habari; nyamazisha vyombo vya habari.

muzzy adj 1 -enye wasiwasi, -a kupumbazika. 2 -enye ukungukungu, -sio wazi.

my poss adj -angu.

mycology n maikolojia: sayansi/taaluma ya kuvu.

myan(h) n ~ bird n mina: kwezi wa Asia anayeigiza sauti ya binadamu.

myelitis n (path) uvimbe wa neva kuu.

myopia n mayopia: kutoweza kuona mbali. myope n mwenye mayopia.

myriad n ~ (of) wingi sana, idadi kubwa mno.

myrimidon n mtu (mtumishi, mtumwa) atekelezaye amri bila kusaili, kibaraka.

myrrh n manemane.

myself pron mimi mwenyewe, nafsi

I live by ~ naishi (mimi) mwenyewe. I hurt ~ nilijiumiza (mwenyewe).

mystery n 1 fumbo, mwujiza. 2 siri;

~ piay n tamthilia juu ya maisha ya Yesu. mystic adj -a siri, -sioelezeka; -a fumbo; -a maana/nguvu ya roho. n mchaji (mtu ajaribuye kumshiriki Mungu kwa kujitoa na kutafakari sana habari za Mungu). mystical; mystic adj. mysterious adj -a fumbo, -sioelezwa; -a kiujiza/ajabu. mysteriously adv. mysticism n imani/mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafkira. mystify vt fumba; tatanisha, tatiza, changanya.

mystique n fumbo; ustadi wa siri/pekepeke.

myth n 1 kisasili: hadithi inayoeleza asili ya watu, matukio n.k.. 2 (fiction) uwongo. 3 mtu/jambo lililobuniwa. ~ical adj -a visasili, -a uwongo, -a kubuniwa. ~ology n 1 mithiolojia: elimu ya visasili. 2 visasili. ~ologist n mwanafunzi wa mithiolojia. ~ological adj -a mithiolojia, -a visasili, -a kubuniwa.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.