TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

N,n n herufi ya kumi na nne katika alfabeti ya Kiingereza.

nab vt (colloq) kamata, shika, bamba.

nabob n (old use) tajiri mpenda anasa.

nacelle n fumbatio/funiko la injini ya ndege.

nacre n lulumizi. ~ous adj.

nadir n nyayoni; (fig) cheo (kadiri) cha chini; kilindi, lindi, sehemu ya chini kabisa.

nag1 n (colloq) farasi (agh. mzee).

nag2 vt,vi ~ (at) sumbua, kefya. ~er n.

naiad n (Gk myth) zimwi wa maji.

nail n 1 ukucha. fight tooth and ~ pigana kufa na kupona. ~-brush n brashi ya kucha; ~-file n tupa ya kusugua kucha. ~-scissors n mkasi wa kucha. ~-polish/varnish n rangi ya kucha. 2 msumari. as hard as ~s -enye afya na nguvu kabisa; -sio na huruma, katili. hit the ~ on the head patia hasa, gonga. right as ~s kweli kabisa. (right) on the ~ mara (moja). vt 1 kongomea, pigilia misumari. ~ a lie (to the counter) thibitisha/onyesha kuwa kauli fulani ni uongo. ~ somebody down (to something) fanya/bana mtu aseme alichodhamiria. ~ something down gongomea, shikiza. ~ something up gongomea, fungia/shikizia (dirisha mlango) misumari. 2 vutia, teka (mtu), kamata.

nainsook n nguo laini ya pamba.

naive adj 1 -nyofu, -sio na hila;

-jinga; shamba. ~ly adv. ~te; ~ty n usungo, ushamba.

naked adj 1 -tupu, uchi. 2 -siokuwa na ala a ~ sword jambia bila ala. see something with the ~ eye ona kwa macho. the ~ truth ukweli mtupu. ~ly adv. ~ness n.

namby-pamby adj (of persons, talk) -enye hisia za kijingajinga. n mtu mwenye hisia za kijingajinga, asiye na msimamo.

name n 1 jina change of ~ kubadili jina full ~ jina kamili list of ~s orodha ya majina assumed ~ lakabu

nap

in one's own ~ kwa uwezo wa binafsi, kwa nguvu do something in somebody's ~ fanya kitu kwa jina la fulani. go under the ~ of fahamika kwa jina la know somebody by ~ fahamu mtu kwa jina lake mention no ~s usitaje majina. in the ~ of kwa jina la; kwa ajili ya; kwa amri ya. in the ~ of God haki ya Mungu! kwa jina la Mungu, Bismillahi. call somebody ~s tukana/kashifu mtu. put/enter down one's ~ for jiandikisha, andikisha jina. not have a penny to one's ~ -tokuwa na fedha kabisa. lend one's ~ to ruhusu jina litumike kwa faida ya wengine. take somebody's ~ in vain tumia vibaya/kashifu jina la mtu. ~ day n siku ya sherehe ya somo. ~ dropping n tabia ya kujikombakomba kwa majina ya wakubwa. ~ drop vi tumia majina ya wakubwa kujikomba. ~ part n mshikilia jina la mchezo/mwajina. ~ plate n kibao cha mlangoni. ~ sake n somo. 2 sifa have a bad ~ -wa na sifa mbaya. win a good ~ for oneself/make one's ~ fahamika, jipatia sifa njema. 3 mtu mashuhuri. vt 1 ~ (after/(US) for) -pa jina the boy was ~d after his grandfather kijana alipewa jina la babu yake. 2 taja ~ what you want taja unachotaka. 3 ~ (for) teua. ~ for an office -pa cheo. 4 ainisha ~ all animals in Serengeti ainisha/taja majina ya wanyama wote katika Serengeti. 5 toa bei ~ your price sema uwezo wako, utatoa ngapi. ~less adj 1 bila jina. 2 -siofaa kutajwa (kwa kuwa -baya mno). 3 -sioelezeka.

namely adv yaani.

nankeen n 1 marekani: nguo ya pamba ya manjano. 2 (pl) ~s n suruali ya marekani.

nanny n yaya.

nanny-goat n mbuzi jike.

nap1 n usingizi kidogo have a ~ lala

kidogo. vi lala kidogo. catch somebody ~ping kuta usingizini; fuma, shtusha, shtukiza.

nap

nap2 n manyoya (nywele) mafupi ya nguo (zulia). vt (kwa nguo) tia/tengeneza manyoya mafupi nguoni.

nap3 n see napoleon2.

napalm n napamu: aina ya grisi (ya kutegenezea mabomu). ~ bomb n bomu la (girisi la) napamu.

nape n kikosi, ukosi.

napery n (old use) vitambaa vya

mezani; vitambaa/nguo za nyumbani.

naphtha n nafta: mafuta mepesi yanayowaka. ~lene n naftalini: dawa yenye harufu kali inayotumika kufukuza wadudu (mende, nondo n.k.).

napkin n (table) ~ n 1 kitambaa cha

mikono/mezani. 2 winda, nepi.

napoleon n 1 sarafu ya dhahabu (ya

Kifaransa ya faranga 20). 2 (also nap) mchezo wa karata.

nappy n (GB colloq) napkin. narcissism n (psych) kujihusudu, kujipenda. narcissistic adj -enye kujihusudu, -enye kujipenda.

narcissus n (bot) nasisa.

narcotic adj -a dawa ya kutia usingizi. n dawa ya kulevya. narcosis n (med) usingizi (wa dawa).

nark1 n (GB sl) mpelelezi, kachero.

nark2 vt (GB sl) kera, udhi.

narrate vt simulia, hadithia. narrator n msimuliaji. narration n usimuliaji, masimulizi. narrative n hadithi, masimulizi; (attrib) -a kusimulia ~ literature fasihi ya kusimulia.

narrow adj 1 -embamba.2 dogo,chache; -a shida living in ~ circumstances ishi maisha ya shida. 3 chupuchupu, nusura. a ~ escape n kuponea chupuchupu. a ~ squeak n (colloq) nusura. 4 halisi, hasa. 5 finyu. ~-minded adj -lio na mawazo finyu. ~-mindedly adv. ~ mindedness n. vt,vi -wa/fanya kuwa embamba ~ something down fanya kuwa chache. ~ly adv 1 kidogo tu, kwa shida he ~ly escaped failing kidogo tu ashindwe 2. kwa uangalifu watch his movement ~ly angalia

native

mwenendo wake kwa uangalifu. ~s n mkono wa bahari/mto.~ness n.

narwhal n nyangumi mwenye pembe.

nasal adj -a pua; -a puani, -a mwanzi wa pua, -a nazali ~ sounds sauti za nazali. n nazali. ~ize vt nazalisha, puza.

nascent adj -enye kuanza kuota/ kuondokea, -a chanzo.

nasty adj 1 baya, -siopendeza. 2 chafu, -sio murua, fisadi. 3 -enye chuki. 4 -enye hatari. 5 balaa, wasiwasi. ~crossing n tambukareli balaa. nastily adv. nastiness n.

natal adj -a kuzaliwa kwao. ~ity n

kima cha uzazi.

nation n taifa law of ~s sheria ya mataifa. ~-wide adj -a taifa zima. ~al adj -a taifa, -a watu wote (wa taifa fulani). N~al Anthem n wimbo wa taifa. N~al Assembly n Bunge. the N~al Debt n Deni la Taifa. ~al monument n kumbu-kumbu ya taifa. ~al park n mbuga/eneo la burudani (la taifa). ~ al service n kipindi cha kujenga taifa; jeshi la kujenga taifa. ~al n mtu wa taifa fulani; raia; mwananchi. (pl) ~als wananchi. ~ality n. ~alism n 1 utaifa; uzalendo. 2 kupigania uhuru. ~alist n 1 mfuasi wa utaifa; mzalendo. 2 mpigania uhuru. ~ alistic adj -a uzalendo/kizalendo. ~ality n uraia. ~alize vt,vi 1 taifisha. 2 andikisha uraia. 3 geuza/fanya taifa. ~alization n.

native n 1 mzaliwa, mwenyeji. 2 (of animals, plants) asili ya the black mamba is a ~ of Africa songwe ni nyoka wa asili ya Afrika adj 1 ~ land n nchi ya watu/kwao ~ law and customs sheria ya mila/kienyeji. 2 (inborn, natural, original) -a maumbile, hulka. ~ intelligence n akili ya kuzaliwa. 3 ~ to (of plants, animals) -a asili ya. the lion is ~ to Africa simba ni wa asili ya Afrika. 4 (of metal) halisi. nativity n uzaliwa; siku ya kuzaliwa. the

natter

Nativity n Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. a Nativity Play n tamthilia ya kuzaliwa kwa Yesu.

natter vt (GB colloq) 1 piga soga. 2 nung'unika.

natty adj (colloq) 1 nadhifu, safi, malidadi. 2 -epesi, -stadi. nattily adv.

natural adj 1 -a asili, -a kawaida she has a ~ ability in languages ana kipaji cha lugha ~ disaster maafa ya asilia ~ forces/phenomena matukio asilia. ~ gas n gesi asilia. ~ history n botania na zoolojia, elimuviumbe. ~ justice n adili ya maumbile, idili. ~ law n sheria/kanuni asilia. ~ philosophy n (old use) sayansi agh. fizikia. ~ religion n dini asilia (ya akili ya binadamu sio ya ufunuo). ~ resources n maliasili. ~ science n sayansi asilia (bayolojia,kemia na fizikia). ~ selection n uchaguzi asilia (namna wanyama na mimea inavyoweza kulinganisha maisha yao na mazingira). 2 (of abilities etc) -a maumbile he's ~ orator ana kipaji cha usemaji. 3 -a kawaida die a ~ death -fa tu kwa kawaida as is ~ kama ilivyo kawaida running comes ~ to him kukimbia ni kawaida kwake ~ note (music) noti/sauti ya kawaida. 4 halisi speak in a ~ voice tumia sauti halisi. 5 (inevitable) pasipo budi, sharti ~ result (consequence, effect) tokeo la faradhi. 6 (arch) haramu. ~ child n mwanaharamu. n 1 a ~ for something inayofaa/stahili he's a ~ to win the race bila shaka atashinda mbio. 2 (old use) punguani. 3 (music) alama ya kuashiria sauti ya kawaida. ~ism n 1 tanakala/uasili. 2 (philosophy) falsafa asili (kueleza asili ya maumbile kwa historia ya viumbe). ~ist n mwanaviumbe, mtaalam achunguzaye mimea, wanyama, wadudu. ~ize vt,vi 1 andikisha uraia. ~ized citizen n raia wa kuandikishwa. 2 (of words) tohoa. 3 zoelea (tabia za nchi nyingine), zoelea (ugenini) ~ization n

nautch

kuandikisha uraia. ~ization papers n cheti cha uraia. ~ly adv 1 kwa asili. 2 kwa urahisi, kwa desturi, kwa kawaida. 3 (neccesarily) bila shaka, wazi. 4 bila kujidai.

nature n 1 (world) ulimwengu,

viumbe vyote laws of ~ utaratibu wa jambo la asili, kawaida ya vitu vyote. ~ study n elimu mimea/ viumbe. ~ worship n kuabudu nguvu za asili; (natural appearance) umbo, sura. call of ~ n haja let ~ take its course acha mambo yatokee kama kawaida yake. 2 asili, nguvu asili. ~cure n matibabu asilia. pay the debt of/pay one's debt to ~ kufa. in the course of ~ katika hali ya asili ya maisha it's in the ~ of things ni tabia zisizoepukika. be in state of ~ wa katika hali ya asili; (joc) uchi. 3 (habit) desturi; mazoea; hulka proud by ~ -enye desturi ya kujivuna a woman with a kind ~ mwanamke mwenye desturi njema a man's second ~ tabia nzuri/ mbaya ya mtu it's in my ~ ni tabia yangu. by ~ kwa kawaida. human ~ n utu (dhidi ya unyama). good ~ n ukarimu. good-/ill ~d adj enye tabia njema/mbaya. 4 (kind) jinsi, namna, aina anything of that ~ chochote cha namna hii. 5 kama, namna ya a request in the ~ of a command ombi la namna ya amri.

naturism n (ukaaji) uchi. naturist n mkaa uchi.

naught n (old use and poet) all for ~ bure, kazi bure. set at ~ dharau, beza. bring to ~ haribu; shinda.

naughty adj 1 -tundu; -tukutu. 2 (books, magazines) -chafu. naughtily adv. naughtiness n.

nausea n 1 kichefuchefu, kigegezi. 2 kuchafuka moyo, kinyaa. nauseous adj -a (kuleta) kichefuchefu; -a kuchafuka moyo. ~te vt tia kichefuchefu/kigegezi; chafua moyo.

nautch n nachi: maonyesho ya ngoma

ya wasichana wa kihindi. ~ girl n mcheza nachi/ngoma wa kike.

nautical

nautical adj -a baharia; -a ubaharia. ~ mile mita 1852.

nave n ukumbi wa kanisa.

navel n kitovu.

navigate vt,vi ongoza chombo majini/angani, safiri baharini; (fig) ~ a Bill through Parliament shawishi Wabunge kupitisha mswada. navigable adj 1 (of rivers, seas etc.) -a kupitika kwa chombo. 2 (of ships etc.) -a kuweza kusafiri majini/ angani. navigability n. navigation n 1 uongozaji vyombo majini/angani hazard to navigation hatari kwa usafiri (wa baharini/angani). 2 usafiri wa majini/angani. navigator n 1 nahodha. 2 baharia. 3 mwongoza njia.

navvy n (GB) kibarua.

navy n uanamaji, jeshi la wanamaji. merchant ~ n uanamaji wa biashara. naval adj 1 -a jeshi la majini. 2 -a manowari.

nay adv siyo, la, a-a. n kura ya hapana I will not take ~ sitakubali kukataa kwako.

Nazi n Nazi: mwanachama wa chama kilichoanzishwa na Hitler adj -a Nazi.

neap n ~ (tide). maji mafu.

near1 adv 1 karibu he lives ~ me anaishi karibu nami. as ~ karibu as ~ as I can remember kama ninavyoweza kukumbuka. ~ at hand karibu, si siku nyingi it is ~ on/upon ni karibu it lasted ~ a century imedumu karibu karne moja. 2 bado he was ~ dead with fright alikaribia kufa kwa woga. 3 karibu na be nowhere ~ something -wa mbali na kitu. ~by karibu na, siyo mbali.

near2 adj 1 -a karibu, (kwa jamaa)

-wa jamaa ya those ~ and dear wale wapenzi na ndugu. 2 -a upande (wa gari ulio karibu na ukingo wa barabara) wa kushoto/kulia. 3 -sio mbali. a ~ thing/escape n kunusurika, kuponea chupuchupu. ~ miss n bomu linalolipuka karibu. 4 (miserly) -a choyo, bahili, -nyimivu. vt,vi karibia, sogea, jongea be ~ing

necessary

completion karibia kumalizika. ~ness n. (prep) karibu na she lives ~ the bank anaishi karibu na benki. ~ly adv karibu, karibukaribu. pretty ~ adv takriban. not ~ly mbali na it is ~ly one o' clock inakaribia saa saba.

neat adj 1 nadhifu, malidadi, liopangwa vizuri, -enye kuvutia (kwa sura na umbo). 2 -enye tabia ya unadhifu. 3 (of liquor) kavu, siozimuliwa 4. (colloq) erevu. ~ly adv. ~ness n.

neath adv see beneath.

nebula n jamii ya nyota nyingi za mbali sana. ~r adj. nebulous adj -a kama wingu; -a unyenyezi, si wazi, si dhahiri.

necessary adj -a lazima, -a faradhi,

-a sharti, -a kujuzu it is ~ for me to go ni lazima niende more than ~ a lazima hasa as he deems ~ kama aonavyo ni lazima. necessaries n pl mahitaji muhimu ya lazima. necessarily adv. necessitate vt lazimisha, sababisha juzu misunderstandings often necessitate war kutoelewana mara nyingi husababisha vita. necessitous adj (formal) -a umaskini, -a ufukara. necessity n 1 haja, shida he was driven to steal by necessity shida ilimsababisha aibe. for use in case of necessity itumike wakati wa shida. be under the necessity of lazimishwa na. bow to necessity kubali wajibu. necessity is the mother of invention shida huzaa maarifa. of necessity kwa vyovyote, haiepukiki, lazima. make a virtue of necessity fanya jambo kwa moyo mkunjufu. 2 kitu cha lazima/muhimu food and drink are necessities chakula na kinywaji ni vitu vya lazima. necessities of life mahitaji muhimu ya lazima kwa kuishi. 3 hali ya ufukara in necessity katika hali ya ufukara. 4 (jambo la) lazima is it a necessity that you go to Tanga? ni lazima uende Tanga?

neck

neck n 1 shingo. break one's ~ (fig)

fanya kazi kwa bidii. breathe down somebody's ~ wa karibu sana na mtu, fuata nyuma, fuatafuata, ingilia mno shughuli za mtu. get it in the ~ (sl) umia sana, pata machungu; karipiwa sana. have the ~ thubutu. risk one's ~ jihatarisha. save one's ~ (infl) okoka kunyongwa; epuka adhabu/fedheha. stick one's ~ out jiweka hatarini, thubutu. win/lose by a ~ shinda/shindwa karibu sana. up to one's ~ in (fig) wa na shughuli nyingi. ~ and crop kabisa. neck and ~ bega kwa bega; sawa kwa sawa. ~ of the woods (esp. US sl) eneo/sehemu ya I don't know anyone in this ~ of the woods sifahamu mtu yeyote hapa. ~ or nothing kufa na kupona. 2 rasi ~ of land rasi . 3 (compounds) ~ band n ukosi. ~cloth n tai. ~erchief n leso. ~lace n mkufu. ~ let n mkufu. ~ line n (women's clothes) mstari wa juu (wa nguo). ~tie n tai. ~wear n (comm) tai n.k.. vi (sl) busanabusana.

necro (pref) -a kuhusu mauti. ~

mancy n ufundi wa kuwasiliana na mizimu (ili kufahamu mambo ya baadaye). ~mancer n. ~polis n (esp. ancient) also makaburini, mava(ni). ~psy n (also necroscopy) uchunguzi wa maiti. ~sis n kuoza kwa sehemu ya mwili.

nectar n 1 (myth) kinywaji cha miungu ya Kigiriki. 2 mbochi, nekta: majimaji matamu katika maua; kinywaji kitamu sana.

nectarine n nektarini: aina ya tini.

nee adj -a kuzaliwa Mrs Brown ~ Robinson, Bibi Brown aliyekuwa Robinson.

need n 1 ~ (for) haja (ya). if ~ be ikiwa lazima, ikibidi. stand in ~ of hitaji there is no ~ for me to do this hakuna haja ya mimi kufanya hivi there is no ~ to hurry hakuna haja ya kuharakisha. 2 mahitaji my ~ s are few mahitaji yangu ni machache. 3 (poverty) umaskini, ufukara; ukata.

neglect

a friend in ~ is a friend in deed (prov) akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. vt,vi 1 hitaji, taka I ~ it nakihitaji. 2 lazimika, wa jambo la lazima he ~ not come si lazima aje you ~ not have spoken haikuwa lazima useme. ~ful adj. do the ~ ful fanya kinacho hitajika; toa pesa (inayohitajika). ~fully adv. ~less adj sio -a lazima, -a bure. ~less to say ni wazi kwamba, inajulikana kwamba. ~lessly adv. ~s adv lazima, sharti, hakuna budi. N ~s must when the devil drives (prov) hali yatulazimisha. ~y adj maskini.

needle n 1 sindano; (packing) shazia, (magnetic) dira thread a ~ tunga sindano. look for a ~ in a haystack (prov) tafuta kitu kisichoweza kupatikana/kuonekana. as sharp as a ~ -enye akili kali, epesi. ~ woman n mshonaji (mwanamke). ~craft/work n ushonaji. 2 (of wood etc) kipande chembamba. 3 majani ya msonobari. 4 (of mountain etc) ncha. 5 (of record player) sindano. 6 the ~ n (sl) mhemko give somebody the ~ chokoza. vt 1 shona. 2 (fig) chokoza.

ne'er adv (poetic) asilani, kamwe. ~-do-well n mtu wa bure, mpotovu.

nefarious adj -ovu, -baya sana. ~ness n ubaya, uovu. ~ly adv.

negate vt 1 kana, kanusha. 2 tangua. negation n 1 kukana, kukanusha. 2 ukosekanaji (wa sifa au maana). negative n 1 kukana he replied in the negative alikana/kataa.2 (of photograph) negativu. 3 (gram) kanusho. 4 (maths) uhasi adj 1 -a kukana, -a kukanusha. 2 hasi negative number namba hasi negative attitude mwelekeo hasi negative criticism uhakiki/maoni hasi. the negative pole ncha hasi. vt 1 kanusha. 2 (render useless) tangua. negatively adv. negativism n ukanaji.

neglect vt 1 totunza, toangalia, -tojali.

neglige;negligee

2 (slight) telekeza. ~ed child n mtoto aliyetelekezwa. 3 (do carelessly) zembea; puuza; purukusha I ~ed to do that nilipuuzia kufanya hivyo. n 1 kupuuza; uzembe; upurukushani. 2 hali ya kutotunzwa. ~ful adj -vivu, -zembe; sahaulifu. ~fulness n uzembe, usahaulifu. negligence n uzembe, upurukushani. gross negligence n uzembe wa halin ya juu. negligent adj -zembe, -enye upurukushani be negligent of something zembea jambo. negligently adv. negligible adj -sio muhimu; dogo sana.

neglige;negligee n vazi (la kike) la kulala; vazi pana lisilo rasmi.

negotiate vt 1 ~ with somebody jadiliana na mtu, fanya shauri ili kuafikiana. 2 (of money) badili kwa fedha. 3 ~ something (with somebody) patana (juu ya). 4 pita. negotiable adj 1 -a kuweza kujadiliwa that dispute is negotiable ule ugomvi waweza kujadiliwa. 2 -a kubadilishika the cheque is not negotiable cheki haibadilishiki. 3 (of road etc) -a kupitika the bridge is negotiable daraja linapitika. negotiator n mpatanishi.

Negro n Mnegro (hasa anayeishi Marekani) adj -a Kinegro. Negress n mwanamke mweusi.~id adj -a watu weusi; -a Kinegro, a kama watu weusi.

neigh vi lia (kama farasi). n mlio (wa farasi).

neighbour n jirani, mtu akaaye karibu. vt,vi ~ (on/upon) wa jirani, kuwa karibu. ~hood n ujirani; (watu waishio katika) eneo (linaloo-ngelewa) that thief is feared by the whole ~hood mwizi yule anaongopwa na watu wote wa eneo lile in the ~hood of upande wa, karibu ya. ~ly adj -a ujirani mwema, karimu; -ema. ~liness n.

neither adj, pron 1 (used with a sing n or pron) si....o ote, si.... wala; hata of the two~ man lived here kati ya

nerve

hawa wawili hapana hata mmoja aliyeishi hapa. ~.... nor si.... wala I can ~ eat nor drink siwezi kula wala kunywa ~Martin nor Selemani came hakuja Martin wala Selemani. 2 (after a negative clause etc) wala; hata I'm not going ~ is she siendi mimi wala yeye.

Nelly n (only in) not on your ~ (GB sl) thubutu.

nemcon adv (abbr Lat) bila kupingwa; kwa kauli moja.

nemesis n 1 kudra; adhabu ya haki (iliyostahili kwa kosa lililofanywa); mshindani/adui asiyeshindika. 2 N~ n mungu wa kike wa kisasi.

neo- (pref) -pya, mamboleo. ~- colonialism n ukoloni mamboleo.

neolithic adj -a neolithi, -a enzi ya mawe. ~ man n mtu wa neolithi/enzi ya mawe.

neologism (also neology) n 1 neno jipya. 2 kuunda/kutumia maneno mapya.

neon n (chem) neoni. ~ sign n tangazo la neoni. ~ light n taa ya neoni.

neonatal adj -enye kuhusu mtoto aliyezaliwa papo.

neophyte n muumini mpya (wa dini, imani).

neoplasm n (path) tezi; uvimbe.

nephew n mpwa (wa kiume); mtoto (wa kiume) wa kaka/dada.

nephritis n uvimbe wa/kuvimba kwa mafigo.

ne plus ultra n (Lat) kikomo, kiwango

cha mwisho, kilele (cha kitu, jambo), upeo.

nepotism n upendeleo wa ndugu (agh katika kuajiri).

Neptune n 1 (Roman) (mungu wa)bahari. 2 Neptuni: sayari mojawapo iliyo mbali sana na jua.

nerve n 1 neva. ~ cell n seli ya neva. ~ centre n fungu la seli neva; (fig) kuni. 2 (pl) wahaka, hali ya wasiwasi; msukosuko in a state of ~s katika hali ya wasiwasi. get on one's ~s sumbua, kera. war of ~s n vita vya kuumbuana/kuvunja

nescience

moyo; jitihada za kumshinda mshindani kwa kumvunja moyo. ~-racking adj -enye kutisha/ kuogofya sana; enye kusumbua (hasa kihisi) suffer from ~s wa na wahaka. 3 ujasiri, ushupavu a man of ~ mtu shupavu. have the ~ to do something wa na ujasiri; thubutu he had the ~ to call me a liar alithubutu kuniita mwongo have a ~ (colloq) thubutu lose/regain one's ~ogopa/pata moyo. 4 (old use) ukano. strain every ~ to do something jitahidi sana, fanya juu chini. 5 mbavu za kati za jani. vt ~ oneself for something/to do something jipa moyo; kusanya nguvu. ~less adj 1 legevu, dhaifu. 2 -siotishika, tulivu. ~lessly adv. ~lessness n. nervous adj -1 -a neva nervous system mfumo w a neva a nervous breakdown fadhaa; kuchanganyikiwa, kuharibikiwa akili. 2 -enye wahaka, -oga. 3 (tense) -enye wasiwasi, liokacha. nervousness n wasiwasi,woga; kiherehere. nervy adj 1 (GB) (colloq) -enye wasiwasi/mfadhaiko. 2 (sl) -enye kudiriki, -enye ukavu wa macho, fidhuli.

nescience (formal) umbumbumbu. nescient adj -jinga be nescient of something -tojua kitu fulani.

ness n rasi.

-ness suff (with adj forming uncontable n) sifa, hali au tabia ya kuwa. good~ n uzuri. quiet~ n ukimya.

nest n 1 kiota, tundu. foul one's own ~ jiaibisha, nyea kambi. ~ egg n akiba ya fedha (kwa matumizi ya baadaye). 2 mahali pa kupumzikia, starehe. 3 mkusanyiko wa vitu vya aina moja vinavyoingiliana (hasa kasha, meza n.k.). 4 (fig) maficho; kivuli a ~ of crime maficho ya majambazi. vi tengeneza/tumia kiota. go ~ing tafuta viota vya ndege (ili kuchukua mayai). ~le vt,vi 1 ~le (down) tulia, starehe, jituliza (mahali pa starehe/kupumzikia). 2

neutral

~le up (against/to) jikumbatiza. 3 pakata, fumbata. ~ling n kinda; (chicken) kifaranga.

net1 n 1 wavu; kimia; jarife mosquito ~ chandarua. 2 (fig) mtego. 3 ~ ball n mpira wa pete, netiboli. the ~s n (cricket) sehemu ya mazoezi. ~work n mistari ipitanayo, tandabui, mfumo mtandao. spy ~work n mfumo wa upelelezi. vt 1 vua kwa wavu. 2 funika kwa wavu. ~ting n 1 wavu. 2 kutega wavu.

net2; nett adj ~ price bei halisi (haipunguziki). ~ gain/profit n faida halisi, faida tupu. vt pata faida halisi.

nether adj (arch) -a chini the ~ world ahera, jahanamu. (joking style) ~ garments n suruali. ~most adj chini sana.

Netherlands n Uholanzi. Netherlander n Mholanzi.

nettle n upupu. ~ rash n mwasho wa upupu. vt udhi he was ~d by my words maneno yangu yalimuudhi.

neural -adj a neva, -a mshipa wa fahamu. ~gia n ugonjwa wa neva (hasa kichwani).

neurasthenia n uchovu wa neva, udhaifu uletwao na uchovu wa neva. neurasthenic adj, n.

neuritis n uvimbe wa neva.

neurology n nyurolojia; elimu ya neva. neurological adj -a nyurolojia. neurologist n mtaalam wa nyurolojia. neurosis n fadhaa, kuchanganyikiwa, jakamoyo. neurotic adj -enye fadhaa/ jakamoyo, -a kuathiri mfumo wa neva. n mtu mwenye fadhaa/ jakamoyo.

neuter (gram) adj 1 sio na jinsi; (of verb) -siochukua shamirisho. 2 (of plants) -siokuwa na pistili wala stameni. n tasa; mnyama aliyehasiwa. vt hasi.

neutral adj 1 siosaidia upande wowote

katika vita. 2 sio pendelea upande wowote. 3 sio na sifa zinazobainika I am ~ mimi simo a ~ person mtu

neutron

asiyependelea upande wowote. 4 ~ gear n gia huru, sioinjikwa. ~ity n kutosaidia upande wowote katika vita declaration of ~ity tamko la kutokuwa upande wowote. ~ize vt 1 tangua, batilisha; zimua ~ize a poison zimua sumu.2 tokuwa upande wowote. ~ization n.

neutron n nutroni.

never adv 1 asilani, kamwe, hata she ~ goes to dances haendi densini asilani it has ~ been used kamwe haijawahi kutumika ~ despair usikate tamaa kamwe ~ ceasing; ~-ending adj sio kwisha ~-failing adj -sioshindwa. ~-more adv -si tena kabisa ~-to-be forgotten adv -siosahaulika. 2 hata kidogo I~ slept a wink last night sikulala hata kidogo. 3 (phrases). Well l~ (did)! lahaula. N ~mind! usijali. the N~ N ~ Land n nchi iliyobuniwa. on the ~ - ~ kwa kubandika.

nevertheless adv hata hivyo.

new adj 1 -pya nothing new hakuna (lolote) jipya. ~ moon n mwezi mwandamo. ~ Year n Mwaka Mpya. ~ Testament n Agano Jipya start/lead a ~ life anza maisha mapya. ~ World n Amerika ~ trial kusikilizwa upya. 2 (strange, novel) -geni she is ~ to me yeye ni mgeni kwangu. ~from kutoka juzijuzi a worker ~ from school mfanyakazi aliyetoka shuleni juzijuzi. 3 (modern) -a siku hizi, -a kisasa. a ~ fashion n mtindo wa kisasa adv karibuni. ~-born adj -liozaliwa karibuni a ~ born baby mtoto aliyezaliwa karibuni. ~-built adj -liojengwa karibuni, -pya. ~-coined adj -lioanzishwa karibuni; liobuniwa karibuni ~-coined word neno jipya. ~comer n mgeni (asiye mwenyeji). ~ found adj -liopatikana hivi karibuni. ~-laid adj (of an egg) -liotagwa karibuni. ~ly adv karibuni a ~ly married couple waliooana karibuni. ~ly-weds n maharusi.~ness n.

newel n nguzo/mhimili ya katikati ya

nib

ngazi.

news n pl 1 habari (za mambo yaliyotokea karibuni), taarifa. The N ~ n (on the radio) taarifa ya habari break the ~ toa habari (hasa ya msiba) ~ of death tanzia he is in the ~ habari zake zimechapishwa gazetini/zimetangazwa redioni. no ~ is good ~ (prov) ukisikia kimya jua ni shwari. ~agent n mwuuza magazeti. ~agency n shirika la habari. ~cast n taarifa ya habari. ~caster n mtangazaji wa taarifa ya habari. ~-boy n mvulana mwuuza magazeti (kwa kuyatembeza mitaani). ~ letter n kijarida. ~monger n mdakuzi, mmbea, mzushi. ~ paper n gazeti popular ~paper gazeti pendwa. ~ paper man n mwandishi wa magazeti/ habari. ~-print n karatasi za magazeti. ~reel n filamu ya taarifa ya habari. ~-room n 1 chumba cha habari (redioni n.k.). 2 chumba cha kusomea magazeti; maktaba. ~-sheet n gazeti rahisi. ~-stand n kibanda cha kuuzia magazeti. ~ less adj sio na habari. ~y adj -enye michapo, -enye habari za mambo yaliyotokea.

newt n mnyama mdogo wa majini kama mjusi.

Newtonian adj linalohusiana na Newton n mfuasi wa Newton.

next adj 1 ~ (to something/ somebody) -enye kufuata; kando their house is ~ to ours nyumba yao inafuata nyumba yetu the ~ best (thing) kitu kinachofuata kwa ubora ~ door nyumba ya pili. ~ door to (fig) inayokaribia. ~ but one -nayofuata baada ya. 2 (of time) wakati ujao ~ week wiki ijayo in the ~ few days siku chache zijazo the ~day kesho yake adv baada ya hapo; halafu what will you do ~? utafanya nini baada ya hapo come ~ fuata.

nexus n 1 kiungo. 2 mfululizo.

nib n nibu.

nibble

nibble vt,vi 1 ~ (at) nyofoa. 2 (fig) onyesha kuvutiwa (bila kutoa uamuzi). n unyofozi.

nice adj 1 -zuri, -a kupendeza; -ema, -enye hisani a ~ fellow! mtu mwema it was ~ of you nakushukuru kwa wema wako, ulifanya vema sana. 2 nyeti, -enye kuhitaji uangalifu. 3 (ironic) -gumu, -baya. 4 -a machagu. 5 -enye makini; -enye uangalifu. ~ly adv 1 kwa vizuri; kwa wema. 2 (colloq) vizuri sana; sawa, barabara. ~ness n. ~ty n 1 usahihi. 2 (pl) ~ties undani, mambo madogo madogo. to a ~ty barabara, sawasawa kabisa.

niche n 1 kishubaka, pembe. have a ~ in the temple of fame -wa na mafanikio yasiyosahaulika. 2 (fig) mahali pafaapo make a ~ for oneself pata sehemu inayofaa.

nick1 n 1 (alama ya) mtai. 2 in the ~ of time wakati ufaao hasa. 3 (sl) in the ~ korokoroni; jela. vt 1 kata; tia mtai. 2 (GB) (sl) iba he ~ed my pen aliniibia peni yangu.

nick2 n (sl) (only in) in good/poor ~ katika hali nzuri/mbaya.

nickel n 1 nikeli. 2 (coin) sarafu ya Marekani yenye thamani ya senti 5. vt chovya nikeli.

nicknack n see knick-knack.

nickname n jina la utani, lakabu. vt -pa jina la utani.

nicotine n nikotini; sumu iliyo katika tumbaku.

niece n mpwa (wa kike); mtoto (wa kike) wa kaka/dada.

niff n (GB sl, dial) mnuko. ~y adj (sl) -enye mnuko.

nifty adj (sl) 1 maridadi, -zuri. 2 -enye mnuko. 3 -epesi; hodari.

niggard n mchoyo, bahili. ~ly adj -a chonyo, -enye kutolewa roho upande. ~liness n ubahili, uchoyo.

niggle vi shughulikia mambo madogo madogo; lalamikia mambo madogo madogo. niggling adj dogodogo.

nigh adv, prep (arch and poet) karibu draw ~ karibia.

nimbus

night n 1 usiku. ~ after night kila usiku uchao. all ~ (long) usiku kucha. ~ and day usiku na mchana, kutwa kucha. at ~ usiku. by ~ wakati/majira ya usiku. get a ~ off pumzika kazi ya usiku. last ~ usiku wa kuamkia leo. to~ leo usiku, usiku huu. have a bad ~ lala vibaya. good ~! alamsiki. have a ~ out enda kutembea jioni. make a ~ of it kesha kwenye starehe. ~ into day fanya kazi ya mchana usiku. work ~s fanya kazi usiku. 2 (compounds) ~ bell n kengele ya kumwamshia daktari usiku. ~-bird n bundi; mtu atembeaye usiku, mzururaji. ~ cap n kofia ivaliwayo usiku; (usu alcoholic) kinywaji cha kulalia. ~club n klabu ya usiku. ~-dress; ~ie; ~y n (colloq) vazi (la kike) la usiku. ~ fall n kuchwa, utusitusi. ~ jar n upwaju. ~life n starehe za usiku. ~ -light n taa ndogo iwakayo kucha. ~ -long adj -a usiku kucha. ~mare n jinamizi. ~ safe n kisanduku cha benki (cha kuwekea amana usiku). ~-school n masomo ya jioni. ~-shade n mtunguja. ~shirt n shati refu (la kiume) la kuvaa usiku. ~-soil n choo kizolewacho usiku. ~-time n usiku. ~-watch n mkeshaji; zamu ya kukesha. in the ~ -watches wakati wa mkesha. ~-watchman n mlinzi wa usiku, korokoroni. ~ly adj,adv -a usiku, -a kila usiku; kila usiku.

nightingale n ndege aina ya kinega.

nihilism n kano: ukataaji wa dini na

sheria za ubinadamu zote. nihilist n. nihilistic adj.

nil n bila, sifuri the result of the game was ~ matokeo ya mchezo yalikuwa bila.

Nilotic adj -a Niloti; -a mto Nile na kandokando zake.

nimble adj 1 epesi, hodari (-a kazi),

elekevu. 2 (of the mind) kali, epesi. nimbly adv. ~ ness n.

nimbus n 1 wingu la mvua. 2 halo:

niminy-piminy

uzingo wa mtakatifu.

niminy-piminy adj -a kujidaidai;

-a kujifanya/kujitendekeza.

nincompoop n mpumbavu, punguani, fala.

nine adj, n tisa a girl of ~ msichana wa miaka tisa. ~ days' wonder kitu

kipya kivutiacho na kusahaulika mara. dressed up to the ~s liovaa kilimbwende, liovaa malidadi sana. ~ times out of ten mara nyingi, karibu kila mara. ninth adj,n sehemu ya tisa; -a tisa. the ninth hour dakika ya mwisho. ~ to five saa (za kawaida) za kazi. ~teen adv,n kumi na tisa. a boy of ~teen mvulana wa miaka 19. (talk) ~teen to dozen sema bila kunyamaza, bubujika. ~ teenth adj,n -a kumi na tisa; sehemu ya kumi na tisa. ~ty adj,n tisini. ~ty times out of a hundred karibu kila mara. the ~ties miaka ya tisini. ~ fold adj, adv (-a) mara tisa.

ninny n mpumbavu, zuzu.

nip n 1 mminyo, mfinyo, mbinyo. 2 mkato. 3 pegi (ya kileo). vt,vi 1 minya, finya, binya, nyakua. 2 (of dog) uma. 3 (destroy) haribu.~ something in the bud haribu mwanzoni, zuia maendeleo. 4 (colloq) ~ in (of car) ingia; (of dress) punguza upana. ~ along enda upesi. ~ ping adj kali; baridi sana. ~py adj (colloq) 1 epesi. look ~ py fanya chapu chapu. 2 (GB) baridi sana.

nipper n 1 (of crab) gando, gendi. 2 (pl) (colloq) (forceps) kibano, koleo. 3 (GB colloq) kitoto.

nipple n 1 chuchu. 2 kitu chenye umbo la chuchu.

Nipponese adj -a Japani.

nirvana n (in Buddhism) nirvana: hali ya kujisahau binafsi kwa kuungana na Mungu.

nisi n (Lat,leg) isipokuwa. decree ~n

amri halali isipokuwa pale inapokuwa na sababu za kubatilishwa katika muda uliowekwa.

nit n yai la chawa, utitiri, n.k.

no

nitrate n naitreti.

nitre/niter n shura. nitrous adj -a (kama) shura.

nitric adj -a naitrojeni, -enye

naitrojeni. nitrochalk n mbolea ya kukuzia majani. nitrogen n naitrojeni. nitrogenous adj -enye naitrojeni, -a naitrojeni.

nitro glycerine n baruti kali.

nitty-gritty n. the ~ n (colloq) kiini, masuala ya msingi.

nitwit;nit n (colloq) punguani. ~ ted adj.

nix n (sl) hapana, la say ~to kataa.

no adj 1 hapana, hakuna, hamna there is ~ food hakuna chakula I have ~ money sina pesa ~ doubt hapana shaka ~ mistake hapana kosa,si kosa it's ~ distance si mbali he had ~ luck hakuwa na bahati he is ~ fool yeye si mpumbavu. 2 marufuku ~ entrance marufuku kuingia ~ smoking usivute sigara. ~ nonsense! hapana upuuzi! 3 (in phrases) it's ~ go (colloq) haiwezekani. be ~ good/ use -wa bure. be ~ wonder (that) tokuwa jambo la ajabu (kwamba). in ~ time haraka sana, mara moja. ~ -go- area n eneo ambapo polisi/jeshi hawawezi kuingia. ~ - man's - land n eneo katikati ya majeshi mawili ya maadui; eneo huru rain or ~ rain mvua inyeshe isinyeshe. 4 (with -ing) there is ~ mistaking what was meant haiwezekani kukosea ni jambo gani lilimaanishwa/lilikusudiwa adv (used with comp) zaidi he's ~older hajazeeka zaidi~ fewer than a hundred haipungui mia moja he will come ~ more haji tena whether or ~ kwa vyovyote whether or ~ you will come upende usipende utakuja. n kukataa; hapana I won't take ~ for an answer hakuna kukataa the ~es have it wapingaji wameshinda (particle) hapana, la are you tired? No Umechoka? Hapana. ~body/ ~one (pron) hakuna, si mtu

nob

~ body is there hapana mtu ~ body knows hakuna ajuaye a mere ~ body mtu wa bure. ~ how adv (colloq) kwa njia yoyote ile.

nob1 n (sl) mkubwa, tajiri, kizito, mtu wa hadhi (ya juu).

nob2 n (sl) kichwa.

nobble vt 1 lewesha (farasi) ili asishinde mbio. 2 (colloq) pata kitu kwa ujanja.

noble adj 1 -a kilodi; (Islam) sharifu. 2 adili, -enye tabia nzuri. n (also) ~man n lodi; (Islam) sharifu; mtu mwenye cheo (daraja) kikubwa. nobly adv vema, vizuri, kwa uadilifu. nobility n 1 ulodi; (Islam) usharifu. 2 (character) wema, uadilifu, uungwana. 3 (class) malodi, waungwana; (Islam) masharifu.

noctambulist n mtembea usingizini. noctambulism n.

nocturnal adj -a usiku.

nocturne n 1 (music) muziki wa polepole/wa kulaza. 2 mchoro unaohusu mambo ya usiku.

nod vt,vi 1 ~ (to/at) kubali/amkia kwa kichwa. 2 ~ (off) sinzia; angusha kichwa kwa kusinzia. Homer sometimes ~s (prov) hata mtu ashuhuri hufanya kosa. 3 ashiria kwa kichwa. n 1 ishara ya kichwa. 2 the Land of N~ n usingizi. 3 on the ~ (US sl) kwa mkopo.

noddle n (colloq) kichwa.

node n 1 (bot) kinundu; chomozo, jicho. 2 (anat) kivimbe. 3 (tech) nukta inayokutanisha mistari miwili n.k. nodule n kinundu, kifundo, kivimbe. nodular adj.

Noel n Noeli, Krismasi.

nog n kileo (agh chenye mayai).

noggin n 1 kipimo kidogo (agh robo painti) cha pombe. 2 (sl) kichwa.

noise n 1 sauti, mlio,kishindo, uvumi. make a ~ (about something) lalamika, piga kelele. make a ~ in the world wa mashuhuri, pata umaarufu. 2(uproar) makelele, zahama. a big ~ n mtu maarufu. vt ~ something abroad tangaza, eneza

non-

habari. noisy adj -a makelele, -a kishindo kikubwa/ghasia. noisily adv kwa kelele/sauti. ~ less adj pasipo mlio/sauti; -a kimya. ~lessness n ukimya.

noisome adj -a kuchukiza, -a kutia kinyaa, -a kukirihi.

nomad n mhamahamaji. ~ic adj -nayohamahama. ~ism n kuhamahama, uhamahamaji.

nom de plume n lakabu.

nomenclature n (mfumo wa) istilahi, utaratibu wa majina; kutia majina.

nominal adj 1 dogo ~ consideration malipo chembe~ rent kodi ndogo ~ value thamani ndogo; thamani iliyo-tajwa, thamani bayana. 2 -a jina tu; iliyotajwa ~ capital rasilimali iliyotajwa, rasilimali bayana ~ plaintiff mdai wa jina tu. 3 si halisi. 4 (gram) -a nomino. ~ly adv kwa jina, kwa maneno tu. nominative n (gram) -a kiima.

nominate vt ~ 1 somebody (for) pendekeza (jina la mtu kwa cheo/kazi, n.k.). 2 ~ somebody (to) teua. nominator n mpendekezaji. nomination n1 pendekezo nomination paper hati ya mapendekezo. 2 uteuzi. nominee n 1 mtu aliyependekezwa. 2 mteule/ mteuliwa.

non- (pref) si, sio, -tokuwa. ~-alcoholic adj sio kileo ~-alignment n kutofungamana (na upande wowote).~ -appearance adj kutoonekana (tena). ~ aggression n kutotaka ugomvi/vita, n.k. ~ aggression pact n makubaliano ya kuzuia vita. ~-combatant n mtu (agh mwanajeshi) asiyepigana vitani. ~-commissioned adj (esp. milit) ofisa wa cheo cha chini.~-committal adj -siojihusisha (na upande wowote). ~ -compliance n kutoafiki, kutotekeleza.~-conductor n kisicho pitisha umeme.~conformist n mtu asiyefuata desturi za jamii. ~ conformity n kutokukubaliana na

nonage

kanuni za jamii. ~-consummation n kutokamilisha ~-consummation of marriage kutokamilisha ndoa (kwa kujamiiana). ~ -contagious adj sio ambukiza. ~ -contentious adj sio na ugomvi.~-cooperation n kutoshirikiana. ~essential adj sio ya lazima; sio ya muhimu. ~-event n (colloq) mpango uliovurugika. ~-existence n kutokuwepo. ~-existent adj sio kuwepo. -sio na uhai. ~-fiction n maandishi yasiyo ya kubuni. ~-flammable adj sioshika moto. ~-intervention; ~-interference n kutoingilia. ~-moral adj -siokuwa -a maadili. ~-observance n kutofuata sheria/masharti. ~-payment n kutolipa. ~-performance n kutotimiza, kutotekeleza. ~-resident adj siomkazi. n asiyeishi hotelini, n.k. ~-skid adj (of tyres) sioserereka. ~-smoker n asiyevuta sigara; behewa la abiria wasiovuta sigara. ~-stick adj -sionata. ~-stop adj,adv bila kusimama, moja kwa moja. ~-union adj 1 siojiunga na chama/jumuia ya wafanyakazi. 2 tofuata kanuni za chama/jumuiya. ~-violence n kutotumia nguvu, kutumia njia za amani. ~acceptance n kutokubali. ~-access n kutofikia, kutoingilia. ~-affiliated adj siyoungana na ingine (k.m. kampuni, shirika).

nonage n (leg) utoto.

nonagenarian n mzee mwenye umri wa miaka kati ya 89 na 100 adj -enye miaka kati ya 89 na 100.

nonce n (arch, or lit) (only in) for the ~ kwa wakati huu tu. ~-word n neno linaloundwa kwa ajili ya muktadha maalumu.

nonchalant adj tepetevu; sioonyesha kupenda; sio na raghba, sio na papara. ~ly adv. nonchalance n.

non compos mentis (Lat) adj (leg) sio na akili timamu; (colloq) liochanganyikiwa.

nondescript n, adj (person or thing)

Nordic

-sioainishika, sioelezeka vizuri, -a hivi hivi.

none (pron) 1 bila, kutokuwepo,hakuna ~ of us hakuna kati yetu. ~ the less hata hivyo. ~ but hakuna mwingine isipokuwa. ~ other than enyewe it was ~ other than the chairman alikuwa ni mwenyekiti mwenyewe. 2 acha! ~ of that acha! ~ of your stupidity acha upumbavu wako adv sio, hapana I am ~ the wiser for your information sikunufaika na taarifa yako.There are ~ so deaf as those who will not hear (prov)wanaokataa kusikiliza ndio viziwi.

nonentity n 1 mtu asiye na hadhi, mtu duni. 2 hobela hobela 3. jambo la kuwazika tu, ndoto.

nonesuch; nonsuch n mtu/kitu kisicho kifani.

non-pareil adj, n (formal) teule, bila kifani; sio kifani (kwa kuwa zuri, bora).

nonplus vt duwaza, pumbaza; shangaza.

nonsense n upuuzi. nonsensical adj sio na maana; -a upuuzi.

non-sequitur n (Lat) (logic) hitimisho lisilofuata mantiki.

noodle1 n baradhuli, mpumbavu.

noodle2 n nudo: chakula aina ya tambi. nook n pembe, kipembe; kificho, upenu.

noon n adhuhuri, saa sita mchana. ~day; ~tide n adhuhuri.

no-one; no one pron see nobody.

noose n tanzi, kitanzi, shalaka, kishwara. put one's head in the ~ (fig) (jisababisha kukamatwa, jifunga mwenyewe. vt tega ~ a cord fanya kitanzi katika kamba.

nope int (sl) la, hasha!

nor1 conj wala neither... nor si... wala

neither Daudi ~ Abdallah si Daudi wala Abdalla ~ must we forget wala tusisahau.

nor2 (pref) north.

Nordic n, adj watu wa Kinodiki; -a

nchi za Skandinavia (Denmark,

norm

Finland, Norway na Sweden).

norm n 1 kaida, kawaida, kanuni, cheo cha kawaida. 2 ngwe, kiwango. ~ative adj -a kusanifisha; sanifu.

normal adj -a kawaida/desturi, -a siku zote. a ~ school n chuo cha Ualimu n kawaida. ~ly adv. ~ity; ~cy n. ~ize vt fanya kawaida. ~ization n.

Norse n lugha ya Norway adj -a Norway.

north n 1 kaskazini. the ~ n upande wa kaskazini, nchi za Kaskazini. 2 (attrib) -a kaskazini N~ Pole Ncha ya kaskazini ~ winds kaskazi. ~east n kaskazini mashariki. ~west n kaskazini magharibi. the N~-West Passage n njia ya baharini kutoka Atlantiki mpaka Pasifiki (kupitia Kaskazini ya Kanada na Alaska). ~-easter n upepo kutoka kaskazini mashariki. ~-eastern adj -a kaskazini mashariki. ~-eastward adj (-a) kuelekea kaskazini mashariki. ~-western adj -a kaskazini magharibi. ~erly adj (of winds) -a kaskazini adv (of wind) kaskazini. ~ wards adj -a kuelekea kaskazini. ~ern adj -a kaskazini. the ~ern lights n miali ya kaskazini ya dunia. ~erner n mwenyeji/mkazi wa sehemu ya kaskazini mwa nchi. ~ ernmost adj -a kaskazini kabisa.

Norwegian adj -a Norway; mtu wa Norway.

nose n 1 pua speak through the ~semea puani. bite/snap somebody's ~ off jibu vikali. count/ tell ~s hesabu watu. cut off one's ~ to spite one's face kata pua uunge wajihi, jiumiza ili kulipa kisasi. follow one's ~ enda mbele moja kwa moja. keep a person's ~ to the grindstone fanyisha kazi bila kupumzika. look down one's ~at somebody dharau; tendea ufidhuli. pay through the ~ lipa gharama kubwa sana. poke/stick one's ~ into ingilia. turn one's ~ up at dharau. as plain as the ~ on one's face, dhahiri. (right) under his very ~

notch

palepale; mbele yake. 2 hisi za kunusa. 3 kitu chenye umbo kama pua, kitu kilicho mbele kabisa. 4 (compounds) ~-bag n mfuko wa chakula cha farasi. ~-band n sehemu ya hatamu (ipitayo juu ya pua). ~-bleed n mnoga, muhina; kutokwa na muhina. ~-cone n kichwa cha roketi. ~-dive (of aircraft) n mteremko wa kutanguliza kichwa. vi anguka kwa mteremko mkali huku kichwa kimetazama chini. ~-flute n zumari ya pua. ~ gay n fungu la maua.~ -rag n (sl) leso ya mfukoni. ~-ring n hazama. ~-wheel n gurudumu la mbele la ndege. ~d adj -enye pua long ~d -enye pua ndefu short ~d -enye pua kipande. vt,vi 1 sogea mbele polepole. 2 ~ something out vumbua/gundua (kwa kunusa). 3 ~ about (for something) nusa nusa; (fig) dadisi. ~ into something dukiza, ingilia kati. ~y;nosy adj -dadisi. n (sl) mdadisi. ~ parker n mdadisi.

nosh n (GB sl) chakula. ~-up n chakula kizuri. vi (colloq) -la.

nostalgia n kiu/hamu ya nyumbani/ mambo yaliyozoewa. nostalgic adj -enye hamu/kiu ya nyumbani/ mambo yaliyozoewa. nostalgically adv.

nostril n tundu ya pua, mwanzi wa pua. nostrum n dawa ya uwongo.

not adv si, siyo, hapana. ~ so sivyo.

~at all; ~ a bit si kitu; hata kidogo, hasha ~but what hata hivyo; ingawa. ~ to say;~ only licha ya ~ a man spoke hakusema mtu hata mmoja as likely as ~ huenda, labda.

nota bene vt angalia kwa makini.

notable adj -a kutambulika, -enye sifa,mashuhuri. n mtu mashuhuri/ maarufu. notably adv. notability n. notary n ~ public n mthibitishaji rasmi.

notation n mwandiko.

notch n 1 mkato wa umbo la v; (US)

note

njia nyembamba katika milima. 2 (of arrow) koleo. 3 (in upright poles for building) makwa. vt fanya mkato wa umbo la v. ~ up (colloq) pata, fanikiwa.

note n 1 muhtasari. 2 (memorandum) ukumbusho; maneno ya kukumbusha. marginal ~s n maelezo ya pembeni. ~ book n daftari. 3 barua; maneno machache drop me a ~ niandikie barua. ~paper n karatasi ya barua. 4 (music) noti. sound a ~ of warning (against something) onya, tahadharisha. strike the right ~ (fig) gusa watu kwa maneno. strike/sound a false ~ udhi watu. 5 bank ~ n noti. 6 (fame) sifa, jina a person of ~ mtu mkubwa/mashuhuri worthy of ~ yafaa ifahamike, -a kufaa, bora. 7 fahamu take ~! fahamu. 8 maoni, tajriba compare ~s peana maoni. vt 1 angalia, ona. 2 ~ something (down) kumbuka,andika. ~d adj maarufu. ~worthy adj -a kufaa kuangaliwa.

nothing n 1 hakuna kitu, si kitu there is ~ to be done hakuna lolote la kufanya he has five foot ~ ana futi tano kamili.2 (phrases) be ~ to tovutia, topendwa. come to ~ tofanikiwa. go for ~ tokuwa na maana all my work went for ~ kazi yangu ilikuwa bure. have ~ to do with tohusu it has ~to do with you haikuhusu, tohusika. make ~ of toelewa, toka kapa. mean ~ to tokuwa na maana kwa. to say ~ of sembuse. think ~ of chukulia (jambo) kuwa kawaida, tojali. think ~ of it usijali. for ~ bure, bila malipo; bila zawadi; bila lengo. ~ but tu. ~ for it but ila...tu there's ~ for it but to tunachoweza kufanya ni, hapana zaidi ya. N ~ doing! La hasha! ~ness n hali ya kutokuwepo kitu.

notice n 1 notisi, taarifa, tangazo put a ~ in the newspaper tangaza gazetini a ~ of marriage tangazo/taarifa ya ndoa. ~-board n ubao wa matangazo

nous

our employer has given us a month's ~ mwajiri wetu ametupa notisi ya mwezi mmoja ya kusimama kazi a tenant was given ~ to quit mpangaji alipewa notisi ya kuhama nyumba. do something at short ~ fanya jambo bila kupata nafasi ya kujiandaa. 2 kuweka maanani, kufahamika. be beneath one's ~ wa kitu cha kutotiwa/wekwa maanani. bring something to somebody's ~ fahamisha mtu jambo fulani. come to somebody's ~ arifiwa/tambua/pata habari sit up and take anza kupata ahueni. make somebody sit up and take ~ amsha. take no ~(of something) tojali, toangalia kwa makini. 3 uhakiki wa kitabu/mchezo mpya n.k. katika jarida. vt,vi 1 angalia, fahamu, ona. 2 hakiki. ~ able adj -a kuonekana kwa urahisi. ~ably adv. notify vt julisha, arifu, tangaza. notification n kutaarifu; taarifa. notifiable adj liolazimu kujulishwa (hasa magonjwa yanayopaswa kujulishwa kwa vyombo vinavyo husika).

notion n 1 wazo, fikira I have no ~ sifahamu hata kidogo. 2 dhana. 3 (pl) (US) vikorokoro. ~al adj 1 (of knowledge) -a kufikirika, -a kuwaza tu. 2 dogo, -a mfano.

notorious adj -enye sifa mbaya, -a kuvuma kwa ubaya. ~ly adv. notoriety n.

notwithstanding (prep) licha adv hata hivyo (conj) ijapokuwa.

nougat n kashata.

nought n 1 si kitu, si neno. come to ~ batilika, tanguka, shindikana. bring somebody/something to ~ batilisha, tangua; angamiza, haribu. set somebody/something at ~ tojali, pinga, dhalilisha. 2 sifuri.

noun n (gram) jina, nomino.

nourish vt 1 lisha; stawisha; rutubisha. 2 tunza (jambo) moyoni. ~ment n chakula.

nous n akili; busara.

nouveau riche

nouveau riche n (F) mtu aliyetajirika hivi karibuni, tajiri wa juzijuzi.

novel1 adj pya, geni ~ ideas mawazo mapya. ~ty n 1 upya, ugeni. 2 kitu kipya; shani. 3 (fig) (pl) vikorokoro.

novel2 n riwaya. ~ette n riwaya fupi. ~ist n mwandishi wa riwaya. ~ize vt badili iwe kama riwaya (k.m. tamthiliya. ~la n riwaya sahili.

November n Novemba: mwezi wa kumi na moja.

novena n (rel) novena.

novercal adj (arch) -a mama wa kambo.

novice n 1 mwanafunzi, mwanagenzi; limbukeni. 2 mwanafunzi wa utawa, mnovisi. noviciate; novitiate n.

now adv 1 sasa, sasa hivi; mara moja. (every) ~ and then/again mara kwa mara ~ then ehe! sasa! ~then what's troubling you? ehe sasa nini kinakusumbua? just ~ sasa hivi. up to ~ mpaka sasa. by ~ hadi/mpaka sasa. ~adays adv siku hizi. ~aday adj -a siku hizi. 2 (conj) kwa kuwa ~ (that) you have mentioned it kwa kuwa umetaja. ~... ~ /then mara ... mara ~ hot ~ cold mara joto mara baridi.

noway adv (sl) si... haiwezekani, sahau will you help me? noway, do it yourself nisaidie! sahau ifanye mwenyewe.

nowhere adv si...mahali popote I went ~ sikuenda popote the man is ~ to be seen yule mtu haonekani mahali popote. be/come in ~ shindwa kabisa.

nowise adv (old use) kwa njia yoyote. noxious adj -a kudhuru, -enye madhara, -a kuchukiza, -baya. ~ thing n kitu cha kudhuru. ~ly adv. ~ness n.

nozzle n ncha ya neli ya mpira/metali.

nuance n tofauti ndogo (katika maana ya neno, rangi, maoni n.k.).

nub n 1 (fig) kiini (agh cha jambo/

hadithi). 2 chenga (ya makaa).

nubile adj -a kuoleka, liofikia umri wa

kuolewa. nubility n.

number

nuclear adj 1 -a kiini. 2 -a nyuklia ~ weapons silaha za nyuklia ~ energy nishati ya nyuklia ~ energy plant mtambo wa nishati ya nyuklia. nucleus n 1 kiini. 2 chanzo, asili.

nude adj 1 tupu, lio uchi, bila kuvaa nguo. 2 (art) bila mapambo. n uchi. in the ~ uchi paint from the ~ chora picha ya mtu aliye uchi. nudist n mtu anayependa kukaa uchi, anayeamini kuwa kukaa uchi juani na katika upepo/hewa huleta afya bora. nudist camp/colony n mahali pa wanaopenda kukaa uchi juani. nudity n kukaa uchi.

nudge vt ashiria kwa kudukua/kugusa na kiwiko. n muashirio wa kudukua/ kugusa na kiwiko.

nugatory adj hafifu, sio na thamani, -a bure.

nugget n kipande, kibamba (cha dhahabu au madini).

nuisance n adha, usumbufu, kero a perfect ~ mchoshi. be a ~ -wa msumbufu.

nuke n US (sl) bomu la nyuklia.

null adj batili, liotanguka. ~ and void -liotanguka/batilika kufa. ~ify vt batilisha. ~ity n. ~ification n.

numb adj -enye ganzi, -zito. 1 vt tia/ fanya ganzi. 2 be ~ to tosikia, tojali.~ly adv. ~ness n.

number n 1 hesabu; kiwango; idadi; watu kadhaa (written)~ of people tarakimu. his/your~ is up (colloq) ame/umepatikana; utakufa. in ~ kwa idadi, kwa jumla. to the ~of kufikia. without ~ sio na idadi, sio hesabika. times without ~ mara nyingi mno; kila mara. ~ plate n kipande cha namba ya gari. 2 namba. the ~ three n namba tatu. ~one n wahedi. look after/take care of~ one jiangalia, jitunza. negative ~ n namba hasi. nominal ~ n namba ya jina. 3 (of magazine, etc) toleo. back ~ n toleo la nyuma (fig) liopitwa na wakati. 4 (mus) onyesho, wimbo (katika mfululizo). 5 (gram) idadi. 6 (pl) wingi they

numbskull

defeated us by ~s walitushinda kwa wingi wao. in great ~ s tele, ingi. 7 (pl) (arithmetic) hesabu. vt,vi 1 tia hesabu/namba my days are ~ed sina siku nyingi za kuishi. 2 pata, fikia the people ~ed fifty watu walipata hamsini. 3 ~ somebody/something among hesabia. 4 (mil) ita, taja namba. ~less adj ingi, pasipo idadi, sio na namba, siohesabika.

numbskull n (US) see numskull.

numeral adj -a numerali, -a hesabu,

-a tarakimu. n numerali, tarakimu, herufi ya hesabu. Arabic ~ n namba k.v. 1,2,3,4, n.k. Roman ~ n namba k.v. I, II, III, IV, n.k.. numerable adj -enye kuhesabika. numerate adj -enye ujuzi wa hesabu. numeration n hesabu, kuhesabu ~ system mfumo wa numerali. numerator n kiasi. numerical adj -a numerali numerical methods mbinu za numerali. numerous adj ingi.

numinous adj -a kuogofya; -a Mungu.

numismatics n elimu ya sarafu na nishani. numismatist n msomi wa elimu ya sarafu na nishani.

numskull n mpumbavu, baradhuli.

nun n mtawa wa kike(wa chama cha dini). ~nery n nyumba ya watawa wa kike.

nuncio n mjumbe au balozi wa Papa (Baba Mtakatifu). nunciature n ofisi ya mjumbe wa Papa.

nuptial adj -a arusi. n arusi.

nurse n 1 muuguzi, nesi. 2 mlezi, yaya. ~ maid n yaya; (fig) mtunzaji wa wengine.wet~ n mama wa kunyonyesha. 3 kulea put a child out to ~ peleka mtoto kwa mlezi. ~-child n mtoto wa kupanga. vt 1 (of a baby) nyonyesha nursing mother mama anaye nyonyesha. 2 tunza; uguza magonjwa; ponyesha. ~ a cold shughulikia mafua. nursing home n hospitali ndogo ya binafsi. 3 angalia, tunza she ~d her beer all evening alitunza bia yake jioni (yaani isimalizike mapema). 4 (in the mind) weka, fikiri.

nymph

nursery n 1 ~ (school) n shule ya watoto wadogo /vidudu/chekechea /awali. 2 chumba cha watoto. ~-rhyme n wimbo wa watoto. 3 bustani ya miche. ~-man n mtunza bustani ya miche. nurs(e)ling n 1 mtoto mchanga. 2 mmea mchanga.

nurture n 1 malezi. 2 mafunzo; elimu. vt 1 lea. 2 elimisha.

nut n 1 kokwa; njugu; lozi. ground/ pea~ n njugu nyasa, karanga; bambara. hard ~ n njugumawe. coco~ n nazi. a hard ~ to crack tatizo gumu, kitu/mtu ambaye vigumu kumshughulikia. ~-brown adj -enye rangi ya karanga iliyokaangwa. ~-butter n siagi ya karanga. ~crackers n kitu cha kubanjia kokwa. ~shell n ganda, gamba la kokwa. (fig) (put something) in a ~shell (sema) kwa muhtasari, kwa ufupi. 2 (tech) nati. ~s and bolts mambo ya msingi na rahisi. 3 (sl) kichwa. off one's ~ wazimu. ~-house n hospitali ya vichaa. 4 (pl) vibonge vya makaa. vi go ~ting chuma kokwa. ~s adj (sl) kichaa. be ~s about/over somebody/something penda sana, shabikia. ~ty adj 1 -enye ladha ya karanga/njugu. 2 -enye njugu nyingi. 3 (sl) liopenda sana. 4 (sl) -enye wazimu. ~tiness n.

nutmeg n kungumanga; (spice)basibasi. nutriment n chakula bora.

nutrition n lishe.

nutrient adj -a virutubishi. n kirutubishi. nutrition n lishe. nutritious adj rutubishi. nutritive adj rutubishi nutritive value thamani ya chakula. n mlisho.

nuzzle vi,vt 1 gusagusa/kumba kwa pua. 2 ~ up (against/to) sugua/sukuma kwa pua.

nylon n nailoni.

nymph n 1 mwanamwali mzuri. 2 (fairy) zimwi. 3 tunutu. ~et n mwanamwali anayetamaniwa. ~o n (colloq) (abbr of ~omaniac) n ugonjwa wa mwanamke kuwa na ashiki sana. ~omaniac n, adj.

 

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.