TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

O1o n 1 herufi ya kumi na tano ya alfabeti ya Kiingereza. 2 sifuri.

o2,oh 1 interj sl o,oh mlio wa mshangao/hofu. 2 ee, enyi. 3 (to stress) oh no! la, hasha. o' prep (abbr of) o'clock.

oaf n bwege. ~fish adj ~shness n.

oak n mwaloni (attrib) -a mwaloni ~door mlango wa mwaloni. ~en adj (esp. lit poetic) -a mwaloni.

oakum n nyuzinyuzi za kamba iliyo- chakaa na kufumuliwa (hutumika kwa kukalafati).

oar n kasia; mpiga kasia. pull a good~ -wa mpiga makasia mzuri. put/shove/stick one's ~ in jidukiza, jiingiza. rest/lay on one's pumzika kwa muda (wakati wa kazi). chained to the ~s liolazimishwa kufanya kazi kwa bidii na kwa muda mrefu. ~lock n kishwara. ~sman/ ~swoman n mpiga kasia. ~smanship n upigaji wa kasia. vi piga kasia.

oasis n oasisi: mahali penye miti na chemchemi katika jangwa; (fig) mahali/jambo lenye raha.

oast n ~-house n tanuru la kukaushia maua yatumiwayo kutengeneza pombe.

oat n usu (pl) shayiri. sow one's wild ~s piga maisha ujanani. be off one's ~s (colloq) tojisikia vizuri. feel one's ~s (colloq) changamka. ~cake n keki ya shayiri. ~meal n unga wa shayiri.

oath n kiapo, kasama, yamini; (curse) laana, apizo. put on/under ~ apisha. upon your ~! apia! exchange ~s apiana administer an ~ apisha commissioner for ~s kamishina wa viapo ~ of allegiance kiapo cha utii take an ~ on the Koran apa yamini; kula yamini. swear on/take an ~ kula kiapo.

obdurate adj shupavu, gumu; kaidi. obduracy n.

obeisance n kuinamisha kichwa (ishara ya kuheshimu, kustahi), kusujudu. pay ~ shika miguu.

object

obelisk n 1 mnara mrefu wenye pande

mraba zilizochongoka juu. 2 (printing) alama (- au +) iliyotumika zamani katika maandishi.

obese adj (of persons) nene sana, -enye kitambi. obesity n.

obey vt,vi tii, sikia; tumikia. obedient

adj -tiifu, -sikivu; (katika barua) your obedient servant wako mtiifu. obedience n. obediently adv.

obfuscate vt 1 fumba, tatiza, changanya. 2 tia giza. obfuscation n.

obi n (Japan) kibwebwe kivaliwacho na watoto/wanawake.

obiterdictum n msemo wa kando.

obituary n tanzia ~ notices taarifa za waliofariki. obituarist n mtangaza tanzia.

object n 1 kitu; jambo ~ lesson somo linalofundishwa kwa vielezo; tukio/ hadithi yenye funzo/onyo no ~ bila kizuizi money is no ~ fedha si kizuizi. 2 (aim, purpose) nia, kusudi, madhumuni my ~ is kusudi langu ni; nataka; ndiyo nitakayo. fail in one's ~ shindwa kutimiza kusudi. 3 (gram) shamirisho direct ~ yambwa indirect~ yambiwa. vt, vi 1 kataa, bisha, pinga. ~ to somebody bishia mtu, katalia mtu. 2 ~ (against somebody) that pinga, toa sababu kupinga/dhidi ya. ~or n mpinzani; mbishi. ~ify vt 1 toa kielelezo ili kuthibitisha. 2 eleza waziwazi (kwa kuonyesha kitu hasa). ~ion n 1 katazo, kinzano, kipingamizi, kizuizi there is no ~ion hakuna kipingamizi raise ~ions toa vipingamizi/vizuizi. 2 (feeling of dislike) uchungu, chuki, kutopenda; take~ ion to something pinga jambo. ~ionable adj -a kuchukiza. ~ionably adv .~ive adj 1 -a kuhusu jambo/kitu. 2 bila upendeleo my advice is quite ~ive shauri langu nimelitoa bila upendeleo. 3 (gram) -a shamirisho. n 1 (phil) halisi. 2 (mil) lengo, shabaha. ~ivism n (phil) nadharia inayotazama mambo kama yalivyo. ~ively adv. bila upendeleo. ~ivity

objurgate

n kutopendelea.

objurgate vt (liter) kemea, karipia. objurgation n kemeo, karipio.

oblate adj (geom) -a kubenuka. oblation n (rel.) sadaka, dhabihu.

oblige vt 1 ~ somebody to do something lazimisha/taka mtu aahidi/ afanye jambo. 2 be ~d to do something shurutishwa, lazimishwa we were ~d to shut the window tulilazimishwa kufunga dirisha. 3 fadhili ~ me by closing the door nifanyie hisani unifungie mlango/tafadhali ufunge mlango. Iam much ~d to you nakushukuru sana. obligate vt obligate somebody to do something wajibisha he was obligated to help me aliwajibika kunisaidia. obligation n 1 wajibu, faradhi, sharti undertake an obligation wajibika meet one's obligation timiza wajibu. 2 ahadi, lazima. 3 deni. put/be under an obligation shurutisha; fadhili (ili naye aone anadaiwa). obligatory adj -a lazima, -a kujuzu, -a wajibu.

oblique adj 1 -a mshazari, -a kukingama ~ prism mche shazari ~ line mstari shazari. 2 -a kuzunguka; si wazi ~ reference to mtajo usio wazi. ~ly adv kwa kukingama. obliquity n 1 mshazari; mafyongo. 2 upotovu; ufidhuli.

obliterate vt futilia mbali, ondoa kabisa, haribu. obliteration n.

oblivion n hali ya kusahau/ kusahauliwa, kutokumbukwa kabisa buried in ~ sahauliwa kabisa. oblivious adj oblivious of -siotambua; sio na kumbukumbu be oblivious of what was happening siotambua lililokuwa likitendeka.

oblong adj -a mstatili. n mstatili.

obloquy n aibu, fedheha, masuto, kashfa.

obnoxious adj -a kuchukiza, makuruhu. ~ly adv. ~ness n makuruhu; karaha.

obscene adj -chafu, -pujufu. ~ly adv. obscenity n.

obsess

obscure adj -a giza, -sio

onekana/eleweka vizuri. vt fanya giza, zuia isionekane, vuruga. ~ly adv. obscurity n 1 giza, uvunguvungu. 2 (indistinctness) fumbo. live in obscurity ishi katika mashaka. obscurantism n 1 upingaji wa kupata maarifa/ufunuo. 2 kutoeleweka kwa makusudi, uvungaji wa (makusudi).

obsequies n mazishi.

obsequious adj ~ (to/towards) -enye kutii kwa unyenyekevu sana/ kujipendekeza sana, -a kurairai, -enye kujikomba. ~ly adv. ~ness n unyenyekevu; ukombi.

observe vt,vi 1 angalia kwa makini; chunguza; hoji. 2 fuata, shika kanuni; adhimisha (sherehe). 3 toa wazo. ~r n 1 mwangalizi, mtazamaji; mchunguzi. 2 mfuata kanuni. observing adj -epesi kutambua. observingly adv. observable adj -a kuonekana; -a kutazamika. observably adv. observance n 1 kushika mila na desturi. 2 kanuni za dini, mila. observant adj 1 -epesi kutambua, -elekevu be observant of something angalia sana kitu fulani. 2 angalifu, chunguzi; sikivu, tiifu. observantly adv. observation n 1 kuangalia by personal observation kwa kutazama/ kuchunguza mwenyewe kwa macho. be under observation angaliwa. keep somebody under observation angalia mtu kwa makini. observation car n (in a train) gari la kuangalilia mandhari. observation post n kituo cha uchunguzi/ kuangalia maadui. 2 uelekevu wa kutambua a man of no observation mtu asiye na uelekevu. 3 (remark) wazo make an observation toa wazo. 4 (usu pl) (taarifa zilizokusanywa na kuhifadhiwa). observatory n mahali pa kuangalilia jua/mwezi/nyota.

obsess vt (usu passive) ~ed (by/with) shika, shikilia, jaza he is ~ed by fear amejawa na hofu. ~ion n 1

obsolete

kushikwa na hofu/wazo n.k. 2 (desire) ~ion (about/with something/somebody) tamaa, shauku (inayojaa moyoni) isiyotulizika. ~ive adj -enye kushika/shikilia (tamaa, shauku).

obsolete adj -siotumika siku hizi, -kongwe, -liopitwa, -siofaa (kwa neno) it is ~ imefutwa, haifai. obsolescent adj -siofaa kwa sasa; -liyopitwa na wakati. obsolescence n hali ya kitu kutofaa kutumiwa sasa, hali ya kupitwa na wakati.

obstacle n kizuizi, kikwazo: put ~s in the way weka vizuizi njiani.

obstetric(al) adj -a ukunga; -a kuzalisha; -a uzazi an ~ ward wadi ya uzazi. ~ian n daktari wa uzazi. ~s n tiba ya uzazi.

obstinate adj 1 -kaidi, -bishi, -enye inadi. 2 (of disease) sio tibika kirahisi, -siokubali dawa kwa urahisi. ~ly adv. obstinancy n ukaidi, usugu.

obstreperous adj 1 tundu; tukutu. 2 -a makelele. ~ness n. ~ly adv.

obstruct vt 1 zuia, pinga, kinza. 2 ~ a bill in parliament zuia mswada bungeni. ~ion n 1 kuzuia. 2 (obstacle) kizuizi, kipingamizi. ~ionism uzuiaji, upingamizi. ~ionist n mzuiaji, mkinzani. ~ive adj -a kuzuia, -a kipingamizi. ~ively adv.

obtain vt,vi pata, jipatia; nunua. 2 (of rules, customs) kubalika; tumika. ~able adj -a kupatikana it is ~able inapatikana; inakubalika.

obtrude vt, vi ~ upon jiingiza, jitia kati, jidukiza. obtrusion n kujidukiza, kujiingiza obtrusive adj -enye kudukiza. obtrusively adv.

obtuse adj 1 pumbavu. 2 butu ~ angle pembebutu. ~ness n.

obverse n 1 sehemu ya juu ya sarafu. 2 uso wa kitu chochote kinachotarajiwa kuwakilishwa.

obviate vt ondoa; toa.

obvious adj wazi; dhahiri, -a kuonekana wazi; -a kueleweka it was

ocean

the ~ thing to do lilikuwa jambo dhahiri kutenda. ~ly adv. ~ness n.

occasion n 1 nafasi, fursa, wasaa take this ~ to do something chukua fursa hii kufanya jambo fulani; (particular time) wakati maalum (kwa jambo fulani); wakati ufaao on the present ~ kwa wakati uliopo we have met on several ~s tumeonana mara nyingi. on ~ mara kwa mara; ikibidi. rise to the ~ onyesha uwezo unaohitajika. 2 haja; sababu if the ~ arises kama ikihitajika this is no ~ for laughter hakuna sababu ya kucheka. 3 tukio. vt sababisha. ~al adj 1 -a mara moja ~al showers rasharasha. 2 -a kufaa wakati fulani. ~ally adv mara chache.

Occident n (liter) the ~ nchi za (Ulaya Magharibi na Marekani), Magharibi. ~al adj -a Magharibi. n mwenyeji wa nchi za magharibi.

occult adj 1 -a mizungu. 2 liofichwa, -a siri, -a fumbo. the ~ n kitu kilichofichwa (kinachofahamika kwa watu maalum).

occupy vt 1 twaa, shika, miliki, chukua. 2 ishi katika nyumba/miliki nyumba. 3 (use, give work to) chukua (muda), shughulisha, tumia. ~ somebody's mind shughulisha akili ya mtu. 4 -wa na, shika ~ an important post -wa na cheo kikubwa. occupant n 1 mkaaji, mwenyeji. 2 mmiliki, mmilikaji. occupancy n. occupation n 1 shughuli, kazi, biashara. 2 (taking possession) kutwaa, kumiliki. 3 kipindi/muhula wa kumiliki. occupational adj -a shughuli, -a kazi. occupier n.

occur vi 1 tokea. 2 (enter the mind). ~ to ingia mawazoni an idea ~s to me wazo hunijia. 3 -wapo mistakes do ~ makosa hutokea. ~rence n tukio, kadhia of frequent ~rence -liotokea mara nyingi.

ocean n 1 bahari. ~ going adj -enye kusafiri baharini. 2 ~ of (colloq) -ingi he has ~s of money ana pesa

ochre;ocher

nyingi. ~ic adj -a bahari kuu, -a kupita baharini; -a kuishi baharini. ~ography n elimu ya bahari.

ochre;ocher n (red) ngeu, ngegu, ukaria.

o'clock n = (of the clock) what ~? it is eight ~ saa ngapi? saa mbili.

octagon n pembenane. ~al adj -enye pembe nane.

octane n oktani.

octave n 1 (music) sauti nane. 2 (poetry) ubeti wenye mistari minane.

October n oktoba: mwezi wa kumi. octogenarian n mzee mwenye umri wa miaka themanini hadi themanini na tisa adj -enye umri wa miaka themanini.

octopus n pweza.

oculist n daktari wa macho. ocular adj -a macho; kwa macho; kwa kuona. ocularist n mtengeneza macho ya bandia.

odalisque n suria; kimada.

odd adj 1 -moja (pasipo mwenzi wake); -moja au zaidi (katika seti/jozi). 2 (number) witiri ~ degree nyuzi witiri ~ number namba witiri ~ power vipeo witiri. 3 pamoja na -ingine a hundred ~ shilings shilingi mia moja na ushei. 4 -sio -a mara kwa mara, -a muda (mfupi), -sio -a kawaida at ~ times katika nyakati fulani ~ moments nyakati fulani ~ job kazi za pembeni. 5 (worthless) -a ovyo, hafifu. 6 (ridiculous) -a mzaha; -a kuchekesha; -a ajabu ~ man mtu wa ajabu. ~ man out mtu/kitu kilichobaki (baada ya vingine kuwa kwenye seti); (colloq) mtu aliyejitenga, aliye tofauti na wenzake wote how ~! ajabu! ~ly adv kwa namna ya pekee. ~ity n ugeni, ajabu, shani, kioja. ~ments n 1 (pl) vikorokoro. 2 mabaki, masalia.

odds n (pl) 1 nafasi/uwezekano (wa kufaulu au kushindwa kufanya jambo) the ~are in our favour tuna nafasi nzuri ya ushindi. 2 kutokuwa sawa. make ~ even sawazisha mambo. 3

off

kutopatana. be at ~ (with somebody) (over/on something) bishana; gombana; zozana. 4 tofauti. it makes no ~ hakuna tofauti; haidhuru; mamoja. what's the ~? haidhuru. 5 ~ and ends n takataka; vikorokoro. 6 the ~ n (gambling) matumaini.

odium n chuki. odious adj -a kuchukiza, makuruhu, -a ikirahi. odiously adv.

odometer n odometa: chombo cha kupima masafa yaliyosafiriwa.

odour;(US)odor n 1 harufu, (pleasant) manukato; (unpleasant) uvundo; (of body) gugumu; (of perspiration under armpits) kikwapa, kutuzi. 2 sifa, upendeleo. be in good/bad ~ with pendelewa/topendelewa na. ~less adj sio harufu. odoriferous adj -a kunukia; -a manukato. odorous adj (poet) -a kunukia.

odyssey n safari ndefu (yenye matukio mengi).

oecumenical adj see ecumenical.

Oedipus complex n (psych) (dhana ya) mapenzi ya binti kwa baba/mtoto wa kiume kwa mama yaliyofungamana na chuki ya binti kwa mama/mtoto wa kiume kwa baba.

o'er adv see over.

oesophagus n see esophagus.

of prep 1 (indicating separation in space or time) kutoka, kutokea. 2 (indicating origin, authorship) -wa; ya/za. 3 (indicating cause) kutokana na, ya, wa. 4 (indicating relief, riddance) na. 5 (indicating material or substance) ya.

off1 adj 1 (of horses, vehicles) -a upande wa kulia the ~front wheel gurudumu la mbele upande wa kulia the ~ horse (of a pair) farasi aliye upande wa kulia. 2 -lio mbali zaidi. 3 -sio fanya kazi; -enye shughuli kidogo tu. ~ hours saa baada ya kazi maalum.

off2 adverbial particle 1 (distance) mbali the University is seven miles ~ Chuo Kikuu kiko umbali wa

off

maili saba; (time) muda the general elections are not far ~ uchaguzi mkuu hauko mbali; (departure) kuondoka he's ~ ameondoka ~we go, tunaondoka take your hat ~! ondoa kofia yako hiyo!. 2 vunjika, tofanyika! the meeting is ~/broken~, mkutano umevunjika/umevunjwa the debate over language policy is ~ mjadala juu ya sera ya lugha hautafanyika. 3 katika the water/gas/electricity is ~ maji/gasi/umeme umekatika. 4 -a mapumziko the workers were given a day ~, wafanyakazi walipewa siku moja ya mapumziko. 5 (of food) -liochacha. 6 (in a theatre) -a nyuma au kando ya/pembeni mwa jukwaa. 7 (phrases) ~ of; (US) ~ (prep). on and ~; ~ and on, mara chache he comes here on and ~ huja hapa mara chache. right/straight ~ mara moja.

off3 prep 1 toka, puuza fall ~ a tree anguka toka mtini the car rolled ~ the slope gari lilibingirika kwenye mteremko cut another piece ~ the material toa kipande kingine kwenye kitambaa cut ~ the price punguza bei. 2 (of a road or street) mchepuo, liochepuka. 3 nje kidogo a building ~ the swamp area jengo karibu na kinamasi an island ~ the coast kisiwa nje kidogo ya pwani. 4 (colloq) acha (tabia fulani) he is ~ drinking) ameacha tabia ya ulevi. ~ish adj (colloq) -liojitenga (na shughuli za wengine). ~-licence n liseni ya kuuza vileo vya kuchukua na kunywea kwingine; stoo/duka (linalouza vileo). ~-load vt teremsha mizigo. ~-print n lopoo: nakala (ya makala iliyo chapishwa katika kitabu, jarida). ~-hand adv bila maandalio; bila kufikiri; kwa haraka, mara moja adj -sioandalia be ~-hand with somebody -tomjali mtu sana. ~-handed(ly) adj,adv (of behaviour) -a kukatiza; bila kujali.

off4 pref (compounds) ~-beat adj (colloq) si -a kawaida, tofauti. ~-day

offer

n (colloq) siku mbaya.

offal n 1 matumbo/viungo vya ndani

vya mnyama. 2 takataka

offence;offense n 1 an ~ against kosa, dhambi, hatia; kuvunja sheria an ~ against the law uvunjaji wa sheria be convicted of an ~ onekana na kosa. capital ~ n kosa lenye adhabu ya kifo. 2 uchungu, chuki. give/cause ~ (to somebody) chukiza (mtu). take ~ (at something) chukizwa (na mtu). no ~! niwie radhi. 3 mashambulizi weapons of ~ silaha za kushambulia. 4 kitu kinachoudhi/ chukiza/kera. ~less adj. offend vi,vt 1 offend against kosa; kosea. 2 chukiza, udhi; tia uchungu. 3 kasirisha, udhi. offender n mkosaji, mhalifu.offensive adj 1 -a kuchokoza; -a kuchukiza; -baya. offensive odour n harufu mbaya offensive to the morals of the community -a kuvunja murua wa jamii offensive words matusi, maneno ya kuchukiza. 2 -a kukasirisha. 3 (attacking) -a kushambulia, -a shari, -a kutaka vita offensive weapon silaha ya kudhuru. n shambulio, mashambulizi. take the offensive anzisha/leta vita/ mashambulizi. peace offensive n kampeni ya kuleta amani. offensively adv. offensiveness n.

offer vt,vi 1 ~ something to somebody; ~ somebody something; ~ something for something toa; tolea, ahidi. ~ battle -pa adui nafasi ya kupigana. ~ one's hand toa mkono ili kusabahiana. ~ one's hand in marriage posa. 2 ~ (to) onyesha ~ no resistance toonyesha upinzani. 3 tukia; tokea. as occasion ~s nafasi inapotokea. n 1 ahadi (ya kufanya jambo/kutoa kitu) an ~ of marriage posa. 2 bei inayotolewa. goods on ~ bidhaa ziuzwazo. be open to an ~ wa tayari kupatana bei. ~ing n 1 kutoa the ~ing of bribes kutoa

office

hongo. 2 sadaka. 3 kitu kitolewacho peace ~ing kitu kinachotolewa kurudisha maelewano baada ya ugomvi. ~tory n sadaka (zinazotolewa kanisani).

office n 1 ofisi. ~-block n jengo (kubwa) la ofisi. ~-boy n tarishi. 2 Wizara; Idara planning ~ Idara ya mipango the Foreign ~ Wizara ya Mambo ya Nje. 3 madaraka; cheo ~ bearer n mtu mwenye madaraka/cheo fulani. 4 wajibu. 5 fadhila; huduma; msaada perform the last ~ for zika, toa heshima za mwisho. ~r n 1 ofisa assessing ~r mthamini public ~r ofisa wa serikali superior ~r ofisa wa juu police ~r afisa wa polisi prison ~r ofisa wa jela. 2 (in the army/police) afande. 3 mtu mwenye madaraka ~rs of a society viongozi wa chama. official adj 1 -a serikali, -enye madaraka rasmi. official liquidator n mfunga hesabu rasmi. official receiver n mpokezi rasmi. official secrets n siri za serikali. 2 (formal) -a kawaida, -a taratibu. n ofisa. officially adv kwa urasimu; kwa utaratibu. officialdom n utawala; urasimu. officialese n lugha ya kirasimu. officiate vt officiate (as) (at) 1 fanya kazi ya mtu wa cheo fulani. 2 (rel) salisha; ongoza. officious adj -a kuingilia, -a kujitiatia. officiously adv. officiousness n.

offing n sehemu ya bahari iliyo mbali (lakini inayoonekana) gain an ~ zidi kuwa mbali toka pwani; (fig) karibu. have something in the ~ -wa na kitu kinachoelekea kutokea karibu.

off-scourings n (usu fig) takataka, uchafu; masimbi; machicha.

offset vt fidia; sawazisha. vi chipua. offshoot n chipukizi; (liter or fig) ziada.

off-shore adj 1 -a bara. ~ shore wind n pepo za bara. 2 mbali kidogo na pwani (kwa baharini). 3 off-shore purchases n (US) bidhaa zinunuliwazo na Marekani kutoka

oil

nchi nyingine ili kutoa msaada kwa

nchi nyingine.

off-side adj,adv (football, hockey) -a

kuotea, -nayo otea.

offspring n mtoto; (of bird) kinda.

offstreet n mbali na barabara kuu.

oft adv (in poetry) mara nyingi.

~-times adv (archaic) mara nyingi; mara kwa mara.

often adv 1 mara kwa mara, mara nyingi more ~ (usually) aghalabu, kwa kawaida, kwa desturi many times and ~ mara nyingi. 2 (in phrases) how ~? mara ngapi? as ~ as kila mara. as ~ as not;more ~ than not mara nyingi sana; mara kwa mara; aghalabu. every so ~ mara mojamoja. once too ~ mara moja zaidi; mara ya mwisho.

ogle vi,vt ~(at) tazama kwa matamanio.

ogre n (in fables) zimwi. ~ish adj -a kizimwi. ~ss n zimwi (la kike).

ohm n (elect) omu: kizio cha

nishati.

oho interj aha!

oil n 1 mafuta palm-~ mawese cod-liver ~ mafuta ya samaki. 2 (phrases) burn the midnight ~ soma usiku. pour ~ on the flame(s) kasirisha zaidi; zidisha ugomvi. pour ~ on troubled waters fanya/sema/tuliza (kwa namna ambayo unamaliza ugomvi/hasira). smell of the midnight ~ onekana kwamba umekesha ukisoma. strike ~ pata mafuta (kwa kuchimba); fanikiwa; (fig) tajirika sana. (compounds) ~ bearing adj (tabaka ya jabali) yenye madini ya mafuta. ~ burner n chombo kiendacho kwa mafuta. ~-cake n mashudu. ~-can n kopo la kutilia mafuta. ~-cloth n kitambaa kisichopenyeza maji. ~-colours n rangi za mafuta. ~ field n eneo la visima vya mafuta. ~-fired n (of a furnace) -enye kutumia mafuta kuwaka. ~- palm n mchikichi. ~-paper n karatasi ya

ointment

mafuta. ~-rig n mtambo/mashine ya kuchimbia mafuta. ~-silk n hariri mafuta. ~-skin n kitambaa cha mafuta (kisichopenyeza maji). ~-tanker n meli ya mafuta. ~-well n kisima cha mafuta. vt lainisha kwa mafuta ~ the machine tia mafuta kwenye mashine (ili kuilainisha); (fig) fanya mambo yaende vizuri. ~ (more usu grease) somebody's palm -pa mrungura/ honga. ~ed adj (usu well-~ed) (sl) -liolewa kidogo. ~er n 1 kopo la mafuta. 2 fundi mafuta. 3 meli ya mafuta. ~y adj 1 -enye mafuta. 2 laini. 3 janja. ~iness n also see oleaginous.

ointment n lihamu; dawa ya kuchua.

okapi n okapi : aina ya paa wa Afrika ya kati.

okay (abbr OK) adj, adv (colloq) sawa, -safi. vt kubali/kubalia. n kukubali; kibali I have got my ~ for nimepata kibali cha.

okra n (plant) mbamia, mbinda; (pods) bamia, binda.

old adj 1 -enye umri wa how ~ are you? Una miaka mingapi/umri gani? 2 zee; kongwe. an ~ man n mzee, shaibu. an ~ woman n ajuza; (colloq) mke. ~age n uzee; ukongwe. ~ age pension n pensheni ya uzeeni. ~ and young watu wote, kila mmoja; (of things) -a zamani; kuukuu, liochakaa. 3 -a zamani; -a muda mrefu. in the ~ days zamani. the good ~ days nyakati njema za kale; zama za. ~ boy/girl n mwanafunzi wa zamani wa shule. one of the ~school mtu wa kale, anayeshikilia mambo ya zamani. ~ country n nchi ya zamani (mtu alikohama). the O~ World n Ulaya, Asia na Afrika. ~ soldier n askari wazamani/muda mrefu. ~ guard n mfuasi/shabiki wa zamani/muda mrefu. ~ offender n mhalifu wa muda mrefu. an ~ hand (at something) mtu mwenye ujuzi mwingi (kutokana na kufanya kazi fulani kwa muda mrefu). ~

omega

fashioned adj -liopitwa na wakati, -a kale. ~ hat adj (colloq) -a kale ~ time world -a wakati uliopita. ~ timer n mtu wa siku nyingi;mtu aliyejihusisha na mahali/kitu (fulani) kwa muda mrefu. come the ~ soldier (over somebody) (colloq) dai kuwa na ujuzi mwingi kutokana na kufanya kazi muda mrefu. 4 (worn out) -kuukuu, -liochakaa. 5 (colloq) (used infront of names and addressing people) mzee listen ~ man sikiliza mzee. ~ Harry/ Nick/Scratch Shetani. the ~ man n baba; mume. the ~ woman mke. n 6 (used as intensifier) (sl) sana. a high ~ time wakati mzuri sana (hasa katika starehe). any ~ thing kitu chochote kiwacho. n zamani, kale. in days of ~ siku za zamani. the men of ~ watu wa kale. ~ish adj -a zamanizamani; zeezee. ~en adj (arch, liter) -a zamani, -a kale. in ~en days siku za kale. ~ster n (colloq) (mtu) mzee.

oleaginous adj -a mafuta; -a kuteleza, laini, -enye mafuta.

olfactory adj -a kunusa; -a kuhusu

harufu ~ nerves neva za harufu.

oligarchy n utawala wa serikali ya

wachache. oligarch n mjumbe wa serikali hiyo.

olive n 1 ~ (tree) n mzeituni. wild ~ tree n mchekele ~ grove bustani ya mizeituni; (fruit) zeituni. 2 jani/tawi la mzeituni (alama ya amani). hold the ~-branch -wa tayari kuzungumzia amani adj -a zeituni. ~ oil n mafuta ya zeituni.

Olympic adj -a Olimpiki: Olympic

games michezo ya Olimpiki. Olympiad n kipindi cha miaka minne baina ya Michezo ya Olimpiki. Olympian adj (of manners etc) -zuri kabisa; -a kama Mungu n mmojawapo wa miungu ya Kigiriki.

ombudsman n the O ~ n Mchunguzi

Maalum (anayechunguza malalamiko ya wananchi).

omega n 1 omega: herufi ya mwisho ya

omelet(te)

alfabeti ya Kiyunani. 2 (end) mwisho. alpha and ~ mwanzo na mwisho.

omelet(te) n kimanda, kiwanda sweet ~ andazi la mayai lenye sukari na jam.

omen n ndege, fali; (sign) ishara, dalili good ~ ndege njema, dalili ya bahati njema bad ~ ndege mbaya, kisirani of ill ~ -a ndege mbaya. vt onyesha dalili, -wa ishara ya. ominous adj -a ndege mbaya, -a kisirani; -a kuogofya. ominously adv.

omit vt 1 ~ to do/doing something acha, ruka; kosa, -shindwa do not ~ to do that usiache kufanya hayo. 2 ruka, acha. omission n 1 kitendo cha kuacha; kukosa kufanya, kutotenda; (error). kosa 2 jambo lililoachwa/ lililorukwa.

omnibus n (old use) basi (gari kubwa la abiria) (attrib) makusudi mengi pamoja; jungu kuu an ~ volume vitabu vingi vilivyo katika jalada moja ~ train garimoshi la abiria.

omnipotence n kudura. omnipotent adj -enye kudura the Omnipotent God Mwenyezi Mungu.

Omnipresent adj -enye kupatikana/ kuwa kila mahala.

omniscience n (formal) maarifa/kujua yote. omniscient adj -enye maarifa yote.

omnivorous adj -a kula chochote; (fig) an ~ reader msomaji wa kila kitabu.

on1 adv part 1 (to show progress, activity) come ~ fanyafanya; fanya haraka. work ~ endelea na kazi. and so ~ na kuendelea, na kadhalika. later ~ baadaye. ~ and ~ bila kukoma/kusita. 2 (to show places) kuwa juu ya; kuvaa your hat is not ~ straight hukuvaa sawa kofia. ~ to, prep juu ya. 3 (contrasted with off) the lights are ~ taa zinawaka; endelea kuwepo is water ~? maji yangalipo?, maji yako? 4 (combined with be and have in various meanings) what's ~? kuna nini? have you anything ~ tonight? unafanya chochote leo usiku? be ~

once

about something (colloq) endelea kuzungumzia/kulalamika juu ya jambo. be ~ at somebody (colloq) sumbua, kera, fuatafuata. be ~to somebody/something wasiliana na; jua juu ya be ~ to a criminal wa na habari juu ya mhalifu. be ~ to a good thing shikilia jambo jema, fanikiwa. 5 kwa kuelekea. head ~collision n kugongana uso kwa uso.

on2 prep 1 juu ya, -ni put posters on

the wall bandika mabango/picha ukutani suffer disaster ~ disaster pata makosi juu ya mkosi. 2 (indicating time) ~ Sunday Jumapili let's meet ~ 1st May Tukutane Mei Mosi ~ Fridays kila Ijumaa ~ arrival nitakapofika. ~ time kwa wakati unaotakiwa/ulioahidiwa. 3 (indicating direction) turn one's back ~ somebody tojali mtu, pa kisogo. 4 (indicating charge) put tax ~ cigarettes wekea sigara kodi. 5 (indicatinga proximity) karibu na a town ~ the coast mji karibu ya pwani. 6 kuhusu, juu ya a lecture ~ publications mhadhara juu ya machapisho be keen ~ the law jihusisha mno na sheria. 7 (indicating membership) she is ~ the commission yeye ni mjumbe wa tume. 8 (expressing the basis/reason for something) kwa a book based ~ facts kitabu tokana na matukio halisi. 9 (followed by n or adj) (indicating action, manner, state) ~ business kikazi ~ tour kitalii buy something ~ the cheap (colloq) nunua kwa bei rahisi be ~ fire ungua.

onanism n punyeto; kujamiiana kuliko katishwa.

once adv 1 mara moja Juma came here ~ Juma alikuja hapa mara moja we go to the cinema ~ a week huwa tunakwenda sinema mara moja kwa wiki. ~ more tena, mara nyingine. ~ or twice; ~ and ~ again; ~ in a while mara chache tu. (for) this

oncoming

~; (just) for ~ mara hii tu. 2 hapo kale, hapo nyuma, wakati fulani he ~ lived here, hapo nyuma/wakati fulani aliwahi kuishi hapa. (in story-telling style) ~ upon a time hapo zamani. 3 never~; not ~ hata mara moja he never ~ agrees with us hakubaliani nasi hata mara moja. 4 at ~ mara moja, bila kuchelewa; papo hapo come here at ~ njoo hapa mara moja at ~ he collapsed papo hapo alizirai; wakati huohuo; kwa wakati mmoja don't do many things at ~ usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja. all at ~ ghafla all at ~ I saw him ghafla nilimwona. get/give somebody/something the ~-over (colloq) tupia kitu/mtu macho, pitia.

oncoming adj -nayofuata, -nayokuja. n kuja, kufika.

one adj 1 -moja ~ hundred, mia moja. 2 -a kwanza standard ~ darasa la kwanza book ~ kitabu cha kwanza chapter ~, sura ya kwanza. 3 -moja (fulani) ~ day siku moja fulani, siku moja. 4 sawa they all did it in ~ style wote walifanya mtindo sawa/mmoja. be at ~ (with somebody) -wa na mawazo sawa. It's all ~ (to somebody) -ote sawa, ni mamoja. become ~; be made ~ ungana; oana. 5 (phrases) ~ and all kila mtu. all in ~ (ote) kwa pamoja. ~ or two chache. by ~s and twos mmojammoja people began to leave the meeting in ones and twos watu walianza kuondoka mkutanoni mmojammoja. ~ up (on somebody) -wa na nafuu (zaidi ya mwingine), zidi. number ~ (colloq) (mtu) mwenyewe. he's always thinking of number ~ daima anajifikiria mwenyewe tu indef pron 1 kitu kimoja; mojawapo the big book and the little ~ kitabu kikubwa na kidogo which ~ do you like ni kipi unachokitaka? pick me out some good ~s nichagulie nzuri ~ of my girls mmojawapo wa wasichana wangu; (colloq) -le: I want the red ~ nataka

only

ile nyekundu. 2 person pron fulani. the little ~s watoto. the Holy O~ Mungu. 3 ~ another -an -a they hate ~ another wanachukiana. 4 impers pron mtu she is not ~ to give up easily yeye si mtu wa kukata tamaa kirahisi. 5 (compounds) ~-armed adj -enye mkono mmoja. ~-armed bandit n (colloq) mashini ya kamari inayoendeshwa kwa sarafu. ~eyed adj chongo. ~-horse adj -enye kuvutwa na farasi mmoja; (fig) -siokuwa na vitu vingi, duni. ~-idead adj -lio na wazo moja tu. ~-man adj -enye kufanywa na mtu mmoja tu. ~-sided adj -a upande mmoja; -a upendeleo. ~time adj -a zamani. ~track mind n -enye wazo moja tu. ~way street n njia moja (hairudi). ~self reflex pron mwenyewe one must do it ~self mtu lazima akifanye mwenyewe.

onerous adj -zito, -a kutaabisha; -a kuhitaji jitihada nyingi.~ly adv. ~ness n.

on going adj -enye kuendelea, -enye

kufanyika muda wote.

onion n 1 kitunguu spring, green ~ kitunguu kibichi. 2 (sl) kichwa. be off one's ~ -wa na kichaa. know one's ~s (sl) fahamu kazi yako tokana na uzoefu/tajriba. ~-skin n ganda la kitunguu; karatasi nyepesi,nyembamba na ngumu sana.

online adj -liounganishwa/tawaliwa/ dhibitiwa na kompyuta kuu.

onlooker n mtazamaji the ~ sees most of the game (prov) mtazamaji (ndiye) mfaidi yote.

only adj -a pekee, -a peke ~ child mtoto pekee adv 1 tu, basi he ~ yeye tu he can ~ say 'no' anaweza tu kusema `la' if ~ he would come laiti angekuja. 2 ~ too sana, kabisa. I shall be ~ too glad nitafurahi sana the news proved ~ too true habari zilithibitika kuwa ni kweli kabisa conj ila, lakini, isipokuwa I would do it with pleasure ~ I have no time

onomatopoeia

ningeifanya kwa furaha lakini sina nafasi. ~that isipokuwa, kwamba, ila tu.

onomatopoeia n onomatopia/tanakali sauti: ujenzi wa neno kwa kuiga sauti/mlio wa kitu.

onrush n mmiminiko mkali.

onset n 1 shambulio. 2 mwanzo (wenye nguvu) at the first ~ mwanzoni mwa.

onshore adj, adv -a ufukoni; kuelekea ufukoni.

onslaught n shambulio, mvamio.

onto prep see on.

ontology n ontolojia: idara/nadharia (yametafizikia) inayojishughulisha na asili ya uhai/maisha.

onus n the ~ n daraka, wajibu; mzigo, jukumu ~ of proof dhima ya kuthibitisha the ~ lies with you wajibu wako (kuthibitisha)/kazi kwako (sasa).

onward adj, adv mbele.

oodles n (sl) ~ of wingi, chungu (nzima) ~ of money pesa kibao/ chungu nzima.

oomph n (sl) mvuto, bidii.

ooze n matope, kinamasi. vt,vi vuja, tona, chirizika their courage ~d away uhodari wao ulitoweka kama maji yalivyotiririka. oozy adj 1 -a matope, -a kinamasi. 2 majimaji.

opal n opali: kito chenye rangi ya maziwa na maji. ~escent adj -a opali. ~ine adj -a opali. n kito cheupe kinachobadili rangi.

opaque adj 1 -siopenyeka nuru. 2 -sio metameta. 3 -pumbavu. 4 gumu kuelewa; -enye utata wa maana. opacity n 1 hali ya kutopitisha nuru. 2 utata wa maana. ~ly adv. ~ness n.

op art n sanaa dhahania mauzauza inayotatanisha ya kisasa.

open adj 1 wazi, -eupe the door is open mlango u wazi. ~ eyed adj -enye macho wazi, -lio na makini; -a mshangao. ~-mouthed adj -lafi; -liopigwa bumbuazi, lioduwaa. ~ vowel n irabu wazi. ~ work n

open

nakshi/urembo katika lesi n.k.. 2 -sio zingirwa, -sio ua, -sio na kizuizi. the ~ sea n bahari kuu. an ~ river n mto unaopitika bila kizuizi. 3 siofunikwa, wazi, siokipaa an ~ boat mtumbwi wazi an ~ drain/sewer mtaro in the ~ air nje. ~-air attrib adj -a kufanyika nje an ~-air dance dansi inayochezewa nje. ~ prison n kifungo/ jela ya nje; isiyobanabana. ~ air theatre n uwanja wa nje wa maonyesho; maonyesho ya nje, jengo la tamthilia lisilo na paa. 4 -liochanua; -liosambazwa the flowers were all ~ maua yote yalikuwa yamechanua the papers lay ~ on the floor karatasi zilisambaa kwenye sakafu. with ~ hands kwa moyo mkunjufu, kwa wingi wa fadhila. ~handed adj karimu. ~ hearted adj (m) kweli. with ~ arms kwa upendo/raghba. ~ order adj (of troops) -lioachana sana kwa nafasi; -a watu wote; -a bure, -a wazi an ~ competition mashindano ya watu wote/wazi. the ~door n sera ya biashara bila ushuru, huru; kuruhusu wafanyabiashara wa kigeni nchini. the ~shop n kiwanda ambapo wafanya kazi wanachama na wasio wanachama wana maslahi na utetezi sawa. keep ~ house wa karimu kwa watu wote. 5 -siotolewa uamuzi. ~ ended adj (of a debate etc) wazi, -sio na hatima maalumu. an ~question n swali lisilokuwa na jibu moja/lisilohitaji kukatiwa shauri. an ~ verdict n uamuzi usomshitaki mtu/unaodhihirisha sababu ya kifo bila kusema kama ni cha ajali/makusudi/faradhi n.k.. have/keep an ~ mind (on something) tofikia uamuzi; -wa tayari kupokea mawazo/mashauri mapya n.k. 6 dhahiri an ~ scandal -kashfa dhahiri. an ~ letter n barua inayo chapishwa jaridani. 7 -siolindwa, -siokingwa. be/lay oneself ~ to something kaa bila

open

kujikinga; karibisha. 8 -siohitimishwa, -siofungwa, -siokamilika. 9 (phrases) ~and shut adj wazi, dhahiri shahiri. ~ cast adj -a juu ya ardhi. an ~ cheque n hundi wazi. ~ court n mahakama wazi/hadharani. the ~ season n (fishing and shooting) msimu huru/wa uwindaji/pasipo kuzuiwa. an ~ secret n siri isiyokuwa siri; siri ya wazi. the O~ University Chuo (Kikuu) Huria: chuo kikuu ambapo masomo yanaendeshwa kwa njia ya posta, redio, televisheni n.k.. ~ weather; an ~ winter n majira shwari ya baridi/yasiyo kuwa na barafu nyingi. n the ~ nje. come (out) into the ~ (fig) jitokeza toa wazo/mpango n.k. hadharani adv waziwazi, bila siri; kwa ukweli; kwa watu wote. ~ness n uwazi; unyofu. vt, vi 1 fungua; funguka; funua; funuka ~ the door fungua mlango ~ the pot funua chungu.~ one's eyes shangaa; zinduka. ~ (somebody's) eyes to something fumbua, elewesha. 2 toboa; kata ~a well chimba kisima ~ a road through a forest kata, toboa barabara katikati ya msitu. ~ something up fungua, fungulia, endeleza; tandaza, sambaza; kunjua ~ out a folding mat kunjua/tandaza mkeka. ~ one's mind/heart to somebody toa/tangaza maoni/hisia za mtu. 3 fungua/anzisha rasmi ~ a shop fungua(rasmi) duka ~ a meeting fungua (rasmi) mkutano ~ a project anzisha/zindua mradi. ~ the bidding anza kunadi. ~ fire (at/on) anza kupiga bunduki/risasi. 4 ~ with anza na. 5 ~ out onekana ~er n mfungua, kifungua. ~ing n 1 nafasi wazi there's an ~ing in the treasury kuna nafasi ya kazi hazina. 2 kipenyo; mlango; tundu, ufa. 3 mwanzo; the ~ing of a speech mwanzo wa hotuba. the ~ing night usiku wa kwanza wa kuonyesha. 4 nafasi/uwanja wazi, upenu adj -a kwanza. ~ ing time n saa/wakati wa

operate

kufungua (shughuli).

opera n opera: mchezo wa kuigiza comic ~ opera ya kuchekesha. grand ~ n opera kali (isiyo na mzaha). ~-cloak n koti la usiku (la madaha). ~-glass n darubini ya kutazamia opera. ~-house n jumba la opera. ~tic adj.

operate vt,vi 1 tenda kazi, endesha ~ a machine endesha mashini. 2 (med) ~ (on somebody) (for something) fanyia operesheni, pasua. operating-table/ theatre n meza ya kupasulia. 3 (of an army) fanya maneva. 4 (of a stock broker) nunua na kuuza. operable adj -a kutibika kwa operesheni/kupasuliwa. operation n 1 kufanya kazi, kutenda; utendaji. come into operation tumika; anza kufanya kazi. be in operation tumika; shughulika. 2 kazi, shughuli. 3 (med) upasuaji. operation set n vyombo vya kupasulia. 4 sehemu maalum ya kazi. 5 (math) tendo la kugawa, kuongeza, kuzidisha kutoa n.k., ukokotoaji. binary operation tendo jozi. 6 (mil) (pl) operations n nyendo za vikosi vya jeshi, wakati wa vita/maneva. operation room n chumba cha kudhibiti/kuongoza mambo. 7 (polit) operesheni, kampeni. operational adj 1 -a uendeshaji. operational cost/ expenditure n gharama ya uendeshaji. operational research n uchunguzi wa njia bora za kutumikisha kifaa n.k. 2 -nayo fanya kazi the computer is already operational kompyuta tayari inafanya kazi. operative adj 1 -a kutenda kazi; -a kutumika become operative tenda kazi, anza kutumika this law became operative on 1 April sheria hii ilianza kutumika tarehe moja Aprili. 2 operative words n maneno yenye athari za kisheria; maneno muhimu. 3 -a kupasua. n mfanyakazi, fundi mitambo. operator n 1 mfanyakazi,

operetta

mwendeshaji. 2 (telephone) mpokeaji/mtumaji simu, opereta. 3 (sl) mwerevu, hodari.

operetta n (music) opereta: opera fupi ya kuchekesha.

ophthalmia n ofthalmia: ugonjwa wa macho. ophthalmic adj -a ofthalmia. ophthalmology n ofthalmolojia ophthalmoscope n chombo cha kufanyia uchunguzi wa macho.

opiate n dawa (ya kutuliza) adj -a kutia usingizi. vt tia afyuni.

opine vt ~ that (formal) wa na/toa maoni.

opinion n 1 oni, wazo,dhana. expressed ~ kauli. in my/your ~; in the ~of somebody kwa maoni yangu/yako; ya mtu. act up to one's ~s tumia/ongozwa na maoni yako. a matter of ~ jambo lisilohakika, si yakini, jambo linalojadilika. be of the ~ that dhani, ona. have a good/bad/high/low ~of somebody/ something heshimu/dharau n.k. mtu I am of your ~nakubaliana nawe. 2 maoni, imani, ya kundi ~ of the court maoni ya mahakama. public ~ n maoni ya umma. 3 ushauri/shauri get a lawyer's ~ pata shauri la mwanasheria. ~ated; ~ative adj -lioshikilia maoni yake, -shupavu.

opium n afyuni. ~ den n maskani ya watumiaji/wavutaji afyuni ~ extract afyuni ~ poppy ua la afyuni; (fig) kasumba.

opponent n mshindani, mpinzani adj -enye upinzani, pinzani, -shindani.

opportune adj 1 (of time) -a kufaa, -a wakati maalumu. 2 (of event) -liotokea wakati unaofaa. ~ ly adv. opportunism. n msimamo wa liwezekanalo/kufuata upepo, kuongozwa na matukio katika kuamua jambo la kufanya. opportunist n mfuata upepo, mtu atumiaye matukio halisi katika maamuzi yake; mtu mwenye kuangalia masilahi yake zaidi kuliko haki au uhalali wa jambo. opportunity n nafasi, fursa, wasaa take the opportunity of tumia

option

nafasi ya, tumia fursa.

oppose vt 1 pinga; shindana; kataa. 2

~(against/to) -linganisha; shindanisha. opposite adj 1 opposite (to) mkabala, -a kuelekeana, -a/ -enye kukabili opposite sides pande zilizoelekeana. 2 kinyume. 3 wajina (wa), wa cheo/nafasi sawa (katika kundi jingine). one's opposite number mtu mwenye cheo sawa na chako katika asasi nyingine. opposition n 1 upinzani. be in the opposition -wa pinzani. 2 kuelekeana, kukabiliana; (resistance) upinzani, kupinga, uzuizi, pingamizi.

oppress vt 1 kandamiza; dhulumu; onea. 2 (fig) elemea, songa; taabisha. ~ion n 1 ukandamizaji. 2 (trouble) mateso, kuteseka, kutaabika. ~ive adj 1 -dhalimu, kandamizaji. 2 zito,-a kuelemea,-a kusonga, -a taabu. ~or n dhalimu; mkandamizaji. ~ively adv.

opprobrious adj (formal) -a kuaibisha, -a aibu, -a kufedhehesha. ~ly adv. opprobrium n dharau; aibu, fedheha; haya.

oppugn vt pinga, bishania.

opt vi 1 ~for something chagua, fanya uchaguzi; amua. 2 ~ out of amua kutoshiriki, jitoa.

optic adj -a macho. n jicho. ~als n elimu ya nuru. ~al adj -a macho. ~al illusion n mazingaombwe, madanganyo ya macho, mauzauza ~al instrument ala ya macho (miwani, darubini n.k.). ~ian n mtengenezaji/mwuzaji miwani.

optimism n msimamo wa kutegemea mazuri, kuwa na matumaini mema. optimist n mwenye msimamo wa kutegemea mazuri. optimistic adj. optimistically adv.

optimum n hali ya kufaa kabisa, bora kabisa; upeo adj -enye hali ya kufaa kabisa; -a juu kabisa. optimise; -ze vt fanya kuwa bora kabisa.

option n 1 uchaguzi, hiari, haki ya kutenda the ~ is yours uchaguzi ni

optometer

wako there is no ~ hakuna budi, sharti, hakuna hiari, lazima I have no ~ but to go ni lazima niende imprisonment without the ~ of a fine kifungo bila hiari ya kulipa faini none of the ~s is satisfactory hakuna uchaguzi wa haja, uchaguzi wa aina yoyote hauridhishi. local ~ n haki ya kuamua (jambo) kwa kura. 2 mambo ya kuchaguliwa. leave one's ~s open tojifunga (na jambo). ~al adj. ~ally adv.

optometer n optomita: chombo

kinachopimia macho nguvu ya kuona mbali. optometrist n mpimaji wa macho.

opulence n utajiri, mali; ukwasi. opulent adj. opulently adv.

opus n utungo (wa kitabu, wimbo n.k.). magnum ~ n utungo mkuu wa msanii.

or conj 1 au, ama. ~ else kama sivyo; la sivyo, ama sivyo. whether... ~ whether you come ~ not it's all the same to me uje usije ni mamoja kwangu. 2 ~ so kama hivyo, kitu kama hicho; hivi.

oracle n 1 (ancient Greece) (place)

mizimuni; uaguzi; mwaguzi; jibu la mizimuni. 2 kahini/mwaguzi aliyetoa majibu hayo. 3 mshauri, mtu mwenye busara work the ~ (fig) fanikiwa kwa njia ya sirisiri. oracular adj.

oral adj -a mdomo; -a kinywa; -a kunena; -a maneno, -sioandikwa; simulizi ~ exercises mazoezi ya kusema. ~ literature fasihi simulizi. ~ly adv.

orange n chungwa; (bitter) danzi;

(mandarin) chenza; kangaja; rangi ya machungwa. ~ade n maji ya machungwa ~ -peel n ganda la chungwa. ~ry n shamba la michungwa.

orate vi (joc) hutubu. oration n hotuba rasmi. orator n msemi, msemaji, mhutubu, mwenye ufasaha wa

order

kusema. oratorical adj -a ufasaha wa kusema; -a hotuba. oratory n 1 ufasaha wa kusema/kuhutubu, usemaji. 2 kanisa dogo, kijumba cha kusalia.

orb n 1 tufe (hasa jua, mwezi au moja ya sayari). 2 kitu chenye umbo la tufe; mviringo; duara. 3 (poetic) jicho.

orbit n mzunguko; mzingo ~ of the earth mzingo wa dunia the earth's ~ round the sun mzingo wa dunia kuzunguka jua eye-~ mzingo wa jicho. vt,vi enda kwa mzingo, weka (kitu) katika mwendo wa kuzunguka. ~al adj. ~al velocity n mwendo wa kuliweka tufe kwenye mzingo.

orchard n shamba la/kiunga cha miti ya matunda. ~man n mkulima wa shamba la (miti ya) matunda.

orchestra n 1 (mus) okestra: kundi la watu wapigao muziki pamoja. 2 ~pit n ukumbi wa wapigao muziki kwenye thieta. 3 ~stalls n viti vya mbele katika thieta. ~l adj -a okestra. ~te vt (mus) tunga; panga, tengeneza utaratibu (kwa ajili ya okestra).~tion n.

ordain vt 1 ~that amua; amuru, agiza. 2 fanya kasisi/padri. ordinand n mtaka ukasisi. ordination n 1 utaratibu, mpango. 2 ibada/tendo la kufanya ukasisi/upadre. Sacrament of Ordination Sakramenti ya Upadre. ordinance n 1 amri, agizo, sheria. 2 (rel) ibada.

ordeal n majaribu, mateso go through an ~ pita katika majaribu ~ by fire jaribu la moto trial by ~ hukumu ya majaribu.

order n 1 mpango, taratibu arrange in alphabetical ~ panga kialfabeti. in ~ of kwa kufuata, kwa mpango wa. 2 in ~ sahihi, sawa. in good ~ kwa utaratibu, hali ya utendaji safi my watch is in good working ~ saa yangu inaenda sawasawa the engine is not in good working ~ injini haiendi vizuri. out of ~ bovu. 3

ordinal

amani, utulivu law and ~ sheria na amani. 4 nidhamu, taratibu (za midahalo). call to ~ kumbusha nidhamu. point of ~ swala la utaratibu. be in ~ to do something ruhusiwa. O~! O~! tusikilizane! ~of the day taratibu ya siku/agizo la siku. 5 amri he is under ~ to go alipewa amri ya kwenda. by ~of kwa amri ya. under the ~s of amriwa na, chini ya amri ya. 6 agizo we have received two ~s for ploughs tumepata maagizo mawili ya plau. on ~ imeagizwa. made to ~ (kitu) kilichotengenezwa kwa maagizo (colloq) a tall/large ~ jambo gumu la kutekeleza ~-book n kitabu cha maagizo; vitu vilivyoagizwa your ~ has been sent maagizo yako yamepelekwa. 7 maagizo (ya maandishi) ya kulipa fedha au kuidhinisha kutenda jambo. 8 aina, jinsi, cheo, daraja, tabaka the lower ~ watu wa tabaka ya chini ability of a high ~ uwezo wa juu kabisa. 9 upadri, ukasisi. be in/take (holy) ~ wa padri/kasisi; pewa upadiri/ ukasisi. 10 chama/shirika la watawa The Franciscan ~ Shirika la Wafransiska. 11 kanuni the ~ of prayers kanuni ya sala. 12 (bio) oda. 13 hawala, hundi, hati money ~ hawala ya fedha. 14 madhumuni, kusudi. in ~ that/to makusudi; ili. in ~ to do that ili kufanya hivyo. 15 kibali I have an ~ to see the house nina kibali cha kuangalia nyumba. vt 1 panga. 2 amuru, agiza. 3 (phrases) ~ about amrishaamrisha, peleka huku na kule. ~ away fukuza. ~ back rudisha. ~ing n mpango, mpangilio. ~ly adj 1 kwa mpango, -zuri. 2 makini, -enye adabu, -a amani n askari mtumishi. medical ~ly n msaidizi (katika hospitali ya jeshi). ~liness n.

ordinal adj -a mpango. ~ numbers n

nambari za mpango.

ordinary adj -a kawaida, -a desturi ~ days's work kazi ya kawaida an

orient

~ person mtu wa kawaida. in an ~ way ikiwa mambo ya kawaida. in the ~ way kama kawaida. n 1 kawaida. in ~ a kudumu; mara nyingi, kwa desturi. out of the ~ si -a kawaida, -geni. 2 (rel) askofu. ordinarily adv. ordinariness n.

ordnance n 1 mizinga; zana za vita. 2 (mil) ~ survey n upimaji halisi wa ramani ~ (survey); ~ map ramani ya upimaji halisi wa nchi. ~ corps n kundi linalohusika kutoa/kuagiza vifaa vya jeshi.

ordure n mavi, kinyesi, taka, samadi.

ore n mbale: mawe yenye madini.

organ n 1 ogani: sehemu ya mwili au mmea ifanyayo kazi maalum k.v. mapafu, moyo, mizizi n.k. ~ of speech ogani za matamshi. 2 chombo ~ of public opinion magazeti, redio n.k.. 3 kinanda. ~ blower n mpuliza kinanda. ~ist n mpiga kinanda. ~ic adj 1 -a ogani; -a kiumbe hai. ~ic chemistry n kemia kaboni. 2 -a mfumo, -a sehemu zinazolingana. an ~ic whole n mfumo unaolingana. ~ically adv. organism n kiumbehai, kiumbe cha kikaboni.

organdie n ogandi: kitambaa kama doria au shashi.

organization n 1 mpangilio, utaratibu, mfumo. 2 (association) chama, shirika. organize vt 1 simamia, andaa, ratibu, panga. 2 unda/anzisha chama cha wafanyakazi. organized adj enye mpango/utaratibu highly organized forms of life viumbe hai vyenye mfumo tata organized labour vyombo vya wafanyakazi. organizer n mtungaji; msimamizi; mwandalizi.

orgasm n (sexual) mshindo, mshushio; upeo wa raha ya kujamiiana.

orgy n 1 karamu ya ulafi, ulevi na

uasherati. orgiastic adj -a karamu ya ulafi n.k. 2 (colloq) kiasi kingi mno.

orient adj 1 (of the sun) -a mashariki,

-a matlai; -a thamani. n the ~ nchi

orifice

za Mashariki (k.v. Uchina, Japan n.k.). ~al adj -a mashariki, -a pande za Asia. n mtu wa nchi za mashariki. ~alist n mtaalamu wa mambo ya nchi za mashariki. ~ate vt 1 jenga kuelekea mashariki (kama ni kanisa ili upande wa madhabahu ukabili mashariki). 2 elekeza mahali ~ate oneself fanya uelewe mahali ulipo; elewa mazingira. ~ation n maelekezo ya mazingira.

orifice n tundu; kitundu, kipenyo, mdomo.

origin n 1 asili; chanzo, mwanzo, chimbuko. 2 (ancestry) wazazi, ukoo, jadi, nasaba. 3 (cause) sababu. ~al adj 1 -a asili; -a kwanza. 2 (peculiar) -pya, geni, ajabu. 3 (inventive) bunifu, -enye akili za kubuni. n 1 lugha ya kwanza/asili (ya utungo), mtindo wa kwanza. 2 asili. 3 (of person) mbunifu, mtu wa (mtindo wa) pekee. ~ality n 1 kuwa na akili za kubuni (za kutunga, za kuvumbua). 2 (singularity) ajabu, upya. ~ally adv 1 kwanza; kwa asili. 2 kwa ubunifu, kwa akili za kubuni. ~ vt,vi ~ from/in something; ~ from/with somebody tokana na her novel ~ated from a short story riwaya yake ilitokana na hadithi fupi. ~ator n mwanzilishi; mtungaji; mwenye kubuni; mzushi; mvumbuaji.

oriole n (bio) kiambizi; (golden) ~ n umbia.

orison n (archaic) sala.

ormolu n 1 shaba iliyopakwa rangi kufanana na dhahabu. 2 vyombo vya shaba za dhahabu.

ornament n pambo, madoido. vt pamba, remba, tia madoido. ~al adj -a kupamba, -a urembo. ~ation n 1 kurembwa, kutiwa madoido. 2 pambo, urembo.

ornate adj -a mapambo; -a/ -enye

madoido. ~ly adv. ~ness n.

ornery adj (US colloq) kaidi; -enye hasira.

ornithology n elimundege.

osteopathy

ornithologist n ornithological adj.

orotund adj (formal) 1 -enye majivuno/ kiburi. 2 -enye staha/hadhi.

orphan n yatima, (mwana) mkiwa adj -a yatima. vt fanya yatima. ~age n nyumba ya yatima.

orthodox adj 1 -enye imani kamili/ halisi. 2 sahihi, halisi, barabara. ~y n imani halisi/inayokubalika. matamshi sahihi yaliyokubaliwa.

orthography n tahajia. orthographic adj.

orthop(a)edics n tiba mifupa; orthopediki: utibabu wa kasoro na magonjwa ya mifupa. orthopaedic adj a (kasoro na magonjwa ya) mifupa.

oryx n choroa.

Oscar n (US) zawadi (ya kila mwaka) ya mshindi wa sinema.

oscillate vt,vi 1 pembeza, bembe(z)a; (fig) wayawaya. 2 (elect) bembea. oscillating current n mkondo bembeo. oscillation n mbembeo. oscillator n kibembeo; chombo cha kufanya mibembeo ya umeme. oscillograph n (elect) osilografu: kipima mibembeo. oscilloscope n (elect). osiloskopu, kionyesha mibembeo.

osier n 1 aina ya matete. 2 ufito wa kusukia viti, meza n.k..

osmosis n (phy) osmosisi: mfyonzo, mnyonyo wa uoeve.

osprey n furukombe.

ossify vt,vi fanya/fanyika ngumu kama mfupa; (fig) -tobadilika; fanya kutobadilika. ossification n. osseous adj -a mifupa, -a kama mfupa. ossuary n mahali pa kupokea/hifadhi mifupa ya wafu; pango la mifupa.

ostensible adj 1 -a juu juu, sio kweli/ halisi. 2 liobashiriwa; liotangazwa. ostensibly adv.

ostentation n majivuno, kuonyesha

ufahari, ushaufu. ostentatious adj shaufu, a kujidai/kujishaua. ostentatiously adv.

osteopathy n matibabu (ya magonjwa) kwa kuchezesha mifupa. osteology n

ostler

elimu mifupa (ya watu na wanyama). osteopath n mganga wa mifupa.

ostler n (old use) saisi.

ostracize vt 1 (people) tenganisha, tenga. 2 (ancient Greece) fukuza nchini (kwa miaka 5 hadi 10). ostracism n

ostrich n mbuni.

other adj, pron 1 -ingine. the ~ -a pili. every ~ (alternate) kila -a pili; kila -ingine. on the ~ hand upande mwingine ~ people watu wengine. ~ than zaidi ya, -sipokuwa some ~ day siku nyingine. the ~day juzijuzi. one after the ~; one after an ~ moja baada ya ingine; mfululizo. ~ things being equal kama mambo mengine yote yangekuwa sawa. the ~s -ingine. or ~ fulani someone or ~ mtu fulani. 2 tofauti I do not want her ~than she is simtaki tofauti na alivyo. prep ~ than isipokuwa, ila there's no teacher here ~ than me hakuna mwalimu hapa isipokuwa mimi adv vinginevyo. ~ -worldly adj -enye kuhusu/kufikiria dunia nyingine; -a kutopenda mambo/anasa za dunia. ~ness n utofauti, wingine. ~wise adv 1 vinginevyo he is stubborn but ~wise likeable ni mkaidi vinginevyo hupendeka all his speeches, political and ~wise hotuba zake zote za siasa na vinginevyo. 2 kwa namna, upande mwingine conj la/ama sivyo do it now ~wise you will regret it ifanye sasa ama/la sivyo utajutia.

otiose adj (formal) sio na maana, bila matumizi maalum, siohitajika; sio na kazi.

otoscope n otoskopu: chombo cha

kupimia tundu la sikio

ottoman1 n kiti kirefu (kisicho na mgongo au mkono) chenye matakia.

Ottoman2 n Uturuki; Mturuki adj -a kituruki.

oubliette n gereza la shimoni.

ouch interj aaa! uui!

ought (aux) bidi; paswa, takiwa I ~ to napaswa, imenipasa, imenibidi.

out

ounce n (abbr oz.) 1 wakia. 2 (pharm)

aunsi.

our adj -etu. O ~ Father n Mungu Baba. O ~ lady n Bikira Maria. O ~ Lord n Bwana Wetu (Yesu Kristu). ~s pron, pred adj -etu a friend of ~s rafiki yetu ~s was a lovely garden bustani yetu ilikuwa nzuri it became ~s by purchase tulikipata kwa kununua. ~selves pron sisi wenyewe! did it by ~selves tulifanya sisi wenyewe. We all by ~selves sisi wenyewe (bila msaada); wenyewe (bila kufuatana na mwingine).

oust vt ~ somebody (from) ondosha, toa, fukuza.

out adv part 1 (kwa) nje he is ~ hayumo (nyumbani) we don't go ~ these days hatutoki/hatutembei siku hizi be ~ tokuwepo; (of book in library) tolewa, azimwa; (of a dress) -siotumika siku hizi; (of workers) goma; (be mistaken) kosa I was ~ in my calculations nilikosea katika hesabu zangu you're not very far ~ hujakosea sana; (of cricket) tolewa. 2 toa, toka ~ of the way! simile! habedari! nipishe. ~ with it toa; sema! onyesha!. (in expressions) be ~ and about pata ahueni the book is ~ kitabu kimetoka the chickens are ~ vifaranga vimeanguliwa the roses are ~ mawaridi yamechanua the secret is ~ siri imetoka, imejulikana, imefichuliwa the sun is ~ jua limechomoza. 3 huko (mbali) my cousin is ~ in America ndugu yangu yuko huko Amerika. 4 (indicating exhaustion, extinction)! kuzimika/kwisha the light is ~ taa imezimika the lease is ~ mkataba umekwisha. 5 (indicating completion) kumaliza before the week is ~ kabla wiki haijamalizika. cry one's eyes ~ lia sana (hadi dukuduku linakwisha). ~ and ~ kabisa, kupindukia. ~and away kwa mbali sana she was ~and away the most intelligent aliwazidi wote

outback

akili kwa mbali sana. 6 kwa kutopatikana ~ of print sichopatikana. 7 (in phrases) be ~ for tafuta. ~ to -enye nia, -enye kujaribu/kutarajia. all ~ kwa jitihada zote. 8 ~ of nje ya fish cannot live ~ of water samaki huishi majini tu; (of motive or cause) (ku)tokana na he did it ~ of kindness alifanya kutokana na huruma; (from, among) 5 ~ of 10 failed watano kati ya kumi walishindwa; (by the use of) kutokana na she made a shirt ~ of a kitenge alishona shati kutokana na kitenge; (without) pasipo I'm ~ of money nimeishiwa (pesa) ~of work pasipo na kazi; (origin or source) kutoka/kutokea kwenye. be ~ of it tokaribishwa tokubaliwa, pweke; tohusika. 9 (used as n) the ins and (the) ~s wale walio ndani (ya shughuli fulani) na wasiokuwemo (of details) adj -a nje; towezekana. put the letter in an ~ tray weka barua katika trei ya (vitu vinavyokwenda) nje your request is ~ of question ombi lako haliwezekani. vt (sl or colloq) timua, fukuza.

outback adj, n (e.g. in Australia) porini, mbugani, sehemu za mbali (na miji).

outbalance vt pita, shinda, zidi uzito.

outbid vt piku; shinda katika mnada.

outboard attrib adj -a nje ya chombo (cha majini).

out-bound adj (of a ship) -a kuelekea mbali.

outbrave vt kabili kishujaa.

outbreak n kuzuka (kwa maasi, vita); mlipuko (wa hasira, ugonjwa n.k.). outbuilding n kibanda (zizi, jiko) njeya nyumba kubwa.

outburst n kutoka kwa ghafla (k.m.

hewa katika puto, mvuke n.k); mlipuko (wa hasira); kuangua kicheko.

outcast n, adj mtu aliyetengwa na jamii.

outcaste n, adj (e.g. in India) mtu asiye na tabaka.

outgrow

outclass vt shinda, -wa bora kuliko.

outcome n matokeo what will be the ~ of this? matokeo yake yatakuwa nini?

outcrop n sehemu ya mwamba inayotokeza juu ya ardhi. ~ rock miamba nundu.

outcry n 1 makelele (ya hofu,

ghadhabu, hasira), yowe. 2 makelele (ya kupinga).

outdated adj liopitwa na wakati.

outdistance vt acha nyuma.

outdo vt pita, shinda, zidi fanya vizuri

zaidi he was not to be ~ne alikuwa hakubali kushindwa.

outdoor attrib adj -a nje ~clothes mavazi ya kutokea nje wakati maalum (k.m. wa baridi kali, mvua n.k.). ~s adv, n nje.

outer adj -a nje the ~ man umbo la nje la mtu (wajihi, vazi n.k.). ~most adj -a mbali zaidi (kutoka kati); -a nje/juu kabisa.

outface vt tumbulia macho; thubutu; aibisha.

outfall n mdomo wa mto.

outfield n (usu the ~) (cricket and baseball) sehemu ya uwanja mbali na mpiga mpira. ~er n.

outfight vt shinda katika pambano.

outfit n 1 mavazi (yote yanayohusu shughuli/kusudi maalumu); zana (zote zinazo-husu shughuli fulani). 2 (colloq) kampuni. vt visha; toa/uza mavazi/zana. ~ter n mwuza nguo.

outflank vt zunguka; (outwit) shinda kwa akili.

outflow n mbubujiko (wa maji, gesi n.k.).

outfox vt shinda kwa ujanja (mjanja mwenzake).

outgo n matumizi (ya hela).

outgoing adj 1 -nayotoka/hama,

-nayoondoka ~ tenant mpangaji ahamaye. 2 changamfu. ~s n matumizi.

outgrow vt kua sana (hata nguo hazifai kwa kuwa ndogo); pita (mwingine) kwa kukua upesi; acha katika kukua (desturi mbaya, fikira za utoto); -wa

outgrowth

kubwa kuliko. ~ one's strength kua haraka mno.

outgrowth n 1 matokeo. 2 chipukizi.

out-herod vt ~ Herod shinda. (katika ukatili, ulafi n.k.).

outhouse n banda la uwani; (US) choo ya nje.

outing n matembezi, mandari: go for an ~ enda matembezi.

outlandish adj -a kigeni, -a ajabu. ~ness n.

outlast vt ishi, dumu kuliko.

outlaw n haramia; mhalifu. vt (ban) harimisha; (person) fukuza (kwenye jamii). ~ry n.

outlay n matumizi (kwa ajili ya

shughuli).

outlet n 1 mlango, tundu la kutokea maji/mvuke n.k. 2 (fig) fursa ya kutoa (hisia n.k. kutumia nguvu n.k).

outline 1 mstari wa kuonyesha umbo au mpaka a map in ~ ramani ya mistari. 2 muhtasari. vt 1 chora mstari. 2 eleza kwa muhtasari.

outlive vt ishi dumu kuliko; dumu hata jambo lisahauliwe.

outlook n 1 mandhari. 2 matarajio. 3 mitizamo, msimamo (wa mambo).

outlying adj -a mbali, -a nje (na kiini). outmanoeuvre vt shinda/pita kwa ujanja.

outmarch vt tangulia mbele ya, enda upesi kuliko.

outmatch vt shinda, pita.

outmoded adj -a mtindo wa zamani.

outmost adj see outermost

outnumber vt zidi, -wa -ingi kuliko.

out-of-date adj -liopitwa na wakati, -siotumika tena.

out-of-door(s) adj see outdoor

out-of-the-way adj 1 -isiyo barabarani, outpace v enda haraka zaidi, zidi mwendo.

out-patient n mgonjwa asiyelazwa (hospitalini), mgonjwa wa nje.

outperform v tenda bora kuliko mwingine.

outplay vt (of games etc) shinda, zidi (katika ustadi wa kucheza).

outpoint vt (boxing etc) shinda kwa

outside

pointi.

outpost n 1 (mil) mahali wanapolinda askari mbali na kundi kuu la jeshi. 2 makazi ya mbali, kituo cha mbali.

outpouring n 1 mbubujiko, miminiko. 2 (usu ~s) kutoa dukuduku/mihemko.

output n 1 mazao ya kiwanda, mgodi n.k.; nishati/nguvu inayotolewa; habari zitokazo kwenye kompyuta.

outrage n kitendo kiovu cha ukatili, jeuri, ufisadi an ~ against morals kitendo cha ufisadi kinachopinga kabisa maadili. vt tendea uovu, halifu. ~ous adj 1 -a kufedhehesha; -a kifisadi, -a kikatili. 2 (of price) -a kuruka. ~ously adv.

outrange vt -wa na masafa marefu zaidi.

outrank vt -wa cheo cha juu kuliko, zidi kwa cheo.

outre adj -enye kuvuka mipaka (ya maadili, desturi nk.).

outride vt kimbiza farasi kuliko. ~er n msindikizaji msafara (kwenye farasi, pikipiki n.k.).

outrigger n mrengu, ndubi, parapi.

outrigged adj -enye mrengu.

outright adv 1 (at once) mara, papo hapo; moja kwa moja he killed him ~ alimwua papo hapo. 2 (openly) wazi, dhahiri adj -a wazi.

outrival vt shinda.

outrun vt shinda kwa mbio, tangulia mbele ya; (fig) zidi.

outsail vt safiri (baharini) haraka kuliko.

outsell vt uza kuliko nyingine.

outset n mwanzo. at the ~ mwanzoni. from the ~ toka mwanzo.

outshine vt shinda, pita (kwa uzuri n.k.).

outside n 1 upande wa nje from the ~ kutoka nje on the ~ nje. 2 sura know only the ~ of something fahamu sura tu ya kitu. 3 (limit) upeo; mpaka. at the (very) - sanasana. 4 jalada. 5 (of football etc) wingi ~ left wingi wa kushoto adj 1 -a nje. 2 (of place) -a mwisho.

outsize

3 (work) -a nje ya kiwanda. 4 (of price) -a juu kabisa adv nje; barabarani; mbele ya nyumba prep nje ya. n 1 mtu asiye wa jamii/kundi/ chama; mtu asiyekubaliwa na jamii. 2 (colloq) safihi. 3 (racing) farasi asiyetegemewa kushinda.

outsize adj kubwa sana. n kipimo kikubwa sana (cha nguo).

outskirts n pl kiunga (cha mjini), pembezo, kando.

outsmart vt (colloq) shinda kwa akili; hadaa.

outspan vt,vi fungulia farasi/ng'ombe/ punda katika gari.

outspoken adj -enye kusema yalivyo, bila kuficha an ~ man mtu asiyeogopa kusema ukweli. ~ly adv. ~ness n.

outspread adj -enye kuenea/ kutandazika; -lionyooka.

outstanding adj 1 -liobaki, -liosalia;

-liopo ~ debts madeni yaliyobaki. 2 (prominent) -liojipambanua/jitokeza.

outstation n kituo cha mbali/mbugani.

outstare vt kodolea sana macho (kushinda mwingine).

outstay vt kaa, baki zaidi kuliko muda unaofaa ~ one's welcome kaa mahali muda mrefu mno (hata kuchukiza wenyeji wako).

outstretched adj -lionyooshwa sana

(hasa mikono ya mtu).

outstrip vt shinda, pita, zidi.

outtalk vt hinikiza, shinda katika kuongea/mazungumzo.

outvalue vt -wa -a thamani kubwa kuliko; thaminisha zaidi.

outvie vt shinda (katika mashindano)

~ each other shindana.

outvote vt shinda kwa kura nyingi zaidi.

outwalk vt shinda kwa mwendo. outward adj 1 -a upande wa nje; -a

kuonekana, -a usoni. 2 a kuelekea nje ~ly (also ~s) adv kwa nje, usoni. ~-bound adj (of ship) -enye kuondoka kwenda mbali.

outwear vt,vi 1 dumu zaidi. 2 chakaa;

chakaza mpaka isiwe na thamani

over

tena.

outweigh vt 1 pita kwa uzito (kwa

nguvu). 2 wa na uzito/maana zaidi, shinda (kwa uzito)/maana zaidi.

outwit vt shinda kwa akili.

outwork n boma la mbele. vt shinda

(kwa bidii, wepesi wa kazi).

ouzel n kizamiadagaa.

ova pl of ovum. ovary n ovari.

oval adj -enye umbo la yai.

ovation n makofi ya shangwe, vifijo.

oven n joko, oveni. ~ware n vyombo

vinavyostahimili joto/vinavyotumika jikoni.

over1 prep 1 juu ya spread a mat ~ the floor tandika mkeka juu ya sakafu the sky is ~ our heads mbingu iko juu ya vichwaa vyetu be ~ one's head (colloq) shinda kuelewa. 2 -enye kutawala/ kuongoza, -enye cheo cha juu zaidi Juma is ~me in the office Juma ni kiongozi wangu ofisini. 3 -ote, sehemu zote she has travelled all ~ Africa ametembea Afrika kote. 4 kule, upande mwingine who is ~ there? nani yuko kule (upande mwingine) look ~ the wall angalia upande wa pili wa ukuta ~the way upande wa pili wa barabara. 5 ~ mpaka mwisho wa muda wa, -ote, hadi can you stay ~ Sunday unaweza kukaa Jumapili yote. 6 zaidi ya they worked for ~ 3 hours walifanya kazi kwa zaidi ya saa 3. ~and above zaidi ya (hayo). 7 wakati ule ule (wa shughuli) he went to sleep ~ his work alisinzia wakati akifanya kazi yake. 8 kuhusu we talked ~ his problems tulizungumza kuhusu matatizo yake adv 1 (full, turn) fall ~ angukia turn~ geuka/geuza. roll ~ biringika. 2 (upwards, outwards) boil ~ furumia. 3 (from start to finish) look ~ pitia; angalia toka mwanzo hadi mwisho. think ~ fikiria. 4 tena say it ~ sema. (all) ~ again tena (toka mwanzo). ~ and ~ again tena na tena, mara nyingi. 5 kwa kuvuka/

over

kwenda upande wa pili come ~to our house karibu nyumbani. ~ against (lit) kinyume cha; kwa kukinzana na. 6 nayobaki is there any wine left~? kuna divai iliyobaki? 7 zaidi children of thirteen and ~ watoto wenye miaka kumi na tatu na zaidi. 8 liokwisha; -liofikia mwisho the meeting is ~ mkutano umekwisha. 9 (from one to another) go ~to the enemy jiunga na adui ~to you! kwako! 10 sehemu zote, kote she is famous all ~ Tanzania ni maarufu kote Tanzania pref mno, -a kupita kiasi, liozidi, sana. ~-cook vi,vt ivisha mno. ~-excited adj enye mpwito- mpwito, liohemkwa/sisimka mno. ~-payment n malipo yaliyozidi.

over2 n (cricket) idadi ya mipira inayotupwa mfululizo.

overact vt,vi zidisha mbwembwe (hasa katika kuigiza).

overall adj -a jumla adv kwa jumla. n (pl) ovaroli, bwelasuti.

overarch vt fanya tao juu ya.

overarm adj, adv (cricket etc) -enye/kwa kurusha mkono juu ya bega.

overawe vt tisha, ogofya, fadhaisha;

stahisha mno.

overbalance vt,vi 1 angusha; anguka. 2 pita, zidi (kwa uzito n.k.).

overbear vt shinda; tiisha. ~ing adj

-enye nguvu; -enye kutiisha/ kulazimisha wengine; dhalimu.

overbid vt,vi 1 (at an auction) shinda bei. 2 toa bei zaidi ya thamani ya kitu. 3 (bridge) taja thamani isiyoweza kufikiwa; taja thamani zaidi ya mwenzio. n kushinda bei; kutoa bei ya juu sana; (bridge) kutaja thamani zaidi.

overblown adj 1 (of flowers) -liochanua, wazi kabisa; -lioanza kuharibika. 2 -enye madoido mengi mno, -a kupita kiasi.

overboard adv kutoka kwenye chombo, toka chomboni fall/jump ~ anguka/ruka kutoka kwenye chombo

overdue

throw somebody~ (fig) tupa, telekeza. go ~ (colloq) vutiwa mno na.

overbore; overborne vt see overbear.

overbuild vt jenga (nyumba) nyingi sana, jaza nyumba mno overbuilt area eneo lililojaa nyumba.

overburden vt lemeza, twisha mawazo mazito mno (k.m. huzuni). n udongo wa juu ya ardhi (ambao ni sharti uondolewe ili kufikia mkaa wa mawe).

overcall vt,vi see overbid.

overcapitalize vt kadiria mtaji mkubwa kupita kiasi. overcapitalization n.

overcast adj 1 (of the sky) -liotanda

mawingu the sky is ~ mawingu yametenda angani. 2 (fig) -a huzuni, -a majonzi.

overcharge vt 1 toza fedha nyingi mno, uza ghali mno. (overload) tia -ingi mno n 1 malipo ya kupita kiasi. 2 (elect) chaji kubwa kupita kiasi.

overcloud vt 1 tanda(za) (mawingu). 2 (fig) tia majonzi, huzuni, uzito.

overcoat n koti kubwa la kuvaa juu ya

nguo nyingine.

overcome vt 1 shinda. 2 be ~ with/by dhoofishwa/lemewa/jawa na.

overcrop vt lima mno hadi ardhi inapoteza rutuba.

overcrowd vt songamana songa. overdo vt 1 fanya (kazi) kupita kiasi. 2 (exaggerate) tia chumvi, zidisha. 3 (cooking) ivisha mno.

overdose n kuzidisha kiasi cha dawa kinachohitajiwa. vt -nywa/toa dawa kupita kiasi.

overdraft n ovadrafti: deni katika

akaunti ya benki.

overdraw vt 1 toa, -wekua zaidi (kuliko fedha zilizopo) ~one's account wekua fedha zaidi (kuliko zilizowekwa). 2 (lit) tia chumvi.

overdress vt,vi jionyesha kwa mavazi (zaidi ya inavyopaswa).

overdrive n gia ya mbio (inayoongeza mwendo bila kutumia petroli nyingi).

overdue adj -a kuchelewa, -a kupitiliza muda long ~ -liopitiliza

overeat

muda mrefu.

overeat vt,vi -la kupita kiasi, lafua. over-estimate vi kadiria kupita kiasi, thamini mno, kuza thamani. n kisio la juu.

overfeed vt,vi -la/lisha mno.

overfill vt,vi jaa/jaza mno.

overfishing n tabia ya kuvua samaki wengi kuliko kiasi hata kupunguza idadi yao mtoni, ziwani, baharini n.k.

overflow vt,vi 1 furika the toilet is ~ing choo kimefurika. 2 ~ with -jaa, jawa na the mother was ~ing with happiness mama alikuwa amejawa na furaha. n 1 mafuriko. 2 (superfluity) ziada. 3 (outlet) mahali pa kutokeza maji.

overgrown adj 1 -liokua upesi mno. 2 -liofunikwa kwa majani au miti. overgrowth n 1 kukua upesi mno. 2 majani/mimea iliyoota sana na kufunika ardhi.

overhang vt,vi 1 tokeza juu ya. 2 elekea/tishia kutokea. n sehemu inayotokeza.

overhaul vt 1 chunguza kwa makini (na kutengeneza ikibidi); (of engine) suka upya; (colloq) go to the doctor to be ~ed enda kwa daktari kwa uchunguzi (kuhusu afya).

overhead adv juu (ya kichwa) adj 1 -a juu (ya kichwa). 2 (of business) -a uendeshaji; (expenses/charges) gharama za uendeshaji k.v. kodi, ushuru, mishahara n.k..

overhear vt sikia bila kukusudia; (deliberately) dukiza.

overheat vt,vi pata/pasha joto kupita

kiasi chake.

overjoyed adj -a kufurahi mno, -liojaa furaha.

overkill n uwezo wa kuharibu/kuua n.k. uliozidi kiasi.

overland adv kwa nchi kavu adj -a

nchi kavu.

overlap vt,vi 1 pishanisha; pishana. 2 (fig) lingana kwa mambo mengine. n kitu kilicho juu ya; sehemu zinazolingana.

overlay vt tia/weka juu ya, funika,

override

tandaza. ~ something with something funika kitu na kitu kingine. n kifuniko.

overleaf adv upande wa nyuma/pili wa (karatasi n.k.).

overleap vt,vi rukia upande wa pili;

(fig) enda mbali, jaribu kupita kiasi, zidi.

overload vt jaza mno, pakia (gari n.k.) kuzidi kiasi; (elect) tia chaji nyingi zaidi.

overlook vt 1. tazama kutoka juu; -wa juu ya. 2 togundua; toangalia; totilia maanani. 3 samehe. 4 simamia.

overlord n (old) kabaila.

overly adv mno, kwa kuzidi kiasi.

overmantel n rafu za mapambo (juu ya meko).

overmaster vt tawala kabisa; shinda.

overmuch adj -ingi mno adv kwa wingi mno.

overnight adv 1 usiku kucha adj -a

usiku. 2 (fig) -a ghafla sana.

overpass n tambukabaraste.

overpay vt lipa mno. ~ment n. overplus n baki; ziada.

over-populated adj lio na watu wengi mno. overpopulation n.

overpower vt shinda (kwa nguvu nyingi); tiisha. ~ing adj -lioshinda kwa nguvu, -enye nguvu nyingi an ~ing stink harufu mbaya tena kali sana.

overprint vt 1 (photog) chapa kuwa nyeusi kuliko ilivyokusudiwa. 2 chapa nakala nyingi. 3 chapa maandishi juu ya maandishi mengine. n maandishi yaliyogandamizwa.

over-produce n zalisha kupita kiasi. overproduction n.

overrate vt thamini zaidi kuliko inavyostahili.

overreach vt 1 shinda kwa hila, ghilibu, rubuni. 2 ~ oneself jiharibia kwa kutaka kufanya kupita kiasi.

override vt 1 puuza; fanya kinyume; (of a horse, donkey etc) chosha kwa kuendesha.

overrule

overrule vt batilisha, tangua.

overrun vt 1 (mil) tanda nchi/mahali,

(agh na kutia hasara). 2 enea weeds have ~ the whole garden magugu yameenea pote bustanini. 3 pitiliza (muda uliopangwa).

oversea(s) adj -a ng'ambo (ya bahari), -a ughaibuni adv ughaibuni, ng'ambo from ~ toka ng'ambo.

oversee vt simamia. ~r n msimamizi.

oversell vt uza kwa wingi mno (kuliko vitu vilivyoko); (fig) sifia mno; toa madai ya kupindukia.

overset vt,vi pindua, tibua; pinduka, tibuka.

oversexed adj -lio na ashiki kupita kiasi.

overshadow vt 1 tia kivuli juu. 2 (fig) toa maanani.

overshoe n buti inayovaliwa juu ya kiatu cha kawaida.

overshoot vt 1 kosea shabaha (kwa

kupiga juu au mbele zaidi). 2 ~ the mark piga chuku, tia chumvi; zidi. 3 (lit, fig) -enda mbali zaidi.

overshot vt pt,pp of overshoot adj ~wheel n gurudumu lenye kuzungushwa na nguvu maji.

overside adv kwa upande, ubavuni mwa (meli, jahazi, n.k.).

oversight n 1 (error, neglect) (kosa la) kupitiwa na jambo. 2 (supervision) usimamizi, uangalizi.

oversimplify vt rahisisha mno (hadi kupoteza maana). oversimplification n.

oversize adj kubwa kupita kiasi. overskirt n sketi ya juu.

oversleep vi chelewa kuamka, pitiliza usingizi, lala mno.

overspend vt (pt, pp overspent) tumia mapesa mengi au zaidi ya kiasi kilichopangwa.

overspill n kufurika (kwa watu/kitu), kuzidiana ~town mji unaojengwa kupokea watu waliofurika.

overstate vt tia chumvi; piga chuku.

~ment n chuku, kutia chumvi.

overstay vt kaa zaidi ya muda unaotakiwa. ~one's welcome chosha

overwhelm

watu kwa kukaa.

overstep vt vuka/kiuka mipaka (ya

jambo, madaraka n.k.).

overstock vt weka/nunua bidhaa nyingi kuliko inayoweza kuuzwa; weka mifugo zaidi ya unayoweza kulisha. n mizigo (bidhaa n.k.) iliyozidi.

overstrung adj -epesi kusisimuka/ kuhemkwa.

overstuff vt jaza mno (kuliko inavyotakiwa). ~ed adj

oversubscribed adj (fig) -liochangiwa/ ombwa kupindukia.

overt adj -a wazi/hadharani. ~ and

covert charges mashtaka ya wazi na ya kisiri. ~ market n soko mjinga.

overtake vt 1 kuta; pita. 2 pata kwa

ghafla he was ~n by a storm alikumbwa na dhoruba.

overtax vt 1 toza ushuru kupita kiasi. 2 (overstrain) lemea; chosha ~ one's strength jichosha mno.

overthrow vt 1 pindua; angusha ~ a regime angusha serikali. 2 (ruin) angamiza; shinda; vunja. n maangamizi, mapinduzi.

overtime n ovataimu: saa za ziada adv work ~ fanya (kazi ya) ovataimu.

overtone n (pl) (music) alama ya juu ya

noti, kidokezo; (often pl)(fig) vidokezo vya maana halisi.

overtop vt 1 (rise above) inuka juu ya;

nyanyuka. 2 (excel) shinda; pita (kiwango cha kawaida).

overtrump vt piku mapiku.

overture n 1 (music) lele, yaleli. 2 (fig) mwanzo. 3 (often pl) mazungumzo ya awali (kabla ya mjadala).

overturn vt,vi pindua; pinduka,

angusha; anguka. n mpinduko.

overweening adj -a kujivuna; -a kutakabari; -a kinaya.

overweigh vt zidisha uzito wa kawaida. vi shinda kwa uzito. ~t n uzito kupita kiasi cha kawaida/kilicho halali adj 1 (of person) nene sana. 2 liozidi (kwa uzito). ~ted adj liolemewa.

overwhelm vt 1 shinda kabisa,

overwind

angamiza; (of feelings) zidi, jawa na be ~ed with jawa/shindwa na. 2 (overrun) ingia kwa shari/nguvu; funika, gharikisha. 3 (cover) funikiza.

overwind vt jaza mno (saa).

overwork vt,vi fanya/fanzisha kazi ya kupita kiasi, chosha; (fig) tumia mno. n kazi ya kupita kadiri.

overwrought adj 1 -liohamanikana. 2 -liotiwa madoido mengi.

ovulate vi fanya/taga mayai. ovulation n.

ovum n (pl.) ovari. oviduct n mirija ya ova. oviform adj umbo la yai. oviparous adj (zool) -enye kutaga mayai. ovoid n, adj -enye umbo la yai. n kitu chenye umbo la yai.

owe vt,vi 1 ~ somebody something; ~something to somebody; ~for something wiwa; -wa na deni be ~d a debt wia deni, dai he ~s me money namdai, awiwa nami; namwia. 2 (owe to) wajibika, paswa na pasa; -wa na (kitu) kwa sababu ya; -wa haki ya I ~ respect to my father inanipasa kumheshimu baba ~ no thanks to omebody -tomwia mtu shukrani. 3 ~ something to something pata kwa, tokana na I ~ my wealth to my father utajiri wangu unatokana na baba yangu I ~ my succes to hard work mafanikio yangu yanatokana na jitihada zangu. owing adj -enye kudaiwa, -siolipwa bado money is owing by me nawiwa fedha na mtu prep owing to kwa sababu ya it is all owing to you yote ni juu yako/kwa sababu yako owing to the floods the road is impassable kwa sababu ya mafuriko barabara haipitiki.

owl n bundi. ~et n bundi mchanga (kifaranga). ~ish adj kama bundi; nzito/enye busara; -a kujifanya/ kuonekana nzito. ~ishly adv.

own vt,vi 1 miliki. 2 kiri, tambua. 3 ~ up kiri (kwa moyo) adj -enyewe my ~ -angu mimi be (all) on one's ~ -wa peke yake I live on my ~ nakaa peke yangu; -enyewe she can work

ozone

on her ~ anaweza kufanya kazi mwenyewe. be one's ~ man/master jitegemea, wa huru come into one's ~ stahili; onyesha. hold one's own simama kidete, jihami, shikilia yako he made the house his ~ alijifanya yuko kwake. ~ brother/sister ndugu wa mama na baba mmoja. get one's ~ back (colloq) lipa kisasi. ~er n mmilikaji mwenyewe. ~er -driver n dereva mwenyewe. ~er occupied adj -a kukaliwa na mwenyewe. ~erless adj bila mwenyewe. ~ership n umilikaji.

ox n 1 ng'ombe. 2 maksai; ng'ombe wa kufugwa strong as an ~ -enye nguvu nyingi sana. ~bow n 1 nira ya ng'ombe. 2 ziwapinde. ~eye (bot) n mmea wenye maua kama jicho. ~-eyed adj -a macho makubwa kama ya ng'ombe. ~hide n ngozi ya ng'ombe. ~tail n mkia wa ng'ombe.

oxbridge n vyuo vikuu vya Oxford na/ au Cambridge.

oxide n (chem) oksaidi mercuric ~ oksaidi ya zebaki. oxidize vt,vi oksidisha. oxidation n uoksidishaji.

Oxonian adj -a Oxford. n mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford.

oxygen n oksijeni (hewa safi). ~ mask n kifuniko cha oksijeni (cha uso). ~tent n kihema cha oksijeni. ~ate; ~ize vt patia oksijeni.

oyes;oyez interj (maneno ya kunyamazisha watu mahakamani) sikilizeni.

oyster n chaza. ~-bed/bank n mahali ambapo chaza huzaa. ~-knife n kisu cha kufungulia chaza.

oz abbr of ounce.

ozone n (chem) ozoni; (fig) kitu kinachochangamsha; (colloq) hewa safi ya kuburudisha pwani. ~ layer n tabaka ozoni.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.