TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

Q,q herufi ya kumi na saba ya alfabeti katika Kiingereza.

qua conj kama, -kiwa ni, -ilivyo.

quack1 vt 1 lia (kama bata). 2 bwata, payuka. n mlio (wa bata) ~- ~ n bata (jina litumiwalo na watoto).

quack2 n bingwatapeli: mtu ajifanyaye mjuzi/mtaalamu (hasa katika tiba). ~ery n utapeli wa kitaalamu.

quadrangle; quad n 1 pembenne: umbo lenye pande nne na pembe nne k.m. mraba, mstatili. 2 (court) behewa kati ya nyumba; uwanja wenye nyumba pande zote. quadrangular adj.

quadrant n 1 roboduara. 2 chombo cha kupimia pembe za kimo.

quadratic adj 1 -a mraba. 2 (maths) ~ equation n hesabu ya kipawa cha pili.

quadrennial adj -enye kudumu miaka minne, -a miaka minne.

quadrilateral adj -a pembe nne.

quadrillion n 1 (GB) milioni kwa

kipawa cha nne. 2 (US) milioni kwa kipawa cha tano.

quadroon n suriama wa chotara; mtoto wa chotara.

quadruped n mnyama wa miguu minne. ~al adj -a miguu minne.

quadruple adj 1 -a sehemu nne. 2

-enye kukubaliwa na pande nne/watu wanne n mara nne. vt zidisha kwa nne.

quadruplet n mmoja kati ya mapacha wanne (waliozaliwa).

quadruplicate adj -lionakiliwa mara nne. in ~ nakala nne.

quaff(lit) vt, vi gugumia; gugumiza. ~er n.

quagmire n 1 bwawa, kinamasi. 2 be in a ~ kwama.

quail vt ~ (at/before) tetema kwa hofu, jikunyata, nywea.

quaint adj -enye kuvutia, -a kupendeza (kwa uzamani/ugeni wake). ~ly adv.~ness n.

quake vt,vi (of the earth, person, etc)tetemeka ~ with cold tetemeka kwa baridi. n (colloq abbr for)

quantum

earthquake n tetemeko la ardhi.

Quaker n 1 mwanachama wa Jamii ya Marafiki; kundi la Wakristo ambalo halipendelei mikutano rasmi na halipendelei ghasia au vita. 2 kitu kitetemekacho/mtu atetemekaye.

qualify vi,vt 1 ~ somebody to do something stahili; stahilisha, wezesha. ~ for something stahili kuwa na, weza; ruhusu. 2 ~ somebody (for something/to do something/as something) wa na/pata sifa, -wa na uwezo. ~ing test n jaribio la ustahilifu. 3 wekea mipaka; pambanua. 4 (gram) vumisha. 5 ~ somebody as elezea sifia. qualified adj 1 -enye sifa zinazostahili. 2 -enye mipaka. qualifier n 1 sharti. 2 (gram) kivumishi. qualification n 1 sifa (itokanayo na mafunzo, mtihani, n.k.), tabia, uwezo. 2 mipaka, kikwazo, sharti he endorsed the plan without qualification alikubali mpango bila kikwazo. qualificatory adj.

quality n 1 aina; ubora; tabia; jinsi. 2 sifa a person of good ~ mtu mwenye sifa, mtoto wa watu inferior ~ duni, sifa duni. marketable ~ sifa ya kununulika. qualitative adj bora, stahilifu.

qualm n 1 shaka, wasiwasi. 2 kigagazi, kichefuchefu.

quandary n utata, shaka; mshangao.

quantify vt pima/eleza kiasi cha. quantification n. quantitative adj -a kiasi. quantity n 1 sifa ya kitu inayoweza kupimwa k.m. ukubwa, uzito, n.k.. 2 kiasi, idadi, wingi. 3 (often pl) idadi kubwa. 4 an unkown quantity n (maths) alama ionyeshayo idadi isiyofahamika; (fig) mtu/kitu kisichoweza kutabirika. quantity surveyor n mkadiria ujenzi. bill of quantity n bili ya makadirio ya ujenzi.

quantum n 1 kiasi, kinachotakiwa. 2 (Physics) namba za kwanta. ~ theory n nadharia ya kwanta (kwamba katika unururishaji nishati ya elektroni hutolewa kwa kiasi

quarantine

maalumu, wala si mfululizo)

quarantine n karantini. vt weka

karantini.

quarrel n 1 ugomvi, mzozo pick a ~ (with somebody) zusha ugomvi. 2 kisa cha ugomvi. vi ~ (with somebody) (about something) 1 gombana. 2 ~ with -tokubaliana, -toafikiana; lalamikia. ~some adj gomvi. ~someness n ugomvi, ubishi.

quarry1 n 1 windo, mnyama (ndege)

awindwaye become the ~ of -wa mawindo ya.

quarry2 n 1 machimbo. 2 karakana ya mawe. vt chimba, chimbua; vunja mawe n.k.. ~man n mvunja/ mchimba/mpasua mawe.

quart n kwati, kisaga. try to put a ~ into a pint pot (fig) jaribu kufanya jambo lisilowezekana.

quarter n 1 robo: a ~ of century robo karne a ~ of an hour robo saa a ~ of the price robo ya bei. a bad ~ of an hour tukio la muda mfupi lisilopendeza. 2 robo saa a ~ to eight saa mbili kasorobo. 3 kwota: kipindi cha miezi mitatu ambapo kodi na malipo mengine hulipwa. 4 (US) senti ishirini na tano. 5 mguu na tako (la mnyama k.v. ng'ombe n.k.). 6 upande from every ~ toka kila upande/kila mahali nothing will come from this ~ hakuna kitakachotoka huku. 7 mtaa, makazi. industrial ~ n mtaa wa viwanda. married ~s n makazi ya watu waliooa (hasa ya wanajeshi) take up ~s pangisha. 8 robo ya mwezi. 9 at close ~s karibu, karibu sana. 10 nafasi (hasa wakati wa kupigana) ask for ~ omba msamaha/huruma. give ~ samehe, hurumia. 11 (compounds) ~ binding n jalada la ngozi nyembamba. ~day n (of payments) siku ya robo mwaka. ~-deck n (naut) shetri, sitaha ya nyuma. ~final n robo fainali. ~ light n kidirisha cha gari. vt 1 gawa sehemu nne. 2 (ml) tafutia malazi. ~master n 1 (of a ship) serehangi;

queer

baharia msimamizi. 2 (army) ugavi. ~ master general n Afisa Ugavi Mkuu. ~staff n gongo. ~ly adj -a mara nne kila mwaka, -a kila mwezi wa tatu adv kwa kila mwezi wa tatu.

quartet n (muziki wa) waimbaji/ wapigaji wanne.

quarto n 1 kwato. ~ size n ukubwa wa kwato. 2 kitabu chenye kurasa kadiri ya urefu wa inchi 12 na upana wa inchi 9.

quartz n kwatzi: namna ya jiwe gumu jeupe la kung'aa. ~ite n

quasar n (astron) mawimbi/mwanga wa radio ya mbali sana.

quash vt 1 tangua, batilisha, tupilia mbali. 2 (suppress) komesha, nyamazisha.

quasi- adj pref (with noun or adj) kwa/ kama kiasi fulani.

quatercentenary n sherehe ya miaka mia nne.

quatrain n (poetry) tarbia, unne; ubeti wa mistari minne.

quaver vi 1 (of voice/sound) tetema, tetemeka. 2 imba/sema kwa sauti ya mtetemo. n sauti ya mtetemo; mtetemeko. ~y adj -a kutetemeka.

quay n gati, liko, diko, kikwezo. ~age n ushuru wa gati.

queasy adj (of food) 1 -a kuchefua moyo, -a kichefuchefu. 2 (of the stomach) -a kuchefuka. 3 (fig) (of person) -enye wasiwasi, oga. 4 (of person) -enye kuchefuka kwa urahisi. queasiness n. quesily adv.

queen n 1 malkia. 2 mke wa mfalme. 3 ~ mother n mame malkia. ~ant/ bee malkia wa mchwa/nyuki. ~bee (fig) n mtu mwenye maringo. beauty ~ n mshindi wa shindano la urembo 4 (sl) rambuza. vt ~ it over somebody tawala kama malkia. ~ly adv kimalkia.

queer adj 1 -geni, -siokuwa -a kawaida. 2 -enye kusababisha wasiwasi. 3 in ~ street (GB sl) -enye shida; -enye madeni. 4 (colloq) -gonjwa kidogo. 5 (derog) -senge; basha. n (derog) (sl) rambuza,

quell

msenge. vt (sl) haribu, potosha. ~ly adv. ~ness n.

quell vt (poet and rhet) zima.

quench vt 1 zima; zimisha (moto). 2 (thirst) kata (kiu). 3 (hope) ondoa, fisha, komesha. 4 poza (chuma) katika maji. ~less adj -siozimika.

quern n kinu (cha mkono) cha kusaga.

querulous adj lalamishi, -gomvi. ~ ness n. ~ly adv.

query n 1 swali. 2 alama ya kuuliza. vt 1 saili, taka maelezo zaidi juu ya jambo. 2 ~ whether/if uliza, dadisi. 3 tia/weka alama ya kuuliza.

quest n kutafuta, uchunguzi. in ~ of -kitafuta, chunguza. vi tafuta, chunguza.

question n 1 swali put a ~ to somebody uliza mtu swali. ~master n mwenyekiti wa jopo la michezo ya maswali na majibu. ~ time n kipindi cha maswali bungeni. ~ mark n alama ya kuuliza. 2 mada, suala. in ~ -nayozungumziwa/jadiliwa. out of the ~ haiwezekani. be some/no etc ~ of -wa/ -tokuwepo na mjadala. come into ~ jadiliwa; -wa muhimu. Q~! swali! hoja! put the ~ itisha/pigisha kura. 3 upingaji (kadamnasi); uonyeshaji wasiwasi. beyond (all)/without ~ bila shaka, dhahiri. call something in ~ saili suala; onyesha wasiwasi juu ya kitu. vt 1 uliza, hoji, saili. 2 ~ (whether/if) (doubt) kuwa na shaka I ~ whether nina shaka kwamba it cannot be ~ed haiwezi kushukiwa. ~ able adj -enye shaka, si hakika; tata. ~ably adv. ~er n msaili. ~ingly adv.

questionnaire n hojaji, kidadisi.

queue n 1 foleni. 2 msururu wa magari. 3 msuko wa nywele (wa mkia). vt ~ (up) (for something) panga foleni; tia shungi.

quibble n kukwepa swala la msingi. vi ~ (over) jadili mambo yasiyo ya msingi (ili kukwepa swala muhimu). ~r n. quibbling adj.

quick adj 1 -epesi, -a haraka a ~

quiet

luncheon mlo mwepesi in ~succession kwa haraka, haraka; upesi be ~ fanya haraka, harakisha; chapuka. (in) ~ time kwa mwendo wa kawaida (wa askari). Q~ March interj (kwa mwendo wa haraka) mbele tembea! ~change actor n mchezaji abadilishaye nguo haraka. ~ freeze vt gandisha (chakula) haraka ili ladha isipotee. 2 hodari, -elekevu, -enye akili ~ at figures -a kipaji cha hesabu. a ~ wit n werevu. 3 (arch) hai, -zima, -enye uhai ~ with child -enye mimba. the ~ and the dead wazima na wafu. n 1 nyama chini ya ngozi (agh. kucha). cut somebody to the ~ choma sana moyoni. ~ly adv upesi, haraka. ~ness n. ~ change adj -liobadilika kwa haraka. ~en vt, vi 1 harakisha, ongeza mwendo. 2 chochea, sisimua; sisimka. 3 (give life to) huisha, fufua; fufuka. 4 (of child in womb) shtuka. ~set adj -a ua wa miti. ~ie n jambo lililofanywa kwa haraka. ~-lime n chokaa isiyolowa maji. ~-lunch/bar n mkahawa, hoteli ya kujihudumia. ~sand n mchanga didimizi. ~ sighted adj -enye macho makali. ~ silver n 1 zebaki. 2 (fig) mabadiliko ya tabia, mwenendo. ~-tempered adj -a hasira fupi. ~-witted adj -erevu.

quid1 n mshuku.

quid2 n (GB sl) pauni ambayo haijavunjwa.

quid pro quo n (Lat) malipizo.

quiescent adj -siojongea, -liotulia; -tulivu, nyamavu. ~ly adv. quiescence n.

quiet adj 1 -siojongea, tulivu. 2 -nyamavu/kimya. be ~ nyamaza! become ~ -wa kimya. 3 (of colours) -siong'aa. 4 -liofichika; -a siri. keep something ~ fanya siri. on the ~ kwa siri. n utulivu, kimya, amani. vt,vi (usually ~en) tulia, nyamaa; tuliza. ~ly adv. ~ness n. ~ism n falsafa ya unyenyekevu; usufii. ~ist

n mnyenyekevu, sufii. ~tude n (lit) utulivu.

quietus n (formal) 1 malipo; stakabadhi. 2 (death) kifo, mauti get one's ~ fariki dunia give somebody his ~ ua.

quiff n bwenzi, sunzu, junju.

quill n 1 (~-feather) unyoya mkubwa

wa mkia. 2 unyoya wa kuandikia. 3 mwiba wa nungu.

quilt n mfarishi. vt tengeneza mfarishi. quin n (colloq abbr of) quintuplet. quince n tunda aina ya pea.

quincentenary n adhimisho la miaka mia tano adj -a miaka mia tano.

quinine n kwinini.

quinquagesima n (rel) Jumapili kabla ya Kwaresima.

quinquennial adj -a kila mwaka wa tano; -enye miaka mitano. n adhimisho la miaka mitano mitano. quinquennium n (pl. quinquennia) kipindi cha miaka mitano.

quinsy n halula.

quintessence n 1 mfano kamili; kiini halisi. 2 sehemu muhimu.

quintet n 1 (mus) sauti tano, waimbaji watano (watu watano wakiimba pamoja). 2 kikundi cha tano.

quintuplet n 1 moja kati ya tano. 2 ~s n watoto watano pacha.

quip n stihizai, kejeli, mzaha. vt kejeli. quire n kitita, fungu la karatasi (za

kuandikia) ishirini na nne zilizokunjwa na kufanya kurasa nane.

quirk n mazoea/tabia fulani pekee ya mtu/kitu; mabadiliko ya ghafla.

quirt n fimbo yenye mkono mfupi ya kuchapa. vt chapa kwa kutumia fimbo.

quisling n kibaraka, msaliti.

quit vt 1 (leave) acha, ondoka, ondosha ~ hold of something achilia kitu. be ~ of ondolewa ~ one's office acha kazi ~ the army acha jeshi. 2 (acquit) achilia. ~ter n aachaye kazi kabla haijamalizika adj -lioachiliwa; lioondokana na we are well ~ of the thief tumeondokana na mwizi huyo.

quite adv 1 kabisa; hasa, kamwe ~

blind yu kipofu kabisa. ~ the thing (colloq) kidhaniwacho/kifikiriwacho kuwa ni sahihi. 2 kwa kiasi fulani ~ a good singer mwimbaji mzuri kiasi. 3 kweli they were all ~ happy kwa hakika wote walifurahi kweli. 4 (indicating agreement/ understanding), sawa, si kitu, sijali.

quits adj -a lipizo sawa (kwa kivita au kwa maudhi). be ~ (with somebody) ridhiana, patana, peana sawa. let's cry ~ tusameheane. call it ~ acha (ugomvi) I will be ~ nitalipa kisasi. quittance n 1 agizo la msamaha, malipo. 2 msamaha (wa deni). 3 hati ya msamaha (wa deni); stakabadhi, risiti.

quiver1 vt,vi tetemeka. n mtetemo.

quiver2 n podo, ziaka. a ~ full of children familia kubwa. have an arrow left in one's ~ -wa na hoja (jambo).

qui vive n (only in) on the ~ -wa macho (na jambo litakalotokea); -wa tayari, -wa na hadhari.

quixotic adj -enye ukarimu (kupita kiasi). ~ally adv.

quiz n jaribio la maswali, chemsha

bongo, fumbo, mtihani mdogo. vt 1 uliza maswali (hasa ya mtihani). 2 (arch) chokoza, dhihaki adj 1 -tani. 2 chokozi. ~ly adv.

quoin n kona ya nje ya nyumba;

pembe ya chumba. vt kaza, inua kona za nyumba.

quoit n pete (duara) ya chuma (ya mchezo).

quondam adj -a zamani, -a siku

zilizopita (lakini si sasa).

quorum n akidi.

quota n sehemu ya haki (iliyopasa);

idadi ya kikomo, kiasi (kilichopasa).

quotation n 1 kidondoa. 2 dondoo. ~-mark(s) n alama za kudondoa (`') au (" ") put words into ~ marks weka maneno katika alama za dondoo. quote vt 1 quote (from) dondoa, tumia maneno ya mtu mwingine. 2 toa maneno kushuhudia. 3 taja. n (colloq)

quoth

dondoo. quotable adj -a kudondoleka. quotability n.

quoth vt (arch) asema; alisema; nasema.

quotidian adj (of fevers) -a kila siku, -a kawaida. n ~ fever homa inayorudia kila siku.

quotient n (maths) hisa.

Quran n see Koran.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.