TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

R,r n 1 herufi ya kumi na nane katika alfabeti ya Kiingereza. 2 the three R's (reading, (w)riting and (a)rithmetic K3 kusoma, kuandika na kuhesabu (kama msingi wa elimu).

rabbi n 1 rabi: mwanasheria (wa sheria za Kiyahudi). 2 mwalimu/bwana: neno la heshima litumiwalo na Wayahudi. 3 kiongozi wa dini ya Kiyahudi. ~nate n 1 ofisi/ muda/kipindi cha urabi. 2 jumuiya yote ya marabi. ~nic(al) adj -a utaalamu wa dini/ sheria za Kiyahudi.

rabbit n 1 sungura. ~-hole/-burrow n shimo la sungura pori. ~-hutch n kijumba cha mbao cha sungura (afugwaye). ~ punch n pigo la ngumi nyuma ya shingo. ~-warren n eneo lililojaa mashimo ya sungura pori. 2 (fig) sehemu ya njia nyembamba na ya kupindapinda. 3 (colloq) mchezaji duni (agh. katika tenisi). vt winda sungura.

rabble1 n 1 msongamano wa watu; umati wenye zogo. 2 the ~ (contemptuous) watu duni, wanyonge na wenye kudharauliwa; akina yahe.

rabble2 n chuma chenye kupinda (upande mmoja) cha kukorogea; chuma kilichoyeyushwa.

rabies n 1 kichaa cha mbwa. rabid adj 1 (of dogs) -enye kichaa. 2 kali sana; -enye hasira iso na urazini go ~ ghadhibika, -wa mkali sana.

race1 n 1 (origin) asili kabisa. 2

(group) jamii. 3 (ancestry) mbari. racial adj 1 -a jamii; -a mbari racial discrimination utenganisho wa kimbari racial segragation ubaguzi wa kimbari. 2 -a ukoo. racialism n 1 ukinzani wa kimbari/kijamii. 2 imani kuwa jamii au mbari ya watu fulani ni bora zaidi kuliko nyingine. racism n ubaguzi wa kimbari.

race2 n 1 shindano la mbio horse ~ shindano la mbio za farasi motor ~ shindano la mbio za magari ~ track uwanja wa mbio. ~-card n ratiba na orodha ya mbio za farasi. ~-course n uwanja wa mashindano ya mbio za

racy

farasi. ~horse n farasi wa mashindano. ~-meeting n siku ya mashindano ya mbio. ~-track n barabara ya mbio. 2 mkondo wa maji wa kasi. 3 (lit) njia ya jua au mwezi; (fig) maisha. vt,vi 1 (with/against somebody) shindana katika mbio. 2 miliki/ shindanisha farasi wa mbio. 3 kimbiza/endesha mtu/kitu kwa mwendo mkali. racing n mashindano ya mbio. ~r n 1 mtu/farasi/baiskeli inayoshiriki katika mashindano ya mbio. 2 mtu, chombo, n.k. chenye mbio sana.

rack1 n 1 uchaga/chanja. 2 shubaka la kuwekea mizigo ndani ya gari/basi. 3 chano cha wanyama. 4 chuma au reli yenye meno ambamo meno ya gurudumu huingia.

rack2 n (usu. the ~) kitanda cha kutesea. be on the ~ (fig) teseka, -wa katika tabu, dhiki, shida kubwa. vt 1 tesa, kwa kutumia kitanda cha kutesea; (of disease or of mental agony) tesa sana he was ~ed with grief aliteseka sana kwa huzuni. 2 ~ one's brains piga bongo, tafakari. 3 nyanyasa (wapangaji nyumba) kwa kuwatoza kodi kubwa. ~ rent n kodi ya kinyonyaji.

rack3 n 1 (lit.) mawingu madogo

yanayopeperushwa. 2 (only in) ~ and ruin angamia.

racket1 n 1 (sing. only) ghasia, makelele,zahama. 2 utapeli, ulaghai (wa kudanganya ili kupata fedha). 3 jaribio. stand the ~ kubali lawama, kubali adhabu yako; shinda jaribio. 4 msukosuko/pilikapilika. vi ~(about) piga kelele; ishi maisha ya pilikapilika. ~eer n laghai, mlanguzi, tapeli. ~eering n.

racket2 n (also racquet) 1 raketi. 2 (pl) mchezo wa (kutumia) raketi. 3 kiatu cha kutembelea juu ya theluji.

raconteur n mtambaji, mweledi wa

masimulizi.

racquet n see racket2.

racy adj 1 (of speech or writing)

changamfu, -enye kusisimua. 2 -enye tabia/sifa za namna yake; -enye kuvutia. ~ of the soil -enye

radar

kuchangamsha; -enye alama za uasili. racily adv. raciness n.

radar n rada: chombo kitumiwacho na marubani kuonyesha vitu kwenye skrini vitu (k.m. ndege, nchi, n.k.) vinavyokaribia eneo lao.

radiate vt 1 nururisha. 2 ~ from

ingia na kutoka katika umbo la miali; onyesha. 3 sambaa kama nusuvipenyo. radiation n mnururisho. radiant adj 1 -enye kupeleka miali ya mwanga; angavu, -a kung'aa, ng'avu. 2 (of person) ng'avu, -enye kuonyesha furaha/ upendo. 3 (Phys) -liosafirishwa kwa miali radiant energy nishati ng'avu. radiance n. radial adj -enye kuhusu miali au nusu kipenyo; -a miali; -liopangwa kama miali au nusu kipenyo. radially adv.

radiator n rejeta.

radical adj 1 -a kiini, -a msingi; -a mzizi. 2 (politics) -a siasa kali. n 1 mtu mwenye siasa kali. 2 (maths) kipeo; (chem) radikali. ~ism n siasa kali. ~ly adv kimsingi; sana, kabisa.

radicle n (bot.) kitungamizizi.

radio1 n 1 redio. 2 simu ya upepo. 3 matangazo ya redio. ~link n matangazo ya redio yanayounganisha sawia watu wa miji tafauti. ~gram; ~gramophone n rediogramu. 4 ~ telescope n darubini inayogundua nyota, sayari, n.k. kwa kutumia mawimbi na mwangi wa redio. ~set n chombo cha kupatia habari (katika meli, ndege n.k.).

radio2 (pref) -a miali, -a radiamu. ~-active adj nururishi, -enye uwezo wa kunururisha. ~-activity n unururifu, chembe alfa au chembe beta za mnururisho. ~graph n picha ya eksirei (miale-X). ~grapher n mtaalamu wa picha za eksirei (miale-X). ~graphy n fani ya upigaji picha za eksirei (miale-X). ~isotope n isotopu (redio). ~location n rada. ~logy n rediolojia: taaluma inayohusu eksirei (miale-X) na radiamu nyingine. ~logist n

rage

mtaalamu wa eksirei (miale-X). ~therapy n tibaredio: matibabu kwa njia ya eksirei. ~therapist n mtaalamu wa tibaredio. ~copy n see ~logy. ~ telephone n simu ya redio. ~ telegraph n simu ya upepo ya redio. ~ telegram n telegramu ya redio.

radish n figili.

radium n radiamu.

radius n nusu kipenyo.

raffia n 1 chane (kama za ukindu). 2 (palm) mwale, mondo.

raffish adj safihi; -siopendelewa na watu; -enye tabia mbaya. ~ly adv.

raffle n bahati nasibu. vt ~something (off) uza (kitu) kwa kutumia bahati nasibu; (pigia) kura kwa fedha.

raft n 1 chelezo. 2 boya. vt,vi safirisha kwa chelezo. ~er; ~sman n mtu anayesafirisha magogo/mbao kwa chelezo.

rafter1 n kombamoyo, pao. ~ed adj

-enye kujengwa kwa kombamoyo/ pao.

rafter2 n see raftsman

rag1 n 1 kitambaa (cha kusafisha). 2 tambara. the ~ trade n (sl) biashara ya kutengeneza na kuuza nguo. 3 kitu kilichochakaa; mabaki ya kitu. ~-bag n mfuko wa matambara; mchanganyiko wa vitu; (sl) mtu aliyevaa ovyo. 4 matambara ya kutengenezea karatasi. 5 (used contemptuously) gazeti. ~amuffin n mtu/mtoto mchafu. ~ged adj 1 (of clothes) -liopasuka, -liotatuka, lioraruka. 2 -sio sawa, -sio kamili. 3 -enye umbo/pande -sio sawa. ~gedness n. ~gedly adv.

rag2 vt, vi tania; dhihaki, piga makelele n (colloq) makelele yenye fujo; sherehe/maandamano yenye makelele na shamrashamra nyingi. ~day n siku ya sherehe ya wanafunzi (agh. mara moja kwa mwaka) yenye lengo la kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasaidia wenye matatizo.

rage n 1 ghadhabu, kiruu, hasira kali.

raglan

be in/fly into a ~ with something kasirikia sana mtu. 2 tamaa, uchu. all the ~ shauku kubwa ya kitu. ~ for kuwa shabiki wa. 3 be (all) the ~ (colloq) tamaniwa sana, shabikiwa sana. vt,vi 1 kasirika sana, ghadhibika, hamaki. 2 (of storm) chafuka, sukasuka. 3 (of disease) endelea vikali, chaga, -wa kali sana.

raglan n kikoti au sweta isiyo na vipindo kwenye mabega. ~ sleeve n mkono shingo.

ragout n mchuzi (wa nyama na mboga za majani).

ragtag n the ~ and bobtail watu hohehahe, makabwela.

ragtime n (in the 1920s) ngoma ya watu weusi Marekani.

raid n 1 shambulio la ghafla la vita.

2 uvamizi wa polisi. 3 shambulio la kupora fedha. vt,vi 1 shambulia. 2 vamia. 3 pora. ~er n mtu, meli, chombo n.k. kifanyacho mashambulio.

rail1 n 1 mti/ubao/chuma ambacho ni sehemu ya ua/uzio. 2 ubao/mti/chuma cha kutundikia vitu; reli go off the ~s (of train) toka relini; (fig) haribika, enda kombo; (colloq) pata wazimu. ~ing n kitalu. ~-car n kiberenge. ~-fence n kitalu. ~-head n mwisho wa reli inayojengwa. ~-road n (US) njia ya reli. vt US 1 safirisha mizigo kwa reli. 2 harakisha mtu kukubali kitu; pitisha hoja kwa haraka. 3 peleka mtu gerezani kwa hila. ~ off/in zungusha/ zunguka kitalu. ~way n reli. 2 mfumo wa reli. ~wayman n mfanyakazi wa reli. ~way-yard n karakana ya reli. ~way-station n stesheni ya garimoshi.

rail2 vi ~(at/against) (lit.) kosoa, karipia, laumu, shutumu. ~ing n ukosoaji.

raillery n (liter) utani.

raiment n (liter) nguo, mavazi.

rain n 1 mvua. long ~s n masika. lesser ~s n vuli. the ~s n mvua za mwaka ~ or shine inyeshe isinyeshe.

raison d'etre

~bow n upinde wa mvua. ~cloud n ghubari. ~coat n koti la mvua. ~ drop n tone la mvua. ~fall n mvua; kiasi cha mvua. ~ forest n msitu wa mvua. ~-gauge n kipimamvua. ~-maker n mgimbi. ~-proof adj -siopenya mvua. ~-shadow n 1 ukame, demani. 2 (fig) ~check tiketi/hundi rubuni; ahadi (ya kufanya tena). ~ vi,vt 1 nya, nyesha. ~ cats and dogs nyesha kwa wingi. 2 ~ something on/ upon toa kwa wingi. 3 tiririka the tears ~ed down her cheek machozi yalim-tiririka. ~y adj -enye mvua nyingi. save/provide/put away/keep something for a ~y day weka akiba kwa siku za shida.

raise n nyongeza (ya mshahara n.k.). vt 1 inua, pandisha, kweza ~ in pay pandisha mshahara. ~ glass to kunywa (kwa afya ya), takia heri. ~ one's hand jongea kama utakaye kumpiga mtu. ~ somebody's hopes pa mtu tumaini. ~ a man to the peerage teua kuwa lodi. ~ the temperature ongeza joto; (fig) ongeza mvutano, ongeza hali ya wasiwasi (kwa kuhamaki, kugomba, n.k.). ~ one's voice paaza/pandisha (sauti). 2 inua, nyanyua. ~ somebody from the dead fufua. 3 sababisha, fanya kutokea. ~ dust/ commotion (sl) sababisha fujo. ~ a laugh fanya kitu cha kuchekesha. ~ cain/hell the devil/the roof (sl) fanya/anzisha fujo. 4 leta mjadala/ dakizo. ~ a new point leta mjadala mpya, dakiza. 5 (crops) otesha, lima; (animals) fuga; (children) lea. 6 (money, loans etc) pata, kopa, kusanya, changa. ~ an army andaa jeshi. ~ funds for changa pesa. 7 ongeza, kuza. ~ an embargo ondoa vikwazo. ~a siege/blockade acha uvamizi. 8 (naut.) ~ land ona nchi kavu.

raisin n zabibu kavu.

raison d'etre n (Fr) sababu (ya kuwepo kwa kitu).

rake

rake1 n reki: zana yenye meno itumiwayo kuokotea taka; chombo kitumikacho kuzolea fedha kutoka meza ya kamari. vt 1 sawazisha, palilia au vunjavunja ardhi (kwa reki). 2 pata/chukua ~ together dead leaves chakura na kukusanya majani yaliyorundikana ~ out the fire toa majivu mekoni. ~ off n (sl) bakshishi, mgawanyo wa faida (usio halali). ~ something in (fig) chuma, pata pesa nyingi. ~ something up fichua; fufua. 3 ~ (over/ through) something tafuta sana katika makaratasi yako habari hiyo muhimu. ~ one's memory jaribu kukumbuka sana. 4 piga kwa bunduki na mizinga kutoka upande mmoja hadi mwingine.

rake2 n kijogoo, mfisadi, mwasherati. rakish adj 1 -a uasherati, zinifu. 2 kichale, -a madaha, kimadaha.

rake3 n (slope) (naut) hanamu, mwinamo. vt vi enda hanamu. rakish adj (of ship) -a mjengeko mzuri/ malidadi na -a kuonekana; -enye kasi.

rally1 vt,vi 1 ungana; unganika; kusanya; kusanyika; anza upya. 2 pata moyo/nguvu; tengenezesha; kusanya tena, rudisha ~ one's wits pata nguvu tena. n 1 (kitendo cha) kujikusanya tena; kupata nguvu upya; kupata afua ya ugonjwa. 2 (in tennis) kurudishiana mapigo ya mpira kwa muda mrefu (kabla ya mmoja kufunga mwenzake). 3 mkusanyiko mkubwa wa watu (hasa uliokusudia kuamsha nguvu mpya). 4 (car) mashindano ya motokaa.

rally2 vt tania.

ram n 1 kondoo dume (asiyehasiwa). 2 mtambo wa kusukumia/kubomolea. 3 (of warship) mdomo wa manowari (uliochongoka na utumiwao kutobolea ubavu wa meli ya adui). vt 1 shindilia, shindika. ~ something down one's throat gongomeza; mwambie jambo mara nyingi mpaka akubali. 2 (of a warship) ponda mbavu, piga kwa nguvu. ~rod n mdeki.

rancid

Ramadan n (rel) Ramadhani: mwezi mtukufu (ambapo Waislamu hufunga).

ramble vt 1 enda kutembea/matembezi; (fig) semasema (bila mpango). 2 (of plants) tambaa. n matembezi, mizunguko go for a ~ enda matembezini, randa. ~r n mtu anayerandaranda; mmea mtambaa. ~r rose n waridi tambaazi. rambling adj 1 (of buildings) siopangwa sawasawa, -liojengwa ovyo, si kwa taratibu. 2 (of speech, essay) -sio na mpangilio mzuri, -enye kuparaganywa paraganywa.

rambunctious adj tundu sana; -enye makelele, -enye fujo; -a maringo/ majivuno.

ramify vi 1 gawanyika katika matawi; zaa matawi. 2 fanya kimia; enea. ramification n kipengee (cha kitu kilicho tata).

ramp1 n 1 mahali penye hanamu, mteremko wa kushukia au kupandia (k.m. hospitalini n.k.). 2 ngazi ya (kushukia au kuingilia) ndege. 3 tuta.

ramp2 n 1 hila ya kupandisha bei. 2 (swindle) madanganyo, ulaghai.

ramp3 vt ~ about (usu joc.) vamia, fanya vurumai; charuka.

rampage n ghasia; ukali. be go/on the ~ fanya ghasia. vi hamaki, ghadhibika. ~ous adj.

rampant adj 1 (of disease, social evils, etc.) -a kuenea pote, -liotapakaa. 2 (of animals) -enye kusimamia miguu ya nyuma tu. 3 (of plants etc.) -a kuenea kwa haraka na majani mengi. rampancy n.

rampart n 1 boma. 2 (fig) ngome; ulinzi.

ramshackle adj -liochakaa, bovubovu;

-a karibu kuvunjika/kuanguka.

ran pt of run.

ranch ranchi: shamba la mifugo, (ng'ombe, kondoo, n.k.). vt fuga wanyama. ~er n.

rancid adj -a mafutaozo, -liooza, kali,

-enye harufu au uonjo wa uozo,

rancour

-liovunda.

rancour n uchungu/machukio/chuki ya muda mrefu sana. rancorous adj.

rand n fedha/sarafu ya Afrika ya Kusini.

random n at ~ bila taratibu maalumu, bila mpango maalumu; kwa kubahatisha adj -sio kuwa na taratibu maalumu, bila kufikiria; -a kubahatisha, -a nasibu, iwezavyo vyovyote.

randy adj 1 -enye ashiki nyingi. 2

(Scot.) -a nguvu, jeuri, -enye makelele ya maudhi. randiness n.

rang pt of ring.

range1 n 1 safu (hasa ya milima); mlolongo wa vitu ~ of mountains safu ya milima. 2 uwanja wa shabaha. 3 mfiko, mtupo (wa risasi ya mzinga, bunduki) out of rifle ~ nje ya mtupo wa risasi ya bunduki at short ~ kwa karibu at long ~ kwa mbali, baidi take the ~ piga shabaha. ~-finder n kitafuta umbali/masafa. 4 umbali ambao mtu anaweza kuona au kusikia, au sauti inakoweza kufika. 5 eneo; kadiri a wide ~ of prices bei anuwai a wide ~ of colours rangi anuwai the annual ~ of temperature kadiri ya vipimo vya joto vya mwaka. 6 (space) nafasi. 7 jiko kubwa (lenye oveni, pleti, n.k.). 8 eneo la kuchungia au uwanda wa kuwindia.

range2 vt,vi 1 (arrange) panga. 2 ~ (through/over) tembea, zunguka, tangatanga, zurura; zungumzia. 3 (extend) fikia, enea. 4 (of guns) fikia umbali/masafa fulani. ~r n 1 mhifadhi, mwangalizi wa hifadhi ya msitu na mbuga za wanyama. 2 (US) askari polisi mpanda farasi. 3 (US) komando.

rank1 n 1 safu (ya watu au vitu). 2 safu ya askari. keep/break the ~ -wa/toka katika msitari. 3 the ~s; the ~ and file; other ~s n askari wa kawaida he has risen from the ~s amepandishwa cheo na kuwa ofisa. be reduced to the ~s fanywa askari

rap

wa kawaida. (US) the ~ing officer n ofisa mwenye cheo cha juu aliyepo. 4 cheo, kiwango, daraja, tabaka high ~ cheo kikubwa, daraja bora he was promoted to the ~ of sergeant alipandishwa cheo cha usajini. pull ~s on somebody tumia cheo/madaraka (juu ya/ kumshinda mtu mwingine). vt,vi 1 weka (katika matabaka, safu, n.k). 2 -wa na cheo, wadhifa, n.k.

rank2 adj 1 (of plants) -enye majani

mengi mno; (of land) -lio na magugu mengi. 2 (strong smelling) -a kuvunda, -a kunuka. 3 baya kabisa, -a kupita kiasi a ~ idler mvivu kabisa a~ liar mwongo sana. ~ly adv. ~ ness n.

rankle vi endelea kuchoma moyo, tia uchungu; kereketa ~ in somebody's mind tia mtu uchungu.

ransack vt 1 ~ something (for something/to do something) pekua, chakura. 2 ~ something (of something) (plunder) nyang'anya, pora.

ransom n fidia/malipo ya kukomboa mateka. hold one to ~ teka mtu na kudai malipo (ili kumwachia huru). worth a king's ~ -enye bei/thamani kubwa sana. vt komboa mtu kwa kulipa fedha.

rant vt jigamba kwa maneno (kana kwamba unaigiza mchezo jukwaani), jitapa. n majitapo/majigambo yenye makelele. ~er n.

rap1 n 1 (of sound) kibao. give somebody a ~ on the knuckles (fig) karipia. 2 (colloq) lawama, madhara. take the ~ (for something) laumiwa; adhibiwa bila sababu. 3 (US) (sl) mazungumzo, majadiliano. vt,vi 1 bisha, gonga, piga kibao, gota. 2 ~ something out sema kwa ghafla au kwa ukali. 3 (US) (sl) zungumza, jadili.

rap2 n not care/give a ~ kutojali kabisa sababu ya zamani isiyo na thamani (phr) I don't care a ~ sijali kabisa.

rapacious

rapacious adj (formal) -enye tamaa

(hasa ya fedha). ~ly adv. rapacity n tamaa ya mali.

rape1 n 1 uporaji. 2 ubakaji. vt pora. 2 baka. rapist n mbakaji. rapine n (liter or rhet) uporaji.

rape2 n rapa (aina ya mimea inayooteshwa kwa ajili ya chakula cha kondoo au nguruwe).

rapid adj 1 -epesi; -a kasi, -a haraka.

2 (of a slope) -a mteremko mkali. n (of river) maporomoko, mkondo wa nguvu. ~ly adv. ~ity n.

rapier n upanga mwembamba.

~-thrust (fig) jibu la mkato.

rapine n see rape1

rapport n maelewano, mapatano. ~ (with) sikilizana na.

rapporteur n mwandishi, katibu (wa

mikutano).

rapprochement n kurejesheana uhusiano/urafiki.

rapscallion n (old use) mhuni.

rapt adj 1 -liozama (katika mawazo,

mazungumzo, furaha n.k). 2 (attention) makini.

rapture n furaha nyingi kupita kiasi. (pl) be in/go into/be sent into ~s (over/about) -wa na furaha sana; -wa na shauku. rapturous adj -enye furaha (kupita kiasi).

rare1 adj 1 (scarce) adimu. 2 zuri mno! -sio na kifani; -siyo ya kawaida. ~ly adv 1 mara chache. 2 vizuri kabisa. ~ness n. rarity n uadimifu; tunu it is a great rarity ni adimu sana.

rare2 adj bichibichi. ~meat n nyama mbichimbichi, -sioiva sana.

rarefy vt,vi 1 punguza, (hewa, gesi, n.k). 2 takasa, chuja.

raring adj (colloq) -liojaa hamu/uchu.

rascal n mhuni. ~ly adv.

rase vt see raze.

rash1 n vipele; ukurutu.

rash2 adj pupa, -tokuwa na subira;

-sio na simile. ~ly adv. ~ness n.

rasher n kipande cha nyama ya nguruwe cha kubanikwa au kukaangwa (au kilichokaushwa kwa chumvi).

rather

rasp vt,vi 1 ~ something (away/off) kwaruza. 2 (irritate) kera, udhi. 3 toa sauti ya bezo n tupa (ya kukwaruzia); sauti ya mkwaruzo.

raspberry n 1 rasiberi: aina ya tunda. 2 (sl) sauti ya bezo give somebody the ~ beza.

rat n 1 panya. 2 ~ (on somebody) msaliti. smell a ~ shuku hila. (look) like a drowned ~ lowa na nyong'onyea. the ~ race n vita vya cheo, hadhi, n.k.. R~s n upuuzi!. vt 1 winda (saka) panya. 2 vunja ahadi, saliti. ~ter n mtu, mbwa au paka akamataye panya. ~ty adj (colloq) -a kuudhi.

ratan n see rattan.

rat-a-tat n see rat-tat.

ratchet n (also ratch) gurudumu la

menomeno. vt fanya menomeno.

rate n 1 birth/marriage/death, etc~ n kiasi, kima kiasi cha uzazi/ndoa/vifo accident ~ n kiasi cha ajali. ~ of exchange n kiasi cha kubadilishana. the discount ~ n kiasi cha kipunguzi. bank ~ n kiasi/kiwango cha riba. 2 mwendo. 3 daraja. 4 at this/that ~ mambo yakiendelea hivyo/kwa kiwango hiki. at any ~ kwa vyovyote vile. 5 (the) ~s n kodi, ushuru (wa serikali za mitaa). ~-payer n mlipa kodi/ushuru. vt 1 ~ (at) kadiria; tathmini; thamini. 2 ~ something (at) tathmini kwa ajili ya kodi. 3 ~ somebody as -pa daraja/cheo. ~able/ratable adj 1 -liostahili kulipiwa kodi. 2 -enye kutathminika; ratability/ ~ability n. rating n 1 kukadiria thamani, kiwango cha kodi (ya ajira, ya cheo). 2 daraja. 3 (navy) baharia.

rather adv 1 (moderately) kidogo, kiasi it is ~ hot kuna joto kiasi! 2 (preferably) afadhali, heri I would ~ die than be a slave afadhali kufa kuliko kuwa mtumwa she ought to have been chosen ~ than Juma. alipaswa kuchaguliwa badala ya Juma I would ~ not nisingependa. 3

ratify

(colloq GB) hakika! kabisa! naam! 4 kwa usahihi zaidi.

ratify vt idhinisha; thibitisha; ridhia (kwa kutia sahihi au kutumia njia nyingine iliyo rasmi). ratification n idhini; uhakikisho, uthibitisho.

ratio n uwiano.

ratiocination mantiki. ratiocinate vi fikiria jambo kwa kutumia mantiki.

ration n 1 posho, mgawo. ~ card n kadi ya mgawo/posho. be on short ~s punguziwa posho/mgawo. vt 1 wekea kiwango cha mgawo. 2 ~ (out) gawa kwa kiwango kilichodhibitiwa.

rational adj 1 razini, -a kirazini. 2

-enye kuweza kufikiri kirazini. 3 -a kimantiki. 4 (maths) -a uwiano ~ expression uonyesho wiano. ~ number n namba wiano. ~ly adv. ~ity n taamuli, busara, mantiki. ~e n urazini, sababu ya msingi. ~ism n falsafa mantiki. ~ist n mrazini. ~istic adj. ~ize vt 1 tazama jambo kimantiki, razini(sha). ~ize ones's fears/behaviour jipa moyo. 2 (of industry etc) panga upya (ili kuzuia ufujaji mali au kuepuka mambo). ~ization n.

rat-line (usu pl.) (also ratlin) n kamba ndogo za ngazi ya kupandia juu na kuteremkia chini merikebuni.

rattan n (also ratan) 1 (of E India) mhenzirani. 2 mkongojo wa henzirani. 3 ~ stems (collectively) chunga ya henzirani.

rat-rat (also rata-tat) n tata: sauti ya

kugonga.

rattle vt,vi 1 chacharisha, lia kama

kayamba; gongagonga the wind ~d the windows upepo uligongesha- gongesha madirisha. 2 ~ away; ~ something off sema, zungumza kwa harakaharaka bila kufikiria au kwa kuonyesha furaha; bwabwaja. n 1 mgongano; mchachariko; mlio wa kugonganisha vitu (agh. chupa). 2 kayamba, manyanga. 3 mazungumzo ya upesi upesi, ubwataji. 4 ~ snake (Am) nyoka atoae sauti ya

raven

kuchacharika kwa mkia wake. 5 (death) ~ n mkoromo wa mtu anayekufa. 6 ~-brain; ~ pate n bozibozi, mjinga; domo kaya. ~-trap n mkweche. ~r n mtu/kitu kinacho- chacharika (hasa agh. nyoka). rattling adj 1 (sl) -a haraka, -a kasi; -a hali ya juu, safi kabisa adv (sl) sana a rattling good speech hotuba safi sana.

raucous adj (of sounds) -a kukwaruza; kali ~ laughter kicheko cha kukwaruza. ~ly adv.

ravage vt,vi 1 teketeza, haribu a house ~d by fire jumba lililoteketezwa kwa moto. 2 (of armies, etc.) angamiza; nyang'anya mali kwa fujo na ghasia. (pl) ~s of n 1 maangamizi, uharibifu. 2 (pl) athari (zinazoleta uharibifu/ madhara) the ~s of heavy rains athari/ madhara ya mvua kubwa. ~r n mwangamizi, mharibifu.

rave vi 1 ~ (at/against/about something) sema kwa hasira, payapaya. 2 ~ about somebody/something sifia sana (bila kufikiri); sema kwa furaha iliyokifu (hata ukaonekana mjinga) (juu ya kitu). 3 ~ it up (sl) -la starehe. ~-up n sherehe ya kusisimua n 1 (colloq) sifa nyingi. 2 (sl) sherehe, safari, dansi ya kusisimua. 3 shauku kuu raving adj -enye kupayuka, -enye kupayapaya adv kiwendawazimu, kichakaramu. ravings n mazungumzo ya kiwendawazimu.

ravel vt,vi 1 (of knitted or woven things) fumua; chambua. ~ out fumua; chambua; tatua. 2 tatanisha; funganisha, sokota; (fig) leta/ sababisha kuchanganyikiwa.

raven1 n mdege mkubwa mweusi (hufanana na kunguru) adj -enye weusi ung'aao. ~ locks n nywele nyeusi.

raven2 vt 1 paparika ovyo kwa kutafuta chakula. 2 lafua. 3 pora. ~ing adj -kali, kinyama (kwenye

ravine

chakula); lafi. ~ous adj 1 -enye njaa kali. 2 -a kulafua, lafi; -enye pupa. ~ously adv.

ravine n korongo.

ravish vt 1 jaza furaha, furahisha. 2 (arch or poet) pora. 3 (arch) najisi; baka. ~ing adj -zuri mno. ~ment n kupendezwa, kufurahishwa.

raw adj 1 bichi, -siopikwa. 2 ghafi ~ materials mali ghafi: vitu vya kufanyizia vitu vingine, k.m. pamba, katani, manyoya, mbata. in the ~ ghafi; -siyosafishwa/tengezwa; (fig) uchi. ~-hide n (-liotengenezwa kwa) ngozi ghafi. 3 (of persons) -sio na ujuzi/uzoefu a ~ recruit askari mpya asiyefundishwa bado, kuruta. 4 (of weather) -enye unyevuunyevu; baridi. 5 (of wounds) bichi, -enye damu; (of a place on the flesh) -liochunika ngozi. ~-boned adj -enye mfupa mkubwa na nyama kidogo; mifupa mitupu. 6 (artistically crude) changa his literary style is still rather ~ mtindo wa maandishi yake bado ni mchanga. 7 (colloq) kali, -onevu. a ~ treatment; ~ deal n uonevu ubichi katika ngozi (agh. ya farasi). touch somebody on the ~ (fig) tonesha, umiza, tonesha hisia za mtu.

ray1 n 1 mwali, mwonzi; (fig) matumaini. not a ~ of hope hakuna matumaini. 2 mstari wowote unaotoka kwenye kitovu cha kitu. vi, vt toa miali.

ray2 n taa: aina ya samaki.

rayon n rayoni: aina ya nguo ya hariri

itengenezwayo kutokana na selulosi.

raze (also rase) vt bomoa; teketeza, haribu kabisa ~ to the ground teketeza.

razor n mashine ya kunyolea. ~ blade n wembe. ~ back n (aina ya) nyangumi. ~edge n 1 makali ya wembe. 2 hali ya hatari. ~ backed adj -enye mgongo mkali.

razzle (also dazzle) n be/go on the ~ (sl) chachawa; enda kustarehe.

re1 prep (in legal style) mintarafu; juu

ya; yahusu.

read

re2 n (mus) noti ya pili.

re3- pref. 1 tena. 2 (fanya) kwa namna nyingine.

reach vt,vi 1 ~ (out) (for) nyosha mkono he ~ed (out) (for) the knife alinyoosha mkono kuchukua kisu; (fig) he ~ed out for help aliomba msaada. 2 chukua, patia please ~that book for me tafadhali nipatie kitabu hicho. 3 fika, nenda hadi ~ Tanga fika Tanga. 4 enea, sambaa, fikia. as far as the eye can ~ kwa upeo wa macho. 5 ~ me-downs n (pl) (sl) mitumba. n 1 (sing) (only) kitendo cha kunyoosha (mkono au kitu); mfiko. 2 uwezo (wa kufikia). within ~ karibu. out of; beyond ~ -siyofikika; nje ya uwezo. 3 mwendeleo (hasa wa mto).

react vi 1 ~ to jibu; onyesha hisia; pokea; furahia ~ed to the article alijibu makala the audience ~ed well to the play hadhira iliufurahia mchezo. 2 ~ on/upon athiri acid ~s on metal asidi huathiri metali. 3 ~ against pinga, kataa, kacha; geukia. ~ion n 1 jibu, mjibizo what was his ~ ion to the news? alizichukuliaje habari hizo. 2 athari. 3 upingaji mabadiliko/maendeleo; hali ya kurudi nyuma. ~ionary adj -a kupinga maendeleo. n mpinga maendeleo/mabadiliko/mageuzi. ~ivate vt fufua. ~or n. nuclear ~ or n tanuri nyuklia; kinu kidhibiti nyuklia; mlundikano wa atomu.

read vt 1 soma ~ a news paper soma gazeti. 2 tamka; soma kwa sauti. 3 soma; jifunza he is ~ing physics anasoma fizikia you had better ~ the subject up inakubidi ujifunze somo hili. 4 fasili/fafanua ~ a dream fasiri/agua ndoto. 5 onekana, toa picha (kama ni zuri) inaposomwa the play ~s better than it acts mchezo ni mzuri zaidi kuusoma kuliko kuuona jukwaani. 6 chukulia kuwa ndivyo; fasili silence mustn't be ~ as consent kimya kisichukuliwe mara zote kama

readdress

makubaliano. ~ into tia chumvi. ~ between the lines tafuta au gundua maana iliyojificha; fasiri. 7 (of instruments) onyesha what does the clock ~ saa inaonyesha ni saa ngapi? 8 bembeleza usingizi kwa kusoma. 9 (pp with an adv) well ~ msomi mno n nafasi iliyotumiwa kwa kusoma ~er n 1 msomaji he is not much of a ~er yeye si msomaji sana. publisher's ~er msomaji/mpitiaji mswada. 2 (GB) profesa mshiriki; kitabu cha kusoma darasani; mfasiri. 3 kitabu cha kiada supplementary ~er kitabu cha ziada he was having a quiet ~er alikuwa anasoma kwa utulivu. ~ership n 1 (GB) uprofesa-mshiriki. 2 (of periodical) wasomaji. ~ing n 1 usomaji. ~ing glasses n miwani ya kusomea. ~ing lamp n taa ya kusomea. ~ing room/library n chumba cha kusomea/ maktaba. 2 maarifa (hasa ya vitabu) a man of wide ~ ing mtu aliyesoma maarifa mengi. 3 kiasi temperature ~ing was 40 degrees centigrade hali ya joto ilikuwa nyuzi 40oC. 4 fasili/ufafanuzi you are ~ing it wrongly unaifasili vibaya. 5 usomaji wa kutumbuiza. play-~ing n ukariri kwa kikundi mchezo ulioandaliwa. 6 (GB parliament) mapitio ya mswada kabla ya kupitishwa. 7 maandishi. (compounds) ~ing book n kitabu cha kujifunzia kusoma; kitabu cha kusoma. ~able adj nayo someka, -enye kusomeka. ~ability n.

readdress vt badili anwani ya barua.

readjust vt rekebisha tena/upya.

~ment n.

ready adj 1 ~ (for something/to do something) tayari (kufanya kitu, kutumika) be ~ to go kuwa tayari kwenda. make ~ tayarisha, andaa. 2 -enye haraka don't be so ~ to rush to conclusions usiharakie kufanya mahitimisho; -epesi. 3 -enye kupatikana kwa urahisi keep your weapon ~ for use weka silaha yako tayari; karibu. ~ money n fedha

realm

(sarafu au noti) iliyotayari kwa matumizi. ~ reckoner n kitabu cha mikokotoo muhimu katika mambo kama biashara. 4 -liokwisha tayarishwa. ~made adj 1 tayari kuvaliwa/kutumika; -a kutungua ~ made clothes nguo zilizo tayari kuvaliwa/nguo za kutungua, ntungulie ~ made answers majibu yaliyokwisha- tayarishwa; majibu ya papo kwa papo. 2 -siyo na upya. readily adv 1 bila kusita, bila wasiwasi. 2 bila shida. readiness n 1 hali ya kuwa tayari. 2 ukubalifu, ikibali. 3 wepesi, haraka.

reaffirm vt hakikishia tena, sisitiza tena, dhihirisha jambo.

reafforest (also reforest) vt panda miti upya, rudisha kuwa msitu. ~ation n.

reagent n (chem) 1 kitendanishi: kitu cha kikemikali kisababishacho au kiletacho utendanaji wa kikemikali. 2 kitu kibainishacho kitu kingine.

real adj 1 halisi ~ life maisha halisi the ~ thing kitu halisi ~ number namba halisi. 2 (leg) ~ property/ estate n mali isiyohamishika. 3 (US colloq as adv) sana I'm ~ sorry nasikitika sana. ~ly adv (kwa) kweli. ~ism n uhalisia. ~ist n. ~istic adj -enye uhalisi; -enye kuwezekana; -a kweli. ~istically adv. ~ity n 1 uhalisi; hakika, hali ya kuwa kweli. in ~ity kwa kweli. 2 ukweli. bring somebody to ~ity fanya (mtu) aone hali halisi; fanya (mtu) aache ndoto.

realize vt 1 elewa, tambua. 2 fanikisha ~ one's hopes fanikisha matumaini. 3 pata (faida, bei). 4 badilisha mali/ hisa kwa fedha. realizable adj -a kupatikana; -a kufanyika; -a kuwezekana it is ~ yaweza kufanyika. realization n 1 utambuzi. 2 matunda, matokeo. 3 kitendo cha kubadilisha mali kwa fedha.

realm n 1 (poet) ufalme, dola the laws of the ~ sheria za dola the persons who are out of the ~ watu walio nje

realtor

ya milki. 2 uwanja, eneo the ~s of poetry uwanja wa ushairi.

realtor n (US) wakala wa shamba.

ream n bunda la karatasi 480 (au 500 kwa Marekani) ~s and ~s ingi sana, chungu nzima.

reanimate vt huisha; (rally) hamasisha.

reap vt vuna; chuma; (obtain) pata, pewa ~ where one has not sown patafaida/sifa kwa kazi ya mwingine. sow the wind and ~ the whirlwind vuna (kibaya) ulichopanda. ~er n mvunaji. ~ing-hook n mundu wa kufyekea. ~ing -machine n mashine ya kuvunia.

reappear vi tokea/tokeza tena. ~ance

n.

reappraisal n tathmini mpya: kitendo cha kukitazama kitu upya na kukifanyia uamuzi. reappraise vt tathmini upya.

rear1 n 1 nyuma. bring up the ~ -wa mwisho take the enemy in the ~ shambulia adui toka nyuma. 2 (colloq) matako. 3 ~ admiral n ofisa wa jeshi la majini chini ya Makamu wa Mkuu wa jeshi la majini. ~ guard n askari walindao nyuma ya jeshi. a ~ guard action n mapigano baina ya jeshi linalorudi nyuma na adui. ~ mirror n kioo cha kutazamia nyuma (katika gari). ~ most adj mwisho kabisa. ~wards adv kwa nyuma, kuelekea nyuma.

rear2 vt 1 lea, fuga. 2 simamisha,

inua. 3 (of horse) simama (kwa miguu ya nyuma). 4 (of a monument) jenga.

rearm vt -pa jeshi silaha tena/upya. ~ament n

rearrange vt panga tena, panga upya. ~ment n.

reason n 1 (intellect) akili; mantiki.

lose one's ~ pata kichaa/wazimu. 2 (ground) sababu, kisa; madhumuni. by ~ of kwa sababu/madhumuni ya. 3 (sense) maana; (truth) kweli; (fairness) haki; (right) adili; urazini. bring somebody to ~ shawishi mtu

rebuff

aache mambo ya kijinga/kipuuzi. it stands to ~ imebainika, ni wazi. do anything within ~ fanya chochote chenye maana (cha kiasi); zindua there is no ~ in what you say usemayo hayana msingi/mashiko. listen to/hear ~ sikiliza ushauri. ~ less adj sio na akili. vi 1 tumia akili, fikiri, waza. 2 ~ with somebody toa sababu/hoja (ili kumshawishi mtu). ~ out fikiri kwa kutumia mantiki. 3 ~ that toa hoja kwamba. 4 jenga hoja. lose all ~ kosa akili kabisa. ~able adj 1 -a akili, -a maana; tayari kusikia hoja. 2 -a kiasi, -a kutosha beyond ~ able doubt bila shaka yoyote ~ able excuse udhuru wa maana. ~ing n hoja; utoaji hoja; (intellectual process) uwazaji wa kimantiki; kufikiri; fikira adj -enye weledi.

reassure vt thibitisha, ondolea shaka/ hofu, -pa moyo, tuliza, poza. reassurance n. reassuring adj. reassuringly adv.

rebate n kipunguo cha bei (kwa sababu ya kulipa fedha tasilimu).

rebel n mwasi. ~lion n uasi, maasi. vt asi, kataa. ~lious adj asi, -kaidi. ~ liousness n. ~liously adv.

rebind vt jalidi upya.

rebirth n 1 (rel) kuzaliwa upya; kuongoka. 2 kufufuka ~ of socialism kufufuka kwa usoshalisti. reborn adj -liookoka.

rebound vi 1 ~ from duta, rudi nyuma; rudishwa nyuma. 2 ~ on/upon rudia his words ~ed on him maneno yake yalimrudia. ~ n tendo la kuduta/kurudi nyuma. on the ~ wakati wa kuduta; (fig) mara baada ya kupata tatizo she married Richard on the ~ (after being rejected by John) aliolewa na Richard baada ya kukataliwa na John.

rebuff vt hakirisha, puuza; kataa kwa dharau. n ukataaji wa kitu kikatili na kwa dharau; kupuuza, kupuuzwa. ~ to hakirisha, dhalilisha. meet with/

rebuild

suffer a ~ pata jibu kali na la dharau.

rebuild vt jenga tena/upya.

rebuke vt ~ somebody (for something) karipia,

kemea; shutumu, laumu. n karipio, kemeo; onyo; lawama. rebukingly adv.

rebus n chemshabongo ya maneno na picha.

rebut vt jibu/pinga hoja; kanusha. ~tal n.

recalcitrant adj kaidi, -siotii amri. n mkaidi, sugu, kiloo. recalcitrance n.

recall vt 1 ~ somebody (from/to) ita tena; rudisha. 2 kumbuka. 3 tangua, batilisha. 4 (poetic) (revive) fufua. n 1 amri ya kurudi. beyond/past ~ -sioweza kurudi, -siofanyika tena; -siyobatilika. 2 (military) alama (filimbi n.k.); mbiu ya kurudi. 3 uwezo wa kukumbuka.

recant vt,vi acha (wazo/imani uliyokuwa nayo); futa maoni yako (kwa kuona kuwa ni makosa). ~ation n.

recap1 vt,vi,n (colloq abbr) recapitulate.

recap2 vt (US) tengeneza tairi iwe mpya; tia tredi upya.

recapitulate vt rudia kwa muhtasari, eleza tena. recapitulation n muhtasari, ufupisho.

recapture vt 1 kamata tena, twaa tena, teka tena. 2 kumbuka (mambo/ uzoefu wa awali).

recast vt 1 mimina katika kalibu tena, subu tena. 2 (alter) fanya vingine, fanya upya. 3 (theatre) badili wachezaji (waliochaguliwa kucheza mchezo fulani). n kufanyiza upya.

recede vi 1 (~ from) rudi nyuma. ~

from view tokomea. 2 -enda hanamu ~ into the background fifia. 3 rejesha nyuma (wazo). 4 pungua (k.m. katika thamani).

receive vt 1 pokea, pata ~ somebody into the Church pokea mtu awe Mkristo ~ a good education pata elimu nzuri ~ a letter pata/pokea

rechauffe

barua. receiving-set n -redio. 2 pokea (wageni, wajumbe n.k.); kubali/ruhusu. ~d adj -liokubaliwa ~ pronounciation matamshi yaliyokubaliwa. receipt n 1 stakabadhi, risiti. 2 kupokea; upokezi. 3 (pl) (income) mapato, uchumi; maduhuli vt andika stakabadhi. ~-book n kitabu cha risiti, kitabu cha stakabadhi. receipt -stamp n muhuri wa stakabadhi. receivable adj -a kupokelewa. ~r n 1 mkono wa simu. 2 mpokeaji Official R~r n Mfilisi. 3 mpokeaji ~r of stolen property mpokeaji wa mali ya wizi. reception n 1 mapokezi; kitendo cha kupokea/ kupokewa. reception desk n sehemu ya mapokezi ya wageni. reception clerk n karani mpokea wageni. receptionist n mpokea wageni. reception room n chumba cha kupokelea wageni/habari. 2 tafrija, karamu. 3 makaribisho, kitendo cha kulaki; mlahaka. 4 upokeaji wa habari za redio; kusikika kwa (habari za) redio. receptor n kipokezi, mpokezi. recipient n mpokeaji; mwenye kupewa/kupata adj -a kupokea/ kupewa/ kupata.

receptacle n 1 chombo cha kuwekea vitu mf. mfuko, kikapu, kasha, n.k. 2 (bot) kikonyo. receptive adj sikivu; -epesi kupokea (mawazo, ushauri, n.k.). receptivity n.

recent adj -pya, -a siku hizi, -a karibuni. ~ly adv.

recess n 1 kipindi cha mapumziko. 2 mafichoni, shubaka, kidaka. vt,vi 1 pumzika. 2 weka nyuma. ~ion n 1 (comm) kupungua/kushuka kwa uchumi/mdororo (wa uchumi). 2 kitendo cha kutoweko; kurudi nyuma.~ional adj -a mapumziko (ya bunge). ~ional n (hymn) wimbo wa mwisho. ~ive adj 1 -a kupungua; -a kurudi nyuma; (bio) -a selipumbazi.

rechauffe n kiporo kilichopashwa

recherche

moto.

recherche adj (of meals) -lotayarishwa kwa uangalifu mno, -a mbwembwe mno.

recidivist n mhalifu sugu. recidivism n.

recipe n 1 mapishi; maelezo ya upishi. ~ book n kitabu cha mapishi; maelekezo ya kufanya jambo. 2 hati ya dawa. 3 mbinu (ya kufanya jambo).

reciprocate vt,vi 1 rudisha, lipa, lipiza (k.m. fadhila, msaada, n.k.). 2 peana, tendeana. 3 (of parts of machine) enda mbele na nyuma. reciprocation n kutendeana sawa sawa. reciprocal adj 1 -a kukubaliana; -a kupeana; -a wao; kwa wao, -a kubadilishana reciprocal affection. n upendanaji reciprocal ~ agreement mapatano ya kukubalina. 2 -a kukubaliana kinyume. 3 (gram) -a kutendana/kutendeana.reciprocally adv. reciprocal n (maths) kinyume katika kuzidisha. reciprocity n kutendana/kutendeana.

recite vt 1 tongoa; ghani. 2 (repeat by heart) kariri (sema kimoyomoyo); soma kwa ghaibu; (narrate) simulia; nena, toa habari ya; (publically) soma mbele ya watu. 3 orodhesha. ~r n. recital n 1 kitendo cha kutongoa; kughani; maonyesho (agh ya muziki). 2 kisa, masimulizi. recitation n 1 utongoaji; kughani; mashairi yanayotongolewa. 2 masimulizi. recitative n (mus) mtindo wa muziki ambao ni mchanganyiko wa kusema na kuimba.

reckless adj -siojali, -zembe ~ fellow mtu wa kujiendea, asiyejali mtu ~ driving kuendesha bila hadhari. ~ ly adv. ~ ness n.

reckon vt,vi 1 hesabu. ~ up jumlisha. ~ something in ingiza katika jumla. 2 ~ on (upon) tegemea. 3 ~ with somebody shughulikia, lipiza; (take into account) zingatia, fikiria. 4 ~ somebody/something as/to be; ~ that dhania; fikiria. ~er n. ~ing n

recommend

1 orodha ya madai (hasa ya hoteli). day of ~ing siku ya kulipa madeni (ya makosa); kiyama. 2 (of ship) kisa.

reclaim vt 1 rudisha katika hali nzuri (k.m. ardhi) the desert was ~ed by hard work jangwa lililimika baada ya kudhibitiwa kwa kazi kubwa. 2 dai kitu fulani kirudishwe. 3 (reform) ongoa, hidi. ~able adj. reclamation n.

recline vi,vt (lean on) tandawaa, jinyoosha.

recluse n mtu peke (ajitengaye na wenzake); sufii adj -enye kuishi peke yake.

recognize vt 1 jua; tambua; fahamu, maizi he ~d the danger of the journey alitambua kuwa safari ilikuwa ya hatari ~ a new government tambua serikali mpya. 2 (acknowledge) ungama; kiri, kubali. recognizably adv. recognition n utambuzi. alter/change beyond/out of (all) recognition badilika kabisa mpaka kutotambulika. recognizable adj -a kutambulika, -a kufahamika, -a kujulikana he is no longer recognizable hatambuliki tena.

recognizance n 1 mdhamana. enter into ~ (mahakani) dhaminiwa. on his/her own ~ kwa udhamini wake mwenyewe. 2 dhamana.

recoil vi 1 ~ (from) rudi nyuma, jivuta nyuma. 2 (of a gun) rejea nyuma baada ya kutoka risasi. 3 (shrink) nywea; ogopa sana; kwepa, kimbia, sita. 4 ~ on/ upon rudi. n kurudi nyuma; kurejea.

recollect vt kumbuka I couldn't ~ him sikumkumbuka. ~ion n 1 kumbu-kumbu within my ~ion kadri ya kumbukumbu zangu it is outside my ~ion sikumbuki. 2 jambo lililokumbukwa have a dim ~ ion of something kumbuka kwa mbali.

recommence vi anza tena.

recommend vt 1 ~ something (to somebody) (for something); ~ somebody; ~somebody (for

recompense

something/as something) pendekeza, sifia. 2 (advise) shauri, nasihi I have been ~ed to take cafenol nimeshauriwa kutumia kafino. 3 pendeza his behaviour does not ~ him tabia yake haimpendezi. 4 ~ somebody to somebody kabidhi mtu kwa mtu. ~able adj. ~ation n 1 sifa. 2 kupendekeza; pendekezo on the ~ation of kwa pendekezo la.

recompense vt jazi. n jaza; fidia.

reconcile vt 1 somebody (with somebody) patanisha; suluhisha. 2 ~ something (with something) linganisha. 3 be ~d to something kubali kuvumilia; ridhi. reconcilable adj. reconciliation n upatanisho, suluhisho; suluhu. reconciliatory adj suluhishi, -a kupatanisha.

recondite adj (of knowledge) adimu;

gumu.

recondition n, vt rekebisha, tengeneza upya (kwa kutia vitu vipya), karabati.

reconnaissance n 1 (mil) upelelezi. ~

party n kikosi cha upelelezi. ~ planes n ndege za upelelezi. 2 uchunguzi/ ukaguzi wa awali.

reconnoitre (US reconnoiter) vt, vi peleleza, jasisi, piga reki.

reconstruct vt jenga tena, tengeneza upya. ~ion n.

record n 1 kumbukumbu, taarifa iliyoandikwa; ushahidi it is on ~ that kuna ushahidi kwamba. put me on ~ as saying that andika kuwa nimesema. off the ~ (colloq) isiandikwe/isichapwe. 2 sahani ya santuri. ~player n santuri gramophone ~ sahani ya santuri. 3 (of games etc.) rekodi. beat/break the ~ vunja rekodi. ~ holder n mshikilia rekodi. 4 sifa a man with a good ~ mtu mwenye sifa nzuri his ~ is against him ana sifa mbaya; sifa yake inamwangusha. ~er n 1 (GB) jaji. 2 kinasa sauti. tape ~er n kinasauti. video tape ~er n video. 3 mwandishi wa kumbukumbu. 4 filimbi. vt 1 andika. 2 (of music etc) rekodi. 3 (of instrument) onyesha.

rectify

~ing n kipindi, muziki, harusi (iliyorekodiwa).

recount1 vt hesabu tena. n kuhesabu

tena (hasa kura ili kuepuka makosa).

recount2 hadithia, simulia.

recoup vt ~ (for) fidia ~ one's losses fidia hasara.

recourse n 1 njia (ya kupata msaada). have ~ to tafuta msaada. 2 msaada; kimbilio.

recover1 vt,vi 1 pata tena (kitu kilichopotea) ~ consciousness pata fahamu tena baada ya kuzimia ~ oneself jikaza. 2 ~ (from) pona, pata nafuu/ashekali/ahueni. ~able adj -enye kupatikana tena. ~y n kupata tena; kupata nafuu tena.

recover2 vt funika tena/upya.

recreant adj -oga; -saliti. n mwoga;

msaliti.

recreate vt buni; sanifu upya; kumbuka. recreation n burudani, mapumziko, burudiko. recreation ground n kiwanja cha burudani. recreational adj -a burudani.

recrimination n shitaka/lawama baada ya shitaka (lililokwishatolewa). recriminate vi toa shitaka kufuatia shitaka dhidi yako. ~ against somebody lipiza kisasi. recriminatory adj indulge in recriminatories baki kulaumiana.

recrudescence n kuanza tena, kuzuka tena (vita, matata, ugonjwa).

recruit n (of army) kuruta, askari mpya (anayejiunga); (of a party) mwanachama mpya. vt 1 (of military, association, etc) andikisha. 2 pata kiasi/nafasi ya kutosha. 3 rudisha katika hali ya kawaida. ~ment n 1 uandikishaji wa askari au wanachama.

rectangle n mstatili. rectangular adj -a mstatili.

rectify vt 1 sahihisha; rekebisha. 2 (chem) takasa; safisha. 3 (electr) badili mkondo. rectifier n 1 mtu/kitu kinachorekebisha, sahihisha. rectification n (phys) kirekebishi.

rectilineal/rectilinear

rectilineal/rectilinear adj -a mstari

ulionyooka; -lio na mistari iliyonyooka.

rectitude n uadilifu; uaminifu; unyofu.

rector n 1 (church of England) paroko; mchungaji mkuu. 2 (of a seminary) mkuu wa chuo/shule; gambera. ~y n nyumba ya paroko/mchungaji mkuu.

rectum n (bio) rektamu. rectal adj -a rektamu.

recumbent adj (esp of a person)

-liolala, -a kulala. recumbency n.

recuperate n, vt,vi pata/rudisha nguvu tena (baada ya ugonjwa, kuchoka, n.k.). recuperation n. recuperative adj.

recur vi 1 rudia. 2 ~ to rejea ~ to what I said yesterday rejea maneno niliyosema jana. 3 (of ideas, events, etc.) -jia akilini tena. ~rence n kutokea tena (mara kwa mara); kurudiarudia. ~rent adj (of events, fevers, etc) -a kutokea mara kwa mara, -a kurudiarudia. ~rent expenditure n matumizi ya kawaida. (maths) ~rent series n mfulululizo wa kurudiarudia.

recurve vt,vi pindia nyuma/chini. recurvate adj -liopindia nyuma/ chini.

recusant adj asi; kaidi (agh. Mkatoliki

aliyekataa kujiunga na Waanglikana). recusancy n ukaidi.

red adj 1 -ekundu. see ~ shindwa kujizuia kwa sababu ya hasira au kuonewa. paint the town ~ (colloq) enda kustarehe kwa shangwe na vifijo. ~ carpet n zulia jekundu (kwa ajili ya wageni wa heshima) ~ carpet welcome mapokezi makubwa. 2 (of Russia) R~ Army n Jeshi la Urusi (wakati wa mapinduzi). 3 (with compounds) R~ bricks n (UK) vyuo vilivyoanzishwa karne ya 19 na baadaye. ~cap n (UK) polisi wa jeshi; (US) mbeba mzigo katika kituo cha reli. ~coat n askari wa Uingereza. R~ Cresent n (in Muslim countries) (mwezi mwekundu). R~ cross n Msalaba

redeem

Mwekundu: Chama cha Kimataifa cha kuwasaidia waliofikwa na maafa. ~deer n aina ya swala wapatikanao Ulaya na Asia. ~ensign (or colloq ~duster) n bendera nyekundu yenye bendera ya Kiingereza pembeni mwake (itumiwayo na meli za wafanyibiashara wa Uingereza). ~flag n bendera ya hatari; alama ya mapinduzi. ~ handed adv papohapo (penye kitendo) catch ~ handed fuma; adv fumania. ~ hat n kofia ya kadinali. ~head n mtu mwenye nywele nyekundu. ~herring n aina ya samaki wa maji ya chumvi aliyekaushwa kwa moshi; (fig) jambo la kupoteza lengo. draw a ~ herring across the trail poteza lengo (kwa kuleta mambo yasiyohusika). neither fish, flesh, nor good ~ herring -siyoeleweka. ~ hot adj (of a metal) -enye moto sana (hata kuwa nyekundu); (fig) -liohemkwa, -liochachafika; -lioghadhabika sana. ~ Indian n (arch) Mhindi Mwekundu, Mmarekani wa asili. ~lead n kipande cha risasi nyekundu. ~-letter day n sikukuu; siku ya kumbukumbu. ~ light n taa nyekundu; alama ya hatari. see the ~ light tambua hatari. ~-light district n mtaa wa makahaba, danguro. ~ meat n nyama ya ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k. ~ pepper n pilipili hoho. ~ rag n. like a ~ rag to a bull kichocheo, hasira. ~ tape n (fig) urasimu. n 1 rangi nyekundu. 2 nguo nyekundu. 3 (colloq) mkomunisti, mfuasi wa ukomunisti. 4 (comm) upande wa madeni katika mahesabu. be in the ~ ishiwa; -wa na madeni. ~den vt,vi tia wekundu; -wa -ekundu, iva usoni. ~dish adj -ekundu kidogo.

redact vt hariri. ~ion n.

redeem vt 1 ~ (from) komboa, okoa ~ one's right komboa haki ya mtu. 2 timiza ahadi. 3 komboa (kwa

redeploy

kulipa). 4 fidia. ~able adj -enye kuweza kukombolewa; -a kukomboleka. the R~er n Yesu Kristo; Mwokozi. redemption n wokovu; ukombozi, fidia the equity of redemption haki ya ukombozi past/beyond redemption -siokombo- leka tena; -siyorekebishika. redemptive adj -a kuokoa; -a kufidia.

redeploy vt ondoa/hamisha na kupanga

upya.

rediffusion n mfumo wa matangazo (ya redio, televisheni, n.k.) hadharani.

redo vt fanya/tengeneza upya.

redolent adj ~ of (formal) -enye harufu kali; -enye kunukia; (fig) -a kuleta kumbukumbu (za jambo fulani). redolence n.

redouble vt,vi 1 ongeza, zidisha they ~d their efforts walizidisha jitihada zao. 2 (bridge) fanya maradufu. n (bridge) kufanya maradufu; kurudufu.

redoubt n kituo muhimu (katika ngome).

redoubtable adj (liter) mashuhuri, -a

kuogofya ~ person gogo.

redound vi ~to (formal) endeleza, kuza, letea, changia ~ to his credit inamletea heshima.

redress vt 1 rekebisha; fidia. 2 ~ the balance sawazisha mambo tena. n fidia; jazi; marekebisho seek ~ tafuta haki.

reduce vt,vi ~ (to) 1 (lessen) shusha; punguza; teremsha ~ one's expenditure punguza matumizi. 2 (subdue) lazimisha ~ to silence nyamazisha ~ to submission tiisha be ~d to begging lazimishwa kuombaomba. ~ to the rank nyang'anya cheo. 3 (change) geuza umbile (kwa kuponda, kusaga,

kusindika) ~ wood logs to pulp sindika magogo. reducible adj. reduction n 1 kupunguza; kupunguka; upungufu price reduction upunguzaji wa bei. 2 (maps, photograph, etc) kupunguza (ukubwa). 3 nakala ndogo. reductio ad absurdum n 1 (Latin) kukanusha

re-entry

hoja kwa kubeza; kugeuza/ kuonyesha kuwa hitimisho fulani ni upuuzi.

redundant adj 1 -siohitajika; -a

kuzidi, -a ziada. redundance, redundancy n uziada; (pl redundacies) kufukuzwa kazi (kwa sababu ya kupunguza nafasi). redundancy pay n malipo ya mfanyakazi anayepunguzwa kazi.

reduplicate vt radidi, rudia; rudufu.

reduplication n uradidi, urudiaji; urudufu.

reed n 1 tete, mafunjo. a broken ~n (fig) kitu/mtu asiyeweza kutumainiwa. 2 (pipe) filimbi, kilimi. ~y adj 1 -a matete. 2 (of sounds, voices) -enye usiyahi.

reef1 n mwamba.

reef2 n tanga take in a ~ fupisha tanga; (fig) endelea kwa hadhari zaidi. ~-knot n fundodufu, rifunoti. vt (of a sail) punguza ukubwa.

reefer n 1 kizibao cha mabaharia. 2 (sl) sigara yenye mariwana/bangi.

reek n 1 uvundo, rihi mbaya the ~of tobacco rihi mbaya ya tumbaku. 2 (liter and Scot use) moshi mzito, mvuke. vi 1 nuka vibaya; toa mvuke/ moshi. 2 ~ with jawa na, hanikiza.

reel1 n kidonge, kigurudumu.

(straight) off the ~ (colloq) bila kupumzika, moja kwa moja; (cinema) ukanda, rili a seven ~film filamu ya rili saba. vt sokota uzi (katika kidonge). ~ something off fanya/sema upesi upesi.

reel2 vi 1 (physically or mentally) shtuka; shtushwa. 2 pepesuka, sepetuka, sesereka, yumbayumba he ~ed like a drunken man alipepesuka kama mlevi. 3 onekana kuchezacheza the street ~ed before his eyes aliona kama mtaa unachezacheza.

reel3 n muziki wa ngoma ya kiskoti vi cheza ngoma ya kiskoti.

re-entry n (of space craft) kuingia tena (kwenye anga ya dunia). re enter vi

reeve

ingia tena.

reeve n 1 (hist) hakimu wa wilaya (au mji). 2 (Canada) mwenyekiti wa kijiji au halmashauri ya mji.

re-face vt (of building) sawiri upya, -pa sura mpya.

refection n viburudisho vya chakula na vinywaji. refectory n chumba cha kulia, mesini.

refer vi 1 ~ somebody/something (back); ~ to somebody/something (send) peleka; (send back) rejesha, rudisha ~ a question to somebody peleka swali kwa mtu ~ a cheque to the drawer rudisha hundi kwa mwenyewe. 2 ~ to nena, taja. the person ~red to mtajwa. 3 husu this word ~s only to persons neno hili lahusu watu tu. 4 tumia ~ to a dictionary tumia kamusi. ~able adj. ~ee n 1 mwamuzi, refa vt chezesha. ~ence n 1 kumbukumbu, marejeo what is the ~ kumbukumbu ni nini? ~ence books n marejeo. ~ence library n maktaba ya marejeo make a ~ence to fanya kumbukumbu, rejea. terms of ~ ence n hadidu za rejea. 2 udhamini. give three ~ences taja wadhamini watatu. 3 in/with ~ ence to kuhusu. without ~ence to bila kujali, bila kuhusisha. ~ential adj. ~endum n kura ya maoni.

refill vt jaza tena, tia tena. n ujazo; (kalamu) kijazi.

refine vt 1 takasa; safisha. 2 (civilize) adilisha; fanya ungwana; staarabisha. 3 ~ upon fanya kuwa nzuri zaidi; rekebisha. ~d adj. ~d sugar n sukari safi. ~ment n 1 utakaso; usafi; uhalisi ~ment of language ufasaha wa lugha. 2 adabu, ustaarabu, uungwana, makini, malezi mazuri. ~r n msafishaji; kinu cha kusafisha sukari, metali n.k. ~ry n kiwanda cha kusafisha sukari, metali, n.k.

refit vt,vi (of a ship) tengeneza tena, karabati, unda upya. n uimarishaji meli.

refract

reflate vt rudisha uchumi/kiasi cha fedha katika hali yake ya awali.

reflect vt 1 akisi, rudisha (nuru, moto). ~ing telescope n darubiniakisi. 2 (consider) fikiri, waza, tafakari. 3 ~ upon (disparage) leta sifa nzuri/ mbaya his action ~ed great credit upon him tendo lake lilimpatia sifa kubwa. 4 (express) akisi literature ~s society fasihi huakisi jamii. ~ion n 1 kuakisi, kurudisha (nuru). 2 (thoughts) fikira, mawazo. 3 (censure) shutuma, masuto. 4 (visual image, likeness) mfano; picha (sanamu, mfano) katika kioo (maji). 5 (maths) pindu. 6 kitu kiletacho sifa mbaya. ~ive adj -a makini; -enye mawazo, -enye kuwaza. ~ively adv. ~or n kiakisi.

reflex adj 1 (of action) -a tendohiari, -a tendohisia (k.m. chafya); -a kujiendea. 2 ~ camera n kamera akisi. 3 (maths) ~ angle pembekuu. n tendohiari; tendohisia. ~ive adj (gram) -a kujirejea.

reflexion n see reflection.

refloat vt fanya kuelea tena, ibua.

reflux n kupwa, kurudi.

reforest vt see reafforest.

reform vt,vi rekebisha; ongoka; ongoa, hidi. n kurekebisha; kuongoa; mageuzi ~ school shule ya kuadibisha. 2 kurekebisha sheria law ~ urekebishaji sheria. ~er n mleta mabadiliko. ~ist n mleta mabadiliko. ~tion n 1 mageuzo, marekebisho. 2 the R~ Mageuzo ya (mgawanyiko wa) Kanisa (la Kirumi karne ya 16). ~atory n shule ya maadili; shule ya kuadibisha; -a kuadilisha. ~ed adj -liotengenezwa, -lioongoka, -liogeuka kuwa -ema, -liotengemaa. the R~ Church n kanisa la Protestanti hasa la mafundisho ya Kalvin; mafundisho ya Kalvin.

refract vt, vi (of water, air, glass, etc) chepuka, pinda; pindisha. ~ion n mchepuko, uchepukaji. angle of ~ion n pembe mchepuko. ~ed ray

refrain

adj lenzi/ mwali mchepuko. ~or n. ~ory adj 1 -kaidi. 2 (of substance) -gumu. ~oriness n.

refrain1 vi ~ (from) jizuia, epuka, acha (kufanya) please ~ from smoking tafadhali acha kuvuta sigara; usivute sigara please ~ from spitting tafadhali usiteme mate.

refrain2 n kiitikio, kipokeo.

refresh vt 1 burudisha/fariji, changamsha. 2 leta nguvu mpya; fanya mpya. 3 kumbusha. ~ one's memory jikumbusha. 4 ~ oneself kula, kunywa. ~ing adj -a kuburudisha, -zuri. ~ingly adv. ~er n 1 (leg) ada ya ziada (alipwayo wakili wakati kesi bado inaendelea). 2 (colloq) kiburudisho, kinywaji. 3 kiamsha akili; kinoa ubongo a ~er course kozi ya kunoa ubongo, kozi ya kupiga msasa. ~ment n 1 chakula, kinywaji, kiburudishacho have some ~ment pata kiburudisho. 2 hali ya kuburudika.

refrigerate vt fanya kuwa baridi; hifadhi chakula katika hali ya kutoharibika (kwa kukifanya kiwe katika baridi isiyobadilikabadilika); gandisha. refrigerant n kituliza joto, kipoza joto. refrigeration n utiaji kitu baridi. refrigerator n friji, jokofu, jorafu.

reft v see bereft.

refuel vt,vi jaza tena mafuta (petrol, diseli, n.k.).

refuge kukimbilia seek ~ omba/tafuta usalama take ~ in silence (jihami kwa) kunyamaza. ~e n mkimbizi. political ~e mkimbizi wa kisiasa ~e camp kambi ya wakimbizi.

refulgent adj (formal) -a kung'aa sana, -nayong'aa sana. refulgence n.

refund vt rudisha/rejesha fedha; lipa. n fedha zinazorudishwa.

refuse1 vt,vi kataa; katalia, nyima;

gahamu, iza I was ~d entry nilikataliwa kuingia the child is refusing to eat today leo mtoto anakataa kula. refusal n 1 kitendo cha kukataa. 2 (the) refusal n (with

regent

definite article) haki/upendeleo wa kukubali au kukataa if ever you decide to publish your manuscript please give me the first refusal of it ukiamua kuchapisha muswada wako tafadhali nipe mimi fursa ya kwanza ya kufikiria kuuchapisha.

refuse2 n takataka. ~ dump/heap n jalala, jaa (la takataka).

refute vt kanusha, thibitisha kuwa

uwongo. refutable adj. refutation n.

regain vt 1 pata tena ~ health pona ~possession of something pata/miliki (kitu) tena. 2 rudia mahali.

regal adj -a mfalme, -a kustahili mfalme. ~ly adv. ~ia n 1 nembo/mapambo ya mfalme. 2 nembo/mapambano ya cheo fulani.

regale vt,vi ~ oneself/somebody (with something) anisi, furahisha sana; burudisha.

regard vt 1 (arch) angalia, tazama kwa makini; kodoa macho. 2 (consider as done) fikiri/ona kuwa. 3 (esteem) stahi, jali, heshimu ~ somebody with esteem heshimu mtu. 4 husu. as ~s/~ing mintarafu ya, kuhusu. ~ful adj -ingi wa heshima. n 1 (arch lit.) utazamaji wa kukodoa macho (kwa muda mrefu). 2 mazingatio. 3 heshima, staha, itibari have little ~ for -toheshimu. 4 salamu (za upendo) my ~s to unisalimie. 5 suala. in this ~ kuhusu suala hili. in/with ~ to kuhusu. ~ful (of) adj. ~less adj. ~lessly adv bila kujali, pasipo kutia maanani.

regatta n mashindano ya mashua (ya kuendeshwa kwa makasia au matanga).

regenerate vt,vi 1 ongoa, ongoka.

2 fufua (jambo/chama, n.k.). 3 (biol) ota tena adj -lioongoka. regeneration n wongofu, ufufuo. regenerative adj.

regent n 1 kaimu, mtawala wa muda (badala ya mfalme); mtawala mshikiliaji. 2 (US) mjumbe wa Halmashauri (ya Chuo Kikuu cha jimbo, n.k.). regency n utawala wa pahala pa mfalme mwenyewe; kushikilia.

raggae n rege: muziki maarufu wa Visiwa vya West Indies.

regicide n 1 mwuaji wa mfalme. 2 uuaji wa mfalme.

regime n utaratibu/mfumo wa

regimen

utawala.

regimen n kanuni za mlo, mazoezi, michezo n.k. kwa ajili ya kuleta afya.

regiment n 1 rejimenti: kikosi chini ya kanali. 2 (fig) ~ of jeshi ~ of red ants jeshi la siafu. vt shurutisha, amuru. ~ation n hali ya kuwa chini ya uongozi au udhibiti wa mtu mwingine; nidhamu kali ya kisiasa; udhibiti mkali. ~al adj -a kuhusu rejimenti. n (pl) mavazi ya askari wa rejimenti moja; mavazi ya kijeshi.

Regina n malkia anayetawala (hutumika wakati wa kutia sahihi tamko rasmi); (leg) dola ~ vs Jones dola dhidi ya Jones. regnant adj -enye kutawala. King ~ n mfalme anayetawala.

region n 1 eneo, uwanja, sehemu. the lower ~s n jahanamu. 2 mkoa. ~al adj. ~ally adv.

register n 1 rejesta, daftari yenye rekodi. 2 kadiri ya sauti. 3 chombo (mashine) cha kuonyesha na kurekodi kasi, kani, namba. 4 kirekebishi (cha kupanua au kupunguza ukubwa wa tundu, uwazi, n.k.). 5 (gram) rejista: lugha itumikayo katika muktadha maalumu. 6 see registry n. ~ (something/oneself) (with something/somebody) (for something) vt,vi 1 sajili, andikisha, rajisi ~ voters andikisha wapiga kura ~ an association sajili chama. 2 onyesha (hisia, kiasi cha joto, hali, n.k.) his face ~ed anxiety uso wake ulionyesha wasiwasi the thermometer ~ed 40 degrees centigrade pimajoto ilionyesha nyuzi 40 sentigredi. 3 tuma barua ya rejesta. registrar n 1 msajili, mrajisi the registrar's office ofisi ya msajili registrar of companies msajili wa makampuni registrar of societies mrajisi/msajili wa vyama. registrar-general n mrajisi mkuu. registration n 1 usajili, uandikishaji registration of deaths usajili wa vifo registration plate bamba la namba (ya kusajiliwa) ya gari. 2 ingizo; rekodi ya mambo. registry n 1 usajili

rehabilitate

central registry usajili mkuu. 2 ofisi ya msajili marriage registry ofisi ya msajili wa ndoa. 3 (also register) masijala.

regress vi rudi nyuma. ~ion n kurudi nyuma. ~ive adj -a kurudi nyuma.

regret n 1 majuto have no ~s usiwe na majuto feel ~ jutia. 2 (pl.) masikitiko with many ~s kwa masikitiko makubwa. ~ful adj. ~fully adv.~ vt 1 juta ~ past actions jutia vitendo vya nyuma. 2 (feel sorry for). sikitikia it is to be ~ted that imesikitisha kwamba. ~table adj -a kusikitisha, -a kujutia. ~tably adv.

regroup vt,vi kusanya/kusanyika tena;

kusanya/kusanyika upya.

regular adj 1 -a kawaida, -a mazoea; -a kila siku ~ customer mteja wa kila siku ~ hours saa za kawaida ~ habits mazoea. 2 -enye sifa zinazotambulika/ zinazokubalika; -liopata mafunzo. 3 -enye kukubalika ~ procedure utaratibu unaokubalika. 4 -enye kufuata mpango, -enye utaratibu unaooana. 5 -enye kulingana na viwango vilivyokubaliwa. 6 (rel) -enye kufuata sheria za dini. 7 (colloq) kamili, kabisa. 8 (gram) -enye minyambuliko na mabadiliko ya kawaida. 9 -a kutokea/kufanyika/ kufanya mara kwa mara. 10 linganifu. 11 (colloq) safi, nzuri. ~ize vt rekebisha, halalisha, panga/fanya kulingana na kanuni. ~ization n.

regulate vt 1 rekebisha. 2 dhibiti;

tiisha. regulator n mrekebishaji, kirekebishaji. regulation n 1 urekebishaji. 2 taratibu, kanuni; (attrib) -enye kufuata taratibu/ kanuni.

regurgitate vt cheua; tapika. regurgitation n mcheuo; matapishi.

rehabilitate vt 1 (of building) karabati, tengeneza upya. 2 rudisha cheo/ heshima/sifa njema; safisha. 3 (of a disabled person, etc) wezesha kuishi

rehash

maisha ya kawaida. rehabilitation n.

rehash vt tumia tena kitu cha zamani. n kitu (cha zamani) kilichotumiwa tena.

rehearse vt 1. fanya mazoezi. 2 kariri, simulia. rehearsal n 1 mazoezi (ya maigizo). 2 masimulizi.

reign n utawala, enzi. vi ~ (over) tawala, miliki he ~ed over the country for twenty years alitawala nchi kwa miaka ishirini silence ~ed kimya kilitawala.

reimburse vt rejeshea gharama (alizotumia mtu). ~ somebody (for) something rudishia, lipa. ~ment n.

rein n hatamu. give free ~s to pa uhuru, achia. assume/drop the ~s of government chukua/acha madaraka. draw ~ (lit and fig) punguza mwendo. hold/take the ~s (lit and fig) ongoza, shika hatamu. keep a tight ~on dhibiti vikali. vt ongoza, zuia (kwa hatamu) ~up/back a horse zuia/simamisha farasi.

reincarnate vt -pa roho mwili mpya adj -a kuzaliwa upya (roho) katika mwili wa kiumbe mwingine. reincarnation n (Rel) imani kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa mtu mwingine.

reindeer n kulungu wa nchi za baridi.

reinforce vt imarisha, ongeza nguvu. ~d concrete n saruji iliyoimarishwa (kwa kutumia chuma). ~ment n 1 uimarishaji; msaada, shime. 2 (pl) askari, manowari za kuongezea nguvu ya jeshi.

reinstate vt rejesha mahali pake, rudishia nafasi yake. ~ment n.

reinsure vt (of insurance comp) weka bima katika kampuni kubwa zaidi reinsurance n.

reissue vt toa mara ya pili, toa tena. n kitu kilichotolewa mara ya pili; chapa ya pili.

reiterate vt sema tena na tena, rudia kusema. reiteration n.

reject vt 1 kana; kataa. 2 tupa; ~ food tapika. ~ion n 1 mtu/kitu kilichokataliwa k.m. mali mbovu

relate

export ~ion bidhaa zilizokusudiwa kusafirishwa nje lakini zikakataliwa kutokana na kasoro/uhafifu au uduni wake. 2 kukatalia; kukataliwa.

rejig vt (of factory, etc) imarisha kwa kuongeza zana na vyombo vipya.

rejoice vt,vi 1 furahisha. 2 ~ (over/at) furahi, furahia, terema, shangilia. 3 ~ in -wa na he ~s in the name of Kambare jina lake ni Kambare. rejoicing n furaha, shangwe, shangilio, nderemo.

rejoin1 vt,vi jiunga tena, rudia tena; rudiana tena, ungana tena.

rejoin2 vt,vi jibu; (leg) jibu mashtaka. ~der n jibu.

rejuvenate vt,vi rudishia ujana, rudishia nguvu za ujana. rejuvenation n.

rekindle vt,vi washa tena; amsha tena. ~ somebody's zeal amsha juhudi/raghba ya mtu.

relapse vt,vi ~ (into) rudia hali fulani

tena (hasa uovu, mwendo mbaya, udhaifu, ugonjwa). n kuugua tena, kurudia hali mbaya, kurudiwa na ugonjwa. relapsing fever n homa ya vipindi.

relate vt,vi 1 ~ (to) simulia (hadithi,

habari, n.k.). 2 ~ to toa maelezo ya kitu/jambo. 3 ~ to/with husisha; husika na. 4 be ~d (to) kuwa na mnasaba (na) he is ~d to me nina mnasaba naye. relation n 1 masimulizi, maelezo. 2 (also relationship) uhusiano the relationship between husomebodyand and wife uhusiano baina ya mume na mke the oldman's death and Juma's disappearance have no relation(ship) kifo cha mzee huyo na kutoweka kwa Juma havina uhusiano. in/with relation to kuhusu. 3 mahusiano have business relations kuwa na mahusiano ya kibiashara we have broken off all relations with that company tumevunja mahusiano yetu na kampuni ile. 4 udugu, mnasaba. relative n 1 ndugu, jamaa. 2 (gram) relative pronoun n kiwakilishi

relativism

rejeshi adj 1 -a kuwiana na. 2 relative to -enye uhusiano na, -nayohusu. relative motion mwendo unaohusiana with relative ease kwa urahisi bila shida. relatively adv kiasi.

relativism n imani kwamba maarifa na maadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa ubongo na wakati.

relativity n 1 nadharia ya Einstein isemayo kwamba vipimo vya mwendo, nafasi na wakati vinawiana/ kadiriana. 2 (gram) linguistic ~ n (Sapir-Whorf hypothesis) nadharia tete ya Sapir na Whorf isemayo kuwa lugha hutawala namna watu wanavyoufinyanga/wanavyouumba ulimwengu wao.

relax vt,vi 1 legeza, punguza. 2 (relieve) pumzika; pumzisha, burudisha; (of bowels) endesha, fungua ~ the limbs pumzisha/legeza viungo. ~ation n ulegezaji; ulegevu; burudani.

relay1 n 1 rilei : ubadilishanaji zamu wa wanyama, watu, n.k. kuchukua nafasi ya waliochoka. ~ race n mbio za kupokezana do by ~s pokezana kazi. 2 (telegraphy/broadcasting) mtambo wa kupokea na kurushia habari. vt rushia habari ~ a message peleka ujumbe.

relay2 vt tandika (kebo, zulia) upya.

release vt ~ (from) 1 fungua, ruhusu kwenda, achia huru; ondoa ~somebody of a debt futa, samehe deni. 2 ruhusu kutolewa (kwa habari, filamu, n.k.). 3 (leg) achia mwingine haki/mali, n.k. n 1 ufunguliaji; ufunguliwaji, uachiaji huru. 2 kutolewa toleo (la filamu, n.k.) the new ~s filamu mpya. 3 wenzo unaoachilia au kufanya huru sehemu ya mashine.

relegate vt ~ (something/somebody to something) 1 wakilisha. 2 teremsha, shusha ~ a team to a third division shusha timu kuwa daraja la tatu.

relent vi tulia, poa, punguza (hasira,

religion

ukali, n.k.). ~less adj bila huruma ~ less persecution mateso yasiyo na huruma. ~lessly adv.

relevant adj husika, -enye kuhusu (yajadiliwayo) give him all the ~ books mpatie vitabu vyote vinavyohusika. ~ly adv. relevance n uhusiano.

relic n 1 (of saints) masalio. 2 ukumbusho, kumbukumbu. 3 (pl) maiti, mabaki ya binadamu.

relict n (leg) mjane, kizuka.

relief1 n 1 (of pain, distress, anxiety) tulizo, shime, faraja, nafuu. 2 msaada (wa kuwapunguzia watu dhiki) a ~ fund mfuko wa msaada be on ~ ishi kwa msaada wa serikali. 3 burudisho. 4 (of a siege) uimarishaji ngome; kukomboa. 5 (taking turns) mapokezano; mtu wa zamu ijayo; (attrib) -a ziada ~ bus basi la ziada. relieve vt 1 fariji, punguza, tuliza she was reliaved to get the news alifarijika kupata habari zile. reliave one's feelings punguza mawazo/hisia. reliave oneself kojoa, tabawali. 2 -wa na zamu, pokea zamu. 3 reliave somebody of something mpokelee mtu kitu fulani, saidia; (joc) iba, ibia mtu; fukuza kazi, achisha kazi; vua madaraka. 4 dhihirisha, fanya ku(ji)tokeza.

relief2 n 1 mbinu ya uchongaji/uumbaji inayofanya sanamu itokeze katika msingi wake. 2 sanamu iliyochongwa/iliyoumbwa kwa kutokeza katika msingi wake. 3 (in drawing etc) uchoraji unaofanya kitu kitokeze katika msingi wake kwa kutumia vitu kama rangi, n.k. ~ map ramani ionyeshayo milima, mabonde, n.k. kwa kutumia rangi ili kuvifanya vitu hivyo vitokeze. 4 (lit or fig) uwazi, sura ya kutokeza be/stand out in ~ against tofautiana na; -wa kinyume na his behaviour stood out in ~ against his principles tabia yake ilitofautiana na taratibu zake.

religion n 1 dini: imani katika kuwepo

reline

kwa Mungu/kiumbe mwenye nguvu zaidi ya binadamu, aliyeumba na anayeudhibiti ulimwengu. 2 dini: mojawapo ya mifumo kadhaa ya imani na ibada zake (k.m. Ukristo, Uislamu, Ubudha). 3 utawa. 4 imani: kitu ambacho mtu huamini na kushikilia sana she makes a ~ of keeping her house clean anang'ang'ania sana usafi wa nyumba yake. religious adj 1 -a dini. 2 -a mcha Mungu. 3 -a utawa 4 -a imani. 5 -a kushikilia sana jambo. n mtawa, mcha Mungu, mswalihina. religiously adv. religiousness n.

reline vt (of garment) tia bitana mpya.

relinquish vt acha, achilia ~ a habit acha tabia fulani. ~ one's hold of/ over somebody/something achilia mtu/jambo.

reliquary n sanduku/kibweta (cha kuwekea masalio).

relish n 1 ladha, utamu; mvuto, kivutio. 2 shauku; moyo have no more ~ for something -tofurahia kitu, kinai kitu. 3 (seasoning) kiungo; kitoweo. vt furahia, pendezwa na.

relive vt kumbukia, pitia tena, rudia.

relocate vt, vi hamisha; hamishwa; hamia makao mapya. relocation n kuhamia/kuhamishia makao mapya; (of war) kuhamishia wananchi katika makazi mapya.

reluctant adj ~ (to do something) -totaka, sita, kaidi; -a kukalifu. ~ly adv. reluctance n.

rely n ~ on/upon tumaini; tegemea; tawakali ~ on oneself jitegemea. reliable adj -a kutegemewa, -a kuaminika; -a kutumainiwa reliable information habari ya kuaminika. reliably adv. reliability n tegemeo; tumaini; uaminifu -a utawa. reliance n imani, tumaini; tegemeo place reliance on tumaini, aminia; tegemea. self reliant adj -enye kujitegemea be self-reliant jitegemee.

remain vi 1 baki, salia nothing ~ed for us but hatukuwa na la kufanya ila. 2 endelea kuwepo/ishi mahali fulani

remiss

au katika hali fulani, bakia. ~der n baki, salio. ~s n 1 masalio, mabaki (of food) makombo; (of building) gofu. 2 (also relics) maiti.

remand vt weka mahabusi, weka rumande. n rumande; mahabusi ~ prison mahabusi ~ house/home rumande ya watoto.

remark vt,vi 1 sema. 2 ~on/upon toa maoni, zungumzia. 3 (arch) ona, tazama n 1 maoni, maneno pass rude ~s about somebody toa maneno mabaya kuhusu mtu fulani. 2 kutazamwa. ~able adj -a ajabu, -a kusifika, -sio kifani. ~ably adv.

remarry vt, vi oa/olewa tena.

remarriage n.

remedy n dawa; tiba the ~ is worse than the disease tiba yake ni mbaya kuliko ugonjwa wenyewe. vt tengeneza, rekebisha. remedial adj -a kuponya; -a marekebisho, -a kutuliza remedial classes masomo ya kujirekebisha. remediable adj -a kuponyeka; -a kutulizika.

remember vt,vi 1 kumbuka, dhukuru. 2 ~ somebody to somebody pa salamu, salimia please ~ me to him tafadhali mpe salamu zangu; unisalimie. 3 tunuka ~ someone in a will tunuka katika wasia. remembrance n 1 ukumbusho, kumbukumbu escape somebody's remembrance sahau. 2 salamu (zilizopelekwa kwa barua au kwa aliyetumwa).

remind vt ~ somebody (to do something/that..); ~ somebody of something/somebody kumbusha that ~s me! hiyo inanikumbusha. ~er n kumbusho.

reminisce vi ~ (about) kumbuka ya

kale, (zingatia na zungumza juu ya mambo yaliyopita). ~nce n 1 ~nce (of) ukumbukaji mambo ya kale. 2 (pl) makumbusho. ~nt (of) adj -a kukumbusha; -a kukumbuka mambo yaliyopita. ~ntly adv.

remiss adj ~ in/of -zembe; vivu, ajizi. ~ly adv. ~ness n.

remit

remit vt,vi 1. (usu. of God) ondolea

dhambi, samehe. 2 (of debts, penalty) samehe, achilia, futa. 3 (money, etc) peleka kwa posta, lipa. ~tee n mpelekewaji malipo. ~ter n mpelekaji malipo. 4 (of pain, effort, etc) punguza, legeza. 5 ~ something to somebody tumia mtu kitu ~ something to higher authority peleka kwa mamlaka ya juu (kwa uamuzi). ~tance n 1 fedha; malipo. 2 upelekaji fedha; kiasi cha pesa kilichopelekwa mahali pengine. remissible adj -lioweza kusamehewa, -a kusameheka; -a kuhurumiwa. remission n 1 msamaha (wa dhambi unaofanywa na Mungu). 2 kusabilia deni au adhabu. 3 kupungua (kwa maumivu, bidii). remissive adj.

remnant n mabaki, masazo; makombo ~ sale seli ya mabaki ya vitambaa.

remonstrate vi lalamika; pinga. ~ with somebody about something pingana na mtu juu ya jambo fulani. remonstrance n ulalamikaji wa kupinga kitu/jambo.

remorse n 1 ~ (for) majuto, toba. 2 huruma without ~ bila huruma. ~ful adj. ~fully adv. ~less adj pasipo kujuta; katili. ~lessly adv.

remote adj 1 -a zamani the ~past

zamani za kale. 2 -a mbali. ~ control -enye kuendeshwa/kufanywa toka mbali, -liotengwa (kwa maono, kwa moyo wa kupenda). 3 (feelings, interests, etc) liopishana sana, liotengana, mbalimbali. 4 (not friendly) baridi. 5 (insignificant) dogo I haven't the ~st idea sijui hata kidogo, sina habari. ~ly adv. ~ness n.

remount vt,vi 1 panda tena. 2 (of photographs, maps, etc) weka katika fremu tena. 3 gawia mtu/wanajeshi farasi mpya. n farasi mpya; ugawiaji watu farasi mpya.

remove vt,vi 1 ~ (from) ondoa, ondosha. 2 ~ (from) hama; hamisha, hawilisha; hajiri. ~ mountains (fig) fanya miujiza. 3 (of clothes) vua; (of

renew

bark) ambua. 4 (from office) uzulu, fukuza. 5 (erase) futa. 6 (of spell) agua, eua, adua, tegua. 7 ~d n (of cousins) mtoto wa binamu. n hatua be one ~ from something pakana, karibiana na. removable adj. removal n.

remunerate vt ~ somebody (for something) lipa, -pa ujira, tuza, -pa zawadi. remuneration n ujira, tunzo, zawadi. remunerative adj -a kuleta faida.

renaissance n (also renascence) 1 the ~ (Europe) kipindi mwamko-sanaa (katika karne ya 14, 15 na 16), kipindi cha kuchipuka upya. 2 mvuvumko.

renal adj -a mafigo.

rename vt pa jina jipya, batiza upya,

ita upya.

renascence n see renaissance.

rend vt,vi 1 tatua, pasua, rarua; penya ~ one's hair (in grief) timua nywele. 2 pokonya, pora.

render vt 1 ~ something (to somebody) toa, lipa, rudisha, onyesha (heshima) ~ thanks toa shukurani. 2 leta, peleka. ~ an account of oneself/one's behaviour elezea, jieleza ~ed account ankara iliyotolewa (kwa kulipwa). 3 fanya, geuza kuwa katika hali fulani the drink ~ed him speechless ulevi ulimfanya kuwa bubu. 4 ~ something (down) yeyusha; safisha siagi/samli kwa kuyeyusha. 5 (of building) piga lipu. 6 tafsiri; fanya; igiza. ~ing n 1 (translation) tafsiri, fasili. rendition n 1 utambaji. 2 ufasiri, ufafanuzi.

rendezvous n 1 mahali pa kukutanika; mahali pa miadi. 2 makutano. vi kutana (mahali palipochaguliwa).

renegade n 1 msaliti, haini; mwasi. 2(rel) muritadi. vi saliti; ritadi; asi.

renege; renegue vi 1 (in card games) kosa kucheza karata iliyochaguliwa hali unayo mkononi. 2 vunja ahadi au kauli.

renew vt 1 tengeneza/fanya upya, tia

renounce

nguvu, -pa moyo. 2 pata/toa tena. 3 anza, rudia tena ~ one's youth rudia ujana. ~able adj. ~al n.

renounce vt 1 (refuse) kataa, kanusha; kana. 2 burai (madai). 3 (give up) acha, jitoa katika jambo, achilia mamlaka ya mtu. renunciation n 1 kano, kanusho. 2 (relinquishment) kuacha, kujinyima, kujihini. renunciatory adj.

renovate vt rekebisha, fanyiza upya,

karabati. renovation n 1 urekebishaji. 2 ukarabati; matengenezo. renovator n mtengenezaji.

renown n sifa, utukufu, umashuhuri,

jina a town of great ~ mji wa sifa kuu. ~ed adj -enye sifa, adhimu, tukufu, mashuhuri.

rent1 pp of rend.

rent2 n kodi. ~ rebate n kipunguo cha kodi ~ restriction usimamiaji wa kodi ~ restriction board halmashauri ya kusimamia kodi. ~ collector n mkusanya kodi. ~ier n mpangishaji, mtu ambaye mapato yake hutokana na kupangisha nyumba. ~-free adj -siolipiwa, -siotolewa kodi; wakfu. ~-roll n daftari ya upangishaji, orodha ya ukodishaji. vt,vi ~ to pangisha, kodisha. ~from panga, kodi. ~able adj a kupangishika. ~al n 1 kodi. 2 mapato ya kodi.

rent3 n 1 mpasuko, mtatuko, ufa. 2 (fig) mfarakano, mtengano.

rep1 n repu: kitambaa cha kufunikia

viti.

rep2 (colloq) (abbr.) repertory n; reputation n; representative n.

repair1 vt 1 karabati, fanya

matengenezo; (of clothes) shona, tia kiraka a road under ~ barabara inayofanyiwa matengenezo. 2 rekebisha, weka sawa. n matengenezo, (state) hali (nzuri au mbaya) in good ~ nzima in bad ~ bovu keep in good ~ tunza vizuri put in ~ fanya matengenezo. ~er n mtengenezaji. ~ing n utengenezaji,

repercussion

ushonaji wa kutia kiraka. reparable adj -enye kuweza kutengenezwa, -a kutengenezeka, -a kuweza kufidiwa, -a kulipika. reparation n 1 ulipaji fidia, kufidia (hasara, uharibifu). 2 fidia.

repair2 vi ~to enda, zuru.

repartee n malumbano.

repast n (formal) mlo.

repatriate vt rudisha kwao, rejesha makwao ~a fugitive rudisha mkimbizi kwao. n ~d person mtu aliyerejeshwa kwao. repatriation n.

repay vt,vi 1 rejesha pesa, kitu, n.k. ulichochukua, lipa. 2 ~ something; ~somebody (for something) lipiza; lipizia. ~able adj -a kulipika. ~ment n malipo; kulipa; kulipiza, malipizo.

repeal vt tangua, batilisha; futa

(sheria). n mtanguo, kufuta; ubatilifu.

repeat vt 1 rudia. 2 kariri, soma/sema kwa ghibu. 3 (of numbers) rudiarudia, tokea tena (mara nyingi). 4 (of taste) bakia mdomoni. 5 (of commerce) toa tena (bidhaa), rudia kutoa. n 1 marudio k.m. mchezo, kipindi cha redio. 2 (music) alama ya kuonyesha mahali pa kurudia katika muziki. ~edly adv -liofanywa tena na tena. ~er n 1 bunduki inayotema risasi. 2 (E.A) mtu anayerudia (darasa n.k.). ~ing adj -a kurudiarudia ~ing decimal desimali ya kurudiarudia. repetition n 1 kurudiarudia; urudiaji. 2 (of poetry) ukariri, usomaji wa ghibu. repetitious; repetitive adj -a kurudiarudia.

repel vt 1 fukuza. 2 kataa; zuia ~ an

enemy fukuza adui. 3 chukiza. ~lent adj -a kuchukiza; -a kukirihi n kiwinga.

repent vt,vi ~(of) tubu; juta. ~ance n toba. ~ant adj -a kutubu; -a kujutia he is ~ant of his wrongs anajutia makosa yake n mjutaji. ~antly adv.

repercussion n 1 mruko/mtupo nyuma, mwangwi. 2 (usu pl) athari, matokeo

repertoire

hasi be followed by ~s fuatiwa na matokeo hasi (yasiyokusudiwa).

repertoire n mkusanyiko wa maonyesho (nyimbo, tamthilia, n.k.) ya msanii mmoja au kikundi kimoja cha sanaa.

repertory n 1 hazina (ya habari, maarifa, n.k.). 2 see repertoire ~ theatre company (abbr. rep) kikundi cha sanaa (kinachobadilisha wachezaji/tamthilia mara kwa mara).

repine vi (formal) ~(at) onea uchungu. ~ against lalamikia.

replace vt 1 rudishia mahali pake. 2 ~ somebody/something by/with chukua nafasi ya, ingia mahali pa, badilisha ~somebody with a machine badilisha mtu na/kwa mashine. ~able adj -enye kuweza kubadilishwa, -a kubadilishika, -enye kuweza kuchukuliwa nafasi. ~ment n ubadili; badala.

replay n marudio ya mchezo. vt rudia mchezo; (colloq) rudia kupiga kanda.

replenish vt ~ (with) jaza tena,

sheheneza. ~ment n ujazaji tena, ushehenezaji tena.

replete adj ~ (with) (formal) tele, -liojaa ~ with food -lioshiba. repletion n (formal) shibe to eat to ~ kuvimbiwa be full to ~ shiba mno/kupita kiasi.

replica n nakala, nakala halisi; rupia/ shilingi kwa nyenziye. ~te vt toa nakala; rudufu.

reply vi ~ (to) jibu, itika; peleka/tuma jibu. n jibu, itikio. ~ paid n jibu lililokwishalipiwa.

report vt,vi 1 toa ripoti, toa taarifa,

pasha habari; simulia mambo (uliyoona, uliyosikia, uliyofanya). ~progress toa taarifa ya maendeleo. ~ something out (US) rejesha pamoja na maoni. ~edly kwa mujibu wa taarifa, inavyosemekana. ~ed speech n kauli taarifa. 2 nakili, andika (kwa hatimkato). 3 (oneself) (to somebody/something) (for something) ripoti ~ to the manager piga ripoti kwa meneja ~ to the

represent

officer in charge piga ripoti kwa afisa mfawidhi. 4 ~ somebody/ something (to somebody) (for something) shtaki, lalamika ~ a child to his parents shtaki mtoto kwa wazazi wake. ~age n (mtindo wa) utoaji habari (wa magazeti). n 1 ripoti, taarifa annual ~ taarifa ya mwaka law ~ ripoti ya kesi. 2 mshindo it burst with a ~ ilipasuka kwa kishindo. 3 uvumi, tetesi the ~ goes inasemekana kwamba, kuna uvumi kwamba. 4 sifa nzuri/njema people of good ~ watu wenye sifa nzuri. ~er n mtoa habari; mwandishi wa habari.

repose1 vt,vi 1 pumzisha, egemeza, weka, laza. 2 ~ on pumzika. n kupumzika; utulivu; raha; kimya. ~ful adj tulivu, -nyamavu, -lio kimya.

repose2 vt something in something/ somebody amini ~ on his promises amini ahadi zake.

reposit vt weka (kitu) kwenye ghala (bohari). ~ory n 1 hazina, mahali pa kuhifadhia vitu k.v. bohari, ghala, makumbusho n.k. 2 hazina, chemchemi ya habari be ~ory of -wa na hazina ya.

repot vt hamishia (mmea) katika chungu kingine.

reprehend vt karipia, kemea, shutumu. reprehensible adj -a kulaumika. reprehension n.

represent vt 1 ~ something (to somebody). 2 leta, toa, sawiri (picha, dalili) mfano wa a picture that ~s the garden of Eden picha iletayo mfano wa bustani ya Aden. 3 wakilisha; eleza. 4 fanya au sema kwa niaba ya. 5 igiza; iga. ~ation n 1 picha, sanamu, mfano, taswira. 2 kuonyesha; onyesho. 3 uwakili; uwakilishi. proportional ~ ation idadi fulani ya viti katika bunge kulingana na idadi ya kura ambazo chama kimepata. 4 (statement) maelezo (ya malalamiko) false ation ghiliba. ~ative adj. ~ative of -

repress

wakilishi, -a uwakilishi, -a ujumbe ~ ative government serikali ya uwakilishi ~ ative action madai ya jumla. ative n 1 mfano. 2 mwakilishi legal ~. ~ative mwakilishi wa kisheria permanent ~ative mwakilishi wa kudumu.

repress vt zima, zuia, nyamazisha, komesha. ~ed (of emotions) adj -liozimwa. ~ion n 1 uzuiaji kwa nguvu; kunyamazisha, kuzima; uonevu. 2 (psych) mfadhaiko. ~ive adj -a kuzuia, -a uonevu, -a kugandamiza, -a kukomesha ~ive government serikali onevu.

reprieve vt ahirisha/chelewesha adhabu (agh. ya kunyonga mtu aliyeua); (fig) -pa, toa nafuu, achilia kwa muda ~ a debtor achilia mdeni kwa muda. n 1 (leg) uzuiaji kwa muda/ucheleweshaji wa kunyongwa mtu aliyehukumiwa. 2 achilio la muda; kuachiliwa kwa kitambo.

reprimand vt karipia, kemea. n karipio/kemeo rasmi.

reprint vt piga chapa tena, toa kitabu mara ya pili. n lopoo.

reprisal n 1 ulipizaji kisasi (kwa kufanya yale yale uliyotendewa). take ~ lipiza kisasi. 2 (pl) vitendo vya kulipiza kisasi (hasa nchi kwa nchi) katika vita.

reprise n kibwagizo, mkarara, kiitikio.

reproach vt ~ somebody (for/with something) laumu, suta, shutumu, kengemeka. ~ oneself jilaumu. n 1 shutuma, lawama, kengemeko. 2 aibu, fedheheka. above/beyond ~ -sio fedheheka/-laumika. live in ~ ishi katika fedheha heap ~es on somebody fedhehesha sana mtu. 3 ~ (to) kitu cha aibu/fedheha. ~ful adj -a kushutumu, -a kulaumu. ~fully adv.

reprobate vt -tokubali, kataa, chukia. n baa, fisadi, fasiki, mpotovu adj -ovu, potovu. reprobation n.

reproduce vt, vi 1 nakili, fanya sura/

mfano/namna ya. 2 fuatisha; rudisha, toa tena, leta mara ya pili. 3 zaa. 4

ota upya. ~r n mtu ambaye/kitu ambacho huzaa. reproducible adj -a kutengenezeka upya. reproductive adj -a uzazi; -a uwezo wa kuzaa (wanyama au mimea). reproduction n 1 kuzaa; uzazi. 2 nakala halisi. 3 (fresh growth) kuota upya; kitu kinachoota upya.

reproof vt fanya tena kitu (k.m. koti) kisipenyeke maji.

reprove vt ~ somebody (for something) shutumu, laumu. reprovingly adv. reproof n 1 lawama, mashutumu. 2 hali ya kuonyesha kulaumu/kushutumu looks of reproof uso wa kulaumu/ kushutumu.

reptile n mtambaazi: mnyama wa ngeli ya reptilia. reptilian adj -a reptilia, -enye kutambaa.

republic n 1 jamhuri. 2 jamii (ya waandishi n.k.). ~an adj -a jamhuri. ~an n 1 mtu apendaye serikali ya jamhuri. 2 (US) mwanachama wa R~an Party. ~anism n falsafa/sera ya serikali ya jamhuri.

repudiate vt 1 kana. 2 kataa kukubali/ kukiri. 3 kataa kutimiza wajibu; kataa kulipa ~ a debt kataa kulipa deni. repudiation n.

repugnant adj 1 -a kuchukiza, -a

kukirihi, -a kutia kinyaa. 2 (contrary) kinzani, -a mgongano. repugnance n 1 kinyaa. 2 ukinzani, mgongano.

repulse vt 1 rudisha nyuma (maadui); shinda; fukuza. 2 kataa (msaada); fanya mtu asizoee, katisha tamaa kwa kufanyia inadi. n 1 kufukuza/kufukuzwa; kushindwa. 2 kanyo, makatazo suffer a ~ rudishwa nyuma (vitani). repulsion n 1 kinyaa. 2 kurudishwa nyuma; kufukuzwa. 3 (phys) hali ya vitu kukimbiana/kutotangamana. repulsive adj. 1 -baya, chushi, -a kutia kinyaa, -a kukirihi. 2 -siovutia. repulsiveness n. repulsively adv.

reputation n sifa of good ~ -enye sifa

njema of bad ~ -enye sifa mbaya live up to one's ~ ishi kufuatana na sifa ya mtu. reputable adj -a sifa njema, zuri, -a kuheshimika. reputably adv. repute n sifa ill repute sifa mbaya a specialist of repute mtaalamu mashuhuri know somebody by repute fahamu mtu kwa sifa yake. vt be reputed as/to be julikana/sifika kwa (attrib.) adj -a kusifika, -a kujulikana, -enye kusemekana he is reputed to be the father inasemekana kuwa ndiye baba. reputedly adv.

request n ombi, matakwa by ~ kwa

maombi I have a ~ to make nina ombi. vt ~ something (from/of somebody); ~ somebody to do something taka, sihi, omba may I ~ you tafadhali ~ somebody's presence alika mtu, omba mtu ahudhurie.

requiem n ~ mass misa ya wafu.

require vt 1 (need) taka, hitaji whatever is ~d chochote kitakiwacho. 2 ~ something (of somebody); ~ somebody to do something; ~ that (often passive) (formal) shurutisha, taka kwa nguvu, amrisha, lazimisha. ~ somebody to do something shurutisha mtu kufanya jambo. ~ment n mahitaji, matakwa; masharti. requisite n. requisite (for) mahitaji adj -liotakiwa; lazima, -liohitajiwa. requisition n hali ya kuhitaji/kutaka/kulazimisha (jambo lifanywe); mahitaji rasmi (ambayo agh huandikwa) requisition order hati ya mahitaji. requisition (for) vt andika/peleka mahitaji. requisition somebody's services taka/hitaji huduma za fulani.

requite vt 1 ~ something/somebody (with something) (formal) lipa. 2 lipiza kisasi. requital n.

reredos n (church-altar) pambo la ukutani nyuma ya altare.

re-run n (cinema, TV) marudio (ya

kipindi, filamu, n.k.). vt rudia (filamu/ sinema/kipindi), n.k.

rescind vt (leg) tangua, futa, vunja,

batilisha. rescission n.

rescript n 1 agizo/tangazo rasmi (hasa litolewalo na mtawala). 2 agizo la Papa.

rescue vt ~ somebody from something/somebody okoa, saidia a ~ team kikosi cha waokoaji. n wokovu, msaada, kuokolewa. come/go to the ~/to somebody's ~ saidia, okoa mtu. ~r n mwokozi.

research n utafiti, uchunguzi ~ work

kazi za uchunguzi. vi ~ (into) chungua, tafiti. ~er n mchunguzi, mtafiti.

reseat vt 1 toa/pa/kiti kipya ~ a chair weka kitako kipya. 2 kaa tena.

resemble vt fanana, landa, shabihi they ~ each other wanafanana. resemblance n.

resent vt chukia, udhiwa, kasirikia, sonona he ~s her coming anachukia kuja kwake. ~ful adj -enye chuki, enye kero, -a kuudhi. ~fully adv. ~ment n uchungu, chuki, maudhi, hasira, mfundo.

reserve vt 1 weka akiba, limbika; ahirisha the judgement was ~d hukumu iliahirishwa; 2 setiri; bakiza, saza. 3 weka/shika/chukua nafasi. all seats ~d viti vyote vimechukuliwa. all rights ~d (leg) haki imehifadhiwa. ~d adj (person) kimya, -siyoonyesha hisia kwa urahisi. ~dly adv. reservation n 1 kusita, shaka; ajizi (ya kukubali jambo) accept something without reservation pokea kitu kwa moyo mkunjufu accept a plan with reservation pokea mpango kwa shaka. 2 (US) ardhi iliyohifadhiwa kwa matumizi maalumu the Indian reservation ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya Wahindi wa Asili. 3 (esp US) kuishika/kuchukua/kuweka nafasi agh. ya usafiri. n 1 akiba, limbiko ~ fund mfuko wa akiba a ~ player mchezaji wa akiba. 2 (mil) the R~ n askari wa akiba (ambao wako nje ya jeshi lakini wanaweza

kuhitajiwa wakati wowote). 3 hali ya kitu kuwekwa kama akiba. 4 hifadhi. game ~ n mbuga (za hifadhi ya wanyama) a forest ~ hifadhi ya msitu. 5 kizuizi. 6 haya, kimya ~ of manner mkimya. reservist n askari wa akiba/msaada.

reservoir n 1 hodhi, ziwa, bwawa, tangi la maji. 2 (fig) hazina.

reset vt 1 noa upya (msumeno, n.k.). 2

panga upya. 3 (printing) seti upya.

resettle vt,vi pa/pata makazi mapya.

reshuffle vt panga upya, badilisha, changanya ~ the personnel badilisha wafanyakazi ofisini ~ the cabinet badilisha baraza la mawaziri. n upangaji upya, ubadilishaji.

reside vt 1 ~ (in/at) ishi, kaa; -wa na nyumba/makao/makazi ~ abroad ishi ng'ambo. 2 ~ in (of power, rights) -wa mikononi mwa/chini ya. ~nce n 1 kuishi, kukaa nce area eneo la makazi. in ~nce (official) nyumbani; (of students) Chuoni. 2 nyumba. ~ncy n nyumba ya balozi, makao ya wageni (wa nchi). ~nt n 1 (inhabitant) mwenyeji, mkaaji, mkazi. 2 R~nt Balozi adj -a mkazi, -a kukaa, a kuishi. ~nt magistrate n hakimu mkazi. ~nt physician n daktari mkazi (katika eneo la hospitali). ~ntial adj -a kukaa watu, -a makazi the ~ntial part of the town eneo la makazi.

residue n mabaki, masalio, masazo,

machicha. residual adj -a masazo, residuary adj -liobaki, -a mabaki residuary clause ibara baki residuary legatee muusiwa wa mabaki/masazo.

resign vt,vi 1 ~ (from) jiuzulu; jitanibu. 2 ~ somebody/oneself ton somebody/something toa, weka mtu chini ya madaraka ya fulani. 3 ~ oneself to something/be ~ed to something kubali bila kulalamika, -wa tayari kukubali, kubali matokeo ya maisha. ~ed adj. ~edly adv. ~ation n 1 kujiuzulu, kuacha kazi, kujitoa. 2 hati ya kujiuzulu. 3 (submission, acquiescence) kukubali.

resolve

resile vi nyumbuka, nepa, nesa. resilience (also resiliency) n unyumbukaji, mnepo, kuvutwa. resilient adj -a kunepa, -a kunyumbuka; (of persons) imara/ thabiti; epesi kujirekebisha/kurudia hali ya awali.

resin n utomvu vt tilia/pakaza utomvu. ~ated -enye ladha ya utomvu; -liojaa utomvu. ~iferous adj -enye kutoa utomvu. ~ous adj -enye utomvu.

resist vt 1 pinga, kinza; bisha ~ arrest pinga kukamatwa. 2 stahamili, jizuia. 3 kataa kusalimu amri. ~er n mpingaji, mkinzani. ~less adj -sioweza kukinzika, -sioweza kukatalika. ~ance (to) n 1 (uwezo wa) upinzani (k.m. dhidi ya adui) they cannot overcome the enemy's ance hawawezi kushinda nguvu ya upinzani wa adui. ~ance movement n tapo/chama cha upinzani (dhidi ya maadui waliovamia nchi). 2 nguvu kinzi the boat failed to overcome the ~ance of the wind boti ilishindwa kukabili nguvu kinzi ya upepo. line of least ~ance uelekeo usio na nguvu kinzi kali; (fig) njia au mbinu rahisi zaidi. 3 uadui; uhasama. ~ant adj kinzani, -enye upinzani, kinzi. ~or n (phys) kikinzanishi: sehemu ya saketi inayopitisha umeme kwa shida.

resole vt tia soli mpya (kwenye kiatu).

resolute adj shupavu, imara, thabiti. ly adv. ness n. resolution n 1 hali ya kuwa shupavu/imara/ thabiti. 2 jambo lililoamuliwa, azimio. 3 utatuzi. 4 ahadi, nadhiri; nia, uamuzi (wa mtu, katika kufanya jambo). 5 mchanganuo, mgawo.

resolve vt 1 ~ to do something; ~ that...; ~ on/upon (doing) something azimu, nuia, kusudia, amua. 2 (of a committe, public meeting etc) amua kwa kupiga kura, pitisha. 3 tatua, maliza, komesha (kwa kutoa jawabu). ~ something (into something) vunja, gawa;

resonance

geuza, geuka kuwa the Parliament ~d itself into a committee Bunge liligeuka kuwa Kamati n azma, azimio, nia, kusudi, uthabiti, ushupavu. ~d adj -lioamriwa, -liokatiwa shauri, -liaozimiwa, -lionuia. resolvable adj. ~dly adv kwa uthabiti.

resonance n mvumo, mwangwi; (phon) sauti yenye kuendelea (kwa mtetemo). resonant adj 1 (of voice) fululizi (kwa mtetemo). 2 (of room) -a mwangwi, -a kuvuma. 3 (of places) -enye mvumo wa sauti. resonate vt,vi vuma, toa mwangwi.

resort vi ~ to 1 kimbilia, ishia, tumia

finally they ~ed to blows mwishowe waliishia kupigana makonde. 2 tembelea mara kwa mara n 1 msaada, kimbilio, tegemeo the only ~ msaada pekee uliopo. in the last ~; as a last ~ hapana budi; mambo yote mengine yakishindikana. 2 matembezi; mahali (maalum) pa kutembelea kutalii.

resound vt,vi ~ (with) 1 vuma na toa

mwangwi; paza sauti. 2 (of fame) enea pote, julikana pote; vuma ~ through the country julikana pote nchini. ~ing adj 1 -a mvuvumo, -a mwangwi. 2 kubwa sana a ~ing victory ushindi mkubwa sana. ~ingly adv.

resource n 1 njia, nguvu, shauri, mali. 2 (pl) mali, rasilimali; uwezo. natural ~s mali asili; rasilimali. 3 zana, msaada, nyenzo; kimbilio, tegemeo open new ~s tafuta njia mpya. 4 werevu, akili, burudani. ~ful adj -a akili, elekevu, -erevu, -a hekima. ~fully adv.

respect n 1 ~ (for) heshima, staha,

taadhima. have ~for somebody heshimu. 2 ~ (to) heshima, kuzingatia, upendeleo. pay ~ to zingatia, fikiria; heshimu; (for persons) upendeleo. (unaoambatana na ukwasi/hadhi/nasaba). 3 kuhusu. with ~ to kuhusu/juu ya. in this ~ kwa hili/haya in all ~s kwa jumla/hali zote. without ~ to bila

respond

kujali. 4 (pl) ~s n salamu my ~s to Joha nisalimie Joha pay one's ~s to somebody zuru/tembelea (kama ishara ya heshima). 5 namna, jinsi ya. in ~ of kulingana na, kuhusu. in some/any/ no ~s kwa kiasi fulani; kwa namna yoyote, hata kidogo. vt heshimu, stahi, jali, pendelea. ~ oneself jiheshimu. ~er n (only in) no ~er of persons n mtu/kitu kisicho na ubaguzi wowote. ~ing prep mintaarafu, kuhusu. ~able adj 1 -a heshima, zuri, nyofu, stahiki. 2 (moderate) -a kiasi, -a kadiri. ~ably adv. ~ability n maadili, unyofu, heshima. 3 (ironic use) -a kushika/kufuata desturi/mila. ~ful adj -stahifu, -a heshima, -a adabu. ~fully adv.

respective adj 1 -a pekee, -a kulingana na, kuhusiana na. 2 (relative) kwa kadiri ya/kwa kila (mhusika) they returned to their ~ homes kila moja alirudi kwake. ~ly adv mtawalia.

respire (formal) vt,vi pumua, tanafusi. respiratory adj -a pumzi resperatory diseases maradhi yanayohusiana na upumuaji. respiration n upumuaji, hali ya kutanafusi, mtweto. respirator n kipumulio.

respite n 1 ~ (from) nafasi ya kupumua, pumziko. 2 kukawiza, kuahirika katika adhabu vt ahirisha, -pa nafasi ~ a condemned person ahirisha kunyonga mhukumiwa kwa kitambo.

resplendent adj -zuri, -a kung'aa; -a

sherehe, -a fahari. ~ly adv. resplendence; resplendency n.

respond vi 1 ~ (to) (of church services) itika; itikia. 2 jibu. 3 ~ (to) (react to) shawishika, athirika, vutika; ongezeka, kubali, pokea he always ~s to kindness kila mara avutika na upole the plane ~s to the controls ndege inaendesheka vizuri kwa vyombo vyake. ~ent n (leg) mshitakiwa, mjibu mashtaka; mtetezi (wa tasnifu); mjibu (hojaji n.k.) adj -a kulingana; -a kujibia.

responsibility

response n 1 jibu, itiko bring no response toleta jibu lolote. 2 kiitikio, mkarara. responsive adj -a kujibu; -a kuitikia; -a kuvutika. responsiveness n.

responsibility n madaraka; jukumu; wajibu, dhima undertake ~ of chukua madaraka/dhima/wajibu a position of ~ kazi yenye madaraka be relieved of one's ~ pokewa/uzuliwa madaraka, vuliwa madaraka. rensponsible adj 1 -enye madaraka/wajibu/jukumu/dhima a responsible office kazi yenye madaraka mengi make oneself responsible for chukua dhamana. 2 (trustworthy) -aminifu; -ema. 3 be responsible for something wajibika, husika he is responsible for this mess ghasia hii ameileta mwenyewe.

rest1 n 1 pumziko, utulivu, raha; (sleep) usingizi take one's ~ pumzika; lala. at ~ tulivu; -liokufa. be laid to ~ zikwa. come to ~ simama, tua. set someone's mind/ fears to ~ tuliza mtu. ~-cure n matibabu ya mapumziko. ~-day n siku ya mapumziko. ~-home n makazi ya wazee. ~-house n nyumba ya mapumziko (kwa wasafiri). 2 ~-room n (US) msala. 3 kiegemeo. 4 kituo. 5 ~ing-place n mahali pa kupumzikia; kaburi. ~ful adj -a kutulia/kutuliza, -a kuliwaza. ~fully adv. ~fulness n. ~less adj -siotulia, -enye wahaka. ~lessly adv. ~lessness n. vi, vt 1 pumzika/ pumzisha, starehe/ starehesha. 2 tulia/tuliza God ~ his soul in peace Mwenyezi Mungu amweke mahali pema peponi. 3 ~ something on/upon/ against egemeza; egemea. ~ on one's oars acha kupiga makasia kwa muda; (fig) pumzika kwa muda. 4 ~ (something) on/upon tandawaa; tegemea (mtu/kitu); (of sight) elekeza na kukazia macho sehemu moja.

rest2 n the ~ 1 baki, salio; mwisho. and (all) the ~ (of it) na mengine

resurgent

yote. 2 (pl) wengine, vingine, nyingine. for the ~ kuhusu wengine/nyingine/vingine. vi 1 kaa, dumu ~ assured that I will do what I can usiwe na mashaka/kaa ukijua kuwa nitafanya kadiri niwezavyo. 2 ~ with -wa mikononi mwa it ~s with him ni juu yake, hiari yake, iko mikononi mwake.

restate vt taja/tamka tena/upya. ~ment n.

restaurant n mkahawa, hoteli ~-car

behewa mkahawa.

restrain vt ~ (from) zuia, rudisha. ~ed adj -liozuiwa. ~t n 1 kizuizi; kuzuia. be put under ~t (esp of a mentally ill person) wekwa katika hospitali ya vichaa. without ~t kwa uhuru; bila kuzuizi. 2 (of persons) self ~t kujihini. 3 (in art, literature) kutokuwa na mbwembwe.

restrict vt ~ (to) zuia, wekea mipaka, tilia amri/sharti, finya ~ed within narrow limits -liozuiwa katika mipaka finyu ~ed code sheria finyu; lugha finyu. ~ed area eneo marufuku kuingiwa. ~ion n kizuio, sharti; amri, mipaka. ~ive adj -zuivu, -a kuzuia. ~ive practices n (in industry) vikwazo katika uzalishaji (k.m. matumizi mabaya ya wafanyakazi, mali ghafi, zana, n.k). ~ively adv.

restructure vt unda/panga upya.

result n 1 matokeo, athari the ~s of the war matokeo ya vita without ~ bila matokeo. 2 jibu, jawabu. vi 1 ~ (from) tokana na, sababishwa na. 2 ~ in sababisha. 3 ishia. ~ant adj -a kutokea (pande zote) ~ant vector (math) vekta tokeo.

resume vt 1 endelea, anza tena, rudia tena ~ one's work anza kazi tena. 2 twaa/chukua tena ~ one's seat twaa/kalia kiti tena. resemption n.

resumé n ufupisho, muhtasari.

resurface vt 1 sakifu tena. 2 ibuka/tokeza tena.

resurgent adj -liofufuka, -liofufuka tena, -lioamka tena, -lioinuka tena.

resurrect

resurgence n.

resurrect vt,vi 1 fufuka; fufua. 2 ondoa kaburini, fukua, (colloq) chimbua. 3 rudisha, anzisha tena (jambo), tumia tena. ~ion n 1 the R ~ion n Ufufuo wa Yesu Kristo. 2 Ufufuko (wa wafu) the day of ~ion siku ya kiyama, siku ya kubaathiwa. 3 kufufua, kurudisha (desturi).

resuscitate vt,vi pata fahamu, rudishia fahamu; amsha, chochea. resuscitation n.

ret vt lowanisha (ili kulainisha).

retail n rejareja; uchuuzaji adj -a rejareja. vt,vi 1 ~ (at) chuuza, uza rejareja. 2 (circulate) eneza (uvumi). ~er n mwuuzaji rejareja.

retain vt 1 zuia; shika, weka. 2 (hire)ajiri (hasa wakili). 3 baki na, bakiza ~ somebody's services bakiza huduma ya mtu. ~er n 1 (arch) mtumishi (wa mtu mwenye cheo kikubwa/wa nyumbani) wa siku nyingi. 2 (lawyers' fee) ada ya wakili, ada ya awali. retention n kuzuia; kufunga, kuweka; kubakiza. retentive adj retentive (of) -a kushika, -a kufahamu. he has a retentive memory ana kumbukumbu nzuri. retentively adv. retentiveness n.

retake vt chukua/twaa/teka tena; piga (picha) upya/tena. n (esp. cinema, TV) onyesho lililopigwa picha tena.

retaliate vi ~ (against/ on/upon) lipiza kisasi ~ upon one's enemy lipiza kisasi kwa maadui. retaliation n. retaliative; retaliatory adj -a kisasi, -a kulipiza kisasi.

retard vt,vi 1 kawilisha, chelewesha. 2 vunja (punguza) mwendo, rudisha nyuma. 3 dumaa; dumaza, via; viza mentally ~ed person mtu aliyevia akili, -a akili taahira. ~ation n ucheleweshaji, mtindio, udumavu, taahira.

retch vi kokomoa, gooka the sight makes one ~ kuona kitu (fulani) kunaleta kugooka/kinyaa n ukokomoaji, ugookaji.

retouch

rethink vt,vi fikiri(a) tena/upya.

reticent adj nyamavu, -kimya, -a maneno machache be ~ on something -tosema mengi juu ya kitu. reticence n unyamavu, ukimya; hali ya kutosema maneno mengi.

reticulate vt gawa/gawanya katika miraba; fanya, panga/kama wavu/ kimia adj -a kimia, -a wavu; -a mtandao. reticulation n mpangilio/ mfumo unaofanana na wavu/kimia; mtandao.

reticule n (arch) kifuko, kipochi,

kibegi cha mwanamke.

retina n retina: sehemu inayopokea

nuru ndani ya jicho.

retinue n jumla ya watu (wanaoandamana na mkubwa), msafara.

retire vt,vi 1 ~ (from); (to) jitoa, ondoka. 2 ~ (to bed) (formal) enda kulala she ~s at 10 o'clock analala saa nne usiku. 3 (of an army) rudi; rudisha; jiondoa ~ an imprest rudisha masurufu; (of an army) rudi nyuma, jiondoa vitani. 4 staafu; ng'atuka; staafisha the manager was ~d meneja alistaafishwa. 5 ~ from the world ingia utawa/usufii, jitenga na mambo ya kilimwengu. ~ into oneself zama katika mawazo, ishi kipekee n (army) ishara ya kurudi nyuma. ~d adj 1 (aliye) staafu a ~d officer ofisa mstaafu/aliyestaafu. 2 -enye kujitenga; pweke, kimya. retiring adj -a kujitenga. ~ment n kustaafu; kujitenga go into ~ment staafu, ingia utawani.

retool vt weka vifaa vipya katika kiwanda.

retort1 vt,vi 1 jibu vikali, rudisha maneno, itika kwa ukali ~ an argument jibu hoja. 2 (rare) lipiza kisasi, rudishia tendo. n jibu kali.

retort2 n 1 kigida (chenye shingo ndefu), chombo cha kutoneshea. 2 chombo cha kutakasisha zebaki na kutengenezea gesi.

retouch vt (of photograph, painting

etc.) sahihisha; rekebisha kwa

retrace

burashi.

retrace vt 1 fuatilia/fuata nyuma; rudi ulikotoka he ~d his steps alifuatilia nyayo zake. 2 rudia mambo yaliyopita.

retract vt,vi 1 futa (usemi, kauli, wazo n.k.). 2 rudisha, rudi a snail can ~ its horns konokono anaweza kurudisha ndani pembe zake. ~able adj -a kuweza kurudi ndani. ~ile adj 1 -a kurudishika ndani. 2 -a kufumbatika, -a kuweza kurudishwa nyuma. ~ion n hali ya kurudi nyuma/ndani.

retread vt tia tredi upya. n tairi lililotiwa tredi upya.

retreat vi ~ (from); (to) kimbia; rudi nyuma. n 1 kurudi nyuma. 2 ishara ya kurudi nyuma sound the ~ rudisha nyuma askari (kwa kutoa ishara). 3 utoaji wa ishara hiyo beat a (hasty) ~ (fig) jiondoa, kimbia, acha kufanya jambo. 4 (refuge) kimbilio; mahali pa raha/usalama/ faragha. 5 kujiondoa kwa muda; (rel) mfungo go into ~ funga.

retrench vt,vi punguza (gharama), bana matumizi. ~ment n kubana matumizi.

retribution n rada, adhabu (anayostahili mtu), malipo. retributive adj -a kulipa, -a rada, -a kupatiliza, -a kuadhibu. retributively adv.

retrieve vt,vi 1 pata tena. 2 rekebisha, hidi. 3 ~ (from) okoa, rudisha; stawisha. 4 (of trained dogs) tafuta na kurudisha. retrievable adj -enye kuweza kupatikana tena. retrieval n upatikanaji tena. ~r n mbwa wa msasi.

retro- pref. kuelekea nyuma, kinyumenyume, -nyuma.

retroactive adj (of laws,etc) see retrospective.

retroflex adj 1 -liopindika/-lioelekea

nyuma, akisi. 2 -liobinuka, (phon.) -a kubinua ulimi.

retrograde vi rudi chini/nyuma; wa

baya zaidi adj -a kurudi nyuma/chini;

return

-lioelekezwa nyuma.

retrogress vi rudi nyuma; enda kinyumenyume. ~ion n. ~ive adj -a kurudi nyuma; -enye kuelekea kurudi nyuma.

retro-rocket n roketi saidizi (ya kupunguza mwendo au kurekebisha njia ya chombo au bomu angani).

retrospect n kuwazia/kukumbuka mambo ya zamani. in ~ ona/fikiria ya zamani n hali ya kutazama yaliyopita. ~ive adj 1 -a kutazama nyuma, -a kuhusu mambo ya nyuma, -liotangulia, -liopita. 2 (of laws, etc.) -a kuanzia nyuma. ~ively adv.

retrousse adj -lioelekezwa juu (hasa

pua), -lioinukia mwishoni.

retroversion n kugeuka nyuma; kuelekezwa nyuma.

return vt,vi 1 ~ (to); (from) rudi,

rejea; rudisha. 2 ~ to rudia (hali ya kwanza) ~ to dust rudi mavumbini, -wa mavumbi. 3 (reply) jibu, itika ~ somebody's greeting jibu salamu. 4 (repay) rudisha, lipa. ~ thanks toa shukurani (k.m. kusali kabla ya kula). ~ed empties n chupa, kreti, n.k. tupu zilizorudishwa. 5 (give account of) toa (hesabu, hukumu, faida, n.k.). 6 (of constituency) chagua mbunge/ mwakilishi. ~ing officer n msimamizi (wa kura). ~able adj -a kurudishika. n 1 kurudi au kurudishwa, kuja; kwenda; kutoa, kupeleka. by ~ kwa posta inayofuata. on sale or ~ kwa kurudishwa iwapo haitauzwa. point of no ~ -sioweza kurejea au kurejeshwa nyuma tena. many happy ~s heri ya sikukuu (ya kuzaliwa). in ~ (for) kama malipo (ya). 2 hali ya kwenda au kurudi. ~ ticket n tikiti ya safari kwenda na kurudi. ~ match n mchezo wa marudiano. ~ fare n nauli ya kwenda na kurudi. 3 (often pl) faida toka kitegauchumi au biashara. 4 taarifa rasmi (itolewayo kwa kufuata agizo maalumu) annual ~s ripoti ya

reunite

mwaka.

reunite vi,vt kutana/kutanisha tena; ungana/unganisha tena; patana/ patanisha, suluhisha. reunion n kurudiana, kupatana, kuunganika tena a family reunion kukutana kwa familia yote (katika siku maalumu).

rev (abbr) revolution. ~ (colloq) ongeza mwendo wa mzunguko (wa injini).

revalue vt thaminisha upya; ongeza

thamani ya fedha. revaluation n.

revamp vt piga jeki, fufua, inua; (colloq) tengeneza/fanya upya.

reveal vt ~ (to) 1 funua, onyesha. 2

gundua (jambo jipya), fichua. ~ed religion n dini iliyoletwa na Mungu. revelation n ufunuo. (Bible) the Book of Revelation Ufunuo. 2 hali ya kudhihirisha kitu kilichokuwa siri/fumbo; kitu kilichodhihirishwa.

reveille n kizinduzi, tarumbeta (ya kuamsha watu, hasa jeshini).

revel vi 1 furahia, shangilia. 2 ~ in

sherehekea. n sherehe, tamasha, shangwe. ~ler n mtu asherehekeaye. n shamrashamra; makelele na vifijo vya sherehe.

revenge vt 1 lipiza kisasi. 2 be ~d on somebody; ~ oneself on somebody jilipiza kisasi. n 1 ulipizaji kisasi. get/take one's ~; take ~ on somebody (for something); have/get one's ~ (on somebody) (for something); do something in/out of ~ (for something) lipiza kisasi. 2 hali ya kulipiza kisasi. 3 (in sports) nafasi ya kulipiza kisasi. give somebody his~; get/take one's ~ -pa mtu nafasi ya kurudia. ~ful adj. ~fully adv.

revenue n 1 mapato; maduhuli; (public) mapato ya serikali (kwa kodi), ushuru ~ officer afisa mapato/ ushuru. 2 vitu mbalimbali vya mapato vikiwa pamoja.

reverberate vt,vi (of sound,) 1 fanya mwangwi tena na tena, vumavuma, nguruma, rindima. 2 (of light) akisi. reverberant adj. reverberation n

review

(pl) miangwi; (fig) athari. reverberator n. reverberatory adj.

revere vt heshimu sana, stahi sana; -cha, tukuza. ~d adj 1 mahashumu, -enye kustahili heshima. 2 the R~nd mchungaji, padri, mheshimiwa. ~nce n 1 heshima kuu; uchaji; unyenyekevu. 2 (arch) ishara ya kuonyesha unyenyekevu mkubwa/kutoa heshima. ~nt adj -a kustahi sana. ~ntial -enye kusababishwa (na) heshima; -ingi -a heshima/staha. ~ntly adv.

reverie n 1 njozi, ruya. 2 muziki wa

njozi/maliwazo.

revers n pinduo: sehemu ya mbele ya ukosi wa koti iliyo karibu na vifungo.

reverse vt,vi 1 pindua, geuza. a ~d

charge n gharama kwa mpigiwa (simu). ~ arms (mil) mtutu chini. 2 rudi/rudisha nyuma. 3 tangua, batilisha. reversible adj -a kupindulika, -a kutumika kuwili. reversibility n. reversal n 1 kupindua, upinduaji. 2 hali ya kupindua adj ~ reversal (to/of) -a kinyume, -a nyuma. in ~ order kuanzia mwisho, nyuma mbele. ~ly adv. n 1 the ~ of kinyume. 2 the ~ (of) nyuma. 3 kitu cha kurudishia nyuma (k.v. gia ya nyuma). 4 ushinde, mkosi.

revert vi 1 ~ (to) rudi, rejea, rudia hali ya kwanza. 2 (leg) rudi (kwa mwenye mali wa kwanza). ~ible adj. reversion n 1 hali ya kitu kurudi kwa mwenye mali. 2 haki ya kumiliki mali katika mazingira fulani maalumu; kitu kimilikiwacho katika mazingira hayo. 3 hali ya kitu kurejea katika hali yake ya awali (k.m. mimea). reversionary adj.

revetment n 1 safu (tabaka, utando) ya

mawe (ya kuzuia, kuimarisha) ukingo. 2 ukuta. revet vt imarisha/zuia kwa mawe.

review vt,vi 1 angalia/fikiri/tafakari/ pitia upya come under ~ chunguzwa/kaguliwa. 2 kagua rasmi

revile

(majeshi, n.k.). 3 pitia maandishi, chambua, hakiki n 1 kutafakari/ kuangalia upya. 2 ukaguzi (wa majeshi). 3 jarida/gazeti la mambo ya leo. 4 uhakiki; mapitio; muhtasari the book under ~ kitabu kinachohakikiwa, n.k. 5 kitendo cha kutafakari jambo (k.m. maisha ya mtu mwenyewe). ~er n mhakiki.

revile vt, vi ~ at/against tukana, shutumu, laani. ~r n. ~ment n.

revise vt 1 fikiria tena; pitia (ili kusahihisha na kufanya bora zaidi). the R~d Version nakala ya Biblia iliyofanywa 1870-84 ikiwa ni masahihisho ya tafsiri ya Biblia iliyofanywa 1611. n nakala iliyosahihishwa. 2 (alter) geuza, badili, tengeneza. ~r n msahihishi. revision n kurudia masomo (k.m. kabla ya mtihani); masahihisho. revisionist n mbadilishaji wa itikadi ya siasa. revisionism n.

revive vt,vi 1 fufua; fufuka; huisha. 2 rudisha, anzisha, amsha; anza kutumika tena. revival n 1 ufufuaji. 2 uhuishaji, uamshaji, urudishaji (hali ya zamani). revivalist n. revivify vt rudishia nguvu/uzima, huisha; amsha. revivification n.

revoke vt,vi batilisha, tangua, futa,

kanusha. revocable adj -a kufutika, -a kutangulika, -a kubatilika. revocation n utanguo, batilisho.

revolt vi,vt 1 ~ (against) asi. 2 ~ (against/at/from) chukizwa, nyarafiwa, kirihishwa. 3 kirihi, chusha. n uasi, maasi. ~ing adj -a kuchukiza, -a karaha. ~ingly adv kwa namna ya kuchukiza.

revolution n 1 mapinduzi. ~ary adj -a mapinduzi, -a kimapinduzi ~ary spirit imani ya kimapinduzi ~ary movement tapo la kimapinduzi. ~ist n mwanamapinduzi. 2 mzunguko. ~ize vt 1 fundisha kanuni za kimapinduzi, fanya mwanamapinduzi. 2 pindua, badili kabisa.

revolve vt,vi 1 ~ (about/ around)

zunguka; zungusha. 2 (consider)

rhubarb

tafakari.

revolver n bastola.

revue n maonyesho (ya ngoma, nyimbo, vichekesho, n.k.).

revulsion n 1 mageuzi ya fikira. 2 ~

(against/from) (disgust) machukio, makuruhu.

reward n 1 thawabu, jaza; zawadi,

tuzo. 2 kiokosi, machorombozi, utotole, kiangaza macho. vt ~ somebody (for something) -pa (mtu) zawadi (kwa..), zawadia, tuza; -pa thawabu may God ~ you Mungu akujaze heri.

rewire vt weka/suka/tandaza nyaya upya.

rewrite vt 1 andika upya. 2 ~ as (ling) andika/fasiri kama... . n (colloq) maandishi yaliyoandikwa tena (attrb.) a ~ man msanifu maandishi.

rhapsody n 1 maneno ya kuonyesha

furaha/shauku, sifa/maneno ya nderemo. 2 (music) tungo isiyokuwa na ulinganifu/isiyofuata kanuni. rhapsodize (about/over/on) vi sema/andika kwa shauku/furaha, sifia sana, husudu.

rheostat n reostati: kidhibitiumeme.

rhesus n (North India) ngedere mdogo mwenye mkia mfupi.

rhetoric n 1 balagha: elimu ya usemaji. 2 (eloquence ) ufasaha wa kusema. 3 chuku. ~al adj 1 -enye balagha, -a usemaji, -a ufasaha. 2 (not serious) -a kutia madoido tu. ~al question balagha, swali lisilodai jibu. ~ian n mgambi, mbalagha.

rheum n (arch) majimaji yatokayo machoni au puani k.m. makamasi.

rheumatism n baridi yabisi, ongo, viungo. rheumatic adj.

rhinal adj -a pua.

rhinoceros (abbr rhino) n kifaru.

rhizome n (bot) rizomu: shina ukoka (k.m. tangawizi).

rhomb/rhombus n msambamba sawa. rhomboid adj.

rhubarb n 1 aina ya mmea ambao majani yake huliwa kama tunda. 2

rhyme; rime

(colloq) upuuzi. 3 mabishano.

rhyme; rime n 1 kina without ~ or reason bila maana, puuzi. 2 mashairi ya vina nursery ~ mashairi/beti za watoto. 3 neno lifanyalo kina. 4 matumizi ya vina. vt, vi 1 fanya mashairi ya vina. 2 -wa na sauti sawa mwishoni. 3 weka pamoja ili kujenga vina. ~ster n mshairichapwa.

rhythm n 1 wizani; mfuatano wiano wa mkazo mkali na hafifu wa lafudhi, sauti; mahadhi n.k. (katika usemaji, muziki, dansi, n.k.). 2 mifuatano maalumu ya namna hiyo. ~ical adj -enye mahadhi (mapigo, mdundo, mwendo) safi.

rib n 1 ubavu. dig/poke somebody in the ~ tekenya. 2 (of ship) taruma. 3 (of coconut leaf) ujukuti. 4 (of leaf) mshipa, chelewa. vt 1 chana, nyambua. 2 (US colloq) kefyakefya, tania; tekenya.

ribald adj pujufu, safihi. n mpujufu,

mwenye mdomo mchafu. ~ry n mizaha, maneno ya upujufu/usafihi.

riband n (old use) ribbon.

ribbon n 1 utepe, riboni white ~ jandani. 2 ugwe matambara. 3 ~ development n msururu wa majumba sambamba na barabaraba kuu.

rice n (paddy/unhusk) mpunga, sena, bungala; (cooked) wali; (burnt layer at the bottom of the pot) ukoko; (burnt layer on top of cooked rice) matandu; (ground) ubwabwa; (husked) mchele, mashendea. ~ paper n (Chinese) karatasi la sanaa. ~-water n maji ya mchele.

rich adj 1 tajiri, -kwasi, -enye mali. 2

-a gharama; -a fahari. 3 ~ in -enye neema, -enye kutoa/kuzaa kwa wingi. 4 (soil) -enye rutuba nyingi. 5 (of colours, sounds) kali, -enye nguvu. 6 (of food) -enye mafuta mengi; -tamu sana, -enye ladha nzuri. 7 (abundant) -ingi, tele ~ in minerals -enye madini tele. 8 (colloq) -a kuanisi that is ~! yachekesha sana. ~ly adv. ~ness n utajiri. ~es n (pl) 1 mali, utajiri, ukwasi. 2 wingi, neema amass

ride

great ~es kusanya mali nyingi.

rick1 n lundo/kitita cha majani ya ng'ombe, farasi, mbuzi, n.k. (yaliyokatwa na kuhifadhiwa pamoja) ~ of corn lundo la mahindi ~ of hay kitita cha majani makavu. vt tita, fanya chungu, lundika.

rick2 vt see wrick.

rickets n matege, nyongea.

rickety adj dhaifu (hasa katika viungo) ~ old car mkweche.

rickshaw n riksho.

rid vt ~ of safisha, ondoa. be/get ~ of ondoa, toa; epuka. ~dance n (US) a good ~dance afadhali their departure was a good ~dance afadhali wameondoka.

riddle1 n 1 kitendawili; fumbo. 2 mtu/ kitu/jambo/hali ya kushangaza/ kutatanisha.

riddle2 n (sieve) chekecheke, chungio, kung'uto. vt 1 chekecha, chunga; kung'uta. 2 ~ (with) toboa (k.m. kwa kupiga risasi); chomachoma ~ with bullets toboa kwa risasi. be ~d with jawa na.

ride n (of a car, bicycle, horseback)

1 kupanda; usafiri (wa kupanda) ~ a child on one's shoulders beba mtoto mabegani. take somebody for a ~ (colloq) danganya/laghai mtu. 2 njia ya farasi na watu (hasa ipitayo katika pori). vi,vi 1 panda/ enda/chukuliwa kwa (farasi, baiskeli, n.k.), endesha. ~ for a fall endesha kwa fujo; (fig) omba maafa, fanya vitendo vinavyoweza kusababisha maafa au kushindwa. 2 shindana katika mbio za farasi/baiskeli. 3 ~ on panda, kaa kwa kutagaa/kutenganisha miguu kama mpanda farasi. 4 beba mtu mabegani (kwa kuning'iniza miguu yake shingoni). 5 (of a jockey or other person) -wa na uzito (fulani wakati wa kupanda farasi). 6 fanya matembezi/mazoezi kwa farasi. ~ to hounds enda kuwinda mbweha. 7 (of ground, etc) -wa katika hali fulani ya kuendesha farasi the

ridge

ground rode hard after the frost uwanja ulikuwa mgumu baada ya jalidi. 8 elea baharini. ~ out a storm (of a ship) toka salama/okoka katika dhoruba. (fig) salimika, okoka kutoka kwenye matatizo, shambulio, n.k. let it ~ (colloq) acha jambo liende bila kulijali/kulishughulikia; acha mambo yalivyo. 9 ~ somebody down fukuza mtu kwa farasi hadi kumfikia; angusha kwa farasi. 10 ~ up (of an article of clothing) ruka. ~able adj. ridden (pp of ride) (esp. in compounds) 1 -liojawa na ridden by fears jawa na hofu. 2 - liotawaliwa/sumbuliwa/ nyanyaswa na priest ridden wanaonyanyaswa na mapadri police ridden wanaonyanyaswa na polisi. riding-breeches n pl suruali za mpanda farasi. riding-habit n vazi la kike la kupandia farasi. riding-light/lamp n taa ya meli inapotia nanga. riding master n mwalimu wa wapandafarasi.

ridge n 1 mgongo, kigongo, utiko. ~ pole n mtambaapanya wa hema. ~ tile n kigae cha mgongo wa paa la nyumba. 2 (of hills) mgongo wa safu vilima/milima/sehemu ndefu iliyoinuka. 3 mstari wa sehemu iliyoinuka inayotenganisha mito. 4 (of farming) tuta.

ridicule vt dhihaki, fanyia mzaha;

kebehi, beza. bezo; mzaha; dhihaka. hold up to ~ dhihaki. lay oneself open to ~ jiaibisha, fanya vitendo vya kubezwa/kudharauliwa. ridiculous adj.

rife adj (pred only) 1 -liotapakaa/enea kote. be ~ tapakaa. 2 ~ with -liojawa na/enea.

riff n msemo unaotumika sana katika muziki.

riffle vt,vi 1 changa karata. 2 pindua karatasi upesiupesi. ~ through something changa, geuza upesiupesi agh. kurasa.

riff-raff n the ~ wahuni; makabwela; watu wasioheshimika (kutokana na

right

tabia mbaya).

rifle1 vt chakura, pekua (ili kuiba).

rifle2 n bunduki; bunduki kubwa

yenye mifuo; (pl.) kikosi cha askari wa bunduki. ~-range n uwanja wa kujifunzia shabaha; mtupo wa risasi. ~-shot n mtupo wa risasi; mpiga bunduki mwenye shabaha. ~ man n askari wa kikosi cha bunduki.

rift n 1 ufa, mwatuko, mpasuko. ~-

valley n bonde la ufa. 2 (of friends) ugomvi.

rig1 vt fanya hila ~ an election pata

ushindi katika uchaguzi kwa hila ~ the market fanya hila katika ununuzi/uuzaji wa hisa (ili kupata faida isiyo halali).

rig2 vt,vi 1 ~ (with) (a ship) weka/patia (meli) mlingoti/tanga; -wa na vifaa hivyo; -andaa kwenda baharini na vifaa hivyo. 2 ~ somebody out/in with something -pa mtu nguo/vifaa vinavyotakiwa; (colloq) nguo, mavazi (ya mtu). ~ something up unganisha, rekebisha kitu; tengeneza. n 1 (of a ship) mpangilio wa mlingoti, tanga, n.k. 2 mtambo, vifaa vilivyowekwa pamoja kwa madhumuni maalumu. test-~ n mahali/mtambo wa kujaribia magari. 3 (colloq) mtindo wa mavazi; namna mtu aonekanavyo kutokana na mavazi yake. ~ging n kamba za melini zinazoshikilia tanga na mlingoti. ~ger n mfunga kamba melini; mwunda ndege.

right1 adj (contrasted with wrong)

1 (of conduct, etc) nyofu, adilifu, -ema. 2 -a kweli, sawa, halisi, sahihi. get something ~ elewa sawasawa. put/set something ~ rekebisha, sahihisha. R~ you are!/R~o! R~! int (colloq) sawa!/ kabisa! All ~/Al~ int. vema! vizuri sawa! ~ minded adj -enye mawazo mazuri/misingi mizuri, -enye akili timamu. 3 -a kufaa, -enye afadhali, -a heri he is the ~ man for the job anafaa kwa kazi hii she is on the ~ side of 40 hajafika miaka arobaini.

right

get on the ~ side of fanya kupendwa/kupendelewa na. 4 (all) ~ zima. not (quite) ~ in the/ one's head -enye wazimu (kidogo), haziko sawa. not in one's ~ mind haziko sawa. ~ as rain/as a trivet (colloq) mzima, safi kabisa. 5 (of an angle) -a pembe mraba. ~ly adv kwa kweli/ haki, kwa usawa, inavyotakiwa. ~ness. n, adv 1 hasa; moja kwa moja. ~ away/off mara moja; moja kwa moja. ~ now kwa sasa; sasa hivi. ~ on! int (colloq) sawa! hasa! 2 kwa usahihi if I remember ~ kama nakumbuka vizuri. it serves him ~ ni haki yake; inamstahilia. 3 sana; kabisa. ~-down adj, adv (more usu down ~) kabisa. n 1 haki, ukweli. be in the ~ -wa mkweli na mwenye haki. 2 haki she has no ~ hana haki. by ~ of kwa sababu ya, kutokana na. in one's own ~ kwa haki/uwezo wake mwenyewe. ~ of way n haki ya kutumia njia (ya jumuia/umma) (in road traffic) haki ya kupita barabarani. by ~ (s) kwa kufuata haki. human ~s n haki za binadamu. women's ~s n haki za wanawake. stand on/assert one's ~s tetea haki. 3 (pl.) hali halisi. put/set things ~ rekebisha, nyoosha. ~s and wrongs ukweli. vt tengeneza/ sahihisha/rekebisha kuwa sawa; simamisha (wima) that fault will ~ itself tatizo hili litajirekebisha lenyewe. ~ the helm (of ship) weka katikati; elekeza mbele. ~eous adj 1 adilifu, -a kutii amri. 2 -enye kukubalika kimaadili, -enye haki. ~ously adv. ~ousness n.

right2 adj (contrasted with left) -a kulia; -a kuume. one's ~ hand/arm (fig) msaidizi mkuu, mwenzi. ~ hand adj -a bidii/nguvu zote put one's ~ hand to the work fanya kazi kwa bidii/nguvu zote. ~-handed adj (of a blow, etc) -a kulia. ~ hander n anayetumia mkono wa kulia/kuume; (of a blow, etc) -a kulia; kofi la mkono wa kulia. ~ turn geuka

ring

kulia. ~ about turn/face geuka nyuma kwa kupitia mkono wa kulia adv kwa upande wa kulia. (mil) Eyes ~! macho kulia!. n 1 (upande wa) kulia, kuume. 2 (politics, usu the~) mrengo wa kulia: chama/vyama visivyopenda mabadiliko/ vinavyopinga mabadiliko. ~ist n mwanachama wa chama cha mrengo wa kulia adj -a mrengo wa kulia.

rigid adj 1 -siopindika/kunjika, gumu, imara. 2 (severe) gumu; -siobadilika/ badilishwa, -isioshawishika. ~ness n ugumu, ukavu, uimara; hali ya kutoshawishika vinginevyo. ~ly adv.

rigmarole n 1 mapayo, upuuzi, porojo. 2 utaratibu wa kuchusha/kutatanisha.

rigour;rigor n 1 ukali/ugumu (wa)

kufuata sheria; msimamo. 2 hali ngumu. ~mortis n ukakamaaji wa misuli (baada ya kufa). ~ous adj kali. ~ously adv.

rile vt (colloq) kasirisha, ghadhibisha, kera, udhi it ~d me ilinikasirisha.

rill n kijito.

rim n (of wheel) rimu; ukingo, mzingo; (of spectacles) fremu. red ~med adj -enye macho mekundu. vt tia/wekea ukingo/rimu; kuwa rimu ya kitu.

rime1 jalidi vt gandisha. rimy adj.

rime2 n see rhyme.

rind n ganda, gome, (of squeezed fruit) kaka. vt menya.

rinderpest n sotoka (maradhi ya ng'ombe).

ring1 n 1 pete nose-~ hazama ear-~

hereni, kipuli lip-~ ndonya. ~ finger n kidole cha pete. 2 kizingo, kipete, kishikizo key ~ kishikizo cha funguo ~ mail, ~ armour ngao ya pete, deraya. 3 duara. run/ make ~s round somebody zidi sana kwa kasi, ubora wa kufanya mambo. 4 jamii, kundi, genge la watu wafanyao kazi kwa pamoja kwa manufaa yao a ~ of thieves genge la wezi. 5 ulingo boxing ~ ulingo wa masumbwi. ~ master n

ring

kiongozi wa kikundi cha wachezaji (hasa wa sarakasi). 6 uwanja (wa maonyesho ya mifugo). 7 (compounds) ~ road n barabara (inayozunguka nje ya mji). ~-side n kando ya ulingo. ~worm n choa, baka, bato. ~-leader n kiongozi wa waasi/maasi/jambo baya. vt,vi 1 zingira. 2 visha pete. 3 tupa shilingi. 4 (of a hunted fox) kimbia kwa kuzunguka. ~let n 1 msokoto, songo la nywele. 2 pete ndogo. ~ed adj.

ring2 vt,vi 1 vuma; lia the telephone rang simu ililia. 2 ashiria, leta athari fulani baada ya kusikika, onyesha dalili. ~ true ashiria ukweli. 3 piga kengele ya tahadhari. ~ (for) ita kwa kengele. 4 piga/liza (kengele) ~ the alarm piga kamsa. ~ the bell (colloq) faulu katika jambo. ~ a bell leta kumbukumbu kwa mbali. 5 vuvumka, jaa. 6 baki (katika masikio/ kumbukumbu). 7 ~ (with) (of the ears) wangwa ears are ~ing masikio yanawangwa. 8 ~ somebody (up) pigia simu, wasiliana kwa simu. ~ off maliza mazungumzo ya simu, kata simu. 9 (of a chime of bells) tangaza (saa, kipindi, n.k). 10 toa ishara (kwa kupiga kengele, n.k. 11 ~ the changes (of church bells) piga kengele kwa namna mbalimbali; (fig) fanya/weka au panga vitu kwa namna mbalimbali. 12 tangaza au sherehekea kuanza au kwisha kwa jambo fulani (kwa kupiga kengele). n 1 sauti au mlio wa kengele (au chuma) ipigwapo. 2 (sing only) sauti kubwa na yenye kusikika. 3 kitendo cha kutoa sauti kama kengele. ~er n mpiga simu/kengele; ala ya kupigia kengele.

rink n kiwanja maalum cha barafu cha kutelezea.

rinse vt 1 ~ something (out); ~ something out of something suuza, osha kwa maji safi; (the mouth) sukutua. 2 ~ something down telemsha (kwa kinywaji). n 1 kusuuza. 2 rangimaji (ya kubadilishia

rise

rangi ya nywele). rinsing n.

riot n 1 ghasia, fujo. the R~ Act n sheria ya kuzuia fujo read the R~ Act soma sheria hii mbele ya wafanya fujo; (joc) kemea sana. run ~ fanya fujo; (of plants) tanda haraka sana. 2 makelele, vurugu. 3 (profusion) a ~ (of) wingi; mvuvumko. 4 a ~ (of) kujiachia. 5 jambo linaloleta shauku kubwa, jazba, ghasia ~ in furaha. ~er n mfanya fujo. vi fanyafujo/ghasia. ~ous adj. ~ously adv. ~ousness n.

rip vt 1 pasua; pasuka; raruka; tatuka ~ open pasua. ~ something/ somebody off iba; ibia, ghilibu, tapeli. ~off n utapeli, wizi. ~-cord n ugwe wa mwavuli wa kurukia (ambao ukivutwa mwavuli hufyatuka na kujaa hewa). 2 kata kwa msumeno (mti, n.k.) kwa kufuata uelekeo wa nyama zake. ~ saw n msumeno wa kufanyia kazi hii. 3 (of material) chana/chanika. 4 endesha upesi; enda kwa kasi. let things ~ acha kuvidhibiti; acha mambo yaende kwa namna yake. n mpasuko mrefu; mahali palipopasuka. ~-roaring adj -a makelele, -a ghasia, -a vurumai.

ripe adj 1 (of fruit) -lioiva, bivu; (of grain) -liokomaa; (of drink) -lioiva. 2 -liokomaa/pevuka. 3 ~ for tayari. ~ly adv. ~n vt,vi iva/ivisha; pevuka/pevusha; komaa/komaza. ~ness n ubivu; upevu; (perfection) ukamilifu.

riposte n 1 jibu kali. 2 (in fencing)

kukinga/kurudishia kwa haraka (baada ya kukwepa upanga). vi toa jibu kali/ hima.

ripple n 1 kiwimbi, lembelembe. 2

mlio wa wimbi. 3 (of sound) sauti/ kicheko cha kimawimbi. vt,vi 1 lia kama wimbi. 2 -wa na viwimbi, fanya viwimbi adj.

rip-tide n mkondo mkali.

rise vi ~ (up) 1 (of the sun, moon)

chomoza, tokeza 2 inuka. 3 amka,

risible

toka kitandani. 4 (from the dead) fufuka. 5 panda, inukia, enda juu. the rising generation n kizazi kinachoinukia. rising twelve (of a person's age) karibia miaka kumi na miwili. high ~ adj -enye maghorofa. 6 ongezeka (nguvu). 7 ibuka. 8 onekana juu ya uso wa nchi kwa mbali (k.m. vilima); tokeza. 9 panda cheo/hadhi n.k. 10 ~ to weza kukabili. ~ to the occasion weza kukabili hali. 11 (of slope) panda. 12 anzia. 13 ~ against asi. rising n maasi. ~ n 1 mwinuko, kilima, kituta. 2 ongezeko (k.m. katika thamani, ukubwa, joto, n.k.). 3 (lit) kuchomoza, kutokeza (agh. kwa jua). 4 kuibuka kwa samaki, kuja juu ya maji. get/take a ~ out of somebody ginginiza/chokoza/fanyia mzaha hadi kumuudhi. 5 mwanzo, asili. give ~

to sababisha, -wa chanzo. ~r n 1 mwamkaji. an early ~r n mwamkaji mapema. 2 sehemu ya wima ya ngazi (inayounganisha vidatu viwili).

risible adj -a kucheka; -a kuchekesha. risibility n

risk n 1 hatari, mashaka. run/take ~s/ a ~ fanya mambo ya hatari; bahatisha; thubutu to succeed you must take ~s ili ufanikiwe sharti uthubutu. run/take the ~ of doing something -wa na dhima, chukua jukumu. at ~ -enye mashaka. at the owner's ~ juu ya mtu mwenye mali. one's own ~ juu yake mwenyewe. 2 (insurance) kiasi/thamani ya bima; kiasi ambacho mtu/kitu kimelipiwa bima; mtu au kitu kilicholipiwa bima. vt hatarisha, bahatisha, jasiri I will ~ it hasara juu yangu. ~y adj -enye hatari. ~iness n hatari, jukumu. ~ily adv.

risque adj -nayoweza kuudhi/ kuaibisha.

rite n kanuni, kaida ya dini; ada, ibada traditional ~ tambiko initiation ~s jando, unyago. ritual n 1 kaida za dini, (taratibu za) ibada; tambiko. rituals n matambiko. 2 taratibu adj -a

road

kanuni kaida. ritualism n. ritualist n. ritualistic adj.

ritzy adj (sl) malidadi.

rival n mshindani; mpinzani adj shindani; pinzani. vt shindana, taka kupita (kushinda); jaribu kuwa sawa na. ~ry n ushindani.

rive vt,vi chana, pasua, tatua.

river n 1 mto. sell somebody down the ~ (fig) saliti mtu. 2 ~ head chanzo; chemchemi. ~-bed n chini ya mto. ~ basin n bonde la mto. ~ bank n ukingo wa mto. ~ side n kando ya mto. ~ horse n kiboko. 3 gharika, mafuriko makubwa (k.m. ya lava ya volkeno); kububujika kwa wingi (k.m. damu), umwagaji mwingi wa damu katika vita. ~-borne adj (of trees) -a mto. rivulet n kijito.

rivet n ribiti. vt 1 piga ribiti. 2 kaza. 3 vuta, vutiwa (na kitu). ~er n mpiga ribiti.

roach; cock~ n 1 mende, kombamwiko. 2 (sl) kishina/kipande cha sigara ya bangi.

road n 1 barabara; njia. on the ~ safarini, njiani. take to the ~ -wa mzururaji. rule of the ~ sheria/ kanuni za kupishana magari/meli, n.k. ~ safety n usalama barabarani. 2 (compounds) ~ bed n jumla ya vifaa k.v. mawe, kokoto, kifusi n.k. vinavyotandazwa katika ujenzi wa barabara. ~-block n kizuizi barabarani. ~ book n kielelezo cha barabara za mji/nchi. ~-hog n (colloq) dereva jahili/mbaya. ~house n mgahawa wa barabarani, hoteli iliyopo kando ya baraba kuu. ~ man/ mender n mtengeneza barabara. ~ metal n kokoto za kutengenezea njia/ barabara. ~ -sense n akili ya udereva. ~ show n maonyesho (yaonyeshwayo na kikundi cha sanaa kinachozunguka sehemu mbalimbali) ~ side n pembeni mwa barabara, kando ya barabara. ~stead n bandari, maelezi, pa kutia nanga. ~way n

roam

(sehemu ya) barabara (yanapopita magari); sehemu ya kati ya barabara. 3 njia (apitapo mtu). 4 ~ (to) (fig) njia (ya kuelekea); namna the ~ to success njia ya kufanikiwa. ~ster n gari ndogo iliyo wazi (agh ya watu wawili).

roam vi, vt tembeatembea; susurika, tangatanga, zururazurura go ~ing about zurura, kata mitaa n.

roan1 adj (of animals) -enye rangi mchanganyiko hususan hudhurungi na nyeupe n farasi/ng'ombe wa rangi mchangayiko.

roan2 ngozi ya kondoo (itumikayo kujalidia vitabu).

roar n 1 ngurumo, rindimo. vt,vi nguruma, rindima. 2 sema/imba kwa sauti kubwa. 3 ~ oneself hoarse pwelewa/kaukiwa na sauti (kwa kuimba au kutoa sauti kubwa/kali). ~ somebody down zima. ~ing adj 1 -a kunguruma, -a kurindima. 2 -a dhoruba. 3 -enye kustawi adv sana. ~ingly adv.

roast vt,vi 1 choma, banika, oka. 2

pasha joto/moto. 3 weka katika hali ya joto ya namna fulani ~ oneself in the sun jianika juani. 4 kemea sana. n 1 nyama iliyobanikwa/okwa; vipande vidogovidogo vilivyokatwa kutoka pande hili. 2 ubanikaji au uchomaji (nyama). ~er n aina ya jiko la kubanikia nyama; chombo cha kuchomea kahawa/buni; aina ya chakula (k.m kuku) kinachoweza kubanikwa au kuchomwa. ~ed adj -liyochomwa; -liobanikwa. ~ing n. give somebody a good ~ing (fig) karipia/kemea vikali.

rob vt ~ somebody/something (of something) 1 ibia, nyanganya, pora. 2 nyima/zuia mtu (haki yake/kilicho chake). ~ber n mwizi, mnyang'anyi, jambazi, mporaji. ~bery n wizi, unyang'anyi. daylight ~ bery n wizi wa kimachomacho, kupandisha bei mno.

robe n 1 joho. bath ~ n joho la kuogea/bafuni; vazi rasmi (la kazi

rocket

k.m. la mapadri, majaji, n.k.). vt,vi vaa; visha.

robot n roboti: mashine ifanyayo kazi kama mtu/badala ya mtu; (fig) mtu afanyaye kazi kama mashine/bila kufikiri au kuuliza, n.k.

robust adj -enye afya/nguvu, imara. ~ly adv. ~ness n.

roc n ndege mkubwa wa ajabu wa hadithini katika sehemu za Uarabuni.

rock1 n 1 mwamba, jabali. as firm/ solid as a ~ isiotingishika, imara kabisa; (of persons) (fig) thabiti. on the ~s (of a ship) -liovunjika juu ya miamba; (fig) -liowamba; (of a marriage) -nayoelekea kuvunjika; (US) (of whisky) kwa barafu. see ~s ahead ona miamba/hatari mbele. the R~ of Ages Yesu. 2 jabali kubwa lijitokezalo juu ya ardhi au majini; (of a person) mtu aliyewamba. 3 genge la mwambajiwe, jiwe kubwa. 4 peremende ngumu. 5 (used with compounds) ~ bottom n kiwango cha chini kabisa. ~ climbing n upandaji miamba (kwa msaada wa vifaa fulanifulani k.v. kamba). ~-crystal n kwazi ya fuwele: namna ya jiwe gumu, jeupe la kung'aa. ~garden n tita kubwa la majabali na mawe na juu yake kukiwa kumeota mimea. ~ plant n aina ya mmea unaoota katika sehemu za majabali au mawe. ~ salmon n see dogfish. ~ salt n chumvi ya mawe. ~ery n see ~ garden. ~y adj 1 -enye miamba. 2 -sio imara.

rock2 vt,vi 1 (swing) pembeza; pembea, chuchia. 2 (shake) tikisa, tingisha ~ the boat (fig) yumbisha/vuruga, jambo. ~ing-chair n kiti cha bembea. ~ing-horse n bembeafarasi: farasi bandia wa mbao wa kupandwa na watoto. ~er n mguu tao (wa kiti cha bembea au farasi bandia). off one's ~ -enye wazimu.

rock3 also ~'n-roll n roki: aina ya

dansi la kurukaruka. vi cheza roki.

rocket n 1 roketi. ~ base n kambi la

rococo

makombora ya roketi. 2 fataki; fashifashi. 3 (colloq) karipio give someone a severe ~ karipia vikali vi panda (kama roketi), paa prices ~ed bei zilipaa.

rococo adj -enye nakshi nyingi/kupita kiasi. n mtindo wa rokoko.

rod n 1 ufito. 2 kiboko, fimbo ya kuadhibia. make a ~ for one's own back karibisha matatizo/adha. spare the ~ and spoil the child (prov) mchelea mwana kulia hulia yeye. have a ~ in pickle for somebody wekea mtu adhabu yake. 3 kipimo cha urefu sawa na yadi 5½. 4 chuma chochote (chenye kipenyo kidogo) kirefu. 5 (US sl) bastola.

rodent n mnyama mgugunaji (k.m. panya, sungura, n.k.) adj -mnyama mgugunaji.

rodeo n 1 (US) kukusanya ng'ombe

(kuwatia alama). 2 maonyesho/ mashindano ya wachunga ng'ombe (kuhusu ufundi wao wa kufunza mifugo).

rodomontade n makeke, majivuno,

maringo, kujidai. vi jivuna.

roe1 n ng'ofu: mayai ya samaki.

roe2 n paa mdogo wa Ulaya na Asia. ~buck n paa dume.

rogation n (Rel.) litania ya watakatifu. R~ Days siku za kuombea watakatifu, siku tatu kabla ya sikukuu ya kupaa.

roger int (of radio communication)

nimeelewa! imefika!

rogue n 1 ayari, laghai, mjanja. 2 jambazi, jangili, mhuni. ~'s gallery n mkusanyiko wa picha za majambazi sugu/wahuni/wahalifu, n.k. 3 (mischievous child) mtundu. 4 mshari ~ elephant tembo mshari. ~ry n 1 ujanja, hila, ulaghai. 2 (fun) mizaha, utundu, ucheshi. roguish adj 1 -a kilaghai, -a kihuni. 2 -a kitundu, -a kidhihaka.

roister vi piga makelele (ya furaha).

~er n mfanya ghasia.

role n 1 wajibu, dhima. 2 nafasi (ya

mwigizaji).

roll

roll vt,vi 1 bingirisha; bingirika heads will ~ (colloq) watu watafukuzwa/ umbuka. 2 ~ (up) sokota; kunja, zongomeza ~ a cigarette sokota sigara. 3 enda, pita the clouds ~ed away mawingu yalitoweka tears ~ed down his cheeks machozi yalimtiririka. 4 geukageuka. 5 (make flat) tandaza; sukuma (k.m. chapati); futa; nyosha. ~ed gold n tabaka nyembamba ya dhahabu (juu ya metali nyingine). 6 sukasuka, yumbayumba. 7 (of surfaces) tia mawimbi. 8 (of waves) panda na kushuka. 9 nguruma ~ one's r's sema kimadende. 10 ~ at (of eyes) geuzageuza, zungusha. 11 ~ing n (compounds) ~ing mill n kiwanda cha kusukuma metali. ~ing pin n kijiti/ mpini/kipande cha kusukuma unga. ~ing stock n mabehewa, mabogi ya reli. 12 (with adv particles and prep) ~ something back rudisha nyuma (k.m. adui). ~ in miminika, wasili/fika kwa wingi. be ~ing in jaa they're ~ing in money wamejaa. ~ on pita; fika haraka. time ~ed on wakati ulipita. ~ on the weekend! wikendi ifike haraka. ~ something on vaa nguo kwa kuzungusha kwenye miguu. ~ something out tandaza. ~ out the red carpet (fig) -pa mgeni rasmi makaribisho makubwa; (of pastry etc) sukuma. ~ up (of a vehicle) fika na kusimama. R~ up! R~up! Njoo! Njoo. ~ something up (mil) rudisha nyuma. ~ n 1 kitu chenye umbo la mcheduara (kutokana na kuviringwa; (of cloth) jora (of paper) gombo; (of film) filamu; (of tobacco) bumba; (of bread) skonzi. ~ top desk n deski lenye mfuniko unaokunjika. 2 ukingo uliogeuzwa (k.m. pindo la nguo lililogeuzwa). 3 mwendo wa kubingiria. 4 orodha rasmi (hasa ya majina). ~call n kuita majina (ya wanafunzi, askari, n.k.) katika orodha. ~ of honour n orodha ya

rollick

majina ya watu waliokufa kwa ajili ya nchi yao. strike off the ~s ondoa jina la mwanasheria katika orodha ya wale wanaoruhusiwa kufanya kazi ya uanasheira. 5 sauti ya mbingirio, ngurumo. ~er n 1 chuma/mti/mpira - mcheduara (-a kukandamizia, n.k.). 2 rola: gurudumu aina ya mcheduara. ~er skates n rolasketi: magurudumu yanayofungwa chini ya kiatu/ubao kwa ajili ya kutelezea. 3 ~er bandage n bandeji ya operesheni. 4 wimbi refu na kubwa.

rollick vi chachawa, cheza, dhihaki;

rukaruka kwa furaha. n kurukaruka kwa furaha, kucheza sana. ~ing adj 1 -enye kelele/furaha/vifijo, -enye kuchachawa. 2 -a makelele.

roly-poly n 1 (also ~ pudding) pudini yenye utando wa unga wa jamu iliyotengenezewa katika umbo la mcheduara na kuchemshwa. 2 (colloq) mtoto mfupi na mnene.

Romaic adj -a Kigiriki cha kisasa. n Kigiriki cha kisasa.

Roman adj 1 -a Kirumi. ~ alphabet n alfabeti ya Kirumi. ~ letters/type n hati za Kirumi. ~ numbers n namba za Kirumi. 2 -a Kikatoliki. R~ rite n ibada ya Kikatoliki. ~ Catholic n Mkatoliki n 1 Mrumi. 2 Mkatoliki. ~ize vt,vi fanya kuwa Urumi; tia tarakimu za Kirumi, fanya kuwa Katoliki; ongoa Kikatoliki.

Romance1 adj -a Kirumi ~ languages lugha za Kirumi (k.m Kifaransa, Kitaliana, Kireno, Kihispania) n lugha za Kirumi.

romance2 n 1 (love story) hadithi ya mahaba (hasa dhanifu); fasihi ya mahaba. 2 mapenzi. 3 hali ya kuvutia/kuvutiwa na hadithi na vitendo/vituko vya mapenzi. 4 uzushi, maelezo yaliyotiwa chumvi. vi (usually romanticize) piga chuku katika kuhadithia. romantic adj 1 (of persons) -enye mawazo/hisia/njozi za mapenzi; -enye kupenda mambo yaliyotiwa chumvi/ya ajabu. 2 -enye hali ya ajabu/mahaba. 3 -enye kubuni

rook

ya usoni. 4 (lit,etc.) -enye kusisitiza hisia kuliko mantiki/akili. n 1 mpenda mahaba. 2 mpendelea hisia na ubunifu. 3 mpiga chuku; mwota njozi. romantically adv. romanticism n tapo la sanaa linalosisitiza ubunifu na hisia. romanticist n mfuasi,mshiriki wa mwelekeo huo. ~ r n 1 mwandishi wa hadithi za mahaba. 2 kidhabi.

Romanesque n mtindo wa uhandisi

majenzi wa Kirumi.

Romany n 1 Mjipsi. 2 lugha ya Wajipsi adj -a kijipsi.

Rome n Roma. (with different phrases.) R~ was not built in a day usione vyaelea vimeundwa. when in R~ do as the Romans do fuatia maadili ya wenyeji.

Romish adj -a Kanisa la Katoliki.

romp vi 1 cheza, randa, rukaruka, chachawa. 2 shinda haraka/bila shida. n 1 mchezo wa kurukaruka na kufanya makelele; kelele. 2 mtoto anayependa kuchezacheza na kurukaruka. ~er n (also a suit of ~ers) ovaroli ya mtoto. ~ish adj -a kuchezacheza.

Roneo n mashine ya kurudufu barua, nakala, n.k.. vt rudufu kwa mashini.

rood n 1 ~ (-tree) (arch) msalaba ambapo Yesu alisulubiwa. 2 sanamu ya Yesu msalabani. 3 robo eka.

roof n 1 paa: sehemu inayufanika juu (ya nyumba, basi, gari, treni, n.k.). raise the ~ (colloq) piga makelele (ndani ya nyumba). ~ garden n bustani juu ya jengo. ~ tree n mti wa ulalo unaounganisha/unaoshikilia paa. 2 kilele, sehemu ya juu kabisa. 3 kaakaa. vt tia paa, tia dari, (thatch) ezeka, vimba. ~ing n (also ~ing material) vifaa vitumiwavyo kuezekea; maezeko, mavimbo. ~less adj sio na paa (of person) -siyekuwa na makazi/ nyumba.

rook1 n ndege mkubwa mweusi kama kunguru. ~ery n 1 makazi ya ndege huyo. 2 jamii ya penguini.

rook2 n ayari, laghai. vt danganya,

rook

ghilibu, laghai (katika kamari).

rook3 n ngome katika sataranji.

rookie;rooky n (sl) askari mbichi/kuruta.

room n 1 chumba. ~ed adj -enye vyumba a five ~ed house nyumba yenye vyumba vitano. 2 vyumba (vinavyokaliwa/tumiwa na mtu mmoja au familia moja). ~mate n mkazi-mwenza (katika chumba/ nyumba). 3 ~ (for somebody (something); ~ (to do something) nafasi there is no ~ for doubt hapana shaka yoyote. 4 mwanya, nafasi (ya kufanya jambo) vi panga chumba/vyumba/nyumba. ~ing house n jengo lenye vyumba vingi vya kupanga (agh. wapangaji wakijihudumia wenyewe). ~er n (USA) mpangaji. ~ful n watu, samani, n.k. inayoweza kujaza chumba. ~y adj -enye nafasi tele. -ily adv.

roost n kijiti cha kutulia; kituo cha

ndege; banda la kuku. come home to ~ (of words) rudia his words came home to ~ maneno yake yalimrudia. rule the ~ tawala (agh. nyumbani); (of birds) jikalia kiotani usiku.

rooster n jogoo, jimbi.

root1 n 1 mzizi. pull up one's ~s (fig) hama (ili kuanza maisha mapya mahali pengine). put down new ~s (fig) anza maisha mapya baada ya kuhama maskani ya zamani. take/ strike ~s (of plants) anza kuota mizizi, anza kukua; (fig) anza kustawi. ~ and branch (fig) kabisa. 2 ~s; ~ crop n mazao yawekayo chakula katika mizizi (k.v. karoti). 3 (of hair, tooth, nail) kizizi. 4 (fig) asili, chanzo, kiini. get at/to the ~ of something fikia/kabili kiini cha jambo. 5 (gram) mzizi: sehemu ya neno ambayo ndiyo kiini/kijenzi cha neno zima (k.m. pik- katika pik-a, pik-i-a, n.k). 6 kipeo (katika hesabu). vt,vi 1 (of plants etc) toa mizizi, anza, kukua. 2 weka/simama imara, kaza, pigwa bumbuwazi. 3 (of ideas,

rose

principles) kuwa na mawazo/misingi thabiti. 4 ~ something out; ~ something up ng'oa; ondoa kabisa (kitu kibaya); angamiza. ~less adj bila mizizi, -sio na mashiko/asili.

root2 vt,vi 1 ~ about (for) (of pigs etc) chimbua; (of persons) pekuapekua. ~ something out gundua/fuma kwa kutafuta. 2 ~ (for) (US sl) unga mkono, shangilia, shabikia. ~er n. ~le vi ~ about for (of pigs) chimbua chimbua.

rope n 1 kamba, ukamba, ugwe. the ~ kitanzi (agh. kunyonga mtu). the ~s n kamba za ulingo/jukwaa (la ndondi, n.k.). show somebody/ know/learn the ~s onyesha/jifunza namna ya kufanya jambo. give somebody (plenty of) ~ mpe uhuru wa kufanya jambo. give somebody enough ~ and he `ll hang himself mwana akililia wembe mpe. 2 (with compounds) ~-dancer; ~walker n mchezaji juu ya kamba. ~-ladder n ngazi ya kamba. ~-walk/yard n sehemu ya ardhi inayotumika kusokota kamba. ~way n reli ya kamba. ~-yarn n uzi wa kamba. 3 vitu kadhaa vilivyosokotwa pamoja. vt 1 funga kwa kamba. 2 ~ something off zungushia eneo kwa kamba. 3 ~ in shawishi mtu ajiunge.

ropy adj (sl) hafifu, duni.

rosary n 1 rosari; tasomebodyihi. 2 bustani ya waridi. 3 (RC) sala ya rozari.

rose1 n 1 waridi. a bed of ~s maisha ya raha. it is not all ~s ina matatizo yake. no ~ without a thorn hakuna kizuri kisicho ila, hakuna furaha bila tabu. gather life's ~s tafuta raha za maisha. 2 rangi nyekundu-nyeupe. see things through ~ coloured tinted spectacles ona/bashiria mema tu (labda bila sababu). 3 vitu vyenye umbo la waridi. 4 (with compounds) ~-bed n tuta la waridi. ~ bud n tumba la waridi. ~ leaf n petali ya

rose

ua la waridi. ~red n waridi, nyekundu ya waridi. ~-water n marashi ya waridi. ~window n dirisha la duara na mapambo. ~wood n mwaridi (mti mwekundu na mgumu unaotumika kutengeneza fanicha) adj 1 -ekundu -eupe. 2 -a waridi. ~ate adj -a waridi, -ekundu, -a rangi ya waridi. rosy adj 1 -a rangi nyekundu/nyeupe (hasa kwa shavu la uso) turn rosy geuka mwekundu. 2 (fig) -a kutia matumaini.

rose2 pt of rise.

rosin n 1 ulimbo (wa baadhi ya miti

kama sandarusi). 2 resini. vt sugua kwa resini.

roster n rosta: orodha ya majina ya

watu na kazi wapaswazo kufanya kwa zamu (pia rota). by ~ kwa zamu.

rostrum n mimbari; jukwaa.

rot vt,vi 1 oza. 2 (of society, prisoners, etc) dhoofika, chakaa. 3 ozesha. ~-gut n gongo chafu lenye kudhuru tumbo.~ n 1 kioza; uoza/uozo. 2 (US the ~) ugonjwa wa ini wa kondoo. (foot ~) ugonjwa wa miguu wa kondoo. 3 (sl) (nonsense) upuuzi, mapiswa. 4 mfululizo wa kushindwa. ~ten adj 1 bovu, viza; -liooza. ~ten eggs n mayai viza. 2 -siyopendeza, baya sana he is a ~ten singer ni mwimbaji mbaya sana.

rota n (GB) orodha ya zamu; zamu.

rotary adj -a kuzunguka/-liozunguka sehemu maalumu ya kati. R~ Club n Klabu ya R~ (ya wanabiashara). Rotarian n mwanachama wa R~.

rotate vt,vi 1 zunguka kitu; zungusha; fuatana kwa zamu. 2 badilisha ~ the crops badilisha mimea. rotative adj. rotatory adj. rotation n 1 mzunguko, mzingo. rotation of the earth mzunguko, mhimili (wa dunia). 2 in rotation kwa zamu.

rote n ghibu. by ~ kwa ghibu, kwa moyo learn by ~ jifunza kwa ghibu.

rotor n rafadha.

rotter n (sl) mkorofi, mwovu, mtu asiye na mwamana; mshenzi.

rough

rotund adj 1 (of person, his face; of

voice) nene; nzito; -a mviringo. 2 (of speech, style) -enye mbwembwe, -a majivuno. ~ly adv. ~ity n.

rotunda n jengo la duara (hasa lenye paa la duara).

rouble n rubo: sarafu ya Kirusi.

roue n fisadi, fasiki.

rouge n 1 poda nyekundu (ya kupaka kwenye mashavu). 2 poda ya kusafishia (fedha, kioo, n.k.). vt jipodoa (kwa kutumia rangi hiyo).

rough adj 1 (of surfaces) -a kukwaruza, -a kuparuza; (of road) -enye mashimoshimo; (of sea) -liochafuka. 2 kali, -enye fujo. be ~ on somebody onea mtu, -wa mkali. give somebody the ~ side of one's tongue karipia mtu. give somebody/have a ~ time -pa/pata matatizo. ~ house n (colloq) ugomvi, zahama, ghasia. 3 ghafi, -siokamilika, -a kukadiria. ~ and ready adj -enye kufaa kutumia (lakini si makini sana). a ~ diamond n (fig) mtu wa thamani lakini asiyestaarabika. 4 (of sounds) nene na -enye kukwaruza. 5 (with compounds) ~-and-tumble adj -a mkikimkiki; -enye vurumai, ovyo na gomvi. ~-neck n (US colloq) mhuni, jambazi. ~-rider n mfunza farasi (ili akubali kupandwa). ~shod adj (of horses) -enye viatu vya njumu. ride ~shod over somebody puuza kabisa. ~spoken adj mwenye mdomo mchafu, mpujufu. ~ly adv 1 kwa ukali, kwa kuparuza. 2 takribani, mnamo ~ ly speaking kwa kukisia. ~ness n fujo, ghasia, ukatili; mparuzo, mkwaruzo. n 1 jambazi, mhuni. 2 hali ya kutokamilika in (the) ~ draft drafti ya awali. 3 hali ya kukwaruza/ kutokuwa sawa; kitu kibaya. take the ~ with the smooth (fig) kubali mabaya yanayoandamana na mema. 4 (golf) the ~ n sehemu ya majani marefu. vt,vi 1 ~ something (up) vurugavuruga, timua timua. 2 ~

roughage

somebody up (sl.) tikisatikisa; pigapiga; fanyia fujo, sumbua. ~ something in sawidi. 3 ~ it ishi maisha ya taabu/shida adv kwa ugomvi/ukali/ukatili play ~ cheza kwa rafu. cut up ~ (colloq) kasirika. live ~ ishi kwa kubabia, ishi maisha ya ovyo. sleep ~ lala majaani. ~en vt,vi -wa/fanya rafu/fujo/vurugu.

roughage n chakula ghafi; vyakula

vigumu.

roulette n mchezo wa kamari (uchezwao kwa gololi na kigurudumu).

round adj 1 -a duara, -a mviringo, -a kuviringa(na). a ~ game n mchezo usio na timu au idadi maalumu ya wachezaji. 2 -enye kufanywa kwa kuzungukazunguka/kuzungu-shazungusha. ~ brackets n mabano upinde. ~ dance n ngoma ya kucheza katika duara. ~ robin n barua ya maombi/malalamiko yenye sahihi zinazofanya mviringo (ili kuficha ni nani aliyeanza kutia sahihi). ~ trip n safari ya kwenda na kurudi. 3 kamili, -ote; nzima. in ~ numbers/figures namba za makumi 10, 100, 1000. 4 wazi, dhahiri, kamili. 5 (with compounds) ~ arm adj -a usawa wa bega. ~backed adj -a kibiongo. ~eyed adj kodozi; -enye macho makubwa. ~ hand n mwandiko wa herufi za kuumba. ~-house n (hist) gereza; (naut) chumba cha staha; karakana ya garimoshi. ~ shouldered adj -enye matao. vt,vi 1 fanya/-wa mviringo, viringisha. 2 zunguka. 3 ~ something off kamilisha jambo. ~ out viringisha. ~ somebody/something up leta pamoja, kusanya. ~ up (a figure/ price) fanya (idadi) kamili. a ~ up msako. ~ on (upon) geuka ghafla. ~ upon somebody geukia mtu na kumshambulia (kwa maneno au kwa vitendo). n 1 kitu kilicho na umbo la mviringo. 2 (of sculpture) umbo linalokiwezesha kitu kuonekana kutoka sehemu zote. in the ~ (arts)

round

-liotengenezwa/fanywa ili kuonekana pande zote. theatre in the ~ jukwaa linalozungukwa na watazamaji. 3 (series) mfululizo, mfuatano, mgawo, mzunguko. make one's ~s fanya raundi za kila siku/mara (k.m. kukagua). go the ~ of; go the ~s fikia (watu, mahali), sambaa, enea haraka the news went the ~ of the school habari zilisambaa haraka shuleni. 4 (games contest, etc) raundi the third ~ of the super league raundi ya tatu ya ligi kuu; duru. 5 mzunguko (wa kitu kinachogawiwa watu, k.m. kwenye unywaji wa pombe). 6 wimbo wa kupokezana. 7 mchezo wa dansi ambapo wachezaji hucheza katika mtindo wa duara prep 1 (expressing movement) kwa kuzunguka. sleep/work ~ the clock (attrib) lala/fanya usiku na mchana, saa zote. 2 (expressing movement) katika njia ambayo inabadili uelekeo kutoka upande mmoja wa kitu hadi upande mwingine. ~ the bend (sl) kichaa. 3 (expressing position) kuwa katika pande zote za kitu they were sitting ~ the table walikuwa wamekaa kwa kuzunguka meza. 4 katika sehemu mbalimbali/zote. show ~ tembeza. ~go tembelea; zunguka. 5 sehemu mbalimbali kutoka kituo maalumu. 6 ~ (about) (fig) takribani adv 1 katika duara; kwa kuzunguka. 2 kwa kurudia mahali ulipoanzia. ~ and ~ kwa mizunguko kadhaa. all ~; right ~ kwa kuzunguka kabisa. all the year ~ kwa mwaka mzima. 3 kwa kuzunguka, katika mzingo. 4 ili kuwa katika duara. 5 kutoka sehemu/ eneo/mtu mmoja hadi mwingine. hand ~ gawia/mpe kila mmoja. go ~ tosheleza. taking it all ~ kwa kulitazama (k.m.) katika ujumla wake/pande zake zote. look ~ tembelea. 6 kwa kutumia njia ndefu zaidi. 7 kwenye sehemu alipo mtu/atakapokuwa mtu. 8 ~ (about) jirani/katika mazingira jirani. ~ly

roundel

adv sana, wazi. ~about adj -enye kuzunguka. in a ~about way kwa kuzungukazunguka. n 1 pembea. you lose on the swings what you make on the ~abouts (prov.) kata pua uunge wajihi. 2 kipulefti, kizingwa, kisiwa (cha trafiki).

roundel n 1 nishani. 2 nembo ya ndege.

roundelay n wimbo mfupi wenye kiitikio.

rounders n mchezo unaofanana na

baseball.

roundsman n mchuuzi (wa nyumba

hadi nyumba).

rouse vt,vi 1 amka/amsha, chochea. 2 ~ somebody (from something to something) zindua/ zinduka; sisimua; chachafya.

rout1 vt shinda kabisa. n 1 kushindwa put the enemy to ~ shinda adui kabisa. 2 (arch) umati/halaiki yenye ghasia. 3 (arch) tafrija, sherehe.

rout2 vt ~ somebody out (of) furusha; amsha (kitandani); winga, fukuza.

route n 1 njia. en ~ njiani. 2 (mil) column of ~ safu ya askari wanaotembea. ~-march n (mil) safari ndefu ya miguu (ya mazoezi). vt peleka/tuma kwa njia fulani; panga njia ya safari.

routine n utaratibu, kawaida, desturi

business ~ utaratibu wa biashara/shughuli adj -a kawaida.

rove vi,vt 1 tangatanga, zurura ~ the streets zurura barabarani. a roving commission n wajibu/kazi zinazohitaji kutembea/kuzunguka sana. 2 (of affections) badilibadili. 3 (of eyes) tazama huko na huko; -totulia. ~r n 1 mzururaji, mtembezi. 2 (arch) sea ~r n haramia wa baharini. 3 skauti wa kiume mwandamizi.

row1 n 1 makelele, ghasia, zahama.

kick up/make a ~ anza ugomvi/ mabishano. 2 ugomvi. 3 matata; karipio. vt,vi 1 karipia, kemea. 2 ~ with gombana kwa makelele na mtu. ~dy n makelele, zahama, vurugu;

rub

mtu mwenye vurugu, mhuni. ~dily adv ~diness n. ~dism n.

row2 n safu; mstari; msafa be in ~s

kuwa katika safu; (colloq) mfululizo two weeks in a ~ wiki mbili mfululizo. a hard ~ to hoe kazi ngumu sana; (of things piled up) rusu; (of fish on a string) mtungo, mtanda; (of plants) mpando.

row3 vt,vi piga (vuta) makasia. n kwenda katika mtumbwi. ~boat; ~ing boat n mtumbwi wa makasia; ngalawa. ~ing club n klabu ya wapiga makasia. ~lock n kileti, kishwara. ~ er n mpiga kasia.

rowel n kikuna farasi (kisumari cha kumchochea farasi mbavuni).

royal adj -a kifalme ~ charter idhini ya kifalme ~ prerogative haki za mfalme (kwa mujibu wa katiba); -zuri sana. ~ road to success njia rahisi/bora ya mafanikio have a ~ time starehe sana. n mmojawapo wa familia ya kifalme. ~ist n mfuasi wa ufalme. ~ty n 1 hadhi, cheo, mamlaka ya mfalme/jamaa wa mfalme. 2 watu wa jamaa/aila ya mfalme. 3 mrabaha: malipo ya mwandishi.

rub vt,vi 1 chua; fikicha ~ hands together fikicha viganja ~ the ears of wheat fikicha ngano; ~ shoulders with (fig) changamana na watu wa aina mbalimbali. 2 sugua. 3 (with adverbial particles and prep) ~ along ishi. ~ along (with somebody/together) ishi vizuri (pamoja), elewana. ~ somebody/ oneself/a horse down sugua vizuri na kwa nguvu (k.m. kwa taulo ili kukausha na kusafisha). ~ something down sugua. ~ something in; ~ something into something chua; sisitizia, tia mkazo. ~ it in kumbusha kila wakati. ~ something off/out ondoa kwa kufuta. ~ somebody out (US sl) ua. ~ something up piga polishi, ng'arisha; fanya kiwe kipya. ~ somebody up the wrong way udhi

rub-a-dub

mtu. n 1 usuguaji, (muda wa) kusugua. 2 (esp in the phrase) (there's the ~) tatizo, mahali ambapo ugumu unaanza kutokea. ~bing n picha ya kusuguliwa.

rub-a-dub n mdundo.

rubber1 n 1 mpira. ~ stamp n mhuri. ~- stamp (colloq) vt pitisha kitu/jambo bila kulizingatia. ~ neck n (US) (colloq) mtalii anayegeuka kila upande (ili ajaribu kuona kila kitu). vi talii. 2 kifutio, raba. 3 viatu vya mpira, raba. 4 mtu afutaye/kitu kitumiwacho kufuta (k.m. sehemu ya mashine). vt funga/funika kwa mpira. ~ize vt funga/funika kwa mpira. ~y adj.

rubber2 n (in cards) 1 seti: michezo mitatu mfululizo ya karata. 2 mchezo wa tatu wa kutafuta mshindi.

rubbish n 1 taka, takataka; kitu cha

kutupwa; kitu kisicho na faida/ thamani. 2 upuuzi; mawazo/fikra zisizokuwa na faida (as expression) mawe! ~-bin/can n pipa la taka a heap of ~ jalala, jaa; (of demolished house) kifusi. ~y adj.

rubble n 1 kifusi. 2 kokoto.

rube n (US colloq) mshamba.

Rubicon n (esp in) pass/cross the ~

jiingiza katika mradi/jambo/uhusiano ambao haiwezekani kujitoa.

rubicund adj (of person's face or complexion) -ekundu.

ruble n see rouble.

rubric n 1 kichwa cha maandiko kilicho andikwa kwa rangi nyekundu. 2 utaratibu, maelezo. 3 utaratibu, mfumo.

ruby n 1 rubi: kito chekundu cha thamani. 2 rangi ya zambarau adj -ekundu.

ruck1 n the ~; the common ~ n kabwela; vitu vya kawaida.

ruck2 n kunyanzi katika nguo. vt,vi ~

(up) kunjakunja, fanya kunyanzi.

rucksack n shanta.

ructions n maneno ya hasira au upinzani; ghasia, zahama; ugomvi wenye makelele.

rugger

rudder n usukani. ~less adj bila usukani.

ruddy adj 1 -ekundu (na -enye afya). 2 (of sky) -ekundu (ekundu). ruddiness n wekundu (wa uso). ruddily adv.

rude adj 1 fidhuli, -juvi, -sio adabu. 2

-a kushtusha; -a fujo na ghasia; kali. get a ~ awakening tambua ghafla ukweli usiopendeza. 3 -a kishenzi. 4 ghafi. 5 -liofanywa kwa haraka- haraka; sahili. 6 -a nguvu. ~ness n. ~ly adv kishenzi.

rudiment n 1 (beginning) mwanzo,

asili, msingi, hatua za kwanza. 2 chipuko, chanzo. ~al adj. ~ary adj 1 -a mwanzo. 2 -sioendelezwa; katika hali isiyokamilika.

rue vt jutia, sikitikia to ~ the day when.... kujutia siku ya .... ~ful adj. ~fully adv. ~fulness n.

ruff1 n 1 kikunjo shingo, kitambaa

chenye vikunjo cha kuvaa shingoni; matimutimu. 2 pete ya manyoya ya rangirangi shingoni mwa ndege au mnyama. ~ed adj 1 -liokunjamana. 2 matimutimu.

ruff2 vt,vi shinda kwa turufu.

ruffian n katili, mgomvi, jambazi, mhuni. ~ism n uhuni; ujambazi, ukatili. ~ly adj -gomvi, huni, -katili.

ruffle 1 vt,vi ~ (up) chafua, timua,

vuruga ~ its feathers timua manyoya (kwa hasira au kutoa baridi). 2 kasirika; chafuka, timka easily ~d -a kukasirika, -a kuudhika upesi. n 1 vikunjo (vya nguo vya kuvaa shingoni; mwisho wa mikono ya vazi. 2 matatizo, shida. 3 kuchafuka, machafuko. ~d adj.

rug n zulia dogo nene; blanketi nene la safari.

rugby n ragbi: mchezo wa mpira wa mikono.

rugged adj 1 -a mawemawe; -a kuparuza; -sionyooka. 2 -enye mikunjomikunjo; -a kunyanzi. 3 -sio laini/taratibu/pole. ~ness n ~ly adv.

rugger n see rugby.

ruin

ruin n 1 maangamizi; uharibifu; utilifu the ~ of my hopes kuharibika kwa matumaini yangu. 2 (in sing. only) sababu ya kuharibika. 3 (of buildings) hali ya kuwa katika maanguko/ magofu/mahame/mabaki a ~ed house gofu la nyumba, hame 4 (business) kufilisika. vt vunja; angamiza; haribu; tilifisha. ~ation n kuangamia, kuharibika; uangamiaji. ~ous adj 1 -enye kuharibu. 2 -liovunjika (na kuanguka). ~ously adv.

rule n 1 (regulation) amri, kanuni, sharti; desturi, mila. by/according to ~ kwa mujibu wa kanuni/sheria. work to ~ timiza mradi, -wa na mgomo baridi (kwa kufuata sana sheria kwa makusudi) kwa kiasi cha kurudisha nyuma uzalishaji (mali). 2 desturi. as a ~ kwa kawaida/desturi. 3 utawala; mamlaka; dola; serikali. ~ of law n utawala wa sheria. 4 (for measuring). rula vt,vi 1 ~ (over) tawala; -wa na mamlaka. 2 (usu passive) (control) ongoza, athiri, tawala. 3 (order) amuru. 4 (decide) amua. ~ something out futilia mbali. 5 piga mstari. ~d paper n karatasi ya mistari mifuo. ~ something off kata, ondoa. ~r n 1 mtawala, mfalme, mkuu. absolute ~r n dikteta, mtawala mmoja. 2 (for measuring) rula, chenezo, kigezo, futi. ruling adj -a kutawala, -a nguvu; -liopo. n amri; hukumu; uamuzi.

rum1 n aina ya pombe kali. ~ runner n mlanguzi (wa pombe zisizoruhusiwa); (US) pombe.

rum2 adj (colloq) kioja; -a kigeni; -sio

-a kawaida; ajabu. also ~my adj.

rumba adj rumba: dansi yenye asili ya Cuba.

rumble vt,vi 1 nguruma; vuma, tutuma; rindima. ~ along enda kwa kunguruma. 2 ~ (out) sema kwa sauti nzito. n 1 ngurumo, uvumi, tutumo, tetemo, mdundo, rindimo. 2 (colloq US) mapambano ya vikundi

run

vya wahuni mitaani.

rumbustious adj (colloq) -a ghasia,

-enye kelele, -a makeke.

ruminant adj 1 -a kucheua. 2 (of person) -liozama katika fikra, -liokaa na kushika tama. n mnyama anayecheua. ~s wacheuzi. ruminate vt,vi 1 cheua; tafuna. 2 waza, tafakari. ~ over (a plan) fikiria jambo/azimio. rumination n.

rummage vt,vi 1 ~ (among, in, through) geuzageuza vitu wakati unatafuta kitu, pekua, chakura. 2 ~ through pekua/chakura sana, chunguza, kagua. ~ sale n see jumbo sale n 1 upekuzi mkali. 2 vitu vilivopatikana katika upekuzi. 3 vitu vikuukuu.

rummy1 adj see rum.

rummy2 n (of cards) mchezo wa karata uchezwao na jozi mbili.

rumour n uvumi, mnong'ono, tetesi, udaku. vt vumisha; toa uvumi. ~ monger n mvumishaji, mzushi.

rump n 1 (animal) tako; (bird) mkiani. 2 (derog) mabaki, masazo (ya kundi kubwa la watu). ~ steak n steki ya tako.

rumple vt kunjakunja; vuruga.

rumpus n zahama, ghasia, ugomvi

wenye makelele/makeke. kick up/make a ~ fanya ghasia.

run1 vt, vi 1 kimbia; kimbiza take a ~ ning jump kimbia na kuruka; (sl) ambaa; usiwe mpuuzi! 2 epuka, toroka, kimbia. ~ for it kimbia (ili kukwepa jambo). cut and ~(sl) toroka. a ~ning fight n mapambano ya manowari (kati ya wanaorudi nyuma na wanaowakimbiza). 3 shiriki katika mbio/mazoezi ya kukimbia. also ran n mshinde. 4 ~ for gombea (uchaguzi, cheo, n.k.). 5 sababisha kukimbia/kushiriki (katika mashindano ya mbio); wasilisha/teua (kushika cheo). 6 sababisha kufikia hali fulani/mahali fulani (kutokana na kukimbia). ~ somebody clean off his feet/ legs (colloq) shughulisha hadi kuchosha

run

kabisa. ~ oneself/somebody into the ground jichosha/chosha (mtu) kwa kazi/mazoezi magumu. 7 enda haraka. ~ its course kua, endelea kawaida; fuata mkondo wa kawaida. ~ the streets (of children) cheza barabarani (bila usimamizi). 8 jiweka wazi; jihatarisha. ~ the danger/ chance of something jiweka katika hali/hatari ya. 9 kimbiza; shindana na. ~ somebody/something to earth fuatilia hadi kupata/kushika. ~ somebody/something close/hard karibia sana (katika mashindano). 10 (of ships, etc) enda safari; (of fish) ogelea. 11 (of machines) fanya kazi. 12 enda mbele kwa mwendo wa kuteleza au kuendelea; enda kama kwamba uko kwenye magurudumu. 13 (of public transport) pita; enda na kurudi (kila mara). 14 chukua (mtu katika gari, basi, n.k. na kumpeleka mahali). 15 peleka, safirisha. ~ errands/messages peleka ujumbe. ~ arms/guns ingiza silaha nchini kwa siri, fanya magendo ya silaha. ~ liquor fanya magendo ya vileo. 16 fanya kusogea au kupanuka kuelekea upande fulani. 17 (of fire, news, emotions, etc) enea haraka. 18 (of liquids) tiririka; churuzika; lowa. 19 fanya kumwagika/tiririka; fanya kuenea. 20 -wa/pitia katika hali fulani. ~ riot fanya fujo na ghasia; (of plants) enea ovyo. ~ wild kaa/kuwa bila mipango/nidhamu. ~ a temperature -wa na homa. 21 endesha, ongoza, simamia. ~ a company endesha kampuni. ~ning costs n gharama za uendeshaji. ~ the show kuwa bosi katika kadhia fulani. 22 (of thoughts, feelings memories, the eyes, etc) pitia/pitisha mara moja/kwa haraka. 23 endelea/ endelezwa katika mpango maalumu a scar that ~s across his cheek kovu linaloanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa shavu lake. the ~ning commentary n tangazo mfululizo. 24 -wa na mwelekeo

run

fulani (wa kitabia), -wa na bei ya wastani; -wa na kiwango cha wastani. 25 (of colour) -sambaa toka sehemu yenye rangi hadi isiyo na rangi 26 andikwa, simuliwa au semwa the story ~s that hadithi imeandikwa/yasemwa kuwa ---. 27 (of woven or knitted material) fumuka. 28 (in special uses) ~ about kwenda huku na huko. ~-about n motokaa ndogo (k.m. ya watu wawili); mtu atangatangaye kutafuta mambo mageni, raha, n.k. (hatulii katika sehemu moja). ~ away kimbia; jaribu kutoroka. ~away n mtu/farasi atorokaye. ~ away with tumia; toroka; iba; shinda vibaya sana washindani wengine; kubali wazo harakaharaka, fikia hitimisho lisilo na msingi; enda kwa kasi kubwa isiyodhibitika. ~ back rejea nyuma (katika mawazo). ~ down (of a clock or other mechanism of the like) simama (kwa kukosa kulishwa); (of a person's health) nyong'onyea, zidi kuwa mbaya (kwa sababu ya kazi nyingi, fikra nyingi, n.k.); (of a battery) isha; gonga/gongana; sema vibaya (mtu au kitu); fukuza na kupita/kamata; punguza nguvu. ~-down n (colloq) upunguzaji orodha/maelezo kamili. ~ in tembelea (mtu mahala) kwa muda mfupi; (colloq of the police) kamata, bamba; endesha kwa uangalifu kwa mara ya kwanza (gari/mashine mpya) kwa muda/umbali fulani ili kuiweka katika hali nzuri ya matumizi. ~ into gongana; sababisha kuingia katika (deni, ugomvi, n.k.). ~ off toroka (na); churuzika/tiririka (kutoka sehemu hadi sehemu); fanya kuchuruzika/kutiririka; andika au soma kwa ghibu (moja kwa moja bila kusita/kwa ufasaha); chapa; toa (makala/kitabu); amua baada ya watu kufungana baada ya majaribio; anzisha (k.m. mbio). ~-off n

run

uamuzi mkata. ~ something on unganisha/endeleza/ endelea; sema mfululizo; (of time) pita, isha time ~s on wakati unapita; (of disease) endelea kutokea/ kusumbua. ~ on/upon something (of thought etc) husika na. ~ out toweka; fikia mwisho, isha; (of tide) kupwa. ~ out of (of tide) kupwa. ~ oneself out of breath jichosha. ~ out on somebody telekeza. ~ over (of a vessel or its contents) furika; pitia (ili kuzingatia au kushika akilini barabara); soma harakaharaka; gonga/kanyaga mtu (kwa gari); tembelea kwa muda mfupi. ~ through pitisha msitari (k.m. katika maneno yaliyoandikwa); choma kwa singe; tumia vibaya (bahati, fedha); chungua kwa haraka; shughulikia kwa haraka; (of play) fanya mazoezi. ~ to fikia; tosha/tosheleza. ~ to fat nenepa mno! ~ to ruin haribika. ~ to waste tumika vibaya. ~ up inua, simamisha (k.m. bendera kwenye mlingoti); jenga/ tengeneza harakaharaka; fanya kuongezeka kwa haraka; fikia kiasi cha/pata/ongeza mwendo kimbia (kabla ya kutupa mpira, mkuki, n.k.).

run2 n kukimbia. ~up n 1 urefu (wa

kukimbia), masafa; kipindi kabla ya tukio kubwa. a ~ for one's money malipo ya kazi au juhudi za mtu; -pa ushindani mkubwa. 2 ziara, matembezi a ~ to Mikumi ziara ya Mikumi. 3 (of a ship) umbali (wa mwendo kwa kipindi maalumu). 4 njia (ya mashua, meli, n.k.). 5 mshuko wa ghafula price came down in a ~ bei zilishuka kwa ghafla. 6 mfululizo wa maonyesho (k.m. ya muziki, tamthiliya, n.k.). 7 kipindi; mfuatano a ~ of bad luck kipindi cha mkosi. a ~ on something, kitu kinachohitajiwa ghafla na watu wengi. in the long ~ hatimaye. 8 (of domestic animals) zizi, banda. 9 (cricket and baseball) pointi. 10 kawaida, mwelekeo, utaratibu the

rupture

common ~ of mankind watu wa kawaida. ~-of-the mill kawaida, wastani. 11 kundi la samaki wakiwa katika mwendo. 12 (colloq) give somebody/get the ~ of something ruhusa ya mtu kutumia kitu bila kulipa. 13 mwelekeo. 14 (music) mfuatano wa nota zinazoimbwa/ zinazochezwa haraka na kufuata daraja mbalimbali. ~ ner n 1 mkimbiaji. ~ner -up n mshindi wa pili katika mashindano. 2 (messenger) mjumbe, tarishi. 3 (surface root) kitawi cha mmea utambaao chini. 4 (plant) mtambaazi. 5 (cloth) kitambaa kirefu, kipambo cha meza. 6 (in compounds) mfanya biashara ya magendo. gun ~ner n mfanya biashara ya magendo ya bunduki. ~ning adj 1 -a kukimbia. 2 (successive) moja kwa moja, -a mfululizo ~ning fire mfululizo wa bunduki/wa mizinga. 3 (after a pl n) katika mfuatano six days ~ning siku sita mfululizo/moja kwa moja. 4 (of water) -a kuchuruzika. 5 (discharging) -a kutoka usaha. n 1 mbio, kukimbia, kwenda mbio. make the ~ning ongoza mbio. take up the ~ning ongoza (baadaye) katika mbio. in/out of the ~ning (of competitions) -enye/ pasipo nafasi ya kushinda. 2 ~ning-board n (old fashioned) sehemu ya kukanyagia, kuingia garini. ~ning mate farasi wa kuongoza mwendo; (US) mgombea umakamu wa rais.

rung1 n 1 kidato (cha ngazi). 2 taruma la kiti.

rung2 pp of ring2.

runnel n 1 kijito, mlizamu, chururu. 2 mfereji wa wazi.

runt n (colloq) kibeti: mtu/mnyama aliyedumaa.

runway n 1 barabara ya ndege. 2 njia ya kusukumia miti iliyokatwa.

rupee n rupia.

rupture vt,vi 1 pasua;pasuka be ~d pasuliwa. 2 farakana. n 1 kupasuka.

rural

2 (discord) farakano. 3 (of bowel) henia.

rural adj -a vijijini, -a mashamba

~ planning mipango ya vijiji.

Ruritanian adj (of a State, its politics) -liojaa hila na fitina.

ruse n hila, ujanja, werevu, mtego.

rush1 n tete. ~light n mshumaa uliotengenezwa kwa utete. ~y adj -enye matete.

rush2 vi,vt 1 ~ (away/off/ out) timua; kurupuka; kurupua the workers ~ed out of the factory wafanyakazi walikurupuka kutoka kiwandani. ~ to conclusions amua bila kufikiria. ~ into print chapisha bila kujali usahihi/ukweli. ~ something through fanya jambo upesi sana. 2 shambulia, vamia ~ the bus vamia basi. 3 harakisha. ~ somebody off his feet harakisha; chosha. 4 ~ (for something) (sl) langua. n 1 mwendo wa kasi, kukurukakara, mkurupuko. 2 mahitaji makubwa ya ghafla a ~ for rain-coats mahitaji ya makoti ya mvua wakati wa mvua. the ~-hour n wakati wa msongamano wa kutoka na kwenda kazini agh. katika miji mikubwa. 3 (cinema, often pl) toleo la kwanza kabla ya kukaguliwa na kuhaririwa.

rusk n tosti.

Russia n Urusi. ~ leather n ngozi ya

kujalidi. ~n adj -a Urusi. n 1 Mrusi. 2 Kirusi.

rust n 1 kutu. 2 (on plants) kizimwili.

vt,vi ingia/shika kutu. ~ preventive adj -a kuzuia kutu; (fig) chakaa (kwa kutotumika); poteza thamani. ~less adj. ~proof adj -siopata kutu. ~y adj. 1 -enye kutu. 2 -enye kuhitaji mazoezi, -liozeeka, -a zamani. 3 (of blackcloth) -liochujuka. ~ness n.

rustic adj 1 -a kishamba ~speech msemo wa kishamba. 2 -a ovyoovyo. n mshamba. ~ity n ushamba.~ate vt,vi 1 ishi maisha ya kijijini. 2 (GB) fukuza (mwanafunzi kwa muda).

rustle vt,vi 1 chakacha. 2 (US colloq) iba (ng'ombe, farasi, n.k.). 3 ~

rye

something up fanya/tayarisha/tengeneza n mchakacho, mchakarisho. ~r n (US colloq) mwizi wa ng'ombe/farasi. rustling n sauti ya mchakarisho, (pl) mrudiorudio wa sauti hii.

rut1 n 1 alama za magurudumu ya magari (katika mchanga, tope, n.k.). 2 (fig) utaratibu wa kufanya jambo. be in/get into a ~ fuata utaratibu ule ule siku zote bila kubadili wala kufikiria mwingine. vt fanya mifuo njiani.

rut2 n nyege ya vipindi ya mnyama. vi

-wa na nyege ya vipindi.

ruthless adj pasipo huruma; -katili,

-korofi. ~ly adv. ~ness n.

rye n 1 shayiri. ~-bread n mkate wa shayiri. 2 wiski ya shayiri.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

İTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.