TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

V, v n 1 herufi ya ishirini na mbili ya alfabeti ya Kiingereza. 2 alama ya kirumi ya kuwakilisha 5 (tano). 3 alama ya ushindi.

vac n (colloq) (abbr of vacation),

likizo.

vacant adj 1 -tupu ~ space nafasi tupu, pasipo kitu/mtu. 2 wazi. a ~ possession n tangazo la kuwa nyumba wazi (isiyo na mpangaji). 3 (of time) -a kupumzika. 4 (of mind) -sio na wazo; (of the eyes) -sio na (dalili za) shauku/wazo.~ly adv. vacancy n 1 kuwa -tupu; uwazi; pasipo kazi. 2 kutotumika. 3 ujinga, ukosefu wa mawazo. 4 (post unfilled) nafasi wazi. vacate vt 1 hama, ondoka. 2 acha wazi, achilia mbali. 3 (formal) samehe. vacation n 1 (formal) kuacha, kuhama, kuondoka. 2 likizo, livu, muda wa kupumzika court vacation likizo ya mahakama. on vacation likizoni. vi vacation at/in (US) enda likizo. vacationist n (US) mtu aliye likizoni.

vaccinate vt ~ somebody (against something) chanja. vaccination n chanjo; kuchanja. vaccine n dawa ya chanjo.

vacillate vi ~ (between) yumba, babaika, kosa msimamo. vacillation n kutangatanga, kukosa msimamo, kubabaika; kuyumba.

vacuous adj -tupu, sio na akili. ~ly adv. vacuity n.

vacuum n ombwe, tupu. ~ cleaner n

kivuta vumbi. ~ flask/bottle n themosi, chupa ya chai. ~ pump n kivuta hewa; kivuta maji. ~ tube/valve n neli/vali ombwe (ya kuchunguza mkondo wa umeme).

vade-mecum n kitabu (ambacho mtu anaweza kutembea nacho) cha kurejelea.

vagabond n msikwao; mzururaji,

mhuni adj -sio na kwao; zururaji. ~age n uhuni; usokwao, uzururaji. ~ism n uhuni, hali ya mtu kutokuwa na kwao.

vagary n tukio au wazo lisilo la

valour(US valor)

kawaida na lisilo na sababu.

vagina n kuma, uke. ~l adj -a uke.

vagrant n mzururaji adj -zururaji, -a kutangatanga. vagrancy n uzururaji, kutangatanga.

vague adj 1 -sio dhahiri, -a mashaka,

sio wazi, si yakini he was ~ on that subject hakuwa wazi katika mada hiyo. 2 (of persons, behaviour) -a wasiwasi; -sio na uhakika. ~ness n. ~ly adv.

vain adj 1 (useless) ovyo, -siofaa, bure. 2 in ~ bure their efforts were in ~ jitihada zao zilikuwa bure; -sio na heshima, -a kufuru take the name of God in ~ kufuru. 3 -a kujishaua, -a majisifu. ~glory n kiburi; kujiona; majivuno; majisifu, makuu. ~glorious adj -a kujiona, -a kujisifu, -a kuona makuu. ~ly adv 1 bure. 2 (conceitedly) kwa kiburi.

valance; valence n pazia fupi (la maridadi).

vale n (lit except in place names)bonde. valediction n (maneno ya) kuaga, kuagana. valedictory adj -a kuaga, -a kuagana a valedictory speech hotuba ya kuagana.

valence1 n (chem) valensi. valency n kizio cha valensi.

valence2 n see valance.

valentine n (of letter, card etc) barua inayotumwa kwa kipenzi/sahibu (bila jina la mwandishi) tarehe 14 Februari.

valet n mtumishi (wa kiume) afanyaye kazi za udobi. vt fanya kazi za udobi.

valetudinarian n mwele, mgonjwa adj -dhaifu; -gonjwa, nyong'onyevu.

valiant adj shujaa, jasiri, hodari.

~ly adv.

valid adj 1 (leg) halali; -enye sababu thabiti, -a nguvu, -a akili. 2 -a sheria halali. ~ly adv. ~ity n uhalali, uthabiti. ~ate vt halalisha, thibitisha.

valise n mfuko, begi dogo la nguo (agh la safari); mkoba.

valley n bonde.

valour(US valor) n ujasiri (agh wa vitani), ushujaa. valorous adj jasiri,

value

shujaa.

value n 1 thamani. ~ added tax n (abbr VAT) kodi ya nyongeza ya thamani ; thamani ya set a ~ on thamini. 2 faida, manufaa this is of great ~ hii ina manufaa makubwa. 3 (in painting) uhusiano wa mwanga na kivuli; (in language) maana; athari; (pl) maadili. artistic ~s viwango vya sanaa. vt 1 thamini/ tia thamani, kadiria. ~d adj -liothaminiwa; -a thamani a ~d friend rafiki halisi. ~less adj hafifu, -siofaa, bure, -sio na thamani. ~r n mthamini. valuable adj -a thamani; -a tunu. (pl) valuables n vitu vya thamani (k.m. vito n.k.). valuation n kukadiria; ukadiriaji draw up a valuation of something kadiria thamani ya kitu. valuator n mkadiria thamani.

valve n kilango, vali. valvular adj -a vali za moyo/mishipa ya damu.

vamoose vi (US sl) ondoka haraka, potea, ambaa.

vamp1 n kipande cha mbele cha kiatu/buti. vt,vi 1 tia kiatu kiraka. ~ something up (fig) ungaunga. 2 tunga tuni ya wimbo; fuatisha wimbo kwa ala ya muziki.

vamp2 n kiberenge.

vampire n mnyonya damu. ~ (bat) n popo mnyonya damu. vampiric adj

van1 n 1 gari la mizigo/ bidhaa 2 (GB) behewa la mizigo, bogi.

van2 n (of army) kikosi cha mbele.

vandal n mharabu, mshenzi. ~ism n uharabu (wa kishenzi).

vane n 1 kishale (kinachoonyesha

uelekeo wa upepo). 2 propela/tanga liendeshwalo kwa upepo/maji.

vanguard n kikosi cha mbele (fig) watangulizi, viongozi wa maandamano au wa chama; tapo.

vanilla n lavani, vanila.

vanish vi toweka, tokomea, yoyoma. ~ into thin air tokomea, yeyuka. ~ing cream n krimu ya ngozi (inayofyonzwa haraka na mwili). ~ing n kutokomea, kufifia. ~ing

vary

point n mahala mistari sambamba inapoelekea kukutana.

vanity n 1 majivuno, majisifu, kiburi. 2 upuuzi, kutoridhisha. ~ bag/case n kikoba cha vipodozi.

vanquish vt shinda, tiisha.

vantage n manufaa. ~ point n (lit. or fig) mahali pafaapo kutazamia jambo fulani.

vapid adj -chapwa, -dufu, baridi. ~ly adv. ~ness n. ~ity n uchapwa, udufu, ubaridi.

vapour n 1 mvuke. ~ bath n mafusho, buhuri. 2 kitu cha udhanifu; kitu kisicho na maana, upuuzi. 3 the ~s n (arch) majonzi. vaporize vt,vi fusha, fanya mvuke. vaporization n kuvukisha, mvukisho. vaporizer n kivukisho. vaporous adj 1 -a mvuke. 2 (fig) -a njozi.

variable adj -a kugeuka, -a kubadilika, -geugeu. n kigeugeu. variably adv. ~ness n. variability n ugeukaji- geukaji, ubadilikajibadilikaji.

variant n 1 tofauti. 2 kibadala adj -a tofauti, -ingineyo. variance n. at ~(with) kuhitilafiana, kutofautiana; (maths) achano. variation n 1 (kiwango cha) kubadilika; badiliko, mageuzo, tofauti. 2 (of music) lahani iliyorudiwa kwa utata zaidi. 3 mabadiliko ya mwili (yatokanayo na hali mpya). 4 (maths) muachano.

varicoloured adj -a rangirangi.

varicose adj (esp. ~ vein) (veni) -liovimba daima.

variegated adj -a rangi rangi, -a rangi mbalimbali, -a namna nyingi mbalimbali. variegation n.

variform adj -enye maumbo mbalimbali.

varlet n (arch) mshenzi, mwovu.

varnish n 1 vanishi. 2 mng'ao; (fig) sura/taswira danganyifu. vt 1 paka vanishi. 2 pamba, puna; (fig) ficha kosa au dosari fulani. ~er n mpaka vanishi.

varsity n (colloq) chuo kikuu.

vary vt,vi geuza, badili, badilisha;

vascular

geuka, -wa mbalimbali. varied adj 1 mbalimbali, tofauti, -a namna nyingi. 2 -enye mabadiliko mengi; -enye tofauti nyingi. various adj (usu attrib) mbalimbali, anuwai, -a tofauti tofauti, aina aina. variety n 1 tofauti. 2 (collection) jamii (ya vitu mbalimbali) a variety of reasons sababu mbalimbali. 3 (species) namna; (many kinds) namna nyingi. 4 maonyesho (ya aina mbalimbali k.v. sarakasi, nyimbo, igizo n.k.).

vascular adj -enye mishipa ya damu/ utomvu.

vase n chombo (cha kuwekea maua), jagi.

vasectomy n kuhasi: operesheni ndogo ya kumhasi mwanaume.

vaseline n vaselini.

vassal n (hist) 1 mtwana, kijakazi;

(fig) kibaraka. 2 mtumwa; mtumishi. ~age n 1 utwana; (fig) ubarakala. 2

utumwa.

vast adj -kubwa mno, -ingi mno. ~ness n. ~ly adv sana, mno.

vat n pipa kubwa.

VAT abbr value added tax (see value) Vatican n Makao ya Papa/Baba Mtakatifu, Vatikani; (fig) serikali ya Papa.

vaudeville n vichekesho, maonyesho (ya aina mbalimbali).

vault1 vt,vi ruka; ruka juu (kwa kujitegemeza au kwa msaada wa upondo). ~ing-horse n zana ya mazoezi ya kuruka n mruko. ~er n mrukaji (wa upondo).

vault2 n 1 kuba. 2 chumba cha chini kwa chini, ghala ya chini. 3 mfuniko wa kikuba the ~ of heaven (poet) anga. ~ed adj -enye kuba.

vaunt vt,vi (liter) jivuna, (ji)sifu, jigamba. ~er n. ~ingly adv.

veal n nyama ya ndama.

veer vi (esp of the wind), (fig of opinion, talk) badili welekeo.

vegetable n mboga ~ soup supu ya mboga (za majani) adj -a mboga, -a kuhusu mboga (za majani). vegetarian n mla mboga (za majani)

vend

adj -a kula mboga (za majani); vegetarianism n ulaji mboga.

vegetation n 1 uoto, uotaji. 2 mimea. vegetate vi (be idle) jikalia, -la na kulala tu, ishi kama mmea bila kutumia akili.

vehement adj 1 (of feeling) -kali, shupavu. 2 -a nguvu, -a juhudi, -a bidii. vehemence n 1 ukali, harara. 2 juhudi, bidii, nguvu. ~ly adv.

vehicle n 1 gari. 2 (instrument, means) chombo. vehicular adj -a magari.

veil n utaji, shela, barakoa; (fig) utando. draw a ~ over something ficha. take the ~ kuwa mtawa vt funika kwa shela; (fig) ficha, fanya siri. ~ed adj 1 -enye kuvaa utaji/ shela/barakoa. 2 (concealed) -liofichwa, sio wazi. ~ing n kitambaa cha shela, mtandio.

vein n 1 vena. 2 (in leaf) vishipajani. venation n vishipajani, mveneko. 3 (in rock) bamba la jiwe, ufa mwambani. 4 mwelekeo wa mwanzo; hali. ~ed adj -enye nyuzinyuzi; -a vena, -a mshipa wa damu.

velar adj -a kaakaa laini.

veld n (S. Africa) mbuga, tambarare, uwanda.

vellum n karatasi ya ngozi.

velocipede n (Hist) baiskeli ya awali. (US) baiskeli ya watoto.

velocity n kasimwelekeo.

velour n kitambaa kama mahameli.

velvet n mahameli, kiludhu. an iron hand in a ~ glove ukatili uliojificha adj laini (kama mahameli), -a mahameli/bahameli. ~een n nguo kama mahameli. ~y adj laini (kama mahameli).

venal adj 1 (of persons) -a kula rushwa, -a mrungura/hongo ~/ judges/politicians mahakimu/wanasiasa wala rushwa. 2 (of conduct) -a kuhongwa. ~ity n ulaji wa rushwa.

vend vt (chiefly legal) uza, chuuza. ~ing machine n mashine sarafu (ya kuuzia bidhaa ndogondogo). ~ee n

vendetta

mnunuzi. ~er; ~or n mchuuzi.

vendetta n kisasi cha kurithi cha mauaji baina ya jamaa na jamaa.

veneer n 1 ubao-vene: ubao safi mwembamba unaobandikwa juu ya ubao usio bora. 2 (fig) uzuri, upole wa kujifanya/bandia. vt bandika urembo.

venerable adj 1 -a kuheshimiwa (kwa

sababu ya uzee, n.k.); -a heshima, -a kustahiwa. 2 (church of England) Dikoni mkuu. venerate vt heshimu, stahi, tukuza, jali. veneration n.

venereal adj -a zinaa. ~ disease n (abbr VD) ugonjwa wa zinaa.

vengeance n 1 kisasi take ~ lipiza kisasi. 2 with a ~ (colloq) kwa nguvu, sana, kabisa. vengeful adj -a kisasi, -a kutaka kulipa kisasi. ~ness n kutaka kulipa kisasi.

venial adj (of a sin/error/ fault) -a kusameheka, -dogo, -epesi. ~ity n (of sin) udogo.

venison n nyama ya paa.

venom n sumu (ya nyoka, au mdudu); (fig) chuki, inda. ~ed adj -a sumu; (fig) -a inda; chuki. ~ous adj 1 -a sumu. 2 -a chuki, -a inda. ~ously adv.

venous adj 1 -a ndani vena ~ blood damu ya vena. 2 (bot) -enye vena ~ leaf jani lenye vishipajani.

vent n 1 tundu, kitundu cha kutokea gesi/hewa/maji. ~ hole n tundu la kutolea moshi, harufu, mvuke. 2 (trade use) mchano. 3 njia ya kutorokea/kupitia. 4 (sing only) liwazo. give ~ to (fig) toa mawazo bila woga. vt ~ something on somebody/something toa nje. ~ilate vt 1 pitisha hewa safi, burudisha kwa hewa. 2 (fig) eneza, tangaza, jadili. ~ilation n. ~ilator n tundu la (chombo cha) kupitisha hewa.

ventricle n ventrikali: uwazi (ndani ya mwili/ogani n.k.).

ventriloquism n kutoa sauti kama kwamba inatoka kwa mtu mwingine mbali kidogo. ventriloquist n.

venture n jambo la hatari ~ scout

verger

skauti n mwandamizi. vt, vi thubutu; jasirisha nothing ~, nothing gain/ win/have (prov) kujaribu si kushindwa adj 1 -a kujaribu (of persons) 2 jasiri, hodari. 3 (of acts, behaviour) -a hatari; -a kubahatisha. venturous adj. ~some adj -a ujasiri.

venue n mahali pa kukutanikia,

makutano.

Venus n 1 (astron) ng'andu, zuhura. 2 (Roman myth) mungu wa kike wa mapenzi/uzuri.

veracious adj (formal) -a kusema kweli, -a kweli, -nyofu. ~ly adv. veracity n 1 kweli, ukweli. 2 unyofu.

veranda(h) n veranda, baraza; roshani. verb n kitenzi auxiliary ~ kitenzi

saidizi. ~al adj 1 -a tendo; -a mdomo. 2 -a maneno tu. 3 (literal) sisisi. 4 -a kitenzi. ~ally adv kwa maneno (si kwa maandishi), kwa kusema. ~alism n 1 msemo. 2 msamiati. 3 maneno tu. ~alist n msemaji ovyo, mropokaji. ~alize vt sema, toa kauli. ~atim adv, adj sisisi; kwa maneno yenyewe hasa, kwa kunukuu, kama ilivyosemwa.

~iage n (use of) domo, maneno mengi ya bure, maelezo ya mzunguko. ~ose adj -a maneno mengi. ~osely adv. ~oseness. n ~osity n.

verdict n 1 hukumu, uamuzi. 2 (decision) maoni, mkataa.

verdigris n kutu ya shaba.

verdure n (lit) majani, miti, mimea, majani ya chanikiwiti. verdant adj 1 (lit) (esp of grass, vegetation field) -a majani mabichi, -a chanikiwiti; -a kustawi. 2 (fig) jinga, siojua mambo, shamba. verdancy n.

verge n ukingo, kando; (limit)

mpaka, mwisho. be on the ~ of. bring (somebody) to the ~ of karibia; leta karibu karibu ya/katika ukingo. vi ~on/upon pakana (na), karibia.

verger n 1 (church of England)

verify

msimamizi (awaonyeshaye watu mahali pa kukaa). 2 mbeba rungu (la askofu au makamu wa mkuu wa chuo).

verify vt 1 thibitisha, hakikisha. 2 dhihirisha. verifiable adj -a kuthibitika. verification n hakika, thibitisho.

verily adv (arch) kweli.

verisimilitude n kuonekana kama kwamba ni kweli. verisimilar adj kinachoelekea ukweli, -a kuaminika.

verity n 1 (old use) kweli. the eternal verities n sheria za Mungu. veritable adj -a kweli, -a hakika. 2 kanuni.

vermicelli n tambi.

vermicular adj -a funza, -a mchango, -a mnyoo. vermiform adj -enye umbo la mnyoo.

vermilion n rangi nyekundu kama damu adj -ekundu, -a rangi ya damu.

vermin n mnyama/mdudu mharibifu; (of human) (fig) doezi. ~ous adj 1 haribifu, angamizi. 2 -enye kupe/ chawa/utitiri n.k. -liosababishwa na wadudu/wanyama waharibifu. vermiverous adj -enye kula wadudu.

vernacular n 1 lugha ya wenyeji. 2

lahaja in the ~ kwa lahaja ya kienyeji adj -a lahaja.

vernal adj -a majira ya kuchipua/ kumea. the ~ equinox n tarehe 21 Machi.

verruca n dutu, sugu ya mguu.

versatile adj 1 hodari na -enye kupendelea mambo mbalimbali. 2 -enye akili nyepesi, elekevu sana. 3 (changeful) geugeu, -badilifu, si thabiti; -enye matumizi mbalimbali. versatility n.

verse n 1 ushairi. 2 (of Bible/Koran) aya. 3 ubeti. give chapter and ~ for toa kumbukumbu halisi; tongoa mstari wa shairi. ~-reading n usomaji wa mashairi (beti na vipande). versification n 1 sanaa ya ushairi. 2 muundo wa shairi. versifier n mtunga mashairi (hasa ya ovyo). versify vt,vi tunga mashairi; geuza kuwa mashairi.

vessel

versed adj ~ (in) -juzi, -enye maarifa ya be ~ in something topea katika jambo.

versicolour adj -enye rangi nyingi,

-a rangirangi.

version n 1 tafsiri. 2 (account) masimulizi, habari kama ilivyotolewa na mtu.

verso n ukurasa wa kushoto; upande wa pili wa sarafu.

verst n kipimo cha kirusi sawa na futi 3500.

versus prep (often shortened to V or vs) dhidi ya.

vertebra n (pl) 1 pingili la uti wa mgongo. 2 (pl) wanyama wenye uti wa mgongo. ~l adj -a uti wa mgongo. ~l column n uti wa mgongo. ~te adj -enye uti wa mgongo n mnyama mwenye uti wa mgongo.

vertex n kilele, kipeo.

vertical adj -a wima; (overhead) utosini. ~ly adv.

vertigo n kisulisuli, kizunguzungu, kisunzi. vertigious adj.

verve n raghba, moyo, hamasa.

very adj 1 enyewe; kweli, hasa in ~deed hasa, bila shaka in ~ truth kwelikweli, kwa kweli. 2 -ileile the ~ same yule yule in this ~ place papa hapa come here this ~ minute njoo sasa hivi adv 1 sana, kabisa; (with superlative adj) the ~ lowest ile ya chini kabisa. 2 (to emphasize/ sameness or difference) the ~ same colour rangi ileile. 3 (to intensify adj and adv) ~ good nzuri sana. ~ well vizuri sana; (often indicating agreement) haya! vema! 4 (to emphasize possession) my ~ own -angu mwenyewe.

Very; Verey adj ~ light n fataki ya rangi (kama ishara ya matatizo baharini).

vesicle n kilengelenge. vesicular adj -a lengelenge.

vesper n 1 nyota ya jioni, zuhura. 2

(pl) ~s n sala za jioni.

vessel n 1 chombo (kama kikombe,

vest

bakuli). 2 (ship) chombo, jahazi, meli, merikebu. 3 (vein) mshipa.

vest1 n 1 fulana. 2 (waistcoat) kizibao.

vest2 vt,vi 1 ~ something in somebody. ~ somebody with something weka, wekea, kabidhi -pa. have a ~ed interest in something wa na maslahi. 2 ~ in (of property etc) -wa na. kabidhiwa, pewa. 3 vaa, vika. ~ed adj.

vestibule n 1 ukumbi. 2 ukumbi wa nje (wenye lango la kanisa). 3 chumba maalum mwishoni mwa behewa.

vestige n 1 alama, dalili baki, sazo. vestigial adj -a alama, -a mabaki; -a kumbukizi. 2 (anat) (kiungo/sehemu) salio la kitu kilichokuwepo zamani adj liobaki kama salio.

vestment n vazi rasmi (hasa la kasisi).

vestry n 1 chumba cha kuvalia nguo kanisani. 2 (parish council) baraza la waumini. 3 chumba cha sala/ mafundisho ya dini/mikutano. ~ clerk n karani (wa baraza la waumini). ~man n mjumbe wa baraza la parokia.

vesture n mavazi. vt visha.

vet n (colloq abbr for veterinary surgeon) mganga wa mifugo. vt 1 (colloq) (hum) pima mtu (afya yake). 2 (manuscript) hakiki, chunguza kwa makini.

veteran n mkongwe;(of cars) -liotengenezwa kabla ya 1916; (in US) askari mstaafu adj -kongwe, aliyebobea. V~s Day n Siku ya kukumbuka mwisho wa vita ya Kwanza ya Dunia (Novemba 11).

veterinary adj -a kuhusu elimu ya

maradhi ya wanyama ~ surgeon n mganga wa wanyama ~ service huduma ya utabibu wa mifugo.

veto n kura ya turufu (ya kisheria) ya kukataza jambo lisifanyike. vt kataza, chelewesha, piga marufuku; tilia guu.

vex vt 1 chokoza; udhi, chukiza. ~ed question n suala tata lenye kuzua mabishano mengi (lakini lisilokatika). 2 (poet, rhet) chafua (bahari). ~ation n 1 uchokozi; maudhi;

chukizo/chusho. 2 jambo la uchokozi; maudhi na chuki. ~atious adj -chokozi; -a kuudhi, chushi.

via prep kupitia, kupita kwa njia ya.

viable adj -a kuweza kuwapo; -enye

uwezo wa kujitegemea. viability n kuwezekana; kujitosheleza.

viaduct n daraja refu linalovuka bonde au korongo.

vial n kichupa kidogo (hasa cha dawa ya maji).

via media (lat) njia/mrengu wa kati.

vibes n (sl) hali/upepo.

vibrate vt,vi 1 tikisa, tingisha;

tikisika, tingishika. 2 yumbayumba, wayawaya, taharuki. vibrant adj -a kutetemeka, -a kutikisika; -a kutaharukia,/kusisimua. vibrancy n. vibration n mtetemo; mtikisiko; vibrator n kitingishi.

vicar n (Anglican) kasisi/ padre wa

usharika; (RC) mwakilishi, naibu wa ~ of Christ wakili wa Kristu. ~age n nyumba/ maskani ya padri/kasisi. ~ious adj 1 -a kuwakilishwa. 2 -liofanywa kwa ajili ya wengine; -liotendwa kwa niaba ya. ~iously adv.

vice1 n 1. uovu. 2 (in a horse) tabia/ mazoea mabaya. vicious adj 1 -ovu, -enye makosa a vicious argument hoja potofu. 2 -a inda, -fisadi, fasiki. vicious circle n mzunguko/hali inayoashiria mkwamo. vicious spiral n upandaji wa bei unaotokana na upandaji bei ya kitu kingine. 3 (animal) -kali, -baya. viciously adv kwa ukali; kwa uovu; kwa makosa. viciousness n ubaya; ukali.

vice2 n jiliwa ya seremala as firm as a ~ imara sana a ~ like grip mbano imara sana.

vice3 (pref) -dogo; naibu; makamu. ~-admiral n makamu wa admirali. ~-chairperson n makamu mwenyekiti. ~-chancellor n makamu mkuu wa chuo kikuu. ~-premier n naibu waziri mkuu. ~president n makamu wa rais.

viceroy

~-presidency n umakamu wa rais.

viceroy n kaimu mfalme, mwakilishi wa mfalme/gavana mkuu. viceregal adj -a makamu mfalme. vicereine n mke wa makamu mfalme.

vice versa adv kinyume chake.

vicinity n 1 ujirani, kuwa karibu. 2

jirani.

vicissitude n mabadiliko, mageuko (hasa katika bahati ya mtu maishani).

victim n 1 kafara, mhanga. 2 mwathiriwa na janga (ambalo hakulisababisha yeye, mtu (au mnyama) anayesumbuka au kuuawa au kupatwa na mabaya asiyostahili, kwa ajili ya mwingine. ~ize vt onea, sumbua. ~ization n maonevu uonevu.

Victorian n,adj (person) (-a enzi ya) Malkia Victoria.

victory n ushindi. victor n mshindi, mshindaji. victorious adj -lioshinda, -liofaulu; -a shangwe, -a ushindi, (-shindi). ~victoriously adv.

victual vt,vi 1 wekea akiba ya vyakula; -pa vyakula. 2 pakia vyakula (melini n.k.). n (pl) vyakula na vinywaji. ~ler n 1 mfanya biashara ya vyakula. 2 licensed ~ler n (GB) mwenye leseni ya baa na hoteli.

vide vt (lat) tazama. ~ infra vi tazama chini. ~ supra vi tazama juu.

videlicet adv (common abbr viz) yaani.

video adj 1 -a video; -a (matangazo ya) televisheni. 2 -a kunasa sauti na picha. n 1 (colloq) video. 2 (US) televisheni. ~ tape n ukanda wa televisheni/video. vt piga picha za video.

vie vi ~ (with somebody) (for something) shindana na/chuana.

view vt 1 tazama, angalia; kagua. an order to ~ hati/madaraka ya kukagua nyumba n.k. 2 fikiria. ~er n 1 mtazamaji televisheni. 2 kifaa cha kukuzia picha. ~less adj 1 -sioonekana. 2 (US) bila maoni. n 1 kutazama, kuangalia; upeo wa macho. in ~ of kwa kuzingatia. in full ~ of -enye kuonekana waziwazi.

villain

on ~ -nayoonyeshwa. come into ~ onekana, tokeza. come in ~ of weza kuona. 2 sura, mandhari; picha ya mandhari. 3 nafasi ya kuona; ukaguzi. 4 (opinion) maoni, rai, shauri. fall in with/ meet somebody's ~s kubaliana na. 5 nia, kusudio. with a/the ~ to/of kwa nia/matumaini ya. 6 (compounds) ~ finder kioo katika kamera cha kutafutia taswira.

vigil n 1 kukesha; ukeshaji (kwa ibada/ulinzi) keep ~ kesha. 2 mkesha (wa shughuli za dini).

vigilance n hadhari, uangalifu, kuwa macho. ~ committee n kamati ya sungusungu/wazalendo ya kudumisha amani katika jamii au mahali ambapo hapana uongozi.vigilant adj macho, -angalifu, -enye hadhari. vigilantly adv. vigilante n memba wa kamati ya wazalendo.

vignette n 1 nakshi/sanamu/picha ndogo nzuri (hasa kwenye jalada la kitabu au mwanzo/mwisho wa sura). 2 picha ya kichwa na mabega (ya mtu). 3 muhtasari wa tabia ya mtu.

vigour (US = vigor) n 1 nguvu. 2

wepesi, bidii, juhudi. 3 makali (ya lugha). vigorous adj 1 -a nguvu. 2 -a juhudi, -epesi, hodari. vigorously adv.

Viking n mmoja wa maharamia wa

Scandinavia walioshambulia na kuteka nyara pwani ya Ulaya kati ya karne ya 8 na ya 10.

vile adj 1 -enye kutia aibu; -a kuchukiza; ovu. 2(colloq) -baya. 3 (old use) -a bure, -sio na thamani. ~ly adv. ~ness n uovu; upotovu; ubaya.

vilify vt tukana, singizia, kashifu; sengenya. vilification n masingizio, maovu, masengenyo

villa n nyumba ya shamba yenye bustani kubwa.

village n kijiji; kitongoji. ~r n mwanakijiji.

villain n mhalifu, mwovu. ~ous adj -baya sana, ovu, halifu. ~y n.

villein

villein n mtwana/kijakazi (wakati wa enzi za ukabaila). ~age n.

vim n (colloq) nguvu, juhudi, full of ~ enye nguvu.

vinaigrette n achari (ya siki, mafuta naviungo).

vindicate vt thibitisha. vindication n uthibitisho.

vindictive adj -siosamehe; -a kutaka

kulipa kisasi. ~ly adv kwa kulipiza kisasi. ~ness n ulipizaji kisasi.

vine n mzabibu. ~-dresser n mlimaji (mtunza) wa mizabibu. ~ry n nyumba inamomea mizabibu. ~yard n shamba la mizabibu.

vino n (colloq) divai, mvinyo. ~us adj -a divai, kama divai.

vint tengeneza divai. ~age n 1 msimu wa zabibu. 2 divai ya msimu fulani. 3 -a kipindi kilichopita/kilichosifika kwa ubora ~age car motokaa iliyoundwa kati ya mwaka 1916 - 1930. ~ager n mvunaji mizabibu. ~ner n muuza divai ~nery n ghala ya divai.

vinegar n siki. ~y adj kama siki; (fig) -enye kughadhibika, -a hamakihamaki.

vinyl n ngozi ya plastiki (ya kutengenezea mikoba, masanduku, viatu, busati n.k.).

viola n fidla kubwa (la sauti nyembamba).

violate vt 1 kiuka (kiapo, mkataba n.k.). 2 ingilia (faragha ya mtu, sehemu iliyo wakfu) bila heshima. 3 baka, ingilia mtu kwa nguvu. violation n. violator n mvunja sheria.

violent adj 1 -a nguvu nyingi 2. -kali sana. ~ly adv. violence n vurugu, nguvu robbery with violence wizi wa nguvu. do violence to something (fig) kuwa kinyume cha; kasirisha.

violet n urujuani.

violin n fidla. ~ist n mpiga fidla.

viper n kipiribao: nyoka mwenye sumu kali; (fig) mtu wa hila, inda na udanganyifu.

virago n mwanamke mgomvi, mwenye

virtuoso

makelele.

virescence n hali ya kuwa kijani kibichi. virescent adj -a kijani kibichi.

virgin n bikira, mwanamwali. (the

Blessed) V~ (Mary) Bikira Maria adj 1 -safi kabisa, -sioguswa ~ snow theluji safi isiyoguswa. 2 -liotakaswa. the ~ birth n uzao mtakatifu. 3 -a asili,-siotumika ~ forest msitu usioguswa bado ~ soil ardhi isiyolimwa bado. ~al adj 1 -a mwanamali, -a bikira 2. -safi. ~ity n ubikira.

virgo n mashuke.

virgule n mkwaju/mstari wa mshadhari wa kutenga maneno (kama katika na/ au).

viridescent adj -a kijani kibichi. viridescence n. viridity n 1 kijani kibichi. 2 ulimbukeni, ushamba.

virile adj 1 -a kidume, -enye nguvu na tabia za kidume, -a nguvu. 2 (of man) rijali, -enye nguvu za kiume. virility n urijali; nguvu za mwanamume za uzazi.

virtu n (only in) articles/objects of ~ vitu vya kupendeza kutokana na usanifu wa sanaa yake/utunu wake n.k.

virtual adj -a kweli (lakini si bayana). ~ly adv.

virtue n 1 wema, maadili. make a ~ of necessity fanya jambo la lazima na kujitia ni kutokana na wema. ~ is its own reward (prov) tenda wema wende zako. the cardinal ~s n nyemi/nemsi za asili. the theological ~s n nyemi/nemsi za kidini. 2 utakatifu, usafi. 3 nguvu, uwezo. 4 ubora; manufaa. 5 by/in ~ of kwa sababu,kwa ajili ya. virtuous adj -ema/adilifu; -enye huruma; -lio bora; -lio safi, takatifu. virtuously adv.

virtuoso n stadi wa elimu hasa ya muziki; mweledi, mtu mwenye maarifa/vionjo vya kazi za sanaa. virtuosity n ujuzi wa mwana sanaa. weledi.

virulent

virulent adj (of poison) -kali, -a kuua;(of words) kali sana; (of diseases) -enye sumu kali. ~ly adv. virulence n.

virus n virusi: viumbe hai ambao kiumbile hawajafikia ngazi ya seli. virology n virolojia: elimuvirusi.

visa n viza. vt -pa viza.

visage n (liter) uso, sura (ya mtu). ~d adj (suff) -enye uso.

vis-a-vis adv 1 uso kwa uso, -a kuelekeana. 2 (fig) kwa kulinganisha na, kwa kuhusiana na. n kitu kinachoelekeana na kingine; mwenzi.

viscera n viungo vya ndani (hasa matumbo). ~l adj -a viungo vya ndani; -a hisia za ndani.

viscid/viscus adj -a kunata (kama ulimbo). ~ity n 1 kunata; unato, mnato. 2 uzito. viscosity n.

vise n (US) jiliwa.

visible adj -a kuonekana wazi.

visibility n hali ya kuonekana wazi visibility is bad mwangaza hautoshi. visibly adv wazi.

vision n 1 kuona. 2 maono; kivuli,

ndoto. 3 (insight) uwezo wa kuona mbali/mbele, busara. 4 mwanga, nuru. ~ary adj 1 -a kubuni tu, si hakika; -a njozi, -a ndoto. 2 (of persons) -enye fikra za kinjozi; -enye uwezo wa kuona mbali. n ary person mtu mwenye uwezo wa kuona mbali.

visit vt,vi 1 zuru, enda kuamkia, tembelea. 2 (chiefly US) kagua. 3 (chiefly US) ~ with tembelea, ongea na. 4 ~ something on somebody (biblical use) patiliza, adhibu. ~ the sins of the fathers upon the children adhibu watoto kutokana na makosa ya wazazi. ~ant adj,n 1 (liter) mgeni mashuhuri; mzuka. 2 ndege mhamaji. n kuzuru, kutembelea; ziara. ~ing n kutembelea, kuzuru. ~ation n 1 tume rasmi. 2 mapatilizo/adhabu ya kidini (agh baa). 3 (of animals) mkurupuko. ~or n 1 mgeni state ~or mgeni wa serikali ~or`s book kitabu cha wageni. 2 mkaguzi.

vivacious

visor n (sun) ~ n kioo cha gari

kinachopunguza mwanga.

vista n 1 taswira, upeo unaoonekana

katika nafasi nyembamba; mandhari. 2 (fig) mfululizo wa taswira/ mandhari/matukio n.k.

visual adj -a kuona, -a macho. ~ aids n (in teaching) vielelezo (vya kufundishia). ~ly adv. ~ize vt pata sura, piga taswira kichwani. ~ization n.

vital adj 1 -a uzima, -a uhai, -a lazima kwa uzima/kwa uhai. the ~ force/principle n roho/uhai. ~ statistics n takwimu muhimu (inayohusu urefu wa maisha na uzazi, ndoa na vifo); (colloq) vipimo vya mwanamke, vya kifua, kiuno na mapaja. 2 -kuu, -a kiini hasa. ~s n (pl) viungo muhimu vya mwili hasa mapafu, moyo, ubongo. ~ly adv. ~ism n imani ya kuwa kuna nguvu katika viumbe inayotawala uhai/roho mbali na ile ya kikemia. ~ist n. ~ity n uzima, uhai, nguvu tendaji; uchangamfu. ~ize vt jazwa na nguvu, ingiza nguvu, jipa tumaini, jadhubisha.

vitamin n vitamini.

vitiate vt haribu, punguza nguvu, rahisisha, dhoofisha. vitiation n 1 kuharibu; kuharibika. 2 upunguo/ upungufu, urahisisho.

vitrify vt,vi geuza kuwa kioo; geuka

kioo. vitrification n mageuzo (hasa kuwa kioo). vitreous adj -a kioo, kama kioo.

vitriol n mrututu, asidi ya salfa; (fig) kejeli. ~ic adj (fig of words feeling) chungu, kali; -a kejeli. ~ize vt.

vituperate vt tukana; laani.

vituperative adj -a kutukana. vituperation n matusi; laana, maneno ya kulaani.

viva n (colloq) see viva voce interj. idumu!

vivace adv (music) kwa kuchangamka/ uchangamfu.

vivacious adj -changamfu, kunjufu, -a furaha, cheshi, -enye bashasha.

viva-voce

~ly adv. vivacity n uchangamfu, ukunjufu, bashasha, ucheshi.

viva-voce adj -a mdomo ~examination or test mtihani wa mahojiano; jaribio la kuzungumza.

vivid adj 1 (of colours etc) -lioiva, nga'vu. 2 liochangamka. 3 wazi, dhahiri. ~ly adv 1 kwa dhahiri, waziwazi. 2 kama kwamba ni kweli. ~ness n udhahiri, ung'avu; kung'aa.

vivify vt (esp fig) 1 tia uhai, amsha, huisha. 2 chochea. vivification n.

viviparous adj (zool) -a kuzaa watoto.

vivisect vt pasua/fanya jaribio la kisayansi (kwa viumbe hai). ~ion n. ~ionist n.

vixen n 1 mbweha jike. 2 mwanamke mgomvi/mwenye gubu/hasira. ~ ish adj -gomvi.

viz adv (lat videlicet, usu spoken) yaani, ndiyo kusema.

vizier n (in some Muslim countries) waziri grand ~ waziri mkuu.

vocable n neno (hasa muundo wake).

vocabulary n 1 msamiati. 2 maneno.

vocal adj 1 -a sauti the ~ organs ala za sauti (ulimi, midomo n.k.) ~ music muziki wa kuimbwa. ~ly adv kwa sauti. ~ist n mwimbaji. ~ic adj 1 -a vokali, -a irabu. ~ism n 1 utumiaji sauti (katika kusema/ kuimba). 2 mfumo wa irabu. ~ize vt sema/imba kwa sauti, toa sauti ya kusikika; tia/andika irabu. vi toa sauti, piga kelele. ~ization n. vocative adj, n kauli ya mneni.

vocation n 1 (sing only) (of social or religious) wito. 2 (special attitude) welekevu, moyo, uwezo. 3 kazi, shughuli, utaalamu; weledi. ~ al adj -a kazi, -a utaalamu.

vociferate vi,vt piga makelele. vociferation n sauti kubwa, makelele. vociferous adj -a makelele. vociferously adv kwa makelele.

vodka n vodka: pombe kali ya Kirusi.

vogue n 1 mtindo wa sasa, fashini. 2 kupendelewa/kupendwa kwa jambo; -kupokelewa; kukubalika. be in/come into ~; be/go out of ~ wa/tokuwa

volt

katika fashini, pendelewa/ -topendelewa. all the ~ mtindo unaopendwa kote.

voice n 1 sauti, mlio. 2 (uwezo wa)

kutoa sauti. 3 sauti ya mtu in a loud ~ kwa sauti kubwa. lift up one's ~ (old use) toa sauti (imba, sema). shout at the top of one's ~ toa usiyahi. with one ~ (liter) kwa kauli moja. 4 a/some/no etc ~ in something haki/kutokuwa na haki ya kutoa maoni. 5 wito; hiari; maono; hisia the ~ of God/Nature; the ~s of the night dhamira. 6 (in phonetics) sauti irabu/konsonanti. 7 (gram) kauli (ya kutenda/kutendwa). vt 1 sema, eleza. 2 tamka irabu/ konsonanti. ~d adj (in compounds) -a ghuna. ~less adj -sioghuna (mfano p,f).

void adj 1 tupu, pasipo mtu, wazi. 2 ~ of -siokuwa na, bila, bure. 3 null and ~ (leg) batili, -siofaa. n uwazi, upweke. vt (leg) tangua, batilisha; futa. ~able adj -a kufutika, -a kubatilika. ~ance n.

voile n kitambaa chepesi cha gauni.

volatile adj 1 (of a liquid) fukivu/ fushi, -a kugeuka hewa (mvuke). volatilize vt,vi fukiza, geuza kuwa hewa/mvuke, fusha. volatilization n. 2 (of a person) cheshi, changamfu, -enye kuingilika, -a watu; epesi kubadilika. volatility n kugeuka hewa.

volcano n volkano. volcanic adj -a

volkano.

vole n buku.

volition n hiari, ridhaa; chaguo, moyo, akili of one's own ~ kwa hiari. ~al adj.

volley n 1 mshindo (wa makombora,

bunduki nyingi n.k. zikipigwa pamoja). 2 mfululizo (wa maapizo, matusi, maswali n.k). ~-ball n mpira wa wavu. vt,vi (of guns) lia sawia; (of tennis) jibu pigo (kabla mpira kugonga chini).

volt n volti, kizio cha nguvu ya umeme. ~age n volteji. ~aic adj.

volte-face

volte-face n mgeuko, badiliko kamili;

ugeukaji kabisa.

voluble adj msemi, -semaji, -epesi/hodari wa kusema. volubility n usemaji. volubly adv.

volume n 1 juzuu. speak ~s for shuhudia sana, onyesha wazi. 2 nafasi, ujazo. 3 (great quantity) ukubwa, wingi, chungu ~ of production wingi wa uzalishaji (bidhaa). 4 nguvu ya sauti, sauti kubwa. voluminous adj. -kubwa; -enye kuchukua nafasi kubwa; (of an author) -enye kuandika vitabu vingi.

voluntary adj 1 -a hiari, bila

kulazimishwa; -a kupenda mwenyewe. 2 -a bure, pasipo mshahara, -a kujitolea. 3 (of muscle) -nayodhibitiwa na utashi wa mtu. n 1 wimbo wa kinanda unaopigwa nje ya ibada. voluntariness n hiari. voluntarily adv.

volunteer n 1 mtu ajitoaye. 2 askari wa kujitolea. vi,vt 1 ~ something/to do something/for something jitolea kitu/ kufanya kitu/kwa kitu (kwa kazi fulani) jiandika (kwa hiari). 2 (offer freely) toa kwa hiari.

voluptuous adj -a anasa nyingi, -a ashiki, -a kutia ashiki, nyegereshi. voluptuary n mpenda anasa/maraha, mwenye ashiki. ~ness n ashiki. ~ly adv.

vomit vt,vi 1 tapika. 2 (emit) toa, foka, bubujisha. n matapiko, matapishi.

voodoo n uchawi, ulozi, vuudu ~ doctor mchawi.

voracious adj -lafi; -enye uroho. ~ly

adv kwa uroho. ~ness n. voracity n ulafi, kula sana, uroho.

vortex n 1 kizingia (cha maji/hewa). 2 (fig) hekaheka, mvuto (katika shughuli fulani); mishughuliko. vortical adj -a kuzingia. vortiginous adj (arch) -liozingia.

votary n mfuasi (wa jambo fulani).

vote n 1 (haki ya kupiga) kura. put something to the ~ pigia kura. 2 idadi ya kura. 3 kasma. vi, vt 1 ~ for/against somebody/something

vulgar

pigia kura ya ndiyo/hapana. ~ on something pigia kura. 2 ~ somebody/something (for something) -pa/toa fedha kwa madhumuni fulani. 3 ~ something down shinda kwa kura. ~ something through pitisha, kubali, idhinisha (kwa kura). 4 (colloq) tangaza kwa kutumia maoni ya watu. 5 pendekeza, shauri. ~r n mpiga kura. ~less adj -sio na haki ya kupiga kura.

votive adj -liotolewa/wekwa wakfu ili kuondoa nadhiri.

vouch vi,vt ~ for somebody/something dhamini, chukua dhima, amini/kiapo.

voucher n vocha, hati ya malipo. gift ~ n vocha ya kupewa zawadi. luncheon ~ n vocha ya kupewa chakula cha mchana hotelini.

vouchsafe vt (formal) kubali, toa/fanya kwa moyo.

vow n kiapo; nadhiri. vt weka

nadhiri.

vowel n irabu, vokali back ~ irabu

nyuma front ~ irabu mbele.

vox n (Lat) sauti. ~ populi n sauti ya

umma; maoni ya watu.

voyage n safari (baharini n.k.). vt safiri (kwa chombo, katika jahazi, meli), abiri. ~r n abiria, msafiri (melini, chomboni).

voyeur n mtu apataye burudani/ashiki kwa kuchungulia uchi wa mtu au watu wakijamiiana.

vulcanite n plastiki ngumu, vulkaniti. vulcanize vt vulkanisha; changanya mpira na salfa kutengeneza plastiki ngumu. vulcanization n.

vulgar adj 1 sio na adabu, -a kishenzi, -tovu wa adabu, pujufu. 2 -a kawaida, -a watu wote; -a wingi wa watu. ~ fraction n fraksheni ya kawaida. (mf 1/2). the ~ herd n makabwela. the ~ tongue n lugha ya kienyeji. ~ly adv. ~ian n mtu tajiri mwenye tabia ya kishenzi. ~ism n usemi (neno) wa kishamba. ~ity n ushenzi, ufidhuli, ujuvi,

vulnerable

usafihi, ukosefu wa adabu, utovu wa adabu; upujufu. ~ize vt tweza; rahisisha; eneza kwa watu wote, fanya -a watu wote. ~ization n.

vulnerable adj -enye kuweza kudhuriwa, sio salama; siolindwa. vulnerability n.

vulpine adj 1 kama mbweha. 2 (cunning) -erevu, -janja.

vulture n 1 tai. 2 mtu mchoyo anufaikae kutokana na mikosi ya wengine. vulturous; vulturine; vulturish adj -a tai, kama tai.

vulva n kuma.

vying vt see vie.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.