TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

W,w n herufi ya ishirini na tatu ya abjadi ya Kiingereza.

wacky adj (of people, ideas, behaviour) (sl) -a kipuuzi; pumbavu.

wad n 1 fusho: matambara/takataka laini za kufungashia/tenganishia vitu. 2 (of notes) bulungutu: kibunda cha noti (fedha) vt 1 ziba/ jaza kwa pamba/matambara/ takataka laini n.k. ~ ding n kitu chororo (agh pamba) cha kushindilia na kuzuia vitu visicheze.

waddle vi tagaa n (sing only) mtagao.

wade vi,vt enda/pita/jivuta kwa shida (matopeni, n.k.). wading bird n ndege atembeaye majini kama kitwitwi. ~ in shambulia kwa nguvu. ~ into sth shambulia vikali. ~r n 1 kitwitwi, kiulimazi. 2 (pl) ~rs n gambuti: viatu virefu vya juu ya magoti.

wadi n (in the middle East, Arabia, Northern Africa) korongo kavu la mto.

wafer n 1 biskuti nyembamba. 2 mkate wa ushirika mtakatifu.

waffle1 n keki ndogo ya rojo ya unga, maziwa na mayai iliyookwa kwenye kikaango.

waffle2 vi (GB colloq) bwabwaja, bwata, payuka n mapayo.

waft vt,vi peperusha; peperuka, chukuliwa (na upepo, maji) n 1 pumzi; harufu nzuri (ya kunukia) n.k. 2 mwendo wa mawimbi.

wag1 vt,vi tikisa ~ one's finger at sb onyesha kidole mtikiso, mtikisiko. ~ tail n kitwitwi.

wag2 n mcheshi, bashasha. ~gery n bashasha, ucheshi. ~gish adj cheshi. bashasha. ~gishly adv.

wage1 vt endeleza, pigana, fanya

(vita, kampeni).

wage2 n (usu pl) 1 ujira; ijara;

mshahara a living ~ mshahara wa kujikimu minimum ~ kima cha chini cha mshahara. ~ claim n dai la mshahara. ~earner n mfanyakazi. 2 (old use; pl in form with sing v) malipo.

wager n 1 dau. lay a ~ pinga vt,vi weka dau, pinga.

waggle vt,vi tikisatikisa.

wake

waggon (US usu wagon) n 1

mkokoteni; gari la kukokotwa na farasi maksai. on the (water) ~ (colloq) siye kunywa pombe. 2 (US freight car) chakara: behewa la wazi la mizigo. station ~ n (US) gari dogo la abiria na mizigo. ~er n mwangalizi wa gari la kukokotwa na farasi wake. ~-lit n behewa la kulala.

wagtail n see wag.

waif n 1 msokwao (hasa mtoto) ~s

and strays watoto wasokwao na waliotelekezwa.

wail vi,vt 1 omboleza, lia kwa huzuni; (of the wind) fanya sauti kama mtu anayelia n maombolezo; uliaji.

wain n (old use or poet) mkokoteni mkubwa wa shambani (wa kukokotwa na farasi).

wainscot n mbao za ukutani (ndani ya nyumba) agh kuanzia chini hadi kufikia nusu ya ukuta vt ~ed adj -liowekwa mbao za ukutani.

waist n 1 kiuno. ~band n mkanda wa nguo. ~-cloth n shuka; kikoi. ~ deep adj, adv -a kufika kiunoni. ~high adj -a kufika kiunoni. ~line n kiuno. 2 (naut) sehemu ya kati ya meli. ~ coat n kizibao.

wait n 1 (kitendo cha) kungoja, kusubiri. 2 lie in ~ for; (less usu) lay ~ for vizia, jificha ili kushambulia. 3 (pl) the ~s n waimbaji wa nyimbo za Noeli waendao nyumba hadi nyumba vi,vt 1 ~ (for) ngoja, ngojea, subiri. keep sb ~ing ngojesha mtu. ~ up (for sb) kesha. No ~ing usingoje ~ and see ngoja uone this can ~ hii inaweza kusubiri. 2 ~ (for) ahirisha. 3 ~ on/upon sb tumikia, -wa kama mtumishi wa kutumwa. ~ on sb hand and foot kidhia haja zote, tumikia kwa kila hali; (colloq) (old use) tembelea, zuru. 4 ~ at/on hudumia mezani. 5 ~ing list n orodha ya wanaosubiri. ~ing-room n chumba cha wanaosubiri. ~ern. ~ress n mhudumu, mwandikaji.

waive vt 1 samehe, acha kudai (haki au dai). ~r n (leg) (written statement) hati ya kusamehe madai.

wake1 vi,vt 1 ~ (up) amka. 2 ~ sb up amsha, zindua. 3 ~ sb (up)

wake

chochea, changamsha. 4 sumbua kwa makelele. waking adj, -wa macho. waken vt,vi amsha; amka. ~ful adj -a kukesha; a kukosa usingizi.

wake2 n mkondo (wa chombo). in the ~ of baada ya follow in sb's ~ fuata nyayo za mtu.

wale n see weal, welt.

walk1 n 1 matembezi; kutembea kwa mguu. 2 namna ya kutembea. 3 njia. 4 ~ of life weledi, wito, kazi (katika maisha) vi,vt 1 (of persons) tembea, enda kwa miguu; (of animals) -enda. ~-about n (Australian sl of Aborigines in the desert) safari; (colloq) kuzunguka kwa mgeni rasmi na kusalimu watu njiani. ~ away from shinda kwa urahisi/ bila taabu. ~ away n ushindi wa bure/rahisi. ~ away with sth shinda kwa urahisi.~ off with sth (colloq) chukua. ~ into (sl) kula kwa raha/buraha; shutumu, tukana; jipeleka. ~ on (drama) tokea jukwaani. ~-out (colloq) goma. ~ out n mgomo. ~ out on sb (sl) acha, telekeza. ~ out with sb (dated colloq) chumbia; posa. ~ over sb shinda mtu kirahisi. ~ over n ushindi rahisi. ~ up pitia; panda juu; (inviting people to ) karibisha ~ up (to sb/sth) karibia, endea, jia. 2 tembeza, fanya kutembea. ~ sb off his feet/legs chosha mtu kwa kumtembeza. 3 tembea/pita kwa miguu. 4 (with various n) ~ the wards -wa mganga mwanagenzi ~ the streets wa malaya. ~er n mtembeaji. ~ing n (in compounds) ~ing shoes n viatu vya matembezi. ~ing-stick n bakora, fimbo ya matembezi. walkie-talkie n (colloq) redio (ya mkononi) ya kupokea na kupeleka habari.

wall n ukuta, kiambaza. with one's

back to the ~ kwa kubanwa sana; kwa kuzingirwa. be/go up the ~ (sl) hamaki, chukia; udhika sana. bang/run one's head against a (brick) ~ jaribu kufanya jambo ambalo wazi haliwezekani; piga ngumi ukutani. see through a brick ~ ona mambo yajayo, ona mbali.

wander

2 (fig) kizuizi, (kitu kinachofanana na) ukuta. 3 upenuni, kando (chiefly fig) go to the ~ tupwa nje (katika mashindano), shindwa kabisa. push/drive sb to the ~ shinda.4 (compounds) ~ flower n aina ya maua ya bustani; mtu aliyekosa mwenzi katika dansi. ~ painting n picha ya ukutani. ~ paper n karatasi za rangi za kupamba ukutani vt 1 (usu pp) zungushia ukuta. 2 ~ sth up/ off ziba (kwa matofali n.k.).

wallaby n kangaruu mdogo.

wallah n (sl in India) mtumishi (aliyeajiriwa kwa kazi maalumu).

wallet n (US pocket book) pochi, mkoba wa kuwekea karatasi/noti za benki.

wall-eyed adj -enye makengeza; -a kama makengeza.

wallop vt (sl or hum) piga sana, twanga, kung'uta; shinda sana/vibaya n konde zito; ushinde. ~ing adj -kubwa sana.

wallow vi gaagaa, vingirika matopeni/ majini; (fig) zamia, jiachia. be ~ing in money (colloq) -wa mkwasi, tajirika sana n magaagao ya wanyama: mahali ambapo wanyama huenda kugaagaa.

Wall-Street n (used for) soko la fedha la Marekani.

walrus n sili wa bahari mwenye pembe.

waltz n (music) msowero: aina ya dansi ya watu wawili wawili kuzunguka pamoja vi sowera. ~ in/out/ into/ out of ingia/ toka kwa mwendo wa furaha.

wampum n kauri; simbi (pambo au fedha).

wan adj (of person, his look etc) -liosawajika; -a /-enye huzuni, wasiwasi. 2 (of light, the sky) liofifia, -eupe, enye rangi kidogo isiyong'ara. ~ly adv. ~ness n.

wand n 1 kijifimbo cha mcheza mazingaombwe/kiongozi wa muziki, n.k. 2 fimbo rasmi ionyeshayo madaraka.

wander vi 1 zurura. 2 (stray ) potea ~ from the subject tofuata suala

wane

linalozungumzwa. 3 changanyikiwa, weweseka. ~er n 1 mhamaji, mzururaji. 2 mwenye kupotea njia. ~ings n 1 mizunguko, safari ndefu. 2 (mental) upayukaji maneno (kutokana na ugonjwa hasa wakati wa homa kali). ~lust n shauku ya kusafiri.

wane n 1 ufifiaji; kufifia. 2 vi pungua, fifia, dhoofu. on the ~ katika kufifia; (of moon) kuingia ndani.

wangle vt (sl) pata/panga kwa hila/ mbinu n hila, mbinu.

wank vi (GB vulg sl) piga punyeto n punyeto. n.k.

want1 vt,vi 1 taka, hitaji; (be without) kosa, -takiwa; -tafutwa. ~ed adj, -a kutakiwa n (colloq) tangazo (gazetini) la kazi. 2 (desire) tamani, -wa na hamu, taka. 3 hitaji, paswa, dai. 4 (progressive tense only) be ~ing kosekana, wa pungufu. be ~ing (in sth) kosa/kosekana; pungua/ pungukiwa na. be found ~ing (with human subject) totosheleza, toridhisha. 5 (impers) pungua, baki it ~s one hour to the class imebaki saa moja kabla ya darasa. 6 wa katika dhiki. ~ for nothing jitosheleza kwa kila kitu. ~ ing (prep) bila; ikikosekana.

want2 n 1 (lack) upungufu, ukosefu, uhaba. 2 (felt need) hitaji, haja; dhiki. 3 matamanio, uchu, matakwa.

wanton adj 1 (lit) -tundu, tukutu, -a kuchezacheza. 2 siozuilika; tele, -a kuzaa sana, -enye kustawi sana; korofi. 3 sio sababu; harabu. 4 (arch) asherati, kware, -a kikware, fasiki n kiberenge, mwasherati vi (lit) chezacheza. ~ly adv. ~ness n.

war n 1 vita, kondo, kitali. at ~ katika hali ya vita. carry the ~ into the enemy camp shambulia (baada ya kuridhika na kujihami/kujilinda). declare ~ (on) tangaza vita. go to ~ against anza vita (dhidi ya). have been in the ~s (colloq or hum) umia (k.m. kutokana na ajali).

warden

make/wage~ on pigana na. 2 ~ baby n mwanaharamu (wa vita) (ambaye baba yake ni askari). ~ bride n mke wa askari (aliye vitani). ~ cloud(s) n dalili za vita. ~-cry n ukelele wa kutiana shime (vitani). ~ dance n ngoma ya vita. ~ god n mungu wa vita. ~-correspondent n mwandishi wa habari za vita. ~-head n kichwa cha kombora; bomu halisi (lenye baruti). ~ horse n farasi wa vita. ~ lord n (rhet) Jemadari wa vita. ~ monger n mchochezi wa vita. W~ office n Idara ya vita. ~ paint n rangi inayopakwa mwili mzima (kabla ya kwenda vitani); (fig) mavazi rasmi ya askari; (sl) vipodozi. ~ path n (only in) on the ~ path tayari kupigana. ~ ship n manowari, meli ya vita. ~ torn adj ilioharibika na vita; -lioangamizwa na vita. ~ widow n mjane wa mwanajeshi aliyefia vitani. 3 sayansi au sanaa ya vita/mapigano/ matumizi ya silaha. 4 (fig) mapambano ~ against bribery mapambano dhidi ya hongo ~ of words mizozo. ~fare n vita, mapigano; mambo ya vita. ~ like adj tayari kwa vita; nayoashiria vita; -enye kupenda vita. ~ time n wakati wa vita. ~rior n (lit or rhet) mpiganaji; askari wa vita.

warble vi,vt (esp of birds) imba (hasa kwa madende/ madoido) n wimbo/ kuimba (kwa sauti nyororo kama ya ndege). ~r n (aina ya) ndege mwimbaji.

ward n 1 keep watch and ~ linda. 2 (guardian) ulinzi, ulezi; mtu (hasa mtoto) aliye chini ya mamlaka ya mahakama. 3 (of a government area) kata. 4 (of hospital) wadi isolation ~ wadi iliyotengwa. 5 (of lock, key) mtoto, jino vt ~ sth off kinga, epuka, kwepa kitu.

warden n 1 msimamizi, mwangalizi. traffic ~ n msimamizi wa maegesho ya magari the ~ of the

warder

hall of residence mwangalizi wa bweni game-~ bwana nyama. 2 (old use except in a few cases) mkuu (wa chuo n.k.). 3 (US) askari jela.

warder n (GB) (US warden) askari magereza/jela. wardress n askari magereza wa kike.

wardrobe n 1 kabati la nguo. 2 nguo, mavazi. 3 maleba: mavazi ya kundi la sanaa za maonyesho.

ward-room n vyumba vya maofisa wa manowari (isipokuwa nahodha).

ware1 vt (imper) angalia! jihadhari! habedari!

ware2 n 1 (in compounds) bidhaa; chombo silver ~ bidhaa za fedha 2 (pl) bidhaa, vitu vya biashara. ~house n ghala, bohari vt weka/ hifadhi ghalani.

warm adj 1 -a vuguvugu, -fufutende. ~ work n kazi ya kusisimua mwili; kazi ya sulubu/hatari. make things ~ for sb letea matata, adhibu mtu. ~ blood n damu ya mamalia na ndege. ~ blooded adj -a damu moto; motomoto; -enye mihemko ya haraka. 2 (hearty) -a shauku. 3 (angry) -a hasira. 4 (cordial) kunjufu, -ema. ~-hearted adj -ema, -kunjufu, -a huruma, -a upendo. ~-heartedness n. 5 (of scent) bichi; (of children games) -a kukimbia. ~ly adv -kwa ukunjufu/upendo; kwa kuzuia baridi. ~th n 1 hasira. 2 uvuguvugu; ukunjufu; wema mwingi vt,vi ~ (sth) (up) pasha/pata moto. ~ to one's work/task/sb changamkia kazi./ mtu. ~ing- pan n (hist) kipashi joto (cha kitanda). ~er n kipashia joto.

warn vt onya; asa; hadharisha. ~ sb off kataza mtu (asiingie/asikaribie). ~ing n onyo, ilani without a moment's ~ing kwa ghafula give a month's ~ing toa notisi ya mwezi mmoja adj -a onyo, -a ilani.

warp1 vt,vi 1 (bend) pinda, pindika. 2 potoka; potosha n kupinda.

warp2 n the ~ mtande.

warrant n 1 haki, sababu. 2 hati (ya

wash

idhini ya kufanya kitu); kibali, waranti search ~ hati ya upekuzi. 3

(marine) hati ya kuteua askari asiye afisa vt 1 tetea; halalisha; wa na sababu. 2 thibitisha; (colloq) thibitishia, hakikishia. ~ee n mtu anayepewa hati (ya kutengeneza/ kubadilisha bidhaa); mdhaminiwa. ~or; ~er n mdhamini. ~- officer n askari asiye afisa. ~y n 1 hati (ya kutengeneza/kubadilisha bidhaa). 2 mamlaka.

warren n eneo lenye mashimo na sungura wengi; (fig) maskani yenye watu/mitaa mingi.

wart n chunjua, sugu, dutu. ~-hog n ngiri. ~y adj.

wary adj -a hadhari, -angalifu, -enye kuwa macho. warily adv kwa hadhari, kwa uangalifu. wariness n.

was vi see be.

wash vt,vi 1 osha; (bathe) oga,ogesha; (hands) nawa. ~ one's hands of sth/sb jitoa kabisa katika jambo, nawa mikono. ~clothes fua nguo. ~ sth down safisha (hasa kwa mtiririko wa maji. ~ sth away/off/out ondoa kwa kuosha, safisha kwa maji. be/look/feel ~ed out (fig colloq) jisikia hoi, choka sana. ~ up (GB) osha vyombo (baada ya mlo); (US) nawa uso na mikono. ~ing up n uoshaji vyombo. (all) ~ed up adj (colloq) -liokwisha. 2 (of material) fulika; (fig) kubalika. 3 (of sea, river) la; pita. 4 (of moving liquid) beba, tupa, chukua. ~ sth down with telemshia. ~ ed out adj (of games) -lioahirishwa, lioshindikana (kwa sababu ya mvua au mafuriko); (of roads etc) -siopitika. 5 chimba (mchanga) kwa maji. 6 (ceremonially) toharisha, eua ~ sb of his sins toharisha/takasa mtu dhambi zake. 7 mwagika. 8 (in compounds often used as a substitute for ~ ing) ~ basin/ bowl/hand-basin n beseni/bakuli la kunawia;

wasp

karai. ~ board n ubao wa kufulia. ~ cloth n kitambaa cha kunawia uso. ~ -day n siku ya kufua. ~ drawing n picha ya rangi za maji. ~ house n chumba/banda la kufulia nguo. ~-leather n ngozi laini ya kusafishia. ~ out n sehemu iliyobomolewa na mafuriko; (fig) mtu wa bure; kushindwa kabisa. ~ room n (US) msala. ~- hand stand n meza ya kunawia. ~ tub n pipa la kufulia nguo. ~ able adj a kufulika n 1 kuosha; josho have a ~ and brush up koga na kujinadhifisha, jitakasa. 2 (sing only) nguo, za kufua; mahali pa kufulia/kufanyia udobi. 3 the ~ (ed) mkondo; sauti inayotokana na mtiririko wa maji; kitu cha maji (kilichotayarishwa kwa shughuli maalum. white ~ n chokaa, wangwa; (sediment) kitope. 4 majimaji. 5 mashata. ~er n 1 washeli: pete bapa ya chuma/ plastiki/mpira au ngozi iliyotobolewa. 2 mashine ya kufulia/kuoshea vyombo. 3 ~erman/woman n dobi. ~ing n 1 kuosha/kuoshwa. 2 kufua; nguo zinazofuliwa au za kufua ~ing day see ~ day ~ing machine mashine ya kufulia. ~ing soda n magadi. ~y adj (of liquids) -a majimaji; (of feeling style) dhaifu; (of colours) hafifu.

wasp n nyigu. ~ waisted adj -enye kiuno chembamba. ~ish adj -a chukichuki; kali.

wassail n 1 (arch) tafrija/ sherehe ya vileo. 2 kileo kinachonywewa katika sherehe hiyo.

waste adj 1 -ovyo, -siofaa, -a takataka, -a bure. 2 (of land) -sio tumika; sio na rutuba. ~ land n kame, ardhi isiyotumika, mbaya; ardhi iliyoharibiwa na vita n.k. (fig) maisha/jamii iliyoharibika. lay ~ angamiza, haribu vt,vi 1 ~ sth (on sth) tumia vibaya, poteza, fuja, tapanya. ~ one's breath poteza nguvu bure. ~ not, want not (prov)

watch

atumiaye vyema hakosi kitu. 2 angamiza/haribu (ardhi). 3 dhoofika, lika, chakaa. 4 potea bure n 1 upotevu, uharibifu, ufujaji go/run to ~ potea bure it is a ~ of time ni kupoteza wakati. 2 (of land) jangwa; mbuga. 3 takataka. ~-basket /bin n. ~ paper basket n jaa/kapu/pipa la taka. ~ pipe n bomba la kuondolea maji machafu. ~r n mharibifu, mfujaji. ~ ful adj haribifu, fujaji, potevu. ~fully adv. wastage n 1 hasara; uharibifu. 2 takataka. wastrel n mfujaji; mzembe; mhuni.

watch1 n 1 (timepiece) saa (ya mfukoni au mkononi). ~ glass n kioo cha saa. ~ guard/chain n mnyororo wa kufungia saa nguoni. ~ key n ufunguo wa saa. ~ maker n fundi saa.

watch2 n 1 ulinzi, lindo. be on the ~ (for) tazamia, weka hadhari, vizia. keep ~ (on/ over) linda, chunga, tunza. ~ dog n mbwa wa kulinda nyumba; (fig) mtu/kitu kinacholinda. ~ tower n mnara wa doria kuchunga moto n.k. 2 the ~ (hist) n walinzi (hasa wa usiku). 3 (in ships) zamu (kipindi cha saa 2 au 4. the first ~ n zamu ya saa 2 usiku hadi saa 6 usiku. the middle ~ n zamu ya saa 6 usiku hadi saa 10 usiku. the dog ~es n nusu ya zamu. keep ~ wa zamu. 4 (old

use) mkesha. ~ night service n ibada ya usiku/mkesha (wa kidini). ~er n 1 mlinzi, mwangalizi. ~ man n mlinzi wa usiku. ~ful adj -a hadhari, -angalifu, -chunguzi. ~fully adv. ~fulness n. ~word n neno la siri la kulindia; wito/neno la shime/kutia hamasa vt,vi 1 tazama, angalia, chunga. ~ one's step -wa mwangalifu; fanya jambo kwa makini na tahadhari; -wa na hadhari. ~ one's time vuta subira, subiri wakati unaofaa. ~ the time jali wakati, angalia saa ili (usichelewe).

water

~ (out) (for sth) -wa macho, angalia. ~ out jihadhari. ~ (over) sth linda, hami; (old use) kaa macho, kesha.

water n 1 maji salt ~ maji chumvi cold ~ maji baridi by ~ kwa dau/meli/boti n.k. in deep ~(s) matatani. in smooth ~ -enye kuendelea vizuri. on the ~ katika dau, meli n.k. under ~ -lio jaa maji, -liofurika. be in/get into hot ~ pata matatizo (kutokana na mwenendo mbaya). cast/throw one's bread upon the ~(s) tenda wema nenda zako (ingawa unaweza kulipiziwa baadaye). drink the ~s -nywa maji ya chemchemi kama dawa. go through fire and ~ (for sb/sth) pitia matatizo na majaribu makubwa (kwa ajili ya mtu/kitu). hold ~ (of theory etc) thibitika inapojaribiwa. keep one's head above ~ epuka matatizo ya kifedha. make ~ kojoa; (of a ship) vuja. spend money etc like ~ fuja mali, tumia, fedha kwa wingi. throw cold ~ on (a plan etc) tilia mashaka, pinga. like a fish out of ~ -enye kujisikia/vibaya kutokana na mazingira asiyozoea; -enye kujihisi ugenini/upweke. still ~s run deep (prov) kimya kingi kina mshindo mkuu; simba mwenda kimya ndiye mla nyama. written in ~ (of a name, reputation, etc) -epesi kusahaulika. the ~s of forgetfulness usahaulifu. table/mineral ~s n maji ya kunywa (yenye madini). 2 hali ya maji kupwa/kujaa. in low ~s (fig) -pungufu ya fedha, -enye fedha kidogo. 3 (pl) bahari. Tanzania. ~s n bahari karibu ya Tanzania. 4 (usu pl) ziwa, mto ~s of the Nile ziwa ambalo ndio chanzo cha mto Nile. 5 kimiminiko, maji. rose ~ n maji ya waridi. 6 of the first ~ bora sana a diamond of the first ~ almasi bora sana. 7 (in compounds). ~-bed n godoro la mpira lililojazwa maji. ~-borne adj 1 (of goods) -a

water

kuchukuliwa kwa meli, dau n.k.; (of diseases) -a kuenezwa na maji machafu. ~-bottle n kiriba, chupa ya maji. ~ buffalo n nyati wa kufugwa. ~cannon n bomba la maji (lenye kanieneo kubwa). ~-cart n gari lenye tangi la maji ya (kunyunyizia barabarani au kuuza). ~-chute n poromoko la maji; mfereji wa maji unaotelemka. ~-closet n (common abbr w.c.) choo cha kuvuta, choo cha maji. ~-colour n rangi za maji; picha ya rangi za maji; uchoraji wa rangi za maji. ~-colourist n. ~-cooled adj -enye kupozwa kwa maji. ~-cooler n gudulia la maji baridi. ~-course n kijito, mfereji wa maji, korongo. ~fall n maporomoko ya maji. ~fowl n ndege wa majini. ~ front n mwambao. ~ glass n ute mzito wa kukandia yai ili lisiharibike. ~-hole n dimbwi, shimo la maji. ~-ice n peremende barafu. ~jacket n fuko la maji la kupozea. ~ jump n kikwazo chenye mfereji wa maji (katika mashindano ya farasi). ~less adj -kavu kame, pasipo maji. ~-level n kina cha maji. ~-lily n yungiyungi. ~-line n msitari maji: mstari ubavuni mwa meli panapofikiwa na maji. ~ -logged adj (of boat, ship, wood, etc) -liojaa maji. ~-main n bomba kubwa la kuleta maji. ~man n mwanamaji; mvushaji. ~-mark n 1 kipimo cha kina. 2 (on paper) alama maalum ionekanayo kwa kuelekeza karatasi kwenye mwanga). ~ melon n tikiti maji. ~-meter n kipimamaji. ~-mill n kinu cha gurudumu maji; kinu kiendeshwacho kwa gurudumu linalozungushwa na maji. ~-pipe n bomba la kupitishia maji. ~ polo n mchezo wa mpira wa mikono majini. ~-power n nishati ya maji (ya kuendeshea mashine). ~-proof 1 adj -siopenya maji ~proof coat n koti (isiyopenya maji) vt fanya maji

Waterloo

yasipenye. ~-rate n (GB) malipo ya kutumia maji. ~ -shed n eneo la mwinuko linalogawa mito; (fig) eneo la mwachano wa mambo, matukio; njia panda. ~side n ukingo. ~-skin n kiriba cha maji. ~-softener n dawa ya kulainisha maji. ~-spout n 1 chamchela ya maji (hasa ya baharini); (of a roof) mlizamu. ~-supply n ugavi wa maji. ~-table n tabaka maji (chini ya ardhi). ~-tank n tangi la maji. ~-tap n bomba la maji. ~ tight adj -siovuja maji; siopitisha maji; (of an agreement) thabiti, -sio pindika. ~-tower n mnara wa maji. ~-wagon n gari la kubebea maji. ~way n njia ya majini. ~-wheel n gurudumumaji; gurudumu lizungushwalo na maji. ~-wings n (pl) vyelezo vilivyojazwa hewa na kufungwa mabegani (ili kumsaidia ajifunzaye kuogelea). ~- works n (pl) mfumo wa ugavi wa maji; chemchem za maji zilizopambwa; (colloq) (kazi za) kibofu; (colloq) machozi. ~y adj -a majimaji; chepechepe vt,vi 1 mwagia /nyeshea/nyunyizia maji. ~ing can n ndoo ya kunyweshea. ~ing cart n gari la kumwagia maji barabarani (agh kuondoa vumbi). 2 patia maji. 3 (of the eyes) jaa machozi; (of the mouth)jaa mate/maji. mouth ~ing adj -a kutia hamu sana. 4 ~ sth down tia/ongeza maji; (fig) fanya hafifu. 5 (fin) ongeza deni au mtaji wa kampuni kwa kutoa hisa mpya bila kuongeza mali. 6 ~ed adj (pp as adj) -liopatiwa maji, -lio na maji. ~ed silk n hariri iliyotengenezwa na kuwa na mawimbi. 7 ~ing place n dimbwi wanaponywea wanyama; see spa; mahali pa kupumzikia pwani.

Waterloo n meet one's ~ komeshwa, koma (baada ya mafanikio mengi).

watt n wati: kipimo cha umeme. ~age n kipimo cha umeme kwa wati.

wattle1 n 1 ufito. ~ and daub hut n nyumba ya mbavu za mbwa;

way

kibanda cha fito kilichokandikwa. 2 miwati. ~-bark n magome ya miwati.

wattle2 n (of a bird etc) upanga/ndevu.

wave vt,vi ~ (at/to/in) peperusha, peperuka; punga; tikisika. ~ sth aside (fig) tupilia mbali. 2 (of a line or surface, of hair) fanya mawimbi, mapindi n 1 wimbi. the ~s n (poet) bahari. in ~s kwa mawimbi. 2 mpepeo, mpungo, mtikisiko. 3 (of hair) msuko. 4 ongezeko a crime ~ ongezeko la uhalifu. 5 wimbi la joto, sauti, mwanga, sumaku. long/ medium/ short ~ (radio) n mawimbi ya sauti ya masafa marefu/ kati/mafupi. ~ length n masafa; urefu wa wimbi. wavy adj -enye mawimbi, -a kuinuka na kushuka, -enye mapindi a wavy line mstari mawimbi. ~er vi 1 yumbayumba, pepesuka, tetereka. 2 -wa na shaka, sitasita. ~rer n.

wax1 n nta. ~-chandler n mtengenezaji mishumaa; mchuuzi wa mishumaa. ~-paper n karatasi nta: karatasi isiyosharabu maji kwa sababu ya tabaka la nta. ~ work n sanamu ya nta. 3 (pl) ~ works n maonyesho ya sanamu za nta vt tia nta. ~. ~en adj -a nta; -a kama -a nta. ~y adj -a kama nta; ororo na eupe.

wax2 vi (esp of moon) pevuka. ~ and wane pevuka na kupungua. 2 kua. ~merry furahi, -wa na furaha.

wax3 n (sl) hasira. ~y adj -enye hasira.

way n 1 njia, barabara. pave the ~ for andalia, andaa. The W~ of the Cross Njia ya Msalaba. 2 mapito; njia (yakupitia/kutumia). go one's ~(s) ondoka. go out of one's ~ to do sth fanya bidii kubwa, fanya jitihada maalum. lead the ~ ongoza njia, toa mfano. make one's ~ in life fanikiwa. make the best of one's ~ fanya hima, enda haraka iwezekanavyo. make one's ~ (to/

way

fowards) enda, jiendea. pay one's ~ epuka madeni; jilipia gharama. the parting of the ~s (fig) njia panda. by ~ of kupitia. out of the ~ geni, tunu, sio -a kawaida, -a ajabu, miujiza. out-of-the- ~ adj (attrib) -a mbali, siofikika kwa urahisi. 3 by the ~ njiani; safarini; (fig) pamoja na hayo. on the/one's ~ njiani. on the ~ out (colloq) -nayo karibia kupitwa na wakati, nayoelekea kupoteza umaarufu. 4 njia; mkakati, mbinu. where there's a will there's a ~ (prov) penye nia pana njia. ~s and means n mbinu, njia. have/ get one's own ~ pata/tenda/ fanya mtu atakavyo; fuata njia yako. go/take one's own ~ fuata matakwa yake mtu, fanya mtu aonavyo. 5 (sing only) masafa, hatua, umbali. 6 upande; welekeo look this ~ tazama upande huu. put sb in the ~ of (doing) sth saidia mtu kuanza jambo. 7 (colloq) karibu na, upande wa. 8 maendeleo, kufuata uelekeo fulani. be under~; have ~ on (of ship) kata maji, enda. gather/lose ~ kaza/legeza mwendo; ongeza/poteza kasi. get under ~ anza kwenda, wa mbioni. make ~ (lit or fig) piga hatua. 9 nafasi/mwanya wa

kusonga mbele, uhuru wa kuendelea. be/put sth out of harm's ~ wa/weka katika hali ya usalama, salimisha. get sth out of the ~ ondosha. make ~ (for) pisha. put sb out of the ~ ondoa (kwa kufunga/kuua kisirisiri); fanya atoweke. put sb in the ~ of (doing) sth saidia kuanza/kupata. see one's ~ (clear) to doing sth ona jinsi/namna ya kufanya mambo; -wa na hakika ya kufanya jambo. 10 mwenendo, desturi good old ~s desturi njema za zamani. to my ~ of thinking kwa maoni yangu. the ~ (colloq adv) kama, jinsi. mend one's ~s jirekebisha, jirudi. 11 namna. no ~ (sl) katu, hasha they are in no ~s

weak

similar hawafanani hata kidogo kwa namna yoyote ile. 12 hali in a bad ~ katika hali mbaya. any ~ vyovyote vile iwavyo. each ~/ both ~s kote kote, kila upande. have it both ~ s taka kote kote. be in the family ~ -wa mjamzito. in a big/small ~ kikubwa/ kidogodogo. 13 mwendo, utaratibu the law had its ~ sheria ilifuatwa. 14 by ~ of kwa kusudi ya; kwa namna ya. 15 (pl) ~s n see sleepway. 16 (compounds) ~bill n orodha ya mali ya abiria (shehena). ~farer n msafiri (agh. kwa miguu). ~faring adj -a kusafiri; -a kupenda kusafiri n safari. ~leave n haki ya kupita njia. ~side n kando ya njia adj kando ya njia adv mbali. ~ behind adv nyuma; kwa mbali sana ~ back in my boyhood zamani katika siku zangu za utotoni. ~ out adj (colloq) -a ajabu. ~lay vt vizia we were ~laid tuliviziwa. ~ward adj kaidi; tundu; tukutu. ~wardness n ukaidi; utukutu.

we pron 1 sisi. 2 (by king, Pope etc) mimi; ni-.

weak adj 1 dhaifu, hafifu ~ in will -enye moyo dhaifu. ~-kneed adj (fig) 1 -nyonge, sio na dhamira, -enye moyo dhaifu. 2 (of senses etc) -pungufu; chini ya kiwango cha kawaida. ~-headed adj -enye akili pungufu. ~ minded adj -enye akili chache, -enye akili afkani. 3 (of solutions, liquids) majimaji; si -kali ~ wine divai isiyo kali. 4 baya, bovu ~ in history ni dhaifu katika historia. 5 (gram) hafifu. ~ verb n kitenzi hafifu. ~ form n maumbo yasiyotiwa mkazo. ~ling n mnyonge/mdhaifu. ~ly adv kwa udhaifu, kwa uhafifu, bila nguvu. ~ness n 1 udhaifu. 2 ubovu. 3 kutojiweza. have a ~ness for penda mno (hadi kuonekana mjinga) vi,vt dhoofu, dhoofika, legea; dhoofisha, punguza nguvu.

weal

weal1 n kovu: alama ya pigo katika

ngozi.

weal2 n usitawi, neema for the public general ~ kwa ajili ya neema ya watu wote. in ~ or woe katika dhiki au faraja.

weald n (GB) mbuga.

wealth n 1 utajiri, ukwasi; mali nyingi a man of ~ tajiri, mwenye mali. 2 wingi wa mali, wingi wa neema. ~ of a/the -ingi sana. ~y adj -tajiri, -kwasi, -enye wingi wa neema. ~ily adv kwa ukwasi.

wean vt 1 likiza: achisha mtoto ziwa. 2 ~ sb from sth fanya kuacha (tabia, marafiki wabaya n.k.) ~ sb of a habit tengua tabia ya mtu ~ sb from bad company ondoa mtu kutoka kwenye kundi baya/marafiki wabaya.

weapon n silaha. ~less adj bila silaha. wear1 vt,vi 1 vaa; valia; paka ~ a hat vaa kofia ~ red lipstick paka rangi nyekundu. ~ the crown tawazwa ufalme, -wa mfalme; wa shahidi. 2 chakaa; chakaza; -la; lika. ~ away chakaa, potea. ~ sth away chakaza. ~ down konga, dhoofu, lika. ~ sth down chakaza. ~ sth/sb down dhoofisha kitu kwa kushambulia/ kusuta mara kwa mara. ~ off pita, pungua, isha. ~ sth off maliza (kidogo kidogo). ~ sth/sb out chosha. ~ (sth) out chakaza, chakaa. worn out chakavu. 3 toboa, tia alama, tengeneza. 4 stahimili, dumu. 5 ~ on/away (of time) potea, pita pole pole. ~er n mvaaji. ~able adj -a kuvalika, -a kufaa kuvaliwa. ~ing adj (exhausting) -a kuchosha.

wear2 n 1 vazi, kuvaa. 2 uchakavu. ~ and tear uchakavu (kwa matumizi). 3 ustahamilivu. 4 (as in compounds) under ~ n chupi. foot~ n viatu. ~ily adv kwa taabu, kwa hali ya kuchoka. ~iness n kuchoka, kuchosha. ~isome adj -a kuchosha, -a taabu, -sumbufu. ~y adj 1 chofu. 2 choshi. 3 -a dalili ya kuchoka/uchovu vt,vi ~y sb (with

wed

sth); ~y of sth chosha/choka.

weasel n mnyama mdogo kama cheche. ~- faced adj -enye sura ya panya.

weather1 n 1 hali ya hewa. be/feel under the ~ (colloq) umwa, jisikia vibaya. keep a/ one's ~ eye open -wa na hadhari, wa macho, kaa chonjo, jiandaa. make good/bad ~ pambana na hali ya hewa nzuri/ mbaya. make heavy ~ of sth sumbuliwa, taabishwa. under stress of ~ kwa sababu ya dhoruba n.k. 2. (compounds) ~ beaten adj iloathiriwa na hali ya hewa. ~ boarding/boards n mbao za kukinga mvua. ~ bound adj liozuiwa safari kutokana na hali ya hewa mbaya. ~ bureau n ofisi ya hali ya hewa. ~ cock n kieleleza upepo (kifananacho na jogoo). ~ man n mtabiri wa hali ya hewa. ~-glass n barometa. ~proof adj -sioathiriwa na upepo/ mvua/baridi. ~-ship n meli ya hali ya hewa. ~-report n ripoti ya hali ya hewa. ~-side n upande wa joshi.

weather2 vt,vi 1 pona, pita, epuka. 2

enda joshi. 3 acha nje. 4 kwajuka, nyauka.

weave vt, vi 1 ~ sth (up) into sth. ~

sth (from sth) fuma kitu. 2 (fig) tunga, sanifu, buni. get weaving (on sth) tia/fanya shime, anza kwa nguvu. 3 nyonganyonga, pindapinda n mtindo wa ususi/ufumaji plain ~ mfumo wa kawaida. ~r n mfumaji. ~r bird n mnana.

web n 1 kilichofumwa; mfumo. 2 (of spider) utando; tandabui, kimia; (of waterbird's feet) utando wa ngozi kati ya vidole. ~bed adj -enye utando (wa hila, njama, uongo n.k.). ~-footed/toed adj -enye ngozi kati ya vidole vya miguu.

we'd we had, we would, we should.

wed vt,vi 1 oa; olewa, funga ndoa; (lit) ungana. ~ded to adj -enye kushika sana; -enye kung'angania. ~ding n arusi, ndoa. golden ~ding sikukuu ya 50 ya ukumbusho wa ndoa adj -a

wedge

arusi. ~ding-breakfast n chakula cha maarusi, ndugu na jamaa baada ya harusi. ~ding garment n nguo za harusi. ~ dingcake n keki ya ndoa. ~ding-card n kadi ya taarifa;

tangazo la ndoa (kwa marafiki); kadi (ya mwaliko) ya arusi. ~ding-ring n pete ya ndoa. ~lock n (legal) ndoa in ~lock katika ndoa, -a ndoa.

wedge n 1 chembeo, kabari. the thin end of the ~ (fig) jambo dogo au badiliko dogo linaloelekea kuzaa jambo kubwa au badiliko kubwa. 2 kitu chenye umbo kama kabari vt tia chembeo, zuia kwa chembeo; bania. ~-shaped adj -enye umbo la kabari, kama kabari.

Wednesday n Jumatano.

wee1 adj dogo sana. a ~ bit (adverbial) kidogo. the ~ folk pepo, mazimwi n.k. the ~ hours (US) usiku wa manane, baada ya saa sita za usiku. bide a ~ kaa kidogo.

wee2wee-wee n (used by and to children) mkojo vi kojoa.

weed n 1 gugu; majani. ~ killer n kiua magugu. 2 mtu mwembamba dhaifu mtu hafifu. 3 (dated sl) sigara; biri; tumbaku; (modern sl) bangi vt palia magugu. ~ sth/sb out ondoa vitu hafifu (visivyofaa kitu), pembua, chagua. adj 1 -enye magugu. 2 (sl) -refu-embamba na dhaifu.

weeds n (pl) widow's ~ nguo (za nyasi) za mjane.

week n 1 juma, wiki. ~ in ~ out endelea bila kukoma. ~-end n wikiendi, Jumamosi na Jumapili ~-end ticket ruhusa ya Jumapili vi enda wikiendi. long ~-end n wikiendi ndefu. 2 siku za juma za kazi. ~-day n siku yo yote ya juma (isipokuwa Jumapili). ly adv kwa juma three times a~ mara tatu kwa juma n gazeti litolewalo kila juma.

weeny adj (colloq) (often teeny ~)

-dogo sana.

weep vt,vi (liter) 1 lia, toa machozi ~ for joy tokwa na machozi kwa furaha.

welcome

2 (drip) tona. 3 omboleza. ~ing adj 1 -nayolialia. 2 (arch) -a mvua, majimaji; (of trees) -enye matawi membamba ya kuinama. ~y adj epesi kutoa machozi.

weevil n mdudu alaye nafaka.

weigh vt,vi 1 pima uzito. ~ sth out

pima. ~ (oneself) (in) for a boxer etc) pimwa uzito kabla ya mchezo. ~ in (with) (of arguments, facts etc) toa hoja zenye nguvu/za maana. ~ bridge n mizani ya kupimia uzito wa magari. ~ing machine n mizani. 2 wa na uzani wa. 3 (of a machine) wa na uwezo wa kupima. 4 ~ sth (with/ against sth) pima (ubora, umuhimu wa kitu) dhidi ya kingine. ~ sth (up) fikiria kwa makini; hakiki. 5 ~ sth down lemea, inamisha. ~ sb down lemeza, chosha, sumbua. ~ on sb/sth sumbua, shughulisha. ~ with sb shawishi; athiri. 6 ~ anchor ng'oa nanga.

weight n uzito, uzani. under/over ~ -enye uzito mdogo/mkubwa. put on ~ nenepa: ongezeka uzito. throw one's ~ about (colloq) tamba, onyesha ukubwa/ubwana, onea. 2 a/ the ~ (of) uzito (wa kubebwa), mzigo. 3 umaarufu, maana. carry ~ -wa na maana; -wa muhimu. 4 jiwe la mizani. ~ lifting n mchezo wa kuinua vitu vizito. 5 mfumo wa vipimo vt 1 tia, ongeza uzito; -pa nguvu, lemeza. 2 ~ sb down lemeza. 3 tumia madawa kufanya kitambaa kuwa kigumu. ~less adj -sio na uzito. ~y adj zito, -a maana. ~ily adv. ~iness n 1 uzito. 2 umuhimu, maana. ~lessness n.

weir n 1 boma la kuzuia maji, kikinga mto. 2 mtego wa samaki.

weird adj 1 -a miujiza, sio -a

kawaida; -a kuogofya. 2 (colloq) -a ajabu. ~ly adv. ~ness n. ~ie n (sl) mtu mwenye tabia ya pekee.

welcome adj 1 -a kupokewa/ kukaribisha kwa furaha; -a

weld

kufurahia; -a furaha; -a kufurahisha. 2 -enye kuruhusiwa/ kuachiwa. ~ to do sth; ~ to sth pewa ruhusa ya kutumia bure; pewa bure. you are ~ karibu; usijali. 3 (as an interj) karibu n mapokezi, makaribisho vt karibisha vizuri; pokea kwa furaha go out to ~ laki.

weld vt unga, tia weko, unganisha (chuma, madini) kwa kufua n kiungo kilichofanywa kwa weko. ~er n mtia weko.

welfare n 1 ustawi, hali njema, neema, afya child ~ ustawi wa watoto. the W ~ State nchi yenye (mpango wa) kutoa huduma za jamii bure; (US) Ustawi wa Jamii. ~ worker n afisa ustawi.

welkin n (poet) mbingu; anga.

we'll we will, we shall.

well1 n 1 kisima. ~ water n maji ya kisima. oil ~ n kisima cha mafuta. 2 chemchemi; (fig) chanzo, chimbuko. ~ head n chanzo cha mto /chemchemi. 3 chumba cha lifti au ngazi katika jengo. 4 (GB) ulingo wa mawakili katika mahakama. 5 ~ deck n nafasi katika staha kuu ya meli iliofungiwa. ~ out (from/of) bubujika. ~ over furika. ~ up (in) foka, chemka.

well2 adv 1 -zima; vema, vizuri,barabara. do ~ fanya, endelea vizuri, sitawi. be doing ~ (progressive tense only) pata nafuu/ahueni. do oneself ~ jipatia mambo ya starehe au anasa. do ~ by sb fanyia mtu ukarimu. wish sb ~ takia mtu heri. 2 (with praise or approval) vizuri, sifia au unga mkono. stand ~ with sb pendwa na. 3 kwa bahati njema. be ~ out of sth jitoa katika jambo bila matatizo/ hasara. ~ off adj -enye mali, -enye neema, tajiri; -enye bahati. ~ off for hajambo kwa; liojawa na ~off for food hajambo kwa chakula; ana chakula kingi. come off ~ (of a person) fanikiwa; (of an event)

well

-liokuwa nzuri, wa na matokeo ya kuridhisha. do ~ to + (inf) fanya vizuri. 4 kwa haki. you may ~ be surprised una haki ya kushangaa. 5 may (just) as ~ hivyohivyo, vilevile, pia. be just as ~ (wa) afadhali. 6 (end position) sana, kabisa shake the bottle ~ tikisa chupa sana. 7 kwa kiasi kikubwa. ~ away -enye kuendelea vema; (colloq) -enye kukaribia (kulewa); -enye kuwaka. leave/let ~ alone usiingilie. 8 as ~ (as) pamoja na; vilevile. 9 (with another adv) pretty ~ karibu. pred adj 1 -zima, -enye afya. get ~ pona, pata nafuu I am pretty ~ karibu sawa! si mbaya! sijambo. 2 sawa; -ema, -a hali njema, heri. its all very ~ (used ironically) ni sawa. 3 -a bahati it was ~ for you ilikuwa bahati yako. 4 afadhali, bora int 1 (expressing astonishment) lo! ~ then je, nini basi? 2 (expressing relief) haya! ~, here we are at last haya, mwishowe tumefika hapa. 3 (expressing resignation) ~, it cant be helped, haya, hatuna la kufanya. ~-being n ustawi; hali njema; afya, raha. ~-doing n (arch) ufadhili, kutenda mema. ~-nigh adv (arch) karibu he was ~-nigh drowned alikuwa karibu azame majini. ~-off adj -tajiri, -enye neema. ~-to-do adj tajiri, -enye neema the ~ to do n matajiri. ~ -wisher n mtakia heri. ~ doer n mfadhili, mhisani. ~ advised adj -a busara. ~ balanced adj -enye busara. ~ appointed adj -enye zana/vyombo vyote. ~ born adj -a ukoo bora. ~-bred adj -enye adabu, -enye malezi mazuri, -ungwana, -a kiungwana; (of animals) -liofugwa vizuri. ~-chosen adj -lio chaguliwa vizuri. ~-conditioned adj -enye hali njema; -a adabu, -enye malezi mazuri. ~-conducted adj lioendeshwa/ pangwa/ongozwa vizuri. ~ connected adj -enye

welsh

uhusiano na watu (wa nasaba) bora (kwa damu/ ndoa). ~ -disposed adj (towards) -fadhili, -a hisani, -ema; -a kupendelea. ~-favoured adj (old use) -zuri, -a kupendeza, -enye sura nzuri ~-fed adj -liolishwa vizuri ~-found adj -enye zana/vyombo vyote. ~-founded adj -enye ukweli. ~-groomed adj maridadi, safi. ~ -grounded n -enye ukweli; -enye mafunzo bora; -enye misingi imara. ~ heeled n (sl) kwasi, kizito. ~-informed adj -enye kujua, kutambua be ~-informed on a subject jua vema somo fulani. ~-intentioned adj -enye nia safi. ~-knit adj kakamavu; -shupavu; kakawana. ~-known adj maarufu, mashuhuri, nayo julikana sana. ~-lined adj (of a purse, colloq) -liojaa fedha. ~-mannered adj -enye tabia njema. ~-marked adj -liodhahiri, bainifu. ~-meaning adj -enye nia safi. ~-meant adj -liosemwa/fanywa kwa nia safi. ~-paid adj -enye malipo (ujira, mshahara) mazuri. ~-read adj -a maarifa (elimu) nyingi, liosoma sana. ~-rounded adj -lio kamilifu na linganifu; -enye maarifa mengi. ~-set adj shupavu, kakamavu. ~-spoken adj -enye lugha fasaha, -enye kusema kwa adabu/heshima. ~-timed adj -a wakati wa kufaa. ~-tried adj (of methods) -liojaribiwa

mara nyingi (na kuonyesha kufaa kwake), mujarabu. ~-turned adj (of a compliment, phrase, verse) fasaha, sanifu, -liotungwa vizuri. ~-worn adj -liotumika mno, -liopoteza maana/ ladha (kwa sababu ya kutumika).

welsh vt,vi 1 ~ on sth/sb kwepa kulipa; toroka bila kulipa. 2 vunja kauli/ ahadi. ~er n.

welt n 1 mshono (unaounganisha ngozi ya kiatu na unyayo wake). 2 alama ya pigo.

welter1 vt gaagaa, vingirika; jinyo-

wet

nganyonga; tota katika damu n.k. n (sing only) vurugu, ghasia, machafuko the ~ of the waves msukosuko wa mawimbi.

welter2 n ~ weight (esp in boxing) uzito wa wastani (agh kati ya kilo

61-66.6). ~ race n mbio za wapanda farasi (wenye uzito mkubwa).

wen n tezi, uvimbe wa kudumu (agh kwenye upara, n.k.); (fig) mji mkubwa uliopanuka mno.

wench n 1 (arch) msichana, mwanamwali. 2 malaya vi zini.

wend vt (old use, only in) ~ one's (home) -enda, elekea (nyumbani).

went pt of go.

wept pt of weep.

were see be.

we're we are.

werewolf n (myth) mtu bweha.

west n magharibi, machweo ya jua. The W ~ Ulaya na America; (world of politics) Ulaya Magharibi na Bara; (US) eneo la kati ya mto Mississippi na bahari ya Pasifiki; sehemu ya magharibi ya nchi yoyote. 2 (attrib) toka magharibi. ~ end adj -a magharibi. go ~ (sl) potea, dhurika. ~ of magharibi zaidi ya. ~ward(s) adv enda upande wa magharibi. ~erly adv, adj -a magharibi, -a upande wa magharibi. ~ern adj -a (toka) magharibi the W~ern Hemisphere n Amerika ya kaskazini na kusini n 1 filamu ya makauboi. 2 riwaya ya makauboi. ~erner n mwenyeji wa magharibi. ~ernize vt,vi fanya -a kimagharibi;leta utamaduni wa kimagharibi. ~ernization n. ~ernmost adj -a magharibi ya mbali.

wet adj 1 -a majimaji, chepechepe, -liolowa maji. ~ dock n gati lenye maji. ~ nurse n mwanamke aliyeajiriwa kunyonyesha mtoto wa mwingine. 2 -a chepechepe, -a mvua. ~ paint. rangi ambayo

wether

haijakauka; rangi mbichi. 3 -enye kuhusu pombe. 4 (sl) (of a person) -oga, -a wasiwasi n 1 the ~ mvua. 2 unyevu; vt tia maji, lowesha, nyunyiza maji. ~ting n kulowanisha, kulowana.

wether n ndafu: kondoo maksai,

we've = we have.

whack vt piga kwa kishindo (mtu/kitu) n 1 (sound of) pigo. 2 (sl) mgawo, mgawanyo. ~ed adj (colloq) (of a person) liochakaa, liochoka, hoi. ~ing n kipigo; kuchapa (barabara). adj (colloq) kubwa ya aina yake/ sana. adv (colloq) sana. ~er n kitu kikubwa cha aina yake.

whale n 1 nyangumi. ~ bone n mfupa wa kinywani mwa baadhi ya aina za nyangumi. 2 (colloq) starehe. a ~ of a time starehe/furaha sana vi winda nyangumi. ~r n 1 mwinda nyangumi. 2 chombo cha kuwindia nyangumi. whaling -gun n bunduki ya kuulia nyangumi.

whang vt (colloq) piga kwa nguvu/kishindo n pigo, mshindo adv (colloq) sahihi, hasa, hapo hapo.

wharf n gati. ~age n 1 ada, ushuru (hasa unaotozwa kwa kutumia gati). 2 gati. 3 kupakia pakua gatini. ~man n kuli. ~-master n mwenye gati; msimamizi wa gati.

what adj 1 (interr) ipi, gani. 2 (exclamatory) unasemaje! kweli! 3 chochote (ambacho); (pron) (inter) nini. ~ for kwa kazi gani, kwa nini. ~ for n (colloq) adhabu. ~ like yukoje. ~ if itakuwaje, itakuwa vipi ~ though (liter) ijapokuwa, ingawa, hata kama. ~ about/of kuhusu nini; kuna habari gani kuhusu. ~ of it? (or, mod colloq) So ~ kwa hiyo? sasa? and ~ not na kadhalika. and/ or ~ have you pamoja na hayo; kadha wa kadha, na kadhalika. ~ not na vinginevyo; kibweta. I know ~ nina wazo/pendekezo, najua. I/I'll tell you ~ (hebu) sikiliza. know ~'s~ tumia akili, elewa mambo.

when

~do you call him/her/it/them; ~'s his/ her its/their name ni nani hii, nani hino, (rel) (pron) kitu chacho. ~ with ... and (~ with) kutokana na (sababu kadhaa). ~ever adj 1 (emphatic for what) oote ile, iwayo yote. 2 (placed after n in a negative contex, giving emphasis to the negative) kabisa do ~ ever you like fanya upendalo (pron) 1 hata iweje. 2 chochote. 3 ~ever (colloq) lolote lingine, -o ote -ingine. ~-so-e'er (poet for) ~-so-ever adv (emphatic for) ~ever, whate'er (US) adj = whatever.

wheat n ngano ~ crop mavuno ya

ngano. ~en adj -a ngano, -a unga wa ngano.

wheedle vt ~ (into/out of) bemba, bembejea, bembeleza, shawishi, rairai. ~r n mbembelezaji.

wheel n 1 gurudumu. ~s within ~s (fig) matata mengi; mchanganyiko wa mambo. put one's shoulder to the ~jitahidi; saidia the man at the ~ dereva, mwendeshaji. ~ barrow n toroli. ~ base n kitako cha gari. ~chair n kiti cha magurudumu. ~ house n chumba cha nahodha katika meli. ~-man n mpanda baiskeli.~ wright n fundi wa magurudumu. 2 potter's ~ n gurudumu la kufinyangia vyungu, kurugo. paddle ~ n makasia. 3 mwendo wa gurudumu vt,vi 1 sukuma; vuta; beba, peleka. 2 enda; pinda, kata. ~ and deal vi fanya hila katika siasa/biashara.

wheeze vt,vi korota, forota, pumua kwa shida. ~ sth out sema kwa kukorota. n 1 mkoroto, mkoromo 2. hila, vitimbi. wheezily adv. wheeziness n.

whelk n aina ya konokono wa pwani.

whelp n 1 mtoto wa mbwa, simba, chui, mbweha, dubu n.k. 2 kijana fidhuli vi zaa.

when 1 (an inter adv) lini? wakati gani? hadi lini since ~ tangu lini

adv (with day, time, etc as antecedent) siku/ saa zipi? (rel) adv amba conj 1 -po, ambapo. 2 ingawaje, ingawa. 3 kama, endapo. 4 wakati ambapo. ~ce adv (form) 1 (in questions) kuanzia kutoka wapi? ~ce does he come? atoka wapi? 2 (in statements) ambapo/ ko/mo toka wapi. 3 kwenye sehemu atokako/aliko kuwa. ~ever adv (conj) 1 wakati wowote. 2 kila. 3 ~ever (colloq) wakati wowote.

where inter adv 1 wapi, mahali gani. 2 (with a prep following the v) mahali gani, wapi; (rel) adv ambapo/ -ko/-mo -po, alipo/ko/mo. ~abouts adv wapi, sehemu gani n makazi I don't know his ~abouts at present sijui alipo sasa. ~as conj (esp leg) kwa maana; kwa kuwa, lakini, wakati ambapo. ~at adv (old use) na hapo, kwa hiyo, hivyo. ~fore adv (old use) kwa nini? kwa sababu hii, sababu, kisa. the whys and the~fores kwa nini na kwa sababu gani? visa na mkasa. ~ by; ~in adv katika hii; -ko -mo, -po; katika nini. ~of adv (formal) ya kitu gani? ~through adv ambacho kwacho. ~upon adv hapo; baadaye; ndipo, kwa hiyo, katika. ~ver adv kokote, po pote ~ver he likes kokote/popote apendapo ~ever that may be popote kiwapo. ~with adv kwa hii, na hii, -enye hii, kwa (na). ~ withal adv (old use); ~with. the ~withal n (colloq) mali, uwezo, nafasi.

wherry n mashua ndogo nyepesi (kwa abiria). ~man n mfanyakazi katika mashua ndogo nyepesi.

whet vt noa, tia makali; (fig) chochea, amsha, zidisha (tamaa ya chakula, kinywaji). ~stone n kinoo.

whether conj 1 (introducing an indirect question) kama. ~ or no kwa vyovyote, ukipenda usipende. 2 (introducing an infinitive phrase) kama. ~ or not kwa vyovyote vile.

whew (often in joke) loo!!

whip

whey n maji baada ya maziwa kuganda.

which adj 1 -ipi (int adj/pron) gani. 2 (rel adj) amba (-ye, -yo-, -zo-); kitu ambacho, -o ~ story he believed hadithi ambayo aliiamini; (rel prons (of things) only not of persons) -o: amba-o the book ~ kitabu ambacho/ kilicho. ~ever adj pron 1 -o- -ote (yo yote, chochote) ~ever you wish chochote utakacho. 2 ye yote, cho chote, yoyote. ~soever; ~ever.

whiff n 1 mpumuo wa ghafla, mpulizo wa ghafla. 2 kishindo cha ghafla cha upepo ~ of fresh air mpulizo wa hewa safi. 3 harufu vt,vi vuma; puliza hewa kidogo kidogo.

while n muda, wakai. once in a ~ mara moja moja vt (only in) ~ sth away pitisha muda/wakati ~ waiting nilipokuwa nikingoja; wakati huo, papo hapo conj whilst while. wakati wa, wakati ule ule, huku, wakati -po/-ki. .

whim n haja; wazo la ghafla.

whimper vt,vi 1 lialia (kwa sauti ndogo), kama mtoto mgonjwa. 2 nung'unika, lalama n sauti ya kulalama.

whimsy; whimsey n 1 kinjozi, ruya. 2 kichekesho cha ajabu ajabu whimsically adv. whimsicality n. whimsical adj.

whine vi,vt lia (kama mbwa anayeogopa); (of person) nung'unika. ~r n mlalamishi; mtu/mnyama anayetoa mlio huu n mlio (wa mbwa anayeogopa); mlio mkali wa kunung'unika (unaoendelea kwa muda mrefu). whinny vi (of horse) lialia n mlio wa farasi.

whip1 n kiboko, mjeledi. have the ~ hand (over sb) tawala, dhibiti,-wa na madaraka juu ya mtu. ~cord n kigwe cha nguvu; nguo ngumu kuchanika. 2 (also ~per in) msimamizi wa mbwa (katika kuwinda). 3 mratibu wa chama cha

siasa au shughuli za bunge (anayehakikisha wanachama wanahudhuria na kupiga kura bungeni); amri ya kuhudhuria na kupiga kura. a three line ~ n amri kali ya (kuhudhuria na kupiga kura) kikao cha bunge. 4 kupigapiga mayai, malai n.k.; mpigaji mijeledi.

whip2 vt,vi 1 chapa, piga (mjeledi). 2 a sth (ups)(into sth) piga, pigapiga, koroga. 3 (colloq) shinda sana, chapa. 4 chukua, chukulia; -ondoka, -ondoshwa, toa, toka (kwa haraka). 5 (GB colloq) iba. ~ round for money etc changisha fedha kwa marafiki au wanachama (ili kununua zawadi). ~ round n mchango huo. 6 shona pindo. ~ping kuchapa kiboko/fimbo. ~ping -boy n (hist) mtwana: kijana anayesoma na mtoto wa mfalme na kuadhibiwa badala yake; (scapegoat) msingiziwa. ~ping -post n (hist) nguzo walipofungwa watu na kuchapwa viboko. ~ping-top n see top.

whipper-snapper n mtu/kijana anayejidai/jikweza sana (pasipo kustahili).

whippet n mbwa wa mashindano ya mbio.

whippy adj -a kunyumbuka, -a kunepa, -a kunesa.

whir n see whirr.

whirl vt,vi 1 zunguka/zungusha kwa kasi. 2 pita/pitisha kwa kasi, vurumisha. 3 (of brain, the senses) zunguka/vurugika; (of thoughts) changanyikiwa n 1 (sing only) mzunguko wa kasi; (fig) kuchanganyikiwa. 2 harakati, michakato, vuguvugu la maisha. 3 (compounds) ~ pool n kizingia cha maji, mzunguko wa maji. ~ wind n kimbunga, kinyamkela, chamchela. sow the wind and reap the ~ wind (prov) panda upepo uvune tufani. ~igig n 1 pia. 2 mzunguko. the ~ igig of life mzunguko wa maisha.

whir(r) vi vumisha n (sing only) uvumi

white

(wa kitu kinachozunguka); mvumo.

whisk n 1 (brush) burashi (ya kupangusia nguo) fly ~ usinga, brashi ya nzi (iliyotengenezwa kutokana na manyoya). 2 mchapo (mayai). 3 pigo jepesi la upesi, panguso. vt, vi ~ sth/sb off/away pangusa upesi, 1 tingisha, punga mkia hewani. 2 chukua/twaa/ peleka kwa ghafla. 4 (egg etc) koroga, pigapiga, chapa.

whisker n ~(s) 1 (person) sharafa,

ndevu za mashavuni. 2 (animals) sharubu. cat's ~s n (sl) kitu kizuri/mtu mzuri. ~ed adj -enye sharafa.

whisky n wiski: pombe kali.

whisper vt,vi 1 ~ to nong'ona;

nong'oneza. ~ing gallery n ukumbi wa kunong'ona. 2 vuma; vumisha, fanya nywinywila; eleza kwa siri/ faragha. ~ing campaign n kampeni za sirisiri za uvumi (dhidi ya mtu). 3 (of leaves) chachatika n 1 mnong'ono, manong'onezo. 2 uvumi. ~er n mnong'onezaji; mnong'onaji; mvumishaji.

whistle n 1 mluzi; mbinja, mlio. ~ stop n (US) kusimama kwa muda mfupi (ili kuzungumza na watu). 2 filimbi, kipenga. 3 wet one's ~ (sl) nywa, pata kinywaji vt,vi 1 piga mluzi/ mbinja/filimbi, lia. ~ for sth ahidiwa/tegemea/wa na ahadi ya uongo. ~ down the wind telekeza kitu. ~ in the dark fanya jambo la kujitoa woga. 2 ~(up) piga mbinja; toa ishara; ita kwa mbinja. 3 pita haraka, (na kutoa mlio wa mluzi).

whit n not a ~. no ~; hapana hata kidogo/chembe. whit see whitsun.

white1 adj 1 -eupe. bleed (sb/sth) ~ (fig) kamua/nyonya mtu. 2 (compounds) ~ alloy n fedha ghushi. ~ ant n mchwa. ~ bait n dagaa. ~ bear n dubu mweupe. ~caps n mawimbi meupe. ~ collar n kazi isiyo ya sulubu. ~ coffee n kahawa yenye maziwa. ~

white

flag n ishara ya kusalimu amri. ~ heat n joto kali linalofanya chuma kuwa cheupe; (fig) hamaki, harara kali. ~ hot adj -a harara, -enye hamaki. the W~ House n Ikulu (ya Rais wa Marekani); sera ya serikali ya Marekani. W ~hall n mtaa wa London (ambapo kuna ofisi za serikali); sera ya serikali ya Uingereza. ~ lead n risasi nyeupe (yenye sumu inayotumiwa katika utengenezaji rangi). ~ lie n uongo mtakatifu, uongo usiodhuru, maneno ya kupoza/kuondosha njiani. ~ lipped adj -enye midomo myeupe (kwa woga). ~ livered adj oga, mwoga. ~ man/woman n mzungu. ~ meat n nyama ya kuku, ndama au nguruwe. ~ metal n see ~ alloy. ~ paper (GB) waraka/ripoti rasmi ya serikali ya habari maalum. ~d sepulchre n mnafiki. ~ slave n msichana mzungu anayelazimishwa kuwa malaya/ kahaba (hasa kwa kudanganywa kwenda ng'ambo kwa ahadi ya kuajiriwa). ~ smith n mfua bati; chokaa. ~ thorn n miti ya miiba inayotumiwa kujengea wigo. ~ tie n vazi rasmi la jioni; tai ndogo nyeupe. ~ wash n chokaa; (fig) mbinu ya kuficha makosa ya mtu vt (fig) ficha makosa ya mtu.

white2 n 1 rangi nyeupe. 2 mzungu, mtu mweupe. 3 ute wa yai. 4 mtoto wa jicho. ~ness n weupe. ~n vt,vi fanya -eupe, paka/tia rangi nyeupe; geuka kuwa -eupe. ~ning n 1 chaki, chokaa. 2 dagaa.

whither adv (old use) -ko, wapi? kwenda wapi? Let him go ~ he will aende apendako. ~soever adv (old use) popote; kokote.

whiting1 n see whitening

whiting2 n see whitening

whitlow n mdudu (katika kidole).

whittle vt,vi 1 ~ (sth) away chonga, kata vipande vyembamba; (fig) punguza. ~ (away) at sth chongachonga. ~ sth down

whop

chongachonga. 2 punguza vipande vidogo vidogo; (fig) punguza idadi/ kiasi. 3 chonga.

whiz n mvumo: mlio wa kitu kilichovu- rumishwa vi vuma.

whizz-kid n (sl) kijana mwerevu (anayefanikiwa haraka).

WHO Shirika la Afya Duniani.

who inter pron (used as the subject and only of persons; object form whom) 1 nani. (know) ~'s who fahamu watu vizuri (maisha yao, kazi yao n.k.). 2 yupi, nani; (rel) pron ambaye/o, -ye-, -o-. ~ the gods love die young wazuri hufa mapema; chema hakidumu. ~ever pron yeyote; -o-ote ~ever he is yeyote awaye.

whodun(n)it n (=who done it (sl) for who did it) riwaya ya upelelezi/ kusisimua/ujasusi.

whole adj 1 -zima, kamili, -timilifu,

ote. 2 -ote, zima. ~ note n (US) noti zima. ~ number n namba nzima. ~ wheat meal n unga wa ngano isiyokobolewa; unga ambao haukukobolewa. ~ milk n maziwa halisi. 3 the/one's ~ -ote, kamili. do sth with one's ~heart fanya kwa moyo mkunjufu/mmoja. 4 ~ hearted adj, (attrib with pl n) kamili, zima. 5 (old use, biblical) -enye afya njema, zima n uzima, kitu kizima. on the ~ kwa jumla; kwa kuzingatia yote. (taken) as a ~ kwa kujumuisha, kwa pamoja. wholly adv kabisa. ~some adj -enye (kuleta) afya/siha.

wholesale n jumla; biashara ya jumla adj -a jumla. ~r n mwuza jumla.

who'll who will nani ata-.

whoop n 1 ukelele (wa shangwe, furaha). 2 sauti ya kikohozi. ~ing cough n kifaduro vt,vi piga ukelele wa shangwe/furaha. ~ it up (sl) la starehe sana. ~ee n. make ~ee (sl) sherehekea, fanya shamrashamra.

whop vt (sl) piga, shinda. ~per n

who're

kitu/jambo kubwa (agh uongo

mkubwa); kitu kikubwa cha aina yake; kubwa sana. ~ ping adj.

who're who are.

whore n (derog) kahaba, malaya. ~dom n umalaya; uasherati. ~-master n asherati.

whorl n mzingo (duara au kama duara). ~ed adj -enye mzingo, -a mzingo, (kama alama zilizo katika ngozi ya ncha za vidole).

whose poss pron (who, of whom; of

which) 1 -a nani? whose is that? h-o ni -a nani? 2 (in rel, defining clauses) amba -ye/o/cho .... ke/ao she is the woman ~ son went to University yeye ni yule mwanamke ambaye mtoto wake alienda Chuo Kikuu.

whoso; whosoever (old use) see whoever.

why adv 1 (interr) kwa nini? mbona? kwa sababu gani. 2 (rel adv) sababu, (kwa nini) maana! I will tell you ~ nitakuambia sababu this is ~ ndiyo sababu/maana; (int) lo!; (expressing surprise) kumbe! ~ look at that! kumbe! ona sasa!; (expressing protest) n sababu, kisa, hoja. the ~s and the wherefores kisa na mkasa.

wick n utambi, mjali, kope.

wicked adj 1 (of person, his acts) -ovu, habithi. 2 -enye inda, -a kuumiza. 3 tukutu; tundutundu. ~ly adv kwa uovu. ~ness n uovu; ufisadi.

wicker n fito (henzerani, matete) zilizosukwa. ~ work n vitu vilivyotengezwa kwa fito.

wicket n 1 ~ (door or gate) kilango. 2 kidirisha cha kuuzia tikiti. 3 (cricket) kilango cha vijiti vitatu kinacholindwa na mwenye kushika beti take a ~ shinda mshika beti. ~-keeper n (cricket) mdaka mpira aliye nyuma ya kilango.

wide adj 1 -pana, -liotanuka. 2 ingi,

kubwa, pana. 3 wazi kabisa. 4. nje ya, -a mbali. 5 (sl) janja, danganyifu; -enye uhodari wa biashara. ~ boy(s)

wild

mtu mjanja/ mdanganyifu; mfanyabiashara hodari adv 1 mbali. 2 wazi kabisa. ~ awake adj (fig) makini, -a macho. be ~ awake -wa macho/tayari. 3 kwa mapana. ~ spread adj -liotapakaa, -lioenea pote, -a kusambaa. ~ly adv 1 sana, kwa kiasi kikubwa be ~ly read somwa sana. 2 hapa na pale, kwa vipindi vipana. 3 kwa kuenea/kutapakaa. ~n vt,vi tanua, panua, eneza.

widgeon n aina ya bata mwitu.

widow n mjane mwanamke. ~er n mjane mwanamume. ~ed adj. ~hood n.

width n 1 upana; (fig) upana wa

mawazo, akili. 2 (kipimo cha) upana. 3 kitambaa cha upana fulani.

wield vt twaa/ shika na kutumia ~ power shika madaraka, tawala ~ an axe tumia shoka.

wife n 1 n mke take a ~ oa she will make a good ~ atakuwa mke mwema. old wives' tale n hadithi za kijinga/ kishirikina. ~like; ~ly adj kama mke/ahali; -a mke, -a kuhusu mke. ~ly duties n majukumu ya mke.

wig1 n nywele bandia. ~ged adj -liovaa nywele bandia.

wig2 vt karipia, kemea. ~ging n (colloq) karipio, kemeo get/ give sb a good ~ging kemewa, kemea mtu vikali.

wiggle vt,vi gaagaa; furukuta, jisombogoa; chezeshachezesha.

wight n (arch) binadamu, mtu.

a luckless ~ mtu mwenye kisirani.

wigwam n hema (la ngozi au mkeka) (la Wamarekani wa asili).

wild adj 1 (animals) -a mwitu, -siofugwa ~ animal mnyama mwitu; (plants) -a gugu, -a kujiotea -enyewe, -a porini. ~ cat n paka shume; (attrib adj) -a uenda wazimu, -siowezekana; siopangwa. ~ fowl n (esp) ndege wa kuwindwa. ~ goose n bata mwitu ~ goose chase n

wildebeest

shughuli isiyo na manufaa. 2 (of horses, game birds) -a kukurupuka. 3 (of persons, tribes etc) -shenzi, -siostaarabika, kali. 4 (of scenery, areas of land etc) -a mahame, -a pori, -siokaliwa. 5 (violent) -a nguvu nyingi, -a dhoruba. 6 (ungoverned) -liohemkwa/vurugikiwa, -sio makini; -a kuchanganyikiwa ~ with anger liohamaki sana. 7 (colloq) -a kupenda sana, -a shauku/raghaba/ hamu. be ~ about sb/sth fia mtu/ kitu, -wa na hamu juu ya kitu. 8 ovyo, mchafukoge. ~ shooting n kufyatua risasi ovyo. run ~ tenda upendavyo (bila kudhibitiwa). spread like ~ fire (of reports, rumours) enea haraka sana. 9 (of a playing card) -enye thamani yoyote the ~s n mwitu, pori, nyika adv ovyo ovyo. ~ly adv ovyo ovyo, bure, bila mpango. ~erness n.

wildebeest n kongoni.

wile n hila, ujanja, werevu. wily adj -erevu, janja.

wilful adj 1 -kaidi, -gumu. 2 -a kusudi, -liokusudiwa ~ damage hasara ya kusudi. ~ly adv makusudi; kwa kusudi, kwa kutaka. ~ness n ukaidi, ugumu; ushupavu.

will1 n 1 the ~ hiari, ridhaa an iron ~ nia thabiti against sb's ~ dhidi ya ridhaa ya mtu. 2 (also ~ power) utashi, rada. 3 dhamira. take the ~ for the deed shukuru kwa nia njema ya mtu (japo hakutenda). of one's own free ~ kwa hiari. at ~ upendavyo. tenant at ~ (legal) mpangaji anayeweza kuondolewa wakati wowote. 4 raghaba, hamasa; bidii, juhudi. 5 mapenzi, kudura. 6 good/ill ~ n makusudi mema/ mabaya, matlaba. 7 (also last ~ and testament) wosia.

will2 vt (pt would) 1 taka, penda what would you~? ungetaka nini. 2 (the subject is often omitted) -nge would it were otherwise laiti ingekuwa vinginevyo. 3 chagua, tamani,

win

pendelea. would be attrib adj -naotarajiwa, -jao the would -be authors waandishi wanaotarajiwa; wanaoinukia vt,vi 1 fanya iwe; dhamiria, taka. 2 andika, jaalia. 3 athiri; taaradhi; tawala. 4 ~ sth to sb; ~ sb sth rithisha.

will3 1 (used as an auxiliary verb of the future tense) (to express willingness, consent, offer, promise etc) -ta tomorrow ~ come kesho itafika she ~ come atakuja all right I'll come sawa, nitakuja. 2 (used with the 2nd person in questions, making polite request) tafadhali give me the book, ~ you tafadhali nipatie kitabu. 3 kazania, shikilia; wa lazima he ~ go to the dance anashikilia kwenda kwenye dansi. 4 wa na mazoea, tabia, desturi. 5 (to indicate probability or likelihood) majaliwa, labda, huenda. 6 (conditional) -nge-, -ngali, -kama they would have seen the thief if they had arrived earlier wangalimwona yule mwizi endapo wangefika mapema.

willies n (pl) (sl) wasiwasi, woga.

willing adj 1 tayari, radhi. 2 -sio swali, bila kusita, bila makeke. ~ly adv. ~ness n.

will-o'the-wisp n mwanga uonekanao katika kinamasi; (fig) kitu/mtu mgumu kufikiwa/kupatikana.

willow n mti umeao karibu na maji. ~y adj mrefu mwembamba.

willy-nilly adv taka usitake, bila hiari au kwa hiari, vyovyote vile.

wilt1 vi (of plants, flowers) nyauka, dhoofu; pungukiwa na nguvu/uzuri (of persons) nywea, ishiwa nguvu.

wilt2 vt (arch form of will 3).

wily adj see wile.

wimple n 1 ukaya/utaji/shela ya hariri yenye marinda vt weka marinda katika shela/utaji.

win vi,vt 1 shinda, pata, jipatia (kwa

jitihada); tia fora. ~ the day/the field shinda, pata ushindi. ~ free/clear/out through

wince

shinda/pita/jinasua/ ondokana na matatizo kwa jitihada. ~ hands down (colloq) shinda kwa urahisi. 2 ~ sb over (to sth); (less usu) ~ sb to do sth vuta, shawishi mtu (kufanya jambo). 3 fikia (mahali) (kwa jitihada) n kushinda, ushindi we had four ~s tulishinda mara nne. ~ner n mshindi.

~ning adj 1 -enye kushinda. 2 -a kushawishi, -shawishi, -a kuvutia. ~nings n (pl) (esp) fedha za ushindi. ~ning post n kifundo: kiguzo cha kumalizia mbio, mwisho.

wince vi nywea; shtuka (kutokana na kuumia kama mtu aliyeumizwa sana kwa kitu au maneno) he heard the news without wincing alisikia habari bila kushtuka n mshtuko.

winceyette n kitambaa cha pamba au sufu.

winch n winchi, manjanika vt sogeza kwa winchi.

wind1 n 1 (often the ~) upepo. fling/ throw caution/prudence, etc to the ~s acha kabisa, tahadhari. get/have the ~ up (sl) ogopa, tishika. raise the ~ (sl) pata fedha zinazotakiwa. put the ~ up sb (sl) tisha/ogopesha mtu. see/find out how the ~ blows tafuta/sikiliza watu wasemavyo. take the ~ out of sb's sails wahi mtu; tafuta mwelekeo wa mambo, zuia mtu kusema/kutenda jambo; katiza faida yake ghafla. there is sth in the ~ kuna njama/mpango wa siri (unaoandaliwa). 2 (pl) pande kuu nne za pepo the papers were blown to the four ~s karatasi zilipeperushwa pande zote. 3 pumzi. get one's second ~ pata pumzi tena; (fig) pata nguvu mpya kutekeleza jambo. sound in ~ and limb buheri wa afya, katika siha nzuri, mabusuti. 4 harufu, fununu. get ~ of (fig) nusa harufu ya, pata fununu ya. 5 maneno matupu, upuuzi. 6 upepo/gesi (ya tumboni). break ~ jamba, shuta. 7 the ~ n ala za kupuliza (za muziki).

window

8 (compounds) ~ bag n (colloq) mpiga porojo, mwenye kupayapaya. ~ break n kikinga upepo. ~ cheater (US ~ breaker) n koti ya kukinga upepo. ~fall n tunda lililoanguliwa na upepo; (fig) nyota ya jaha. ~-gauge n kipimaupepo. ~ instrument n ala ya muziki ya kupuliza. ~-jammer n (colloq) chombo (jahazi n.k.) cha mfanyabiashara. ~ mill n kinu cha upepo. fight/tilt at ~mills pigana na adui, maovu ya njozi/ kubuni. ~ pipe n koromeo. ~ screen (US = shield) n kioo cha mbele cha gari. ~-sock n fuko la upepo. ~storm n dhoruba (ya upepo mwingi na mvua kidogo). ~ swept adj wazi kutokana na upepo, liofagiliwa na upepo; -a kukabiliana na upepo. ~less adj -sio na upepo. ~ ward adj -a upande wa upepo wa joshini n upande wa upepo. get to the ~ward of sb epa harufu ya mtu. ~y adj 1 -a upepo mwingi. 2 -a maneno mengi. 3 (sl) -enye hofu. ~ly adv. ~iness n.

wind2 vt 1 gundua kitu kwa

harufu. 2 kosa pumzi; kosesha pumzi. 3 pa nafasi ya kupumua.

wind3 vi,vt 1 zunguka, pinda, nyonganyonga; zungusha, pindisha. 2 sokota (kitu) kwa mfano wa mpira. ~ sth off sokotoa; fumua. ~ sb round one's (little) finger fanya mtu atende kila utakalo. 3 ~ sth round sb/sth; ~ sb/sth; ~ sth funika vizuri, kumbatia. ~ing sheet n sanda. 4 ~ sth (up) zungusha, nyonga; pandisha kwa kunyonga mpini. 5 jaza ufunguo, lisha saa. 6 wound up (to) sisimka, changamka; panda. 7 ~ (sth) up maliza; katisha, komesha. ~ up a business/ company kamilisha kila kitu kabla ya kufunga kampuni. ~ up one's affairs kamilisha na kufunga shughuli n mzunguko mmoja.

windlass n winchi.

window n dirisha. ~ box n sanduku la

kuoteshea maua dirishani. ~-display n maonyesho ya bidhaa dirishani. ~-dressing n 1 mpangilio wa bidhaa (dirishani). 2 (fig) (ustadi wa) kujionyesha vizuri/kujipendezesha, upendezeshaji. ~-ledge n ukingo wa dirisha. ~ envelop n bahasha (enye kioo/ kidirisha). ~-pane n kioo cha dirisha. ~-seat n kiti cha dirishani. ~shopping n kutia macho nuru, kuangalia bidhaa dirishani. a ~ on the world (fig) kifunua macho; njia yoyote ya kujua ulimwengu vizuri zaidi.

wine n divai, mvinyo. new ~ in old bottles mambo mapya yasiyoweza kuzuilika. ~ glass n bilauri ya divai. ~-grower n mlimaji zabibu. ~-press n kishinikizo cha zabibu. ~-skin n mfuko (wa ngozi yote ya mbuzi) wa divai. ~-taster n mwonja divai. 2 pombe (inayofanana na divai). palm ~ n tembo vi,vt kunywa mvinyo. ~ and dine sb karibisha mtu chakula (na mvinyo). ~ry n kiwanda cha mvinyo.

wing n bawa, ubawa. clip the ~s of zuia. lend/add ~s to fanya kuchapuka. take (to itself) ~s potea, toweka. take sb under one's ~ linda, hami, engaenga. ~nut/screw n nati. ~span; ~-spread n kipimo cha ubawa toka ncha mpaka ncha. 2 (of building. army) upande, pembe; sehemu. 3 (mil) vikosi vya pembeni. 4 wakereketwa, wanazi; wenye msimamo mkali. 5 pembe za chaki. 6 on the ~ nayoruka/puruka. take ~ anza kuruka. 7 kitu kama ubawa. 8 (football, hockey) wingi. 9 (GB) vikosi viwili au zaidi vya jeshi la anga; (pl) beji ya rubani. ~

-commander n ofisa wa jeshi la anga. ~ed adj 1 -enye mabawa. ~less adj bila ubawa. ~er n wingi.

wink 1 vi,vt ~ (at) pesa, pepesa,

kupia, konyeza. as easy.... as ~ing rahisi sana. ~ at sth achilia, samehe, fumbia macho, jidai huoni. 2 (of star) meta n 1 ukope, konyezo

wire

give a ~ to kupia, konyeza. a ~ is as good as a nod ishara ni sawa na kuitikia/ kukubali. 2 muda mfupi sana. forty ~s n usingizi kidogo. tip sb the ~ pasha mtu habari (kwa siri), nong'oneza mtu.

winkle n konokono la pwani. vt ~sb/sth out chokoa/chokonoa kitu (mpaka kukitoa).

winnow vt pepeta, pembua, puliza.

winsome adj a kuvutia, -a kupendeza. ~ly adv. ~ness n.

winter n majira ya baridi (kali) a man of 50 ~s mwenye umri ya miaka 50. ~ garden n mimea ndani ya chumba cha glasi vi,vt kaa majira ya baridi ~ in France kaa Ufaransa majira ya baridi. ~ tide n kipindi cha baridi. ~of wintry adj -a majira ya baridi, -a baridi kali; (fig) baridi, a uongo -a ~y smile tabasamu baridi.

wipe vt pangusa, safisha kwa kufuta, futa. ~ the slate clean anza upya. ~ sth away futa, pangusa. ~ sth off pangusa; ondosha, maliza, futa. ~ sth out pangusa (ndani ya), ondosha, futa, sahau; angamiza, teketeza kabisa. ~ sth up kausha n kufuta. ~r n 1 kifuto. 2 waipa.

wire n 1 waya. pull (the) ~s (fig) tumia njia za siri kupata jambo; endesha kikaragosi. live ~ n waya wenye umeme; (fig) mashughuli, mtu afanyae kazi kwa bidii. ~-cloth n wavu wa nyuzi za chuma. ~-cutter n chombo cha kukatia waya. ~-netting n wavu wa nyuzi za chuma shaba. ~-puller n mtu avutaye mambo kwa siri. ~-pulling n 1 ushawishi. 2 shauri la siri. ~ rope n kebo, kamba ya waya. ~ haired adj -a kipilipili. ~ wool n kumbi la waya/chuma. 2 (colloq esp US) simu ya upepo vt,vi 1 funga, kaza kwa waya. 2 weka, tia (nyuzi za) umeme. 3 (telegraph ) piga simu, arifu kwa simu. 4 tega/nasa kwa waya. wiring n (mfumo wa) waya za umeme. wiry adj embamba

wise

na shupavu. ~less n simu ya upepo; redio vt peleka habari kwa redio adj -a redio, -a simu ~less station stesheni ya simu ya upepo.

wise1 n (sing only old use) namna, jinsi. in no ~ sivyo kabisa, sivyo kwa jinsi yoyote.

wise2 adj -a busara/hekima. be none the ~r tojua zaidi kuliko mwanzo. be/get ~ to sb/sth (sl) zinduka. put sb ~ to sb/sth pasha, letea fulani habari, eleza. ~acre n mtu ajifanyaye mjuzi; mchushi. ~ crack n (sl) mzaha, msemo vi toa mizaha/ misemo. ~ly adv kwa hekima vt,vi ~ up (US infml) pata habari. wisdom n 1 busara, hekima; idili. wisdom tooth n gego la mwisho. 2 mawazo ya busara, methali, misemo.

wish n 1 matakwa, mapenzi, matamanio. if ~s were horses, beggars might ride (prov) atakalo mtu hapati hupata ajaliwalo. the ~ is father to the thought (prov) tunaamini tunalotaka kuamini. 2 kitakiwacho, matilaba. ~ful adj tamanifu, -enye kutaka. ~ ful thinking n ndoto za mchana. ~fully adv vt,vi 1 ~ (that) taka; penda; tamani. 2 ~ sb well/ill takia mema/mabaya. 3 taka she ~s to be alone anataka faragha I ~ you would be more careful tafadhali kuwa mwangalifu zaidi. 4 ~ for wa na hamu, tamani, ombea jambo. ~ bone n mfupa wa kuku ulioko kati ya shingo na kifua. ~ ing cap n (in fairy tales) kofia ya kuombea. 5 ~ sb/sth on sb (colloq) takia baa/balaa. ~er n mtakia bahati.

wishy-washy adj (of soup, tea etc)

-dufu, -rojorojo; (of talk, person) chapwa, sio na nguvu/msimamo, -a wasiwasi.

wisp n kichopa, kitita adj -a kitita,

kama kitita/kichopa.

wistful adj -enye kusononeka; -enye

kutamanitamani; -enye tamaa isiyoridhishwa. ~ly adv.

with

wit1 to ~ (leg) maana yake, yaani, ndiyo God ~s Mungu anajua.

wit2 n 1 akili. be at one's ~'s end taka kuchanganyikiwa, tojua la kufanya. out of one's ~s liochanganyikiwa, -enye wazimu, -enye fadhaa. have a ready ~ wa na majibu/vichekesho vya haraka. have/ keep one's ~s about one -wa mahiri, tayari kung'amua na kutenda. live by one's ~s ishi kwa ujanja. 2 mwerevu, mtu hodari na mcheshi. 3 werevu, ucheshi, mzaha, utani. ~ty adj cheshi, chekeshi. ~ticism n misemo/maneno ya akili/ kuchekesha. ~less adj -pumbavu.

witch n 1 mchawi; mlozi mwanamke; (fig) mwanamke mwenye ucheshi, mvuto ajabu. ~craft n ulozi, uchawi, usihiri remove ~craft adua, sua, zingua, tegua. ~doctor n mlozi wa kiume, mganga, mchawi. ~ hunt n msako wa wachawi; (fig) msako na uonevu wa watu (k.m. wale wanaodhaniwa kuwa wasaliti). ~ery n 1 uchawi. 2 (fascination, charm) ucheshi, ushawishi wa kushinda moyo, uzuri wa kupoteza akili, mvuto, maliwazo vt,vi fanya uchawi, loga. ~ ing adj.

with prep 1 (equivalent to constructions with have) -enye, na, -a, kwa. ~ child (of woman) mjamzito. ~ young (of an animal) mwenye mimba. 2 (to indicate what is used for filling, covering) na, kwa fill ~ sand jaza na/kwa mchanga. 3 (means or instrument) kwa, na write ~ a pen andika kwa kalamu. 4 (accompaniment or relationship) na, pamoja na discuss a problem ~ jadiliana tatizo na. in ~ -enye kushirikiana na. 5 (antagonistic, opposing) -ana na quarrel ~ gombana na compete ~ shindana na. fall out ~ gombana na. 6 (causal) kwa sababu ya, kwa tremble ~ fear tetemeka kwa (sababu ya) woga. 7 (manner) kwa handle ~

withal

care shughulikia kwa uangalifu. 8 sawa na, pamoja; wakati mmoja na move ~ time enda na wakati. 9 (indicate care, charge or possession) -wa na had no money ~ him hakuwa na fedha. 10 (separation) -ana na break ~ achana na. 11 (in agreement or sympathy) -ana na I am ~ you naafikiana na wewe. be/ get ~ it (sl) enda na wakati. 12 licha ya ~ all our effort licha ya juhudi yetu yote.

withal adv (arch) zaidi, tena, juu ya

hayo, aidha.

withdraw vt,vi 1 chukua. ~ sth/sb (from) toa; jitoa; ondoa/ondoka; chukua. 2 futa, tangua ~ a charge futa mashtaka, ondoa mashataka. 3 rudi nyuma; rudisha nyuma; (ji) tenga. ~al n kuondoa, kuondoka; kufuta, kuchukua. ~al symptoms n kujitenga; hali (ya kimaumbile/ kiakili) itokeayo kutokana na kuachishwa kitu ulichozoea (agh madawa ya kulevya) adj pweke, kimya, -liojitenga; -enye mawazo ya mbali.

withe; withy n ufito, ubugu.

wither vi,vt 1 ~ (sth) up; ~ (away)

chakaa, nyauka, -fa, fifisha, nyausha. 2 aibisha, fadhaisha she gave him a ~ing glance alimtupia jicho la kufadhaisha. ~ingly adv.

withers n (pl) nundu (ya farasi n.k.).

withheld pt,pp withhold.

withhold vt ~ sth (from) nyima, katalia; zuia ~ consent kataa ~ the truth from sb ficha mtu ukweli.

within (prep) ndani ya; karibu; chini ya ~ an hour haipati saa ~ my power/ strength chini ya uwezo wangu ~call karibu adv (lit) ndani.

without (prep) 1 bila, pasipo.

~ fail bila kukosa ~ doubt kwa hakika, bila shaka. 2 (before gerunds) bila, pasi people can't live ~ eating watu hawawezi kuishi bila ya kula. go ~ saying wa wazi mno, fahamika pasi kuelezwa. 3 (old use) nje adv (lit or old use) nje.

woman

withstand vt himili.

withstood pt pp withstand.

withy n see withe n see wit.

witness n 1 (often eye ~) shahidi.

~ box n (US also ~stand) kizimba cha shahidi kortini. 2 ushuhuda, ushahidi. bear ~to sb/sth unga mkono; thibitisha sahihi. 3 shahidi, mtu anayethibitisha sahihi ya mtu mwingine. 4 kielezo cha ushahidi, kithibitisho vt,vi 1 shuhudia, ona -enyewe. 2 ~ to sth/ doing sth toa ushahidi. 3 thibitisha sahihi ya mtu mwingine. 4 onyesha, thibitisha.

witticism n see wit.2

wittingly adv kwa makusudi; kwa kujua.

witty adj see wit.2

wive vt,vi (arch) oa.

wizard n 1 mchawi, mlozi. 2 mtu

mwenye uwezo wa ajabu adj (sl) safi sana; bora, -zuri sana. ~ry n uchawi ulozi.

wizen adj -liosinyaa, -liokauka, -kavu.

wobble vi,vt 1 yumbayumba, wayawaya, sesereka. 2 (fig) sitasita, yumba; -to kuwa na uhakika n mtu/ kitu kinachoyumba. wobbly adj 1 -a kutikisika, legelege, -sio imara.

woe n 1 (chiefly poet; sometimes hum) huzuni, majonzi, masikitiko. 2 (pl) sababu za huzuni; matatizo; shida. ~ begone adj ~ful adj. -a huzuni. ~fully adv -a huzuni nyingi, -a kuhuzunisha.

woke pt wake.

wold n pori, mbuga, nyika.

wolf n mbwa mwitu. ~ cry n kilio cha uongo. a ~ in sheep's clothing chui aliyevaa ngozi ya kondoo. keep the ~ from the door weza kujikimu. ~-cub n mtoto wa mbwa mwitu. ~-hound n mbwa wa kuwindia mbwa mwitu. ~whistle n mluzi wa ashiki vt lafua, la kwa pupa ~ ish adj -a kama mbwa mwitu.

wolfram n see tungsten.

woman n 1 mwanamke; (young,

unmarried) msichana; mwanamwali;

womb

(old) (bi) kizee, ajuza; (slave) mjakazi, kijakazi. 2 (without article) jinsi ya kike. 3 tabia ya kike. ~ hood n 1 (collective) uanamama; wanawake. 2 hali ya kuwa mwanamama. ~ish adj -a kike; -a kikekike; -enye tabia ya kike. ~ize vt,vi fuata wanawake sana. ~izer n mfuata wanawake. ~kind n akina mama, wanawake wote. ~like; ~ly adj -a kike, kama mwanamke. ~folk n akina mama; wanawake wa familia ya mtu.

womb n (anat) 1 uterasi: tumbo la

uzazi, mji wa mimba. 2 (fig) it still lies in the ~of time muda ndio utafichua yote.

won pt, pp win.

wonder n 1 mshangao. no/little/ small ~ si shani/ajabu. ~ land n nchi ya neema; nchi ya kubuni/kufikirika lioduwaa/kinduwaa. ~ struck adj -liopigwa na bumbuwazi, -a kustaajabu, lioshangaa mno. 2 ajabu, kioja, mzungu, shani. signs and ~s miujiza. work ~s fanya miujiza, fanya vizuri sana. a nine days' ~ shani ya muda mfupi; kitu kinachovuma kwa muda mfupi. for a ~ ni ajabu. it is a ~ (that) ni ajabu kwamba. what a ~ ajabu ilioje! ~ vi,vt 1 ~ (at sth) staajabu, shangaa, ona ajabu. 2 ~ (about sth) fikiria, wazia. 3 jiuliza. ~ingly adv kwa ajabu, kwa mshangao. ~ful adj -a ajabu, -a shani, -a kustaajabisha, -zuri sana. ~fully adv. ~ment n ajabu, mshangao. wondrous adj (arch, or liter) -a ajabu/shani, -a kustaajabisha, -a kushangaza adv (only with adj) he was wondrous kind alikuwa mwema ajabu.

wonky adj 1 (GB) -a wasiwasi, goigoi, bovu. 2 -dhaifu. feel ~ tojiweza, jisikia vibaya.

wont n (arch or lit) (sing only) mazoea, desturi. use and ~ desturi/ada /tabia madhubuti. pred adj be ~ to zoea he is ~ to travel amezoea kusafiri,

wool

mara kwa mara husafiri. ~ed attrib adj -a desturi; -a kawaida.

won't will not.

woo vt 1 (old use) chumbia, bembeleza (kwa nia ya kuoa). 2 tafuta, jaribu kupata (mafanikio, sifa, usingizi n.k.). 3 tafuta kuungwa mkono (na wapiga kura, wateja, wafanya biashara n.k.). ~er n.

wood n 1 mbao, ubao. 2 (often pl) msitu mdogo, kituka, kichaka. out of the ~s (fig) liookoka, liopona toka hatarini/mashakani. be unable to see the ~ for the trees (fig) shindwa kuona vema kutokana na msongamano. 3 in/from the ~ ndani/ kutoka kwenye kasiki. 4 (compounds) ~ alcohol n spiriti ya mti. ~-block n gogo la kuchongea vinyago. ~-carving n kuchonga vinyago; uchongaji vinyago. ~-craft n ujuzi wa misitu, uzoefu wa mambo ya misitu; ufundi wa kuchonga miti. ~cut n muhuri wa mbao wa herufi au picha. ~ cutter n mtema kuni. ~land n eneo lenye miti, mwitu, msitu. ~man n 1 bwana miti; mkata miti. ~sman n 1 (esp US) bwana miti; mkata miti. ~-pecker n gogonola, kigogota, gogota. ~ pile n lundo la kuni. ~-pulp n ubao uliosagwa (kwa ajili ya kutengeneza karatasi). ~ shed n banda la kuwekea kuni. ~-wind n filimbi ya mti. ~ -work n 1 vitu vya mbao, sehemu ya jengo la miti/ mbao; useremala. ~worker n seremala.~ed adj -a mwitu, -a msitu, -enye miti. ~en adj (attrib) -a mti; -a mbao; -a miti. ~ en headed adj zito, -a akili ngumu, rasimu. ~y adj 1 -enye miti. 2 -a mwitu, -a msitu.

woofer n kipaza sauti kinachotoa sauti ya chini chini.

wool n 1 manyoya; sufu. dyed in the ~ -liotiwa rangi kabla ya kufumwa; (fig) barabara, kamilifu. much cry and little ~ maneno mengi yenye

word

matokeo haba; pigia kelele kitu kisicho na maana. pull the ~ over sb's eyes danganya mtu. ~ gathering n 1 usahaulifu, chechele adj -enye kusahausahau. 2 kitu kama sufu. 3 (of a person) nywele nene zilizosokotwa, nywele za kipilipili. lose one's ~ (colloq) kasirika. 4 (compounds) ~-ball n bonge la sufu. ~ -carder n mchambuaji sufu. ~-carding n utengenezaji wa sufu fupi na ndefu tayari kwa kufumwa. ~len (US woolen) attrib adj -a sufu. ~lens n (pl) nguo za sufu. ~ly adj 1 -enye manyoya mengi, -a sufu; (fig) (of the mind, ideas, arguments) -liochanganyikiwa, siodhahiri n (colloq) nguo za sufu (agh sweta). ~-shears n makasi ya sufu.

word n 1 neno. a play on/upon

~s ulimbuaji maneno. be not the ~ for it tokuwa maelezo yake; wa maelezo yasiyoridhisha. (repeat sth) ~ for ~ (rudia) neno kwa neno (translate sth) ~ for ~ tafsiri sisisi/neno kwa neno. in a/one ~ kwa kifupi. by ~ of mouth kwa mdomo. 2 taarifa, kauli, neno. eat one's ~s kiri kosa; futa kauli na kuomba radhi. have a ~ with sb zungumza na mtu. have ~ (with sb) gombana na. have the last ~ funga mjadala. put in/say a good ~ (for sb) tetea mtu. suit the action to the ~ timiza mara moja jambo ulilosema. take sb at his ~ amini kauli yake. big ~s n majisifu, majigambo. on/with the ~ mara tu baada ya kusema. a ~ in/out of season ushauri unaotolewa wakati unapohita jika/usipohitajika. the last ~ on (a subject) neno la mwisho. the last ~ (in sth) taarifa/ habari motomoto, -a kisasa, bora kabisa. 3 (sing, without def art) habari, taarifa. 4 (sing only with a possessive) ahadi, uthibitisho. be as good as one's ~ timiza ahadi. give sb one's ~ (that) ahidi. keep/ break one's ~ timiza/

work

vunja ahadi. take sb's ~ for it amini mtu asemacho. upon my ~ kweli kabisa; lo, lahaula. 5 (sing only) amri; ishara. 6 (in the Christian religion) the W~ (of God); God's W~ Neno (la Mungu) (agh Injili), (jina la) Yesu Kristo. 7 (compounds) ~ book n kamusi ndogo; faharasa. ~ division n kutenga neno katika sehemu. ~-formation n uundaji wa maneno. ~ painter n mtu hodari wa kujieleza kwa maneno. ~ -painting n kueleza kwa maneno. ~-perfect adj -enye kujua somo kwa moyo, hodari wa kusoma kwa ghibu; lokariri. ~-picture n taswira ya maneno, maelezo (mafafanuzi) stadi (kwa maneno). ~-play n mchezo wa maneno. ~-processor n kichambua maneno, kompyuta. ~splitting n 1 udanganyifu; utengaji maana za maneno vt eleza kwa maneno (sing only) jinsi jambo linavyoelezwa; uteuzi wa maneno katika kuelezea maana. ~less adj kimya; bila maneno. ~y adj -a maneno mengi (pasi lazima). ~ily adv kwa maneno mengi. ~iness n.

wore pt wear.

work n 1 kazi. make hard ~ of sth

fanya kitu kionekane kigumu kuliko kilivyo, taabika na. make short ~ of sth maliza (kazi) haraka. set/ get to ~ (on sth/to do sth) shika/anza kazi. set/go about one's ~ anza kufanya kazi, shughulikia. at ~ on (sth) -wa kazini. all in the day's ~ kawaida. 2 ajira, kazi ya kipato, kibarua. at ~ kazini. in/out of ~ enye/ sio na kazi. 3 shughuli (yoyote). 4 vifaa vya kazi. ~ bag/basket/box n begi n.k. la kuwekea vifaa vya kazi (hasa vya ushonaji). 5 kazi; zao; kipande, kila kilichozalishwa kwa kazi. 6 kazi za akili (k.m. kitabu, muziki n.k.). 7 (pl) mashine (sehemu inayofanya kazi). the ~s of a watch mashine

work

ya saa. 8 (pl with sing or pl v) (jengo la) kiwanda. brick ~s n jengo la kiwanda; kiwanda cha matofali. ~s council/committee n baraza/ kamati ya pamoja ya waajiri na waajiriwa. 9 public ~s n ujenzi (wa barabara, madaraja n.k. na idara ya serikali). 10 (pl v) ngome. 11 (compounds) ~ bench n benchi la makanika. ~ book n kitabu cha mazoezi. ~-day n siku ya kazi. ~ force n wafanyakazi wote (wa mahali/ taasisi fulani). ~house n (GB hist) nyumba ya serikali kwa wasio na makazi; (US) jela ya wahalifu wenye makosa madogo ambapo wanafanyakazi. ~man n 1 kibarua, mtendaji, mfanyakazi, fundi (wa kazi fulani), msanii. ~-manlike adj -stadi, -a ufundi. ~manship n ustadi; usanii. ~-room n chumba maalum cha kufanyia kazi. ~shop n karakana; warsha. ~-shy adj vivu, -zembe, goigoi. ~study n utafiti wa utendajikazi. ~ table n (esp) meza yenye saraka za kuwekea vifaa vya ushonaji vi,vt 1 fanya kazi. ~ in n mgomo wa kuendelea kufanya kazi (kupinga amri ya kufukuzwa n.k.). 2 (of a machine, apparatus, bodily organ, plan, method etc) fanya, tenda kazi iliyokusudiwa; fanikiwa. 3 fanyisha kazi, tendesha kazi. 4 faulu, fanikiwa. ~ one's passage pata nauli kutokana na kazi (kwenye chombo). ~ one's way (through college etc) fanya kazi ili ulipe gharama za kusoma chuo. ~ one's will (on sb) fanya mtu afanye utakavyo. ~ it (sl) fanya mpango. 5 shughulikia, hudumia; dhibiti. 6 sogea, penya, fikia; sogeza, penyeza, fikisha. 7 umba, unda/ finyanga. ~ clay finyanga udongo. ~ dough kanda unga. 8 umuka; vimba; chemka; shtukashtuka the yeast began to ~ unga ulianza kuumuka. 9 tarizi. 10 (special uses with adverbial particles and preps). ~ away (at sth) endelea kufanya/kuchapa kazi. ~ in;~ into

world

(sth) penya, ingia. ~ sth in/into ingiza, tia ~ a few jokes into your story ingiza/tia utani kidogo katika hadithi yako. ~ sth off ondoa, achana na; shughulikia. ~ on/upon sb/sth athiri, gusa; shughulikia. ~ out toa ufumbuzi/ jawabu; tokea; fanya mazoea. ~ out n (muda wa) mazoezi. ~ sth out kisia, toa hesabu; pata jawabu, unda, buni, panga, fumbua; (usu passive) maliza -ote, tumia -ote. ~ up to sth panda taratibu (hadi upeo), fanya kwa hatua, endeleza; sisimua, amsha, hamasisha. ~ sb/ oneself (into) pandisha (furaha, huzuni n.k), endelea, jazibisha. ~ upon sb/sth see ~ on. ~ able adj nayowezekana. ~er n mfanyakazi. ~ing n 1 machimbo (ya madini, mawe) n.k. 2 utendaji kazi. in ~ing order -enye kufanya kazi vizuri. (attrib) (in various senses of the v) ~ing clothes n nguo za kazi. ~ing breakfast/lunch/ dinner n kifunguakinywa/chakula cha mchana/jioni kinachoambatana na mazungumzo ya kikazi. ~ing capital mtaji. ~ing day n siku ya kazi; muda wa kazi (kwa siku moja). ~ing hypothesis n dhanio. ~ing knowledge n maarifa yanayotosheleza kusudio. ~ing out upangaji, makisio (ya matokeo ya kazi); utekelezaji. ~ing party n kamati teule (ya kazi/ shughuli fulani). ~ing part adj -enye kuchapa kazi a hard ~ing woman mwanamke mchapa kazi. the ~ing class n tabaka la wafanyakazi (za mikono/ sulubu).

world n 1 the ~ n dunia, nchi zake na watu wake. the Old W ~ n Ulaya, Asia na Afrika. the New W~ Marekani. make a noise in the W~ vuma, -wa maarufu. a citizen of the ~ raia wa dunia. It's a small ~! vilima havikutani. 2 (as 1 above; used attrib) -a dunia, -a ulimwengu

worm

a ~ language lugha ya ulimwengu. the W ~ Bank n Benki ya Dunia. ~ wide adj -a duniani kote. 3 wakati, maisha this ~ and the next maisha ya sasa na baada ya kifo. ~ weary adj -liochoka kuishi. 4 ulimwengu. in the ~ ulimwenguni. all the ~ like sb/sth nayofanana kabisa na. be all the ~ to sb -wa pekee kwa mtu fulani. not for the ~ kamwe, kabisa, asilani. be/feel on top of the ~ jawa na furaha/ hamasa. be out of the ~ (of sth) (sl) -wa bora sana, wa -a ajabu. carry the ~ before one fanikiwa. a ~ of sth (-ingi/ kubwa) sana. think the ~ of sb/sth penda/husudu/ stahi sana mtu/kitu. 5 vitu/ shughuli za watu, mambo ya dunia. the ~, the flesh, and the devil majaribu. the best of both ~s mema kutoka pande zote (hata ya kikinzana). forsake/ renounce the ~ fuata mambo ya kiroho, hama dunia. 6 mambo ya kibinadamu; maisha, malimwengu. know the ~ pata uzoefu wa maisha. 7 ulimwengu, jamii the ~ of sports ulimwengu wa michezo. 8 the ~ n watu, jumuia (pamoja na taasisi na kawaida zake) what will the ~ say? watu watasemaje? ~ly adj -a dunia; -a malimwengu, -a kupenda anasa za dunia. ~ly wisdom n akili/ hekima ya kuendeleza maisha. ~ liness n.

worm n 1 (in earth ~) mnyoo; funza; (in bowels) mnyoo, mchango. ~ cast n kichuguu cha mnyoo. the ~ of conscience majuto, toba. 2 (in compounds) ~-eaten adj liotobolewa na funza; (fig) -liochakaa, -a zamani. ~ hole n tobo la funza katika tunda/ mti. 3 (fig) bwege, boza. even a ~ will turn (prov) uvumilivu una kikomo, hata bubu atasema, msalie mtume. 4 miduara/nyuzi za hesi vt 1 ~ oneself/one's way in/into/ through penya/pita (polepole au kwa shida). ~ out (of sb) pata habari (kwa kusaili sana). 2 toa minyoo. ~y

worship

adj-enye minyoo; -kama minyoo; -lioharibiwa na minyoo.

worn pp of wear.2

worry vt, vi 1 udhi, sumbua, hangaisha. 2 ~ (about/over sth) kerwa na jambo fulani, ona wasiwasi juu ya jambo fulani. ~ along (colloq) jikongojakongoja. 3 (esp of dogs) kamata kwa meno na kutikisa, ng'ata. 4 ~ a problem, etc out shughulikia tatizo tena na tena hadi liishe, n 1 (hali ya kuwa na) wasiwasi/wahaka/ kiherehere. 2 (usu pl) masumbuko. worried adj -enye wasiwasi, wahaka. ~ing adj. ~ingly adv. worrisome adj sumbufu; -enye kutia wasiwasi.

worse adj -baya zaidi make things ~ tibua, fanya mambo yawe mabaya zaidi. the ~ for wear -liochakaa sana; (fig) hoi, -liochoka sana. 2 (pred only) dhaifu; duni; gonjwa. be none the ~(for sth) todhurika, toumizwa (nacho) adv 1 vibaya zaidi he has been taken ~ hali yake imekuwa mbaya zaidi. none the ~ vilevile. 2 (used to intensify) zaidi n ubaya zaidi, mambo mabaya zaidi a change for the ~ badiliko linaloleta matatizo zaidi. ~n vi,vt ongeza/ongezeka (ubaya). worst adj -baya kuliko -ote, baya kabisa n sehemu/hali/tukio baya kuliko yote. if the worst comes to the worst mambo yakiwa mabaya kabisa. get the worst of it komolewa, shindwa kabisa. the worst of it is that baya zaidi ni kwamba. at (the) worst mambo yakiwa mabaya. do your worst/let him do his worst fanya upendalo/ afanye apendalo vt shinda. worship n 1 ibada. 2 heshima kubwa, pendo kuu. 3 your/his W~, (GB) Mheshimiwa, Mstahiki vt,vi abudu; sali. ~per n (US ~er) mwabudu. the ~ers n watu waabuduo. ~ful adj (in GB titles of respect) -a kustahili heshima, mstahiki.

worsted

worsted n uzi wa sufu; nguo za sufu

(iliyosokotwa) adj -a sufu.

worth pred adj 1 -enye thamani fulani. for what it is ~ bila ahadi juu yake. ~ while adj -a kufaa, -a maana. 2 -enye mali ya thamani fulani. for all one is ~ (colloq) kwa bidii zote. 3 -ema, zuri, stahili the book is ~ reading kitabu ni kizuri kukisoma n 1 thamani. 2 kiasi chenye thamani fulani. ~less adj bure ghali, siofaa kitu, sio na thamani. ~lessness n. ~y adj 1 ~ (of sth/to be sth) -a kustahili. 2 (often ironic or used with a patronizing effect) -a kustahili heshima n 1 mtu mashuhuri (wa kipindi fulani). 2 (hum or ironic) mheshimiwa. ~ily adv. ~iness n. wot God wot (arch or hum) Mungu anajua, ajuaye Mungu, Allahu yaalamu.

wotcher int (GB sl) (as a greeting) halo!, mambo! vipi!

would see will.

wound1 n 1 jeraha. 2 kidonda, mchubuko (katika mti n.k.). 3 (of feelings) uchungu, maumivu vt 1 jeruhi, umiza, tia jeraha. 2 udhi, choma moyo, tia uchungu.

wound2 pt, pp of wind.

wove; woven pt, pp weave.

wow1 n (sl) mafanikio makubwa; ushindi wa kustusha. int la-la-la-la,lo.

wow2 sauti ya kupanda na kushuka inayotokana na kasoro katika kinasa sauti.

wrack n mwani (majani) wa baharini uliotupwa ufukoni.

wraith n mzuka, pepo.

wrangle vi 1 ~ (with sb) (about/oversth) zozana, gombana n mzozo ugomvi. ~r n mgomvi.

wrap vt,vi ~ (up) (in sth) 1 fungia,

setiri, funika. ~ sth up (sl) kamilisha. 2 ~ sth round sth viringishia; zungushia. 3 be ~ped up in fungwa, fungashwa; (fig) fichwa; zamia, penda sana n vazi la

wrestle

nje kama skafu, vazi la kufunika au la kujitanda. keep sth under ~s ficha. take off the ~s onyesha (kwa mara ya kwanza). ~per n 1 shali, nguo ya kujifunika. 2 karatasi ya kufungia kitu, k.m kifurushi. 3 kitambaa (kama khanga) cha Afrika Magharibi, vitu vya kufunikia/ kufungia. ~ping n.

wrath n (lit) ghadhabu, hasira. ~ful adj enye ghadhabu, enye hasira. ~fully adv.

wreak vt ~ sth (on sb) (lit) tolea, lipiza.

wreath n 1 shada la maua. 2 zingo (la moshi n.k.). ~ vt,vi (esp in pp) funika; zingira. 2 ~ itself round jizingia; zongomea/ viringisha. 3 ~ sth into fanya taji. 4 (of smoke, mist etc) fanya kuwa katika mzingo kama wa shada.

wreck n 1 kuvunjika (hasa chombo, merikebu, jahazi, meli), kupanda mwamba, (fig) kuvunjika kwa mipango, matarajio ya mtu. 2 meli iliyopata baa la kuvunjika. 3 gofu, chombo au jengo lililoharibiwa sana; mtu aliyetambarika vt haribu, bomoa; angamiza. ~age n mabaki ya chombo (kilichovunjika). ~er n 1 mtu anayelipwa kurudisha meli iliyoharibiwa. 2 mbomoaji majengo ya zamani. 3 (hist) msababisha kuvunjika kwa meli (ili apore).

wrench vt 1 sokota, vuta kwa ghafula. 2 umiza kwa kusokotoa/kutegua. 3 (fig) potosha, haribu maana n 1 kusokota/kuvuta kwa ghafla, uchungu mkali kutokana na kuachana/ kutengana na. 3 spana malaya, spana (inayorekebishwa).

wrest vt 1 ~ sth from/out of pokonya, nyang'anya. 2 ~ sth from pata kwa juhudi. 3 geuza, potosha maana.

wrestle vi ~ (with sb) piga mwereka; (fig) shindana (na vishawishi, majaribu n.k.) n shindano la mwereka, pambano. ~r n mpigaji

wretch

mweleka.

wretch n 1 maskini, fukara, mtu

mnyonge. 2 fidhuli. 3 bazazi; mhuni. ~ed adj 1 nyonge; -a huzuni; duni, dhalili. 2 -a kudhalilishwa. 3 -baya, -a ovyo. ~ edly adv. ~edness n 1 ufukara, unyonge, umaskini. 2 aibu. 3 wasiwasi.

wrick; rick vt shtusha; tegua kidogo n shtuo; teguko.

wriggle vi,vt 1 jinyonganyonga,

(ji)pindapinda. ~ out okoka kwa hila/werevu. ~ one's way into sth jiingiza katika jambo. 2 chezesha n kujinyonganyonga, kugaagaa; mapindi. ~r n buu la mbu.

wright n (rare except in compounds) fundi stadi.

wring vt 1 popotoa, songonyoa. ~ one's hands minya mikono. 2 ~ sth out; ~ sth out of/from sth kamua; (fig) lazimisha kutoa (habari). ~ing wet adj (of clothes) liolowa chepechepe, liotota n kamuo, mpopotoo. ~er n guruto.

wrinkle1 n kunyanzi; mkunjo vt,vi ~

(up) fanya makunyanzi; kunyata, kunjakunja; kunjikakunjika. wrinkly adj.

wrinkle2 n (colloq) kidokezi cha kufaa, shauri la manufaa.

wrist n kifundo (cha mkono). ~ band n sehemu ya shati ifikayo kwenye kifundo cha mkono. ~watch n saa ya mkono. ~let n utepe, pambo la mkononi.

writ n 1 hati serve a ~ on mpa mtu hati ya kumwita mbele ya mahakama. 2 the Holy W~ n Maandiko Matakatifu ya Biblia.

write vt,vi 1 andika. 2 ~ sth down

andika; punguza bei/ thamani. ~ sb down as mtu. ~ in for sth omba kwa barua. ~ off (for sth) agiza kwa barua. ~ sth off tunga haraka haraka; futa, maliza. ~ off n kitu kisicho na thamani tena, kitu kilichokwisha. ~ sth out andika kwa kirefu. ~ sth up andika vizuri,

wrong

kamilisha; tia thamani kubwa kuliko; elezea, sifia. ~ up n maandishi ya tukio. 3 (of book etc) andika, tunga. 4 ~ (to) -andikia. 5 (US pass) onyesha wazi; dhihirisha. written (also writ) large adj dhahiri, wazi. ~r n 1 mwandishi. ~r's cramp n kibibi (cha mkono). 2 (GB) karani. 3 (author) mwandishi wa vitabu, mtunzi. writing n 1 mwandiko. 2 (pl) maandishi give sth in ~ writing eleza jambo kwa maandishi. writing-desk n dawati. writing-ink n wino (wa kuandikia). writing-pad n kitita cha karatasi za kuandika. writing -paper n karatasi ya kuandikia (agh barua).

writhe vi jinyonga, tapatapa, furukuta, gaagaa; (fig) sononeka, umia/teseka akilini. ~ with shame jikunyata kwa aibu.

written pp of write.

wrong adj 1 -baya, -ovu; -a dhambi. 2 (mistaken) -enye (ma)kosa, si sawa, si sahihi. ~ side out nje/ndani. be caught on the ~ foot fumaniwa, shtukizwa, fumwa, kutwa bila kujitayarisha. get out of bed on the ~ side amka vibaya; amka na hasira. get hold of the ~ end of the stick kosa kabisa kuelewa jambo fulani, kuwa na dhana tofauti ya jambo, elewa vingine. in the ~ box mahali pasipostahili/pasipofaa. on the ~ side of fifty etc zidi/vuka miaka hamsini n.k. ~headed adj -kaidi; -potovu. ~ headedly adv. 3 enye shida, hali mbaya adv vibaya; visivyo, kwa makosa. get sth ~ -elewa/hesabu vibaya kitu. go ~ potea njia/barabara; -shindwa, tofaulu; vurugika; (colloq) (of a machine etc) haribika n 1 ubaya, dhambi, uovu. ~ doer n mwovu, mtenda mabaya/dhambi; mhalifu. ~ doing n utendaji maovu, dhambi; uhalifu. 2 dhuluma, uonevu. 3 in the ~ -enye makosa vt tendea ubaya; onea; dhulumu; hasiri. ~ful adj si a

wrote

haki, si sawa, kinyume cha sheria. ~fully; ~ly adv.

wrote pt of write.

wroth adj (pred only, poet, biblical or

in mod use, hum) -liokasirika/ ghadhibika, -enye hasira.

wrought 1 liyofuliwa (agh metali). ~ iron n chuma mfuo. 2 (arch or lit) ~ on/upon sb/sth hemsha; gusa. ~-up adj -liohemkwa, -liohamanika.

wrung pt of wring.

wry adj -a upande; liojikunyata/ kunjika. make a ~ face (mouth) kunja/finya uso a ~ smile tabasamu ya kulazimisha. ~ly adv.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.