TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

Y,y n herufi ya ishirini na tano ya alfabeti ya Kiingereza.

yacht n 1 yoti:boti dogo/jepesi la mashindano vi tembea/ shindana katika yoti. ~-club n klabu ya wenye yoti. ~ing n mashindano ya yoti; kutembea na yoti. ~sman n mwanariadha wa yoti. ~smanship n ustadi wa kuimudu yoti.

yak n (central Asia) nzao wa manyoya marefu.

yam n 1 kiazi kikuu. 2 (US) kiazi kitamu.

yammer vi (colloq) 1 lalamalalama, nung'unika. 2 bwabwaja, bwata.

yank (colloq) vt vuta kwa nguvu/ ghafula n mvuto mkali.

Yankee n 1 (colloq) (outside U.S.A) (sl) mtu wa Amerika, Mmarekani. 2 (US) mwenyeji wa New England. 3 (American Civil War) mwenyeji wa Majimbo ya Kaskazini.

yap vi 1 (of dogs) bwekabweka kwa sauti kali. 2 (sl) bwata, payuka n mbweko.

yard1 n 1 yadi, mita (=0.914 ). ~ measure n yadi, fimbo n.k. ya kupimia (ya yadi moja). ~-stick n (fig) kigezo, kipimo. 2 (naut) foromali. man the ~s panga watu mstarini ili kutoa heshima. ~age n 1 jumla/ idadi ya yadi.

yard2 n 1 (enclosure) ua, uga, (US) kitalu; uwanja school ~ uwanja wa shule railway ~ yadi. ~-master n bwana yadi. 3 (usually in compounds) (work ~) n kiwanda, karakana. brick -~ n kiwanda cha matofali. 4 the Y~ (colloq abbr for) New Scotland Y~ n Makao Makuu ya Upelelezi ya Uingereza.

yarn n 1 kitani, nyuzi zilizosokotwa. 2 (colloq) hadithi, kisa, masimulizi. spin a ~ simulia hadithi vi simulia hadithi.

yashmak n barakoa, ukaya.

yaw vi (of ship or aircraft) enda mrama n kwenda mrama.

yawn vi 1 piga miayo. 2 (lie open) fumbuka, -wa wazi (kama pango) n mwayo.

yaws n (pl) buba.

ye1 pron (old formal you) ninyi.

yen

ye2 defart (old written form of) the

yea adv in (arch) ndiyo, naam n

the ~s wasemao ndiyo, waunga mkono. ~h adv (sl) ndiyo.

year n 1 mwaka; kipindi tangu Januari 1 hadi Desemba 31 (mwaka wa kalenda). ~ in ~ out mwaka hadi mwaka, awamu baada ya awamu, mwaka baada ya mwaka. all (the) ~ round mwaka mzima. ~ of grace; ~ of Our Lord mwaka (wowote uliobainishwa baada kuzaliwa Yesu), mwaka. the ~ dot (colloq) zama za kale. 2 mwaka, kipindi chochote cha siku 365 mfululizo. ~-book n kitabu cha taarifa (ripoti, takwimu n.k.) za mwaka. ~ long adj -a mwaka mzima mfululizo. the academic ~ n mwaka wa masomo. the financial/fiscal ~ n mwaka wa fedha. 3 (pl) umri. ~ly adj -a kila mwaka adv (kwa) kila mwaka. ~ling n mnyama wa umri kati ya mwaka mmoja na miwili.

yearn vi ~ (for sth/to do sth) tamani sana, taka sana, onea shauku. ~ing n tamaa, uchu, shauku, kiu adj -enye uchu/shauku. ~ingly adv kwa shauku/uchu.

yeast n hamira, chachu. ~-powder n unga wa hamira (chachu). ~y adj -enye povu, lioumuka, kama chachu. yell vi,vt 1 piga yowe, piga kite. 2

~ sth (out) sema kwa sauti kubwa n ukelele (wa hofu, mashindano, maumivu n.k.).

yellow adj 1 -njano, -a rangi ya manjano. ~ flag n bendera ya manjano (inayopeperusha na meli iliyopigwa karantini). ~ press n magazeti yenye lengo la kusisimua tu. ~ fever n homa ya manjano 2. -oga. yellow bellied adj oga, -enye hofu n 1 rangi ya manjano vt,vi geuka kuwa manjano, geuza manjano. ~ish adj -a njanonjano. ~ness n unjano.

yelp vi piga unyende, lia (kama mbwa akipigwa) n unyende, mlio mkali na mfupi.

yen1 sarafu ya Kijapani.

yen2 n ~ for (colloq) tamaa, uchu, shauku vi tamani sana, ona shauku (ya kufanya kitu).

yeoman

yeoman n 1 (hist) mkulima. ~ service n utumishi bora wa muda mrefu; msaada (wakati wa matatizo /dhiki). 2 ~ of signals (GB) mwanamaji ahusikaye na ishara (kwa kutumia bendera, taa n.k.) (US) afisa mdogo mwenye kazi za ukarani. 3 askari mkulima. ~ry n kundi la wakulima askari (wa kujitolea).

yes particle ndiyo, naam, vema, vyema n ndiyo, kibali. ~-man n barakala, bwana ndiyo.

yester- pref a kabla ya hivi. ~day n 1 jana ~day week siku nane zilizopita ~ morn(ing) adv jana asubuhi. ~night adv jana usiku, usiku wa jana. ~year adv n mwaka jana.

yet adv 1 (in neg and conditional contexts) bado; -ja- he has not ~ come hajaja (bado) they haven't ~ done anything hawajafanya kitu bado. 2 (in interr and neg contexts) bado sasa there is ~ time bado kuna wakati need you go ~ lazima uende sasa. 3 (in affirm sentences) bado -ngali be thankful you are ~ alive shukuru bado ungali hai. 4 tena, baadaye, bado the enemy may strike again ~ adui huenda akashambulia tena baadaye. 5 as ~ hadi sasa we have not discussed the matter as ~ hatujayajadili mambo hadi sasa. nor ~ (lit) wala nor ~ beautiful wala sio mzuri conj hata hivyo, lakini he worked well ~ he failed alifanya kazi vizuri lakini akashindwa.

yeti n mnyama afananaye na binadamu ambaye yasemekana anaishi katika milima ya Himalaya.

Yiddish n Kiyahudi (kinachotumika hasa Ulaya ya Kati).

yield vt,vi 1 acha, jitoa, shindwa 2. toa matunda, zaa the cow ~s 3 litres of milk ng'ombe anatoa lita tatu za maziwa. 2 (of material, objects) topea, bonyea, nepa. 3 ~ (to sb/ sth) kubali (kushindwa). ~ (up) sth (to sb) salimu amri, ruhusu, acha upinzani, acha, achia. ~ up the

you

ghost (lit or rhet) -fa n mazao, mavuno, chumo, mapato. ~ing adj laini, teketeke, -a kubonyea; (fig) -tiifu, -epesi kushawishika. ~ingly adv.

yippee int huree!

ylang-ylang n mlangilangi; langilangi. yob yobbo yobo n (GB sl) mhuni. yodel vi imba kwa madoido n wimbo (wa madoido).

yoga n 1 yoga, mfumo wa kihindu wa kutafakari na kujidhibiti. 2 mfumo wa mazoezi ya maungo na kudhibiti pumzi. yogi n mwalimu bingwa wa yoga.

yogurt; yoghurt; yoghourt n mtindi.

yo-heave-ho int halambe! harambee! hrrrrr - tii!.

yoke n 1 (for cattle) nira. 2 (slave's) kongwa, mkatale. 3 (pair) (la maksai) jozi. 4 (bondage) utumwa; (authority, power) mamlaka, himaya the marriage ~ pingu za maisha vt,vi 1 fungia nira, fungasha, vaa nira. 2 unganisha; oza. yoke n mshamba.

yolk n kiiniyai.

yon (arch or dial) adj -le/ko adv kule, huko. ~der adj,adv (liter) kule, huko.

yore n of ~ kale, hapo kale, zamani.

you pron 1 wewe; u-; -ku-; (pl) ninyi, m-, -wa- between ~ and me kati yako wewe na mimi. 2 (colloq) yeyote ~ can never tell haijulikani, huwezi kujua. 3 (preceding a n, esp. in vocatives) wee, (pl) nyie/nyinyi. ~ girls nyie wasichana. ~r adj -ako, (pl) -enu give me ~r book nipe kitabu chako this is ~r room hiki ni chumba chenu. ~rs pred adj, pron 1 -ako; -enu is this cup ~rs? je, kikombe hiki chako? 2. (at the end of a letter) wako. ~rself (reflex pron) mwenyewe, -ji- did you make it ~rself? umeitengeneza mwenyewe? did you make it for ~rself? umejitengenezea? come by ~rselves njooni peke yenu. (all) by

young

~rself peke yako; bila msaada. ~'re; ~are ~'d ; ~ had; ~ would. ~'ll; ~ will. ~'ve ; ~ have.

young adj 1 changa. 2 -bichi the night

is still ~ usiku bado mbichi. 3 the ~er mdogo. be sb's ~er wa mdogo kuliko mwingine. 4 (used to distinguish a son from his father) kijana, mdogo ~ Ali kijana Ali, Ali mdogo. 5 (as a familiar or condescending form of address) ~ man/woman bwana mdogo/bi mdogo. 6 sio na uzoefu, chipukizi he is ~ in crime ni mhalifu chipukizi. 7 ~ and old kila mtu, wazee na vijana. the ~ watoto; vijana n mtoto; (of birds) kinda; (of animals) ndama. with ~ (of an animal) -enye mimba, (m) jamzito. ~ish adj -a ujana kiasi; kijana kijana. ~ster n mtoto; kijana.

yule

youth n 1 ujana, ushababi. 2 vijana; shababi. 3 mvulana,ghulamu, kijana. ~ festival n tamasha la vijana. ~ful adj -a ujana, shababi. ~fully adv. ~fulness n.

yowl vi piga unyende/ukelele, piga yowe.

Y-shaped adj -enye umbo la Y, -a panda.

yule n (also yule-tide) (arch) sikukuu ya Krismasi; sikukuu ya kuzaliwa Yesu. ~log n kigogo kinachochomwa mkesha wa Krismasi.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.