TUKI ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY
KAMUSI YA  KIINGEREZA-KISWAHILI

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

 

Z,z n herufi ya z: herufi ya mwisho katika alfabeti ya Kiingereza.

zany n mcheshi kidogo; mpumbavu; mpuuzi adj pumbavu; puuzi.

Zap (sl) piga; shambulia; shinda.

Zanzibar n (town) Unguja; (Island) Kisiwa cha Unguja; (Country) Visiwa vya Unguja na Pemba. A Z~ Islander n Muunguja, Mzanzibari. Z~ dialect n Kiunguja.

zeal n ari, raghba, moyo, ghera. ~ous adj -enye raghba. ~ously adv.

zealot n mlokole; mnazi; shabiki; mkereketwa. ~ism n ulokole, unazi, ushabiki. ~ry n.

zebra n punda milia. ~ crossing n alama (ya milia) ya kuvuka barabara kwa miguu.

zebu n (in Asia and E. Africa) zebu:

ng'ombe mwenye nundu.

zee n (US) jina la herufi Z.

zenith n anga; (fig) upeo (wa ustawi/ umashuhuri) wa watu/ mtu, ufanisi. ~al adj -a juu sana, -a kiwango cha juu.

zephyr n pepo za magharibi; (poet) upepo mwanana.

Zeppelin n zepelini: puto kubwa lililotumiwa na Wajerumani katika vita kuu ya kwanza.

zero n 1 sifuri, ziro, alama 0. 2

nukta kati ya hasi na chanya. ~ hour n (mil) saa ya kuanza mashambulizi. ~ in (on) (sl) jizatiti, kaa tayari, -wa makini, elekeza mawazo kwenye.

zest n 1 bidii, shauku kubwa. 2

(often with indef art) ladha, kiungo cha kukoza.

zeta n herufi ya sita ya Kigiriki.

zigzag adj -a mshazari, zigizaga, -a

kupindapinda n zigizaga adv kwa zigizaga, pindapinda, mshazari.

zinc n zinki. ~ plate n bamba la

zinki, zinki ferasi adj -enye zinki.

zing n (sl) bidii, nguvu.

zion n Uyahudi: Israel ~ist n.

zip n 1 sauti ya risasi hewani. 2 (fig) bidii put a ~ into it tia bidii katika jambo vt fungua. ~ sth open fungua kitu kwa zipu. ~ sth up funga kitu kwa zipu. ~fastener; ~per n zipu.

zipcode n (US) see postcode.

zither n nanga; zitha: ala ya muziki.

zygote

 

~ist n mpiga zitha.

zodiac n 1 zodiaki: ukanda wa anga wenye njia za sayari zote kuu. signs of the ~ nyota (za unajimu). 2 mchoro wa zodiaki.

zombi(e) n 1 dubwana; kizuu. 2 (colloq) zuzu; punguani, afkani.

zone n 1 ukanda, zoni northern ~ ukanda wa kaskazini equatorial ~ ukanda wa ikweta. 2 eneo maalum. zonal adj -a kanda, -a zoni vt gawa katika kanda. zoning n ugawanyaji wa maeneo mbalimbali.

zoo n (zoo) mahali wafugwapo wanyama pori; bustani ya wanyama. ~logy n zuolojia: sayansi ya miundo, umbo na ugawanyikaji wa wanyama. ~logical adj -a zuolojia. ~logical gardens n bustani kubwa za wanyama. ~logist n mwana zuolojia.

zoom vi 1 panda/ruka juu kwa kasi sana. 2 (of a camera) vuta picha. ~ in/out vuta karibu/mbali n 1 mlio wa eropleni inayopuruka kwa kasi. 2 ~ lens n (of a camera) lenzi ya kuvuta.

zoophyte n matumbawe zufiti: mnyama au mdudu kama mmea, yaani nusu mnyama nusu mmea.

zucchini n see courgette.

Zulu n 1 Mzulu: mwenyeji wa Afrika ya Kusini. 2 lugha ya Kizulu adj -a kizulu.

zygote n zaigoti: seli ya gameti mbili; kiumbe kichanga.

A | B | C | D | E | F | G | H | I | J | K | L | M | N | O | P | Q | R | S | T | U | V | W | X | Y | Z

INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, P. O. Box 35110, DAR-ES-SALAAM, TANZANIA.

ęTaasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) 2000 Second Edition 2000
ISBN 9976 911 29 7
All rights reserved. No part of this dictionary may be reproduced, stored in a retrieval system or transmitted in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording or otherwise, without the prior permission of the Institute of Kiswahili Research.