click here for ENGLISH-KISWAHILI
DICTIONARY
Ever since the
publication of Frederick Johnsons Swahili-English Dictionary in 1939, no new
dictionary of similar magnitude recording the development of the Swahili language in the
last 60 years has appeared. Hence learners and speakers of Swahili and English have faced
the problem of lack of an up-to date reference tool for Kiswahili. This Swahili-English
dictionary is intended to fill that gap.
This dictionary was
compiled by lexicographers in the Institute of Kiswahili Research at the University of Dar
es Salaam. It was, moreover, reviewed and critiqued by language and linguistics experts
from various universities in Tanzania and Kenya. Compilation of the dictionary began
formally in 1997; it was completed in the year 2000. It has more than 30,000 entries.
This dictionary is
an indispensable reference tool for students in secondary schools and colleges, language
learners, teachers, specialists and all speakers of Kiswahili and English. |
 |
click here for KAMUSI
YA KISWAHILI-KIINGEREZA
Tangu kuchapishwa
kwa kamusi ya Frederick Johnson ya Kiswahili-Kiingereza mwaka 1939, hakujatolewa tena
kamusi nyingine ya kiwango hicho yenye kuzingatia maendeleo ya lugha ya Kiswahili ya miaka
60 iliyopita. Hivyo wanafunzi na wazungumzaji wa Kiswahili na Kiingereza wamekuwa wakipata
matatizo kutokana na kukosekana kwa kifaa cha kurejelea kinachoakisi hali ya sasa ya lugha
ya Kiswahili. Kamusi hii ya Kiswahili-Kiingereza imekusudiwa kuziba pengo hilo.
Kamusi hii
imetayarishwa na wataalamu wa leksikografia wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, imepitiwa na kuhakikiwa na wataalamu wa lugha na isimu
kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania na Kenya.Uandishi wa Kamusi hii ulianza rasmi
mwaka 1997 na kukamilika mwaka 2000. Ina vitomeo (maneno yanayofafanuliwa) zaidi ya
30,000.
Kamusi hii itawafaa wanafunzi wa
sekondari na vyuo, wakurufunzi wa lugha, walimu, wataalamu na wazungumzaji wote wa lugha
za Kiswahili na Kiingereza. |